Search This Blog

Thursday, July 21, 2022

I KILLED MY BELOVED ONE (NILIMUUA NIMPENDAYE) - 1

 





    IMEANDIKWA NA : AZIZ HASHIM



    *********************************************************************************



    Simulizi : I Killed My Beloved One (Nilimuua Nimpendaye)

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jina langu naitwa Eunice, mtoto wa tatu kati ya watano wa familia ya baba yetu, mzee Ansbelt. Nilizaliwa miaka 26 iliyopita katika Kijiji cha Mtae, Lushoto mkoani Tanga lakini nimekulia jijini Dar es Salaam kwani baba yangu aliyekuwa akifanya kazi ya uhandisi katika Kampuni ya Usambara Civil Engineering, alihamishiwa kikazi jijini na akafanikiwa kujenga nyumba Tabata.

    Ni hapo ndipo mimi na ndugu zangu wa tumbo moja tulipokulia hadi tulipokuwa wakubwa. Kwa kweli kwa kipindi cha utotoni, tuliishi maisha mazuri sana kwani baba yetu alikuwa akijiweza kifedha hivyo alituhudumia vizuri kwa mavazi, chakula na elimu bora.

    Nakumbuka sisi ndiyo tulikuwa wa kwanza kumiliki runinga mtaani kwetu na ndiyo tulikuwa wa kwanza kupelekwa shuleni na ‘school bus’, tukisoma katika shule iliyokuwa inafundisha masomo yote kwa Kiingereza (English Medium), iliyokuwa nje kidogo ya jiji.

    Mama yetu hakuwa akifanya kazi, alikuwa akishinda nyumbani kuhakikisha sisi wanaye tunapata kila tulichokihitaji, ikiwemo malezi bora. Kutokana na aina ya malezi tuliyolelewa, tulikuwa tofauti sana na watoto wengine tuliokuwa tukiishi nao mtaani kwetu.

    Mimi na ndugu zangu wengine wa kike hatukuwa sawa na wasichana wengine mtaani kwetu ambao walianza kujihusisha na mapenzi wakiwa na umri mdogo, wengi wakitoka na wanaume wenye umri mkubwa, sawa na baba zao.

    Hata kaka zetu wawili, nao hawakuwa kama vijana wengi wa mtaani kwetu. Hawakuwa wakijichanganya na vijana wa kihuni waliokuwa wakitega kwenda shule na kushinda vijiweni kucheza kamari, kunywa pombe na kuvuta bangi.

    Ratiba tuliyokuwa tunapangiwa na wazazi wetu, ilitubana kwani hakuna aliyekuwa anapata muda wa kufanya mambo hayo. Tulipotoka shule, hatukuruhusiwa kuzurura mitaani bali sote tulikuwa tukikaa kwenye chumba cha kusomea na kuendelea kufanya ‘home work’ baada ya kula na kupumzika kidogo. Kila mmoja mtaani kwetu alikuwa akituita watoto wa geti kali na wengine walituchukia kwa madai kwamba tulikuwa tunaringia fedha za baba yetu.

    Hata hivyo, tuliendelea kuishi kwa misingi bora, tukiwaheshimu watu wote, wakubwa kwa wadogo. Siku zilizidi kusonga mbele, tukawa tunazidi kuwa wakubwa, wenye afya bora, wenye nidhamu na ndoto nyingi maishani.

    Nakumbuka mimi kila siku nilikuwa nikiwaambia wenzangu kwamba nikiwa mkubwa nataka kuwa rubani. Ndoto hizo zilinifanya niyapende sana masomo ya Fizikia, Jografia na Hesabu pamoja na masomo mengine ya sayansi.

    Niliamini hakuna kinachoweza kunirudisha nyuma kwenye ndoto zangu hizo kwani kila kitu kilikuwepo na wazazi wangu siku zote walikuwa wakiahidi kunisomesha mpaka nitakapotimiza malengo yangu.

    Maisha yalianza kuingia doa siku moja wakati tukirudishwa kutoka shule, mimi na kaka yangu. Tulipokaribia kufika nyumbani, tulishtushwa na umati mkubwa wa watu waliokuwa wamekusanyika nje ya nyumba yetu, wakionesha kuwa na nyuso za huzuni.

    “Nyumbani kuna nini? Mbona watu wengi namna hii,” nilimuuliza kaka yangu, Gisla ambaye tulikuwa tukisoma naye shule moja. Naye hakuelewa chochote, tukabaki tukitazamana na kutazama upande wa nyumba yetu bila kupata majibu.

    Baada ya kuteremka kwenye basi la shule, tulikuwa tukishauriana kama twende nyumbani au la kwani hali tuliyoiona ilitufanya tupatwe na woga wa ajabu. Tukiwa bado tumepigwa na bumbuwazi, tulimuona mama mmoja ambaye tulizoea kumuita mama Dotto akija mbiombio mpaka pale tulipokuwa tumesimama.

    Tulipomtazama usoni, macho yake yalikuwa mekundu sana kuonesha kwamba alikuwa amelia kwa muda mrefu. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Twendeni huku wanangu,” alisema mama Dotto na kutushika mikono, mmoja kushoto na mwingine kulia, akatupeleka mpaka nyumbani kwake, tukaingia sebuleni kisha akafunga mlango, akatusogelea na kutushika mabegani.

    “Wanangu kuna matatizo nyumbani. Nawaomba mjikaze kwani kazi ya Mola haina makosa,” alisema mama Dotto huku akijifuta machozi, tulitazamana tukiwa bado hatujapata majibu ya alichokuwa anakimaanisha. Ilibidi nivunje ukimya na kumuuliza tena alikuwa anamaanisha nini.

    “Baba yenu amepata ajali mbaya akiwa kazini, hivi tunavyozungumza hatunaye tena duniani,” alisema mama Dotto, kauli iliyoamsha vilio vya nguvu kutoka kwangu na kwa kaka Gisla.

    Awali hatukuamini alichokuwa anakizungumza, tukawa tunahisi labda tupo ndotoni. Tulitoka mbiombio ndani kwa mama Dotto, tukawa tunakimbilia nyumbani kwetu huku tukipiga mayowe ya nguvu.

    Tuliwapita watu wengi waliokuwa nje ya nyumba yetu ambao walijitahidi kutuzuia bila mafanikio, tukaingia mpaka sebuleni ambapo tulishangaa kukuta vitu vyote vimetolewa na kutandikwa mazulia ambayo yalikuwa yamekaliwa na watu waliokuwa wanaomboleza.

    Tulipoangalia kwenye kona moja, tulimuona mama akiwa ameshikiliwa na wanawake wenzake wengi, akiwa analia kwa uchungu huku akilitaja jina la baba. Nilishindwa kujizuia, nilijaribu kumkimbilia mama pale alipokuwa ameshikiliwa lakini mwili uliniisha nguvu, miguu ikanilegea kisha nikaanza kuhisi kizunguzungu kikali, nikaanguka chini kama mzigo, puuh!

    Mwili uliniisha nguvu, miguu ikanilegea kisha nikaanza kuhisi kizunguzungu kikali, nikaanguka chini kama mzigo, puuh! Nilikuja kushtuka saa kadhaa baadaye, nikajikuta nimelala nje ya nyumba yetu huku nikipepelewa kwa vitenge na wanawake ambao niliwatambua kwamba ni majirani zetu.

    Niliporejewa na fahamu tu, nilikumbuka kilichonifanya nikawa katika hali hiyo, nikaendelea kuomboleza msiba wa baba huku nikiwa na hamu kubwa ya kujua nini kilichotokea. Nililia sana huku nikiwa bado siamini kama ni kweli baba ametangulia mbele ya haki.

    Nikawa naendelea kuomboleza, huku wanawake wengi ambao ni majirani na marafiki wa familia yetu wakitumbembeleza. Kati ya waombolezaji wote, mimi na mama ndiyo tulikuwa na hali mbaya zaidi. Niliumizwa sana na kifo cha ghafla cha baba kwani nilishaona ambacho kingetokea mbele yetu. Mama hakuwa na kazi yoyote na kwa kipindi chote tangu nikiwa mdogo, sikuwahi kumuona akijishughulisha na shughuli yoyote ya kutuingizia kipato.

    Hakuwa kama wanawake wengine mtaani kwetu ambao walikuwa wakifanya biashara mbalimbali ambazo ziliwaongezea kipato zikiwemo ufugaji wa kuku wa nyama na mayai, kukopesha vitu kama vyombo vya nyumbani, mashuka au nguo, ufundi cherehani na shughuli nyingine za kiujasiriamali.

    Sitaki sana kumlaumu mama lakini nadhani maisha aliyozoeshwa na baba ndiyo yaliyomfanya awe hivyo. Wakati nikiendelea kulia kwa uchungu, nilikuwa nikifikiria nini hatima yetu mimi na ndugu zangu kwani hakuna hata mmoja kati yetu aliyekuwa amefikia hatua ya kujitegemea. Sote bado tulikuwa tukitegemea malezi ya baba na mama.

    Wakati tukiendelea kuomboleza, nilimuona mfanyakazi mmoja aliyekuwa akifanya kazi na baba akifika nyumbani kwetu, akiwa ameongozana na wanaume watatu huku mmoja akiwa na bunduki mkononi. Bila hata kuuliza, nilijua kuwa lazima amekuja na polisi. Sikuelewa sababu iliyomfanya aje na polisi msibani, nikahisi lazima kuna tatizo kubwa.

    Sikutaka kupitwa na jambo, nikajifanya nainuka ili niende chooni, nikasogea mpaka upande waliokuwa wamesimama huku nikiwa nimetega masikio kwa makini.

    “Mkewe ni yupi kati ya hawa,” aliuliza mmoja kati ya wale askari, yule mfanyakazi mwenzake baba ambaye tulizoea kumuita baba Sufiani, akaongea nao jambo kwa sauti ya chini kisha nikaona wote wamenigeukia mimi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikawa natetemeka kwani sikuwa najua kilichokuwa kinaendelea. Wakanisogelea mpaka pale nilipokuwa nimesimama, wakanipa mikono ya pole kisha baba Sufiani akanitambulisha. Akawatajia wale askari jina langu kisha akawaeleza kuwa mimi ndiyo mtoto wa kike mkubwa wa marehemu Ansbelt.

    Ikumbukwe kwamba tulizaliwa watano kwenye familia yetu, wavulana wawili na wasichana watatu, mimi nikiwa ndiyo mkubwa kwa upande wa wasichana na nikiwa ndiyo wa pili kuzaliwa baada ya kaka yangu Gisla.

    Baada ya hapo, aliwatambulisha watu hao kwangu na kunieleza kuwa ni polisi kutoka Kituo Kikuu ambao walikuwa wakifuatilia tukio la mauaji ya baba. Aliposema ‘mauaji ya baba’ nilishtuka kidogo kwani awali nilisikia kwamba baba amepata ajali akiwa kazini. Sasa kama amekufa kwa ajali, kwa nini wanazungumzia mauaji? Nilijiuliza bila kupata majibu.

    Wale askari walisema wanahitaji kuzungumza na mimi kwa ufupi kabla hawajazungumza na mama. Tulisogea pembeni ambapo jambo la kwanza waliniuliza jinsi tulivyokuwa tukiishi na marehemu baba. Niliwaeleza kuwa siku zote tulikuwa tukiishi kwa amani na upendo, huku akituonesha mapenzi makubwa.

    “Umewahi kusikia kama baba yako ana ugomvi na mtu yeyote?” aliniuliza yule askari aliyekuwa ameshika bunduki, nikawa natazama juu kwa lengo la kuvuta kumbukumbu. Kiukweli sikuwahi kusikia kama baba ana ugomvi na mtu yeyote, siyo kazini kwake wala nyumbani. Alikuwa akiishi vizuri na majirani na kila mmoja alimpenda kutokana na ucheshi wake.

    Niliwajibu kwamba sijawahi kusikia baba akikorofishana au kuwa na ugomvi na mtu yeyote. Wakaniuliza kabla halijatokea tukio hilo, baba yangu alikuwa katika hali gani? Nilivuta kumbukumbu na kujaribu kuzitazama siku kadhaa nyuma, nikagundua kuwa baba hakuwa na tofauti yoyote na siku zote. Nikawajibu kwamba alikuwa kawaida tu.

    Mmoja kati yao alikuwa akiyaandika majibu yote kwenye kitabu cheusi alichokuwa nacho kisha baada ya hapo, waliomba kwenda kuongea na mama. Kabla hawajaondoka, niliwauliza nini kilichotokea mpaka baba yangu akafa. Mmoja kati yao akaniambia kwamba baba alikuwa amepigwa na kitu kizito kichwani na kusababisha apasuke sehemu ya nyuma ya kichwa chake, hali iliyosababisha kifo chake.

    Nilishtuka mno kusikia hivyo, kwa mara nyingine nikajikuta nikiishiwa nguvu, miguu ikanilegea na mwili wote ukanyong’onyea, nikaanguka tena. Kwa bahati nzuri, baba Sufiani aliniwahi kabla sijajibamiza chini, akanidaka na kusaidiana na wale askari wengine kunipeleka kwenye kundi la wanawake waliokuwa wanaendelea kuomboleza.

    Wakaanza upya kunipepelea mpaka nilipozinduka.

    Niliporejewa na fahamu, nilijikuta nikiwa pembeni ya mama ambaye bado alikuwa akiendelea kulia kwa uchungu. Wale askari waliokuwa wamekuja na baba Sufiani hawakuwepo tena.



    Mwili uliniisha nguvu, miguu ikanilegea kisha nikaanza kuhisi kizunguzungu kikali, nikaanguka chini kama mzigo, puuh! Nilikuja kushtuka saa kadhaa baadaye, nikajikuta nimelala nje ya nyumba yetu huku nikipepelewa kwa vitenge na wanawake ambao niliwatambua kwamba ni majirani zetu.

    SASA ENDELEA...



    Niliporejewa na fahamu tu, nilikumbuka kilichonifanya nikawa katika hali hiyo, nikaendelea kuomboleza msiba wa baba huku nikiwa na hamu kubwa ya kujua nini kilichotokea. Nililia sana huku nikiwa bado siamini kama ni kweli baba ametangulia mbele ya haki.

    Nikiwa naendelea kuomboleza, huku wanawake wengi ambao ni majirani na marafiki wa familia yetu wakitumbembeleza. Kati ya waombolezaji wote, mimi na mama ndiyo tulikuwa na hali mbaya zaidi. Niliumizwa sana na kifo cha ghafla cha baba kwani nilishaona ambacho kingetokea mbele yetu. Mama hakuwa na kazi yoyote na kwa kipindi chote tangu nikiwa mdogo, sikuwahi kumuona akijishughulisha na shughuli yoyote ya kutuingizia kipato.

    Hakuwa kama wanawake wengine mtaani kwetu ambao walikuwa wakifanya biashara mbalimbali ambazo ziliwaongezea kipato zikiwemo ufugaji wa kuku wa nyama na mayai, kukopesha vitu kama vyombo vya nyumbani, mashuka au nguo, ufundi cherehani na shughuli nyingine za kiujasiriamali.

    Sitaki sana kumlaumu mama lakini nadhani maisha aliyozoeshwa na baba ndiyo yaliyomfanya awe hivyo. Wakati nikiendelea kulia kwa uchungu, nilikuwa nikifikiria nini hatima yetu mimi na wadogo zangu kwani hakuna hata mmoja kati yetu aliyekuwa amefikia hatua ya kujitegemea. Sote bado tulikuwa tukitegemea malezi ya baba na mama.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati tukiendelea kuomboleza, nilimuona mfanyakazi mmoja aliyekuwa akifanya kazi na baba akifika nyumbani kwetu, akiwa ameongozana na wanaume watatu huku mmoja akiwa na bunduki mkononi. Bila hata kuuliza, nilijua kuwa lazima amekuja na polisi. Sikuelewa sababu iliyomfanya aje na polisi msibani, nikahisi lazima kuna tatizo kubwa. Sikutaka kupitwa na jambo, nikajifanya nainuka ili niende chooni, nikasogea mpaka upande waliokuwa wamesimama huku nikiwa nimetega masikio kwa makini.

    “Mkewe ni yupi kati ya hawa,” aliuliza mmoja kati ya wale askari, yule mfanyakazi mwenzake baba ambaye tulizoea kumuita baba Sufiani, akaongea nao jambo kwa sauti ya chini kisha nikaona wote wamenigeukia mimi.

    Nikawa natetetemeka kwani sikuwa najua kilichokuwa kinaendelea. Wakanisogelea mpaka pale nilipokuwa nimesimama, wakanipa mikono ya pole kisha baba Sufiani akanitambulisha. Akawatajia wale askari jina langu kisha akawaeleza kuwa mimi ndiyo mtoto wa kike mkubwa wa Ansbelt. Ikumbukwe…

    Baada ya hapo, aliwatambulisha watu hao kwangu na kunieleza kuwa ni polisi kutoka Kituo Kikuu ambao walikuwa wakifuatilia tukio la mauaji ya baba. Aliposema ‘mauaji ya baba’ nilishtuka kidogo kwani awali nilisikia kwamba baba amepata ajali akiwa kazini. Sasa kama amekufa kwa ajali, kwa nini wanazungumzia mauaji? Nilijiuliza bila kupata majibu.

    Wale askari walisema wanahitaji kuzungumza na mimi kwa ufupi kabla hawajazungumza na mama. Tulisogea pembeni ambapo jambo la kwanza waliniuliza jinsi tulivyokuwa tukiishi na marehemu baba. Niliwaeleza kuwa siku zote tulikuwa tukiishi kwa amani na upendo, huku akituonesha mapenzi makubwa.

    “Umewahi kusikia kama baba yako ana ugomvi na mtu yeyote?” aliniuliza yule askari aliyekuwa ameshika bunduki, nikawa natazama juu kwa lengo la kuvuta kumbukumbu. Kiukweli sikuwahi kusikia kama baba ana ugomvi na mtu yeyote, siyo kazini kwake wala nyumbani. Alikuwa akiishi vizuri na majirani na kila mmoja alikuwa akimpenda kutokana na ucheshi wake.

    Niliwajibu kwamba sijawahi kusikia baba akikorofishana au kuwa na ugomvi na mtu yeyote. Wakaniuliza kabla halijatokea tukio hilo, baba yangu alikuwa katika hali gani? Nilivuta kumbukumbu na kujaribu kuzitazama siku kadhaa nyuma, nikagundua kuwa baba hakuwa na tofauti yoyote na siku zote. Nikawajibu kwamba alikuwa kawaida tu.

    Mmoja kati yao alikuwa akiyaandika majibu yote kwenye kitabu cheusi alichokuwa nacho kisha baada ya hapo, waliomba kwenda kuongea na mama. Kabla hawajaondoka, niliwauliza nini kilichotokea mpaka baba yangu akafa. Mmoja kati yao akaniambia kwamba baba alikuwa amepigwa na kitu kizito kichwani na kusababisha

    apasuke sehemu ya nyuma ya kichwa chake, hali iliyosababisha kifo chake.

    Nilishtuka mno kusikia hivyo, kwa mara nyingine nikajikuta nikiishiwa nguvu, miguu ikanilegea na mwili wote ukanyong’onyea, nikaanguka tena. Kwa bahati nzuri, baba Sufiani aliniwahi kabla sijajibamiza chini, akanidaka na kusaidiana na wale askari wengine kunipeleka kwenye kundi la wanawake waliokuwa wanaendelea kuomboleza.

    Wakaanza upya kunipepelea mpaka nilipozinduka.

    Niliporejewa na fahamu, nilijikuta nikiwa pembeni ya mama ambaye bado alikuwa akiendelea kulia kwa uchungu. Wale askari waliokuwa wamekuja na baba Sufiani hawakuwepo tena.

    “Mama eti ni kweli kuna watu wamemuua baba?” nilimuuliza mama huku nikitokwa na machozi. Alinijibu kwa kutingisha kichwa kisha sote tukaendelea kulia. Ndugu wa

    marehemu baba kutoka kijijini Mtae, Lushoto walianza kuwasili kwa makundi baada ya kupata taarifa za msiba huo. Watu wote wa muhimu walipofika, mipango ya mazishi ilianza kufanywa.

    Siku iliyofuatia, wanafamilia, ndugu na baadhi ya majirani tuliongozana mpaka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako mwili wa baba ulikuwa umehifadhiwa, baada ya taratibu zote kukamilika, tulikabidhiwa maiti kwa ajili ya mazishi. Siwezi kueleza

    jinsi nilivyojisikia kumuona baba yangu akiwa ndani ya jeneza, akiwa amevalishwa suti yake aliyokuwa anaipenda sana pamoja na tai nzuri.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ungeweza kudhani kwamba amelala na baada ya muda angeamka lakini haikuwa hivyo, baba alikuwa amekufa. Tulirudi na mwili wa marehemu baba mpaka nyumbani

    huku mama akipoteza fahamu mara kwa mara. Ndugu zangu wengine wa damu nao walikuwa na hali mbaya kwa majonzi kwani tulipata pigo kubwa sana bila kutarajia.

    Baada ya kuufikisha mwili wa marehemu nyumbani, watu wengine walipata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho kisha safari ya kuelekea makaburini ikaanza. Ilikuwa ni siku ambayo siwezi kuisahau kwenye maisha yangu.

    Hatimaye tulimpumzisha baba katika nyumba yake ya milele, tukarudi nyumbani kuendelea na msiba lakini tuliporudi tu kutoka makaburini, niligundua kwamba hali ya pale nyumbani haikuwa sawa ingawa kwa haraka sikubaini kumetokea nini.

    Japokuwa baada ya msiba kutokea vitu vyote vya thamani tulivifungia kwenye chumba kimoja kwa sababu ya usalama na funguo akabaki nayo mama, baada ya kurudi niligundua kuwa mlango wa chumba hicho ulikuwa umefunguliwa na baadhi ya vitu vya thamani havikuwepo.

    Nilitaka kwenda kumuuliza mama kwa sababu yeye ndiyo mtu pekee aliyekuwa na funguo za chumba hicho lakini nikaona itakuwa ni sawa na kumtonesha donda ambalo bado halijapona kwani hali aliyokuwa nayo, bado haikuwa nzuri.

    Niliwafuata kaka zangu na kuwauliza kama wana taarifa juu ya vitu hivyo vilikopelekwa, wote wakaniambia kuwa hawajui. Wadogo zangu nao walinijibu hivyohivyo na kwa sababu sote tuliondoka kwenda makaburini kumzika baba, hakukuwa na mtu wa kumlaumu.

    Nikaamua kufanya upelelezi kimyakimya kwa wanawake wachache ambao walibaki pale nyumbani wakipika wakati sote tulipoenda makaburini.

    “Watoto wa siku hizi bwana, yaani msiba bado mbichi kabisa umeshaanza kuulizia mali za baba yako? Utafikiri ulikuwa unaombea afe,” alinijibu mwanamke mmoja kwa nyodo nilipomuuliza kuhusu suala hilo.

    Sikufurahishwa na majibu yake lakini kwa kuwa tulikuwa matatizoni, na yeye alikuwa amenizidi sana umri niliamua kunyamaza. Kuepusha matatizo ya upotevu wa vitu vingi zaidi, niliamua kwenda kumtafuta fundi ambaye alikuwa ni jirani yetu, nikamwambia kwamba nataka akabadilishe kitasa haraka iwezekanavyo.

    Kwa kuwa nilikuwa na fedha kidogo za akiba nilizopewa kama pole ya kuondokewa na baba, nilimpa kwa ajili ya kwenda kununulia hicho kitasa pamoja na hela ya ufundi. Kwa bahati nzuri, baada ya muda mfupi tayari alisharudi kununua vifaa, nikamuingiza mpaka ndani na kazi ikaanza mara moja.

    Kitasa kipya kikawekwa, nikakifunga tena chumba hicho na funguo moja nikaenda kumpa mama, nyingine kaka yangu mkubwa na ya tatu nikabaki nayo mimi. Nilimueleza mama kwa kifupi kwa nini nimechukua uamuzi huo ambapo na yeye alionesha kushtushwa na taarifa kwamba kuna vitu vya thamani vimechukuliwa.

    Hatua niliyoichukua ilisaidia sana, siku hiyo ikapita salama. Siku ya tatu ilipowadia, tulianua matanga kama ilivyo mila na desturi za kabila letu, wanafamilia wote tukaogeshwa kwa maji maalum na kunyolewa nywele.

    Baada ya hapo, wanandugu wote walikaa kikao lakini sisi tukazuiwa kushiriki kwa madai kuwa mambo yaliyokuwa yakijadiliwa yalikuwa ya kiutu uzima. Ndugu wa baba waliosafiri kutoka Mtae, Lushoto wakakaa pamoja na mama na wanandugu wengine.

    Japokuwa hatukushiriki, nilimsikia mama akizungumza kwa sauti ya juu kuwaambia ndugu wa baba kwamba wamuache na maisha yake kwa sababu hajashindwa kutulea sisi watoto wake. Nikasikia akisema hata katika wosia aliouacha baba, aliandika kuwa akifa mali zote ziwe chini yake mpaka sisi watoto wake tutakapokuwa wakubwa na kufikia hatua ya kujitegemea.

    Baada ya kikao hicho ambacho sikujua muafaka gani ulifikiwa, ndugu wote waliaga na kuondoka siku hiyohiyo, tukabaki wenyewe pale nyumbani. Maisha yakawa yanasonga mbele huku taratibu tukianza kusahau msiba wa baba. Miongoni mwa vitu ambavyo Mungu anapaswa kushukuriwa, ni kutuumba binadamu na akili za kusahau matatizo yanayotukuta, hata yawe makubwa kiasi gani.

    Siku baba aliyokufa nilidhani nitakuwa na uchungu na huzuni kwa siku zote za maisha yangu lakini haikuwa hivyo, kwa kadiri siku zilivyokuwa zinasonga mbele ndivyo nilivyokuwa nazoea hali ile na kuona kama kilichotokea ni cha kawaida.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ndugu zangu wengine nao waliiona hali hiyo kama mimi, tukawa tukikaa pamoja hatuzungumzii tena habari za baba bali mambo mengine. Mama naye alionesha kumsahau baba haraka kama ilivyokuwa kwetu. Baada ya siku ya arobaini, tulihitimisha matanga kwa kufanya sherehe ndogo ya kuwashukuru watu wote waliojumuika nasi katika kipindi kigumu cha msiba wa baba.

    Siku chache baada ya arobaini, mama alianza tabia ambayo awali hakuwa nayo. Alianza kuondoka nyumbani asubuhi na kurudi jioni, jambo ambalo wakati wa uhai wa baba hakuwahi kulifanya. Kingine kilichonishangaza, kabla ya kutoka, mama alikuwa akitumia muda mrefu kujiremba na kujipodoa, huku akijipulizia marashi mazuri na kuvaa nguo zilizomfanya aonekane kijana.

    “Hee! Kumbe mama ukivaa hivyo unaonekana mrembo hivyo? Zamani ulikuwa hupendezi hivyo,” mdogo wetu mmoja alimweleza mama siku moja wakati akijiandaa kutoka, sote tukacheka kwa furaha. Hata hivyo, mimi nilikuwa nikiyatazama mambo yote yanayotokea kwa jicho la tofauti.

    Siku moja mama alichelewa sana kurudi nyumbani kuliko siku zote, ilipofika saa mbili za usiku, nikiwa jikoni nawaandalia ndugu zangu chakula cha usiku, nilisikia muungurumo wa gari lililokuja na kupaki jirani kabisa na nyumbani. Nikafunua pazia

    la jikoni na kuchungulia nje, nikamuona mama akiteremka kisha akateremka mwanaume mwingine ambaye kutokana na giza sikuweza kumtambua.

    Kwa macho yangu nikawashuhudia wakikumbatiana kisha wakapigana mabusu, yule mwanaume akarudi kwenye gari na kuliwasha, akaondoka huku mama akimpungia mkono mpaka alipopotelea mitaani. Nilishika mdomo kwa mshangao nikiwa ni kama siamini kile nilichokiona.



    Nilijiuliza mama amekumbwa na nini mpaka kufikia kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine katika kipindi ambacho hata miezi mitatu ilikuwa haijapita tangu baba alipofariki! Nikakosa jibu. Harakaharaka nikafunika pazia na kujifanya sijui chochote kilichotokea.

    Muda mfupi baadaye, nikamsikia mama akigonga mlango. Kwa kuwa ndugu zangu walikuwa sebuleni wakitazama runinga, hakuna aliyesikia mlango ukigongwa, ikabidi niache kupika na kwenda kufungua mlango.

    Nilimfungulia mlango mama na kumuamkia kwa adabu kama ilivyokuwa kawaida yetu, alipofumbua mdomo wake kunijibu, nilisikia harufu ya pombe kutoka kinywani mwake, nikabaki nimeduwaa nikiwa siamini kile kilichotokea.

    “Ina maana mama ameanza kunywa pombe? Mbona wakati baba akiwa hai sikuwahi kumuona akinywa pombe hata mara moja?” nilijiuliza kimoyomoyo huku nikijitahidi kuficha mshtuko nilioupata.

    Nadhani mama naye alijishtukia kwani hakupitia sebuleni kama ilivyokuwa kawaida yake bali alipitiliza chumbani kwake moja kwa moja.

    Alipoingia chumbani kwake, nilisikia akibamiza mlango kwa nguvu. Hakutoka tena wala hakuja kujumuika nasi kula chakula cha usiku kama ilivyokuwa kawaida. Ndugu zangu walikuwa wanauliza kwa nini mama hajajumuika nasi kula chakula wala kuwasalimu baada ya kurudi kama ilivyokuwa kawaida yake?

    Kwa kuwa tayari nilikuwa najua kinachoendelea, niliwadanganya kwamba mama ameniambia kuwa anajisikia vibaya ndiyo maana amepitiliza moja kwa moja chumbani

    bila hata kuwasalimu. Walinielewa, tukaendelea kula mpaka sote tulipotosheka.

    Tukaendelea kutazama tamthiliya kwenye runinga mpaka kila mmoja alipochoka, tukaagana na kutakiana usiku mwema, kila mmoja akaenda kulala. Nikiwa chumbani kwangu ambako nilikuwa nikilala na wadogo zangu wawili wa kike, niliendelea kujiuliza kuhusu mabadiliko aliyokuwa nayo mama bila kupata majibu.

    Sikutaka kuamini kama mama anaweza kufanya mambo hayo katika kipindi ambacho sisi wanaye tulikuwa tunamtegea sana kutuongoza hasa baada ya baba kufariki. Nilianza kuingiwa na wasiwasi mkubwa juu ya hatima ya maisha yetu ya baadaye hasa ukizingatia kuwa watoto wote watano tulikuwa tukisoma, tena kwenye shule za gharama.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Baba kwa nini umeondoka na kutuacha tukiwa bado wadogo? Kwa nini usingesubiri kila mmoja awe mtu mzima na kuanza kujitegemea?” nilijikuta nikitamka maneno hayo bila kujielewa huku machozi yakinitoka.

    Mdogo wangu mmoja alishtuka baada ya kunisikia nikizungumza mwenyewe, akaniuliza kama nilikuwa na tatizo lakini nikajikaza na kujifanya hakuna chochote

    kilichotokea. Nikageukia upande wa pili kwani sikutaka agundue kwamba nilikuwa nalia. Niliendelea kuwaza mpaka usiku wa manane ndipo nikapitiwa na usingizi. Saa kumi na moja alfajiri, usingizi ulinipaa, ikanilazimu kuamka na kuanza kuwaandaa wadogo zangu kwa ajili ya kwenda shule. Niliwaamsha na kaka zangu ambao nao walianza kujiandaa.

    Tukiwa tunaendelea kujiandaa, mama naye aliamka na kuanza kujiandaa kama kawaida yake. Akatumia muda mrefu kujiremba kisha akatuaga na kuondoka

    wakati sisi tukiendelea kusubiri magari ya shule tulizokuwa tunasoma yatupitie pale nyumbani.

    “Mama siku hizi yupo bize sana, anaondoka asubuhi na kurudi usiku. Kwani amekwambia anafanya kazi gani?” kaka yangu mkubwa aliniuliza, nikamwambia sielewi chochote kwani hatujawahi kukaa na mama na kunieleza huwa anakwenda wapi.

    Kaka yangu mwingine ambaye alikuwa kipenzi cha mama, alidakia na kusema kuwa ni lazima mama ahangaike kututafutia mahitaji yetu muhimu ikiwemo ada za shule kwani majukumu yote aliachiwa yeye baada ya baba kutangulia mbele za haki. Sikutaka kufumbua mdomo wangu na kusema chochote, nikatingisha kichwa kuashiria kumuunga mkono kaka kwa alichokisema, tukaendelea kusubiri gari.

    Muda mfupi baadaye, gari la kwanza lilifika ambapo niliwapakiza wadogo zangu wawili wa kike na kaka yangu wa pili ambao walikuwa wakisoma shule moja. Wakaondoka na kwenda zao shule. Mimi na kaka yangu mkubwa tukaendelea kusubiri gari lingine kwani na sisi tulikuwa tukisoma shule moja.

    Hakuna aliyemsemesha mwenzake na muda wote nilikuwa nimejiinamia, nikionesha kuwa na mawazo mengi, hali ambayo hata kaka yangu aliigundua.

    “Dada Eunice, upo sawa kweli? Mbona unaonekana kuwa na mawazo sana.”

    “Aaah! Kawaida tu, si unajua siku hazifanani, leo nahisi kama naumwaumwa hivi.”

    “Basi usiende shule, nenda hospitali ukapime,” aliniambia kaka yangu lakini nikamhakikishia nitakuwa sawa baada ya muda mfupi. Nashukuru alinielewa,

    tukaendelea kusubiri gari na baada ya muda liliwasili, tukapanda na kwenda shuleni ambapo ratiba za masomo ziliendelea kama kawaida mpaka jioni.

    Wakati tunarudi nyumbani jioni, mimi na kaka yangu ndiyo tulikuwa wa kwanza kuwasili. Tulipokaribia nyumbani, niliona kuna gari limepaki nje ya nyumba yetu, nilipolitazama nililitambua kwa haraka kuwa ndiyo lile lililomleta mama usiku uliopita.

    Tulipolikaribia, dereva aliliwasha na kuondoka, likapita karibu yetu lakini kwa kuwa lilikuwa na vioo vya ‘tinted’ hatukuona ndani kulikuwa na nani. Kaka yangu hakuelewa chochote kinachoendelea na wala hakujua kwamba gari lile lilikuwa limetoka pale nyumbani kwetu.

    Sikutaka kumfumbua macho, nilinyamaza kimya na tukaendelea kutembea taratibu mpaka tulipofika nyumbani. Mama alikuwepo ndani kwani tulikuta mlango upo wazi, tukagonga na kuingia, mimi nikapitiliza moja kwa moja mpaka chumbani kwa mama kumsalimu.

    Kama ilivyokuwa usiku uliopita, mama alionesha kulewa chakari ingawa bado ilikuwa mapema. Nilipomsalimia aliitikia kilevi na kunitaka niufunge mlango wa chumba chake, akaniambia wadogo zangu wakimuulizia niwaambie anajisikia vibaya hivyo amepumzika.

    Kumbe wakati akizungumza maneno hayo, kaka yangu naye alikuwa mlangoni akisikiliza, akashangaa mno kugundua kuwa mama alikuwa amelewa, nikamuona ameshika mdomo wake kwa mshangao. Nilifunga mlango kama nilivyoagizwa, nikatoka na kumshika kaka mkono kwani bado alikuwa amepigwa na butwaa, tukaenda kukaa sebuleni.

    “Mama ameanza lini kunywa pombe?” kaka yangu aliniuliza huku akiwa bado ameduwaa, sikumjibu chochote, nikainuka na kwenda jikoni kuanza kuandaa chakula. Muda mfupi baadaye, ndugu zetu wengine waliwasili kutoka shuleni. Walipomuulizia mama, niliwajibu kama nilivyopewa maagizo, nikamuona kaka yangu naye amezama kwenye dimbwi la mawazo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tabia ya mama iliendelea kuota mizizi kila kukicha, ikawa haiwezi kupita siku bila kunywa pombe na kuchelewa kurudi nyumbani. Ndugu zangu walishangazwa sana na mabadiliko hayo lakini nikawa najitahidi kuwatuliza mara kwa mara na kuwapa moyo kwamba mama atarejea katika hali yake ya kawaida baada ya siku chache.

    Siku zilizidi kusonga mbele, muhula wa kwanza wa masomo ukawa umemalizika. Tukafunga shule kwa muda wa takribani mwezi mmoja. Tofauti na likizo zote, mama aliamua kutusafirisha wote kwenda nyumbani kwa wazazi wake. Alichokifanya ilikuwa ni kutusafirisha hadi kijijini kisha akatuacha na yeye akarudi jijini Dar es

    Salaam kwa madai kwamba anaenda kuendelea na biashara zake.

    Hakukuwa na wa kumhoji kwani tangu zamani, babu na bibi hawakuwa na uwezo wa kumsemesha jambo lolote baya kutokana na misaada mingi aliyokuwa anawapa. Kabla mama hajaondoka, alituita wote kisha akatuambia kuwa hakuna mwenye ruhusa ya kuwaeleza bibi na babu siri za maisha yetu, akatuonya kwamba endapo atasikia mambo yoyote kutoka kwa bibi na babu, tutamtambua.



    Mama alikuwa amebadilika sana, hata namna ya kuzungumza na sisi haikuwa kama ilivyokuwa wakati wa uhai wa baba. Mara kwa mara alikuwa akiongea kwa jazba na kutufokea hata bila sababu. Kama alivyotutishia, hakuna aliyethubutu kufumbua mdomo wake na kuongea juu ya mabadiliko aliyokuwa nayo mama.

    Tukaendelea kuishi na babu na bibi. Maisha yalikuwa magumu sana kijijini kwani hatukuzoea kuishi kwa taabu. Kipindi cha nyuma, tulikuwa hatukai sana kijijini na hata tulipoenda, wazazi wetu walikuwa wakitubebea vyakula tunavyovipenda lakini safari hii, hali ilikuwa tofauti. Tulikonda na kupauka sana kutokana na ugumu wa maisha ya kijijini, likizo ilipoisha tulifurahi sana.

    Mama akaja kutuchukua na kuturudisha jijini Dar es Salaam. Kingine kilichozidi kuninyong’onyesha, ni kwamba tayari shule zilishafunguliwa lakini hakuna hata mmoja wetu aliyeenda kuanza. Tulipomuuliza mama, alituambia kuwa kuna fedha anazisubiri baada ya siku chache tutaanza masomo.

    Hata hivyo, ahadi yake haikutimia, wiki ya kwanza ikapita tukiwa nyumbani tu, hatimaye ikafika wiki ya pili. Bado mama aliendelea na tabia yake ileile ya kuondoka nyumbani asubuhi na mapema na kurejea mida mibovu akiwa ameshalewa.

    Nilipoona hakuna dalili zozote za kwenda shule, niliamua kwenda hivyohivyo. Asubuhi moja nikajiandaa na kuvaa nguo zangu za shule, nikatoka na kwenda kusubiri basi la shule. Kwa bahati nzuri halikuchelewa siku hiyo, nikapanda na kuungana na wenzangu, safari ya kwenda shuleni ikaanza.

    Wenzangu niliokuwa nasoma nao wakabaki kunishangaa huku kila mmoja akisema kwamba nilikuwa nimekonda na kuwa mweusi sana. Niliwaambia kwamba ni kwa sababu likizo yangu niliimalizia kijijini ambako kulikuwa na baridi sana.

    Safari ikaendelea mpaka shuleni, tukateremka kwenye basi la shule na kuelekea kwenye geti la kuingilia ndani. Kwa bahati mbaya, baada ya kufika getini, mlinzi alinizuia kuingia kwa maelezo kwamba alipewa orodha ya majina ya wanafunzi ambao hawaruhusiwi kuendelea na masomo mpaka watakapokamilisha malipo ya ada.

    Niliishiwa nguvu, nikajaribu kumbembeleza aniruhusu ili nikaongee na mkuu wa shule lakini ombi langu lilishindikana. Ikabidi nigeuze na kuanza kurudi nyumbani huku machozi yakinilengalenga. Roho iliniuma sana kuwaona wenzangu wakiingia darasani bila shida wakati mimi nimezuiwa.

    Kibaya zaidi, hata nilipoondoka nyumbani, sikuchukua fedha ya akiba kwani niliamini nitapelekwa na gari la shule na kurudi nalo nyumbani baada ya masomo kuisha. Nikaendelea kutembea taratibu kwenye barabara ya kutokea shuleni huku kichwa nikiwa nimekiinamisha.

    Nilitoka eneo la shule na kuingia kwenye barabara kubwa ya lami huku mawazo yakiendelea kukitesa kichwa changu kiasi cha machozi kunitoka. Kumbe wakati natembea, nilishahama upande wa watembea kwa miguu na kuingia barabarani bila mwenyewe kujijua.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikashtuka ghafla baada ya kusikia honi kali ya gari iliyofuatiwa na kelele za breki, nikajikuta nikitetemeka kupita kiasi, nikakimbia na kutoka barabarani huku mapigo ya moyo yakinienda kasi kuliko kawaida. Gari dogo la kifahari lilikuwa limesimama nyuma yangu.

    “Ooh! Maskini, pole dadaangu, siku nyingine uwe mwangalifu unapotembea barabarani, halafu mbona kama unalia? Una tatizo,” alisema kijana mtanashati baada ya kuteremsha vioo vya gari hilo dogo la kifahari. Nilishindwa kumjibu kitu kutokana na hofu niliyokuwa nayo, nikaongeza mwendo huku nikijifuta machozi.

    Cha ajabu, lile gari lililotaka kunigonga liliendelea kunifuata taratibu huku yule kijana akiendelea kunisemesha kwa upole. Nilipoona anaendelea kunifuata, nilisimama na kugeuka, nikamtazama. Akasimamisha gari na kuteremka, akaja mpaka pale nilipokuwa nimesimama.

    “Samahani kwa kutaka kukugonga lakini wewe ndiyo ulikuwa na makosa kwa kuingia barabarani,” alisema kwa upole huku akinishika begani. Nilimjibu kwa kutingisha kichwa kuonesha kukubaliana naye.

    Akaniuliza kama anaweza kunipa lifti, mwanzo nilijifanya kuvunga lakini nilipofikiria kwamba sikuwa na nauli na nyumbani ni mbali, nilimkubalia. Akanifungulia mlango wa gari na kuniambia niingie. Yeye akazunguka upande wa pili na kuingia, akakaa nyuma ya usukani.

    Taratibu akaondoa gari huku muziki laini ukiendelea kutumbuiza, sambamba na kipupwe kilichonifanya nisahau kwa muda shida zangu. Nilitulia kimya, safari ikaendelea huku mawazo yakiendelea kupita kichwani mwangu. Nilipoinua macho yangu na kuangalia kwenye kioo kilichokuwa juu ya gari, nilishangaa kugundua kuwa kijana huyo alikuwa akiniangalia kwa macho ya wizi.

    Alipogundua kuwa nimemuona, haraka alikwepesha macho yake huku akiachia tabasamu hafifu usoni mwake. Safari iliendelea huku nikianza kujihisi aibu kwani hakuna kitu nilichokuwa nakiogopa kama kutazamwa na mwanaume kwa muda mrefu.

    “Kwani unaishi wapi?” aliniuliza kijana huyo huku akibadili gia na kulifanya gari lizidi kwenda kasi. Nilimjibu kwa kifupi kwamba naishi Tabata. Na yeye aliniambia kwamba anaishi Buguruni, moyoni nikafurahi kwani nilikuwa na uhakika kwamba atanifikisha jirani kabisa na nyumbani.

    Safari iliendelea mpaka tulipofika Buguruni, nikategemea kwamba atanishusha kwa sababu yeye alishafika mwisho wa safari yake lakini haikuwa hivyo, aliniuliza mtaa ninaoishi, akanipeleka mpaka jirani kabisa na nyumbani.

    “Nashukuru sana kaka’angu, Mungu akuzidishie,” nilimwambia kwa adabu, nikafungua mlango ili nishuke. Kabla sijashuka akaniita:

    “Samahani, sidhani kama itakuwa vibaya kufahamiana, mimi naitwa Jimmy au kwa kifupi Jay sijui mwenzangu unaitwa nani,” aliniuliza huku akiwa amenikazia macho.

    “Eunice!” nilimjibu kwa kifupi, akaniambia amefurahi kunifahamu kisha akaingiza mkono mfukoni na kutoa waleti yake, akachukua ‘bussines card’ yake na kunipa akiwa ameiambatanisha na noti kadhaa za shilingi elfu kumikumi.



    Nilishtuka sana kutokana na kitendo hicho kwani sikutegemea, nikajifanya kuvungavunga lakini mwisho nikapokea. Akaniambia katika kadi hiyo kuna namba zake za simu, nikipata muda nimtafute na hizo fedha alizonipa ni kwa ajili ya kununulia vocha.

    Nilitabasamu, na yeye akafanya hivyohivyo, nikateremka na kuanza kutembea harakaharaka kuelekea nyumbani. Hakuondoka haraka, aliendelea kunitazama mpaka nilipopotea kwenye upeo wa macho yake.

    “Mbona ananiangalia sana? Halafu kwa nini amekuwa mwema kiasi hiki kwangu?” nilijiuliza huku nikizihesabu vizuri fedha alizonipa. Nilitabasamu baada ya kugundua kuwa ilikuwa ni shilingi elfu arobaini, nikaitazama vizuri na ile kadi, nikaiweka kwenye mkoba wangu wa madaftari, nikaendelea kutembea mpaka nilipofika nyumbani. Nilipoingia tu, ndugu zangu walinishangaa kwa nini nimewahi kurudi kabla ya muda wa masomo kuisha.

    Sikuficha kitu, niliwaeleza kwamba nimezuiwa kuingia shuleni kwa sababu sikuwa nimelipa ada, nikawaona wote wamenyong’onyea. Tayari mama alishaondoka kama kawaida yake, tukawa tunajadiliana wenyewe nini cha kufanya.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ina maana baba hakuacha fedha hata kidogo kwenye akaunti yake? Halafu si aliwahi kutuambia kwamba alikuwa na bima ya maisha? Inabidi tumwambie mama afuatilie ili tupate ada ya shule, masomo yanatupita,” alisema kaka yetu mkubwa, kauli ambayo wote tuliiunga mkono.

    Tukakubaliana kwamba jioni mama akirudi, lazima tuzungumze naye na kumweleza tulichokuwa tumeamua. Nilienda kuvua nguo za shule kisha nikaendelea na kazi ndogondogo za nyumbani ikiwa ni pamoja na kuanza maandalizi ya kupika chakula cha mchana.

    Wakati nikiendelea na kazi, bado taswira ya yule kijana mtanashati aliyenipa lifti wakati nikitoka shule ilikuwa ikiendelea kujirudiarudia kichwani mwangu kama mkanda wa video. Niliwaza mambo mengi sana, nikashusha pumzi ndefu nilipokumbuka fedha alizonipa wakati tukiagana.

    Niliendelea na kazi, nikapika chakula cha mchana ambapo tulijumuika sote kula kisha nikaenda kujisomea chumbani kwangu kama ilivyokuwa kawaida yangu. Hata hivyo, akili yangu haikutulia kabisa, kila nilipojitahidi kuelekeza akili yangu kwenye masomo, nilijikuta taswira ya Jimmy ikiutawala ubongo wangu.

    “Mbona namfikiria sana huyu kijana? Eeeh Mungu muepushie mbali ibilisi anayeninyemelea,” nilijisemea mwenyewe kimoyomoyo, nikaendelea kujisomea kwa kujilazimisha. Jioni ilipofika, nilianza tena maandalizi ya mapishi kwani mimi ndiyo nilikuwa msimamizi mkuu wa familia.

    Kazi zote ambazo awali zilikuwa zinafanywa na mama, sasa nilikuwa nazifanya mimi. Wakati nikiendelea na mapishi, nilisikia muungurumo wa gari nje ya nyumba yetu na muda mfupi baadaye, mama akaingia akiwa amelewa kama kawaida yake.

    Kama tulivyokuwa tumekubaliana, tulimbana mama na kutaka kuzungumza naye. Japokuwa alikuwa mgumu sana wa kukubali, tulipoonesha kuwa hatuna masihara, alikubali kwa shingo upande, akaenda kuoga kwanza kisha akarudi sebuleni huku akitafuta ‘Big G’, kaka akamueleza tulichomuitia kwa niaba yetu.

    Majibu aliyotupa yalitushangaza sana, alisema kwamba hakuna fedha zozote kwenye akaunti ya baba, pia akatuambia kwamba tayari alishafuatilia na kulipwa fedha zote ambazo ndiyo alizozitumia kama mtaji wa biashara zake. Kila mmoja aliishiwa nguvu kutokana na majibu hayo, akatuahidi kwamba wiki hiyo haitaisha kabla hajaenda kutulipia ada.

    Baada kusema hivyo, aliinuka na kuelekea chumbani kwake huku akipepesuka kutokana na pombe alizokuwa amekunywa. Tulibaki kutazamana huku kila mmoja akiwa haamini kile tulichokisikia kutoka kwa mama.

    Kengele ya hatari ililia ndani ya kichwa changu, nikajua lazima kuna mchezo mchafu ambao mama alikuwa akiucheza nyuma ya pazia. Nilishangaa sana iweje fedha zote hizo ziyeyuke ndani ya muda mfupi sana tangu kifo cha baba. Kwa uelewa wangu, nilijua kwamba wakati baba anafariki, akaunti yake ilikuwa na fedha za kutosha.

    Kama hiyo haitoshi, lazima mama alilipwa fedha nyingi sana kutokana na bima aliyokuwa nayo baba kwa sababu alikuwa ni mfanyakazi wa ngazi ya juu katika kampuni yao huku akilipwa mshahara mnono.

    “Mama ana matumizi gani ya kumaliza mamilioni yote hayo ndani ya kipindi kifupi namna hii?” nilijiuliza huku nikijaribu kutafakari mambo mengi ndani ya kichwa changu, sikupata jibu. Kwa mbali nikaanza kuona jinsi familia yetu ilivyokuwa inaelekea kwenye shimo kubwa la ufukara, roho iliniuma sana.

    Kwa kuwa sikuwa na usingizi, nilienda kumuomba kaka yangu simu, nikarudi nayo chumbani ambapo nilifungua mkoba wangu wa madaftari na kuchukua ile kadi ya mawasiliano niliyopewa na Jimmy, nikaandika namba kwenye simu na kumpigia.

    Alipokea haraka na kuniuliza mimi ni nani, nilipojitambulisha, nilimsikia akicheka kwa furaha, akaniambia nikate simu anipigie yeye. Sekunde chache baadaye, akanipigia, tukaanza kuzungumza.

    “Vipi bado hujalala mpaka muda huu,” aliniuliza Jimmy kwa sauti iliyotulia, nikamdanganya kwamba nilikuwa najisomea ndiyo maana nilichelewa kulala. Tulizungumza mambo ya kawaida, Jimmy akanichangamkia sana mpaka nikafurahi.

    Sikusita kumshukuru tena kwa fedha alizonipa siku hiyo. Akaniambia nisijali hilo ni jambo dogo kwake, pia aliniuliuza kama hiyo simu niliyokuwa naitumia ni ya kwangu. Nikamjibu kwamba nimeazima kwa kaka yangu kwa sababu mimi sikuwa na simu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Usijali, kesho nitaenda kukununulia simu nzuri kwa ajili yako, nikikupigia mchana uje pale nilipokushusha leo,” alisema Jimmy, kauli iliyoongeza furaha kwenye moyo wangu. Tukaagana kisha akakata simu, nikabaki nachekacheka mwenyewe.



    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog