Search This Blog

Thursday, July 21, 2022

NILIISHI DUNIA YA PEKE YANGU - 5

 







    Simulizi : Niliishi Dunia Ya Peke Yangu

    Sehemu Ya Tano (5)



    “Uone nini? Wakati wewe ndiye uliyemtafutia balaa hili. Kama angeendelea kufanya kazi kwenye magari ya watu haya yasingemkuta.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Hata mkisema nini bado siwezi kukubali hali hii iendelee.” “Mchukue na akifa utamla nyama,” baba aliendeleza malumbano. “Sawa, lakini Mungu ndiye anayejua kila kitu.” “Kuanzia sasa hivi sisi hatushughuliki na mumeo, elewa kuanzia sasa hivi atakuwa wako, akifa utajua ufanye nini, umle nyama au umzike.” “Hata msemeje lazima nimpeleke hospitali na Mungu atanitangulia kwa hili.” “Sawa, lakini sisi tena hatumo.” “Sawa, naondoka, kesho nitakuja kumchukua nimpeleke hospitali.” “Utajua utakavyofanya lakini sisi hatumo tena.” “Baba Victor hebu kwanza punguza hasira umsikilize mkweo,” mama mkwe aliingilia kati. “Nimemaliza na wewe ukiingia katika mkumbo huo utaondoka hapa, kwanza ingia ndani, huoni mtoto huyu mwanga anataka kumtoa karafa mwanangu?” Baba mkwe alikuwa mkali sana kitu kilichonishangaza na kujiuliza ana ajenda gani na ugonjwa wa mume wangu. Walitoka na kuniacha peke yangu chumbani kwa mume wangu ambaye alikuwa bado ana maumivu makali. Nilimlaza vizuri kisha nilizima taa na kufunga mlango kisha nikaondoka zangu huku nikiwa nimechanganyikiwa, mtoto wa kike ambaye kila kukicha niliiona dunia ikinitenga kama ilifikia hatua ya kususiwa mgonjwa. Nilijiuliza kama mgonjwa atanifia mikononi mwangu nitamfanyaje ikiwa wazazi wake tayari wamenisusia kwa sababu tu nataka kumpeleka hospitali. Nilitembea huku nikilia kilio cha sauti ya chini na kujiona kiumbe niliyekosa thamani katika dunia ambayo niliamini naishi kwa bahati mbaya. Kutokana na kuchanganyikiwa na matatizo mazito yaliyokuwa kichwani mwangu, nilijikuta nimefika kwa Azizi Ali bila kujitambua. Kama nisingeshtuka naona ningefika hata Mivinjeni, kwani nilishtukia naukabiria ukumbi wa Ikweta. Nilirudi na kuelekea hospitali, sikuwa na haja ya kupanda tena gari kwani nilikuwa nimekaribia kufika. Nilikwenda hadi hospitali wakati huo muda ulikuwa umekwenda sana hata sikujua ni saa ngapi. Nilipofika getini mlinzi alitaka kunikatalia kuingia, nilimwelewesha hivyo akaniruhusu kuingia. Nilikwenda hadi wodini na kufika kwenye kitanda alicholala mwanangu, nilimkuta yupo kama nilivyomuacha. Kutokana na kutembea sana nilikuwa nimeloa jasho chapachapa. Nilitoka nje kwenye upepo ili kupunguza jasho, mwili wote ulikuwa ukiniuma na sehemu za mapaja zilikuwa zimechubuka na kunifanya nitembee kwa shida. Baada ya kupunga upepo nilirudi ndani na kukaa pembeni ya kitanda cha mwanangu aliyekuwa bado amelala. Nilitaka kumgeuza mtoto baada ya kumwona amelala upande mmoja kwa muda mrefu. Nilipomshika nimgeuze nilishangaa kumuona mtoto akigeuka mzimamzima kitu kilichonishtua. Alipomwangalia hakuwa kwenye hali ya kawaida alikuwa ametulia kama mtu aliyelala lakini mwili wake ulikuwa umepoteza joto la kawaida. Nilimtikisa Fatuma huku nikimwita, lakini hakuonesha kushtuka. Kitu kile kilinishtua sana na kutaka msaada wa jirani yangu ambaye alikuwa amepitiwa na usingizi. “Dada...dada,” nilimwita dada wa kitanda cha pili. “Vipi mama Fatu?” aliniuliza dada mwingine aliyekuwa macho akimbadili nguo mwanaye. “Mbona mwanangu simwelewi?” “Kwani vipi?” alimwacha mwanaye bila kummalizia kumfunga nguo na kuja kitandani kwangu. “Hebu mtazame,” nilimwonesha mwanangu alikuwa amelala.

    Alimwangalia kwa muda huku akimpima sehemu za kifuani kisha alinieleza: “Mfuate daktari mwanao atakuwa na tatizo tu.” Nilielekea ofisi ya madaktari na kumkuta daktari amejilaza kwenye kiti kajifunika koti lake miguuni kuzuia mbu. “Dokta...dokta.” “Eeh...vipi?” alishtuka usingizini. “Kuna tatizo,” nilimweleza kwa sauti iliyohitaji msaada wake. ”Tatizo gani?” “Mwanangu.” “Mwanao amefanya nini?” “Hata simwelewi.” “Tangulia nakuja.” Niligeuka na kurudi kwenye kitanda cha mwanangu na kukuta asilimia kubwa ya kina mama mule ndani wameamka na kusogea karibu ya kitanda changu.” “Daktari yupo wapi?” aliniuliza dada niliyemwacha kitandani.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Upasuaji ulikwenda vizuri na mume wangu baada ya siku kadhaa alitoka hospitali. Kwa kweli mume wangu alikuwa na mabadiliko makubwa miguu yake ilirudi katika hali ya kawaida lakini mkono ulibakia vilevile katika hali ya kusinyaa. Nilimshukuru Mungu kwa kumponya kitu kimoja katika magonjwa yake ambayo yalikuwa yakitishia amani ya moyo wangu.

    Kwa vile vitu vya dukani vilikuwa vimebaki vichache, niliamua kuviuza kwa bei ya kutupa na kufunga duka nikaanza kuishi kwa kumtegemea Mungu kwa vile sikuwa na chanzo cha fedha cha uhakika tena. Niliendelea kumshukuru shoga yangu Salome aliyehakikisha kunipatia kidogo alichopata katika mihangaiko yake.

    Hata majirani nilioishinao vizuri walijikusanya na kunipa kiasi cha fedha kwa ajili ya kujikimu kimaisha. Kwa kweli moyo wangu ulikata tamaa baada ya kuamini kuwa sitaweza tena kunyanyuka hata hatua moja kwenda mbele. Wazazi wa mume wangu baada ya kuona sina ujanja wa kuyaendesha maisha kutokana na kufunga duka, waliona ni heri wanipunguzie majukumu kwa kumchukua mume wangu na kwenda kuishi naye na kuniacha na mwanangu ambaye alikuwa na bahati mbaya kuishi maisha ya kubahatisha kwani kila kukicha ilikuwa ni afadhali ya jana.

    Siku mbili baada ya kuondoka kwa mume wangu nilikaa ndani peke yangu na kuanza kulia huku nikimuuliza Mungu mimi ni kiumbe wa dunia gani. “Eeh, Mungu mimi ni kiumbe wa dunia gani? Kosa langu kubwa nililokutendea ni lipi? Ni laana? Hata kama ni laana ya mama yangu kubeba mimba ya nje ya ndoa, mimi kosa langu nini? Eeh! Mungu nimlilie Mungu gani atakayesikia kilio changu na kuyaona mateso yangu.

    “Haya ni maisha gani jamani mimi? Heri unichukue nikapumzike kuliko kuendelea kuteseka hivi. “Kwa nini kifo hakinichukui kwani nimekikosea nini? Kwa nini hakinichukui? Ni heri kifo kinichukue, kwa nini wasiotaka kufa kinawasikiliza, miye ninayekihitaji kinanikimbia kila siku? Hebu kifo nichukue nami nikapumzike. Hii siyo dunia yangu, maisha ninayoishi nina amini naishi dunia ya peke yangu. Nimekuwa nacheka kwa bahati mbaya lakini kilio ndiyo maisha yangu ya kila siku.

    “Hapana...hapana..hapana...nataka leo nipate jibu naishi dunia ya nani? Najua sitakiwi duniani kwa nini kifo hutaki nife. Vitabu vitakatifu vinasema mtoto hawezi kuhukumiwa kwa dhambi ya mzazi wake, kwa nini nihukumiwe kama kosa kalifanya mama yangu?”

    Kwa kweli nililia kwa sauti mpaka ikanikauka, kichwa kiliniuma na kutaka kupasuka, macho nayo yalivimba nusura yazibe. Wazo la haraka lilikuwa ni kujinyonga, Nilijinyanyua nilipokuwa nimepiga magoti na kwenda hadi jikoni na kuchukua kisu kikubwa ili nijiue. Maumivu ya kisu yalinitisha na kuona nitakufa kwa mateso makubwa, pia niliio na kama ni njia ndefu sana.

    Wazo la kwenda kununua sumu sikuweza kulitekeleza japokuwa ndiyo njia ya kimyakimya. Lakini ningetoka watu wangenishangaa hali niliyokuwa nayo. Niliona njia nyepesi ilikuwa ni kujinyonga kwa kamba. Nilichukua kamba ya kuanikia nguo na kuifunga kwenye feni, kisha nilisogeza sturi na kujivisha shingoni. Nikaanza kumuomba Mungu anipokee huko niendako kwa kuamini ndipo sehemu yangu sahihi.

    Kabla sijajifyatua kitanzi, mwanangu aliyekuwa amelala kitandani alishtuka na kuanza kulia. Nilishtuka na kujishangaa kama nina mtoto, wakati nilipokuwa nikipanga yote hayo wazo la kuwa na mtoto sikuwanalo kabisa, nina imani kama asingelia ningekufa na kumuacha amelala.

    Nilitulia nikimuangalia mwanangu aliyekuwa akilia huku akijipindua kitandani kama aliyeumwa na kitu. Wazo la kujinyonga nilikuwa nalo, lakini huruma ikawa kwa mtoto, nilihofia kufa na kumuacha akiwa yatima. Wazo lingine lililonijia ni kuanza kumnyonga mwanangu kisha nijimalizie miye. Niliteremka na kumfuata kitandani alipokuwa amelala, nilimnyanyua na kumbembeleza anyamaze, baada ya kufanikiwa, nilimbeba hadi juu kwenye sturi ili nimtundike.

    Mwanangu muda wote alikuwa akicheka huku akiniita.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Sikumjibu, niliinama chini bila kumwambia neno lolote, lakini Salome aliendelea kuniuliza kwa sauti ya uchungu. Niliamini kilichomshtusha kilikuwa kitanzi nilichokiandaa kwa ajili ya kujinyonga. “Ester shoga yangu, unataka kufanya nini, kipi cha ajabu ulichokipata mpaka utake kujiua. Unajua Mungu kakupangia nini katika maisha yako mpaka unataka kukatisha

    maisha yako? Kwa nini unataka kujiua hujui kufa ni lazima kwa nini unalazimisha kifo? Kwa nini unaiingilia kazi ya Mungu?”

    “SAMAHANI shoga yangu,” nilijikuta nakiteremka kwenye kochi na kumpigia magoti Salome baada ya kuona nimemuumiza sana kwa kitendo changu cha kutaka kukatisha uhai wangu. “Ester, mimi si wa kuombwa msamaha bali muombe Bwana Mungu wako akusamehe, pia akujaze moyo wa ujasiri wa kukabiliana na matatizo.” “Nakuahidi mbele ya muumba wa ardhi na mbingu sitarudia tena kujaribu kujiua, nilikuwa na wazo baya Salome nilitaka kumuua na Fatuma.”

    “Mungu wangu! Na Fatuma?” “Ndiyo, nimechanganyikiwa rafiki yangu.” “Tena nikitoka hapa naondoka naye kama unaendeleza ujinga wako kufa peke yako, unataka kuniulia mwanangu kakosa nini?” “Ndiye aliyefanya niache kujiua, niliamini hana kosa, bila ya yeye ungekuta mzoga unaning?inia.” “Ester rafiki yangu iko siku utasahau yote haya.” “Nitasahau kwa vipi, hebu angalia afya ya mume wangu haina mabadiliko, lini na mimi nitacheka kama wengine?”

    “Utacheka tu Ester, ipo siku utacheka na kusahau kama ulipitia matatizo na kumueleza mtu kama historia iliyokuumiza.” “Hakuna..nakataa kitu hicho, hakitatokea labda jua litoke magharibi kwenda mashariki.” “Wewee Ester hebu temea mate chini, iko siku nitakusuta.” “Labda uje kunisuta kwenye kaburi langu.” “Nakuhakikishia kuwa hakuna mateso ya milele.” “Kwa wengine lakini si kwangu, naamini hivyo, mateso yangu ni ya milele, nimezaliwa nayo na nitakufa nayo.”

    “Nakuomba muepuke shetani si rafiki mzuri, yupo kwa ajili ya kuwakatisha watu tamaa na mwisho kuingia katika chukizo la Mungu na kuangukia katika moto wa milele.” “Nitajitahidi, lakini nakuahidi nilichotaka kukifanya leo naomba Mungu anisamehe, sitarudia tena hata niteseke vipi, sitayadhurumu maisha yangu,” nilijiapiza mbele ya shoga yangu. “Nimefurahi kusikia hivyo rafiki yangu, nitapigana nawe mpaka muda wako wa mwisho, najua umenitoa wapi na mimi leo mtu mbele ya watu, sitakuacha kamwe.”

    Salome aliyasema maneno yale huku akitokwa na machozi akiwa amenikumbatia, nami nilijikuta nikiamsha kilio upya baada ya kuamini nifanyayo hayampendezi Mungu. Siku ile Salome alikuwa ameniletea fedha kidogo za matumizi, pia alishinda kwangu kuhakikisha ananirudisha katika hali ya kawaida.

    Pamoja na maumivu ya moyo nilijikuta nikiyasahau na kucheka, kweli Mungu wa ajabu sana. Jioni ilipofika Salome alinichukua na kwenda nyumbani kwake kukaa naye kwa muda wa wiki

    nzima ili kutuliza akili yangu. Pamoja na kukaa kwake bado alipoteza muda wake mwingi kuhakikisha tunakwenda pamoja kwa mume wangu angalau mara moja kwa wiki kumpelekea mahitaji muhimu kama sukari, sabuni na mahitaji mengine madogomadogo.

    Nilimshukuru mume wa Salome kwa ubinaadamu na muda mwingi aliutumia kunisii niachane na mawazo mabaya ya kutaka kujiua, nami nilimhakikishia sitafanya kitendo chochote cha kuyadhuru maisha yangu hata kama nitateseka kiasi gani. Siku moja nilipokwenda kumtembelea mume wangu tukiwa tumekaa alinieleza kitu ambacho kilinitoa machozi.

    Kilichinishangaza, hali ya mume wangu ya kujikunja kila wakati au kukunja uso kuonesha ana maumivu makali iliniumiza sana. “Vipi mume wangu?” Nilimuuliza. “Tumbo.” “Tumbo, limekuwaje tena jamani?” “Huwezi kuamini wiki sasa silali, usiku tumbo linaniuma kama vile kwa ndani kuna kidonda kibichi.” “Mmh! Au ule upasuaji?”

    “Hata mimi nawaza hivyo.” “Umewaelezea wazazi?” “Wee acha tu, kila kitu nimerogwa, nimewaeleza wanipeleke hospitali lakini wamekaa kila siku kunipa dawa za kunywa lakini hakuna mabadiliko yoyote zaidi ya kuteseka, heri nife kuliko mateso haya.”

    ILIPOISHIA;

    Wakwe zangu nao walikuja kunijulia hali na kunieleza hali ya mume wangu, walinifahamisha kuwa aliendelea vizuri lakini sikuwaamini. Nilijikuta nikiwa na hamu ya kumuona mume wangu nijue hali yake lakini sikuwa na mtu wa kumuachia mwanangu pale hospitali. Wakati nikisubiri vipimo, dawa alizopewa kwa wakati ule zilimwezesha kula kidogo japokuwa choo kilipatikana kwa shida lakini kulikuwa na mabadiliko madogo yenye kutia matumaini.

    SASA ENDELEA...

    Ilikuwa ni Jumapili saa mbili baada ya mwanangu kupitiwa na usingizi, nilijikuta nikiwa na hamu ya kwenda kumuona mume wangu ambaye nilikuwa sijamuona zaidi ya mwezi mmoja na nusu. Moyo

    wangu siku hiyo ulinisukasuka sana nikawa na hamu kubwa ya kumuona mume wangu. Niliamini kama nitaondoka muda ule ningeweza kwenda hadi Mtoni Kijichi na kurudi kabla mwanangu hajaamka. Kulikuwepo na dada mmoja aliyekuwa amelazwa na mwanaye kitanda cha jirani, nilimuomba anitazamie mwanangu kwa kuamini kwamba Fatuma anapokuwa amekula huwa hasumbui. “Samahani dada yangu naomba unitazamie mwanangu nafika dukani.” “Hakuna tatizo.” Nilimtengeneza vizuri mwanangu aliyekuwa kwenye usingizi mzito, baada ya kumuweka vizuri nilitoka nje ya hospitali na kupanda daladala la Mbagala na kuteremkia Msikitini ili nikatize kwa miguu japokuwa njia kama zile kwa usiku huwa si nzuri sana kutokana na kuwa na wahuni. Baada ya kuteremka nilitembea kwa mwendo wa kasi kukatiza mpaka barabara kubwa ya kutokea Mbagala Misheni. Nilitembea kwa mwendo wa kasi kidogo muda ule bado watu walikuwa wengi barabarani. Nilichukua dakika ishirini kutoka maeneo ya hospitali ya Buruda mpaka nyumbani kwa wakwe zangu. Nilikuta wameshafunga milango na kulala, kwa kuwa nyumba ilikuwa imezimwa taa. Niligonga hodi chumba cha wakwe zangu, japokuwa haikuwa heshima kufanya hivyo katika chumba cha wakwe hasa usiku kama ule, kwa kuwa wanaweza kuwa katika starehe zao. Lakini sikuwa na jinsi niligonga mlango na sauti kutoka ndani iliuliza: “Nani?” ilikuwa sauti ya baba mkwe. “Mimi baba,” nilijitambulisha. “Wewe nani?” “Mimi mama Fatuma.” “Mama Fatu! Mbona usiku hivi, kuna usalama?” “Upo baba, nimekuja kumuona mume wangu.” Baada ya muda walitoka nje huku wakionesha kwamba walikuwa bado hawajalala kutokana na nguo walizokuwa wamevaa. “Vipi mama kuna usalama?” Mama mkwe aliniuliza. “Upo mama,” niliwatoa wasiwasi. “Mbona usiku?” baba mkwe alirudia swali la awali. “Nimejikuta siwezi kuipitisha siku ya leo bila kumuona mume wangu.” “Na mwanao umemuachia nani?” “Kuna dada jirani yangu nimemuachia.” “Sasa mbona usiku mwenzio amelala, kama ujuavyo usiku kwake adhabu,” baba mkwe aliniambia. “Wazazi wangu, nini mwisho wa mateso ya mume wangu?” “Sisi siyo Mungu tunayejua hatima ya mwanadamu,” alijibu baba mkwe. “Basi naomba nimuone.” “Akiamka nani atapata kazi ya kumtuliza alale?” “Nitamtuliza mimi,” nilijibu kwa kujiamini. Nilikwenda kwenye chumba cha mume wangu na kufungua mlango kwa kuwa haukuwa ukifungwa kwa ndani. Niliusukuma na kuingia, ndani kulikuwa na kiza kizito, hivyo ilikuwa vigumu kumuona mgonjwa. “Jamani naomba kiberiti,” nilisema. “Kimekwisha,” alijibu mama mkwe.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Nilitoka kwenda dukani kununua kiberiti na kuelezwa ninunue na mafuta ya taa kwani kandili haikuwa na mafuta. Nilichukua chupa na kwenda kununua niliporudi niliweka mafuta kwenye kandili na kuiwasha. Mume wangu kweli alikuwa amelala lakini alikuwa akigugumia kwa maumivu. Alikuwa anazidi kuisha kitu kilichoonesha kwamba alikuwa akisubiri kifo tu. “Wazazi wangu hivi mnasubiri nini kwa mume wangu?” Niliwauliza kwa uchungu. “Tusubiri nini wakati anaendelea kutumia dawa?” “Naomba mume wangu apelekwe hospitali,” nilijikuta nikitoa amri bila kujielewa. “Kama unaweza mpeleke mwenyewe,” baba mkweli alinijibu kwa hasira. “Nitampeleka, hamuwezi kuniulia mume wangu huku nikiona,” maneno ya hasira yalizidi kunitoka. “Uone nini?

    ILIPOISHIA;

    “Tangulia nakuja.” Niligeuka na kurudi kwenye kitanda cha mwanangu na kukuta asilimia kubwa ya kina mama mle ndani wameamka na kusogea karibu ya kitanda changu.” “Daktari yupo wapi?” aliniuliza dada niliyemuacha kitandani. SASA ENDELEA...

    “Anakuja,” nilisogea kwenye kitanda cha mwanangu ambaye alikuwa ametulia kama nilivyomuacha bila kujigeuza. “Hebu jamani tupeni nafasi,” daktari alifika kwenye kitanda na baadhi ya kina mama waliokuwa wamesimama karibu na kitanda walisogea pembeni kumuacha daktari afanye kazi yake. “Samahani naomba kila mmoja arudi sehemu yake,” daktari alisema huku akianza kumuangalia mwanangu. Nilimuona akimpima mapigo ya moyo kisha alimkandamiza sehemu za kifuani kwa muda kisha aliushika mkono wa mwanangu na kuuminya kwa muda kisha alirudia tena kumpima mapigo ya moyo. Wakati huo wenzangu wote walikuwa macho wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea kitandani kwa mwanangu. Ilionekana hata waliokuwa wamelala waliamshwa na majirani zao wote walikuwa wakiangalia kitandani kwangu. Baada ya kufanya vipimo vya muda mrefu aliniangalia na kutaka kuniambia kitu lakini kwanza alizungumza na muuguzi aliyekuwa pembeni yake kwa kunong’ona kisha aliniambia huku akijifuta jasho kwa koti alilovaa. “Samahani njoo ofisini.” Nilimfuata bila kuzungumza lolote huku nikijiliza mbona amemuacha bila kufanya kitu chochote. Nilipofika ofisini alinieleza nikae kwenye kiti cha wageni nami nilitii amri. “Mumeo yupo?” “Ndiyo.”

    “Tunaweza kumpigia simu sasa hivi?” “Hana simu pia anaumwa sana yupo kwa wazazi wake.” “Ndugu zako?” “Sina.” “Unaishi na nani?” “Nilikuwa naishi na mume wangu ambaye kwa sasa hivi ni mgonjwa sana.” “Ndugu wengine?” “Sina ila nina shoga yangu anayeishi Gongo la Mboto.” “Tunaweza kupata namba zake za simu?” “Dokta kwani kuna nini mbona unaniuliza maswali hayo?” “Utajua muda si mrefu.” “Kwani mwanangu amefanya nini? Amekufa?” “Hapana.” “Si kweli, kuna kitu unanificha hebu niambie, si hali ya kawaida lazima mwanangu atakuwa amekufa,” nikaingiwa na wasiwasi kutokana na mazingira yote niliyoyaona. “Dada hebu nipe namba za shoga yako.” Sikutaka kubishana naye nilimpa, baada ya kumpa alitoka nje na kuniacha nimekaa kwenye kiti nikijiuliza kuna nini mbona amechukua namba ya Salome na kutoka nje. Baada ya muda alirudi na kunikuta nikiwa bado nimekaa kwenye kiti. “Ester.” “Abee.” “Naomba nikueleze kitu ambacho najua kitakuumiza.” “Sidhani,” nilijibu kwa kujiamini kwa kuamini sikutakiwa kushtuka kwa lolote litakalokuja mbele yangu. “Bahati mbaya mwanao hatunaye.” “Eeeh!” nilishtuka. “Mwanao hatunaye,” alirudia alichonieleza. “Sijakuelewa hatunaye ndiyo nini?” Nilikuwa nimemsikia lakini sikumuelewa. “Vipimo vinaonekana amefariki muda mrefu kidogo, bila wewe mama yake kujua kwa kuamini amelala.” “Ooh!” Nilishusha pumzi ndefu na kuinama chini kwa muda huku machozi yakifuatia. Nilinyanyua mikono juu na kumshukuru Mungu kwa kusema kwa lugha ya kiarabu japo sikuwa Muislam: “Alhamdulilah,” nilifuta mikono usoni na kufuta machozi kwa upande wa khanga niliyokuwa nimejitanda na kumtazama daktari aliyekuwa akinitazama kwa macho ya huruma. “Pole sana.” “Asante,” nilijibu huku nikishindana na machungu mazito moyoni yaliyonitaka nipige kelele lakini moyoni nilijiuliza nitalia mpaka lini kwa vile matatizo yaligeuka utamaduni wa maisha yangu. “Umesema na mumeo anaumwa sana?” “Ndiyo, hata yeye nikisikia amekufa siwezi kushangaa.” “Ooh! Pole sana anaumwa nini?” “Sijajua ila alifanyiwa upasuaji wa kunyoosha utumbo.” “Sasa tatizo ni nini?” “Wazazi wa mume wangu wanajua.” “Kuna watu wengine wanaotakiwa kupelekewa taarifa?”

    “Wakwe zangu ambao hawana simu, shemeji yangu kaka wa mume wangu yupo Temeke Mikoroshini Magenge Mapya.” “Namba yake unayo?” “Ndiyo.” Nilimpa namba ya shemeji ambaye alimpigia nikiwa palepale na kumjulisha msiba wa mwanangu Fatuma mwenye jina la mama yangu mzazi aliyekuwa naye ametangulia mbele ya haki. Baada ya kumaliza kumjulisha shemeji ambaye alisema angefika hospitali usiku ule, nilimuuliza daktari nini kiliendelea.

    “Dokta nini kinaendelea?” “Ndugu zako na jamaa watafika muda si mrefu..” Kabla hajamalizia Salome na mumewe waliingia kuonesha baada ya taarifa hawakuchelewa kuja kwenye tukio. Salome aliponiona alinikumbatia na kuanza kulia kitu ambacho kwa upande wangu sikutaka kulia zaidi ya kumshukuru Mungu.

    Kilio cha Salome kilinifanya nami nilie kwa uchungu lakini nilinyamaza baada ya kuja shemeji aliyetubembeleza ili tujue tutafanya nini. Shemeji alisema msiba utakuwa Mtoni Kijichi ukweni. Sikuwa na pingamizi kwa vile nilikuwa muolewaji.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Majira ya saa kumi na moja alfajiri tulianza safari ya kwenda Mtoni Kijichi huku moyoni nikijiuliza taarifa za msiba wa mtoto mume wangu atazipokeaje. Nilipofika tulipokelewa na kilio kilianguliwa upya, pamoja na uchungu wa kifo cha mwanangu kipenzi ambaye nilimuona kama mama yangu mzazi, bado wasiwasi wangu mkubwa ulikuwa kwa mume wangu pamoja na hali yake, taarifa za kifo cha mwanaye angezipokeaje.

    Mipango ya mazishi ilipangwa na kukubaliana mwanangu azikwe saa saba mchana kwenye makaburi ya kifamilia yaliyokuwa kwenye shamba la wazazi wa mume wangu. Baada ya mazishi nikiwa chumbani nilifuatwa na shemeji yangu baada ya kusogea karibu yangu alininong?oneza: “Hali ya mwenzio siyo nzuri hata kidogo.” “Nini tena?” Nilishtuka.

    “Kumbe wakati watu wanalia mume wangu alijinyanyua na kutoka nje na kuulizia msiba wa nani, aliyemjibu hakumjua alimweleza ukweli, hapo ndipo aliposhtuka na kuanguka na kupoteza fahamu. Mpaka muda huu fahamu zake hazijarudi kitu ambacho kimetuchanganya.” “Huu ni mwaka wangu,” nilijibu kwa sauti ya chini nikipata jibu la lile nililowaza kabla ya kuuleta msiba wa mwanangu ukweni kuhofia hali ya mume wangu.

    “Sasa itakuwaje?” nilimuuliza nikiwa nimechanganyikiwa. “Watu wamefuata gari ili wamuwahishe hospitali.” “Mungu wangu, lazima niende na mume wangu.” “Hapana wacha nimpeleke mimi, wewe mfiwa tulia,” shemeji alinibembeleza lakini sikukubali.

    Gari lilipofika nilitoka ili niingie, watu walinisihi nisiende kwa vile mimi ndiye mfiwa, lakini sikuwa tayari kuwasikiliza. Niliingia ndani ya gari na kumpakata mume wangu aliyekuwa ametulia kama mtu aliyepoteza uhai. Gari lilikwenda kwa mwendo wa kasi kutokana na hali yake tulikwenda moja kwa moja Muhimbili. Tulipofika tulipelekwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi, baada ya kufanyiwa vipimo ilibidi awekewe mashine ya kupumulia kutokana na mapigo yake ya moyo kuwa ya chini sana. Nilikaa nje ya wodi ya wagonjwa mahututi na shemeji yangu kwa kuw watu wengine waliamua kuondoka.

    Salome na majirani nao walitoka msibani na kunifuta hopsitali na kunikuta nimekaa kwenye msingi nikiwa nimejishika tama huku machozi yakikosa kizuizi na kujiuliza ina maana napoteza watu wawili kwa mpigo. Salome na majirani zangu walinifariji kwa maneno ya kunipa moyo. Niliwakubalia kiungwana tu lakini moyo wangu ulikuwa kwenye wakati mgumu, kila dakika nilijitahidi kushindana na hali iliyotaka kunijia mbele yangu. Japo sikuwa na uhakika Mungu gani ninayemuomba, niliomba tena kuomba huruma yake. *** Sikurudi tena ukweni, nilikaa nje ya wodi aliyolazwa mume wangu kwa siku mbili huku hali yake ikiwa haina mabadiliko yoyote. Nilipoingia ndani ya wadi kumtazama hakuonesha mabadiliko yoyote zaidi ya mitambo kuendelea kufanya kazi. Shoga yangu na majirani waliniomba nikalale nyumbani kwani hata kama nitaruhusiwa kulala kitanda kimoja na mgonjwa kama kufa atakufa tu.

    Pamoja na maneno yao sikuwa tayari kuwa mbali na mume wangu, walikubaliana kuniacha huku wakijipangia zamu ya kuniletea chakula. Usiku nililala kwenye mabenchi ya pale hospitali na asubuhi nilikaa nje ya I.C.U. Siku ya nne nilipewa taarifa ambazo zilikuwa pigo lingine maishani mwangu kwamba mume wangu kipenzi Victor amefariki dunia alfajiri ya siku ile. Najua kisa changu kama mchezo wa kuigiza ambao unasikitisha sana, mtu kutokewa na misiba miwili ndani ya siku nne.

    Niliendelea kumshukuru Mungu na kuyakumbuka maneno ya marehemu bibi yangu kila kitu ni mapenzi ya Mungu. Mume wangu naye tulimzika siku ya pili pembeni ya kaburi la mwanaye, baada ya misiba ile nilikuwa kama mtu niliyechanganyikiwa, nisiyejua nifanye nini.

    Moyo wangu ulikufa ganzi na kuyaona yote yaliyotokea kuwa ni ya kawaida. Kwangu ilikuwa ajabu baada ya kusikia mume wangu amefariki nilishukuru tena na kukaa kimya.

    Baada ya kifo cha mume wangu nilikaa nikiwa kama zuzu, kuna kipindi niliwasikia majirani zangu wakiniteta kwa kusema kuwa nimechanganyikiwa kutokana na kuzungumza peke yangu. Sikuwashangaa kwa wao kuamini kuwa nimechanganyikiwa kwa kuzungumza peke yangu au kukaa peke yangu nikiwa nimehama kimawazo. Salome naye alikuwa na wasiwasi baada ya vifo vile mfululizo alihisi naweza kujinyonga, lakini moyoni mwangu sikuwa tena na wazo la kujinyonga au kunywa sumu niliamua kusubiri Mungu alichokipanga mbele yangu.

    Niliamini nilikuwa nakilazimisha kifo wakati hakikunihitaji kwa muda ule. Niliyakumbuka maneno ya marehemu bibi kuwa kila mwanadamu hufa kwa ahadi hata waliofanikiwa kujiua, basi nao ahadi yao huwa imefika.

    Nilihamia kwa Salome ambaye pamoja na mumewe waliniomba nipumzike kwa zaidi ya miezi mitatu kabla ya kuanza kujishughulisha na kitu chochote. Chumba cha Temeke nikirudisha na kuhamia Gongo la Mboto na kukaa nyumba moja na rafiki yangu ambaye ndiye aliyegeuka kuwa ndugu wa damu. Niliyaanza maisha mapya ya kukaa chini ya mtu bila kujua nini kinafuata mbele yangu. Wasiwasi wangu ukawa kwa ninayemtegemea kama naye akipatwa na matatizo nitaishije. Nilipanga nitoroke niende sehemu yoyote ili kutomtia kwenye matatizo. Kwa kweli kipindi chote cha kukaa bila kazi kilikuwa mzigo mkubwa sana kwangu, nilitamani angalau nifanye shughuli yoyote ili kuniweka bize kutokana na kuwa mtu wa mawazo kila nilipokuwa peke yangu kitu kilichofanya nilie kila siku. Salome na mume wake walishauriana na kukubaliana baada ya wiki mbili nianze biashara yetu ya zamani ya kukopesha khanga, nguo za kike na vipodozi. Niliwakubalia na kusubiri kuanza hiyo biashara, Salome ambaye alikuwa mwenyeji maeneo yale alinitambulisha kwa baadhi ya wateja. Baada ya kupewa mtaji mdogo na mume wa shoga yangu niliingia mjini kununua vitu na kurudi navyo. Nilianza kazi mara moja ya kuzunguka kwa majirani kutembeza khanga, nguo za kike na vipodozi. Nilimshukuru Mungu kwa muda mfupi nilizoeleka kwa vile nilikuwa mcheshi kwa kila mtu, kitu kilichoifanya biashara yangu kuwa rahisi. Siku zote biashara tabasamu na ucheshi. Japokuwa hali yangu kidogo ilianza kubadilika huku Salome na mumewe wakinilea kama mtoto mdogo kuhakikisha sipati maudhi ambayo yataniweka katika mawazo ya kunikumbusha yaliyopita. Siku zilikatika huku nikitatizwa na mwenendo wa shoga yangu ambaye alionekana kama amebadili dini, mwenendo wake ulinishtua sana. Baada ya kutatizwa na mwenendo wa shoga yangu niliamua kumuuliza: “Shoga unajua sikuelewi?” “Kivipi shoga?” “Siyo yule Salome niliyemzoea.” “Kivipi?” “Kwanza naomba kujua shem ni dini gani?” “Muislam, ina maana ulikuwa hujui?” “Walaa nilijua shem ni Mkristo, mmh! Sasa nimeelewa.” “Umeelewa nini?” “Inaonesha wazi nawe umebadili dini?” “Ni kweli, shemeji yako alikuwa Mkristo mwanzo alikuwa akiitwa Paulo, lakini bosi wake ni Muislam na asilimia kubwa wafanyakazi wake ni Waislam. Kutokana na maelezo yake muda mrefu alikuwa akiifuatilia mihadhara ya Kiislam na kuvutiwa na vitu vilivyokuwa vikizungumzwa na kuyafanyia kazi. Baada ya kuupata ukweli alijikuta kwa hiyari yake mwenyewe bila kulazimishwa na mtu akabadili dini na sasa anaitwa Swamadu.” “Wewe ulipokeaje?” “Kwanza nilishtuka na kumuomba kila mmoja abakie na dini anayoipenda.” “Ikawaje?”

    “Hakunikatalia lakini aliniweka chini na kunieleza dini yake mpya ilivyo. Amini kuna vitu nilikuwa sivielewi lakini aliniambia kwa ufasaha nami kwa hiyari yangu nikakubaliana naye kubadili dini. Basi shoga nikatiwa maji na kupewa jina la Ilham.” “Mmh! Makubwa, sasa mbona nilikuwa nakuita Salome ulikuwa ukiitika?” “Sikutaka kukuchanganya, nilipanga siku moja nikueleze kila kitu na baada ya kusilimu tulifunga ndoa ya Kiislam.” “Siamini Salome unabadili dini unaolewa bila kuniambia?

    Kwa kweli pamoja na kunifanyia mambo mengi mazuri lakini kufichwa kule kuliniumiza sana. “Shoga nisamehe kwa hili, harusi yenyewe harusi? Yaani nimetiwa maji saa moja usiku ndoa saa mbili.” “Hata kama ni hivyo bado hukutakiwa kunificha.”

    “Niliona aibu kukueleza nimebadili dini hata ndoa yenyewe haikuwa hata na andazi la kutafuna zaidi ya kufungwa msikitini na kurudi nyumbani.” “Bado sijakukubalia, mimi nani kwako?” “Rafiki.” “Siyo ndugu yako?” “Ndugu yangu.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Kwa nini umenificha?” “Naomba unisamehe sana mpenzi wangu nilichokifanya sicho kizuri.” “Sina budi kukusamehe, lakini wewe ni zaidi ya ndugu wa damu hutakiwi kunificha jambo.” “Nimekuelewa mpenzi, sitarudia tena kukuficha jambo linalonihusu.” “Hongera kwa uamuzi wako siwezi kuupinga nauheshimu,” nilimpa moyo kwa uamuzi wake. “Basi shoga mwenzako nimeingia ulipotoka, sasa hivi mi Muislamu safi.” “Mbona sijakuona ukiswali?”

    “Mmh! Hapo ndipo mtihani, mume wangu mwenyewe kuswali mpaka Ijumaa.” “Sikiliza dada yangu, unapoingia kwenye dini usiingie jina ingia kwa vitendo kwa kujifundisha ili uwe Muislamu wa kweli.”

    “Kweli kabisa kuna vitabu shemeji yako alininunulia ili niwe navisoma.” “Huwezi kujua kwa kusoma tu bila maelekezo.” “Kuna kikundi cha akina mama kilinifuata kwa ajili ya kunipa mafundisho ya dini, lakini muda wao ukawa tofauti , uliingiliana na kazi zangu.”

    “Dada kama umeamua kuiacha dini yako ya zamani basi tumia muda wako kuijua dini yako mpya na kujifunza tofauti na hivyo una haki ya kuirudia dini yako kama uliyoiingia unaona ina upungufu.” “Kwa kweli kutoka moyoni mwangu, siwezi kurudi dini yangu ya zamani, nimegundua upungufu mkubwa nilipotoka. Sasa hivi kama ulivyonieleza ni kujifunza kwa undani dini yangu

    ya sasa. Nampenda sana mume wangu na dini yangu pia.” “Basi jifunze dini ili uwe muumini mzuri si jina.” “Nawe si ulizaliwa kwenye dini hii unaonaje ukarudi kwenye dini yako ya kuzaliwa?” Ilham aliniuliza swali la mtego.

    “Mmh! Ni haraka sana kuchukua uamuzi huo, nahofia kutangatanga naweza leo kubadili dini kesho akatokea mwanaume Mkirsto na kutaka kunioa huoni nitakuwa natangatanga?” “Ni kweli, lakini si lazima uolewe na Mkiristo.”

    “Shoga niache kwanza hukuhuku nitajua nifanye nini muda si mrefu.” “Basi uwe unaenda hata kusali.” “Wiki hii nitaanza kwenda.”

    Jumapili iliyofuata nilikwenda kanisani na niliporudi nyumbani nikawa kama nimemtia ufunguo Ilham, akaanza kufuatilia dini yake kwa karibu huku akizingatia mfunzo yote na kumfanya kwa muda mfupi ajue mengi na kufikia kuswali swala zote tano.

    Kwa kweli maisha ya shoga yangu na mumewe kwa muda mfupi yalibadilika na kuwanyookea. Upendo uliongezeka kiasi cha kuanza kuwaonea wivu na kutamani nami niishi maisha kama yao ambayo hata waumini wengine wa Kiislamu hawakuyaweza. Kwa mara nyingine nikawa kigeugeu na kushawishika kurudi kwenye dini yangu ya zamani kutokana na mabadiliko makubwa ya shoga yangu. Nilimueleza shemeji uamuzi wangu ambao ulitoka chini ya moyo wangu huku nikimuomba Mungu anisamehe kwa kuwa kigeugeu na anijalie nifie katika dini yangu ya haki. Nilitiwa maji na kurudi katika dini yangu ya Kiislamu na kutumia jina langu lilelile la Salha jina la marehemu bibi.

    Kwa vile dini haikuwa ngeni kwangu nilirudi kwa kasi ya ajabu, kwa kutafuata yote yampasayo kufanya mwanamke wa Kiislam huku nami nikijifunza zaidi. Ilham alifurahia uamuzi wangu wa kurudi katika dini yangu ya awali na kuongeza mapenzi kwangu.

    Malezi niliyoyapata kwa shoga yangu na mume wake siwezi kuyaelezea, kutokana kuwepo kwangu pale, shoga yangu alinielezea kuwa hali imezidi kuwanyookea eti nimekuwa na baraka kuwepo pale, nilimshukuru Mungu hali iendelee kuwa hivyo. Kitu kingine katika mabadiliko ya maisha yao walifanikiwa kununua kiwanja maeneo ya Tabata Kisukuru ambacho kutokana na shemeji yangu kuongezwa fedha na tajiri yake baada ya kubadili dini, pia kutokana na kuonesha kuipenda na kuifuata. Mungu alizidi kuwangazia kwa kuweza kufanikiwa kujenga nyumba ambayo tulihamia baada ya miezi sita.

    Katika siku zote Ilham aliniambia kuna kitu anataka kunieleza na kuniomba nimkubalie.

    Nilijiuliza kitu gani tena hicho shoga yangu anataka kuniambia ambacho kilionekana kikimsumbua moyoni mwake. Kila nilipomuuliza kitu gani hicho anachotaka kuniambia alisema nivute subra. “Shoga mbona unanipa mtihani.” “Najua nitakuchanganya lakini ni jambo la heri.”

    “Jambo gani si unidokeze hata kidogo.” “Ikifika siku nitakueleza,” Ilham bado alifanya siri.

    KWA kweli nilikuwa na maswali mengi juu ya kitu alichotaka kunieleza na kuniomba nikubali. Wazo langu lilikimbilia kwenye ndoa nikahisi labda kuna mtu amevutiwa na mimi na amemwambia kuwa aniambie ili anioe. Kauli ile ilinifanya niongeze umakini japokuwa nilikuwa nakisia bila kuwa na uhakika. Ilionesha mtu anayenitaka huenda anafuatilia nyendo zangu kupata uhakika na kile alichokuwa akikiona kwangu. Niliamini tabia ya utulivu ilikuwa tabia yangu ya asili na hasa baada ya kufiwa sikuwa na wazo la kuwa na mwanaume tena. Niliamini kuwa baada ya matatizo nilikongoroka mwili na hakuna hata mtu mmoja aliyenitazama kwa jicho la matamanio. Baada ya kutuliza akili huku nikifuatilia mawaidha ya masheikh mbalimbali yaliyotuelezea masahibu yaliyowakuta maswahaba enzi ya Mtume Muhammad (SAW), matatizo yangu niliyaona madogo na kuendelea kumuomba Mungu anipe faraja ya duniani na ahera. Siku zote nilisali swala za usiku na kufunga suna ili kumuomba Mungu katika hilo ninaloliwaza kama kweli basi nipate mume mwema mwenye kumjua Mungu. Siku moja nikiwa nimekaa kitandani kabla ya kulala mlango uligongwa, sikunyanyuka nilimuuliza mgongaji nikiwa bado nimekaa palepale kitandani. “Nani?” “Mimi,” ilikuwa sauti ya Ilham. Nilinyanyuka hadi mlangoni na kuufungua mlango. “Karibu.” “Asante, ushalala?” “Wala, nilikuwa nimejiegemeza nikiwaza ya dunia kabla ya kulala.” “Basi samahani kwa kukukatisha mawazo yako,” Ilham aliniomba radhi. “Mbona kawaida, karibu.” “Asante,” Ilham aliitikia huku akisogea na kukaa kitandani. Kwa ujaji ule nilijua kuna kitu, nami nilikaa pembeni yake kusubiri kusikia kilichomleta chumbani kwangu usiku ule. “Salha,” aliniita bila kunitazama. “Abee dada.” “Kuna kitu nataka nikuambie, najua utashangaa lakini naomba unikubalie.”

    “Kitu! Kitu gani dada yangu?” Nilishtuka. “Huwezi kuamini nimejigeuza mshenga wa pande mbili, kwa muoaji na muolewaji.” “Una maana gani?” Mawazo yangu yalikuwa sahihi kuna mwanaume anataka kunioa. “Salha huwezi kuamini tabia yako imenigeuza sana kimaisha, umekuwa mwanamke tofauti na wanawake wengi. Kutokana na matatizo uliyokumbana nayo yangeweza kukuyumbisha na kuishi maisha mengine, lakini siku zote umekuwa mtu wa msimamo. “Huwezi kuamini tangu nilipokuwa na wewe niligundua nini thamani ya mwanamke na faida ya msimamo.” “Umekuwa siku zote ukiamini kile unachokijua, pia kutokuwa na tamaa kama wanawake wengine wanapopatwa matatizo hukimbilia kujidhalilisha. “Kabla ya kukutana na wewe siwezi kukuficha nilikuwa na mabwana nisiowajua idadi yake hiyo ilitokana na kazi niliyokuwa nikiifanya. Kazi ya baa na ugumu wa maisha ni hatari kubwa sana kwetu wanawake. Mshahara mdogo na lazima umkubali bwana yeyote atakayekuja mbele yako ili kupunguza makali ya maisha. “Salha ndugu yangu, sikupenda ila hali ndiyo ilinifanya niwe vile, ukimkataa bwana utakula mawe? “Hivyo kila aliyekuja mbele yangu alikuwa ni halali yangu, hatari kubwa ilikuwa katika ugonjwa wa ukimwi kutokana na wanaume wengine niliokutana nao kutotaka kutotumia kinga. Unajijua kabisa kwamba unakikimbilia kifo lakini utafanyaje, kwa vile njaa ndiyo inayonisukuma kukuubali kuchezea umeme kwa mikono, namshukuru Mungu mpaka nakutana na wewe nilikuwa salama. “Nina imani mwanzo tulipokutana nilikueleza historia yangu kwa kifupi japokuwa kuna mengi nilikuficha, hata kupatikana kwa mwanangu aliyekosa baba kulitokana na kutembea na wanaume bila mpangilio. “Kuja kwako kulikuwa kama ukombozi kwangu, kwa muda niliokaa na wewe nilijifunza vitu vingi vikiwemo mavazi ya heshima, tabia na msimamo. Baada ya kufuata nyenzo zako niliweza kuonekana mbele za watu hata kumpata mume niliyenaye leo.

    “Pia ulikuwa na moyo wa huruma na mtu mwenye maono ya mbali japo moyo wako tayari ulikuwa umekata tamaa. Kila lililokupata moyoni mwangu maumivu yalikuwa mara mbili. Sikuwa na kitu lakini nilimuomba Mungu usiku na mchana akuepushe na matatizo huku nikumuomba amfungulie mume wangu riziki ili niweze kukulea rafiki yangu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Kwa kweli Mungu alisikiliza kilio changu na wakati wa matatizo yako nilikuwa angalau na kitu cha kuweza kukusaidia. Salha umeyabadili maisha yangu, bila wewe sijui ningekuwa wapi sasa hivi kama sio kudhalilika mbele ya wanaume wapenda ngono. “Ulichokuwa nacho wakati Mungu kakupa neema ulikitoa bila ajizi, wakati wa neema niliringa na kuamini nina sehemu ya kukimbilia na nilipofika ulinitatulia mara moja.

    “Matatizo yangu uliyapokea kama yako na kuhakikisha navuka salama wakati wa matatizo. Salha umeijenga nyumba yangu kwa mikono yako umekuwa mshauri katika lililokosa jibu kwangu na leo hii nimesimama mwenyewe. Matatizo ni sehemu ya maisha, najua kiasi gani ulivyoumizwa na msululu wa matatizo yenye historia ndefu isiyotakiwa kurudiwa.

    “Namshukuru Mungu kukuondolea mawazo mabaya na kuweza kumkimbilia yeye kwa kila jambo. Nashukuru pia bado umeendelea kuwa mwalimu wangu mwema hata katika mambo ya dini. Baada ya kuwaza yote yaliyopita kuna kitu kilinijia, siamini ni wazo langu bali kama ufunuo ambao kila siku umeniumiza akili yangu. “Kama nilivyokueleza Salha, una sifa ya kuwa mwanamke wa mfano, pia unafaa kuwa mke wa mtu mwenye kujua nini thamani ya mwanamke mstaarabu. Kabla ya kukueleza nilichokikusudia siku ya leo naomba uniambie ukweli, maisha ya hapa unayaonaje?” Ilham aliniuliza swali akiwa ananitazama usoni.

    “Kwa kweli nimeishi na watu wengi lakini mliyonitendea wewe na mumeo ni Mungu pekee wa kuwalipa. Umekuwa nguzo yangu imara iliyopigana usiku kucha kunisimamisha. Nilishakata tamaa lakini ulijitoa kwangu kwa hali na mali kuhakikisha sipotei ndugu yako. Sina cha kuwalipa ila Mungu pekee atawalipa,” nilijikuta nikisema kwa uchungu mpaka machozi yakanitoka. “Unamuonaje shemeji yako?” “Kumuona kivipi?” sikumuelewa kidogo. “Maisha ninayoishi naye.” “Maisha mnayoishi yananikumbusha jinsi marehemu mama yangu alivyoishi na baba japo mama yangu hakuuthamini upendo wa baba na kuamua kuwa mwingi wa habari. Tofauti ya baba na mumeo ni ndogo, baba hakuwa na moyo wa huruma, lakini mumeo ana moyo wa huruma. Kwa kweli maisha mnayoishi ndiyo wanayotakiwa kuishi wanandoa.”

    “Nashukuru kuliona hilo, nina imani hata wewe unatamani kuishi maisha kama haya?” “Ni kweli, kila mwanadamu hupenda kuishi kwa maelewano na masikilizano na mwenzake.” “Vizuri, sasa ni hivi naomba unisikilize kwa makini.” “Nipo makini dada,” nilimjibu huku nikimtazama usoni.

    “Katika maisha yangu sijawahi kumuona kiumbe kama wewe, mtu ambaye kila kukicha humuomba Mungu anipe moyo na tabia zako. Japo nitakachokueleza utaona kama utani lakini amini ni kitu cha kweli kabisa,” Ilham alitulia na kumeza mate kisha aliendelea.

    “Miezi minne iliyopita nilikutazama sana na kupata maswali ambayo yalinisumbua sana kupata jibu. Nilimuomba Mungu anipe jibu la maswali yangu, nilitamani sana kukaa na wewe na tutenganishwe na kifo. Lakini nilipata ugumu. Je, akitokea mtu anataka kukuoa itakuwaje?

    “Wakati nikijiuliza vile, siku hiyo mume wangu aliniletea taarifa kuwa rafiki yake kipenzi amevutiwa na wewe anataka kukuoa, bila hata kujiuliza nilimjibu kuwa tayari una mchumba,” majibu ya Ilham yalinishtua na kujiuliza nina mchumba? Mbona huyo mchumba mimi simjui? “Najua utashangaa kusema una mchumba usiyemjua, ni kweli nilimjibu kwa vile bado sikutaka tutengane japo hukuwa na mchumba yeyote. Baada ya jibu lile alishukuru Mungu na kusema

    haikuwa riziki ya rafiki yake na kuongeza chumvi kwenye kidonda cha moyoni mwangu kwa kusema kuwa atakayekuoa hakika atapata mwanamke wa kweli.

    “Baada ya kuachana naye nilibakia na siri iliyoutesa moyo wangu, nitawezaje kuwa na wewe kwa kipindi kirefu? Siku moja nikiwa nimelala usiku niliota ndoto moja kuwa wewe ni mke mwenzangu tunayeelewana sana. Nilishtuka usingizini nilitawadha na kuswali rakaa mbili na kumuomba mwenyezi Mungu njozi ile iwe ya heri.

    “Baada ya hapo ilipita tena wiki nikilifanyia kazi suala la ukewenza kwa kuulizia kwa mashehe hata kwa wanawake walioolewa ukewenza. Wapo walioukataa kwa kusema ukewenza ni vita ya ndani. Lakini wapo walionieleza ukewenza ni mzuri hasa mkiwa na mioyo ya kumuogopa mwenyezi Mungu na kupendana kama ndugu.

    “Baada ya kuridhika na upembuzi wangu, nilikaa na mume wangu na kumueleza uamuzi wangu wa kutaka wewe uwe mke mwenzangu.” Moyo ulinipiga pa! Nilishika mikono kifuani na kusema: “Ha! Ilham!” “Tulia basi, unisikilize sijamaliza mbona unashtuka?” “Haya dada.” “Nilipomueleza mume wangu naye alishtuka na kuniulizia kuhusu yule mchumba wako kaishia wapi. “Nilimueleza kama nilivyokueleza juu ya kutaka kukaa na wewe siku zote za maisha yangu. “Nilimpa sababu zilizoshiba na akaniuliza kama utakubali? Nilimweleza kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu utakubali. Basi shoga ombi langu kwa usiku huu ni hilo, nakuomba ukubali tuolewe pamoja ili tuuendeleze udugu wetu.” Kabla ya kujibu nilishusha pumzi nzito na kutulia kwa muda huku nikilifanyia kazi ombi lake. Katika maisha yangu sikuwaza kumuudhi Ilham hata siku moja. Kwa kuwa niliamini ukewenza unaweza kuwa chanzo cha uadui na kufikia hatua ya mimi na yeye kuwa chui na paka. “Dada nimekusikia, lakini naogopa udugu wetu utakuja kugeuka kuwa uadui, sipendi kukuudhi, wewe ni mtu muhimu sana kwangu,” nilimjibu kwa upole. “Salha mpaka nalitamka hili mbele yako tayari nimeshalifanyia kazi kubwa na nakuhakikishia, moyo wangu hautakuwa radhi kukufanyia kitu chochote kibaya na kama itatokea hivyo, basi Mungu siku hiyohiyo anigeuze kuwa mbwa au nguruwe.” “Dada mbona umefika mbali.” “Siyo mbali, nakupenda sana Salha.” Sikuwa na pingamizi, nilimkubalia baada ya kufikisha majibu kwa mumewe mipango ya ndoa ilipangwa na nikaolewa na bwana Swamadu na kuwa mkemwenza wa shoga yangu kipenzi Ilham. Nashukuru maisha yetu Mungu ametuangazia kwani upendo umetawala kwa kuwa tumemtanguliza Mungu kwa kila jambo. Sasa hivi nina watoto wawili kwa mzao mmoja uliokuwa wa mapacha na mzao mmoja mwingineCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    mtoto hakuwa riziki kwani alifariki akiwa na miezi sita. Namshukuru Mungu nami leo nacheka na kusahau yote, ambayo nimekuwa nikiyazungumza yamebakia kama historia. Mimi na mke mwenzangu tunaishi kama ndugu wa tumbo moja, lake langu na langu lake. Japokuwa maisha yanaendelea lakini huu ndiyo mwisho wa simulizi hii ambayo najua imekuliza na kukuumiza moyoni. Lakini yote kwa yote namshukuru Mungu kwa yaliyotokea kwa imani yangu yote ni mipango yake. Nachukua fursa hii kuwashukuru wote waliosafiri pamoja nami tangu mwanzo wa simulizi hii mpaka leo imefika mwisho. Simulizi hii ni moja na mitihani tunayokutana nayo wanadamu na kufikia hatua ya kuamini dunia tunayoishi huenda siyo yetu na kuona tunaishi dunia ya peke yetu. Nakuombeni wote mnaokutwa na matatizo mrudieni Mungu bila kuchoka kwa vile neema zake hazina siku wala saa,msikate tamaa kwani hakuna mwingine ila Allah, muombe atakupa. Nakutakieni maisha marefu yenye furaha na wenye matatizo Mungu awaepushie.



    MWISHO.



0 comments:

Post a Comment

Blog