Search This Blog

Thursday, July 21, 2022

PENZI KABLA YA KIFO - 3

 







    Simulizi : Penzi Kabla Ya Kifo

    Sehemu Ya Tatu (3)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikuwa ni lazima kwa Elizabeth kurudi nchini Tanzania, hakutaka kukaa sana nchini Uganda kwa kuona kwamba kulikuwa na mambo mengi alitakiwa kuyafanya nchini Tanzania likiwemo suala la binti mdogo aliyekutana naye katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

    Moyo wake ulimuuma mno na kila wakati alikuwa akifikiria kuhusu mtoto huyo, alimuonea huruma na msukumo mkubwa ulimjaa moyoni mwake na hivyo kuona kwamba kulikuwa na haja ya kumsaidia kutokana na ugonjwa wa kupooza aliokuwa nao.

    Ndani ya ndege ni watu wawili tu ndiyo waliomfanya kuwa kwenye hali ya mawazo, wa kwanza alikuwa msichana huyo mdogo, Glory na wa pili alikuwa Olotu, bilionea aliyekutana naye nchini Uganda ambaye alimwambia wazi kwamba alikuwa akimpenda.

    “Vipi tena?” aliuliza Candy, haikuwa kawaida ya Elizabeth kukaa kimya muda mrefu.

    “Poa.”

    “Mbona una mawazo?”

    “Hapana! Kuna vitu navifikiria.”

    “Halafu hujaniambia, yule mkurugenzi alisemaje?”

    “Yupi?”

    “Yule wa ile hoteli!”

    “Alitaka kunishukuru tu,” alijibu.

    “Sawa.”

    Hakutaka kuzungumza ukweli, kitu pekee alichokuwa akikitaka mahali hapo ni ukimya tu ili aweze kupata muda wa kufikiria kile kilichokuwa kikiendelea kichwani mwake. Candy alilifahamu hilo, hakutaka kumsumbua sana, alichoamua ni kumuacha na yeye kufanya vitu vingine.

    Baada ya masaa kadhaa wakafika nchini Tanzania na moja kwa moja kutoka ndani ya Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere huku akiwa amevalia jumba lake na nikabu ili asiweze kugundulika na watu wengine kwa kuhofia kuzungukwa na kusumbuliwa.

    “Saa yako inasema saa ngapi?’ alimuuliza Candy.

    “Saa nane mchana.”

    “Hakuna kwenda nyumbani, nataka twende hospitali.”

    “Muhimbili?”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ndiyo! Ninataka kumuona yule mtoto,” alisema Elizabeth.

    Huo ndiyo uamuzi alioamua kuuchukua muda huo, hakutakakurudi nyumbani kwake, kitu pekee alichotaka kukiona mahali hapo ni mtoto yule mdogo aliyekuwa kwenye mateso makubwa. Bado moyo wake ulikuwa na msukumo mkubwa wa kumuona msichana huyo, alijiona kuwa na uwezo mkubwa wa kumsaidia na kupona kabisa.

    Kilichomkera ni foleni za barabarani tu. Walijikuta wakisimama muda mrefu kuliko kutembea. Ila pamoja na hayo yote, ndani ya dakika hamsini wakajikuta wakiwa ndani ya jengo la hospitali hiyo ambapo wakateremka na kuanza kuelekea humo.

    “Samahani,” alimwambia nesi mmoja.

    “Bila samahani.”

    “Nataka kufika katika wodi ya Mwaisela.”

    “Nendani kule mbele.”

    Hawakutaka kusubiri, walichokifanya ni kuondoka na kuelekea huko. Si kwamba Elizabeth hakufahamu mahali ilipokuwa hiyo wodi, alifahamu vilivyo lakini kutokana na kuchanganyikiwa kwake, hakuweza kufahamu mahali ilipokuwa.

    “Yule kule,” alisema Elizabeth na kuanza kuelekea kule alipoonyeshea kidole chake ambapo kulikuwa na nesi aliyekuwa akimshusha Gloria kutoka kitandani, japokuwa ndani ya wodi ile kulikuwa na wagonjwa wengi, ila wote walimuonea huruma Gloria.

    Alipofika katika kitanda kile alichokuwa mtoto yule, Elizabeth akashindwa kuvumilia, hapohapo machozi yakaanza kumbubujika mashavuni mwake, aliumia mno na hakuamini kama kulikuwa na watu waliokuwa wakipata mateso makali vitandani kama ilivyokuwa kwa mtoto yule.

    Kila alipomwangalia, nikabu yake ikazidi kulowanishwa na machozi yaliyokuwa yakimtoka, huruma nyingi ikautawala moyo wake, akajikuta akisimama tu huku akimwangalia Glory aliyekuwa amepooza, hakutingishika kabisa zaidi ya kupeleka shingo yake huku na kule.

    Alibaki akiwa amesimama tu, japokuwa ndani ya wodi ile kubwa kulikuwa na watu wengi lakini hakukuwa na yeyote aliyeweza kugundua kama mtu aliyekuwa amesimama karibu na kitanda alichokuwa mtoto aliyepooza alikuwa Elizabeth.

    Glory hakuweza kusimama na kwenda chooni, hapohapo alikuwa amewekewa mipira ambayo ilimsaidia kujisaidia haja kubwa na ndogo, ni manesi, tena wenye upendo wa hali ya juu ndiyo waliokuwa na jukumu kubwa la kubadilisha mipira ile kadiri ilivyokuwa ikitumika, tena kila baada ya siku mbili.

    “Samahani nesi,” alimwambia dada aliyekuwa akimshughulikia kwa kutoa mipira ya haja kubwa na ndogo.

    “Bila samahani.”

    “Huyu mtoto amekwishapata fedha za kumpeleka India kwa matibabu?’ aliuliza Elizabeth.

    “Bado, ila michango inaendelea kukusanywa,” alijibu nesi yule.

    “Na kama nitataka nimsaidie?”

    “Hakuna tatizo, unatakiwa kuwasiliana na daktari,” alijibu nesi yule.

    “Nataka nimuone, unaweza kunipeleka sasa hivi?”

    “Hakika!”

    Huruma iliyomjaa moyoni mwake, kitu pekee alichokiona kufanya kwa kipindi hicho ni kumsaidia Glory aliyekuwa hoi kitandani. Kwa sababu nesi yule alikuwa akiendelea kumhudumia Glory, wakamsubiri mpaka atakapomaliza ndipo waende kwa daktari yule.

    Kila alipokuwa akimwangalia Glory, hakuacha kulia, maumivu makali ya moyo yalimkamata na kujiona akishindwa kabisa hata kumwangalia, alichowambia Candy ni kutoka na kusogea pembeni, wakafanya hivyo.

    Baada ya nesi yule kumaliza kumhudumia Glory, hapohapo akawachukua na kumpeleka katika ofisi ya daktari aliyehusika katika suala zima la wagonjwa waliokuwa katika Wodi ya Mwaisela. Walipofika, wakaanza kuelelezea shida yao ambapo hapohapo daktari akaonyesha sura iliyokuwa na tabasamu pana.

    “Tumekubaliana na msaada wenu, hakika tumehangaika sana,” alisema daktari yule.

    Kuhusu fedha halikuwa tatizo lolote lile, alichokifanya Elizabeth ni kuaga na kuahidi kurudi tena kesho yake kwa ajili ya kutoa kiasi hicho ili safari ya kuelekea nchini India ianze. Alipofika nyumbani kwake, akajifungia chumbani na kuanza kulia kwa uchungu.

    Alikuwa na maumivu makali mno ya moyo, kila alipokaa na sura ya Glory kumjia kichwani mwake, akajikuta akilia kwa uchungu kwani hakuamini kama kulikuwa na binti mdogo aliyekuwa kwenye mateso makali kama alivyokuwa Glory.

    Siku iliyofuata, asubuhi na mapema akaondoka na kuelekea hospitali. Hakutaka kuacha kuvaa baibui na nikabu usoni. Hakutaka kuleta usumbufu wowote ule na ndiyo maana hata gari alilokuwa akilitumia ni lile ambalo halikuzoeleka kabisa.

    Alipitia benki ambapo akachukua kiasi cha shilingi milioni kumi na kuelekea huko. Alipofika hospitali, moja kwa moja wakaenda kwa daktari yule na kumuona kwa ajili ya kumwambia kwamba kila kitu kilikuwa tayari na ni safari ya kuelekea India ndiyo iliyotakiwa kufanyika mahali hapo.

    “Kiasi cha fedha hiki hapa,” alisema Elizabeth huku akiweka bahasha kubwa ya kaki mezani, ndani yake kulijaa noti tu.

    “Kiasi gani?”

    “Milioni kumi. Si zitatosha?”

    “Ndiyo! Basi subiri tukuitie ndugu yake. Tulimwambia kuhusu suala lako, alilia sana kwa furaha, hakuamini kama mwisho wa siku ndugu yake angeweza kupata msaada,” alisema daktari yule.

    “Hakuna tatizo.”

    Alichokifanya ni kunyanyua simu na kupiga upande wa pili, baada ya sekunde kadhaa simu ikapokelewa na mtu wa upande wa pili na sauti laini ya kike ikaanza kusika. Alichoagiza daktari huyo ni ndugu wa Glory alitakiwa apelekwe ofisini kwake kwa ajili ya kumuona mdhamini ambaye alijitolea kumsaidia.

    “Hakuna tatizo!” sauti ya upande wa pili ilisema na kisha simu kukatwa.

    Walikaa na kuzungumza mengi, Elizabeth hakuacha kumwambia daktari yule jinsi alivyokuwa akijisikia kuhusu hali aliyokuwa nayo Glory, alionekana kuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakimuonea huruma sana binti yule mdogo na hivyo daktari kumtakia baraka nyingi pasipo kugundua kwamba mtu aliyekuwa akizungumza naye alikuwa Elizabeth, msichana mwenye fedha na umaarufu mkubwa.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya dakika kumi, mlango ukaanza kugongwa, daktari akaruhusu waingie, nesi mmoja alitangulizana na kijana mmoja aliyeonekana kupigwa sana na maisha, Elizabeth alipoyageuza macho yake na kumwangalia kijana huyo, akausikia moyo wake ukipiga paaaaa.





    Alikata tamaa, hakuamini kama angeweza kupata tena fedha kwa ajili ya kumsaidia mdogo wake aliyekuwa hoi kitandani. Kila siku alimuomba Mungu masimamie katika suala zima huku wakati mwingine akiona kama Mungu amemsahau.

    Kila alipokwenda, alilia sana lakini mwisho wa siku hakusikilizwa kabisa, kila aliyemuona na kumsikiliza, alimpuuzia na kujifanya hakuwa na fedha. James hakujua afanye nini, wakati mwingine alitamani hata akutane na rais, amwambie ukweli kwa kuamini kwamba anesaidiwa, lakini hakujua ni kwa namna gani angeweza kumpata mtu huyo.

    Baada ya kusota sana huku akiwa amepata kama milioni moja, ndipo alipoamua kurudi hospitalini na kukutana na taarifa nzuri, taarifa iliyompa matumaini makubwa na kuona kwamba Mungu alisikia kilio chake.

    Mwanamke fulani aliyevalia baibui na nikabu alifika hospitalini hapo, alipomuona Glory kitandani akiteseka, aliingiwa na huruma na kuamua kumsaidia. Alipoyasikia maneno ya nesi yule, hakuamini, wakati mwingine alihisi kama alikuwa usingizini na muda mchache angeamka na kujikuta akiwa kitandani, ila ukweli ulibaki palepale kwamba hakuwa usingizini.

    “Unasemaje?” aliuliza James huku akionekana kutokuamini.

    “Ndiyo hivyo! Huyo mwanamke ameahidi kumsaidia.”

    “Ahsante Yesu. Anakuja lini?”

    “Kesho! Unatakiwa kuwahi sana hapa ili atakapokuja basi aweze kuzungumza nawe,” alisema nesi yule.

    “Hakuna tatizo! Lakini si naweza kulala hapahapa?” aliuliza James.

    “Kulala hapahapa?”

    “Ndiyo!”

    “Hapana! Kesho ukija utaonana naye.”

    Alishindwa kujua ni kwa nama gani alitakiwa kushukuru, hapohapo pasipo kuhofia macho ya watu akajikuta akipiga magoti na kuinyoosha mikono yake juu na kuanza kumshukuru Mungu kwa kile kilichokuwa kimetokea.

    Hakuamini kama mwisho wa siku angeweza kumpata mtu ambaye aliahidi kwamba angeweza kumsaidia mdogo wake aliyekuwa kwenye mateso makali kitandani. Kwa mara ya kwanza tangu mdogo wake apate matatizo, uso wake ukajawa na tabasamu, moyo wake ukatawaliwa na furaha tele.

    Siku iliyofuata hakutaka kuchelewa kufika hospitali hapo, asubuhi na mapema alikuwa amekwishafika kiasi kwamba hata wale manesi ambao hawakujua kilichokuwa kikiendelea kubaki kumsahangaa tu, hakujali, alitulia huku akisubiri muda wa kuona wagonjwa ufike na kuingia.

    Ulipofika, akaelekea huko na kukaa karibu na mdogo wake. Moyo wake uliendelea kuwa na maumivu makali, alibubujikwa na machozi kama kawaida yake ila wakati mwingine aliisikia sauti ikimwambia kwamba anyamaze kwani Mungu alikisikia kilio chake.

    Ilipofika saa tano akaitwa na nesi na kumwambia kwamba alikuwa akihitajika katika ofisi ya daktari, hakutaka kuchelewa, hapohapo akaelekea huko huku moyo wake ukiamini kwamba mtu aliyetaka kumsaidia mdogo wake alikuwa amefika hospitalini hapo.

    “Shikamoo daktari,” alimsalimia daktari.

    “Marahaba!”

    Hapo ndipo daktari alipoanza kumtambulisha James kwa watu waliosimama mbele yake. Walikuwa wanawake waliojitolea kumsaidia mdogo wake kwa kumpeleka nchini India kupatiwa matibabu. Kabla hata James hajazungumza lolote lile akapiga magoti chini na kuanza kuwashukuru.

    “Hautakiwi kufanya hivyo!” alisema Elizabeth huku akimuinua.

    “Nawashukuru sana, nimeteseka na kuhangaika sana kwa ajili ya mdogo wangu, nashukuru sana,” alisema James kwa sauti iliyojaa na kilio cha chini.

    Hakukuwa na sababu ya Elizabeth kuendelea kuvaa nikabu, alichokifanya ni kuvua nikabu ile, kila mtu aliyemuona na kugundua kwamba alikuwa Elizabeth, akashangaa, si James tu, daktari na nesi wake, wote wakapigwa na mshtuko, kukutana na Elizabeth halikuwa jambo dogo.

    *****

    Elizabeth akachanganyikiwa, hakuamini kile alichokuwa akikiona, kijana aliyesimama mbele yake, James alikuwa mzuri wa sura,mapigo ya moyo wake hayakutaka kutulia hata kidogo, yaliendelea kudunda kwa nguvu kana kwamba moyo ulitaka kuchomoka.

    Mapenzi makubwa yakamkamata, yakampelekesha na kujikuta akiwa hoi, pasipo kulazimishwa na mtu yeyote yule, akajikuta akiingiwa na ugonjwa wa kupendapenda, na hapohapo akaanza kumpenda kijana yule masikini asiyekuwa na kitu chochote kile.

    Alipoyaona machozi ya James, alihisi moyo wake ukishikwa na maumivu makali, hakutaka kuyaona machozi ya mtu aliyekuwa akimpenda, alitaka kumuona akitabasamu milele yote, kilio kile kwake kilimaanisha maumivu makubwa kitu ambacho hakutaka kuona James akikipata.

    Candy alilifahamu hilo, alimjua vilivyo rafiki yake huyo, kila alipomuona mwanaume mzuri wa sura, alichanganyikiwa na kujikuta akitaka kuwa naye, alipomuona James, jinsi alivyokuwa mzuri alijua fika kwamba hata rafiki yake angempenda vilivyo.

    “Ninahitaji nimsaidie mdogo wako, ni binti mzuri ambaye hastahili kuwa kwenye mateso makali namna ile,” alisema Elizabeth huku akimwangalia James.

    “Nashukuru sana Elizabeth, sina cha kukulipa, nashukuru sana.”

    Usijali! Usinishukuru mimi, mshukuru Mungu ambaye amefanikisha mimi kukutana na mdogo wako,” alisema Elizabeth, hakutaka kujiweka juu, kila siku alikuwa mtu wa kujishusha tu.

    Huo ndiyo ukawa mwanzo wa wawili hao kufahamiana. Hata Elizabeth aliporudi nyumbani, kichwa chake kilikuwa kikimfikiria mvulana aliyekutana naye hospitalini. Moyo wake ulikuwa kwenye mapenzi ya dhati, hakutaka kukumbuka tena kuhusu Edson, mwanaume aliyetokea kuuteka moyo wake kwa kipindi hicho alikuwa James.

    Mara kwa mara bilionea kutoka nchini Uganda, Olotu alikuwa akimpigia simu lakini Elizabeth hakutaka kuipokea, mtu pekee aliyekuwa ameuteka moyo wake kwa kipindi hicho alikuwa James pekee.

    Alikuwa kijana masikini ambaye hakuwa na kitu chochote kile, kwake, hakujali hata kidogo, alichokuwa akikiangalia moyoni mwake ni mapenzi tu. Japokuwa aliteseka sana usiku lakini hakujua kama mwanaume huyo angekubaliana naye au la, alichokitaka ni kujaribu bahati yake tu.

    “Candy!” aliita kwenye simu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Niambie shosti.”

    “Nimeshindwa kulala.”

    “Kisa?”

    “James ananiumiza jamani, nimekaa nikimuwaza yeye tu,” alijibu Elizabeth.

    “Jamani! Yaani kukutana naye leo tu umechanganyikiwa?”

    “Mmmh! Shoga yangu wewe acha tu, ninateseka kwa mapenzi yake. Ninamtaka, natumaini atanikubalia tu,” alisema Elizabeth.

    “Jaribu bahati yako,” alisema Candy.

    Hilo ndilo alilolitaka, hakutaka kuona akipingwa, kila wakati alipofikia hatua ya kumwambia mtu yeyote kile alichokuwa akikihitaji alitaka kuona akiungwa mkono hata kama jambo lingekuwa baya kiasi gani.

    Kwa Candy kumwambia kwamba alitakiwa kujaribu na angeweza kufanikiwa, akafurahi na kuahidi kufanya hivyo. Alichokifanya ni kwenda hospitali pale mara kwa mara, huko alikutana na James na kuzoeana naye ili baadae ije kuwa rahisi hata kumwambia alichotaka kumwambia.

    James hakuonekana kujali, alionyeshewa ishara zote za kimapenzi lakini kutokana na msongo wa mawazo aliokuwa nao, hakuzigundua ishara hizo, yaani kwa Elizabeth ilionekana ni kama alikuwa akimuonyeshea ishara zile kipofu.

    Baada ya wiki moja, kila kitu kilipowekwa tayari, safari ya kuelekea nchini India katika Hospitali ya Apollo iliyokuwa katika Jiji la Chennai nchini humo ikaanza. Baada ya saa ishirini, ndege binafsi ya Elizabeth ikaanza kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chennai uliokuwa katika jiji hilo.

    Mlango ukafunguliwa, tayari gari la kubeba wagonjwa la Hospitali ya Apollo lilikuwa limefika uwanjani hapo na hivyo kumbeba Glory aliyekuwa kitandani na moja kwa moja safari ya kuelekea hospitalini kuanza.

    “Elizabeth! Hivi atapona kweli?” aliuliza James huku akionekana kutokuamini.

    “Atapona tu, ninayaamini sana matibabu ya hapa, usijali James,” alijibu Elizabeth huku akimwangalia mwanaume huyo kwa macho yaliyojaa mahaba tele.

    “Nashukuru kwa faraja yako.”

    Walichukua dakika ishirini na ndipo gari hilo lililokuwa likipiga king’ora likafika katika hospitali hiyo kubwa na kuingia ndani ya eneo la hospitali hiyo. Manesi ambao tayari walijiweka nje ya jengo la hospitali ile walipoliona gari hilo likiingia, wakaanza kusukuma machela na kisha kuufungua mlango na kumteremsha Glory na kuanza kuisukuma machela ile ndani.

    “Hatuwezi kuwa hospitalini hapa siku zote za matibabu, inatupasa tukachukue vyumba hotelini,” alisema Elizabeth.

    “Hakuna tatizo!”

    Huko ndipo Elizabeth alipotaka kumaliza kila kitu. Hakuwa radhi kuendelea kuvumilia zaidi na wakati moyo wake ulikufa na kuoza kwa mwanaume huyo, alichokuwa akikitaka ni kuona anakuwa mpenzi wake na kuendelea na maisha kama kawaida.

    Kwa sababu tayari Elizabeth alikuwa amekwishaweka oda ya vyumba vya hoteli kubwa na ya kifahari ya Pentagon iliyokuwa katikati mwa Jiji la Chennai, walichokifanya ni kuchukua gari na kwenda huko ambapo vyumba vyao vilikuwa jiranijirani tu.

    “Hapa ndipo tutakapolala! Ushawahi kulala hotelini?’ aliuliza Elizabeth.

    “Hapana!”

    “Sawa! Baada ya hapa, turudi hospitali,” alisema Elizabeth.

    Hapo ndipo walipopata muda wa kuoga na kujiandaa tayari kwa kurudi hospitalini. Chumbani, Elizabeth alikuwa na mawazo tele, kila alipokuwa akimwagikiwa na maji ya bomba la mvua, aliyainua macho yake juu na kisha kukishikashika kifua chake hali iliyomletea mhemko mkubwa na kutamani kuwa na James mahali hapo.

    Alikuwa kwenye wakati mgumu mno, hakutaka kuona akishindwa hata mara moja, alimhitaji sana James kiasi kwamba wakati mwingine aliona hakuwahi kumhitaji mwanaume moyoni mwake kama alivyomhitaji James.

    “James! Ninakupenda kipenzi,” alisema Elizabeth huku maji ya bomba la mvua yakiendelea kummwagikia.

    “Kwa nini unanitesa, naomba unikubalie na usinifanyie kama wanaume wengine walioamua kuniumiza, ninahitaji kuwa na wewe tu,” alisema Elizabeth huku akiwa katika hisia kali za kimapenzi.

    Alipomaliza kuoga akatoka bafuni kisha kuendelea kujiandaa na baada ya dakika ishirini, walikuwa ndani ya gari maalumu lililokuja kuwachukua kwa gharama zake na kuelekea hostelini huku tayari ikiwa imetimia saa kumi na moja jioni.

    Katika kipindi chote hicho, Elizabeth alikuwa akijifikiria kama huo ulikuwa muda sahihi wa kumwambia James alivyokuwa akijifikiria au la. Muda ulizidi kuyoyoma, madaktari tayari walikuwa ndani ya chumba cha upasuaji wakiendelea kumfanyia upasuaji Glory na matokeo kuonyesha kwamba uti wake wa mgongo ulikuwa umevunjika kidogo.

    “Will she be okey?” (Atapona?) aliuliza Elizabeth.

    “We are trying our best, we don’t know yet, but you have to wait,” (Tunajaribu kwa uwezo wetu, bado hatujajua , lakini mnatakiwa kusubiri) alisema Dk. Ajay, alikuwa bingwa wa upasuaji hospitali hapo.

    Walichoambiwa ndicho kilichokuwa kikiendelea. Mbali na Dk. Ajay, pia kulikuwa na madaktari wengi waliokuwa na utaalamu wa hali ya juu, kila mmoja mahali hapo alitaka kuhakikisha binti yule mdogo anapona na kuwa kama zamani.

    Waliingia kwa zamu ndani ya chumba kile, hakukuwa na kitu walichokuwa wakikisubiri kwa hamu kama kumuona Glory akiwa mzima na hata kama hawatofanikiwa lakini ule upasuaji waliokuwa wakiufanya basi baadaye uweze kusaidia na binti yule mdogo kuwa mzima wa afya.

    Baada ya upasuaji kufanyika kwa masaa nane, hapo ndipo madaktari walipowaruhusu kuingia katika chumba cha mapumziko kwa ajili ya kumuona Glory aliyekuwa kimya kitandani. Kila aliyemuona, hakika aliumia moyoni mwake, alikuwa msichana mdogo ambaye hakustahili kupitia mateso kama aliyokuwa akiyapitia mahali hapo.

    “Glory! Utapona tu mdogo wangu,” alisema James huku akimwangalia mdogo wake huyo kitandani alipokuwa.

    Ilipofika saa nne usiku, wote wakatoka hospitalini hapo na kurudi hotelini. Walipoingia vyumbani mwao, Elizabeth hakutaka kukubali, kiu kubwa ya kufanya mapenzi na James ilimshika kiasi kwamba akashindwa kabisa kuvumilia.

    Alichokifanya ni kuoga kisha kuchukua nguo yake ya kulalia tu na kwenda katika korido ambapo akaanza kuugonga mlango wa James aliyefika na kuufungua. Hata kabla hajamuuliza Elizabeth kilichokuwa kikiendelea, akajikuta akisukumwa na kuingia ndani, taulo alilolivaa Elizabeth likatoka mwilini mwake na kumbakiza na nguo ya ndani tu.

    “Elizabeth!” alisema James kwa sauti iliyoonyesha mshangao mkubwa.

    “James! Nakuhitaji, nataka uupoze moyo wangu usiku wa leo!”

    “Elizabeth! Are are out of your mind?” (Elizabeth! Umechanganyikiwa?)

    “No! I want you James! Please, come to me baby!” (Hapana! Ninakuhitaji James! Njoo kwangu mpenzi) alisema Elizabeth.

    Hapohapo akamsogelea James na kujikuta wote wakiangukia kitandani. Kasi ya  udundaji wa moyo wa James yalikuwa juu mno kiasi kwamba mpaka Elizabeth aliyasikia.

    Elizabeth aliumbika mno, kifua chake kilikuwa kizuri, kila James alipokuwa akimwangalia, alijikuta akiingiwa na hamu ya kufanya mapenzi na msichana huyo mrembo. Umbo namba nane, alikuwa na hipsi zilizojengeka vilivyo, nyonga nzuri kiasi kwamba kwa kila mwanaume rijali asingeweza kumuacha msichana kama Elizabeth, tena kwa sehemu kama hiyo, chumbani.

    James aliogopa, kwanza hakuamini msichana kama Elizabeth angeweza kukutana naye sehemu kama ile, kila alipomwangalia, wakati mwingine alihisi kama alikuwa ndotoni na kama si hivyo, basi alihisi kulikuwa na jini lililomtokea.

    Kulikuwa na wanaume wazuri, wenye fedha ambao kila siku walitamani kulala na msichana huyo, kwake, kila alipokuwa akimwangalia Elizabeth alijiona kuwa na bahati ya ngekewa ambayo hakutakiwa kuichezea kabisa.

    Mapigo yake ya moyo yalizidi kuongezeka, kwa mbali, kijasho chembamba kikaanza kumtoka, akajikuta akiwa kwenye wakati mgumu ambao hakuwahi kuwa nao tangu kuzaliwa kwake. Macho yake aliyakaza kumwangalia msichana huyo, alitaka kupata uhakika kama msichana aliyekuwa juu ya kifua chake alikuwa Elizabeth au mtu mwingine.

    “Elizabeth....” aliita James kwa sauti ya chini iliyoashiria hofu.

    “Unasemaje James...”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Why are you doing this?” (Kwa nini unafanya hivi?) aliuliza huku hofu ikiongezeka.

    “Because I love you James, please, don’t ask me such a question, I truly love you,” (Kwa sababu ninakupenda James, tafadhali usiniulize swali kama hilo, nikakupenda mno) alisema Elizabeth.

    Hakuwa na jinsi, alijiona akiwa amebanwa kila sehemu, akashindwa kujua ni kitu gani alitakiwa kufanya mahali hapo. Elizabeth alikuwa mtu pekee aliyekuwa akimpenda kutokana na hali aliyokuwa nayo, umasikini mkubwa uliomtesa kwa kipindi kirefu.

    Msichana huyo alijitolea kumsaidia mdogo wake, Glory aliyekuwa hoi kitandani. Hakumlipa kitu chochote kile, alikuwa radhi kutoa mamilioni ya shilingi ili mdogo wake awe mzima na kurudi kama zamani, hivyo kukataa kufanya mapenzi na msichana huyo aliona kama lingekuwa tatizo kubwa.

    Akajivika ujasiri mkubwa, akamkazia macho zaidi msichana huyo, hofu iliyokuwa moyoni mwake akajaribu kuitoa na kukishika kiuno cha Elizabeth, kilichofuata baada ya hapo ni sauti za mahaba na kelele za kitanda tu.

    Huo ukawa mwanzo wa uhusiano wao wa kimapenzi, kufanya ngono ikawa sehemu ya maisha yao, mara kwa mara walipotoka hospitalini, kitu cha kwanza kilikuwa kukumbatiana na kuonyesheana mahaba ya dhati tu.

    “James....”

    “Naaam!”

    “Nataka unioe....”

    “Nikuoe wewe?”

    “Ndiyo! Ninataka unioe James...”

    Walikuwa kwenye mahaba mazito, wakati Elizabeth akitoa maneno ya kutaka kuolewa, tayari alikuwa juu ya kifua cha James, alichanganyikiwa mno na hakuona kama kulikuwa na mwanaume sahihi wa kuweza kuwa naye zaidi ya James.

    “Mimi nikuoe wewe?”

    “Ndiyo James...naomba unioe...” alisema Elizabeth.

    James hakuzungumza kitu, alibaki kimya. Kitu cha kwanza kabisa kilichokuja kichwani mwake ni kujidharau. Alikuwa masikini mno, hakuona kama alistahili kumuoa msichana mwenye mvuto na mwenye pesa kama Elizabeth.

    Aliuliza mara kwa mara kama Elizabeth alimaanisha kile alichokuwa akikizungumza au alimwambia kama kumfurahisha kwa kipindi hicho.

    “Unamaanisha unachoniambia?”

    “Hakika! Ninahitaji uwe wangu milele,” alisema Elizabeth.

    “Sawa! Hakuna tatizo!”

    Hali ya Glory haikubadilika, bado alikuwa kama alivyofika. Madaktari walihangaika mno lakini hakukuwa na chochote kile kilichobadilika, bado aliendelea kupooza na kulala kitandani tu.

    Madaktari walihangaika usiku na mchana, wengine wakashindwa kulala na familia zao kwa ajili yake lakini pamoja na juhudi zote zile, matokeo yake ni kwamba binti huyo mdogo aliendelea kuwa vilevile jambo lililoleta hofu kubwa.

    “Nini kinaendelea daktari?’ aliuliza Elizabeth.

    “Bado hali ni ngumu, kama inawezekana, inatakiwa apelekwe hospitali nyingine.”

    “Ipi?”

    “Rechts der Isar.”

    “Ipo wapi?”

    “Jijini Munich nchini Ujerumani.”

    “Sawa! Hakuna tatizo!”

    Hawakutaka kumuona Glory akifariki dunia au akiendelea kuugua ugonjwa ule wa kupooza, Elizabeth aliamua kujitoa kwa kuamini kwamba kitu pekee ambacho kingempa furaha mpenzi wake ni kumtibu Glory mpaka pale atakapopona na kurudi kama alivyokuwa kipindi cha nyuma.

    Alijitahidi kwa nguvu zote, walipoambiwa kwamba Glory alitakiwa kupelekwa nchini Ujerumani, hakuwa na jinsi, akaahidi kulipia gharama zote. Mawasiliano kati ya hospitali hizo mbili yakaanza kufanyika, utaratibu ukaandaliwa tayari kwa kuanza safari ya kuelekea nchini huko.

    James hakuacha kulia, kila alipokuwa akimwangalia mdogo wake aliyekuwa hoi kitandani moyo wake ulimuuma mno. Kidogo Glory alipokuwa India aliweza kupata nafuu kwani hata kuzungumza, alijitahidi kufanya hivyo japo kwa sauti ya chini mno.

    James akafarijika, akaona kwamba inawezekana mambo yangekwenda kuwa mazuri endapo tu wangekwenda nchini Ujerumani kwa ajili ya matibabu zaidi. Baada ya siku mbili, safari ya kuelekea Ujerumani jijini Munich ikaanza.

    Ndani ya ndege, muda wote James alikuwa pembeni ya kitanda alichokuwa mdogo wake. Moyo wake uliumia mno, kila alipokuwa akimwangalia Glory, alisikia kitu chenye ncha kali kikiuchoma moyo wake.

    Elizabeth alikuwa pembeni yake akimfariji tu. Hakukukuwa na mtu mwingine yeyote yule ambaye angeweza kumfariji katika kipindi hicho zaidi yake, hivyo alihakikisha anakuwa naye karibu kila wakati.

    “Elizabeth! Hivi Glory atapona kweli?” aliuliza James huku akibubujikwa na machozi.

    “Atapona tu! Tumuamini Mungu!” alisema Elizabeth huku akimpigapiga James mgongoni.

    Ndege iliendelea kukata mawingu mpaka baada ya saa ishirini ilipoanza kutua katika Uwanja wa Ndege wa Munich nchini Ujerumani. Tayari gari la wagonjwa la Hospitali ya Rechts der Isar lilikuwa mahali hapo, walichokifanya ni kumshusha na kisha kumuweka garini humo na safari kuanza.

    Japokuwa katika maisha yake yote James alitamani mno kupanda ndege na kufika katika nchi yoyote barani Ulaya, ndoto yake ilitimia ila kwa wakati huo alifika katika moja ya nchi hizo huku akiwa katika huzuni tele.

    Hakuona raha kabisa ya kuwa Ujerumani, wakati gari likikatisha barabara mbalimbali za Ujerumani, macho yake yalitulia kwa Glory, alikuwa akimwangalia huku akiendelea kububujikwa na machozi tu.

    Hawakuchukua muda mreu wakafika katika eneo la hospitali hiyo ambapo mlango wa gari ukafunguliwa, machela ikaletwa na kupandishwa kisha kuanza kusukumwa kuelekea ndani ya jengo la hospitali hiyo.

    “Wir müssen unstreffenals ärztedieser wird derpatient,“ (Inabidi tukutane tuizungumzie hii hali ya huyu mgonjwa) alisema daktari mmoja huku akionekana kuwa na haraka.

    “Rufen sieandere ärzte, hierher zu kommen,“ (Waite madaktari wengine waje huku) alisema daktari mmoja mwenye miwani ya macho machoni, nywele zake zilikuwa na mvi, alivalia koti kubwa jeupe lililokuwa na kiplastiki kidgo pembeni ya kifua kilichoandikwa Dk. Zeus.

    Mara baada ya Glory kupelekwa katika chumba cha uchunguzi, jopo la madaktari saba likakutana ndani ya chumba kidogo kwa ajili ya kuizungumzia hali aliyokuwa nayo hata kabla hawajaanza kufanya upasuaji.

    Wakaiweka mezani ile ripoti iliyotoka nchini India na kuanza kuipitia kwa ukaribu zaidi. Walitaka kujua tatizo lilianzaje na madaktari wa India walifanikiwa kwa kiasi gani. Wakaanza kuichambua ripoti ile.

    “Uti wa mgongo umevunjika kidogo,” alisema Dk. Zeus.

    “Unahisi tunaweza kutumia muda gani?”

    “Mpaka apone?”

    “Ndiyo!”

    “Si chini ya miaka mitano.”

    “Mmh!”

    “Ndiyo hivyo! Hakuna kitu kibaya katika mwili wa binadamu kama kuvunjikwa kwa uti wa mgongo, mpaka kurudi na kuwa kama zamani, uhitaji muda mrefu mno na wakati huo wote, chakula chake kikubwa kiwe kongoro kwa ajili ya kuurudisha mti huu katika hali yake ya kawaida,” alisema Dk. Zeus, daktari bingwa wa upasuaji katika hospitali hiyo.

    “Sawa!”

    Hawakuwa na muda mwingi wa kupoteza, walichokifanya ni kuondoka chumbani mule na kuendelea na kazi zao. Moja kwa moja Dk. Zeus akawaita James na Elizabeth ndani ya ofisi yake na kuanza kuzungumza nao.

    Hakuwaficha, aliwaambia ukweli kwamba japokuwa mgonjwa huyo aliletwa hospitalini lakini bado uhakika wa kupona kwa haraka chini ya miaka mitano ulikuwa mdogo mno. Walipoambiwa hivyo, kila mmoja akahuzunika, matumaini ya Glory kupona haraka iwezekanavyo yakapotea kabisa.

    “Kwa hiyo tutatakiwa kusubiri kwa miaka mitano?’ aliuliza James huku machozi yakijikusanya machoni mwake.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ndiyo!” alijibu Dk. Zeus.

    Machozi yale yakaanza kububujika mashavuni mwa James. Aliendelea kuwa kwenye maumivu makali.

    ******

    Rasheed alishtuka kutoka usingizini, kitu cha kwanza kabisa alichokifanya ni kuchukua simu yake na kuangalia saa, ilikuwa ni saa tisa usiku. Uso wake ulijawa na tabasamu pana, ndoto aliyokuwa ameiota kipindi kifupi kilichopita kilimfanya kuwa na furaha mno.

    Aliota akiwa na msichana mrembo mno, msichana aliyemfahamu ambaye alikuwa naye siku chache zilizopita, Elizabeth. Kwenye ndoto hiyo aliota akiwa naye sehemu fulani ambayo hakujua ilikuwa sehemu gani, walikuwa na furaha mno na muda wote walikuwa wakibusiana kwa furaha, walishikana mikono na kuzunguka huku na kule na kila aliyewaangalia, aliyaona mapenzi mazito yakiwazunguka.

    Kama njiwa, walikuwa wamekumbatiana muda wote, kila kitu kilichokuwa kikiendelea kiliwapa furaha mno. Wote walikuwa mabilionea na wote walikuwa na mioyo iliyojaa mapenzi kiasi kwamba hakukuwa na mtu yeyote yule ambaye angewatenganisha.

    Ndoto hiyo ikampa mawazo mengi, akaanza kumkumbuka msichana huyo ambaye kipindi cha nyuma wala hakuwa kabisa mawazoni mwake, aliyeseka kwa siku nzima na kila alipoichukua simu yake kwa lengo la kumpigia, akaacha na kujikuta akisikilizia.

    Ilipofika saa tisa alasiri, akashindwa kuvumilia, hapohapo akajikuta akichukua simu yake na kumpigia Elizabeth kwa lengo la kuwasiliana naye. Alipojaribu kupiga simu, haikuwa ikipatikana kitu kilichomfanya kuwa na mawazo tele.

    Hakutaka kukubali hata mara moja, alichokuwa akikifikiria ni kwamba inawezekana alikuwa amepumzika hivyo alizima simu yake, alichokifanya ni kuvumilia, ilipofika saa kumi, akampigia tena lakini majibu yalikuwa yaleyale, simu haikuwa ikipatikana.

    Akashikwa na mawazo mengi, akakosa raha kabisa, kila alipokuwa akimpigia simu majibu yaliendelea kuwa yaleyale kwamba simu haikupatikana. Alichokifanya ambacho aliona kwamba kisingekuwa na tatizo lolote lile ni kumtumia barua pepe ili kama hakuwa nchini Tanzania basi aweze kuipata.

    Katika barua pepe hiyo alimwambia kwamba alitaka kuonana naye, alikuwa akitamani kuzungumza naye na hivyo ingekuwa vizuri kama wangekutana sehemu na kuzungumza.

    “Kwa sasa ni ngumu,” alijibu Elizabeth, haphapo Rasheed akajua kwamba mwanamke huyo alikuwa ‘online’.

    “Kwa nini vigumu?”

    “Nipo nchini India, nimepata tatizo kidogo.”

    “Tatizo gani?”

    “Kuna mdogo wangu anaumwa, alipooza hivyo hapa nimechanganyikiwa mno,” ilisema barua pepe aliyoandika Elizabeth.

    “Nakuja hukohuko, siwezi kubaki nyumbani na wakati upo huko,” alimalizia Rasheed.

    “Sawa! Ila keshoasubuhi tunaondoka kuelekea Ujerumani,” aliandika Elizabeth.

    Waliendelea kuwasiliana na mwisho wa siku Rasheed akaambiwa kwamba lingekuwa jambo zuri kama wangekutana nchini Ujerumani na kuzungumza. Moyo wa Rasheed ukapoa, ukatulia na akahisi burudiko kubwa moyoni mwake mithili ya maji yaliyokuwa yakimwagika kwenye maporomoko.

    Alichokifanya ni kujiandaa, ilikuwa ni lazima aelekee huko kuonana na msichana huyo. Ile ndoto aliyokuwa ameiota, aliomba Mungu iweze kutimia.





    Huo ndiyo kwanza ulikuwa mwaka wa kwanza na waliambiwa kwamba walitakiwa kusubiri kwa miaka mitano. Kilikuwa kipindi kirefu mno lakini hawakuwa na jinsi. Katika kila hospitali waliyokuwa wamepitia, waliambiwa kwamba Glory asingeweza kupona, angeendelea kuwa vilevile mpaka pale atakapofariki dunia.

    Japokuwa miaka mitano ilikuwa mingi sana lakini hawakuwa na jinsi walitakiwa kusubiri kwa kuamini kwamba uvumilivu wao mwisho wa siku ungewaletea matunda. Hawakuacha kulala pamoja, kila ilipofika usiku, walikumbatiana kitandani na mambo mengine kuendelea.

    Wakati Elizabeth akipata barua pepe kutoka kwa Rasheed alikuwa chumbani amekaa peke yake, alikuwa akiangalia mambo mengine kwenye mtandao, alitaka kuona jinsi dunia ilivyokuwa ikiendelea kwa wakati huo.

    Hapo ndipo alipoona barua pepe kutoka kwa Rasheed, alichokifanya ni kuifungua na kuanza kuisoma. Kwanza alishtuka, hakushtuka kupokea barua pepe bali kitu kilichomfanya kushtuka ni kuona akiambiwa kwamba alitakiwa kuonana na Rasheed.

    Hapo ndipo uzuri wa mwanaume yule ulipoanza kumjia kichwani mwake, alimkumbuka vilivyo, mara ya kwanza kukutana naye tu alihisi kwamba alikutana na malaika kwani mwanaume huyo alikuwa mzuri kupita kawaida.

    Huku akimfikiria Rasheed, hapo ndipo picha ya James ilipoanza kumjia kichwani mwake, alihisi moyo wake ukiwa kwenye mapenzi mazito kwa James kiasi kwamba hakutaka kumuona mwanaume yeyote yule akiliingilia penzi lake.

    Alichokifikiria ni kwamba inawezekana mwanaume huyo alitaka kuonana naye kwa ajili ya kuzungumzia biashara kwani ndivyo ilivyokuwa kila alipokuwa akikutana na mabilionea wengine.

    Ila kwa upande mwingine wa moyo wake, alikuwa na wasiwasi kwamba inawezekana mwanaume huyo alikuwa na kitu kingine tofauti na kufanya biashara. Hakutaka kuonyesha wasiwasi wowote ule, alimwambia kwamba alikuwa nchini Ujerumani kwa kuwa alikuwa na mgonjwa hivyo kama alitaka kuonana naye, basi angemfuata huko.

    “Mbona unaonekana hivyo mpenzi?” aliuliza James huku akimwangalia Elizabeth usoni.

    “Kivipi?”

    “Unaonekana una mawazo sana, tatizo nini?”

    “Hakuna kitu baby!”

    “Hapana bwana! Huwezi kuwa hivyo halafu kusiwe na kitu! Naomba uniambie,” alisema James huku akimsogelea zaidi Elizabeth na kisha kuipelaka mikono yake begani mwa msichana huyo.

    “Kuna mtu amenitumia barua pepe.”

    “Anasemaje?”

    “Anataka tuonane!”

    “Nani? Mwanaume, mwanamke?”

    “Mwanaume. Ni mfanyabiashara mmoja mkubwa nchini Morocco, alinisaidia kipindi nilichokwenda kutangaza mavazi Morocco, anataka kuonana nami, sijajua anahitaji nini,” alisema Elizabeth huku akionekana kukosa raha.

    “Usijali mpenzi, litakuwa jambo la kibashara.”

    “Mmhh!”

    “Nini tena?”

    “Sidhani mpenzi! Kweli mwanaume aonane na mwanamke hivihivi tu!”

    “Inawezekana! Onana naye tu.”

    Baada ya siku mbili Rasheed akafika nchini Ujerumani ambapo moja kwamoja akapanga sehemu nzuri ambayo angeweza kuonana na Elizabeth ili kumwambia ukweli kile kilichokuwa kikimtesa moyo wake kwa kipindi hicho.

    Mawasiliano yalikuwa yakiendelea kama kawaida, siku iliyofuata, walichokifanya ni kuonana katika Mgahawa wa Mamarita uliokuwa katikati ya Jiji la Munich. Kitendo cha kumuona Elizabeth tu, akahisi moyo wake ukiridhika, kila alipokuwa akimwangalia, aliuona uzuri aliokuwa nao kipindi cha nyuma ukiwa umeongezeka zaidi.

    “Umependeza sana, uzuri wako umeongezeka maradufu,” alisema Rasheed huku akimwangalia Elizabeth kimahaba.

    “Nashukuru sana.”

    Walizungumza mengi mpaka pale Rasheed alipoona kwamba huo ndiyo muda maalumu kwa ajili ya kulitoa dukuduku lake. Kwanza akaanzia mbali, tangu alipomuota msichana huyo, uzuri aliokuwa nao na jinsi walivyokuwa wakifurahia pamoja.

    “Sijaelewa unamaanisha nini! Ni ndoto au kuna jingine?” aliuliza Elizabeth.

    “Ndiyo! Jingine lipo.”

    “Lipi?”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Rasheed akameza mate tayari kwa kulitoa dukuduku la moyo wake.

    Macho ya Rasheed yalitulia usoni mwa Elizabeth, uzuri aliokuwa nao kipindi cha nyuma uliongezeka na kuvutia zaidi, kila alipomwangalia, moyo wake ulizidi kumpenda zaidi. Hakukuwa na kitu kingine alichokuwa akikitaka kwa msichana huyo zaidi ya kuwa mpenzi wake tu ili baadaye wafunge ndoa na kuishi pamoja.

    Alimeza mate na kumkazia macho msichana huyo mrembo ambaye wala hakuonyesha dalili zozote za kujisikia aibu. Alijua namna ya kuzungumza na mwanaume, hakutakiwa kuonewa aibu hata mara moja kwani kitendo cha kufanya hivyo ni kumpa ushindi juu ya kile alichotaka kukifanya.

    “Ninakupenda Elizabeth!” alisema Rasheed kwa sauti ndogo.

    “Unanipenda mimi?”

    “Ndiyo! U msichana mrembo mno, nimeshindwa kuvumilia na nimeamua kukwambia ukweli na ndiyo maana nimesafiri kutoka mbali kuja kukwambia hili,” alisema Rasheed.

    Elizabeth alikaa kimya kwa muda, akaanza kumwangalia Rasheed usoni, alionyesha kile alichokuwa akikisema, alimaanisha kutoka katika mtima wa moyo wake, alichokuwa akikisikilizia ni jibu kutoka kwa msichana huyo mrembo.

    Elizabeth hakuwa na haraka ya kujibu, alitulia tu huku akichukua grasi ya juisi na kunywa juisi iliyokuwemo. Uso wake ukaanza kuonyesha tabasamu pana lililompa matarajio Rasheed.

    “Umechelewa Rasheed.”

    “Hapana! Sijachelewa, nimekuja muda muafaka.”

    “Umechelewa. Ninaye mtu nimpendaye, ungeniambia tangu kipindi kile, nahisi ningekukubalia, bali niliporudi nchini Tanzania tu, kila kitu kikabadilika baada ya kukutana na James,” alisema Elizabeth.

    “James ndiye nani?”

    “Mwanaume wangu mpya.”

    “Ana hela kama mimi? Ana akili kama mimi?”

    “Rasheed! Fedha si mapenzi, ukiwa na fedha ni rahisi kununua ngono la si rahisi kununua mapenzi,” alisema Elizabeth huku akionyesha tabasamu pana.

    Rasheed akabaki kimya, hakuamini kile alichokuwa amekisikia kwamba alichelewa na wakati huo Elizabeth alikuwa na mwanaume mwingine. Moyo wake uliumia mno, hakuamini kile alichokisikia, alitamani kama kingekuwa ndoto lakini ukweli ni kwamba vyote alivyovisikia, alivisikia katika ulimwengu halisi, haikuwa ndoto hata mara moja.

    “Elizabeth.....”

    “Ndiyo hivyo Rasheed. Sitaki kukuumiza baadaye kwa kuwa nilikuficha ukweli, ni bora uumie sasa hivi huku ukiufahamu ukweli. Nisamehe kwa hilo,” alisema msichana Elizabeth, tabasamu halitoka usoni mwake.

    Hakuwa na jinsi, japokuwa alijitahidi sana kumwambia msichana huyo namna alivyokuwa akimpenda lakini bado msimamo wa Elizabeth ulikuwa uleule kwamba hakutaka kuwa naye kwa kuwa alikuwa na mwanaume mwingine aliyempenda kuliko wote.

    Alichokifanya Rasheed ni kurudi nchini Morocco huku moyo wake ukiwa kwenye maumivu makali, kukataliwa na Elizabeth kilikuwa kitu ambacho hakutaka kukubaliana nacho kirahisi, aliamua kufanya jambo moja, mwisho wa siku ampate msichana huyo.

    *****

    “Kila kitu tumefanya, sidhani kama tunatakiwa kufanya zaidi ya hapa,” alisema Dk. Zeus.

    “Kivipi?”

    “Tumejitahidi kumtibu, hakuna tunachoweza kufanya zaidi, tumemaliza kila kitu, cha msingi, naomba mrudi nyumbani, ataendelea kupona kadiri siku zitakavyokwenda mbele,” alisema Dk. Zeus.

    “Cha kuzingatia?”

    “Mumpe sana kongoro ale, zitasaidia sana kuurudisha uti wa mgongo katika hali ya kawaida,” alisema

    Huo ndiyo ulikuwa mwisho wa kila kitu, madaktari walijitahidi kwa miezi mitatu mfululizo kumtibu Glory na mwisho wa siku waliona ni bora kumruhusu kurudi nyumbani kwani hawakutegemea kama kungeweza kutokea muujiza mwingine zaidi ya hapo.

    Hawakuwa na jinsi, baada ya siku mbili, safari ya kurudi nchini Tanzania ikaanza mara moja. Siku ambayo walikuwa wakifika uwanja wa ndege jijini Dar es Salaa, tayari idadi kubwa ya watu walikuwa mahali hapo, walipata taarifa juu ya kila kitu kilichokuwa kikiendelea.

    Walimpenda Elizabeth, alikuwa msichana maarufu, alijulikana zaidi ya alivyokuwa akijulikana rais wa nchi hiyo. Uwanjani hapo, waandishi wa habari hawakuwa mbali, walifika mapema sana kwa ajili ya kupiga picha kile ambacho kingeweza kutokea uwanjani hapo.

    Ndege ilipotua na kusimama, wakateremka huku kukiwa na watu wawili waliowasaidia kukishusha kiti alichokuwa amekalia Glory. Wakaanza kutoka nje ya uwanja ule ambapo mara baada ya kuingia ndani ya jengo la uwanja huo, wakapigwa na mshangao baada ya kuwaona watu wengi wakiwa wamekusanyika, walipoonekana tu, kila mtu akaanza kwenda kule alipokuwepo.

    Pasipo msaada wa walinzi waliokuwa mahali hapo hali ilionekana kuwa mbaya sana. Walinzi hao wakawazuia watu na kuwaambia wafuate utaratibu uliotakiwa kufuatwa. Miale ya kamera iliendelea kumulikwa na waandishi wa habari ambao walikuwa bize wakipiga picha matukio kadhaa.

    “Anaendeleaje?” aliuliza mwandishi mmoja.

    “Nani?” aliuliza Elizabeth.

    “Huyu msichana.”

    “Anaendelea vizuri, si mnamuona kidogo anatabasamu.”

    “Tunafurahi kuona hivyo!:

    Hawakutaka kukaa sana uwanjani hapo, walichokifanya ni kuondoka kuelekea nyumbani. Huko, James hakutakiwa kurudi alipokuwa akiishi bali safari hiyo alichukuliwa na kupelekwa nyumbani kwa Elizabeth.

    Maisha yake yalibadilika ghafla, hakuamini kama kweli katika kipindi hicho alikuwa na msichana bilionea ambaye aliyabadilisha maisha yake kwa asilimia mia moja. Muda mwingi alibaki akimshukuru Mungu kwani kila kilichokuwa kikiendelea kwake kilionekana kuwa muujiza mkubwa.

    “Utaishi hapa mpenzi,” alisema Elizabeth.

    “Mmmh!”

    “Nini tena?”

    “Nitaweza?”

    “Kwa nini usiweze?”

    “Mtaa wa matajiri!”

    “Ila si hata wewe ni tajiri pia!”

    “Hahaha! Sawa!”

    Hakuwa na jinsi, kwa wakati huo msichana Elizabeth ndiye aliyekuwa akisimamia kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Glory akapewa chumba maalumu kwa ajili ya kukaa humo pia kukakodiwa maaktari maalumu waliokuwa na kazi ya kumhudumia Glory kila siku na hata kuibadilisha mipira ya haja.

    Mapenzi yalikuwa motomoto, Elizabeth alijisikia uhuru na kila siku katika maisha yake hakukuwa na mtu aliyempenda na kumthamini kama alivyokuwa James. Kwake, hakukuwa na mtu aliyeuteka moyo wake vilivyo kama mwanaume huyo.

    Kila siku, kama njiwa walikuwa pamoja, James akawa huru, akawa anatumia mali za Elizabeth alivyopenda. Ili kuonyesha ni kwa jinsi gani alikuwa akimpenda mpenzi wake huyo, akamuingizia kiasi cha shilingi bilioni moja katika akaunti yake benki.

    James akachanganyikiwa, fedha zile zikaongeza mapenzi zaidi na kumchanganya vilivyo. Elizabeth hakutaka kujali sana, alichokiangalia kwa kipindi hicho ni mapenzi ya kweli tu kutoka kwa mwanaume huyo.

    Elizabeth na James ndiyo waliokuwa gumzo nchini Tanzania, vyombo vya habari viliwaripoti sana kwamba ndiyo walikuwa watu waliopendana kuliko watu wote nchini Tanzania. James akaanza kuupata umaarufu kwani kitendo cha kuwa karibu na msichana huyo tu tayari kilibadilisha maisha yake.

    Mbali na upendo aliokuwa akipewa, bado Elizabeth alikuwa na mawazo tele kuhusu mtoto, hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya ili aweze kupata mtoto, hakuwa na furaha kabisa, kila alipokuwa, mawazo mengi yaliusumbua moyo wake.

    Hakukuwa na kitu alichokitamani sana kwa kipindi hicho kama mtoto, hata kama alikuwa tajiri mkubwa ambapo alistahili kuitwa bilionea, alikuwa na jina kubwa lakini bado mtoto alionekana kuwa kila kitu katika maisha yake.

    Hakutaka kumuweka wazi James kwa kuona kwamba angeharibu kila kitu, alibaki kimya huku akimuomba Mungu kila siku naye apate mtoto na hatimaye kunyonyesha kama wanawake wengine.

    “James....” alimuita mpenzi wake.

    “Naam!”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kuna kitu ninaomba tukifanye,” alisema Elizabeth.

    “Kitu gani?”

    “Ninahitaji unioe, ninahitaji uwe baba wa watoto wangu,” alisema Elizabeth, kwa mbali machozi yalianza kumlenga mara baada ya kukumbuka kwamba hana uwezo wa kupata mimba.

    “Mbona unalia?” aliuliza James huku akimwangalia Elizabeth usoni.

    “Inaniuma.”

    “Inakuuma nini tena? Nitakuoa mpenzi.”

    “Kweli?”

    “Ndiyo! Nakuahidi hilo, nitakuoa tu,” alisema James huku akijiapiza viapo vya kila aina kwamba angemuona Elizabeth.

    Hakujua kile kilichokuwa kikimliza Elizabeth mahali hapo hakikuwa kuolewa kama alivyofikiria bali kile kilichomtoa machozi kilikuwa ni kutokupata mtoto. Moyo wake ulimuuma mno, hakuamini kama yeye ndiye aliyekuwa akipitia katika maisha hayo.

    Hakuwahi kutoa mimba katika maisha yake, alipokwenda hospitali, madaktari hawakuona tatizo lolote lile, hakuwa mgumba, kitu kilichowashangaza wote ni kwa ninimsichana huyo hakufanikiwa kushika mimba?

    James alimbembeleza na kumbembeleza, hakupenda kumuona msichana huyo akilia, kwake, alijiona kuwa faraja kubwa katika maisha ya msichana huyo. Elizabeth alifarijika lakini bado moyo wake ulimuuma mno.

    Kuna wakati alitamani kumwambia James ukweli kwamba asingeweza kupata mimba hata kidogo lakini kila alipotaka kufanya hivyo, alisita, hakuwa tayari kuweka wazi kwani kama angefanya hivyo basi ilikuwa ni lazima angemuacha kwa kuona kwamba hakukuwa na mwanaume aliyekuwa radhi kuwa na mke asiyekuwa na uwezo wa kuzaa.

    “Inaniuma sana James...”

    “Inakuuma nini tena jamaniiiiii?”

    “Basi tu, inaniuma mpenzi.”

    “Niambie, usiogope, kipi kinakuuma?” aliuliza James.

    “Glory, kwa nini Mungu ameamua kumtesa hivi?” aliuliza Elizabeth, alibadilisha kila kitu.

    “Atapona tu, tufanye kile walichosema madaktari,” alisema James.

    Jambo hilo halikuweza kubadilika moyoni mwake, alichukuana na James na kwenda sehemu mbalimbali kwa ajili ya kufurahia maisha tu, huko, walifanya mambo mengi huku waandishi wa habari wakiwa beneti kuwafuatiliwa.

    Waliwatoa sana katika magazeti na mitandaoni, kila walipokuwa, kulikuwa na waandishi waliokuwa bize wakiwafuatilia kama ilivyokuwa kwa Kanye West na Kim Kardashian. Magazeti mengi yakawa yakiandika kuhusu wawili hao, kupitia mgongo wa Elizabeth, naye James aliendelea kuwa maarufu.

    Wakati hayo yote yakiendelea, wakiyafaidi mapenzi na ndipo jamaa mmoja akaibuka, huyu aliitwa Hamisi, kijana aliyekuwa mzuri wa sura ambaye alivuma sana kutokana na kazi ya mitindo aliyokuwa akiifanya.

    Mwanaume huyu kipindi cha nyuma alifanikiwa kuwa mpenzi wa Elizabeth, alipeana naye mapenzi motomoto lakini pale ambapo msichana huyo alimhitaji kwa sana, yeye hakuwa na taarifa naye, hapo ndipo walipoachana.

    Kipindi hicho Hamisi alikuwa ameibuka na lake, aliweka wazi kwamba alikuwa na picha za utupu za msichana huyo, aliwahi kumpiga wakati walipokuwa jijini Arusha. Watu wengi wakatamani kuziona picha hizo, marafiki wengi wakamsisitizia Hamisi aziachie ili kila mtu aone kile kilichokuwa ndani ya mwili wa Elizabeth.

    Baada ya kuzuka kwa tetesi hizo, hapo ndipo maneno mengine yalipojengwa kwa kusema kwamba msichana huyo alikuwa malaya wa kutupwa. Yalikuwa ni maneno yenye uchungu sana ambapo mara baada ya Elizabeth kuyasikia, alihisi moyo wake ukiumia mno.

    Huo wala haukuwa mwisho, maneno hayo yakaenda mbele na kusema kwamba msichana huyo hakuwa na uwezo wa kuzaa kwa sababu alitoa mimba nyingi mno hivyo kuharibu mfumo wa uzazi. Hayo ndiyo yaliyomuuma zaidi, hakuamini kama kitu hicho kingejulikana kwa wote, mtu aliyemshuku alikuwa Hamisi tu.

    “Huyu atakuwa Hamisi,” alisema Elizabeth huku akilia.

    Alichokifanya ni kwenda kushitaki polisi tu juu ya zile picha za utupu alizotaka kuziachia katika mitandao ya kijamii. Polisi walichokifanya ni kumuita Hamisi na kumfungulia kesi kwa kile alichotaka kukifanya na hivyo kujitetea kwamba hakuwa na picha hizo.

    “Anazo.”

    “Una uhakika kuna siku tuliwahi kupiga picha za namna hiyo?” aliuliza Hamisi, walikuwa kituo cha polisi.

    “Hatujawahi lakini anazo.”

    “Hapana! Siwezi kufanya hivyo.”

    Elizabeth alikosa raha kabisa, kila alipokuwa akimwangalia Hamisi, alimchukia kupita kawaida. Tetesi za kushindwa kupata mtoto kwa kuwa alikuwa malaya ndizo zilizokuwa zikienea kipindi hicho, waandishi wa habari waliandika na kuandika, wengi walimhuzunikia sana na wengine, hasa wale waliokuwa wakimpenda kulia.

    “Jamani! Mimi si malaya!” alisema Elizabeth huku akilia, alikuwa akizungumza na waandishi wa habari.

    “Ni kweli hauwezi kupata mtoto?’ aliuliza mwandishi mmoja.

    “Jamani...jamani....” alishindwa kuzungumza kitu, alishindwa kulijibu swali hilo, hakutaka kuzungumza tena, alichokifanya ni kuingia ndani ya gari na kuondoka zake.

    Hakukuwa na kipindi kigumu kilichowahi kutokea katika maisha yake kama hicho, kila alipopita, alihisi watu wakimnyooshea vidole na kumwambia kuhusu suala hilohilo la kupata mtoto, akakesha akilia, alikosa amani kabisa katika maisha yake.

    James hakumuacha, alikuwa akimfariji kila siku kwa kumwambia kwamba suala la kuwa na mtoto, Mungu ndiye aliyeamua nani awe naye na nani asiwe naye. Japokuwa maneno hayo yalimfariji lakini bado aliendelea kulia mno.

    Alimuomba sana Mungu tena kwa kutoa sadaka, maadui zake waliendelea kumsema vibaya huku maneno yakiongezeka na kuitwa malaya na watu wengi waliokuwa wakimchukia huku wengine wakianza kuweka picha kwenye mitandao wakiwa na watoto wao na kuandika maneno yaliyoonekana kama dongo kwake.

    “Mchungaji naomba uniombee....” alimwambia mchungaji Kimaro wa Kanisa la Praise And Worship.

    “Unahitaji nini Elizabeth?”

    “Nahitaji kuwa na mtoto.”

    “Hilo tu?”

    “Ndiyo!”

    “Usijali! Mungu anatenda mambo yake kwa wakati, ila inakupasa uolewe kwanza,” alisema mchungaji huyo.

    “Nitapata mtoto kweli?”

    “Mwamini Mungu! Utapata tu. Hakuna linalomshinda aliye juu,” alisema mchungaji huyo.

    Kidogo maneno hayo yakamfariji kwa kuona inawezekana kwamba Mungu alitaka aanze kupata mtoto akiwa ndani ya ndoa, alichokifanya ni kuzungumza na James na kumwambia dhamira yake kubwa ya kutaka kuolewa naye.

    Alijua kwamba msichana huyo hakuwa na uwezo wa kupata mtoto lakini hilo hakutaka kujali, kila kitu alichokiona ni kuhusu moyo wake. Sababu haikuwa fedha, sababu haikuwa maisha mazuri, alichokifikiria kwa wakati huo ni mapenzi mazito aliyokuwa nayo kwa msichana huyo.

    Alimpendasana Elizabeth, hakukuwa na mwanamke aliyekuwa na thamani kubwa moyoni mwake kama aliyokuwa msichana huyo, suala la kumuoa, wala halikuwa tatizo kwake, akakubaliana naye kwani pia alipofikiria kuhusu wema aliomfanyia, alijisikia kuwa na deni kwa msichana huyo.

    “Umekubali?’ aliuliza Elizabeth.

    “Nimekubali mpenzi,” alijibu James.

    Alichokifanya ni kuwaambia marafiki zake wa karibu kwamba alitarajiwa kuolewa hivi karibuni hivyo alimkaribisha kila mtu kuhudhuria harusi hiyo ya kipekee. Watu hawakuamini, walimfahamu sana Elizabeth, ilikuwaje akubali kuolewa kirahisi namna hiyo na wakati wanaume wengi walijaribu kufanya hivyo ila alikataa.

    “Mbona umeamua ghafla?” aliuliza

    “Basi tu! Nimeamua nifunge ndoa, si unajua nishakuwa mtu mzima sasa!” alisema Elizabeth.

    Taarifa za harusi hiyo zikaanza kuandikwa sehemu mbalimbali, watu wengi wakatamani kuifuatilia harusi hiyo iliyowafanya watu maarufu kutoka nchi nyingine na kwenda nchini Tanzania kwa ajili ya kushuhudia tu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tetesi zikaanza kusikika kwamba harusi hiyo ilitarajiwa kufanyika ndani ya ndege, wengine wakasema kanisani lakini kuna watu wengine walisema kwamba harusi hiyo ilitarajiwa kufanyika katika moja ya boti kubwa na ya kifahari ambayo iliagizwa kutoka nchini Italia, kila mtu alisema lake.

    Elizabeth hakutaka kuzungumzia juu ya mahali ambapo harusi hiyo ingefanyika, alichokitaka ni watu kusubiri na kuona kwa macho yao. Shela la bibi harusi likaagizwa kutoka nchini Ufaransa huku suti ikiagizwa kutoka nchini Uholanzi, kwa kifupi, maandalizi yalikuwa yakiendelea vizuri.

    Kila kitu kilichokuwa kikiendelea James hakuamini kabisa, hakuamini kama kweli alikuwa akienda kuwa mume wa Elizabeth, msichana maarufu na bilionea barani Afrika. Taarifa zile zilisambazwa kama upepo, japokuwa ulikuwa kimebaki kipindicha mwezi mmoja lakini kila mtu akawa na hamu ya kushuhudia hausi hiyo ambayo ilionekana kama kulazimishwa na msichana Elizabeth.







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog