IMEANDIKWA NA : ZUBERI MARUMA
*********************************************************************************
Simulizi : Penzi La Fukara Mateso
Sehmu Ya Kwanza (1)
UTANGULIZI
Kila ninapojaribu kufumba macho yangu nikusahau uwa nashindwa.
Siuamin moyo wangu kama kweli ipo siku ungeniacha
Tena katika kipindi ambacho nakuitaji zaidi.kipindi ambacho ndo ningetakiwa nile matunda ya masomo yako
Leo hii Mimi na wewe tumekuwa kama paka na panya
Lazima nilipize kwa ulilolitenda?!
************
Uso wake ulikunjamana kwa hasira,mapigo yake ya moyo yaliongezeka kila muda ulipokuwa ukipotea,
Akalifungua kabati lililokuwa Mbele ya macho yake na kupeleka mkono ndani ya kabati lile,akawa anatafuta kitu katikati ya nguo
Akakipata
Ilikuwa ni bastola ndogo,akaiangalia kwa sekunde kadhaa na kuipachika kibindoni
Akalifunga vizuri kabati lile
Hakika moyo wake ulijaa majonzi,simanzi
,sononeko,maumivu tele yaliushambulia moyo wake....
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kama kulia alishalia sana mpaka machozi yakamkauka!
maumivu makali yalikishambulia kichwa chake! yamkini ni kutokana na msongo wa mawazo ama kitendo chake ya kulia sana.....
kulilia mapenzi.
Akalifata droo lake akalifungua na kutoka na kalamu na karatasi akakaa katika meza na kuanza kuiandika barua,
huku machozi mepesi yakiloanisha mashavu yake na baadhi ya matone yakiangukia karatasi lile...
barua ile aliianza kwa kuiandika hivi:
"Kwako mpenzi SHONAIZAR!,
najua u mzima wa afya!,mimi kifikra sipo vizuri!
sidhani kama utaniuliza kwa nini!
sababu nadhani waijua
ila tambua kama mapenzi ni hisia!, hisia zangu zilikuwa kwako , uliniteka kifikra sikutaka nichomoke moyoni mwako, ulinifanya mfungwa katikati ya moyo wako, sikuona mwanamke kwa uzuri afikiaye umbo lako...
Ulitumia udhaifu huo kuntesa mwenzako, ni ahadi ngapi ulini ahidi kwamba utonisaliti?!, ni mara ngapi ulinambia kwamba UNANIPENDA sana?!,
kumbe wewe ni mwanahizaya ulojaa unafki eeh!?!...au kisa mimi ni fukara?,au kisa sina pesa?!
shone penzi langu kwa gharama yoyote lazima litalipwa!, machozi yangu niyatoayo kwa sababu yako yatakugarimu my x!,
tambua kama uliunyakua moyo wangu kwa kuni adaa kwamba unanipenda,
malipo yako nitakunyanganya roho yako,...
leo nayachukia mapenzi
kumbuka wewe ndo ulinifanya niyapende!
nakumbuka kipindi kile kwa mara ya kwanza tulipo onana, ndo kwanza ulitoka masomoni TABORA GARLS na kuja kijijini kwetu kufanya utafiti wa mimea na majani ukiwa na wenzako
mimi nikiwa mchungaji wa Mbuzi ndo kazi nlostaili kwa kipindi kile.
mbona marafiki zako wote walikukimbia pale nyoka mwenye sumu kali alipokugonga?
ZUBERI nikajitolea SHONAIZAR kukusaidia!
kosa langu lipo wapi hapo?
najuta kukufahamu
CHOZI LANGU LAZIMA LILIPWE
niliamua kukuchukua mpaka nyumbani kwangu nilipo kuwa naishi peke yangu
nikaanza kuku hudumia kwa madawa asili mpaka ukapona....
Malipo yangu yalikuwa nin?!
kama si kufungwa?
ulishindwa kunsaidia pale marafiki zako walipokuja na wazazi wako wakanikamata heti nimekuteka!!
msaada wangu ukawa adhabu kwangu ,kwa mara ya kwanza mchunga mbuzi kutoka kijijini nikaingia mjini nikiwa chini ya ulinzi mkali!
nyumbani kwangu pakawa segerea!
yani ung'atwe na nyoka nkuchukue nkutibu nionekane nlikuteka?! ila yote nilivumilia,
ulikuja kuniangalia!
na dhamana ukanitolea!, ukisema wazi kwamba mimi ndiye niliyekusaidia! nadiriki kusema msaada wako ndo ulikuwa huo kwangu!
mpz nishkuru kwa ilo!
kwa kunitoa mahabusu na kunitafutia kazi DAR!
sawa pengine labda kwa kuwa sikujua lengo lako mpaka pale ulipontamkia kwamba UNANIPENDA wewe ndo ulinambia siyo mimi niliyekutamkia!.
.kama kweli ulikuwa unanipenda iweje leo hii uje unsaliti?! utamu wa penzi lako ugeuke shubiri kwangu?
naapa my! lazima penzi langu utalilipa!...
hata ikibidi kwa ncha ya upanga!
ila sitokuacha mzima ama zangu ama zako!
SHONE mpenzi kumbuka!!!.....
nilikukubali kwa kuwa u! mwanamke mrembo,mwenye wajihi wa "black beuty" na macho malegevu kama unasinzia!,
dimpozi mashavuni, ulijaliwa miguu minene ya bia!, ni vigumu kwa mwanaume kukataa ombi lako!...
ni mara ngapi ulililia kifuani kwangu?,
ukinielezea jinsi unavyonyanyasika kwenu?! kisaa.....
hata ulivyonielezea stori yako ya maisha, iliniuma mpenzi sikusita kulia kwamba mama yako alishafariki na sasa unaishi na mama wa kambo,
anayekunyanyasa kwa masimango bila huruma kukupatia! sikuweza kuzuia machozi kunitoka!
shetani mkubwa wewe!
nilikulilia nikikuonea huruma kwa nini nisingekuacha ukateseka? nakuchukia wewe mwanamke! nawachukia wanawake wote.....
sababu ikiwa ni wewe kahaba mmoja!
nitaridhika nitakapo ugawanya ubongo wako! kwa furaha sitosita kuula kwa ukatili ulontendea nipo tayari kufungwa,nipo tayari kunyongwa,pindi nikisababisha mauti yako....
Nakumbuka ile siku ulikuja kwangu huku unalia!,
kukwangalia nikashindwa majonzi kunishika sikuvumilia!
ndipo ulipoanza story yako kunisimulia!
kwamba baba yako amekataa ada kukulipia!!!
kutokana na maneno ya mama yako wa kambo...my love!
mwanamke nlokupenda unakumbuka nilikujibu nini?!
najua unakumbuka!
kwamba mimi nitakusomesha!,
sertificate na hata diploma!
si NILIKUPENDA?!
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
shetani mkubwa wewe!, nilidiriki kufanya kazi kwa nguvu ili hata degree upate! no sikujua ZUBERI mimi,
tenda wema uende zako shukran usiingoje!
shukran ya punda ni mateke ,nawe ni binadamu si punda, ila una roho mbaya zaidi ya shetani!
ulifurah pale ulipofukuzwa ulikuja kuishi kwangu!
si kama mke wangu!
Latasha!!!
kama dada yangu, mara chache tukimtumia SALAMA kwa madai kwamba mimi ni wako ukimaliza degree ndo tupate watoto
mwanahayuni mkubwa wewe
WATOTO?!!,...
SITOKUSAHAU abadani asilani
nishakula yamini kukuondoa duniani,uhai wako ni halali yangu!,
sikutishi ila nakwambia ukweli, nakumbuka siku ya graduesheni yako ya kumaliza diploma hata ukunambia!
unajua kwanini?!!...
unajua ulichokifanya!
PATRICK! PATRICK! PATRICK!
PATRICK,ndo kisa cha yote haya?
au kwa kuwa yeye ana pesa kunipita mimi? ,ndo alifaa kuwa mpenzi wako etiee?! nakuuliza wewe kabla sijakufikia labda uniwahi wewe!,
penzi la kweli alifi,likifa aliozi,likioza alinuki!,likinuka basi unukia vizuri
ila langu kwako limeoz linanukia uvundo! unajua kwa nini bibie? kwa kuwa ile siku ya gradueshen yenu marafiki zangu ndo walonipigia simu wakanambia uendi kwenye mahafali ya mpenzi wako?
wakinibeza nije nione utombo wako!,
kwa kuwa nilijiamini kwako, sikukubali kusikia lolote baya kutoka kwako.
kufika kwako nilishangaa!
hata wewe lazima ungeshangaa
yah sikuzoea maneno ya shombo kutoka kwako, ila siku hiyo niliyapata, ukujali maumivu moyoni kiasi gani nayoyapata, eti nipige hesabu nimekugharamia kiasi gani utanlipa!
nililia!!!....
nililia kwa kuwa Nakupenda shonaizar,kwa Mara ya Kwanza nikaanza kuionja ladha ya shubiri katika penzi lako.
Ule usemi penzi ni Tamu kama asali akageuka na kuwa chungu hata zaidi ya shubiri...
..
Yah nililia, nililia kwa kuwa NAKUPENDA, fukara hana thamani sasa iweje uniharibie maisha yangu!?,
mapenzi ayalazimishwi kwa kulitambua ilo nikakubaliana na ukweli nikiangalia maisha yangu sikupenda UFUKARA nilipenda utajiri ila si niliachana na wewe?!
iweje uwatume wanaume waniteke?
wanitese?
kwa mangumi na mateke?,
kosa langu lipi hasa?!
ni uamuzi wako sawa!
ulishughudia yote yale, nkatupwa ufukweni mwa bahari....
hata pale nilipotupwa kandokando ya bahari kama si wavuvi ni nani angeniokoa?
mwanayuhani mkubwa wewe!,
Leo NIKUSAMEHE?,
siwezi labda, labda uanze kuniua wewe ama zangu ama zako!....
hiyo ni tisa,
kumi ni pale GLADS mwanamke alokuwa kama mboni ya macho yangu
japo nakiri hata robo ya uzuri wako hakuufikia! lakin alikuwa ndo mfariji wangu iweje UMUUE?
si yeye tu kila mwanamke niliyetokea kuwa naye aliishia kuwa maiti! kwa nini!?
ukupenda mimi niwe na furaha kisa pesa ulizokuwa nazo!?, kwani nani asiyejua kuwa uliwauwa wazazi wako ili mali zao zibaki chini yako?
usiulize nimejuaje ila naisi ni ushauri wa PATRICK japo mama yako alikutesa akustaili adhabu hii,
kwa kifo ulichompatia hata MUNGU sidhani kama atakusamehe, hatakama yeye akikusamehe!!! ila sidhani kama itatokea ila kwa nini ulitenda yote haya?,
japo mimi nakaa katika kibanda wewe wakaa katika hekalu la urithi, japo mimi nipo peke yangu wewe upo na walinzi lakini damu yako ni halali yangu
MWANAHIZAYA wewe
kila muda fikra zangu zinanikumbusha unafiki wako pindi tukiwa kitandani!
sauti yako ya mahaba ukiwa kwangu kifuani!
kwamba UNANIPENDA na utoniacha asilani!
kumbe hivyo vyote vilikuwa ni usanii?!!
Mwisho jiandae kwa ujio wangu nakuja kukumaliza labda wewe uniwahi.
nakutakia kila la kheri
ni mimi my x wako fukara nisiye na thamani!...
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ZUBERI MUSA MARUMA
MWISHO WA BARUA:
**********
Kijana yule alimaliza kuiandika ile barua yake ndefu yenye kuchukua kurasa nne
akaikunja vizuri na kuiweka katika bahasha yake na kutoka
akaelekea mpaka posta akaituma kwenda kwa SHONAIZAR mwanamke katili na aliyeweka kisasi cha kumaliza!!!...
Baada ya kuituma barua ile akatoka taratibu posta!
kichwani bado mawazo yalirindima wakati akiwa anaelekea barabarani mbele yake aliona gari nyeusi ilokuwa na tinted katika vioo vyake!
akuitilia shaka kabisa gari ile!
alipofika usawa wa gari ile kwa ghafla walichomoka vijana wawili wakambeba na kumtupia garini
wakafunga mlango na kuiondoa gari kwa kasi!,
Ilikuwa ni tukio la haraka
na la ghafla! gari likapotea!
kwa mwendo mkali! watu wakabaki wakishangaa! bila ya kujua la kufanya....
fukara miye nisiye na nguvu!,katika sayari hii ya viumbe wakatili na wasio hata na lepe la huruma nani angeniokoa?
sikuwa na ndugu! je nani angenitafuta?!,
yah ni kweli hata serikali isingejua juu ya utekwaji wangu nani angeitaharifu?,
hali ya kuwa hata viumbe wachache waloshughudia nikibebwa mzobezobe!
na gari lile walibaki wakishangaa kwa kushika mdomo kama kushika mdomo kule ndo kutoa msaada!
makubwa!!!
sikuwa jasiri kuacha kupokea kipigo kikali ndani ya gari ile nzuri,
Je ni nani angeuona ukatili ule hali ya kuwa vioo vyote vilizungushiwa tinted?!
ndani ya gari lile kulikuwa kuzuri,na kusafi ila kulichafuka
yah! damu za mwili wangu ndizo zilizochafua ndani kule,
eti vile viumbe vilizidi kunipiga wakidai nimechafua gari yao!
Duniani kuna mambo!!!
Mwisho wa safari ile yakuogofya ilikuwa ni katika nyumba ya msichana mrembo SHONAIZAR,
yah nilijua tu!
kwamba muhusika wa kutekwa kwangu atakuwa ni yeye,kwa kuwa ndiye hasimu wangu mkubwa hapa duniani yah si duniani tu pengine na kesho khaera!
niliingizwa katika chumba kimoja kipana! kisicho na kitu zaidi ya utelezi na chini utelezi ule ulijumuishwa na chumvi na mimi si nilikuwa na majeraha ya mavidonda katika mwili wangu?
nilijuta kutoka katika tumbo la mama yangu AMINA bint ATHUMANI.
Bora ningeachwa nipumzike peke yangu
lah! mashababi wawili walojengeka kimazoezi walikuwa eneo lile na waya wakinisulubu kama mwanaume katili mwenye makosa lukuki!,
hata kama ningelia sauti yangu ingefika wapi!!!?...
Niligugumia kwa maumivu,nilikata tamaha ya kuiona kesho yangu!
"HIVI HUYU MWANAMKE NI KOSA GANI NILILOMKOSEA MWANAHARAMU HUYU!?"
Nilikuwa na haki ya kujiuliza ili swali lakini sikuwa na haki ya kulitambua jibu lake kwa siku hiyo....
mwanga mngaavu katika pande za macho yangu ulianza kufifia,giza lilianza kushika hatamu,sikuweza kuendelea kustahimili maumivu yale,mwili ulilegea na atimaye nkapoteza fahamu
ndipo vijana wale "nguvu kazi ya taifa!" walipoacha kunipiga na kutoka!
masaa mengine badaye ndipo mwili na roho vilianza kushabiana!, maumivu makali nliyasikia kwa mbali yakija kwa kasi kutokana na kipigo nlichopigwa..
Fahamu zilikuwa zinanirudia! na hatimaye kwa shida sana macho yangu yakafumbuka na kukubali kuupokea mwanga ule mdogo wa "chublight" ndogo chumbani mule!
mwanga ambao katu haukudiriki kuyaumiza macho yangu, maskio nayo yalijinasibu kupokea sauti...
ila ubongo wangu aukukubaliana na sauti iliyoziskia nkabinua shingo yangu kuielekeza ule upande sauti ilitokea...
ni bora ukatili ule nliotendewa ni kiwa chumba cha mateso kuliko ukatili huu,
macho yangu ayakukubaliana na ukweli wa yale waliyoyaona!
"is this true?!"
nilijiuliza kwa lugha geni sijui labda nlipatia kwa mwanamke ambaye ukumpenda hapo sawa! ila si kwa SHONE,
binti huyo nilimpenda hapo kabla!
Kabla ya kisanga hiki kilichojaa utata ndani yake, chembechembe hai za upendo wangu juu yake bado zilikuwa zikiishi, masikio yangu yalipokea miguno! yah miguno ya kimahaba!
macho yangu yalishindwa kuendelea kushughudia tendo lile mahsus kwa wanandoa kati ya SHONE na PATRICK!!!...
moyo wangu uligawanyika katikati na kuchuruzika damu ndani kwa ndani!
yah!...
ilo nililitambua baadaye sana kumbe kwa kuwa nilikuwa bado NAMPENDA
eeh!?!!
LAKINI KWA NINI ANIFANYIE YOTE YALE?!!!
niliwaza, mtoto alijua kulalamika nilishindwa kuangalia utumbo ule walipomaliza mwanaume aliingia bafuni kuoga! SHONE akiniangalia kwa dharau akanifata akiwa kanibetulia mdomo akiwa kajifunga kaupande cha khanga
"Unajua kwa nini nimefanya hivi?" akusubiri nijibu akaendelea
"ZUBERI staki nikupe mateso ya mwili tu! no! mpaka mateso ya moyo hapa utayapata!"
Nilitaka kumuuliza kwa nini anfanyie yote yale! lakini akunipa muda huo akawa tayari kashaondoka kwa mikogo ya kuvutia yah ndo maisha niliyoishi hayo.
nilirudishwa katika chumba changu cha mateso nkaendelea kula dozi!.Sasa nlishayazoea maisha hayo,mwili ulishakuwa sugu kwa kipigo.Waenga walinena
"maisha safari ndefu" yamkini waliongopa! kwangu maisha yalibaki nusu kama si robo! muda wowote Izrael angentembelea!.
yah! siku hiyo nilikuja kutolewa mzobazoba,nkajua ndo mwisho wa uhai wangu nkapelekwa mpaka sebuleni nilipowakuta walinzi wa nyumba ile wakiwa na silaha kali za moto katika kochi alikaa SHONE na bastola yake....
pembeni yake alikuwa boyfrand wake PATRICK,binti yule alifura kwa hasira,yah macho yangu yakatua kwenye meza ile ya vioo iloundwa kisasa na kuleta tashhiti ya uzuri wake katika mboni ya macho ya aitazamaye!.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
juu yake kulikuwa na ile BARUA,barua niliyoiyandika kwa mbwembwe na vitisho tele!
yako wapi?!,
ni wazi moyo uliingia ubaridi!,meno mdomoni yakagongana,mkojo bila kujielewa ukanitoka!
Taharuki!!!
macho ya shonaizar yalimuwiva kwa hasira!,aliyarudia yale makaratasi kuyasoma,sikuweza kuyazuia machozi kun'dondoka.
"ZUBERI mpenzi unafikiria kuniuwa mimi?"
alinioji huku viganja vyake vya mkono vikilipapasa shavu langu kwa m bembelezo wa kiburi,mdomo kaukunja kwa dharau!
"paaaaa!" kibao kitakatifu kikatua katika shavu langu.
ghadhabu,hasira zilishampanda kitendo cha mimi kukaa kimya alikitafsiri kama dharau! japo watu usema kibao cha mtoto wa kike hakiumi ni sawa lakini si kibao cha binti yule!
kwani aikukawia kuona nyotanyota zikielea hewani!
"KABLA UJANIUA ZUBERI WANGU MI NTAKUUA KAMA ULIVYOANDIKA KWENYE BARUA YAKO TENA UTAKUFA TARATIBU SANA KWA MATESO MAKALI....."
SHONE aliongea bila mzaha katika uso wake! sura yake ya urembo alojaliwa ilibadilika na kuwa ya kikatili
Nikajikakamua nikamuuliza!
"sawa SHONE nipo tayari kufa! tena kwa mateso makali lakini haya yote yanatokana na nini?"
tofauti na matarajio yangu SHONE alincheka sana tena sana akachukua plaizi akawa amrisha walinzi wawili wanishike mdomo bila ganzi,plaizi akaingiza mdomoni alipoitoa ikatoka na jino ambalo lilikuwa ni lizima,ambalo lilikuwa alitingishiki,lilikuwa imara!,damu zikajaa mdomoni maumivu yakatawala akacheka tena na kutamka
"zuberi my love! nimekungoa jino mdomoni coz usiongee staki uniulize ulize maswali kwanza ingepaswa nikukate ulimi kabisa mwanaharamu wewe!"
SHONE alinijibu akiwa kakaa katika mapaja ya PATRICK walinzi wawili wananbeba na kunrudisha chumbani! wakansukuma nkadondokea chumbani
"hivi huyu jimwanamke nimemkosea nini hasa?"
swali ili lilizidi kusumbua kichwa changu, katika chumba kile kisicho na kitu chochote zaidi ya sakafu iliyotawala maji ya baridi yenye chumvichumvi ndipo sehemu nilipoitajika kulala ndani kukiwa na ndoo ya kuwekea uchafu wangu,
mlo kwa siku nilipata mara moja tena usiku ugali mdogo bila mboga! si bora kufa kuliko mateso haya? niwafate wazazi wangu uko walipo? ila huko ndani akukuwa na kitu ambacho kingeniwezesha kujitoa uhai,si kamba kwamba ningejinyonga,wala kisu kwamba ningejichoma mpaka kifo kilintenga.
"MUNGU kwa nin wanipa majaribu haya?"
niliwaza kabla sijapata jibu kipi cha kufanya ili ntangulie kumbe nilikuwa na shati? nkatabasamu sala zangu za mwisho nkaanza kusali nikalirukia dirisha na kuanza kujitaidi kulifunga shati lile
"kitanzi" juu ya paa nkafanikiwa
"MUNGU BABA NIPOKEE SINA THAMANI YA KUENDELEA KUISHI PENZI LANGU NDO CHANZO CHA MATATIZO HAYA SIPO TAYARI KWENDELEA KUONA MAUMIVU HAYA NIPOKEE MUNGU WANGU NA UNSAMEHE AMEEN"
Niliomba machozi yakintiririka,mwili wote uliloa jasho baada ya ile sala fupi NKAJIACHIA,
macho yalintoka pima!,haja kubwa na ndogo vilintoka bila kutarajia, mwili ukaisha nguvu...
watu walovaa nguo nyeupe kwa shangwe wakawa wakinpokea....
Macho yalikuwa mazito kufunguka,pua zilinusa harufu kali za madawa
Ghafla macho yalipokelewa na mwanga mkali katika chumba kile
'Nipo wapi?!'. Nikajiwazia bila kupata jibu
kilikuwa ni chumba kipana
nilichugundua kuwa ni wodi nilijaribu kugeuza shingo upande wa pili nikalakiwa na maumivu makali ya shingo.
"ZUBER umeamka? MUNGU aibuniwe,mpz kwa nini ulitaka kuwa mbali na mimi? kwa nini ulitaka kuutoa uhai wako my love?"
Nikashtuliwa na sauti ndogo ilojaa hisia ndani yake
alikuwa ni SHONAIZAR!!!
khaa!!
nilipigwa na butwaaa shone alikuwa akilia huku akiniuliza,mikono yake laini akiiweka kifuani mwangu.
"NI NINI KINACHOENDELEA HAPA MBONA MI SIELEWI?"
nilijiuliza huku nikiwa na mshangao wa waziwazi kichwani mwangu..dakika hiyo hiyo nesi akaja:.....
"ooh my GOD kazinduka?"
nesi alitahamaki huku akienda kumuita daktari wakati huo huo SHONE alichukua hotport ilokuwa na "mtori" akanimiminia na kuanza kuninywesha.
sikuwa tayari kufungua mdomo japo alinibembeleza huku akiniomba msamaha lakini sikuwa tayari.
SIKUMUAMINI!
Nilijua mda wowote angetumia njia yoyote kuniangamiza hata kwa kuniwekea sumu katika chakula kile shetwani yule asingeshindwa.
Dakika chache badaye daktari aliwasili na kuanza kupimapima,akimuomba SHONE ampishe niliendelea kukaa pale hosptali chini ya ulinzi mkali huku mara kwa mara bint yule akija kuntembelea na kuangalia hali yangu.
akiwasisitizia madaktari juu ya uzima wangu.
Wiki tatu badaye niliruhusiwa juu ya ulinzi mkali,nkapakiwa kwenye gari kurudishwa nyumbani.
moyoni nilikuwa na mawazo sana,
Mawazo juu ya uko niendako...je bado ningeendelea kupata mateso makali kutoka kwa mwanamke aliyenijali hospitalin?!
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
jibu lilikuwa rahisi sana kwani tukiwa ndani ya gari binti yule aliniangalia kwa kimapembe kwa jicho kali!,
Uchangamfu wa hospitali hakuwa nao nikang'amua kuwa mateso ni vile vile!
pasina ya kupata jibu,.Ya kipi anitesacho? je ni kosa gani asa nilomkosea?! Niliwaza....
Nilipofika nyumbani nikamkuta PATRICK kakasirika balaa.
"sasa ZUBER si unataka kujiua? sasa mimi ntakuua nilisema unatakiwa ufe tarrrratibu sana! siyo ivyo ulivyokuwa ukitaka!"
aliongea kijana yule mwenye mafanikio katika maisha yake,akanpiga na kitako cha bunduki yake kichwani
"MUDIGO na ASAMOLE mpelekeni chumba cha mateso akateswe mpaka akiogope kifo MUDI akikisha ulinzi wa uyo maiti kwamba ajidhuru 24 HOURS pasikosekane mtu wa kukaa naye saivi akabembee katika feni apate kuitengeneza adabu yake kwetu akaaa!"
Aliongea kijana yule PATRICK kwa ukali nikanyanyuliwa kama mkosaji na kuingizwa chumbani nikafungwa mikono juu ya feni na manyila ilokata mikono yangu kwa maumivu makali feni ikawashwa ikanzungusha kizunguzungu kilinishika,
ila fukara mimi ningefanya nini?!!!....
mikono ilivimba ila hiyo haikuwa kichocheo cha mimi kuteremshwa
MAPENZI ndo chanzo cha matatizo yote haya!
KUMPENDA SHONE!!!
Nilikuwa nimejipalia mkaa kwenye uso wa chotara wa kizungu mweupe,
baada ya mateso yale makali nkaletewa chakula cha jioni nile kama kawaida ulikuwa ni ukoko wa ugali na vichwa vya samaki
MUDI alonletea chakula kile akanipa na barua ikabidi niifungue nianze kuisoma
sikuamini macho yangu ilitoka kwa SHONAIZAR taratibu nikaanza kuisoma....
"Kwako kipenz cha moyo wangu bila shaka u mzima! wa afya tele dhumuni la barua hii ni kukujibu barua yako yenye kichwa cha habari
(PENZI LA FUKARA MATESO)
yah ni kweli ZUBERI ila naomba univumilie tambua NAKUPENDA sana! tena zaidi ya sana mpenz wangu!
nakupenda zaidi ya wazazi wangu,nakupenda zaidi ya kitu chochote katika dunia hii mapenzi ni hisia ZUBER huu upendo nikupendao ndo chanzo cha mateso yako nakutesa hivi kwa kuwa NAKUPENDA...."
heee! nikaguna kwa mshangao kama alijua lazima nitaguna akaendelea
"usigune! wala usishange mimi kukwambia hivyo mpz wangu japo unateseka kwa sababu yangu hata mimi naumia sana lakini ni lazima uteseke hivyo my buu!
uwezi epuka mateso haya nipo tayari kwa HUKUMU yoyote utakayoitoa juu yang lakini sina jinsi mpz................
Lakini hata kama wewe ungekuwa ni mimi nami ndo wewe UNGENTESA zuber
NI KWA NINI NAKUTESA?
unatamani sana ujue jibu ilo! ila
NAKUTESA KWA KUWA NAKUPENDA
'Unanitesa kwa kuwa unanipenda?!!!..'
Nikawaza uso wangu ukiwa na butwaa...nikaendelea kuisomaaa
Najua wajiuliza na maana gani ila kwa sasa fahamu hilo mengine utajua badaye
ila kimoja nataka nikusisitizie uhai wako ni muhimu kwa uhai wangu,na mateso yako ni muhimu kwa uhai wako
fahamu hayo tu ni mimi my x wako SHONAIZAR!
nilishusha pumzi ndefu sikuielewa kabisa ile barua SHONE alikuwa na zaidi ya upendo kwangu kivipi?
kutesana ndo kupendana?,
ananipenda zaidi ya wazazi wake?
mbona sielewi hapo?
mateso yangu ndo uhai wangu kivipi?
nikashusha tena pumzi ndefu sikuielewa kabisa ile barua
eti! SHONE alinipenda na si kunipenda tu alikuwa na zaid ya upendo kwangu! kama ndo ivyo kwa nin alintesa?
tena mateso makali? maswali kibao yakazidi kutiririka katika kichwa changu.
"lazima nifanye kitu! siwezi kuendelea kukaa kibwege bwege humu ndani bila ata kujaribu kujikomboa?...."
niliwaza kabla sijagutushwa na sauti mawazoni mwangu sauti tamu,sauti ya SHONE!
"ZUBER mpz wangu usijaribu kutoroka tambua mateso yako ndo uhai wako NAKUPENDA zuberi!"
heeee!!!...
nilibaki na mshangao!,mkubwa ila nikaipuuza ile sauti ambayo aikuwa na mantiki yoyote katika masikio yangu
kwa haraka nikajinyanyua na teke kali mpaka kwa MUDIGO, lililomfanya akayumba,nkamuwah kwa ngumi nzito yenye ujazo wa kutosha mdomoni akatema jino!
nikaiwahi silaha ilokuwa hatua chache na kuikamata barabara.nkamuamrisha aweke mikono yake juu akatii
nkamsogelea taratibu na kwa umakini, lakini ghafla kama umeme alijigeuza na teke kali lililoipiga mikono yangu
silaha ile ikaruka hatua chache toka tulipo sisi kwa haraka nikakaa sawa mkao wa mapigano tukaangaliana kila mmoja akimtegea mwenzake afanye kosa la kuitazama silaha ile kosa ambalo lingemgharimu.
uzur mmoja sote tukagundua ilo
"UNAYAWEZA?!"
Akaniuliza nilishachafukwa na roho kwa jeuri nikamjibu
"Nikuulize wewe!"
ghafla mlango ukafunguliwa na vijana 6 wenye SMG mkononi wakaingia na kunizingira!
Vijana wale walonizingira na silaha walipoona nimepwaya! wakanvamia na kuanza kunipiga kwa kunchangia!
"STOOOOP mnafanya nini?"
ilikuwa ni sauti ya kike ambayo niliitambua vyema kuwa ni ya SHONE!
"Msimpige mleteni hapa sebuleni ntamwadhibu mwenyewe...."
aliendelea kufoka mwanamke yule akiwaambia walinzi ambao sikujua kama walikuwa wanajeshi,migambo au polisi wakanibeba mzobezobe mpaka sebuleni na kunibwaga chini!
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
SHONE akansogelea mkononi kashika rungu aina ya "mama mkanye mwanao"
"ZUBERI kwa nini wataka kuntoroka nimekukosea nini love wangu!...."
akalishusha rungu lile katika vidole vyangu vya miguuni nilihisi maumivu makali akatabasamu akaendelea
"my love naongea na wewe kipenzi changu kwa nini unaleta fujo nyumbani kwangu!?"
akalishusha tena sasa vidole vikawa vinasagika sagika
"ZUBER wangu au kwa kuwa NAKUPENDA?"
akanipiga tena mimi sikujibu kitu nikikuwa niking'ata vidole kwa maumivu niliokuwa nikiyapata ningejibu nini wakati nilitaitika?
baada ya mwanamke yule katili NILIYEMPENDA kunipiga na kutosheka vidole vyangu vya miguuni na rungu lake nilirudishwa katika chumba changu ambacho ndimo kilikuwa makazi yangu,nilijilaza huku maumivu yakinipanda mguuni.
nusu saa badaye nilisikia majibizano ya risasi kitendo kilichopelekea yule mlinzi alokuwa akinilinda atoke nje mbio silaha yake ikiwa mkononi kabla mvua ya risasi ijamminikia kifuani mwake.
nilijaribu kunyanyuka lakini nikashindwa kutokana na maumivu makali ya mguu. nkaishia kudondoka chini kama mzigo,ikabidi nijiburuze kwa kutambaa hivyo hivyo kutoka chumbani kule nilipoufikia mlango nikachungulia nje nikitarajia kuwaona maaskari ila tofauti na matarajio yangu nikawaona walinzi wakipigana wenyewe kwa wenyewe
furaha yote ikatoweka katika ngome ile kulikuwa na walinzi kumi 5 nje na 5 ndani hivyo walinzi wa geti la nje walikuwa wakipambana na walinzi wa geti la ndani
KUNA NINI KIMETOKEA!?
nilijiuliza pasina kupata majibu SHONE na mumewe PATRICK hawakwepo.
mpambano wa tupa nitupe risasi ukaendelea....
Mpambano wa tupa,nkutupie risasi uliendelea na hatimaye walinzi wa tatu! wa geti la ndani walitunguliwa na walinzi wa geti la nje,
wale wawili walobakia katu hawakurudi nyuma kusamli amri mpaka na wenyewe walipogeuka majina na kuitwa "maiti!" wale walinzi wa nje walokuwa na kiongozi wao alokuwa kavaa "kininja" sikuweza kumtambua ila nilihisi alikuwa ni mwanausalama
Ninja yule alinisogelea akanionesha ishara ninyanyuke nikisaidiwa na walinzi wale ambapo sikujua walitokanaje na mwanausalama yule wakanipakia katika gari
"ninja" akawapa fedha kwenye begi lililotuna wakafungua geti "ninja" akalitoa gari kwa speed!
sikujua napelekwa wapi! katika safari ile sote tulikuwa kimya kila mtu akiwaza kivyake! ukimya ule ulinipa nafasi ya kujipa maswali yaso na majibu!
'yule "ninja" ni nani? kwanini kaniokoa? kama ni mwanausalama kwa nini asiwakamate wale walinzi na badala yake awaonge fedha? mbona yupo kimya aongei kitu? ananipeleka wapi? ni mwema au muovu?'
Rundo la maswali tata yalikitekenyua kichwa changu! ila skupata majibu bado nilikuwa kifungoni na skuwa na budi kutulia kuona kitakachotoke.
tulikatiza mitaa kadhaa mpaka katika nyumba moja ya kifahari yenye ulinzi ule ule wa walinzi kumi,
geti mbili nje ndani,tukaingia ndani tulipopokelewa na sebule nzuri
hakukuwa na mtu aloishi katika vyumba vile vya ndani ila palikuwa pasafi na pakuvutia machoni
"ninja" akaketi kwenye sofa na kuiweka bastola yake mezani kisha akaanza kujifungua ushungi ule alojifunga
ghafla nilipigwa na butwaa!,mshangao ukiuvaa uso wangu
kumbe "ninja" yule alikuwa ni bibie "SHONAIZAR"
furaha yote ikatoweka,uso ukauvaa uoga,kumbe nilikuwa bado nipo kifungoni? kifungo cha mapenzi ama kweli ngombe wa maskini hazai,binti yule katili alikuwa akiniangalia kwa tabasamu pana moyo wangu ulinienda mbio!!!
nilitetemeka,meno yakinicheza kwa hasira,hasira kuu.taratibu SHONAIZAR akaufungua mdomo wake....
SURA YA PILI
KUFUMBULIWA KWA FUMBO
"ZUBERI najua unanichukia sana ila Mimi NAKUPENDA zaidi ya kitu chochote ZUBER na mapenzi yangu kwako ndo yapelekayo maumivu haya uyapatayo my love
nadhani unakumbuka matatizo yalipoanzia kule kijijini ulipoamua kuniokoa baada ya kuumwa na nyoka mwenye sumu kali na wenzako kukimbia ukanichukua na kunitibu ukiniweka kwako
ulikuja kukamatwa na kuishia segerea unajua sababu?!
ujui nini kipo nyuma ya pazia Zuberi...
ujui!!!
mimi ni mtoto wa kwanza katika familia ya mzee YEZIAN familia yetu ni ya kawaida yenye kipato cha kati
baba yangu ni mfanyakazi katika kampuni moja ya "tour" hivyo mimi nilitokea kupendwa na bosi wa kampuni ya baba yangu aitwaye PATRICK na ndo alikuwa akinisomesha na ndo nilikuwa nikiishi naye....
msema kweli ni mpenzi wa MUNGU ukweli SIKUMPENDA ila ningefanyeje? pindi nikiwa
"field" kule kijijini kwenu na kuumwa na nyoka ukaamua kunchukua bila kujua kuwa jamaa huyo alijua baada ya kuambiwa na wanafunzi wengine walonikimbia....
stupid man!!!
yeye ndo alokufunga kabla mimi sijakutoa kwa dhamana,kitendo cha mimi kukutoa kilimuumiza sana PATRICK na kuamua kunfukuza ndipo nlipokuja tukaishi sote ZUBERI ukakubali kunsomesha yamkini ukijua nimefukuzwa nyumbani baada ya wazazi wangu kukataa jukumu ilo
baada ya kufukuzwa na dhalimu yule!
ila PATRICK hayupo kama unavyomfikiria ana genge la ualifu na ni miongoni mwa vibaraka wa kundi la "mafia" nchini kwetu,CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
na pia anamiliki kikundi chake cha ulinzi ivyo kudhihirisha ukatili wake akawateka wazazi wangu akiitaji nirudiane naye lasiivyo angewaua,kwa mapenzi yangu mazito kwako sikukubali,ndiyo maana hata kwenye barua nilikwambia
"NAKUPENDA ZAIDI YA NIWAPENDAVYO WAZAZI WANGU"
ni kweli aliwauwa wazazi wangu na kuwatupa kandokando ya fukwe......
alipofika hapo SHONE alinyamaza na kuanza kulia
sikumbembeleza!!!
kwani bado nilikuwa na hasira juu yake kwani sikujua sababu ya kuntesa akaendelea....
"Baada ya kuwauwa wazazi wangu tena kikatili sikuweza kwenda popote kushtaki sheria si kaikamata?!
Nikaiachia serikali ifanye uchunguzi wake ila baada ya vitisho sana na kuapa kukuua ilibidi nimkubalie kulinda uhai wako,
ila akahisi ntakuwa na uhusiano wa siri na wewe ikabidi akuteke tena ikanilazimi mimi ili kukulinda NIKUCHUKIE, ilo nilifanikiwa"
Japo nilikuwa nakutesa vile Zuberi moyo ulikuwa unaniuma sana ningefanyaje mimi?!.....
Macho ya SHONE yalikuwa mekundu kwa kulia alijikaza akanyamaza akaendelea na simulizi yake....
"ZUBERI,PATRICK ni katili,ni muuaji ana miliki kikundi cha uhalifu,na cha ulinzi kila baada ya miezi sita upeleka na kupokea walinzi wa kutosha wengine uwaingiza katika ualifu na wengine uwa katika ulinzi wa kawaida nami nilishapitia katika mafunzo haya kwa vipindi vitatu nkiwa na maana mwaka mmoja na nusu,
mafunzo haya ndo niliyotumia kukuokolea wewe,kama PATRICK aliweza kuwauwa wazazi wangu angeshindwa kukuuwa wewe? hata barua yako alipoisoma alijua mimi na wewe kurudiana isingewezekana.
akujua mimi nilichofikiria juu yake
nakupenda ZUBER ila tambua PATRICK yupo nje ya nchi wale walinzi wa nje nilipanga nao mpango wale walinzi wa ndani walikataa ndo vita ile ikazuka pale, hii ndo nyumba nilofanikiwa kuijenga kwa fedha nilizo muhadaa yule fedhuli ila hapa si salama lazima tukimbilie nje ya nchi kwa usalama wetu na fedha za kutosha kaa pumzika nikaangaikie usafiri nakupenda ZUBER..."
Hasira yote iliyeyuka,chuki yote ilifutika,fumbo lote la rundo la maswali lilifumbuka,upendo wangu juu YA SHONE kama uyoga ukazaliwa
naam!
Nikamkumbatia,sikutaka kumuachia,naye akanipa ushirikiano.tulisahau hatari ilokuwa mbele yetu,
katu atukujua kuwa nyumba ile tayari ilishazingirwa na wazee wa kazi,
nilizidi kumpapasa naye akigugumia kwa utamu,tayari alishabadilika uso wake ukiitaji kitu kingine nami nilikuwa tayari kumtimizia pasipo kujua vijana wa kazi "team patrick" walishawafyeka walinzi wetu wakiwa na silaha nzito kifuani LAITI TUNGEJUA?!!!
Mimi nilizidi kumshughulikia mpenzi wangu! na niwakati nikianza kumchojoa nguo tuliposikia kishindo nje!
ghafla kama umeme SHONAIZAR aliruka na kuikamata bastola yake mkononi,hisia zetu zote zilikata! mbele ya hatari?!
binti yule akantupia silaha ndogo ilhali ata kuitumia mchunga mbuzi mie sikujua! nikabaki nimemtumbulia macho! kwa haraka SHONE akalisogelea dirisha na kuchungulia nje.
salaaaleee!!!....
hakika mshangao aliouonesha baada ya kuganda na kutupa silaha chini,uliniogop
esha,nami kwa haraka nikasogelea dirisha na kuchungulia.
kulikuwa na watu "mathalani" wasopungua 10 wote walikuwa na silaha nzito! kifuani wakiwa wamezaa kombati za mabaka mabaki ya kijani kama wavaavyo wanajesh wa JWTZ
"kum(tusi)mamake! hawa waseng(tusi) wametukuta mama yangu!!!"
SHONE alitukana yamkini alipwaya ni wazi atukuweza kupambana na kikundi kile ambacho sasa chote kiliingia ndani na kuangaika kuvunja mlango wa pale sebuleni
SHONE kwa sekunde kadhaa akaangalia juu kama anawaza mara akaparamia meza na kupanda juu yake akagusa mlango wa singbord ile ghafla ukafunguka akajirusha ndani yake
nami sikusubiri kuitwa nikampa mkono akaukwapua na kunivuta juu wote tukawa ndani tukaanza kutambaa ili tusiguse bati kutoka nje ya nyumba ile.
singbord ile kwa bahati nzuri ilikuwa muunganiko chumbani kuelekea nje baada ya kufika nje ya chumba kile tokatokea karibu na jiko tukatokea dirishani tukaruka na kuanza kukimbia tukiruka miili ya maiti ambao walikuwa ndo walinzi wetu tukaingia katika gari na SHONE akaitoa kwa spidi kelele za gari lile ndizo zilizowashtua maadui na wao wakatoka nje haraka na kuingia katika gari yao.
gari mbili corola na mandoline zilikuwa barabarani kila dereva akionesha uwezo wake,kwa mantiki nilitegemea aghalabu labda SHONE angeelekea polisi au palipo na usalama nikashangaa akiacha lami na kuelekea njia ya kwamtei barabara ya vumbi
watu barabarani wakipiga mayowe ya ushangiliaji ni wazi sisi tulionekana wahalifu dah ilikuwa tabu
KIMBEMBE TENA?
Kila hatua moja SHONE alopiga MANDOLIN lile lilizidi mkaribia,
vimbelembele maeneo kama haya awakukosekana baadh ya bodaboda walianza kupiga mbinja huku wakifata mando ile kwa nyuma na baadhi yao wakijaribu kutukinga kwa mbele!
SHONE alikuwa kama kichaa alochanganyikiwa akujali wala kupiga breki kitendo kilichowatoa bodaboda wale mbele yake watu walikuwa wengi kama mashughuda,
naam vigingi vya kimakundi makundi vikaundwa na kuachwa nyuma wakisimulia tukio lile huku wausika wakizidi kukata mbuga na wanafki wachache wakifata nyuma wale majambazi kila mara walipiga bastola juu kutawanya wingi wa watu.
tuliiacha kwa mtei na kuifata barabara ya msaranga nkazidi pigwa na butwaaa!
"we mwanamke tunaelekea wapi?"
nikamuuliza kwa hasira,SHONE akujibu alizidi kanyaga mafuta ghafla akakata mitaa miwili mitatu na kusimamisha gari
"naomba ZUBER ushuke!"
aliongea pasina mzaaa
"what?" nilipigwa na butwaaCHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
SHONE akunijibu kitu akafungua mlango na kunipiga busu kwa haraka akanskumia njee
"wacha nikafe mwenyewe zubeee kimbiaaaaa"
niliskia sauti ya SHONE kwa mbali sikuamini macho yangu sikuwa na muda wa kupoteza maeneo hayo nkakimbia mpaka katika kibanda kimoja nkajificha ghafla nkaliona MANDOLINE lile likitokea nami sikubaki nyuma baada ya MANDOLINE kutoweka katika macho yangu kwa kukimbia na tahadhari nikaanza kuelekea upande ule ni wazi hata majambazi wale waliushangaa uamuzi wa SHONAIZAR kukimbilia huko.
Ni wazi alijua asingeweza kuishi tena aliona bora akafie msituni kuliko kufia mikononi mwa PATRICK kiumbe katili,kisicho hata na chembe ya ubinadamu taratibu nilishughudia SHONAIZAR akiiacha barabara ya msaranga na kuelekea LANGONI panapo msitu mnene,msitu wa maajabu (rejea:jini la mapangoni) kuutambua msitu huu.
taratibu MANDOLINE likaanza kuifikia gari ile,watu walishatoweka na sasa walibakia mkimbizwaji na mkimbizaji wakiingia taratibu katika msitu ule mnene.
hapo majambazi wale wakaanza kuitupia risasi gari ile katika matairi ghafla gari la shone likapinduka.
SURA YA NNE
MVULE WA AJABU:
KILIMANJARO:
Ulikuwa ni msitu mnene ulotawala wanyama wakali,ulikuwa ni msitu uloshamirh ujangili na ilikuwa ni kipindi tembo walipouwawa sana ndipo ndipo serikali ilipo ongeza wanajeshi wengi wa maliasili kwa lengo la kupambana na ujangili huo
ni katika kipindi icho wakati SHONE na majambazi walovaa uniform za kijeshi wakitupiana risasi,milio ile iliwashtua wale maliasili na kuanza kusogelea eneo lile ilipotokea milio ile! kabla awajagutushwa na mlio wa mkimbizano wa magari kwa haraka ikabidi wajifiche katika vichaka na kuangalia kule mlio wa magari ulipotokea walishughudia gari mbili zikija kwa speed!
corola likiwa mbele huku mandoline likisaga mbuga huku walioko kwenye mandolin wakifyatua risasi katika corola ile ndogo!,bado mshangao ulitawala katika vichwa vyao macho yao bila kuambizana kwa wakati mmoja wote walizikagua zile kombati aikuwawia ugumu kutambua kuwa ni nguo feki kwanza azikuwa na namba,
walibaki na butwaa mpaka pale,corola ya SHONE ilipopigwa tairi ya mbele na kukosea mwelekeo ikapinduka,tairi zikaangalia juu.
"SHAMBULIA!!!..."
Kwa wahka alokuwa kiongozi alitoa amri ilotekelezwa mara moja,risasi zisizoesabika zikacheua kutoka katika magobore ya maaskari wale,lakini majambazi hawakuwa nyuma kujibu mashambulizi
"ndiyo ovar....karibu na mvule wa ajabu ovar!,...394,yah...ambulence na nguvu kazi ovar...."
aliongea afande mmoja akiomba msaada ilikuwa ni vita kama ya nusu saa hivi mpaka mwisho maliasili wale walishinda na kuwaweka nguvuni majambazi wale.
maaskari kutoka kituo kikuu mjini MOSHI dakika zilezili wakajipanga makundi wengine wakilisogelea gari la SHONE na wengine wakiwachunguza maiti wale na kuwapiga pingu majeruhi wakapakiwa katika ambulance moja maiti wakafungwa katika manailoni maalumu.
kule SHONE alitolewa katika gari lake hali yake ikiwa mbaya akapakiwa naye katika ambulance huku mapigo yake ya moyo yakipiga kwa mbali,mdomoni hewa ya oxgeni ikimsaidia.
"Eeh! huyu si mke wa PATRICK?!" Nesi mmoja alitamka akimshangaa
"Ndiyo ni yeye tena na namba zake ngoja nimpigie kumjulisha"......
Moyo wa PATRICK ulikuwa ukienda mbio kwa hasira,sura yake ilibadilika na kuwa sura ya UKATILI
alikuwa kasimama huku akijaribu kupiga namba kadhaa ambazo bado azikupokelewa,mbele yake walikuwa wameketi watu 5 katika viti vya umeme wakiwa vifua wazi! pia kulikuwa na watu wa tatu wenye sura zilizokomaa,sura zisizopendeza kuzitazama machoni,sura mbaya!,watu wale wa ajabu,makatili,walikuwa wakiwa adhibu vijana wale wa tano walokuwa vitini
"UZIMA WENU NI KUNIELEZA KWA NINI MMENISALITI?"
PATRICK aliongea na kuwapa ishara wenye "sura mbaya" kuendelea kuadhibu nao awakusita kuiwasha swichi! shoti ya umeme ikaambaa katika miili yao....
wakati wakiendelea kugugumia kwa maumivu ghafla simu ya PATRICK ikaita! akasogea pembeni kidogo kupokea.....
"alooh MUNIRA....unasema?..mke wangu? yupo peke yake!...na majambazi...wam
euwawa?..mnaelekea KCMS...poa 5 mints ntakuwa hapo....."
akakata simu!,akamgeukia mmoja wapo ya wale watu wenye "sura mbaya" kumpa habari aloipata!
"RANJONTO,jeshi zima lipo mkononi mwa jeshi la polisi operesheni imebuma! yule mwanaharamu wa kike amepata ajali anakimbizwa hosptali wacha mi nimuwah nkamwangamize kabla ajavujisha siri atangulie KUZIMU,
wewe na (ROHO YA PAKA) mtabaki hapa kambini!,msaliti adhabu yake ni kifo hawa mafedhuli walidhani wataweza kunikimbia? wakawauwa wenzao na kushirikiana na wale mfu hai kuntoroka? waingizwe kwenye mapipa ya gesi hata mifupa yao isionekane MULAR na XY ongeza jeshi mkiwa na vitambulisho vya wanausalama zameni MSITU wa tembo mkamtafute ZUBERI wote lazima wafe kwa kifo kibaya sana sawa?!....."
PATRICK alimaliza kutoa majukumu ya kazi watu wale walinzi wa geti la nje waloshirikiana na SHONE "Ninja" kumwokoa zuberi na kutoroka wakipewa fungu kubwa la hela wakanyanyuliwa mmoja mmoja na kutupwa kwenye pipa la gesi wakayeyushwa mpaka mifupa yao.....
pesa walizokula zikiwatokea puani
MULAR kijana katili asiye na chembe hata robo ya ubinadamu na XY mwenye tabia kama ya MULAR wakaingia
MULAR na "XY" wakaongeza vijana wengine nane
vijana kumi wenye uwezo kimapambano kupigana wakaingia msituni kumsaka ZUBERI...wakati huu wakiwa na vitambulisho vya usalama kutoshukiwa na maliasili
walijipanga!!!
***********
KWA UPANDE WA SHONE
bado hali yake ilikuwa mbaya,mdomoni alipumulia hewa ya Oxygen,bado akuwa na fahamu alikuwa kama mfu alosubiria kuzikwa,
pembeni yake aliketi mwanaume aliyejidai ANAMPENDA sana!!! lakini kumbe moyoni mwake kulikuwa kumejaa chuki ya kuua,roho mbaya,alikuwa kashika tama kiunyonge kama aliyopo pembeni yake ni mtu muhimu katika maisha yake
muhibu wa moyo wake kwa haraka haraka ukimwona unaeza kuhisi moyon ana majonzi makuu kumbe moyoni aliwaza njia staiki ya kummaliza,
tatizo manesi walokuwa wakiangaikia wagonjwa wengine wakawa kizuizi kumaliza alichowaza pale wodini apakuwa mahala salama kwa kufanya mauji yale.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
akapata wazo! wazo alilolifurahia ni juu ya kujifanya anamuamisha hospitali! yah akakubaliana nalo,akaachia tabasamu afifu,tabasamu la furaha akamwangalia SHONE kwa chuki...
wakati huo huo daktari akawasili
"samahani wewe ndo mume wake huyu dada?!"
"ndiyo dokta!"
PATRICK alijibu kwa wahka akinyanyuka kwenye kitanda alicholala mpenziwe,dokta akatabasamu tena kumtoa khofu,...
"nakuitaji ofisini!...."
alitamka dokta wakati huo huo akageuka kutoka nje ya wodi ile,PATRICK akawa nyuma yake akiwaza pia kuwasilisha ombi lake la kupewa rufaa ya kumwamisha hospitali na kumpeleka nje ya nchi.
kwa lengo la kumuangamiza kuficha siri zake.walifika hofisini wakaketi kijana yule wakati dk akipembua pembua makabrasha yaliyopo katika meza yake yamkini akitafuta la SHONE yeye alikuwa akiusanifu uzuri wa ofisi ile....
hatimaye dokta akalipata kabrasha aliyoliitaji! kabla ajaongea akalipitia pitia baada ya kuridhika akatoa miwani yake na kuifuta futa jasho au sijui ni vumbi akairudisha machoni akaendelea....
"mimi naitwa DK PAUL MZIGWA ndo dk mkuu wa magonjwa ya ubongo hapa kcms...sasa tatizo la mke wako ni kubwa"
Ni kwamba ubongo wake umetingishika!,hivyo umepoteza KUMBUKUMBU zote,atokumbuka chochote kilichotokea kwenye maisha yake,atomkumbuka yeyote akizinduka atakuwa ni kama mtoto ambaye ni lazima ajifunze a,b,c,d na kuongea
PATRICK machoni alionekana kuuzunika,lakini moyoni alifarijika....
Baada ya maongezi ya muda mrefu aliomba haruusiwe ili akamwandalie chakula wazo la kumuua lilifutika palepale.baada ya kugundua mtu yule atokuwa na kumbukumbu tena.
wakati PATRICK akiwa ametoka ghafla SHONE akafumbua macho yake na kuangaza ndani ya chumba kile bila kuongea kitu,
alionesha kushangaa eneo lile nesi alikimbia kumwita daktari,daktari alikuja na kumchukua vipimo akiandika katika "file!" aliloshikilia alionesha kuridhishwa na hali ya mgonjwa wake.
SHONE hakuonesha kukumbuka kitu ajali aliyoipata ilionesha kuathiri sana ubongo wake ilikuwa ni kama "memory card" ilofutwa kila kitu.
Alibaki bila kuongea na mtu hata madaktari walipomsemesha akuongea kitu,
ila mpaka kufumbua macho ilikuwa ni hatua moja wapo kubwa,SHONE akuwa yule wa mwanzo huyu alikuwa ni kama mtoto aloitaji kufundishwa kuongea,Siku ziliendelea kukatika hatimaye hali yake ikatengemaa PATRICK akamchukua sasa akiwa na jukumu jipya.....
Upande wa pili baada ya ZUBERI kushushwa kwenye gari moyo wake haukuwa na amani kabisa kwa sekunde kadhaa alijificha kwenye kichaka akiliangalia gari la mpenzi wake SHONE na mandoline yakikimbizana.
aliitaji kulifata nyumanyuma kuelekea msitu ule lakini moyo wake ulisita,akujua kwanini SHONE aliamua kukimbilia kule.
mawazo hayo yalikatika na majonzi kutawala ale aliposikia milio ya risasi moyo ulimwenda mbio na alijua huo ndo mwisho wa mpenzi wake kwa vyovyote alijua lazima atakuwa amekufa.
ilibidi apige magoti na kumwombea muda huo huo akanyanyuka na kuanza kuelekea vichakani akiacha njia ya kuelekea porini masaa matano alikuwa bado yupo kwenye mwendo akipita vijiji kwa vijiji sasa njaa ilimtafuna utumbo wake na aliitaji kula akuwa na fedha.angekula nini?!
Angekula wap!?
Akaendelea na safari ghafla akatokezea katika kioski bila kuwaza mara mbili aliingia na kuketi mama ntilie akamuuliza amletee chakula gani
"ugali nyama"
akanawishwa mkono na kuanza kula,alikifakam
ia chakula kile hadi akakimaliza,akanawa na kumwangalia mama ntiliye yule ambaye naye alimshangaa
walishangaana!!!
"mama chenji yangu...."
alitamka ZUBER hapo hapo mzozo ukaanza,wanaume watatu walokuwa wakipasua kuni wakaitwa na kuanza kumpiga kijana yule wakimlazimisha atoe hela.
zuber akuweza kujitetea.
ugomvi ule uliamuliwa na dada mmoja ambaye alimlipia hela ile alodaiwa.
"unakaa wapi?"
dada yule alimuoji ZUBER,naye kwa kuwa alikuwa ana dira akamweleza ukweli kwamba ni kijana wa mtaani,
dada yule kwa kuwa alikuwa akiitaji kijana wa kazi mkoani SINGIDA ikabidi amchukue.zuber alifrahi akijua atakuwa mbali na mkono wa PATRICK katu akuwaza wala kufikiri kuwa yule atakuwa ni ndugu yake wa damu na PATRICK na kama angelijua ilo asingelikubali kabisa kwenda lakini usilolijua ni kama usiku wa kiza,
kizaazaa!
maisha yake yalikuwa rehani!,pasina mwenyewe kujua
UPANDE WA PILI
SHONE akiwa katika ngome ya muuaji PATRICK akiwa kitandani patrick alijitaidi kuwa naye karibu,akijaribu kujiweka kimapenzi zaidi kwa binti yule,kila dakika alikuwa akiwasiliana na vijana wake waloshindwa kumtia nguvuni ZUBERI.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
shone ilibidi akubaliane na hali halisi,kwani akukumbuka chochote akamkubali patrick kama mumewe.
patrick akapanga kwenda kwa mama yake mdogo SINGIDA kutoa kujadiliana juu ya harusi yake katu akujua mbaya wake yupo huko.
akaingia ndani ya gari lake na kuianza safari.
baada ya zuberi kumaliza kazi zake akaambiwa ajiandae kuna ugeni unakuja muda mchache.
Badaye honi ikasikika na ZUBER akaenda kufungua geti pasina kujua kuwa PATRICK ndo alikuwa KAWASILI.
PATRICK aliingiza gari lake taratibu,akuangaika kumwangalia mtu alofungua geti!, japo ZUBER alimwona PATRICK moyo ulimwenda mbio hapo hapo alitoka akusubutu hata kuingia ndani khofu na hatari aliiona mbele ya mboni za macho yake.
ndani ya dakika 10 alikuwa tayari yupo katika kata ya unyaghumpi.
Hakika PATRICK alifurahi kumuona mama mdogo wake,walikumbatiana mgeni akakaa katika kochi kubwa la sofa.
"ZUBER! ZUBER! ZUBEE..."
Aliita mama yule kwa sauti kubwa,
moyo wa PATRICK ukashtuka kama kapokea taharifa ya msiba ya mpendwa wake,
akili yake ilijaribu kukataa kuwa siyo zuberi yule amtaftaye kwa "udi na uvumbi!" dada yule baada ya kuita bila kuitikiwa akanyanyuka kwenda kumtafuta!
ZUBERI akuonekana!!!
Hapo ndipo jibu la PATRICK likapatikana!
"zuber yupo singida!"
Akajiwazia akaishika simu yake kwa siri sana akatuma msg
"RANJONTO, ule mzigo upo singida! panga vijana! xy akiwemo mkwaye pipa dakika tano kutoka sasa muwepo hapa mkoani"
akaituma meseji ikapokelewa na ikajibiwa
"sawa"
maongezi ya mtu na mama yakafata waliongea kwa furaha na bashasha lakini mawazo ya kijana yule hayakuwa hapo.
Ni kijana apaniaye kitu lazima atimize.
alimchukia zuberi!!!
ilikuwa lazima amuuwe,ndipo "nusra" ya moyo wake ingepatikana.
mpaka anaondoka SINGIDA siku mbili zile aliitaji zuberi awe maiti...
*********
Katika uwanja mdogo wa MAKIUNGU, ndege ndogo ilitua,vijana 6 wenye mwonekano wa kishari walovaa suti nyeusi wakashuka.
pembeni ya uwanja kulikuwa na gari ya PATRICK alokuja kuwapokea.
safari ya kuelekea MADUKANI mji mkuu wa makiungu ikaanza walifikia katika hoteli nzuri.
mara moja kikao kikaanza!
"ZUBER yupo huku huku singida,ndani ya siku mbili hizi kabla sijarudi MOSHI naitaji nirudi na kichwa chake,nawaamini na jua amshindwi na kazi..."
PATRICK alitoa maelezo jinsi alivyopishana na zuberi na mwisho kutoa kazi.
vijana wale katili wakatawanyika wakiwa na shauku muktahiya ya kumtia zuber mkononi.....
***********
Mawazo ya ZUBERI yalibadilika!, akuitaji kuendelea kubaki SINGIDA ilikuwa lazima aondoke!
ataondoka kwa namna gani?!!
ilo akulitambua, ila kama aliitaji kuishi ilikuwa lazima aondoke.
"PATRICK kwa nini ananitafuta? ni kosa gani hasa nililomkosea mpaka atake kuinyakua roho yangu? ni mapenzi tu au kuna la nyuma ya pazia! SHONE kafa chanzo yeye sasa anataka kuniangamiza na mimi kwa nini ni mimi? hivi kweli MUNGU upo? kwa nin unakubali mja wako nateseka kwenye dunia yako?!,kwa nini usinchukue nkapumzike katika ardhi yako?"
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ZUBER alilalamika kwa hisia kali, machozi ya kuuwakilisha uchungu uupatao moyo kwa majonzi makuu yalitiririka katika mashavu yake.
Japo alikuwa kwenye malalamiko makubwa kuna sauti ya "utukufu" ilimjibu
"usikate tamaha! jikaze wewe u mwanaume yote ni majaribu yangeisha..."
"mpaka lini?!"
aliuliza ile sauti ambayo ilimfariji,japo mawazo katika kichwa chake hasi na chanya yaligongana, hakuwa tayar kusimama mahala popote
alipokwenda akupajua.
Ila sasa alikuwa katikati ya msitu bila uelekeo maalumu!,bila dira ya aendapo,
kwa mbali alisikia sauti za fisi na simba zilizompa woga miguu ilimvimba kwa kutembea,njaa ilimuuma kwa kutoingiza chochote mdomoni.
Angekula nin wakati yupo katika hatari ile? hatari ilotishia kuyapokonya maisha yake?,
hatari isababishwayo na kiumbe kama yeye.
patrick!!!
mwanzilishi wa hatari hiyo, hata kama malaika angemshukia na kumpa chakula hiyo hamu na muda wa kula chakula hicho akuwa nao japo alihisi njaa alikimbia, akatembea,akakimbia tena mpaka kigiza giza kikalitawala anga,
alichoka! ikabidi asitishe safari yake na kutafuta mahala salama pa kupumzikia mbele yake palikuwa na mti mkubwa akaukwea na kupanda kuelekea juu...
akujua ni saa ngapi usingizi mnono ulimuopoa! labda kutokana na uchovu wa kukimbia mchana kutwa.
alishtukia maumivu makali ya mguu yakipanda mwilini alipofumbua macho alimshughudia nyoka mkubwa wa kijani akipanda kuelekea juu,alikuwa kamdunga...
Zuberi alishindwa kustahimili maumivu Yale, taratibu mikono ikaachia mti akadondoka toka juu ya mti ule na kutulia chini! Akutingishika
Fisi walokuwa karibu na eneo like wakamkimbilia wakijua ni mzoga wakaanza kuudonoa mwili wake wakitokwa na mate ya uchu
ZUBER akashindwa kuhimili,maumivu yale taratibu mikono ikaachia mti akadondoka.na kupoteza fahamu.
fisi walokuwa karibu na eneo hilo wakamkimbilia wakijua ni mzoga,wakaanza kumdonoa miguuni.
ghafla wakashtuliwa na mlio wa risasi...
mlio ambao ulisikiwa moja kwa moja hata na vijana 6 katili! wenye uchu na roho ya kiumbe mwenzao.japo walisikia mlio ule kwa mbali wakaongeza mwendo kuelekea upande ule....
fisi wale wakakimbia,mtu yule aliyeshika gobole akasogea kwa tahadhari,kimuonekano alikuwa na ndevu nyingi kwenye mwili wake,katu usingeshindwa kumtofautisha na miongoni mwa sokwe waliyoko katika msitu ule,alivaa nguo kuukuu,mwili wote ulitawaliwa manyoya! alikuwa mawindoni akiwa hatua chache kutoka kwenye mti ule.aliopo ZUBER mara ghafla akaskia kishindo...
alipotupa macho eneo lile kilipotokea kishindo kile bumbuwazi likauvaa uso wake ni baada ya kumuona binadamu akidondoka toka juu.macho yakamtoka pima mtu yule...
akashindwa kujizuia kupigwa na butwaa,wakati akiwa katika taharuki hiyo akashughudia fisi wakimlaki kwa fujo shangwe na nderemo ndipo akagutuka na kujua wajibu wake muda ule.akalikamatia vizuri gobole lake.na kupiga risasi juu!!
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mlio ule ukakimbiza fisi wale wenye uchu! kwa hatua za tahadhari akamsogelea mtu yule kwa dhamira stahiki ya kumsaidia akaweka kichwa chake katika kifua cha majeruhi yule! bila shaka alikuwa akisikiliza mapigo yake ya moyo kama ni mzima au mfu.kwa mbali yaliskika yakidunda akamkwapua na kumuweka mabegani,bila kuitambua hatari ilokuwa mbele yake na laiti angeijua katu asingeuchukua mwili ule...
mtu yule japo alionekana amezeeka ila alionekana bado ana nguvu za kutosha,maswali kibao yalimiminika katika ubongo wake.Lakini akuyapa nafasi kwa kujua fika angejiumiza tu! kikubwa ajaribu kuuokoa uhai wa kiumbe kile.alimbwaga zuber katika kitanda chake akachukua kijiti kilichochongwa vizuri ncha na kuanza
Kukiingiza katika jeraha lile,akitoa sumu ya nyoka yule,kijana yule alijitingisha akatulia tuli,yule mtu akasikiliza mapigo ya moyo kwa mbali bado yalidunda,mtu yule akatabasamu,tabasamu la mbali lililo onesha meno yake ya njano yalopangilika bila mpangilio maalumu katika mdomo wake!,akachukua aina flani ya majani akayatwanga na kumpaka mareruhi katika kidonda kile.akakifunga kile kidonda.na kumuacha hapo apumzike,akatok
a,dakika chache akarejea na matunda flani aliyoyakamua juisi na kumnywesha.hali ile iliendelea kwa siku mbili mfululizo.hatimaye hali ya ZUBERI ikaanza kutengemaa...
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment