IMEANDIKWA NA : ZUBERY R. MAVUGO
*********************************************************************************
Sehemu Ya Kwanza (1)
Upepo na jua ni mahasimu wa toka zamani, mara nyingi ubishani wao wa kutaka kujionyesha yupi ni bora kuliko mwenzie, ndio sababu pekee ambayo hutupatia jua kali sana. Jua ambalo huua mazao yetu na kusababisha ukame upelekeao kupotea kwa maisha ya binadamu, sijua peke vilevile hata upepo ukiwa kwenye ubishi huo, huweza kuvuma kwa kasi kikubwa ambachohumfanya binadamu apate tabu katika macho yake dhidi ya vumbi izolewayo na upepo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilikuwa mida ya saa sita, kamili mchana mida ambayo wanafunzi washule nyingi za Tanzania hutolewa darasani kwa ajili ya kwenda makwao,kupata chakula chamchana iliwaweze kurudi shuleni na kusoma pasina kuwazia chakula. wakati yote hayo yakiendelea, ziliweza kusikika sauti za marumbano katika pande za duka la kina Nurdini, sauti zile zilikuwa zikibishana juu ya uandishi wa maneno uliokua ukiendlea kwenye moja kati ya karatasi iliyochanwa kutoka kwenye daftari ya mahesabu.
"Unatakiwa uandike iluv u, eti we boya unaandika kiswahili" Ni maneno ya Samir, aliyokuwa akimwambia rafiki yake Nurdin. Huku akiwa ameinyooshea kidole karatasi iliyokuwa ikiandikwa.
"poa lakini mbona huku chini tume sahau kuandika sahihi, unadhani mtoto atajua imetoka kwa nani?" Lilikuwa ni swali kutoka kwa nurdin, swali alilomtupia rafiki yake samir.
" we nurdini ni boya kichizi, hivi unataka tuandike saini iliiweje. je, barua ikikamatwa na mwalimu unadhani utasalimika, jaribu kutumia akili hapa chamsingi ni kuandika bila sahihi kisha nikimpelekea nitamwambia imetoka kwa nani, kwanza malizia fasta;fasta kwani sasa hivi ni saa saba na dakika kumi na tano, zimebaki dakika ishirini tu wanafunzi waingie madarasani, si unajua wakiingia madarasani kumpata ilivyo inshu jombaa." Aliongea maneno yale samir na kuukata mzizi wa fitna juu ya swala la kuandika sahihi katika karatasi ile.
"Tayari nimeikili, ngoja nikuskilizishe maneno atakae ya skia mtoto na ku acept my request" Aliongea nurdini.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"ok isome mzazi ilinimuwaishie dogo, siunajua tena hii ndo mida yenyewe?"
Baada ya kuruhusiwa na samir basi nurdini alianza kuisoma barua ile ambayo ilikuwa inasomeka hivi:
MPENZI WAKO,
S.L.P. MOYO,
2/1/2009.
Dear sumaiyah......
Salamu sana, natumaini utakuwa mzima wa afya, japo hofu inaendlea kunitanda ila naamini hivyo. Kuhusu mimi, usiwena shaka kabisa, kwani mimi nipo safi ki afya. Dhumuni la barua hii si kwa ajili ya salamu pekee, bali kuna jambo nyeti ninalotaka kukujuza.
Mpendwa sumayyah dhumuni la barua, nikukujuza kuwa, nimezunguka mashariki na hata magharibi, bila kusahau kusini na kaskazini lakini kama wewe sijamuona. tafadhali naomba unikubalie ombi langu kwani ni wewe pekee ambae umeuteka moyo wangu. Kila ni kinywa maji huwa na kuona kwenye grass, hata nikilala huwa nakuota , shahidi ni rafiki yangu alie kuletea barua hii tafadhali nakuomba kubali ombi langu iliuuokoe moyo wangu.
Sumayyah, wewe nimegundua wewe ni zaidi hata ya mambo yote muhimu ikiwemo chakula,malazi, na hata mavazi kwani kila wakati huwa nakuwaza wewe, misikufichi hadi muda mwingine huwa nachanganya mahesabu ya dukani kwa sababu yako sumayyah. U mrembo sana sumayah, maana kila ukipita karibu yangu huwa na jihisi kama nimetembelewa na malikia wa dunia. Mapenzi si barafu eti yataganda na kuwa kimiminika, wala mapenzi si dafu eti utayala na kuyanywa. Tafadhali unusuru moyo wangu, moyo ambao umeangukia ndani ya bahari ya mapenzi. Nadiliki kusema kuwa wewe ni mvuvi ulie livua pendo langu kama samaki na kuliweka kwenye mtego, halifurukuti wala halijinasui juu yako. Nakupenda tafadhali kubali ombi langu...
... Mwisho....
Endapo kuna makosa yoyote katika barua hii basi ujue ni machozi yaliyodondoka kipindi naandika barua hii.
Wako akupendae ......
**********
"Ewaaa, maneno matamu sana nurdini na, nina amini mtoto atakubali kwani vitu ulivyoandika vinateka sana moyo wa mtu. Imependeza japo nilikwambia uandike neno 'iluv u' ila hata hilohilo likopoa sana mwanangu chamsingi, ipulizie unyunyu io barua na uiweke vizuri katika bahasha ilihata akiishka ajue imetoka kwa kijana smati au sio mwanangu?". Aliongea samiri, na kukazia baadhi ya pointi.
"Ndio, hivyo mwanangu alafu tuweke na karatasi nyngine kwa ajili ya majibu au vpi mwanangu?" Ulikuwa ni ushauri kutoka kwa Nurdin.
"Acha uboya Nurdini majibu utafata mwenyewe unamuogopea nini huyo, au uliambiwa ana kunya keki,kisha anakojoa soda?. Acha mambo yako mtoto wa kiume huwa haogopi nyau, wewe utafata jibu mwenyewe kiume au sio mwanangu?"
"poa, lakini siunajua jinsi anavyonioneaga aibu hvi unadhani ataweza kunijibu kweli au unaniambia tu wangu"
"we utaöna mwenyewe kwa manen yaliyomo humu ngoja kwanza mimi niende nikamtegee kwenye ilekona anayopenda kupita akiwa anaenda shule."Aliongea samir na kuanza kujiondoa taratibu ...
Alifika maeneo yashule samir na kuketi katika moja kati ya mawe yaliyokuwapo eneo lile, punde kidogo samiri aliweza kumuona sumayah akipita katika maeneo yale, kwakuwa hakutaka kujionyesha kuwa yupo pale kwa ajili ya kumsubiri sumayah, basi alijifanya yuko bize na kufunga nyuzi za viatu vyake.
Sumayyah alipofika mkabala na samir alimpa salamu ya kiislamu.
"Asalaam alyk samir" Alisalimu sumayah huku akiwa ameuelekeza mkono wake karibu na kichwa cha samir, ambae kwa muda huo alijifanya yuko bize na kufunga nyuzi za viatu vyake.
Baada ya kuskia salamu ile ndipo samir alijifanya ameshtuka kuskia sauti ya sumayah kana kwamba hakutegemea kama angeweza kuiskia sauti ile.
"waalaykah salam sumayah. Vp mbna umetokea wapi au nawewe ni mzimu nini"
" jamaani samir unavituko, mbona mimi nimetokea njia yangu ya kila siku."
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"ahaa, lakini umenishtua. Enhe leta story mrembo."
" samiri mbna unaniita mrembo, mispendi kuitwa mrembo, warembo wapo kwenye makopo ya mafuta, labda na waigizaji kama kina aishwaria rai, kajor, prety zinta, na kina... Kina....." Kabla hata sumayah, haja maliza maelezo, samir akaingilia.
"Sumayyah, unajua we hujui tu kiasi gani ulivyo mrembo. Wewe ni mzuri sumayah, hebu tazama macho yako,midomo unavyo ikunja dah," Sumayah, akatabasamu kidogo kwa kusikia vituko vile, na samir akatumia tabasamu lile kama spana ya kukazia manen0 yake.
" Tazama tabasamu lako lilivyo zuri, kwa tabasamu hilo hata kajor inabidi akasome, dah cheki unavyonikosha mtoto wakiume na dimpozi zako, sikutofautishi na Prettyzinta alioigiza movi ya Soldier akiwa na bob-deo."
Furaha ya sumayah ilizidi kumjaa, hata kumpelekea ashindwe kukabiliana na tabasam lake.
Samir aliendelea kukomaza sifa mbele ya sumayah, na kumfanya asitamani kutoka maeneo yale iliaendlee kupata sifa kem,kem, kutoka kwa samir.
"sumayah mtoto mzuri, tena uliyejawa na urembo kwenye sura yako. tafadhali chukua ujumbe huu, uusome na uuzingatie"
"ujumbe!! ujumbe gani huo?, na umetoka kwako au kwanani?" Ni maneno yaliyomtoka Sumayah, huku akiwa kwenye bumbuwazi na maswali lukuki.
"anhaa, tulia muigizaji wa nafsi yangu, mbona unakuwa na haraka utadhani mkojo wa asubuhi?, ok, ujumbe huu umetoka kwa rafiki yangu kipenzi, mpole, mcheshi, mwenye wingi wa vituko tena zaidi yangu nae simwingine bali ni NURDINI"
Sumayah baada ya kuskia vile, alishangaa sana, kwakuwa hakuw na mazoea na Nurdin.
" nurdini!!! Mmh!!, Haya acha niwahi shuleni nitausoma nikifika nyumbani"
"sawa sumayah wewe wahi shuleni siunajua limwalimu lenu lile la zamu linavyojifanyaga linajua kuchapa"
"ok, baadae samir"
Sumayah, baada ya kuaga, hakuwa na laziada ila kuondoka maeneo yale na kwenda maeneo salama. Akiwa katika hatua zake, huku nyuma Samir alibaki hoi na kujisifu kwa ushujaa wa kufanikisha kufikisha kile ambacho kilikuwa ni ahadi kati yake na rafiki yake.
Ingawa muda ulikuwa unazidi kuyoyoma, lakini samir hakuondoka maeneo yale, aliendlea kutabasamu na kujipongeza kwa kazi ile ya kishujaa.
"dah, huyu boya amepata kisu kichizi, najua mishe itatiki na lazima au bebe mzigo. Na kwa jinsi jamaa alivyooza, sjui tu atakuaje." Ni maneno aliyoongea Samir huku akiwa anaendlea kutafakari na kuzidi kulichanusha tabasamu lake.
Kengele ya kuingia madarasani ilipogongwa, samir hakuingia na badala yake aliamua kurudi kwa rafiki yake ilikwenda angalau kumpasha habari juu ya yaliyotokea.
Alifika na kumpa habari ya yaliyotokea, lakini katika masimulizi yake, chumvi ndio ilisheheni kwenye maneno yake. Mara mtoto akachelewa darasani, mara tumekaa nae zaidi ya nusu saa, ilimradi tu, kuzidisha chumvi katika maneno yake.
" Kwa hiyo umemwambia kabisa na jina langu alafu akafurahi?" Aliuliza nurdini.
"unanichezea mimi wewe. Mtoto nimemtupia maneno mpaka yeye mwenyewe akarespekti na hawezi kuchomoa maana, inaonyesha wazi kabla hata hajasoma maudhui , kichwa cha habari kimeweza kusadifu yaliyomo" Aliongea samiri katika hali ya kujigamba mfano wa mwanajeshi asimuliapo matukio ya vita alizo pigana kwa kuitetea nchi yake. Ilikuwa ni furaha tu kwa rafiki yake na aliamua kumuagiza kwa Ma'ntilie maarufu maeneo yale iliafate ukoko. Ikiwa ni kama kipongezo cha kazi nzuri waliyofanya.
"Dah, mzee samir, singo la leo tamu au we unaonaje?" Aliongea Nurdin kuusifia ukoko ule.
" singo ni tamu kwa sababu mambo yanaenda fresh, na hii ni ishara nzuri ya kuonesha jinsi gani mtoto atakubali tena bila kuzingua" Aliongea samir, huku akiendlea kukokoa ukoko.
"Nakuaminia sana mtu wangu kwa show zako, hebu nipe tano kwanza". Aliongea nurdin, na kugongesha tano.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" ebana ee mimi ndio samir, mkali wa show za kibabe, mzee wa michongo yenye kuchongoka, mtaalam wa michongo ya busara kuliko panya kadogo aliefanikisha kumfunga paka kengele". Aliongea samir kwa majivuno huku akitamba utadhani yupo jukwaani.
" we ngoja tusubiri majibu, mtoto amesema ataisoma akifika mahome kwao"
"ok, sasa mbna wewe hurudi skuli siunajua nyie ni L.Y "
"usijali nurdini minitatia tim kesho,coz leo nishaaribu kuna dogo mmoja ameniletea class nikamchukua mkono, ameenda kusema kwa mwalimu kwa hiyo skul pamenuka"
"Dah, pole sana mkali wangu lakini huo ndio uanaume boya akikuzingua mfanyizie amanini mwanangu?" Aliongea nurdin na kumalizia kwa swali.
Waliendelea na maongezi yao mpaka ulipofika muda wa wanafunzi kurudi makwao, ndipo samiri alipotoka kwenye duka la rafiki yake nurdini na kuanza kujongea ilikuelekea kwao kwa ajili ya kubadilisha nguo iliawe huru, hakuwaza chakula kwakua tayari alishapata kwa rafiki yake Nurdin
. Akiwa njiani samir aliweza kukutana na rafiki zake wengne na kuwauliza yaliyojili baada ya yeye kumpiga mwanafunzi mwenzake na kwenda kusema kwa mwalimu. Wanafunzi wenzake walimuhakikishia kwamba hakuna tatizo na kumfanya ajiskie huru, samiri alipofika nyumbn kwao alibadili nguo pamoja na kuoga. Baada ya kuoga aliamua kujipumzisha geto kwake na kuanza kukumbuka jinsi alivyokuwa akimchekesha summayah.
Usingzi ulimchukua, hata alipoamka aliamua kwenda moja kwa moja hadi kwa rafiki yake nurdin kwa ajili ya kupanga mipango ya kumuwinda sumayah.
"Oy, mzee samir yule mtoto amejipitisha hapa muda tu wewe ulipoondoka."
"Mtoto yupi huyo Mkali wangu?"
"mmmh, unajifanya humjui. Si mtoto Zulfa, amesema kakumis ile mbaya."
"Huyo nae, mimi nisha mwambia simpendi, mbna si muelewa huyo msichana. Mi sipendi hata kumuona," Aliongea samir huku akionesha kukasirika.
"Tena staki habari za sjui Zulfa"
"poa kaka bt sio fea"
Waliongea meng muda ule.
Hatimae ilifika usiku na wakaenda kumuwinda sumayah maeneo ya kwao.
" Mkali mbona hatokei inamaana leo hatumwi hata mafuta ya taa, au ndo tuseme mafuta yao ya jana yapo hadi leo!" aliongea manen0 yale nurdini huku akibadirisha pozi katika mawe yale waliyokuwa wamekalia.
"Aaaah,,gundu hizo mwanangu. Mbona unajichulia, we unadhani mafuta yale walio yanunua jana yanaweza yakatosha kubaki hadi leo acha mambo yako, mtoto atapita tu kwenda dukani we skilizia kiaina siunajua sisi wapiga mingo tulivyo"Aliongea samiri manen ya kuwatia ujasiri wa kuendelea kubaki maeneo yale.
Walikaa takribani saa nzima huku wakipongezwa na mmbu ambao waliwauma na kuwafanya wajiwashe makofi kila mara katika miili yao kwa minajili ya kuuwa mbu, kuachilia mbali mbu wale waliokuwa wakiwauma kwa zamu, vile vile kulikuwa na baridi kali:baridi ambalo waliweza kulivumilia kwakua walikuwa wakimsubiri mschana yule lakini laiti kama angelikuwa mtu mwingine basi wasingeliweza kulivumilia baridi lile.
"oyaaaa samir sio yeye huyo anatoka nyumbni kwao"
"ndio yeye nurdini, hapa chamsingi mfate moja kwa moja kabla hata hajafika dukani iliakupe jibu letu mapema sisi tuambae geto tukatulie amanini mwanangu"
"ya, ndo hvyo jombaa". Hayo yalikuwa maongezi waliyo yaanzisha baada ya kumuona sumayyah kwa mbele na bila kupoteza muda nurdini alienda mpaka alipokuwa sumayah.
"ha! Nurdini. Umetokea wapi usiku huu"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nilikua kwa dada, na ninarudi nyumbni ila kama bahati nimekutana nawe sumayah"
"dah! Usiku mwema nurdini acha mie niwahi kwenye mafuta kwani ninavozidi kuchelewa ndivyo muda unavyo zidi kwenda" Aliongea sumayah na kumfanya nurdin avunjike moyo na kutengeneza maswali akilini kwamba huenda ujumbe wake haukufika. Lakin akalijikakamua kiume na kuuliza.
"vip sumayyah. Samir alikupatia ujumbe wangu?" Alitoa sauti ile sauti iliyotoka kiunyonge zaidi.
"ndio nurdin ujumbe wako nimeweza kuupata na nimeusoma" sumayah alijibu maneno yale huku macho yake yakiwa yameangalia chini.
"ok,gud so what about my answer" Aliongea nurdin manen yale ya kiingereza.
"mimi sijui kingereza, na sipendi watu wanaoongea ongea kiswa-english" Aliongea maneno yale yaliyomfanya Nurdin ajionee aibu lakini kwa kuwa ni mtoto wa kiume, hakutaka kudhihrisha aibu ile.
" sawa naomba unisamehe kwa kutumia kingereza. Swali langu ni kwamba, kama umeupata ujumbe wangu vipi kuhusu majibu yangu?.. Aliongea nurdini kwa kujitetea na kumalizia kwa swali, ambalo lilileta ukimya katika maongezi yao.
Baada ya muda kidogo nurdin alikata kimia kile.
" vip mbna kimya sumayah?" Aliuliza swali lile huku kwa muda wote akiwa ameyakaza macho yake na kuya angalizisha bara'bara,usoni mwa summayah ambae kwa muda huo alikua bado ameinama chini huku akiziadhibu kucha zake kwa kuzing'ata kama ishara ya aibu.
" samahani nurdini, hebu tafadhali nipe muda iliniweze kukufikiria kwani jambo hili si lakukurupuka kama unavyodhani wewe"
Aliongea maneno yale sumayah huku akiendlea kuziuma kuchazake.
"skia sumayah, binti mrembo na mwenye kila sifa za kuwa wangu, tafadhari naomba unijibu hapa hapa ili roho yangu isuuzike" Aliongea nurdin huku akinadi sifa mbalimbali kwa minajiri ya kumshawishi sumayah.
"hapana nurdini siwezi kukujibu kwa muda huu, nachokuomba jaribu kunielewa" Aliongea sumayah maneno yale yenye msimamo wa kauli yake.
" mmmh,, sumayah mbona unaendlea kutaka kuniweka kwenye sintofahamu, kwani ukinijibu sasa hvi na ukienda kufikiria, nadhani jibu la sasa hivi na utakaloenda kulifikiria hakutokuwa na utofauti, kwahiyo, nakuomba nijibu sasa hivi iliniondoke hali yakuwa nimeshajua" Aliongea maneno yale yenye ushawishi wa hali ya juu na aliamini kwamba angeweza kumtoa pangoni nyoka huyo alie ng'ang'ania msimamo wake.
" nurdin nakuomba kuwa muelewa najua una mengi yakusema kama ushawishi wa kutaka nikujibu kwa muda huu, lakini waweza ongea hadi koo likakauka kwa kila aina yamaneno ila mimi nikabaki kuwa na msimamo wangu. Tafadhali nitakujibu siku nyngine, kwanza nachelewa kununua mafuta" Aliongea maneno yale na kuanza kujongea bila hata kuaga kwa nurdini.
"hey, sumayah,,why unaondoka bila kuaga wala kunitakia usiku mwema?". Aliuliza swali lile nurdin huku ameushikiria mkono wa sumayah, ambae kwa muda huo alikua akiondoka.
"naondoka kwa sababu hutaki kunielewa nurdin" Aliongea maneno yale huku akiutoa mkono wa nurdini uliokua umeshkilia ilikuweza mzuia asiondoke.
"ok,fine. Lakini sio fea. Basi niambie jibu langu utanipatia lini iliniwe na uhakika." Aliongea nurdin huku akilaumu.
" nitakujibu jumatatu" Alijibu sumayah kwa mkato.
"aaah, sumayah, hebu fikiria hata wewe, huöni jumatatu ni parefu sana?"
Aliongea nurdin huku akionesha wazi kutolizika na kauli ya sumayah.
"nurdin, ujue hata hapo nimekusaidia sana kwani hata muda niliokupa ni mdogo. Vipi ningekupa mwaka au miezi. Basi naomba unielewe usinifanye ni badili maamuzi"
" ok, fine. Nimekuelewa bt fikiria jibu zuri jibu ambalo litanifanya niweze kujiskia amani katika moyo wangu" Aliongea nurdini nakuagana vizuri usiku ule.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sumayah alienda kununua mafuta na kurudi nyumbani kwao, huku muda wote huo macho ya Nurdin yalikuwa yakimsindikza mpaka alipofika nyumbni kwao.
Ndipo nurdini akaondoka na kurudi alipomuacha rafiki yake samir.
"mwanangu, umenizindisha sana, ila poa nadhani kwa sasa mtoto ameeleweka maana muda niliokaa!, enhe, nipe ripoti mtoto amesemaje." Aliongea samiri pindi tu alipomuona rafiki yake nurdin amefika.
"dah, mwanangu yule mtoto mgumu sjapata kuona, nimemzungusha ilawapi, nimetumia kila aina ya stayle, hadi ile style ya kwenye mkanda wa 'ITS LOVE' lakini wapi, ila mtoto anaonekana amenielewa kwani hata majibu yake yanadhihrisha. Harafu istoshe kile kitoto kina aibu mpaka raha."
"Harafu we jamaa, choko sana. Eti, 'mtoto anaaibu', kwani we ulitaka asiwe na aibu. Kingne huwezi kunizindisha hapa muda wote huo then unanitel eti, dem kazngua, haupo makini."
"sasa, mi mtu kang'ang'ania nimfanyeje. Sibora hata hapo nimewahi kuliko ningeendlea kuongea bila majibu"
"hahahaha, ndomaana na kwambia jamaa yangu. Wewe mapenzi unayaona kwenye movi tu. Jifunze, usinilete mapicha,picha hapa. Kwanza umenilostisha ile mbaya. Nadhani hom watakuwa wamesha lala, so nalala bila njaa kwa ajili ya utumbo wako."
"mkali nawewe mambo yako, sasa hvyo tu ndo unamaind ndugu yangu. Kuhusu menyu twende kwenye vijiwe vya uji vilivyowazi tukajiachie. Sio kumaind, maindi. Then nikifika hom lazma nimuombe broo phne yake ili nisikilize ule wimbo mpya wa yule msanii usiempenda huenda nikaongeza point."
"Hapo umenena, twend sasa kwenye vijiwe," Aliongea samir, na wakaanza kujongea.
"umesema kale ka wimbo kapya?, sikale ka yule msanii mwenye domo kubwa kama la yule mshkaji wetu"
" yeah, hako hako"
"anha,, si wimbo wake unaitwa,, unaitwa,,,"
" Unahangaika nini?, wimbo unaitwa, kamwambie"
"hahahahaha, nilikuwa nimesahau, siunajua siipendi video ya uo wimbo, ila naipenda audio. Mshkaji anaitwa Diamond kama sikosei."
" eeh, waa. Ndo jina lake. Ila mjinga anajua kuimba, nitamsikilizisha na Sumayah siku moja huo wimbo."
waliongea sana siku hyo. Hata walipofika kwenye vijiwe vya uji walikunywa lakini, sumayah hakukatika vinywani mwao.
Walipo maliza kunywa uji, waliagana kwa matani, na kila mmoja akaenda kwao huku wote wakisubiri siku ya jibu kwa hamu ya hali ya juu.
Baada ya Nurdin na samir kuagana na kwenda makwao. Nurdin alifika huku kichwa chake kikiwa kimetingwa na mawazo kuhusiana na Sumayah. Hata alipofakamia kitanda, hakuna alichowaza zaidi ya yale maneno waliyoongea na Sumayah. Mpaka kuna pambazuka hakuweza kubahatisha angalau usingzi hata wa kulingishia.
Upande wa Samir, yeye alipofika kwao alikiendea kitanda chake na kuutafta usingzi ulio mpelekea hadi asubuhi.
Na hata kwa upande wa Sumayah, hali ilikuwa kama kwa samir, hakutaka kuangaisha mawazo yake na kutoutendea haki usingzi wake kisa Nurdin. Nae alilala mpaka asubuhi.
Ilikuwa tayari imeshafika siku ya j'mosi. Kama kawaida Nurdin alijiandaa na kwenda dukani kwao, huku rafiki yake Samir akiumalizia usingzi kama ilivyo kawaida ya wanafunzi kwa siku ambazo hawaendi shule.
Sumayah, muda huo alikwisha amka na tayari alikuwa amesha deki nyumba, kuosha vyombo, kazi aliyo kuwa nayo kwa muda huo ilikuwa ni kupika tu. Hakika hakuwa mvivu kwenye suala la kazi, alipenda kujituma sana hali iliyokuwa ikimpelekea hata mama yake kumuonea huruma.
Nurdin baada ya kufika dukani alifungua duka na kupanga baadh ya vitu kisha akakaa kwa ajili ya kusubiri wateja, haikupita hata nusu saa mara Nurdin akamuona Zulfa akijongea maeneo yale.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kiufupi... Zulfa ni msichana mrembo lakini asie na mashauzi. Ni msichana alieshndwa kuzizuia hisia zake pale zilipompeleka kwa Samir. Aliamua kumfuata samir na kumueleza ya moyoni, lakini samir hakuweza kukubaliana na binti huyo. Alimkataa na kumwaga machozi, si kwasababu Zulfa ni mbaya, Laa! Hasha, bali ni kwa sababu Samir huwa haamin kama msichana anaweza kumtamkia mvulana masuala ya kimapenzi, lakini hapo kabla hata samir mwenyewe alikuwa akimuhtaji sana Zulfa. Japo Zulfa alikataliwa na samir, hiyo haikumfanya kukata tamaa, yeye alibaki kuamini ipo siku Samir atakua wake. Hakuwa mwenye kuchoka, mara kwa mara alijipitisha maeneo apendayo kukaa samir, lakin samir kama wavulana wengine, aliishia kumsanifu na kumnadi mbele ya rafiki zake kwa vijembe huku wakipongezana kwa vicheko vya kejeli. Lakini ilikuwa tofauti sana kwa rafiki yake Nurdin, maana yeye alimjali na kumthamini huku akimpa moyo kwa kumwambia ipo siku ataweza kuwa na Nurdin. Na hiyo ndo sababu kubwa ya Zulfa kupenda kwenda kwenye kibanda cha Nurdin.
"Mambo, Nurdin." Alisalimia Zulfa pindi tu alipofka dukani kwa Nurdin.
"Safi tu lete habari."
"Mie sina jipya zaidi ya kumuulizia huyo mzinguaji"
" mzinguaji yupo tena ni mzima wa afya, mashaka ni juu yako ila kwake ondoa shaka"
"jamaani, Nurdin, nashkuru sana kuskia taarifa hizo, lakini nakuomba nenda kamwambie sitochoka kumfuata japo barua yangu aliichana na kunirejeshea Majibu yaliyoniumiza. Natambua wazi kuwa anafanya yote hayo kwakua anajua nimpendavyo, hanifanyii sawa kabisa. Hebu fikiria hata wewe Nurdin, nimemtumia barua kwa heshma lakini yeye ameiwekea mavi ya njiwa na kuniletea huku akiwa ameichana chana, bado akaona haitoshi akachukua kalamu na karatasi kisha akaandika maneno ambyo yameniathiri sana, japo yeye anajifanya hajui."
" Ni kweli sumayah, una haki ya kulalamika tena sana tu, lakini pia unapaswa utambue kwa muda huu wewe upo vitani. Kuishia kulalamika na kutoa machozi pekee hakuwezi kumfanya adui yako kukuhurumia badala yake atatumia mwanya huo kuku angamiza."
" Unadhani nitafanya nini? Kila nimfanyiacho yeye anaona ni bure, inauma, inauma Nurdin. Nadhani unatambua mpaka sasa nimesha dondokwa na machozi mengi juu yake, lakini nasikitika yeye haweki hata chembe ya kunionesha japo ananihtaji. Basi nipe ushauri nurdin nifanye nini iliaelewe ninacho maanisha?, maana mpaka inafikia wakati nawaza kumuacha lakini nashndwa." Aliongea Zulfa huku machozi yakianza kujichora na kuporomoka kutoka kwenye macho nakuongoza hadi kwenye mashavu, sasa machozi yalifika kwenye kidevu, yakaungana na kuanza kutengeneza matöne ambayo yalianza kuanguka kutoka kidevuni hadi chini ya ardhi, ndipo Zulfa aliposhtuka na kuanza kuyafuta lakini tayari alikuwa ameshachelewa kwani ingawa aliyafuta lakin hyo haikuweza kusaidia kutomtoka mengine. Alipoelemewa na machozi ndipo uchungu ukampanda zaidi kutoka kifuani hadi kwenye koo, na sauti ya kilio ikashndwa kuepukika huku kamasi jepesi likiendlea kumtoka kama ishara ya Maumivu ayapatayo.
"Ina bidi uwe imara Zulfa, unapaswa ujue mapenzi ni kama shule. Iliuweze kutoka darasa moja kwenda jingine basi ni lazma ukumbane na mtihani, sikuzote hakuna mtihani mwepesi. Hata huu ni mtihani kwako, hivyo usikate tamaa shemeji yangu mtarajiwa. Huwezi jua labda samir anakupima iliakuone msimamo wako kwake, hupaswi kukata tamaa kwenye mapenzi. Usiniulize kipimo gani cha maumivu kwani hata uendapo hospital daktari hutumia sindano na kukuchoma lengo si kukuumiza bali ni kukuchukua vipimo iliapate kujua ni ugonjwa gani ukusumbuao. Usikate tamaa kwenye penzi lako." Aliongea Nurdin na kumfanya Zulfa kusahau kilio na kuporomokwa na hasira.
"Sjui nikushukuru vipi Nurdin. Unanipa moyo kwa maneno yako na kunifanya nijihisi sipo peke yangu. Ama kweli mapenzi yana mtihani, basi nakuomba endelea kuwa Mwalimu wangu ilinipate kujisomea mengi na niufaulu mtihani huu."
"Usijali Zulfa, tupo pamoja sana. Hauna kigezo asichokihitaji rafki yangu. Ila wewe tambua tu, Mapenzi ni kikohozi. Hakuna awezae kuficha mapenzi, na ukificha lazma ya kuumbue kama ilivyo katika kikohozi. Nakuomba nenda kapumzike usijiumize bule ilhali kitu ni chako. Pia tambua wahenga walisema, kama ipo ipo tu, hivyo usichoke kuingoja kesho."
"Kila muda maneno yako huniokota pale yanikutapo nimeanguka, misemo yako inanifuta vumbi la manyanyaso, hakika maneno yako ndio kufuli la machozi yanitokayo kwa sababu ya mapenzi, na nina uhakika chozi linitokalo kisa samir, ndilo litakuja kumtoka samir kisa mimi Zulfa. Nampenda sana. Ukimuona mwambie sina kinyongo na yeye bali na htaji sana upendo wake kwani yeye ni zaidi ya taa katika maisha yangu, na muhtaji animulikie pendo langu." Aliongea Zulfa kisha akamuaga Nurdin na kuondoka dukani pale, moja kwa moja hadi kwao.
"Hivi, watu wengne wana akili gani?, sijisemei kwa nia mbaya bali nia nzuri tu. Huyu rafiki yangu nahsi atakuwa amelogwa. We mtoto kama yule anakulilia harafu unalinga,linga. Dah, haya ngoja nione mwisho wao." Nimaneno aliyokuwa akijisemea Nurdin ndani ya nafsi yake. Akiwa katika marumbano hayo ya kinafsi mara ghafla aliingia rafiki yake mpendwa Samir.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"oy, mbna una zubaa, niaje?"
"cøol, mishe nini?"
"dah, full mlimbwanda, vipi home wazima wote?"
"yea, wapo pouw sana tu."
Waliendelea kusalimiana, na hata baada ya kusalimiana ndipo Samir, alipomchokoza Nurdin kwa swali la utani ikiwa kama kifungua maada.
"Vip, mbona mawazo, au mtoto Sumayah amejaa akilini nin?" Aliongea Samir huku akimuangalia rafiki yake.
"Hapana Samir, siwezi kumuwaza ilhali natambua fika kwamba yeye yupo na mzima wa afya. Inatosha kumuombea kwa mwenyezi Mungu tu, na sito acha kumvumilia mpaka hyo J'tatu maana mvumilivu hula mbivu, staki niwe king'ang'anizi kwa haraka zangu. Natambua wazi haraka haraka huwa haina baraka, ndomaana naenda pole pole ilinisijikwae. Staki nipate jibu changa, jibu ambalo litanifanya nile tunda langu kwa ukakasi utakao nipelekea kulichoka mapema. Ninachohtaji ni kuvumilia ili nile tunda likiwa mbivu." Aliongea Nurdin huku rafiki yake Samir akiwa kimya na kumsikiliza mwenzie kwa umakini.
" Na wewe nurdin una viswaga, mara ooh, mvumilivu hula mbivu, mara ooh, haraka,haraka haina baraka. Ha,ha,ha. Unanifurahshaga sana rafki yangu. Kama unawafuata wahenga mbna haohao wahenga ndio waliosema kwamba. Ngoja ngoja huumiza matumbo, kuchelewa utakuta mwana si wako. Inamaana maneno hayo hauku yaona.
Hebu ngoja nikupe kitu ambacho hauna kuhusu mapenzi. Unajua mtu aliependa ni sawa sawa na mlevi, mlevi huwa hatumii akili yake bali huendshwa na pombe na ndio maana hujikta akifanya mambo ambyo laiti angelikuwa hana kilevi akilini ni wazi asingeliweza kuyafanya. Vivyo hivyo kwa mtu aliependa, hufanya mambo kwa kuendshwa na upendo tu na si akili yake. Nadhani sibusara kwako mpenda kujifanya mgumu wakati tayari umeshapenda, elezea hisia zako popote pale, muda wowote ule, pasina kujali. Hata huyo aliekupa mtihani hebu muoneshe athari na sikubung'aa tu. We unadhani kupitia vijimaneno vyako anaweza kuku amini?, muda mwingne ina bidi mapenzi ya chukue nafasi yaliyo nayo." Alimaliza Samir kuongea huku muda wote huo Nurdin akiwa ameyaazima maskio yake kwa samir. Walipiga sana soga za kumhusu Sumayah, na kumuongelea kwa mengi mazuri bila shaka kama ile imani ya wazee isemayo, Uongelewapo hutokosa kujing'ata. Basi ilifanya kazi.
Wakiwa katika burdani ile ya Maongezi huku wote kwa pamoja wamesha tekana hisia na kuwa kama watoto ndipo Nurdin alipotumia nafasi ile kufikisha ya Zulfa.
"Harafu nimekumbuka, Z, alikuja hapa na kuanza kulaumu vipi umemkwaza nini?"
"oya, nurdin kama umekosa maada za kuongea basi ni bora ukakaa kimya, staki umuongelee huyo dem."
"kwanini samir, au siku hizi unanificha mambo yako. Mimi kukuuliza kuhusu Zulfa tayari nimekosea. Ok."
"Sio, hivyo jemedari langu. Unajua laiti kama ningelikabidhiwa kalamu ya kuandika madhambi unifanyiayo. Basi dhambi kubwa lingekuwa ni hilo la wewe kumuongelea Zulfa mbele yangu. Nakuomba mkali wangu, mteme huyo binti"
"Siwezi kuvumilia kumuona msichana anaumia kwa ajili yako ilhali wapo wavlana wengi, Samir kama unahsi mimi nimetenda dhambi kwa kumtaja Zulfa basi nakuomba usinisamehe na ni hukumu niende motoni kwa dhambi hii, ila taka usitake lazma uwe nae huyo msichana. Hebu fikiria mambo mangapi anakufanyia, upendo gani anakuonesha, na uwaze mimi nilishafanyiwa hvyo na Sumayah?, ndipo upate nafasi ya kumjaji. Kwani anakosoro gani yule msichana hebu niambie leo."
"Unajua Nurdin yule binti hata mimi namuelewa lakini mimi huwa najua waschana vicheche ndio huwa wanatongoza wavulana." Aliongea Samir.
"Nani alikwambia mwanangu?, au unaleta pigo zako tu hapa. Ngoja nikwambie kitu kimoja.. Unajua kuna kitabu kimoja alikuja nacho broo. Si unajua nami nilivyo spendi kupitwa?, ni kakichukua na kuanza kukisoma ndipo nikakutana na suala la mapenzi kwa magashi. We utajulia wapi unakalia kubung'aa tu na kukalili." Aliongea Nurdin.
"Acha kuniletea mkali wangu, sasa mambo ya kubung'aa hapo yamekujaje. We unachotakiwa unitel ma inshu na si kunipogomea kishamba hapa, ohoo, tutaharibiana." Aliongea Samir huku mikono yake akiichezesha, utadhani mwanamziki wa hiphop.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kwahyo unanipandishia sio?, afu skiliza we bwege usjifanye unamikato yaki blanta. Mi mwenyewe muhuni, lione kwanza dume zima unashndwa kuelewa hisia za mtu."
"ok, basi mkali wangu kama vpi kausha. Unajua mimi sikuongea kwa kukurupuka, ila nilisha waskia kina broo wakiongelea mishe hizi za madem. Wakasema madem hata kama wakipenda vipi huwa hawa semi, na wale ambao huwa wanawatamkia washkaji masuala ya mapenzi, hao huwa ni vicheche ila dem wa kweli huwa na aibu na hawezi kuongea kama huyo Zulfa" Aliongea Samir na kumfanya Nurdin aangue kicheko kilichompelekea ashikirie mbavu.
"oy, mbna unacheka,cheka. Kama mamy? Kwani hiyo mishe inachekesha. Au unataka mimi niingie kwa huyo du, kicheche." Aliongea Samir huku akionesha wazi kukerwa na kitendo cha rafiki yake kumcheka.
"Unajua nini mwanangu"
"sijui"
"ok, unajua hata mimi nilikuwaga naamini mishe hiyo ila kale ka kitabu alikonitoa broo... Ndiko kaliko nifumbua mengi. Ni hivi, sisi mamen na hao magashi tuna tofauti kubwa sana. Magashi huwa wana aibu na uoga wa kutojiamini kwenye mambo nyeti kama hayo, ila mamen huwa tunatabia ya kujiamin na kujitosa. Hiyo ndio tofauti yetu, lakini hakuna sheria inayosema eti, dem akikufata ujue ni kicheche, hzo ni longolongo tu za kitaa. Harafu unapaswa utambue wazi kuwa. Msichana anauwezo mkubwa sana wakujizuia zaidi ya mvulana, ila mpaka kufikia kukuteli kwamba anakupenda ujue ameshndwa kujizuia na anakupenda sana. Nadhani umeni manya." Aliongea Nurdin na kumfanya rafiki yake ashangae sana.
" Yaweza kuwa kweli, lakini bado hujanishawishi. Kwani yale mamalaya yanayojiuza mtaani, menyewe sindo huwa yanawatongoza wanaume?, mi bado sijashawishka na maneno yako mwana" Aliongea Samir huku akionesha kutokuridhka na majibu ya Rafiki yake.
"Hahahaha, we bado choko kweli, nilidhani naongea na mtu aliekua. Kumbe bado unanuka maziwa kabisa, hivi we unadhani yale madem yanayo jiuza huwa yanapenda mtu au pesa. Ok, tufanye Zulfa anajiuza kwako. Je, wewe unamapene?, au unanini cha kumpa yule dem. Hauna kitu fukara mkubwa unategemea hom, ila ona anavyokupenda. Haya class huwa yanakupita ina maana hata picha hujui kusoma?" Aliongea Nurdin na kumfanya samir apandwe na hasira lakin hasira zake zilimshuka kadri Nurdin alivyozidi kuongea.
"Hee!!, mwanangu umeyajulia wapi yote hayo?" Aliongea Nurdin kwa mshangao ulioambtana na swali.
"Mimi mwenzako huwa nasoma majarida, magazeti na vitabu, we sihuwa unajifanya mvivu wa kusoma."
"Kwahyo mwanangu, unataka kusema mimi ninapendwa!, mbna sijawah kutarajia maishani mwangu kwamb nitapendwa, mi najua magashi ndo huwa wanapendwa."
"Yea, unapendwa tena sana tu. Unajua wewe huwezi kuvijua vivutio ulivyoumbwa navyo, ila mtu tofauti na wewe ndio anae viona. Labda nikwambie kitu, huyo dem amekufa na kuoza kasoro kunuka tu, kwa ajili yako. Sema we unajifanya boya, shauri yako ila mimi ndo mwanao lazma ni kutonye"
"Dah, poa mwanangu. Nitajifikiria, ok, tuachane na hayo ya Z, twende kwa Sumayah, vipi mwanangu"
"Mzee samir, yule du, bora kumuacha mpaka j'tatu. Ila tuking'ang'ania, anaweza kuchomoa"
"ok, mkali wangu"
Waliongea mengi sana. Na ndipo Nurdin alipomfahamisha rafik yake Samir kuwa Tayari ameshakamilisha vifaa vya skul, hvyo J'tatu atawasili shule kwa ajili ya kuanza masomo ya Sekondary.
Samir alifurahi baada ya kuskia hvyo na hakusita kumshauri mwenzie asome kwa bidii.
Labda tu mpenzi msomaji nikufahamishe kitu kimoja. Samir na Nurdin ni marafiki ambao wanazidiana darasa moja. Kwa muda huo Nurdin alikuwa amechaguliwa na taifa kuendlea na elimu ya vidato, lakini Samir alikuwa bado yungali darasa la saba na alikuwa daraja moja na Sumayah lakin, walikuwa wakitofautiana shule ila wote waliitwa, L,Y(last,year) au mwaka wa mwisho kwa lugha ya nyumbani. Na kuhusu Zulfa, yeye alikuwa darasa la sita katika shule moja ya binafsi huko nje ya mkoa, lakin kwa wakati huo alikuwa yupo nyumbni kwao kutokana na likizo ya Mwezi wa nne. Hakuna kati yao aliekuwa amefikisha miaka kumi na sita, wote walichezea miaka kumi na tano hadi kumi na nne tu. Nadhani utashangaa sana vijana hawa kuwa na ujuzi wa mambo pengine kuliko hata umri wao, lakini hiyo ilitokana na wao kuyawahi mapenzi tu, na kujikuta wanasoma sana mambo yanayo husiana na mapenzi. Na kipindi chao ilikuwa ni zaidi ya tabia mbya mvulana kuwa na msichana kutokana na rika lao, ila wao waliyawahi sana...
Hatimae ilifika siku ya j'tatu na kama ilivyoada, siku hiyo huchukiwa na wengi. Si wanafunzi, wala wafanyakazi wa maofisin. Samir alijiandaa japo kivivu na kwenda shuleni, vivyo hvyo kwa Sumayah, bila kumsahau Nurdin ambae nae kwa Mara yakwanza alikuwa njiani kuelekea shule ya vidato kwa ajili ya kwenda kuripoti, alikuwa na zaidi ya furaha kwani hali ya yeye kila siku kukaa dukani na kuwaona wenzake wakitoka shule, si tu ilikuwa kero bali ilimuumiza pia. Alifika shuleni na kuripoti, siku ya kwanza tu ilimtosha yeye kuyazoea mazingra ya shuleni pale.
Upande wa zulfa, yeye alifanya kazi za nyumbani na hata baada ya kumaliza alichukua kitabu cha MAGIC WOMAN kilichoandikwa na mtunzi kwa jina la ZUBERY RAZUUR MAVUGO.
"hamjambo wanafunzi?" Aliongea mwalimu mmoja wa sayansi, anaefundisha katika shule wanayosomea kina Samir. Wanafunzi wote kwa pamoja waliitikia na kumsalimia Mwalimu yule wa Sayansi.
"Wanafunzi, leo tutaanza mada yetu mpya ya uzazi. Ila kabla hatujaanza ningependa kuwa uliza maswali mawili matatu yanayoshabihiana na mada hii, nadhani mlisoma kipindi mpo darasa la sita. Bila kupoteza muda, ningependa mwanafunzi mmoja asimame na kuniambia kubalehe ninini?" Aliuliza mwalimu yule wa sayansi, swali lililowapelekea wengi kati ya wanafunzi wale kucheka, na wachache wao hasa wasichana kuhisi aibu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hiyo ilikuwa tofauti kwa kijana samir, na hakusita kusimama na majibu yake yalikuwa hivi; "kubalehe, ni ile hali ya kutoka kwenye daraja la utoto na kuelekea kwenye utu uzima. Na mtu anaebalehe lazma akumbwe na mabadiliko mbalimbali amb..." Hata kabla haja malizia. Mwalimu alimkalisha chini kutokana na maneno mengi aliyokuwa nayo.
Alichukua chaki yake na kuandika ubaoni maada ya uzazi, kisha akatoa ndondoo juu ya maada ile. Hata alipokaribia kumalza kufundisha ndipo alipotoa muda wa maswali. Aliulizwa Maswali mengi sana na yote aliyajibu kwa ufasaha. Wanafunzi waliishiwa kiu ya maswali kuhusu mada ile, ndipo mwalimu aliporuhusu maswali hata ya nje ya mada.
Ni dhahri kwamba Samir kuna jambo lililokuwa likimtatiza, ndipo alipotumia nafasi ile kuuliza swali hilo kwa mwalimu wake. Alijua wazi kuwa adhabu yake itakuwa ni kuchapwa lakin hakuwa na jinsi, aliona liwalo na liwe lakin lazma aulize swali lile.
"Samahani Mwalimu kama nitakosea lakin lengo langu si baya," Aliongea na kutolewa shaka, kisha akaendelea na Swali lile.
"Mwalimu, watu wengi wamekuwa wakilia, na wengne kufurahi, pia kuna wale ambao huwaona malimbukeni wenzao kwa sababu ya Mapenzi. Hata juzi kuna mtu kajinyonga na kuacha barua kwamba, kajiua kisa mapenzi. Je, Mwalimu waweza niambia Mapenzi ninini?" Aliuliza Samir, na kupelekea hali ya ukimya darasa zima. Kila mwanafunzi alimshangaa, si mwanafunzi tu. Hata mwalimu hakusita kushangaa swali lile.
"Swali zuri sana samir, na lipo ndani ya mada. Ila linahtaji mapana ya hali ya juu na muda nadhani hautoshi, ila kipindi kijacho tutaanza na mada hiyo ndogo, samahani kwa kutokukujibu kwa sasa." Aliongea mwalimu na kumfanya Samir kujiona si mwenye Makosa kama alivyokua akijifikiria. Wanafunzi wote walijawa na shauku ya kutaka kupata maana ya neno Mapenzi, na walikisubiri kipndi cha sayansi kwa hamu sana.
Hata ulipofika muda wa kutoka shule, Samir alienda kwao. Alimkuta rafiki yake Nurdin katika chumba chake na kushangaa.
Aliuliza uwepo wa Nurdin muda kama huo, lakini Nurdin alimwambia kua wao wanatoka shuleni saa 8:30(nane na nusu).
Samir alioga kisha akafata chakula na kula, baada ya kula walianza kupiga soga. Nurdin alikuwa muongeaji sana kutokana na ushamba wa kwenda sekondari, alimuhadithia mengi mwenzie, mpaka ukafika muda wa saa kumi na mbili jioni.
Wote kwa pamoja waliamua kwenda kusaidia kufunga dukani, na baada ya hapo wakaenda msikitini kuswali, swala ya saa moja ijulikanayo kama Magharibi. Swala hiyo inaitwa magharibi kutokana na kusaliwa baada ya jua kuzamia upande wa magharibi.
Hata walipo maliza kuswali, hawa kuwa na laziada zaidi ya kwenda kujipitisha kwa kina Sumayah, kwani hiyo siku ndio ilikuwa siku ya ahadi kati ya Sumayah na Nurdin.
Walikaa sana bila hata dalili ya kumuona Sumayah. Baridi liliwapiga lakini hawakutaka kukata tamaa, mbu nao hawa kuwa nyuma, waliwang'ata kuliko kawaida, lakini hiyo haikuwafanya wawindaji hao kukata tamaa kwani waliamini kuwa Muwindaji wa kweli huwa hakati tamaa.
Adhana ya saa mbili usiku ililia pasina wao kumuona Sumayah, muda ulizidi kuyoyoma kwanzia sekunde, hadi dakika. Hatimae ulifika muda wa kuswali swala ya saa mbili, ijulikanayo kama swala ya ISHA.
"Oy, mwana huyu du, anazingua we kama vipi twende tukapige rakaa tu, hata kesho ni siku." Aliongea Samir, lakini majibu yale hayakuweza kumuingia hata kidogo rafki yake Nurdin ambae alikuwa na shauku ya kuonana na Sumayah.
"Dah, mwanangu. We kaswali tu, mi siondoki hadi dakika ya mwisho." Aliongea Nurdin.
Nurdin aliachwa pale. Hazikupita hata dakik tano mara ghafla akamuona Sumayah akitoka kwao.
Hakuamini kama taswira aionayo mbele yake ilikuwa ya Sumayah. Alipikicha macho kwa ajili ya kujitoa hofu kisha akatazama tena. Ndipo alipoamini kuwa akionacho ni ukweli na si ndoto.
Mwili mzima ulimsisimka, bila hiyari yake vipele vya uogo vikatanda mwilini mwake. Aliwaza huenda akapewa jibu lisilo kuwa zuri kwake, lakini alipiga moyo konde na kuangaza kulia na kushoto kisha akajitosa.
Hata alipomfikia, walisalimiana na baada ya hapo Nurdin aliomba jibu lake.
"Nurdin, niskupotezee muda wako, nawe pia usinipotezee muda wangu. Ingefaa zaidi ni chunguze kwa umakini lakini sina jinsi kukubaliana na matakwa ya ulichokiomba." Ni maneno yaliyomponyoka Sumayah na kumfanya Nurdin asiamini aambiwacho.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Siamini!!, kwa hiyo umekubali, kuwa mpenzi wangu, na yote yaliyokuwemo kwenye barua ile" Aliongea Nurdin huku akionesha jinsi jambo lile lilivyo muathir.
"Ninapo sema nimekubali, na kuwa na maana ya kukabili kila tatizo ulilonalo. Ulisema usiku haulali kisa mimi, basi natumai niwakati wako wa kuchukua shuka na kupata usingzi nyororo na hata kulipiza siku usizo lala. Ninachoongea nimekidhamiria na siongei tu ilimradi, nimechukua muda wangu kukufikiria na hayo ndo majibu yangu" Aliongea Sumayah.
Kilio cha furaha kilijithihirisha wazi usoni mwa Nurdin kupitia machozi yaliyo mtoka bila hiyari yake, huku akichanua midomo yake na kusababisha tabasamu pana.
"Nizaidi ya shukrani kukubaliwa jibu langu nawe Sumayah, naomba unitamkie dhahiri kuwa unanipenda, ili naminiiskie sauti yako ikitamka hivyo."
"Nakupenda Nurdin na nimeamua kukukabidhi ufunguo za moyo wangu. Na kuahidi nitaendelea kukupenda na wewe ni zaidi ya mume wangu mtarajiwa." Aliongea Sumayah na hata kujikuta machozi yakishndwa kujizuia, palepale mboni za macho yake ziliruhusu machozi na kumpelekea alie kutokana na maneno yake. Ni wazi kuwa Sumayah hakuwahi kupenda, lakini alipendlea sana muvi za mapenzi, nadhani hata alipokuwa akiongea basi alifanya kama anaigza, lakini hakujua kuwa ulimwengu wa mapenzi ni ulimwengu usio na matani hata kidogo na ndio maana alijikta akichomokwa na machozi.
Maneno ya Sumayah, yaliuathiri vilivyo moyo wa Nurdin hasa ukizingatia vijana wale walikuwa bado wadogo, hakika walijikuta wakishndwa kuzizuia hisia zao na wote kwa pamoja wakakumbatiana, huku machozi ya kiendlea kuloanisha nguo za wawili hao.
Waliongea mengi sana ikiwa ni pamja na kuweka ahadi za kuaminiana. Hata walipoagana kila mmoja alikuwa na furaha. Sumayah alipofika kwao aliambulia matusi mfululizo lakini hiyo haikumfanya ajutie uamuzi wake wa kuonana na Nurdin. Na wala hakujiona mkosaji. Upande wa Nurdini nae alijawa na Maji ya furaha, hata alipofika nyumbani alisahau kitu kinachoitwa chakula. Alienda na kujitupia kitandani bila hata kutandika na mawazo yote akayarejesha katika kumbukumbu ya Maneno ya Sumayah.
Hata alipopatwa na usingizi, hakusita kulala na alipoamka tu, tayari ilikuwa ni j'nne tena iliyopevuka. Alijigundua kuwa amechelewa namba shuleni, ndipo akajiandaa kwa haraka na kwenda shuleni hivyohvyo.
Upande wa Samir, yeye aliwahi shule na hata baada ya wao kuingia darasani. Haukupita muda akaingia mwalimu wa Sayansi huku mkononi akiwa ameshikiria chaki ilhali hakuwa na kipindi kwa siku hiyo. Aliwasalimu wanafunzi wake nao wakaitikia kwa heshma.
"Natumai, ujio wangu utakuwa umewashangaza sana. Nimeamua kuomba kipindi ilinije kukamilisha ile ahadi yangu ya kiporo cha swali la Samir." Aliöngea na kuwafanya wanafunzi wote kufurahi sana kwani hakuna kati yao ambae hakuwa na shauku ya kufahamu Maana ya mapenzi. Mwalimu huyo alichukua chaki na kuandika neno mapenzi kwa herufi kubwa kisha akalipgia msitali.
"Kabla hatujaanza mada yetu. Je, kuna mwanafunzi ambae anaweza kutuambia maana ya mapenzi jinsi ajuavyo.?" Aliongea Mwalimu yule na pasina matarajio yake alishangaa kuona darasa zima limeinua mikono juu na kuruhusu vidole vyao vya shahada kuwakilisha adhma zao za kujibu swali.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"ok, mmekuwa wengi sana. Nitachagua msichana mmoja na mvulana mmoja kwa ajili ya kujibu." Alisema mwalimu yule na kuteua mvulana mmoja na msichana mmoja kisha darasa zima likatulia kwa ajili ya kuskiliza kisemwacho.
"Mapenzi ni kama gereza lenye manyanyaso ndani yake" Yalikuwa ni majibu kutoka kwa msichana aliechaguliwa na Mwalimu. Kisha akafuata mvulana.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment