Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

RAHA YENYE MAUMIVU - 1

 





    IMEANDIKWA NA : ALLY MBETU



    *********************************************************************************



    Simulizi : Raha Yenye Maumivu

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    RAHA YENYE MAUMIVU

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hali ya hewa katika mji wa Arusha ilikuwa ya ubaridi kila mmoja alikuwa na nguo nzito za kukabiliana na hali ya hewa. Ila kwa wenyeji wa mkoa huu walikuwa na nguo za kawaida kwao ile hali ya ubaridi kwao ilikuwa ya kawaida hata nguo walizovaa zilikuwa nyepesi tofauti na mgeni wa mkoa huo.

    Katika hotel ya New Arusha kila mmoja alikuwa bize na unywaji wa pombe na utafunaji wa nyama choma. Mmoja ya waliokuwa wakipata moja moto moja baridi alikuwepo mama mmoja ambaye umri wake ulikuwa umekwenda kidogo lakini kutokana na uwezo wake wa kipesa alionekana bado.

    Yule mama mmoja ya wafanya biashara wakubwa pia alikuwa wanawake wenye pesa nyingi. Pale Arusha alikuwepo kibiashara akiwa safarini nchi za Ulaya. Ni mkazi wa jiji la kila aina ya maraha jiji la Mheshimiwa Rukuvi hapo mwanzo lilijulikana kama jij la Muheshimiwa Kandolo.

    Katika maisha yake alibahatika kupata mtoto mmoja wa kike ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 19 ambaye alikuwa yupo kidato cha tano moja ya shule za gharama nchini.

    Kwa muda huo hakuwa na mume baada ya kuachana na mume wake, kwa jeuri ya pesa ilimpelekea kuachana na mumewe kwa kuona maisha ya ndoa ni utumwa ambao yalikuwa yakimwekea mipaka ya kazi zake.

    Toka aachane na mumewe hakuwa na haja ya kuolewa tena na mwanaume zaidi ya akili yake kuielekeza kwenye biashara ambayo ilimfanya awe na uwezo mkubwa kipesa na kuwa na uwezo wa kufanya lolote atakalo.

    Biashara zake zilivuka mipaka mpaka nje ya nchi alijikuta muda mwingi aliutumia kusafiri kwa ajili ya biashara zake hata jina lake lilikuwa moja na watu wenye uwezo wa kifedha jijini. Kitu kilichomfanya asiwe na wazo la kuolewa tena na kuchukulia mwanaume ni kitu cha starehe kwake.

    Kutokana kuwa na pesa nyingi alipokuwa akishikwa na haja za kimapenzi alimhonga mwanaume yoyote amtakaye na amalizapo kumstarehesha huupa ujira ambao alijua lazima utamfurahisha hakuwa na bwana maalumu kwa kuogopa kuoneana wivu. Kitu kilichomfanya kuwa na uhuru wa kufanya mambo yake bila kuingiliwa na mtu.

    Mam’ kubwa kama jina lake maarufu jijini Dar, akiwa jijini Arusha ambako alipita kufuatilia madeni yake akiwa njiani kwenda Uingereza baada ya kukusanya madeni yake alipanga kwenye Hotel ya new Arusha. Majira ya saa moja usiku alijumuika sehemu ya vinywaji kupata moja moto moja baridi.

    Akiwa ametafuta meza ya pembeni aliagiza bia yake ya castle ya kopo na kunywa taratibu huku akifikiria safari yake ya asubuhi katika uwanja wa ndege wa KIA alikuwa amepanga kuondoka na ndege ya saa kumi na mbili asubuhi ya shirika la Gurf Air.

    Pombe zilivyo kuwa zikimzidi kumpanda alijikuta akipata hamu ya kuwa na mwanaume kama kawaida yake alivutiwa na kijana mmoja aliyekuwa mhudumu upande wa uchomaji wa nyama. Kijana ambaye alikuwa akimletea nyama, wakati akiendelea kukata maji taratibu kama mamba mzee kwenye bwawa.

    Wakati yule kijana akimletea maji ya kunawa alijikuta anamuuliza kwa sauti ya kilevi kidogo.

    "Samahani kijana sijui unatoka kazini saa ngapi?"

    "Muda si mrefu kuanzia sasa wanaokuja kutupokea wameisha ingia hapa najiandaa kwenda kuoga."

    "Mmmmh sawa," alijibu huku akichukua kopo la bia na kupeleka kinywani.

    "Kwani vipi?"

    "Hapa Arusha una kaa wapi?" Alimuuliza baada ya kumeza funda ya pombe.

    "Unga limited."

    "Umeoa?"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Maisha ya kuoa yapo wapi ma’ mkubwa, hela ninayo pata hailingani na hali halisi ya maisha. Mwenyewe tu maisha yananipeleka mchakamchaka huyo mwanamke nitamlisha hewa."

    "Mmmh pole sana...Sasa ni hivi naomba kabla ya kuondoka tuonane shika na hii hela njoo na vinywaji nipo chumba namba 033 ...sawa."

    "Sawa mama," yule kijana aliondoka kwenda kujiandaa kukabidhi kazi kwa wenzake, wakati huo mam’ kubwa alimsindikiza kwa macho alijua kijana kaisha nasa kwenye mtego wake.

    Mam’ kubwa alibeba kinywaji chake kilichobakia na kwenda nacho chumbani kwake kusubiri mtego wake kama utanasa japo alikuwa na imani kwa asilimia 99%. Alipofika chumbani kwake alikwenda bafuni kuoga harakaharaka na kuvaa nguo nyepesi ya kulalia na nguo moja ya ndani.

    Alipulizia mafuta yenye harufu nzuri na kukaa mkao wa mamba majini wa kumvizia mwanadamu. Akiwa anamalizia kinywaji chake alisikia mlango ukigongwa moyo ulimpasuka alimkaribisha.

    "Pita mlango upo wazi," mlango ulifunguliwa na kuingia mkusudiwa alipomuona aliachia tabasamu pana.

    "Oooh karibu sana."

    "Asante," alikuwa ameshikia vinywaji alivyo agizwa.

    "Karibu jisikie uhuru wa lolote utakalo nina imani usiku wa leo utakuwa pamoja nami," Mam’ Kubwa alisema huku akiachia tabasamu la jisikie huru.

    "Hamna tabu mama."

    "Usiniite mama niite Sweet."

    "Hamna tabu Sweet."

    "Ukinifurahisha na wewe nitakufurahisha, hutanisahau kama vile utavyonifanya nisilisahau penzi lako."

    Kijana hakuwa nyuma waliendelea kupata vinjwaji huku wakipapasana hapa na pale kila mmoja akijitahidi kumfurahisha mwenzake. Muda ulipotimu kijana alitumia ujuzi wake wote kuhakiki anamkata jimama kiu.

    Mtinange ulikuwa mzito uliomfanya kijana wa watu awe hoi kama dume la bata na kujikuta akipitiwa usingizi mzito. Penzi alilopewa jimama lilimrusha akili kama isingekuwa safari angeongeza siku za kuwepo Arusha ili kuendelea kukatwa kiu na kijana. Penzi ambalo anakumbuka alilipata wakati anavujwa ungo.

    Jimama aliamka alfajiri ili kuwahi safari yake wakati huo kijana alikuwa bado amelala hajitambui. Hakutaka kumsumbua aliamua kumuachia pesa ambayo alijua itamsaidia maishani mwake na kumuachia ujumbe mfupi uliosema:

    Mpenzi..Tino nina imani jana ilikuwa siku yangu ambayo itakuwa ya kuikumbuka maishani mwangu. Penzi ulilonipa sijui kama nitalipata tena.

    Kama nilivyokuahidi nami sina budi kukupa zawadi ambayo itakusaidia kusogezea siku. Bakia salama Mungu akijalia tutaonana ni mimi mama Teddy.

    Alikiweka kile kikalatasi na shilingi laki saba kwenye mfuko wa suruali wa kijana Augustino Tamilway kisha alimpiga busu kwenye shavu na kuondoka kuwahi usafiri wa ndege uwanja wa ndege wa kimatafa wa Kilimanjaro (KIA)

    Aliwasiri kiwanjani nusu saa kabla ndege haijaondoka na kufuata taratibu zote zilizomwezesha kukamilisha taratibu za usafiri na saa kumi na mbili juu ya alama Mam’ kubwa au mama Teddy aliiaga anga ya Tanzania.



    Kijana Augustino Tamilway au kama wengi wapendavyo kumwita Tino aliposhtuka usingizini alijishangaa kujikuta yupo peke yake kitandani. Alipepesa macho yake akijua labda jimama amekwenda kuoga lakini alikumbuka jana alimweleza ana safari alfajiri.

    Aliona yule mama alimdanganya na kumkimbia hata bila ya kumuasha, lakini alijipa moyo kuwa kuna chenji ambazo hakumrudishia Mam’ Kubwa wakati akimtuma pombe ambazo si chini ya elfu nane alijua zitamtoa kwa asubuhi.

    Lakini wazo lilimjia huenda yule jimama amezichukua zile hela zitazomfanya aone siku ngumu kwake wazo lake la kwanza ni kwenda kuziangalia zile hela zake kama zimo au la.

    Alinyanyuka hadi sehemu aliyoweka suruali yake kitu kingine kilichomtia hofu ni ile hali ya suruali ilivyo kuwa ni tofauti na yeye alivyoiweka. Aliichukua suruali na kuingiza mkono mfuko alishangaa mkono kukutana na uzito alishika vizuri kilichokuwemo na kukitoa hakuamini macho yake zilikuwa pesa nyingi zilizo zungurushiwa kalatasi ndogo nyeupe.

    Alizirudisha zile pesa mfukoni na kukisoma kile kikalatasi kilichokuwa na maneno matamu ambayo yalimfanya azitoe zile hela na kuzihesabu zilikuwa laki saba. Tino alishukuru Mungu kweli unaweza kulala maskini na ukaamka tajiri ule usemi ulijidhihirisha kwake.

    Katika kitu alichokuwa akikitafuta maishani mwake ni kupata mtaji ambao utamsaidia maishani yeye katika kuhangaika aliomba siku moja apate laki moja ya mtaji lakini siku ile amepata laki saba. Alijua huo ndio mwisho wa kufanya kazi za kuajiliwa alipanga kukimbila jijini Dar kuanzisha biashara ya mitumba.

    *****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Augustino Tamilway baada ya kupata kiasi kile kikubwa cha pesa hakuwa na haja ya kupoteza muda aliamua siku ya pili kukimbilia jijini Dar bila kuwaaga watu zaidi ya rafiki yake mkubwa Dani kuwa anakwenda Dar kujaribu maisha. Lakini hakumweleza kuwa ana pesa za kumfanya asiyumbe kimaisha katika jiji linalo aminika ndilo linaloongoza kwa matumizi ya pesa kila kitu kinanunuliwa mpaka uchafu.

    Aliondoka jijini Arusha majira ya saa kumi na mbili na basi la Dar express na kuwasiri jijini majira ya saa tisa mchana hakuwa mgeni wa jiji alikwenda kwa rafiki yake Flibert aliyekuwa anakaa Keko Mwanga.

    Kwa bahati alimkuta rafiki yake ambaye alikuwa akifanya kazi kampuni ya Plasitic. Hapo ndipo Tamilway alipoanza maisha yake kwa kuulizia biashara gani zinazofaa alielekezwa na kuanza na biashara ya kutandaza chini mtaa wa Kongo .

    Alijikuta akipata faida kila kukicha na kufikia hatua ya kusajili watu kumuuzia biashara zake. Alijikuta akipata pesa zilizomfanya aongeze biashara zingine ikiwa pamoja na kununua fremu ya kuuzia biashara zake zilizompa utajiri wa haraka sana.

    Wakati huo alikuwa ameishahama kwa rafiki yake Filbert na kupanga chumba chake mwenyewe maeneo ya Temeke Wailes.

    ********

    MIEZI MITATU BAADAYE JIJINI LONDON UINGEREZA



    Mabadiliko ya hali ya mam’ kubwa au mama Teddy yalimtia wasiwasi baada ya kupoteza siku zake kwa muda wa miezi miwili kitu kilichomtia wasiwasi na kumfanya aende hospital kuangalia afya yake ajue ile hali ya kutokuziona siku zake inatokana na nini.

    Baada ya vipimo vyote ilionekana Mam’ kubwa ni mjamzito wa miezi miwili kitu kilicho mshtua na kuuliza mara mbilimbili.

    "Ni kweli usemayo dokta?"

    "Kwa nini nikudanganye wewe ni ujamzito wa miezi miwili."

    Baada ya kusikia taarifa ile ilimfanya arudishe kumbukumbu zake nyuma na kujiuliza ni mwanaume gani aliye kutana naye miezi mitatu nyuma. Jibu lilikuwa ni Tino kwani ndiye anayekumbuka alikutana naye siku za hatari lakini hakuwa na wasiwasi kwa kujua muda ule hawezi kuzaa tena.

    Toka afike jijini London akuwahi kutembea na mwanaume kwa kupindi cha mwezi mzima, kwa kuwa alikuwa bize ma masuala ya biashara. Mara nyingi alipenda kufanya starehe baada ya kumaliza pilikapilika zake za biashara.

    Kama ujauzito ungekuwa wa mwezi mmoja angejua ameupatia pale lakini wa miezi miwili lazima alijua ameupatia Tanzania tena jijini Arusha na aliyempatia si mwingine ni Tamilway yule muhudumu wa hotel ya New Arusha.

    Pamoja na kupata mshituko haukuwa wa kujuta bali wa furaha kwani ni baada ya miaka 19 toka ajifungue mtoto wake wa kike ambaye kwa sasa anakimbilia miaka 20. Japo alikuwa na hamu ya kupata mtoto mwingine lakini hakubahatika pamoja na kumsaka kwa udi na uvumba lakini aliambulia patupu.

    Alitumia dawa za mwanga na kiza zote zilidunda pamoja na kujitahidi kubadilisha wanaume kila kukicha. Alijua Mungu alimpa mtoto mmoja wa kike hata hivyo alimshukuru Mungu kwa kumpatia mtoto wa kike kwani wapo waliokosa kabisa.

    Ilikuwa ni furaha isiyo na kifani baada ya kupata uhakika kuwa ana ujauzito wa miezi miwili. Aliamua kubakia Uingereza ambako alipanga angekaa kwa muda na kutimkia Marekani ambako angeendelea kuutunza ujauzito wake karibu na hospitali kubwa duniani ili kuhakikisha hampotezi mwanaye.

    Aliogopa kurudi Afrika kwa kuwa wanawake walio wengi upoteza watoto kwa sababu za kizembe. Hata mwanaye anayesoma Hi-lavel alimwagiza amalizapo mtihani wa kidato cha sita amfuate mama yake ulaya.



    MIEZI TISA BAADAYE



    Muda wa kulipo timu aljifungua salama mtoto wa kiume aliye kuwa na afya njema, aliyempa jina la baba yake mzazi Malon. Baada ya miezi sita ndipo alipoamua kurudi jiji Dar, siku aliyofika hakupumzika alikwea ndege hadi jijini Arusha kumtafuta kijana Tamilway ambaye alimuona anamfaa kuwa mumewe japo kijana mdogo kwa sababu penzi halichagui umri.

    Mam’ kubwa au kwa sasa analipenda aitwe mama Malon aliwasiri Arusha majira ya saa kumi jioni na kwenda moja kwa moja Hotel ya New Afrika na kumuulizia Tamilway. Kutokana na muda mrefu kupita aliwakuta wafanyakazi wageni, walisema hawamjui lakini alijaribu kutafuta wenyeji ambao nao walimjulisha kuwa hayupo hata uondokaji wake ulikuwa wa ghafla hivyo hawajui yupo wapi kwa muda ule.

    Majibu yalimkatisha tamaa na kuamua kurudi jijini akiwa amelowa na kujiona kama mtu aliyepotelewa koti lake wakati wa baridi kali. Alijua huo ndiyo muda wake wa kutulia baada ya kupata mtoto na kumfanya mume mwanaume aliyemzalisha.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kauli ya mwanaye siku zote ilimuumiza sana pale alipomuonya mama yake tabia ya kuchanganya wanaume vijana na wazee bora atafute mtu mmoja atulie naye tena anayejiheshimu kuliko kurukaruka ipo siku watachangia mwanaume watashindwa kutazamana.

    Baada ya kupata ujauzito ule alijua jawabu ya kilio cha mwanaye limepatika lakini siku zote wa moja havai mbili. Alirudi Dar akiwa amechoka aliamua kumlea mwanaye kwanza hata baadhi ya biashara zake alizimamisha kwa ajili ya kumlea mwanaye ambaye alijua ndiye kichwa cha familia.

    Malon alipo fikisha miaka miwili alipelekwa shule ya kulelea watoto iliyo nchini Marekani ambako alimpeleka ili yeye aendelee na biashara zake pamoja na kulipa hela nyingi lakini alijua ndiyo sehemu iliyo salama ambako mtoto hupata malezi na elimu ya hali ya juu.



    JIJINI DAR

    Kijana Tino Tamilway akiwa hana habari kuna neema inamtafuta ya kukabidhiwa utajiri na mam’ kubwa baada ya kuutafuna mfupa ulio washinda wengi. Naye kwa upande wake mambo yalizidi kumnyookea kwa muda wa mwaka na nusu alikuwa tayari ameisha jenga nyumba mbili na kununua gari la kutembelea hakuwa yule mhudumu wa nyama choma bali mtu maarufu jijini kwa kuwa na maduka ya kuleta vitu vya kisasa.

    Kila kukicha alibuni mradi mpya ambao ulimuongezea kipato na kujikuta naye anamiliki magari ya kusafirisha mizigo mikoani jina lake lilijengeka kila kukicha wengi walimwita Tell me way sio tena Tamilway. Pamoja na utajiri aliokuwa nao hakuwa na mwanamke kwa kuogopa kuvurugwa akili na wanawake ambao siku zote aliwaona viumbe wenye vituko.

    Alipanga mambo yake yakishatulia hapo ndipo atapotafuta mwanamke atakaye mpenda yeye kama yeye na sio utajiri wake.



    CHUO KIKUU MLIMANI JIJINI DAR



    Msichana Gift alikuwa na mawazo tele juu ya tabia ya kijana Kanuth kumng'ang'ania kimapenzi pamoja na kumkatalia alikuwa akimnyima raha kwa kumng'ang'ania kutaka urafiki naye. Kama sio tabia zake chafu zilizoenea chuoni za kubadili wanawake kama nguo angemkubali, kwani hata yeye alimpenda kutokana na kuwa na umbile la mvuto kwa kiumbe yoyote wa kike.

    Kutokana na upendeleo aliopewa na Mungu Kanuth kila msichana alimtaka yeye pale chuoni. Alikuwa ameisha tembea na wasichana zaidi ya kumi tena wote wanajuana miongoni mwao ni rafiki zake wa karibu pamoja na kumkatalia bado aliendeleza kumfuatafuata kitu kilichomnyima raha.

    Gift tatizo lile alimfikishia rafiki wake wa karibu Eliza juu ya kero za Kanuth, Eliza alimpa jibu jepesi kuwa ampe masharti kama kweli anampenda aende akapime HIV na kama yupo safi basi ampe sharti la kutokuwa na msichana mwingine pale chuoni.

    "Unafikiri Gift lazima atatoa nje, hapo ndio utakuwa mwisho wa kukusumbua."

    "Mmh, kweli wacha nifanye hivyo."

    Kama kawaida Kanuth hakuchoka kumfuata Gift cha ajabu mara nyingi anapo mwita huwa hasimami lakini alishangaa kumwona Gift akisimama kumsikiliza. Alijua huo ndio muda muafaka kwani alijiamini kumpata msichana yoyote atayekubali kusikiliza sera zake. Baada ya kufika alimsalimia.

    "Za saizi msichana mrembo."

    "Nzuri tu mvulana hand some," kauli ile ilimfanya Kanuth ajione kuwa ushindi umekuwa mwepesi tofauti na alivyotegemea alijua pangechimbika kutokana na msimamo wa Gift.

    "Za masomo?"

    "Nzuri sijui zako?"

    "Mmh, kwa kuwa nipo mbele na msichana mrembo kama wewe lazima ziwe nzuri."

    "Mmh, nieleze ulichonisimamishia naona umeanza nahau."

    "Unajua Gift unautesa moyo wangu kila siku hasa pale unapokataa hata kusikiliza kilio changu," Kanuth kama kawaida akaanza tenzi zake.

    "Hicho kilio umewalilia wangapi?" Gift alimuuliza huku akimpandisha na kumshusha.

    "Unajua Gift sifa yangu imekuwa mbaya hapa chuoni kutokana na tabia za watu kunipakazia, mazoea na wasichana imekuwa nongwa unajua nina damu ya kupatana na watoto wa kike."

    "Haya tuachane na hayo, ulikuwa unasemaje?"

    "Hilo ndilo swali ulitakiwa kuniuliza mapema, Gift nina imani sote tupo mwaka wa tatu bado mwaka mmoja tumalize masomo yetu na baada ya hapa kila mmoja anatakiwa kupata kazi kwa watakaojaaliwa kwa upande wangu suala la kazi silifikilii sana kwa kuwa wazazi wangu wana kila aina ya utajiri ninacho fikiria ni kujenga familia ya kuwa na mke mwema ili anizalie watoto watakao fuata maadili mema ya wazazi wao.

    "Nina imani ombi langu kama utalipokea kwa mikono miwili na kunipa jibu litakalo upa moyo faraja la milele sijui mtoto mrembo unasemaje?"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nasikia hayo maneno ameyanukuu kila mwanamke unaye kutananaye unamueleza hivyo."

    "Aah, ni nani niliyemweleza maneno kama hayo?"

    "Mwaija."

    "Ni kweli nilikuwa nina nia kweli ya kumuoa lakini hakuwa muaminifu kitu kilichopelekea tuachane najua ndiye mbaya wangu anayeeneza maneno ya uongo ili kunichafulia jina lakini si kweli sina sifa hizo," Kanuth alizidi kujitetea.

    "Pamoja na maneno yako lakini bado sikuamini."

    "Nifanye nini ili uniamini."

    "Ukapime HIV."

    "Haa! ili iweje?"

    "Ndio nikuamini."

    "Ina maana nikukuletea cheti ndio utanikubali?"

    "Ndio jibu jepesi."

    "Basi tegemea jibu jioni ya leo."

    "Sawa."

    Waliagana kila mmoja alishika hamsini zake, Taarifa zile alimfikishia rafiki yake Eliza.

    "Nimemweleza kama ulivyo nieleza."

    "Ehe, alisemaje?"

    "Kwanza alishtuka kisha akasema eti cheti atanileleta jioni ya leo."

    "Thubutu atawahi unafikili ni kwenda kupima maralia, alikuwa anatafuta njia ya kuondokea najua umemkata maini hakufuati tena."

    "Mmh, kama ni hivyo nitashukuru maana alikuwa kero, ya nini kuniua na UKIMWI mwana wa mwenzie akafie mbele na haohao vichangudoa vyake vyenye tamaa sina tamaa ndogondogo sina ninachokikosa kwa mzazi wangu na vile nipo peke yangu mtoto wa kike kama jicho nini nikitake nikikose."

    *****

    Majira ya saa mbili usiku baada ya chakula cha usiku Gift akiwa na Eliza alisikia sauti ya Kanuth ikimwita alipogeuka walikutana uso kwa uso.

    "Vipi Kay?"

    "Ule mzigo huu hapa," alisema huku akimkabidhi bahasha.

    "Mzigo gani?"

    "Kwani asubuhi tuliongea nini nilifanyie kazi maneno yako na majibu ni haya."

    "Ina maana ulienda kupima?" Kauli ile ilimshtua Gift

    "Gift nilitaka kukuonyesha maneno yote uliyosikia ni kunipakazina tu."

    "Mmh, majibu yanasemaje?"

    "Nenda kasome mwenye nina imani kesho utanipa jibu zuri," Gift aliipokea ile bahasha na kuelekea nacho chumbani mwake ili akakisome, alijikuta amepagawa hata kumpita shoga yake Eliza aliyekuwa akimsubiri pembeni.

    "Shosti mbona unanipita kuna nini tena?"

    "Kaniletea majibu."

    "Yanasemaje?"

    "Kanipa nikayasome mwenyewe."

    "Atakuwa muongo kanunua tu cheti atawahi hivi unafikili kupima mchezo akose umeme kicheche kama yule."

    Walikwenda hadi chumbani na kukisoma kile cheti kilicho onyesha yupo safi alichopima ANGAZA.

    "Sasa itakuwaje?"

    "Mwambie humuamini ikiwezekana muende wote."

    "Mmh, na tukienda wote na akaonekana yupo safi itakuwaje?"

    "Nakuhakikishia hawezi," Eliza alimtia moyo Gift.

    "Mmh, nitajaribu."

    Waliagana kila mmoja alijiandaa na masomo ya usiku lakini Gift hakuhudhulia aliamua kulala.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog