Simulizi : Inatosha
Sehemu Ya Pili (2)
Ilipoishia jana..
Nilipokuja kuzinduka tayari nilikuwa narudishwa gerezani,kitu kilichonifanya nishtuke ni tumbo la uchungu ambalo lilikuwa likiniuma na kunivuta sana haswa kwa maeneo ya kitovuni ndipo palikuwa pakiniuma sana.
"Uuhh...! Uhh....! Hapa ni wapi...? Nauliza hapa ni wapi....?"
"...yani kuua uue sasa hivi unazinduka nakujifanya hujui ulichofanya...? Si ndio...?"
"...nisameheni jamani aiyaaa...! iyaaaa...! iyaaaa....! Levina mimi naozea jela uwii...!"
Songa nayo sasa…
Nakumbuka ilikuwa mida ya saa tatu za asubuh huku nikipandishwa kizimbani tena kwa mara ya pili nakusomewa mashtaka yangu juu ya mauaji niliyofanya,yule mama niliokuwa nikiishi naye alikuwepo huku akitoa machozi yaliochochea hisia zangu nakunifanya nitamani japo kumumuuliza kuhusu miradi yangu lakini ilishindikana kwani nilikuwa chini ya ulinzi mkali,nilikuwa nikitetemeka mdomo huku meno yangu yakiumana.
Hatimaye jopo la mahakimu likiongozwa na mawakili waliojitokeza angalau kunisaidia kesi yangu japo haikusaidia kitu, nakujikuta nikihukumiwa kifungo cha maisha gerezani,nilishindwa kuzuia uchungu nilionao nakujikuta nikizimia na kupoteza fahamu zangu zote.
~ BAADA YA MIEZI 2 ~
Nilikuwa tayari natumikia kifungo changu cha maisha huku nikiwa na mimba ya miezi mitano kama na nusu hivi, niliwekwa sehemu maalumu na wasichana wenzangu ambao nao walikuwa ni wafungwa wenye mimba kama nilivyo mimi.
Nilijitahidi sana kusahau mambo yote yaliyonitokea huku nikijishughulisha kwenye vijikazi vidogo vidogo vya humu ndani ya gereza, sikuhitaji kabisa kuwa na marafiki humu ndani kwani niliamini kama nitajenga upya mazoea namarafiki humu ndani basi watajua ukweli wangu toka nilipotokea hivyo aibu kubwa iliyoambatana na siri kubwa niliiweka moyoni mwangu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*********
Siku zilizidi kusonga mbele kwani sasa ilikuwa imefika kama miezi mitatu toka niingie hapa gerezani bila hata ya kupata taarifa yoyote kutoka nyumbani,nilizidi kuumia sana moyoni huku nikiwa sijui nini haswa cha kufanya,
Usingizi kwangu ulikuwa ni wa shida sana kwani mara nyingi usiku katika ndoto nilikuwa nikitokewa na baadhi ya matukio niliowahi kufanya hapo nyuma na hata ile ya kumpoteza mwanangu 'Jelly katika treni kipindi kile alichopigwa risasi na Gervas kwa bahati mbaya,nikiwa bado kwenye dimbwi la mawazo ya hapa na pale huku nikizitafakari ndoto zangu ninazoota mara kwa mara,
Ghafla tumbo likanizidia nakuanza kuniuma sana huku likinikata kata nafikiri ilitokana na mimba niliokuwa nayo,sikuwa na msaada kwa muda huu kwani wenzangu karibu wote walikuwa wakijishughulisha na wengine wamejilalia mara nikashuhudia watuhumiwa wengine wanaletwa pale gerezani lakini kati ya yao alikuwepo mtu mmoja niliokuwa namfahamu..
"Oooh My God...! kafuata nini huku huyu..."
Nilianza kuingiwa na woga huku mwili ukinitetemeka nakufanya
Meno yaumane kwa woga na mshangao wa kumwangalia yule mtu huku akinifuata eneo nililopo.
"Mamaaaaaa....?"
Niliita kwa mshangao kwani aliponikaribia kwa karibu sana nilivuta hisia nakuweza kumtambua mara moja kuwa ni yule mama niliokuwa nimemwachia miradi yangu.
"Levinaaaaaaa...?"
"Vipi...? ....imekuwaje tena na wewe umeletwa huku...?" nilipigwa nabutwaa kwa nilichokiona huku nikiwa sijielewi elewi mara, "Embu tulia ukoo mpumbavu mkubwa weee...!"
Sauti ya askari wa magereza ilimuamrisha yule Mama kuwa anyamaze kwani aliponiona tu alizidi kulia nakuniacha mwili wote ukiendelea kunitetemeka nisielewe nini chakufanya,hisia kali zilinijaa akilini zikiambatana na hasira.kiukweli nilitamani nimshike yule mama kwa nguvu zote nakumnyongea mbali kwani kumuona sura yake tu kulinizidishia hasira kali na dukuduku moyoni huku nikitaka kujua chanzo cha yeye kuacha mali zangu nakuja huku kufungwa
"nani sasa atasimamia mali zangu...? na huyu mtoto nitakayemzaa atasimamia mali zipi...?"
Ni kati ya maswali niliokuwa nikijiuliza sana moyoni bila kuyapatia majibu yeyote.
Haraka haraka nilikimbia kwenye jumba la la upande mwingine kwenda kupumzikia kisha nikachukuwa shuka nakujifunika huku nikiulazimisha japo usingizi niweze kusahau kwa muda lakini bado hilo halikusaidia chochote,nilisumbuka kwa muda mrefu kidogo pale kitandani huku nikitapatapa kitandani,nikiwa bado nipo najigeuza huku na kule mara sura yangu ikakutana tena kwa mara ya pili na yule Mama akijongea huku kavalishwa jezi zetu za huku gerezani na kwa muda huu alikuwa ameshanyolewa upara mkubwa,alikuwa akiangaza huku na huku.
"We mama unakwenda wapi...? au na wewe una mimba kama sisi...?"
Aliropoka Yuni,mmoja wa wafungwa huku akimtolea macho yule Mama kwani sisi wafungwa tuliokuwa na mimba tulikuwa tumetengewa sehemu maalumu tofauti na wengine ambao hawakuwa na mimba,yule Mama hakusikia lolote akawa anazidi kusogea huku akiendelea kuangaza huku na kule mara wafungwa wenzangu kama watatu wakamvamia nakutaka kumpiga.
"Mwacheni.. Mwaaacheeeee....!"
Niliongea kwa sauti kali na ya juu nakufanya kila mtu anishangae na pia nilikuwa naogopeka ndani ya muda mfupi niliokuwa nimepelekwa pale gerezani,basi wale wafungwa wenzangu walinielewa na kumwacha huku akinifuata mpaka kwenye kitanda changu.
"..Levina...?"
"..unasemaje...?"
".....kuwa mpole Levina nikusimulie kilichonikuta.."
Moyo wa huruma ukaanza kunitawala,kutokana na kila mmoja wetu kunitolea macho mimi na yule mama,nilichokifanya nilimshika mkono nakumtoa mpaka nje kisha.
"Haya niambie Mama kilichokusibu huko uraiani...?"
"...mwanangu Levina...? Ni stori ndefu lakini haina budi kukuelezea..."
"we niambie tu imekuwaje huko....?"
"ni kuhusiana na Gervas...!"
"Gervaaaaas....? Gervas yupi tena...?"
"...si yule aliyekuwa mumeo....!"
"Enhe...! Kafanyaje tena si alishakufa....?"
"Hapa ninavyokueleza nikuwa Gervas hajafa yupo hai na anaishi mpaka sasa..!"
"anaishi na nani tena Jammy..? Uhhh...! Uhh...!"
Nilijihisi mkojo unapenyeza ndani ya nguo yangu ya ndani huku nikijihisi kama uchungu wa kujifungua mimba kabla ya muda wake, kijasho chembamba kilianza kunitiririka kikiambatana na msisimko mwilini uliofanya mishipa ya kichwani kunitoka na kusababisha kubaki mdomo wazi kwa muda huku macho yakiendelea kunitoka yakiambatana na mchozi kwa mbaali ulioanza kunidondoka..,
"unasema kweli mama...?"
"Levina,ujue niliumia sana pale maaskari waliposhirikiana na wafanyakazi wa Gervas na Bosi,Happy kufanya maamuzi ya haraka ya wewe kuhukumiwa kifungo cha maisha bila hata kufanya mazishi..."
"Mama...! Nilistahili kufungwa kifungo hiki hiki cha maisha wala hawakukosea....?"
"lakini mbona Gervas mzima...?"
"hata kama....! Nilivyoona huko nyuma mpaka nikasema Sitaki tena,nastahili kufungwa maisha...! enhe embu nieleze ilikuwaje baada ya mimi kuhumiwa Gerezani maisha....?"
"Levina...,unakumbuka siku ulipowapiga risasi Gervas,Jammy na omari...?"
"...nakumbuka na siwezi kusahau katika maisha yangu,kwani ilikuwaje....?"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"basi Levina baada ya wewe kuwapiga risasi pale wakaanguka chini na kilichofuatia miili yao kuwaishwa hospitali ya 'LUTAHIA ' moja kwa moja mpaka chumba cha wagonjwa mahtuti kwani walikuwa bado wanahema,hivyo niliwafuatilia mpaka kujua hatma ya miili yao,nilikaa peke yangu pale hospitali mpaka usiku nikijibanza huku nikitaka kujua kama kweli atapona mtu au la,mpaka ilipofika usiku sana kwenye mida ya saa sita nikashuhudia jopo la madokta wakiongozana na manesi huku wakishikilia dripu na wengine mirija ya kutolewa hewa (oxygen) wakiwa wanaburuta mgonjwa kwenye kile kibaiskeli lakini yule mgonjwa sikuweza kumtambua kama ni Gervas,Omari au Jammy kwani alikuwa mbali,pale pale ndio ukawa mwanya kwangu kuingia kwenye chumba kingine nikitaka kujua aliyebaki ni nani?
Nilipofika tu ndani ya kile chumba cha wagonjwa mahtuti nikakutana na askari mmoja akiwa na manesi huku wakimsimamia yule mgonjwa aliokuwa amebaki...."
"nani sasa Gervas...?"
"tulia sasa nikumalizie Levina mbona una haraka hivyo....?"
"na we nawee....! haya endelea,ikawaje sasa...?"
"...pale pale nikachukuwa bunduki ya yule askari kinguvu na kumuua kwanza yule askari kisha nikawafyatua wale manesi mule chumbani nikausogelea ule mwili nakwenda kuufunua nikidhania labda atakuwa ni Gervas, nikaufunua,kumbe alikuwa ni Jammy tena anaonesha hakufa vizuri kwani alikuwa akipumulia mirija,pale pale nikammalizia kwa ile bunduki kisha nikatoka nje huku nikifuata mwili wa Gervas ulipo,mwili wangu wote ulikuwa umechafuka damu,watu wengi waliniona jinsi nilivyo ikiwa ni pamoja na manesi na baadhi ya wagonjwa walinikimbia huku na kule kwa usiku ule,makelele yalitawala sana karibu eneo lote,hatimaye nikawa nimeingia wodi aliyekuwa amepumzishwa Gervas,niliwakuta maaskari takribani sita na madokta huku wakiwa hawajui kinachoendelea kwani walikuwa wakisadiana na manesi bila kupoteza muda nikalikoki lile bunduki nakuanza kupiga baadhi ya maaskari na manesi,nilifanikiwa kuwapunguza kwani maaskari wote sita walikuwa tayari nimeshawaua wakiwa ni pamoja na madokta wawili,baada ya hapo nikausogelea mwili wa Gervas nikaunyoshea ile bunduki nakuanza kufyatua huku Gervas akionesha kuniangalia kwa macho ya huruma,
"....kwa hiyo ukamfyatua....?"
"hapana Levina..?"
"shit...!!! Sa kwanini ukamwacha na wewe...? Au umesahau alivyonitendea...?"
"....nakumbuka levina na ndio maana nilikuwa na uchungu naye wa kutaka kumuua...!"
"sasa kwanini ulishindwa kumuua Mama...?"
"hapana...!! Ile nataka tu kufyatua nilishtukia napigwa sindano ya usingizi shingoni mwangu na Dada mmoja alioonesha kuwa ni nesi wa pale hivyo nikamgeuzia bunduki nakumfyatua,nilimmiminia risasi kwa hasira mpaka nguvu zikaniisha nakujikuta usingizi mzito ulioambatana na kulegea kwa viungo vyangu vya mwili, papo hapo nadhani ndipo nilipokamatika,kwani nilipozinduka nilijikuta nipo mikononi mwa polisi huku mikono yangu ikiwa na pingu nikisomewa mashtaka ya mauaji.
"...sasa imekuwaje umeletwa hapa...?"
"Levina....!! Nilisota sana katika gereza la 'USANTU ' pale Mtwara na kutokana na umri wangu kuzeeka sana hivyo nikaletwa huku kuwasaidia baadhi ya wafungwa wajawazito sana sana wale wanaokaribia kujifungua..."
"...pole sana Mama kwa yaliokukuta....!"
"Ahsante Levina mwanangu..., na hivi ninavyokuambia nimeletewa taarifa kuwa mali zote anazimiliki Gervas hivyo kaa ukijua Gervas kapona nakuwa sasa anafanya kila njia kuhakikisha tumekufa huku gerezani...."
"Hamuwezi mtu hapa..."
Moyo wa kishujaa ulianza kunitawala nakuona sasa acha niwe Levina yule wa zamani.'
"Mama...? ingekuwa hii mimba ina miezi miwili au mitatu ningeshaitoa..."
Hasira zilizonitawala akilini mwangu nakunifanya niropoke maneno huku nikimwacha mdomo wazi yule Mama.
"Mama....? ama zake ama zetu.... Nitahakikisha mali zote zilizo kwa Gervas, anasimamia huyu mtoto wake huku tumboni na siyo huyo msaliti mkubwa asiyekuwa na hata chembe ya huruma..."
*******
Siku zangu za uchungu wa mimba zilifika huku yule mama akiwa ni mtu wa karibu sana na mimi kuhakikisha najifungua salama, kwakuwa alishawahi kuwa nesi hivyo alinisaidia yeye na baadhi ya manesi nikajifungua salama namshukuru mungu nilipata mtoto mzuri wa kike,
~ BAADA YA WIKI 1 ~
Uchungu ulishapotea na sasa ilikuwa ni furaha tu juu ya mtoto niliekuwa naye, ilifika kipindi hadi nikajisahau kuwa ni mfungwa kutokana na furaha niliyokuwa nayo.. "Mama embu niambie huyu mtoto tunamwita jina gani sasa...?" "Daah.. Kwa mimi ningependelea umwite Happy...!"
"Nani...? Happy...? Umeshamsahau yule mpuuzi wa Zambia, si anaitwa Happy... hapana hilo jina silitaki..." "kweli Levina, sasa tumwite nani...?" "Lauryn..." "ndio limaanisha nini sasa...?"
"mh..! nawe Mama umezidi sana ushamba, hayo majina ya kizungu na halina mana yeyote na kifupi chake ni Lau..." Furaha ilizidi maradufu kwani tuliafikiana mtoto aitwe jina la 'Lauryn' nakuanzia siku hiyo mtoto akawa anajulikana jina la Lauryn au Lau. Maisha yalizidi kuwa mazuri.
***********
"Levina...?"
"abee..."
Ilikuwa ni sauti ya yule Mama ambaye alikuwa karibu sana na mimi na kwa muda huu alikuwa ametoka na amerudi huku akihema,
"unasemaje Mama,kwanza mbona upo hivyo...?"
"Levina...? Amini usiamini nimemuona Gervas mwenyewe..."
"Gervaaaaaaaaaaas...?"
"ndio,yupo kule anaongea na maaskari tena nimemshuhudia akimpa kibahasha kidogo cha kaki askari mmoja pale..."
"sasa we Mama...? Unafikiri mimi naogopa kitu...? Hapa hanitishi chochote....!"
Tangu nimzae mwanangu Lau nilizidi kujiamini kwa kila kitu na ndicho kitu kilichonisaidia huku gerezani 'UKONGA' kwani kiukweli niliogopeka sana Levina mimi,nikiwa bado nipo na yule Mama tunaongea mara akaja askari mmoja wapo hadi eneo tulilokuwepo,
"Levina...? Unahitajika ofisini sasa hivi...!"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"sehemu gani...?"
"upande wa mapokezi tena ufanye haraka.."
Sikuwa na hali ya hofu kabisa zaidi ya kuzidi kujiamini huku nikiamini kabisa Gervas hawezi kunifanya chochote,
"Mama...? Embu nipe mtoto wangu niende naye kabisa..."
"Levina mwanangu,mimi nakuomba umuache hapa utamkuta tu mwanangu..."
Nilimuamini sana yule Mama hivyo nikaamua kumuachia mwanangu,huku nikiondoka taratibu mpaka kwenye ile ofisi,
Nilipofika tu macho yangu yalikutana uso kwa uso na Gervas akionesha mwenye afya tele tena akionekana kung'ara sana kuanzia ngozi yake mpaka mavazi,
"umefuata nini malaya mkubwa wee...?"
"Levina mpenzi...."
"Naaaaani...? Nani mpenzi wako...?"
"naomba unielewe najua kuwa ni vigumu kwa mimi nawewe kurudiana ila...."
"....ila nini? Ulivyonisaliti Gervas inatosha..., inatosha Gervas...?"
"kumbuka una damu yangu Levina,na mtoto anahitaji apate malezi bora kutoka kwako na kwangu pia..."
"leo hii unakumbuka hilo...?"
Nikamjibu na kumfyonza pale pale huku nikiinuka nakuondoka zangu kurudi kwa mwanangu nilipomuacha na Mama
"Levina pliz..!,usiondoke mpenzi,pliz Levina..!"
Sikulijali hilo zaidi ya kugeuza jicho langu la ukali huku nikimshuhudia Gervas akitokwa na machozi kwa mara ya kwanza tangu tulipoachana naye kipindi kilee.
Kiukweli nilikuwa na jazba ya hali ya juu,maaskari wote pale walikuwa wakitushangaa na wasielewe kitu gani kinaendelea kati ya mimi na Gervas,nilitoka pale na nilipofika sehemu yangu ya kupumzika sikumkuta yule Mama pale nilipokuwa nimemuacha,hofu na akili kunibadilika vilinianza huku nikichanganyikiwa nisijue Mama alipoelekea,
"eti yule Mama ninayekuwa naye karibu umemuona wapi...?"
Nilimuuliza mmoja kati ya wafungwa wenzangu naye hakujua alipoelekea,nilizidi kuchanganyikiwa huku nikielekea kumtazama japo chooni,napo nilipofika sikumkuta hivyo nikarudi tena bwenini huku nikiendelea kuchanganyikiwa mara mfungwa mwenzangu mwingine akanifuata nakuniambia kitu..
"umesema...?"
"kweli,ulivyoondoka tu kwenda ofisini,walikuja maaskari wawili wakamchukua nakwenda naye huko huko ofisini ulipokuwa"
"pamoja na mwanangu...? Au mwanangu kamwacha na nani...?"
"ameondoka huku kambeba mtoto"
Sikutaka kusikiliza tena chochote zaidi ya kukimbia huku nikirudi eneo la ofisini,nilipofika napo sikuweza kumwona,kijasho chembamba kilichoambatana na mkojo vikianza kunitoka huku nikijihisi kama nina presha tena ile ya kushuka,
"namtaka mwanangu.., namtaka mwanangu...?"
"we acha upumbavu hapa,huyo mwanako kaletwa na nani hapa mpaka umtake...? Na yuko wapi...?"
Aliongea askari mmoja wa kike aliyeoneshwa kukasirishwa na kitendo cha mimi kung'ang'ania mtoto huku simuoni,wale maaskari walinipiga vibao huku wakinivuta kuelekea ndani ya bweni, lakini kwa bahati nzuri macho yangu yaliweza kupenyeza mpaka kwenye kakorido kapale ofisini kwa maaskari nakumshuhudia Mama akiwa amembeba mwanangu 'Lau' huku akiwa na Gervas namaaskari kwa pamoja wakitoka nje kabisa,
"Mama unakwenda wapi mama..? mlete mwanangu?"
Nilizidi kuumia huku wakiendelea kuniburuza na kunipiga,niliumia sana lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kubaki nikirudishwa ndani huku mwili wote ukinilegea na kupoteza nguvu kabisa hapo hapo nikajihisi kizunguzungu.
**********
Nilipokuja kuzinduka nilijikuta bado nipo ndani ya bweni,nikaamka pale kitandani nilipokuwa nimelala haraka haraka nikainuka nakuelekea nje huku nikiwa na shauku ya kujua kama ni kweli mtoto wangu 'Lau sina tena au la!
Kagiza kalikokuwa kametawala huku ubaridi mkali ulioambatana na upepo ulinifanya nirudi tena ndani huku wenzangu wakinishangaa jinsi nilivyokuwa nimechanganyikiwa,
"Lau..! Lau mwanangu....? Umekwenda wapi Lau...?"
Nilikuwa mtu wakuongea mwenyewe huku mchozi ukiendelea kunidondoka,ndipo nilipofika hadi eneo la kitanda changu na kwa safari hii niliweza kutambua kama kuna kitu nilikiacha pale,haraka haraka nikaangalia nakugundua kuwa nikikaratasi tena kilichokunjwa kunjwa ovyo huku nisielewe ule mwandiko ulivyokuwa umeandikwa,nilijitahdi kuusoma vizuri tena kwa mara ya pili,
"SAMAHANI SANA LEVINA KAMA UTAKERWA NA MIMI LAKINI IMENIBIDI KUFANYA MAAMUZI HAYO..., KWA TAARIFA TU MIMI SIYO MFUNGWA ILA NILITENGENEZWA TU ILI KUHAKIKISHA HUYU MTOTO WAKO 'LAURYN' ANAKUWA MIKÖNONI MWA GERVAS..,
GERVAS AMENITUMA NA HATIMAYE NIMEWEZA,HIVYO YALE YOTE NILIOKUSIMULIA HAPO NYUMA KUHUSIANA NA GERVAS NA JAMMY NI UONGO MTUPU KWANI BADO WOTE WANAISHI PAMOJA KAMA WANANDOA WANAOTAMBULIKA,
NAKUTAKIA KIFUNGO CHEMA HUKO GEREZANI,
MIMI NI MAMA ULIYENIACHIA MTOTO WAKO..."
Niliumia sana baada ya kusoma kile kikaratasi huku nikizidi kuchanganyikiwa nisijue nini cha kufanya,
"....Yani Mama ndio wakunifanyia mimi hivi...? Mama...? Ama kweli nimeamini rafiki yako ndio adui yako, na umuaminiaye ndiye akugeukae..! ama zangu ama zao na niwe hai ama nimekufa nitahakikisha mtoto wangu Lau anarudi mikononi mwangu kwa njia yeyote ile hata ya kumwaga damu,miye ndio Levina yule unayemfahamu..."
Nilijisemea kimoyomoyo huku akili yote nikiiamishia ni jinsi gani mwanangu anarudi tena mikononi mwangu.
~ BAADA YA WIKI TATU ~
Bado nilikuwa katika majonzi mazito huku nikiwachukia zaidi wale maaskari waliokuwa wakinipiga mara ile ya mwisho nilipompoteza mwanangu Lau kwenda kwa Gervas, nikaanza mipango taratibu huku nikiangalia njia zote zakuweza kupambana na Gervas pamoja na Mama na huyo Jammy wao, kila muda nilikuwa sibanduki maeneo ya ofisi za maaskari huku nikijiamini kwa asilimia mia kuwatoka wale nitakuwa kama nimelamba dume kwani ndio utakuwa mwanzo wa mimi kutoroka.
Nilifanikiwa kujua kila kitu ikiwa ni pamoja na wafungwa wote wanapoachiwa huru kwa msamaha wa Rais huwa majina yao na rekodi yao kwa ujumla huwa zinafutwa kwa kupigiwa mistari majina yao.
Nakumbuka siku moja niliamua kutokulala kabisa huku usiku wote nikiutumia katika kuhakikisha natoroka,wafungwa wenzangu karibia wote walikuwa wamepitiwa na usingizi,kila muda nilikuwa mtu wakutoka nje huku kisingizio kikubwa ikiwa nikuelekea chooni.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"safari hi iwe na isiwe lazima nitoroke tu, mie ndio Levina"
Nilijisemea kimoyomoyo huku nikijivika moyo wa kijasiri nakuhakikisha kwanza breki ya kwanza naelekea katika mitambo nakuzima umeme eneo lote la gerezani,nilinyatia huku nikijiziba ziba katika kijigiza huku nikijiamini kuwa nitafanikiwa,hatua mbili tatu kabla sijafika sehemu ya mitambo nilikutana na askari lakini kwa bahati nzuri hakuweza kuniona hivyo ilikuwa kama mwanya,nilivuta kipande kidogo cha chuma kilichoonekana chini kwangu nakumuwahi kumziba mdomo kisha nikampiga na kile chuma maeneo ya utosini mwake kwa nguvu na hasira na hatimaye nikamuua,nilimlaza pale chini kisha kilichofuata niliichukuwa bunduki yake nakuingia mpaka chumba cha mitambo kisha nikazima 'main swtich' (umeme mkubwa unapotokea ),
Kisha kilichofuata nigiza lililofanya wafungwa wote wapige kelele gereza zima huku na kule,giza kali lililokuwepo limetanda pale ilikuwa jibu tosha kwa mimi kuongoza mpaka lango la kutokea huku kila askari niliyekutana naye nilikuwa nikimfyatua tu,nilijihisi kama umati wa wafungwa wenzangu unanifuata huku risasi zikiendelea kurindima humu ndani.
Hatimaye nilifanikiwa kutoka mpaka nje ambapo kulikuwa hamna giza lolote,nilijibanza kupitia magari ya pale gerezani yaliokuwa yamepaki nje, nikiwa bado nasikilizia ni jinsi gani nitaendelea na safari yangu mara umeme ukawa umewashwa mule ndani gerezani,hofu ikaanza kunitanda ,huku nikiwa nimeshatoka nje ya gereza nikishuhudia mapolisi kama wanne wakitoka nje ya hili gereza huku wakiambizana,
"kapitia huku,we pita huku siye tunapita upande wa huku..."
Nilijihisi kama mkojo unataka kunitoka kwani nilikuwa nimejificha uvunguni mwa gari,wale askari walizunguka huku na kule lakini mwishowe niliwasikia wakipanda gari ambayo nilikuwa nimejificha uvunguni mwake,nilitamani nichoropoke lakini isingekuwa rahisi kwani askari kama wawili walikuwa wamebaki eneo like lile la pale magereza,gari ilianza kuwashwa,hatimaye uzalendo ukanishinda nakuamua kutoka pale uvunguni mwa gari,
"kamata huyo,kamata afande..!
Kama kawaida Levina mimi ujasiri niliokuwa nao ndio ulinisaidia kuchoropoka mbele ya wale maaskari kwani na ndani ya sekunde chache tu nilikuwa nimeshajificha tena kwa mara ya pili huku nikiwasikilizia wale maaskari kama kweli watakuwa wameniona nilipojificha..
"...Mkuu limepita kwa huku..."
"Sasa wewe nenda upande wa huku nami wa huku sawa....?"
Zilikuwa ni sauti za wale maaskari wakiambizana njia ya kunitafuta,nikiwa bado nipo maeneo ya pale pale mara nikahisi kama naguswa na kitu mabegani mwangu,akili yote ikaanza kunihama na ujasiri kunipungua huku nisielewe nini cha kufanya kwa muda ule,nilitamani sana nigeuke ili nimjue ni mtu gani mara tena nikaskia sauti za wale maaskari wakiongea,
"Mkuu nimerikamata hili hapa...!"
Pale pale nikaendelea kupata hisia tofauti nakugeuka nyuma haraka huku nikianza kutetemeka nakuona sasa mwisho wangu utakuwa umefika na kama nitarudishwa tena gerezani itakuwa nikifungo cha kunyongwa na wala si cha maisha tena nilipogeuka tu,
"....Uuuhfff...."
Kumbe ulikuwa ni uoga wangu tu kwani hakuwa mtu yeyote bali ukuta niliokuwa nimeuegemea ulinipa hisia tofauti, fasta fasta nikatoa macho yangu nakuangaza ili nijue ni mtu gani aliyekamatwa na wale maaskari ile naangalia upande wa pili namuona ni mfungwa mwenzangu 'Yuni' ambaye naye alikuwa ametoroka na kwa muda huu alikuwa yupo mikononi mwa wale askari waliokuwa wakinitafuta na kiukweli walikuwa wanahasira sana kwani walimvamia yule 'Yuni' bila kujali alikuwa anamimba au la!
"Maskini Levina mimi, nimenusurika pale....?"
Nilijisemea kimoyomoyo huku nikijiondokea eneo lile taratibu nikinyatanyata huku nakule huku nikijificha kwenye magari moja baada ya jingine, kwa muda huu sikuwa natetemeka tena kwani nilijikuta woga wote umenitoka japokuwa nilikuwa sijatoka lile eneo la magerezani na tena bado nilikuwa ndani ya zile sare za magereza lakini kwa sasa nilishaanza kulivuka bila kukutana na mtu yeyote wala kitu chochote mara,
"...we mama unakwenda wapi utakufa wewe...?"
Ilikuwa ni sauti ya dereva taksi mmoja ambaye kidogo anigonge nilivyokuwa navuka barabara kwa uoga na kwa muda huu alisimamisha gari yake nakuniongelesha,
"...Achana na mimi endelea na safari yako..."
"Wamama wengine bwana mnamatatizo kweli, haya nenda ukafungwe huko....?"
Japokuwa nilimjibu vibaya yule dereva lakini alipoongea suala la kurudi gerezani moyo wangu ukaniripuka ghafla,
"we dereva...?"
"si umeniambia niachane na we Mama...? Sasa unachoniitia nini tena"
Hasira kali zilimshika yule dereva akawasha gari kwa kasi huku akitaka kuondoka,
"....Dereva..!, Dereva..!, simama pliz....?"
Akalisimamisha gari lake na hapohapo sikutaka kupoteza muda nikaufungua mlango wa ile teksi nakuingia palepale,
"Nipeleke kurasini...?"
"Samahani sana siwezi kubeba mfungwa mie...?"
Alijibu kwa nyodo huku akikataa kuondoka na mimi katukatu, tukiwa bado tunajibizana pale pale nikageuza kichwa changu nakuaangalia upande wa nje macho yangu yakakutana na rundo la maaskari wakiwa wanakaribia eneo ambalo nipo pale,
".....Dereva pliz washa gari twende, nitakamatwa mimi...?"
"Ni heri ukamatwe kuliko niongozane na wewe, wafungwa kama nyinyi ni kesi tu..."
Yule dereva aligoma katu katu na mpaka akaamua kulizima kabisa gari lake huku akiwatizama wale maaskari waliokuwa bado kidogo wafike eneo tulilopo, nikajivaa sura ya Levina yule wazamani nikaona kama nitaendelea kumbembeleza huyu dereva atanifanya nikanyongwe gerezani,nilichokifanya nikamsukuma upande aliopo mpaka akatoka na mlango akadondoka nje kabisa kisha kabla hajainuka pale chini nikaliwasha gari nakuanza safari,lakini huyu dereva alionesha kuwa mbishi sana kwani aliingia kupitia mlango wa pili hivyo nikaliendesha gari kwa kasi huku nikiliyumbisha huku na kule japo adondoke lakini alinishika 'mstering' hapo hapo nikagundua kuwa hapo kitu cha kufanya nikuwasha kile kidude cha moto wanachotumia kuwasha sigara kwenye gari nikakiwasha nakukichomoa huku nikiendelea kuendesha gari kwa kutumia mkono mmoja wa kulia na mwingine nikiutumia kumchoma yule dereva shingoni na usoni mwake,alinipiga vibao na mangumi lakini sikujali zaidi yakuendelea kuliyumbisha gari mpaka mwenyewe akasalimu amri baada ya mimi kufunga breki ya kushtukiza akagonga kioo cha mbele nakuzimia papo hapo, ikanibidi kupunguza mwendo lakini ile namshangaa yule dereva alivyozimia mara king'ora cha polisi nikakisikia kikiashiria kinanifukuzia, hapohapo bila kupoteza muda nikafungua mlango kisha nikamsukumiza yule dereva aliyekuwa amezimia na kilichofuata nikutoka kwa kasi ya ajabu huku nikiitafuta barabara ya 'Pugu' kwa usiku ule wa mida kama ya saa 5 na nusu usiku huku nikielekea barabara ya 'Chanika',spidi ilikuwa kali kwani niliendesha mpaka spidi 160 lakini bado gari la polisi lilikuwa nyuma yangu likinifukuzia, ndani ya dakika kama kumi na tano nilikuwa njia panda ya 'Kajiungeni' huku nikiendelea na safari ya kuwakimbia mapolisi waliokuwa wakinifukuza kwa nyuma,
"Oooh.., my God...!, Why...!Why...! Why...! Why...?"
Ile gari niliokuwa nayo ilikuwa imeshaanza kuishiwa nguvu na kwa muda huu ilikuwa imepungua sana spidi kwani ilikuwa inashindwa kupanda hata kamwinuko kadogo,ma kwa muda huu ilipungua kabisa spidi mpaka ikafika spidi 40 na haikuzidi zaidi ya hapo kila nilipoizidisha hivyo sikuwa na jinsi zaidi ya kusimamisha lile gari kisha nikaingia uvunguni mwa ile gari nakujificha ili kama liwalo na liwe,
Haikufika muda sana kwani ndani ya dakika kama mbili tatu nilisikia sauti za watu wakiongea wenyewe kwa wenyewe,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"ritakuwa rimekimbiria wapi sasa....?"
Hapo hapo halmashauri yangu ya kichwa ikanituma moja kwa moja kuwa itakuwa ni wale maaskari tu,niliendelea kujibanza pale uvunguni mwa gari huku sala zangu zote nikizielekezea kuwa waondoke eneo lile nililopo.
Mara nikaanza kuhisi majimaji yananidondokea mwilini,hivyo nikachukuwa mkono wangu nakugusa kisha nikanusa ili nijue nikitu gani,
"Mungu wangu...!"
Yalikuwa ni mafuta yalioonesha kuvuja sana kutoka kwenye lile gari nililokuwamo tena ya petroli na kwa muda huu yalikuwa yakivuja kwa kasi huku yakiniloanisha nguo zangu (sare za magereza) nilitamani nichoropoke lakini haikuwezekana,wale mapolisi nao hawakutaka kuondoka haraka pale hivyo wakaniweka katika wakati mgumu.
Mara nikahisi kama kipisi cha sigara kimeangushwa na polisi mmoja wapo,pale pale moto kwa mbaali ukaanza kunifuata,nikajibiringisha upande wa pili fasta kabla moto hujanilipukia na kwa bahati nzuri nikawashuhudia kwa mbaali wale mapolisi wakiondoka pale na kuelekea kwenye gari lao kwa ajili ya kuondoka,walipoingia tu kabla hawajaondoka nikaliwahi gari lao nakudandia kwa nyuma, mara moto ukalipuka katika lile gari nililoliacha hivyo ikawafanya wale askari washuke kwenye gari lao nakurudi tena maeneo ya lile gari lilipolipuka,
"Bora rife..., ripumbavu kabisa..."
Nilisikia sauti ya askari mmoja akishukuru kuwa ni bora nimekufa kwenye ule moto ulioripuka pale,
"Afe nani...? mtakufa nyie...!!!!!"
Nilijisemea kimoyomoyo
Huku nikiingia ndani ya gari lao kiulaini bila wao kujua kisha nikaliwasha gari lao fasta nakuligeuza huku nikiwafuata pale walipo,nadhani hawakujua kama ni mimi hivyo niliongeza spidi kali pale pale nikawapitia baadhi ya mapolisi nakusonga mbele huku nikijiamini kwa asilimia mia kuwa hawaniwezi na hataniweza mtu yeyote,
"....na bado Gervas, Jammy na huyo Mama aliyenichukuliwa mwanangu Lauryn, ole wao niwakute huko...?"
Njia nzima nilikuwa mtu wakuongea mwenyewe huku nikiendesha gari lile kwa kasi,nililipita lile eneo la magereza kwa kasi ya ajabu bila wao kulitambua kama ni gari lao,hivyo ndani ya kama nusu saa nilikuwa raundi abauti ya pale 'Kamata' (k/köo) huku nikiitafuta 'Kurasini' nilipokuwa nikiishi mimi na Gervas.
Kadri nilivyokuwa napakaribia ndivyo mapigo yangu ya moyo yalikuwa yakinienda kasi hivyo nilipokaribia kufika tu nikalitelekeza gari barabarani kisha nikachukuwa bastola iliyokuwepo ndani ya lile gari nakutembea kwa mguu mpaka maeneo alipokuwa akiishi Gervas.
Giza kali lililokuwa limetanda halikunitisha hata kidogo eneo lile hivyo ndani ya kama dakika kumi nilikuwa nje ya geti la nyumbani kwa Gervas.
Nilipiga hodi taaratibu huku nikiamini tu lazima mlinzi atafungua,
"....wewe ni nani na unataka nini usiku huu...?"
"naitwa Mamamia Mango, pliz nifungulie...?"
Yule mlinzi akawa na moyo wakunifungulia.
"...unataka nini usiku wote huu...? Na unatokea wapi....?"
"Nakaa mtaa wa pili huko, ona Mume wangu amenipiga kweli na amenifukuza,hivyo nimekuja kwa mjomba wangu Gervas kupata hifadhi...."
"sikiliza binti, Bosi Gervas huwa hapendi kuamshwa wala kugongewa anapolala hivyo kama utaweza kuvumilia kwani sasa ni saa tisa kasoro hivyo jipumzishe hapa pembeni 'then' kesho asubuhi atakupokea vizuri tu..."
Nilihisi kama yule mlinzi anamachale kwani angeniachia mwanya kidogo tu ningeharibu kila kitu,hivyo nilichokifanya sikukata tamaa zaidi ya kuendelea kumbeleza amuamshe Gervas anifungulie,
"...nimesema siwezi kumuamsha bosi wangu sawa...? Na ukiendelea kunilazimisha na mimi nitakupiga kama huyo Mumeo, nikufukuzilie mbali mpumbavu mkumbwa wee....!"
Niliona sasa yule mlinzi anataka kama kunizoea hapohapo mkono wangu ukapapasa mpaka mifukoni mwangu nakuchomoa ile bastola na kilichofuata nikumnyooshea,
"haya twende ukamuamshe huyo bosi wako fala wee..."
Akawa bado mbishi japo alikuwa amenyoosha mikono juu kujisalimisha huku akielekea mlango wakuingilia nyumba kubwa ya Gervas,nikamuwahi kwa mgongoni nakumfyatua risasi mbili za fasta akawa amekufa na kilichofuatia nikuuburuza mwili wake mpaka kwenye kibanda chake,na hapo nikaanza kulitafuta dirisha analolala Gervas.
Madirisha yote yalikuwa yale ya vioo tena ya 'kuslide' hivyo ikawa rahisi kujipenyeza ndani ya dirisha mojawapo huku nikiamini ni lakina Gervas,kulikuwa ni giza sana hivyo nikaingia hivyo hivyo kisha breki ya kwanza ni kuangaza kitandani huku mkononi mwangu nikishikilia ile bastola kikamilifu,nilipofika kitandani tu,
"Sshh...! nyamaza kimyaa,ole wako upige kelele...? Mwanangu yupo wapi...?"
Hakuwa Gervas wala Jammy bali alikuwa ni yule Mama aliyemtorosha mwanangu na kwa muda huu alikuwa mikononi mwangu.
"yupo kalala na Gervas chumba cha pili..."
Alipomalizia tu kusema hivyo hapo hapo nikamfyatua yule Mama kimyakimya akafa na kilichofuata nikuenda chumba cha Gervas, nilipofika kila nikijaribu kufungua mlango wake ilishindakana kwani kulikuwa kumelokiwa hivyo halmashauri yangu yakibhwa ikafanyakazi fasta nakugundua kuwa nipitie dirishani kama nilivyofanya kwenye chumba hiki,ndani ya dakika kama mbili nilikuwa nimeshaslide dirisha la Gervas kimyakimya nakuingia kiulaini bila ya wao kujua,nilipoingia tu nikawasha taa sambamba na bastola yangu nikawanyoshea.
"Levina...? Umefuata nini hapa...?"
Nilihisi kama wananipotezea muda wangu tu,nikaikoki vizuri bastola yangu ile nataka kuwafyatua tu mara sauti ya mwanangu 'Lauryn' nikaanza kuisikia analia hivyo mwili wote ukanisisimuka nakuachia ile bastola ikinidondoka huku nikimfuata kwenye kakitanda chake cha kulalia huku nikiwaacha Gervas na Jammy wakiendelea kunishangaa, nilipomfikia karibu tu nguvu ziliniishia nakujikuta nikidondoka kwenye kitanda alicholala Gervas na Jammy hapo hapo kwikwi ikanishika na macho yakageuka huku mishipa ya shingoni ikinitoka ikiambatana na mapovu pembeni ya mdomo wangu ikiashiria kama sio kifafa basi itakuwa ni dalili kupooza mwili wangu.
Nilipokuja kuzinduka tayari nilijikuta nipo kwenye kibaiskeli cha kubebea wagonjwa sebuleni kwa Gervas huku macho yakinitoka kwani kwa muda huu nilikuwa mtu niliyepooza, uwezo wa kuona nilikuwa nao lakini sikuweza kutambua kitu chochote ikiwa hata na sababu ya mimi kuwa hapa,kifupi sikuwa na fahamu yeyote lakini kilichokuwa kinanishangaza ikifika muda wa kula kuna dada mmoja ndio alikuwa akinilisha chakula na ninapokitema au kutapika naambulia kupigwa vibao na makonzi, nilikuwa si Levina yule aliyekuwa mtukutu kutokana na kupooza kwangu.
***********************************
::: Levina mikononi mwa Gervas na Jamila upya huku Levina akiwa amepooza na haelewi chochote kinachoendelea. Kweli mapenzi yanaumiza sana ten asana. Je unavyodhani Jammy na Gervas wataweza kweli kumlea Levina tena akiwa katika hali ya kupooza..
:::: Kila panaposhia ni kama unatamani iendelee..?? Vipi kuhusu mtoto wa Levina ‘Lauryn’? Nini Mwisho wa hii Simulizi kali na ya kuvutia..??CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
::: Hii ndio INATOSHA… Mwendelezo wa SITAKI TENA ni zaidi ya ile ya kwanza ni nzuri kuliko.. Kamwe usithubutu kuikosa hata siku 1..
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment