Simulizi : Inatosha
Sehemu Ya Nne (4)
Ilipoishia juzi..
"Gervas..., Gervas..., Jammy nimekukosea nini jamani...? Gervas kakukosea nini...?"
"embu nyamaza huko...?"
Aliongea jammy kwa ukali huku akiondoka kwa mwendo wa makogo nakuniacha nikipiga makelele kwa kulia huku kwikwi ikinibana.
Songa nayo sasa…
Niliendelea kulia huku nikitoka nje kwa kutoamini kwamba kweli Gervas ametoka mikononi mwangu kweliau la...!
Umati mkubwa wa watu waliokuwa wanachota maji hapa nje kwangu na wengine majirani walijaa kushuhudia ni kitu gani kimetokea hapa,niliendelea kulia tena kwa sauti ya juu huku wakimpakiza Gervas kwenye gari lao nakuondoka naye, niliendelea kuumia zaidi pale Gervas aliponyanyua mikono yake nakuniaga kwa kupitia dirisha la lile gari huku Jammy akiwa pembeni yake akioneshwa kufurahishwa na alichokitenda.
"...mi ndio Levina a.k.a mamaa Sammy, nitahakikisha Gervas anarudi kwenye himaya yangu..."
Nilijisemea kimoyo moyo huku nikirudishia geti nakurudi ndani,
"mama...! Mama...."
Ilikuwa ni sauti ya mwanangu akirudi toka shuleni na kwa muda huu alishuhudia umati wa watu ukisambaratika kutokea hapa nyumbani kwangu,
"....eti mama kuna ninì hapa leo mbona watu wamejaa hivi...?"
"...wala hamna kitu mwanangu twende ndani..."
"Baba yangu anaendeleaje...?"
Nilijikuta nasisimka huku nikipatwa kigugumizi cha ghafla nishindwe nitamjibu vipi,
"twende yupo ndani"
Niliongozana naye mpaka ndani na tulipofika tu ilinibidi nimwambie ukweli japokuwa alilia sana nakutaka nimpeleke alipokuwa baba yake.
¤¤¤¤¤¤¤¤¤
Siku hiyohiyo muda wa usiku kama saa moja moja nilimchukuwa mwanangu japo alikuwa akilia sana nikawasha gari langu na safari yakuelekea kwa Jammy kumtafuta Gervas ikaanza japo nyumbani kwao nilikuwa napakumbuka kidogo toka kipindi kile nimetoroka na mwanangu akiwa mdogo, nilijitahidi kukumbuka mtaa mpaka nikafikia ile nyumba nakusimamisha gari kisha nikamwambia mwanangu anisubiri ndani ya gari nakuelekea getini moja kwa moja,
"...samahani mlinzi hapa ndio kwa Gervas...?"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Gervas..? Gervas yupi tena...?"
"kuna kaka mmoja anaitwa Gervas anaishi na mke wake anaitwa Jammy, nimewakuta...?"
"...aanhaa unamzungumzia bosi Jamila...?"
"huyo huyo..!"
"sasa yule ameshahama hapa muda mrefu na hii nyumba alishaiuza muda kidogo..."
"kwahiyo sasa hivi anaishi wapi...?"
Yule mlinzi akainuka nakuanza kunielekeza,
"unaona njia hii...? Nyooka nayo moja kwa moja mpaka inapokata kona then hesabu nyumba mbili kutokea hiyo kona kuna nyumba kubwa inafensi yapinki ndio hapohapo.."
"ahsante,nimekupata wacha niende..."
Niliingia kwenye gari nakwenda mpaka nilipoelekezwa tulipofika nje tu nilisikia makelele ya kama mtu anapigwa tena akitoa sauti kubwa tu na yakiume moja kwa moja halmashauri yangu yakichwa ikanituma kuwa atakuwa ni mume wangu Gervas bado wanamuonea na kumtesa huko ndani,
"maskini Gervas mh...?"
Nilijisemea kimoyomoyo huku nikimwangalia mwanangu ambaye tayari alikuwa amelala.
Nilipaki gari nje kidogo na ile nyumba huku nikijishauri jinsi ya kuingia na nikiangalia saa yangu ilikuwa inaniambia saa 4 kasoro,mara nikashuhudia geti linafunguliwa kisha gari jeusi likatoka,niliangalia vizuri jibu nikalipata kuwa ni Jammy,hivyo nikaliwasha gari langu nikaanza kulifukuzia kwa nyuma taaratibu mpaka linapoelekea, ilikuwa ni njia ya kuelekea bagamoyo ambapo Jammy alikuwa akielekea,
"...leo ama zake ama zangu nitahakikisha namtoa duniani mshenzi mkubwa sana.."
Kiukweli nilijivika sura ya Levina yule wazamani huku nikiingiwa na hasira kali juu ya upumbavu alionifanyia Jammy.
~ BAADA YA MWENDO WA KAMA NUSU SAA ~
Sasa ilikuwa ni kama nyumba hazionekani kwani nakumbuka ilikuwa nimaeneo ya mbele (Bunju) ambapo Jammy alikunja kona yakuingia ndani ndani hivyo nilisimamisha gari langu nakujipachika kwenye magari yaliolazwa kisha nikazima taa zote,nikashuka nakuwafatilia taratibu huku nikimwacha mwanangu Lau akiendelea kulala ndani ya gari,mara akasimamisha gari lake kisha wakatoka wanaume kama watano hivi huku wakibebea kiroba kikubwa nakukitupa kisha wakaingia ndani ya gari nakugeuza,
Nilijificha bila wao kujua na waliponipita tu ukawa ndio mwanya wangu wakwenda pale kuangalia walichokuwa wamekitupa,
"maskini Gervas..."
Kumbe alikuwa ni Gervas amefungwa katika kile kiroba alikuwa nyang'anyang'a miguuni kwa kupigwa huku mdomoni mwake kukiwa na plasta iliyosababisha asipige kelele nikamfungua akatapika pale pale nakukohoa,nikiwa bado namshangaa Gervas pale mara mwanga mkali wa gari ukawashwa mbele yangu nakunimulika huku höni zikipigwa kwa nguvu zikiashiria kuna watu wameniona na wako ndani ya gari inayonimulika taa.
Sikuonesha kushtuka kwa hali yoyote,kwa moyo wakijasiri nikamwinu Gervas pale chini nikaanza kumburuta kuelekea upande ule uliokuwa unanimulika nilipofika karibu,
"uuhff uhfff..!"
Ilinibidi nipumue kwanza kwa nilichoshuhudia na kutokuamini kwani kiukweli lilikuwa ni gari langu mwenyewe na ndani yake mwanangu Lau alikuwa amehamka toka usingizini hivyo aliwasha taa sambamba na kupiga honi japokuwa hajui kuendesha lakini aliniogopesha sana,
"mama...? Huyö ni Baba...?"
"ndio mwanangu embu fungua mlango nimweke..."
Gervas alikuwa hajiwezi hata kuongea mwili wake ulikuwa na damu damu kuanzia kichwani hadi kwenye nguo zake zilizochanika chanika, nilimbeba nakumpakiza kisha safari ya kuelekea nyumbani ikaanza.
Ndani ya kama dakika 40 nilikuwa tayari nimeshaingia nyumbanì huku mlinzi akitufungulia mpaka ndani,tulisaidiana na kumbeba Gervas mpaka ndani na kwa bahati nzuri kile kibaiskeli chake cha wagonjwa kilikuwepo ndani hivyo ikawa rahisi kumuingiza mpaka ndani.
Hasira kubwa juu ya Jammy bado zilinishika lakini nilijipa moyo kwanza apone mume wangu Gervas then atanijua mimi ni nani?
***********
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hatimaye Gervas alianza kupata unafuu kidogo kidogo kwani ni mwezi 1 tu ulikuwa umepita toka walivyomuumiza wakina Jammy, nilijitahidi kumuhudumia nakuhakikisha anaendelea kupata matibabu vizuri kupitia kwa dokta wetu anayetutibia hapa nyumbani,vitisho vya kutaka kuniua bado viliendelea kupitia simu yangu tena kutoka kwa Jammy na sijui namba yangu aliipata wapi.
Nilikuwa na mazoea kila inapofika mida ya jioni namchukuwa mwanangu pamoja na Gervas huku tukizunguka naye kwa kutumia kibaiskeli chake, nakumbuka siku moja nilipokuwa natoka nje ya geti huku namsukuma Gervas kwa bahati mbaya alidondoka nakutapatapa huku vidonda vyake vilivyoanza kupona vikawa uinatoa damu nikabaki nikipiga sana makelele kuomba msaada huku nikisisimka nakutetemeka mwili mzima huku nikishindwa nianzie wapi kumnyanyua pale chini,sikupata msaada wowote hivyo nikawa namweka Gervas peke yangu kwenye kibaiskeli chake mara nilishangaa geti kusukumwa kwa nguvu huku nikimshuhudia Jammy akiwa na watu waliovalia nguo ndefu,
Aliingia kwa dharau huku akinitolea macho,
"Levina..., Levina...?"
"hivi Jammy unanitakia nini mimi...?"
"Mchungají huyu ndio binti niliokwambia amenichukulia mume wangu tena wa ndoa"
Jammy alikuja na mtu aliyedai kuwa nimchungaji na eti alikuja kutoa mashitaka kwangu hivyo nikabaki nawasikiliza,
"binti Gervas ni mumeo wa ndoa..?"
Aliniuliza mchungaji,
"hapana mchungaji ila ni mchum..."
Kabla sijamalizia kujibu nilishangaa napigwa bonge la kibao kutoka kwa Jammy, sikumwonesha hasira yeyote ya kutaka kupigana naye na nilichokifanya,
"Jammy si umesema huyu ni mumeo wa ndoa,haya mchukueni sasa mimi simuhitaji"
"No no Levina nooooo?siwezi kwenda kuishi tena na Jammy ataniua ataniua huko anapotaka kunipeleka,jaman nionee huruma levina,
"Gervas mimi siyo mkeo wa ndoa nenda na Jammy ambaye ni halali kwako"
Nilimwacha Gervas akichukuliwa tena na Jammy huku akipakizwa ndani ya gari na kwa muda huu sikuonesha kulia sana kwani hali ile nilishaizoea hivyo nikawa kama mtu aliyepigwa ganzi.
Jammy alipomaliza kumpakiza Gervas katika gari akanifuata,
"Levina? Haya kamuage mara ya mwisho kwenye gari na kwa taarifa tu tunaenda kumuua"
"unasemaje Jammy,unasemaje?"
Alinichanganya kiakili hivyo nikakimbia hadi kwenye gari aliokuwamo Gervas pale nje,
"Gervas.., Gervas shuka, shuka watakuua hao.."
Ndani ya sekunde chache nilikuwamo mlangoni mwa ile gari lakini chakushangaza nilivutwa kwa nguvu na mchungaji mule ndani ya gari na baada ya hapo Jammy akaingia nakilichofuatiwa niku lockiwa milango na madirisha yote na baada ya hapo yule mciungaji alivua nguo zake za uchungaji huku akitoa kisu na kamba ndefu sana nakuanza kunifunga funga,
Nilipiga makelele lakini haikusaidia chochote mule ndani kwani vioo vyote vilifungwa,
Kumbe hakuwa mchungaji yule bali nikama muuaji,
"hakikisha tunamdhalilisha humuhumu ndani ya gari huyo Gervas wake anayemng'ang'ania amshuhudie"
Aliongea Jammy huku akiliwasha gari. Yule mtu alivua nguo zake sambamba na zakwangu
Huku akitaka kunibaka.
Nilianza kupiga makelele nakutapatapa huku yule mchungaji akianza kunishika shika matiti yangu kisha akaanza kutelezesha mikono yake mapajani mwangu,sikuwa na hisia zaidi ya hasira kali,kwa muda huo Gervas hakuwa na jinsi ya kunisaidia zaidi kunitolea macho,kamba alizonifunga yule mchungaji zilinibana haswa haswa mpaka nikajikuta sina tena jinsi ya kujinasua zaidi ya kumwachia yule mchungaji afanye anavyotaka kwenye mwili wangu.
Alinibaka na kuniumiza haswa na baada ya kuridhika alichukuwa vidole vyake nakunidumbukizia katika sehemu zangu za siri tena kwa nguvu,nilichoka namwili wote kunilegea huku Gervas akishindwa hata kutoa sauti,
"Adrian...? Adrian...?"
Aliita Jammy aliyekuwa anaendesha gari hapo hapo halmashauri ya kichwa ikanituma kuwa atakuwa ni yule mchungaji ndio anaitwa Adrian,
"Naam mkuu..."
Aliitika kwa sauti huku akiniachilia nakuvaa nguo zake,
"Tumeshafika nyumbani sasa hakikisha hatoki mtu humu ndani ngoja niende nikakuongezee majeshi sawa Adrian...?"
Aliamrisha Jammy huku akimsisitiza Adrian, alishuka ndani ya gari nakutuacha mimi na Gervas pamoja na huyo Adriani.
Ndani ya dakika kama kumi Jammy alikuwa akifungua mlango wa gari kwa kutumia ufunguo wake kisha nikamshuhudia akiwa na wanaume kama wawili huku mikononi mwake akiwa kashkilia bastola moja pamoja na burungutu la pesa sambamba na karatasi kubwa ilioambatana na picha kubwa mbili huku akiwapa maelezo wale watu wake,
"hii ni ramani ya mpaka hapo zambia mjini,na hizi picha ni zakwao hii ni ya bosi wa hapo mpakani mkifika na hii ni ya mke wake anaitwa Happy hakikisha mnawakabidhi hawa watu na hii bastola ni ya kujiami chukueni hii simu na bastola kwa usalama zaidi"
"sawa bosi tumekuelewa,tunakuhakikishia tutatekeleza kama ulivyotuambia..."
Wale wanaume waliingia ndani ya gari wakaliwasha na safari ya kuondoka pale ikaanza huku tukimwacha Jammy pale nyumbani kwake,
Gervas alikuwa keshalala muda nafikiri nikutokana na maumivu aliyoyapata.
Ndani ya masaa kama manne tulikuwa tumeshavuka morogoro huku tukikaribia kufika Mikumi,akili yangu ilikuwa kama imeshachanganyjiwa kwani nilikuwa kama siamini amini kama kweli narudishwa kule ambapo sikufikiria hata kidogo kama nitaonana na hawa watu yani bosi na Happy,pili nilichanganyikiwa sana kwani muda wote nilikuwa uchi huku Gervas akiwa kaniegemea mapajani mwangu kapoteza fahamu kabisa.
Baridi kali lililofanya nianze kutetemeka mwili mzima huku meno yangu yakiumana yalimaanisha kuwa tupo katika mji huu wa Iringa,mara nikasikia simu inaita mwazoni nikajua labda huenda ni simu ya wale wanaume lakini haikuwa hivyo kwani mlio wasimu ulizidi kuwa juu na ulikuwa ukitokea kwenye nguo zangu zilizokuwapo pale chini,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mara mwanaume mmojawapo akatoka nakuichukuwa simu yangu kisha akabonyeza batani ya kupokelea akaniwekea masikioni niongee nayo.
"Mum uko wapi mama...? Baba na yeye yuko wapi...?"
Ilikuwa ni sauti ya mwanangu Lauryn akiniuliza nilipo,mwili wote ulinisisimka nakufanya mchozi uanze kunidondoka sambamba namkojo uliojipenyeya kupitia mapajani mwangu huku nikitaka kumjibu,
"Baba yako huyu hap...."
Kabla sijamjibu nilishangaa napigwa kofi huku simu ikikatwa nayule mwanaume.
Sikuwa nakumbukumbu yeyote,nilijitahidi sana kufikiria, mtoto wangu ndio alikuwa pembeni yangu huku Gervas akitetemeka meno nakunifanya niendelee kusisimka bila ya kuelewa chochote, nilitaka kuinuka haraka haraka pale kitandani,
"...no no Levina usifanye hivyo ona utajitonesha..."
Ilijuwa ni kauli ya Gervas akinisihi nisiinuke kwani kiukweli sikuwa najitambua vizuri,hapo hapo hisia zikanijia kuwa pale ni hospitalini, lakini nimefikaje fikaje hapa, kwa hapo sikuweza kujua chochote,
"mwanangu Lau, mbona unalia jamani kwani vipi...?"
"hapana mumy, ona ulivyo...! ona mumy umekuwa kama dady..."
Aliendelea kuongea mwanangu kwa uchungu na kunisababishia nijiangalie vizuri,
"oh my God...! nini tena, nini tena...! why me...! why me Levina...?"
Maskini Levina mimi nilikuwa nimekatwa mguu mmoja na sikujua chanzo ni nini,
"Gervas, Gervas embu niambie ilikuwaje mume wangu niko hivi...? Ilikuwaje Gervas...?"
"Levina kaa utulie kwanza ni stori ndefu.."
"Hapana Gervas niambie tu..."
"unakumbuka mara ya mwisho ulipokuwa unanitoa nje kwenye kibaiskeli...?"
"sikumbuki Levina kwani ilikuwaje..."
"siku ile ilikuwa kama bahati mbaya nikaanguka nakuumia sana,ulipiga makelele kwa ajili ya msaada lakini geti lilifunguliwa.."
"enh ikawaje...?"
"....wakaingia watu watatu waliovalia mavazi meusi marefu kama wachungaji"
"...nimeshakumbuka na Jammy si alikuwepo...?"
"hapana..., walikuwepo wenyewe wakakushika kwa nguvu nakuanza kukupiga kwa kutumia magongo yao pamoja na panga huku wakitaka kukuua..."
"Mungu wangu ikawaje...?"
"makelele yako yalifanya umati wa watu ukusanyike pale nyumbani na hata hivyo walikuwa wameshakuumiza sana mpaka ukapoteza fahamu na damu kukutiririka sana,tukakumbiza hapa hospitali na umezinduka hapa siku ya pili leo"
Nilianza kupiga makelele pale hospitali huku nikimwangalia mwanangu Lau kwa huruma nakugundua kumbe vile vyote vilivyonitokea vingine ilikuwa ni ndoto kama vile eti mchungaji amenibaka mara eti wananipeleka Zambia kwa bosi na Happy,
"kwanini Levina mimi nina mikosi hivi jamani...? Aaah?"
Nilijisemea kimoyomoyo huku nikijilaumu kwani kiukweli nilikuwa nimekatwa mguu mmoja na sikuweza tena kutembea...
********
Nilikaa muda mrefu kidogo hospitalini. Nilikuja kuruhusiwa baada ya mwezi lakini kila siku ilikuwa inatakiwa niwe naripoti hospitalini mpaka nilipoanza kupata unafuu kidogo lakini nikawa si mtu wakuendesha gari tena ilinibidi nimtafute dereva wakutuendesha na kumlipa na nilipatiwa kibaiskeli cha wagonjwa hivyo nikawa sawa na Gervas wote walemavu, mwanangu Lau hakuwa mtu wa furaha kwani alipungua sana na kufanya afya yake kuzorota.
Nakumbuka siku moja tuliporudi kutoka hospitali na Gervas tulioga na baada ya hapo ilikuwa muda wa kulala lakini kabla ya kulala,
"Levina mke wangu..."
"niambie Gervas..."
"kunakitu kinaniumiza sana moyo..."
"kitu gani hicho Gervas...?"
"Vipimo vya madokta baada ya wewe kufanyiwa opereshen..."
"vimefanyaje tena..."
"Levina mi sitakuja kukuacha kamwe wewe ni wangu milele yote..."
"Gervas...? We niambie kitu gani lakini..."
"Levina..,Dokta aliniambia nifanye siri mpaka utapopata unafuu lakini nimeshindwa kujizuia Levina,siwezi Levina na siamini mpaka sasa..."
Mchozi ulianza kunitoka huku ukiteleza mashavuni mwangu na makamasi ya majimaji. Hasira kali ikinishika nakunisababishia maumivu kwa mbaali yalioanza kunitoka kupitia mapajani,nikahisi kama ganzi si ganzi,mishipa mikubwa iliyokuwa imeanza kunitoka kuanzia shingoni na mpaka machoni ilinifanya nifanye maamuzi ya ajabu kwani niliona kama Gervas ananichelewesha kuniambia hivyo nilijikuta nachukuwa mikono yangu miwili nakumbana nayo Gervas shingoni mwake kimahaba,
"Gervas niambie Gervas niambie pliz..."
"Levina niache nikwambie ukweli..."
Nilimwachia,
"haya niambie Gervas"
"Levina, UMEATHIRIKA....!"
"niiiiiini Gervas....?"
"vipimo vinaonesha hivyo na yote hiyo ilisababishwa na lile panga ulilokatwa nalo na wale watu mwezi uliopita. Inasadikiwa kuwa lilikuwa lina damu damu za mtu aliyeathirika kwa ukimwi."
Nilinyong'onyea mwili wote na nisijue nifanye kitu gani na nilishangaa mtoto wangu akiwa mlangoni kwangu na kumbe muda wote alikuwa akutusikiliza,
"maskini mwanangu kashajua nimeathirika mimi..."
nilijisemea kimoyomoyo huku nikimwangalia mwanangu Lau kwajicho la huruma,
Kwangu ilikuwa ni wiki ya ajabu maishani mwangu kwani kuanzia hapo Gervas alikuwa kabadilika sana na kunakipindi alikuwa hataki kula hata chakula,nilijisikia vibaya sana haswa pale alipokuwa akishtuka ndotoni na kuniambia nimeathirika mara hawezi kuishi na mimi.
Nilipungua sana Levina mimi na sio kimawazo tu bali kwa ugonjwa niliokuwa nao kuna kipindi nilikuwa nakata tamaa ya kuishi kabisa kwani hata marafiki niliokuwa nao walininyanyapaa na ilifika kipindi nikawa nabadilisha wafanyakazi wa ndani na hiyo yote ni pale wanaponigundua nimeathirika walikuwa wakinitoroka.
Nakumbuka siku moja nikiwa sebuleni na mwanangu Lau huku Gervas akiwa chumbani kwake mwanangu aliniuliza,
"Mumy...! mumy...."
"unasemaje mwanangu...?"
"eti mumy na mi nimeathrika...?"
Nilinyamaza kama dakika moja bila kumjibu kisha nikavuta pumzi nakumjibu,
"hapana mwanangu,ni mimi peke yangu tu..."
"hapana mumy unanidanganya, mbona shuleni wananitenga wananiambia eti nimeambukizwa ukimwi na mama yangu..."
"hapana mwanangu waongo hao we mzima kabisa"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilijitahidi kumwelewesha mwanangu lakini alinielewa japo kishingo upande huku akiondoka,nikiwa bado nipo na mwanangu pale sebuleni nilishangaa Gervas akitoka na mabegi yake ya nguo,
"Levina..., Levina nashukuru kwa yote mema uliyonifanyia haina budi kukuacha sasa uendelee kuishi na mwanao..."
"hapana Gervas unakwenda wapi...?"
"levina siwezi kuishi tena na wewe siwezi, bora nikaishi popote pale duniani lakini siyo hapa"
"Gervas nilitegemea kuwa wewe ndio mtu wakaribu aliokuwa akinipa ushauri na vit.."
Kabla sijamalizia kuongea nilishuhudia Gervas akijikongoja na kibaiskeli chake huku kakumbatia mabegi yake yanguo nakutoka mpaka nje huku akiniacha nikipigwa na butwaa!
"mumy...,mwache aende mi nipo kwa ajili yako"
Maneno ya mwanangu Lau yalinifanya nisisimke mwili mzima huku mchozi ukiendelea kunitoka nisielewe chakufanya, hapo hapo mwanangu akatoka mpaka getini kumfungulia,
"bye dady...! bye..."
Mwanangu alizidi kuniliza sana na maneno yake kwani alikuwa na hasira kama za mama yake.
Ikawa haina jinsi zaidi ya kumwacha Gervas akijiondokea na kutuacha mi na mwanangu japo niliumia sana moyoni.
¤¤¤¤¤¤¤¤
Ni mwezi sasa umekatika bila ya kuiona hata sura ya Gervas wala hata kuisikia sauti, mwanangu Lau alipungua sana si kwa ajili ya kumwaza baba yake tu bali ni ugonjwa uliokuwa umemtokea wa kifafa kwani alikuwa akidondoka mara kwa mara nakutoa mapovu,nilimpeleka kwenye maombi makanisa mbalimbali ili aombewe lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya.
Nakumbuka siku moja tulipokuwa tunatoka hospitali kumpeleka mwanangu ghafla nikamwona Gervas na kwa kipindi hiki hakuwa na kile kibaiskeli na magoti yake yalionesha kupauka sana ikiashiria kuwa anatambaa kwa kutumia miguu,kwa kipindi hiki alikuwa omba omba wa mtaani,dereva alisimamisha gari lakini Gervas baada ya kutuona alikimbia hivyo hatukutaka kumwita zaidi ya kumsikitikia nakuendelea na safari yetu,nilikuwa si Levina yule unayemjua kwani nilibadilika sana na muda wangu wote nilikuwa nikiutumia katika kusoma biblia na vitabu vya stori na sana sana nilikuwa napenda kusoma novel ya 'ULINIACHA MARIA' iliyotungwa na Andrew Carlos, niliipenda sana haswa nilipenda kujifunza mambo mbalimbali ya maisha yanayotuzunguka. Kiukweli ilikuwa ikinigusa sana maisha yangu ya kila siku.
~ BAADA YA MIEZI MIWILI ~
Kwa kípindi hiki mwanangu aliisha kabisa na sikutaka hata aendelee na shule zaidi kubaki na mimi hapa nyumbani,vipimo nilifanya kwa mara nyingine tena na ni kweli vilionesha kwa madokta kuwa nimeathirika na kwa muda wote huu nilikuwa natumia madawa ya kuongeza kuishi.
Siku moja nikiwa ndani nimetulia sebuleni kulikuwa kimya sana hivyo nilimwita sana mwanangu lakini kimya kilizidi kutanda nakufanya nianze kuingia na wasiwasi,niliingia vyumba vyote lakini niliambulia patupu!
Niliporudi sebuleni niliona kama miujiza kwani nilikutana na kikaratasi,
LEVINA,
SIKU NYINGI NILIMTAFUTA MTOTO WAKO LAKINI NILISHINDWA NA SASA NAFURAHI NIMESHAFANIKIWA,
KACHUKUE MAITI YA MWANAKO CHOONI,
Mi Jammy.."
Sikutaka kuamini amini kwani nilihisi kama mchezo nachezewa kwani ile karatasi kiukweli ilikuwa na damu damu sa swali kubwa kwa kipindi kifupi ile karatasi imefikaje fikaje pale sebuleni?
Nilitoka fasta na kuelekea huko chooni na nilipofika,
"Mamaaa.., My God..! Uuuhf....! Uuuuhf....!"
Kiukweli ilikuwa maiti ya mwanangu ipo imelalia sinki la chooni,nilitetemeka sana huku nguvu zikiniisha nilimgeuza huku na kule ili kuhakikisha kama kweli kafa au la, lakini kiukweli alikuwa ameshakufa,nililia sana pale chini huku nikimburuza lakini ile nageuka nyuma tu nakutana uso kwa uso,
"Jammy...? Kwanini umenifanyia hivi kwanini Jammy..? Mwanangu kakukosea nini Jaman...?"
Hakusikia lolote zaidi ya kunifuata panga lake huku akitaka kuniua.
Jammy hakutaka kuendelea kunisikia na matokeo yake ile ananikaribia tu akateleza mpaka chini kwani kulikuwa na marumaru sambamba na majimaji ya chooni yalimfanya Jammy kuteleza na kuliacha panga likimdondoka chini,pale pale bila kupoteza muda nililiwahi lile panga na kumkata mkono wake wa kulia kisha nikamalizia mkono mwingine,
"Levina nisamehe...! Levina utaniua..?"
"...ni bora nikuue roho yangu itaridhika, umeniharibia sana maisha yangu Jammy..."
Nilimkata kata mpaka akapoteza fahamu kwani damu nyingi zilimtoka nilipomaliza nilipiga makelele kwanguvu nikiomba msaada,yule kijana wangu anayeniuzia maji nje ndio alikuwa mtu wa kwanza kuja huku akienda kuwaita majirani kwa ajili ya msaada zaidi.
Waliuchukuwa mwili wa marehemu mwanangu Lau kisha wakamuwaisha Jammy hospitali kwa haraka ikaitishwa msiba huku nikipewa pole na majirani, siri kubwa nilikuwa nayo moyoni kuwa ninani aliyemuua mwanangu na kumjeruhi Jammy.
***********
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hatimaye siku ya mazishi ilifika,nilimlilia sana kwa mwanangu Lau na niliamini kuwa ndiye mtoto pekee niliyekuwa naye kwani sikuwa na uwezo tena wakupata mtoto licha ya kwamba nimeathirika, mchungaji aliitwa pale nyumbani kwa ajili ya kuuombea mwili wa marehemu mwanangu huku umati wa watu ukifurika,
"...umefuata nini hapa, toka sitaki kukuona Gervas sitaki tokaa..."
Wakinamama wengi waliniwahi nakunishìka huku wakiniomba nipunguze hasira kwani Gervas alikuwa amekuja kuhudhuria mazishi.
"Simtaki jamani aondoke,kwani ye ndiye chanzo cha yote.."
Nilichoropoka nakumvamia kisha kilichofuata nikumtupia Gervas vibao nakumng'ata eneo la mapajani mwake,
"Levina..? Levina unamatatizo gani mke wangu...?"
"...nani mkeo, mkeo Jammy si..."
Kabla sijamalizia kusema umati wote ukawa kimya ghafla nakunifanya nijishtukie nitulie zangu.
Misa ilianza na baada ya pale tulienda moja kwa moja hadi makaburini, hasira kali nilikuwa nayo haswa nikimwona Gervas ndipo ilinijaa,muda wa kutupia mchanga kwenye kaburi la mwanangu ulifika na nilishindwa kujizuia nakujikuta nimedondokea kaburini,walinitoa kama mara mbili,nilikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa kwani kiukweli nilimpenda sana mwanangu Lau.
Hatimaye mwanangu walimzika kisha watu wote tukatawanyika na baadhi yakinamama walikuwa pamoja kunifariji japokuwa wengi wao waliondoka kimyakimya bila kujua chanzo cha ule msiba,Gervas sikumuona tena na ndivyo nilikuwa nikitaka.
Kesho yake mapolisi walikuja kuchukuwa maelezo kitu gani kilichopelekea kifo cha mwanangu. Uchunguzi ambao waliuchukuwa siku ya tukio haukuwa umekamilika vizuru. Wakaongezea maneno mengine kutoka kwangu. Ilinibidi niwaambie tu ukweli halisi kuwa Jammy ndiye kamuua mwanangu Lau, Nikawaelezea yote kuhusu maisha jinsi nilivyomjua Jammy na hata kunisaliti kwake.
~ BAADA YA WIKI ~
Ile hali yangu ya huruma ilianza kunijia baada yakusahau yale machungu yote ya nyuma niliamua kufuatilia hospitali nakujua hali ya Jammy,
Maskini alikuwa chini ya ulinzi mkali huku bado akipatiwa matibabu,kila aliyemuona alikuwa akimuogopa nakumtenga kiukweli alionekanika kama chizi chizi.
Nilifikiria sana maisha yangu ya nyuma jinsi alivyonisaidia wakati anaishi na mama yangu,sikutaka kulipiza ubaya wowote juu ya kunisaliti na kuolewa na Gervas wala juu ya kumuua mwanangu Lau,hivyo nilichokifanya niliwahonga polisi hela nyingi kisha mapolisi wakaifuta kesi kwa kuwa mhusika mkuu wa mtoto aliyekufa ni mimi. Niliifuta kesi kwa maandishi yangu mwenyewe polisi. Nilimchukuwa Jammy nakwenda kuishi naye nyumbani kwangu.
*********
Nilizoeana na Jammy tukawa zaidi ya marafiki kwani ule urafiki wetu wa kipindi kilee ukawa umesharudi japokuwa wote tulikuwa walemavu,kwa upande wa kwangu nilikuwa mlemavu wa miguu na Jammy alikuwa mlemavu wa mikono yote,
"Jammy nikuulize kitu..?"
"embu niambie ulipokuwa unaishi ulimwacha nan...?"
Kabla sijamalizia kumuuliza mara mlango ukagongwa ikiashiria kuna mtu anabisha hodi,
"karibu,naja kukufungulia..."
Haraka haraka nikatoka kwenda kufungua lakini mtu niliydkutana naye kumbe ni Gervas...
"umefuata nini hapa Gervas..?"
"...namtaka Jammy nimeambiwa anakaa hapa na yeye ndiye chanzo cha kifo cha mwanangu sasa leo ama zake ama zangu..."
"hivi we Gervas,kwanza ni nani aliyekudanganya kuwa Jammy anaishi hapa...?"
"Levina...? Usinione kama chizi,nina akili zangu..."
Gervas alinisukuma na kuingia ndani kinguvu moja kwa moja mpaka sebuleni huku akiita kwa nguvu,
"Jammy...?, Jammy nimesema toka mwenyewe nikuone la sivyo unajitafutia mengine....!"
Kimya kilizidi kutanda huku nikimwacha Gervas akitambaa na miguu yake huku akizunguka huku na kule akiita,na kwa muda huu Jammy alikuwa kajificha hata mi mwenyewe sikujua yupo upande upi.
"Gervas usiniue pliz...! pliz...!"
Jammy ilibidi ajitokeze na hakuweza kujisalimisha kwa kuinua mikono kwani mikono yake yote ilikatwa,
Gervas alipomuona tu Jammy na hali ile ghafla akabadilika,
"Jammy...! Jammy..."
"abee...!"
"ni we wee au naota...? Umefanyaje tena mikono...?"
Gervas alianza kutokwa na machozi hivyo kumfanya asahau alichokifuata,alinifanya na mi nisisimke sana nakuanza kuwonea huruma wote,
"Gervas...! Ni stori ndefu,ila naamini ni shetani alinitawala kwa muda mrefu nakunifanya niwachukie wewe na Levina,
Gervas kwanza nisamehe kwa yote niliyokutendea hapo nyuma ikiwa ni pamoja na mauaji niliyowahi kufanya"
"endelea...?"
"umeshanisamehe Gervas...?"
"nimesema endelea..."
"unakumbuka kipindi kile nilivyokutimua nyumbani kwangu..?"
"mmm... hhh..."
"basi kipindi kile mganga wa kienyeji ndiye aliyenishawishi zaidi nakupelekea nikufanyie vitu vya ajabu,na lengo langu kubwa lilikuwa nikuue kabisa ikashindikana ukanikimbia hivyo bado niliendelea na tabia ya ajabu ikanibidi nimuue hadi mfanyakazi wa ndani"
"nani Nosim...?
"hapana ni Mary, nilipomuua nikarudia tena kukutafuta wewe mpaka nikupate,nilitumia watu na pesa za kutosha mpaka nikafanikiwa kukuteka hapa hapa kwa Levina hadi tukakufunga kwenye kiroba.."
"Jammy, embu ishia tu hapo hapo, Gervas"
Ilinibidi nikatishe ile stori kwani Gervas alizidi kulia,
"unasemaje Levina...?"
Mi naona cha msingi hapa nikusameheana na pili kuangalia tunaishi vipi, napenda kama wote tukaishi kwa amani bila kuwa na malumbano yeyote"
Nilishangaa kwa mara nyingine tena Gervas akimfuata Jammy nakumkumbatia kisha bada ya pale Gervas alinifuata na mi nakunikumbatia,
"Levina...? Nakupenda na Jammy nawapenda sana"
"hata sisi Gervas tunakupenda...!"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***********************************
::: Ni kweli upendo umerudi kwa wote watatu, Gervas, Jammy na Levina?? Itakuwaje hapo.. Nini hatma ya Levina na Gervas.
:::: Kila panaposhia ni kama inavyoendelea.. Levina kahukumiwa kifungo cha maisha gerezani. Hana msaada wowote kwa sasa.. maisha yake yatakuwaje?? Nini Mwisho wa hii Simulizi kali na ya kuvutia..??
::: Hii ndio INATOSHA… Mwendelezo wa SITAKI TENA ni zaidi ya ile ya kwanza ni nzuri kuliko.. Kamwe usithubutu kuikosa hata siku 1..
:::: Kesho ndio sehemu ya mwisho kabisa wa INATOSHA je unavyodhani mwisho wake utakuwaje?? Unaweza kuotea mwisho wa INATOSHA..??
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment