Simulizi : Adhabu Ya Penzi Lako
Sehemu Ya Tatu (3)
Jackline hukuamini kabisa kama mama amefariki, hakutaka kuukubali ukwel kwamba tayari mama hayupo duniani. Akili yake iliruka kiasi cha kutokutegemea kama kweli hatokuja kumuona tena mama yetu, Kuna wakati alikuwa analia kwa uchungu sana, pia Kuna wakati hakutaka hata kumsikia mtu yeyote akilia, "msilie sababu mama hajafa, amelala tu ngoja nikamwamshe" akisema hivyo basi akili inamkumbusha kuwa hakulala ila amefariki na hawezi kuamka milele, Kuna wengine pale hawakuwa wakimlilia marehemu ila Jackline aliyeshindwa kuzuia maumivu na kujikuta akilia kilio kikuu "mama weee! Mama yangu mimi jamani! Kwa nini Sasa umeniacha, umenikimbia wakati mimi nimekuja karibu yako" hakuna aliyeweza kumzuia Jackline asilie, "Gabriel kwani mimi nina lia, wala silii mimi, kwanza namlilia nani wakati mama ameenda shambani kuchuma mboga aje apike" masikini Jackline akili haikutaka kukubali kuwa mama amefariki, kikubwa ambacho kilimfanya achanganyikiwe zaidi ni kwamba alijua wazi kifo cha mama mimi ndo nimesababisha "mhh Rose, mhh siamini, Rose" Kuna wakati aliishia kusema vile bila ya kuendeleza sentensi "Sawa Rose, haya umeshinda," uchungu ukizidi aliishia kucheka kicheko kikuu sana sababu alihisi machozi hayatoshi kuelezea maumivu aliyokuwa nayo moyoni. "masikini Jackline, mhh kifo hiki kisikie tu kwa jirani kisikukute" majiran walisema hasa pale wakimwona Jackline akilia kwa uchungu
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Zilipita siku kama Tatu ivi sikupokea simu kwa yeyote yule aliyeko kwa mama, sikuwa najua kinachoendelea, wala sikuwa najua kama mama amefariki. Nilianza kuhisi si kawaida ya wao kukaa kimya kiasi kile, nilipompigia simu Gabriel hakupokea, Jackline nae hakuwa anapatikana, nilikumbuka mfanyakazi wa ndani anayo simu basi nilimpiga kujua kulikoni "mama amefariki tangu sikuile uliyokuwa unaongea nae" niliposikia ivo nilishtuka sana, sikuamini kama nimesababisha kifo cha mama, nilianza kulia kwa kujutia kifo chake, "nisamehe mwanangu labda sababu nataman kukuona" Ile kauli ya mama kwa nguvu ilinivaa akilini, nilikosa nguvu na kuanza kulia sana, "mama jaman ningejua ningekuja kukuona" nililia huku nikiendelea kutafuta mawasiliano na Jackline kujua kulikoni kwa bahat nzuri simu yake Iliita japo haikupokelewa, kama sekunde ivi Jackline alinipigia "unasemaje" bila ya salamu aliniuliza "mimi na wewe undugu umeishia hapa na sitaki kukuona kwenye mazishi ya mama yangu, kamtafute mama yako" kwa hasira ambazo sikutegemea Jackline alitamka "Iwapo utakuja nitakuaibisha sana Rose" kauli za Jackline zilibadilisha maumivu yangu na kuwa sumu, Nilikata simu, nilishusha pumzi kisha niliingia chumbani na kutafakari sana "nisipojihami mapema Lazima nitaumbuka Lazima nifanye jambo" niliwaza hayo huku nikipanga nguo zangu kuelekea msibani.
Siku ya kuzika ilifika, "mbona Rose hayupo kaenda wapi" majiran na baadhi ya ndugu walianza kuhoji huku wakishangazwa na kitendo cha Jackline kulazimisha mama azikwe bila ya mimi kuwepo. Gabriel alikaa kimya sababu hakuwa na sauti pale kwani yeye ni mgeni tu ila alikuwa upande wa Jackline kuwa wamzike bila ya mimi kuwepo. "Sawa hamna tatizo" walisema ndipo ratiba ziliendelea, ibada na maombezi ya mwisho yalifanywa hatimae walibeba jeneza kuliweka kaburini tayari kwa kumpumzisha mama kwenye nyumba yake ya milele, msiba ule ulibeba watu wengi sana sababu ya kujulikana kwa mama yetu, watu walikuwa wengi kiasi cha sisi kufika pale bila ya wakina Jackline kutuona, niliposhuka kwenye gari, nilianza kulia kwa sauti Ili kuwafanya watu wageuge na kunitazama "huyu si Rose, mhh makubwa" sauti za minong'ono ilianza kusikika, "Jackline umemuua mama, Jackline namtaka mama yangu" Nilisema kwa sauti kuu hali iliyosababisha kusitishwa kwa shughuli zote Ili wanisikilize, niliongozana na polisi waliomshikilia mbaba mmoja, jeusi kweli aliyekuwa amevaa mavazi yaliyomtambulisha kama mganga, pia kulikuwa na wapiga picha na waandishi wa habari katika msafara wangu "Jackline namtaka mama yangu, Jackline umeniulia mama, jamani majiran huyu mtu muuaji sana" Nilisema machozi yakinitika, "nimeshagundua mbona zako Jackline sikubali" watu wote walichanganyikiwa pale msibani, Gabriel na Jackline walikaa kimya sababu hawakuwa wananielewa "ebu tulia utueleze kwanza" mchungaji alisema hayo kisha nilifuta machozi na kuanza kueleza "kifo cha mama yangu kimesababishwa na huyu mwana haramu, kamtoa mama yangu kafara Ili afanikiwe kwenye biashara zake" niliposema tu vile kila mtu alitoa sauti ya mshangao ajuavo "yarabiii weee!" wengine "mama weeee" na wengine "heeeeeeeeeeee" kila mmoja alishika mdomo wake. Jackline kwa jazba alinyanyuka alipokua amekaa na kunifata kisha alinivamia Ili tupigane kwani alijua wazi namsingizia "Jackline sijali kama wewe ni ndugu yangu nachotaka nirudishie mama yangu" niliendelea kueleza mengi ya kumfedhehesha Jackline aliyekuwa akilia kwa uchungu, "huyu mtu hapa unamfahamu? Huyu ndie aliyekupa masharti ya Kuja kumuua mama" basi kila neno ninalolitamka lilikuwa gumzo kwa waliopo pale, wengine walificha nyuso zao kwa kanga ishara ya aibu na wengine walishika vichwa, kijana yule niliyemkodi Ili ajidai mganga alianza kujieleza "huyo binti alikuja kwangu kutaka dawa ya kusafisha nyota Ili awe tajiri," aliguna kidogo kisha aliendelea "nilimpa sharti La kujenga nyumba ya kifahari kwa mama yake kisha kabla hajaingia kwenye hiyo nyumba majini yatakuja kumkaba na kumuua" Gabriel alimtazama Jackline kwa hasira, alikuwa amemshikilia ghafla alijitoa kwenye mwili wa Jackline na kusogeza mbali nae, "mama yake tumemfanya msukule atakae kuwa akitumikishwa na Jackline, ila ameshakosea masharti hivyo hatoweza tena kumsaidia," Jackline kusikia yale alikosa nguvu miguuni hatimae alidondoka chini karibu na kaburi La mama, alilia kwa uchungu haamini kama dunia imeamua kumuadhibu kiasi kile, "alinitaka pia nivuruge ndoa ya dada yake sababu hakutaka Dada yake kuolewa na mchumba aliyemsaidia maisha" maneno ya huyo mganga feki yalimfanya Jackline kuchukiwa pale pale "muuaji mkubwa wewe mzike huyo msukule mwenyewe" wazee wenye heshima kijijini pale walighadhabika sana kusikia Yale maneno "Rose tafadhal Sema ukweli, unaniadhibu kiasi hiki" machozi ya Jackline hayakuwa na thaman tena pale msibani, kila mmoja alifyonza, alisunya na kubeza "hata aibu huoni unamuua mama yako kisa mali" Gabriel alisema na hasira akiamini wazi Jackline kweli kumuua mama "roho yangu ilikuwa ikisita sana Kuja huku kumbe ulikuja kufanya ushetani niliendelea kumkandamiza Jackline aliyekuwa akikana kuwa hajui chochote" kwa nini hamjiulizi kuwa Jackline anataka kuzika bila ya mimi kuwepo " niliposema vile wengi waliamini na kuwa upande wangu. Mmoja mmoja alianza kuondoka pale msibani" mzike msukule wako mwenyewe sababu uliyataka mwenyewe, "tafadhal naomba mnisikilize, mchungaji naomba unisikilize" Jackline alikuwa akitembea kwa magoti akiwa omba watu wamsikilize "Gabriel hata wewe huniamini tafadhal nisikilize" Jackline alisusiwa maiti na kaburi ambalo halikufunikwa. Gabriel alimchukia sana Jackline hakutaka hata kumsikia, aliingia ndani na kuchukua mizigo yake pamoja na ya Anthony kisha walipanda gari na kumwacha Jackline pale nje akilia na kulaani kwa nini alizaliwa, majiran wote waliondoka wakiwa hawawezi kula vyakula vya kafara, nilianza kuhisi huruma, ule undugu ndo uliokuwa unanikosesha amani, Jackline alinitazama na kucheka kwa uchungu "utabaki kuwa Dada yangu, na ukweli unaujua wewe, kikubwa niseme nashukuru kwa yote" kabla sijajibu Gabriel alinitaka niingie kwenye gari kisha wote tuliondoka tukamwacha Jackline peke yake pale, hakuna jirani wala mtu yeyote pale, alilia huku akifukia kaburi La mama yake kwa mikono, ilikuwa saa nane za mchana, hakuchoka kufukia, aliendelea huku maneno yangu yakimtawala kichwan, ghafla aliona kundi kubwa La watu likiingia mle ndani, alikuwa ni mchungaji na baadhi ya watu, wengi walikuwa wageni alipopepesa kuwaona wageni hao alibaini mmoja wapo alikuwa Mary mke wa Victor akiongozana na familia yake, marafiki zake, na baadhi ya marafiki zetu ambao tunaishi nao mjini
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati Jackline akiwa pale kaburini hajui afanye nini, aliona kundi kubwa La watu likiingia mle ndani, alikuwa ni mchungaji na baadhi ya watu ambao walionekana ni wageni, Jackline alishtuka na kushangaa kulikoni, kwani yule mchungaji aliyemuacha ndiyo aliyerudi, moyo wake ulihisi kupata nguvu kwani Kuna baadhi ya marafiki zake aliwaona, alisimama kwa tahamaki Ili aweze kuwatazama na aendelee kubaini miongoni mwa hao watu, kwa mbali kidogo alipotupa jicho lake Ili atazame alimwona Mary, mke wa Victor, hakuamini alipomwona mwanadada huyo ambae kwa historia ni maadui tena Jackline aliapa Iwapo atamuona popote Lazima atampiga, moyo wake ulizimia ghafla kwani alipomtazama vizuri alibaini alikuja msibani hakuwa kishari, alivaa mavazi ya msibani, kichwan alijifunga kitambaa kufunika nywele zake, mkononi alishikilia kitambaa chakujifutia machozi, Jackline alipomwona hakujali kama ni maadui, alijikuta akilia kwa uchungu sana huku akimfata Mary "Mary, mama yangu, Mary ameniacha pekee tangu" alianguka kwenye miguu ya Mary na kulia sana, "Mary kweli mimi naweza kumuua mama" kitendo cha Jackline kumuona Mary kilisababisha Jackline kuuanza msiba ule upya, "najua huwezi Jackline, tafadhali jikaze" Mary alimkumbatia Jackline na kumfariji "wote wameniambia, Mary hadi Rose kanikimbia, Nani wakunishika mkono mimi" kwa maumivu makali Jackline alieleza "ndo maana niko hapa kuku shika mkono, usijali Jackline" Mary aliyaongea hayo utadhani hakuwahi kupigwa na Jackline, utadhani hawakuwahi kugombana, muda si mrefu baadhi ya majirani walirudi msibani "loooh Rose mbaya sana, kwanini Sasa amefanya hayo" walianza tena kujirudi baada ya kuujua ukweli kutoka kwa Mary ambae baada ya sisi kuondoka yeye alikuja na kuwaeleza ukweli majirani, alienda hadi kwa mchungaji yule na kumweleza yote aliyokuwa anayajua Kuhusu ule msiba. "Rose si binadamu kabisa" aliwaita viongozi wa kijiji na kuwaeleza "huu ni mpango wa kumfedhehesha Jackline Ili ukweli usipatikane kwamba yeye ndo chanzo cha kifo cha mama yao" Mary hakusita kueleza yote aliyokuwa anayajua "yule hakuwa mganga wala polisi Bali ni michezo tu iliyofanyika" aliendelea "mume wangu mimi ndiye aliyefanya michezo hii ndo maana nina uhakika na nisemacho" siku zote ukweli hujitenga na uongo, Mary alieleweka kuliko hata mimi niliyeenda kwa machozi "kama Rose anauchungu na mama yake kwanini hayupo, kwanini ameondoka na kumuacha Jackline" alibadilisha kauli na kuongea kwa hasira "Jackline analia kwa uchungu tena usio na unafki, ni nani anaetoa kafara akaililia maiti hiyo" jazba zilimpanda Mary, "hata wewe mchungaji?" alimgeukia na kumtazama "unaongozwa na Mungu au unajiongoza, hata bibilia unayoisoma kila siku haikusaidii" machozi ya hasira yalimtoka "Jackline si rafiki yangu ni moja ya maadui zangu tena wakuuana kabisa, Lakin mbona sijafurahi unyama unaofanywa na mume wangu na Rose" maneno ya Mary yaliwajutisha wengi na kukiri walikosea "OK mlivomsusia kaburi mlitaka nani alifukie, huo ni u binadamu au," alisema "Kati ya Jackline na nyie ni nani ambae ni mnyama" alipozidi kusema mchungaji alimkatisha na kukiri kukosea, "jaman turudini tukamzike marehemu kisha tumuombe msamaha Jackline" mchungaji alisema ndipo wote walipongozana kurudi kwa Jackline Ili wamzike mama, Jackline hakuamini kabisa kama leo hii adui yake mkubwa ndiyo faraja yake. Alijuta kwanini alijiingiza kwenye migigoro isiyo mhusu. "usijali Jackline huwa hatujui mbele Kuna nini ndo maana tunafanya mema au mabaya" Mary alimdhihirishia wazi Jackline kuwa Hana tatizo na yeye na alishamsamehe. Walimzika mama kisha wote walitawanyika akabaki Jackline na Mary pamoja na watu waliotokea mjini.
Baada ya mazishi kuisha, Mary alionekana kuwa karibu sana ya Jackline kwani aliutambua uchungu alionao kwa kumpoteza mama yake pia kusalitiwa na Dada yake. "usilie Jackline, tayar yameshatokea na huwezi kuzuia" alimfariji kiasi ambacho Jackline hakutegemea, "Mary sikujua kama una roho ya u binadamu kiasi hiki" Jackline alimweleza Mary aliyetabasamu kusikia vile, "pamoja na yote leo umekuja kwangu kama Dada yangu kipenz" Jackline alikuwa akilia na mengi, siyo msiba tu wa mama yake ila pia jinsi matukio yalivyomwandama utadhani yalihifadhiwa ndo yamefunguliwa. "Mary mimi siwezi kumuua mama yangu" kile kitendo kilimuumiza sana Jackline, bora angeambiwa chochote ila si La kumuua mama, akikumbuka jinsi alivyotamani siku moja apendwe na mama kwani mama hakuwa anampenda alizidi kuumia. "mama amekufa mkononi mwangu, amekufa kwenye mikono ya mtoto aliyemtenga miaka mingi" Mary alijitahidi sana kumtuliza Jackline akimhakikishia yeye yupo pamoja nae asiwe na shida, "hata Gabriel amenitenga hakuna wakunisaidia mimi" alizidi kujieleza kwa Mary ambae alilazimika kutumia ukorofi Ili Jackline anyamaze "Jackline utanikwaza Sasa, kwani sisi tuliopo hapa siyo binadamu" aliuliza "kwaiyo bila ya Rose na Gabriel wengine hawawezi kukufanya ukaishi" ukali ule ulifanya Jackline awe mpole na kulia kimoyo moyo. Mary alinyanyuka alipokuwa amekaa akaenda jikoni kumpikia Jackline chakula sababu hakula siku tatu mfululizo. "nahitaji ule chakula saivi, usije ukatufia saivi" Mary alimsogelea Jackline na kumpa chakula, Jackline alikula kwa kumheshimu Mary, sababu ya njaa alikula chakula kingi sana. "Asante sana dada Mary nimeshiba" Jackline alishukuru,"Dada Mary... " kwa mara ya kwanza Jackline alimwita Mary dada nae aliitika kwa adabu," Asante kwa wema wako " Jackline alishukuru ila Mary alimsogelea na kukaa karibu nae." mdogo wangu katika hii dunia usimfanyie mtu ubaya ukiamini umemkomoa " Mary aliposema hayo Jackline aliguna" kama ni ivo mbona wewe ulimuumiza Rose, ukamsababishia matatizo makubw" Jackline alihoji maana Mary alijitapa kuwa hatupaswi kuumizana. Mary alikaa kimya kwa dakika kisha alimtazama Jackline kwa umakini, "mshukuru Mungu Rose amekutendea hayo, wapo wanaotamani Rose afe hata kesho" Jackline kusikia vile aliguna alishtuka pia alistaajabu "mimi na Rose hatujakutania Mwanza, nimesoma nae tangu darasa La tano, kisha sekondari kipindi icho wewe ni mdogo sana" Mary alimweleza Jackline kisha alianza kumsimulia mambo ambayo nilishawahi kumfanyia
* *****
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mimi na Rose tulikuwa tunasoma shule moja na darasa moja, tulikuwa marafiki wakusaidiana kwa kila jambo, tulikuwa tunapenda sana starehe, basi tunatoroka shule na kwenda kwa wanaume, tunafanya starehe alaf tunarudi nyumbani, siri ya Rose ndiyo yangu, kila kitu tulikuwa tunafanya Sawa, hatukuwahi kugombana hata siku moja na tulisikilizana sana. Siku ya kufanya mtihani wa kidato cha nne iliwadia tukafanya na kumaliza shule, matokeo yalipotoka mimi nilifaulu alafu Rose alifeli, alilia sana na kunilaumu mimi kuwa nilikuwa nampoteza, aliamin mimi nilikuwa nasoma alaf namdanganya yeye asisome, nilijitetea ila hakunielewa, hata mimi mwenyewe sikuwa najua nimefaulu vipi. Tangu siku hiyo Rose alianza kunitenga na kunikwepa. Sikumjali sana japo roho ilikuwa inauma sababu sikutaka kugombana nae. Muda wa kwenda shule ulifika na niliondoka nikamuacha nyumbani, kufaulu kwangu kulinifanya nipende shule na nikianza kuzingatia masomo, nikiwa kidato cha tano mwishoni nilipata taarifa baba yangu amefariki, nilirudi nyumbani kwa ajili ya mazishi, na kama unavojua kwetu hatukuwa na uwezo sana zaidi tulikuwa tunamtegemea baba ivo ndoto zangu za kuendelea kusoma ziliisha, nilijaribu kutafuta msaada ila sikufanikiwa. Mama yangu aliniambia nisahau shule kwani hatoweza kunisomesha. Nilipiga moyo konde na kuisahau shule, nikawa namsaidia mama kuuza mboga kibandani kwake, siku moja Rose alinikuta kibandani na kuanza kunicheka "ngombe wa masikini hazai na akizaa anazaa dume, heri yetu tulishazoea maisha ya mtaani" sikuyajali Yale maneno kwanza sababu nilimzoea ni mtu wa vimaneno, pamoja na yote ila urafiki bado ulikuwepo japo wakusua sua.
Siku moja nikiwa kibandani alikuja Kaka mmoja anahitaji mboga, "unaweza kunisaidia kukata kata maana hata siwezi" aliposema sikubisha niliziosha vizuri kisha nilimkatia Ile mboga vizuri, "tayari Kaka hii apa" kwa roho ya ukarimu nilimpatia "Asante sana basi ngoja nikulipe na ya kunikatia" alipotoa pesa nilikataa kuichukua nae alinilazimisha sana "hapana Kaka, zawadi yangu ni wewe kuwa mteja wangu" niliposema vile yule Kaka alicheka na kukujali. Yule Kaka akawa mteja wetu hadi mama akawa anampenda. Nilianza kushangaa mama akienda sokokuu kuleta bidhaa Lazima atenge matunda ya Elibariki, "basi tu mwanangu nikimuona Elibariki najisikia aman" mama alimsifia sana ila mimi nilimwona wa kawaida. Siku moja nikiwa nyumbani, nilimsikia mama akimkaribisha mtu ndani "Mary! We Mary Kuna mgeni njoo" nilitoka chumbani kuendelea sebuleni "aah Elibariki ni wewe, karibu" nilimkaribisha na kukaa nae, "ngoja niende kupika chai" Ni destur ya watu wa Arusha kumpikia mgeni Chai huenda ni sababu ya hali ya ubaridi wa mkoa huu. Nilibaki na Elibariki tukaanza kupiga stori za hapa na pale, kijana huyo alikuwa mcheshi sana nahisi ndo sababu ya mama kumpenda. Nilianza kujihisi kumpenda Elibariki sababu ya ucheshi wake. Muda wa kuondoka ulipowadia mama alinitaka nimsindikize kwani ni kijana mwenzangu. Tukiwa njiani Elibariki alikuwa akinisifia sana na kunieleza chanzo cha yeye kuzoeana na mama yangu. "Mary ninakupenda tangu zamani, nikaona bora niwe rafiki wa mama yako Ili niwe huru Kuja kwenu kama ivi nilivokuja" nilivosikia vile nilicheka sana kwani sikutegemea, "kweli vile Mary tena mama yako mwenyewe ndo Kaniambia nije kuona mnapokaa wakati mimi napajua tangu zaman" nilicheka sana na kujikuta nazidi kumpenda. Wakati tunasindikizana tulijishtukia tumefika kwa Elibariki. "haya na wewe ingia uone ninapoishi" niliingia ndani na kukaa kwenye kochi kubwa, aliwasha TV iliyopachikwa ukutani "hakuna mwanamke aliyewahi kujua nyumba yangu iko vipi zaidi yako" nilitabasamu na kuficha macho kwa aibu. "Mary nakupenda sana na Iwapo utanikubalia nitakuwa tayari kukuchumbia hatimae nikuoe" nilipo sikia vile moyoni nilifurahi sana japo machoni nilijidai kujiumauma kwamba sitaki, elibariki alinisogelea na kuanza kunichezea mwili wangu, sikuweza kujizuia ndipo na mimi nilipojisogeza kwake na kuanza kupokea utamu kutoka kwa Elibariki. "looh Mary nitakupenda daima" Elibariki aliyasema hayo huku akizidi kujilia matunda yake kwa mitindo na ufundi wa kila namna. "nakuahidi kukupenda kwa dhati" kwa siku hiyo ilikuwa ni Shoo ya haraka haraka sababu hatukupanga. Tangu siku hiyo Elibariki alikuwa mpenzi wangu ambae tayari alienda nyumbani kujitambulisha. Ndipo Rose alipopata tetesi kuwa nina mchumba.....
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Rose alijua wazi kuwa Nina mchumba ambae yupo mbioni kunioa, Hakupenda kabisa bahati Ile ambayo iliniangukia, kila mara alinisema kwa watu na marafiki zetu, chuki yake kwangu sikuweza kuitambua mapema japo kila wakati hakusita kunikosoa hasa iwapo sitaki kufanya jambo alitakalo,
Kwa Elibariki upendo ndo ulizidi kwangu, alinisikiliza na kunijali sana, aliyaheshimu mawazo yako na kunipa nafasi ya kuyajua maisha hasa pale alipotumia muda mwingi kunionya baadhi ya mambo ambayo hayakuwa yakimpendeza, Elibariki aliahidi kunisomesha na kuniendeleza na masomo yangu. Nilimshukuru na kuzidi kumpenda zaidi, ikawa siambiwi wala sisikii kwa Elibariki.
Siku moja nikiwa na Rose, alikuja Elibariki kibandani pale, tulisalimiana kisha nilimenya embe Ili nimpatie, "Elibariki sikuizi Mary anaringa sana sijui umempa nini" sikutegemea kama Rose angeweza kuongea yale hasa kwa Elibariki, nae Elibariki alicheka tu na kula embe lake "Mary utanikuta nyumbani leo Nina mazungumzo muhimu" Elibariki alisema na kuondoka "Rose ujue sipend kuingiliwa mambo yangu" kwa ukali Nilisema ila yeye hakujali "mhh nawe unajifanya umefika na huyo Elibariki wako" alisema na kuniacha nikiwa nimekasirika yeye akaondoka zake. Rose hakuwa akinisumbua sana sababu nilimzoea
Wiki kama Tatu ivi Zilipita, Elibariki hakuwepo alisafiri kikazi sababu alikuwa mwajiriwa, siku iyo nilikuwa naumwa sana na sikuweza hata kwenda kibandani, Rose alikuwa nyumbani na kunikuta nimelala, nilimweleza jinsi ninavyojisikia nae akanishauri twende hospital kujua tatizo, wakati naenda nilimtafuta sana Elibariki kwenye simu ila hakupokea, "we na we kwani Lazima Elibariki ajue kila kitu kama hapatikani basi achana nae" alisema hayo ila mimi nilizidi kumtafuta. Baada ya majibu nilijitambua kuwa mimi mjamzito. Sikushtuka sana wala sikuogopa sababu nilijua Elibariki asingenikana maana alitaman sana niwe mama wa mwanae, japo nilihisi ndoto zangu za kusoma zimeyeyuka. Nilipompata kwenye simu Elibariki nilimweleza yote. Alifurahi kusikia ilo japo mimi sikufurahi sababu nilitaman kusoma "Mary utasoma tu mpenzi, nizalie kwanza mtoto" Elibariki alinifariji na kunihakikishia kuwa nitasoma. Nilitabasamu na kufurahi kuona kuwa Elibariki yuko upande wangu. "sijaona mtu mjinga kama wewe" Rose alinisema sana baada ya mimi kumweleza kilichojiri "hapo anakudanganya tu, tangu lini ukishazaa unasoma" kwa mfedhehesho alinieleza "bora utoe hiyo mimba alaf usome kwanza" aliposema vile nilikataa katu katu kumsikiliza huku nikibaki na msimamo wangu kuwa nitajifungua kisha ndo nisome, "haya utaona" Rose alijibu na kukaa kimya ila nilijua wazi hakupenda kabisa.
Elibariki alizidi kunipenda sana na kuniahidi mambo makubwa sana "nitahakikisha maisha yako ni ya furaha na amani milele mpenzi wangu" nilijiona mwenye bahati sana kuwa na Elibariki ambaye alinisaidia mambo mengi.
Siku moja siku ambayo sitoisahau, nilikuwa nyumbani kwa Elibariki nimelala alikuja Elibariki nyumbani amekasirika, niliamka nikiwa mchovu nikamsogelea Ili kujua kulikoni, nilipomsogelea alinisukuma kwa nguvu nikaangukia kitandani, "mpenzi Kuna tatizo?" kwa hamaki niliuliza ila hakunijibu wala kunisemesha, nilizidi kuhoji tatizo nini lakini bado alikuwa mkimya "ebu niache kwanza nipumzike" Elibariki alibadilika sana siku iyo, nilimwogopa mno,. Nilielekea jikoni kumpakulia chakula chakula napo alikataa kula chakula nilichopika. "nimekufanya nini kwani mbona sikuelewi" nilihoji ila bado hakunijibu "kama huwezi kukaa kimya amka uende nyumbani ukalale kwenu" aliposema vile nilianza kugomba na kutaka kujua kosa langu, kwa kuwa hakuwa tayari kunieleza aliamka na kuondoka kulala nisikokujua. Aliniacha chumbani peke yangu, alinitelekeza mle ndani bila ya kujua kosa langu, sikuweza kulia sababu siwezi kulilia kitu nisichokijua, zaidi nilijawa na mawazo, nilikosa amani na usingizi pia, nilipompigia simu hakuwa anapokea wala kujibu sms, hofu ilinijia, nikaamka pale kwenye sofa na kuelekea kwa Rose, nilipofika sikumkuta Rose, nilipompigia simu hakuwa anapokea, sikujua kinachoendelea. Shida yangu ni kujua Elibariki anatatizo gani hivyo sikuwaza chochote kibaya, wakati narudi nyumbani, nilikutana na moja ya rafiki zetu, nilipomuulizia Rose alinipa jibu lililonichanganya sana "alikuwa na shem Eli wanaelekea nadhani nyumbani kwa Elibariki" aliposema vile niliguna tu kisha Nilielekea nyumbani nikijua labda nitawakuta nyumbani Lakin bado sikuwaona. Nilianza kuingiwa na hofu juu yao ila niliamua kunyamaza kumsubiri arudi.
Palipokucha alirudi nyumbani asubuhi sana, alinikuta nimelala. Alipoingia alinitazama sana kisha aliguna, sikumsemesha chochote zaidi nilimwandalia maji ya kuoga nika mwandalia na chai kama kawaida, sikutaka tena kujua Kuna nini, nilijawa na hasira baada ya kuambiwa kuwa walikuwa wote na Rose ndio maana hamu ya kujua Kuna tatizo gani sikuwa nayo tena "Ina maana Rose ananigeuka leo" nilijiuliza sana hali sijielewi, wakati nachukua nguo zake chafu Ili nizihifadhi ilidindoka boksi La condom, "whaaaaaaaat?" sikuamini macho yangu, pale pale machozi yalinitoka, "Ina maana Jana walikuwa wote" nilijiuliza "kwaiyo yote Yale yalikuwa Ili aende kulala na Rose" 'sikutaka kuamini kabisa. Wakati najiuliza aliingia ndani kutokea bafuni. Kwa hasira niliweka condom Ile mezani Ili aone, nae alipoiona alishtuka kwa hasira alihoji "umetoa wapi hizo takataka" aliposema vile kwa hasira nilimrushia kikombe cha plastic walau nimpige tu "umechanganyikiwa nauliza umetoa wapi" maswali yake yalizidisha hasira kwangu kwani nilihisi wazi ananifanya mtoto. "kwaiyo Jana ndo ulienda kufanya upuuzi huu si ndio" nilihoji huku nikimpiga nayo usoni boksi lile, Eli alionesha kutokunielewa, alibaki ameduwaa na kunishangaa "we iyo mimba naona inakuchanganya sasa" Elibariki aliniambia hayo, nami niliamka zangu na kuondoka, lengo ilikuwa kumfata Rose anieleze alikuwa wapi na Elibariki Jana, nilipofika tu kabla sijahoji chochote Rose aliniwahi "afadhali umekuja apa nilikuwa napanga kukufata kwako" aliposema vile nilitulia kwanza kumsikiliza "Jana nilipigana na mtu kisa shemeji" alinieleza nikajikuta nahamu ya kujua ilikuaje "Jana shem sijui kaokota wapi mwanamke anataka kwenda nae guest nilivowaona nikamkamata yule Dada nilimpiga kweli, kwani Elibariki alikuja Jana saa ngapi" looh Rose alifanikiwa kunifanya nisielewe kabisa Nani wakumuamini. Nilishusha pumzi kwa tahamaki kisha nilibaki mkimya, "karibu chai" alinipa chai jambo ambalo siyo kawaida yake kunipa kitu mkononi hasa chakula ila siku iyo alinipa, sikujali chochote nilipokea na kunywa "mbona Chai ya leo mbaya ivi alafu chungu" Nilisema ila yeye alicheka tu, "we nawe unayako inauchungu gani" kiukweli ilikuwa chungu ila nilihisi labda mdomo wangu ndo mchungu nikaendelea kunywa, nilipomaliza kile kikombe tu ivi nikaanza kusikia tumbo linasokota, "Rose umenipa nini" wakati namuhoji nilianza kushtukia damu zinanitoka Sehemu za siri
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilijihisi damu zikinitoka Sehemu za siri, huku tumbo langu likiuma kwa kuhisi kama Kuna kisu kinachokata kata nyama za tumboni, jasho kali na La kuloanisha mwili lilinijaa mwili mzima, nilihisi maumivu makali na uchungu ambao sikuwahi kuupata kabla na baada ya hapo, "Rose umenipa nini kwani" nilimuuliza Rose ambae hakunijibu ilo swali akijidai halisikii, alianza kuita watu Ili wamsaidie kwani hali yangu ilizidi kuwa mbaya, "sijui imekuaje ghafla tu nimeshangaa kuona hali hii" alijitetea kwa majirani ambao walinibeba na kunipeleka hospitali kwa haraka, nguvu ziliniishia na damu iliyochanganyika na mabonge bonge yaliendelea kunitoka kwa kasi sana, nguvu za kuongea ziliniishia na mwili wote ulikosa nguvu ila nilikuwa nasikia kila kikichosemwa na kuona kila kinachoendelea, "mimba imeharibika tayari, kikubwa ni kumuokoa tu mama" madaktari walionipokea walielezana huku wakishangazwa na dawa hiyo iliyotumika kuharibu mimba hiyo "sijui ni nini ametumia ila inaonesha ni kali sana kwani imefanya kazi kwa muda mfupi" kiukwel nilikuwa nasikia japo uwezo wa kujibu sikuwa nao, akili ya kulia au kutafakari sikuwa nayo labda sababu ya dawa Ile ilinilegeza. Walinichoma sindano ambayo kwa dakika chache sikuelewa tena kipi kinachoendelea.
Taarifa zangu zilimfikia mama yangu na baadhi ya ndugu zangu, kila aliyemuuliza Rose nini kimenipata alijibu majibu mabaya sana "hata sielewi maana alikuja nyumbani analia kisha alichemsha maji ambayo aliweka kitu kama majani ya Chai alafu akanywa ndo hali ikabadilika" looh Rose aliwaaminisha watu kuwa niliitoa Ile mimba mwenyewe. Akiwa pale hospital alikuja Elibariki huku akikimbia kuelekea kwa daktari "hapana doctor Mary hawezi kutoa mimba kirahisi ivi" Elibariki alilia sana sababu alitamani sana mtoto kwangu "huo ndo ukweli na pamoja na kutoa mimba, sumu hiyo imeenda pia kuathiri mfukoni wake wa uzazi kiasi kwamba kila atakapo beba mimba Lazima itatoka" daktari alizidi kumchanganya sana Elibariki, "Lakin nashindwa kuelewa kwanini ameitoa ujauzito wa miezi mitano, mligombana" daktari aliuliza swali ambalo lilimchosha Elibariki ambae hajui chochote kinachoendelea, "hapana ila leo alinionesha condom, akadai ilikuwa kwenye mfuko wangu, wakati si kweli" Elibariki akiwa pekee yake na daktari alimweleza, "unauhakika hukuwa na hizo condom" daktari aliuliza "hapana tangu niwe nae sijawahi kumsaliti, nampenda sana," Elibariki alijitetea, daktari alikaa kimya kwa muda, alishusha pumzi kisha aliendelea, "alikuwa tayari kubeba mimba" aliulizwa "ndio na alikuwa na ndoto nyingi sana na mwanae" majibu ya Elibariki yalimfanya daktari kushindwa kujua chanzo cha mimi kutoa mimba Ile. Elibariki alitoka kwa daktari hajielewi alimkuta Rose amekaa kwenye benchi La watu wanaosubiri wagonjwa wao, alipomwona Elibariki alisimama na kumfata "vipi mbona unalia, unamlilia Mary, mtoto au wote wawili?" kwa kejeli Rose alimuuliza "nilishakueleza huwezi kuishi na Mary kwani si mtu wa kuolewa yule, kashazoea uhuni ila hukunisikia" Bila ya aibu wala huruma, Rose alidiriki kupandikiza chuki kwa Elibariki ambae hakutaka kuamini kabisa kama kweli mimi naweza kuwa mhuni, kabla hata hajaongea alikuja Kaka mmoja pale alipo Rose na kuanza kuongea na Rose mbele ya Elibariki "shem vipi hali ya Mary, je mwanangu aliyeko tumboni" kwa macho ya tahamaki Elibariki alishangaa, Rose nae alijidai kuona aibu mbele ya Elibariki, "shem niambie Mary kapatwa na nini" kijana yule alionesha kuwa na mahusiano na Mary hali iliyomchefua Elibariki ambae hakutaka tena kukaa pale hospitali. Alipoondoka Rose na yule Kaka walibaki wakicheka, "umefanya kazi nzuri sana asante mwaya" wakati wanapongezana Rose aliitwa na daktari yule aliyekuwa akiongea na Elibariki. "ukiwa muungwana kwangu na me nitakuwa muungwana kwako" kwa macho yaliyojaa ujasiri daktari alisema, "wewe ndie uliyemuwekea sumu Mary kwenye Chai yake" Rose kusikia vile alishtuka sana, "nimekuwa nikikufuatilia tangu siku uliyokuja kutoa maelezo Kuhusu tukio hilo" aliguna na kuendelea "huyo kijana uliyokuwa unaongea nae ni nani yake Mary" maswali ya daktari yalimfanya Rose aogope sana, alianza kulia na kulalamika "tafadhal usije ukanisema popote sikuwa na namna zaidi ya kufanya vile" alianza kujitetea huku akilia "Mary alinifanya nikaachwa na mpenzi wangu kwa hasira niliamua kufanya vile" Rose alibarikiwa roho ya ushawishi na alifanikiwa kumshawishi daktari ambae alimuhurumia, "kwa hiyo saivi huna mpenzi" daktari alisahau kumhoji vya maana akajikuta anauliza maswali mengine huku akionekana kumtamani Rose "OK, ukikubali kuwa wangu nitakufichia siri hii" maneno Yale yalitoka kwenye kinywa cha daktari na hii ilikuwa ni sababu Rose alitengeneza mazingira ya kumshawishi daktari.
Nilipozinduka nilijiona mwepesi tumboni, "pole mwanangu unajisikiaje saivi" mama aliniuliza "mama mimba yangu imetokea?" Niliuliza huku machozi yakinitoka kwani awali niliwasikia madaktari wakisema "huku machozi yakimtoka mama yangu aliitika kwa kichwa" Rose umeharibu mimba yangu" kwa sauti nilisema, mama yangu alishtuka kusikia vile, "alinipa Chai baada ya kunywa hali ilibadilika" nilipomweleza mama alilia sana, "usijali mama wala hakuna haja ya kumuuliza sababu hatoweza kunirudishia mwanangu" Yale maneno sikuyatoa kana kwamba nimemsamehe hapana ila sikutaka mama yangu ayaingilie. Mama aliponiaga kuwa anarudi nyumbani nilianza kulia na kulalamika sana, "kwanini Rose umenikosea ivi" nililia nilipojua sitoweza kubeba tena mimba kwani mfuko wangu wa uzazi umelegea "umenipa jeraha ambalo siyo rahisi kulifuta akilini" nililia sana sababu nimepoteza sifa ya kuitwa mama.
Tangu nizinduke sikumuona Elibariki, kila nikimuuliza mama yangu alinijibu hajui chochote Kuhusu yeye, hofu ilianza kunivaa kwani nikikumbuka zile condoms ndo kabisa Sina imani, niliomba Mungu siku za kutoka zifike Ili nirudi nyumbani kwa kuwa kila nikimpigia simu hapokei,
Niliruhusiwa na kurudi nyumbani, Ile naingia tu ndani, nilisikia vicheko vya majirani "hata aibu haoni kutoa mimba kubwa kiasi kile, amshukuru Rose La sivyo angeitwa marehemu saivi" nililia sana kusikia vile, moyo ulizidi kujaa maumivu ambayo sikuweza kuyazuia, kesho yake nilienda kwa Elibariki, nilimkuta anafua, Daaaa aliponiona alijawa hasira sana, "kilichokuleta kwangu, kipo umesahau, nguo zako, OK subiri hapo hapo nikuletee" bila ya salamu nilivamiwa na maneno yakukatisha tamaa, aliingia ndani na kutoa nguo zangu kisha alinitupia begi miguuni "mwanamke nyoka sana wewe, kipi umekosa mpaka kunifanyia unyama huu" Aliponieleza hayo nilikaa kimya kwanza sababu sikuamini "sahau ndoa kwangu, pia sitaki kukuona tena kwangu siwezi kumuoa malaya" Aliponieleza vile, nilijikuta nikilia Kwani Elibariki hakutaka kunipa nafasi ya kujieleza, niliinua begi langu, nikalivaa begani, nilifuta machozi kisha nilifungua mdomo wangu kuongea "nafsini mwako hautokuwa huru kwani umefungwa na uongo, hautokuwa na amani milele mpaka siku nitakayo kueleza ukweli kwani mwenye ukweli siyo Rose ila mimi" niliposema vile nilivua Pete ya uchumba na kumkabidhi kisha niliondoka zangu hali nikilia barabara nzima, nilipofika nyumbani nilianguka kwenye miguu ya mama yangu na kulia sana, mama alinibembeleza huku akinitia moyo, "Elibariki anakupenda a mini ilo," alinifuta machozi yangu "usidhani umekomolewa, hii ni nafasi pekee ya Mungu kudhihirisha utukufu wake siku zijazo, futa machozi mwanangu" mama alinifariji japo moyo wangu ulikusudia mabaya juu ya Rose na niliapa kulipiza hata kama nitakuwa mzee.
Baada ya wiki moja mjomba wangu alikuja kunichukia Ili nikaishi nae Mwanza, sikutamani kuondoka alafu nimwache Elibariki sababu bado nampenda ila kwa kuwa sikuwa na namna niliondoka zangu.
Baada ya mwaka mmoja nilisikia tetesi kuwa Elibariki aliamua kuondoka mtaani pale na kuhama kabisa mkoa, niliumia sana kwani sikuwa na mawasiliano nae pia huko Mwanza nilianza maisha mpya japo sikuhitaji tena mahusiano kwani Elibariki alikuwa bado anaishi moyoni mwangu.
Pia nilipata habari kuwa Rose alitoroka mtaani sababu alifumaniwa na mume wa mtu, na tabia zake za kugombanisha watu zilikithiri akaona bora atoroke
*********
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilipokuja kumwona Mwanza, sikuamini kabisa, pia sikutegemea kama ningemkuta katika hali ya kubadilika kiasi kile, et ni mtu anaejua maisha na anapambana na maisha, pia nilishangaa sana kuona yuko na Victor pekee yake Hana mahusiano na watu wengine, kiukwel nilishangaa sana pia sikuamini. Kwa kuwa moyo wangu ulishaapa kumwadhibu sikujali kubadilika kwake, nililazimika kujifanya nimesahau ya nyuma Ili malengo yangu yatimie,
Victor na Rose wanapendana sana ila niliamua kuwatenganisha, nilitumia nguvu nyingi sana kumbadilisha Victor Ili awe wangu, wakati mwingine Victor alipenda kumsifia Rose kuwa ndie mwanamke pekee anaependa, me sikujali sababu lengo langu haikuwa mapenzi ila kumkomoa Rose.
Sikuile wewe umenipiga, ilikuwa siku mbaya sana kwangu, tulipofika nyumbani Victor alinipiga sana kwani alidai mimi ndie niliyesababisha matatizo, "umeniachanisha na Rose bado leo umenikutanisha na mwanaume nisiyempenda ambae yuko na Rose" Kuna wakati nilikuwa namwonea huruma Victor kwamba amemuoa mtu asiyempenda ila sikuwa na lakufanya sababu lengo langu lilikuwa kisasi
Nilianza kumwonea huruma Victor ambae alikuwa akimpenda wazi Rose, alikua simpi haki yake na uhuru wa kuwa na mtu amtakaye sababu ya tayari tulifunga ndoa halali kabisa kanisani, alijitahidi kunipenda lakini hakufanikiwa, alipogundua hawezi kunipenda aliamua kuishi na mimi kwa mazoea, heshima ya mke na mume kwangu haikuwepo, Victor alianza matendo ya ajabu kwangu, hakuwa anataka nimuandalie nguo asubuhi, akikuta nimepika anajipakulia mwenyewe, chochote alichohitaji alifanya pekee yake, mimi sikuona ajabu wala sikukonda wala kuumia kwa Yale matendo sababu sikuolewa na mwanaume ninaempenda, Japo Kuna wakati nilihitaji kuwa karibu nae, siku akiwa vizuri huwa namfurahia ila siku akimkumbuka Rose wake mweee! Nikikosea kidogo basi Rose atatajwa siku nzima, kiukwel Yale maisha hayakunisumbua pia niliona bora iwe ivo Ili nifanikiwe kutimiza malengo yangu kwamba kabla sijafa Lazima nilishuhudie chozi La damu La Rose.
Mara nyingi Victor huwa alichelewa kurudi nyumbani, siku nyingine harudi kabisa, nilianza kumfatilia nikabaini Kaka wa watu hanisaliti ila tu nyumba Ile ni kama jehanamu kwake kwamba anaishi na mtu asiyekuwa chaguo lake japo alijitahidi sana kutokunikwaza, Siku hiyo alirudi nyumbani saa saba za mchana jambo ambalo siyo kawaida kwake, alinikuta nafua nguo, yeye akaingia ndani hadi chumbani, niliacha kufua na kumfuata ndani, "mwanangu hali ishakuwa ngumu hapa sina namna" nilimsikia akiongea na simu tena kwa hali ya upole, "itanibidi niuze tu magari yangu yote nilipe maana najua hayo ndo nitayapata tena ila si kuachia kampuni zangu" nilipo sikia vile nilishtuka sana, niliogopa na nilijua atakuwa anadaiwa na mtu. Niliingia ndani na kumkuta amekaa chini sakafuni kanyoosha miguu kama mfiwa, aliponiona alinitazama tu na kuendelea kuongea hadi alipomaliza, "najua nyie wanawake mnatupenda tukiwa na magari Sasa naenda kuuza, sijui utaendelea kuningangania" aliposema vile badala ya kusononeka nilijikuta nacheka, nachocheka ni jinsi alivijihami kwangu, "saivi unacheka ila baadae nitakusikia sijui una mbunge, mara waziri mara huyu kisa mimi nimefilisika" aliendelea kunipa mabango ambayo mimi sikuyawaza. "we unahisi nimekupendea gari?" huku namsogelea ili niwe karib nae niliuliza "tangu umenioa ulishasikia nikijivunia kuwa na wewe tajiri?" aliposikia hayo alinigeukia na kunitazama "mwone saivi unaongea kwa upoleee mhh kesho kutwa utaanza kunitukana" nilianza kumshangaa kwanini sikuiyo amekazana kunieleza hayo wakati mimi na yeye huwa hatuna muda wa kumfatilia mwingine, "wewe ni mke wangu iwe nakupenda au sikupendi utabaki kuwa mke wangu" alisema huku akitafuta makaratasi muhimu kabatini, "yani upo hapa kwangu mpaka leo sababu nimegundua wewe si mhuni, tangu nimekuoa hujawahi nisaliti" kwa mara ya kwanza sikuiyo aliongea neno lililo nifanya nitabasamu "nimekuwa nikikufatilia kuanzia ukiamka mpaka ukilala, nikabaini niko peke yangu" alianza kunieleza matukio mengi ambayo nilikuwa nikikutana nayo, "unakumbuka Kuna siku ulikutana na mtu mkaanza urafiki, alipoanza kukuhitaji kimapenz ulimtukana sana basi yule alikuwa mfanya kazi wangu" nilipo sikia vile moyoni nilifurahi sana japo machoni nilijidai kujiumauma, "kwaiyo nakufahamu vizuri sana ndo maana upo kwangu mpaka leo, japo ukweli ni kwamba mimi nampenda Rose" Victor hakuwahi kuogopa kunieleza ukweli ule ambao niliuzoea "Sasa si uwe nae kama bado unampenda" nilimjibu kumsikia atasema nini "siwezi na haitotokea, mimi nina mke tayari japo simpendi ila siwezi kumsaliti, labda nitampenda sikuzijazo" maneno yake alinisisimua kiasi cha kuhisi vimachozi, nilinyanyuka pale kisha nilianza kupiga hatua kwenda kuendelea kufua "Sasa unaenda wapi, mhh umechukia? Basi njoo mke wangu" kitendo kile ndo kilinifanya nishindwe kuvumilia machozi, "tangu nimekuoa leo ndo nimeona machozi yako" Victor alijaliwa roho ya kubembeleza acha tu, aligundua amenikosea akasimama haraka na kunifuata kisha alijisogeza kwenye mgongo wangu nakunibusu shingoni, "naanza kukupenda kuanzia leo mke wangu" Victor alisema hayo huku akinishika kiuno changu, "nisipokupenda wewe Sasa nimpende nani" alinibusu tena shingoni. "haya twende nikakusaidie kufua mke wangu" Victor alinivuta hadi nje tukaenda kufua wote, unajua muda wote anayafanya yale mimi nimebaki nimezubaa kiasi kwamba sikuamini kama Victor ndo anaefanya Yale yote, alifua huku akinipigisha stori nying ambazo nilikuwa nacheka muda wote, "siyo uongo we jua nampenda Rose ila mke wangu ni wewe" aliyaongea hayo japo siku iyo ilikuwa kwa utani, "ila kuanzia leo nitajifunza kukupenda wewe Sawa mke wangu" aliposema vile alinimwagia maji ya kufua tukaacha kufua tukaanza kumwagiana maji, siku iyo nilijiona wakipekee sana, nisijihisi mtoto ambaye anacheza na baba kipenzi, pale pale tukasahau kufua hatimae tuliingia ndani hali Victor akiwa amenibebe kama mtoto, alipofika chumbani aliniweka kitandani kisha alisogelea radio iliyoko chumbani na kuweka wimbo ambao huwa anaupenda sana, wimbo wa USHER unaitwa GOOD KISSER, alivua nguo zote akabaki na vest na kaptula, alianza kunichezea hali akinionesha mapenzi ambayo sikutegemea kabisa kama angenipa, uso wangu ulijawa tabasamu, alinisogelea na kunivuta, nilipojivuta nikatua kwenye kifua chake, alinishika mashavu yangu na kunisogeza mdomoni kwake akanibusu kwenye paji La uso, mwili wangu wote ulitepeta nikabaki sijiwezi, tukiwa wote tumesimama Victor alinikamata kiunoni huku akizidi kunichezea shingoni kwa mdomo wake, hatimae alianza kunisasambulia nguo zangu hadi kufikia hatua ya wote kubaki watupu, alinisogeza hadi kitandani, "jaman Victor kumbe mtundu ivi siamini kama leo ameamua kunionesha mapenzi haya" moyoni nilijisemea sababu sikuamini, sikuwahi kupata mahaba kama hayo tangu namfahamu, alipokuwa juu yangu alinitazama kwa umakini "Mary una macho mazuri sana," sifa zilianza kumiminwa huku akicheza na viungo vyangu "siku ya leo nakukabidhi moyo wangu kama mke wangu" aliposema vile nilifurahi sana na kumkumbatia kwa huba na bashasha zote. Victor alinipa penzi ambalo sikutegemea kulipata na sikutarajia kama ningelipata. "nitakupenda mke wangu"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Maisha mapya kwenye ndoa yangu yalianza, nilianza kujua thamani ya ndoa baada ya Victor kunionesha nini maana ya mapenzi, kila siku kwetu ni valentine, mapenzi yalidumu acha kabisa, furaha ndani ya nyumba ilirudi, utasikia "mke wangu usipike leo tunaenda kula hotelini" mara "beby Nina zawadi yako najua utaipenda" siku nyingine "beby leo nikija nataka uniliwaze nimechoka sana mke wangu" upendo aliouonesha Victor kwangu ni upendo ambao pamoja na kwamba alimpenda Rose ila hakuwahi kuwa karibu yake kama ilivo kwangu, nilianza kapendeza kwa sababu ya furaha, rangi yangu Iking'aa kama jua.
Baada ya mwezi ivi nilianza kujihisi tofauti," mume wangu najihisi kama kuumwa umwa "kila mara nilikuwa namweleza Victor ambae Kuna wakati kila akija ananikuta nimelala," inabidi twende hospital maana nakuona haupo sawa" Victor aliniambia hayo huku akinitafutia nguo za kuvaa. Aliniandalia Chai kisha tulienda hospital, tulipofika daktari alitusikiliza sana, "kabla ya kupima Lazima itakuwa mimba" daktari alisema vile "unasemaaaaa?" Nilihoji "kwani hujasikia mke wangu, una mimba" Victor alidakia huku akionesha furaha. Mimi niliogopa na kushtuka sana, "yawezekana vipi mimi kubeba mimba" nilijisemea. Taarifa zile sikuzifurahia ila nilijifanya ninafuraha kuficha siri Ile ya kutokubeba mimba. Victor alifurahi sana, upendo wake ulizidi mara dufu, nilianza kuhudumiwa kama malikia, nililetewa dereva wakuniendesha, wafanya kazi ndani wakaletwa, Lakin mimi nilijawa na hofu sana, sikupata nafasi ya kuonana na daktari sababu ya ulinzi niliyowekewa na Victor. Nikisema nataka kwenda mahali Victor alitaka tuwe wote, sikujua nitaonana vipi na daktari, "Leo ngoja nitembee tembee hata miguu ichangamke" nilitegea ameenda kazini ndo nikasema ivo "upo wapi" aliuliza "hapa hapa mtaani natembea tu" alipojua ni maeneo ha nyumbani alikubali, "nipeleke hospital mara moja, ila Victor asijekujua kama tulitoka" nilimweleza dereva aliyekubali. Nilipofika kwa daktari nilimweleza kisa chote, alinichukua na kunipeleka kwenye vipimo. "mhh una mtihani sana Mary" daktari alisema hayo "unaweza kujifungua ila ni Lazima uhakikishe maisha yako ni ya kulala kuanzia mimba ikifika miezi mitatu La sivyo huwezi kujifungua" daktari aliposema vile nililia sana nilizidi kumlaani Rose sababu sikuwa na namna, sikuwa na namna yoyote Ile nilirudi nyumban Ili nikatafakari kipo chakufanya sababu Nina hamu sana na mtoto.
Mimba ilifikisha miezi mitatu, sikuona tatizo lolote, nikifika clinic naambiwa nijitahidi kutokufanya kazi wala chochote maisha yangu yawe ya kulala, nilizidi kujitahid kufata masharti hadi mimba ilipofikisha miezi mitano,
Sababu ya kulala muda wote nilianza kuwa mvivu hadi kutembea, sikupenda kumweleza Victor chochote Kuhusu tatizo langu, basi akawa anajua tu ni uvivu ndo unanisumbua ndo maana nalala ovyo. Siku moja niko chumbani niliamka kitandani nikataka kwenda bafuni kuoga, nilipofika mlangoni nilishika kitasa Ili nifungue mlango, kumbe kanga yangu ilishikiliwa na mlango kwenye kambao kalikopasuka kidogo, nilipopiga hatua Ili niingie zaidi nilivutwa na mlango ambao nilikosa balance nikajikuta nateleza hatimae niliangukia tumbo, nilipiga kelele mfanyakazi alikuja na kunisaidia, taarifa zilimfikia Victor ambae nae alikuja mbio hadi hospital. Alipofika alinikuta nikiwa hoi sijiwezi. "pole Victor, mkeo ameanguka vibaya hali iliyompelekea kuharibu mimba yake" Victor aliposikia vile alinyamaza kimya "ila mke wangu mzima?" alihoji kujua tu hilo "kama mzima naweza kumwona" alihoji "hapana mwache apumzike hata ivo hata yeye hajui kama imeharibika" daktari alijibu. "basi sawa" majibu ya Victor yaliwashangaza watu sababu hakuonekana kuumizwa "mlitaka nitoe machozi ndo mjue nimeumia, kikubwa ni mke wangu kuwa hai" alisema na kuendelea kunisubiri niamke,
Nilipoamka nilimwona Victor yuko karibu yangu, "nakupenda mke wangu" Victor aliniambia huku akibusu mkono wangu "mimba yangu imetoka" Nilihoji "usijali nitakupatia mtoto mwingine, mimi nipo mke wangu" maneno ya Victor yalinichoma sana moyo uliuma, machozi yalitoka, nililia kwa sababu kuu Tatu, mimi kutokupata mtoto, Victor kunifariji kitu ambacho hakiwezi kuwa, na pia kumbukumbu ya mambo ya nyuma yalinirudia. "usilie, mbona mimi silii mke wangu," Victor alinifariji lakini haikuwa rahisi mimi kumwelewa japo sikuwa naongea chochote. Roho ya kisasi ndo ilitawala akili yangu sana
Ilipita wiki mimi bado sijarudi katika hali yangu ya kawaida. "sitoweza kuishi na Victor tena kwani Sina sifa za kuwa mama" nilijiwazia hayo huku nikiwaza ondoka zangu kurudi Arusha kwa mama. Nilitegea Victor ameenda kazini ndipo na mimi nilipanga nguo zangu Ili niondoke. Nilimuachia barua Victor iliyomtaka ajue kuwa mimi nimeondoka kwake na siwezi kurudi tena. "Victor akija mpe hii barua" nilimpa dereva ambae alihoji sana naenda wapi ila si kumweleza. Hakuna aliyefurahi kuondoka kwangu ndipo mfanyakazi alimpigia simu Victor na kumweleza, muda mfupi tu tangu niachane na dereva nae alimpigia simu, "yupo hapa Nyegezi, we njoo nikupeleke hotel aliyoko" dereva alisema na ndani ya dakika kadhaa Victor alikuja hadi hotelini pale, aliingia na kuuliza kisha aliletwa hadi chumbani na mhudumu wa pale. Victor aliponiona tu alinitazama kwa jazba huku macho mekundu, alikagua nipo na nani. "una matatizo? Ahaaa so ulitoa mimba Ili uje kunitoroka si ndio" Victor alianza kuongea vitu ambavo havijui. "nataka kujua kwanini unanitoroka" wakati huo wote mimi nilikuwa nalia tu, niliona Sina namna nikaamua kumweleza yote, baina yangu na Rose, nilieleza vyote bila kubakisha chochote, "hayo ndo yaliyonipelekea mimi kuolewa na wewe sijaolewa sababu nakupenda" nilimaliza kwa kumweleza hayo
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kitendo namaliza kumwadithia Victor, sikuamini kabisa kuona chozi La Victor, unajua katika maisha yangu niliyoishi na Victor, huwa naamin Victor ni mwanaume mkorofi sana, basi siku hiyo nilishuhudia chozi lake kwani alinihurumia hasa pale aliponiona nikimwelezea kwa uchungu matatizo Yale, sababu sikuweza kuzuia maumivu hasa nikifika eneo ambalo lilikuwa likiniumiza sana, "kwanini hukuniambia siku zote" kwa sauti ya chini Victor aliniuliza huku akinifuta yale machozi, "sikuweza kukueleza sababu usingenielewa pia siyo rahisi kuaminika" nilijitetea kwa Victor, "kwanini umekubali kuolewa na mtu usiyempenda" Victor alizidi kunihoji j maswali magumu sana kwangu, "Victor kutoka moyoni, namchukia sana Rose, hawezi kuwa rafiki yangu hata dunia ikibadilika na kuwa ya njano sitoweza, sikuwa nahitaji ndoa ila kisasi" Nilisema kwa ukali uliomshangaza Victor, "kwa hiyo mpaka sasa hunipendi?" aliuliza "nilipobeba mimba yako ndiyo siku pekee ambayo nilikuweka moyoni na nilipobeba mimba hali ya kumsamehe Rose ilianza kupotea, ila kwa Sasa Sina uhakika kama nakupenda au laa" kwenye kitabu kitakatifu kinasema kipimo upimacho ndicho utakachopimiwa basi neno hilo liliwakuta wanandoa hao kwamba awali Victor alionesha kutokunipenda saivi imebadilika na kuwa mimi simpendi yeye. Victor alikaa kimya kwa muda, "unahitaji kulipiza kisasi?" Victor alinihoji baada ya mimi kubaki na msisitizo kuwa Lazima nilione chozi La Rose lenye Majuto ndani yake, nilikiri kuhitaji kufanya vile. "Mary nakupenda sana mke wangu" Victor alisema hayo, "unajua wewe ni mwanamke pekee ambae kwa ghafla ulinifanya nijiamini kuwa niko mwenyewe sababu tangu nakuoa sijawahi kuona chochote chenye mashaka" Victor alisema hayo huku akinisogelea, "tangu sikuile mchana nilimtoa Rose moyoni na huwezi amini moyo wangu umejaa penzi lako" Victor pamoja na ukali wake niliouzoea, siku iyo alikuwa mpole na mwelewa sana "kiukwel sikulaumu kwanini ulinitoa kwa Rose, labda Mungu kaniepusha jambo" alinibusu kwenye paji La uso kisha aliendelea "ila nalaumu nimempenda na kumpa moyo mwanamke ambae yupo kwangu Ili alipize kisasi" aliposema vile, aliinamisha kichwa chini matone ya machozi yakimtoka "nilikuahidi kukufanya uwe na furaha maisha yako yote," alisema "nimekuruhusu kulipiza kisasi, huenda ukifanikiwa basi nitapata nafasi ya kweli moyoni mwako" nilipo sikia vile nilishangaa sana, "usishtuke mke wangu, nina akili timamu na ninajua niyafanyayo" alinilaza kwenye kifua chake, "ninakuamini na Sina hofu na wewe, unaweza kwenda popote na kufanya lolote kuanzia leo, yani nimekuacha huru ila jua wewe ni mke wangu" aliposema vile nilianza tena kulia kwa sababu sikujua kama Victor ni mstaarabu kiasi kile, "nachokitafuta kwako ni furaha yako, na hata siku ukiamua pia kumtafuta Elibariki nakuruhusu, ndoa siyo kigezo ila kigezo ni ulipo uwe na furaha" aliposema vile nilifurahi sana, nilimkumbatia na kumshukuru "una busara sana mume wangu, naamini utakuwa na furaha siku zijazo" alitabasamu na kunitekenya huku akinilaza chini yeye akawa juu yangu "nakupenda sana mke wangu" alinibusu na kunipa mapenzi yale matamu tena kama ilivo kawaida yetu. Kisha alinirudisha nyumbani
********
Mimi na Victor, tulizidisha mapenzi kwani kila mmoja alikuwa huru kwa mwenzie, Victor alitaka tuishi kama wapenzi, akidai mimi na yeye bado hatujafunga ndoa katika mioyo yetu, "siku ukinipenda ndo tutakuwa tumeoana" maisha yetu yalikuwa mazuri kuliko hata Rose ambae anakila kitu, hapo ndipo nilipoanza kumfurahia Victor.
Siku moja niliamua kumfuata Victor kazini kwake, "Leo nataka tukakae mahali tuongee jambo" nilimweleza huku yeye akiwa na shauku ya kujua nachotaka kumwambia, alifanya kazi zake huku mimi nikiwa ofisini kwake, kila aliyeingia alinikuta "usijali huyu mke wangu, eti ananichunga" wageni walioingia walitambulishwa vile "nyie mnavituko sana Sasa huyu leo kaja kuchunga mali yake" wafanya kazi na marafiki zake Victor walianza kututania, "haya tunaenda wapi sasa" Victor aliuliza na kunwelekeza kuwa tukakae ufukweni mwa ziwa Victoria, alikubali na kuendesha gari hadi ufukweni. Tulianza kuchezea maji huku tukikimbizana, lengo langu ni kumwandaa Victor kusikia nachotaka kumwambia, "Victor mpenzi" niliita huku nikimpapasa kifua,, "Mary mke wangu" aliniita nae, nilianza kumwelezea jinsi navotaka kumwaribia Rose huku nikimuomba amrudie Rose, "eti niniii?" kwa mshangao aliuliza "ndio wewe na Rose nataka mrudiane, Ili Gabriel ajue alafu akijua lazima ataachika" nilipomweleza hayo, kwa jazba alisimama "sitaweza kufanya vile, nyanyuka tuondoke" Victor alikasirika sana akidai namtumia kufanya uhalifu, "Asa unakasirika nini me nimeomba tu kama haiwezekani basi" nilimjibu tukajikuta wote tumezira njian hakuna anaemsemesha mwenzie mpaka tulipofika nyumbani. Victor alichukia sana akiamini nimemdharau "yani mimi niende kujishusha kwa Rose, nianze nae tena mahusiano, looh itakuwa ngumu" alikataa katu katu, nilipoona kakataa nilikaa kimya wala si kumwomba tena,
Palipokucha aliondoka zake kwenda kazini, nikijisikia vibaya nikajuta kumweleza, sikuwa na lakufanya kwani tayari nimekosea, nilikosa raha siku nzima, nikiwaza Victor anaichukuliaje,. Nikiwa kwenye dimbwi La mawazo, ghafla simu yangu iliita, alikuwa ni Victor akitaka tukutane kule tulikokwenda jana. Nilivaa haraka haraka kisha nilienda zangu, nilipofika nilimkuta amekaa mwenyewe. Tulisalimiana kisha nilikaa kumsikiliza. "Mary unauhakika na uliyoniambia niyafanye?" aliniuliza kwa sauti ya kuhitaji uhakika na nikiombacho, "ndiyo ninauhakika" nilijibu "unafanya ivi kwa sababu hunipendi au sababu gani" Victor alidhani nimemwomba sababu nilimwambia sikuolewa na mtu nimpendae "hapana, ni kwa sababu uliahidi kunifanya niwe na furaha, na nimekuomba sababu ulishakuwa mpenzi wake" nilijitetea, "Victor unakumbuka uliniambia kuwa unahisi mtoto wa Rose ni wako? mimi nikakukatalia?" nilimhoji nae akakaa kimya kunisikiliza "Anthony ni mwanao, tena halali kabisa, nilikuficha Ili usiwe na mahusiano yoyote na Rose" nilizidi kumchnganya Victor huku nikiendelea kumshawishi "najua ni vigumu sana kunielewa ila wewe una mtoto kwa Rose" nilimweleza "me shida yangu ni kuvuruga penzi lao, ila Sina maana ya kwamba ukavuruge maisha ya mtoto" Victor alichanganyikiwa maana hakuamini kama kweli Anthony ni mwanae. "mwache akae na Gabriel ambae amemzoea miaka inavosonga utamchukua tu" nilimshawishi nae alishawishika "ujue mchezo unaotaka kuucheza ni mgumu sana" alinisisitiza "utawezaje kufanya mapenzi na mimi wakati nishafanya na Rose" aliposema vile nilitabasamu tu, "mimi ni mkeo, yule ni dili tunafanya, siku nikikuhitaji utasitisha kwake" nilimweleza "nikiwa nachelewa kurudi hautagomba?" alinihoji "mimi ndo nimekuomba ivo usiwe na shaka" Victor alikubali kunisaidia na nilimshukuru sana
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ndipo ikawa mwanzo wa Rose na Victor kurudiana, minutes zote za kumpata Rose nilikuwa namfundisha Victor, tulipanga kuwa tunapiga picha kila atakapoenda na Victor, ila sijui ilikuaje picha zile zilipotea, najua zile picha zingesambaa kila mahali na tungemshusha hadhi sana kiasi cha Gabriel asingeweza kuvumilia,
Msiba wa mama yako ulipotokea, Rose alimweleza yote Victor, hapo ndipo nilipojua kuwa Rose kasababisha kifo cha mama yake, Lakin sikujua walishauriana nini na Victor kwa muda ule kwani, usiku wakati tunalala Victor alinieleza wazi alichomshauri "umekosea Victor, hapo anaeenda kutumia ni Jackline siyo Rose" tulianza kubisha huku Victor akijitetea yeye ndo aliona njia sahihi ya kumchanganya Rose "Ni lazima umpigie simu umweleze asifanye vile" nae Victor alimpigia simu mbele yangu wakawa wanabishana, Victor alimzuia asifanye ila yeye alikazana kuwa atafanya "hata ivo Jackline ameshagundua mambo yetu ivo Lazima nimwangamize mapema Ili achukiwe na Gabriel" hayo yalikuwa maneno ya Rose akimweleza Victor, tulijitahidi sana kuhakikisha haya hayatokei ila Rose alikomalia, ikamlazimu Victor kuniruhusu mimi nije huku kwa ajili ya kukusaidia, ndiyo maana unaona tumekuja wengi wa mjini. Mimi niliwahi Kuja kabla ya Rose na nimeshuhudia yote, ila hakuna aliyenifahamu sababu nilijitenga na watu.
***,,,,, ******
Hiyo ndiyo iliyokuwa historia fupi ya Mary akimwadithi Jackline juu ya mambo niliyomfanyia, Jackline hakuamini kabisa, hakutegemea kama kweli mimi naweza kuwa mnyama kiasi kile "wewe ndo yule ambae hapa kijijini ulisemekana umekunywa sumu Ili kujiua Rose ndo akakusaidia?" Jackline alikuwa mtoto sana kipindi hicho, mimi na Jackline tumepishana miaka karibia nane, hivyo siyo rahisi kukumbuka yaliyopita, ila taratibu alianza kukumbuka, moyo wa Jackline ulijaa simanzi hakuamini kama Ana Dada mnyama kiasi kile, wakati wanaendelea kuongea Victor aliingia mle ndani.......
Wakati bado wanaongea na kuelezana mambo, Victor aliingia mle ndani, kwa macho ya kutahamaki Jackline alijikuta akitahamaki huku amesimama wima kama anaimba wimbo wa taifa, "usishangae Jackline, ndiyo mimi nimeingia Victor" kwa sauti ya kumtoa wasiwasi Jackline, Victor alisema huku akimpa pole za kufiwa na mama yao, Victor hakujua kama Mary amemhadithia Jackline kila kitu, alikaa kwa wasiwasi sababu hakuwa anajua Jackline anamchukulia vipi, "poleni kwa msiba, Rose yuko wapi?" Victor aliendelea kujikanyaga baada ya kumwona Jackline amebaki ameduwaa "Victor, imenilazimu kumweleza ukweli Jackline Ili ajue kinachoendelea" Mary alisema, "sikuona sababu za kumfumba Jackline hasa baada ya tukio hili kutokea" wakati anaendelea kuongea Jackline alimvaa Victor, "wewe ndiye uliyempa ushauri Rose aje kunifanyia haya" alianza ghafla tena kulia huku akimpiga Victor ambae alimsogelea na kumbana kwenye kifua chake ishara ya mkumbatio wa kumpooza "wewe bado mtoto hujui chochote Jackline" Victor alisema hayo huku akimpapasa mgongoni, "sikumpa wazo ila yeye ndo alitoa wazo baada ya kuona amesababisha kifo cha mama yake" Victor alisema hayo huku akijitahidi kumtuliza Jackline aliyekuwa analia baada ya kumwona Victor. "kaa chini tuongee maana yanayoendelea ni makubwa kuliko hata msiba uliokupata" Victor alisema huku akifungua begi alilokuja nalo kisha akatoa magazeti kama manne yenye vichwa vya habari tofauti, Jackline aliyachukua na kuanza kuyasoma yalikuwa yameandikwa vichwa vya habari vilivyo mliza tena Jackline AMTOA KAFARA MAMA YAKO KISHA UTAJIRI, mara MREMBO NA MLIMBWENDE ANAEVUMA NCHI ZA UGHAIBUNI AMFANYA MAMA YAKO MSUKULE KISA AWE MAARUFU kibaya zaidi ni ASUSIWA MSIBA NA DADA YAKO BAADA YA KUGUNDULIKA AMEMTOA KAFARA MAMA YAO, vichwa hivyo vya habari viliambatana na picha za Jackline akiwa kwenye mavazi yake ya mitindo, zingine ni picha za matukio ya siku Ile ya msiba, masikini Jackline alianguka chini kwa mshtuko na kuanza kulia upya "Rose, Rose Dada yangu kipenz ninaempenda kwa moyo wangu wote kwanini unaniadhibu ivi" Jackline akipata tena machungu yaliyokuja kivingine. "nimenyonya titi ulilonyonya wewe, nilikaa tumbo ulilokaa wewe, kwanini leo umenisaliti na kuudhihirishia umma kuwa hunipend" Jackline alitiririsha machozi kama mvua, alitamani afe kama alivyofariki mama yetu, "nitaificha wapi sura yangu mimi, dunia nzima imejua uuwiiiiiiiiiiiiiiiii mamaaaaaa!!!" alihisi kulia taratibu hakumfanyi kupunguza machungu akajikuta akilia kama chizi "angeniacha tu jaman kuliko kuniharibia maisha yangu" Victor alimchukua na kumbembeleza kwani muda huo wote Mary nae alikuwa akilia kwa uchungu sababu alitambua ni kwa kiasi gani Jackline ameumia sababu anayatambua maumivu hayo, "Jackline, jikaze ebu tulia kwanza haya yatapita tu," Victor alisema "ivi ni nani aliyefanikiwa hajapitia matatizo, jifunze kupokea changamoto, jikaze tafadhali" Victor mwanaume aliyeaminika kuwa ni mbaya na mwenye roho mbaya alijitahidi kumtuliza Jackline ambae alijitahidi kutulia japo si kirahisi ivo. Mary na Victor walifanya kazi za ziada zakumtuliza Jackline ambae alitulia. Ndipo Mary aliamua kumjaza sumu Jackline Ili afanikiwe kuniangamiza, "ni lazima umwoneshe Rose kuwa umechukia, kwanza huoni amekudhalilisha" Mary alisema hayo "kubwa zaidi namsikitikia Gabriel sababu laiti angejua mipango aliyonayo Rose juu yake asingeendelea kuwa nae" Victor alidakia, Jackline alimtazama Victor ambae aliendelea kueleza "anampango wa kumuua Ili achukue mali zake, Lakin kabla hajachukua ahakikishe amefanikiwa kupata hati za mali zake" Victor aliposema vile Jackline alishtuka, aliinamisha kichwa chini kama anatafakari jambo. Ghafla aliguna "muda wote sikuwa nawaamini ila kwa hili nikubali" Jackline alijibu baada ya kujua hayo, alikumbuka siku moja alinikuta nakagua sana chumba ambacho Gabriel alikitenga kama ofisin yake akiwa nyumbani, na aliponiuliza sikumjibu kitu ila baadae nilimdokeza kuwa natafuta documents muhimu za Gabriel. "mpango alionao saivi ni kuhakikisha anafunga ndoa na yeye Ili atakapo muua iwe rahisi kwa yeye kumiliki mali" Victor alizid kufichua siri zangu ambazo hakuna anaejua zaidi yake. "pamoja na kwamba lengo letu ni kulipiza kisasi haimaanishi tu nataka na wengine wakati matatizo" Victor alisisitiza "mimi ni mwanaume najua uchungu wa kutafuta pesa, sikuwa tayari kumwangamiza Gabriel" maneno ya Victor yalimfanya Jackline kuduwaa "nilikataa na kumwambia sipo tayari, alipojua sitaki basi mapenzi yakaanza kupungua kwangu na mpaka leo sijajua amefikia wapi sababu sikuiz hanishirikishi mambo yake" aliposema vile Jackline alichoka akili. Ikawa kila mmoja ananishangaa Nina roho ya namna gani, mwanamke ambae Sina fadhila.
*******
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya wiki kama mbili tangu msiba utokee, Jackline alirudi Mwanza, kitendo anashuka kwenye ndege kila mtu aliyeko eneo lile alionekana kumfananisha na mwanadada aliyeandikwa sana kwenye magazeti, alipojua hilo, alivaa miwan yani kisha alijizingushia mtandio mdogo shingoni hatimae alifanikiwa kuficha sura yake kwa staili ile aliyokuwa amevaa. Moyoni alikosa aman na kujiamini mbele za watu sababu alichafuliwa sana na magazeti, hakutaka kufika moja kwa moja nyumbani Bali alienda kwanza kwenye ofisin zangu, alipoingia tu kila mmoja alibaki akimtazama na wengine wakikonyezana, Jackline alishalitambua hilo ivo hakuwajali japo ilikuwa si rahisi kwake kuishi maisha yale, "umekuja kufanya nini kwangu" bila huruma nilianza kugomba huku nikionesha kutokumwitaji, Jackline alisimama tu bila ya kujibu chochote, muda huo huo waandishi wa habari waliwasili Ili kumhoji Jackline ambae alijikuta yuko katikati yao huku mwanga wa picha zikimulika kwa fujo, Jackline alishindwa afanye nini, alinisogelea huku machozi yakimtoka, unajua Kuna namna ya kuelezea hisia ambapo unakuta macho yanatoa machozi ila mdomo unacheza basi hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Jackline kwani, macho yake yalijaa machozi ila alitoa sauti ya kicheko sababu moyo wake ulichoka kulia, matukio hayo yalishuhudiwa na wateja poa waandishi hao, "mama yako na baba yako ndiyo wazazi wangu, unahisi Kuna chochote kinachoweza kuuvunja undugu huu," alisita huku akifuta machozi yaliyojaa machoni mwake, "huyu ni Dada yangu, pamoja na kuwa inasemekana nimemuua mama ila bado hakutaufuta undugu wetu," aligeukia camera na kuionesha sura yake, "manabii na mitume wengi waliuwawa si kwa sababu ya dhambi zao, ila sababu ya dhambi za wengine, sitashangaa leo hii mimi nikifa kwa sababu ya dhambi ya mtu mwingine hasa nimpendae" aliposema vile hadi waandishi walianza kuwa na mashaka na uvumi ule wa awali. Mimi nilijawa na hasira kwani nilijua akiendelea kukaa pale mengi yatafichuka japo kwa Jackline hakuona ajabu sababu alijiamini sana, "ipo siku utautambua umuhimu wangu na utanitafuta" aliposema vile alipita katikati yao na kuondoka zake kuelekea nyumbani. Alipofika nyumbani alishangaa kuona hakuna anaemsemesha hadi wafanyakazi wao. Aliwapuuza na kuingia chumbani kwake kuchukua kila kilicho chake, wakati bado anavipanga Gabriel aliingia nakumkuta, walisalimiana vizur tu kisha Gabriel aliingia chumbani kwake bila kusema lolote. Kilimuuma sana Jackline lakini napo hakujali kitu, alipomaliza alifungasha na kutaka kuondoka "Jackline!" alisikia sauti ya Gabriel, aligeuka na kumtazama bila ya kujibu chochote, "Mungu akulinde huko uendako" Jackline aliposikia vile alitabasamu tu na kuondoka zake, alipofika tu kwenye gari, ghafla machozi yalianza kumtoka, alilia sana kuona hata Gabriel hamuamini,
Siku tatu kupita alinunua magazeti tena, alishtuka kujiona tena AANGUKA MIGUUNI KWAMBA DADA YAKE AKIKIRI KUMUUA MAMA YAO, lingine AIBU KUBWA KWAMBA MWANAMITINDO AMBAE AAMUA UUNGAMA MAOVU YAKE KWA DADA YAKE, alipoyaona alishtuka sana, alijawa na hasira akaona dawa ya moto ni moto, aliingia ndani ya gari na kuliendesha hadi ofisini kwangu...
Jackline alikereka sana na tabia zangu za kujisafisha kwa kutumia njia ya kuwaangamiza wengine, alikuwa nyumbani nayasoma yale magazeti ambayo waandishi wengi walifanya biashara sana kupitia yeye, mitandao ya kijamii picha zake zilizagaa huku na kule wakimtukana sana kwa shutuma za ushirikina, alipoteza marafiki wengi wakaribu kisa habari hizo, kila aendapo, bank, sokoni, supermarket na kwingineko kwenye mkusanyiko hakuacha kutazamwa na kuoneshewa vidole, alikereka sana ila hakuwa na jinsi, lakini kitendo cha mimi kumsingizia kuwa alinifata kuniomba msamaha kilimfanya akose uvumilivu, alijawa na hasira, mwili wote ulinuka hasira, akili haikuwa tayari kujishusha tena kibaya zaidi aliondoa neno dada moyoni mwake akaweka neno adui ndipo alipoingia chumbani kwake na kubeba ufunguo wa gari hatimae aliamua kunifuata ofisini kwangu, Jackline ni binti mdogo sana ila mara nyingi yeye alionekana mkubwa kwa mwili sababu ya urefu wake, alivaa suruali yake nyeusi na blauz nyeusi yenye maua ya rangi mbalimbali, miwani yake, kiatu aina ya Travolta chenye kisigino, na kofia ambayo watu wa Spain na Mexico hupenda kuvaa, kiukwel alipendeza utadhani anaenda Sehemu ya maana kumbe ananifata, alipofika ofisini kwangu aliegesha gari kwa fujo kisha alitoka garini, mwendo wake wa madaha huku akitembea kama Miss na kuacha harufu nzuri ya manukato kila apigapo hatua, watu hawakuacha kumtazama nae alikuwa anatembea utadhani hakuna kitu ndani ya moyo wake, alipoingia tu, mimi nilibetua mdomo kwa dharau, nilikuwa nimekaa na wenzangu tunahabarika na matukio ya jiji kwa kupeana umbea, alipoingia alinitazama bila kuonesha sura yoyote ya hasira, wenzangu walipomuoa walibaki kutazamana huku wakimcheka, hapo ndipo walipokosea, Jackline akaanza kupiga hatua moja baada ya nyingine huku akivua miwani wake aliyoiweka kwenye koti, hakuna aliyejua anachokifanya tukabaki kumtazama, muogope mtu anaefanya jambo bila kukupa taarifa kwani aliponikaribia alinivuta na kunisogeza karibu yake, "heee huyu vipi kwani" shogaangu mmoja alijidai kuropoka kabla hajamalizia alishtuka kibao kikitua kwenye uso wake "don't dare me! (usinijaribu)" ni maneno machache aliyomweleza kisha alinigeukia mimi, hakuwa anaongea chochote zaidi alifungua mkanda uliopo kiunoni kwake, aliuchomoa na kuunyanyua juu, sikuamini kama mvua ya mikanda ikinishukia, kutokana na hasira ambazo alikuwa nazo hakuna aliyeweza kumsogelea, nilipojitahidi kujinasua ndo niliendelea kupokea kichapo cha maana, "pumbavu kama mama yako hakukufunza utu ngoja me nikufundishe" Jackline aliongea utadhani mtu mzima mwenye miaka mingi yakunifunza adabu kumbe ni katoto kadogo sana kwangu, wenzangu walianza kupiga kelele huku wakihitaji msaada sababu hakuna aliyeweza kumtoa Jackline kwenye mwili wangu, alinichapa sana mikanda kiasi cha kukosa hadi nguvu za kujihami zaidi nilifanikiwa kumvuta blauzi yake iliyoachia kifua chake kikabaki wazi sababu vifungo vilitoka. Alikuja mlinzi wangu ambae nae hakuweza kuniokoa kwani Jackline alibadilika na kuwa zaidi ya nyati aliyeona adui, ndipo polisi walipoingilia Kati na kumtoa Jackline kweny mwili wangu japo haikuwa kazi rahisi. Kwa kuwa Jackline hakumaliza hasira zake alijikuta akilia kwa hasira kiasi cha hadi kujikunja huku akiuma meno yake mikono ikiwa imekakaa hakuna aliyeweza kumshika ndipo polisi mmoja alimpiga maeneo ya shingoni kwa lengo ya kuushtua mshipa wa fahamu Ili apoteze fahamu ndipo ikawa pona yake.
Mimi nliivimba na kuumuka mwili wangu kama andazi lililozidishiwa amira, nilienda polisi nikapewa PF3 kisha nilienda hospital, habari zikaanza kurindima jiji zima hatimae nchi nzima hadi nchi jirani kuwa MWANAMITINDO JACKLINE AMTWANGA DADA YAKO HADHARANI, mitandao ya kijamii ilipata picha nzima ya matukio kwani Kuna waliokuwa wanarekodi, habari, television na magazeti ndo ikawa habari ya mjini, kila mahali gumzo ila wengi waliamini Jackline ndo mbaya kuwa ananionea, wengine walienda mbali zaidi kwa kusema labda kafara aliyoifanya Jackline imemfanya awe chizi, yani kila mmoja alimsema Jackline ajuavo ndipo na mimi nilipoamua kumfungulia kesi Jackline ambae hata mshipa wa hofu hakuwa nao,
Alipozinduka kutoka usingizin alijikuta yuko ndani ya pingu mahabusu, kutokana na hasira alizozionesha aliwekwa chumba chake mwenyewe wakihofia asije kufanya fujo tena, mara nyingi alizoea kulia lakini tangu siku hiyo alijawa na ujasiri tena alijiamini kuliko hata neno lenyewe kwa lugha ya wenzetu inaitwa confidence, alipelekwa mahakamani na kusomewa shitaka japo. Wengi waliamini angekana au kujitetea lakini alipohojiwa alitoa majibu yaliyomchosha hakimu "sikupigana nae, kukumpiga ngumi, sijatumia silaha hatarishi ila nilimchapa kwa mkanda" siku hiyo ya hukumu kila mmoja alihudhuria Gabriel, Victor, hadi Mary na wengine wengi, alipoulizwa kwanini amemchapa alishangaza umati "mimi naitwa Jackline Macha, je yeye anaitwa nani?" alihoji "anaitwa Rose Macha" alijibiwa "Sasa ndugu akimwadhibu ndugu yake kuna tatizo?" alisema "alinikosea adabu nikamwadhibu narudia sijampiga ila nimemwadhibu" Jackline alijawa na ujasiri uliwafanya watu waliokuwa upande wangu hasa mwana sheria wangu kuishiwa maneno, "mimi nashangaa matatizo ya familia yawezekanaje kuwa hadharani, mimi ni mdogo wake, alienda kinyume na msingi ya utu na nidhamu nikaona nimchape kama mtoto huenda akajitambua, kumbe bado" aliguna na kunitazama "hii inaonesha dhahira bado hajasikia na anahitaji nimuadhibu tena, kwa kuwa ni ndugu yangu nitamwadhibu tena" nilihisi kimfuata hakimu pale na kumwambia amfungue hata kifo, nilipohojiwa mimi nliionekana kuto kukidhi maelezo sababu maswali ya mitego yalinifanya nibaki namumunya maneno "nasikia hukwenda kumzika mama yako na tangu siku hiyo umekuwa ukimsakama sana mdogo wako, huoni hiyo ni sababu ya yeye kukuadhibu" swali lile nilishindwa kujibu ukimya wangu ulimfanya hakimu kuandika jambo ambalo sikulijua, "mbona nasikia habari kuwa kipindi ndugu yako yuko Arusha kwa mama wewe ulikataa kwenda na ulimjibu vibaya sana Jackline, huoni hiyo nayo ni sababu ya yeye kukuadhibu" nilipo sikia vile nilidakia "hayo hayajatuleta hapa hayo ni ya kwetu binafsi" bora nisingesema vile maana niliwapa sababu za kuniuliza tena "kama ni yenu binafsi mbona hata hili usingelifanya kuwa binafsi ukaweka hadharani kwetu" alinihoji nikabaki kimya. Kiukwel katika siku niliyojichanganya ilikuwa siku hiyo. Baada ya maelezo kukamilika hakimu alitoa huko, "Rose ningekuwa sijavaa hili joho jeusi ningeongea jambo ila ebu uwe makini maana nahisi Jackline kukuadhibu hujakosea japo sheria ni msumeno, nadhani ningekuwa mimi Jackline ningekuadhibu zaidi ya hapo" hakimu ambae hanijui wala simjui aliweza kuusoma moyo wangu na kubaini jambo japo hakuweka hadharani, "ivi msiba unaweza kutokea wa mama usiende, nadhani ni sahihi kabisa Jackline alichokifanya" japo kuwa hakimu hakuwa anajua mambo yetu alisema vile nahisi alisema kutokana na Yale Jackline aliyoyaongea, Jackline alihukumiwa kifungo cha miezi sita, kwa kufanya fujo hadharani au kulipa faini ya sh. Million moja pia anitibu hadi nipone.
*****
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Asikwambie mtu habari zetu zilizagaa sana, mimi na Rose ndiyo ikawa mwanzo wa uadui, Jackline kama kawaida yake haachi msemo yake, aliniambia tena " labda nifungwe ila kama niko uraiani Lazima utachezea kichapo popote nitakaposikia umenitaja"
Gabriel alishindwa nae afanye nini, hakujua akae upande wa nani sababu ghafla hakutuamini wote, hakuniamini wala Jackline, alianza kuwa mtu asiyeeleweka huku muda mwingi akiniuliza uliza maswali yahusuyo kifo cha mama, wakati huo mimi ndo kabisa Sina muda nae, kila mmoja alianza kuishi maisha yake binafsi japo tunaishi wote, mapenzi Kati yetu yaliisha, wakati mwingine narudi usiku wa manane, wakati mwingine sirudi kabisa, tukatengana vyumba, kila akiniuliza sababu za kufanya vile nilikuwa nikimtukana sana mwishowe nae alizoea, Gabriel alianza kuishi maisha yenye msongo wa mawazo, sura yake ya utanashati ilipotea, wakati mwingine alikuwa akiduwaa na muda mwingine alikuwa akiongea mwenyewe. Alianza kupata adhabu ya penzi langu ambalo lilimchanganya nakumfedhehesha sana. Alianza nae yeye kuchelewa kurudi nyumbani, ghafla nae akaanza kutumia pombe kama zana ya kujiliwaza. Hakuwa tayari kuniacha wala kunifukuza sababu alinipenda kwa dhati kabisa. Aliamua kunivumilia akiamini ipo siku nitarudi kama zamani.
Mwaka Sasa tangu hekaheka zile na Jackline zitokee, sikuwahi kumwona tena Jackline na sikuwa nahitaji kujua habari zake sababu tangu siku ya hukumu mimi na yeye tuliufuta undugu, Gabriel ndo kabisa akawa chapombe kiasi kwamba hatamaniki, hatua Ile ilinifurahisha kwani ndiyo ingekuwa nafasi pekee ya mimi kumfilisi mali zake, hasa hoteli yake ya kitalii anayoimiliki Arusha inayomwingizia pesa nyingi sana, nilipata kiburi hicho sababu hata akifa hakuna atakaejitokeza kuwa ni ndugu sababu Hana ndugu yoyote na popote sababu alizaliwa mwenyewe, na alishawahi kuniambia Hana ndugu popote pale, Nilimfata Victor na kumweleza yote Yale, Victor aliposikia alitabasamu tu, "mpenzi yani hii itakuwa fursa yetu ya kugawana mali za huyu mshenzi ambae simpendi hata kidogo" Nilisema hayo huku Victor akiguna "mali zote ulizo nazo hazikutoshi?" akiniuliza, "Bwana eeh, hata Bill Gate anapesa lakini bado anazitafuta kama hutaki Sema nisikueleze tena" kwa ukali Nilisema hayo huku nikijilaza kitandani Ili Victor anipe utamu kama kawaida, nae bila hiyana alinipa tena kwa ufundi zaidi
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment