Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

ADHABU YA PENZI LAKO - 2

 





    Simulizi : Adhabu Ya Penzi Lako

    Sehemu Ya Pili (2)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ni mwaka Sasa tangu nianze maisha mapya na Gabriel kama mchumba wangu, pia maisha bila ya mdogo wangu Jackline. Mapenzi ya Gabriel yalinifanya nijihisi kama sitakufa wala yeye hatokufa, upendo wake ulizidi hata thaman ya neno lenyewe nahisi ulikuwa kama ule upendo wa kwenye bibilia ule wanaoita wa agape, upendo usioleta malumbano, kisasi wala kudharauliana,. Tulisikilizana na kuheshimiana sana. Nachoamini ni kuwa jinsi tulivopendana kulisababisha hata Mungu kufungua milango ya baraka na neema. Biashara yangu ilianza kujulikana, wateja nao ndo walizidi kuongezeka. Sikuweza kutarajia kama salon yangu ingekuwa miongoni mwa salon zinazotumiwa na watu wenye pesa yani wake wa matajiri walifanya kama Ile ndo salon yao, kiukwel biashara yangu iliendelea vizuri sababu kupitia biashara hiyo niliongeza chuo cha kufundisha mambo ya urembo na nywele, chuo hicho ndo kilinipa umaarufu kwani walimu wake walitokea Italy ambapo Jackline ndo alinitafutia, kikubwa ni miongoni mwa vyuo vilivyokuwa na hadhi ya kimataifa ilikuwa chuo changu , wanafunzi kutoka nchi jirani walikuja chuo changu, nilinunua magari matatu ya kutembelea na magari manne daladala ya kufanyia biashara. Maisha yetu yalibadilika kwa hali ya juu, kumbuka hayo yote ni kutoka katika biashara yangu mimi kama mimi, bado magari ya Gabriel na mitaji yake mbalimbali japo mitaji yake mingi nilikuwa siifahamu, Gabriel hakuwa na mabiashara mjini zaidi nachojua alikuwa na kampuni yake iliyohusika na mambo mengi. Maisha yangu yaliuaga umasikini kwa asilimia kubwa sana.

    Mapenzi yangu na Gabriel yalisababisha sisi kuwa mfano kwenye maisha ya watu, wengi walitaman kuwa kama sisi. Tukienda kwenye sherehe ama tafrija yoyote tulioalikwa macho yote kwetu, tulipendezea kuanzia kutembea, mavazi na hata mikao yetu ilidhihirisha tunapendana.

    Baada ya miaka mitatu kupika Jackline alishindwa kurudi Tanzania sababu pamoja na kuwa chuoni, alipata nafasi ya kuajiriwa kwenye makampuni ya Waitaliano, walimngangania sababu ya ufanyaji wake kazi kuwa mzuri, nae alikataa kurudi Tanzania akidai anajipanga kimaisha Ili asipate shida akirudi Tanzania, hatukutaka kupingana nae sababu yalikuwa maisha yake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwanangu Anthony nae alianza shule, tulimpeleka shule tuliyohisi inamfaa kwa umri wake pia yenye u bora wa elimu. Sikuwahi kushuhudia mtoto ambae hawana undugu na mtu wakafanana, basi hii ilitokea kwa Anthony na Gabriel, kwanza Anthony alimpenda sana Gabriel na kwa Gabriel ndo kabisa husemi chochote, Anthony alifanana na Gabriel vitu baadhi, miguu na macho pia cha ajabu zaidi Anthony alikuwa na kaalama cheusi karibu na mdomo wake hivyo hivyo alivyo Gabriel. Ukifatilia tabia za Gabriel ndizo za Anthony, mwanangu hakuwa mwepesi wa kukasirika Iwapo atabaini kaonewa, mara nying hupenda kukaa Sehemu za ukimya, ni mpole sana na si mkorofi, pamoja na udogo wake huo wa miaka minne matendo yake yalikuwa ya mtu mzima. Nadhan kufanana kwao huko ndiko kulipelekea watu hao kupendana. Kila ifikapo mwisho wa wiki, Gabriel humchukua mwanae na kwenda Sehemu za michezo Ili Anthony akutane na watoto wenzie. Gabriel alijitahidi sana kumfundisha kujiamini, kujikubali na tabia nzur Anthony akiamini huo ndo msingi mzuri. Gabriel alipenda kumfundisha kuchezea gitaa Anthony tangu akiwa mdogo, sikuwa najua kwa nini alipenda kumfundisha pia sikujali sana. Mwanangu alikuwa kwa malezi ambayo nilihisi Victor pamoja na kwamba ni mwanae asingeweza kumlea vile. Nilijihisi fahari sana

    "mume wangu natakiwa niende Dubai mzigo umeisha Yan ungekuwa huna majukumu tungeenda wote" Nilideka kwa huba tukiwa kitandani, "mhh ivi lini wewe utajitegemea maana kila kitu mpaka mimi." Gabriel alisema huku akiyafinya mashavu yangu kwa mapenzi "basi nenda alaf nikipunguza kazi nitakufata, Sawa mke wangu," loo mwanamke mimi nilikuwa na bahati sana. Nilimsogelea na kumbusu kisha tulipeana mapenzi moto moto kama kawaida yetu.

    Baada ya siku kadhaa nilisafiri kwenda Dubai, sikuwa na hofu na familia yangu sababu najua iko salama. Siyo mara moja wala mbili kufika Dubai na nchi nyingine jirani. Huwa nikisafiri mara kwa mara na napajua vizuri tu huko Dubai.

    Siku moja katika pita pita zangu nilikutana na mtu ambae sikuamini kama ningeweza kuonana nae mle, sura yangu Ilibadilika na kujawa na jazba pamoja na hasira, Nilijua hajaniona ivyo niligeuka haraka haraka na kutaka kuondoka ghafla nilisikia "Rose, Rose" moyo ulienda mbio, sikutaka kugeuka zaidi nilizidisha mwendo na kuingia ndani ya taxi Ili niondoke, Ile nafunga mlango wa gari, Victor aliniwahi na kuzuia nisifunge ule mlango hatimae nae aliingia mle ndani ya tax, sikuwa na La kufanya zaidi nilikaa kimya. Victor alitoa mwongozo kwa dereva atupeleke hotelini. "kufanya nini ebu niache me niendelee na mambo yangu" kwa ukali nilisema ila Victor alisisitiza nae dereva alifanya alivo ambiwa



    Nikiwa kwenye Ile taxi nilijiona kama niko jehanamu, moyo wangu ulizidi kwenda mbio kama nakimbilia riadha, sikutaka kabisa kumtazama Victor ambae alikuwa akiniuliza uliza maswali yaliyozidisha hofu ndani yangu, kiukwel kuwa karibu ya Victor kwangu ilikuwa Sawa na kuwa karibu na shetani tena mwenye sura mbaya na ya kutisha. Kila mara nilizidi kutazama nje ya gari sitaki hata kumwona usoni. Niliubeba mdomo kama vile mtoto aliyedokoa nyama Sasa hataki kuongea Ili asikamatwe. Tulifika hotelini hapo, Victor alinifungulia mlango Ili nishuke garini, kwa dharau nilishuka na kusimama bila ya kufanya chochote, "Twende ndani basi mbona umesimama tu" Victor alihoji huku akiwa amenishika mkono wangu. "unanipeleka wapi umesikia nina shida ya kukaa na wewe" kwa ukali nilisema ila Victor alitabasamu tu hatimae alinivuta mkono wangu na kuniingiza hotelini. Tulipokaa, Victor alisimama na kuelekea kuongea na mhudumu, "Rose, utanichukia mpaka lini?" Victor alisema, alijidai kama hakuwahi kusababisha majeraha makubwa moyoni mwangu kabla sijajibu mhudumu alisogelea meza yetu. Alileta juice yenye rangi kama nyekundu ivi mbili, sikujali wala si kuhoji, nilisogeza mrija mdomoni na kunywa juice ile, "Victor naomba unikome tena usije ukajaribu kunisogelea maana mimi na wewe haitokaa ikatokea kurudiana" Nilisema kwa kiburi na dharau huku nikivuta tena Ile juice, "Rose kiukwel bado nakupenda tangu yote Yale yatokee Sina amani kabisa naomba unisamehe" aliposema tu hayo nilisimama kwa haraka Ili niondoke zake kwani maneno anayoongea hayana tena nafasi kwangu kwa dharau nilisunya na kuondoka zangu, wakati napiga hatua moja, mbili, tatu ya nne nilihisi kajasho kembamba kanatoka huku nguvu zikiniishia, "Rose tatizo nini" nilisikia sauti ya Victor ambapo sikujizuia niliangukia kifua chake nae alinishikilia kisha tuliingia kwenye taxi hali sijitambui.

    Nadhani nilipoteza fahamu kwa muda wa masaa kama mawili, Nilizinduka nikajikuta niko kitandani nimevaa taulo tu, pembeni alikuwa Victor ananitazama na kunipapasa uso na nywele zangu. Nilinyanyuka pale kitandani nimeshikilia taulo. "unafanya nini hapa, kwanza niko wapi" kwa ukali nilihoji "badala ushukuru nimekusaidia, we unagomba" Victor alijibu, nilimtazama kwa hasira, niliwaza kama dakika ivi kisha nilimsogelea "wakat unaongea na mhudumu ulimwambia nini" nilihoji "nataka kujua kinywaji changu kilikuwa na nini" ilinilazimu kuhoji sababu sikuwa mgonjwa iweje niishiwe nguvu ghafla. "usiponiambia nitaenda kumuuliza na ujue nitajua" kwa ukali nilisema huku natafuta nguo zangu "zilichafuka nikaagiza zifuliwe" Daaa majibu ya Victor yalinichosha "hata ivo unaenda wapi usiku huu wa saa mbili" Victor alisema, nilitazama diridhani nikabaini kuna giza kwamba ni kweli usiku. Nilijawa na hasira, kulikuwa na kitabu karibu yangu basi nilimpiga nacho kwa hasira tu sababu sikuwa na jinsi. "simu yangu iko wapi niagize mtu aniletee nguo mimi niondoke?" niliuliza huku natafuta "sijui iko wapi sababu sijaiona" Duuuu sikuamini kile nilichokiona, ila Victor hakuwa na wasiwasi wala hakutaka kunisaidia kwa lolote zaidi alijilaza kitandani akichezea simu yake. Sikuwa na jinsi yoyote Ile, nilijua wazi leo Lazima nitakuwa na Victor usiku ule. Nikiwa katika vazi La taulo, nilijisogeza diridhani na kutazama hali ya jiji La Dubai, sikutaka hata kuongea na Victor, muda mfupi Victor alinyanyuka pale na kuwasha redio iliyoko mle ndani, wimbo ule ulikuwa wa taratibu na wenye ladha ya

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kimahaba, sikumjali wala kumtazama. Nilishtukia amenisogelea na kunishika kiuno "wewe ni mpenzi wangu, bado unaishi moyon" sauti ya kunibembeleza ilipenya masikini mwangu. Nilicheka kwa dharau sana "huna hadhi ya kuwa na mimi, Gabriel ndiye mume wangu na nampenda sana" Nilimwonesha Pete kisha niliendelea kutazama nje, "Rose yaliyopita tuyaache bado unaishi moyoni mwangu" Victor alisema tena "heeyy stop!! Usinishike kamshike Mary" nilimsukuma mbali ila hakujali, alinisogelea na kunitazama machoni bila kutarajia alishika taulo na kulivuta nikabaki mtupu Sina nguo hata moja "Victor unafanya nini, naomba uniache" Nilisema "wakati umelala nilikukagua sana, ningetaka ningekufanya lolote ila sikutaka" Victor aliniambia huku macho yakiwa kwenye kifua changu, Victor si mgeni kwangu huwa najua anapenda sana kutazama na kushika maziwa yangu. "nitawezaje kukuacha wakati najua una damu yangu, pia sipo tayar kukuacha kirahisi wewe utabaki kuwa wangu" kitendo anasema vile nilimpiga kibao ambacho kutokana na nguvu zangu basi niliamini kilikuwa kibao cha nguvu "umesahau uliyonitendea mbele ya Mary, sikuhitaji Victor" Nilisema huku Machozi ya hasira yakinitirika. Ghafla Victor alinisogelea na kunitupa kitandani nikiwa vile vile mtupu,. Nae alikuja juu yangu na kunipapasa. Masikini mimi sikutegemea kama ningeweza kumsaliti Gabriel, mwanaume aliyenitoa kwenye huzuni na mateso. Nilijikuta nikipokea ule mpapaso hatimae niliruhusu Victor amege tunda ambalo kila wakati nilikuwa nikimwahidi Gabriel kuwa hakuna atakae limega. Nilijisahau kabisa kama mimi ni mchumba wa Gabriel. Nilijikuta nikigawa uroda utadhani nina muda wa miaka sijapata uroda ule kumbe hata wiki haijaisha tangu niupate kwa Gabriel. Victor alinipa mapenzi ambayo sikutegemea kabisa kama angenipa, Yale mapenzi yalinifanya nikumbuke mapenzi yetu ya Zaman. Baada ya yote tulikubaliana kama tutafanya iwe siri Mary wala Gabriel asijue. "mimi najua tunapendana saiv sitakuacha tena" Victor alisema na me nilitabasamu. "nguo zako nilificha tu pia simu" Victor alisema na me nikaona kawaida tu.

    Palipokucha niliamka Ili nijiandae kwenda hotel niliyokuwa naishi, tuliongozana na Victor hadi hotelini, "twende ukaone chumba nachoishi" nilimwambia Victor "hapana si umesikia saiv naongea na mtu anadai nimuwahi nitakuja jioni" Victor alinibusu shavuni na kuondoka. Nilipofika mapokezi niliomba kadi ya kufungulia mlango "mlango upo wazi wewe nenda tu" majibu Yale yalinishangaza sababu si kawaida "usiogope Dada wewe nenda tu" . Niliguna tu kisha nilielekea chumbani, "suprizzzzzz" Nilisikia hayo huku mtu akiwa tayari mlango, Alikuwa Gabriel, nilishtuka sana, niliogopa pia sikutegemea "mke wangu kipenz mambo mhh nimeshindwa kukaa mwenyewe nyumbani pia niliikuahidi nikipunguza kazi nitakuja" Nguvu ziliniishia badala ya kutabasamu nikajikuta nashangaa "mbona tangu Jana umezima simu" Mungu wangu ndo nilichoka kabisa kusikia alikuwa tangu Jana. "Sasa nitajibu nini" nilijiwazia, "mbona upo kimya mke wangu Kuna tatizo" aliniuliza hali mimi nimebanwa na kigugumizi. "aah... Mume wangu yani nimeshtuka sababu sikutegemea kama ungekuja me nilijua unanitania" Nilijitetea huku nikimkumbatia "Jana sikurudi sababu nilipochelewa kwenye mizunguko niliona nilale hotel jirani alafu sikuwahi na chaji." Gabriel aliyaamini maneno yangu sababu ananiamini. Alinivuta na kuanza kunipapasa Ili nimpe utamu. Sikuamini kama usiku nilimpa Victor alafu asubiri Gabriel "ningejua nisingekuwa na Victor" nilijisemea. Kiukwel nilikuwa nimechoka sana ila sikuwa na namna zaidi ya kumpa. Nilivuta hisia Ili tu nimridhishe pia asinishtukie. "Rose unajua nakupenda sana, siwezi ishi bila ya penzi lako mke wangu" asikwambie mtu Yale maneno yalinisuta sana, roho iliuma sana, aibu machoni pia fedheha hata kujibu ila nilitabasamu "hata mimi nakupenda mume wangu kisha nilikaa kimya" Rose una tatizo? Siyo kawaida yako kuwa mpole ivi" nilijitahidi kuchangamka ila sikuweza sababu ya nafsi kunisuta "kichwa mume wangu kinauma labda nipumzike kwanza". Nilisema kisha nikajilaza ghafla Victor alipiga simu nikiwa na Gabriel.



    Simu yangu Iliita na nilipo tazama alikuwa Victor, nilishtuka hali moyo wangu ukienda kasi, niliwaza nitaongea nae vipi, "heee afadhali sana huyu Kaka amepiga" Nilipoteza lengo Gabriel asielewe. "Habari nilikuwa nasubiri sana simu yako kujua kama umepata Ile mizigo au laah maana hapa nipo na mume wangu ndo tunataka Kuja huko" Nilitoa maelezo mengi nikiamini Lazima Victor atanielewa, nae alinijibu "ahaaa kama umepata mengine basi nisubiri hapo hapo nakuja dakika hizi usiondoke" bila aibu nilimfanya Gabriel kama mtoto. Victor alikuwa yuko hotelini amekuja kama alivoniahidi ila kwa kuwa Gabriel alikuwepo niliona bora nimfuate mimi. "mume wangu Kuna mizigo naenda kuitazama, nipe kama nusu saa narudi" nilimpa taarifa huku nikivaa nguo kwa haraka. "hata ivo nimechoka sana we nenda utanikuta tu mke wangu" Gabriel aliniambia hayo huku akinibusu shingoni kama ilivo kawaida yake. "Rose unajua nakupenda sana yani wewe ni furaha yangu, nikikuwaza huwa najisikia kama nina bahati sana" Gabriel alinieleza hayo kwa huba alinikumbatia, nilitabasam ila moyon nilijiona kama Kuna misumari inanichoma na kunikata kata, maumivu yalinijia nikajuta kwa nini nilimsaliti. Nilijisogeza kifuani kwake na kujilaza "nakupenda pia mume wangu wewe ni furaha yangu pia" wakati tunapeana maneno matamu simu Iliita "ebu nenda asije kukasirika mke wangu" laiti angejua ninapokwenda asingeniharakisha. Nilivaa kisha niliondoka zangu moyo ukinisuta, niliufunga mlango na kuondoka kumfata Victor aliyekuwa yuko kwenye taxi. Sura yangu ilikunjamana kiasi cha kumshtua Victor. "mpenzi, mbona mnyonge Kuna nini?" Victor aliniuliza hali mimi nikiwa bado natafakari maneno ya Gabriel. Tukiwa bado garini nilianza kumweleza Victor "naomba haya mahusiano yaishe" kwa ukali Nilisema "Gabriel hana kosa najisikia vibaya kumsaliti" Nilizidi kuongea "kwanza ulinitesa Gabriel ndo amenisaidia sikutaki mimi" maneno yangu yalionekana kutokuwa na mashiko "ebu nitazame kwanza, Gabriel kwel amekusaidia ila najua mimi unanipenda" Victor aliniambia "ebu nitazame uniambie unampenda Nani?" kwa ujasiri Victor alinieleza "kwanza mimi Nina mtoto na wewe huoni siyo rahisi kuachana" Victor alijitahidi kunishawishi nisahau lengo La kumwacha. "nakupenda mama ebu sogea kwanza unibusu" nilitabasam na kumbusu, hali ya hofu na msuto moyon Kuhusu Gabriel ghafla ulitoweka. Tulielekea hotelini kwa Victor nikiwa huru tena simkumbuki kabisa Gabriel.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tuliingia chumbani bila kupoteza muda Victor alianza kunichezea "ivi kwel Gabriel ndo huwa anafaidi utamu wangu huu" aliniambia huku mikono yake ikipenya kila mahali. Nilimsahau kabisa Gabriel kwa mahaba niliyokuwa nayapata kwa mpenzi wangu kizungu tunasema to my ex. Nilichizika na penzi hilo ambalo nililimiss haswa. Nilibaini utofauti Kati ya Gabriel na Victor katika mapenzi. Looh penzi La Victor lilikuwa tamu haswa. Nilijisahau kabisa kama Gabriel yupo Dubai tena yupo ananisuburi na alinifata mimi. "bebi kesho mimi ndo naondoka ivo tutakutana Tanzania" Victor alisema hayo wakati mimi nachezea kidevu chake na kidole changu "niahid tukirudi hautakuwa unanikwepa maana sitaki kukupoteza tena" aliendelea kunifanya nizidi kuvutiwa nae "nitakupenda zaidi Sawa ee" alinibusu shingoni na mimi nilideka kwa huba kwake "usijali sitakukwepa ila tujitahidi iwe siri sitaki Gabriel ajue" nilitoa ilani kwake nae alikubali . Niliamka pale kitandani "heeee unajua saiv saa kumi na moja alaf Gabriel amenitafuta sana" kwa sauti ya tahamaki Nilisema, muda huo huo nilimpigia simu Gabriel "mume wangu samahan sikusikia mlio wa simu, vipi upo wapi, usiniambie mara hii tu ushanimiss" Nilisema huku nikionesha ishara za kejeli usoni nae Victor akicheka jinsi ninavomdhihaki Gabriel "ulijuaje nimekumiss mke wangu" Gabriel wa watu hakuwa na wasiwasi na mimi yani tunasema Hana complain. "niko njiani nakuja kipenzi changu" nilimjibu kisha nilikaa simu "Sasa acha mimi nijiandae niondoke" Niliingia bafuni nikaoga hatimae nilidondoka

    Mambo yote niliyoyafanya Dubai, Gabriel hakujua wala kuhisi chochote, tulimaliza mizunguko yetu na kurudi Tanzania.

    Mapenzi yangu yalianza kukosa nguvu sababu tayari nimeyagawa, asilimia kadhaa kwa wote wawili Gabriel na Victor. Nililazimika wote kuwatendea haki, kwa Gabriel ilikuwa sababu ni mume wangu na kwa Victor sababu alisharudiana na mimi. Nilianza kutumikia mapenzi ya wanaume wawili ambao wote niliamini wananafasi kwangu. "mke wangu una tatizo lolote" kila mara Gabriel aliniuliza kutokana na mabadiliko ya ghafla niliyoanza kuyafanya. Nilijitahidi sana kutokubadilika ila Kuna wakati nilishindwa. Nilipunguza simu za mara kwa mara kwa Gabriel. Zawadi za mara kwa mara nilisitisha. Majibu ya mkato yalianza kujitokeza mdomoni mwangu. Kibaya zaidi nianza kuchelewa kurudi nyumbani na nikirudi naelekea kitandani moja kwa moja, Ile desturi ya kumkagua Anthony mambo ya shule iliisha, kukaa na wafanya kazi wanielezee shida zao sikuwa nayo tena. Kumsubiria Gabriel na kumpokea Ili anipe Zawadi na kuongea nae changamoto za maisha nilisitisha kabisa. Mambo hayo yalimchanganya sana Gabriel kila wakati alinihoji "Sina tatizo lolote niko sawa" nilimjibu kwa mkato huku nikichana nywele zangu asubuhi Ili niende kazini "mimi ni mumeo napaswa kujua mambo yanayokusumbua" Gabriel alinisogelea na kuniambia "heeeeeee kama Sina tatizo nifanye nini niseme nini Sasa, nimesema niko sawa" nilimjibu kwa ukali kisha nilinyanyua mkoba wangu na kuondoka zangu hali Gabriel amebaki ameduwaa. "mamy kesho wazazi wanatakiwa shule nilikusubiri Jana nikupe barua ila niliwahi kulala" Anthony aliniambia "kamwambie baba yako mimi sitapata muda" kwa ukali napo nilimjibu Anthony aliyeenda kwa Gabriel huku analia "mama amekataa kwenda shule alafu amenigombeza" Anthony alilia kwa uchungu sababu hakuwai kugombezwa na mimi "mama yako anaumwa kichwa ndo maana ila hajakugombeza mwanangu" Gabriel alimkumbatia na kumwahidi ataenda yeye.

    Victor alizidisha mapenzi kwangu kiasi cha kuisahau familia yangu. Sikuwa tena na hofu wala sikujali hata kama Gabriel atajua. Kila nikitoka kazini Lazima nikutane hotelin na Victor, tunafanya yetu mpaka mida ya saa tatu ivi ndo narudi nyumbani. Sikumoja niliwahi kutoka kazini na kuelekea kwa Victor. Tulipoonana tulikaa bar na kuanza kunywa "Gabriel hapendi mimi ninywe ivo acha tu me nitumie kinywaji laini" nilijitetea "utamwaogopa huyo mumeo mpaka lini kwani yeye ndo anakunywa au wewe" Victor alisema na mimi nilikubaliana nae na kuagiza bia. Nilikunywa sana huku tukipapasana hadharani na kupeana mabusu. Rafiki zake Victor ambao wengine nawajua tangu zaman nao walikuja. "kwel mnapendana alafu mnapendana" sifa kemkem zilimwagwa na mashemeji. Muda nao uliendelea kukimbia utadhani Kuna mtu anaukimbiza. Ilipowadia saa tatu nilitaka kuondoka kwenda nyumbani, "jaman mbona mimi simwogopi Mary ebu kaa bana tuendelee" Victor alianza kunishawishi ila nilikataa "naona hapa ananipigia labda Kuna tatizo" Lakin bado Victor alizidi kunizuia. Kitendo tunaendelea kubishana Mary alifika pale "eheee nataka kujua unafanya nini na Victor hapa" Mary kwa ukali aliuliza. Looh usiombe kufumaniwa na mume wa mtu. Moyo ulishtuka ajabu. Mary aliwaka kama Hana akili nzuri alinivamia na kunipiga, nadhani alimalizia hasira za kichapo kile cha Jackline. Daaa Mary alinipa kipigo kitakatifu, Victor aliingilia kati na kumkamata Mary "pumbavu izo tabia umeanza lini, nitakuharibu sura sasaiv nadhan unanijua" Victor aligomba ila Mary alizidi kuwa mkali. Shemeji zetu walimchukua na kumpeleka Mary nyumbani nikabaki na Victor aliyeniomba sana msamaha "nitaendaje nyumbani sasa ukiangalia huu ni usiku." Victor aliwaza kwa muda kisha akanichukua hadi kwenye gari langu. "najua unapesa utalitengeneza" aliposema hayo alichukua kitu kama rungu na kuliponda ponda gari langu. Kwa muda ule sikutaka kuhoji Kuhusu gari zaidi nilikubaliana nae kwa kila alichokifanya. Muda huo damu ilikuwa ikichuruzika mkononi kwani chupa ilinikata pia usoni shavuni nilikwaruzwa vibaya sana. Victor alinipeleka hospitalini "naomba sana mtusaidie mume wa huyu Dada asijue chochote zaidi ajue alipata ajali" haikuwa kazi rahisi doctor kutusaidia ila nashukuru alikubali. "habari unaongea na daktari, naomba uje hospitalin mkeo kapata ajali mbaya ya gari" doctor alimpigia simu Gabriel kisha me nilipelekwa kwenye chumba kama mgonjwa.



    Baada ya daktari kuongea na Gabriel, mimi nilipelekwa kwenye chumba, walianza kunihudumia Yale majeraha ya chupa mkononi na mikwaruzo ya usoni. Nilikuwa nanuka pombe kiasi kwamba daktari alinisaidia tu sababu nilimwahidi pesa nzuri. Ndani ya muda mfupi Gabriel alikuja mbio mbio. "hali ya mke wangu inaendeleaje, ameumia sana, ebu nieleze daktari" Gabriel kwa hofu ya kunihurumia alimuuluza daktari "alipatwa na hiyo ajali baada ya kutokuona kivukio cha waenda kwa miguu hiyo alikosa mwelekeo na kuvamia mti" daktari alimweleza Gabriel aliyenisikitikia mno "huwezi kumwona leo sababu tunamhudumia ila hajaumia sana" daktari alizidi kumpa matumaini Gabriel aliyekosa furaha sababu ya ajali tuliyojitungia na Victor. Sikutaka Gabriel anione kwani angejua nimelewa. Basi Gabriel aliambiwa aondoke aje siku inayofuata. Nae aliondoka kurudi nyumbani mnyonge , "mama yuko wapi mbona umekuja bila mama?" Anthony alimuuliza Gabriel aliyetabasamu kuficha uchungu "si unakumbuka nilikwambia anaumwa kichwa?" alimuuliza "basi yuko hospital anatibiwa atakuja kesho." alimweleza Anthony mwanae huku akimpeleka chumbani kwake kulala. Alimlaza kitandani kwake kisha alimfunika shuka Ili alale "haya ulale mwanangu nakupenda sana" Gabriel alimfunika na kutaka kuondoka "baba kila siku unaniambia Mungu ndo anaetusaidia na kutulinda basi njoo tumuombe Mungu amponyeshe mama haraka" Gabriel aliposikia vile alifurahi mno. Alimsogelea Anthony na kumpapasa kichwa "haya tumuombee" Gabriel alisema nae Anthony alifunga macho na kuanza kusali "Asante Mungu sababu wewe ni mponyaji naomba umponye mama yangu kichwa chake haraka, Mungu msaidie mama awe na furaha kama zaman Ili asiwe ananigombeza mimi tena.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mungu msaidie akipona awe ana cheka kama Zaman tukiwa sebuleni tunaangalia TV. Amen" Anthony alipomaliza alifungua macho na kumkuta baba yake anamtazama huku macho yake yakiwa yameduwaa "hee baba ushakuwa mtoto wa shetani sababu mimi nasali wewe unanitazama" maneno ya Anthony yalimshangaza sana Gabriel. "njoo mwanangu kwanza, hupendi mama akikugombeza?" Gabriel alihoji "Zaman mama alikuwa ananisaidia homework ila saiv nikimfata ananifukuza, mama hanipendi tena sikuizi" Gabriel alishindwa kuvumilia machozi, tone moja La chozi lilimtoka ila hakupenda mwanae aone. Alibaini kubadilika kwangu hakumuathiri yeye tu ila na mtoto "unajua saiv mama yako ana kazi nyingi sana ila zikipungua atakuwa anakusaidia" Gabriel alinikania mabaya kwa mtoto "kwani umemchukia mama" Gabriel aliuliza "hapana mimi nawapenda wote ila mimi nakupenda wewe sana kuliko mama" umri wa Anthony ulikuwa mdogo sana kuongea yale labda kutokana na jinsi Gabriel anavomlea anajikuta akijitambua zaidi. "basi lala salama mwanangu" waliagana na Anthony kisha alimzimia taa na kurudishia mlango.

    Palipokucha pombe ziliisha kichwani, nikaanza kuhisi maumivu ya Yale majeraha, walinifunga bandeji mkononi na kunisafisha mikwaruzo yangu usoni. Nilipojitazama nilibaini wazi Mary alinipiga sababu kwenye jicho kulivia damu, alaf uso ulivimba haswa.. Sikuamini kilichotokea, niliomba Mungu sana Gabriel asijue kilichotokea, nikiwa pale kitandani, mlango ulifunguliwa, alikuwa Gabriel na Anthony. Gabriel alishikilia mfuko wenye vyakula na pia maua kama ilivokuwa kawaida yake "unaendeleaje mke wangu" kwa upendo Gabriel alisema "naendelea vizuri mume wangu" kwa aibu Nilisema japo nilikaza macho nisishtukiwe "nimekutengeneza supu ya samaki mke wangu najua utafurahi" Gabriel kwa tabasamu alisema "mama pole sana" Anthony alisema akiwa karibu na tumbo langu huku Gabriel akiniandalia supu hiyo. Lait angejua nilipokuwa asingefanya hayo na mimi nilijikausha nikijidai kweli naumwa. Alinikalisha kitako na kuanza kunilisha "siku nyingine mke wangu uwe makini barabarani" Gabriel alinionya huku nikiitikia kwa kichwa. "Gari liko wapi Sasa" Gabriel alihoji na mimi nilijidai sijui chochote "anyway pole sana ngoja nifanye mchakato nijue lilipo alafu nikalitengeneze" Gabriel alisema na kuninywesha samaki. Muda huo huo Victor alipiga simu. Simu ilikuwa karibu na Gabriel ambae alichukua Ile simu na kuipokea. Victor alipojua ni Gabriel alibadili lugha "naomba kuongea na Rose sababu nimefika ofisin kwake hayupo" Victor alisema "yuko hospitali alipata ajali Jana" Gabriel alisema nae Victor alikataa simu. Gabriel hakutaka kujua chochote Kuhusu aliyepiga "nadhan leo jion ataruhusiwa sababu hajaumia sana" daktari alisema "Asante sana daktari yani nashukuru sana" Gabriel alishukuru sana. "ngoja nikafatilie gari lako mke wangu" Gabriel na Anthony waliondoka zao nikabaki mwenyewe. Nilimpiga simu Victor nae alikuja. Tulianza kupongezana kwa ujanja tulioutumia daktari nae aliingia wote watatu tukawa tunacheka "ila mumeo muelewa sana mshukuru Mungu kumpata mume kama yeye" daktari hakuwa anajua chochote baina yetu na hakuwa anajua kama Victor nae ni mpenzi wangu yeye alidhani tulifanya yote Yale Ili nisijulikane kama nimekunywa pombe.

    Gabriel alilichukua gari langu na kulitengeneza. Liligharimu pesa nyingi sana, kwa jinsi nilivobahili nadhan ningetumia muda mrefu kutengeneza ila kwa Gabriel lilichukua siku Tatu tu gari limerudi jipya. "Asante sana" jibu ambalo nililitoa baada ya kupewa gari lililotengenezwa liliashiria sikuona ajabu niliona kawaida sababu sikufurahia wala kumkumbatia kama ishara ya Asante. Awali alikuwa akiniletea hata pipi Lazima nitabasamu, nideke, pia nimpe maneno matamu ya asante ila ajabu ni kuwa kitendo cha kutengenezewa gari niliona cha kawaida sana. "jaman mke wangu hata kunibusu hutaki au hujalipenda baada ya kutengeneza" Gabriel alijisikia vibaya sana sababu alichotegemea sicho alichokipata. "hee jamani usipende kuishi kwa mazoea, si kila kitu Lazima nikukumbatie mimi ndo najua nimefurahi au laa je nisingesema Asante" mhh sikujihisi kama ninakosea nilijiona niko kawaida na niko Sawa. Gabriel alichukia sana ila hakutaka kugombana na mimi, aliguna na kunirushia ufunguo wa gari kisha alielekea chumban. Sikumjali wala kujirudi na mimi niliamka kochini na kuelekea chumbani, nilioga hatimae nilivaa nguo zilizoashiria nataka kutoka, "unaenda wapi saivi" Gabriel alihoji siku mjibu kitu. Nilipomaliza kuvaa nilinyanyua mkoba na kutaka kuondoka "wewe Rose nauliza unaenda" sikumjali Gabriel niliendelea kupiga hatua kuelekea kwenye gari. Nilifungua gari na kuingia kisha niliondoka zangu hali Gabriel ananitazama.

    Niliondoka zangu hadi mahali ambapo Victor alitaka niende.. Nilipofika nilimkuta amevaa na Mary. Nilipowaona nilikasirika nikataka kuondoka zangu, Victor alinizuia kisha nikakaa kuwasikiliza "Rose naomba nisamehe sikujua kama mlikuwa mnaongelea biashara" Mary aliomba radhi kwa yaliyotokea sikuamini kama Victor angeweza kumdanganya vile Mary. Na mimi nilijitia kiburi "usidhani Nina shida ya mumeo nakushangaa unaleta fujo." Mary alikuwa mpole sikuiyo kiasi sikuamini. "basi poa acha mimi niondoke zangu" niliinuka na kutaka kuondoka zangu. Wakati naondoka Victor alinitumia ujumbe "usiondoke mpenzi wangu nampeleka tu huyu nyumbani alaf nakuja" na mimi nilijibu "poa usichelewe". Basi nilimsubiria na hatimae alikuja. Tulianza kunywa huku tukicheka jinsi tulivyowafanya wajinga wapenzi wetu. "Leo tu nakunywa mpaka tukome" Nilisema. "twende zetu kwenye nyumba ya kulala wageni tukapeane raha mpenzi wangu" Victor alisema. Tulinyanyuka na kuelekea hotelini. Humo chumbani tulikunywa na kufanya kila aina ya ufuska, kila mmoja alionesha kuwa na kiu na mwenzio. Sikujali kama masaa yanaenda. Nilikaa pale mpaka saa tano za usiku. Ndipo nilipo rudi nyumbani na kumkuta Gabriel na Anthony wamekaa sebuleni wa nasoma vitabu. Niliingia kwa fujo huku nayumba yumba. Gabriel aliponiona alitahamaki. Alisimama na kuanza kunikagua. Kabla hajaongea chochote alimchukua Anthony na kumpeleka chumbani kwake. "tangulini umeanza kunywa pombe tena" alihoji huku mimi nikisunya na kubetua midomo "wewe kama Nani unanihoji" niliuliza kwa dharau "kwanza huna hadhi ya kuwa na mimi nakushangaa unaniuliza uliza ebooo ebu nipishe mimi" Nilisema huku nikijikongoja kuelekea chumbani, Gabriel alikuwa na hasira kias cha kitokujali chochote alinikamata mkono na kunivuta kisha aliunyanyua mkono wake Ili anipige kibao "baba muda wa kusali umefika" Anthony bila ya kujua kinachoendelea alitufata sebuleni na ikawa pona yangu ya kupigwa na Gabriel. Aliushusha mkono wake haraka alaf alinitazama tu akaondoka na Anthony kwenda kusali. "nyoooooooo heee ungejaribu kunipiga uone ungenijua mimi ni nani mwone kwanza jitu lenyewe baya kwel" nadhan Yale yalitoka kinywani mwangu sabb ya pombe. Nilielekea chumbani na kujitupa kitandani nikiwa na viatu na si kubadili hata nguo

    Palipokucha nilishtuka kujiona nimelala mwenyewe kitandani, cha ajabu Gabriel alinivua nguo zile na kunivalisha za kulalia, sikujua amefanya hayo yote muda gani. Nilipotazama mlangoni nilimwona Gabriel amesimama wima ananitazama kwa hasira,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilipozinduka kutoka usingizin, nilibaini Gabriel hakulala na mimi, nilipojitazama nilishangaa kuona kuwa nimevaa nguo ninazolala nazo, nilijihoji nilivaa saa ngapi sababu nakumbuka nilijitupa tu kitandani bila ya kuvua nguo, nilijua wazi ni Gabriel ndo amenivalisha, nilipotaka kuamka kitandani pale nilimwona Gabriel amesimama mlangoni, nilipomtazama kwa umakini nilitambua ana hasira "za asubuhi mume wangi" kwa sauti ya chini huku macho nimeyaficha sitaki kumtazama nilimsalimia. Hakunijibu zaidi alisogeza kiti karibu yangu na kukaa, "pombe zimeisha kichwani?" alihoji ila mimi sikuweza kumjibu kitu . Gabriel alimwita Dada wa kazi na kumwambia alete supu ambayo aliitengeneza maalum kwa ajili yangu. "supu hiyo hapo kunywa upate nguvu" Gabriel aliniambia. Niliogopa nikiamini siku hiyo ndo mwisho wangu. Sikubisha nilichukua bakuli lile na kuanza kunywa kwanza niliamka nina njaa kweli. Nae alikuwa anakunywa Chai yake ya maziwa bila kitafunwa "Rose" aliita "abeee" Nami nilijibu haraka haraka Ili kujua anayosema "ulikuwa wapi jana" bila sura ya mapenzi usoni Gabriel aliniuliza. Nilikaa kimya sababu sikuwa na jibu, alirudia tena kuniuliza "na kwa nini Jana napiga simu hupokei" maswali ya Gabriel yalinifanya niwe na adabu kwani nilijua nikikosea tu nikajidai kiburi ningeambulia makubwa zaidi. "samahan sana mume wangu sikukuaga sababu napo sikuwa na taarifa mapema" nilianza kupika uongo Ili kumfanya Gabriel apunguze hasira, "Jana rafiki yangu alikuwa anavalishwa Pete ya uchumba Asa ndo tulienda kwake" nilijitetea "simu sikuweza isikia sababu kulikuwa na makelele kwake samahan baba Anthony" majina yote mazuri sikuiyo nilimwita "kiukwel hata mimi sijui nilianzaje kunywa maana nakumbuka nilikuwa nakunywa kinywaj laini ila mpaka sasa sijui nilianzaje nadhani hata wewe unajua wazi niliacha" Niliendelea kujitetea huku nikitengeneza sura ya mtu anaejutia makosa yake. "Nisamehe bure mume wangu ni bahati mbaya" nilishuka chini nikapiga hadi magoti na vimachozi vya unafiki vikitoka. Gabriel ni mwanaume mpole sana na mwelewa japokuwa alijawa na hasira juu yangu, aliniinua pale na kunikumbatia "basi mke wangu nimekuelewa basi mama Anthony" Hee! Sikuamini moyoni nilisonya na kubeza kuwa Nina mwanaume fala ambae machozi ni udhaifu wake. "siku nyingine jitahidi sana kutoa taarifa Ili niwe najua mapema" Gabriel alinieleza huku akinifuta Yale machozi "nilikusudia leo kukuadhibu sana ila nimekusamehe" alisema huku akinilisha kipande cha nyama. Mimi nilitabasamu japo halikutoka moyoni, moyo wangu haukuthamini msamaha ule ila uliubeba na nilijiona mjanja na mtu mwenye maneno ya kuficha ubaya tena moyoni nilikuwa nikimtukana sana "limwanaume gani ambalo hajui hata kuhoji yani vimachozi vidogo ndo vimemfanya anihurumie, lijinga kweli" Nilimbeza sana Gabriel aliyenisamehe kutoka moyoni. Niliamka pale kitandani na kuelekea bafuni kuoga. Siku hiyo sikutaka kutoka kuelekea popote. Gabriel aliondoka na Anthony, alimpeleka shule na yeye kazini kwake. Akiwa ofisini kwake alianza kunitumia sms na mimi namjibu, muda huo pia nilikuwa nachati na Victor nikimwelezea yaliyotokea, wote wawili walionesha kuwa shapu kujibu ila kwa Gabriel Kuna muda nilikuwa nazikwepa sms zake. "mke wangu siku nyingi hujanipa mahaba mazuri kama zamani" Gabriel aliutuma ule ujumbe, alafu siku mjibu, niliupuuza na kuendelea kuchati na kipenzi changu Victor. "hanitishi wala hanibabaishi hata akiniacha bado nitaishi" looh! Wazungu wanasema wrong path, basi maana yake sms Ili fanya kitendo cha kukosea njia na kupita njia isiyokusudiwa, niliituma Ile sms kwa Gabriel badala ya Victor. Nilitaka macho kama fundi saa, sikujua nitajibu nini akiniuliza basi nilikaa kimya nikisubiri kuulizwa ila hakuniuliza, nikabidi kujibu Ile sms aliyoituma "usijali mume wangu leo nitakupa mapenzi uliyoyazoea si unajua nakupenda sana" niliituma nae akajibu kwa ufupi "nitashukuru" Jibu lile lilinichanganya sana. Nilianza kuogopa na kujihoji kama ameipata au laa, sikutaka kumuuliza ivo na mimi nilikaa kimya. Aliporudi jioni nilimpokea na kumkaribiasha kwa mahaba. Lengo langu ni kujua kama aliipata Ile sms, Nilijitahidi sana kuwa mchangamfu kwake ila si kuona dalili za kuulizwa Kuhusiana na sms Ile. Nilipuuza na kujidai kama sijali japo nikimtazama Gabriel nabaini hayuko Sawa kabisa,

    Palipokucha asubuhi Gabriel alinigeukia na kunichezea usoni kisha alinibusu kama ilivo kawaida yake aamkapo, ila sikuiyo aliendelea kunitazama usoni na kuziweza Sawa nywele zangu ambazo zilikuwa zimegusa uso wangu. Nilifungua macho yangu na kukutana na tabasamu zito La Gabriel, "mke wangu umeamka" kwa upole alisema na mimi niliitikia kwa kichwa "ivi ikitokea leo tumeachana utafanyaje" aliposema vile basi pale pale nilishtuka ila yeye alionekana kuwa kawaida, niliguna kwanza kisha nikamtazama machoni. Nilianza kulia tena kinafki "yani unanikumbusha maumivu ambayo nilishayasahau au na wewe unataka kuniacha" Nilisema hali iliyomshangaza Gabriel ambae hakuwa na mawazo kama yangu "jaman mke wangu Sina na mbaya nimeuliza tu" Gabriel alijitetea ila mimi nilikataa katu katu kujibu zaidi nilianza kumgeuzia kibao "kama umempata mwanamke mwingine niambie kuliko kunihoji hoji maswala kama hayo" Niliendelea kulalamika "jamani mbona ivi yani me Sina maana mbaya niliuliza tu sababu, Rose mimi nakupenda sana, huwa sitamani tuachane sababu nahisi tukiachana naweza nikafa," masikini Gabriel alichokuwa anaweza ni tofauti kabisa na mawazo yangu, niliona aibu na kujidai kama nimezira japo moyoni nilikuwa najizomea kuwaza vitu ambavo ni vibaya wakati Gabriel ananiwazia mazuri. "unajua kwa nini nilikuwa nalia?" nilimuuliza "sababu sitaki uniache, nakupenda sana" Nilisema hayo huku Gabriel akicheka

    **

    Jackline alikaa Italy kwa muda mrefu sana kiasi kusahaulika, Jackline alijikuta akijiwekea msingi mizuri sana ya maisha yake kama alivo Sema kuwa anataka kufanya kazi Italy kwa lengo ka kukusanya mtaji wa Kuja kufanya biashara zake Tanzania. Mungu alimbariki, kwanza ilifika hatua ya ukizungumzia wanamitindo watano wanaofanya vizuri nchini Italy kwa upande wa Waafrika basi Jackline Lazima atajwe. Alijikuta akipokea tupo nyingi pia alijikuta akiwavalisha watu maarufu karibia bara lote La ubaya na Amerika. Sifa kubwa aliyekuwa nayo ni mwanamitindo mdogo kuliko wote ila naefanya kazi nzuri. Alijulikana sana na alifanya kazi kwenye makampuni mengi sana, alibahatika kutengeneza manukato yake yani perfume yenye lebo ya Gabrielo, alipohojiwa alidai hiyo ni moja ya shukrani za dhati ambazo anazitoa kwa rafiki aliye kama ndugu yake ambae ni Gabriel. Kila apatapo tuzo mtu wa kwanza kumshukuru alikuwa Gabriel. Aliutambua uwepo wa Gabriel na hakuona aibu kumtaja wala kujitaja kwa watu kuwa yeye asingefika hapo aliko kama asingekuwa Gabriel. Ujasiri ule wa kujishusha ndio uliozidisha umaarufu wake katika nchi za Ulaya na Amerika. Utajiri wa Jackline ulikuwa ni mara tatu ya utajiri wangu. Jackline alikuwa anamiliki perfume iliyotumika karibia nchi zote za ulaya, Afrika kusini, Nigeria na nchi zingine, alikuwa ana miliki kipindi cha television nchini Italy ambacho ni yeye alikuwa mwafrika wa kwanza Italy kumiliki kipindi kilichohusisha mitindo na urembo. Bado alitumiwa na makampuni mbalimbali kufanya matangazo, Hakika Jackline alikuwa ni binti aliyejituma, hayo yote aliyafanya bila msaada wa mtu yoyote zaidi ya ada aliyolipiwa na Gabriel, ila mpaka hapo alipofikia zilikuwa jitihada zake mwenyewe japo yeye aliamin ni nguvu za Gabriel.

    Baada ya kufanya kazi huko kwa miaka kadhaa aliamua pia kurudi Tanzania, aliamua Kuja kuwekeza kwenye nchi yake. Japo maisha yake yalikuwa ya safari za mara kwa mara sababu Italy anabiashara zake

    Jackline alitoa taarifa ya siku ambayo anatarajia kurudi nyumbani, basi Gabriel alifurahi sana kusikia kuwa Jackline anarudi. Ila mimi sikufurahi hata kidogo, nilijua akija Lazima ananishtua michezo yangu. "Beby unaonaje tukimtafutia Jackline nyumba yake Ili aweze kuishi maisha yake ya kujitegemea" nilianza

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kumshawishi Gabriel "kwani hapa hawezi kujitegemea" Gabriel alinijibu kwa dharau sababu hakufurahishwa na maneno yangu "kwani wewe shida ni nini, vyumba vyote hivi bado unataka Jackline akaishi wapi" majibu ya Gabriel yalinikera sana, "wewe unamtetea nini Jackline, me nimesema hatuwezi kuishi humu ndani na Jackline sababu kashakuwa mtu anaeweza kujitegemea" Nilisema hayo kwa ukali "nimesema Jackline hapa hatoki na sitaki kujadili hilo" Gabriel alisema kisha alikaa kimya "basi utakaa na huyo Jackline wako mimi nitaondoka humu ndani" maneno yangu yalimshangaza sana Gabriel ambae hukuamini kama mimi namkana ndugu yangu "badala ufurahi upweke unatoweka ila wewe unalewa habari za ajabu, ivi umekuaje sikuiz kila kitu kwako kibaya" alinieleza ila mimi kwa dharau nilinyanyuka na kuelekea chumbani





    Tulizidi kugombana na Gabriel kisa Jackline. Nilianza kuonesha jeuri za waziwazi kwake huku msimamo wangu uliendelea kubaki kama ulivo kwamba Jackline hatoishi na sisi. Nilianza kuwa mkali na majibu yangu ya mkato yalizidi. Tabia yangu Ile hatimae Gabriel aliizoea, hakuwa anataka maneno mengi na mimi, akibaini nimebadilika basi yeye hunyamaza na kuniacha kama nilivo. Ila siku akikasirika huongea maneno mazito kiasi cha wakati mwingine nafsi hunisuta, "unajua Nina mambo meng yakufanya, usitegemee kama ipo siku nitakupiga yani sitokupiga" wakati mwingine hukereka zaidi na kunitazama tu "hicho kinachokupa kiburi ipo siku kitaondoka ndipo utajitambua" Gabriel alikereka sana na tabia zangu ila hakuwahi kuhisi kama nina msaliti au niko na Victor, alishanipeleleza sana, alishakagua simu zangu sana, alishaniwekea walinzi sana ila hakuwahi kubahatika kunikamata sababu ya umakini wangu. Gabriel alihisi labda umaarufu na pesa ndizo zilizokuwa zinanipa kiburi. Upendo wake kwangu haukubadilika japo ulipoa sababu mimi ndo niliupooza.

    Ziliwadia siku za Jackline kurudi Tanzania na siku husika zilijulikana. Niliendelea kusisitiza kuwa Jackline hatoishi mle ndani "wewe kataa kubali ataishi alaf sijawahi kuona mtu anamkataa mdogo wake" Gabriel alisema tena akionesha kunishangaa haswa "Rose Nina mashaka una matatizo ya akili na Lazima nitakupima maana sikuelewi kabisa sikuiz" aliposema hayo nilimtazama tu na kunyamaza kwani siku hiyo nilikuwa na haraka ya kukutana na wageni kutoka Kenya waliokuja kutembelea chuo changu.

    Wakati niko katika biashara yangu, Gabriel alinipigia simu sana ila sikupata nafasi ya kuipokea na hata nilipoiona sikuijali sana. Nilitaka chuoni pale na kurudi kwenye ofisi zangu. Nilipofika niliingia ndani kisha nilipanda ghorofani sababu huko ndiko kulikuwa na salon alaf chini ni maduka ya vipodozi na nguo, wakati niko saloni hapo, aliingia mfanyakazi wangu "duuuu! Jaman Mungu anaumba bana" alisema huku akionesha kutahamaki "Kuna mdada yuko huko chini heeeeeee! Kiboko ya wadada wanaoringa hapa mjini" maneno yake yalitupa kiu ya kujua anamaanisha nini "mwanadada mrefu, mwembamba wa wastani mzuri ajabu, achana na hiyo Sasa manukato yake kiboko sijawahi yasikia" kwa hasira nilimnyamazisha asitoe tena sifa aeleze Kuna nini. Kabla hajaendelea aliingia mwingine, "Dada Rose, mhh shemeji yuko na mdada mmoja mzuri anakuzidi wewe wanaongea na kukumbatiana utadhani wapenzi" nilipo sikia sikutaka maelezo zaidi nilishuka haraka haraka kwenda kumwona huyo mdada aliyeparamia mume wa mtu. Nilipofika niliwaona, "looh siamin kama huyu mshenzi anatembea na binti mzuri kiasi hiki" nilijisemea sababu uzur wa binti yule ulizidi. Nilisogea na kusimama mbele ya Gabriel. "woow mume wangu naona leo mapema salon" Nilisema lengo ni kumfanya huyo binti ajue mimi ndo mke wa Gabriel "habari anti" kwa kiburi nilisalimu ila Jackline aliyebaki anatabasamu alikaa kimya. Jackline alibadilika kiasi cha hata mimi dada yake kumsahau. Alizidi uzur, rangi yake niliyoizoea ilipotea na kubaki rangi nyororo na nyeupe ambayo ilivutia mno, nywele zake zilizoongezewa nywele za kununua (weaving) ndo ulimfanya awe zaidi ya mzungu, manukato yake ndiyo kabisa akipita karibu yako Lazima ugeuke na kumtazama, macho yake yalifunikwa na miwan iliyozidisha uzuri wake kiasi cha mimi kumsahau. "supriseeeeeeeeeee" Gabriel alitoa sauti ya furaha nae Jackline alicheka na kunisogelea "sitaki kuamini kama umenisahau" Jackline alinieleza japo lugha yake ya kiswahil iliathiriwa na lugha ya huko aliko kuwa "woow Jackline jamani mdogo wangu" ujue kile kitendo cha mimi kumfurahia Jackline kilimchosha Gabriel ambae kila siku alikuwa akiwaza itakuaje siku nikionana na Jackline. Damu ni damu tu, au ndugu ni ndugu tu kwani nilipomuona Jackline nilisahau kama nilikuwa napanga kumtimua nyumbani. Nilimkumbatia kwa furaha huku nikimkaribisha kwa shangwe sana mle ndani. Nilimtambulisha kwa wenzangu na kwa wafanya kazi wangu na wote walimpokea kwa furaha. Kwa furaha niliyokuwa nayo, nilimwomba Gabriel atupeleke dinner familia yote, Gabriel alitupeleka tukaenda hadi na wasaidizi wa kazi nyumbani.

    Tukiwa hotelini pale Jackline alionekana kutumiss sana, Anthony hakuwa akimkumbuka akawa akihoji maswali mengi yakutaka kumjua Jackline. Gabriel ndo kabisa alifurahi mno ujio wa Jackline. "ehee maisha vipi ya huku Tanzania, mhh vipi Mary na mume wake" kitendo cha Jackline kuuliza vile nilijikuta nikipaliwa na kinywaji kiasi cha wote kushangaa "kulikoni tena au ndo...." kabla Jackline hajamalizia alichotaka kusema nilidakia "hakuna kitu nimepaliwa tu, aah sikuiz tuna maisha yetu hata hatuna muda nao" niliposema nilitazamana na Jackline machoni, "OK that's good" (Sawa ni vizuri) alisema na kuendelea kula. Muda huo huo nilikosa amani dinner ikaingiliwa na jinamizi. Jackline aliendelea kupiga story "laiti huyo Victor angeshuhudia maisha tunayoishi saivi angejinyonga" kiongozi mmoja hupenda kusema anatumbua majipu basi nahisi kwa Jackline hakuwa anatumbua ila analiivisha Ili litumbuke lenyewe bila kutumbuliwa, niliposikia tena vile nilimwaga kinywaji kilichopo kwenye glass kwa bahati mbaya. "duu anyway ehee Gabriel nambie nimekumisije" Jackline aligundua wazi stori zake zinanikera akaona abadilishe mada....

    *****

    Ilipita wiki tangu Jackline arudi nyumbani "afadhali Jackline umerudi walau huyu Dada yako anawahi kurudi sikuizi" Gabriel alimweleza Jackline bila ya kujua nimekwazika. Sikujibu chochote ila niliguna tu. Kivumbi ni tulipoingia chumbani kulala, tulianza kugombana sana na Gabriel "unadhani namwogopa huyo Jackline wako" kwa ukali nilisema "Sasa ngoja nikuoneshe kuwa simwogopi mtu" Gabriel alikaa kimya akinitazama "Nina uwezo wa kukupiga, nikaiharibu sura yako na mtu yeyote asinifanye kitu" kwa hasira alisema "naona sikuiz unanipanda kichwani kiasi kwamba wewe ndo mume alaf mimi mke" pamoja na ukali ule lakini sikujali "usinibabaishe kama unaona kero mimi kuishi humu ndani niambie niondoke" niliposema vile Gabriel alisimama na kunipiga kibao kimoja ambacho sikutegemea "pumbavu hayo maneno kamweleze mjinga mwenzio siyo mimi" nilipoona Gabriel kanipiga nilianza kulia "kisa Jackline amekuja ndo maana leo umenipiga mbona Zaman hukunipiga" nililia sana nae Gabriel alikaa tu kimya "najua Jackline ndo furaha yako maana amekuja hunijali tena" kwa ukali Gabriel alidakia "mwanamke gani huna nidhamu, huna kauli, unachelewa nyumbani" alisema "biashara zako zote ni Sawa na pesa ya kununulia gari moja kwangu na bado pesa isitoshe lakini ulishaniona mimi nikija nyumbani usiku?" sikuiyo Gabriel aliamua aligomba sana ila mimi sikujali chochote, nilisusa hadi kulala nae nikaenda kulala chumba kingine

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Palipokucha, niliondoka mapema sana, sikumsalimia yeyote yule, niliondoka zangu hadi kazini, nikamwacha Jackline na Gabriel nyumbani, "acha shemeji nampeleka mwenyewe Anthony shuleni wewe nenda tu kazini" Jackline alimwambia Gabriel ambae hakubisha. Alimpeleka mtoto shule na ilipofika saa tano Jackline alinifuata ofisin. Nilipomwona sikumchangamkia "nahitaji kuongea na wewe" Jackline alinitazama kwa ukali "Sina muda" nilijibu "okay naamin masikio yanasikia ivo utanisikia tu" Jackline alikazia "ulipokuwa Dubai uliniambia umekutana na Victor, ehee baada ya kukutana ikawaje maana nilikuwa nikikuuliza unanijibu mkato" Jackline alianza kunikera kiasi cha kutamani kumfukuza "tuachane na hayo nasikia ulipataga ajali, mhh ajali ya gari au ya kipigo kutoka kwa Mary" kitendo cha Jackline kusema vile nilichanganyikiwa "heeey stoooop"





    Sikutaka kuamini kabisa kama Jackline aliyeko mbali na mimi anayajua mambo yangu kuliko Gabriel ambae nina lala nae, Nilibadilika haswa, sikutaka kuendelea kumsikiliza maana angeendelea kuongea mambo mengi ambayo kwangu nilihisi ni siri kubwa na hakuna anaejua, "OK, ulijiona kama malkia baada ya Mary kukuomba msamaha" Jackline alizidi kuchimbua mambo yangu hali nimebaki mdomo wazi hata siamini. "wewe ni mwanamke wa aina gani, mama na baba yako ni nani, familia yako ni ipi, ambayo haina hata chembe chembe za utu ambazo ulirithi" kwa tahamaki Jackline alieleza tena akionekana dhahiri hajafurahia matendo yangu. Alifungua pochi yake na kutoa bahasha "tizama hizo picha, unajua nimezikomboa kiasi gani cha pesa Ili kusudi tu wewe usiingie kwenye skendo chafu" Niliinua ile bahasha na kuzitazama picha zangu "mtume weee" Nilijikuta nikitoa sauti hiyo baada ya kuona picha zangu nikiwa na Victor hasa chumbani tukimsaliti Gabriel na Mary. Sikuamini nilifungua mdomo wangu kwa aibu nikijua huo ndo mwisho wangu hasa Gabriel akiziona "usishtuke kinafki huo unafiki mfanyie Gabriel ambae hajui chochote ila kwangu sitaki kabisa" Jackline alinitazama kwa ukali "ivi hata akili ya kujiongeza huna" Jackline alipaza sauti yake kwangu "Ni mwanamke gani na wa nchi ipi anaweza akakuruhusu uwe bar na mume wake et mnajadili biashara na yeye akaridhika kabisa kibaya zaidi anakufata kukuomba msamaha" alizidi kunifumbua macho yangu japo bado sikuwa najielewa. "Victor hakupendi ila anapenda pesa zako, na yuko mbioni kukufilisi na tayar kashaanza kukufilisi" maneno ya Jackline yaliufumbua moyo wangu na kunifanya nijitambue. "looh najuta kwa nini nilijiingiza huku" niliinamisha kichwa changu chini nikijutia makosa "Gabriel anakupenda sana Rose, hakuna mwanaume anaepaswa kuabudiwa maishani mwako kama Gabriel" alizidi kunipa ushauri na saha "kumbuka nyumbani kwetu hakuna hata mmoja anaeweza kutusaidia mama ndo huyo hajiwezi hizo pesa unazochezea bar na kumbi za starehe kwa nini usingemjengea mama walau nyumba ya maana, au umesahau maisha ya kwenu" Jackline alikuwa anaongea huku analia maana aliumizwa sana na matendo yangu "sijui wewe labda Victor ndo chaguo lako ila kumbuka si kila chaguo huwa linatufaa," aliendelea kunifanya nijute haswa na kuahidi sitorudia tena. "naomba hizi picha uzichane watu wasizione hasa Gabriel." Jackline alitabasamu na kuniahidi hatomwonesha mtu. Tulikumbatiana na kuahidiana kuwa tutaishi kama zamani. "Kuna mambo yangu nafatilia ngoja mimi nikuache uendelee na kazi" Jackline alisema na kuondoka zake. Sikuiyo sikuwa na raha kabisa "inawezekanaje Victor atake kunifilisi, mbona hajawahi kuniomba pesa" niliwaza hayo hali akili yangu ikiwa haiwezi tena kuchambua mambo "hizi picha Nani alikuwa anazipiga, mhh yani hata sijielewi" nilijihoji bila ya majibu

    *****

    Maisha yalirudi tena kama Zaman, ilikuwa ni siku ya tatu tangu tuongee na Jackline Kuhusu tabia yangu. Wote tulirudisha mapenzi kwa kila mmoja, tangu siku hiyo Victor hakuwahi kunipigia simu, sikujua kwa nini na sikutaka hata kujua kwa nini. "nataka niende kijijin kumsalimia mama sababu ni miaka sijaenda" Jackline siku moja tukiwa tumekaa familia nzima alisema "nataman sana kwenda ila mambo ni mengi we ukifika tu msalimie mama, utachukua kanga zangu na nguo zile nisizovaa unampeleka" maneno yangu yalimshangaza Jackline "huyo ni mama anapewa nguo chakavu je angekuwa omba omba si ndo ungemwagia maji" Jackline alisema kwa kejeli sababu akiangalia uwezo wa mimi kumnunulia mama nguo mpya nilikuwa nao. Jackline hakujali sana na wala hakukubali kuchukua hizo nguo. "Jackline siku unaenda uniambie nikusindikize sababu saivi Sina kazi nyingi" Gabriel alisema nae Anthony akalilia kwenda. "mimi naondoka kesho kutwa ivo mnaoenda mjiandae" Jackline alijibu "yes! Yes! Naenda kumwona bibi woooow" Anthony alifurahi sana kusikia habari za bibi yake kwani tangu azaliwe hakuwahi kumwona bibi yake

    Safari ya kwenda kijijini iliwadia, wote waliondoka hadi mfanyakazi alienda kasoro mimi tu. Niliweka biashara mbele kuliko mama yangu. Sikupata uchungu wa kutokwenda na niliona kawaida. Jackline alikuwa na hamu ya kumwona mama, alibeba zawadi nyingi sana za kumpeleka mama, alibeba magunia ya vyakula, vitenge, nguo na kila aina ya zawadi ambayo yeye aliona inamfaa mama, hakubeba chochote chakavu vyote vilikuwa vipya. Jackline alikuwa tajiri ambae yuko Tanzania ila biashara zake Italy ziliendelea, ila Jackline hakuwa anapenda maisha ya juu kama nilivyo mimi, alipenda kuishi maisha ya kawaida hata maduka aliyokuwa anaingia yalikuwa ya watu wa maisha ya kawaida. Wakiwa kwenye gari La Gabriel wote walikuwa na furaha, Anthony ndo kabisa hakuwa ametulia alikuwa akiruka na kuongea sana "inaonesha mnawapenda sana ndugu zenu maana kila mwisho wa mwez Lazima Rose aje huku kumsalimia mama yake" Gabriel alisema huku akionekana kufurahishwa na maisha yetu. Jackline hakutaka kusikia habari zozote zaidi ya mama yake kwa jinsi aliivomkumbuka...kutokana na Gabriel kuzoea kuendesha magari umbali mrefu pia aina ya gari walilokuwa nalo lilikuwa linahimili umbali mrefu, walianza kuikaribia Arusha na ilibaki kama lisaa tu wafike nyumbani, Jackline aliomba kwanza wasimamishe gari Ili atazame mkoa wa Arusha jinsi ulivoendelea. "mhh siamin kama bado mama yuko kwenye kale kajumba wakati watu wanajenga majengo mazuri ivi" Jackline alionekana kusikitika sana huku moyo wake ukikosa Amani. "aibu Gabriel yani tunaenda nyumbani na gari zuri zawadi nyingi ila anapoishi mama paovyo" Jackline alikosa raha sana. "we twende Sasa tuishie njian?" Gabriel alisema huku akiendesha gari kuelekea kwa mama yetu. Walipokaribia kila jirani walitokea kwenye majumba yao kuona gari La kifahari linakoelekea "hata aibu hawaoni baada ya miaka mingi leo ndo wanakuja kwao" majiran walipoliona gari na wakabaini ni Jackline yuko kwenye gari basi walianza kubeza na kukashfu "ebu ona maisha ya mama yao ya kuomba omba alaf watoto wana miliki magari" hakuna aliyefurahishwa na ujio wa Jackline kwani tangu tuondoke tena kwa kutoroka hatukuwahi kurudi zaidi ya miaka kama kumi ivi, Mama yetu alipomuona Jackline alilia sana. Kwa uchungu alilishika tumbo lake na kulia sana "nimewabeba miezi tisa nikawalea kwa shida ila mlipojitambua mlinikimbia mkaniachia upweke utadhani sijazaa" Mama alilia "mmekuja kuniringishia gari na nguo za thaman wakati mimi naishi nyumba iliyoshikiliwa bati kwa mawe, tokeni kwangu siwataki" wanasema uchungu wa mama aujuae mama ila asikwambie mtu mama mchungu kuliko hata mtoto, Jackline alimsogelea mama yake na kupiga magoti pale pale nje "nisamehe mama yangu, ebu niruhusu nikukumbatie walau nijivunie Nina mama

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    anaenipenda kama wewe" Jackline alilia kuona mama analia "nilienda kutafuta Sasa nimerudi, nipokee mama, nimerudi mwanao" Gabriel na majirani waliishia kulia kwani hawakutegemea kama Jackline angejishusha kwa mama yake. Kwa upendo mama alimwinua Jackline pale chini na kumkaribisha ndani, wote waliingia ndani. Walitambulishana na kufurahiana sana kiasi cha wote kujiongeza kwa mama yao hasa Jackline "mama sitaki kula chakula cha yeyote aliyepika zaidi yako" Gabriel alisema "hata mimi bibi" Anthony alisema na yeye kwa furaha mama aliamka na kuelekea shamban kuchuma mboga kisha alielekea shambani tena kutafuta vikuni Ili apike. Gabriel alionekana kuyafurahia Yale maisha. "Rose yuko wapi mbona yeye hajaja" Mama aliuliza "mama alisema yeye alishakuja" Anthony alidakia "amekuja wapi" kwa tahamaki mama aliuliza "si hapa kwako bibi au umesahau" Anthony aliendelea kujibu "tangu siku muondoke sijawahi kuona sura yake tena" majibu ya mama yalimshangaza Gabriel kwani kila mwisho wa mwez huwa naaga naenda kumsalimia mama



    Anthony alizidi kuwa changanya. "Tena ukampa embe Ili aniletee, bibi umesahau eee" Gabriel alijisikia vibaya sana sababu hukuamini kama kweli mama hajui chochote, nae mama alikazana kusema hakuwahi kuniona hata siku moja. Jackline alipowatazama wote aligundua kutaibuka ugomvi mkubwa sana Iwapo watarudi nyumbani, "Gabriel ebu nisindikize nje mara moja" Jackline alisimama nae Gabriel alinyanyuka kumfuata Jackline. "usishtuke sana shem wangu" Jackline alitabasamu Ili kumfanya Gabriel apunguze hasira "unajua mama yetu Ana ugonjwa wa kusahau, Kuna wakati kumbukumbu zake zinapotea" Jackline alifanikiwa kurudisha imani ya Gabriel kwa asilimia zote, "looh nilianza kuwaza mengi sana ila nimeshaelewa" Gabriel alitabasamu na kurudi ndani.

    Palipokucha Jackline aliwahi kuamka kuliko wote kisha alifata mama, "shikamoo mama, za kuamka" Jackline kwa adabu alimsalimia mama, baada ya muda kidogo wote waliamka "woow! Jackline kumbe unapendeza ukivaa khanga" Gabriel alimtania Jackline. "Chai tayari kila mmoja akapige mswaki na kunawa uso" Jackline alisema "umepika Chai na kitafunwa gani" Gabriel alisema "na wali mwanangu au hujapenda" kwa ukarimu wa hali ya juu mama alijibu "Jana niliona boga ndani tupike boga, alaf mama kuanzia leo uwe unapika vyakula vya asili ukimruhusu Jackline apike mimi sitakula" wote walicheka kisha mama aliingia ndani na kutoa boga Ili lichemshwe,

    Jackline sikuiyo alionekana kukagua sana eneo La mama huku akionesha dhahiri Kuna jambo analiwaza "mbona ivi Kuna tatizo" Gabriel aliuza "hapana niko sawa" Jackline alijibu "na hilo karatasi uliyoishika Ina nini" Gabriel alihoji tena, "usijali shem wangu niko Sawa tu" Jackline alijitahidi kuwa msiri japo hakufanikiwa kufanya siri yoyote. Gabriel alimnyanganya karatasi Ile "unataka kumjengea mama.?" alimuuliza Jackline kwa tahamaki, "acha nijaribu kumjengea nyumba walau nzuri hii nyumba itakuja kudondoka siku yoyote" Jackline kwa sauti ya chini alisema "kwa nini usimshirikishe Rose kwanza" Gabriel alipendekeza. Jackline aliguna kwanza kisha alinyamaza, "Ili uweze kupata nguvu ya kujenga mkiwa wawili" alimshawishi Jackline ambae kwa shingo upande alikubali japo alijua wazi sitokubali. Aliinua simu yake na kunipigia "yani kwa Sasa Sina hata pesa, nyie acheni mpaka nitakapojipanga," kwa ukali niliwajibu "mnadhani pesa zinatolewa kirahisi tu, hata kama ni mama Lazima nimuweke kwenye bajeti siyo kukurupuka" niliposema nilikataa simu "Ni Rose huyu huyu ama mwingine" kwa mshangao Jackline alijihoji, "amesahau katika watoto waliokuwa wanapendwa na mama ni yeye?" kwa huzuni alisema "amesahau Kati ya mimi na yeye, anaethaminiwa ni yeye tangu zaman?" Jackline aliumia sana "nitasimama katika zamu yangu na nitafanya kwa nafasi yangu" Jackline alimweleza Gabriel aliyepigwa na butwaa kwa majibu yangu. "usijali Jackline mimi nipo na wewe tutamjengea mama" Gabriel alisema hayo "hapana Gabriel, uliyonifanyia ni makubwa kuliko hili" kwa masikitiko Jackline alimkataza Gabriel asimsaidie, alimhurumia kwani amekuwa akitusaidia na kujitoa kwa hali na mali, Japo kwangu sikuliona hilo, "Jackline, pesa tunatafuta siyo Ili tuhifadhi Bali tuzitumie na matumizi ndo haya" Gabriel alitabasama huku akimweleza Jackline "huyu ni Sawa na mama yangu, anapaswa kuishi pazuri kama sisi tunavoishi" maneno ya Gabriel yalimpa nguvu Jackline aliyemkumbatia na kumshukuru, siku hiyo hiyo michakato ilianza bila ya mama kujua kwani Jackline na Gabriel waliondoka bila ya kuwaeleza wanapokwenda, Mida ya mchana ivi mama alishangaa malori yakiongozana Kuja kwake, aliogopa na kuhisi huenda wamekosea njia, ndipo Jackline na Gabriel nao walifuata wakiwa na mafundi wa ujenzi waliokuja kupima wapi pakujenga nyumba ya mama. "mama huu ni muda wako wa kujivunia kuwa una watoto" kwa furaha Jackline alimweleza mama, kwa shangwe na nderemo mama alianza kuimba, alianza kuruka ruka huku machozi ya furaha yakimtoka, alianza kulia kwa sauti na kukumbuka matusi ya majirani zake "oohh Mungu wangu, wewe uliyeniahidi kuwa utapigana nao watakaopigana nami Asante kwa yote" alitembea kiwanja kizima akiimba na kumtukuza Mungu wake "'ulinifundisha kuwa na moyo wa subira.. Haya ndiyo matunda ya uvumilivu wangu" mama hakuchoka kuimba na kulia kwa furaha zilizochanganyika na uchungu "nilipoenda kuomba chumvi, nilijibiwa majibu ya kejeli wakati mwingine niliambulia matusi hasa wa watoto wadogo" alifunga kanga kiunoni na kuendelea "nililia usiku kucha na mchana kutwa nikilalama kumbe Mungu uliwaondoa wanangu mbali na mimi Ili waje leo kunipa heshima mbele za maadui zangu" Jackline alimsogelea Ili ampooze "niache nilie mwanangu, hujui nimepitia mangapi," alijitoa kwenye mikono ya Jackline Ili aendelee kusema "sitasahau siku niliyolala njaa, usiku wa manane njaa iliponizidia nilienda kwa jirani kuomba walau. Kiporo, aliamka kwa ukali na kunitukana" alilia mama yetu kwa uchungu kisha aliendelea "alinijibu kuwa WATOTO WAKO WAMEENDA KUFANYA UMALAYA UNAKUJA KUTUSUMBUA" maneno ya mama yaliwahuzunisha watu sana "Leo wanangu wamerudi, wamekuja kuniondolea aibu, Mungu asante, asante Baba" alipiga magoti pale chini na kumshukuru Mungu wake, Alimsogelea Jackline na kumbariki "kabla sijafunga kinywa changu acha leo nikubariki" kwa unyenyekevu Jackline alimsogelea na kupokea baraka "yeyote atakaekusudia mabaya juu yako akaaibishwe mchana kweupe" alisema huku akimbusu mikono yake "kila siku Mungu azibariki hatua zako, upitapo kwenye uvuli wa mauti basi Mungu na akuvushe" alipomaliza alimsogelea Gabriel "tumbo lililokubeba libarikiwe, mikono iliyokubeba ikumbukwe milele, maana ndiyo iliyokufanya kuwa mbarikiwa leo, basi Mungu na akupe mke aliyebarikiwa kama ulivobarikiwa wewe" mama aliwabariki sana. Majiran hawakuamini kabisa, kila mmoja alihisi kama wanaota kwa maana nyumba iliyokuwa inajengwa mtaa mzima hakuna mwenye nayo, nyumba iliyosimamiwa na mafundi kiboko zaidi ya wawili, kiwanja chote kilizungushiwa fensi na get kuwekwa. Ama kweli ujio wa Jackline uliwaneemesha wengi walioko pale mtaani, vijana wasio na kazi walipata vibarua, kila mmoja alimzungumzia Jackline kwa mema. Enzi za utoto Jackline alikuwa hapendwi na mama sababu katika mimba yake baba alitukimbia basi chuki yote ya baba ikahamia kwa Jackline, "mtoto aliyeishi kwa shida shida leo ndo mkombozi wa mama yake." majiran hawakusita kuyaongea

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "jaman natamani Jackline angekuwa mwanangu, jumba hili lote kamjengea mama yake" kila aliyepita eneo lile alistaajabu kuona mabadiliko makubwa kiasi kile. Jackline alimjengea mama yake jumba La kisasa ndani ya wiki mbili, umeme na vitu vya ndani kila kitu kilikamilika nyumba ikawa tayari kutumiwa ila mama alikataa kuingia akidai ananihitaji mimi pia na sherehe ifanyike, "nitakuja ila kwa Sasa nimesafiri niko China" nilimjibu Gabriel ambae alitoa amri kuwa Lazima niende "sherehe na pesa kipi bora,?" Nilijibu kwa kiburi sana walihisi nikiongea na mama huenda nitaogopa "Jackline si yupo huko Ina maana hiyo nyumba huwezi ingia bila ya mimi" nilimjibu mama yangu kwa dharau "kwanza hizo pesa za kukujengea mtu mwenyewe ushazeeka si bora wangekuja kuishi na wewe huku mjini" nilizidi kujitenga na upendo wa mama yangu kwa maneno ya kashfa na kujiinua "nisamehe mwanangu, tatizo ninahamu ya kukuona mwanangu" kwa upole mama alijishusha "picha yangu iko kwenye simu ya Jackline unaweza kunitazama" Gabriel alipoona majibu machafu yameanza kunitoka alimnyanganya mama simu na kuongea na mimi, kabla hatujaanza kuzozana na Gabriel kwa mbali nilisikia kama Jackline anapiga kelele ishara za kuhitaji msaada. "Gabriel mama! Nooo mama umekuaje" kwa kuwa hawakukata simu nilisikia yote kuwa mama amedondoka kapoteza fahamu, niliposikia vile nilishtuka sana, nilikaa kimya kusubiri kama watanijulisha kilichojiri japo tayari najua mama alidondoka na kupoteza fahamu.

    Mama yetu alidondoka na kupoteza fahamu hivyo walimpeleka hospital kwa msaada zaidi. Jackline alikuwa akilia kama mtoto "mama yangu, Gabriel tumuombee mama" Gabriel kwa uchungu alimkumbatia Jackline na kumpooza, wakiwa pale nje walimuona daktari akitoka kwenye chumba alichokuwa mama, macho yake yahuzuni, midomo yake ikiwa mizito kuongea, aliishia kupumua tu, wakati bado wanasubiri aongee, kwenye koo cha dirishani Jackline alishuudia mama yake akifunikwa na shuka hadi usoni ishara tayari mama ametoweka duniani, kama vile swala alivo mwepesi kukimbia ndivo ilivokuwa kwa Jackline, aliponyoka kwenye mikono ya Gabriel na kukimbilia chumbani kule, alimsukuma nesi aliyekuwa anamfunika mama kisha alimfunua mama yetu aliyekuwa amefumba macho yake, "nooooooooooooooo.... mamaaaaaaaaaa...... Nooooooooooooooo" Jackline alipiga yowe ambayo hakuna aliyetegemea hatimae alishindwa kulia, hakuweza hata kuongea tena zaidi alimlalia mama kisha alianza kuuchezea uso wa mama kwa mikono yake, machozi yalitoka kama maji, daktari alishauri wasimsemeshe ivyo wakamuacha "mama kesho wageni wanakuja Ili uamie kwenye nyumba yako, basi amka twende tukafanye maandalizi" Jackline hakutaka kuamini kama mama yake ameshafariki "mama ebu amka bana twende nyumbani" Jackline alibadilika pale pale na kuwa chizi. "nipeni mama yangu, huyu si mama yangu" alimgeukia daktari na kumkaba koo "mamaaaaaaaaaa," Jackline alilia kilio ambacho asikwambie mtu, hakielezeki. Hakutaka kuamini kama mama yake amefariki

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog