Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

BLOOD DEAL - 2

 







    Simulizi : Blood Deal

    Sehemu  Ya Pili (2)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Baada ya wiki tatu hofisi zote za marehemu Emanuel zilikuwa zikiendelea kufanya kazi zikiwa chini ya usimamizi wa David kwa huo muda mfupi, hakuwa na roho mbaya kama kipindi cha mwanzo enzi ya uhai wa kaka yake, hali hiyo Iliwashangaza baadhi ya wafanyakazi ndani ya hofisi hizo tatu mbili zikiwa za usafirishaji na moja ikijihusisha na mitandao achilia mbali hoteli na maduka ya nafaka pamoja na ya simu, ilikuwa ni lazima jioni apite kila hofisi kuangalia biashara ilikwendaje, hali hiyo ilianza kuibadili hakiri yake, tamaa mbaya ikaanza tena kuuandama ubongo wake dhidi ya shemeji yake.

    "babu shukamoo "

    "Mar haba mjukuu wangu vipi ulifanikisha? "

    "ndio babu ila natatizo tena "

    "niambie nitakusaidia "

    "nataka kukamaliza katoto ,ila kwa njia ya ajari, huwa kinakwenda shule kwa gari je babu unaweza ukanitengenezea ajari katika mambo yako ".

    David aliongea bila huruma usiku huo baada ya kutoka kazini, hakuwa na hofu na mganga wake mwenyeji wa kasuru mkoa wa kigoma, mzee huyo alikuwa akifahamika Kwa jina la Songoro aliekuwa amejaliwa ujuzi mkubwa katika ulozi, na ndo huyo huyo aliempatia David dawa za kujikinga endapo yangetokea ya kutokea baada ya kumua kaka yake.

    "usijali mjukuu nitumie picha yake ndani ya siku moja " aliongea mganga huyo kwa kujiamini

    "sawa nitaituma kesho mchana "

    David alikata simu ,alipiga makofi ya ushindi, picha ya poul mtoto wa kaka yake aliekuwa ndani ya jeneza ilianza kupita ndani ya ubogo wake.

    Kwa kuwa hakuwa na picha yeyote ya mtoto huyo ndani ya nyumba yake alipanga kesho kwenda nyumbani kwao kuchukua picha hiyo ili akamilishe mambo yake.



    kichwa chake kiliendelea kuwaza mambo mengi sana , taswila ya kumiliki utajiri tayari ilianza kupita ndani ya ubongo wake ,alijiona jinsi anavyomiliki utajiri huo, akiwa kama boss, hakika David alikuwa duniani nyingine kabisa! Hakutaka kulala mapema alichofanya ni kwenda kuonga kisha alivaa pensi yeusi ya jinsi , tsheti nyeupe aliyoiambatanisha na marashi aina ya blue men, alichukua saa na kuitazama.

    "aaah! Bado mapema sana , acha nimtafute salama " David aliwaza huku akifunga mlango , Safari yake iliishia katika gari lake aina ya Rav4 ,alibinya ufunguo kabla ya kuingia lilifunguka kisha alifungua na kuingia.

    "Salamaa mtoto wa kimanga njoo Villa tutafune duniaa "

    David aliongea baada ya simu kupokelewa, upande wa pili, katika wanawake David aliokuwa akiwakubali Salama alikuewemo, kwanza alijua kutumia pesa, pili alijipenda, hakuwa mtu wa mariongo ,alijariwa umbo zuri ambalo kila mwanaume aliepita mbele yake lazima shingo igeuke , sauti yake tu ilikuwa na uwezo wa kumtoa nyoka pangoni , kitandani usiniulize.

    Kutoka pansiasi hadi Villa hakukuwa mbali sana na ukizingatia usiku hakuna foleni, alijikuta akitumia dakika saba tu, akawa ameegesha gari lake,sehemu sahihi, hakuta kushuka haraka, alichofanya alikiegemeza kichwa chake, juu ya kiti baada ya kukikunjua, alifungua radio pole pole alianza kusikiliza mziki huku akiendelea kumsubili Salama.

    "khoook!Khoook!"

    Sauti ya kugongwa kwa dirisha la gari lake ndio iliyomshtua David, hakuwa na haraka sana maana alijua ni Salama tu ,kweli mawazo yake hayakukosea alimfungulia mlango.

    "niambie mme wa mie "

    Salama alizungumza huku akimbusu David mdomo, nae hakuwa nyuma alimpokea kwa mikono miwili

    "leo kula pesa yangu kadri unavyojua, jichetue ujuavyo linga mtoto wa kike" David alizungumza hayo baada ya wote kuachiana, hakutaka kukaa sana ndani ya gari,walishuka na kuingia ndani ya Club hiyo, ambayo ni maarufu na ni pendwa kwa wakazi wa mji wa mwanza.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Saa kumi na moja alfajili ndipo walipotoka ndani ya club hiyo, David alimpitisha Salama nyumbani kwao kisha alielekea kwake!,Kwa kuwa ilikuwa jumapili, hakuwa na haja ya kuamka mapema sana, alilala hadi saa sita mchana, kisha alielekea nyumbani kwa marehemu kaka yake, kichwani akiwa na lengo la kupata picha ya Poul kwa njia yeyote.

    "waaooooo Baba shikamooo "

    "mar -haba hujambo mzee wetu "

    David alijibu salamu hiyo huku akimnyanyua kutoka chini na kumpakata, kisha alianza kuelekea ndani.

    "Safi sana umekwisha! " Alijikuta akiwaza maneno hayo huku macho yake yakimtazama mtoto Poul aliekuwa amejawa na tabasamu usoni mwake, laiti angefahamu huyo alikuwa adui yake namba moja duniani, asigedhubutu kumsogelea,

    "Mama yuko wapi? "

    "Kalala "

    "aaaah!, Kamwambie nimekuja "

    "sawa "

    Poul aliondoka eneo hilo akikimbia kuelekea ndani, huku nyuma, David akimtazama kwa uchu kana kwamba alikuwa akitamani kumtafuna mbichi mbichi!. Akiwa katika lundo la mawazo Janiphar shemeji yake alitokea sebuleni hapo.

    "nakuona mke mwema "

    "shemu huuishiwi na maneno " Janiphar aliongea huku akikaa na kumpakata mwanae.

    "Unajua nataka nikuridhi, hahahaha! "

    David alichomeka utani hali iliyopelekea wote kucheka kwa furaha, ili asijulikane adhima yake, alishinda hapo siku nzima huku tayari akiwa amefanikiwa kuchukua picha ya Poul, kupitia simu yake ya mkononi.Safari yake ilianzia studio iliyopo karibu kabisa na sheli ya moili raundi abauti ya mwalimu Nyerere, mkakabala na benki ya stabick.

    "Babu kila kitu kipo tayari, na nimeituma kabisa ipokee kesho katika basi la Zuberi "

    David aliongea baada ya kukamilisha zoezi la uchapishaji wa picha hiyo, kisha alielekea hofisi za mabasi yaliyokuwa yakienda kigoma, mtaa wa natta barabara ya Igoma.

    "Sawa babu kesho kutwa utaona jibu, si tayari na majina yake umeyaandika kama nilivyokueleza? "

    "Ndio! "

    "Tegemea ushindi, mjukuu wangu "

    "nitafurahi sana babu! "

    "Lazima ufurahi "

    "hahahaha! "

    David alimalizia kwa cheko, kubwa na lenye ushindi mkubwa ndani yake, siku hiyo hakutaka kwenda kokote, kutokana na uchovu wa jana aliamua kwenda nyumbani kwake moja kwa moja bila kumpitia msichana yeyote.

    ******

    "Mama leo siendi shule "

    Kwanini Poul? "

    Mama yake alimuuliza huku akiendelea kunyosha nguo za shule za mwanae, asubuhi ya jumanne.

    "sitaki tu nimemkubuka Baba, harafu hutaki kuniambia baba yuko wapi? "

    "Puuuuh!,

    Mama yake alishusha pumzi ndefu, kisha aliichomoa pasi kwenye soketi na kumsogelea mtoto wake ,aliekuwa amelala chali macho yakimtazama Mama yake.

    "Nikweli mwanangu, naomba uende shule ukirudi tu nitakuelezea kuhusu Baba atarudi lini, sawa Baba? "

    Japo Janiphar alizungumza maneno hayo, huku akitoa tabasamu, tabasamu hilo lilikuwa la bandia tu , moyoni aliumia alihisi moyo ukivuja damu, lakini hakutakiwa kumuonesha picha hiyo mwanae.

    "Kweli Mama na utanipeleka? "

    "Ndio, ni.... nit.. akupe.... leka "

    Alijikuta akishindwa kuongea vizuri, baada ya kukabwa na kitu kizito kooni.

    "Naenda kuoga mwenyewe leo "

    Poul alizungumza huku akitupa pembeni shuka, alivua pensi na kujifunga taulo la Baba yake , vitendo vyote hivyo mama yake alikuwa akivitazama tu, ila kilichomuhuzunisha zaidi ni kitendo cha mwanae kujifunga taulo la mmewe, chozi jembamba lilianza kutiririka na kulowanisha kope zake.

    "Masomo mema baba "

    "haya Mama, nikirudi unaniambia sawa? "

    Mtoto Poul aliongea, maneno hayo huku akimbusu mama yake mkononi, kisha alipanda ndani ya school bus, safari ya kuelekea Alliance international school ilianza. Hadi bus hilo linapotea machoni mwake Janiphar alikuwa bado ameganda eneo hilo akiyatafakari maneno ya mwanae!, Taratibu alianza kuondoka eneo hilo kwa unyonge usioelezekea, hofu kubwa ikaanza kuushambulia moyo wake, mawazo mabaya kwa mwanae yakaanza kupita ndani ya kichwa chake.

    "Kunanini? "

    "Kwani vipi Mama? "

    Janiphar alijikuta akishtuka ,baada ya kuulizwa swali hilo na Mama mkwe wake ambaye alikuwa bado nyumbani hapo pamoja na baadhi ya ndugu wengine. Alibaki ameduwaa asijue cha kuongea, hata hakujua amefikaje sebuleni hapo, alichokuwa akikikumbuka ni uwepo wa yeye barabarani, sasa ndani humo ameingiaje?, nani aliemfungulia geti?.

    Kutokana na mawazo mengi kumzidia alijikuta akitembea bila kujua.

    "Tuambie mama tatizo nini? "

    Mama mkwe aliendelea kumdadisi baada ya kumuona amebadirika ghafla,

    "hata sijui nasikia moyo ukiniuma sana "

    "Pole sana mama punguza mawazo mwanangu "

    Mkwe wake alisema hayo huku akimkalisha chini.

    "Griiiiiii! Griii"

    Mlio wa simu ya Janiphar ndio uliowashtua wote , haraka bila kuchelewa aliichukua kutoka juu ya meza, alimwangalia mpigaji, lahaullaa! Alihisi moyo ukichomoka ndani ya kifua chake, baada ya kukuta jina la dereva wa poul, hakuweza kuipokea simu hiyo kutokana na mikono kutetemeka, moyo ukienda mbio, taarifa za habari mbaya zilianza kujitengeneza ndani ya hakiri yake, iliita hadi ilikatika yenyewe. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mama mbona hujapokea si... ?"

    Hakumalizia , mara simu iliita tena, mama mkwe ilibidi aichukue na kubofya kitufe cha kupokelea, kisha aliiweka sikioni.

    "Halo! "

    "Kuna tatizo limeji.... "

    Hakuweza kumalizia alikatishwa

    "nini? "

    "Ndio, tumepata ajari hapa Natta, mtoto wenu ame.... "

    "mamamamamamama weeeee Poul mwanang... "

    Mama mkwe alishindwa hata kusikiliza vizuri, alijikuta akilia kwa sauti ya juu, hali hiyo ilipelekea kila mtu kuacha kile alichokuwa akikifanya, kelele za vilio zianza kusikika ndani ya nyumba hiyo, kila mtu alijua Poul amefariki, Mama yake tayari alikuwa ameshazimia ,alijuta kumlazimisha mwanae kwenda shule, laiti angemsikiliza yote hayo yasingetokea.

    Ilibidi dereva wa familia hiyo aliekuwa akifahamika kwa jina la Dominic, atoke nje akiwa na simu ya boss wake, ndani hapakufa tena, alitafuta namba za Dereva huyo katika kitabu cha namba, huku akitetemeka alitafuta jina hilo na kupiga kabla ya kuweka sikioni.

    "Niambie mwanangu Poul amekufa?"

    Domi aliuliza huku naye akilengwa lengwa na machozi, miguu ikikosa nguvu,

    "hajafa ila yupo hospitali ya Aghakhan hali yake mbaya sana, katika wote yeye ndie alieumia sana"

    Dereva aliongea huku akitetemeka kupita maelezo,

    "daaaah! Ilikuwaje mwanangu? "

    "Hata sijui lori lilitokea wapi?, nimeingia freshi barabara ya Igoma, ghafla lori lilitoea ubavuni na kunigonga kwa nyuma hali iliyopelekea bus letu kuanguka, huku Poul akikandamizwa na kiti kifuani ."

    Alitoa Maelezo hayo kisha alikata simu.

    "Jamani Poul hajafa yuko Aghakhan, twendeni "

    Hakuna alietaka kubaki nyumbani hapo, kwa masada wa ndugu Janiphar alisaidiwa kutembea, kuelekea kule gari lilikuwa limepakiwa.

    Kweli walifanikiwa kumkuta Poul akiwa katika hali mbaya sana, mwili wake karibia wote ulijaa madonda, jinsi alivyokuwa akitisha haikuwa rahisi, kuamini kama alikuwa mzima,

    Ilibidi wakae kidogo kusubili majibu ya daktari, nusu saa waliweza kuonana nae, aliwapa matumaini ya mwanao kupona japo alikuwa ameumia sana kifuani , kisha wengine waliondoka wakimuacha Mama yake na Bibi yake kumuangalia.

    *****

    Kazi ya kutengeneza ajari ya kiini macho haikuwa ngumu sana kwa mzee Songoro, baada ya kuipokea picha hiyo majira ya saa mbili usiku, hakutaka kulala , aliichukua na kuitumbukiza ndani ya dawa nyeusi, huku akizunguka zunguka eneo hilo, mkononi alishika usinga mweusi, dakika tano aliitoka na kuiweka ndani ya ungo uliokuwa umejaa kila aina ya dawa, alileta kioo kilichokuwa kimevikwa kitambaa chekundu na cheupe nacho alikitumbukiza ndani ya ungo huo, alichukua dawa iliyokuwa na asili ya kimiminika, kidogo alimimina ndani ya kiganja chake na kukipakaza kioo hicho kwa juu huku chini yake akiwa amekandamiza picha ya Poul, vitendo hivyo viliambatana na maneno aliyokuwa akiyatamka kumuita Poul.

    Dakika saba, sura ya mtoto Poul ilitokea juu ya uso wa kioo, hapo hapo aliachia tabasamu, alichukua dawa nyeupe na kuipaka sura hiyo, dawa hiyo ilimsaidia kuyatambua majina yote ya koo mbili ,kwa Mama na kwa baba, akiwa katika zoezi hilo ghafla yalitokea majina yote, hivyo akawa ameimchoma kisu kikali picha ya Poul sehemu ya kifua.

    Baada ya zoezi hilo alichukua, ile picha na kuifunga ndani ya karatasi kisha aliweka tena, juu ya kioo na kuanza kuongea maneno yake, mara juu ya kioo ilianza kuonekana school bus ya akina Poul, hapo hapo alianza kutengeza ajari ,kwanza alitengeneza eneo sahihi la ajari itakapotokea, akimpiga upofu dereva, baadae alichomeka lori feki litakalo ingonga gari la shule. Hakutaka kulala aliondoka kigoma usiku huo hadi jijini mwanza akiwa ndani ya umbo la bundi, safari yake ilianzia Natta alipopawagia, kisha alienda kuliwangia school bus na hata kiti alichota mtoto Poul kukaa alikiwangia, akiuchochochea moyo wake kukaa pale pale.

    "nimemaliza subili matokea kesho! "

    "Kweli mzee? "

    David aliuliza kwa shauku ya hali ya juu, hakuamini kama kazi hiyo ingekuwa rahisi kiasi hicho . Furaha ilizidi kuongezeka kadri muda ulivyokuwa ukiyoyoma, hakuweza kupata usingizi mapema hadi jongoo wa kwanza kuwika alikuwa macho , saa kumi na nusu ndipo alipopitiwa na usingizi, alikuja kushituka jua likiwa limechomoza.

    "acha nimpigie Baba simu, najua ataniambia tu "aliwaza hayo huku akiiangalia saa iliyokuwa ikionesha saa mbili na nusu asubuhi.

    "Shikamo Baba "

    David alisalimia baada ya simu kupokelewa, sauti yake tu ilionesha hali mbaya

    "vipi mzee mbona unaongea kinyonge hivyo? "

    David aliuliza swali hilo ma kusudi ila tayari alikuwa ameshaanza kuhisi jambo.

    "Poul amepata ajali hali yake mbaya sana, kaumia kifuani ya... "

    Mzee huyo alishindwa kuongea vizuri, maumivu ya kuondokewa kwa mwanae yalikuwa bado yakiisumbua hakiri yake, leo tena mjukuu wa pekee alieridhi jina lake nae amepata tatizo kubwa, na linaweza kupelekea kupoteza maisha yake! Kweli alikuwa na haki ya kulia.

    "Pole sana Baba je yuko wapi kwa sasa?".

    Aliuliza David huku akiwa amechanganyikiwa, hakupendezwa na taarifa hizo, alichotaka yeye ni kusikia taarifa ya kifo si majeruhi.

    "nitaenda kuongea na daktari "

    Aliwaza hayo huku akinyanyuka kitandani.



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alibaki ameduwaa kama dakika tano baada ya kukata simu, taarifa za kujeruhiwa kwa mtoto Poul hazikukaa vyema ndani ya mtima wake, pamoja na kichwani, alichokuwa akifikiria yeye ni kifo tu! Si majeruhi.

    "Nitaongea na dokta ".

    Alizidi kuisistiza kauri yake, hakutaka tena kulala, alinyanyuka na kuelekea bafuni alikokoga haraka haraka na kutoka, alivaa vazi la kinaijeria alilowahi kununuliwa na kaka yake pindi alipohitimu shahada ya biashara, miaka miwili iliyopita.

    "sijui nianzie hofisini? Au acha nielekee hospitali. "

    Njia nzima aliongea peke yake, muda mwingine aliweza kutoa maneno ya kashfa pindi alipokwaruzwa kidogo, hakuwa David wa siku zote, hasira alizokuwa nazo dhidi ya Poul hazikuelezeka.

    "Shikamoo mama "

    "mar haba, kwema huko? "

    "Kwema tu, vipi anaendeleaje? "

    David aliuliza huku usoni akiweka huzuni ya bandia, baada ya kufika hospitalini hapo,

    "Bado mtoto kaumia vibaya sana, lakini majibu ya daktari yanatushangaza!"

    "Kwani vipi? "

    "Inaonekana hajaumia kokote, wakati yupo katika hali mbaya sana, kila kipimo alichofanyiwa hakuna tatizo, Chest T-scan nayo wamefanya kuangalia kama kuna mfupa uliovunjika ama la, jibu hakuna, hakuna damu iliyovujia kwa ndani, hata hatuelewi "

    Aliongea bibi yake Poul kwa majonzi makubwa.

    "Mama yake yuko wapi "

    Alioneshwa na kuelekea eneo alilokuwa Janiphar, waliongea mawili matatu kisha aliomba kumuona mtoto aliekuwa Icu, kwakuwa ilikuwa hospitali binafsi hakukuwa na pingamizi. Macho yake yalikereka sana kumkuta Poul akiwa hai japo alikuwa akipumlia mashine ya oxygen, dripu za maji na damu zikiendelea kuingia ndani ya mwili wake, wa kitoto kupitia mishapa ya damu .

    "Pole sana shemeji, mungu atatusimamia, je kuna daktari yeyote aliechukua jukumu la kumhudumia?"

    Aliuliza David, wakiwa wanatembea kutoka ndani ya wodi hiyo

    "ndio nimemkabidhi kwa Dokta Atanasi rafiki mkubwa wa marehemu mme wangu, najua hataniangusha "

    "aaaah! Kwe..kweli, umefanya vyema " alijikuta akipata kigugumizi cha ghafla mara baada ya kusikia njina hilo.

    Dokta Atanasi alikuwa rafiki mkubwa sana na marehemu Emanuel , urafi wao ulizaliwa siku ambayo mzee Poul ,Baba mzazi wa marehemu Emanuel na David, alipougua ghafla presha ya kupanda, majira ya sasa mbili usiku, wakiwa ndani ya gari wakielekea nyumbani. Japo Dk. Atanasi alikuwa bingwa wa upasuaji, alijikuta akiwaonea huruma kutokana na hali mbaya akiyokuwa nayo mzee huyo, alichofanya usiku huo huo alimpingia simu Dk. Andrew akimsistiza kufika hospitali hapo, ilikuwa ngumu sana kwa Dk. Andrew kufika hospitali hapo usiku huo, ukizingatia tayari alikuwa amelala, kitendo hicho kilimfanya Emanuel kuwa karibu sana na Dk. Atanasi kwa muda wote aliokuwa amelazwa mzee wake hospitalini hapo.Hata baada ya kuagwa Emanuel hakusita kumsalimia japo kwa simu na muda mwingine waliweza kukutana na kuzungumza.

    Taarifa za kukabidhiwa mtoto huyo kwa Dokta huyo, hazikumfurahisha David hata kidogo, toka uhai wa kaka yake, David na Dk. Atanasi walikuwa paka na panya kisa kikiwa msichana, japo Dk. Atanasi alikuwa ameoa lakini michepuko haikukosekana na mbaya zaidi aliwahi kuchepuka na msichana wa David aliemtoa kijijini kwao Simiyu. David alibaki na hasira hiyo hadi leo, hakuwa na roho ya kusamehe.

    "nifanyeje? "

    Alijikuta akiwaza peke yake, lakini hakupata jibu, ghafla alitoka ndani ya hospitali hiyo kwa kasi ya ajabu, lakini kabla hajatoka nje ya geti, alikutana na kijana, mwembamba na mrefu, macho yake yalipendezwa sana na sura ya kijana huyo, alionekana ni mwanafunzi wa udaktari, japo alikuwa mwanafunzi akiekuwa akisomea udaktari ,pia alionekana wa hali ya chini sana, hata mavazi yake tu yalitosha kumtambulisha haiba yake,

    "yes (ndio) nitamtumia huyu huyu! "

    David alijisemea peke yake, kisha aligeuka na kuanza kumfuata,

    "samahani Dokta "

    "bila samahani ndugu "

    "sijui naweza kuongea na wew? "

    David aliongea huku akiwa amemkazia macho, alichongundua haraka sana kutoka kwa Daktari huyo alikuwa akisumbuliwa na njaa, pamoja na mawazo yaliyopelekea kuonekana kijana kama mwanzo alivyomtazama, kumbe hakuwa kijana wala mwanafunzi, ila ukata ulimfanya apoteze hadhi yake.

    "kwa sasa sina muda, nipe dakika ishilini nitakutafuta baada ya kutoka kunywa chai "

    "aaah! Ingekuwa vyema sote tungeambatana, maana hata mie sijapata huduma hiyo "David aliongea huku akiachia tabasamu, uso wake akiupamba kwa furaha ya ulaghai laghai.

    "mie naenda kunywa chai ya hofisi ina... "

    "aaaah! Dokta heshima yote hiyo bado unakunywa chai ile ile ya mandazi ya mia na vitumbua vya mamantilie jamaniii "

    "hahahaha (alicheka kwa aibu ),heshima wapi kaka njaa tupu "

    Nae alijaribu kuongea huku akibandika tabasamu usoni, ambalo David alilitambua haraka sana.

    "wew wa kunywa supu, bhana twende " aliongea huku akianza kuondoka eneo hilo, akimuacha Dokta huyo akijishauri, mita chache David aligeuza Shingo na kumtazama Dokta huyo, nae kuona vile alianza kumfuata.

    "Hapa hapa! " Aliwaza hayo huku akimfungulia Daktari huyo mlango, kisha nae alizunguka upande wakeCHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "nimesahau nikatoka na koti hili "

    "unaweza ukalivua, wala usijali "

    Hakuna alieongea tena, hadi gari hilo linafunga breki ndani ya maengesho ya Glod crest hoteli, mkabara na mwanza hoteli, walishuka na kuingia ndani.

    "Agiza unachotaka, mie nipe maji makubwa ya Kilimanjaro na supu ya mbuzi bila chochote ".

    Nusu saa tayari walikuwa wameshamaliza kunywa supu, Safari ya kulejea hospitali ilianza, lakina kabla hawajafika hospitalini hapo, David aliegesha gari lake na kumtazama Dokta huyo, alieonekana bado anasumbuliwa na kitu flani

    "naitwa David naishi pansias , kazi yangu biashara , sijui unaitwa Dokta nani? "

    "Dokta Eddyson Swai, mwenyeji wa mkoa wa moshi, kwa hapa mwanza naishi Nyakabungo "

    "haaaaa! Dokta? "

    David alishangaa, hadi alishika kichwa, hakuamini ,Kama Daktari huyo anaweza kuishi eneo hilo, Nyakabungo ilisadikiwa kuwa ni mtaa uliojaa vibaka si mchana wala usiku, uswahili uliopitiliza na sifa nyingine ni idadi kubwa ya kabila la wakurya, ambao husemekana ni wakorofi kupita maelezo , zaidi na zaidi hakukuwa na majengo mazuri zaidi ya vijumba vidogo na vifupi, vilivyojengwa bila utaratibu ,kwa wakazi wa mwanza Nyakabungo ilitambulika kama ushashini.

    "Nini?"

    "wewe wa kuishi Nyakabungo? "

    "Eeeh !"

    "Hapana, naomba nikupatie nyumba ya kuishi, iko Nyakato National kama utakuwa tayari, na je umeoa? " Safari hii aliongea kwa upole na umakini wa hali ya juu , alikuwa na kazi moja tu, ya kumrubuni Dokta huyo, kwa kutumia umasikini wake ama tamaa ya pesa, angeweza kufanikisha adhima yake.

    "Ndio namke na watoto wanne, pia nipo tayari kupokea msaada huo " alizungumza kwa sauti ya chini, yenye asili ya kukata tamaa kabisa.

    "Hata leo naweza kukupa nyumba hiyo endapo utanisaidia nami kitu kidogo " David alizungumza bila kumtazama

    "nini hicho? Nitakusaidia, maana hata wewe umenisaidia pia "

    "ok sawa, je upo Aghakhan kwa muda gani? "

    "Miezi ishirini na sita sasa "

    "sawa mshahara unalipwa bei gani? "

    Dk. Eddyson alijikuta akikaa kimya kwa muda huku macho yakiwa yametazama nje , alipokuja kumtazama David alikuwa akilengwa lengwa na machozi.

    "Silipwi mshahara wowote kwa sasa hadi miaka mitatu ipite... "alianza kusimulia

    "kwanini? "

    "Miezi tatu kuajiriwa hapa nilijikuta nikipoteza mashine ya T-scan baada ya kuvamiwa na majambazi , majira ya saa tano asubhi nilipokuwa natoka uwanja wa ndege kuipokea, kwa kuwa nilikuwa Daktari mkubwa kuliko wote katika swala la upasuaji, nikitokea hospitali ya Muhimbili, hofisi iliniamini sana kutokana na utendaji wa kazi toka nikiwa Muhimbili"

    "kwanini ulitoka Muhimbili? "

    "masirahi yalikuwa madogo na mbaya zaidi mshahara hautoki wakati mwafaka, ukitoka ni wa mwezi mmoja tena wa deni, sasa unajikuta hujapata mshahara wako hata miezi sita! "

    Dk Eddyson alizidi kuongea kwa hisia ya hali ya juu.

    "Pole sana ,hiyo mitihani midogo midogo tu, na tambua wakati wako wa kufurahi umewadia! Endapo utanisaidia tu!".

    *****

    "Nitakusaidia! "

    "Ahsante sana, kuna mtoto ameletwa hapo leo asubuhi, akiwa na hali mbaya chanzo kikiwa ni ajari, sijui umemsikia? "

    "Si kumsikia tu bali nimehusika hata kumtibu nikiwa na Dk Atanasi , si kile cha kiume kirefu maji ya kunde? "

    "Eeeeh!, hicho hicho "

    "vipi nikisimamie kwa hali ya juu? "

    "Hapana, nataka ukamchome sindano ya sumu itakayomuua baada ya miaka mitano ,mama yake nae mchome damu ya virusi vya ukimwi, utapata nyumba na gari hili".

    Aliongea huku akiwa amemtazama machoni, maneno yake hayakuwa na utani hata kidogo, akichokuwa akisema alikimanisha.

    "puuuuuuuh! "Dk. Eddyson alishusha pumzi ndefu, kabla ya kuongea chochote.

    "kwanini? "

    "Wazazi wake wamehusika kumuua kaka yangu, huko Afghanistan, sijui unamfahamu tajiri Emanuel Poul anaemiliki kampuni la sasatel hapa Tanzania? "

    "hua nasikia tu, ukizingatia mie mgeni hapa "

    "basi huyo alikuwa kaka yangu, ameu.... "

    David hakuweza kuongea , alijikuta akianza kulia, kilio cha utapeli wa fikla, na ili lengo lake litimie alitakiwa acheze na hakiri za Dokta huyo.

    "pole sana"

    "naumia sana kuwaona wakiishi duniani, huku familia yake ikiteseka "

    "kimoja nitakusaidia, ila kingine sidhani "

    "kipi? "David akiuliza, huku mkono wake ukiyafuta machozi bandia

    "dhambi kumuua malaika, ila kwa mama yake ni kazi rahisi sana, kazi hiyo nitaifanya baada ya mtoto kutolewa icu, najua Mama yake atakuwa akilala na mwanae "

    Dokta Eddyson alijikuta akikubali Kumuangamiza Janiphar bila kujua chanzo sahihi cha yote hayo! Hali ngumu ya kimaisha inapelekea yeye kutaka kufanya ukatili huo.

    "kuua hapana! Naogopa, ila ukimwi kawaida tu maana siui atakufa mwenyewe taratibu "

    Dk.Eddyson aliwaza hayo,picha ya maisha mazuri ilianza kuutesa moyo wake,

    "sio mbaya tekereza kama ulivyokusudia, ukienda tofauti na hilo tusilaumiane , pia utakuwa rafiki yangu mkubwa na nitakufanya uache kazi hiyo ya kusubili pesa mwisho wa mwezi , tena ukiwa na mawazo chungu nzima "

    "nitashukru sana "

    "kingine tunza siri hiyo ".

    Ilibidi David akubaliane na wazo la Dk. Eddyson, kuondoka kwa Janiphar kungemsaidia kumuua Poul kiurahisi sana , pia angejikuta akiziendesha biashara zote na mwisho wa siku angekuwa ndie mmiliki halali wa mali hizo. Ilibidi David amrudishe Dk Eddsyson kazini kwake, kisha nae aliondoka , akiwa na mawazo chungu nzima.



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    DK Eddyson alianza kutembea taratibu kuingia hofisini kwake, mkononi alishika koti lake la kazi, alionekana mtu mwenye mawazo sana, kweli hakiri yake ilikuwa imevurugwa kupita maelezo, nafsi mbili zilizidi kushindana , moja ikipinga shauri hilo, ila nyingine ilizidi kumtia nguvu, ikimtamanisha maisha mazuri.

    "puuuuuuuuuh! ".

    Alishusha pumzi ndefu, akiwa ameegemeza mikono yake juu ya meza, akiwa amesimama, hakujua achague lipi kati ya kutekeleza ama kukataa.

    "my Jesus (Yesu wangu), lakini kanuni na taratibu za udktari hazi r..... " alishindwa kuyaendeleza mawazo yake, baada ya kukatishwa na ujumbe mfupi uliongia katika simu yake. Ukitoa sauti ya juu sana.

    Haraka sana aliitoa simu hiyo ndani ya mfuko wa shati, alienda moja kwa moja upande wa meseji, ili kujua ujumbe huo ulitoka wapi,

    "mmmmmh "aliguna baada ya kuona Meseji hiyo, akiwa haamini hata kidogo, kitendo cha kupokea laki tisa kutoka kwa David, kama moja ya malipo kilimtisha na kumshangaza sana, alibaki ameduwaa huku akiwa ameitumbulia macho simu yake.

    "duuu! Mtihani kweli, huu je nimchome? Aaah! Potelea mbali dhambi ngapi nimefanya?, pesa kwanza maisha yangu "

    Dk. Eddyson alijikuta akidhamiria kufanya kazi aliyotumwa na David, na kilichomchanganya zaidi ni zile laki tisa, tayari zilikuwa zimeshapata kazi, jioni hiyo hiyo alipanga kupita bar kidogo, kama ishara ya kujipongeza! Kwa kazi ndogo iliyokuwa mbele.

    ******

    Baada ya David kumrudisha Dk. Eddyson kazini kwake, yeye alielekea moja kwa moja Nyakato National majanini, huko kulikuwa na moja ya nyumba aliyokuwa ameijenga marehemu kaka yake, bila kumshirikisha mkewe zaidi ya kumshirikisha mdogo wake David,hata hati za nyumba alikuwa nazo David. Kama ujuavyo wanaume huwa hawana utaratibu wa kuwashirikisha wake zao baadhi ya mali, wakiamini mwanamke hatakiwi kutambua kila kitu anachokifanya mwanaume, hivyo hata Emanuel hakuwahi kumshirikisha mkewe baadhi ya mali, ikiwemo nyumba hiyo, iliyokuwa bado haijakamilika vyema,

    "nitampa hii hii itamtosha ,ila akinizingua namuondoa duniani! "

    David aliongea huku akiuma meno kwa hasira, safari yake iliishia hapo alishuka na kuikangua ,baada ya zoezi hilo aliondoka akipitia ATM alikotoa kiasi cha shilingi milioni moja na laki mbili, laki tisa alimrushia ,Dk. Eddyson na zilizobaki alimtumia shemeji yake.Akimpumbaza.

    "Umeiona picha ya nyumba? "

    "Ndio!, Tena nzuri sana, tajarajia ushindi ndani ya siku tano, ama tatu"

    "mimi nimeshamaliza ,kazi imebaki kwako, unatakiwa ufanye sio ombi tena, tambua kuanzia sasa upo ndani ya Blood deal, nikimanisha mpango wa damu, maana kile unachokwenda kukifanya lazima damu imwagike ndo mpango wako ufanikishe, kuwa makini, nakupenda sana "

    David aliongea kwa msistizo sana, akimanisha alichokizungumza, daima hakuwa mtu wa kukata tamaa, ama kughairi, hakuwa na tabia hiyo , lazima afanye alichokiamu hata kama kingehatarisha maisha yake, ilikuwa ni lazima. Alikata simu na kuuma kidole gumba cha mkono, huku akiwaza kupita maelezo, dakika tano alipata wazo la kumtafuta Deus rafiki yake mkubwa.

    "Acha nimtafute Deus "

    Hapo hapo alichukua simu yake na kulitafuta jina la Deus, dakika moja alilipata , alibonyeza kitufe cha kijani kisha aliweka sikioni, sekunde mbili simu ilianza kuita .

    "Dogo Safari hii umeamua sio masihara ".

    Deus aliongea baada ya kupokea simu

    "hasira niliyonayo hata nikikupunguzia, huna pa kuiweka kaka "

    "safi sana, huo ndio uanaume, mwanaume lazima awe shujaa , mwenye kujitoa tena kwa viungo vyote, na ikiwezekana hata kupoteza maisha yake, babu alinieleza kila kitu "

    Eeeeh! Kaka lazima nimalizie ,kama damu tayari nimeshamwanga, na mpango utimie "

    "hahahahaha! "

    Deus alicheka kwa furaha sana, hali iliyopelekea hata David kuunganisha cheko hilo. Kisha alielekea hofisini kwake bila kujua tena habari za Poul zaidi ya kusikia taarifa za kifo kutoka hospitali hiyo , muda mwingine alidriki hata kusali akimuombea mtoto Poul afe.

    ******

    Siku tano baada ya ajari, Poul aliruhusiwa kutoka ndani ya chumba cha wagonjwa mahuti huti, baada ya hali yake kutengamana, kwa asilimia sabini lakini alikuwa bado akilalamika kifua kilikuwa bado kikimsumbua sana, kwa upande wa Dk. Atanasi alikuwa makini sana kuhakikisha Poul anakuwa nafu kama si kupona kabisa ndani ya muda mfupi tu! Kila baada ya masaa matatu ilikuwa lazima apite kitandani hapo, ukaribu huo na umakini huo ndio uliochangia mtoto Poul kupata nafu kwa asilimia kubwa.

    "Mama "Poul alimuita Mama yake kwa sauti ya chini yenye maumivu ndani yake ,dakika moja Janiphar alibaki kimya bila kuitika akimtazama mwanae, hakuamini kama kijana wake angeweza kutoa kauri, picha ya ufu aliyokuwa nayo ndani ya chumba cha wagonjwa mahuti huti ilikuwa bado ikimsumbua.

    "Abee Baba "

    Alitika kwa unyonge huku akimtazama machoni, hakika alikuwa na huruma sana na maumivu makubwa ndani ya mtima wake , muda mwingine alitamani mmewe angekuepo.

    "niambie kuhusu baba ,siku ile ulikataa ndo maana niliumia "

    "hapana, sikukataa mwanangu "

    "haya Mama , baba yuko wapi? "

    Poul aliuliza huku akimtazama Mama yake usoni, macho yenye usiriazi na kile alichokiuliza, hakujali maumivu aliyokuwa akiyapata pindi alipozungumza, yeye alihitaji kufahamu wapi Baba aliko, tayari moyo na masikio yake vilichoka kusikia taarifa za Baba kuja kesho.

    "Pona kwanza mwanangu "

    "hapana mama ,niambie natakaaa"

    Poul alizungumza huku akianza kulia, Mama yake hakutaka hali hiyo itokee, kulia huko kungezidi kuongeza maumivu ndani ya kifua chake, ilibidi ambembeleze akimuahidi kumueleza ukweli wote, japo aliamini kufanya vile kungezidi kumuumiza hata yeye mwenyewe.

    "Baba hayupo mwanangu "alianza Kuongea, bila kumtazama mwanae, maumivu aliyokuwa akiyapata pindi asimuliapo habari hiyo ilikuwa siri yake na mungu wake

    "atakuja lini? "CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Haji mwanangu "

    "kwanini Mama, inamana hatupendi tena? Kumbe Baba mbaya akinidanganya ataniletea baskeli ha... "

    "shiiii! Sio hivyo Poul "

    "kumbe? "

    "Baba amefariki mwanangu "

    "amefariki? Ndo kwenda wapi? "

    Poul alikuwa na maswali kama mtu mzima, hata mama yake alimshangaa kupita maelezo , umri wake haukuendana na maswali hayo.

    "kufariki ni kuondoka duniani, hatakuja tena kutuona, hawezi kuja mwanangu, huna Baba tena, mpende Baba mdogo David, huyo ndie aliebaki pamoja na anti Agnesi, Babu na Bibi, sawa mwanangu "ilibidi Janiphar ajikaze .

    "Amefarikiiiiii, haji aaaaaah! "

    Poul alishindwa kuvumila alianza kulia sana, neno kutomuona Baba yake tena lilimuumiza sana, haikuwa kazi rahisi kumtuliza, alipotulia alipitikiza kusinzia kabisa.

    Janiphar alinyanyuka na kuelekea bafuni, alioga na kurejea, alijilaza pembeni ya mwanae aliekuwa bado amesinzia, akiwa ndani ya mawazo nae alijikuta akipitiwa usingizi, hiyo ndo ikawa nafasi ya Dk. Eddyson kutekele kazi yake, aliyokuwa ameipanga kwa muda mrefu, kila kitu kilikuwa tayari, damu yenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi ilikuwa imeshaandaliwa siku moja nyuma, tena ikiwa ndani ya chupa. Siku hiyo hakutoka hospitalini hapo, mara baada ya kugundua uwepo wa Poul ndani ya vyumba vya kawaida , kila hatu iliyokuwa ikitendeka alihakikisha anaifatilia.

    Baada ya kumuona Janiphar amepitiwa na usingizi alinyanyuka haraka sana akiwa na bomba mbili zenye damu hiyo pamoja na kichupa kidogo kilichokuwa na dawa ya usingizi, ndani ya koti lake, alitazama huku na huko kuhakikisha usalama wake, alipogundua hakuna akiemuona alinyata kuingia ndani ya chumba cha Poul na Mama yake ,taratibu akiurudisha mlango, kisha akitoa kichupa cha dawa ya usingizi , aliitikisa na alipohakikisha imekaa sawa alimpulizia Janiphar kidogo sana, maana ilikuwa Kali sana kisha alitoa bomba la damu iliyokuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na kumchoma nayo Janiphar kupitia ndani ya mshipa mkubwa wa mkono wake wa kushoto , huku akiwa amefumba macho, kiwa anamalizia kuchomoa sindano ya pili mara mlango ulifunguliwa, alihisi haja kubwa ikizichafua nguo zake, mwili wote ulianza kutetemeka asijue la kufanya.



    Dk. Eddyson hakujua afanye kipi? Moja kwa moja alijua ni Dk. Atanasi, haraka bila kuchelewa alizirushia bomba za sindano ndani kabisa ya shati lake , lililokuwa limechomekwa ndani ya suruali, kisha likafungwa kwa mkanda, kwa muonekano huo isingekuwa rahisi mtu yeyote kufahamu kilichokuwa kikiendelea.

    "Khook! Khoook! ".

    Alikohoa kikoozi kikavu, ili kumshitua mtu aliekuwa bado akiusukuma mlango

    "vipi Mama? "

    Dk. Eddyson aliuliza, mara baada kuufungua na kukutana macho kwa macho na mama mkwe wa Janiphar, kiasi alihisi, mwili wake ukipoa, mapigo ya moyo yaliyokuwa yanaenda kwa kasi, sasa yalipungua, picha ya kufumaniwa iliondoka hakirini mwake.

    "Aaaah!, Nilikuja kumuaga mie nataka kuondoka! "

    "OK, sawa ila kalala, sijui utafanyanje? "Dk Eddyson alizungumza huku macho yake makubwa kiasi , yalikuwa makini kumtazama mwanamke huyo, kujua kama aligundua ama la.

    "Basi nisimchoshe, kesho nayo siku nitakuja kuwatazama "

    "haya mama ".

    Kwa pamoja walitoka ndani ya chumba hicho, wakimuacha Poul na Mama yake wakiwa ndani ya usingizi,

    "haloo boss mambo tayari"

    "kweli? "

    "Ndio sasa nikutanie, keshaisha huyo, na nzuri zaidi nimemchoma chupa moja kabisa "

    Dk. Eddyson aliongea huku akicheka cheka, furaha aliyokuwa nayo, ndani ya moyo wake aliifahamu mwenyewe.

    "daaah!, safi sana, cha muhimu tunza siri hiyo milele "

    "kutunza siri, ni moja ya sheria ya udaktari, kwa hilo ondoa wazo "

    "basi sawa, naomba nikutakie usiku mwema, kesho tukutane Nyakato nikumalize kabisa "

    "haya ".

    Dk. Eddyson alikata simu na kubaki amesimama, moyo wake ulijaa furaha, hakuamini kama zoezi hilo lingekamilika salama, hakutaka tena kukaa neno hilo ,alianza kujiandaa kuelekea kwake, moyoni akiwa na amani sasa. Usiku mzima ulikuwa wa furuha kupita maelezo, hadi kunapambazukua alikuwa na tabasamu tu, hali hiyo ilimshangaza hata mke wake, lakini hakuweza kumuuliza .



    Safari ya kwanza, asubuhi hiyo ilikuwa ni kuelekea Nyakato national majanini, huko alikutana na David, aliekuwa amemsubili muda mrefu.

    "Nakupa nyumba hii, ila hati sitakupatia leo, utazipata baada ya kifo cha Janiphar, hapo ndipo nitakapoamini, na kuanzia muda huu, umeshakuwa rafiki kwangu na ndani ya Blood deal, hutakiwi kukataa kufanya chochote, ukienda nje ya utaratibu, kichwa chako kitakuwa chakula cha hii "

    David alizungumza huku, akitoa bastola ndani ya suruali yake, wote wakiwa ndani ya gari lake, alianza kuipangusa pangusa, akiwa ameitumbulia macho, upande wa Dk. Eddyson, hali haikuwa nzuri, kulikuwa na nafsi iliyoanza kumbeza na kumsunta, muda mwingine alijuta kukutana na David, kukubali kufanya kazi yake, alidhani mambo yatakuwa rahisi sana! Masikini Dk Eddyson alianza kutetemeka, bila mwenyewe kutegemea.

    "Sasa unatetemeka nini? Mbona unakuwa kama mwanamke! Daima mwanaume huishi popote, hufanya lolote, na tambua mwanajeshi hachagui adui wa kumshambulia hata mtoto mdogo anaweza kushambuliwa akiwa upande wa adui, wewe mwanaume kaza mjomba " alizungumza maneno hayo David akiwa anakipiga piga kifua cha Dk Eddyson, kilichokuwa kidogo na cha kawaida sana .

    "Lakini makubaliano yetu hayakuwa hivyo? "Alizungumza kwa unyonge, muda mwingine alitamani kuitoa damu yenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi ndani ya mwili wa Janiphar, lakini haikuwezeka, tayari maji yalikuwa yamemwangika ndani ya bahari, na ni ngumu sana kuyachota yaleyale, lazima utoke na mengine, majuto ambaye ni mjukuu tayari ,alikuwa rafiki yake kuanzia dakika hiyo. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "hahaha Dk Eddyson!! Hahahaha! Unanifurahisha kweli baadala ufu....."

    David alicheka kwa furaha, huku akiongea, aliyakata maneno yake, baada ya kuchukua mzinga wa konyangi, aliutikisa tikisa kama dakika moja, huku macho yake yakiendelea kumtathimini Dk. Eddyson ,aliekuwa mnyonge kupita maelezo ,

    "puuuuh! Sikiliza bwana mkubwa, siku zote ahadi huvunjwa kutokana na sababu za kila mmoja, hujawahi kuona penzi la watu waliokuwa wakipendana sana, na kila mtu akiwatamani lakini mwisho wa siku wanaachana? Na hata wakikutana hawasemeshani? "

    "kweli "

    "sasa Kama ni kweli!, Je mimi nitakuachaje, na tayari umeshafahamu kila kitu changu, ukitaka nikuache labda nikuue "

    "nini? "Dk. Eddyson alipayuka kupita maelezo,

    "ndio lazima ufe, ndipo utakuwa huru la sivyo karibu ndani ya Blood deal, kuna swali?"

    "ha.... hap... aaana "

    Alijikuta akishindwa kujibu vyema, zaidi ya kuendelea kutetemeka, ile furaha ya asubuhi aliyoamka nayo ilotoweka ghafla.

    "Basi kama hakuna, karibu kwako, unaweza ukarudi kuishi hapa kuanzia leo, fanya usafi, tutazidi kuwasiliana, unaweza kuondoka chukua pikipiki wahi hofisini "

    David alimkabidhi noti tatu za elfu tano tano mpya, Kama nauli.

    *****

    Usiku mzima hakuna alieshituka, zaidi ya kujigeuza geuza, saa kumi na mbili, Poul alikuwa wa kwanza kuamka, aliyafuta macho yake ili kuiondoa hali ya usingizi singizi, kisha alinyanyuka na kuketi, hakutaka kumuamsha mama yake, muda huo, alichofanya alishuka taratibu hadi chini alikoanza kufanya mazoezi kama Dk. Atanasi alivyokuwa amemweleza,

    "Mama nataka kuoga "

    Poul alimuongelesha Mama yake, huku mikono yake ikimtikisa tikisa, dakika mbili alishituka akiwa mchovu mchovu sana,

    "shikimoo Mama "

    Mar- haba ,umeamka salama? "

    "Ndio mama, wewe je? "

    "Salama ila nahisi, mwili mchovu, na mkono unauma hapa "aliongea huku akipashika shika eneo lililokuwa likimuuma, hakujua ni kipi kilimpata zaidi ya kuhisi uchovu tu, hakuta kulala tena, alimchukua mwanae na kumpeleka bafuni alimsafisha, kisha nae alijisafisha, baada ya kumrudisha chumbani huko,dakika kumi wasalimiaji waliingia, hata kabla hawajakaa Dk. Atanasi alifka chumbani humo kumjulia hali rafiki yake Poul, aliwaomba wampishe kidogo na baada ya vipimo aliondoka, akiahidi kurudi mchana huku akiwapa matumaini ya kuondoka siku chache.

    Ilikuwa jumatano asubuhi Janiphar alikuwa akijiandaa kuelekea kazini, baada ya wao kuruhusiwa kutoka hospitali siku tano nyuma, hakuwa na furaha hata kidogo, kutokana na upweke uliokuwa ukimsumbua, siku zote alizoea kuondoka na mmewe ,tena wakiwa wanacheka kwa furaha,

    "mpenzi nilikuzoea sana, sikujua kama siku moja utaniacha peke yangu, nilijua tutaishi milele ndani ya vicheko na tabasamu zisizo na kikomo, leo umeondoka na kuniachia mtoto, leo umeondoka na kuniachia lawama na hata uaduni, laiti ningekuwa na uwezo ningekufuata, nit...... "Janiphar alishindwa kuongea, alijikuta akilia sana huku akiwa ameikumbatia picha ya mmewe, siku wakifunga ndoa, miaka mitatu nyuma, hakiri yake, moyo wake vyote vilishindwa kuzoea kabisa, kila siku kwake kilikuwa kilio,tena kibichi, muda mwingine alidhani ni ndoto, ama yuko Safari na siku moja angelejea, lakini haikuwa hivyo, Emanuel alikuwa ameshafariki! Na asingeonekana tena ndani ya uso wa dunia.

    Taratibu aliitoa picha hiyo kifunia kwake, aliibusu, kisha aliirudisha ndani ya kabati lake la nguo, hakutaka tena kuiona kwa muda huo,

    "bwana nipe uvumilivu "papo hapo alichukua funguo za gari lake aina ya BMW ,mkoba mkono wa kushoto na kutoka chumbani humo, aliwaga ndugu waliokuwepo kisha aliondoka, bila kuyafuta machozi yaliyokuwa yamesambaza sambaza powder yake.

    Kila mtu alifurahi kumuona, neno Pole ndilo aliloshinda nalo masikioni mwake, siku hiyo alishinda mnyonge sana, lakini kadri siku zilivyozidi kusonga alijikuta akianza kuzoea zoea na kusahau ,ndani ya miezi mitatu alikuwa keshazoea, kule kulia lia kulipungua kiasi, tabasamu likaanza tena kuonekana usoni mwake, ngozi nayo ikaanza kukujuka na kurudi katika muonekano wake, wa kawaida.

    Mwezi wa sita alianza kuugua ugua hovyo hovyo, muda mwingine alihisi ni maralia hivyo alinunua dawa, ama aliongea na Dk. Atanasi aliemshauri cha kufanya, lakini hakupona akawa mtu wa homa homa baada ya muda mfupi, hali ilivyozidi kuendelea ilibidi aende Aghakhan kuchukua vipimo.

    "Janiphar Emanuel! "

    " Abeee Dk "

    Akiitika Janiphar huku akinyanyuka na kuelekea chumba alichokuwa Dk Larry, raia wa Hindia

    "karibu Janiphar "Dk. Larry aliongea kiswali chenye rafudhi ya kihindi hindi huku akimtazama machoni ,

    "ahsante "

    Kimya kilitawala huku Dk. Larry akikagua kagua karatasi zake,

    "Dk. niambie vipi namaralia sugu nini ? "

    Aliuliza Janiphar baada ya kuona kimya kimetawala muda mrefu.

    Dk Larry hakutaka kuongea chochote zaidi ya kumtazama kama dakika tatu, kisha aliachia kikohozi kikavu kutengezeza koo lake,

    "Janiphar "alianza kwa kuita, kisha akiendelea

    "majibu yako utapata, ondoa wasiwasi, hebu niambie mmeo alikufa kwa ugonjwa gani? "

    "aaaah! Aliuawa nchini Afghanistan, kwa ufupi hakufa kwa ugonjwa wowote "

    "sawa, na kabla ya kifo chake, aliwahi kuugua ugua kitu chochote?"

    "mmmmmh! Hapana, mme wangu hakuwa na tabia ya kuugua hovyo hovyo, kwani vipi? "

    "hakuna tatizo, nilikuwa nataka kujua tu, je wew hukuwa ukiugua chochote? "

    "hapo nyuma hapana!, ila miezi mitano ama sita baada ya mme wangu kufariki, mwili wangu ulianza kuumwa umwa hovyo, mwanzo nilijua mawazo, lakini hali iliendelea endelea tu "

    "ok sawa, samahani kwa swali hili, sina nia mbaya, je baada ya kufiwa uliwahi kushiriki tendo la ndoa na mtu mwingine? ".Safari hii Janiphar alishituka, hakujua kwanini Daktari huyo alikuwa na maswali, mengi kiasi hicho!.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hapana sijawahi, na siko tayari kwa muda huu, nampenda mme wangu sana, je nimeonekana na Ukimwi? "

    "mmmmmh! Janiphar ondoa wasiwasi, bado tunashughulikia vipimo, na hatuwezi tukakueleza, kuwa umeambukizwa ila njoo baada ya miezi mitatu tutajua zaidi "

    Maneno ya Dk. Larry alimchanganya sana Janiphar, hakutaka kuendelea kukaa tena ,chumbani humo alitoka mbio mbio hadi ndani ya gari lake, safari ya kuelekea mwananchi hospital ilianza, njia nzima alikuwa akitoa machozi, hakujua alifikaje hapo, alipaki gari lake mbele ya jengo la zamani la Tanesco,alishuka haraka, huku akikimbia kukifuata kijia cha kuingia soko la makoroboi, lakini hakufika huko ,alikunja mkono wa kushoto na kuingia ndani ya hospitali hiyo iliyojificha ficha, kwa mtu mgeni jiji la mwanza ni vigumu sana kuifahamu.

    "Agines ninaukimwi! "Janiphar aliongea bila hata kukaa, Wifi yake Agines aliekuwa daktari mpya ndani ya hospitali hiyo alimshangaa, haikuwa kawaida ya Janiphar kwenda pale bila kumtarifu.

    "nani kakueleza wifi? "Agnesi aliuliza kwa upole, huku akiacha kumuhudumia mgonjwa aliekuwemo ndani,

    "nimetoka Aghakhan dakika hii nimeelezwa, ninaukimwi wifiiii, na nani kaniambukizaaaa"Janiphar alishindwa kuongea vizuri, zaidi ya kulia, alikiona kifo kikimkabili muda si mrefu , kifua nacho kilichemka kupita maelezo .

    "Mamy tulia Kwanza, acha nimalizie kumuhudumia huyu nije tujue zaidi " Agnes alizungumza hayo, huku akimalizia kumuhudumia mgonjwa wake, dakika kumi alianza kuongea na wifi yake ,Janiphar alianza kumuelezea kila kitu, huku akitia huruma,

    "acha tuchukue kipimo ".

    Papo hapo alichukua damu kutoka kwa Janiphar, na kuipeleka sehemu husika, dakika mbili alilejea kuongea na wifi yake, akimtia moyo, kidogo Janiphar akianza kufarijika, wakiwa wamezama ndani ya mazungumzo, majibu ya Janiphar yaliletwa na kukabidhiwa Dk. Agines ambaye ni wifi yake kabisa, kabla hajafanya chochote Janiphar alimnyakua na kuyasoma, papo hapo alidondoka chini kama mzigo puuuu, na kupasuka kichwa upande wa kisogoni, Agines alibaki amepigwa bubuwazi, hakujua afanye nini, zaidi ya sekunde arobani na tano alikuwa hajielewi ,alikuja kushituka baada ya kuona damu nyingi zikiipamba taizi, kelele akizozipiga zilichangia kujaza watu, dakika saba ndizo zilizotumika kumsaidia Janiphar aliekuwa akihema kwa mbali sana ,huku akiwa amepoteza fahamu , huduma ya kwanza ilitolewa ,kabla ya kwenda Bugando hospitali kwa uchunguzi zaidi.

    Machozi na kamasi nyepesi nyepesi hazikukatika machoni, na puani kwa Agines pindi alipogundua majibu ya wifi yake, yaliyokuwa yakionesha maambukizi ya virusi vya ukimwi, hakujua muda gani walifika Bugando, wakiwa bado getini Janiphar alipandisha kifua juu, macho yakiwa yametoka, huku mdomo ukiachama na alipokuja kushusha kifua tayari alikuwa amefariki, kila mtu ndani ya ambulance hiyo hakuamini hasa hasa wifi yake, alieona kama maigizo flani lakini ukweli ndo ulikuwa huo.







    Agines alihisi nguvu zikimuishia mwili mzima, alitetemeka bila kujua na hata mwili wake ulianza kuota vipele vya baridi ,hakuamini kama kweli wifi yake kipenzi na wa pekee alikuwa amefariki!Tena mbele ya macho yake! Zaidi ya dakika moja alibaki ameganda asijue la kufanya, kulia alishindwa, kila kitu hakuweza kufanya. Kilichokuja kumshtua ni hatua ya madaktari toka mwananchi na Bugando walipoanza kuyarudisha macho pamoja na mdomo.

    "Mama Poul? "

    Agines alimuita huku akimlalia kifua, machozi yalianza kuchora barabara katika mashavu yake, aliona ni mkosi uliokithili,

    "hata mwaka hujapita wote wanafariki? Na wifi kautoa wapi ukimwi? "Yalikuwa ni mawazo yenye mfumo wa maswali , yakipita ndani ya kichwa chake.

    Mwili wa Janiphar ulitolewa ndani ya ambulance hiyo, na kulazwa juu ya kitanda kilichokuwa na matairi mawili mawili, mbele na nyuma, huku ukiwa umefunikwa,kuanzia kichwani hadi miguuni. Safari ya kuelekea chumba cha daktari kwa uchunguzi zaidi ilianza, huku Agines akiwa ameushilia,

    "Naomba ufanye uchunguzi Dokta siamini kama kweli wifi amefariki? "

    Aliongea Agines huku akitoa machozi

    "kuwa na subila binti, kaa kwanza hapo nje "

    "hapana naomba nikae humu humu, nami ni daktari "aliongea huku akitoa kitambulisho ,Dk George hakuwa na jinsi , ilibidi afanye kazi hiyo, akiwa amesimamiwa, dakika tatu alikinyanyua kichwa chake na kumtazama, uso wake ukivaa vazi la huzuni.

    "Amekufa? "

    "Ndio! "

    "Ooooosh!" Alitoa neno hilo huku akikaa juu ya kiti kilichokuwemo chumbani humo, alihisi kichwa kizito kupita maelezo, macho yalianza kuona giza, huku mapigo ya moyo yakienda kasi ,lakini alijikaza sana.

    "OK Dokta "

    Dk. Agines alitoka chumbani humo, mbio, alitoka hadi nje ya geti, alichukua pikipiki iliyimpeleka nyumbani kwa kaka yake, mita chache kutoka hapo.

    "Ma... maaaa wifiii ,wifi amefa.... " Dk. Agines alianza kupiga kelele, pindi alipoukanyanga uwanja wa nyumba hiyo, ile ahadi ya kujikaza kwanza ilitoweka ghafla, sauti yake hiyo ilipelekea mama yake kutoka mbio.

    "nini? "

    Aliongea Mama yake, huku akinyanyuka , alihisi kama kisu cha moto kikiuchoma moyo wake, hakutaka kusikia habari mbaya ,masikio yake yameshachoka.

    "Agi niambie, kunanini? "

    "Mamaaa, wifiii kafarikiiiiii! "Aliongea huku akitoa kilio cha hali ya juu, hali hiyo ilisababisha mji huo kujaa watu, na kutanda kwa vilio kila kona, hakuna alieweza kumsaidia mwenzake, hakuna aliamini kama Janiphar nae alikuwa amefariki! Na asigeweza kuja tena, maswali yalikuwa mengi kwa kila mtu, wengi wao walijiuliza kafa kwa kitu gani? Wakati asubuhi alikuwa mzima kabisa ! Ilibidi wamtulize Dk. Agines ili aweze kuwaeleza nini hasa kilipelekea kifo cha Janiphar? Japo haikuwa kazi rahisi kumtuliza, lakini walifanikiwa kwa kiasi kidogo.

    "Ukimwi "CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nini!!!!!!!!!!!! "watu wote walishangaa kwa pamoja, Hakuna alieweza kuamini kama kweli, Mama Poul alifariki kwa ukimwi.

    "Puuuuuuh! "Alishusha pumzi ndefu, kisha aliyafuta machozi, alianza kuwaeleza kila kitu, japo ilikuwa ngumu kwa kila mtu kuamini,ilibidi waamini maneno hayo, kati ya watu waliokuwa wameumizwa sana na msiba huo ni mtoto Poul, alilia kupita maelezo, maneno aliyowahi kuambiwa na Mama yake miezi saba nyuma yalimuumiza sana, sasa alikuwa akifahamu nini maana ya kufariki, alijua Mama yake nae hatakuja tena,

    "kama Baba aliondoka na hakurudi, itawezekanaje Mama arudi? Amekufa sina Mama mimi msinidanganye niacheniii" Poul alitoa maneno hayo huku akilia, kilio kisichoeleweka ni muda gani kingekoma, hakuyaamini maneno ya bibi yake aliona ni uongo mtupu, mtu aliekufa , alikufa tu, na asingerudi tena, iweje bibi yake amdanganye? Mama atarudi! Poul alitia huruma sana , kila aliemtazama alishindwa kujizuia kutoa chozi, maneno yake yalikuwa miiba miyoni mwao.

    *****

    Hakuna siku iliyokuwa njema masikioni mwa David kama siku hiyo! Alijiona mshindi kupita maelezo, kila sekunde alitoa tabasamu

    "Kaka mambo tayari"

    "Unasema? "

    "Kaondoka mchana huu, kuanzia dakika hii, mie boss hapa mjini "David aliongea kwa kujingamba, habari ya kifo cha Janiphar, ilikuwa njema sana masikioni mwake, furaha aliyokuwa nayo hakika haikuelezeka, mara baada ya kupokea ujumbe huo kutoka kwa baba yake, alibadirika sana, alijiona mwili mwepesi si mfano, papo hapo alitoa agizo kwa wafannya kazi wote wagawiwe soda, walishangaa! Sana .

    "Hogerea sana sasa umekomaa, na Dk. Utampatia nini? "

    "Nitamkabidhi rasimi nyumba yake, na kumtumia katika mambo yetu, mara baada ya kumpika vyema "

    "hilo nalo neno jema "

    "tena anatufaa sana "

    "kweli "

    "sasa acha nikazuge msibani, jioni tutaonana "

    "kwanini tusiambatane wote, kusherekea ushindi leo ni kunywa kwenda mbele "

    "kweli Deus, nakuja kukupitia "

    David alikata simu, na kushusha pumzi ndefu ya ushindi, aliitazama hofisi hiyo, bila kuamini kama kweli ilikuwa yake, hakuwa na adui tena wa kuisumbua hakiri yake, mtoto Poul alimuona kama mkia wa ngo'mbe, kuukunja na kuurushia mdomoni haikuwa kazi ngumu.

    "Daaaa! Nimemaliza "

    aliongea Peke yake huku akinyanyuka na kutoka hofisini kwake , hakujali macho makali ya wafanyakazi wake na Marehemu Janiphar, waliokuwa wakilia sana, kwake aliona maigizo tu!

    "muda wa kufunga hofisi ni ule ule, na kesho ,kazi Kama kawaida "

    David alitoa maagizo hayo kwa mhasibu wake, Dada huyo hakuamini, kile kilichozungumzwa, alibaki ameshangaa.

    "Umenielewa? "

    "Ha.... hapanaa,lakini mwenyekiti amefar...... "

    "shiiiii! Toa ngojera hapa, yule kaenda na tumbo lake, maisha yake yameishia hapo hapo, tukikaa kumuabudu, madeni yatalipwaje?, Msharaha wako!, muda mwingine uwe unatumia hakiri ".

    David alizungumza kama hana hakiri, hakujali kabisa kifo cha Shemeji yake, makelele yake yalipelekea , wafanyakazi wote kuzunguka eneo hilo, wakiwa wamevimba sura.

    "Boss tunataka kwenda msibani "

    "nani kafa? "

    "Mama Poul? "Kijana aliekuwa akijiamini Kupita maelezo alijibu, bila wasiwasi,

    "hakuna cha msiba hapa, tazemeni kazi ,ndicho kilichowaleta hapa, si vilio, ok anaetaka kwenda aende, ila atambue kuanzia dakika hii hahesabiki mfanyakazi wa hapa ". Wafanyakazi wote walinyanyuka na kutoka, kama kukosa kazi, walikuwa tayari, David hakuamini macho yake, alibaki amesimama katika ya mlango, bila kujielewa.



    Macho ya David hayakuamini hata kidogo, aliona kama mawenge, taa ya hatari ikawaka kichwani kwake , tayari alikuwa ameshagundua udhaifu wake, kwa wafanyakazi wake. Hivyo alihitaji hakiri ya ziada kurudisha hali ya kawaida, na si kesho ama masaa kadhaa, ilitakiwa afaye papo hapo! Kuondoka kwa wafanyakazi wote kulionesha picha ya mambo yake ambayo sasa yanaweza kuharibika kwa muda mchache, hilo David hakutaka litokee, na ili kurudisha hali ya kawaida ilitakiwa atumie hakiri ya ziada.

    "Mossee "

    "Naam boss "

    "hebu njoo mara moja "David aliongea huku akitembea taratibu kumfuata kijana huyo, alionekana ndie kihelele

    "nikimtuliza huyu wote, watakuwa nziiii! " David aliwaza, akiendelea kumfuata Moses .

    "Sasa Mosse kuwatania tu mnaondoka? "Aliongea huku, uso wake akiupamba kwa tabasamu la bandia, ilihali moyo haukuwa radhi kabisa .

    "Unajua tunashindwa kukuelewa kabisa boss, hofisi yetu imepoteza mtu wa muhimu sana, aliekuwa akitegemewa na kila mtu, mji wote umezizima iweje wew ukatae sie tusiende? Picha gani tutaionesha? Binafsi niko radhi kupoteza kazi, ila si kumterekeza Janiphar! Mama huyu ameondoka ingali anahitajika, upole wake, na huruma yake kwetu,siku zote leo iwe hivi? Hatukuelewi watu wanahisi yawezekana umehusika! Hiyo siyo roho mbaya bali ni mbaya roho, hatuwezi kumfanyia hivi, hatuko nae kimwili ila kwa imani tuko nae kiroho tunaenda kumhani kwaheri "

    "hap.... apanaaa! Aaah! Mosse, punguza jazba, tuongee kama wanaume, muda ule nilikuwa sijielewi, si unajua pombe "

    David aliongea taratibu, tena kwa aibu ,ule ukali wake , siku hiyo ulikwama, lakini hakutaka kukubali kushindwa alitakiwa apambane hadi mwisho wake.

    "Pombe? Pombe na msiba aaaaah! "

    Kijana Mosse alishangaa kupita maelezo , hadi mishipa ya kichwa ilimsimama, macho ameyatoa kupita maelezo, hakudhamiria kusikia maneno kama hayo.

    "Usinishangae Mosse, nimawazo ndo yanayopelekea kufanya vile, kifo cha shemeji yangu kimeniumiza sana, na ili kuondoa mawazo ilibidi nifanye tafadhali nisameheni "ilibidi ajishushe ili mambo yaende sawa CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "poa acha tuwahi, hayo yamepita "

    "chukueni gari za hofisi mtumie "

    Toka uhai wa Emanuel, hakutaka wafanyakazi wake wasumbuke kwa usafiri, hivyo alinunua magari mawili kwa ajiri ya usafiri, asubuhi na jioni, pia usafiri huo ulirahisisha kazi yake kwenda alivyotaka, wakati muafaka, hakukuwa na visingizio vya usafiri mgumu.

    "Sawa tutatumia "

    Alijibu Mosse huku akianza kuondoka taratibu eneo hilo, David aliyauma meno yake kwa hasira, huku akiikandamiza aridhi, kwa kiatu chake upande wa mbele

    "Sitakiwi kuonesha dhamila yangu muda huu ,acha nigonje muda utimie " aliongea huku akiingia ndani ya gari lake Safari ya kumpitia Deus ilianza, akiwa njiani alijikuta akikumbuka mambo mengi sana ya nyuma.

    *******



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog