IMEANDIKWA NA : MODEL TEDDY
*********************************************************************************
Simulizi : Blood Deal
Sehemu Ya Kwanza (1)
Ndege kubwa toka shirika la ndege duniani Qutar ilionekana ikitafuta uelekeo mzuri wa kutua ndani ya uwanja wa kimataifa wa Hamid karzai international airport ndani ya mji wa kabul Afghanistan, kabla ya kutua taratibu ilishusha matairi ya mbele na kisha ya nyuma huku teyari abiria wote ndani ya ndege hiyo wakiwa wamefunga mikanda na kutulia katika viti vyao ,huku wengine wakiomba taratibu mioyoni mwao kumsihi mungu wao awasimamie katika nafasi hiyo iliyokuwa imesalia katika safari yao. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Tunapenda kuwatakia mapumziko mema na shughuri njema ndani ya nchi ya Afghanistan "
Sauti nyororo ya msichana aliyekadriwa kuwa chini ya miaka ishirini na tano ilisikika ikipenya taratibu ndani ya kila ngoma za masikio ya kila abiria aliyekuwa ndani ya ndege hiyo. Lugha hiyo ilizungumzwa kwa kiarabu lakini ilitafasiliwa kwa lugha zaidi ya nne kiswahili, kingereza, kifarasa, na, kichina hali hiyo ilisaidia baadhi ya abilia waliokuwa wangeni na lugha ya kiarabu kuelewa kilichozungumzwa .
Taratibu ilianza kushuka chini kwa Kasi huku tairi zote zikiwa nje teyari kuikanyanga aridhi ya nchi hiyo na kabla ya kusimama ilianza kuseleleka kwa kasi huku ikiendelea kupungunza kasi hiyo kisha ilisimama ,mlango ulifunguliwa huku ngazi ikiwa teyari .
"so tutaonana lini Ema?"
"aaaah!! sijui... "
"stop Ema ndo unataka sema hatutaonana tena ?"
Juliet aliongea kwa madeko sana kana kwamba walikuwa wanafahamiana kwa muda mrefu, yale mazoea mafupi na kufahamiana kwa muda mfupi ndani ya ndege hiyo yalimfanya Juliet kuwa karibu sana na Bwana Emanuel
"tutaongea"alijibu kwa ufupi huku akinyanyuka kitini hapo
"basi nipe contact zako "Safari hii Juliet aliongea kwa madeko zaidi macho akiwa ameyarembua akiyapa hali ya usingizi usingizi ili tu kumkoleza Emanuel, sura yake yenye umbo la yai ikiwa imezawadiwa mashavu meupe na makubwa kiasi yakiwa na vishimo pindi alipocheka ilimfanya azidi kuvutia zaidi.
"+25575620228.."
"ahsante sana "
"usijali"
"Mhhhh! samahani ulisema utakuwa hoteli gani?
"intercontinetal"
"waooo! kumbe upo hapa hapa Kabul, mie naelekea Ghazni"
"vyema zaidi"
Kadri muda ulivyozidi ndivyo maongezi na mazoea yalizidi kuongezeka hali hiyo ilimfanya kila mtu kumuamini mwenzake, kwakuwa ulikuwa wakati wa kutoka ndani ya ndege hiyo ilibidi wakatishe mazungumzo na kufuata taratibu zote zikiwemo za ugongewaji wa passport
"kimepotelea wapi hiki? Emanuel alijiuuliza peke yake akiwa anasukuma kitoroli kilichokuwa na begi Lake dogo pamoja na kifuko kidogo, shingo yake aliipa kazi ya kuzunguka huku na huko kumtafuta Juliet akiwa na lengo la kumuaga kabla ya kuondoka ndani ya uwanja huo
"samahani kaka tunaweza tukachunguza begi lako? "aliongea mmoja wa askari waliokuwa eneo la lango kubwa, kwa lugha ya kingereza
"hakuna shaka angalieni tu! "
Kwa kuwa hakuwa na wasiwasi wowote juu ya mizingo yake aliwapa begi lake huku akiwasaidia kufungua, macho yake yalishituka kidogo baada ya kukutana na nguo tofauti na iliyokuwa imewekwa juu na mkewe
"nini hiki? "
"s... si... jui"
Alijikuta akipata mshituko wa hali ya juu baada ya kutolewa mfuko mkubwa wa rambo rangi nyeusi ukiwa umefungashiwa vitu mithili ya unga
"drugs abuse(madawa ya kulevya) "
Askari aliekuwa akiufungua mfuko huo alijikuta akishituka Sana
"hapana begi hili silo langu! "
"kiaje wakati umekamatwa nalo wewe? " ilibidi askari asimame huku akimsogelea Emmanuel aliekuwa bado akilikagua kagua begi hilo ambalo lilikuwa lake kwa kila kitu kuanzia kimdori kidogo kilichokuwa pembeni alama iliyokuwa ubavuni lakini alichanganyikiwa na mzigo uliokuwemo ndani yake ,kwa macho yake mawili alishuhudia mkewe akipanga nguo moja baada ya nyingine huku yeye akiwa amejilaza pembeni akimtania,
"sasa madawa yameingiaje? "alizidi kuumiza kichwa chake bila kupata jawabu sahihi.
"kuanzia muda huu upo chini ya ulinzi? "alinzungumza askari aliekuwa akifahamika kwa jina la Nurdin , papo hapo alifungwa pingu mikononi na kutolewa nje ya uwanja huo akiwa chini ya ulinzi mkali sana
"lakini sihusiki na mzigo huu "
"hayo hatujui sie wewe subili ukifika pahali sahihi utaongea"
Emanuel alipakizwa ndani ya gari la polisi akiwa haamini tukio hilo ambalo aliliona kama ndoto ya mchana muda mfupi angeshituka, kutoka uwanjani hapo hadi kituo cha polisi hakukuwa na umbali mrefu walijikuta wakitumia dakika saba tu
"shuka"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Taratibu alishuka na kuanza kuelekea ndani ya kituo hicho kilichokuwa kikifahamika kwa jina la muhazrat police station.
"inakuaje raia wa Tanzania unaingia na madawa ya kulevya hapa ili hali nchi yako inasifika kwa amani, utulivu na kila kitu chema? " Asikari polisi aliekuwa amesimama nyuma ya meza kubwa aliongea huku akimtazama machoni, japo alikuwa amevaa miwani lakini macho yake makubwa na mekundu yalionekana dhahili
"si.. hu.. siki... na... tukio hili! "
"acha kudanganya kaka hapa si Tanzania ,tambua uko Afghanistan hatuna tamaa ya rushwa kama asksri wenu wasiotekeleza kazi zao,hebu lete na hiyo passport yako yawezekana umegushi "
Emanuel alimpatia huku akianza kuingiwa na woga, aliijua vyema nchi hiyo, teyari alianza kujihesabu mfungwa mpya nje ya nchi yake hakika aliumia sana, maneno matamu aliyoyapata toka kwa mkewe Janiphar pamoja na kijana wake Mdogo Poul wakiwa uwanja wa ndenge wa mwanza yalimuumiza sana
"Baba utaniletea baskeli ?"
"ndioo baba, tena niache aaaah! masihara hayo ".Alijikuta akikumbuka na kumfanya atoe machozi namna ushahidi ulivyokuwa wazi dhahili gereza lilikuwa halali yake.
Baada ya mahojiano hayo aliamriwa kuvua kila kitu kisha alipelekwa mahabusu.
******
"haloo "
"ndio niambie umefanikisha? "
"aaaah! mie tena ,andaaa pesa yangu tu "
"poa "
Simu ilikatwa huku kila mtu akiwa na furaha ndani ya moyo wake, kiasi cha milioni kumi kwa kazi ndogo kama hiyo kilimfanya dada huyo kucheka na kufurahi, teyari alikuwa tajiri mtoto
"kwanza nanua gari, nguo za kufa mtu watanikoma mwanza hahaha "
Aliongea peke yake akiwa kitandani ndani ya hoteli ya Intercontinetal ghorofa ya kumi na mbili chumba na 231 ,kwa furaha aliyokuwa nayo ilimrazimu kuanza fakamia vinywaji vilivyokuwa ndani ya jokovu ndogo. Ghafla alisikia mlango ukingongwa taratibu alinyanyuka huku mkononi akiwa na chupa ya kileo ,mwili wake mweupe akiufunga taulo lililoishia katikati ya mapaja
"nani? "
"mhudumu "
Jibu hilo lilimfanya afungue haraka bila kuwa na wasiwasi wowote
"shiii! kaa kimya "
Alijikuta akiamriwa baada ya kukutana na watu wawili wakiwa wamevaa mavazi yaliyowaficha sura zao, walimsukumia ndani ya chumba bila kuongea chochote huku mwingine akiwa ameshikilia bastola aina ya m-32
"sikia binti wewe ni mzuri sana kama hutaki kufa tupe penzi "Homayoun aliongea huku akumsogelea karibu kisha alilivuta taulo hali iliyopelekea wote kutoa macho na udenda baada ya kukutana na mwili mweupe ukiwa na ngozi nyororo
"naanza mimi "
"wapi acha nianze mie "
Walianza kubishana kwa lugha ya kiarabu ambayo ilikuwa ngeni masikioni mwa binti huyo aliekuwa akitetemeka Sana
"basi tukose wote paaaaaa! "
Murtaza aliongea huku akiyasindikiza maneno hayo na risasi moja iliyokifyatua vyema kichwa cha binti huyo.
"sasa nini? "
"kazi yetu ilikuwa kuua si vingine tuondoke "
Walitoka kwa tahadhari wakipitia mlango wa nyuma bila kuinewa na mtu yeyote.
"Juliet unatakiwa usafiri hadi Afghanistan na Emanuel hakikisha unakuwa nae karibu sana ili asije shituka kwa lolote sawa? "
"sawa boss vipi malipo yangu lakini tambua kazi ya kwanza hujanipatia " Juliet aliongea huku akinyanyua glass ya bia iliyokuwa mezani ndani ya mwanza hoteli na kuipeleka mdomoni alikunywa fundo moja kisha aliirudisha glass hiyo pahali pake na kumtazama David usoni
"pole Juliet malipo yote nitayaunganisha nitakupa milioni kumi keshi "
David alizungumza huku akimtazama machoni akisindikiza na tabasamu bashasha ili kumteka Juliet alikuwa ameshamjulia udhaifu wake
"sawa so lini ataondoka? "
"kesho na ndege ya saa mbili asubhi na nzuri zaidi nimekukatia kiti kimoja na yeye unatakiwa umchangamkie maana namjua hana tabia ya kuongea ongea "
"hilo niachie mie mmakonde halisi natema checheka kama sijielewi hahaha! "
Juliet aliongea huku akikitikisa kifua chake kilichojaliwa chuchu kubwa kiasi kulingana na mwili wake ,maneno hayo yalizidi kumpa faraja ya ushindi bwana David. Waliongea mengi sana na jambo kubwa kuliko yote lilikuwa ni kumkamata bwana Emanuel msukuma toka wilaya ya Simiyu mkoani shinyanga tajiri kupindukia akiwa chini ya miaka thelathini na tano ,alikuwa akiishi jijini mwanza wilaya ya nyamagana maeneo ya Bugando karibu kabisa na chuo cha udaktari Bugando.
Japo alikuwa tajiri sana hakuwa na moyo wa kichoyo kuanzia nyumbani kwao alikowajengea wazazi wake nyumba ya kisasa kabisa huku wadogo zake wawili mmoja wa kiume aliekuwa hajaoa alimshirikisha katika biashara zake, Dada yake alikuwa bado mwanafunzi ndani ya chuo cha udaktari Bugando.
Katika umri huo alikuwa teyari na familia mke na mtoto mmoja aliefahamika kwa jina la Poul, mkewe aliitwa Janiphar mwenyeji wa mkoa wa Moshi wilaya ya Rombo kijiji cha mashati, kutokana na upendo na uchapakazi kati ya wanandoa hao walijikuta wakifanikiwa sana kila iitwapo leo, utajiri wao haukuishia kuwasaidia wazazi na ndugu pekee bali kila iitwapo jumapili hawakusita kutoa misaada kwa wafungwa ndani ya gereza la Butimba na baadhi ya vituo vya kulelea watoto yatima pia jumamosi hawakusita kusambaza misaada kwa wazee na watoto waliokuwa wakiishi maisha ya mtaani arimarufu kama ombaomba vitendo vyote hivyo vilimfanya apendwe na kila mtu si mkubwa ama mdogo pia jina lake lilikuwa mswaki ndani ya vinywa vya wakazi wa mwanza na mkoani shinyanga.
*****
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Saa moja na dakika kumi na tano Emanuel aliondoka nyumbani kwake akiwa na mdogo wake pamoja na familia yake ndani ya gari lake la kifahari aina ya Vorvu
"inatakiwa ufanye kazi kwa nguvu, utii, moyo wa kujituma na heshima lazima ufanikiwe tu "
"kweli kaka "
Hadi wanafika uwanja wa ndege walikuwa wakizungumzia maswala ya Kazi
"nitakukumbuka Sana mpenzi " Janiphar aliongea huku kichwa chake akikilaza juu ya bega la kushoto la mmewe Emanuel
"usijali mama siku tano tu "
"baba utaniletea baiskeli? "
"ndio baba wewe tena masihara nisipoleta"
Baada ya maongezi hayo Emanuel aliangana na familia yake kisha alielekea chumba cha ukaguzi na baada ya zoezi hilo kukamilika aliiendea ndege.
Akiwa katika mawazo dhidi ya familia yake ghafla alitokea msichana aliekuja kukaa pembeni yake na Safari ikawa imeanza hadi wanaingia Nairobi hakuna akiemsemesha mwenzie lakini baada ya kutoka Nairobi msichana aliekuwa pembeni yake alijifanya akiumwa tumbo tena lenye maumivu makali sana hali hiyo ilimfanya Emanuel kushituka sana papo hapo alianza kutoa huduma ya kwanza kabla ya wahusika maarumu
"ahsante kaka" Juliet aliongea mara baada ya kupatiwa msaada
"usijali duniani kusaidizana leo kwako kesho kwangu, "
"kweli kabisa"
Kimya kilichukua nafasi tena kama dakika kumi kisha Juliet alianzisha mazungumzo tena
"naitwa Juliet naelekea Afghanistan kibiashara sijui mwenzangu nani? "alizungumza huku akimtazama machoni
"Emanuel pia naelekea huko huko uendako ".
Huo ndio ukawa mwanzo wa urafiki wao hadi wanaingia mjini Kabul walikuwa marafiki kabisa hali hiyo ilimfurahisha sana Juliet aliemshukuru muumba wake, baada ya kutoka ndani ya ndege hiyo alijichanganya na abilia waliokuwa wakitembea makundi makundi kuelekea sehemu ya kuchukulia mizigo haraka sana alichukua begi la Emanuel lililokuwa likifanana kila kitu na lake alilokuwa amelijaza madawa ya kulevya kazi aliyopewa na bwana David aliefananisha begi hilo na la Emanuel ,kazi aliyoifanya akishirikiana na mmoja wa wafanyakazi wa uwanja wa ndege mjini mwanza kuyapitisha madawa hayo.
"kushi nei kafie mbele "Juliet aliongea peke yake akiwa anamtazama Emanuel aliekuwa bado akimtafuta yeye, pia alishuhudia tukio la uchukuaji begi hilo, papo hapo alielekea getini alikokwenda kuongea na askari kisha aliondoka akitumainia ushindi mkubwa.Kweli Emanuel alipofika eneo hilo alikaguliwa na kukutwa na mzingo mkubwa wa madawa ya kulevya.
Juliet alikuwa na shauku ya kupata milioni kumi mara baada kufika ndani ya hoteli ya intercontinetal iliyokuwa katikati ya mji wa Kabul mji mkubwa kwa shughuri mbalimbali za taifa hilo alimpigia simu David kumpa taarifa hiyo kisha alianza kujiburudisha na vileo vilivyokuwa vimesheheni ndani ya jokovu dogo la kisasa.
*****
"Hamayoun uko wapi? "
"niko internet house " Hamayoun akijibu ujumbe huo ulioingia ndani ya simu yake kupitia njia ya whatsapp
"naomba uelekee intercontinental hoteli ghorofa ya kumi na mbili chumba no 231 ukammalize msichana unaemuona kwenye picha hiyo "
"sawa malipo je? "
"nishawaeka dolla elfu tatu ndani ya acount yako "
Baada ya mawasiliano hayo kutoka Tanzania hadi Afghanistan Hamayoun aliondoka eneo hilo akikodi pikipiki hadi nyumbani kwa rafiki yake Murtaza mtaa wa tano toka eneo hilo. Murtaza alikuwa jambazi na mafia mkubwa aliekuwa akifanya kazi na kundi la Taliban lililokuwa tishio sana nchini humo,
"mwanangu twende dili limewaka "
"kweli? "
Aliuliza Murtaz akiwa haamini habari hiyo kwani alikuwa na siku tatu bila kuingiza pesa zaidi ya kuzitumia, aliitupa sigara yake chini na kuikanyanga kisha alivaa suruali nyeusi pamoja na koti lake na mwisho kabisa aliichomeka bastola yake kiunoni kisha walitoka nje wakiliendea gari lake
" tunahitaji vyumba Kwa matumizi ya masaa matano tu " aliongea Hamayoun na dada aliekuwa mapokezi
"vipo dolla mia saba tu! "
"poa "
Hamayoun alilipia kisha walipandisha ngazi hadi ngazi ya pili toka hapo kisha walichukua lifti iliyowapeleka gharofa ya kumi na mbili
"tufanyeje sasa? "
"we subili utaona "
Murtaza alizungumza huku akitembea kuelekea mbele akikipita chumba cha Juliet hata kabla hajafika mwisho akitokea mfanyakazi aliekuwa na mashuka machafu dhahili alionekana alikuwa mfanya usafi.
"samahani dada "
"bila samahani " alijibu msichana huyo huku akiizuia miguu yake kusonga mbele hilo likawa kosa kubwa sana
" tunaomba ukatusaidiea kuongea na mgeni aliomo ndani ya chumba kile "
Murtaza alisema huku mdomo wa bastola yake ukiwa kichwani mwa msichana huyo aliekuwa ameanza kutetemeka
"sawa nitaenda "
"twende "
Ashirafa aliongoza hadi mlangoni mwa chumba hicho na kugonga waliposikia kitasa kikiguswa walimtoa Ashirafa mlangoni hapo akiwa amemfunikwa puani na kitambaa cheupe sekunde kumi tu alianza kulegea akikosa nguvu papo hapo Hamayoun alimlaza chini karibu kabisa na chumba hicho kisha alilejea kwa mwenzake aliekuwa amesimama katika ya mlango akigojewa kufunguliwa.
" boss teyari "CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"basi sawa "
Alijibu David huku akikenua meno ishara ya ushindi. Japo aliishi Tanzania lakini kazi zake kokote duniani zilifanyika tena kwa wepesi.Usiku mzima aliumaliza akitafuna nyama choma na bia ndani ya Tilapia Hoteli pembeni akiwa na wapambe pamoja na wasichana watatu waliokuwa wakimlisha, kumbusu na kila aina ya mapenzi.
*****
Kukamatwa kwa mtanzania nchini Afghanistan akiwa na madawa ya kulevya kulienea kwa kasi sana kila kona ya dunia mithili ya moto wa kifuu, David alikuwa na hamu ya kumuona Emanuel akiwa nyuma ya nondo kweli katika taarifa ya habari ya saa mbili usiku kupitia ITV na radio one habari hiyo ilitangazwa hadhalani hapo ndipo furaha yake ilizidi kuongezeka mara dufu alijiona mshindi kupita maelezo.
"shemu mme wangu amekamatwa jamaniiiiii! "
"nini? "
"kweli eti na madawa ya kulevyaa jamaniii "
Mama Poul aliongea huku akianza kulengwa lengwa na machozi hakuamini tukio hilo
"Yesu na Maria Shemu njoo nyumbani jamaniiiii" alizidi kulalamika ndani ya simu akimsihi David kufika nyumbani kwake Bugando usiku huo huo hata chakula kitamu alichokuwa akikila kilikwama akawa wa kulia peke yake akiongea kichanga,
" ilikuwaje shemu?" aliuliza David mara baada ya kufika nyumbani hapo akijifanya kuchanganyikiwa sana, ilibidi Mama poul aelezee tukio zima jinsi alivyoshuhudia huku akiendelea kububujikwa na machozi kila alipotoa neno
" shemu jikaze atatoka tu "
"nashindwa kuelewa madawa hayo yamefikaje ndani ya begi lake ilihali nguo nilimpangia mwenywe "
" hata mie nashangaa ila amini atatoka tu, na kesho itabidi nisafiri "
"wapi tena ?"
" huko huko shemu nikajue cha kufanya "
" kweli shemu"
" basi itabidi uanadae pesa za kutosha shemu "
" usijali Shemu hata nyumba nitauza ili mme wangu atoke "Janiphar alikuwa radhi kupoteza kila kitu ili ampate mmewe aliempenda kupita Maelezo
"basi sawa "
Baada ya mazungumzo hayo David aliondoka huku wakiahidiana kuonana kesho.
"Jamani mie sihusuki kwa lolote jamani "
" kijana usilete ujanja kwa hiki na hapa hakuna cha kutafuta uchunguzi wowote kuhusu hili ushahidi uko wazi na kesho jiandae kuelekea mahakamani "
Aliongea mmoja wa Askari aliekuwa zamu usiku huo wa siku ya pili, japo balozi wa Tanzania nchini Afghanistan alijitahidi sana kumsaidia raia wa nchi yake lakini ilishindikana kabisa hivyo bwana Emanuel akawa amesubili kifungo tu, usiku huo aliutumia kumuomba mungu ili amuepushe na hukumu iliyokuwa mbele yake lakini haikuwezekana siku iliyofuata ambayo ilikuwa jumatatu alipelekwa mahakamani kusomewa shitaka lililompeleka jela miaka saba, hakuwa na ndugu ama rafiki yeyote wa kumfariji alilia peke yake kadri alivyoweza, ama kumuwekea dhamana.
" sikuwahi fikiria siku moja ningeingia gerezani tena nje ya nchi yangu, leo hii mie Emanuel nafungwa na kudhalilishwa kwa tuhuma za uuzaji madawa ya kulevya, heshima yote imevunjika nani ataniamini tena ,namuacha mwanangu mdogo bila penzi la baba je siku akijua aibu hii sura yangu nitaificha wapi? "
Yalikuwa maneno ya kuhuzunisha sana aliyoyatamka Emanuel akiwa ndani ya gari la wafungwa tayari kwenda kutumikia kifungo cha miaka saba katika gereza la Guantanamo mjini Kabul, ilikuwa imepita miaka mingi sana bila kundondosha chozi lakini siku hiyo alilia kama mtoto mdogo, machozi hayo yalitoka si kwa kifungo hicho lahasha! aliwalilia wazazi wake, wadogo zake pamoja na mkewe kipenzi Janiphar mwanamke alikuwa akimpenda kupita maelezo, kijana wake Poul alikuwa mdogo sana leo hii anakwenda kuishi maisha ya mzazi mmoja kwa miaka saba daaaah! hakika alikuwa na haki ya kulia .
" jikaze mkubwa "
" naumia sana kaka "
"najua ila tambua wewe ni mwanaume na ukizaliwa mwanaume lazima uyapitie haya hapo utakuwa umekamilika na kuitwa mwanaume piga moyo konde kaka "
kwa mara ya kwanza toka aingie ndani ya gereza hilo alijikuta akiongea na mtu, kwani toka afike ndani humo hakupenda kuongea chochote zaidi ya kulia kila alipopata muda wa kufanya vile.
" Omar nashindwa kuelewa madawa yaliingiaje ndani ya begi langu na pia askari walijuaje? "
" daaaa!, je kwani nguo alipanga nani? "Omari aliuliza huku akikaa chini pembeni akiweka fagio lake
" mke wangu na nilikuwa namshuhudia na hata asubhi yake nililifungua na kukagua upya lakini sikuona chochote"
"mmmh!., kweli? "
" ndio!"
" je huna adui yeyote na kabla hujasafiri nani aliijua safari yako? "
"aaaah!, mke wangu na mdogo wangu wa kiume "
" je uhusiano wako na mdogo wako ukoje? "
" hakuna shida tunapendana japo ni mvivu kujituma lakini nishamzoea"
Kuanzia siku hiyo Omari aliekuwa raia wa Omani mfungwa wa maisha ndani ya gereza hilo kwa kosa la mauaji makubwa alijikuta akipatana na Emanuel mtu mweusi aliekuwa hathaminiki mbele ya waarabu ,muda mwingi alitumia kumfariji na kumsihi kutokata tamaa kweli Emanuel alijikuta akianza kuyazoea maisha ya jela na kila kulipopambazuka hakusita kupunguza siku katika karenda iliyokuwa ndani ya kila chumba cha wafungwa.
" mambo Ema "
"sa... safii t... u."CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alijikuta akipata kigugumizi kujibu salamu hiyo kutokana na lugha iliyozungumzwa hakuamini Kama siku moja angeweza sikia mtu akizungumza kiswahili ndani ya nchi hiyo
" najua utanishangaa sana ila fahamu nami ni mtazania natoka mkoa wa Tabora wilaya ya Nzega " kijana huyo alizidi kuongea kiswahili fasaha huku akiwa amesimama karibu kabisa na mlango wa kuingilia chooni, mkononi akiwa na kopo pamoja na fagio ilionekana alitoka kufanya usafi
"aise karibu kabisa na nyumbani kwetu mie natokea Shinyinga wilayani Simiyu (kabla ya kupewa heshima ya mkoa),nashukuru kukufahamu "
Emanuel aliongea huku akinyosha mkono kumsalimia vizuri, siku hiyo alifurahi sana kukutana na mtanzania mwenzake, huo ukawa mwanzo wa urafiki wao.
Siku ya tano toka Mtanzania huyo aliekuwa akifahamika kwa jina la Yuda kuingia gerezani humo Emanuel alitekwa usiku wa saa tano saa za huko, akiwa usingizini aliamshwa na Yuda aliemuomba amsindikize chooni kwakuwa alimpenda na kumjali kama ndugu yake Emanuel alijikuta akitoka nje, bila kujua chochote hata kabla hajafika katikati ya uwanja alishangaa kuona vijana wawili wakimsogelea na kumkabwa wakiwa wamefunika sura zao, walimbemba mzobemzobe hadi nje ya jengo hilo kwa kuruka ukuta akiwa hajitambui baada ya kupigwa kitu kizito kisogoni kilichosababisha apoteze fahamu kwa muda wa dakika saba, fahamu zilipomrudia alijikuta akiwa katikati ya vijana saba ndani ya jengo bovu, Yuda mtanzania aliekuwa akiishi Afghanistan kwa kazi ya ujambazi, Murtaza, Hamayoun na wenzao wanne
"Yuda nimekukosea nini lakini? ,upendo wangu leo unaniua? "
" kaka sio mie " Yuda alizungumza huku akimpiga teke la mbavu
"mmmmmh,!! achaaaaa! "
Sauti hiyo ilipenya vyema katika ngoma za masikio ya Emanuel hali iliyopelekea Emanuel kugeuza haraka shingo maana haikuwa ngeni masikioni
"David!?,Mdogo wangu!??? "
Alishangaa kupita Maelezo kumuona mdogo wake wa damu toka nitoke akiwa maeneo hayo,, akijaribu kunyanyuka lakini ilishindikana kutokana na kamba akizokuwa amefungwa miguuni na mikononi
" ndio ni mie bwana mkubwa "
David alizidi kuongea huku akimsogelea kabla hajamfikia vizuri alimpiga teke la kifuani lililopelekea kutema damu
" kaka ulijifanya mjanja sana leo umepatikana sali sala yako ya mwisho "
" la... khooo! khooo.... lakini sijui kosa langu mdogo wangu, kipi ulikikosa toka kwangu, leo hii unaniua kweli, ok niambie chanzo cha wewe kunifanyia hivi? "
Emanuel aliongea kwa taabu kutokana na kuzidiwa maumivu ndani ya kifua chake
"mali nataka kumiliki zote, siwezi miliki ukiwa hai nitakuteketeza wewe na familia yako "
" kweli!? "
"ndio "
"niko radhi kukuandikisha kila kitu naomba usiniue tafadhali "
" safi sana andika "
Emanuel alikabidhiwa kalamu na karatasi akawa ameandika mali zote kumkabidhi mdogo wake David
" safi sana kaka naomba umsalimie babu na bibi Nyambele "
David aliachia risasi sita zilizokitoboa vibaya kifua cha Emanuel na kupoteza maisha papo hapo, David aliwaamru vijana wake kumpeleka gerezani usiku huo na kumtupia ndani ya ngome kisha wao walitokomea.
*****
Siku iliyofuata David ambaye ni Mdogo wake Emanuel alifika nyumbani kwa kaka yake kama walivyoahidiana na Shemeji yake usiku wa jana yake, swala lililompeleka hapo ni kupanga mikakati ya yeye kwenda Afghanistan kumsaidia kaka yake, Janiphar ambaye ni shemeji yake alikuwa teyari keshajianda kwenda benki kuchua pesa kwa ajili ya Safari hiyo
" usilie shemu, hata sie tunaumia sana "David aliongea huku akijifuta machozi ya kinafiki ili asijulikane
" naumia shemu "
"nafahamu"
Walifka mjini majira ya saa tatu na nusu asubuhi na kupaki gari lao kisha Janiphar akashuka na kuusogelea mlango wa benki ya CRDB, iliyopo jengo la PPF karibu kabisa na GOLD CREST HOTEL barabara ya Kenyatta.
Kwa kuwa siku hiyo hakukuwa na foleni alijikuta akitumia dakika kumi kuchukua pesa kwa ajili ya safari ya shemeji yake
" milioni sitini hizi hakikisha unarudi na kaka yako "
" sawa shemu "David aliongea huku akiipokea bahasha hiyo akijivika sura ya uchungu kupita maelezo
Baada ya kukabidhiana walielekea hofisi za ukataji wa tiketi za ndege mita chache kutoka hapo jengo moja na Mwanza Hotel kwa mkono wa kulia, kushoto kwake kuna tawi la benki ya NMB Kenyatta road.
Japo hakukuwa na nafasi ya kupata nafasi kwa ajili ya David, Janiphar alijikuta akinunua tikeki kwa malipo ya mara tatu ili mradi tu mmewe akasaidiwe. Siku hiyo jioni ya saa moja David aliondoka Tanzania, japo Janiphar alijua shemeji yake anaelekea Afghanistan kama walivyokubaliana lakini alijikuta akiishia Kanya akikoanza kusuka mipango ya kumuangamiza Kaka yake huko huko,
Kwanza kabisa aliwapa kazi vijana wake murtaza na Hamayoun kufatilia kesi ya kaka yake, kujua gereza gani alifungwa, baada ya kufahamu hilo alitulia kwanza kwa muda wa miezi miwili ndipo alipomtuma Yuda kufanya fujo ili tu aingie ndani ya gereza hilo kweli siku saba tu Yuda alifungwa siku mbili baada ya Yuda kufungwa David alisafiri hadi Afghanistan alikokwenda kuungana na vijana wake waliomteka Emanuel gerezani wakisaidiwa na Yuda kisha alimuua.
Hadi kunapambazuka mwili wa Emanuel ulikuwa bado uko pale pale nje, askari wa zamu ndio aliekuja kuuona ukiwa umetapakaa damu ukitisha pia
"kule kuna mfungwa ameuawa "CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"wapi? " mkuu wa gereza aliuliza akiwa haamini alichokisikia
" kwenye domu la watukutu, na ni yule mwafrika toka Tanzania "
" mmmh! " mkuu wa gereza alishusha pumzi ndefu kabla ya kusema chochote , alikikuna kichwa chake kilichokuwa na upala kidogo huku nywele karibia zote zilikuwa zumeanza kujaa mvi,
" twende! "
Alinyanyuka kutoka katika kiti ndani ya hofisi yake Safari ya kwenda ndani ya hospitali ndogo iliyokuemo ndani ya gereza hilo ilianza huku kila mtu akiendelea kuwaza Lake
" inaonekana ameuawa kwa kupigwa risasai na mbaya zaidi macho nayo yametobolewa "alizungumza daktari aliekuwa akifahamika kwa jina la Mohammed Said baada ya kufika kwa asksri magereza hao
" je wafungwa wote wapo? "
" hapana mkuu yule mwafrika mpya nae hayupo "
" aaaah,! shida kweli "
Baada ya maongezi hayo waliondoka eneo hilo wakiwa na wazo la kuutarifu ubalozi wa Tanzania nchini humo kuhusiana na tukio hilo, hakika zilikuwa taarifa za kusikitisha masikioni mwa balozi huyo baada ya kupewa taarifa hizo nae aliamua kuwasiliana na serikali yake kuhusiana na tukio hilo la kuuawa kwa Emanuel.
Taarifa zilipoifikia familia yake hakuna alieamini hata kidogo mke wake alilia kupita maelezo achilia mbali ndugu jamaa na marafiki ,ulikuwa msiba mkubwa sana uliolikumba taifa la Tanzania hata serikali iliumia sana kumpoteza kijana aliekuwa akiingiza pato la taifa kila iitwapo leo ,mji wa mwanza ulijaa wangeni kutoka mikoa mbalimali.
"Mama mme wangu wamemuua mamaaa! "
Janiphar alikuwa akimlilia Mama mkwe mara baada ya wazazi wa Emanuel kufika nyumbani kwake majira ya saa tisa alasili wakitokea Simiyu, kilio ndicho kilichowapokea ndugu hao waliokuwa wamekonda kutokana na kulia kwa muda mrefu sana , toka siku waliyopata habari ya msiba huo kilichokuwa kikifanyika ni kilio tu .
"pole mamaaaa ha.. hata... sisi linatuumiza sana nimempoteza Emanuel wangu " Mama mkwe aliongea kwa huzuni huku akilia kama mtoto mdogo akiwa amekumbatiana na mke wa Emanuel
"shemeji nae amepigwa vibaya sana"
"nani David! !?"
"ndio mama walitekwa wote usiku "
" masikini watoto wangu "
Hakika yalikuwa maumivu yasiyopimika ndani ya mioyo yao kuuawa kwa Emanuel na kupigwa kwa David kama walivyopata habari kutoka Afghanistan iliwaumiza sana, hakuna hata mmoja aliekuwa anaujua ukweli . Baada ya David kutekereza adhima yake aliamua nae ajiumize kiaina ili kuficha ukweli halisi ,kweli usiku huo huo aliiamua kujipiga risasi ya mguuni sehemu aliyona ingepona mapema, mikono nayo aliijeruhi achilia mbali usoni japo aliumia lakini hakujali roho ya dhuruma ilikuwa imemtawala kupita maelezo.
" bwana alitoa na bwana ametoa jina lake lihimidiwe, najua tunaumia sana kumpoteza mpendwa wetu ila kazi ya mola haina makosa, leo Safari ya mpendwa wetu Emanuel imeishia hapa nasi tumuombe mungu atusaidie kuishi maisha ya utakatifu hapa duniani, zaidi na zaidi tumuombe mungu ampumzishe pahali pema peponi ndugu yetu alietutangulia "
Yalikuwa ni maneno ya kuhuzunisha na kufariji kiasi flani kutoka kwa Padri Biruru ndani ya kiwanja cha kanisa kathoric bugando jijini mwanza, kutokana na idadi kubwa ya waombolezaji kufurika kanisani hapo misa ya mazishi ilifanyika nje ya kanisa ndani hakukufaa kabisa. Hakuna mtu alieshindwa kutoa machozi pindi alipoyatupia macho yake katika jeneza la Emanuel kipenzi cha watu mkoani hapo, mashirika mbalimbali nayo hayakuwa nyuma, vituo vya watoto yatima alivyokuwa akivisaidia navyo havikukosa kumsindikiza mpendwa wao.
" Mama Baba atakuja lini? "
"sass! ha..... "Janiphar alishindwa kujibu swali hilo kutoka kwa mwanae mdogo poul aliekuwa na miaka mitatu tu, swali hilo lilizidi kuumiza moyo wake, hakujua ajibu vipi ama aseme nini
" mama baba mbona haji? "
Poul alizidi kumsumbua mama yake aliekuwa hajiwezi kwa lolote na kila alipoyaruhusu macho yake kulitazama jeneza alipoteza fahamu.
Baada ya misa hiyo kumalizika safari za kuelekea makaburi ya Kangae wilaya ya Ilemela ilianza wakipitia barabara ya musoma, walipofika buzurunga walikata kushoto kuitafuta nyakato mecca, papo hapo kituo cha mecco walikata kushoto tena wakifuata barabara ya vumbi hadi makaburini, zoezi la kumhifadhi Emanuel halikuchukua muda mrefu hivyo Safari ya bwana Emanuel tajiri kijana ikawa imefika mwisho
" hakikisha unaitunza hiyo hati ya hoteli "
" sawa baba, ila vipi kuhusu hizo zingine? "
Msichsna wa kazi alimuuliza David ambaye hakuhuzuria maziko ya kaka yake kuanzia kanisani hadi makaburini akijifanya kuzimia kutokana na kulia sana hivyo ndugu hao waliamua kumuacha nyumbani, nusu saa baada ya kutoka nyumbani waombolezaji hao alizinduka na kuelekea chumbani kwa kaka yake alikoiba kila nyaraka za maana akiwa dakika za mwisho Vero msichana wa kazi alimfumania.
"zipo... zipooo kwani... vipi? "
Alishindwa kuongea vizuri baada ya kukaziwa macho makali na msichana huyo aliekuwa ameanza kumstukia muda mrefu hata kabla ya kifo cha boss wake ila hakuwa na uhakika hata kidogo.Hakutaka kukaaa tena chumbani humo alitoka akiwa anachechemea akielekea chumbani kwake
" huyu hanijui eeeh! ,nampa masaa 120".
" huyu hanijui nampa masaa 120"
David aliwaza maneno hayo huku akitembea kwa kuchechemea kutoka ndani ya chumba cha kaka yake, moyo wake ulijaa hasira isiyoelezeka hata kidogo aliona kila kitu kitaenda fyongo na siri yake ingetambulika na hilo hakutaka litokee hata kidogo.
" puuuuuuh! "
Alivuta pumzi ndefu baada ya kufika chumbani kwake alikojitupia kitandani kama mzigo puuu akiwa chali macho yake akiyaruhusu kutazama dali lilokuwa limenakishiwa kwa jipsamu rangi nyeupe ikiwa imepambwa vyema na maua ua. Dakika saba alitumia kufikiri ni kifo gani kingemfaa Vero tena kisicho na makelele ama maumivu
" hahaha! "
David aliachia cheko changa lenye maumivu ndani yake baada ya kupata jibu la kazi yake.
" Hail poison itamtosha huyu "
Hii ilikuwa ni sumu hatari sana yenye asili ya hewa hewa ambayo mtu ama kiumbe hai kikipewa sumu hii dakika tatu kinapoteza maisha huku akikiwa amebadirika rangi ya ngozi kuwa nyeusi, sumu hiyo aliipata nchini Austaria kwa gharama kubwa sana ndio aliona suruhisho tosha kutekeleza adhima yake aliyokuwa amekusuudia ya kumuangamiza Vero.
" atakoma" aliongae huku akinyanyuka kitandani hapo na kuliendea Begi lake dogo lililokuwa na sumu hiyo lakini kabla hajafanya chochote alipatata wazo la kurudisha nyaraka alizokuwa aneziiba chumbani kwa shemeji yake ,kweli alikubaliana na wazo hilo alinyanyuka haraka sana.
" sijui nimweleze Mama" Vero aliwaza akiwa bado amesimama ndani ya chumba cha boss wake mkononi akiwa bado ameshikilia hati ya hoteli aliyokuwa amepewa na David baba mdogo wake, kilichomshitua ni kufunguliwa kwa mlago tena kwa kasi ya ajabu haraka aliigeuza shingo yake na kukutana na David akiwa ameshika karatasi tano
" unafanya nini "
" aaaaah!, ba... baba.. nina... "
Vero ama Veronica alishindwa kuongea baada ya kukaziwa macho makali na Baba yake huyo Mdogo aliekuwa bado asimama katikati ya mlango
" pishaaa"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliongea huku akianza kutembea kuliendea kabati, Vero hakutaka kuendelea kubaki hapo aliondoka na ile hati hadi chumbani kwake na kuificha ndani ya begi lake dogo la nguo aina ya Omega rangi ya ugoro lililokuwa sakafuni bila kuwekewa kitu chochote chini .
" kazi ipo hapa daaa sijui tutasalimika huyu ni nyoka tena koboko daaa!. yawezekana hata Baba alimuua huyu "
Kwa kuwa Vero alikuwa Binti aliejitambua na kujaliwa uelewa mkubwa alianza kumstukia David na kupanga mikakati ya kupambana nae bila kujua kama mwenzake alikuwa mafia na jambazi mkubwa.
" kesho nakiondoa duniani kijinga sana "
Aliwaza huku akiondoka chumbani humo kwa Mara ya pili.
*****
Kesho nakiondosha duniani kijinga sana "
Aliongea huku akiondoka chumbani humo kwa Mara ya pili.
Baada ya lisaa limoja kuondoka waombolezaji walilejea kutoka makaburini hivyo David aliendelea kujiuguza tena.
Kesho yake kikao cha familia kilichukua nafasi na pendekezo lililopatikana Janiphar ataendelea kuwa msimamizi mkubwa wa mali zote akisaidizana na David, kwa kuwa hakuna na shaka nae yeyote akuwa na budi kumkataa na ukizingatia walikuwa wakifanya kazi nae muda mrefu hata kabla ya kifo cha mmewe.
"afadhali mambo yangu yameanza kwenda vyema sasa"
" kiaje David? " Eric miongoni mwa marafiki zake waliokuwa hawafanyi kazi zaidi ya kutegemea kodi kutoka kwenye nyumba zao za uridhi zikizokuwa mtaaa wa uhuru mkabara na mount meru university
" si kuhusu yule demu? " David alisema huku akichukua kipande cha nyama choma ndani ya sahani wakiwa Kumalija Hoteli iliyoko nyegezi stendi usiku huo
"aaah!,sikia huwezi kukiua kibinti kizuri kama kile bila kukila kwanza, tukiteke kikiwa kinaenda sokoni tukakibake kwanza harafu ndo tukiue "
" kile hakifai kichafu "
"mie naugwadu mtu wangu nipe nipunguze mafuta mwilini "
" basi poa kesho jiandae, "
Japo zilikuwa siku mbili tu baada ya kuzikwa kwa Emanuel David alikuwa tayari ameanza kunywa pombe, hakuwa na huruma hata chembe na mbaya zaidi alikuwa akianza kumuwinda Vero ambaye nae alikuwa amedhamilia kupambana nae.
kikao kati ya David na Eric kilivunjwa baada ya wao kwa wao kuanza kutoleana maneno ya kashifa usiku huo, hakiri ya David ilikuwa ikifanya kazi zaidi ya computer, vyovyote vile aliamini lazima Erick angemsaliti na hilo huwa hakubaliani nalo hata siku moja
" lest in peace Erick ( pumzika kwa amani Erick) "
David alizungumza maneno hayo huku akiwa anatoa machozi ya hasira iliyochanganyikana na uchungu, mkononi alishika bastola yake aina ya Berreta isiyo na sauti, aliibusu huku akiendelea kuiomba ifanye kazi yake sahihi,japo Erick hakuepo lakini tayari alishapanga kumuua usiku huo huo. Aliwasha gari na kuondoka hotelini hapo akiwa na hasira zisizo elezeka safari yake iliishia mtaa wa uhuru nyuma ya Wande hoteli hapo ndipo Erick alikuwa akiishi zaidi ya dakika 180 alikuwa eneo hilo akiwa anaendelea kuvuta sigara aina ya ESM ndani ya gari la kaka yake.
" safi sana " aliongea peke yake mara baada ya kumuona Erick akija eneo hilo, papo hapo aliichomoa bastola yake iliyokuwa kiunoni , aliikagua kama ilikuwa na risasi, alitabasamu mara baada ya kukutana na risasi tatu alimulenga Erick kichwani ,risasi moja tu ilikimaliza kichwa chake kisha aliondoka eneo hilo bila mtu yeyote kuona hiyo ilisababishwa na hali ya mvua usiku huo. Hakuwa na hofu yeyote dhidi ya vyombo vya dola, zaidi ya viogozi wakubwa walikuwa marafiki zake, pia heshima ya marehemu kaka yake aliitumia kufanyia uovu na uozo uliopindukia.
******
"lete bia hapa wewe kahaba! "
Erick aliongea kwa Sauti ya kilevi iliyochanganyikana na ukali kiasi,
"mshikaji punguza maneno machafu"
" wewe acha kuongea pumba hawa ni mamalaya tu yanat **** ,kila siku "
Erick aliendelea kuporomosha maneno makali dhidi ya wasichana wale hasa hasa akina Dada waliokuwa wamebarikiwa ama kujaliwa makalio makubwa ,hakujali maneno yake kwamba yalikuwa mwiba kwa wengine, yeye aliona kila muhudumu ndani ya kumalija hoteli alikuwa malaya.
Wakiwa wanaendelea kunywa na kutafuna nyama choma ghafla alitokea Diana rafiki yake na Erick, David alipomtazama tu alihisi mapigo ya moyo kuongezeka, kutokana na uzuri wa Diana alianza kutumia nguvu za kumchukua Diana hali hiyo Erick hakukubaliana nayo hivyo nae alianza kumrushia maneno bila kujua kama mwenzake hakuwa mtu wa kawaida hata kidogo
"tena umkome Diana muone kama kituo cha polisi nakuambia hujui tulikotoka "
" wewe unahela gani ya kumpa mtoto mkali Kama huyu, hebu njoo mchumba " aliongea huku akianza kumfuata Diana, alifika na kumkumbatia kwa lazima , mikono yake akipapasa mgongoni kwa Diana aliekuwa ametulia kama maji mtungini, kitendo hicho kilimkera sana Erick alinyanyuka katika hali ya kilevi levi akiwa na chupa mkononi hata kabla hajawafikia vyema aliirusha ile chupa iliyotua vyema kichwani kwa David na kusababisha mpasuko kidogo
" mtu mbaya sana wew izoee familia yako, hapa umefika nitakuua muuaji mkubwa wew "
"Erick!!!!!!!!!? "
"ndio hivyo nakueleza si umezoea kuua wengine kwangu huwezi, nitakuonesha na kesho unaenda kuishi nyuma ya nondo "
Erick alizidi kutoa maneno makali sana yaliyozidi kuukera moyo wa David, tayari ndani kwa ndani alianza kutoa machozi, alihisi moyo wake ukivuja damu, macho yalianza kuona ukungu ukungu achilia mbali nyota nyota zisinzo na idadi, kwa hasira akitoka ndani ya Hoteli akiwa anaendelea kulia kimoyo moyo akimuhurumia Erick .
*****
"Mama naomba uwe makini sana na ba Mdogo "
" kwanini vero? "CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliuliza Janiphar akiwa anaendelea kupanga panga vitu ndani ya chumba chake
" aaaah! ,basi tu ila nakuomba tu ufanye hivyo laz..... "alishindwa kuendelea baada ya kuhisi nyayo za mtu zikitembea kuja eneo hilo
" aaaah!, shemu nakuona uko.... "
David aliyakatisha maneno yake baada ya kukutana na macho makali kutoka kwa Vero
"wewe mshenzi wewe utanikoma nakuondoa duniani leo "David aliwaza ndani ya moyo wake huku akimtazama Vero macho makali sana.
" niambie shemu najiandaa wiki ijayo niruhusu baadhi ya hofisi ziendelee na kazi na wew utakuwa unasimami nikiwa bado sijaanza kutoka "
"sawa sawa shemu tena itakuwa njema vipi Vero huendi sokoni nataka kukuagiza "
"haendi leo anasafari ya kwenda kwao mara moja "
"aaaah!, sa.. wa ,ataondoka saa ngapi? "
"yuko tayari muda huu huu Dominic ndie anaemchelewasha "
"anaondoka nae ama? " Erick alizidi kupeleleza ili ajue jinsi ya kummaliza Vero kabla hajafungua mdomo wake , japo alikuwa akitumia mdomo kuongea lakini hakiri iliwaza njia ya kummaliza Vero
"atampeleka Buzuruga stendi , kisha ataondoka kwa bus la Zakaria "
Masikini Janiphar hakujua kama alikuwa akimua Vero tena bila huruma.
"oky, Vero nakutakia safari njema yenye mapumziko ya amani ila tutakukumbuka sana "
Vero hakuyajibu maneno hayo maana yalikuwa na ujumbe mzito ila umkiyachukulia poa yalikuwa ya poa tu.
" shemu baadae "
" haya shemu "
"lakini Mama David sio mtu mzuri hata kidogo sikiliza maneno yangu "
Vero alizungumza huku akitia huruma alimuonea huruma tajiri yake , hakujijali yeye maana uwezo wa kupambana na David alikuwa nao, na kilichomuuma zaidi ni poul kitoto kilichokuwa kidogo sana lakini kilikuwa kinapelekwa kubaya kama Mama yake asipokuwa makini
"Vero sipuuzii maneno yako ila David tumefanya nae kazi muda mrefu sana, na tabia yake naijua sio mtu mbaya kama unavyofikiria , istoshe nikimfukuza mapema hii huoni nitamtenga mwanangu na ndugu zake, hapana Vero "
"sawa Mama acha niondoke naona Domi keshafika " aliagana na ndugu waliokuwa bado wapo nyumbani hapo kisha aliondoka
" naomba tupitie barabara ya Igogo kisha tukaikamate ile ya kutoka Shinyanga inayoelekea airport ,tutaiacha baada ya kufika kona ya kuelekea kilimahewa kisha tunaekekea Nyasaka man... "
"sina mafuta ya kuchezea Vero "
"oky niache nichukue pikipiki"
"lakini Mama kadai nikupelekea Buzuruga "
"nifuate nisemacho kama hutaki acha "
Vero alizungumza kwa ukali huku akifungua mlango wa gari akiwa na nia ya kushuka, kabla hajafanya hivyo Dominic alimzuia na kuwasha gari akifuata maelezo ya Vero.
Dakika sirufuri wao kuondoka David nae aliondoa gari lake eneo alilokuwa amejificha akiwafatilia kwa nyuma nyuma huku akiendelea kuwasiliana na vijana wake ambao tayari walikuwa wameshafika Buzuruga stendi.
"Domi hebu simama kwanza "
Vero aliongea huku macho yake yakiwa bado yametazama setimira, kana kwamba alikuwa ameona kitu
"Vero acha usumbufu bhana ndo kwanza dakika kumi tu, toka tumeanza Safari tambua na mambo ya kufanya si kukupeleka wew tu "
Domi alizungumza bila kumtazama usoni, ila muonekano wake tu ulionesha dhahili alikuwa amechukizwa na kitendo kile
"Domi nisikilize kuna kitu sikielewi kabisa "
" kiaje? "
"nahisi nafuatiliwa sasa fanya hivi endesha gari kwa kasi, ukifika pale kwenye kona punguza mimi nitaruka " Vero alizungumza huku akitoa begi lake nyuma ya siti aliyokuwa amekaa, japo kilikuwa kitendo cha hatari sana lakini hakujali bora afe kwa ajali ila si kifo cha mateso kutoka kwa David .
" unajua sikuelewi Vero? "
" utanielewa muda mfupi fuata ninachokuambia Domi "
Japo aliongea lakini macho yake hayakutulia upande mmoja, kila sekunde alitazama nyuma kupitia setimira,
" punguza mwendo Domi "
"unajua u..... "
hata kabla hajamalizia sentesi yake, tayari Vero alikuwa ameshafungua mlango akijilazimisha kuruka ndani ya gari, ilibidi Domi apunguze mwendo akiwa hajui kinachoendelea
" maisha mema Domi, ila nakuomba usimwambie mtu chochote, pia ondoka eneo hili kabla ya David kufika "
"Vero.. Vero sikuelewi jamani "
"ondokaaaaaa "
Aliongea huku akikimbia kuelekea ndani ya makazi ya watu eneo hilo la Igogo sehemu inayosifika kuwa na idadi kubwa ya watu, wenye hali ya chini kabisa ndani ya jiji la mwanza ama unaweza ukapaita uswahini. Kwa kuwa hakukuwa na njia ya moja kwa moja zaidi ya vichochoro chochoro vilivyompa Vero nafasi ya kutokomea ndani ya dakika mbili tu.
"piiiiii!, piiiii!"
Sauti kali na yenye kustua ilimshitua Dominic aliekuwa bado amesimama eneo hilo asijue cha kufanya
".........nakuomba uondoke eneo hili mapema kabla ya David haja.... "
Alijikuta akiyakumbuka maneno ya Vero aliyokuwa amezungumza nae muda mfupi kabla ya kutokomea uswahilini, nae hakutaka kuendelea kusisimama tena eneo hilo wala hakujali mfurulizo wa honi kutoka kwa David aliekuwa akija kwa kasi sana.
"duuu! hatari" David aliongea peke yake huku akizidi kumfukuza Dominic, lakini ajikuta akiambulia patupu hiyo ilisababishwa na uwezo mdogo wa gari lake kupambana na landcurser vus8 aliyokuwa nayo Dominic .CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"shitii! mfyuuuuuuuu"
David alijikuta akisonya kwa hasira baada ya kumkosa Dominic , aliupiga ngumi usukani kwa hasira zisizoelezeka, tayari uso wake ulikuwa umeanza kutengeneza matuta matuta, mishipa ya shingo nayo haikuwa nyuma kuisindikiza hasira hiyo, alijihisi joto jepesi jepesi japo ndani ya gari hilo kulikuwa na ac.
" siwezi nikazidiwa ujanja na mafala hao " aliongea huku akiongeza gia, hakiri yake ilishahama tayari. Kutoka Igogo hadi Buzuruga stendi hapakuwa mbali sana ukizingatia mji wa mwanza hauna foleni sana hivyo alijikuta akitumia dakika kumi na tano tu.
"vipi mmemuona? "
"hapana hajafika mtu yeyote,kwani vipi ?"
" vimenitoroka, sasa fanyeni hivi jigaweni kuanzia hapa hadi kisesa hakikisheni kila basi linalopita mnalisimamisha na kulikagua lazima atapatikana tu "
Sawa boss ".
Vijana wale hawakutaka kupoteza muda walitekeleza maelezo hayo kutoka kwa boss wao lakini hadi inaingia usiku Vero ama Dominic hakuonekana, ikambidi David kuahilisha adhima yake na kulejea nyumbani kwake akiwa amekasirika bila kipimo.
*****
Vero alizidi kukimbia bila kutazama nyuma,hakujali michubuko aliyokuwa anaipata pindi alipokuwa akijikwaa, muda mwingine alianguka lakini alinyanyuka na kuendelea kukimbia akizidi kutumbukia ndani ya makazi hayo. Dakika thelathini ndipo aliposimama na kukaa sehemu iliyokuwa imejificha,huku akihema mithili ya mbwa aliekuwa akikimbiza mwizi,
" sasa nitetokaje ndani ya mji huu? ,au eeeeh! "aliwaza peke yake huku akisimama tayari alikuwa ameshapata wazo la kutoka mwanza akiwa salama, hofu tena ya kukamatwa na David ilikuwa imetoweka kivyovyote vile asingeweza kumpata uchochoroni humo . Alinyanyuka na kujipangusa vumbi lililokuwa limeushambulia mwili wake kisha alinyanyua begi lake alijitwika na kuanza kusonga mbele bila kufahamu ni wapi angetokea, zaidi ya saa moja alitumia kutembea bila kuona barabara yeyote zaidi ya vichochoro
"hujambo mtoto mzuri "
"sijambo shikamoo dada "
"mar -haba , hivi hii njia inaelekea wapi? "
Vero aliuliza huku akiwa amesimama mzigo kichwani
"kwani wew unaenda wapi? "
"nataka barabara kubwa ya kwenda nyegezi stendi "
"ooooh!, umepitiliza njoo nikuoneshe, kwanza umeshafika kona ya butimba "
Kile kitoto cha kiume kilichokadiriwa kuwa na miaka saba ama nane kilimuonesha Vero njia ya kutokea kona ya butimba, kichwani akiwa na dhamira ya kwenda Kwao akipitia barabara ya busangala.
Baada ya kupata maelekezo hayo alikapatia noti ya shilingi mia tano kama ishara ya shukurani, kweli kalifurahi sana na kumuombea safari Norma, dakika tatu tu alijikuta alitokea barabarani hapo alipochukua daladala hadi Nyegezi stendi kisha alitafuta usafiri uliompeleka busangala, alishuka hapo na kugojea usafiri wa aina yeyote utakaompeleka Bunda , bahati ilikuwa yake ndani ya dakika kumi alipata lori lililokuwa likielekea Musoma, Vero alishukuru sana pia alijipa ushindi wa kutoka ndani ya jiji la mwanza akiwa salama.
"kaka ahsanteni sana mungu awabariki "
"usijali Dada "
Aliwashukuru vijana wale kwa msaada waliompatia kutoka Busangala hadi kona ya kwenda Tarime bila malipo yeyote
"je nitapata usafiri kweli? "
"aaaaah! mapema hii ,bando kuna basi la Zakaria linalotoka mwanza saa kumi na mbili na la kutoka Musoma kwenda Tarime halijapita ondoa wasiwasi dada ".
Baada ya mazungumzo hayo Vero alishuka ndani ya lori hilo na kutafuta sehemu ya wazi, alikaa, huku akiendelea kuwatazama wafanyabiashara wadogo wadogo waliokuwa wakifanyaka biashara eneo hilo .CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Tarime tarime elfu tano "
Sauti ya konda ndiyo iliyomsitua Vero kutoka katika lindi la mawazo alinyanyuka na kuelekea ndani ya basi huku akiwa haamini kama kweli alikuwa amesalimika.
*****
Usiku mzima David hakupata lepe la usingizi hata kidogo zaidi ya kujigeuza kila upande wa ubavu wake, hali ilipozidi kuwa mbaya zaidi alinyanyuka kitandani hapo na kuelekea sebuleni, kilichokuwa kikimuumiza zaidi ni jinsi ya kumpata Vero, uwepo wake duniani ungechangia yeye kutopata kile alichokuwa amekisudia
"nitakamalizaje? "
David alizidi kuongea peke yake huku akiwasha television usiku huo wa saa tisa , japo macho yalikuwa yakiitazama television hiyo lakini mawazo hayakuepo hata kidogo,
"acha niongee na Deus atajua nini cha kunishauri ".
Aliongea huku akinyanyuka kitini hapo ,alielekea chumbani kuifuata simu yake ili aongee na Deus mwananaume aliemfundisha kazi ya ujambazi, pia Deus huyo huyo alikuwa rafiki wa kaka yake Emanuel lakini walikosana baada ya Deus kumzurumu Emanuel kiasi kikubwa cha pesa.
"niambie kaka? "
Upande wa pili ulisikika ukiongea baada ya simu kupokelewa
"si kama nilivyokueleza mchana kaka kile kimalaya kimenipotea sasa nahofia usalama mjomba "
"hahahaha kweli wew hujakomaa , lala kesho njoo hofisi nikupe njia "
Deus alizungumza hayo kisha alikata simu, akimuacha David njia panda.
David alibaki ameishikilia simu sikioni kana kwamba alikuwa bado anaongea na mtu ,zaidi ya dakika tatu alikuwa bado yuko katika hali hiyo hiyo.
"puuuuu! ".
Alishusha pumzi ndefu kisha aliutoa mkono wake, alichukua rimoti na kuizima television, taratibu alianza kutembea kuelekea chumbani kwake akiwa bado amechanganyikiwa, hakujua ni kipi Deus angeenda kuongea nae hiyo asubuhi tarajiwa ,alifika na kujitupia kitandani huku sendozi zikiwa bado miguuni, macho yake yaliendelea kulitazama dari, kila alilowaza halikufanya kazi muda mwingine alitamani kulia lakini alishindwa .
" au nikifuate kijijini kwao?, ila sipafahamu! "swali na jibu alilipata yeye, hadi inaingia saa kumi na mbili asubuhi hakuwa amepata usingizi, aliamka na kuelekea bafuni alionga kisha alielekea jikoni alikoandaa chai, baada ya kuvaa alilejea na kukuta chai ikiwa tayari, hakutaka kuelekea kokote pale pale jikoni ndiko alikonywea chai na kipande kimoja cha mkate.
" Baba uko hofisini kwako? "
aliuliza David huku akiingia ndani ya gari lake
"aaaah dogo mie hadi muda huu niwe sijafungua hofisi, nina pesa gani, ninyi ndo wenye utajiri sema mnauchezea "
"hahahaha, una masihara mtoto wa kasuru wewe, unatafuta pesa kama mchanga ?"
"nimetoka kigoma kutafuta pesa sio kushangaa rami, kata simu njoo "
"poa kaka dakika ishirini ".
"puuuuu! "David alishusha pumzi ndefu kisha alichomeka funguo wa gari na kuwasha, Safari ya kuelekea hofisini kwa Deus hofisi zilizokuwa mtaaa wa rumumba katikati ya jiji la mwanza ilianza, njiani alikuwa na mawazo chungu nzima, zaidi na zaidi alimuwazia Deus, hakumuelewa mtu huyu japo walikuwa marafiki wa muda mrefu sana lakini hakuwa akimfahamu zaidi, alikuwa na pesa nyingi sana lakini kilichokuwa kikimshangaza zaidi ni tabia ya rafiki yake huyo kufungua hofisi yake asubuhi ya saa kumi na moja, huku wafanyakazi wake wakiingia kuanzia saa moja na robo hadi saa mbili.
"kila mtu na maisha yake bhana kivyake "ilibidi David ayapuuzie mawazo yake yaliyokuwa yakimuumiza bila kupata jibu, mji wa mwanza hauna foleni sana na hata ikiwepo huwezi tumia muda mrefu sana barabarani, David alijikuta akitumia dakika arobani tu kufika hofisini hapo akitokea pansiasi soko jipya huko ndiko alikokuwa amejengewa na kaka yake marehemu Emanuel.
"habari yako dada "
"nzuri,mambo kaka "
"safi tu sijui boss yupo? " David aliuliza baada ya kufika hofisini hapo, japo alikuwa akifahamu uwepo wa Deus, lakini alitaka kujihakikisha zaidi.
" yupo tena huyooo aaah! "
Dada aliekuwa akifanya kazi ya ulinzi hofisini hapo nyakati za usiku aliongea huku akiendelea kunywa kahawa, modomo ukiwa umejaa tabasamu tele , kwa kuwa David hakuwa mgeni hofisini hapo mara moja akipandisha ngazi kuelekea hofisini humo.
"aaah! Kaka niambie,"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"safi tu, karibu dogo nipe michakato"
Deus aliongea huku akimimina kawa ndani ya kikombe kidogo na kumkabidhi David alieipokea kwa mkono wa kushoto, na kunywa fundo moja, kabla ya kukaa, alikiweka mezani kikombe hicho, akinyosha mkono kusalimiana na Deus.
"eeeh!, leta habari bwana mdogo "
"sina mengi ni kuhusu kile kitoto"
"aaah hicho achana nacho, hakiwezi kuongea chochote, kwanza kishamba kipotezee, fuata taratibu ya pili ambayo ni ya muhimu zaidi na ndo itakayokupa maisha sawa dogo"
"nakuelewa ila... "
"toa neno ila David, kama uliweza kumuua fala utawezaje kukimalizi hiki kidogo ,ondoa mawazo fanya kazi, "
"basi sawa "
******
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment