Simulizi : Mungu Pekee Ndiye Atakayenisamehe
Sehemu Ya Tano (5)
Tunawatia nguvuni, naamini hilo” Polisi mmoja alisema katika kipindiambacho walikuwa wamebakiza kilometa mbili kabla yakufika sehemu husika yakuuvuka mpaka ule na kisha kuingia nchini Marekani.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Antoniohakuonekana kuwa na furaha, kifo cha baba yake kilikuwa kimemletea huzuni kubwamoyoni mwake, hakuonekana kuamini kama kweli urafiki mkubwa ambao alikuwa naopamoja na Alan siku hiyo ungefikia kama hapo ulipofikia. Hakumpenda Alan,alimchukia kupita kawaida na katika kipindi hicho alikuwa akitaka kumuua tu.
Hakutaka kwenda hospitalini kuusindikizamwili wa baba yake, alikuwa amebakia nyumbani huku akiwaataarifu watu kuhusianana msiba huo na huku akisubiri simu kutoka kwa Pablo na kumwambia ni kitu ganiambacho kilikuwa kimeendelea. Hakukuwa na simu ambayo aliitaka iliyoingiasimuni, kila simu ambayo ilikuwa ikiingia ilikuwa ni kutoka kwa watu wenginetena huku wakiuliza mengi kuhusiana na msiba.
Watu nyumbani hapo wakawa wamejaa na kila mtualikuwa akitaka kuuona mwili wa mzee Sanchez ambao ulipangwa kuagwa sikuinayofuatia. Alan alikuwa bize, alikuwa akizunguka huku na kule kama mtu ambaye alikuwa amechanganyikiwa, hakutakakuongea na watu wengi mahali hapo, kitu ambacho alikuwa akikifikiria ni kupokeasimu kutoka kwa Pablo tu.
Muda ulizidi kusonga mbele, mshale wasekunde, dakika na saa ikazidi kwenda mbele lakini hakukuwa na simu yoyoteambayo iliingia kutoka kwa Pablo. Antonio akaonekana kuchanganyikiwa, hakujuani kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea mpaka Pablo kuwa kimya kiasi kile,hakujua kama Alan alikuwa amekamatwa au la.Alichokifanya ni kuchukua simu yake na kisha kumpigia Pablo.
“Imekuwaje sasa? Mmempata?” Antonioaliuliza.
“Vijana wamenipigia simu muda mchache uliopita”Pablo alijibu.
“Wamesemaje? Wamewapata?”
“Hapana”
“Ila?”
“Wamesema kwamba wanakwenda mpakani PiedrasNegras” Pablo alimjibu Antonio.
“Piedras Negras?” Antonio aliuliza hukuakionekana kushangaa.
“Ndio”
“Kivipi na wakati Mendez alisema wanakwenda Laredo?” Antonioaliuliza.
“Hata mimi nashangaa. Nadhani walimdanganya”
“Sawa. Sasa kuna uhakika wa kuwapata wote?”
“SIjajua, ila wamesema kwamba inawezekana”
“Basi waambie wawahi, sitaki huyo mtu nawenzake waingie nchini kwao, wakiingia nitakuwa nimeshindwa kukamilishaninachotaka kukamilisha” Antonio alimwambia Pablo.
“Hakuna tatizo”
Antonio hakujua ni kitu gani ambachoalitakiwa kukifanya, mategemeo yake yote yalikuwa ni kwa polisi hao ambaowalikuwa wakielekea mpakani huku wakiwafuatilia Alan pamoja na watu ambaoalikuwa nao. Hapo ndipo akagundua kwamba Alan alikuwa mtu hatari katika kuchezana akili yake pamoja na polisi hasa kwa kile kitendo alichokitumia chakumdanganya Mendez.
Muda ukazidi kusonga mbele, hakukuwa na simuiliyoingia. Antonio alibaki kwenyehuzuni, hakuamini kama polisi walikuwawamelitia maanani suala lake au walikuwa wamelipuuzia. Saa la kwanza likapitalakini hali ikawa kimya, saa la pili nalo likapita lakini mambo yalikuwa vilevile. Antonio akawa na presha kubwa, alikuwa akitaka kufahamu ni kitu ganiambacho kilikuwa kikiendelea, alitaka kufahamu kamaAlan na wenzake walikuwa wamekamatwa mpakani au la.
“Vipi?”
“Walisema kwamba wamefika mpakani” Pabloalijibu.
“Wakasemaje?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Simu ilikatika, bila shaka chaji ilizima”Pablo alimwambia Antonio.
“Simu ilizimika?”
“Ndio”
“Ya nani?”
“Yao”
“Kwa nini hawakutumia redio call?”
“Sijajua. Ila nafikiri kazi imekamilika hasamara baada ya kufika mpakani” Pablo alimwambia Antonio.
“Kwa hiyo unadhani kazi imekamilika?”
“Ndio”
“Sawa. Fuatilia kwanza mpaka ukabidhiwe huyomtu mikononi mwako” Antonio alimwambia Pablo.
“Hakuna tatizo” Pablo alijibu.
****
Dokta Pedro akaambiwa kila kilichokuwakikiendelea kwamba kulikuwa na mgonjwa ambaye alikuwa akihitaji huduma mahalihapo. Dokta Pedro akapelekwa mpaka katika gari lile na kisha kuanza kumwangaliaJocelyn. Jocelyn alionekana kuwa kwenye wakati mgumu, muda wote alikuwaakilalamika kana kwamba alikuwa akienda kujifungua muda mchache ujao. Alan badoaliendelea kuwa bize, kila wakati alikuwa akimfuta maji Jocelyn, maji ambayoyalionekana kuwa kama jasho pajini mwake.
Alan hakugundulika, kofia yake ya kipolisiilikuwa kichwani mwake tena akiwa ameishusha huku akiwa amemuinamia Jocelyn.Sura yake haikuwa ikionekana jambo ambalo halikuwa rahisi kugundulika kama alikuwa yeye. Dokta Pedr akaufungua mlango wa garilile na kisha kuanza kumwangalia Jocelyn, pamoja na udaktari wake na uzoefumkubwa ambao alikuwa nao hakuwa akifahamu kamayule mtu ambaye alikuwa akimwangalia hakuwa na ujauzito bali zilikuwa nguo.
“Kumbe mjauzito!” Dokta Pedroalisema hukuakionekana kushtuka.
“Ndio” Mkuu wa polisi alimwambia.
“Mbona hamkuniambia kamahuyo mtu mwenyewe ni mjauzito?” Dokta Pedro alimuuliza polisi yule.
“Kwani kijana wangu hakukwambia?”
“Hakuniambia”
“Sasa hiloni tatizo?”
“Ndio. Ningekuja na machela ili nimbebe,yupo kwenye hali mbaya” Dokta Pedro alimwambia polisi yule.
“Kwa hiyo sasa itakuwaje?”
“Inanipasa nirudi hospitalini kuchukuamachela. Ngoja nirudi na kijana wako” Dokta Pedro alimwambia polisi yule.
Bwana Maxwell akashusha pumzi ndefu,hakuamini kile ambacho alikuwa amekisikia, kwake ikaonekana kuwa habari njemana hapo ndipo ambapo aliona kwamba alitakiwa kufanya kitu kimoja cha muhimu sana, kumhonga mkuu yulewa polisi. Mfukoni alikuwa amebakiwa na dola elfu themanini na aliona kwambaendapo angemwachia kiasi fulani cha fedha basi angeweza kumsaidia kuuvuka mpakaule.
Alichokifanya ni kumsogelea polisi yule nakisha kumvuta pembeni, kabla hajaongea kitu chochote kile, akatoa mabunda yadola, polisi yule akayatoa macho yake, noti zile zikaonekana kuanza kumlevya.
“Fedha za nini hizo?” Polisi yule aliuliza.
“Zako”
“Zangu?”
“Ndio”
“Za nini sasa?”
“Yule mwanamke alinipa na mwenzangu, alisemakwamba endapo tutamfikisha Marekani na kujifungua huko, basi hizi fedha nimalipo yetu” Bwana Maxwell alimwambia polisi yule.
“Mmmh! Mbona kiasi kikubwa hicho?”
“Kwa sababu ana kiu ya kujifungulia nchinikwake” Bwana Maxwell alimwambia polisi yule.
“Sasa umesema zangu, kivipi?”
“Kamaukifanya mchakato wa haraka haraka tumvukishe huyu mwanamke, nadhani hizizitakuwa ni zako” Bwana Maxwell alimwambia polisi yule.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Fedha…Fedha…hicho ndicho kilikuwa kitu chamwisho kabisa ambacho Bwana Maxwell alikuwa akikitegemea kuwavukisha mpakani,aliamini katika fedha kwani kupitia fedha nae alikwishawahi kufanya mambo mengimaovu ambayo hayakuwa yakiruhusiwa. Aliifahamu fika nchi ya Mexico, wananchi walikuwa na matatizo makubwa,hawakuwa wakilipwa mishahara katika muda muafaka huku hata mishahara yao ikiwa kidogo.
Kwa polisi yule alikuwa akilipwa kwa wiki,kwa kila wiki alikuwa akilipwa dola mia nane, kiasi ambacho kwa matumizi yakawaida, ukizingatia na upandaji wa bidhaa madukani, mshahara ule haukuwamkubwa sana. Kwanza akaziangalia vizru na kisha kumvuta Bwana Maxwellpembeni zaidi.
“Kiasi gani hicho?” Polisi yule alimuulizaBwana Maxwell.
“Dola elfu hamsini” Bwana Maxwell alimwambiapolisi yule.
“Ila hii si hatari sana, ikitokea akafariki?”
“Hiyo sisi hatujui, yeye alisema anatakaakajifungulie nchini Marekani, haina jinsi” Bwana Maxwell alimwambia polisiyule.
Kiasi kile kilikuwa kikubwa sana, asingeweza kukiachia na wakati mshaharawake haukuwa ukitosheleza. Alijua fika kwamba kamaangekipokea kiasi kile si kwamba chote kingeishia kwake bali angezipiga pasumpaka kwa polisi wengine na wanajeshi ambao walikuwa pale. Hakutaka kujifikiriamara mbili mbili, ile ilionekana kuwa nafasi ya dhahabu ambayo endapoangeichezea basi isingeweza kujirudia mara ya pili.
Kwa haraka sana polisi yule akazichukua na kisha kuanzakuelekea sehemu ya kivukio ambako akamvuta polisi kadhaa na kisha kuongea nao,aliongea nao kwa maneno matamu huku akiwaonyeshea fedha zile, akawazipiga pasukidogo na kuwafuata wanajeshi. Fedha zikaonekana kuwa silaha kubwa mpakani,fedha zikawachanganya polisi wale pamoja na wanajeshi wao na bila kuulizwaswali lolote lile, wakaruhusiwa kuvuka.
“Sasa mtazweza kuvuka geti lile la waleMarekani?” Polisi yule alimuuliza Bwana Maxwell.
“Usijali. Tutavuka tu” Bwana Maxwellalijibu.
Hakutaka kuchelewa, akaliwasha gari. DoktaPedro akatokea mahali hapo huku akiwa na machela yake pamoja na polisi yulemwingine, kilichomshangaza, gari ambalo alikuwepo mwanamke aliyedhania kwambani mjauzito lilikuwa likiondoka.
“Washachelewa” Bwana Maxwell alijisemea.
Kulivuka geti lile lililokuwepo mpakaniupande wa Mexicoilikuwa imewezakana sasa kazi ilibaki kulivuka geti la Marekani. Hilo lilionekana kuwa naugumu lakini kwa Bwana Maxwell wala hakuonekana kulihofia. Wakaagwa kishujaa napolisi wa pale mpaka na wanajeshi wao, fedha zile zilikuwa zimetengenezatabasamu nyusoni mwao.
Walipolifikia geti la kuingilia Marekani kwaupande wa Marekani, Bwana Maxwell akatoa kitambulisho chake cha kazi na kishakuwaonyeshea. Hakukuwa na mtu ambaye alionekana kushikwa na wasiwasi, swalikubwa ambalo lilikuwa likija vichwani mwao ni kwa sababu gani Bwana Maxwellalikuwa amevaa sare za polisi wa Mexico.
“Walitaka kutuua” Bwana Maxwell alimwambiamwanajeshi upande wa Marekani.
“Kivipi?”
“Mexicowana roho mbaya sana”
“Kwa nini walitaka kutuua”
“Wamarekani hatupendwi, wanatuona kama shetani” Bwana Maxwell alimwambia mwanajeshi yule.
“Na wale kule garini ni nani na nani?”Mwanajeshi yule alimuuliza Bwana Maxwell.
“Mke wangu, Jocelyn am
“Amini. Ugumu ulikuwa upande wa walewapumbavu tu” Bwana Maxwell alimwambia Alan.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwa hiyo ndio tunaingia nchini Marekani?”Jocelyn alimuuliza mumewe
“Tumekwishaingia mke wangu. Unajua sana kuigiza, nitakutafutia fomu uende Hollywood” Bwana Maxwell alimwambia mkewekiutani.
Huo ndio ukawa wakati wao wa kuingia ndaniya nchi yaowenyewe. Walipogeuka nyuma, kwa mbali waliliona gari la polisi likiingiampakani pale. Tayari wakajua fika kwamba wale walikuwa ni polisi ambao walikuwawakiwafuatilia, hawakutaka kujali, walichokifanya ni kugongesheana mikono kwafuraha, safari iliendelea zaidi, tayari walikuwa wameingia nchini Marekani.
*****
Polisi walikuwa wamefika mpakani pale.Walijiona kama wamechelewa vile, wakaanza kuangalia huku na kule, hakukuonekanakuwa na dalili zozote zile za Alan kuonekana mahali pale jambo ambaloliliwafanya kumfuata polisi ambaye alikuwa mpakani pale akiongea na dokta Pedroambaye muda mwingi alikuwa akilalamika.
“Kuna mtu tunamtafuta” Polisi mmoja alimuuliza.
“Nani?”
“Huyu hapa”
“Hapana, Sijamuona mahali hapa”
“Kweli?”
“Ndio”
“Hajavuka hapa?”
“Atavukaje na wakati mimi mwenyewenamtafuta?”
“Sawa. Kuna polisi wamevuka mpakani hapa?”
“Ndio”
“Walikuwa wangapi?”
“Walikuwa polisi wawili pamoja na mwanamkemjauzito” Mkuu wa polisi yule alijibu.
“Mwanamke mjauzito?”
“Ndio”
“Yupo vipi?”
“Mweupe, kwa mbali ana asili ya hapa Mexico”
“Ndio wenyewe” Polisi mmoja alijibu, alikuwamiongoni mwa wale waliovuliwa sare zao.
“Wakina nani tena?”
“Umemruhusu huyu mtu”
“Hapana bwana. Mimi sio chizi”
“Unasema walikuwa polisi wawili?”
“Ndio”
“Huyu mwingine ulimuona sura?”
“Mmmh! Sikumbuki. Ila sikumuona surakwani alikuwa akimhudumia mwanamke mjauzito ambaye walikuwa wamekuja nae hapa”Polisi yule alijibu.
“Umefanya makosa. Mmmoja wapo ndiyemwenyewe. Walikuwa ndani ya gari ndogo?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ndio. Tena ile kuleeee upande wa Marekani”
“Daah! Umefanya makosa. Huyu mtuhumiwa ndiyehuyo polisi mmoja” Polisi yule alimwambia mkuu wa polisi na kisha kuanzakuelezea kile kilichokuwa kimetokea.
Mkuu wa polisi akashika kichwa, ni kwelialikuwa amefanya kosa moja kubwa sanala kumruhusu mtuhumiwa kuvuka mpakani kirahisi namna ile. Wakabakiwakiliangalia gari lile ambalo lilikuwa limeanza kuondoka upande wa Marekani.Roho zao zilikuwa zimewauma, lakini hawakuwa na jinsi, Alan, Bwana Maxwell naJocelyn walikuwa wameingia nchini Marekani.
****
Ilikuwa ni taarifa mbaya kwa Antonio,hakuamini kile alichokuwa ameambiwa kwamba Alan alikuwa amefanikiwa kuvukampakani pale. Antonio alijisikia uchungu moyoni, hasira zikamjaa na kishakuanza kutokwa na machozi. Alikuwa akihitaji kumuua Alan lakini mpaka kufikiahatua hiyo tayari alijiona kushindwa kutekeleza kile alichokuwa akitakakutekeleza.
“Nitamuua. Nitamuua kwa gharama zozote zile.Yaani hapa ndipo ugomvi wetu utakapoanzia. Nitahakikisha namtafuta usiku namchana mpaka nimpate na kumuua” Antonio alijisemea kwa hasira huku akionekanakumaanisha kile alichokuwa akikiongea.
Vaada ya siku moja, mazishi ya baba yake,mzee Sanchez yakafanyika. Watu walihuzunika sana, maswali kibao yakaanza kumiminikavichwani mwa waombolezaji juu ya sababu iliyomfanya mzee huyo kujipiga risasi,hakukuwa na watu wengi ambao walikuwa wakiufahamu ukweli kwamba mzee huyoalikuwa ameuawa na Alan ila Antonio aliudanganya umma kwa sababu alitaka kumuuaAlan kwa mikono yake na pia hakutaka watu wajue kwamba baba yake alikuwaamemuua Bwana Kurt.
****
Nchini Marekani kila kitu kilionekana kuwahuzuni, kila wakati Alan alikuwa akiongea na mamayake kwenye simu huku akilia kama mtoto, alikuwa akimuelezea mama yake kla kitukilichokuwa kimetokea na katika kipindi hicho ni mwili wa baba yake tu ndioambao alikuwa amefanikiwa kurudi nao nchini Marekani.
Hiyoilikuwa taarifa mbaya na yenye kushtua sana kwaBi Bertha, hakuamini kama kweli mume wake mpendwa, Bwana Kurt alikuwa ameuawanchini Mexico.Juu ya kifo chake, familia haikutaka FBI ichunguze sana na ndio maana hata mwili wake ukazikwamahali ambapo hakukuwa na mtu aliyekuwa akipafahamu zaidi ya familia pamoja nandugu wa familia hiyo.
Huo ukaonekana kuwa mwisho wa kila kitu,fedha ambazo Bwana Kurt alikuwa ameziangaikia katika maisha yake yote ndiofedha hizo ambazo zilimfanya kuuawa na mtu ambaye alimini kwamba ni adui nambamoja wa familia yake. Fedha zikaonekana kuleta chuki, zilileta chuki kwa wazazina chuki hizo kuhamia kwa watoto. Antonio alikuwa amejiahidi kumtafuta Alanamteketeze na hata kama itashindikikana basiateketeze hata kizazi chake, hakutaka kumuona Alan akiendelea kuvuta pumzindani ya dunia hii.
“Pumzika kwa amani baba” Alan alisema kilaalipokuwa akiziangalia picha za baba yake zilizokuwa ukutani nyumbani.
Siku zikakatika, majonzi ambayo walikuwanayo yakapungua. Bwana Maxwell akaonekana kuwa msaada mkubwa sanakwake, yeye pamoja na mama yake, Bi Bertha wakakaa chini na kukubaliana BwanaMaxwell alipewe kiasi cha dola milioni tano kamashukrani ya kila kitu alichokifanya.
Fedha hizo ambazo ni zaidi ya bilioni kumikwa fedha za kitanzania, Bwana MAzxwell akaamua kuzifanyia biashara mbalimbali,biashara ambazo aliamini kwamba zingeweza kumpa fedha nyingi na kumfanya kuwatajiri mkubwa nchini Marekani. Hakutaka tena kunywa pombe, hakutaka tenakucheza kamari, akaamua kuishi na mke wake pamoja na watoto wake ambaowalifuatwa nchini Mexico, kidogo Bwana Maxwell alionekana kuwa milionea na kamaangeendelea kufanya biashara zaidi na zaidi basi nae angekuwa bilionea.
“Nimetuma kila kitu, njooni Marekani, natakakufunga ndoa na wewe na hatimae tuwe mke na mume” Alan alisikika akiongeasimuni, ilikuwa imepita miezi mitatu toka siku ya mwisho aonane na Albertina.Katika kipindi hicho alikuwa amewatumia kadi ya mualiko, alikuwa akiihitajifamilia nzima ya Bwana Ruttaba ifike nchini Marekani na hatimae kufunga ndoapamoja na Albertina.
Watu wengi wakaalikwa tayari kwa kuhudhuriaharusi hiyo, Alan hakutaka kuwapa taarifa ni mwanamke yupi ambaye alikuwaakienda kumuoa, alitaka hiyo iwe siri mpaka pale ambapo Albertina angeonekana kanisaniakiwa ndani ya shela huku akionekana kung’’aa na kuvutia. Hakutaka kuwaambiawatu kuhusu Albertina, alitaka kuwashtukiza watu.
Baada ya wiki moja, Bwana Ruttaba na familiayake wakafika nchini Marekani. Wakapangishiwa vyumba ndani ya hoteli ya Rooseveltambayo ilikuwa nje kidogo ya jiji la Washington.Kwa sababu siku ya harusi ilikuwa imekwishapangwa, watu wakaanza kuisubiriaharusi hiyo ya kifahari ambayo ilitangazwa sanakatika vyombo vya habari japokuwa hawakutakiwa kufika watu wengi kwani ilikuwani ndoa ya kifahari sanahivyo walitakiwa kufika wageni waalikwa tu. Cha kushtukiza, Alan alikuwa amempakadi ya mwaliko mpaka Stacie, alimtaka audhurie harusi hiyo na Stacie akatoaahadi ya kuwepo katika bustani nzuri nyumbani kwa kina Alan kwa ajili yakuhudhuria harusi hiyo.
.....................................
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku ya harusi ikawa imewadia, watu mbalimbali maarufu pamoja na watu ambao walikuwa na fedha nchini Marekani walikuwa wamekusanyika katika jumba kubwa la kifahari, jumba lililokuwa katika mtaa wa kitajiri Hampheert ndani ya jiji la Dar es Salaam. Nyumba hiyo ilikuwa na eneo ukubwa wa hekari kumi na mbili, kulikuwa na kila kitu ambcho jumba kubwa la kifahari lilitakiwa kuwa navyo.
Idadi ya watu haikuwa kubwa sana, kulikuwa na watu kama hamsini tu ambao kwa muonekano tu walikuwa ni watu wenye fedha zao au watu ambao nyuso zao hazikuwa zikikatika katika kurasa za mbele za magazeti mbalimbali kama New York Times, Daily Mail na mengine mangi. Viti vilikuwepo mahali hapo lakini hakukuwa na mtu ambaye alitaka kukaa, wengi walikuwa wamesimama huku wahudumu wakipitisha vinywaji mahali hapo, aliyetaka kunywa, alichukua na kunya na asiyetaka aliachana navyo.
Brian pamoja na Bwana Ruttaba walikuwa ndani ya suti nzuri nyeusi, walionekana kupendeza kupita kawaida. Muda wote walikuwa wametawaliwa na nyuso zilizokuwa na tabasamu pana, nyuso ambazo zilionekana kufurahia kila kitu kilichokuwa kikiendelea mahali hapo. Ukiachana na hao, pia kulikuwa na Bi Janeth, mwanamke wa kiafrika, mwanamke ambaye alikuwa amevaa vazi zuri lililoshonwa na kitenge kutoka nchini Kongo.
Kati ya wahudhuriaji wengine ambao walikuwa ndani ya sherehe hiyo ya harusi alikuwepo Bwana Maxwell pamoja na mkewe, Jocelyn. Wote wawili walionekana kupendeza kupita kawaida na muda mwingi walikuwa wakionekana kuwa watu wenye furaha kupita kawaida. Vinywaji vyao vilikuwa mikononi huku wakipiga stori pamoja na watu wengine ambao walikuwepo mahali hapo.
Ukiachana na hao, pia kulikuwa na waigizaji wa filamu mbalimbali, wanamuziki, wacheza tenisi na pia kulikuwa na mtu ambaye alionekana kuhitajika na Alan mahali hapo, huyu alikuwa Stacie. Stacie alipendeza sana, mavazi yake yalikuwa ni ya kisasa yaliyoonekana kuwa ya gharama kubwa, kila wakati uso wake ulikuwa kwenye tabasamu pana, alijua fika kwamba mtu ambaye alikuwa akielekea kuoa kwa wakati huo alikuwa mpenzi wake ambaye alimpenda sana lakini katika kipindi hicho hakutaka kukumbuka kitu chochote kile.
Kitendo cha Stacie kumuona Brian mahali hapo akamfuata na kisha kumkumbatia kwa furaha. Alifahamiana na Brian toka katika kipindi ambacho alikuwa chuoni ambapo alipenda sana kuonana na Alan. Brian alikuwa rafiki mkubwa wa Alan, alifahamiana nae sana, na ilipita miaka kadhaa hakuwa ameonana nae, siku hiyo, wakawa wameonana, ilionekana kuwa furaha kwa msichana Stacie.
“Mmmh! Umebadilika Brian” Stacie alimwambia Brian huku akionekana kuwa na furaha kupita kawaida.
“Nimekuwa vipi?”
“Umekuwa na mwili mkubwa sana, bado unakwenda gym?” Stacie alimuuliza Biran ambaye akaanza kutoa kicheko kidogo hata kabla ya kulijibu swali lile.
“Mara chache sana”
“Umekuwa mkubwa sana na umependeza pia” Stacie alimwambia Brian.
“Hata wewe umependeza pia”
“Asante sana. Hivi unamjua msichana anayeolewa na Alan?” Stacie alimuuliza Brian.
“Ndio. Kwa nini unauliza hivyo?”
“Alimpata alivyokuja Tanzania, bila shaka utakuwa ukimfahamu tu”
“Yeah! Ninampata, anaitwa Albertina” Brian alimjibu Stacie.
“Ni msichana mzuri?”
“Yaap! Ni msichana mzuri sana”
“Sawa. Mambo mengine ni vipi lakini?”
“Kama kawaida. Mimi nipo safi sana” Brian alimwambia Stacie.
Wawili hao wakanatana, muda mwingi walikuwa pamoja, walikuwa wakitumia muda mwingi kuanza kutembea huku na kule na vinywaji vikiwa mikononi mwao. Walionekana kuwa marafiki sana huku kila mmoja akimchukulia mwenzake kuwa kawaida sana. Waliongea mambo mengi, Stacie akamwambia Brian kile ambacho kilikuwa kimetokea mara baada ya Alan kurudi kutoka nchini Tanzania.
“Iliniuma sana” Stacie alimwambia Brian.
“Pole sana. Jipange upya bado una nafasi kubwa maishani mwako” Brian alimwambia Stacie.
Ukaribu wao siku hiyo haukuishia hapo, waliendelea kuwa pamoja zaidi na zaidi huku wakiendelea kutembea huku na kule. Mpaka muda ambao maharusi wanaingia mahali hapo, walikuwa wamekwishaongea vya kutosha.
Alan alionekana kupendeza mno, alikuwa amevalia suti yake nyeusi pamoja na shati la rangi ya dhahabu huku hata tai yake ikiwa na rangi hiyo. Kwa kumwangalia tu, Alan alionekana kuvutia kupita kawaida. Ukiachana na Alan, Albertina alionekana kupendeza sana, alikuwa amevalia shela jeupe ambalo lilikuwa na urefu wa mita kama kumi na tano kwa nyuma, uso wake ulikuwa umependezeshwa na virembo ambavyo vilikuwa viking’aa kila wakati.
Mara baada ya kusimama mbele ya umati ule, mchungaji akafika na kisha bila kupoteza muda akaifungisha ndoa hiyo. Hiyo ikaonekana kuwa furaha kwa kila mtu mahali hapo, harusi ambayo kila mtu alikuwa akiitamani mahali hapo tayari ikafanyika, Albertina akawa mke wa Alan huku Alan akiwa mume wa Albertina. Shughuli za upigaji picha zikaanza kufanyika mahali hapo, kila mtu ambaye alikuwa akitaka kupiga picha na maharusi akaruhusiwa kufanya hivyo.
“Nataka kupiga picha na wewe” Stacie alimwambia Brian.
“Usijali. Tukapigie wapi?” Brian alimuuliza Stacie.
“Popote pale” Stacie alimjibu Brian.
Wawili hao wakapiga picha kama ukumbusho mahali hapo. Alan alionekana kufurahia sana, ujio wa Stacie mahali pale ukamfanya kuwa na amani, furaha ikaongezeka kwani japokuwa alikuwa amemuacha msichana huyo na kumuumiza moyoni mwake, kwa wakati huo alionekana kusahau kila kitu ambcho kilikuwa kimetokea.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nakuona upo karibu sana na Stacie” Alan alimwambia Brian.
“Yeah! Yaani mpaka nashangaa”
“Kama vipi mchukue, kila ninapomwangali, ule mtazamo ambao alikuwa akiutumia kuniangalia mimi, naona anautumia kukuangalia wewe” Alan alimwambia Brian.
“Hahaha! Mtazamo upi?”
“Mtazamo wa kimapenzi” Alan alimwambia Brian, wote wakaanza kucheka na kisha kugongesheana mikono.
“Acha utani”
“Huo ndio ukweli Brian. Nafikiri kwa sasa amepata mwanaume wake halisi, mwanaume aliyepangwa kuwa nae katika maisha yake” Alan alimwambia Brian.
“Mwanaume yupi?”
“Wewe hapo”
“Acha utani Alan. Bado namheshimu sana Stacie”
“Najua Brian”
“Sidhani kama unachokiongea kina ukweli wowote ule” Brian alimwambia Alan.
“Nafikiri wewe ni mwanaume sahihi katika maisha yake” Alan alimwambia Brian.
Maneno aliyokuwa akiongea Alan yalionekana kumuingia sana Brian moyoni mwake lakini hakutaka kuyatilia maanani. Kwake, alimuona Stacie kuwa rafiki wa kawaida sana na kile alichokuwa amekisema Alan wala hakuweza kukigundua kabisa machoni mwake, alimchukulia Stacie kuwa msichana wa kawaida, kama rafiki tu.
Kwa upande wa Stacie, kitendo cha kumuona Brian mahali hapo kilionekana kumshtua sana, machoni mwake, Brian alikuwa amebadilika sana, alikuwa na mwili mkubwa na pia alikuwa na mvuto sana. Kila alipokuwa akimwangalia Brian, mapigo yake ya moyo yalikuwa yakimdunda, aliyasikia mapenzi yakianza kuchomoa moyoni mwake.
Ni kweli kwamba alikuwa amejaribu kuwafuata wanaume mbalimbali na kuzielezea hisia zake kwao lakini kwa Brian alijiona kuwa tofauti sana. Kila alipokuwa akimwangalia Brian na ndivyo ambavyo maneno ya Alan yalipokuwa yakijirudia moyoni mwake kwa kumwambia kwamba ilimpasa kusubiri na mwanaume wake wa maisha yake angeweza kuja katika muda ambao hakuwa akiutarajia.
Stacie alikuwa na uhakika kwamba Brian ndiye alikuwa mwanaume huyo ambaye alizungumziwa na Alan, akajiona kutokujiweza, mapenzi ambayo yalikuwa yakichipukia moyoni mwake yalikuwa yakiendelea kuchipuka kadri muda ulivyozidi kwenda mbele mpaka kufikia kipindi ambacho akaamua kumfuata na kuanza kuongea nae.
Aliuleta uchangamfu lakini bado alikuwa muoga moyoni mwake. Maswali mengi yalikuwa yakimiminika moyoni mwake kama alitakiwa kumwambia Brian ukweli wa moyo wake kwa jinsi alivyokuwa akijisikia au alitakiwa kukaa kimya. Swali hilo likakosa jibu, akajikuta akishindwa kumwambia na mwisho wa siku kupiga nae stori kama marafiki.
Moyo wake ulikuwa umeingia katika mapenzi kwa haraka mno kitu ambacho hakuwa akikitarajia hata siku moja. Hakuwa kumpenda mwanaume kwa haraka kiasi hicho, hiyo ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kumtokea katika maisha yake.
“Mbona hali imekuwa hivi? Mbona haraka mno?” Stacie alikuwa akijiuliza lakini akakosa jibu kabisa.
Hali hiyo iliendelea kutokuwa ya kawaida moyoni mwake, alijisikia kuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanaume huyo, alijisikia kupenda sana kuliko kawaida. Maneno ya Alan yaliendelea kumpa nafasi ya kuona kwamba Brian ndiye alikuwa mwanaume wake sahihi ambaye alikuwa ametoka ubavuni mwake na hivyo alitakiwa kukaa pamoja nae.
Harusi ilipomalizika, kukafanyia sherehe kubwa, katika ukumbi wa hoteli ya Transiperia iliyokuwa hapo hapo Washington. Huko kote Stacie alikuwa pamoja na Brian, walikuwa na ukaribu mkubwa mno, ukaribu ambao ulimfanya Brian kuona kwamba maneno aliyokuwa ameongea Alan yalikuwa ni kweli kabisa, kwa hali zote, kwa kila hatua, Stacie alionekana kuwa na dalili zote za kuwa katika mapenzi yake.
Brian hakutaka kuzubaa, aliitamani sana nafasi hiyo toka zamani, alitamani sana kuwa na mahusiano na msichana yeyote wa kizungu. Alichokifanya kwanza kabla ya yote ni kushikana mikono ya Stacie. Hilo wala halikuwa tatizo kabisa, alipoona kwamba hilo limewezekana akaja hatua nyingine, akaanza kumbusu shavuni.
Kila kitu ambcho alikuwa akiendelea kukifanya alitaka kuona kama Alan alikuwa ameongea maneno ya kweli au alikuwa amekisia na wala haukuwa ukweli wenyewe. Kitendo cha kumpiga busu la shavuni likaruhusu tendo jingine kabisa, wakaanza kubadilishana mate.
Hapo ndipo Brian alipoona kwamba kila kitu kilikuwa kweli, Stacie alikuwa ameangukia katika mapenzi yake, nae bila shida yoyote ile akauruhusu moyo wake, ukamuingiza Stacie. Wawili hao wakaanza uhusiano wa kimapenzi ndani ya sherehe ya harusi hiy
“Labda inaweza kuanza hata sasa hivi” Alan alimwambia Albertina.
Muda mwingi Alan alionekana kutabasamu, japokuwa alikuwa akiendesha gari lakini wakati mwingine alikuwa akiligusa tumbo la Albertina na kisha kuanza kulibinyabinya. Kwake, Alan alithamini sana mtoto, alikuwa akitamani sana na yeye kuitwa baba, kuwa na mtoto ilionekana kuwa kama ndoto ambayo iliishi moyoni mwake kwa kipindi kirefu sana, hapo ndipo alipogundua sababu zilizomfanya wazazi wake kumpenda namna ile.
Baada ya dakika kadhaa wakaanza kuingia ndani ya hospitali ya Wahshington Medical Center ambapo Alan akapaki gari na kisha kuteremka na kuelekea ndani ya jengo la hospitali ile. Watu walikuwa wengi ndani ya jengo la hospitali hiyo, muda wote madaktari na manesi walikuwa bize huku wakiendelea na kazi zao. Moja kwa moja Alan akaelekea sehemu ya mapokezi na kisha kuomba kuonana na dokta Steve Goby, dokta wa magonjwa ya wakinamama hospitalini hapo.
“Kwa dalili alizozielezea, nahisi ana ujauzito” Dokta Goby alimwambia Alan.
“Unasema kweli dokta?”
“Yeah! Ngoja nichukue vipimo” Dokta Goby alimwambia Alan.
Akachukua vipimo kutoka kwa Albertina na kisha kuelekea maabara. Alipofika huko, akaanza kuupima mkojo wa Albertina na baada ya dakika kadhaa akarudi ndani ya ofisi yake na kumwambia Alan kwamba hisia zake zilikuwa sahihi, Albertina alikuwa mjauzito.
“Siamini”Alan alimwambia Albertina huku akimkumbatia kwa furaha.
Miezi ikakatika huku Albertina akiendelea kuulea ujauzito wake. Kila wakati alikuwa mtu wa kula vizuri huku Alan akitumia muda mwingi kuwa na mkewe mpendwa. Kwake, ujauzito ule ulionekana kuwa kila kitu katika maisha yake, alipenda sana kumuona mtoto wake akizaliwa na kisha kuanza kumlea huku akiahidi kuwa nae karibu hata zaidi ya wazazi wake walivyokuwa karibu nae.
Albertina akawaeleza wazazi wake kuhusiana na ujauzito ule, wazazi wake wakaonekana kuwa na furaha, kitendo cha Albertina kuwa mjauzito kiliwafanya kufurahia sana. Wote wakapanga safari ya kuelekea Marekani, walipofika wakamuona na kisha kurudi nchini Tanzania.
“Dokta kasemaje?” Alan alimuuliza Albertina.
“Amesema kwamba ni mapacha” Albertina alimwambia mume wake.
“Unasemaje?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Amesema ni mapacha, mmoja wa kiume na mmoja wa kike” Albertina alimwambia mume wake.
“Nimefurahi sana kusikia hivyo, wa kiume ataitwa Hans, wa kike ungependa aitwe nani mpenzi?” Alan alimuuliza mke wake simuni huku akisikika kuwa na furaha.
“Catherine”
“Hilo jina zuri pia. Nakupenda sana mke wangu” Alan alimwambia Albertina.
“Nakupenda pia”
Miezi ikaonekana kwenda taratibu sana, Alan alikuwa akitamani sana kuwaona watoto wake wakizaliwa na kuwabeba mikononi mwake, alikuwa na kiu kubwa mno ya kuiona mbegu yake pamoja na kazi yake kubwa ambayo alikuwa ameifanya katika visiwa vya Hawaii. Kila wakati alijitahidi kuwa karibu na mke wake, hakutaka afanye kazi zozote zile, kama ni fedha zilikuwa zikiingia kila siku na hivyo Albertina alitakiwa kutulia nyumbani huku wafanyakazi wakifanya kila aina ya kazi.
Baada ya muda wa kujifungua kufikia, Albertina akaanza kujisikia uchungu, tayari alijiona kuwa kwenye hatua za kutaka kujifungua. Kwa sababu dereva wake alikuwa nyumbani hapo tayari kwa hali kama hiyo, akamchukua na kisha kumpeleka katika hospitali ya Washington Medical Center ambapo huko akachukuliwa na kupelekwa ndani ya chumba kilichokuwa kimeandikwa Labour kwa ajili ya kujifungua.
Muda wote Albertina alikuwa akiugulia kwa maumivu makali, alikuwa akitaka kujifungua kwani tayari alikwishalisikia tumbo likiwa kwenye maumivu makali huku chini ya kitofu kukivuta kupita kawaida. Madaktari wakamuweka tayari, wakaanza kuiangalia hali yake katika kitanda cha kujifungulia, alionekana kuhitaji kama dakika thelathini na ndipo ambapo angeanza kujifungua. Kama kawaida ya madaktari wa hospitali za Marekani walivyo, wakashikana mikono na kisha kuanza kusali hata kabla ya tukio la kuwatoa watoto kuanza baada ya nusu saa.
****
Mara baada ya kupigiwa simu kwamba mke wake alikuwa amejisikia uchungu na hivyo alikuwa amepelekwa hospitalini, Alan hakutaka kubaki ofisini kwake, moja kwa moja akatoka nje na kisha kulifuata gari lake, akaingia na kisha dereva wake kuliwasha na kuanza kuanza kuondoka mahali hapo. Usoni alionekana kuwa na furaha kupita kawaida, hakuamini kama siku hiyo ilikuwa ni siku ya kuwaona watoto wake ambao alikuwa amewasubiri kwa muda wa miezi tisa.
“Unafikiri wanafanana na nani?” Alan alimuuliza dereva wake.
“Anafanana na wote. Wa kike atafanana na mama yake na wa kiume atafanana na wewe” Dereva alimwambia Alan ambaye alionekana kuwa na furaha sana.
“Ni muda mrefu sana nimewasubiri kipindi kama hiki, nadhani leo ndio siku ambayo nitakuwa na furaha kuliko siku zote” Alan alimwambia dereva wake.
Hawakuchukua muda mrefu wakaingia ndani ya eneo la hospitali hiyo. Kwa haraka sana Alan akashuka kutoka garini na kisha kuanza kuelekea ndani ya jengo la hospitali hiyo. Mwendo wake ulikuwa ni wa haraka haraka sana , alijiona kama alikuwa akichelewa, alikuwa na kiu ya kutaka kuwaona watoto wake.
“Nadhani mke wangu yupo humu” Alan alimuuliza nesi mmoja ambeya alikuwa akipita, nesi yule alionekana kumfahamu sana.
“Ndio. Madakatri wanataka kuanza kazi yao, nakuomba usubiri pale” Nesi yule alimwambia Alan na kisha kumuonyeshea kviti ambavyo alitakiwa kusubiri mahali hapo.
Alan akawa na presha kubwa, katika kipindi chote alikuwa akiiangalia saa yake, alitamani kuusikia mlango ule ukifunguliwa na sauti za watoto kusikika ndani ya chumba kile. Alan aliona hiyo kutokutosha, alichokifanya ni kumpigia simu mama yake na kumueleza kwamba Albertina alikuwa ndani ya chumba cha kujifungulia na hivyo muda wowote angeweza kusikia sauti za wajukuu zake. Alan hakuishia hapo, aliendelea kuwapigia simu marafiki zake wengine na kisha kuwaambia kuhusu jambo hilo, kwake lilionekana kuwa la furaha mno.
Dakika ziliendelea kukatika, nusu saa ikapita na dakika arobaini na tano kupita na hatimae saa moja kukamilika. Mlango wa chumba kile haukufunguliwa, hakukuwa na dokta yeyote ambaye alitoka ndani ya chumba kile. Alan akaonekana kuwa na wasiwasi mwingi, hakuonekana kuelewa ni kitu gani kilikuwa kikiendelea ndani ya chumba kile. Alichokifanya ni kumsimamisha dokta mmoja ambaye alikuwa akipita.
“Samahani. Hivi huwa inachukua muda gani mwanamke kujifungua?” Alan alimuuliza dokta yule aliyemsimamisha.
“Dakika chache, wakati mwingine si zaidi ya dakika ishirini” Dokta yule alimjibu.
“Hili ni saa moja sasa, mke wangu hajatolewa ndani ya chumba hicho” Alan alimwambia dokta yule.
“Saa moja?”
“Ndio”
“Sidhani kama ni kweli”
“Ndio hivyo, mke wangu hajatolewa ndani ya chumba hicho” Alan alimwambia dokta.
Dokta yule hakutaka kubaki hapo, alichokifanya ni kuufuata mlango ule na kisha kutaka kuufungua, mlango ulikuwa umefungwa. Alichokifanya ni kuelekea ofisini kwake, aliporudi alikuwa na kadi ambayo akaipitisha katika kimashine kidogo kilichokuwa karibu na kitasa na kisha mlango kujifungua.
Alan hakutaka kubaki, tayari alionekana kuwa na wasiwasi, alichokifanya na yeye ni kuanza kumfuata dokta kwa nyuma. Hakukuwa na mtu aliyeamini mara baada ya kuingia ndani ya chumba kile, miili ya madaktari ilikuwa chini huku ikiwa imetobolewa na risasi kadhaa, walipoangalia katika kitanda cha kujifungulia, Albertina hakuwepo. Alan akahisi kufakufa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Huzuni na uchungu havikuisha moyoni mwa Antonio, kila wakati alikuwa akimfikiria baba yake ambaye alikuwa ameuawa wiki moja iliyopita. Hasira zake zilikuwa juu ya Alan, hakumpenda hata kidogo Alan, mapenzi yote ambayo alikuwa nayo juu yake katika kipindi cha nyuma yalikuwa yamepotea na chuki kubwa kuujaza moyo wake.
Kila siku akawa mtu wa mawazo tu, hakula vizuri, hakuongea vizuri na watu wengine zaidi ya kumfikiria Alan ambaye alikuwa amemharibia furaha yote ambayo alikuwa nayo moyoni mwake. Kitu ambacho alikuwa akikitaka kwa wakati huo ni kumuua Alan tu, hakutaka kumuona Alan akiendelea kuishi, alitaka kummaliza kama alivyommaliza baba yake.
Japokuwa alikuwa ameamua kwa moyo wake mmoja kwamba ilikuwa ni lazima kumuua Alan lakini kuna kitu kingine kikamjia moyoni, angempata vipi Alan ili aweze kumuua? Alan alikuwa mtu tajiri, kitendo cha kuwa tajiri tayari alionekana kuwa na ulinzi wa kutosha hivyo asingeweza kumpata hata mara moja.
Alichokifanya Antonio ni kuwaita washauri wake, kwanza akawaelezea kila kilichotokea na kisha kuwaambia lengo lake lilikuwa ni nini kwa wakati huo. Alitaka kushauriwa ili apate kujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya ili iwe njia rahisi ya kumpata Alan na kisha kumuua.
“Tuma vijana waelekee Marekani” Mshauri wa kwanza alimwambia Antonio.
“Wakishakwenda huko?”
“Wamtafute na kumuua”
“Unafikiri itakuwa rahisi?”
“Sidhani lakini nadhani itakuwa hivyo”
“Haiwezekani. Au kama una kingine” Antonio alimwambia mshauri yule.
Mshauri wa pili alikuwa amebaki kimya, alionekana kujifikiria kwa muda fulani, kwa muonekano ambao alikuwa akiuonyesha mahali hapo alionekana kuja na wazo zuri ambalo lingeonekana kuungwa mkono na kila mtu ndani ya chumba hicho.
“Na wewe unashauri nini?” Antonio alimuuliza mshauri wa pili.
“Watume vijana wako nchini Marekani” Mshauri wa pili alimshauri Antonio.
“Na wewe pia unasema niwatume vijana Marekani?”
“Ndio. Baada ya hapo waambie kwamba wanachotakiwa ni kumtafuta huyo mtu wako, wakishindwa basi waue hata watoto wake” Mshauri yule alimwambia Antonio.
“Hana familia” Antonio alimwambia.
“Hata mke?”
“Hana”
“Kwa hiyo hatooa?”
“Nadhani ataoa ila sijajua ni lini”
“Ninachoshauri ni kwamba uwatume vijana wako, ikitokea siku akioa na kupata watoto, wewe ua watoto, nadhani hayo yatakuwa malipo mazuri” Mshauri yule alimwambia Antonio.
“Sasa nitajuaje katika kipindi cha kuoa kama ameoa?” Antonio aliuliza.
“Tuma vijana ambao kazi yao itakuwa ni kuufuatilia mwenendo mzima wa maisha yake” Mshauri yule alimwambia Antonio.
Suala hilo likaonekana kukubalika moyoni mwake, alichokifanya siku iliyofuatia ni kuwaita vijana wawili, Perez na Javier na kisha kuwaambia kila kitu ambacho kilitakiwa kufanyika nchini Marekani. Hilo kwa vijana wale wala halikuonekana kama ni tatizo, baada ya wiki mbili wakaanza safari ya kuelekea nchini Marekani huku kila mmoja akiwa na kumbukumbu kwamba walitakiwa kuimaliza familia ya Alan endapo itashindikana kumuua yeye mwenyewe.
“Ni lazima nimuue Alan mama” Antonio alimwambia mama yake.
“Kuwa makini mwanangu, Alan anaonekana ni mtu hatari sana, sitaki kukupoteza” Bi Shakira alimwambia Antonio.
“Usiwe na wasiwasi mama, nitafanya kila kitu bila ya yeye kufahamu juu ya mchakato huo” Antonio alimuondoa wasiwasi mama yake.
Perez na Javier wakafika nchini Marekani ndani ya jiji la Washington, kitu cha kwanza ambacho walikifanya ni kuelekea hotelini ambapo huko wakachukua chumba kimoja tayari kwa kuanza kazi hiyo ambayo walikuwa wamepewa na bosi wao, Antonio. Hawakujua ni kwa namna gani kazi ile ingeendelea mpaka kumalizika lakini waliamini kwamba kwa msaada wa magazeti na majarida mbalimbali ya nchini Marekani wangeweza kufahamu kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea katika maisha ya Alan.
Siku zikakatika, wiki zikasonga mbele na mwezi wa kwanza kuingia. Bado waliendelea kuwa wavumilivu mpaka pale ambapo mwezi wa tatu ulipoingia na kuanza kusikia tetesi kupitia katika magazeti mbalimbali kwamba Alan alikuwa akitaka kuoa. Taarifa hiyo ikaonekana kuwa nzuri kwao, wakaona kwamba muda huo ndio ambao wangeweza kukamilisha kile walichokuwa wakikitaka.
Kitu cha kwanza kabisa wakahitaji kumfahamu msichana ambaye alikuwa akienda kumuoa. Msichana hakutajwa na wala picha yake haikuonekana, ilionekana kuwa siri kubwa, msichana huyo hakutakiwa kujulikana kwanza mpaka pale ambapo wangekuwa kanisani, sehemu ambayo bila kificho chochote kile msichana huyo angeweza kujulikana.
“Kwa hiyo tumuue msichana mwenyewe?” Javier alimuuliza Antonio simuni.
“Mmemfahamu?”
“Hapana ila tutamfahamu hivi karibuni” Javier alimwambia Antonio.
“Basi hakuna shaka. Muueni” Antonio aliwaambia vijana hao ambao katika kipindi chote hicho walikuwa wakiendelea kukaa hotelini.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
SIku ya harusi ikawadia na baada ya siku mbili wakaweza kumuona msichana huyo kwenye magazeti na majarida mbalimbali. Hiyo kwao ikaonekana kuwa kama furaha kwa kuamini kwamba wangeweza kukamilisha kile ambacho walikuwa wamekipanga.
Mishemishe zao zikaanza upya kwa kuanza kumsaka Albertina lakini mpaka miezi mitano inawadia hawakubahatika kumuona mwanamke huyo. Hali hiyo tayari ikaonekana kuwa ngumu kwao kukamilisha kile ambacho walikuwa wamekipanga kitu ambacho wakaamua kumpigia simu bosi wao, Antonio na kuwaambia hali ambayo ilikuwa ikiendelea kule Marekani.
“Vumilieni, nitataka muendelee kukaa huko mpaka niwaambie kurudi huku” Antonio aliwaambia.
“Hakuna tatizo, ila naona fedha ulizotuachia zinaanza kutuishi” Javier alimwambia Antonio.
“Msijali. Nitatuma dola milioni mbili kwa ajili ya matumizi yenu, hakikisheni mnafanikiwa” Antonio aliwaambia vijana wake.
“Hakuna tatizo”
Perez na Javier waliendelea kukaa nchini Marekani huku wakifuatilia kwa karibu kila kilichokuwa kikiendelea kwa Antonio kupitia magazeti na majarida mbalimbali na hata wakati mwingine kupitia internet. Kazi haikuwa kubwa lakini miezi minne baadae ndipo hapo waliposikia kwamba mke wa Alan, Albertina alikuwa mjauzito na ndani ya siku chache angeweza kujifungua na tajiri huyo kuwa na mtoto.
Hiyo ilionekana kuwa taarifa ya mshtuko sana, hawakuamini kama kweli taarifa hiyo ilikuwa imetolewa katika jarida la Forbes au walikuwa wakiota. Alan alionekana katika picha ya mbele kabisa kwenye gazeti hilo huku akiwa amesimama na mke wake, Albertina, nyuso zao zilijawa na tabasamu, Albertina alionekana kuwa mjauzito.
Hawakuishia hapo, walichokifanya ni kufuatilia kwa ukaribu kwamba ni hospitali gani ambayo Alan angeweza kumpeleka mke wake kwa ajili ya kujifungua. Walichokifikiria ni lazima ingekuwa Washington Medical Center kwa sababu matajiri wengi, watu maarufu walikuwa wakiitumia hospitali hiyo kila wake zao au wao walipokuwa wajawazito.
Wakanunua makoti meupe kama yale waliyokuwa wakivaa madaktari pamoja na vifaa vyote ambavyo madaktari hupenda kuvishika kama mashine za kusikilizia mapigo ya moyo pamoja na vifaa vingine vidogo vidogo. Walipoona kwamba walikuwa tayari kwa kila kitu, wakaenda sehemu ya kukodisha magari ambapo huko wakahitaji gari ambalo lilifanana na gari la wagonjwa na kisha kuweka oda.
“Nyie mnataka la nini?” Lilikuwa swali la kwanza kutoka kwa mtu ambaye alikuwa akikodisha magari, gari hilo lilikuwa likikodiwa na hospitali ndogo hasa zilizokuwa mbali na mjini.
“Tunakwenda kucheza mechi ya NFL chuo kwa chuo” Javier alimwambia mkodishaji.
“Kwa hivyo vyuo havina magari?”
“Magari yapo ila kwa gari la wagonjwa bado” Perez alimwambia mwanaume yule.
“Sawa. Dola elfu mbili” Mwanaume yule aliwaambia.
“Kwa siku ngapi?”
“Siku moja tu”
“Hakuna tatizo. Tutakuja kulichukua siku yoyote ile” Perez alimwambia mwanaume yule.
“Basi sawa. Ili kuepuka kuchukuliwa na watu wengine, lipieni nusu” Mwanaume yule aliwaambia, hilo halikuwa tatizo, wakalipia dola elfu moja na kisha kuondoka mahali hapo.
Kazi yao kubwa ambayo ilikuwa imebakia ni kuanza kutembelea hospitali ya Washington Medical Center kwa ajili ya kujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea. Wote wawili walikuwa na uhakika kwamba Albertina angeweza kuletwa ndani ya hospitali ile kwa ajili ya kujifungua kitu ambacho kingewafanya kumteka na kisha kuondoka nae mahali hapo.
Hawakuchoka, kwa sababu walikuwa wamekuja kipindi kirefu nchini Marekani kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kumteka Albertina, hilo wala halikuonekana kuwa tatizo, walikuwa tayari kupoteza muda lakini mwisho wa siku wafanikishe kile ambacho walitakiwa kufanikisha kwa wakati huo.
Albertina ilitakiwa atekwe na kisha kuuawa, kitu ambacho walikuwa wakitaka kukifahamu ni kwamba ni mahali gani ambapo Albertina alitakiwa kuuawa, kama ilikuwa hospitalini au nje ya hospitali hiyo.
“Popote pale, ila ningependa muende kumuua mbali na hospitali, yaani ikiwezekana hata mwili wake usionekane” Antonio aliwaambia vijana wake kupitia simu.
Hilo ndio lilikuwa neno kutoka kwa bosi wake, walitakiwa kumteka Albertina na kisha kumpeleka sehemu yoyote ambayo ilikuwa imejificha, huko wangemuua na kisha kuondoka huku wakihakikisha kwamba hakukuwa na mtu yeyote ambaye angeweza kuuona mwili wake.
“Umefikiria wapi?” Javier alimuuliza Perez.
“Kwenye pori la Juddy Stone” Perez alimjibu Perez.
Hicho ndicho walichokuwa wamekipanga kwa wakati huo. Walikuwa wakitaka kumteka Albertina na kisha kumpeleka katika pori hilo la Juddy Stone kwa ajili ya kumuua mwanamke huyo na kisha kuutelekeza mwili wake na wao kuondoka zao. Wakakubaliana wote kwa pamoja kulifanya jambo hilo bila kuhofia kitu chochote kile.
Saa sita mchana gari alilokuwa akilitumia Albertina likaonekana likianza kuingia mahali hapo. Walikuwa wakilifahamu sana gari hilo kwani w
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
,..............................
haikuonyesha kama kulikuwa na mauaji ambayo yalikuwa yamefanyika ndani ya chumba kile alichokuwa ameingizwa Albertina kwa ajili ya kujifungua watoto mapacha ambao walipanga kuwapa majina ya Hans na Catherine.
Ilikuwa mwaka 1990, mwaka ambao Marekani alikuwa akijiandaa kupigana vita na nchi ya Iraq, vita ambavyo vilipewa jina la Ghuba katika kipindi ambacho Iraq ilikuwa chini ya utawala wa Sadam Hussein huku Marekani ikiwa chini ya rais wa kipindi hicho, baba wa rais George Bush, rais aliyejulikana kwa jina la George Herbert Walker Bush.
Katika kipindi hicho ndicho ambacho wanajeshi wa Marekani pamoja na wanajeshi wa Uingereza walikuwa wakijiandaa kumkabili Sadam Hussein ambaye alikuwa amekimbilia katika nchi ya Kuwait, moja ya nchi ambayo ilikuwa ikipatikana katika kanda za nchi za Kiarabu barani Asia. Kutokana na vita hivyo ambavyo vilitegemewa kuanza muda wowote ule ndio kitu kilichopelekea wanajeshi wengi ambao walikuwa wamestaafu nchini Marekani kurudishwa kazini huku wakiambiwa kwamba huo ulikuwa ni wakati wa kurudisha heshima ya nchi hiyo katika masuala ya kivita.
Wanajeshi wengi wakakusanyika huku mwanajeshi wa kike ambaye alionekana kuwa mpole, Juddy Simon kupelekwa vitani. Katika siku za kwanza vitani ndani ya nchi za Uarabuni, Juddy alionekana kuwa mpole, mtu ambaye hakuwa muongeaji sana lakini alikuja kubadilika katika kipindi ambacho rafiki yake ambaye alikuwa mwanajeshi kulipuliwa na bomu ambalo lilikuwa limezungushwa katika mwili wa mtoto ambaye alianguka na kwenda kumsaidia.
Kitendo cha kuliona tukio lile, Juddy akaonekana kuwa na hasira sana, hakutaka kumuamini mtu yeyote katika kipindi hicho, kifo cha rafiki yake kipenzi kilimleta hasira kupita kawaida. Juddy, msichana mrembo akageuka kuwa muuaji mkubwa, akaanza kuua waarabu wengi uarabuni, hakujali kama huyu alikuwa mtoto, mkubwa, mwanamke kama yeye, alichokuwa akikifanya ni kuua tu.
Mikono yake ikajaa damu, wanajeshi wenzake wakaonekana kushanganzwa na hali ambayo alikuwa nayo katika kipindi hicho, Juddy alikuwa amebadilika mno kiasi ambacho wenzake wakaanza kumuita kwa jina la Stone yaani wakiwa na maana ya ‘Jiwe”. Kutokana na mabadiliko yake na kuwa mtu wa ukatili sana, Juddy akaonekana kuwa kama jiwe, hakumuonea mtu hurma, chuki yake kubwa ikawa kwa waarabu tu ambao alikuwa akiwachukia hata zaidi ya alivyokuwa akimchukia shetani.
Japokuwa aliendelea kubaki na urembo usoni lakini roho yake ilikuwa imebadilka kabisa. Watu walipokuwa wakitakiwa kukamatwa mateka, Juddy alikuwa akiwaua tu, hakuonekana kuwa na masihala hata mara moja. Mauaji yake dhidi ya waarabu yaliendelea zaidi na zaidi mpaka pale ambapo Marekani akashinda vita na kurudi nchini Marekani.
Bado alikuwa na roho mbaya, Juddy alikuwa na hasira kila wakati, mauaji ambayo alikuwa ameyafanya sana Uarabuni yakamfanya kuwa na roho mbaya hata katika maisha yake ya uraiani. Kila wakati alionekana kuwa mwingi wa hasira, alikuwa akijisikia akinuka damu na hivyo kila wakati alikuwa mtu ambaye alitamani kuua tu.
Kwa majirani zake hali ilikuwa hivyo hivyo. Juddy alikuwa akifanya fujo sana na kama ulikuwa ukijibizana nae, alikuwa akielekea ndani kuchukua bunduki yake. Damu za waarabu zikawa kama zinamlilia, usiku hakuwa akilala kwa raha, kila alipokuwa akilala, alikuwa akiota ndoto mbaya mbaya ambazo zilimfanya kukurupuka kila siku.
Alikuwa na mpenzi wake ambaye alipendana nae sana, Gilbert lakini kwa wakati huo hakuwa nae tena. Mara ya mwisho kusikia kwamba alikuwa nae ilikuwa ni katika ukumbi wa Livingstone, sehemu ambayo Gilbert alikuwa pamoja na msichana mwingine. Kitendo kile kilimkasirisha sana Juddy, baada ya siku tano, Gilbert hakuonekana tena huku tetesi zikisikika kwamba Juddy alikuwa amemuua mwanaume huyo.
Baada ya majirani kulalamika sana, serikali ikaamua kumkamata Juddy na kisha kumpeleka katika chumba maalumu na kisha kuwaita wataalamu wa Saikolojia na kisha kuanza kuongea nae. Hiyo haikuonekana kubadilisha kitu chochote kile, kelele za waarabu zilikuwa zikisikika masikioni mwake huku kila alipokuwa akiviangalia viganja vyake aliviona vikiwa vimetawaliwa na damu.
Juddy Simon akaonekana kuwa kama shetani, jina lake likawa likitawala mara kwa mara katika vyombo vya habari. Japokuwa polisi walikuwa wamemshikilia, baada ya mwezi mmoja, akatoroka na kukimbilia kusipojulikana. Serikali ikaanza kumtafuta lakini hawakufanikiwa kumpata mpaka pale ambapo walisikia tetesi kwamba Juddy alikuwa amekimbilia katika pori moja lililokuwa hapo Washington ambalo liliitwa Burnesvile.
Polisi wakajitahidi sana kuingia ndani ya pori hilo lakini kumtafuta Juddy wengi wao walikuwa jawatoki. Hiyo ikaonekana kumshtua kila Mmarekani, ilikuwaje kila polisi ambaye alikuwa akiingia ndani ya pori hakutoka? Je Juddy alikuwa akiwaua au ilikuwaje? Hilo ndio lilikuwa swali kubwa ambalo lilikosa jibu kabisa vichwani mwao.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Serikali haikuonekana kuelewa kabisa, walikuwa wakizidi kutuma polisi kwa ajili ya kumtafuta Juddy ndani ya pori hilo lakini matokeo yalikuwa ni yale yale, hakukuwa na mtu ambaye alitoka. Hapo ndipo pori lile likawekewa vizuizi, hakukuwa na mtu ambaye aliruhusiwa kuingia ndani ya pori hilo kwa kuona kwamba kulikuwa na mambo ya kishirikina bila kujua kwamba Juddy ndiye ambaye alikuwa akiwauawa.
Jina la pori hilo la Burnesvile likapotea na watu kuanza kuliita jina la Juddy Stone kama kumbukumbu ya jina lake. Pori likatengwa na hakukuwa na mtu yeyote ambaye aliruhusiwa kuingia humo kwa imani kwamba angeuawa. Juddy aliendelea kuishi ndani ya pori hilo huku kila alipokuwa akitoka alikuwa na sura ya bandia kwa ajili ya usalama wake.
Alikuwa akitoka na kwenda uraiani kununuaa vyakula na kisha kurudi porini usiku bila kujulikana. Kwa mikono yake akajenga nyumba ndogo porini mule, nyumba ambayo aliijenga kwa mbao tu. Mwaka 2001, Juddy alifariki dunia ndani ya nyumba yake porini humo lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa akilifahamu hilo, mwili wake ukawa umelala kitandani mpaka kuoza na kubaki mifupa mitupu.
Baada ya miaka mingi kupita, mwanaume mmoja ambaye alikuwa milionea alikuwa akitaka kufanya kazi ndani ya pori hilo. Kitu ambacho alikuwa akikitaka ni kutengeneza mizinga ya nyuki ndani ya pori hilo kwa ajili ya kujipatia asali na kuiuza hapo nchini Marekani. Hakuruhusiwa kuingia ndani ya pori hilo lakini alilazimisha mpaka watu kuona kwamba hakukuwa na tatizo, wakamruhusu kuingia ndani ya pori hilo pamoja na mkewe, huyu aliitwa Bwana Maxwell.
Siku ya kwanza kwa Bwana Maxwell kuingia ndani ya pori hilo alikuwa akitetemeka kupita kiasi, alikuwa haamini kama siku hiyo alikuwa akiingia ndani ya pori hilo ambalo lilikuwa likijulikana kuwa na mambo ya kishirikina. Bwana Maxwell hakutaka kujibu, aliamini kwamba kusingeweza kutokea kitu chochote kile kwa sababu hakupenda kuamini sana katika mambo ya kishirikina.
Jocelyn alikuwa akitembea nyuma nyuma, alionekana kuwa na hofu sana, historia mbaya kuhusiana na pori hilo la Juddy Stone ilionekana kumtisha na kujaza hofu moyoni mwake. Walikuwa wakitembea huku na kule porini mule mpaka pale ambapo walipofanikiwa kuiona nyumba moja, huku wakionekana kuwa na hofu zaidi, wakaamua kuifuata na kuingia ndani.
Nyumba ilionekana kuchoka sana na hata mbao zake zilionekana kuliwa sana na mchwa. Bwana Maxwell na mke wake hawakutaka kujali, wakaingia mpaka ndani na kisha kuanza kuangalia kila kitu kilichokuwa ndani ya nyumba hiyo.
“Nadhani humu ndipo alipokuwa akiishi Juddy” Bwana Maxwell alimwambia mke wake huku akiwa na bunduki mkononi.
“Mungu wangu! Kunatisha” Jocelyn alimwambia mumewe.
“Hebu tuingie ndani zaidi” Bwama Maxwell alimwambia Jocelyn.
“Hapana. Siwezi kuingia”
“Kwa nini?”
“Naogopa”
“Unaogopa nini?”
“Hapana. Naogopa tu” Jocelyn alimwambia Bwana Maxwell.
“Basi wewe baki hapa sebuleni na mimi niingie chumbani” Bwana Maxwell alimwambia Jocelyn.
“Hapana. Tuingie wote” Jocelyn alimwambia Bwana Maxwell.
“Si umeniambia unaogopa?”
“Siwezi kubaki peke yangu hapa” Jocelyn alimwambia Bwana Maxwell.
Wote wakaanza kupiga hatua kuelekea chumbani mule. Kila kitu ambacho kilikuwa kikionekana kulikuwa ni kitu cha zamani sana kutumika. Kulikuwa na nyumba za buibui, kulikuwa na vumbi huku kila kitu kikionekana kuchakaa kupita kawaida.
Walipoingia chumbani, wakakutana na kitanda ambacho kilikuwa na godoro ambalo lilionekana kuharibika sana huku juu ya godoro lile kukionekana kuwa na mifupa na harufu kali ikiwa ndani ya chumba hicho. Bwana Maxwell na Jocelyn walikuwa wameziba pua zao na kisha kukisogelea kitanda kile. Muda wote Jocelyn alikuwa akitetemeka kwa hofu kubwa, alikuwa ameanza kutokwa na kijasho chembamba mwilini mwake.
“Huyu atakuwa Juddy” Bwana Maxwell alimwambia Jocelyn.
“Umejuaje?” Jocelyn alimuuliza mumewe ambaye aliupeleka mkono wake mpaka katika sehemu ya kifua cha mifupa ile na kisha kuchukua kitu kimoja ambacho kilikuwa kama cheni na kuanza kukiangalia.
“Hii cheki hupewa wanajeshi tu” Bwana Maxwell alimwambia Jocelyn, akaichukua ile cheni na kisha kuiangalia, aliiona imeandikwa Juddy Simona.
“Ndiye yeye”
“Mungu wangu! Kumbe alikuwa akiishi humu?” Jocelyn aliuliza kwa mshtuko.
“Na ninadhani yeye ndiye alikuwa akiwaua watu waliokuwa wakifika ndani ya msitu huu. Hebu twende nyuma ya nyumba” Bwana Maxwell alimwambia mke wake na kuanza kuelekea nyuma ya nyumba, alikuwa ameona makaburi kupitia dirishani.
Jocelyn akazidi kutetemeka kupita kawaida. Nyuma ya nyumba ile kulikuwa na makaburi kadhaa, wakaanza kuyaangalia huku kila mmoja akionekana kujawa na hofu moyoni mwake. Hawakutaka kujiuliza sana, wakagundua kwamba makaburi yale yalikuwa ni watu ambao waliuawa na Juddy ndani ya msitu huo.
“Hali inatisha sana” Jocelyn alimwambia Bwana Maxwell.
“Nadhani humu hakuna ushirikina wowote ule bali Juddy ndiye ambaye alikuwa akiwauawa watu waliokuwa wakiingia ndani ya pori hili” Bwana Maxwell alimwambia Jocelyn ambaye akachukua kamera na kisha kuanza kupiga picha
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
.........................
Walipomfikisha ndani, wakamlaza juu ya kochi na kisha Perez kuchukua bunduki yake na kumnyooshea Albertina kochini pale tayari kwa kumuua.
“Kufa mpumbavu wewe” Perez alimwambia Albertina na kisha milio ya risasi kuanza kusikika mahali hapo.
Alan alionekana kuchanganyikiwa, hakujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kimeendelea ndani ya chumba kile. Alibaki akiwa amesimama huku mwili wake ukiwa umepigwa na ganzi, hakuamini kile ambacho alikuwa akikiona mahali pale kwa wakati ule. Madaktari wote waliiokuwa ndani ya chumba kile walikuwa wameuawa, yeye hakuhuzunishwa na mauaji ya polisi wale bali alihuzunishwa na kutokuonekana kwa mke wake mpendwa.
Akili zake akazihisi kama zimeruka kidogo, akachomoka na kisha kuelekea nje ya chumba kile, ndani ya dakika moja tu polisi wakaanza kujaa ndani ya chumba kile. Alan alikuwa amechanganyikiwa, hakujua ni kitu kipi alitakiwa kukifanya na neno gani alitakiwa kuongea mahali hapo. Alipotoka ndani ya jengo la hospitali ile, akaanza kuzunguka huku na kule, yaani mawazo yake yalimtuma kwamba watu ambao walikuwa wamemchukua mke wake walikuwa ndani ya eneo la hospitali hiyo.
Machozi yakaanza kumtoka, moyoni aliumia juu ya kile kilichokuwa kimetokea kwa wakati huo. Hakujua ni wapi ambapo alitakiwa kwenda, alibaki akilia kwa kilio kikubwa kiasi ambacho watu wengi wakaanza kumshangaa, haikuwa kawaida.
Polisi wanne wakamfuata na kisha kumchukua, wakampeleka katika chumba kimoja kidogo na kisha kuanza kumuuliza maswali kadhaa. Alan akaanza kuelezea kile kilichokuwa kimetokea, taarifa ile ilionekana kuwa taarifa yenye kutisha na kusisimua kutokea ndani ya hospitali hiyo. Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akifahamu ni kitu gani kiliendelea mpaka madaktari kuuawa na mke wa Alan kutokuonekana katika chumba cha huduma ya kujifungulia, Labour.
“Inawezekana vipi?” Polisi mmoja aliuliza huku akionekana kuchanganyikiwa.
“Hata sisi hatufahamu”
“Mmewauliza walinzi?”
“Hapana”
“Hebu twende tukawaulize. Wewe tusubiri hapa” Polisi huyo aliwaambia wenzake na kisha kumwambia Alan awasubiri ndani ya chumba kile.
Alan alikuwa akiendelea kulia, hakuamini kwamba mwisho wa furaha kubwa ambayo alikuwa nayo ingeishia namna ile. Alimpenda sana mke wake, Albertina na alikuwa radhi kuwapenda watoto wake ambao wangezaliwa, kitendo cha Albertina kutoroshwa hospitalini pale kilionekana kumchanganya kupita kawaida.
Walinzi wakafuatwa na kisha kuanza kuulizwa maswali juu ya kitu kilichokuwa kimetokea. Hakukuwa na mlinzi ambaye alikuwa akifahamu kitu chochote kile, hawakuwa na uhakika kama waliwaruhusu watu ambao walikuwa tofauti na madaktari waliokuwa ndani ya hospitali hiyo na wala hawakujua kama kuliwa na watu ambao waliingia na bunduki ndani ya jengo hilo kutokana na ukaguzi kufanyika kwa kila mtu aliyekuwa akiingia, hasa asiyehusika na hospitali hiyo.
“Kwa hiyo mlimkagua kila mtu?”
“Ndio”
“Hadi madaktari?”
“Hapana. Hatujawekea utaratibu wa kuwakagua madaktari” Mlinzi mmoja aliwajibu.
“Ooopss! Hakuna gari lililotoka ndani ya eneo la hospitali hii?” Polisi yule aliendelea kuuliza maswali mfululizo huku nae akionekana kuchanganyikiwa.
“Yametoka magari mengi sana”
“Hakuna gari ambalo waliingia watu zaidi ya watatu ambapo mmojawapo ni mjauzito?” Polisi yule aliendelea kuuliza maswali.
“Hapana” Mlinzi alijibu.
Kila kitu ambacho walikuwa wakiuliza mahali hapo, majibu ya mlinzi yalionekana kuwapa wakati mgumu wa kugundua ni kitu gani ambacho kilikuwa kimetokea. Hali hiyo iliendelea kuwachanganya mpaka katika kipindi ambacho waliamua kuelekea katika chumba ambacho kilikuwa kikihusiana na kompyuta zilizokuwa zikionyesha sehemu kubwa ya hospitali hiyo kutokana na kamera za CCTV ambazo zilikuwa zimepachikwa katika maeneo mengi ndani ya hospitali hiyo.
“Tunataka tuone ni kitu gani kilitokea toka asubuhi” Polisi yule alimwambia mwanaume aliyekuwa mbele ya kompyuta yale, alichokifanya ni kuanza kuwaonyesha video ambazo zilikuwa zimechukuliwa toka asubuhi.
Hali ilikuwa ikionekana kuwa ya kawaida sana, hakukuonekana kuwa na mtu yeyote ambaye alionekana kuwa na wasiwasi, kwa kila kamera ambayo ilikuwa ikionyeshwa, video yake ilionekana kuwa ya kawaida sana. Madaktari wengi walionekana kuwa bize huku wengine wakiongea na wagonjwa na hata wengine wakitoa ushirikiano kwa watu mbalimbali waliokuwa wakiwaleta wagonjwa ndani ya hospitali ile.
“Hii ni kameara ya wapi?” Polisi alimuuliza jamaa yule wa ndani ya chumba cha kamera.
“Hii ni kamera ya kule nyuma”
“Huwa madaktari wanaruhusiwa kupeleka wagonjwa kule?” Polisi yule alimuuliza.
“Hapana”
“Sasa kwa nini wale madaktari wanamsukuma mtu kwenye machela kuelekea nyuma ya hospitali ile? Ndio wenyewe” Polisi yule alisema huku akiwa ametoa macho.
Walichokifanya ni kurudia video zile na kisha kuvuta sura za watu wale wawili ambao walikuwa wakimsukuma mgonjwa katika machela na kisha kuziprinti na picha kuondoka nazo mpaka katika chumba ambacho alikuwepo Alan na kisha kuanza kumuonyeshea.
“Unawafahamu hao?” Hilo lilikuwa swali la kwanza aliloliuliza polisi yule huku akimuonyeshea Alan zile picha ambazo zilikuwa mikononi mwake.
“Hapana” Alan alijibu.
“Hauwafahamu kabisa?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Siwafahamu”
“Hebu ziangalie sura zao, tunahisi hawa ndio wamehusika” Polisi yule alimwambia Alan na kisha kumkabidhi zile picha.
“Hapana. Siwafahamu”
“Ooopss! Hebu ngoja” Polisi yule alimwambia Alan na kisha kutoka ndani ya chumba kile.
Kitu alichokifanya polisi yule ni kuondoka na kisha kumfuata dokta mkuu wa hospitali ile na kisha kuanza kuongea nae. Katika muda wote ambao alikuwa akiendelea kuongea nae, polisi yule alionekana kuchanganyikiwa, tukio ambalo lilikuwa limetokea lilimuumiza sana kichwa kwani kila siku walikuwa wakiweka ulinzi ndani ya hospitali hiyo, pamoja na ulinzi wao wote, kulikuwa na mauaji yalitokea na mgonjwa kuibwa bila kujulikana alikuwa wapi kwa wakati huo.
“Umesikia kilichotokea?” Polisi yule alimuuliza dokta yule.
“Nimesikia kuna mauaji yamefanyika ndio nataka nianze kazi ya kujua zaidi” Dokta yule alimwambia polisi.
“Unaweza kunijibu maswali yangu?”
“Hakuna tatizo”
“Kuna madaktari wangapi humu?”
“Wapo wengi, kama mia nane”
“Sawa. Mna madaktari wenye asili ya Mexico?”
“Mmmh! Sikumbuki. Ila nadhani hakuna” Dokta yule alimwambia polisi yule.
“Sawa. Unaweza kuwafahamu hawa watu?” Polisi yule alimuuliza huku akimgawia picha zile zilizokuwa zimechapishwa na kisha Dokta yule kuanza kuziangalia.
“Hapana. Hawa wala siwafahamu” Dokta alijibu.
Polisi yule hakutaka kuendelea kukaa ndani ya chumba kile, tayari alikwishaona kwamba hao ndio ambao walikuwa wamehusika katika mchakato mzima wa mauaji yale na hata utekaji ule. Alichokifanya ni kuanza kupiga hatua kurudi ndani ya chumba kile ambacho alikuwa amemuacha Alan akilia pamoja na polisi wengine.
Waandishi wa habari tayari walikuwa wamekwishafika ndani ya hospitali ile na walikuwa wakiendelea kuwauliza madaktari wengine pamoja na wagonjwa kile kilichokuwa kimetokea ndani ya hospitali ile. Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akifahamu kipi kilichokuwa kimetokea mpaka madaktari kuuawa, yaani hata suala la mgonjwa kutekwa hawakuwa wakilifahamu.
“Hawa si madaktari. Hebu waangalie vizuri, hauwafahamu hawa Wamexico?” Polisi yule alimwambia Alan na kisha kumuuliza.
Polisi yule alipolitaja neno ‘Wamexico’ likamfanya Alan kuanza kukumbuka, mtu wa kwanza kumkumbuka alikuwa Antonio, hapo akaanza kupata picha ambayo ilionyesha kwamba kulikuwa na asilimia sabini Antonio alikuwa amehusika katika kila kitu kilichokuwa kimetokea.
“Antonio” Alan alijisemea.
“Umesemaje?”
“Huyu atakuwa Antonio”
“Adiye nani huyo?”
Alan akaanza kumuelezea Antonio kwa kirefu, aliuelezea uadui wao ambao ulikuwa kati yao lakini pamoja na kuelezea hayo yote hakutaka kuelezea kuhusiana na kuuawa kwa baba yake wala kuuawa kwa mzee Sanchez, mambo hayo aliyafanya kuwa siri.
“Sidhani kama amehusika, unaonekana kuwa uadui wa kawaida sana” Polisi yule alimwambia Alan, kuficha kwa Alan kukamfanya polisi yule kumuona Antonio kutokuwa mhusika.
“Inawezkana amehusika”
“Hapana. Hilo ni jambo gumu. Kwa mambo hayo madogo hawezi kuua madaktari na kumteka mke wako” Polisi yule alimwambia Alan.
Alan akabaki na lake moyoni mwake, tayari alijua fika kwamba Antonio ndiye ambaye alikuwa amehusika katika kila kitu kilichokuwa kimeendelea. Moyo wake uliumia sana, aliona kwamba japokuwa yeye alikuwa amesahau kila kitu kilichokuwa kimetokea lakini bado Antonio alikuwa na kisasi moyoni mwake na wakati huo alikuwa amemteka mke wake na hakujua ni mahali gani alipokuwa.
Alan akakata tamaa, hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya mahali hapo. Yule adui wake ndiye ambaye alikuwa ameamua kufanya kila kitu kilichokuwa kimefanyika. Akaanza kuomba kimya kimya huku machozi yakimtoka, akaanza kumuombea mke wake na watoto wake huko walipokuwa, zaidi ya hilo, nae alipanga kulipa kisasi, alitaka kumuua Antonio mwenyewe.
Alan aliendela kubaki ndani ya chumba kile huku polisi wakiingia na kutoka bila kuzungumza kitu chochote kile kilcihokuwa kikiendelea, hakukuwa na polisi yeyote ambaye alimwambia kwamba ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea mahali pale. Huku akiwa katika lindi la mawazo, mara simu yake ikaanza kuita, akaichukua, alipokiangalia kioo cha simu yake, aliiona namba ya Bwana Maxwell, akaikata simu kwani hakutaka kuongea na mtu yeyote katika kipindi hicho.
Alan aliendelea kukaa ndani ya chumba kile mpaka pale ambapo alikuja kutolewa tena na kupelekwa nje, hatua iliyofuatwa ni kupelekwa kituo cha polisi kwa ajili ya kuchukua maelezo zaidi. Katika kipindi ambacho alikuwa ndani ya gari huku akiendelea kutokwa na machozi, simu yake ikaanza kuita, alipoichukua na kuangalia kioo, alikuwa Bwana Maxwell, akaamua kuipokea.
“Alan…!” Alisikia akiitwa na Bwana Maxwell simuni.
“Unasemaje?” Alan aliitikia,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Alan…!” Alisikia akiitwa na Bwana Maxwell simuni.
“Unasemaje?” Alan aliitikia, muitikio wake tu haukuonekana kama alikuwa katika mudi ya kuongea.
“Mkeo nipo nae hapa” Bwana Maxwell alimwambia Alan.
“Unasemaje?”
“Mkeo nipo nae hapa” Bwana Maxwell alirudia.
“Upo nae? Wapi?”
“Hapana McMillan Medical Center. Njoo haraka” Bwana Maxwell alimwambia Alan ambaye alionekana kuchanganyikiwa. Kitu alichokuwa akijiuliza, Bwana Maxwell ilikuwaje awe na mkewe mahali hapo, kila alichojiuliza, akakosa jibu.
****
Milio ya risasi ilikuwa imesikika mahali hapo, Javier na Perez walikuwa wameanguka chini, damu zilikuwa zikiwatoka vifuani mwao. Bwana Maxwell na mkewe, Jocelyn wakatoka kule walipokuwa wamejificha, kitu cha kwanza kilikuwa ni kumwangalia mwanamke yule aliyekuwa amelazwa kochini. Hawakuamini mara baada ya kumwangalia usoni na kugundua kwamba alikuwa Albertina.
“Mungu wangu! Imekuwaje tena?” Bwana Maxwell aliuliza kwa mshangao.
Hakukuwa na cha kuuliza, kwa sababu Alabertina alikuwa katika hali mbaya, walichokifanya ni kuanza kumsaidia katika kujifungua. Bwana Maxwell na mkewe wakawa madaktari wa muda kipindi hicho na kisha kuanza kumzaliwa Albertina.
Kila mmoja alikuwa makini, mtoto wa kwanza wa kiume akatoka, mtoto alikuwa ametoka huku mwili mzima ukiwa na damu, alikuwa kimya kana kwamba alikuwa amekufa. Jocelyn akamchukua na kisha kumtingisha kidogo, mtoto yule akaanza kulia. Hawakuishi hapo, mtoto wa pili nae akatoka, kama alivyotoka wa kwanza na ndivyo alivyotoka wa pili, Bwana Maxwell akamchukua na kisha kumtingisha na mtoto kuanza kulia.
Bwana Maxwell akavua shati lake na kisha kumbeba mtoto mmoja na Jocelyn kubaki na mtoto mwingine na kuelekea garini huku Albertina akiwa ameachwa ndani ya nyuma ile. Alichokifanya Bwana Maxwell ni kumwachia Jocelyn mtoto yule na kisha kurudi ndani ambapo akambeba Albertina kwa mikono yake miwili na kumpeleka ndani ya gari lile walilokuja nalo Javier na Perez. Bwana Maxwell akaushika usuknai, alichokifikiria ni kwenda katika hospitali ya McMillan Medical Center ambayo haikuwa mbali na pori hilo la Juddy Stone.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/.......
Hilo wala halikuonekana mbele ya macho ya wazazi wake, babu wala bibi, hicho kilikuwa ni kitu kilichokuwa moyoni, kitu ambacho kilikuwa tofauti na sura yake ya upole mara anapokasirishwa na mtu yeyote yule.
Katika muda mwingi wa kipindi cha ukuaji wa Hans na Catherine, wazazi wao walikuwa pamoja, Kila mmoja alionekana kuwa na mapenzi ya dhati kwa watoto wao hao ambao walionekana kuwa kila kitu katika maisha yao. Alan alikuwa mfanyabiashara lakini ukaribu ambao alikuwa nao kwa watoto wake ukamfanya wakati mwingine kutokwenda kazini kabisa.
Alikuwa akiwapenda watoto wake kupita kawaida, alikuwa radhi kufanya kitu chochote kile kwa ajili ya watoto wake. Hivyo ndivyo ilivyokuwa hata kwa Albertina, muda mwingi alikuwa akiwabeba watoto wake, wakati mwingine aliona kama angewaacha basi wangepotea kabisa na asiweze kuwaona tena.
Ndugu, jamaa na marafiki wa karibu wakawa wakifika mara kwa mara nyumbani hapo, kutokana na taarifa za watoto wa Alan kuandikwa mara kwa mara kwenye magazeti, habari zikawafikia watu wengi. Kila mmoja ambaye aliziona picha za watoto wale alizipenda, walionekana kuwa na mvuto mkubwa huku wakiwa wanafanana kupita kawaida.
Brian na mkewe, Stacie walikuwa miongoni mwa watu ambao walikuwa wakifika katika nyumba hiyo kwa ajili ya kuwaona watoto hao ambao walionekana kuwa na mvuto sana. Hawakuwa watoto wa kulia kila wakati, muda mwingi walikuwa wakiutumia kucheka na hata kutabasamu mara pale walipokuwa wakifanyiwa kitu chenye makusudi ya kuonyesha tabasamu yao.
Hao ndio walikuwa watoto wao pekee ambao waliwaunganisha wazazi wao na kuyafanya mapenzi yao kushamili zaidi na zaidi. Ulinzi haukupunguzwa, haikujalisha kama alikuwa ndugu, jamaa au rafiki, kila aliyekuwa akiingia ndani ya nyumba hiyo alikuwa akipekuliwa na mitambo maalumu ambayo iliwekwa ndani ya nyumba hiyo huku nao walinzi wakihakikisha usalama kwa sehemu yao.
Mwaka wa kwanza ukakatika, Hans na Catherine waliendelea kukua zaidi. Malezi na upendo kutoka kwa wazazi wao wala haukupungua hata kidogo. Kila siku walihakikisha kwamba wanakuwa karibu nao kwa ajili ya kuwapa mahitaji yote ambayo walikuwa wakiyahitaji. Mwaka wa pili ukaingia na hata kuisha huku mwaka wa tatu nao ukichukua nafasi. Uzuri wao ulikuwa ukionekana kwao, watoto wote walikuwa wakimya sana kitu ambacho kiliwapelekea wazazi wao kufikiri kwamba walikuwa na matatizo kiafya.
“Hali hii huwatokea watoto wengi sana” Dokta Lucy aliwaambia Alan na mkewe, Albertina.
“Kwa nini hutokea namna hii?” Alan aliuliza huku akimwangalia Hans ambaye alikuwa amemshika mkononi.
“Ni kawaida. Hii inaonyesha ni watoto wa aina gani umewapata. Watoto wako inaonekana watakuja kuwa wapole sana, ila nayo hiyo hautakiwi kuiweka akilini sana, kutokana na kukutana na watoto wengine, napo hali inaweza kubadilika” Dokta Lucy aliwaambia.
“Sawa. Kuna kingine cha umuhimu ambacho ungependa kutuambia?” Alan alimuuliza Dokta Lucy.
“Nadhani hakuna ila cha zaidi ni kuwa karibu na watoto wenu. Watoto wengi wanaokuwa katika hali hii wanapopata tatizo kama ugonjwa, wewe kama mzazi endapo haupo nao karibu itakuwa ngumu sana kufahamu, hivyo jitahidini kuwa karibu nao” Dokta Lucy aliwaambia.
Ushauri ambao walipewa na Dokta Lucy waliufanyia kazi. Mara kwa mara waliendelea kuwa karibu na watoto wao huku wakiwafanyia kila kitu ambacho kilitakiwa kufanywa. JApokuwa ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na wafanyakazi zaidi ya watano lakini hawakutaka wafanyakazi washughulike sana na watoto hao, wao walitaka wao kama wao ndio wawe washughulikaji wakuu wa watoto wao.
Mwaka wa tatu ukaingia. Hapo ndipo walipoamua kuwaanzisha watoto wao shule ya chekechea iliyokuwa hapo hapo Washington, Franklin Montessori, moja ya shule ambayo ilikuwa na gharama kuliko shule zote za chekechea ndani ya jiji la Washington. Shuleni hapo, bado Hans na Catherine walionekana kuwa wakimya sana, hawakuwa waongeaji kwa sana kama walivyokuwa watoto wengine.
Maisha yao shuleni hapo yaliendelea zaidi na zaidi. Kila siku walikuwa wakipelekwa na kurudishwa nyumbani. Kote huko bado Alan alikuwa akiendelea kuhakikisha ulinzi mkubwa wa watoto wake. Kutokana na kukutana na watoto watundu, Hans nae akajikuta akiingia kwenye mkumbo huo na kuwa mtundu kama watoto wengine.
Hali hiyo wala haikuwashangaza walimu kwani walijua huwa hutokea kwa watoto wote ambao hukutana na watoto wengine wenye hali fulani ila kitu ambacho kiliwashangaza zaidi ni kwamba Hans alikuwa mtundu zaidi ya watoto wote shuleni hapo, yaani hata wale ambao walikuwa wamemfanya kuwa mtundu, akaonekana kuwapita kwa utundu.
Hans akawa hashikiki, kila alipokuwa akifanyiwa hili, yeye alifanya hili. Akaonekana kuwa kama msumbufu kwa walimu wake kwani kila walipokuwa wakimuweka katika kiti hiki, yeye alikuwa akielekea katika kiti kingine, tena akimtoa mtoto mwingine na kukaa yeye.
“Huyu ameshindikana kwa utundu” Mwalimu mmoja aliwaambia walimu wenzake huku akimwamngalia Hans ambaye hakuwa na habari, ndio kwanza alikuwa akiliendesha gari lake dogo ukutani kwa kutumia mkono wake.
“Mmmh! Hivi amerithi au?”
“Hata sisi wenyewe tunashangaa. Yaani aliletwa hapa akiwa mpole sana, ila sasa hivi amekuwa balaa” Mwalimu yule aliwaambia wenzake.
Katika kipindi chote hicho ambacho Hans aliendelea kuwa mtundu, kwa Catherine hali ikaonekana kuwa tofauti kabisa. Upole wake ulikuwa ukiendelea kama kawaida. Catherine hakuwa muongeaji au mchezaji kama alivyokuwa kaka yake, Hans. Wakati mwingine walipokuwa wakiachwa darasani, Hans alikuwa akiondoka na kuelekea nje, huko alikimbia kimbia huku na kule mpaka walimu walipokuwa wakimfuata na kumuingiza tena darasani.
Mwaka wa nne ukaingia, wa tano ukaingia na ulipofika mwaka wa sita, hapo ndipo walipoanzishwa grade one katika shule ya Washington International School. Hapo ndipo ambapo walianza masomo yao. Kama kawaida wazazi wao hawakutaka kuwaacha, mara kwa mara walikuwa wakienda kuwachukua shuleni huku wakati mwingine dereva ndiye ambaye alipewa jukumu hilo. Walijua fika kwamba wao ndio walikuwa watoto wao pekee ambao waliletwa hapa duniani kwa ajili yao hivyo walikuwa na kila sababu ya kuwatunza na kuwalinda.
Mwaka huo ukakatika na mwingine kuingia, bado hali iliendelea kuwa vile vile. Katika mwaka wa pili shuleni hapo Hans alikuwa akijulikana na wanafunzi wote, walimu pamoja na wafanyakazi kwa ajili ya utundu wake. Hans hakuwa akitulia, alikuwa akipenda sana kucheza michezo mbalimbali kiasi ambacho walimu walimtabiria kwamba angekuja kuwa mchezaji wa mchezo wowote pale huko mbeleni.
wowote pale huko mbeleni.
“Hapana. Nataka mwanangu awe daktari” Alan alimwambia mwalimu.
“Ila anaonekana kupenda sana michezo, nadhani anaweza kupata nafasi ya mchezaji wa mchezo wowote ule” Mwalimu alimwambia Alan.
“Haiwezekani. Yaani kila nikimwangalia Alan, naona kabisa kwamba atakuwa kuwa dokta mkubwa sana hapo mbeleni, sasa nyie mnavyoniambia kwamba atakuja kuwa mwanamichezo mnanishangaza sana” Alan alimwambia mwalimu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Basi ngoja mpaka atakapofikisha grade la sita tutaweza kufahamu” Mwalimu alimwambia Alan.
Kwa mtazamo tu ulionyesha dhahiri kwamba Alan angekuja kuwa mwanamichezo mkubwa hapo baadae japokuwa haikuwa ikijulikana ni mchezo wa aina gani ambao baadae angekuja kuupenda sana. Alikuwa akicheza mpira wa miguu na watoto wenzake, wakati mwingine alikuwa akiuchezea mpira wa tenis na hata katika kipindi ambacho alionekana kuwa na uchovu, alikuwa akikaa chini na kuanza kuvaa kofia ivaliwayo na wachezaji wa mchezo wa NFL.
Miaka ikazidi kusonga mbele kama kawaida. Mwaka wa sita ulipoingia, wakamaliza na hatimae kuanza masomo katika shule ya Anacostia High School. Hapo, Hans pamoja na Catherine wakaanza masomo yao ambayo kwa nchini Tanzania yalionekana kama kidato cha kwanza. Kwa kiasi fulani Hans alikuwa akijitambua sana na hivyo akawa amepunguza utundu wake na kutulia huku akianza kusoma.
Uwezo wake ulikuwa ukionekana darasani, alikuwa akifanya vizuri darasani tofauti na Catherine ambaye upole wake ukaonekana kuwa tatizo kwani muda mwingi alikuwa akipenda kukaa peke yake tofauti na Hans ambaye alionekana kuwa mtu wa kujichanganya. Hans alipoonekana kwamba haelewekieleweki hapo ndipo Bwana Alan alipoamua kumuamisha shule na kumpeleka katika shule iliyokuwa ikichukua wanafunzi wa Sayansi ya Washington Public Charter School.
Washington Public Charter School ilikuwa ni miongoni mwa shule ambazo zilikuwa zikifundisha sana masomo ya Sayansi nchini Marekani ndani ya jiji la Washington. Madaktari wengi ambao waliokuwa na uwezo mkubwa walikuwa wamepitia katika shule hiyo ambayo ilionekana kutoa elimu bora zaidi ya shule nyingine jijini Washington.
Katika mwaka wa kwanza wa Hans kufika shuleni hapo, moja kwa moja akajiingiza katika suala la kupenda sana kwenda maktaba na kujisomea vitabu mbalimbali ambavyo vilikuwa vikihusu miili ya mwanadamu. Kwa kupitia vitabu hivyo, Hans akaanza kutekwa akilini, akawa na hamu kubwa ya kutaka kuwa daktari na mwisho wa siku akajikuta akijiita Dr Hans.
Darasani hakuwa mchovu, alikuwa akitumia muda mwingi sana kujisomea, kila siku alikuwa akishinda na vitabu vingi katika chumba chake, hakuonekana kutaka mchezo wowote ule, kazi yake kubwa ilikuwa ni kusoma vitabu tu.
Kitendo cha kusoma sana vitabu kkikampelekea kufahamu mambo mengi, akaanza kutorka shuleni na kuelekea katika hospitali nyingi jijini hapo na kwenda kuwauliza madaktari maswali mbalimbali ambayo alikuwa nayo katika karatasi yake. Hans akaonekana kuwa mwanafunzi wa tofauti, mambo ambayo walikuwa wakifundishwa darasani yeye alikuwa akiyafahamu toka kipindi kirefu cha nyuma.
Hans alionekana kudhamiria kuwa dokta, alichokifanya ni kununua koti kubwa pamoja na mashine ya kusikilizia mapigo ya moyo na kisha kuvaa katika kila kipindi alichokuwa akielekea darasani. Kwa mtazamo alionekana kuwa kituko lakini akilini mwake kulikuwa na kitu ambacho kilijengeka, alikuwa akiishi kwa imani kwa kuamini kwamba kuna siku angekuja kuwa dokta mkubwa nchini Marekani.
“Nataka kuwa dokta” Hans alimwambia Juliet, msichana ambaye alikuwa akisoma nae.
“Kwa sababu gani?”
“Nataka utakapopata ujauzito nikuzalishe” Hans alimwambia Juliet na kisha kuanza kucheka.
“Yaani unataka kuwa daktari kwa sababu unataka kunizalisha tu?” Juliet alimuuliza Hans.
“Ndio”
“Kwa nini sasa?”
“Basi tu”
“BAsi usijali, utakuwa tu daktari na watoto wangu wote nitakuja kujifungulia katika hospitali yako” Juliet alimwambia Hans.
Kutokana na utundu wake, ucheshi pamoja na mambo mengine kama kuongea sana na watu, Hans akatokea kupata marafiki wengi shuleni hapo, alikuwa akiongea na kila mtu ambaye alikuwa akitaka kuongea nae. Hans hakubagua, hakujali kama yule alikuwa msichana, mvulana, mnene, mwembamba, mrefu, mfupi, mweusi au mweupe, yeye kila mtu mbele ya macho yake alionekana kuwa sawa na mwingine.
Ucheshi wake aliokuwa nao ukawafanya wasichana wengi kumpenda, Hans alionekana kuwa na mvuto mbele ya wasichana ambao walikuwa wakimfuata lakini mpaka katika kipindi hicho hakuwa tayari kuwa na msichana kwani alikuwa na hofu kubwa sana kuongea na msichana yeyote kuhusiana na mahusiano ya kimapenzi.
Mwaka wake wa tatu kuwa shuleni hapo ndipo kukamfanya kuanza kuzoeana zaidi na Juliet, huyu akaonekana kuwa rafiki yake mkubwa lakini hakukuwa na mtu yeyote miongoni mwao ambaye alikuwa akifikiria kitu chochote kile kuhusiana na mahusiano. Mioyo yao ilikuwa ikiutambua urafiki wao, hawakuwa na hisia zozote zile kuhusiana na mapenzi, walikuwa wakijichukulia kama watu wa kawaida sana ambao walitakiwa kupeana kampani katika kila kitu.
Mambo yalikuja kubadilika walipoingia mwaka wa nne. Hapo ndipo hisia za kimapenzi zilipoanza kuchipua mioyoni mwao. Wakaanza kama utani, leo walikuwa wakishikana, wiki ijayo walikuwa wakibusiana mikono, wiki iliyofuata walikuwa wakibuasiana mashavuni na mwisho wa siku kuja kubadilishana mate kabisa.
Hapo ndipo ambapo kila mmoja akaonekana kuwa muwazi kwa mwenzake, mapenzi ambayo walikuwa nayo hayakujificha, walikuwa wakionyesheana waziwazi. Kila siku walikuwa pamoja, walikula na kufanya mambo mengine pamoja. Hans akatokea kumpenda sana Juliet na hata Juliet akatokea kumpenda sana Hans.
Walijitahidi kuwa wasiri sana katika uhusiano huo lakini mapenzi hayo yakaonekana kuwa kikohozi, baada ya mwezi mmoja tu, kila mmoja shuleni hapo akaufahamu uhusiani huo. Hawakutaka kujificha tena, kwa sababu walijiona kuwa wakubwa, wakajiachia na kuendelea kuonyesheana mapenzi ya waziwazi.
“Dokta wewe mbaya sana” Humphrey, mmoja wa marafiki wa Hans alimwambia huku akicheka.
“Kwa nini?”
“Nimeona kazi yako, unatisha” Humphrey alimwambia Hans.
“Hebu niambie, umeona nini?” Hans alimuuliza Humphrey huku akionekana kushtuka.
“Kazi yako”
“Ipi”
“Wewe si umekuwa dokta wa magonjwa ya wanawake” Humphrey alimwambia Hans.
“Hapana. Hebu niambie, umeona nini”
“Mbona unakuwa na haraka hivyo? Usiogope bwana”
“Sawa, siogopi. Niambie umeona nini”
“Juliet”
“Amefanya nini?”
“Wewe mbaya sana. Ninakupigia saluti”
“Hebu niambie umeona nini Humphrey?”
“Uhusiano wenu, mmejificha weeee, mwisho wa siku tumefahamu. Jana tu nimeona ukijifanya mwakasarakasi. Wewe mbaya sana dokta” Humphrey alimwambia Hans na kisha wote kuanza kucheka.
“Kumbe uliona! Kweli dunia haina siri”
“Nilikuja mpaka chumbani kwako, nikafungua mlango na kuingia, bila shaka lilikuwa ni tendo la kushtukiza mpaka mlango mkasahau kuufunga” Humphrey alimwambia Hans.
“Hahaha! Achana na hayo”
“Poa. Usijali. Hiyo ni siri yangu japokuwa watu wengi wanajua mpo kwenye mahusiano” Humphrey alimwambia Hans.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Najua wanajua ila mambo kama yale uliyoyaona hawajui kama tumeanza kuyafanya” Hans alimwambia Humphrey.
Walifanya sana mapenzi kama wapenzi, hawakutaka kujisahau kabisa, bado walikuwa wanafunzi, waliona kuwa kuna kila sababu za wao kutumia mpira, na hvyo ndivyo walivyokuwa wakifanya kila walipokuwa wakikutana kimwili. Kila mmoja akaonekana kuwa muwazi kwa mwenzake huku kila mmoja akiendelea kusoma kwa bidii sana.
“Unajua nafikiria nini mpenzi?” Hans alimuuliza Juliet.
“Hapana”
“Nataka kuwa dokta wa kutengeneza dawa za kuua sumu mwilini mwa binadamu” Hans alimwambia Juliet.
“Kivipi?”
“Mwili wa binadamu huwa unakuwa na sumu sana, wakati mwingine hata watu wanapopata ajali ni lazima kuwe nadawa za kuulia bakteria pamoja na wadudu wengine, sasa mimi ndiye nataka kutengeneza dawa hizo. Watu wakipata ajali, dawa zangu zitumike katika majeraha yao makubwa, au kama mtu mwili wake utakuwa na sumu kubwa, atumie dawa yangu” Hans alimwambia Juliet.
“Utaweza?”
“Sana tu. Ila kwanza kabla ya kutengeneza dawa, ni lazima nijue kutengeneza sumu” Hans alimwambia Juliet.
“Kwa nini?”
“Hivyo ndivyo inavyokuwa. Unapotengeneza dawa ya kitu fulani basi inabidi ujue kukitengeneza hicho kitu, hapo utafanikiwa sana” Hans alimwambia Juliet.
“Hakuna tatizo. Mimi nataka kuwa dokta wa magonjwa ya wanawake tu inatosha” Juliet alimwambia Hans.
“Utafanikiwa sana, nakuamini mpenzi, utafanikiwa sana” Hans alimwambia Juliet.
“Asante kwa kunitia moyo” Juliet alimwambia Hans.
Siku ziliendelea kwenda mbele huku mapenzi yao yakizidi kuongezeka, kila mmoja aliendelea kumjali na kumsikiliza mwenzake, mapenzi yao ndani ya mioyo yao yalikuwa makubwa kiasi ambacho kiliwashangaza hata wao wenyewe. Shule iliendelea zaidi huku Hans akiendelea kujiita Dokta. Kila wakati alikuwa akivaa koti refu jeupe pamoja na mashine ya kusikilizia mapigo ya moyo ikiwa shingoni mwake.
Baada ya miaka mingine miwili, wakamaliza kabisa elimu ya sekondari na kisha kuingia
chuo. Kutokana na mapenzi makubwa ambayo walikuwa nayo hawakutaka kuwa mbali mbali,
walichokifanya ni wote kuchagua kujiunga na chuo cha kulipia cha St; Corneus University ambacho kilikuwa pembezoni mwa jiji la Washington.
Ukaribu wao ukazidi kushamiri huku wote wawili wakitumia muda mwingi kusoma pamoja na kufanya mambo mengine maishani mwao. Japokuwa maisha yalikuwa yakiendelea lakini Bwana Alan na Bi Albbertina hawakutaka kuwaambia watoto wao juu ya kile kilichokuwa kimetokea katika miaka ya nyuma, hawakutaka kuwaambia juu ya uadui mkubwa ambao walikuwa nao na Mmexico, Antonio.
Bwana Alan alihakikisha watoto wake wanapata ulinzi wa siri katika kila sehemu
watakazokwenda, hakutaka kuwapoteza wala kusikia kwamba watoto wake walikuwa wametekwa na kuanza kuingia gharama. Bwana Alan aliposikia kwamba mtoto wake, Alan alikuwa katika uhusiano na msichana Juliet, hakutaka kuchelewa, akawaagiza watu wake kuanza kumchunguza huyu Juliet alikuwa na nani na alikuwa mtoto wa nani.
Hakutaka kumwamini mtu yeyote katika maisha ya watoto wake, alikwishawahi kuwa rafiki
mkubwa wa Antonio lakini nyuma ya pazia Antonio alikuwa mtu mwingine kabisa ambaye alileta matatizo makubwa katika familia yake. Bwana Alan akaanza kusubiri majibu juu ya Juliet na majibu yalipokuwa tayari akapewa kwa kuambiwa kwamba Juliet alikuwa mtoto wa tajiri Mike, tajiri ambaye alikuwa akimiliki kampuni ya kutengenezea karatasi nchini Marekani. Bwana Alana akaonekana kuwa huru, hapo hakukuwa na tatizo kabisa kwa kuamini kwamba mtoto wake, Hans angekuwa salama na si kama alivyokuwa akifikiria. Katika kipindi ambacho Hans na Catherine wanafikisha miaka kumi na nane ndio kipindi ambacho Hans akachaguliwa na kuwa Dokta katika hospitali ya Mississippi Medical Center iliyokuwepo hapo Mississippi. Hiyo ikaonekana kuwa furaha kwake, alikuwa amesoma kwa kipindi kirefu sana na alitegemea kwamba kuna siku angekuja kuwa dokta na katika kipindi hicho ndoto yake ikaonekana kukamilika japokuwa bado alikuwa akihitajika kusoma zaidi na zaidi kwa ajili ya kuwa bora zaidi ya alivyokuwa katika kipindi hicho.
Hilo halikuwa tatizo kwa Hans, bado alikuwa akiendelea kusoma na kufanya kazi kama kawaida. Aliwahudumia wagonjwa kwa kuwapa huduma bora ambazo walivutiwa nae kila siku. Kutokana na ucheshi wake, Hans akajikuta akitengeneza urafiki na madaktari wenzake pamoja na wagonjwa ambao walikuwa wakifika mahali pale.
Hakuwa amefikia uwezo wa kutengeneza dawa za kuua sumu ndani ya miili ya binadamu lakini kila siku alikuwa akielekea maabara kwa ajili ya kuifanyia kazi dawa hiyo. Ilimchukua Hans miaka miwili, hapo ndipo alipofanikisha kutengeneza dawa aliyoipa jina la HAAC4, dawa ambayo ilikuwa inaherufi za mwanzo za majina yote ya watu wa katika familia yao yaani Hans, Alan, Albertina, Catherine huku namba 4 ikiwakilisha idadi ya watu hao.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Dawa ikapelekwa katika sehemu za vipimo. Madaktari mabingwa wakakutana na kisha kuanza kuiangalia dawa hiyo. Dawa ilionekana kuwa yenye ubora na kila walipokuwa wameitumia kama jaribio kwa wagonjwa ilionekana kufanya kazi sana kwa kuua sumu mwilini mwa mwanadamu. Hiyo ikaonekana kuwa sifa kwake, jina lake likazidi kuvuma zaidi na zaidi. Kulikuwa na madaktari wakubwa ambao walikuwa na masters zao lakini hakukuwa na madaktari hao ambaye alikuwa ametengeneza dawa yoyote ile. Kitendo cha Hans kutengeneza dawa kilionekana kuwa cha tofauti sana, alionekana kuwa na kitu cha ziada kichwani mwake. Dawa ile ikaanza kutangazwa na kisha kuingizwa sokoni.
Dunia ikaonekana kupata ahueni, watu wengi walikuwa wameathiriwa na sumu miilini mwao, dawa ile ikaonekana kuwa mkombozi. Serikali ya Marekani ikaingia mkataba na Hans kwa kumlipa zaidi ya dola milioni mia moja na thelathini kila mwaka kwa ajili ya kuisambaza dawa hiyo duniani kote. Hans hakuonekana kuwa na tatzio, japokuwa fedha hazikuwa za kutosha lakini akaamua kuruhusu kwa sababu alitaka watu wengi wapate tiba juu ya sumu ambazo walikuwa nazo miilini mwao. Hans hakumsahau Juliet, bado alikuwa akiendelea kuwa nae kila siku. Katika kipindi hicho Juliet alikuwa Dokta kama alivyotaka kuwa, Dokta ambaye alikuwa akishughulika na magonjwa ya wanawake tu. Ukaribu wao ukaongezeka mara baada ya Juliet kuomba uhamisho wa kuhamishiwa katika hospitali ya Mississippi Medical Center, hakukataliwa, akaruhusiwa kwenda kufanya kazi katika hospitali hiyo.
“Nimekukumbuka sana mpenzi” Hans alimwambia Juliet.
“Hata mimi kipenzi”
“Umekumbuka nini kutoka kwangu?” Hans alimuuliza Juliet.
“Kila kitu”
“Kama kipi?”
“Tabasamu, kicheko, meno yako meupe, macho yako mazuri, yaani kila kitu” Juliet alimwambia
Hans. Wawili hao waliendelea kuwa karibu zaidi na zaidi. Mioyo yao bado ilikuwa na mapenzi mazito, walipendana na kujaliana kila siku katika maisha yao. Hawakuwa na muda wa kugombana, mara kwa mara walikuwa wakiyafurahia maisha yao ya mahusiano ya kimapenzi.
“Nataka nikuoe. Upo tayari?” Hans alimuuliza Juliet.
“Kwa nini nisiwe tayari mpenzi” Juliet alimuuliza Hans.
“Inawezekana usiwe tayari”
“Nipo tayari. Unataka tuoane lini?”
“Kuna mkutano wa matajiri utafanyika kwa ajili ya kuzisaidia nchi masikini duniani, nadhani baada
ya hapo, tutaoana” Hans alimwambia Juliet.
“Sasa harusi yetu inahusika vipi na huo mkutano?” Juliet alimuuliza Hans.
“Baba amehitaji niwe pamoja nae”
“Wapi?”
“Kwenye mkutano huo” Hans alimjibu Juliet.
“Basi sawa. Utaanza lini?”
“Miezi sita ijayo”
“Hakuna tatizo”
KIla mmoja akaonekana kuwa na presha, wote kwa pamoja walikuwa wakitamani sana kuingia katika maisha ya ndoa. Ndoa baada ya miezi sita kilionekana kuwa kipindi kirefu sana lakini hawakuwa na jinsi, walitakiwa kusubiria mpaka pale ambapo mkutano huo ungefanyika na kisha kumalizika. Hapo ndipo miezi ikaanza kukatika, ukaanza mwezi wa kwanza mpaka ulipotimia mwezi wa sita. Katika kipindi hicho Bwana Alan hakuonekana kuwa na raha hata kidogo. Alikuwa tofauti na kipindi cha nyuma hali ambayo ilionekana kumjaza maswali mengi Hans lakini hakuwa na cha kuuliza zaidi ya kubaki kimya huku akijitahidi kupeleleza ni kitu gani kilikuwa kikiendelea kwa baba yake.
“Antonio nae atakuwepo” Bwana Alan alimwambie mke wake, Albertina.
“Kwenye huo mkutano?”
“Ndio”
“Mungu wangu!”
“Yaani nimeshtuka sana, sijui nitakaa vipi na mbaya wangu meza moja” Bwana Alan alimwambia
mke wake.
“Haina jinsi. Kuna mwingine?”
“Watakuwepo matajiri kutoka sehemu mbalimbali duniani pamoja na katibu wa Umoja wa Mataifa,
Bwana Powell” Bwana Alan alimjibu mke wake, Albertina.
“Usijali mume wangu, nadhani Antonio atakuwa amesahau kila kitu”
“Sina uhakika juu ya hilo. Ngoja tusikilizie” Bwana Alan alimwambia mke wake, Albertina.
*****
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nchi masikini zilizidi kuongezeka duniani, uchumi ulikuwa umeyumba sana kiasi ambacho Umoja wa Mataifa ukaonekana kushangaa. Vyakula havikuwa vikipatikana vya kutosha hasa katika nchi zilizokuwa katika bara la Afrika kitu ambacho kilionekana kuleta maafa ya njaa. Maswali mengi yakaanza kumiminika vichwani mwa watu wengi kwamba ni kitu gani ambacho kilikuwa kimetokea. Msaada ulikuwa ukihitajika sana, kilichofanyika, mwenyekiti wa Umoja wa Mataifa, Bwana Powell akaandaa mkutano jijini Washington, mkutano ambao ungehudhuriwa na matajiri kutoka katika bara la Afrika, Marekani kusini na kaskazini, Ulaya na Asia huku bara la Ulaya wakipewa nafasi ya kuhudhuria matajiri wawili tofauti na mabara mengine. Bwana powelndiye ambaye alikuwa msimamizi wa mkutano huo, yeye ndiye ambaye alikuwa amewaita matajiri hao kwa ajili kuhudhuria mkutano huo ambao ulikuwa ukisikiliziwa na mataifa mengi duniani ili kujua ni kitu gani ambacho kilikuwabaliwa kufanywa kama njia mojawapo ya kutokomeza njaa.
Bill Gates alitakiwa kuwepo kwenye mkutano huo ila kwa sababu alionekana kuwa bize barani Afrika katika kutembelea vituo mbalimbali vya watoto yatima, nafasi yake ikachukuliwa na Bwana Alan ambaye alihakikisha kuiwakilisha vyema Marekani.
“Jiandae, kesho ndio siku ya kwanza ya mkutano” Bwana Alan alimwambia Hans.
“Hakuna tatizo, nimekwishajiandaa vya kutosha” Hans alimwambia baba yake.
Kesho ilipofika, wote wakaanza kuondoka kuelekea katika hoteli ya kimataifa ya MGM Grand
iliyokuwa Las Vegas na kisha kuanza kuhudhuria mkutano huo. Muda wote Bwana Antonio hakuwa akimwangalia kwa macho mazuri Bwana Alan, kwa mtazamo ambao alikuwa akimuonyeshea, alionekana kuwa na kitu moyoni mwake, alionekana bado kuwa na kila sababu za kumuua Bwana Alan, ikiwezekana hata Hans pia. Huo ndio ulikuwa mkutano ambao ulimfanya Hans kuizunguka dunia kwa ajili ya kuwaua matajiri hao, mauaji ambayo yalimfanya kuwa mtu anayehitajika zaidi duniani kuliko mtu yeyote yule. Kwa kutumia sindano iliyokuwa na sumu, alikuwa akiwateketeza matajiri wote, sababu kubwa, ilikuwa ni njia mojawapo ya kulipiza kisasi kwa kile kilichokuwa kimetokea.
SHUKRANI.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment