Simulizi : Mungu Pekee Ndiye Atakayenisamehe
Sehemu Ya Nne (4)
Ilipoishia jana
“Basi ichukue na maiti yake ukaizike, hii ni kazi yako na sitaki mtu mwingine ajue” Mzee Sanchez alimwambia Mendez huku akiupeleka mkono kiunoni kwa lengo la kutoa bunduki yake na kumfyatulia mtu ambaye alikuwa ameingia pamoja na Mendez.
Songa nayo
“Kuna mtu anaitwa Mendez”Jocelyn alimwambia mumewe, Bwana Maxwell.
“Amefanya nini huyo?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Huyo ndiye mtu ambaye anaingia ndani ya nyumba ile kiurahisi sana” Jocelyn alimwambia Bwana Maxwell.
“Kivipi sasa?”
“Yeye ndiye huwa anachukua maiti kutoka ndani ya nyumba ile na kisha kwenda kuzizika” Jocelyn alimwambia Bwana Maxwell.
“Huwa anakwenda kuzizika wapi?”
“Hilo wala silijui. Cha msingi kama unataka kuingia ndani ya nyumba ile na kama unataka kuonana na huyo Alan haina jinsi kufanya ninachokwambia” Jocelyn alimwambia mumewe.
“Sawa. Nitampata vipi huyo Mendez?”
“Kazi rahisi. Ila nahisi atahitaji fedha”
“Kama dola ngapi?”
“Nafikiri kuanzia elfu ishirini” Jocelyn alimwambia Bwana Maxwell.
“Mbona kiasi kikubwa hicho?”
“Sasa unafikiri kuingia ndani ya nyumba ya Sanchez utaingia na dola ngapi? Ili upate ruhusa ya kuingia mule basi ni lazima uhonge kiasi kikubwa cha fedha” Jocelyn alimwambia Bwana Maxwell.
Hata kabla hajakubali, Bwana Maxwell akaifuata suruali yake na kisha kuanza kutazama mifukoni mwake. Kiganja chake kikakutana na noto kadhaa, alipozitoa na kuanza kuzihesabu, zilikuwa ni dola laki moja na kumi. Akachukua dola elfu thelathini na kisha kuanza kumfuata mkewe, Jocelyn pale kitandani.
“Niambie huyo Mendez anapatikana wapi”
Hawakutaka kubaki ndani ya chumba kile, moja kwa moja Bwana Maxwell akaivaa suruali ile iliyokuwa na fedha zake na zile alizozichukua kuzirudisha tena na kuondoka ndani ya chumba hicho kwani hawakuwa na mpango wa kurudi tena ndani ya chumba kile. Hapo wakaanza safari ya kuelekea katika baa iliyokuwa maarufu sana hapo Monterrey, Laspinho ambayo ilikuwa pembezoni kidogo mwa jiji hilo.
Baa hiyo ndio ambayo ilikuwa ikisikika sana katika kipindi hicho, watu walikuwa wakijazana kwa wingi kwa sababu vinywaji vyake havikuwa na bei kubwa kama katika baa nyingine. Watu ambao walikuwa ni walevi kupindukia walikuwa wakimiminika kwa wingi ndani ya baa hiyo ambayo asilimia kubwa ya watu waliokuwa wakiingia walikuwa ni wale wenye maisha ya chini.
Kama zilivyokuwa baa nyingine, wanawake hawakukosa mahali hapo, wanawake walikuwa wengi tena wale ambao walionekana kuwa wa bei rahisi kabisa, wanawake ambao hawakutaka hata kupelekwa hotelini kwa ajili ya kumaliza shida zako, wao hata vichochoroni walikuwa tayari kukidhi haja ya mwili wako.
Biashara zilizokuwa zikifanyika hapo Laspinho zilikuwa nyingi na tena nyingine zilikuwa ni za hatari hatari. Watu ambao walikuwa wakifanya biashara za madawa ya kulevya walikuwa wakikutania ndani ya baa hiyo, watu ambao walikuwa wakitafuta wanawake wazuri, wanawake ambao walikuwa wakiyajua mapenzi kitandani nao walikuwa wakifika ndani ya baa hiyo, Laspinho.
Katika kipindi cha nyuma baa hii ilionekana kuwa kama baa nyingine jijini hapo, hazikuwa na watu wengi lakini baada ya kampuni ya filamu nchini Marekani, 20 Century Fox ilipoandaa filamu yake ya Dusk Till Down iliyoigizwa na George Clooney mwaka 1996 ambayo ilimaliziwa ndani ya baa hiyo, hapo ndipo ambapo baa ya Laspinho ilipoanza kupata wateja.
Watu wengi walikuwa wakimiminika ndani ya baa hiyo kwa ajili ya kuyaona mazingira ambayo yalikuwa yakionekana katika filamu hiyo. Kitendo cha kufika ndani ya baa hiyo na kukuta kwamba vinywaji vilikuwa vikiuzika kwa bei rahisi ndicho ambacho kiliwafanya watu kuendelea kumiminika zaidi na zaidi na kuipa jina baa hiyo.
Hapo ndipo ambapo Mendez alipokuwa akipenda sana kwenda kunywa nyakati za usiku. Mendez hakuwa na fedha nyingi, kwa sababu alikuwa mlevi mashughuli ndani ya baa hiyo, kiasi kidogo ambacho alikuwa akilipwa kama malipo ya kwenda kuzizika maiti porini kilikuwa kikimtosha sana kwa kununulia mizinga kumi ya pombe na kunywa mpaka kupoteza network.
“Bado mapema mno. Mpaka saa mbili usiku ndio huwa anaingia ndani ya baa hii” Mhudumu wa baaa ile, msichana ambaye alionekana kuwa mrembo machoni mwa Bwana Maxwell aliwaambia mara baada ya kumuulizia Mendez.
“Asante” Bwana Maxwell alimwambia msichana yule, wakatafuta viti na kisha kwenda kukaa.
Mtu ambaye walikuwa wakimsubiri mahali hapo alikuwa Mendez, huyu ndiye ambaye alionekana kuwa muhimu kwa wakati huo. Kwa sababu sifa zake zilikuwa ni ulevi, hilo wala halikuonekana kuwa tatizo kwa Bwana Maxwell, alikuwa akijua sana jinsi ya kwenda sawa na watu wa namna hiyo. Waliendelea kusubiri mahali hapo, walipoona kwamba muda unazidi kwenda na Mendez hatokei mahali hapo, wakaamua kuondoka kuelekea katika hoteli iliyokuwa karibu na baa ile huku wakimwachia mhudumu yule namba ya simu kwamba awape taarifa mara Mendez atakapofika hapo.
Ilipofika saa tatu kasoro usiku ndio muda ambao Mendez akawa anaingia ndani ya baa hiyo, mhudumu yule alipomuona, kwa haraka akawapigia simu na kuwaambia kwamba mtu wao alikuwa amekwishafika kitu ambacho kikawarudisha mpaka ndani ya baa ile, Laspinho.
“Kuna nini?” Mendez aliwauliza.
“Kuna kitu nataka utusaidie” Bwana Maxwell alimwambia Mendez mara baada ya kujitambulisha.
“Kitu gani?”
“Kwanza unakunywa kinywaji gani?” Bwana Maxwell alimuuliza Mendez.
“Bud Light Chelada” Mendez aliwaambia na Bwana Maxwell kumuita mhudumu.
“Chupa ngapi?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tano zinanitosha” Mendez alimjibu.
Bud Light Chelada ilikuwa ni moja ya pombe ambayo ilikuwa ikipatikana sana nchini Mexico japokuwa haikuwa ikitengenezwa ndani ya nchi hiyo. Hii ni pombe ambayo ina umaarufu kuliko pombe zote ambazo zilikuwa zinapatikana nchini hapo. Umaarufu mkubwa wa pombe hii ulitokana na kuwa na asilimia kubwa ya kilevi kitu ambacho walevi wengi walikuwa wakitamani sana kuinywa kwani waliamini kama ungekunywa glasi moja tu basi hamu yako ya pombe yote ingekutoka siku hiyo.
Pamoja na umaarufu wake, pombe hii ilikuwa ni gharama sana. Ilikuwa ikiuzwa kuanzia mia nane kwenda juu na ni walevi wachache sana tena wenye uwezo mkubwa kifedha ndio ambao walikuwa wakinywa Bud Light Chelada. Kwa Mendez, pombe ile aliwahi kuinywa siku mbili tu tena zote zikiwa ni za kununuliwa tena glasi moja tu. Shauku yake kila siku ilikuwa ni kuwa na chupa nyingi za pombe ile ndani ya nyumba yake, alitamani sana kuinywa pombe ile akiwa chumbani, sehemu ambayo haikuwa na kelele nyingi, siku hiyo akaona kwamba ni siku ambayo alikuwa akiitamani sana ifike katika maisha yake.
“Yaani hata haushtuki” Mendez alimwambia Bwana Maxwell mara baada ya kumwagiza mhudumu kuleta chupa za pombe hizo.
“Kushtuka na nini?”
“Na bei. Nilifikiri ungeguna” Mendez alimwambia.
“Kwani ni kiasi gani pombe hiyo?”
“Chupa moja dola mia nane”
“Sasa mbona bei rahisi sana. Kwa nini usichukue chupa kumi kabisa kama kweli wewe ni mnywaji?” Bwana Maxwell alimwambia Mendez kana kwamba hakuwa akijua bei za pombe zile.
Maneno yale hayakuonekana kuaminika kwa Mendez, ni kwa kipindi kirefu sana alikuwa akitaka kupata ofa kama ile ambayo alikuwa akipewa mahali pale. Mara ya kwanza aliwaambia kwamba alihitaji chupa tano za pombe ili awaone lakini cha kushangaza Bwana Maxwell alikubaliana nae bila kuonyesha wasiwasi wowote ule. Mendez akagundua kwamba watu ambao alikuwa amekaa nao mahali pale walikuwa na fedha, hivyo alitakiwa kuwatumia vizuri. Chupa tano zilipoletwa, mhudumu akaagizwa chupa tano nyingine.
“Ila kwa nini mnanifanyia haya yote?” Mendez aliwauliza.
“Ni kwa sababu kuna kazi nataka unifanyie” Bwana Maxwell alimjibu.
“Kazi gani?”
“Natafuta maiti kwa ajili ya kusafirishia madawa ya kulevya” Bwana Maxwell alimwambia.
“Unatafuta maiti?”
“Ndio”
“Sasa kwa nini usiende hospitalini?”
“Huko nitatumia fedha nyingi”
“Sasa mimi nitatoa maiti wapi?” Mendez aliwauliza.
“Kwa mzee Sanchez”
“Kwa mzee Sanchez?”
“Ndio. Wewe si huwa unakwenda kuchukua maiti na kwenda kuzizika? Nataka maiti moja uniuzie” Bwana Maxwell alimwambia.
“Ndio. Ila hajanipigia simu na kunipa taarifa ya maiti”
“Ila kuna mtu ametekwa, nadhani atauawa na maiti yake ndio ninaitaka” Bwana Maxwell alimwambia Mendez.
“Alitekwa lini?” Mendez aliuliza.
“Toka jana”
“Mmh! Sikupewa taarifa”
“Najua ila hapa ndio nakupa taarifa”
“Kwa hiyo itakuwaje?”
“Nataka twende na wewe mpaka huko ili nikaichukue maiti hiyo” Bwana Maxwell alimwambia Mendez.
“Sasa kwa nini nisiende peke yangu halafu nikakuletea maiti nje?”
“Tatizo nataka kuiona kama inafaa. Wakati mwingine kwenye shughuli za usafirishaji wa madawa ya kulevya inatakiwa ipatikane maiti nzuri” Bwana Maxwell alimwambia Mendez.
“Hakuna tatizo. Sasa kama haitofaa ndio tuseme hautonilipa?” Mendez alimuuliza Bwana Maxwell.
“Kwani si tayari nimekwishakulipa”
“Unamaanisha hizi pombe?”
“Ndio maana yake. Maiti ifae, isifae wewe ushakula chako” Bwana Maxwell alimwambia Mendez.
“Basi sawa. Nadhani tufanye kesho asubuhi. Ila una uhakika?” Mendez alimwambia na kisha kuuliza.
“Asilimia mia moja”
“Sawa”
“Kwa hiyo tukutane wapi hiyo asubuhi?”
“Wewe unapatikana wapi?”
“Popote pale”
“Basi tukutane hapa baa saa moja asubuhi” Mendez alimwambia Bwana Maxwell.
“Hakuna tatizo”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya hapo maongezi mengine yakaendelea. Muda wote Mendez alionekana kuwa na furaha kupita kawaida, kitendo cha kupewa ofa ya pombe kali kilimfurahisha sana. Kwake, alimuona Bwana Maxwell kuwa kama malaika ambaye alishushwa kwa ajili ya kuufurahisha moyo wake. Katika kila kitu ambacho Bwana Maxwell alikuwa akimwambia mahali hapo alikuwa akikubaliana nae, ofa ya pombe kali ambazo alikuwa amemnunulia zilionekana kulegeza kila kitu.
Baada ya saa moja Bwana Maxwell na Jocelyn wakaaga na kuondoka mahali hapo na Mendez nae kuelekea nyumbani kwake huku akiwa na chupa za pombe zile mikononi mwake. Bwana Maxwell na mke wakaona kwamba tayari walikuwa wamemaliza kila kitu ambacho kilitakiwa kumalizwa kwa mikono yao na kilichokuwa kikifuatia ni utekelezaji wa vitu vidogo tu.
Usiku huo huo Bwana Maxwell hakutaka kuelekea hotelini. Alijiona kuhitaji kitu kimoja kwa wakati huo, alikuwa akihitaji chombo kidogo ambacho hufungwa mbele ya bunduki kwa ajili ya kuzuia mlio wa risasi usiweze kusikika hata kwa mtu ambaye alikuwa karibu na mpigaji. Hicho ndicho ambacho alikuwa akikihitaji mahali hapo.
Alichokifanya mara baada ya kuelekea hotelini, akamuacha mke wake na kisha kuanza kuzunguka sehemu zote ambazo zilikuwa zikihusika na uuzaji wa vifaa vya bunduki kimagendo. Wala hakupotea, kwa sababu alikuwa mwenyeji hapo Monterrey, alikwenda moja kwa moja mpaka sehemu hizo.
“Hicho kifaa huwa ni dola hamsini. Unazo?” Jamaa mmoja alimuuliza Bwana Maxwell, tayari ilikuwa saa tano usiku. Bwana Maxwell akaingiza mkono mfukoni na kutoa kiasi hicho cha fedha na kumgawia.
“Poa. Nisubiri” Jamaa yule alimwambia Maxwell na kisha kuanza kuelekea ndani ambapo baada ya dakika kadhaa akarudi akiwa na chombo kile na kisha kumkabidhi.
Bwana Maxwell hakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, akaondoka zake na kurudi hotelini. Usiku kucha alikuwa akipanga mipango na mke wake juu ya namna gani ambapo wangefanikisha kuondoka mahali hapo bila kugundulika na mtu yeyote yule. Mipango yote ikapangwa usiku huo na kisha kulala.
Saa moja asubuhi walikuwa macho, mpaka simu ya Mendez ilipokuwa ikiingia walikuwa wamekwishaamka tayari kwa kujiandaa na safari. Alichokifanya Bwana Maxwell na Jocelyn ni kutoka nje na moja kwa moja kuondoka kuelekea katika baa ya Laspinho ambapo huko wakakutana na Mendez na kisha kuanza kuelekea nyumbani kwa mzee sanchez.
“Sasa huyu mwanamke itabidi atusubiri, anaweza kuunguza picha” Mendez alimwambia Bwana Maxwell, Jocelyn akatakiwa kushuka garini.
“Alikupigia simu?” Bwana Maxwell alimuuliza mara baada ya Jocelyn kuteremka kutoka garini.
“Bado ila kama una uhakika maiti ipo, hakuna noma”
Walipolifikia geti, Mendez akapiga honi na geti kufunguliwa. Walinzi walikuwa wakimwangalia Mendez ambaye alimtambulisha Bwana Maxwell kama msaidizi wake mpya na kisha kuruhusiwa kuingia ndani ya jengo hilo, walipofika sebuleni, akaanza kumpigia simu mzee Sanchez.
“Kuna nini” Sauti ya mzee Sanchez iliuliza kwa hasira.
“Nimekuja kuchukua mzigo mzee” Mendez alimwambia mzee Sanchez
“Kuchukua mzigo? Nani alikwambia kwamba kuna mzigo leo?” Sauti ya mzee Sanchez iliuliza.
“Nilipigiwa simu”
“Na nani?”
“Na Zhikov”
“Sawa. Njoo kwanza uuchukue huu mzigo mmoja na kisha baadae uurudie huu pale ambapo Zhikov atakuwa amekamilisha kila kitu” Mzee Sanchez alimwambia Mendez.
“Sawa mkuu”
“Umefika wapi kwa sasa?”
“Nipo sebuleni”
“Basi njoo” Mzee Sanchez alimwambia Mendez.
Mendez akainuka kutoka kwenye makochi ya kifahari pamoja na Bwana Maxwell na kisha kuelekea ndani ya chumba kile kilichokuwa ardhini. Walipofika huko, Mendez akaufungua mlango na kuingia huku Bwana Maxwell akiwa nyuma yake, kitendo cha mzee Sanchez kumuona Bwana Maxwell, akaonekana kushtuka.
“Huyu ni nani?” Mzee Sanchez aliuliza huku akionekana kumshangaa Bwana Maxwell.
“Huyu ni mwenzangu, nimemwambia leo aje kunisaidia bosi” Mendez alimwambia mzee Sanchez maneno ambayo yalionekana kutokumuingia akilini.
“Aje kukusaidia?” Mzee Sanchez aliuliza kwa mshangao.
“Ndio bosi”
“Basi ichukue na maiti yake ukaizike, hii ni kazi yako na sitaki mtu mwingine ajue” Mzee Maxwell alisema huku akiupeleka mkono wake kiunoni kwa ajili ya kuchukua bunduki yake.
Kwa haraka sana hata bila kuchelewa, Bwana Maxwell akaupeleka mkono wake kiunoni na kisha kutoa bunduki ambayo ilikuwa na chombo cha kuzuia mlio wa risasi. Kitu cha kwanza alichokifanya ni kumyooshea bunduki ile mzee Sanchez na kumuamuru kuiacha bunduki yake. Mzee Sanchez akaonekana kushtuka, akapigwa na butwaa, hakuamini kile kilichokuwa kikiendelea mahali pale.
“Wote wawili ufuateni ukuta na muuangalie, atakayegeuka roho yake halali yangu” Bwana Maxwell aliwaambia.
Kwa haraka bila kupoteza muda, mzee Sanchez na Mendez wakaufuata ukuta na kuanza kuuangalia, Bwana Maxwell akachukua bunduki ya mzee Sanchez na kisha kuwa nayo. Hapo ndipo akapata nafasi ya kumwangalia Alan ambaye alikuwa chini akilia. Bwana Maxwell akaonekana kuumia sana, hakuamini kama Alan yule ambaye alikuwa amekuja nae nchini Mexico alikuwa vile.
“Alan, tuondoke” Bwana Maxwell alimwambia Alan huku akimuinua. Alan akasimama na kisha kuanza kuuangalia mwili wa baba yake.
“Tuondoke”
“Hapana, siwezi kuondoka mpaka tuondoke na mwili huu” Alan alimwambia Bwana Maxwell.
“Mwili wa nani huu?” Bwana Maxwell aliuliza.
“Baba yangu”
“Baba yako?”
“Ndio”
“Imekuwaje tena?”
“Mzee Sanchez alimuua. Ni lazima nilipize kisasi” Alan alimwambia Bwana Maxwell.
Alan hakutaka kuchelewa, alichokifanya ni kuchukua bunduki ya Bwana Maxwell, huku mzee Sanchez akiwa ameugeukia ukuta, risasi tatu mfululizo zikapenya kisogoni mwake, damu zikarukia ukutani, kichwa kikafumuka na kuanguka chini kama mzigo, muda huo wote, Mendez alikuwa akitetemeka.
“Imeniuma…imeniuma sana” Alan alimwambia Bwana Maxwell.
“Tuondoke”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ngoja niubebe mwili wa baba yangu” Alan alimwambia Bwana Maxwell.
“Haiwezekani. Acha huyu aubebe” Bwana Maxwell alimwambia Alan na kisha kumwambia Mendez aubebe.
“Sikiliza, ukionyesha hofu yoyote tutakapotoka nje, nitakuua. Wewe ubebe mwili huu na moja kwa moja ukauingize ndani ya gari, tofauti na hapo, nitakuua” Bwana Maxwell alimwambia Mendez ambaye akaonekana kutii.
Hapo ndipo walipoanza kutoka nje. Mendez akawa ameubeba mwili wa Bwana Kurt na kisha kutoka nje. Walinzi wala hawakuonekana kushangaa, hiyo ndio ilikuwa kazi ya Mendez aliyokuwa akiifanya kila alipokuwa akija mahali hapo. Bwana Maxwell alikuwa amemshika Alan begani huku bunduki yake akiwa ameirudisha kiunoni kitu ambacho walinzi wale wala hawakuiona. Walipolifikia gari lao, mwili wa Bwana Kurt ukaingizwa ndani ya buti la gari na kisha wote watatu kuingia na kuondoka mahali hapo huku walinzi wakiwa hawafahamu kama bosi wao alikuwa ameuawa ndani ya chumba cha mauaji.
“Tuondoke” Bwana Maxwell alimwambia mke wake, Jocelyn walipofika alipokuwa, akaingia garini.
“Imekuwaje?” Jocelyn aliuliza.
“Tutaongea mbele ya safari” Bwana Maxwell alimwambia mke wake.
“Tunaelekea wapi sasa hivi?” Mendez aliuliza huku akionekana kutetemeka.
“Hospitali” Bwana Maxwell alijibu.
“Hospitali gani?”
“Christus Muguerza” Bwana Maxwell alisema na kisha safari kuelekea katika hospitali hiyo iliyokuwa katikati ya jiji la Monterrey kuanza huku katika kipindi chote hicho Alan akiwa analia kama mtoto.
Zhikov na Andrei walikuwa ni vijana wawili ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kufanya kila kitu ambacho kiliamuriwa kufanywa na mzee Sanchez. Hawa walikuwa vijana wawili ambao walitolewa nchini Urusi na kuletwa nchini Mexico kwa ajili ya kufanya kazi ambayo mzee Sanchez alikuwa akiitaka kufanyika. Miili yao ilikuwa mikubwa iliyojawa na misuli mingi, huku kwa kuwatazama tu walionekana kuwa watu tofauti.
Zhikov na Andrei walikuwa watu wenye roho mbaya. Hawa walitoka katika jeshi la Urusi ambapo walitoroka na moja kwa moja kuja nchini Mexico kwa ajili ya kufanya kazi chini ya mzee Sanchez kwa malipo makubwa. Roho zao mbaya ndizo ambazo ziliwafanya kutokumuonea huruma hata mtu mmoja ambaye alikorofishana na bosi wao, mzee Sanchez. Kila walipokuwa wakiambiwa muueni huyu, walifanya hivyo hivyo tena kwa mateso makali.
Mzee Sanchez akawa karibu na vijana wake hawa wawili ambapo kila alipokuwa akienda nao walikuwa pembeni yake. Walikuwa wakifika nyumbani kwake saa tatu ambapo wanamsubiri mzee huyo aamke na kisha mishemishe kuanza na kurudi katika nyumba ambayo alikuwa amewajengea katika mtaa wa pili kutoka hapo Espanoza.
Siku hii Zhikov na Andrei walikuwa wamefika nyumbani hapo kama kawaida yao, saa tatu kamili tayari walikuwa wakipiga hatua kuelekea sebuleni ambapo wakafungua mlango na kisha kuingia. Hakukuwa na mtu na kwa sababu vijana hawa walikuwa wenyeji, wakalifuata kochi na kisha kutulia kama kawaida yao huku wakimsubiria mzee Sanchez afike sebuleni hapo na kuwaambia ni kipi ambacho kilitakiwa kufanyika siku hiyo.
Kama kawaida yao wakaanza kusubiri sebuleni pale juu ya makochi, walisubiri zaidi na zaidi lakini mzee Sanchez hakuweza kutokea sebuleni pale. Ile haikuonekana kuwa kawaida ya mzee huyo, kila walipokuwa wakifika ndani ya sebule ile, mzee Sanchez huchukua dakika kumi na kisha kufika sebuleni pale na kuwagawia majukumu yao.
Leo hali ilionekana kuwa tofauti kabisa, walikuwa wamefika na walikaa sebuleni kwa muda wa saa moja lakini mzee Sanchez hakuweza kutokea sebuleni pale. Hiyo ikawatia wasiwasi lakini wakajipa moyo kwamba hakukuwa na kitu chochote kile kilichotokea. Muda ulizidi kwenda, baada ya saa moja kukaa sebuleni pale, nusu saa nayo ikapita mpaka dakika arobaini na tano lakini hali ilikuwa vile vile, mzee Sanchez hakutokea sebuleni pale zaidi ya wafanyakazi wa ndani ambao walikuwa wakija kwa zamu sebuleni.
“Mbona amechelewa sana leo? Hayupo nini?” Andrei alimuuliza Zhikov.
“Sijajua kwa sababu gani. Au tuulize?”
“Tutamuuliza nani na wakati mke wake pamoja na mtoto wake wapo ndani?” Andrei alimuuliza Zhikov.
“Hata wafanyakazi”
Hapo ndipo wakaanza kuwauliza wafanyakazi kama mzee Sanchez alikuwa ametoka au la. Kila mfanyakazi ambaye walimuuliza alisema kwamba hakumuona siku hiyo. Kumpigia simu kila mmoja alikuwa akihofia kufanya hivyo kwani mzee Sanchez hakuwa akipenda kupigiwa simu hasa nyakazi za asubuhi kwa sababu wakati mwingine huchelewa kuamka kutokana na uchovu wa usiku uliopita.
Walichokiamua ni kuondoka sebuleni pale na kisha kutoka nje. Wakaanza kuwauliza walinzi kama walimuona mzee Sanchez asubuhi hiyo lakini hakukuwa na mlinzi yeyote yule aliyesema kwamba alimuona, kila mmoja alikataa. Mpaka kufikia hatua hiyo wakaona hakuna jinsi, ilikuwa ni lazima waingie tena ndani na kisha kuelekea katika mlango wa chumba cha mzee Sanchez na kisha kupiga hodi ili waweze kupata uhakika zaidi kama mzee huyo alikuwepo chumbani kwake au la.
Hivyo ndivyo walivyofanya, wakaelekea sebuleni na kisha kupitiliza mpaka ukumbini na kwenda moja kwa moja katika mlango wa chumba alichokuwa akilala mzee Sanchez na mke wake na kisha kuanza kupiga hodi. Sauti ya Bi Shakira ikasikika ikiwaambia kwamba angefika mahali pale na hivyo kusikiliza shida za mgongaji wa mlango ule, wala hazikupita sekunde nyingi, Bi Shakira akaufungua mlango ule na macho yake kukutana na macho ya vijana wale.
“Mbona mzee leo amechelewa sana kuamka? Mwambie tumekwishafika” Zhikov alimwambia Bi Shakira.
“Mmmh! Mbona alitoka chumbani kitambo! Tena leo amewahi kuamka sana” Bi Shakira aliwaambia.
“Amewahi kuamka?”
“Ndio”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ndani hayupo?”
“Hayupo”
“Basi anaweza kuwa kule ardhini” Zhikov alimwambia Andrei.
Hapo hapo wakaanza kupig hatua kuelekea katika kile chumba cha mateso kilichokuwa ardhini. Hakukuwa na mtu yeyote yule ambaye alionekana kuwa na hofu moyoni, kila mmoja alijua fika kwamba ilikuwa ni lazima mzee huyo awe ndani ya chumba hicho kwani asubuhi hiyo walitakiwa kufanya kazi moja tu, kumuua Alan na kisha kusikilizia kipi kifanyike baada ya hapo.
Walipoufikia mlango wa chumba kile kilichokuwa ardhini, wakakishika kitasa na kisha kuanza kuufungua. Mlango ulikuwa umefungwa na ufunguo. Hapo ndipo wakaanza kuwa na wasiwasi, hawakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea mpaka muda huo. Zhikov akachukua simu yake na kisha kuanza kuitafuta namba ya simu ya mzee Sanchez na kisha kuipiga.
Mlio wa simu ukaanza kusikika kutoka ndani ya chumba kile, kila mmoja akaonekana kushtuka, mzee Sanchez alikuwa ndani ya chumba kile lakini cha kushangaza zaidi mlango ulikuwa umefungwa kwa ufunguo. Hawakutaka kuishia hapo, wakazidi kuugonga mlango wa chumba kile ili mzee Sanchez awafungulie mlango lakini hali ilikuwa kimya kabisa.
Hapo ndipo walipokubaliana kitu kimoja kwamba ilikuwa ni lazima wauvunje mlango wa chumba kile. Kazi ya kuuvunja mlango ule ikaanza na baada ya dakika moja tu, mlango ule ukafunguka na kisha kuingia ndani. Walichokikuta ndani ya chumba kile hawakuamini, mzee Sanchez alikuwa chini, damu zilizoanza kuganda sakafuni zilikuwa zimetapakaa chumbani mule, si Alan wala mwili wa baba yake, Bwana Kurt ambao ulikuwa ukionekana ndani ya chumba kile.
Huku wakionekana kuchanganyikiwa, Andrei akachomoka ndani ya chumba kile na moja kwa moja kupanda juu. Breki yake ya kwanza ilikuwa nje ya chumba cha mzee Sanchez na kisha kuanza kupiga hodi huku akionekana kuwa mwenye haraka, mlango ulipofunguliwa, Andrei alionekana kuwa na wasiwasi mwingi usoni.
“Kuna nini?” Bi Shakira aliuliza huku nae akianza kuonekana kuwa na wasiwasi.
“Twende chini” Andrei alimwambia Bi Shakira.
“Kuna nini?”
“Twende chini” Zhikov alimsisitizia.
Tayari hali ilionekana kubadilika kwa wakati huo, Bi Shakira hakutakiwa kupuuzia kitu chochote kile, akaanza kushuka ardhini pamoja na Andrei mpaka ndani ya chumba kile. Kile alichokiona, kwanza mwili wake ukapigwa na ganzi, hakuamini kama mwili ambao ulikuwa pale chini ulikuwa ni mwili wa mume wake kipenzi, mzee Sanchez.
Kilio kikaanza kusikika kutoka kwa Bi Shakira huku akianza kumtikisa mume wake kwa kudhani kwamba alikuwa amelala na angeweza kuamka tena. Sauti ile ya kilio ambayo ilikuwa ikisikika ndio ambayo iliwafanya wafanyakazi kuanza kuusogelea mlango wa kuingilia ardhini ili kujua kulikuwa na kitu gani kilichokuwa kikiendelea.
“Kuna nini?” Antonio wauliza wafanyakazi ambao walikuwa wamesimama katika mlango wa kuingilia ardhini.
“Hatujui. Tunasikia tu mama akilia” Msichana mmoja alimjibu Antonio.
Antonio hakutaka kubaki hapo, akaingia mpaka ardhini na kisha kuanza kuelekea katika chumba kile. Alichokiona hakutaka kukiamini, mwili wa baba yake ulikuwa chini, kichwa kilikuwa kimefumuliwa na risasi na ni damu tu ndizo ambazo zilikuwa zimetapakaa ardhini.
“Alan….!” Antonio alisema kwa hasira, machozi yalikuwa yakimtoka.
“Unasemaje?” Zhikov alimuuliza Antonio.
“Alan amefanya haya” Antonio alimjibu Zhikov.
Tayari Antonio akaonekana kuchanganyikiwa, kwa haraka sana akatoka chumbani mule na kisha kuelekea chumbani mwake. Moyo wake ulikuwa kwenye presha kubwa huku mwili wake ukitetemeka kupita kawaida. Baridi lililokuwa likitoka katika viyoyozi ndani ya nyumba ile wala hakuihisi mwilini mwake, alichokuwa akikihisi ni joto tu tena huku kijasho chembamba kikianza kumtoka.
Alipofika chumbani, akachukua simu yake na kisha kuanza kutafuta namba za mtu fulani. Kila alipokuwa akiangalia namba hii, mkono wake ulikuwa ukitetemeka kwa hasira, alijiona akifanya kila kitu kwa taratibu sana na alitakiwa kufanya kila kitu kwa haraka mno. Alipoiona namba ya simu ya mtu ambaye alikuwa akitaka kumpigia, akaanza kupiga.
“Njoo nyumbani haraka. Njooni wote” Antonio aliongea na mtu wa upande wa pili na kisha kukata simu.
Antonio hakuonekana kuridhika, akaanza kupiga tena simu sehemu nyingine, simu ikaanza kuita, iliita mpaka simu kukatika. Antonio alionekana kuwa mwenye hasira kali, akaanza kupiga tena, wala simu haikuita muda mrefu, ikapokelewa na sauti nzito ya mwanaume kusikika simuni.
“Nikusaidie nini?” Sauti ya mwanaume upande wa pili iliuliza.
“Baba ameuawa” Antonio alimjibu mtu huyo.
“Unasemaje?”
“Baba ameuawa. Njoo nyumbani mara moja” Antonio alimwambia.
“Naongea na nani?”
“Njoo nyumbani, baba ameuawa” Antonio alisema kwa sauti ya juu yenye ukali.
“Wewe ni nani?”
“Antonio Sanchez”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nani ameuawa? Mzee Sanchez?”
“Ndio. Njoo nyumbani haraka” Antonio alimwambia mwanaume huyo na kisha kukata simu.
Antonio aliona akili kwa wakati huo kutokuwa yake, alionekana kuchanganyikiwa kupita kawaida, tukio la kuuawa kwa baba yake lilikuwa limemchanganya kupita kawaida. HApo ndipo alipoanza kumchukia Alan, alijua fika kwamba Alan ndiye ambaye alikuwa amemuua baba yake. Kisasi kizito kikaanza kujengeka moyoni mwake, alikuwa na hasira kupita kawaida.
Baada ya dakika kadhaa, magari mawili ya vijana walioonekana wahuni yakaingia ndani ya eneo la nyumba hiyo na kisha kuteremka. Kila mmoja alikuwa na sura isiyoonyesha matumaini yoyote yale maishani mwao, sura zilionekana kuchoka na maisha ambayo walikuwa wakiyaishi, vijana hao wote zaidi ya ishirini walikuwa na bunduki viuononi mwao.
Wakasimama ndani ya eneo la nyumba la mzee Sanchez na kisha kusubiria ni kitu gani ambacho walikuwa wameitiwa mahali hapo. Japokuwa jua lilikuwa likiwaka lakini hakukuwa na mtu ambaye aliondoka, baada ya dakika kumi, Antonio akatokea mahali hapo, uso wake ulikuwa umevimba kwa hasira kupita kawaida huku macho yake yakiwa mekundu.
“Ninamtaka mtu huyu akiwa mzima” Antonio aliwaambia vijana wake huku akiwapa picha ya Alan ambayo ilimuonyesha katika kipindi walichokuwa chuoni.
“Yupo wapi kwa sasa?”
“Sijui. Ila nadhani anaelekea Marekani kwa kutumia gari” Antonio aliwaambia.
“Akileta ubishi wa kufika mahali hapa?” Kijana yule aliuliza.
“Mnaweza kumuua na kuniletea maiti yake” Antonio aliwaambia na kisha kuondoka mahali hapo.
Huo ndio ulikuwa wakati ambao moyo wa Antonio ulikuwa katika maumivu makali, kitendo cha baba yake kuuawa kilimuumiza kupita kawaida. Jina la Alan ndio ambalo lilikuwa likijirudia kichwani mwake, alikuwa na hasira zilizopitiliza juu ya Alan. Kitendo cha kumuua baba yake kilimaanisha kwamba wasingeweza kukaa sehemu moja katika maisha yao na iwe isiwe ilikuwa ni lazima kutafutana hata kama itachukua maisha yao yote.
Baada ya dakika kadhaa, Antonio akaitwa sebuleni, mkuu wa polisi wa jijini Monterrey, Pablo alikuwa amekwishafika mahali hapo na kitu alichokuwa akitaka kukisikia ni nani alikuwa amemuua mzee Sanchez.
“Hebu niambie vizuri” Pablo alimwambia Antonio.
“Baba ameuawa” Antonio alijibu.
“Nani amemuua?”
“Rafiki yangu”
“Nani?”
“Anaitwa Alan”
“Ilikuwaje tena?”
“Alikuja nyumbani kunitembelea, leo asubuhi amempiga baba risasi ya kichwa, mwili wake upo ndani” Antonio alimwambia Palo.
“Mbona inachanganya sana”
“Elewa hivyo”
“Sawa. Kwa hiyo nifanye nini?” Pablo alimuuliza Antonio.
“Hilo ni swali la kijinga, hauujui wajibu wako?”
“Wajibu wangu naujua, ni kumtafuta muuaji, sasa nitamtafuta vipi na wakati simjui yupo vipi” Pablo alimwambia Antonio ambaye akainuka mahali hapo na kisha kuelekea chumbani na aliporudi alikuwa na picha ya Alan.
“Hakikisha anapatikana, nitakugawia dola laki moja kama zawadi” Antonio alimwambia Pablo.
“Hakuna tatizo. Nimtafute kisiri au?”
“Waambie na polisi wako. Ila wakiuliza sababu, waambie yoyote ile” Antonio alimwambia Pablo.
“Kwa nini nisiwaambie ukweli?”
“Wewe fanya hivyo. Mtu akuliza juu ya kifo cha baba yangu, mwambie amejiua” Antonio alimwambia Pablo.
“Mbona unanichanganya sasa?”
“Wewe sema kama nilivyokwambia”
“Sawa. Kwa hiyo niseme amejiua?”
“Ndio”
“Hakuna tatizo. Sasa huyu mtu naweza kumpata wapi?”
“Popote pale. Ila jua anataka kuvuka mpaka kuingia nchini kwao, Marekani” Antonio alimwambia Pablo.
“Basi hakuna tatizo”
“Hakikisha anapatikana akiwa hai, akileta ubishi, muue yeye na watu aliokuwa nao na kisha niletewe maiti yake” Antonio alimwambia Pablo.
“Hakuna tatizo. Kama anaondoka kuelekea Marekani, ndani ya masaa mawili atakuwa amepatikana. Ngoja niwasiliane na polisi wa mpakani wakamilishe kila kitu” Pablo alimwambia Antonio.
“Hakuna tatizo” Antonio alijibu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walichokuwa wakikitaka kwa wakati huo ni kwenda katika hospitali ya Christus Muguerza kwa ajili ya kuchukua dawa za kuifanya maiti ya Bwana Kurt isiweze kuharibika katika safari yao ya kuelekea nchini Marekani. Safari ya kwenda huko tayari ilikuwa ikiendelea huku muda wote Mendez akionekana kutetemeka kupita kawaida.
Hawakuchukua muda mrefu sana wakawa wamekwishafika katika hospitali hiyo ambapo moja kwa moja Bwana Maxwell na Mendez kuteremka na kisha kuanza kupiga hatua kuelekea ndani ya hospitali hiyo. Ukimya ulikuwa umetawala ndani ya eneo la hospitali hiyo, magari ya aina mbalimbali pamoja na magari ya wagonjwa yalikuwa yamepakiwa katika eneo la hospitali hiyo.
Wakaanza kupiga hatua kuelekea huko huku lengo lao likiwa ni kutaka kuongea na dokta yeyote ambaye angekuwa na uwezo wa kuwasaidia kile ambacho walitaka kusaidiwa wakati huo. Mendez alikuwa amekwishapigwa mkwara kwamba hakutakiwa kuonyesha hofu yoyote ile, alitakiwa kuwa kawaida kama alivyokuwa katika siku nyingine. Katika kipindi hicho chote, bunduki ya Bwana Maxwell ilikuwa kiunoni mwake, Mendez alilifahamu hilo.
“Tunahitaji dawa” Mendez alimwambia daktari mmoja ambaye alikuwa amevalia koti kubwa jeupe huku akiwa na mashine ya kusikilizia mapigo ya moyo shingoni mwake.
“Dawa gani?”
“Ya kuzuia maiti isiharibike kwa haraka” Bwana Maxwell alimwambia daktari yule.
Alichokifanya daktari yule ni kuwachukua na kisha kuanza kuelekea ndani ya ofisi yake pamoja naeo. Walipofika kule akawaambia wakae vitini na kisha kuanza kuwaangalia kwa zamu, alionekana kuwa na mshangao usoni.
“Mnahitaji dawa hiyo kwa matumizi gani?” Dokta yule aliwauliza.
“Kuhifadhia maiti kwa muda” Bwana Maxwell alimjibu dokta yule.
“Haiwezekani”
“Kwa nini?”
“Haturuhusiwi kutoa dawa nje ya hospitali, hasa dawa hizo” Dokta aliwaambia.
“Tunajua. Naruhusiwa kuongea nawe kiutu uzima?”
“Hilo ndio lililobakia. Nashangaa unataka nikupe kitu ila wewe kutoa” Dokta alimwambia Bwana Maxwell.
Hakukuwa na cha kujiuliza, kila mmoja alitaka kufanya kila kitu kwa haraka ili waweze kuondoka mahali hapo. Alichokifanya Bwana Maxwell ni kuingiza mkono mfukoni na kutoa noti za dola na kisha kumpa dola elfu tano. Hizo zikaonekana kuwa nyingi kwa dokta huyo, bila kuzihesabu, akaziweka mfukoni, akawaambia wasubiri, akatoka nje ya chumba kile kwa ajili ya kwenda kuchukua dawa hiyo.
“Kwa nini unafanya hivi?” Mendez aliuliza.
“Kuna siri kubwa sana. Sitaki kukujeruhi na wala sitaki upate tatizo lolote chini yangu. Tukitoka hapa, nitakuacha huru” Bwana Maxwell alimwambia Mendez.
“Ila kuna nini kinaendelea?”
“Kuhusiana na nini?”
“Mpaka kumuua bosi”
“Wewe unavyoona alikuwa mtu mzuri?”
“Kwa sababu huwa ananipa fedha za kuniweka mjini, alikuwa mzuri” Mendez alimwambia Bwana Maxwell.
“Hapana. Hakuwa mzuri hata kidogo. Ameua watu wengi sana na kukupa wewe maiti kwenda kuzizika, uongo?” Bwana Maxwell alisema na kisha kuuliza.
“Ni kweli”
“Sasa huyo kweli ni mtu mzuri?”
“Sidhani”
“Sio hudhani. Hakuwa mtu mzuri” Bwana Maxwell alimwambia Mendez.
Baada ya maongezi mafupi, dokta akarudi ofisini huku akiwa na dawa hiyo, akawaonyeshea namna ya kutumia na kisha kuwataka kuondoka na hawakutakiwa kumwambia mtu yeyote juu ya mahali ambapo walikuwa wameipata dawa ile kwani hakuwapa kwa njia ya halali. Hilo wala halikuwa tatizo, wakakubaliana nae na kisha kuondoka.
Wakarudi garini, wakaingia na kisha kuondoka mahali hapo. Walichikuwa wakikitaka kwa wakati huo ni kutafuta sehemu nzuri ambayo ingewafanya kuupulizia vizuri ule mwili hata kabla ya kuanza safari yao rasmi. Safari hiyo ikaishia katika barabara ndefu iliyokuwa ikielekea Monclova, Bwana Maxwell na Mendez wakateremka na kisha kufungua buti la gari, hapo ndipo walipoanza kuupulizia mwili wa Bwana Kurt dawa ile kwa ajili ya kuukinga uchukue muda mrefu kabla ya kuharibika.
“Nashukuru kwa kila kitu, nadhani unatakiwa kuishia hapa” Bwana Maxwell alimwambia Mendez.
“Hakuna tatizo”
“Kama utaitwa naomba usiwaambie kama tunaelekea nchini Marekani, hapa tunakwenda Nuevo Laredo, huo ndio mpaka tutakaoutumia kuingia nchini Marekani” Bwana Maxwell alimwambia Mendez.
“Hakuna tatizo” Mendez alimwambia Bwana Maxwell na kisha kuruhusiwa kuondoka.
Huo ndio ujanja ambao alikuwa ameutumia Bwana Mendez, alijua fika kwamba vijana wa mzee Sanchez ni lazima wangewatafuta na hata kuwatuma polisi zaidi katika mpaka wa kuingilia nchini Marekani kwa upande wa kusini, Nuevo Laredo, mpaka ambao walikuwa wameingilia ndani ya nchi hiyo. Alijua fika kwamba Mendez angetafutwa na kuelekeea kile ambacho kiliendelea baada ya kutoka ndani ya nyumba ile na kama angemwambia ukweli kila kitu basi hilo lingeonekana kuwa tatizo kwao.
Alimwambia kwamba walikuwa safarini kuingia nchini Marekani kwa kupitia mpaka wa Nuevo Laredo lakini ukweli ni kwamba wakati huo hawakutaka kuingia ndani nchini Marekani kupitia mpaka huo wa Nuevo Laredo na kutokea Texas bali walikuwa wakitaka kuvuka kwa kutumia mpaka wa Piedras Negras na kuingia katika jimbo kubwa la New Mexico nchini Marekani.
*****CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hasira zilikuwa zimemkaba kooni, kitendo cha kuona baba yake ameuawa kilionekana kumtia hasira kupita kawaida. Chuki yake kubwa ilikuwa juu ya Alan, kitendo cha baba yake kuuawa ndani ya chumba kile cha mateso kilimhuzunisha sana. Alijua fika kwamba baba yake, mzee Sanchez alikuwa amemuua Bwana Kurt lakini hakuona kama hiyo ilikuwa sababu ya kumfanya Alan kumuua baba yake.
Baada ya mwili wa baba yake kuchukuliwa na kupelekwa hospitalini, Alan akawafuata walinzi na kuanza kuongea nao. Kitu ambacho alikuwa akikifahamu ni kwamba walinzi walikuwa wakifahamu kila kitu kuhusu mtu ambaye alikuwa ameingia ndani ya nyumba yao mpaka kutoka, alitaka kufahamu ni kitu gani ambacho kilitokea mpaka Alan kuondoka ndani ya nyumba hiyo.
“Nani alikuja kumchukua Alan?” Antonio aliwauliza walinzi huku akionekana kuwa na hasira.
“Mendez alikuja na mtu mmoja ambaye wala hatukuwa hatumfahamu, alisema kwamba alikuwa msaidizi wake, hatukuwa na hofu, tukawaruhusu kuingia ndani” Mlinzi mmoja alimjibu Antonio.
“Baada ya hapo?”
“Wakatoka ndani ya dakika kadhaa huku wakiwa na huyo kijana ambaye alikuwa ametekwa huku mwili wa baba yake ukibebwa na Mendez” Mlinzi yule alimwambia Antonio.
“Baada ya hapo?”
“Tukawaruhusu kuondoka”
“Yaani mliwaruhusu bila ya kuwauliza chochote kile?” Antonio aliuliza kwa mshangao.
“Hatukuwauliza”
“Kwa nini?”
“Kwa sababu tulijua mzee ameruhusu kila kitu” Mlinzi alimwambia Antonio.
“Hata kama, ilitakiwa muulize kila kitu kwani haikuwa hali ya kawaida” Antonio aliwaambia walinzi.
Antonio hakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuondoka huku akiacha maagizo kwamba ndani ya nusu saa Mendez alitakiwa kuwa ndani ya nyumba hiyo. Hiyo ilikuwa ni amri ambayo ilitakiwa kufuatwa kwa wakati huo. Walinzi watatu wakaondoka mahali hapo na gari lao na safari ya kuelekea sehemu alipokuwa akiishi Mendez kuanza.
Kila mmoja ndani ya gari alikuwa na bunduki yake mkononi, kitendo cha kwenda kumchukua Mendez na kumleta ndani ya nyumba hiyo wala halikuwa tatizo lolote lile. Mendez alikuwa akihitajika kwa ajili ya kutoa maelezo yote kuhusiana na mahali ambapo Alan pamoja na hao wenzake walipokuwa.
Ndani ya dakika kumi wakafika katika nyumba ya Mendez na kisha kumchukua na kuanza kurudi nyumbani kwa mzee Sanchez. Muda wote huo Sanchez alikuwa akitetemeka wa hofu, kitendo cha kuziona bunduki zikiwa mikononi mwa watu wale kikamfanya kukosa amani kabisa, muda wowote ule alikuwa akihisi kwamba alikuwa akienda kuuawa.
Baada ya kufika ndani ya nyumba hiyo, akateremshwa na kisha kuanza kupelekwa ndani. Mwili wake ulikuwa ukitetemeka, hakuwa akiamini kama kwa wakati huo alikuwa amebakisha kipindi kichache cha kuvuta pumzi ya dunia hii. Moja kwa moja akafikishwa mbele ya Antonio, bado alionekana kuwa na wasiwasi.
“Nataka uniambie ukweli” Antonio alimwambia Mendez ambaye alikuwa akitetemeka tu.
“Ndio bosi”
“Alan yupo wapi?”
“Aliondoka”
“Na nani?”
“Na mtu mmoja ambaye wala sikuwa nikimfahamu” Mendez alimjibu Antonio.
“Kwa hiyo haukuwa ukimfahamu?”
“Ndio bosi”
“Sasa kwa nini ulimruhusu kuingia ndani ya nyumba hii?” Antonio alimuuliza Mendez ambaye alizidi kutetemeka zaidi.
“Aliniambia kwamba anahitaji maiti” Mendez alijibu.
“Alikuwa akihitaji maiti?”
“Ndio”
“Sasa ilikuwaje mpaka kukufuata wewe?”
“Aliniambia kwamba alipata taarifa kwamba kulikuwa na maiti ndani ya nyumba hii” Mendez alijibu.
“Nani alimpa taarifa?”
“Sijui ni nani”
“Sawa. Uliondoka nao hapa, mlielekea wapi?” Antonio alimuuliza Mendez.
“Tulikwenda hospitalini, nikamsindikiza huyo mtu mwingine kwenda ndani ya hospitali hiyo ambapo akanunua dawa ya kuuzuia mwili kuoza” Mendez alimjibu.
“Ilikuwaje ufanye mambo yote hayo pamoja nao?” Antonio alimuuliza.
“Nilikuwa chini ya ulinzi mkubwa, alikuwa na bunduki mkononi, aliniambia nifuatishe alichokuwa akikitaka la sivyo angeniua” Mendez alimwambia Antonio.
“Baada ya kutoka hospitali mlielekea wapi?”
“Waliniambia nirudi nyumbani na wao kuondoka”
“Hawakukwambia wanaelekea wapi?”
“Walisema wanakwenda Marekani na wangepitia katika mpaka wa Nuevo Laredo” Mendez alijibu.
Antonio akaonekana kuridhika, hapo akawa na uhakika kwamba wabaya wake walikuwa wameianza safari ya kuelekea nchini Marekani kwa kuvukia katika mpaka wa Nuevo Laredo. Kwa haraka sana akawapigia simu vijana wake na kuwaambia kwamba waongeze kasi kuelekea Nuevo Laredo. Hakuridhika, kitu ambacho alikuwa akikihitaji ni kuwaona watu hao wakikamatwa na kufikishwa katika mikono yake. Akampigia simu mkuu wa polisi, Pablo na kumwambia kwamba watu hao walikuwa njiani kuelekea Nuevo Laredo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nimekwishapiga simu huko, hakuna tatizo, vijana watafanya kazi ya ziada mpaka wakamatwe” Pablo alimwambia Antonio.
“Na kuna kingine”
“Kipi?”
“Nataka pia polisi wa mpaka wa Piedras Negras. Muwazuie wasivuke mipaka hiyo miwili” Antonio alimwambia Pablo.
“Hakuna tatizo, kuhusu mpaka wa Piedras Negras, ngoja niwaambie vijana wawe makini” Pablo alimwambia Antonio.
“Hakuna tatizo. Ninachokitaka ni watu hawa kukamatwa tu. Hakikisha unazisambaza picha za huyu mtu kwa polisi wengine” Antonio alimwambia Pablo.
“Hakuna tatizo” Pablo alijibu na kisha kukata simu.
“Nitaua mtu. Nitamuu tu hata kama itachukua muda gani, nitamuua tu na hata kama kuteketeza kizazi chake chote, NITAMUUA TU” Antonio alisema kwa hasira, alionekana kuchanganyikiwa.
Antonio hakutaka kuzungumza ukweli, taarifa ambazo alikuwa akizifikisha kwa watu wengine zilisema kwamba mzee Sanchez alikuwa amejiua kwa kujipiga risasi chumbani kwake. Ni watu wachache sana ambao alikuwa amewaambia kwamba Alan ndiye ambaye alikuwa amempiga risasi mzee Sanchez na kumuua. Antonio alikuwa akiangalia mambo mengi ya mbele, kama angesema ukweli kwamba Alan ndiye ambaye alimuua baba yake basi mwisho wa siku Alan angekamatwa na kisha kupelekwa mahakamani ambapo huko angezungumza ukweli, ukweli ambao hata yeye Antonio ungeweza kumtia katika matatizo.
Alikuwa ameongea na Pablo na kumwambia kwamba Alan ndiye alikuwa amehusika lakini hakutaka Pablo awaambie polisi wengine. Kila kitu kilitakiwa kufanyika kimya kimya na hata kama Alan angekamatwa basi angeweza kumuua kama kulipiza kisasi kwa kile ambacho alikuwa amekifanya kwa baba yake.
Antonio alionekana kuwa mwenye mawazo mengi, kila wakati alikuwa karibu na simu yake kwa ajili ya kusikia ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea, kama Alan alikuwa amekamatwa au la. Katika dakika chache za nyuma Mendez alikuwa amemwambia kwamba Alan pamoja na mtu ambaye alimtorosha walikuwa wakielekea nchini Marekani kwa kupita katika mpaka wa Nuevo Laredo na kuingia ndani ya jimbo la Texas. Moyoni aliyaamini maneno yale lakini bado alijiona kuwa na sababu nyingine zaidi ya kufanya kitu kingine, kumwambia Pablo kwamba alitakiwa kuwataarifu hata polisi walio katika mpaka wa Piedras Negras kwa ajili ya kuimarisha ulinzi katika mpaka huo.
Picha za Alan zilikuwa zimekwishasambazwa kwa watu wote ambao walitakiwa kuwa nazo. Polisi mipakani wakawa wamekwishazipata picha za Alan kwani walikuwa wametumiwa kwa kupitia email na kisha wao kuzichapisha na kuwa na picha hizo mikononi mwao. Mipakani ulinzi ukawa umekamilika na ni Alan tu ndiye ambaye alikuwa akisubiriwa na kisha kukamatwa na kurudishwa Monterrey.
“Mmefikia wapi?” Pablo aliwauliza polisi wake simuni.
“Hapa tupo kwenye mwendo wa kasi kuelekea Laredo” Sauti ya polisi mmoja ilisikika simuni.
“Hamjafanikiwa kukutana nao hata njiani?”
“Hapana mkuu.”
“Mmejaribu kuwa makini njiani?”
“Ndio mkuu lakini hatujafanikiwa. Tunakutana na magari machache ambapo humo kote watu hao hawapo” Sauti ya polisi yule ilisikika.
“Sawa. Kuweni makini sana”
“Hakuna tatizo”
Pablo hakutulia ofisini kwake, kila wakati alikuwa akijaribu kupiga simu huku na kule na kuwasikilizia polisi wake kama walikuwa wamekwishafanikisha kumkamata mtu ambaye alikuwa akimhitaji. Kwa kila polisi ambaye alikuwa akimpigia simu, jibu lilikuwa ni lile lile, Alan hakuwa ameonekana machoni mwao na bado walikuwa wakiendelea na safari ya kuelekea mipakani.
“Nadhani leo hawatofanikiwa kuvuka mpakani” Pablo alimwambia Antonio simuni.
“Kwa nini?”
“Ni mbali sana. Watahitaji kulala njiani, hata kama gari lako linakimbia kama magari ya Formula 1, bado itakupasa ulale njiani kwani ni mbali mno na pia barabara ina kona nyingi” Pablo alimwambia Alan.
“Kwa hiyo unavyohisi watalala njiani?”
“Pamoja na kuhisi hivyo, huo ndio ukweli”
“Sawa. Hakikisha mpaka usiku unaingia polisi wako wawe wamefanya kazi kwa asilimia fulani kabla ya kuendelea kesho” Antonio alimwambia Pablo.
“Hakuna tatizo”
****
Baada ya kutoka katika hospitali ya Christus Muguerza, moja kwa moja safari yao ikaanza upya. Bwana Maxwell akashikilia usukani na kuanza kuendesha gari hilo. Mwendo ambao alikuwa akiutumia kwa wakati huo ulikuwa ni wa kasi sana kwani alitaka wafike mpakani mapema japokuwa alijua fika kwamba ilikuwa ni lazima kulala njiani.
Suala la kulala wala halikuonekana kuwa ni tatizo japokuwa ndani ya gari hilo kulikuwa na maiti ya Bwana Kurt. Walikuwa wamekwishaipulizia kiasi kikubwa cha dawa na hivyo isingeweza kuharibika kwa haraka na kutoa harufu mbaya. Alilifahamu hilo lakini hakuona kama kulikuwa na sababu ya kupoteza muda njiani, walitakiwa wafanye haraka hata kabla watu hawajagundua kile kilichokuwa kimetokea ndani ya nyumba ya mzee Sanchez.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati huo Alan hakuwa akilia lakini muda mwingi alionekana kuwa mpole huku akionekana kuwa na mawazo mengi. Hakuzungumza kitu chochote kile, mawazo yake yalikuwa kwa baba yake ambaye aliuawa kikatili na mzee Sanchez. Alimpenda sana baba yake na hakutaka kuona akifariki hata kabla ya kuhudhuria harusi yake ambayo angefunga siku si nyingi kuanzia siku hiyo. Alitamani kumuona baba yake akiwa pamoja nae kanisani huku akishuhudia jinsi harusi hiyo ilivyokuwa ikifana, harusi ambayo ingemuingiza katika ndoa na msichana Albertina.
Mategemeo yake yalikuwa yamebadilika, baba yake alikuwa ameuawa na hivyo asingeweza kuhudhuria harusi hiyo tena. Hilo likamuumiza sana Alan na kujiona kuwa miongoni mwa watu waliokuwa na bahati mbaya katika maisha yake japokuwa alikuwa amezaliwa katika familia iliyokuwa na fedha nyingi.
Ukimya uliendelea kutawala ndani ya gari, ilipofika saa saba na nusu mchana, wakafika katika sehemu iliyoitwa Bustamante, sehemu ambayo zamani ilikuwa ikitumika sana kwa mchezo wa ng’ombe vichaa, mchezo ambao ulikuwa maarufu sana nchini Mexico. Walionekana kuchoka na pia walihitaji kula hata kabla ya kuendelea na safari yao. Kwa sababu Bwana Maxwell na Alan walikuwa wenye wasiwasi mwingi, wakamtuma Jocelyn supermarket kwa ajili ya kuwanunulia chakula.
“Vipi?” Alan alimuuliza Bwana Maxwell mara baada ya kuona akimwangalia sana.
“Unahitaji chakula gani?”
“Sijisikii kula”
“Hapana Alan. Tuna safari ndefu sana, ni lazima tule na kuendelea na safari” Bwana Maxwell alimwambia Alan.
“Sijisikii kula”
“Tuna safari ndefu mno, ni lazima ule la sivyo utaweza kupata tatizo huku mbele” Bwana Maxwell alimwambia Alan.
Alichokifanya ni kutoa fedha mfukoni na kisha kumgawia Jocelyn na kumwambia alete vyakula mbalimbali ila sandwich kilikuwa muhimu zaidi. Jocelyn akateremka kutoka garini na kisha kuanza kuelekea katika supermarket ile, baada ya dakika chache, akarudi garini huku akionekana kuwa katika hali ya mshangao.
“Kuna nini?” Bwana Maxwell alimuuliza Jocelyn.
“Nimeona kwenye televisheni wanatangaza habari juu ya kifo cha Sanchez” Jocelyn alijibu.
“Sasa hicho ndicho cha kushangaza?”
“Hapana. Ila wanasema amejiua”
“Wanasema amejiua?”
“Ndio”
“Kuna kitu hapo”
“Kitu gani?” Alan akaingilia kwa kuuliza swali baada ya kukaa kimya katika kipindi chote hicho.
“Bado sijajua. Antonio anajua dhahiri kwamba wewe ndiye umemuua baba yake, inakuwaje polisi watangaze kwamba mzee huyo alijiua? Hauoni kama kuna kitu hapo?” Bwana Maxwell alimwambia Alan na kisha kumuuliza.
“Nafikiri”
“Hatutakiwi kujali. Cha msingi tuombe Mungu tufike salama” Bwana Maxwell alimwambia Alan.
Hawakutaka kupoteza muda hapo Bustamante, walichokifanya ni kula haraka haraka na dakika kumi zilipokwisha wakaendelea na safari yao. Hapo kila mmoja akaonekana kuwa na nguvu kwani miili yao ilionekana kuleta nguvu ambayo ilikuwa imetoweka katika kirefu kilichopita. Japokuwa kila mmoja alionekana kuwa na amani lakini bado kuna swali moja tu ndio ambalo lilikuwa likijirudia vichwani mwao kwamba ni kwa namna gani wangeweza kuvuka mpakani.
Hilo likawa swali ambalo lilikosa majibu kabisa. Uwezo wao wa kufikiria ukaonekana kufikia tamati kwani kama kutumia fedha walikuwa wamekwishatumia katika kipindi kilichopita na kwa wakati huo walitakiwa kutumia mbinu nyingine zaidi. Hawakupata jibu la swali hilo, walichokifanya ni kuendelea na safari kwa kuamini kwamba jibu lingepatikana mara baada ya kufika mpakani.
“Zimebaki kilomita mia nne kabla ya kuingia mpakani na sasa hivi ni saa kumi jioni.Haina budi kulala tukifika Anahuac” Bwana Maxwell aliwaambia.
“Hakuna tatizo” Jocelyn alijibu.
Safari ilikuwa ni ndefu na yenye kuchosha sana lakini hawakutaka kusimama sehemu moja muda mrefu zaidi ya kuendelea zaidi na zaidi. Wakati wao wakiendelea na safari na ndivyo ambavyo muda ulivyokuwa ukisonga, masaa yaliendelea kukatika zaidi na mpaka inafika saa moja usiku walikuwa wamekwishafika Lampazos de Naranjo.
Kutoka hapo Lampazos de Naranjo mpaka Anahuac hakukuwa na umbali mkubwa, walikuwa wamebakiza kilomita sitini. Hawakutaka kulala hapo Lampazos kitu ambacho kiliwafanya kuendelea na safari yao kama kawaida. Kutokana na mwendo ambao walikuwa wakienda nao walichukua dakika arobaini na tano na ndipo walipofika Anahuac, sehemu ambayo ilikuwa ni njia panda ya kuelekea katika mipaka yote ya Mexico na Marekani. Hapo kulikuwa na njia ya kuelekea katika mpaka wa Nuevo Laredo na pia kulikuwa na njia ya kwenda katika mpaka wa Piedras Negras.
“Cha kwanza safisha uso wako” Bwana Maxwell alimwambia Alan.
Uso wake bado uliendelea kuwa na damu zilizokuwa zimeganda na pia ulikuwa umevimba kutokana na kipigo ambacho alikuwa amepigwa siku hiyo. Alan akachukua maji na kisha kuanza kuuosha uso wake huku akilivua shati na kuliacha mahali hapo. Baada ya hapo, Bwana Maxwell akaendesha gari mpaka walipofika katika hoteli ya Panama Hill ambapo wakateremka na kisha kwenda kuchukua vyumba viwili.
Muda mwingi dada wa mapokezi alikuwa akimwangalia Alan kwa mshangao. Uso wa Alan ulikuwa umevimba sana kitu kilichompeleka dada yule wa mapokezi kujiuliza maswali mfululizo kuhusiana na Alan lakini mwisho wa siku akaamua kuachana nae kwani ilikuwa ni kawaida sana kwa watu wa hapo Anahuac kuonekana hivyo kutokana na vurugu ambazo zilikuwa zikitokea mara kwa mara.
Usiku huo wakalala ndani ya hoteli hiyo. Bado Alan hakuonekana kuwa mwenye furaha, mawazo yake yalikuwa yakiendelea kumfikiria baba yake ambaye alikuwa ameuawa. Wakati mwingine moyoni alikuwa akijilaumu kwa kulazimisha kusafiri kuelekea nchini Mexico ambapo kulikuwa na matatizo lakini wakati mwingine akaziondoa lawama hizo upande wake na kuzipeleka kwa wazazi kwani kwani hawakuwa wamemwambia ukweli juu ya kile kilichokuwa kikiendelea.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Asubuhi ilipofika, saa moja asubuhi wakaendelea na safari yao. Kila mmoja alionekana kuwa na nguvu upya, kitendo cha kulala usiku na kuipumzisha miili yao kilionekana kuwa kitu muhimu sana. Safari hiyo iliendelea mpaka pale walipofika Sabinas, mji pekee ambao ulikuwa ukifanyika biashara kubwa ya nguo kutoka Marekani huku watu wengi kutoka sehemu mbalimbali nchini Mexico kufika mahali hapo kwa ajili ya kujinunulia nguo.
Bwana Maxwell hakutaka wapite, alichokifanya akaegesha gari pembeni na kisha kuteremka hali ambayo ilimshangaza Alan na Jocelyn. Akatokomea katika maduka hayo ya nguo ambayo yalikuwa na watu wengi ambao walikuwa wakiendelea kujinunulia nguo huku katika sehemu mbalimbali maeneo hayo kukiwa na idadi ya polisi wengi katika kila kona.
“Ulikwenda wapi?” Lilikuwa swali la kwanza alilouliza Alan mara baada ya Bwana Maxwell kurudi garini huku akiwa na mfuko ulioonyesha kuwa na nguo.
“Kununua nguo”
“Za nini sasa na wakati tunakwenda Marekani kwenye nguo nyingi?” Alan aliuliza huku akionekana kushangaa.
“Chukua shati hili” Bwana Maxwell alimwambia Alan huku akimkabidhi shati, akamtaka kulivaa.
“Mbona umechukua nguo nyingi hivyo?” Jocelyn alimuuliza Bwana Maxwell.
“Tupo vitani. Hizi ni silaha zetu” Bwana Maxwell alimwambia mke wake, Jocelyn.
“Silaha zetu?”
“Ndio”
“Kivipi?”
“Za kuvukia mpakani?” Bwana Maxwell alimwambia Jocelyn ambaye aliendelea kubaki na mshangao.
Bwana Maxwell wala hakuonekana kuwa na wasiwasi, alichokifanya hata kabla ya kuondoka mahali hapo ni kumuita mwanaume mmoja ambaye alikuwa akiuza maji yaliyokuwa kwenye madumu maalumu makubwa na kununua maji ya lita kumi na kuyaingiza garini. Kila kitu ambacho alikuwa akikifanya mahali hapo kilionekana kumshangaza kila mmoja, Bwana Maxwell alionekana kama mtu aliyechanganyikiwa kutokana na yale ambayo alikuwa akiyafanya.
“Na maji ya nini tena na wakati tuna maji ya kutosha?” Jocelyn alimuuliza Bwana Maxwell.
“Nayo ni njia mojawapo ya kuwaepuka wabaya wetu” Bwana Maxwell alimwambia mke wake.
“Kuwaepuka kivipi?”
“Kila unachokiona nimekinunua kitakuwa msaada mkubwa sana kwetu. Niamini” Bwana Maxwell alimwambia Jocelyn ambaye hakuonekana kuishiwa na mshangao usoni mwake, si yeye tu bali hata Alan alikuwa akishangaa.
“Kuna kitu unatuficha” Jocelyn alimwambia Bwana Maxwell.
“Hapana. Ila kuna kitu”
“Kitu gani?”
“Niliporudi kutoka kununua nguo, kuna polisi walikuwa wakiangalia sana ndani ya gari hili” Bwana Maxwell aliwaambia, maneno hayo yakawashtua.
“Polisi?”
“Ndio”
“Wapo wapi?”
“Wale pale nyuma” Bwana Maxwell alimwambia Jocelyn na kisha wote kwa pamoja kugeuka nyuma, kulikuwa na polisi wawili ambao walikuwa wakiangalia sana mule garini, tena mmoja akiwa amekwishatoa redio call yake, na alikuwa akiongea na mtu mwingine huku macho yake yakiendelea kuangalia ndani ya gari.
“Mungu wangu!” Alan alisema kwa mshtuko.
“Usiogope. Mpo pamoja nami, hamtakiwi kuhofia kitu chocchote kile” Bwana Maxwell aliwaambia huku akionekana kujiamini sana.
Tayari hali ya amani ikaonekana kuharibika mahali hapo, kitendo cha polisi wale wawili kuangalia sana mule garini kulionekana kuwatia wasiwasi sana. Wakajua kwa namna moja au nyingine tayari walikuwa wamejua kwamba Alan alikuwa ndani ya gari lile. Alichokifanya Bwana Maxwell ni kuwasha gari na kuanza kuliondoa mahali hapo. Wote wakageuka nyuma, mmoja kati ya polisi yule akaanza kuangalia picha ambayo alikuwa nayo mkononi na kisha wote kuanza kukimbia kuelekea katika sehemu iliyokuwa na maegesho ya magari na kuingia ndani ya gari lao.
“Bila shaka wanataka kutufuata” Bwana Maxwell aliwaambia, akaliingiza gari katika barabara kubwa, akaweka gia namba tatu na kisha kukanyaga moto, kadri alivyozidi kwenda na ndivyo alivyozidi kukanyaga moto zaidi.
“Nafikiri hawakuwa na habari na sisi” Jocelyn alimwambia Bwana Maxwell baada ya kuona wamekwenda kwa umbali mrefu bila gari la polisi wale kuonekana.
“Hapana. Walikuwa na habari na sisi, na bila shaka wanakuja huku huku, cha msin….” Bwana Maxwell alisema lakini hata kabla hajamalizia sentensi yake, king’ora cha gari la polisi kikaanza kusikika kutoka mbali kwa nyuma, japokuwa hawakuwa wakiliona gari lakini walijua dhahiri kwamba walikuwa wakifuatwa wao.
“Wanakuja” Bwana Maxwell aliwaambia, hapo hapo akaingiza gia namba tano na kisha kuongeza kasi, alichokuwa akitaka kwa wakati huo ni kuwakimbia polisi hao ambao kwa mbali gari lao lilikuwa limeanza kuonekana, tena lilikuwa likija kwa kasi ya ajabu.
“Wanakuja” Alan alisema kwa mshtuko.
“Acha waje. Nataka tukutane na kona tu” Bwana Maxwell alimwambia Alan.
Mwendo ulikuwa wa kasi mno, Bwana Maxwell alikuwa akiomba Mungu wakutane na kona yoyote ile barabarani kwa sababu akilini mwake alikuwa amepata wazo moja muhimu ambalo alitaka lifanyike kwa haraka sana. King’ora cha polisi kilikuwa kikiendelea kusikika huku gari lao likiwa linakuja kwa kasi sana nyuma, lilikuwa kama mita mia mbili kutoka pale walipo. Kila mmoja ndani ya gari alionekana kuwa na wasiwasi, tayari polisi wale walionekana kumgundua Alan kupitia picha ambayo walikuwa nayo mikononi mwao.
Alan ndiye ambaye alionekana kuwa na wasiwasi mkubwa zaidi, alijua fika kwamba polisi wale walikuwa wamemgundua na ndio maana walikuwa wakiwafuatilia na gari lao. Hakutaka kukamatwa hata kabla ya kufika nchini Marekani, alitaka kufika mapema na kuhakikisha kwamba baba yake anazikwa kwa heshima zote zinazostahili na si kuzikiwa porini.
Baada ya dakika kumi, wakaanza kuingia katika pori kubwa ambalo lilikuwa pembezoni mwa barabara hiyo. Hiyo ikawaonyesha kwamba walikuwa wameanza kuingia Nava Municipality, sehemu pekee ambayo ilikuwa na mapori mengi nchini Mexico.
“Wanazidi kukaribia, ongeza kasi” Alan alimwambia Bwana Maxwell.
“Yaani hapa ndio imeifika kasi ya mwisho kabisa, zaidi ya hapa nadhani gari linaweza kupaa” Bwana Maxwell alimwambia Alan.
Kingora kilizidi kusikika zaidi nyuma yao, polisi wale walikuwa wakija kwa kasi sana kuwafuata kule walipokuwa. Bwana Maxwell hakutaka kusimamisha gari, aliendelea kuliendesha kwa kasi zaidi na zaidi. Mungu akaonekana kuwa upande wao, kona ambayo alikuwa akiitaka Bwana Maxwell ikaonekana kuwa mbele yao, Bwana Maxwell akaonyesha tabasamu pana, tabasamu lilikuwa na wingi wa mafanikio.
“Vipi tena?” Alan alimuuliza Bwana Maxwell bara baada ya kumuona akitabasamu.
“Kuna kona mbele yetu”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Unamaanisha nini? Huo ndio msaada wetu?” Jocelyn alimuuliza Bwana Maxwell.
“Hapana. Kona hii inamaanisha hapa ndipo akili yangu itakapotumika” Bwana Maxwell alimjibu Jocelyn.
“Kivipi?”
“Usiwe na wasiwasi, niachie mimi” Bwana Maxwell alijibu, walipoifikia, Bwana Maxwell akakata kona na kisha kusogea mbele kama mita themanini na kisha kulisimamisha gari hilo hali ambayo ilimfanya kila mmoja kumshangaa.
“Mbona umesimamisha gari?” Alan aliuliza huku akitetemeka.
“Nataka tuwapoteze”
“Kivipi”
“Hapa ndipo mchakato wa kuvuka mpakani unapoanzia” Bwana Maxwell alitoa jibu ambalo lilizidi kumshangaza kila mmoja, hawakujua alimaanisha nini, alichokuwa akikisema ni kwamba alikuwa na akili hata zaidi ya polisi wale, yaani alikuwa akijiona mtu mwenye akili zaidi ya mtu mwingine yeyote duniani.
“Tunakamatwa!” Alan alimwambia Bwana Maxwell huku sauti ya king’ora kile kikiwa kinasikika kwa karibu sana, yaani ilionyesha kwamba gari lile la polisi lilikuwa limekaribia kuikata kona ile.
“Hakamatwi mtu hapa. Usiwe na hofu, fanyeni kila nitakachowaambia. Tumebakiza kilometa themanini kabla ya kuingia Guerero na kilomita mia na ishirini kabla ya kuingia mpakani, Piedras Negras” Bwana Maxwell aliwaambia huku akitoa dumu lile la maji nje ya gali lile.
Polisi wale wawili walikuwa ndani ya gari lao wakilifuatilia lile gari ambalo waliweza kumuona mtu mmoja ambaye alikuwa akitafutwa sana kwa wakati huo na picha yake walikuwa nayo mikononi mwao, Alan. Kila mmoja alikuwa na uhakika kwamba mtu huyo ndiye ambaye walikuwa wamepewa picha yake na ndiye ambaye alikuwa akihitajika sana wakati huo.
Kitendo cha Bwana Maxwell kuwasha gari na kuondoka kilionyesha kwamba endapo wasingelifuatilia lile gari basi wasingeweza kumkamata mtu huyo na kumfikisha sehemu husika. Walichokifanya nao ni kulifuata gari lao, wakaingia na kisha kuanza kulifuatilia. Njiani, polisi mmoja alikuwa bize akiongea na wenzake kwa kutumia redio call, aliwapata taarifa kwamba mtu ambaye walikuwa wakimtafuta tayari walikuwa wamemuona na alikuwa njiani kuelekea Guerero.
Kuna kipindi gari lile hawakuweza kuliona kabisa mbele ya macho yao kitu ambacho kilionyesha kwamba endapo wasingeongeza kasi ya gari basi gari lile lingepotea zaidi na zaidi. King’ora kilikuwa kikisikika, walikiwasha kwa lengo moja tu kwamba gari lile lisimame na kisha kulipekua na kuwaachia waondoke ila kwa jinsi gari lile lilivyokuwa likizidi kusonga mbele, walikuwa na uhakika kwamba mtu yule ambaye walikuwa wamemuhisi alikuwa ndiye mwenyewe.
“Ongeza kasi zaidi ya hii” Polisi mmoja alimwambia mwenzake ambaye alikuwa akiendesha gari lile.
“Hakuna tatizo”
Dereva akaongeza kasi, ndani ya sekunde arobaini na tano tu, wakaweza kuliona tena gari lile ambalo lilikuwa mita kama mia mbili kutoka pale walipokuwa. Hiyo ikaonekana kuwa nafuu kwao, walikuwa na matumaini kwamba wangeweza kulifikia na kisha kumwamuru dereva alisimamishe gari lile.
“Hawa hawafiki Guerero tutakuwa tumekwishawakamata” Polisi yule ambaye alikuwa pembeni ya dereva alimwambia.
“Ngoja niweke gia ya mwisho kabisa”
“Hakuna tatizo. Ila kumbuka kule mbele kuna kona, tusije tukapinduka”
“Hilo lisikutie shaka”
Gari likaongezwa kasi, dereva akaweka gia ya mwisho kabisa, namba tano na kisha kukanyaga moto zaidi. Hiyo ikaonekana kuwa msaada kwao, gari lile likaonekana kuanza kusigea kwa nyuma kuwafuata, hiyo ilimaanisha kwamba walikuwa wakikaribia kulifikia. Polisi wale wakaingia na nguvu, yule ambaye alikuwa amekaa pembeni akachukua bunduki yake na kisha kuanza kuangalia kama kulikuwa na risasi za kutosha, alipoona zote zipo, akairudisha kiunoni.
Ni kama mita mia moja na ishirini zilikuwa zimebakia na mbele kulionekana kuwa na kona kubwa, gari lile ambalo walikuwa wakilifuatilia kwa nyuma likakata kona hiyo kubwa. Polisi wale hawakutaka kuishia hapo, baada ya sekunde kama hamsini, nao wakaifikia kona ile na kisha kulikata gari lao na kisha kuanza kutazama mbele kama kulikuwa na gari lolote lile.
“Lile pale” Polisi mmoja alimwambia mwenzake huku akilinyooshea kidole.
Wakaanza kulisogelea gari lile, kila mmoja akapigwa na butwaa kubwa. Ni kweli gari lile lilifanana na gari ambalo walikuwa wakilifuatilia lakini kuna kitu ambacho kilikuwa ni tofauti kabisa. Mwanamke mrembo, mwanamke aliyeonekana kuwa umbo zuri, mwanamke ambaye alionekana kumvutia mwanaume yeyote yule alikuwa amekaa katika boneti la mbele la gari lile huku akionekana kuwa mnyonge.
Walipofika karibu kabisa na gari lile, wakalipaki gari lao na kuteremka. Wakaanza kumfuata mwanamke yule, Jocelyn na kisha kuanza kumwangalia. Uzuri wake ndio ambao uliwaduwaza polisi wale ambao wakaonekana kama kusakiziana ni nani ambaye alitakiwa kumuuliza swali lolote lile.
“Samahani” Polisi mmoja alimwambia Jocelyn huku akiwa amemsogelea pamoja na mwenzake.
“Bila samahani” Jocelyn alimwambia, akauinua uso wake na kuanza kuwaangalia, tabasamu pana ambalo alilitoa nalo lilikuwa chanzo cha kilichowafanya kuvutiwa nae.
“Mbona unapaki gari porini namna hii?” Polisi mmoja akauliza, tabasamu pana likautawala uso wake, yule mwenzake, kwa kutumia macho ya kuibia akaanza kumwangalia Jocelyn maungo yake.
“Gari limechemka sana” Jocelyn aliwajibu polisi wale.
“Kwani upo peke yako?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ndio. Nipo peke yangu nakwenda kwenye sherehe hapo Guerero” Jocelyn alimjibu polisi yule.
“Kwani wewe ndiye ulikuwa unaliendesha gari hili?” Polisi aliuliza.
“Ndio”
“Kuna gari tulikuwa tukilifuatilia, linafanana na hili, umeliona likipita?” Polisi yule aliendelea kuuliza.
“Ndio. Limepita mahali hapa kwa kasi sana, nilijaribu kulisimamisha lakini halikusimama kabisa” Jocelyn alimjibu polisi yule.
“Pole sana. Hauungui na jua hapo?”
“Naungua ila sina cha kufanya. Hata ndani ya gari kuna joto, kiyoyozi kimeharibika kwa hiyo nimeona bora na mimi nikae hapa nje” Jocelyn alimjibu polisi yule.
“Sasa kwa nini tusiende hata kwenye gari letu kupata kiyoyozi? Kwa jinsi ulivyo hautakiwi kuungua na jua. Nimekosea afande?” Polisi yule alimwambia Jocelyn na kumuuliza mwenzake.
“Haujakosea. Upo sahihi kabisa asilimia mia moja” Polisi yule mwingine alijibu huku akionekana kupagawa na uzuri wa Jocelyn.
Muda wote huo Jocelyn alikuwa akiwaangalia kwa macho mazuri yaliyojaa mahaba, alikwishawasoma polisi hao kitambo kwamba walikuwa ni watu waliojaa tamaa ya kutaka kulala na mwanamke muda huo. Pori lile ambalo lilikuwa limezunguka barabara ndio lililoonekana kuwahamasisha na kuona kwamba endapo wangeenda nae sawa basi wangeweza kukamilisha kukidhi tamaa zao.
Kutokana na tamaa ambazo walikuwa nazo, wakasahau kuendelea na safari yao kulifuata gari hilo ambalo Jocelyn aliwaambia kwamba lilipita muda mfupi uliopita, vijidudu vya mshawasha wa kufanya mapenzi vikaanza kuwatembelea miilini mwao, waliona ni bora kuongea na mwanamke huyo kwani wangeweza kupata kitu chochote kile kuliko kulifuatilia gari hilo ambalo mpaka muda huo hawakuwa na uhakika kama yule mtu waliyekuwa wakimfuatilia alikuwa mwenyewe au au.
Jocelyn hakutaka kuishia hapo, kwa sababu tayari alikuwa amekwishagundua udhaifu wa polisi wale, akalichukua dumu la maji ambalo lilikuwa limejaa maji na kisha kulifungua. Polisi wale wakatulia, walikuwa wakimfuatilia Jocelyn kwa kila kitu alichokuwa akikifanya. Alipoona kwamba tayari amelifungua, akaanza kujimwagia maji yale kama sababu ya kuondoa joto mwilini mwake.
Huo ndio ukawa kama msumali wa mwisho kwa polisi wale, mwili mzima wa Jocelyn ukaloweshwa na maji yalemwili mzima, gauni jeupe ambali alikuwa amelivaa likaushikilia mwili wake. Matiti yake yaliyosimama yakaanza kuonekana. Polisi wale wakabaki na mshangao, kila mmoja akabaki akiyaangalia matiti yale, walionekana kuchanganyikiwa kupita kawaida.
Katika kipindi chote hicho Jocelyn alikuwa akiwafuatilia kisiri. Hakuridhika, alichokifanya ni kuendelea kujimwagia maji kwa mara ya pili, nguo yake ya ndani, bikini iliyokuwa na rangi nyekundu ikawa inaonekana vizuri kabisa kana kwamba hakuwa amevaa gauni lile. Hatua hiyo ikaonekana kuwachanganya zaidi, kitu cha kwanza kabisa, suruali zao maeneo ya zipu zikasogea mbele, macho hayakutoka katika maeneo ya bikini ile, walikuwa wakiendelea kuiangalia kana kwamba walikuwa wakitaka kujua ni aina ya mshono gani ambao ulitumika.
Akili zao zilikuwa zimekwishahama kwa wakati huo, alichokifanya Jocelyn, akageuka na kuwapa mgongo, akajimwagia maji kuanzia mgongoni maji ambayo yakashuka chini mpaka kwenye makalio yake, gauni likashika ngozi, kwa sababu alikuwa amevaa bikini tu, makalio yakaonekana, akaufungua mlango wa gari na kisha kuinama na kuliingiza dumu lile garini.
Jocelyn alikuwa ameinama kwa mbele na kuwapa nafasi nzuri ya kuyaangalia makalio yake kwa jinsi yalivyokuwa yameumbika. Polisi wale hawakuwa wakitulia, mara waingize mikono mfukoni na kuvipeleka vidole vyao mbele ili wasishtukiwe kile kilichokuwa kikiendelea katika maeneo ya zipu. Alipoliweka dumu lile garini, akaufunga mlango, akawageukia na kisha kuanza kuipandisha gauni yake juu na kuanza kuyashikashika mapaja yake kana kwamba alikuwa akijipaka mafuta.
Polisi walisimama kama sanamu, kila kilichokuwa kikiendelea mahali pale kilizidi kuwapa ashki ya kufanya mapenzi, mawazo yao yakawa yamehama na kwenda mbali kabisa, walichokuwa wakikifikiria ni kufanya ngono tu na Jocelyn. Mikono yake ikapanda mpaka mapajani, akaipandisha zaidi mpaka katika bikini yake, Jocelyn hakuonekana kujali.
“Mlisemaje vile?” Jocelyn aliwauliza, polisi wote wakashtuka kama walikuwa wametolewa katika kulifikiria jambo fulani, wakayahamisha macho yao kutoka katika eneo la chini ya kiuno la mwili wa Jocelyn na kisha kumwangalia usoni.
“Unasemaje?” Polisi mmoja aliuliza, alikuwa amekwishatamanishwa vya kutosha kiasi ambacho hata swali la Jocelyn hakulisikia vizuri.
“Nani anaweza kuja kunipaka mafuta mgongoni mpaka huku chini?” Jocelyn aliwauliza polisi wale.
“Mimi naweza”
“Hata mimi naweza. Nilikuwa mtu wa massage kipindi cha nyuma” Polisi mwingine aliingilia.
“Sasa nani mtaalamu? Huku nyuma siwezi kupafikia”
“Mimi mtaalamu”
Kila mmoja alikuwa akitaka kumgusa Jocelyn, ni kweli tayari walikuwa wamekwishakula kwa macho na katika kipindi hicho walitaka japo kugusa tu ili waweze kufurahia zaidi. Pepo la ngono lilikuwa juu kwa asilimia mia moja miilini mwao, kitu ambacho walikuwa wakikifikiria ni kufanya mapenzi na Jocelyn tu.
“Unataka tukupake mafuta hapa?” Polisi mmoja aliuliza.
“Ndio. Mnaogopa?”
“Hapa kumekaa wazi sana. Au tusogee pale porini kidogo” Polisi yule alimwambia Jocelyn.
“Ila naogopa mtanipandisha mzuka. Mkiupandisha mtaushusha?” Jocelyn aliwauliza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Swali hilo,neno kupandishwa mzuka lilivyotajwa, suruali zikazidi kusogea mbele maeneo yazipu, neno liliwachanganya sanana kuona kwamba tayari Jocelyn alikuwa ameelekea katika anga zao na walitakiwakumfyatua hata kabla hajaleta unjanja wowote ule wa kuwazuia. Bila kuitwa, wotekwa pamoja wakaanza kupiga hatua kumsogelea Jocelyn, tayari macho yao yalikwishaonyeshakwamba ni kitu gani ambacho walikuwa wakikitaka muda huo.
Matiti ya Jocelyn yaliyokuwa yamesimama nayoyalikuwa moja ya sababu iliyowafanya kuwachanganya sana na kuona kwamba hawakutakiwa kumuachahivi hivi. Wakawasahau wake zao ambao walikuwa nyumbani kwao, mtu ambayewalikuwa wakimfikiria ni Jocelyn tu ambaye alionekana kuwa radhi kwa kituchochote kile.
“Msitingishike, tulieni hivyo hivyo” Sautiilisikika nyuma yaokatika kipindi ambacho walikuwa wamekwishamfikia Jocelyn na kilichokuwakimebakia ambacho walitaka kukifanya ni kusogeza vinywa vyao kifuani mwaJocelyn na kuanza kumruhusu shetanikuanza kuwaambia nini cha kufanya.
Kitu cha kwanza, wakashtuka sana,walikuwa wameguswa na vitu vichwani mwao, hawakutaka kujiuliza sana,walijua vika kwamba vitu hivyo vilikuwa ni bunduki, wakatakiwa kutulia kama maji ya mtungini.
****
“Maji ya nini sasa?” Jocelyn alimuulizaBwana Maxwell.
“Kazi yake kubwa sana” Bwana Maxwell alimjibu Jocelyn.
“Ipi?”
“Watamanishe mpaka wazubae” Bwana Maxwellalimwambia Jocelyn.
“Kivipi?”
“Nadhani unajua, tumia udhaifu wa mwanaumekumfanya azubae” Bwana Maxwell alimwambia Jocelyn.
Kwa haraka haraka akaanza kumuelekezaJocelyn ni kipi ambacho kilitakiwa kufanyika mahali hapo. Hakuchukua hatasekunde kumi, akamaliza, akateremka kutoka garini na Alan na kisha kuelekeakatika miti iliyokuwa imezunguka barabara huku wakimwacha Jocelyn mahali pale.
Wote wakatulia huku bunduki zikiwa mikononimwao. Baada ya sekunde kumi toka wajifiche kwenye miti ile, wakaliona gari lilela polisi likikata kona na kuingia barabara hiyo, hawakuwafuata, wakawaachampaka walipoteremka na kisha kuanza kumsogelea Jocelyn.
Kila kilichokuwa kikiendelea walikuwawakikiangalia. Jocelyn alikuwa akihakikisha anafanya kamaalivyoambiwa na mume wake. Japokuwa alikuwa amemzoea sana mke wake lakini kwa vile ambavyo alikuwaakiwafanya polisi wale nae vikaanza kumchanganya kule kule porini. Alikuwaamempa Jocelyn maelekezo madogo sana lakini kwakile alichokuwa akiwafanyia polis wale alionekana kamaalipewa mafunzo kwa zaidi ya wiki.
“Twende” Alan alimwambia Bwana Maxwell.
“Bado.Subiri kwanza” Bwana Maxwell alimwambia Alan.
Waliendelea kubaki pale nyuma ya miti ilempaka walipohakikisha kwamba polisi wale walikuwa wamechanganyikiwa sana juu ya umbo zuri laJocelyn, walipoona kwamba polisi wale wanaanza kumsogelea Jocelyn, wakatokanyuma ya miti ile na kisha kuwaweka chini ya ulinzi.
Polisi wakapigwa na mshtuko, Jocelynhakutaka kubaki hivi hivi, akazichukua bunduki za polisi wale na kishakuziingiza ndani ya gari. Hapo ndipo ambapo polisi wale wakajua kwamba kila kilichokuwakikiendelea mahali pale kilikuwa ni mtego wa kuwatega wategeke na kisha kuwekwachini ya ulinzi.
Pepo la ngono likawatoka, wakabakiwakitetemeka kana kwamba walikuwa wakihisi baridi. Pamoja na mafunzo mengi yakipolisi waliyokuwa wamepewa muda huo walionekana kufanya uzembe mmoja mkubwa sana kitukilichowapelekea kuwa chini ya ulinzi.
“Pigeni hatua kuelekea porini bila kugeukana kutuangalia” Bwana Maxwell aliwaambia, walichokifanya ni kuanza kupiga hatuakuelekea katika upande mwingine wa barabara.
“Kwa nini tusiwaue tu?” Alan alimuulizaBwana Maxwell huku wakiwa wamewaweka chini ya ulinzi.
Huo ulikuwa ni ujanja alioutumia Alan,aliyatamka maneno yale kwa sababu alitaka kuwatia hofu zaidi polisi wale iliwajue kwamba watu ambao walikuwa wamewaweka chini ya ulinzi hawakuwa watu wakawaida, walitaka kuonekana kuwa na roho mbaya.
“Kwa hiyo tuwaue?” Bwana Maxwell aliuliza.
“Ndio. Kwani nani atajua kamasisi ndio tumewaua?” Alan alijibu na kuuliza.
Maneno yale yakawatia hofu zaidi polis wale,wakagundua kwamba kama hawakufanya kileambacho watu wale walikuwa wakikitaka wakifanye basi wangeweza kupigwa risasi.Wakaanza kuomba Mungu ili aweze kuwanusuru na balaa ambalo lilikuwa mbele yao, kwa presha ambayo walikuwa nayo mahali hapo, surualizao maeneo ya kwenye zipu zilirudi kamakawaida.
“Tunaomba mtusamehe” Polisi mmoja aliwaambiahuku akionekana kuogopa sana.
“Vueni nguo zenu” Bwana Maxwell aliwaambia,kwa haraka bila kupoteza muda wakaanza kuzivua nguo zao.
Kachukue kamba garini” Bwana Maxwellalimwambia Alan ambaye akatoka mahali hapo, baada ya sekunde chache akarudihuku akiwa na kamba na kisha kuwafunga miguu, mikono kwa nyuma na kuzizungushakamba zile mtini huku nao wakianza kuzivaa nguo zile za kipolisi na kisha kuondoka.
“Safi sana” Bwana Maxwellalimwambia Jocelyn.
“Kumbe nyie wanaume wadhaifu kiasi hicho!”
“Kuna wengine ni wadhaifu sana. Nawajua polisi wa hapo Sabinas, wengihuwa ni wadhaifu sanakwa wanawake na ndio maana nikakwambia hivyo” Bwana Maxwell alimwambia Jocelyn.
“Bado kuvuka mpakani” Alan alimwambia BwanaMaxwell.
“Kwa muonekano kunaonekana kuna ugumu ilanaomba mfahamu kwamba hakuna ugumu mahali hapo, tutavuka kirahisi bila kutumiafedha. Nguo hizi za polisi zitatuvusha” Bwana Maxwell alimwambia Alan.
“Tutavukaje?”Jocelyn alimuuliza BwanaMaxwell.
“Utaigiza” Bwana Maxwell alimjibu.
“Nitaigiza?”
“Ndio”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kivipi?”
“Utaona tu”Bwana Maxwell alimjibu Jocelyn nakisha kuliwasha gari na kuanza kuelekea Guerero ambapo wasingekaa balikuunganisha mpaka mpakani PiedrasNegras.
****
Barabara ilikuwa na kona hyingi sana, katika kipindihicho Bwana Maxwell alikuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kawaida. Hawakuwa napresha tena kuhusiana na kufuatiliwa na polisi nyuma yao kutokana na wale polisi ambao walikuwamstari wa mbele kuwafunga kamba polisi. Walichukua saa moja mpaka kufikaGuerero ambapo kama kawaida Jocelyn akateremkana kisha kwenda kununua vyakula.
Mpaka katika kipindi hicho bado Jocelynalikuwa akiendelea kujiuliza kutokana na matumizi ya nguo ambazo Bwana Maxwellalikuwa amezinunua. Hilolilikuwa swali muhimu kwake lakini hakuwa akipata jibu. Alipafahamu vilivyompakani Piedras Negras, hakukuwa sehemu ya kupita kirahisi rahisi, ilikuwa nisehemu ambayo kulikuwa na ulinzi mkubwa sana.
Waliponunua vyakula, wakaendelea na safari yao ya kuelekea mpakaniPiedras Negras. Hapo kidogo wakapata nafuu kwani hawakuwa wamebakiza umbalimrefu sanampaka kuingia mpakani hapo. Ndani ya saa moja na nusu, tayari wakaanza kuingiampakani. Pilikapilika za watu zilikuwa nyingi, kulikuwa na maduka mengi pamojana soko ambalo lilikuwa likitumiwa kununulia vyakula mbalimbali.
Sehemu hiyo ilionekana kuchangamka kwasababu watu wengi kutoka Marekani na Mexico walikuwa wakikutana hapo kwaajili ya michezo mbalimbali ukiwepo mchezo wa kugombanisha majogoo, mchezoambao uliletwa na Wathailand mahali hapo. Mji wa Piedras Negras haukuwa kamamiji mingine, mji huu ulionekana kuwa na uchangamfu mkubwa sanahuku watu ambao walikuwa wakiishi mahali hapo wakiwa wanaongoza kwenda nchiniMarekani kuliko sehemu yoyote nchini Mexico.
“Tumekwishafika Piedras” Bwana Maxwellaliwaambia huku macho yaoyakiangalia huku na kule.
“Nini kifanyike?” Alan alimuuliza BwanaMaxwell.
“Jocelyn utaumwa, utakuwa katika hali mbaya”Bwana Maxwell alimwambia Jocelyn.
“Nitaumwa! Kivipi?” Jocelyn alimuuliza BwanaMaxwell.
“Unaziona hizi nguo?”
“Ndio”
“Huu utakuwa ujauzito wako” Bwana Maxwellalimwambia Jocelyn ambaye akabaki akiwa na mshangao.
“Mmmh!”
“Ndio hivyo. Haina jinsi, hiki ndichokizuizi cha mwisho, tukifanikiwa kukivuka hiki, tutakuwa tumeingia nchinikwetu” Bwana Maxwell alimwambia Jocelyn.
“Sasa itakuwaje?”
“Wewe ndiye unajua kuigiza. Jifanye mwanamkemjauzito, ila yakupasa kutaka kitu kimoja tu” Bwana Maxwell alimwambia Jocelynhuku Alan akiwa kimya akisikiliza.
“Kitu gani?”
“Utakuwa unataka kujifungulia nchiniMarekani, nchini kwako” Bwana Maxwell alimwambia Jocelyn.
“Mhhh!”
“Nini sasa?”
“Hauoni kama nina asili ya Mexico?”
“Najua ila hilo si tatizo. Utasema umechanganya wazazi,yaani usitie shaka” Bwana Maxwell alimwambia Jocelyn.
“Nisitie shaka kwa nini?”
“Hauyaoni mavazi tuliyoyavaa? Sisi ni polisiambao tutakusaidia kuvuka mahali hapa” Bwana Maxwell alimwambia Jocelyn.
“Sawa. Hakuna tatizo” Jocelyn alijibu.
Hakukuwa na muda wa kupoteza mahali hapo,tayari walikuwa wamekwishafika katika kizuizi cha mwisho kabisa kabla yakuingia nchini Marekani. Alichokifanya Jocelyn ni kuanza kuziingiza nguo zilesehemu ya tumbo lake na kisha kuzibana vizuri.Kwa muonekano ambao alikuwa akionekana nao wakati huo alikuwa kamamwanamke ambaye alikuwa mjauzito kwa asilimia mia moja.
Jocelyn hakutakiwa kukaa katika hali yakawaida, alitakiwa kuwa kama mwanamke ambayealikuwa akisikia uchungu wa kutaka kujifungua. Kwanza akaambiwa aigize kama mwanamke aliyekuwa kwenye hali hiyo, akafanikiwa nakuonekana kwamba alikuwa akifaa kwa asilimia mia moja.
“Hautakiwi kukaa” Bwana Maxwell alimwambiaJocelyn.
“Natakiwa kufanya nini sasa?” Jocelynalimuuliza Bwana Maxwell.
“Unatakiwa kulala”
“Wapi? Chini?”
“Hapana. Juu ya hicho kitu, tena ukiwaumekiegemeza kichwa chako mapajani mwa Alan” Bwana Maxwell alimwambia Jocelyn.
Jocelyn akajilaza kitini na kisha kukiwekakichwa chake mapajani mwa Alan ambaye nae akaonekana kuujua wajibu wake,akaanza kujifanya kama anamhudumia Jocelynmahali pale, katika kiti cha nyuma garini. Hiyo ndio ilionekana kuwa njianyepesi ya kuweza kufanikisha mchakato wao mzima wa kuvuka mahali pale, kilakitu kilipokamilika, Bwana Maxwell akashuka akachukua maji, akajimwagia kidogoili aonekane kama mtu aliyekuwa akitokwa na jasho jingi na kisha kuwafuatapolisi wawili ambao walikuwa wamekaa sehemu moja wakinywa kahawa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Necesito tu ayuda (Ninahitaji msaada wenu)“ BwanaMaxwell aliwaambia polisi wale kwa lugha ya kiispaniola, lugha ambayo alikuwaamejifundisha sana Texas kwa ajili ya kukabiliana na Wamexicoambao walikuwa na utamaduni wa kuzamia kuelekea nchini Marekani.
“Qué podemos ayudarle?(Tukusaidienini?)” Polisi mmoja alimuuliza Bwana Maxwell.
“Hay mujer embarazada en mi coche (Kunamwanamke mjauzito garini mwangu)”Bwana Maxwell alijibu.
“Cómo debemos ayudar? (Sasa tukusaidievipi)” Polisi mmoja alimuuliza Bwana Maxwell.
Hapo ndipo ambapo Bwana Maxwell alipoanzakujielezea. Japokuwa alikuwa mlevi na mcheza kamari mkubwa lakini katikakipindi hicho akili yake ilikuwa imetulia kupita kawaida katika kutoa maelezokuhusiana na Jocelyn. Aliwadanganya kwamba walimkuta akiwa njiani akiwaamelipaki gari lake, walipokwenda kumwangalia na polisi mwenzake, wakagunduakwamba mwanamke huyo alishindwa kuendesha gari kutokana na hali ambayo alikuwaakijisikia.
Maelezo yake yakaonekana kuwashtua polisiwale, wakamwangalia Bwana Maxwell kimshangao na kisha kutaka wapelekwe katikagari hilo.Bwana Maxwell hakuwa na wasiwasi wowote ule kwani alikuwa akiamini kwambaJocelyn alikuwa muigizaji mkubwa sanaambaye alikuwa na nguvu ya kumshawishi kila mmoja.
Polisi walipolifikia gari lile, wakaanza kuchunguliakupitia dirishani. Jocelyn alikuwa akilalamika kamamwanamke ambaye mtoto wake alikuwa akikaribia kutoka. Alan alikuwa bize, kofiailikuwa kichwani mwake, hakuuinua uso wake, alikuwa amekiegemeza kichwa chaJocelyn mapajini mwake huku akijifanya kumsaidia katika kila hatua, mara ampemaji anywe, mara amfute maji yaliyokuwa pajini mwa uso wake kwa kujifanyayalikuwa jasho.
Hali ambayo alionekana nayo Jocelynilionekana kuwa mbaya na alitakiwa kupatiwa huduma haraka iwezekanavyovinginevyo mimba ingeweza kuharibika na mtoto kufa papo hapo. Polisi walewakamvuta Bwana Maxwell pembeni na kisha kuanza kuongea nae.
“Hali yake mbaya sana. Muda wowote anajifungua” Polisi mmojaalimwambia Bwana Maxwell.
“Sasa mtamsaidia vipi?”
“Mpeleke katika hospitali moja hapo nyumaili akahudumiwe haraka iwezekanavyo” Polisi yule alimwambia Bwana Maxwell.
“Nilishauri hilo lakini alikataa katakata” Bwana Maxwellaliwaambia polisi wale.
“Kwa nini?”
“Anasema kwamba anataka kujifungulia nchinikwake, Marekani” Bwana Maxwell alijibu.
“Kumbe ni Mmarekani?”
“Ndio”
“Hawa wamarekani wasumbufu sana, wanakuja nchini kwetu wakiwa wajawazitohalafu kujifungua wanataka kwenda kujifungua nchini mwao. Huyu ni mwanamke watatu kutoka Marekani amekuwa na hali hii” Polisi mwingine alimwambia BwanaMaxwell maneno ambayo yalionyesha kila dalili kwamba walikuwa wakielekea kuvukahapo salama.
“Kwa hiyo itakuwaje? Nataka kuruhusiwakumvukisha huyu mwanamke mpaka kwao” Bwana Maxwell aliwaambia polisi wale.
“Hiyo ni ngumu sana”
“Kwa nini?”
“Hali yake ni mbaya sana. Anaweza kufa njiani” Polisi mwinginealimwambia Bwana Maxwell, tayari kwa maneno hayo hali ikaonekana kuwa mbaya.
“Sidhani”
“Huo ndio ukweli. Haina jinsi, inabidiajifungulie hapa hapa” Polisi yule alimwambia Bwana Maxwell.
Kama nimaigizo, Jocelyn alikuwa ameigiza kwa uwezo mkubwa zaidi mpaka kuonekana kwambaalikuwa njiani kujifungua na alitakiwa kujifungulia katika hospitali mojailiyokuwa hapo Piedras Negras. Bwana Maxwell hakuwa na cha kujitetea tena,akabaki kimya na kuona kwamba kulikuwa na uhitaji wa kutumia fedha lakinihakujua ni kwa namna gani angeweza kuzitumia fedha zile kwa polisi wale.
“Kamuite dokta Pedro” Polisi mmoja ambayealionekana kuwa mkubwa kivyeo alimwambia polisi mwenzake.
Hapo ndipo polisi yule akaanza kuondoka nakuelekea katika hospitali ya St’ Adrian ambayoilikuwa hapo Piedras kwa ajili ya kumuita dokta ambaye alikuwa maarufu sana hapo, RodriguezPedro. Bwana Maxwell mwili wake ukakosa nguvu, hakuamini kamaujanja wake wote siku hiyo ndio ungekuwa mwisho, akashusha pumzi ndefu na nzitona kisha kuyapeleka macho yake ndani ya gari lile, bado Alan alionekana kuwabize akimhudumia Jocelyn huku akiwa makini kutokuiruhusu kofia yake kumtokakichwani.
Wala hazikupita dakika nyingi, dokta pedroakafika mahali hapo. Alionekana kukurupushwa huko alipokuwa kwani alifika hukuakiwa kama mtu ambaye hakuelewa ni kitu ganiambacho kilikuwa kikiendelea. Akapelekwa kwa polisi yule mkubwa na kuambiwa nikipi kilitakiwa kufanyika, Bwana Maxwell akanyong’onyea zaidi kwani hali yahatari zaidi ilionekana mbele yake, kilichokuwa kimemshtua zaidi ni kwamba kwambali sanaalikuwa akisikia king’ora cha polisi kikija kule walipokuwa, bila shakawalikuwa polisi ambao walisikia kwamba tayari walikuwa wamefika Piedras Negras.
*****CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Msako wa kumtafuta Alan bado ulikuwaukiendelea kama kawaida na ni mawasiliano ndioambayo yalikuwa yakitumika kwa wakati huo. Polisi wa kituo kikuu cha polisi chaAnahuac walikuwa wamepokea mawasiliano kupitiaredio calls zao kwamba mtu ambaye alikuwa amefanana na Alan alikuwa akionekanandani ya gari moja ambalo lilikuwa likitaka kuondoka maeneo ya sokoni.
Redio call ile ambayo ilikuwa imewafikiandio ambayo iliwafanya polisi wanne ambao walikuwa na bunduki kujiandaa kwendahuko ambapo mtu huyo alikuwa ameonekana. Kwa sababu hakukuwa mbali sana, ndani ya dakikakumi wakawa wamekwishaingia mahali hapo ambapo mawasiliano kwa njia ya rediocall yalipofanyika tena wakaambiwa kwamba tayari watu hao walikuwa wame
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment