Search This Blog

Friday, July 15, 2022

LET ME DIE - 3

 







    Simulizi : Let Me Die

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Safari yao iliishia kwenye meza kuu na kukaa hapo pamoja. Camera nyingi zilimulika picha pale walipo na wengine wakichukua video kabisa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mshehereshaji alipanda jukwaani na kuaza kuitangaza ratiba yake.

    “Miss Diana, please come in the stage with your partner.”



    Aliongea mshehereshaji na watu wote wakapiga makofi. Alinyanyuka na kumnyanyua Abdul na kwenda naye jukwaani. Alisalimia na kumtambulisha Abdul kama mwenza wake mbele ya halaiki ya watu waliohudhuria pale. Baada ya hapo walishuka na kuendelea na ratiba nyingine.



    Sherehe iliisha saa sita usiku, na wageni wote wakaambiwa waende kwenye vyumba vyao kwakua vilishalipiwa. Abdul aliingia kwenye kile chumba alichoingia mwanzo akiongozana na Diana.



    Kinywaji alichokunywa Abdul kilimlewesha kisawa sawa, na alipofika tu kitandani, alijibwaga na kuuchapa usingizi muda huo huo.

    Diana alianza kumvua viatu na kulegeza tai ya Abdul. Kisha akamgeuza na kumlaza vizuri.

    Kisha na yeye akajitupa kitandani na kuanza kumuangalia Abdul ambaye kwa wakati huo alikua hoi kutokana na kilevi alichojitwika.



    Usiku uliisha na kuingia asubuhi bila Diana kufanya lolote na Abdul ambaye alikuwa amechoshwa vilivyo na pombe alizozipiga.



    Asubuhi ilipofika, miale ya jua la asubuhi ilimpiga Abdul machoni na kuanza kufungua macho yake kivivu. Alishangaa mazingira aliyokuwepo. Alipo tupa macho pembeni, alimuona Diana ambaye alikua bado amelala pembeni yake. Alishtuika na kutoka kitandani. Alijishangaa kujikuta akiwa na boxer peke yake huku suti alizozivaa usiku zikiwa zime tapanyika chini.



    Alizivaa nguo zake, bila ya kumuamsha Diana aliamua kutoka hotelini hapo na kwenda kwenye kituo cha mabasi kwa ajili ya kurudi kambini kwao.



    Watu wote waliokuwa kwenye bendi hiyo ya Mr. Zungu walishangaa kumuona Abdul akirudi asubuhi ile. Hawakutaka kuuliza, bali majibu yao kuwa alikua amelala na mtoto wa bosi wao yalimuingia kila mmoja wao.



    Sapna alipomuona, aliondoka na kwenda chumbani kwake, hakutaka hata salamu yake. Aliwasalimia washikaji zake ambao wote walionyesha kumkataa kutokana na tabia aliyoionyesha. Hakuna aliyeitikia. Kila mmoja aliendelea na shughuli yake huku akionyesha kila aina ya dharau mbelel yake.



    “Adam, nisikilize basi.”

    Alimfuta rafiki yake kipenzi ambaye naye alionyesha kumchunia wakati huo.



    “hakuna kisichojulikana Abdul, hivi una masikio yaliyokufa useme kuwa hayasikii dawa?,,, umekuwa kama nazi. Una macho matatu lakini huoni… nakuhurumia rafiki yangu.” Aliongea Adam huku akionyesha wazi kuwa alikua anaongea kwa hasira.



    “najua mtanifikiria vibaya, ila situation yenyewe hata mimi mwenyewe nashindwa kutambua ilikuaje mpaka nikalala nje ya kambi. Sijawahi kufanya hivyo hata siku moja. Naweza sema nilikabidhiwa jezi na mchezo sijauelewa” Alijitahidi kujitetea abdul.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “hivi unajua kuwa hapa bongo na popote uendapo u super star ulionao upo mikononi mwa Mr. Zungu. Unafikiri akigundua kuwa hujalala hapa kambini kwakua ulikua una mechi na mtoto wake tena ampendaye kwa dhati. Ni kipi atakachokufanya wewe.???” Aliongea Adam na kumuangalia Abdul ambaye mpaka wakati huo alikuwa mdogo sana na hakujua nini kilichomfanya mpaka kukubali kulala nje ya pale.



    “kwani kajua kuwa sijalala hapa?” aliuliza Abdul kwa mshangao.



    “huo ndio ukweli wenyewe. Alikuja usiku wa saa nne kutupa ratiba ya sherehe ya harusi ambayo imetualika katika kutumbuiza nyimbo yetu ya harusi. Ndio akakuulizia, hakuna aliyejibu ni wapi umeenda. Ila kiukweli Mr. Zungu amekasirika kwa kitendo cha wewe kutoonekana kambini mpaka mida ile.” Aliongea Adam na kumuacha Abdul akiwa amejishika kichwa kuashiria kuwa taarifa zile zilimchanganya.



    Saa tano asubuhi, gari ya Diana ndio ilionekana nyumbani kwao. Aliposhuka tu kwenye gari, alimkuta Mr. Zungu akiwa nje na yeye akielekea ofisini kwake.



    “ulikuwa wapi mwanangu toka jana, halafu umeanza lini tabia ya kulala nje ya nyumba hii??” aliuliza Mr. Zungu kwa hasira kiasi kwakua hakupenda kumuudhi mtoto wake huyo.



    “jana nilikuwa kwenye party ya partnership huko Kibaha. Ndio maana nikaona nilale kabisa tu kwakua hiyo sherehe ilichukua muda mrefu sana na kuisha saa saba usiku… sorry Dady.”

    Aliongea Diana na kumfuata Mr. Zungu na kumkumbatia.

    “sasa huyo Partner wako alikuwa nani?’ aliuliza Mr. Zungu huku akionyesha wazi kuwa hasira zake zilikua zimepoa wakati huo.



    “ABDUL!”



    Jina hilo lilikita katika ubongo wake haraka Mr. Zungu na kumkumbusha kuwa kweli Abdul hakuwepo mpaka usiku wa saa nne alipoondoka yeye mida hiyo kule kambini.

    Hakujibu chochote zaidi ya kwenda kwenye gari yake na safari ya kuelekea ofisini kwake ilanza.



    Njia nzima Mr. Zungu alikua anawaza na kukasirika sana kwa kitendo alichokifanya mwanaye kutoka na msanii wake. Alienda ofidsini kwake. Hakuna alichoweza kukishika kutokana na hasira.



    Wakati anarudi kazini. Mr.Zungu alilaani sana baada ya fikra za kiusaliti kumjia kuwa Abdul itakuwa alilalal na mtoto wake usiku kucha. Alisonya kila wakati huku akiupiga piga usukani wa gari yake kwa hasira.



    Safari iligota kwenye geti la kambi ya bendi ya Dreams. Alishuka kwa hasira na kuingia ndani ambapo aliwakuta wanakikundi w ote wakiwa wanafanya mazoezi.



    Alimiuita Abdul kwa hasira na vyombo vyote vya mziki vilivyokuwa vinasikika hapo kabla vikazimwa.

    “njoo ofisini, muda huu.”



    Maneno hayo yaliwashangaza kiasi wafanyakazi wenzake ambao walijua fika kuwa Mr. Zungu atakuwa na hasira kwa kitendo cha Abdul kwenda kulala na mtoto yake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Abdul alipiga moyo konde na kuelekea ofisini alipoitwa na Mr.Zungu

    “unaweza kunipa sababu tatu muhimu zilizokufanya jana ukalale nje ya hii kambi?”



    Abdul alikutana na swali hilo ambalo lilimuacha katika njia panda.

    “hujaelewa swali au huna majibu ya kunipa?” aliuliza Mr.Zungu huku akiwa amejawa na hasira.

    Abdul hakujibu kitu zaidi ya kunyamaza na kumuangalia tu Mr.Zungu.



    “najua ni kwa jinsi gani umekua na hivi sasa una jina kubwa sana hapa nchini na nje ya nchi. Lakini kwangu mimi hivyo vyote naweza kuvizima kama vile niwezavyo kuzima moto kwa maji. Najua kwaninin hutaki kuniambia ulikua wapi jana kwakua umejua nitakuuliza kuwa ulikua na nani?.... hakuna mtoto niliyetokea kumpenda kama wewe, ila kwa sasa ni mtoto anbaye hata kukuona tu napatwa na hasira kubwa. Wewe hadhi yako ni vinyang`au vinavyokushobokea uwapo jukwani ukiwa unaimba. Na sio mwanangu mimi. Nikikuuliza kuwa kwanini uliamua kutoka na mwanangu utakua na jibu la kunipa?” aliongea Mr.Zungu huku akiwa ameyatoa macho yake yaliyoanza kuwa mekundu kutokana na hasira.



    “kusema ukweli alikuja kunifuata mwe….”



    Kabla hajamalizia kauli yake, alikutana na kofi zito lilitua sawia shavuni kwake na kumfanya ayumbe kidogo.”



    “pumbavu…. Unaniongelea uozo gani hapa??... angekuambia kula mavi ungekula??... sasa nakuambia hivi, kuazia sasa nakatisha mkataba na wewe, na nakunyang`anya kila kitu nilichokupa. Kuanzia nyumba , gari na kila kitu chenye sign yangu. Na kamwe hutasikika katika ulimwengu huu… utaishia kuimba kwenye mabaa tu shenzi wewe.” Aliongea Mr. Zungu na kutoa bahasha kwenye mkoba wake na kutoa karatasi kubwa yenye maandishi na kumuamuru Abdul asaini.



    Abdul alibembeleza sana kwa Mr.Zungu huku machozi yanamtoka, lakini Mr. Zungu alikataa katu katu.

    “tena unavyoendelea kukaa hapa naweza kukupiga risasi.. saini na utoke.” Aliongea Mr.Zungu kwa ukali.



    Abdul hakua na jinsi. Alianguka saini yake na kutoka ofisini huku sura yake ikiwa imejawa na huzuni huku mashavu yake yakiwa yamelowa machozi ambayo alikua analia mpaka muda huo. Wenzake walimuangalia kwa huruma. Walijua kuwa ni mazito yaliyompata mwenzao.



    Baada ya dakika kumi, alitoka Abdul akiwa na mizigo yake kiasi na kuwaangalia wenzake kwa huzuni. Kila mmoja alibubujikwa na machozi kuondoka kwa kinara wao waliyempenda sana.



    Aliwaaga kwa kuwambatia kila mmoja. Alipofika kwa Sapna, hakuna aliyeweza kuvumilia kuirihusu sauti yake ya kilio cha uchungu kutokea.

    “nakupenda Sapna… mungu akipenda tutakuja kuonana tena.”



    Hayo ndio maneno aliyoyaongea Abdul na kuondoka kwenye ile kambi na kwenda kuanza kuishi maisha mapya kabisa huko ambapo hata yeye hakujui.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hela kidogo alizokuwa amezihifadhi benki zilimsaidia kupata chumba na kununua vitu muhimu vya ndani. Kwakua mziki ndio kipaji chake, aliamua kurecord nyimbo yake na kuipeleka katika vyombo mbali mbali vya matangazo.



    Cha ajabu miezi ilipita bila nyimbo yake hiyo kusikika hata mara moja. Ndipo aliamini kuwa Mr.Zungu atakuwa ameenda kuhonga fedha katika media zote ili yeye asisikike tena.



    Kutokana na elimu yake kuwa ndogo, hakuweza kupata kazi sehemu yoyote iliyokuwa inaendana na hadhi yake pamoja na jina lake. Zaidi alitumia pesa alizokuwa nazo na baadae zilianza kumuishia kwakua alikua anatumia bila kuingiza chochote.



    Mawazo ya kushindwa yalimjia kwa kasi, lakini aliamini kuwa hiyo ni mitihani tu ya mungu na kupambana ndio uanaume.



    Kiasi kigogo alichokuwa nacho akaamua kwenda kununua gitaa huku akiamini kuwa muziki utamuendeshea maisha yake na kumnyanyua yeye kama yeye kwa njia yoyote hata kama media zote zilimkataa.



    Siku moja aliamua kwenda maeneo ya coco beach akiwa na gitaa lake. Alichukua kiti kimoja kilichokuwa kwenye ile baa na kukaa katikati kwenye uwanaja ambao kwa kwakati huo ulikua una watu wachache. Akaa na kuanza kulikung`uta gitaa lake kwa hisia kali yenye kuhuzunisha. Na baadae sauti nyororo ilifuatiwa ikiwa inaimba nyimbo iliyoendana na ala za muziki zilizokuwa zinasikika pale.



    Mvuto wa sumaku uliwavuta watu kutoka kila pande na kuwakusanya pale na kuweka duara. Umati ulizidi kuongezeka na kufanya lile jambo kuwa ni tukio kubwa lenye mvuto.

    Waliomjua walimshangaa kwa kutoa burudani ile bila ratiba wala kiingilio. Ila ambao hawakupata nafasi ya kumuona live, walibaki wanashangaa tu uwezo wa msanii huyo.



    Baada ya kuimba kwa hisia hiyo nyimbo iliyowateka wengi pale, alinyanyua shingo na kuangalia umati uliokuwa pale na wote kwa pamoja wakampigia makofi. Bila kuambiwa, watu ziliwatoka hela mifukoni na kumrushia Abdul.



    Tukio hilo lilimpa hela nyingi kiasi na kumfanya aifurahie I dea yake. Baada ya kuokota hela zake zote, aliponyanyua shingo kuangalia mbele, alikutana na mtu mnene kiasi aliyevalia suti ya rangi ya kijivu akiwa amesimama mbele yake.



    :habari yako kijana.” Alisalimia yule mtu na kumuangalia Abdul.

    “salama tu.” Aliitikia Abdul huku akiwa na mashaka kiasi na mtu huyo.

    “nimekutafuta kwa muda mrefu sasa, na leo kama bahati nimekuona hapa. Nilikua nina issue na wewe. Kama utakubali basi tutapeana mkataba mnono.” Aliongea yule mtu aliyekuwa ameninginiza dhahabu shingoni kama anamiliki mgodi mererani.



    “issue gani hiyo.” Aliuliza Abdul kwa shauku ya kutaka kujua kitu hicho.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “mi ninamiliki kampuni ya fashion designer. So mwili wako na jinsi nguo ziklivyokuwa zinakukubali kila nikikuona ndivyo vimenishawishi kukutafuta.” Aliongea yule mtu na kumfanya Abdul atabasanu moyoni.



    “tunaweza ongea biashara.” Aliongea Abdul na kumfanya yule mtu atabasamu.

    “nashukuru sana kijana, chukua business card yangu hii, tukutane kesho asubuhi ofisini kwetu posta kwenye jingo la uchumi ghorofa ya saba. Fika pale mapema ili tupeane huo mkataba.” Aliongea yule mtu na kumpa mkono wa heri Abdul aliyekuwa amepigwa na bumbuwazi kwa zali lililompata.



    Saa moja kamili juu ya alama, tayari Abdul alishafika posta eneo aliloelekezwa. Alikiangalia kile kikaratasi alichopewa na kusomeka jina la Alvin Rojas.



    Aliingia ndani na kupanda lifti mpaka ghorofa ya saba. Aliona jina na logo iliyojitokeza kwenye ile business card na kujiridhisha kuwa ni pale alipoelekezwa.

    Aliulizwa maswali mawili matatu na mlinzi na baadae aliruhusiwa kuingia ndani.



    Alilazimika kukaa kwenye chumba cha wageni kwa sababu bosi huyo alikua bado hajafika.



    Ilipofika saa tatu, alikuja kuitwa na kuruhusiwa kuingia katika chumba cha bosi huyo ambaye ndio alikua ameingia mida hiyo.



    Alifika ndani na kukutana na bosi huyo aliyempokea kwa furaha, alikaa chini na kuanza kuongea maswala yao ya kupeana hiyo mikataba kwa ajili ya kazi ya kutangaza kazi za Mr. Alvin Rojas.



    Waliongea mengi na baadae Abdul alipewa mkataba akaupitie na kupewa siku mbili kutoa majibu na kuanguka saini yake pale.



    Alirudi nyumbani na ule mkataba ambao ulikua unaonekana ni neema tosha kwake. Allifika chumbani kwake na kujitupa kitandani na kuusoma mkataba huo kwa umakini mkubwa.



    Sheria zote zilizokuwa pale hazikuwa na shida kwake, ila mshahara ambao atakuwa analipwa kwa mwezi ndio uliomfanya asiamini akionacho pale.



    “ 2.5 milions…..ooohsh, thenks allah”



    Alishukuru Abdul baada ya kupewa ofa hiyo kwa mwezi ambao ulikua una marupurupu kibao na posho za siku zikiwa pembeni. Alifurahi sana na kuona hiyo siku ya kurudisha huo mkataba ilikua mbali



    Siku ya kurudisha mkataba ilifika na Abdul kama kawaida yake alikua anazingatia swala lake la kuwahi. Alienda mapema na kumsuburi Mr. Alvin.



    “nategemea majibu mazuri kutoka kwako.” Aliongea yule bosi baada ya kusalimiana.

    “ni kweli usemacho.” Alijibu Abdul huku anatabasamu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “thenks… leo tunavyoongea ndio umeshaanza kazi. Nitakupa kiasi cha fedha kwa ajili ya kujikimu kwa nusu mwezi na baadae nitakuongeza nyengine. Mchana atakuja mwalimu kwa ajili ya kukufundisha steps. Maana kesho nina maonyesha ya mavazi Mlimani City na naamini itakuwa mshangao kwa watu waliokuzoea.” Aliongea Mr. Alvin na kumuangalia Abdul ambaye muda wote alikua anafuraha ya ajabu.



    Baada ya masaa kadhaa, alifika mwalimu aliyeambiwa Abdul kuwa atakuwa anamfundisha kila kitu kuhusiana na kazi yake siku hiyo kwa ajili ya kupita usiku wa siku inayofuata mkatika maonyesho hayo ya Fashion show.



    Bidii na maarifa aliyokuwa nayo Abdul, yalimuwezesha kukamata haraka kila alichokuwa anafundishwa na mwalimu wake. Hali hiyo ilifanya zoezi lao kuisha mapema.

    Siku ya pili yake kazi ilikuwa ni ndogo tu kurudia yale waliyoyafanya jana na kumuongezea baadhi ya pozi ambazo jana yake hawakuzifikia.



    Usiku huo ulifana sana kwa ubunifu wa hali yajuu. Wabunifu kutoka nchi mbali mbali za Afrika walikua wanaonyesha kazi zao pale.

    Ilipofika zamu ya mbunifu Alvin, basi umati wote ulipiga makofi kwakua walikua wanajua kuwa kazi zake zilikuwa za pekee na zisizotabirika.



    Watu walipigwa na butwaa na kujikuta wanangeza makelele na vifijo baada ya kumuona Abdul akiwa amepanda na nguo zilimtoa kipekee sana. Mapozi na tabasamu murua ambalo kwenye muziki walikuwa wanalikosa ndio lilizidi kuwauwa wanawake waliohudhuria pale.



    Tukio hilo lilimfurahisha Alvin na kujiona kuwa alikua ana kila sababu ya kujisifia kumuajiri mrtu aliyekuwa anamuota kila siku.



    Muda wa kuendelea kukaa nchini Tanzania uliisha na Diana akaruka na kuelekea ulaya kumalizia elimu yake ya juu. Tukio la kuacha kuimba kwa Abdul lilimsikitisha sana Diana. Hakujua kuwa baba yake ndio chanzo, ila matangazo ya kwenye media mbali mbali yalikua yanamuelezea mwana muziki huyo wa kundi la Dreams alivyoamua kukacha mziki na kuingia katika fani nyengine.



    Siku waliyolala wote kule hotelini, ndio ilikuwa siku ya mwisho kumtia machoni mvulana huyo aliyejikuta amempenda ghafla.



    Mr. Zungu alifurahi sana tukio la mtoto wake kwenda chuoni bila kuonana na Abdul. Aligharimu pesa nyingi kumchafua Abdul kila awezavyo. Alibana media zote kupiga nyimbo zake atakazozileta pale.



    Skendo zinazoendelea kusikika katika radio mbali mbali nchini zilimfanya Abdul kuanza kuchukiwa na watu wasioujua ukweli juu yake na huyo bosi wake.



    Abdul hakujibu chochote hata baada ya kuhojiwa na waandishi wa habari kadhaa aliogumiana nao na kumfuata kwa ajili y a kumuuliza juu ya ukweli wa skendo zinazoendelea kusikika.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “kinachoongeleka kila kona ya jiji hili… kuna ukweli ndani yake?” aliuliza Alvin baada ya kumuita Abdul na kumuwekea kikao cha watu wawili.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog