Simulizi : Let Me Die
Sehemu Ya Nne (4)
“kaka, hakuna cha ukweli hata kimoja kati ya ulivyosikia na unavyoendelea kusikia. Sijawahi kumtukana Mr. Zungu hata siku moja. Nilikua namuheshimu mpaka sasa naendelea kumuheshimu sana. Sema ukweli anauficha na ni kumdhalilisha kama ukweli halisi utabainika. Kwa sababu kosa nililolifanya ni kutokuwepo kambini siku moja na kwenda kumsindikiza mtoto wake hotel. Bila shaka aliamini kuwa natembea na mtoto wake ndio maana akaamua kunifukuza na kuninyan`ganya kila kitu kilochokuwa pale. Ingawaje kuna jasho langu pale. Nimeamua kuacha haki zangu zote pale na kuamua kuanzisha maisha yangu tena katika hali ya chini kabisa. Nashangaa bado ananifuatilia na kunikandamiza ili nisiweze kunyanyuka tena…..lakini yote hayo ni hisia tu kuwa natembea na mtoto wake ndio ameamua kunichukia kiasi hicho.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliongea Abdul kwa hisia na uchungu mkubwa juu ya taarifa zile mbaya zinazoendelea kumchafua kila siku.
Kwakua Alvin ailikua muelewa, alimuelewa Abdul na kumuahidi kuwa naye bega bega . alijua kabisa kua kutokana na sababu aliyoelezewa na Abdul ni lazima watu wazito kama wale ni watakupoteza kwa njia yoyote.
Matamasha mballi mbali yaliyofanyika ndani na nje ya nchi, Abdul aliwakilisha vizuri sana. Mwili wake ambao ulikubali kila nguo, ulimfanya mbunifu huyo wa Mavazi kujinyakulia tuzo mbali mbali.
Siku moja wakati maonyesha yakiendelea, alitoka ndani na gitaa lake na kuamua kutumbuiza nyimbo yake mpya iliyopendwa na kila mmoja wapo aliyehudhuria tamasha lile.
Kutokana na kukosekana kwa mtunzi mzuri na mtu aliyekua anawatia moyo na kuwapa mawazo mapya, kundi la Dreams lilianza kufifia taratibu. Kila show waliyofanya, watu walikua wanalitaja jina la Abdul. Baada ya nyimbo zao za zamani kuchokwa, walijitahidi kutunga nyimbo mpya ambazo hazikuwasaidia kunyanyuka. Zaidi ziliwashusha na kupoteza mashabiki kila siku kwakua waliamini kuwa hawakua na jipya tena.
Kutokana na utendaji mbovu wa bendi hiyo, Mr. Zungu aliamua kuisambaratisha na kila mmoja akamfukuza na aendelee na maisha yake.
Mashindano ya mavazi yaliyofanyika nchini Kenya yalimuibua kidedea Alvin na kuingia katika mashindano ya Afrika yaliyofanyika nchini Afrika kusini. Hata hayo mashindano waliibuka kidedea na kufanya majina yao kupaa na kujulikana Africa nzima.
Kwakua mziki ndio sehemu ya maisha yake, hakuupiga kikumbo. Aliachia nyimbo yake kama solo artist akishirikiana na kundi la Mafikizolo. Nyimbo hiyo aina ya kwaito ikishirikisha lugha mbili. Kiswahili na kizulu. Ilikua kivutio sio bara hili tu. Hata ulaya na Asia walitokea kuikubali nyimbo hii na ziara za kutembelea nchi mbali mbali kwa ajili ya kupiga show ziliwafikia.
Uwezo wake wa kupiga vyombo vya muziki ulikua kivutia kingine. Maana Abdul kila baada ya kumaliza Show yake alipanda upande wa drums na kuanza kuzitandika kisawa sawa na kuwafanya watu wapendao michezo hiyo kupagawa sana na yeye.
Ziara ya miezi mitatu zilizofanyika nchi mbali mbali duniani, zilimuingizia fedha nyingi Abdul.
Aliporudi nchini Tanzania, alipokelewa kama rais na wananchi. Watu walijaa uwanja wa ndege na kujipanga katika bara bara kwa ajili ya kumuona shujaa huyo aliyeipeperusha vizuri bendera ya Tanzania huko nchi za ughaibuni.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Abdul alipanda gari la wazi na kuwaopungia mikono mashabiki wake waliokuwa wamejaa pembeni ya barabara wakimfurahia. Kuna wengine walibeba mabango mbali mbali ya kumpongeza na wakina dada nao walivaa nguo mbali mbali zenye maandishi ya kumuonyesha ni jinsi gani walikua wanamzimia.
Sapna nae alikuwepo katika lile kundi la watu wengi. Yeye alikua anashida nae sana ya kumuona. Alimuita sana Abdul lakini sauti yake ilimezwa na sauti za watu waliokuwa wakipiga makelele kumshangilia Abdul.
********************
Kutokana na kutoonana na Abdul kwa muda mrefu, Diana aliamua kumpigia simu na kumuambia baba yake kua alitaka kurudi Tanzania hata ikiwezekana aje amalizie elimu yake huku kwakua tu alitaka kuongea na Abdul na ikiwezekana ndoa ipite kati yao.
Baba yake alimpiga marufuku kabisa kulitaja jina hilo kwakua alikua haitaji kabisa kulisikia masikioni mwake. Alimfokea sana mtoto wake huyo ambaye hakuwahi hata siku moja kumfokea hivyo toka alipozaliwa mtoto wake huyo aliyekuwa anampenda kupita kiasi.
“kwanini baba?... mimi nampeda.” Aliongea Diana huku analia.
“wanaume wapo wengi tu wenye hela na msimamo kuliko huyu. Hivi unajua ni kiasi gani anavyoweza kubadilisha idadi ya wasichana kwa siku?... umalaya aliuanza hata kabla hajawa staa. Unafikiri hivi sasa ni nani atamzuia wakati ana hela ya kununua wasichana zaidi ya wanne wenye nyota tano kwa siku?.. sihitaji mwanangu unidhalilishe kwakua na yule mtoto aliyelelewa katika mikono yangu na kufundishwa kwa hela zangu.” Aliongea Mr, Zungu na kumfanya mtoto wake amuelewe kwa singo upande.
Uzuri wa Diana uliwavuta watu wengi wa hapo chuoni, ila ni kijana mmoja tu ndio alipata bahati ya kukubaliwa na yeye na kuanzisha mahusiano ya kimapenzi baada ya kukatazwa na baba yake juu ya ndoto zake za kuwa na Abdul ambaye alimwagiwa sifa mbaya kede kede alizokuwa anzifanya.
Walimaliza chuo na uongozi wa chuo hicho kikaamua kumuita msanii kutoka nchini Tanzania ili awa burudishe katika Bash ya chuo hicho.
Posters za Abdul zilibandikwa na wanachuo wote waliufurahia ujio huo kuliko baadhi ya wasanii waliowazoea kutoka nchini kwao.
Kwa Diana ilikua furaha mara mbili yake. Alimkumbuka sana Abdul japokuwa kwa muda huo alikua katika wakati mgumu wa kumtoa moyoni na kumuweka huyo mtu aliyekuwa naye kwa sasa.
Siku ya siku ilifika na chuo walifika katika ukumbi huo wa kimataifa uliochaguliwa kufanyika shoo hiyo kubwa ya kufunga mwaka wa chuo hicho.
Watu wachache walitulia kwenye viti, ila wengi walimwagika katika dancing floor zilizo tawanyika sehemu zipatazo nne katika ukumbi ule mkubwa uliokuwa kati kati ya jiji.
Masaa yalikatika na wasanii wazawa wa nchi ya Marekani walianza kutumbuiza na kushangiliwa sana huku baadhi ya wanafunzi wakiimba nyimbo hizo walizokuwa wanazijua vizuri.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Usiku ulipokua mkubwa, ndipo yule aliyekuwa anasubiriwa kwa hamu alitangazwa kua ilikua zamu yake kuingia jukwaani.
Taa zote zilizimwa na sekunde kadhaa walianza kusikia sauti ya Abdul live ikichombeza kwa kuimba kipande cha nyimbo yake pendwa. Watu wote walishangilia na kupiga makelele sana.
Taa ziliwashwa na Abdul akaonekana akiwa na wacheza shoo wake wapatao nane wakiwa wamevalia sare kasoro yeye ambaye alitofautiana nao rangi tu.
Kabla hajaanza kuimba, kwanza walianza kucheza style ambazo wamerekani hawajawahi kuziona hapo kabla na kuwafanya wachizike kwa kushangilia hata kabla hajaanza kuimba.
Baada ya kucheza kwa muda, walitulia na Abdul akaanza kuimba nyimbo zake pendwa. Hakika wazungu waliburudika sana japokuwa lugha iliyotumika walikua hawaifahamu.
Baada ya show hiyo, Abdul alipelekwa kwenye hotel kubwa yenye hadhi ya nyota tano. Huko alikutana na waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbali mbali vya nchi hiyo na kumuhoji maswali mawili matatu.
Asubuhi ya siku inayofuata, Abdul alisindikizwa na mashabiki wake mpaka uwanja wa ndege. Diana nae alikua miongoni mwa watu waliokua wakimsindikiza Abdul. Moyo wake ulimuuma sana kwakua ndoto zake zote zilikua ni kuishi na mwanaume huyo.
Safari ya kurudi Tanzania ikaanza huku mashabiki wake wakimpungia mkono Abdul kama ishara ya kumuaga.
Hali ilikua kama alivyoondoka. Maana show yake ilirushwa live DSTV. Watu wengi walijitokeza kumpokea Abdul. Wengine walijipanga barabarani kama kawaida yao ili mradi tu waweze kumuona.
Ahadi yake Abdul ya kuandaa show ya bure itakayowahusisha watoto yatima wote watakao pata nafasi ya kuhudhuria, aliitimiza kwa kupiga show hiyo kali ya mchana iliyopigwa katika uwanja wa taifa.
Watoto waliohudhuria pale walifurahi sana. Hata watu wengine waliokua wanaangalia show nyumbani, walifarijika na kuburudika na show hiyo ya ajabu iliyoandaliwa kwa gharama za Abdul na kushirikisha wasanii wapatao thelathini wa hapa Tanzania na sita kutoka nchi mbali mbali za Afrika.
Jina la Abdul lilikua kila siku iendayo kwa Mungu. Kila mtu alitamani apate japo sihihi yake. Wengine walitamani hata kumshika mkono tu kutokana na kumpenda mtu huyo.
Magazeti yameandika mengi sana kuhusu mwanamuziki huyu na mwanamitindo ambaye mpaka muda huu hajaweka wazi mahusiano yake. Yaani ilisemekana hakua na hata rafiki wa kike anayetambulika au aliyemtambulisha kwa watu.
Hilo liliumiza vichwa vya watu wengi na wakaamini kuwa labda alitingwa sana na kazi au mazoezi hivyo swala la mapenzi halikua kichwani mwake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hilo swala pia lilimpa moyo Sapna akiamini kuwa labda kuna ukweli kuwa toka alivyomtamkia siku ile kuwa alikua anampenda yeye. Ndio alikua anamsubiri ajitokeze.
Maisha ya Sapna yanakua magumu siku hadi siku baada ya ndoto zoa kuzimwa kama mshumaa na Mr. Zungu.
Kundi hilo lilisambaratishwa huku kila mmoja kutokua na haki hata ya kumiliki gari walilonunuliwa kutokana na kazi walizomfanyia Mr.Zungu.
Waliojaribu kuleta mdomo au kudai haki zao, waliishi muda mfupi sana. Waliuliwa kwa hila na kesi zao ziliishia polisi na hakuna aliyechukuliwa hatua kwa unyama huo waliotendewa na Mr.Zungu ambaye hawakumtarajia kuwa angekuja kubadilika na kuwa na roho ya kinyama kiasi kile.
Hila za mwenye hela humuumiza zaidi mdai haki. Na haki hupindishwa kwa wenye madaraka kwa sababu wote wanamilikiwa na wenye hela.
Masikini hujikuta anapoteza mpaka uhai wake kwa kugombania kitu ambacho ni haki yake kukipata bila hata kutumia nguvu.
Uoga wa watu wachache kama aliokuwa nao Sapna, ndio ulikua salama yao. Kwani wao waliondoka mikono mitupu. Walifaidika na fedha kidogo tu walizojiwekeka wenyewe kwenye account zao benk. Fedha ambazo ziliwawezesha kupanga vyumba tu maeneo ya kinondoni na nyingine kama msingi wa biashara ndogo ndogo.
Jina la bendi ya Dreams lilifutika katika ramani ya muziki na kubebwa na mmoja aliyekuwa kichwa katika bendi hiyo. ABDUL.
Siku moja Abdul alirudi katika kituo cha kulelea watoto yatima na kuomba kama kuna uwezekano wakupata picha zake za utotoni kwa sababu alikua ana shida nazo katika Docomentary ya maisha yake aliyokua anataka kuitengeneza.
Alifanikiwa kuzipata picha kadhaa alizozifurahia sana.
Maandalizi ya documentary hiyo yalianza mara moja baada ya kukusanya picha hizo na picha zake za sasa kuanzia alipokua kwenye kundi mpaka alipokuwa mwanamitindo.
Aliifanya kazi hiyo kwa ustadi mkubwa na kuuza nakala zake zilizonunuliwa kama njugu. Katika Docomentary hiyo alizungumzia pia safari yake ya mapenzi. Alimtaja Diana kama msichana wa kwanza aliyemtongoza mwenyewe kitu ambacho wasichana wengi hawawezi kufanya hivyo. Pia alizungumzia maisha yake na Sapna. Msichana aliyekua anampenda muda mrefu na kudiriki kumwambia. Lakini walikuja kutengana hata kabla hajakubaliwa ombi lake.
Kwa sasa hivi alionyesha wazi kuwa ameyaweka pembeni mapenzi na anajalali kazi zake kuliko kitu chochote.
Documentary hiyo ilisambaa sio katika bara hili la Africa tuliopo tu. Bali ilisambazwa nchi nyingi alizowahi kuzitembelea na kumfanya azidi kujiongezea utajiri.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nakala ile ilitua mikononi mwa Diana na kumfanya alie sana baada ya kugundua kua tukio lile la kwenda nae hotelini ndio lilisababisha yote yale yatokee. Alijikuta anamlaumu sana baba yake kumdhalilisha na kumchafua kijana wa watu ambaye alimuhukumu kwa makosa aliyoyafanya yeye mwenyewe.
Kwa Sapna ilikua ni kilio baada ya kugundua upendo wa dhati aliokuwa nao Abdul kwake. Alitamani siku zirudi nyuma na amtongoze tena ili apate kumjibu siku hiyo hiyo.
“NAKUPENDA PIA ABDUL”
Aliongea kwa uchungu Sapna huku akimgusa Abdul kwenye Tv. Kauli yake ilisikika na yeye mwenyewe peke yake kwakua hakukua na mtu mwengine. Roho ilimuuma sana na kujilaumu kwanini asingeanza yeye kusema labda ingekua hadithi nyengine kati yake na Abdul.
Masikitiko yake yalikua sawa na bure, kwani mpaka sasa Abdul alijitangaza kufunga kabisa jalada la mapenzi na kumchagua mziki kuwa demu wake wa maisha.
Kwa msaada wa mwenyekiti, nakala ilifika mpaka Mbeya kwenye kijiji alichozaliwa Abdul.
Wanakijiji walipoziona picha za Abdul wakati akiwa mdogo, walimtambua na kwenda kuwajulisha wazazi wa Abdul ambao kwa sasa walishazeeka.
Wazee hao walifika mpaka kwa mwenyekiti na kuwekewa Docomentary hiyo ya maisha ya Abdul. Walijikuta wanalia na kukumbatiana baada ya kuona taswira halisi ya mtoto wao huyo wakati alipokua mdogo. Kilio hicho cha uchungu kilichochanganyika na furaha kiliwafanya watu wote waliokuwa pale na wao kudondosha machozi bila kutoa sauti huku wakijaribu kuwatuliza wazee hao waliokua wanalia kwa sauti kubwa.
Waliwatuliza wazee hao na baada ya muda walinyamaza kulia. Mwenyekiti aliamua kuita kikao cha dharura kijijini hapo na kuwatangazia harambee ya kuwachangia wazee hao fedha ili waende kumtafuta mtoto wao.
Kwakua kijiji hicho kilisifika katika kusaidiana. Hawakua na hiyana zaidi ya kuchangia zoezi hilo lililofanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Aliwakabidhi wale wazee fedha zao na safari ya kuelekea Dar kwa ajili ya kumtafuta mtoto wao ambae kwa sasa ni gumzo hapa jijini ilianza siku mbili baadae.
Waliikanyaga ardhi ya Dar kwa mara ya kwanza. Walichagua nyumba ya kulala ya bei rahisi na mara moja wakaanza kazi ya kufuatilia na kuulizia sehemu anayoishi mtoto wao.
Iliwagharimu wiki nzima bila mafanikio. Ndipo mtu wa karibu na Abdul alipokutana na wazee hao na kuwafahamisha mahali ambapo Abdul anaishi.
Walifika kwa msaada wa mungu kutokana na maelekezo waliyopewa. Waliishia getini kwakua mlinzi aliwaambia kua wasikaribie eneo hilo.
Walikaa nje ya nyumba hiyo kwa masaa yapatayo matatu. Ndipo wakaona gari aina ya range nyekundu ikiingia mule ndani. Walisimama na kumuangalia dereva wa gari hiyo. Walimgundua kua alikua ni Abdul.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walisikitika kwa kutomuona mapema. Walirudi getini na kuomba uwezekano wa kuonana nae, walikataliwa katu katu na wao wakaamua kuondoka zao.
Siku ya pili yake, walirudi mapema na kukaa nje mpaka walipoiona gari ya Abdul ikitoka tena mida ya saa tano. Walitoka na kuisimamisha hiyo gari ambayo ilisimama na kioo cha gari hiyo kikaanza kushuka taratibu. Hakua mwengine aliyeonekana pale zaidi ya Abdul aliyekua peke yake kwenye gari hiyo.
Abdul aliwasikiliza wazee hao ambao walimuomba kua walikua wanahitaji kuongea nae. Aliwapa appointment na kuwaandikia memo itakayowaruhusu kuingia nyumbani kwake siku inayofuata.
Waliondoka kwa furaha kidogo wazee hao na kurudi nyumba ya wageni ambapo kulikua ndio makazi yao kwa sasa. .
Siku ya pili yake ndio siku waliyoambiwa kua atakua na muda wa kutosha wa kukaa nae na yupo tayari kuwasikiliza shida zao.
Walifika bila kukosa na bila kuchelewesha muda. Kile kikaratasi kilichokua na muhuri na sahihi ya Abdul. kiliwafanya wapite safari hii bila usumbufu. Walikutana na wafanya kazi kadhaa waliokua wamevaa sare wakiendelea na majukumu yao. Alikuja mtu na kuwapokea. Huyo dada aliwafikisha wazee hao kwenye ofisi ya Abdul iliyokua ndani kwa ndani katika jumba lake hilo la kifahari.
Walifika na kukaribishwa vizuri. Walihudumiwa chakula na baada ya hapo Abdul aliwaruhusu waongee shida yao.
“baba, sisi tumetokea huko Mbeya vijijini. Ni wakulima na tuna mifugo kiasi. Dhumuni la kuja hapa si kwamba tunahitaji msaada wa fedha au matibabu kama wengi wananyokuja hapa kuomba msaada. Sisi tumekuja kukutafuta mtoto wetu. “ aliongea mzee huyo na kumeza mate. Abdul alishtuka kidogo kusikia habari kuwa yeye ni mtoto wao. Lakini akawa mstahimilivu ili azidi kuwasikiliza.
“miaka mingi sana yalitokea mafuriko huko mbeya na watu wengi walikufa lakini mtoto wetu ukapotea katika mazingira ya kutatanisha. Ingawaje kuna watu walinifuata na kuniambia kuwa ulizama na maji ya mafuriko. Kiukweli tulikata tamaa ya kukutafuta kutokana na kisanga hicho kilichotupata. Mpaka sasa unavyotuona, mungu hajatupa mtoto mwengine ila tunamshukuru pia kutuonyesha wewe ambaye siku nyingi tulikua hatufahamu kwamba ndie wewe uliondoka ukiwa na umri mdogo kabisa. Ule mkanda wa historia ya maisha yako ndio iliyowafanya watu wote kijijini kwetu kukutambua baada ya kuona picha zako za utotoni.” Aliongea huyo mzee kwa majonzi makubwa huku Abdul akiwa kimya muda wote akijaribu kumsikiliza mzee huyo.
“una ushahidi wowote ambao utanifanya mimi niamini kua nyinyi ni wazazi wangu?” hatimaye Abdul aliuliza swali hilo.
“tuna picha kadhaa tumekuja nazo. Ila kuna kitu nikikutajia lazima utaamni kua sisi ni wazazi wako.” Aliongea mzee huyo na kumfanya Abdul akae vizuri na kumsikiliza mzee huyo.
“ni kitu gani hicho ambacho kitanifanya ni waamini tofauti na picha zangu za utotoni nilizopiga nikiwa na nyinyi?” aliuliza Abdul huku akionyesha wazi kua mpaka wakati huo alikua haamini kua wale ni wazazi wake.
“juu ya hazina yako, kuna kovu la kushonwa nyuzi tatu na mgongoni una chale nne. Mbili zimekaa juu na mbili zimekaa chini kwa kufuatana.” Aliongea mzee huyo na kumfanya Abdul atoe macho. Hakuamini kua mambo yote hayo yule mzee aliyajua wakati hakuna ambaye alishawahi kumuona mpaka huko ambapo ilikua ni siri yake yeye mwenyewe.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alijikuta amesimama huku akionyesha wazi kua ile taarifa ilimchanganya sana aliwasogelea pale walipo na kuichukua bahasha ambayo huyo mzee alikua anataka kutoa picha alizokuja nazo. Abdul alianza kuzipitia moja baada ya nyengine. Alijikuta machozi yanambubujika tu baada ya kuona picha za pamoja akiwa na baba na mama yake. Aliamini kabisa kuwa hao ndio wazazi wake halisi ingawaje alilelewa katika kitua cha kulea watoto yatima.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment