Simulizi : Usilie Tena Geneviv
Sehemu Ya Nne (4)
SHED NO MORE TEARS GENEVIV
Baada ya kula chakula cha usiku, walimshukuru Mungu kama kawaida yao na kwenda kulala. Walijadiliana pia kama kuna umuhimu wa kumuongezea mashtaka Bwana Magafu baada ya kitendo chake cha kutaka kumfanyia kitu mbaya Geneviv.
“Mum we should forgive him, let the world teach him” (mama mi nafikiri tumsamehe tu, dunia ndio itayomfunza), aliongea Geneviv kwa upole na mama yake akamuunga mkono. Wakakubaliana kumsamehe na kutomuongezea kosa lingine la kutaka kumbaka Geneviv.
Usiku wa manane wakiwa wamelala, walianza kusikia mambo ya ajabu juu ya paa la nyumba yao. Paka wengi walikuwa wakicheza juu ya bati huku wakilia milio ya ajabu, wengine kama watoto wachanga huku wengine wakicheka kama watu.
“Mama!... mamaa!… hebu sikiliza huko nje…”
Geneviv alikuwa akimnong’oneza mama yake baada ya kusikia kelele za mapaka zikizidi kuongezeka juu ya paa la nyumba yao.
Kelele zile ziliendelea kwa muda mrefu sana huku pia sauti za milio ya bundi zikaanza kusikika na kupafanya pale nyumbani kwao patishe sana hasa ukizingatia kuwa ilikuwa ni usiku wa manane. Bi Patricia na mwanae waliamka wakiwa na hofu kubwa, wakachukua Biblia zao na kuanza kusali kwa kukemea kwa nguvu zao zote. Waliendelea kusali kwa muda mrefu huku kelele za mapaka nazo zikizidi kuongezeka.
Ilifika mahali ikawa ni kama vita kati ya nguvu za Mungu na nguvu za shetani. Baada ya kudumu kwa muda mrefu, hatimaye zile kelele zilitulia kwa muda, kisha vikaanza kusikika vicheko vya watu kutoka nje ya nyumba yao. Baada ya vicheko, ikaanza kusikika sauti ya mwanaume ikitoa amri kwa ukali. Ilikuwa ikimuamuru Bi Patricia kufanya chochote kinachowezekana kuhakikisha ndugu yao Bwana Magafu anaachiwa huru siku inayofuata la sivyo angekiona cha mtema kuni. Ujumbe ulikuwa mzito na mkali na ilionyesha dhahiri wamedhamiria kweli kuwafanyia kitu kibaya.
Wote walipigwa na butwaa baada ya kugundua kuwa kumbe kelele zile za mapaka, bundi na watu kucheka juu ya paa la nyumba usiku wa manane zilikuwa ni kwa sababu ya Magafu kufungwa jela. Walijikuta wakiingiwa na hofu kubwa kwani siku za nyuma katika enzi za uhai wa Mzee Rwakatare aliwahi kuwasimulia kuwa kijijini kwao kuna wachawi magwiji na walioshindikana na wengi walikuwa ni ndugu kutoka ndani ya ukoo wao mmoja. Walikuwa hawaaamini kwa sababu hawakuwahi kushuhudia kwa macho yao kama kweli kuna kitu kinaitwa uchawi, lakini kwa miujiza ya usiku huo, walijikuta wakiamini yale waliyokuwa wakiambiwa.
Pamoja na kukumbwa na hofu ya ajabu, lakini waliendelea kuomba na kusali kwa Mungu wao ili awaepushe na dhahama ile iliyokuwa mbele yao. Waliendelea kumlilia Mungu wao kwa muda mrefu na hatimaye zile kelele zikatoweka na kukawa kimya. Hata baada ya hali kutulia waliendelea kumwomba Mungu wao mpaka alfajiri. Hakuna aliyepata hata tone la usingizi.
“Mama hivi kumbe ni kweli ndugu zake baba ni wachawi? Basi tumwambie baba yake Kim wamwachie baba mdogo wasije kutudhuru kichawi, mi nawagopa sana wachawi” Geneviv alikuwa akiongea na mama yake baada ya kupambazuka. Yaliyotokea usiku ule yalitisha mno na yaliweza kummaliza Geneviv imani yake kabisa.
“Mwanangu hatupaswi kuuogopa uchawi kwa sababu Mungu wa Israeli yu pamoja nasi. Hatupaswi kuogopa kabisa kwani tukianza kuruhusu hofu ndani ya mioyo yetu tunaukaribisha huo uchawi utuingie vizuri. Tuzidi kumwamini Mungu kwani damu ya Yesu itatulinda kama alivyotuahidi kwenye vitabu vitakatifu.”
Maneno yale hayakumwingia Geneviv kwani aligopa sana uchawi kwa yale aliyoyashuhudia usiku. Aliona ni bora kumtoa gerezani baba mdogo wao na hata ikibidi kuwaachia nyumba waliyokuwa wanaitaka kuliko kuendelea kushindana na wachawi. Baada ya mazungumzo marefu alfajiri ile, Bi Patricia alianza kujiandaa kuelekea kazini kwake kama kawaida. Alimuacha Geneviv amelala. Wakati anatoka mlangoni, alikutana na mambo ya ajabu. Pembe za mlango zilikuwa zimepakwa vitu kama dawa za kienyeji halafu pale chini palikuwa na bahasha iliyofungwa ndani ya kitambaa chekundu. Palikuwa pia na shanga nyingi zilizomwagwa chini kuizunguka ile bahasha.
Bi Patricia alijikuta akiingiwa na hofu kupita kawaida. Ni kweli kwamba alikuwa akimuamini Mungu, lakini mambo yale aliyoyashuhudia yalimtisha sana. Alitamani kurudi ndani, lakini akapiga moyo konde na kuamua kutoka nje na kuviruka vile vitu pale mlangoni. Alipotoka alianza upya kusali kwa kukemea na kwa ujasiri wa hali ya juu aliichukua ile bahasha na kuanza kuifungua. Akiwa anaendelea kuifungua, akakutana na vitu vya ajabu. Ni ujumbe mzito kama ule aliousikia usiku wa manane, tena huu ukiwa umeandikwa kwa kitu kama damu kwenye karatasi nyeupe. Unazidi kumsisitiza kuwa asipofanya kama alivyoamriwa atakiona cha mtema kuni.
Alishusha pumzi ndefu na akajikuta mwili mzima ukitetemeka. Hata nguvu za kwenda kazini zilimuishia akabaki amekaa chini akiwa amekumbwa na hofu ya ajabu. Aliendelea kuwaza na kutafakari kwa makini nini cha kufanya. Aliona njia bora ni kwenda kwa mchungaji wake kuomba msaada zaidi wa kiroho kwani alianza kuona imani yake ikimezwa na hofu ya uchawi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Anakutana na mambo ya kishirikina yaliyotegwa mlangoni kwake, yote yakiwa yamefanywa kichawi kwa lengo la kuzidi kumtia hofu na kumshinikiza akamtoe haraka shemeji yake , Bwana Magafu gerezani. Anapatwa na hofu kuu na anajikuta akianza kuhaha kutafuta msaada. Lakini anapiga moyo konde na kuamua kumkimbilia Mungu wake amuokoe. Anapanga kwenda kuonana na mchungaji wake ili kumpa msaada wa kiroho wa jinsi ya kupambana na jaribu kali la kiroho lililokuwa linamkabili.
Anaamua kuahirisha kwenda kazini kwa siku hiyo na badala yake anafunga safari kuelekea nyumbani kwa mchungaji wake kumuelezea yaliyowatokea usiku kucha mpaka alfajiri ile. Anamuacha Geneviv akiwa bado amelala…
****
Bi Patricia alikuwa akitembea kwa haraka kuelekea nyumbani kwa mchungaji Edward Simkoko aliyekuwa akiishi ndani ya kanisa la Holly Spirit alilokuwa akiabudu. Japokuwa ilikuwa bado ni asubuhi sana, Bi Patricia alikuwa akitokwa na kijasho chembamba. Hofu ya uchawi ilikuwa ikizidi kuongezeka na kumtesa akilini kwa kadri muda ulivyokuwa unazidi kwenda na kumfanya akose kabisa amani ndani ya moyo wake. Alikuwa akiwafikiria ndugu zake jinsi walivyogeuka na kuwa kikwazo kikubwa kwake na kwa mwanae baada ya kufiwa na mumewe. Badala ya kuwa msaada kama alivyotegemea, wanageuka na kuwa sumu kali ndani ya maisha yao.
Zaidi alikuwa akimhofia mwanae Geneviv kwani endapo jambo lolote baya lingemtokea kama ndugu zake walivyokuwa wakimtishia, Geneviv angebaki bila msaada wowote kwani baada ya kifo cha baba yake, mama yake ndio alibakia kuwa mtu pekee mwenye msaada maishani mwake. Ndugu wote walikuwa wamegeuka na kuwa kama wanyama wakali wa porini, waliingiwa na tamaa ya mali na ubinadamu wakauweka pembeni.
Akiwa anakaribia kufika nyumbani kwa mchungaji, alianza kuhisi maumivu makali ya kichwa yaliyoambatana na kizunguzungu kikali. Alipga moyo konde na kuzidi kusonga mbele. Mara akaanza kusikia kama kelele za watu wengi wakicheka kwa nguvu. Aligeuka huku na huko lakini hakuona mtu yeyote.
“Oooh My God! What the hell is this?... Ooh my Lord save me!” (Mungu wangu! Balaa gain tena hili? Eeh Bwana niokoe).
Bi Patricia alikuwa akiongea peke yake huku moyoni akisali na kukemea nguvu za giza zilizokuwa zinamuandama, akatafuta sehemu ya kukaa baada ya kuzidiwa na maumivu ya kichwa na kizunguzungu. Alikaa chini ya mti na baada ya muda mfupi hali yake ilitulia na kurudi kuwa ya kawaida. Bila kupoteza muda alinyanyuka na kuendelea na safari yake.
Cha ajabu ni kwamba alipoanza tu kutembea kuelekea kule kwa mchungaji, hali yake ilianza kubadilika na kuwa kama ile ya mwanzo. Kizunguzungu kilizidi kuongezeka huku kichwa nacho kikiwa kinamgonga mithili ya mtu anayepigwa na nyundo. Zile kelele za watu kucheka zikaongezeka kuliko mwanzo na kusababisha vurugu kubwa kichwani mwake, ingawa alipogeuka tena huku na kule bado hakumuona mtu yeyote. Akagundua moja kwa moja kuwa zile ni nguvu za kichawi kutoka kwa ndugu zake. Aliamua kupiga moyo konde na kuzidi kusonga mbele huku akilitaja jina la Mungu wake.
Aliendelea kutembea mpaka alipoikaribia kabisa nyumba ya mchungaji, lakini kwa kadri alivyokuwa akizidi kuikaribia, ndivyo alivyozidi kuumia ndani kwa ndani, ikafika mahali akawa anahisi kama akili inaacha kufanya kazi. Kichwa kilikuwa kikimuuma sana na kizunguzungu kilizidi kumbana kiasi cha kushindwa kuendelea kutembea. Aliamua kukaa tena chini, cha ajabu alipokaa tu, maumivu yote yalitoweka kabisa na akawa mzima. Alibaki akijiuliza ni kitu gani kinachosababisha hali ile. Alitambua kuwa nguvu kubwa ya giza kutoka kwa ndugu wa marehemu mumewe ilikuwa ikimzuia asiende kuonana na mchungaji.
Wazo la mwisho aliloliona linafaa ilikua ni kurudi nyumbani kutafakari upya nini cha kufanya kwani hilo la kuonana na mchungaji lilionekana kushindikana kwa muda huo. Kwa jinsi hali ilivyoonesha, hakutakiwa kufanya mzaha tena kwani dalili hizo alizokumbana nazo wakati akielekea kwa mchungaji, zilitosha kumfanya aelewe kilichokuwa mbele yake kama angekaidi yale aliyoambiwa usiku.
Alinyanyuka pale chini na kugeuka kuelekea kule alikotoka bila kuingia ndani ya nyumba ya mchungaji. Aliamini kuwa ni kweli kuna uchawi na una nguvu kubwa sana kwani alivyolifuta wazo la kwenda kwa mchungaji na kuanza kurudi kwake, ile hali haikujirudia tena mpaka anafika nyumbani kwake.
Alikuwa akijiuliza maswali mengi njia nzima bila kupata majibu. Alipofika karibu na nyumbani kwake Alimuona mwanae Geneviv akiwa amekaa nje katika mkao ambao ulionyesha dhahiri kuwa lazima kuna jambo baya lililomsibu. Alichokifikiria kilikuwa ni kweli kwani alipofika karibu, alishangaa kumuona Geneviv akiwa anajikuna ovyo mwili mzima huku akiwa ameanza kutokwa na vipele vya ajabu.
“Jamani! Umepatwa na nini tena? Mbona nimekuacha ukiwa mzima kabisa!”
Geneviv hakujibu kitu zaidi ya kuendelea kujikuna huku akivua nguo na kuzitupa pembeni . Mwili mzima ulikuwa ukimuwasha mithili ya mtu aliyemwagiwa upupu. Jinsi alivyokuwa akizidi kujikuna, mwili ulikuwa ukianza kutoa vipele vidogovidogo na ngozi yake kubadilika rangi na kuwa nyekundu.
Bi Patricia alishindwa namna ya kumsaidia mwanae kwani hakuelewa amekumbwa na nini mpaka awe vile. Ni muda mfupi tu alipoondoka, alimuacha akiwa mzima wa afya, na alikuwa bado amelala. Alivyozidi kumhoji kilichomsibu alimwambia kuwa aliamka akiwa salama kabisa ila alipofungua tu mlango aliona vitu vya ajabu vikiwa vimewekwa mlangoni na baada ya kuviruka na kutoka nje, ndipo alipoanza kujisikia mwili mzima ukimuwasha.
Haikuwa kitu kingine, bali nguvu za uchawi uliotegwa usiku. Alijikuta akishindwa kujizuia kutoa machozi kwa jinsi alivyokuwa akimuonea huruma mwanae. Geneviv alikuwa akijikuna mwili mzima na vipele vilikuwa vikizidi kuongezeka na kuifanya ngozi yake ianze kutisha. Wazo jingine likaja kuwa ni lazima akaonane na baba yake Kim haraka iwezekanavyo ili kama inawezekana waende kuifuta ile kesi mahakamani asubuhi ile ile na kumuachia huru Bwana Magafu ili kuepusha shari kubwa iliyokuwa mbele yao.
Akanyanyuka na kuanz akuhaha kama mwendawazimu. Alianza kukimbia kuelekea nyumbani kwa Bwana Magwaza, baba yake Kim. Muda mfupi baadae akawa ameshafika na kuanza kugonga mlango kwa nguvu. Ulifunguliwa na Kim na alipomuuliza kama baba yake yupo, alimjibu kuwa ameondoka alfajiri na mapema kwa safari ya kikazi na angerudi kesho yake kwani safari yake ilikuwa ndefu.
Whaaat? Hakuna namba zake za simu? Please mwanangu nisaidie! Mwenzio Geneviv anaumwa ugonjwa wa ajabu, hapa nilipo nahisi kuchanganyikiwa. Kim kusikia Geneviv anaumwa na yeye alianza kuchanganyikiwa. Kwa haraka aliingia ndani na kutoka na simu yake ya mkononi. Akabonyeza namba na kuanza kumtafuta baba yake hewani. Simu ya bwana Magwaza ilikuwa haipatikani. Wakabaki kutazamana wakiwa hawajui nini cha kufanya.
Akawa anatembea taratibu kurudi kwake, akiwa amekata tamaa kabisa. Hakujua nini hatma ya mwanae Geneviv, wala nini hatma yake. Mawazo mengi yalikuwa yakipita akilini mwake kiasi cha kumfanya aanze kuongea peke yake barabarani kama mwendawazimu. Machozi yalishakauka kwani alilia sana maishani mwake, ikafika kipindi moyo wake ukawa kama umekufa ganzi.
Wazo pekee lililokuwa limebakia ilikuwa ni kwenda kumbeba Geneviv na kwenda naye kwa mchungaji wao, bila kujali ambacho kingemtokea.
“Potelea mbali, saa hizi nimeshaamua, liwalo na liwe ila lazima nifike na mwanangu kwa mchungaji, hata nikifia njiani sitajali, lakini lazima nifike.”
Alipofika nyumbani kwake alikuta hali ya Geneviv ikizidi kuwa mbaya zaidi. Vile vipele ambavyo mwanzo vilikuwa vidogo, sasa vilibadilika na kuwa vidonda vikubwa vikitoa majimaji yaliyozidi kumfanya ajikune zaidi. Yaani ndani ya muda mfupi sana kila kitu kilikuwa kimebadilika. Geneviv aliyeamka akiwa mzima kabisa, masaa manne yaliyofuata alikuwa taabani utadhani ameugua mwaka mzima.
Ama kwa hakika nguvu ya uchawi ilikuwa imefanya kazi yake. Bi Patricia alibaki kumtazama mwanae kwa huruma, bila kupoteza muda akamuinua na kumfunika kitenge kisha wakaanza upya safari ya kuelekea kwa mchungaji. Hakutaka kujali kitakachotokea njiani kwani aliona ni bora afe akiwa anahangaika kuliko kuendelea kumalizwa na woga.
Alipita njia ile ile aliyopita asubuhi. Geneviv alikuwa akilalamika njia nzima kwa maumivu aliyokuwa anayahisi.
“Jikaze mwanangu mpaka tufike kwa mchungaji, kwa Mungu hakuna linaloshindikana, jikaze mama…”
Bi Patricia alikuwa akimfariji mwanae. Alikuwa akiumia mno kwa jinsi alivyokuwa akimuona Geneviv anateseka.
Walipokaribia kufika Bi Patricia akaanza kuhisi hali kama ile iliyomtokea asubuhi ikianza upya. Aliamua kumuuliza Geneviv kuona kama na yeye anahisi vilevile. Cha ajabu Geneviv alikuwa hazisikii zile kelele ambazo mama yake alikuwa anazisikia.
“Nasikia kabisa watu wanacheka na kutuzomea huku wakiniita jina langu.”
Japokuwa Geneviv alikuwa kwenye maumivu makali, alishtushwa na alichokisikia kutoka kwa mama yake. Akahisi ameanza kuchanganyikiwa akili. Bi Patricia alizidi kukazania kuwa anasikia kelele za ajabu tena zikisikika karibu kabisa na hapo walipo.
“Mbona sikuelewi mum, kelele gani mbona mi sizisikii? Nifikishe kwa mchungaji please, nakufa mum!”
Maneno yale ya Geneviv yalimfanya Bi Patricia apige moyo konde na kuendelea kusonga mbele licha ya mauzauza aliyokuwa akiyahisi. Kwa kadri alivyokuwa akijikaza na kuzidi kuelekea kule kwa mchungaji, maneno ya ajabu yalianza kumtoka bila mwenyewe kujielewa. Sasa akawa ni kama anayeanza kuchanganyikiwa. Akaanza kupiga mayowe kwa nguvu, na Geneviv akiwa bado anashangaa kinachoendelea, akashuhudia mama yake akianza kukimbia huku na huko akizidi kupiga mayowe.
Mum! Muuum! Whats happening to you? (mama! mamaaa! Umepatwa na nini) Geneviv alizidi kumshangaa mama yake, kwani alianza kujipaka udongo usoni na kichwani huku akitoa maneno yasiyoeleweka. Kwa kifupi alikuwa amechanganyikiwa akili. Alianza kuvua nguo alizozivaa na kuzichanachana huku akicheka kwa sauti ya juu. Mara akaanza kutimua mbio kuelekea kusikojulikana.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Safari ya kwenda kwa mchungaji ikawa imeishia kwa Bi Patricia kuchanganyikiwa akili. Alitia huruma mno.
Geneviv hakutaka kuamini macho yake kama kile kilichotokea ni kweli. God where are you? (Mungu uko wapi?) Geneviv alikuwa akiongea kwa uchungu huku akijikongoja kuelekea kule mama yake alikokimbilia. Alikuwa na hali mbaya kwani vidonda vilikuwa vikizidi kuongezeka mwili mzima na kumfanya awashwe vibaya mwili mzima.
Alijikongoja mpaka kule mama yake alikoelekea. Alizidi kumfuata mpaka alipofika kwenye dampo karibu na soko kuu. Hakuamini alichokiona. Mama yake alikuwa ndani ya lundo la takataka akichakura huku na huko kama anayetafuta kitu.
“Mum, stop that! Don’t leave me alone! Come back to me mum” Geneviv alianza kupiga kelele zilizowakusanya watu. Hakuna aliyeamini kuwa kweli yule Bi Patricia wa siku zote.
“kwani amepatwa na nini? Mbona asubuhi ya leo nimekutana naye akiwa mzima kabisa na tumesalimiana vizuri?” Alikuwa akiuliza mama mmoja akionekana kushangazwa mno na hali ya Bi Patricia. Wasamaria wema wakajitosa kwenda kutaka kumkamata lakini haikuwezekana kwani alicharuka na kuanza kumpiga kila aliyemsogelea, na baadae akakimbia na kuondoka kabisa eneo lile kuelekea kusikojulikana.
Geneviv alikuwa akimfuata huku akizidi kulia na kuomba msaada wa watu kumkamata. Hatimaye alimpotea kabisa. “Nitafanya nini mimi jamani? Nitakuwa mgeni wa nani ndani ya dunia hii! Eeh Mungu kwanini uliniumba nije kuteseka namna hii hapa duniani. Geneviv alikuwa akilia peke yake wakati akizidi kutembea huku na huko kumtafuta mama yake.
Kwa kadri jua lilivyokuwa linazidi kukolea, yale madonda yaliyomtoka geneviv mwili mzima yalikuwa yakimsababishia maumivu makali kama amemwagiwa maji ya moto mwili mzima. Ilibidi atafute mahali penye kivuli, akajisogeza chini ya mti na kukaa. Hakujua hapo ni wapi kwani pilika za kumkimbilia mama yake zilimfanya afike mbali sana.
Akakaa chini ya mti na kuendelea kujiuliza ni nini kilichotokea mpaka mambo yote yakageuka ndani ya masaa machache na kumfanya aishie katika hali kama ile aliyokuwa nayo. Alijitazama mwilini, mwenyewe hakuamini kama ni yeye kweli kwani ni siku hiyohiyo alimka asubuhi akiwa mzima wa afya njema kabisa.
Masaa machache tu, ngozi yake ilibadilika na kuwa kama ameugua kwa muda mrefu. Alijikuta machozi yakimmwagika, na zaidi alipomfikiria mama yake.
Hakutaka kuamini kuwa ni kweli ameshakuwa kichaa na kumuacha peke yake.
Alikuwa akiyafikiria yote yaliyotokea kuanzia usiku uliopita ambapo walianza kushuhudia mambo ya ajabu.
Sasa aliamini kuwa ni kweli hapa duniani kuna uchawi na una nguvu kupita kawaida. Ni uchawi wa ndugu zake dio uliomfanya mama yake achanganyikiwe na kuwa kichaa, ni uchawi huohuo ndio uliomfanya awe mahututi pale chini ya mti akiwa hajui nini hatma yake.
Alishindwa kuelewa ndugu wa baba zake wana roho za namna gani mpaka wasiwe na huruma na kuamua kuwatesa namna ile. Zaidi alibaki kumwachia Mungu kwani aliamini yeye ndiye mpangaji wa yote na kamwe asingeendelea kuvumilia kuona watu wasio na hatia wakinyanyasika namna ile.
Aliwachukia mno ndugu wa baba zake, aliwachukia pia wanaume kwani aliamini yale yote yaliyokuwa yanawakuta yeye na mama yake yalisababishwa na wanaume.
Alijiapiza kuwa kamwe hatarudi nyumbani kwao kwani kama angerudi inawezekana ule uchawi uliokuwa umetegwa ungeweza kumdhuru zaidi. Aliendelea kuugulia maumivu makali akiwa hana msaada wowote. Masaa yakawa yanazidi kukatika na hatimaye jioni ikaanza kuingia. Kwa kadri masaa yalivyokuwa yanakatika ndivyo hali yake ilivyozidi kuwa mbaya.
Akawa anajifariji kwa kurudia rudia vifungu vya Biblia alivyokuwa amevikariri kichwani
Kila jambo huja kwa wakati wake…
Kuna wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa,
Wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna vilivyopandwa
A time to kill and a time to heal;
A time to tear down and a time to build up.
A time to weep and a time to laugh;
A time to mourn and a time to dance…
A time to love and a time to hate;
A time for war and a time for peace…
********
Habari zilizokuwa zinatapakaa kama moto wa nyika zilimfikia Kim kuwa mama yake Geneviv amechanganyikiwa akili na kuwa kichaa. Hakutaka kuamini kama ni kweli kwani ni asubuhi ya siku ileile alikuja pale nyumbani kwao kuja kumuulizia baba yake mzee Magwaza.
Kim alikumbuka kila kitu mpaka wakati anaaga na kuondoka. Iweje masaa machache baadae aambiwe amechanganyikiwa na kuwa kichaa? Hilo halikumuingia kabisa akilini, akaona ni bora aende nyumbani kwa kina Geneviv akahakikishe mwenyewe.
Alipofika nyumbani kwao alikuta eneo lote likiwa kimya kabisa.
Aliposogea mlangoni aliona mambo ya ajabu ambayo moja kwa moja yalimfanya aanze kuamini yale aliyokuwa akiyasikia mtaani kutwa nzima. Kwa macho yake alishuhudia vitu kama dawa za kienyeji zikiwa zimemwagwa pale mlangoni.
Alijikuta akitetemeka kwa hofu na kuanza kurudi nyuma. Alihisi hizo ndizo zilizomfanya achanganyikiwe, Swali lililokuwa kichwani mwake ni mahali aliko pamoja na mwanae Geneviv.
Alijaribu kumuita Geneviv kwa mbali lakini bado kuliendelea kuwa kimya. Akaanza kuondoka eneo lile huku akikimbia. Alipofika mbele alikutana na msichana ambaye alimsimamisha na kuanza kumuuliza maswali…
“We vipi mbona unakimbia kimbia kama chizi, umepatwa na nini?
Ilibidi Kim asimame na kuanza kumueleza aliyoyaona kule alikotoka.
“Niulize mimi nikupe full story, mi nakaa jirani kabisa na kina Geneviv na isitoshe Geneviv alikuwa rafiki yangu mpenzi ingawa kwa sasa tuna Beef”.
Kim alikuwa amekutana na Alice. Baada ya kuambiwa kuwa yeye ndio alikuwa akifahamu kila kitu kilichokuwa kinaendelea, ilibidi aanze kumdadisi kwa undani.
“Mi ukitaka nikuambie kila kitu kilichotokea niko tayari, ila lazima na wewe uwe tayari kunitimizia ninachokitaka.
Kim bila kuelewa Alice alichokuwa anamaanisha, alikubali haraka ili mradi aambiwe kilichowatokea Geneviv na mama yake. Alikuwa na shauku kubwa ya kujua. Akakubali kuongozana na Alice mpaka kwenye chumba anachoishi. Alice alikuwa akifahamu kuwa Geneviv na Kim ni marafiki na ukaribu waliokuwa nao ulimfanya ahisi wana uhusiano mwingine zaidi ya urafiki ingawa hakuwa na uhakika.
Akaona huo ndio muda muafaka wa kulipiza ksasi kwa Geneviv kama alivyomuapia baada ya kumsaliti kwenye kazi yao ya uchangudoa kipindi cha nyuma. Alipanga kufanya kitu ambacho kitamfanya asimsahau kamwe. Aliamini ni rahisi sana kulipiza kisasi kwa Kim kwa kuwa yeye Kim alikuwa hamfahamu Alice. Akajifanya mpole ili atomize azma kwa urahisi.
Kim bila kuelewa kuwa yuko chini ya mikono ya msichana hatari, Alice… alikuwa akimfuata nyuma kuelekea kwenye chumba chake kama kondoo anayepelekwa machinjioni. Akilini mwake alikuwa na hamu ya kutaka kufahamu kwa undani kilichomtokea Geneviv ili aone kama anaweza kutoa msaada wa haraka kuokoa jahazi.
Karibu ndani kakaangu, jisikie uko nyumbani na hapa ndio umefika, utafahamu kila kitu. Kabla ya kuanza kuongea naomba nikuhudumie kinywaji unachokitaka.
Alice alikuwa akimkaribisha Kim kwa uchangamfu mno. Kim alibaki kushangaa jinsi kile chumba kilivyokuwa kimejaa vitu vya thamani.
Alihisi huenda Alice anaishi na mtu mwingine mle ndani, lakini alimtoa wasiwasi kuwa yuko peke yake.
Baada ya kuendelea kumng’ang’aniza aseme kinywaji anachokitaka, Kim aliomba soda. Alice akatoka na kwenda kumletea. Aliona ho ndio muda muafaka wa kumfanyia Kim alichokitaka.
***********
Geneviv alikuwa akizidi kuomboleza pale chini ya mti alipokuwa amekaa kwa muda mrefu. Maumivu aliyokuwa akiyahisi yalimfanya ahisi kama anakaribia kufa. Japo kuwa giza lilikuwa linaanza kuingia, hakutaka kabisa kurudi nyumbani kwao, aliona ni bora alale palepale chini ya mti ili hata akifa, watu wauone mwili wake kwa urahisi.
Aliona kama Mungu amewatupa na ndio maana wanapatwa na yote yale. Japokuwa aliendelea kuvikumbuka vifungu vya Biblia ambavyo aliamini vitampa moyo, bado ukweli uliendelea kuwa uleule.
Maumivu yalikuwa yakizidi kuogezeka na vile vidonda vilivyomtoka mwili mzima sasa vilianza kutoa usaha na kusababisha nzi waanze kujaa.
Masaa yalizidi kukatika na hatimaye ikawa usiku.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Upande wa pili, Bi Patricia ambaye sasa alikuwa tayari ni kichaa alikuwa akihama kutoka jalala moja kwenda jingine, akiokota vyakula majalalani na kula bila hofu. Alikusanya takataka nyingi na kuzibeba mgongoni kama mtoto. Kila aliyekuwa akimfahamu alikuwa akitoa machozi alipomuona.
Siku moja tu ilitosha kumuhamisha moja kwa moja kutoka ulimwengu wa kawaida na kumpeleka mahali ambapo alipoteza kabisa kumbukumbu za yeye ni nani. Alikuwa akiimba na kucheza majalalani kwa lugha ambayo haikuwa ikieleweka.
Ilipofika usiku alianza kutafuta mahali pa kulala, ambapo alijilaza kwenye lundo la takataka na kujifunika matambara machafu.
**********
Baada ya Kim kunywa soda aliyoletewa na Alice alianza kuhisi kichwa kikiwa kizito na muda mfupi akaanza kuhisi usingizi mzito ukimuelemea.
“Umeweka nini kwenye hii soda, mbona nahisi kama nimelewa!”
Aliuliza Kim kwa sauti ya kilevi akijilaza kwenye kochi. Alice alikuwa akishangilia ushindi kwani lengo lake lilikuwa likikaribia kutimia.
Bila kupoteza muda alimuinua Kim na kwenda kumlaza kitandani.
Kim alikuja kushtuka baada ya kusikia jogoo akiwika. Alianza kuvuta kumbukumbu ya pale alipo. Alijishangaa kuona kuwa amelala bila nguo hata moja, kitu ambacho hakikuwa kawaida kwake. Kilichomshtua zaidi ni kwamba alikuwa amekumbatiwa na mwanamke. Hakutaka kuamini kwa haraka kama ni kweli, akahisi yuko ndotoni.Ilikuwa tayari ni alfajiri.
Alipozidi kuvuta kumbukumbu akagundua kuwa haikuwa ndoto bali ni kweli. Kumbukumbu zake zilimrudisha jioni alipokuwa akitoka nyumbani kwa kina Geneviv na kukutana na msichana alijitambulisha kuwa anaitwa Alice. Alijaribu kukumbuka kilichoendelea lakini kumbukumbu zilikuwa zikiishia alipokaribishwa soda na Alice akiwa ndani ya chumba chake.
My God! What happened to me? Alice umenifanya nini? Cant believe this
Alishtuka kwa nguvu Kim na kuinuka kutoka pale kitandani. Hakuyaamini macho yake alipogundua kuwa alikuwa amelala na Alice usiku mzima bila kujitambua.
Kwa haraka aliinuka na kuanza kutafuta nguo zake zilipo. Alice alijifanya bado yuko usingizini, akawa anamuangalia alivyochanganyikiwa kwa jicho la wizi. Moyoni mwake alikuwa akishangilia ushindi kwani alichokitaka alikuwa ameshakipata. Alijipongeza kwa mtego wake kumnasa Kim kirahisi namna ile.
Kim alivaa nguo kwa haraka na bila kuaga akafungua mlango huku akiendelea kumlaani Alice kwa kitendo kichafu alichomfanyia. Tayari ilikuwa ni saa kumi na moja alfajiri.
Alitoka na kuanza kukimbia akiwa hajui anakoelekea. Kitendo alichofanyiwa na Alice kilimfanya awe kama mwendawazimu. Alikimbia kwa umbali mrefu mpaka akaanza kuhisi kuchoka. Alitafuta mahali akakaa na kuanza kutafakari kwa makini juu ya kilichomtokea. Alikuwa akimlaani vikali Alice na alimuona kama shetani aliyejivika ngozi ya malaika.
Baada ya kutafakari sana, aliamua kuchukulia kawaida na kusahau yote yaliyotokea. Wazo pekee lililokuwa kichwani mwake ilikuwa ni kumtafuta Geneviv kwa udi na uvumba. Aliinuka kutoka pale chini alipokuwa amekaa na kuanza kutembea taratibu kukatiza mitaani.
Baada ya kwenda umbali mfupi, aliona kitu ambacho kilimfanya ashtuke. Alikuwa ni mtu amelala chini ya mti. Kwa kuwa bado ilikuwa ni Alfajiri, ilionyesha moja kwa moja kuwa amelala pale usiku kucha. Ilibidi aanze kusogea taratibu kutaka kuona ni nani aliyeweza kulala nje usiku kucha ilhali mitaani kulikuwa kumejaa vibaka na watu wa wabaya.
Kwa kadri alivyokuwa anasogea mapigo ya moyo yalianza kumwenda kasi. Hii ni kwa sababu yule mtu alikuwa amejifunika kitenge ambacho Kim alikhisi kama anakifahamu ingawa hakukumbuka haraka kuwa alimuona nani akiwa amekivaa.Alisogea mpaka jirani kabisa. Aliinama chini na kumfunua yule mtu usoni…
“Geneviv! Geneviv! Oooh my Lord, what happened to you? Mimi ni Kim! Nimekutafuta sana my dear, hebu nieleze, umetokewa na nini” Hakuamini macho yake. Alikuwa ni Geneviv akiwa amelala chini ya mti. Alishangaa kwa jinsi alivyokuwa amebadilika mwili mzima, uso ulikuwa umejaa vidonda na alipomchunguza vizuri, alikuwa na madonda mwili mzima. Hakuyaamini macho yake.
Alimuinamia kwa upole huku machozi yakimwagika. Alijikuta akiumia mno kwa hali aliyomkuta nayo Geneviv. Hakuelewa amepatwa na nini mpaka awe katika hali kama ile. Geneviv alikuwa kimya akimsikiliza Kim. Alijikuta na yeye akimwaga machozi kwani hakutegemea kama anaweza kukutana naye tena.
“Just leave me Kim, leave me alone please! Im ready to die”
(We niache tu Kim, Niache peke yangu! Niko tayari kufa.
Geneviv anarudia tena kauli yake, safari hii kwa sauti ya juu zaidi huku akianza kumwaga machozi kwa uchungu…
“Shed no more tears Geneviv, kila kitu kina mwanzo na mwisho, haya yote yatakwisha! Amini Mungu ana makusudi na wewe!”
Kim alikuwa akiongea kwa majonzi huku naye akibubujikwa na machozi. Hali aliyokuwa naye Geneviv ilimliza sana. Aliendelea kumbembeleza kwa maneno ya kumtia nguvu na taratibu Geneviv akaanza kumuelewa.
Geneviv alikuwa akishangaa kitu kimoja, kwa hali aliyokuwa nayo, yeye mwenyewe alijiona anatisha na kutia kinyaa, lakini alishangaa kumuona Kim akiwa hajali kabisa, alikuwa amemuinamia karibu kabisa bila ya kuogopa wala kuona kinyaa. Ilibidi amwambie Kilichokuwa moyoni mwake, aliamini lazima angekufa, lakini kabla hajafa alitaka Kim afahamu kuwa amekuwa mtu wa kipekee mno katika maisha yake.
“Before I die…let me tell you that I have never meet with a boy of your kind… I have nothing to pay you back…May God grant you long living…let me go!”
(Kabla sijafa… naomba nikwambie kuwa sijawahi kukutana na mvulana mwenye roho kama yako, sina cha kukulipa… Mungu akupe maisha marefu…acha mi nitangulie).
Maneno yale machache yalimchoma sana Kim mtimani na akajikuta akizidi kulia kama mtoto mdogo.
“No Geneviv! Don’t Go! Bado nakuhitaji Geneviv, you are everything to me! Usiende…”
Aliongea Kim huku akilia na kumkumbatia Geneviv kwa nguvu. Hakujali kama mwili wake ulikuwa na vidonda vinavyotoa usaha. Ilikuwa bado ni alfajiri sana, na taratibu jua likawa linachomoza.
“Angalia jua linavyochomoza Geneviv, hivi ikitokea kuwa kabla halijachomoza likazama na kurudi lilikotoka, unafikiri dunia itakuwaje?” Kim alimpiga swali la kimitego huku akifuta machozi. Geneviv alilitazama lile jua kwa makini na kutafakari kile kilichozungumzwa na Kim.
“Unamaana gani!”
Alijikuta akipata nguvu za kuinuka, akakaa kwa shauku akiugemia mti huku akizidi kutafakari Kim alikuwa na maana gani.
“Namaanisha kuwa wewe ni kama jua linaloanza kuchomoza moyoni mwangu na maishani mwangu, lakini ghafla unataka kuondoka na kurudi ulikotoka, unafikiri mi ntabaki na hali gani hapa duniani endapo jua langu litazimika asubuhi?”
Japokuwa alikuwa kwenye maumivu makali, alijikuta akiachia tabasasmu hafifu. Hakuwahi kuambiwa maneno kama yale na mtu yeyote na kwa mara ya kwanza alijihisi ana umuhimu mkubwa katika maisha ya Kim. Aligeuza uso wake na kumtazama Kim machoni. Alionekana kweli anamaanisha kile alichokisema.
Wakabaki kutazamana. Ile hali ya kupoteza matumaini iliyokuwa imetawala mawazoni mwake ikaanza kuondoka na kuchukuliwa na taswira ya Kim.
Kim aliendelea kumwaga sera na hatimaye akawa amefanikiwa kumteka Geneviv kimawazo. Akambembeleza kuwa amchukue mpaka nyumbani kwao ili wakaangalie namna ya kumtibu ugonjwa wake wa ajabu.
“And how about my mum?” (na vipi kuhusu mama yangu?) Aliuliza Geneviv wakati Kim akimsaidia kuinuka tayari kwa kurudi nyumbani kwa kina Kim.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Worry not my dear, everything is going to be alright, nothing is impossible under the sun.”
(Usihofu mpendwa, kila kitu kitakuwa sawa, hakuna lisilowezekana). Kim alimjibu na wakaanza kutembea taratibu, Kim akiwa amemshikilia Geneviv kwani mwili wake haukuwa na nguvu kabisa.
Wakawa wanatembea taratibu kuelekea nyumbani kwa kina Kim. Jua lilizidi kuchomoza na watu wakawa wanaendelea na shughul zao kama kawaida. Kila walipopita Geneviv na Kim, watu walikuwa wakiwakodolea macho kama wanaojiuliza ni nini kilichotokea. Hakuna aliyeelewa, wakabaki kuduwaa.
*************
Bwana Magwaza, baba yake Kim, alikuwa amepata safari ya dharula ya kikazi kwa ajili ya kwenda kumsaidia mjane mmoja ambaye naye alikuwa na tatizo kama la Bi Patricia ambapo ndugu zake walikuwa wameuza mali zote zilizoachwa na mume wake na kumuacha akiteseka na watoto.
Alipanga kulala huko huko kuhakikisha kuwa anasaidia mjane yule kupata haki yake. Akiwa njiani wakati anaenda, alipigiwa simu na mmoja wa wafanyakazi wenzake ambaye alimpa taarifa ambayo ilimshtua na kumfanya aahirishe safari yake.
Alipigiwa simu na kupewa taarifa kuwa yule mwanamke ambaye jana yake walifanikiwa kuzuia nyumba yake kuuzwa kwa nguvu baada ya mumewe kufariki,( Bi Patricia) alikuwa akionekana mitaani akiwa na dalili zote za kuchanganyikiwa akili.
“Amepatwa na nini? Cant believe it! Lazima watakuwa ni ndugu zake tu…maskini! Basi hata hii safari inabidi niiahirishe. Lazima nije tuwashikishe adabu wote waliohusika.”
Bwana Magwaza alikuwa akiongea kwa simu na yule mfanyakazi mwenzake. Mara moja akaanza safari ya kurudi mjini. Kichwani alikuwa akijiona kama hajafanya kitu kumsaidia Bi Patricia kwani kama amechanganyikiwa lazima ile nyumba ingechukuliwa tena na kazi yote waliyoifanya ilikuwa ni bure.
Alitaka kuhakikisha kuwa anamuokoa na kumfanya apone kabisa. Alijua namna ambavyo angefanya kwani alikuwa na uzoefu wa kutosha wa masuala kama yale na haikuwa mara yake ya kwanza kushughulikia kesi zinazohusisha imani za kishirikina.
Safari yake ya kurudi ilimchukua masaa mengi , lakini hatimaye jioni ya siku ileile akawa tayari amesharudi. Alipitiliza mpaka nyumbani kwake ili akapate taarifa kutoka kwa mwanae Kim kwani alijua kwa vyovyote anaelewa kinachoendelea. Alipofika hakukuta mtu nyumbani kwake, akajua lazima watakuwa nyumbani kwa kina Geneviv, lakini hata alipofika kule nako hakukuwa na mtu.
Hakutaka kupoteza muda, akaanza kupeleleza hali ilivyokuwa. Haikumuwia vigumu kufahamu stori nzima kwani karibu kila mtu kwa siku ile alikuwa akilizungumzia suala lilelile. Kwa kutumia pesa aliwatafuta vijana wa kusaidia kuhakikisha wanampata bi Patricia siku ileile. Kazi ikaanza mara moja. Walianza kufuatilia njia zote na mitaa aliyokuwa anapita Bi Patricia.
Walizunguka karibu maeneo yote ambayo vichaa hupendelea kuishi. Walizunguka karibu majalala yote lakini kila mahali walipofika, waliambiwa kuwa mtu wanaemtafuta alikuwepo na walimuona muda mfupi uliopita. Kazi ile iliwachukua masaa mengi sana mpaka giza likawa limekolea. Bwana Magwaza hakutaka kukata tama mapema, aliendelea na kazi akisaidiwa na vijana wa mitaani. Mpaka inatimia saa sita za usiku bado walikuwa hawajafanikiwa kumpata Bi Patricia wala mwanae Geneviv.
Wakawa wameanza kukata tamaa.
“Hebu tujaribu kwa mara ya mwisho kwenye lile jalala pale. Kama tukimkosa basi turudi kulala tutaendelea Kesho”
Aliongea Bwana Magwaza akionyesha kuwa ameshachoka kwani kazi walioyoifanya ilikuwa si ya kitoto. Walikuwa wamezungukia karibu mitaa yote bila mafanikio.
Wakalivamia jalala la mwisho kujaribu bahati yao kwa mara ya mwisho. Wote walishtuka kuona mtu akiinuka kwa kasi kutoka katikati ya takataka na kuanza kuwafukuza kwa mawe na fimbo.
“Ndiyo mwenyewe! Mkamateni kwa uangalifu msimuumize, mkamateni…” Bwana Magwaza aliwaamuru wale vijana baada ya kugundua kuwa yule ndio Bi Patricia waliyekuwa wakimtafuta. Hakuyaamini macho yake…
Baada ya purukushani ya muda mrefu hatimaye wale vijana walifanikiwa kumkamata na kumfunga kamba mikononi na miguuni.
Kwa haraka wakambeba juu juu mpaka barabarani ambako waliita taksi na kumkimbiza hospitali. Walipofika Hospitali, manesi walimpokea kwa kumdunga sindano ya usingizi ili atulie kwani alikuwa akifanya vurugu kubwa sana. Baada ya sindano ya usingizi kumlewesha, walianza kwa kumuosha mwili mzima kwani alikuwa hataminiki kwa uchafu. Baada ya kuwa safi walienda kumlaza kwenye wodi maalum ya wagonjwa wa akili. Wakaanza kumpatia tiba ya haraka.
Bwana Magwaza alikuwa akizunguka huku na kule akiwa kama asiyeamini yale yaliyomkuta Bi Patricia. Muda mfupi baadae aliitwa kwenye chumba cha daktari…wakawa wanazungumza. Alikuwa ni daktari Zayumba, yule aliyewahi kuwa msaada mkubwa sana kwa Bi Patricia na mwanae Geneviv siku za nyuma, kabla hata ya kifo cha Mzee Rwakatare.
Kwa pamoja wakawa wanatafakari nini cha kufanya ili kuyamaliza mateso ya muda mrefu aliyoyapata Bi Patricia na mwanae Geneviv.
“Lazima tuwasaidie sana kwa kweli! Mimi ni shahidi wa matukio ya kutisha yaliyowapata. Kwa kweli inahitaji moyo jasiri kuweza kuvumilia” Aliongea Daktari Zayumba wakati wakiendelea na majadiliano na Bwana Magwaza.
***********
Kim alimsaidia Geneviv mpaka wakafika nyumbani kwao. Walipofika alimkalisha kwenye kiti na kwa haraka akaanza kuandaa maji ya moto kwa ajili ya kumsafishia Geneviv ambaye sasa mwili wake ulikuwa umeanza kutoa harufu.
Muda mfupi baadae maji yakawa tayari…
“Would you allow me to wash your body?”
(Utaniruhusu nikuogeshe?)
Kim alimuuliza Geneviv kimasihara akitaka kuona atamjibu nini.
“Stop kidding kim, I will do it on my own, I know you care intensely for me, thank you very much”
(Acha utani Kim, ntaoga mwenyewe…najua unanijali kupita kawaida, ahsante sana)
Wakawa wanatabasamu. Taratibu furaha ilianza kurudi moyoni mwa Geneviv kwani Kim alikuwa akijitahidi kwa kadri ya uwezo wake wote kumhudumia. Akamsindikiza mpaka bafuni na kumuwekea kila kitu tayari. Geneviv akaanza kuoga kwa kutumia dawa maalum ya kusafishia vidonda.
Baada ya kumaliza kuoga, Geneviv alijikuta akipata nguvu mpya. Kim alikuwa akihangaika kuandaa kifungua kinywa kwa ajili ya Geneviv, na alipomaliza kuoga alimkaribisha mezani. Wakati wanaendelea kupata kifungua kinywa, baba yake Kim akawa anaingia.
Alishtuka kwa jinsi Geneviv alivyokuwa. “Unamshangaa saizi wakati hapo ana nafuu kubwa kabisa, alikuwa na hali mbaya sana. Tumshukuru Mungu kwa kumnusuru” Aliongea Kim wakati akimkaribisha baba yake aliyeonekana bado kaduwaa kwa hali aliyomuona nayo Geneviv. Bwana Magwaza hakutaka hata kupumzika. Aliingia ndani na kubadilisha nguo, kisha akawa anajiandaa kumpeleka Geneviv hospitali.
“Malizeni haraka twende Hospitali Geneviv akatibiwe”
Muda mchache baadae wakawa tayari kwa kuondoka. Bwana Magwaza hakutaka kumwambia Geneviv mahali aliko mama yake, alitaka kufanya kama Surprise ili kuwaongezea nguvu ya kupona haraka. Wakaingia ndani ya gari na safari ya kuelekea Hospitali ikaanza. Walienda kwenye hospitali ile ile aliyolazwa mama yake.
Baada ya kuhakikisha Bi Patricia anahudumiwa kisawasawa, Bwana Magwaza na daktari Zayumba wanajadiliana nini cha kufanya ili kukomesha mateso ya muda mrefu yaliyoharibu maisha ya Bi Patricia na mwanae Geneviv. Baada ya kufikia muafaka wa nini cha kufanya, Bwana Magwaza anaaga na kurudi nyumbani kwake akiacha Bi Patricia anashughulikiwa kikamilifu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Anapofika nyumbani kwake, anashangaa kumkuta mwanae Kim akiwa na Geneviv, na kinachomshtua zaidi ni hali ya Geneviv kwani mwili wake umeharibika vibaya kwa ugonjwa wa ajabu. Bila kupoteza muda, anaamua kumpeleka Geneviv Hospitali usiku huo huo
“Malizeni haraka twende Hospitali Geneviv akatibiwe” Aliongea Bwana Magwaza akimharakishe Kim amalize kumsaidia Geneviv kula haraka ili waende Hospitali.
Muda mchache baadae wakawa tayari kwa kuondoka. Bwana Magwaza hakutaka kumwambia Geneviv mahali aliko mama yake, alitaka kufanya kama Surprise ili kuwaongezea nguvu ya kupona haraka. Wakaingia ndani ya gari na safari ya kuelekea Hospitali ikaanza. Walienda kwenye hospitali ile ile aliyolazwa mama yake.
Walipofika Hospitali, Bwana Magwaza alipitiliza mpaka ofisini kwa Daktari Zayumba na akamueleza alichokutana nacho nyumbani kwake juu ya hali ya Geneviv.
“Are you serious? Its like a miracle! Where is she?” ( unasema kweli? Ni kama muujiza! Yuko wapi?) Alikuwa akiongea mfululizo daktari Zayumba akiwa kama haamini vile. Alikuwa na shauku ya kumuona Geneviv alivyo. Bwana Magwaza alimuelekeza kuwa amewaacha ndani ya gari pale nje. Kwa haraka wakatoka na kueleka pale Bwana Magwaza alipokuwa amewaacha Geneviv na Kim.
Daktari Zayumba hakuyaamini macho yake kama kweli Yule ni Geneviv aliyekuwa akimfahamu. Alijikuta akisikia uchungu mkali moyoni na kumuonea huruma sana. Hakutaka kupoteza muda zaidi, akawaita manesi ambao nao bila ya kupoteza muda walimchukua hadi wodini walikoanza kumhudumia.
Walianza kwa kumsafisha mwili wote kwa kutumia dawa maalum ya kuzuia uambukizo (Disinfectant) kisha wakamtundikia dripu ya dawa. Alilazwa na matibabu yakawa yanaendelea. Hakujua kuwa mama yake yuko hapohapo Hospitali katika wodi nyingine akipewa huduma nzito.
Baada ya kuhakikisha wote wanahudumiwa vizuri,Bwana Magwaza alirudi nyumbani kwake, akimuacha Kim pale Hospitali. Alikuwa akienda kuandaa mipango madhubuti ya kuwashikisha adabu ndugu wa mzee Rwakatare ambao ndio walikuwa sababu kubwa ya Bi Patricia na mwanae kupata mateso makubwa namna ile. Alijiapiza kuwashikisha adabu ili iwe fundisho kwa wote wenye tabia kama ile.
Hakupata shida kuamua nini cha kufanya kwani tayari alishakuwa na uzoefu wa kutosha wa kupambana na jamii zinazoamini ushirikina. Aliendelea kupanga mikakati kabambe, na akawa anasubiri kupambazuke ili aanze kazi mara moja.
Saa kumi na moja Alfajiri, Bwana Magwaza alikuwa mbele ya gereza kuu alimokuwa amefungwa Bwana Magafu (Shemeji wa Bi Patricia).
Aliomba kuonana na mkuu wa gereza ambapo alimsimulia kila kitu kilichosababishwa na Bwana Magafu na ndugu zake kwa Bi Patricia na mwanae.
Tofauti na nchi nyingine, serikali ya Blaziniar ilikuwa ikiamini juu ya uchawi na nguvu za giza na ilipitisha sheria kadhaa za kuwatia hatiani watu wanaoshutumiwa kuwadhuru wengine kichawi, ambapo hukumu yao ilikuwa kali kuliko ya wezi au majambazi.
Bwana Magwaza na mkuu wa gereza walifikia uamuzi wa kwenda kuwatia nguvuni wote waliohusika na nguvu za giza zilizowadhuru Bi Patricia na mwanae Geneviv. Kulipopambazuka, Bwana Magafu alienda kutolewa gerezani na akiwa chini ya ulinzi mkali, alitakiwa kuwapeleka askari zaidi ya sita kijijini kwao ili wakawashughulikie wote waliohusika na kuwadhuru Bi Patricia na mwanae.
Magari mawili ya polisi aina ya Defender, yalikuwa yakitimua vumbi kuelekea kijijini iliko asili ya ukoo wa mume wa Bi Patricia, ukoo wa Rwakatare. Bwana Magafu alikuwa amefungwa pingu akiwa chini ya ulinzi wa polisi wenye silaha akitakiwa kuonyesha njia ya kuelekea kijijini kwao. Baada ya safari ndefu, hatimaye wakawa wamekikaribia kijiji wanachoishi ukoo wa Rwakatare.
Wanakijiji walipoona magari mawili yanakuja kwa kasi huku yakitimua vumbi, wakajua ni Bwana Magafu, waliyemtuma kwenda kuuza nyumba na kumrithi mjane ndio alikuwa anarudi. Waliamini ameshamaliza kazi aliyotumwa na ukoo, wakawa wanapiga vigelegele na kushangilia wakijua utajiri wote sasa ni mali yao.Walishangaa kuona polisi wenye silaha wakishuka garini wakiwa na ndugu yao Magafu, akiwa amefungwa pingu. Kila mmoja akianza kutafuta njia ya kukimbilia, lakini polisi waliwawahi na kuwaweka chini ya ulinzi mkali.
Bila ya kupoteza muda, viongozi wa ukoo walitiwa nguvuni na kuunganishwa na ndugu yao Magafu na baada ya kuwapakia ndani ya magari ya polisi, Bwana Magafu alipewa nafasi ya kuzungumza na wanaukoo wanaobaki. Aliwaonya kuwa wakitaka ndugu zao waachiwe huru, lazima wahakikishe Bi Patricia na mwanae wanapona haraka iwezekanavyo,vinginevyo ndugu zao wangeishia jela.
Aliwatolea vitisho vingi ikiwa ni mbinu kali ya kisaikolojia ya kuwamaliza nguvu za uchawi. Mbinu kama ile ilikuwa ilikuwa ikitumiwa sehemu nyingi kunapotokea shutuma za matumizi ya nguvu za giza na matokeo yake ilikuwa ni kufanikiwa kuwamaliza kabisa wachawi na kuwafanya waishiwe nguvu za kuroga tena.
Baada ya kuwachimba mkwara wa nguvu, magari ya polisi yalianza safari ya kurudi mjini, viongozi watano wa ukoo wakiwa wameunganishwa na Bwana Magafu na kutiwa pingu chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Baada ya masaa mengi ya safari ngumu, hatimaye waliwafikisha gereza kuu na wakaingizwa ndani chini ya ulinzi mkali. Walifungiwa kila mmoja kwenye chumba chake peke yake ili kuwazuia kuwasiliana na kukusanya upya nguvu ya giza.
****
Masaa machache baada ya ndugu wa ukoo wa marehemu Rwakatare kutiwa gerezani kwa makosa ya kusababisha mateso kwa Bi Patricia na mwanae kwa kutumia nguvu za giza, wana ukoo waliokuwa wamebakia kijijini waliitana kwenye kikao cha dharula cha kujadili nini cha kufanya ili kuwaokoa wenzao.
Walifikia muafaka wa kutegua mitego yao yote ya kichawi waliyokuwa wamewategea Bi Patricia na mwanae ili wapone. Hawakuwa na njia nyingine zaidi ya hiyo kwani walishaambiwa kuwa mpaka wapone ndipo ndugu zao watakapoachiwa huru. Wazee wa mila walianza kufanya mambo yao wakizivunja nguvu zote walizokuwa wamezitega ili kuwadhuru Bi Patricia na mwanae.
Katika hali ya kushangaza, Bi Patricia alirudiwa na akili zake kwa haraka na akajikuta yuko wodini manesi wakikimbia huku na huko kumsaidia.
“She is awake! Amepona!” manesi walikuwa wakipeana taarifa baada ya kuona Bi Patricia amerejewa na fahamu zake kwa haraka mno.
Hakuna aliyeamini kilichotokea kwani Bi Patricia alikuwa amepona kabisa ndani ya muda mfupi. Alikuwa hajui ni nini kilichomtokea mpaka akawa na hali kama ile. Akawa anawauliza manesi ambao kila mmoja alikuwa akimpa pole kwa yaliyompata.
Muda huo huo, kwenye wodi aliyokuwa amelazwa Geneviv, manesi walikuwa wakishangaa kilichotokea. Ndani ya muda mchache mno, Geneviv alipata nafuu kubwa mno. Vidonda vyote mwilini vilikauka na alama zikawa zinapotea haraka.
“What is happening here?”(Nini kinachotokea hapa) Aliuliza nesi mmoja baada ya kushindwa kuelewa kilichokuwa kikiendelea kwani mtu na mama yake walikuwa wakipata nafuu kwa kasi ya kushangaza.
“Ama kweli hapa duniani kuna uchawi! Kumbe ni kweli walikuwa wamerogwa…maskini! Mungu wao amewapigania” manesi walikuwa wakizidi kujadiliana. Muda mfupi baadae, Bwana Magwaza na mwanae Kim walikuja kutazama hali za wagonjwa wao zinavyoendela. Hakuna aliyeamini kumuona Bi Patricia akiwa amerudiwa na akili zake timamu huku Geneviv naye naye akiwa ameshapona ugonjwa wa ajabu. Walienda ofisini kwa daktari Zayumba na wakamuomba wawakutanishe rasmi, mtu na mama yake kwani kwa muda wote huo hakuna aliyejua mwenzake yuko wapi.
Bi Patricia alikuwa bado akishangaa shangaa mle wodini, mara akaona mlango unafunguliwa na wanaingia watu wanne, wakiongozwa na mwanae Mpendwa Geneviv. Alijikuta akiinuka kwa nguvu na kumkimbilia mwanae. Walikumbatiana kwa nguvu hadi wakadondoka wote hadi chini. Hakuna aliyeamini kuwa hatimaye wamekutana tena baada ya kupitia kipindi kigumu kuliko vyote maishani mwao. Waliendelea kukumbatiana pale chini huku kila mmoja akitoa machozi ya furaha.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kim naye alikumbatiana na baba yake kwa furaha. Hakika walijiona kama mashujaa baada ya kufanikiwa kuwaunganisha Geneviv na mama yake. Daktari Zayumba alikuwa amesimama pembeni akiwatazama walivyofurahi. Baada ya muda, waliinuka na Bwana Magwaza akawa anaongea na Bi Patricia wakati Kim akiwa bega kwa bega na Geneviv.
Baada ya kuhakikisha hali zao zimekuwa nzuri na za kuridhisha, Bwana Magwaza aliomba waondoke hadi nyumbani kwake hadi watakapopona kabisa. Bi Patricia aliridhia na wakaanza kujiandaa kutoka kuelekea kwa kina Kim. Baada ya muda wakawa tayari wameshatoka Hospitali na wakawa wanaelekea nyumbani kwa kina Kim.
*******
Baada ya kufika nyumbani kwa Bwana Magwaza, Bi Patricia na mwanae walikaribishwa kwa ukarimu mno, wakaingia ndani na bila kupoteza muda Kim akaingia jikoni kuanza kuandaa chakula cha jioni.
Historia ya Kim na baba yake, ilikuwa tofauti na ambavyo ungewadhania. Kwa kuwa walikuwa wakiishi wawili tu, Kim alikuwa na uwezo wa kufanya shughuli zote za nyumbani.
Aliweza kupika, kuosha vyombo, kupiga deki, kufua na kazi zote ambazo vijana wengi wa kiume wa siku hizi hawawezi. Alilazimika kujua kufanya shughuli zote hizi sio kwa kupenda ila kwa matatizo ambayo yalitokea akiwa bado mtoto mdogo. Kwa kifupi ni kwamba Kim alikuwa hamjui mama yake zaidi ya kumuona kwenye picha, kwani alifariki dunia kutokana na matatizo aliyoyapata akiwa na ujauzito wa Kim na alimuacha akiwa na siku tatu tu duniani.
Baada ya kuondokewa na mkewe kipenzi, Bwana Magwaza alikuwa na wakati mgumu sana kwani kichanga Kim alikuwa akihitaji sana malezi ya karibu ya mama, lakini aliyakosa. Alilelewa na mahausigeli na alikulia maziwa ya ng’ombe mpaka alipokuwa mkubwa. Bwana Magwaza alijiwekea nadhiri ya kutooa tena siku za karibuni kwani aliamini asingeweza kumpata mwanamke aliyekuwa sawa na mkewe.
Kwa kuwa baba yake alikuwa ni mfanyakazi, Kim alipoongezeka umri kidogo, alilazimika kujifunza kufanya shughuli za nyumbani mwenyewe. Baba yake alikuwa na kazi ya ziada ya kumfanya asimkumbuke mama yake na alijitahidi kumtimizia mahitaji yake yote ikiwa ni pamoja na kumtafutia wafanyakazi wa kumlea, lakini Kim alipenda kujilea mwenyewe.
Kwa kuwa hakuwahi kupata penzi la mama, uwepo wa Bi Patricia na mwanae Geneviv pale nyumbani kwao, ulimfanya ajisikie hali tofauti ambayo hakuwahi kuihisi hapo awali. Alijisikia amani sana kukaa na ‘mama’ wa kufikia. Akawa anahangaika jikoni kuandaa chakula ili kuwafurahisha wageni. Bwana Magwaza alikuwa sebuleni na wageni, akiendelea kubadilishana mawazo na Bi Patricia. Geneviv naye alikuwa ametulia pembeni akiwasikiliza mama yake na baba Kim wakiwa kwenye mazungumzo yao. Baadae aliamua kumfuata Kim jikoni aliyekuwa bize kuandaa chakula cha jioni.
“Nataka nikusaidie Kupika na wewe ujisikie raha, maana najua kila siku unajipikia mwenyewe…”
Aliongea Geneviv akimtania Kim, wakawa wanacheka huku Geneviv akianza kumsaidia kazi ndogondogo. Ilikuwa ni jioni ya kipekee sana kwao. Bwana Magwaza naye aliendelea kuongea na Bi Patricia sebuleni, wakijadiliana namna ya kukomesha kabisa matatizo mfululizo yaliyokuwa yanamuandama yeye na mwanae.
Alimsimulia siri ya wao kupona ghafla namna ile, na akamueleza namna walivyoenda kuwatia nguvuni ndugu wa ukoo wa mumewe.
“Do You mean they are under arrest right now?”( Unamaanisha kuwa sasa wako chini ya ulinzi?)
Aliuliza Bi Patricia akionekana kushtuka. Bwana Magwaza alimueleza kila kitu na akazidi kusisistiza kuwa wao (Bi Patricia na Mwanae) wamepona baada ya ndugu zao kuwekwa gerezani kwa muda huku wakiacha vitisho kwa ndugu wengine waliobakia kijijini. Bwana Magwaza alitegemea Bi Patricia atafurahishwa sana kusikia ndugu zake waliomsababishia matatizo makubwa wamefungwa jela, lakini hali ilikuwa tofauti.
Bi Patricia alijisikia vibaya ndugu wa mumewe kufungwa kwa ajili yake…japokuwa walikuwa wamemfanyia unyama na ukatili wa kutisha. Hata baada ya kifo cha mumewe, bado alikuwa akiwapenda na kuwaheshimu sana ndugu wa mumewe na hakupenda wapatwe na jambo lolote baya.
“ Mi nilishawasamehe kwa yote waliyonifanyia na Mungu ndiye atakayenilipia, naongea kutoka ndani ya moyo wangu…”
Aliongea Bi Patricia kwa masikitiko akimueleza Bwana Magwaza kilichokuwa moyoni mwake. Zaidi alimsisitiza kuwa kwa kuwa wao wameshapona, basi kama kuna uwezekano afanye mpango wa kuwatoa ndugu zake wote gerezani, kuanzia bwana Magafu na wale wengine wote. Bwana Magwaza alibaki kumshangaa Bi Patricia kwani hakutegemea kusikia kauli kama ile kutoka kwake.
Alitegemea kuwa kwa sababu waliwafanyia unyama sana kiasi cha kutaka kuwatoa uhai, angekuwa na chuki kali dhidi yao. Aligundua kuwa Bi Patricia alikuwa wa kipekee sana. Ilibidi naye aeleze kilichokuwa moyoni mwake.
“You are soo unique Patricia, tangu kifo cha mke wangu mpendwa sijawahi kukutana na mwanamke mwenye roho kama yako, You deserve good!”
Bi Patricia alitabasamu baada ya kusifiwa na Bwana Magwaza na muda si mrefu, Kim na Geneviv wakawa wameshamaliza kupika na wakawa wanasaidiana kuandaa meza.
Ilikuwa ni jioni ya kipekee sana kwao. Walikuwa wamekaa kama familia iliyokamilika, ikiwa na baba, mama na watoto wawili. Wote walikuwa na furaha isiyo na kifani, huku Bwana Magwaza akiwa mwingi wa masihara, hali iliyowafanya wakifurahie sana chakula chao. Baada ya kumaliza kula, Geneviv na Kim walisaidiana tena kutoa vyombo na kusafisha meza. Wakarudi kujumuika na wazazi wao.
“Natamani sana familia hizi ziungane na kuwa familia moja, hakika tutaishi maisha ya furaha sana na bila shaka kila mmoja atasahau matatizo yaliyompata” Aliongea kwa sauti ya chini Bwana Magwaza akiwa anamtazama usoni Bi Patricia. Bi Patricia hakujibu kitu, wakawa wanaendelea kutazamana na Bwana Magwaza.
Geneviv naye alikuwa akiongea kwa sauti ya chini akimnong’oneza Kim kuwa anatamani siku moja yeye (Geneviv) awe mama na Kim awe baba na wawe na watoto wawili kama walivyokuwa pale sebuleni, Kim alitabasamu na wakawa wanatazamana na Geneviv. Baadae ukimya mkubwa ukatawala mle ndani. Bwana Magwaza alikuwa akitazamana na Bi Patricia huku macho yao yakiwa kama yanayoongea lugha moja, huku Geneviv naye akiwa anatazamana na Kim, nao wakionekana kuzungumza lugha moja ya ishara.
Baadae Bwana Magwaza aliuvunja ukimya na kuwataka wageni wakapumzike kwenye chumba chao maalum walichoandaliwa. Wakatakiana usiku mwema na Kim akainuka kwenda kuwaonyesha chumba chao. Bwana Magwaza naye aliinuka na kuelekea chumbani kwake. Kim alirudi sebuleni, na kama kawaida yake akachukua daftari zake na kuanza kujisomea. Kwa kawaida kila siku alikuwa akijisomea mpaka usiku wa manane kwani masomo ya sekondari yalikuwa magumu kwake hivyo kulazimika kutumia muda mwingi kujisomea.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Geneviv hakupata usingizi mpaka usiku sana, alikuwa akitamani kumfuata Kim pale sebuleni anapojisomea, lakini akaogopa kumuudhi mama yake kwani asingefurahia kitendo kile na angemuhisi ameanza tena tabia mbaya. Alipohakikisha mama yake amelala kabisa, alinyata na kufungua mlango. Akatoka mpaka sebuleni ambako alimkuta Kim akiendelea Kujisomea.
“Vipi! Ulikuwa bado hujalala?” Aliongea Kim kwa sauti ya kunong’ona akimuuliza Geneviv.
Geneviv hakuwa na jibu zaidi ya kumdanganya kuwa alipolala tu amemuota na ndio maana ameamua kuamka na kumfuata. Kim akatabasam kwa uchovu na kumkaribisha Geneviv, ambaye alimsogelea na kukaa jirani kabisa na Kim, akiwa amevaa kigauni cha kulalia. Kim alielewa kwa haraka kilichokuwa kinataka kutokea. Moyoni mwake alikuwa na jeraha kwani bado alikuwa na kumbukumbu ya kuangukia kwenye mikono ya msichana hatari, Alice, ambaye alimuwekea madawa ya kulevya kwenye soda na kufanikiwa kulala naye mpaka asubuhi bila ridhaa yake.
Kwa kuwa alimuamini sana Geneviv, aliona huo ni muda muafaka wa kumwambia kilichomtokea kwani aliamini angepata ahueni moyoni mwake. Alimpenda Geneviv na alitaka afahamu kila kitu kumhusu yeye. Wakiwa wamekaa jirani kabisa, alianza kumueleza kwa upole kilichomtokea . Geneviv alitega masikio kwa makini kutaka kusikia Kim atamwambia nini.
Kim alimueleza kila kitu kilichomtokea mpaka alipojikuta akilala kitanda kimoja na Alice.
“Whaaat! Ulilala na Alice? Mlitumia Kinga?”
Aliuliza kwa mshangao wa ajabu Geneviv, hali iliyomshtua Kim. Alijibu kwa kutingisha kichwa kuonyesha kuwa hakuna tahadhari yoyote iliyotumika alipokutana na Alice.
“My God! Alice is a harlot…and the great possibility is that she is living with H.I.V!” (Mungu wangu! Alice ni changudoa na uwezekano mkubwa ni kwamba anaishi na virusi vya Ukimwi) Aliongea Geneviv huku akimkumbatia Kim ambaye sasa alishtuka kupita kawaida kusikia kuwa Alice alikuwa ni changudoa. Kilichomstua zaidi ni kwamba hawakutumia kinga yoyote. Hiyo ilimaanisha kuwa kama ni kweli Alice alikuwa na virusi vya Ukimwi, basi Kim naye alishavipata.
Alijikuta akishindwa kujizuia na kuanza kulia kwa sauti, hali iliyowafanya Bi Patricia na Bwana Magwaza kushtuka. Wote wakatoka vyumbani mwao na kwenda sebuleni kuangalia kumetokea nini usiku wote ule mpaka Kim apige kelele.
“Whats happening here?”
Aliuliza bwana Magwaza akitembea kwa haraka kuelekea pale Geneviv na Kim walipokuwa wamekaa.
Ilibidi Kim atumie uongo ili kuwatuliza baba yake na Bi Patricia. Alidanganya kuwa kichwa kimeanza kumgonga ghafla na ndio maana alikuwa akilia . Aliogopa kueleza ukweli halisi kwani hakujua aanzie wapi kueleza. Geneviv alikuwa amekaa pembeni yake akiwa kimya, uso kauinamisha chini. Bi Patricia na Bwana Magwaza waliamini uongo uliosemwa na Kim kwani hawakudhani kuwa anaweza kuwa amewadanganya.
“Unasoma sana ndio maana kichwa kinakuuma, haya nenda kapumzike mpaka asubuhi, kama bado hali sio nzuri itabidi tuende Hospitali kupima damu!”
Aliongea Bwana Magwaza wakati akimsaidia Kim kunyanyuka kutoka pale alipokuwa amekaa. Alimpeleka mpaka chumbani kwake na akahakikisha amelala, ndipo naye akatoka na kuelekea chumbani kwake.
Geneviv na mama yake nao walienda kulala kwenye chumba chao.
“Sasa wewe usiku wote huu ulikuwa unafanya nini sebuleni wakati mwenzio anajisomea?” Aliuliza Bi Patricia akionyeshwa kukerwa na kitendo cha Geneviv kutoka na kumfuata kim sebuleni. Ilibidi adanganye kuwa alikuwa akimuomba amfundishe masomo ya sekondari.
Bi Miriam alimkubalia kwa shingo upande ingawa alishahisi kuwa zaidi ya urafiki wa kaka na dada, kuna kitu kilichokuwa kikiendelea kati ya Kim na mwanae.
“Yule ni kaka yako kabisa, na kuna uwezekano tukawa tunaishi hivi siku zote, usije kunitia aibu tena kwa ujinga wako, mheshimu kama kaka yako na sio zaidi ya hapo”
Aliongea Bi Patricia wakati akimpa somo mwanae Geneviv, ambaye hakujibu kitu zaidi ya kugeukia ukutani akiwa amekunja sura na kujifunika mpaka usoni. Aliona kama mama yake anamuimbia wimboasioupenda.
Aliendelea kutafakari kauli ya mama yake na hakuelewa alikuwa akimaanisha nini alivyomwambia kuwa yule ni kaka yake na wataendelea kuishi vilevile siku zote.
Alishampenda Kim na alikuwa tayari kuwa naye katika hali yeyote ile kwani alionyesha kumjali sana wakati walipokuwa na matatizo makubwa.
Fikra nyingine zilizomtesa Geneviv usiku kucha, ilikuwa ni kitendo cha Alice alichomfanyia Kim. Alimuona Alice kama muuaji na alijikuta akimchukia mno. Aliendelea kumlaumu sana kwa kumharibia uhusiano wake uliokuwa unataka kuchanua kama ua ridi.
Pamoja na yote, alijiapiza kuwa lazima awe na Kim hata iweje. “I Love him, He is my heart!”( Nampenda nay eye ndio moyo wangu).
Geneviv alikuwa akijisemea kimoyomoyo huku akijifuta machozi yaliyokuwa yanaliloanisha shuka lake. Kim naye hakupata usingizi hata tone. Hakutaka kuamini kuwa ni kweli amenaswa kirahisi namna ilê kwa Alice. Katika maisha yake hakuwahi kujihusisha kimapenzi na msichana yeyote, alikuwa mgeni kabisa katika uwanja wa huba.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alice ndio alikuwa wa Kwanza kwake, ingawa naye haikuwa dhamiri yake kufanya nae waliyoyafanya. Kilichomtisha zaidi ni kusikia kuwa alikuwa changudoa. Siku zote alikuwa akiwaogopa machangudoa kama moto wa Jehanum. Kamwe hakutaka kuamini kuwa anaweza kuwa ameambukizwa ugonjwa hatari na Alice.
Alipanga kuwa kutakapopambazuka tu, lazima ajihimu nyumbani kwa Alice. Hakuelewa anataka kwenda kufanya nini ingawa alijikuta akiingiwa na roho kali ya kisasi.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment