Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

USILIE TENA GENEVIV - 5

 











    Simulizi : Usilie Tena Geneviv

    Sehemu Ya Tano (5)



    SHED NO MORE TEARS GENEVIV



    Alice ndio alikuwa wa Kwanza kwake, ingawa naye haikuwa dhamiri yake kufanya nae waliyoyafanya. Kilichomtisha zaidi ni kusikia kuwa alikuwa changudoa. Siku zote alikuwa akiwaogopa machangudoa kama moto wa Jehanum. Kamwe hakutaka kuamini kuwa anaweza kuwa ameambukizwa ugonjwa hatari na Alice.



    Alipanga kuwa kutakapopambazuka tu, lazima ajihimu nyumbani kwa Alice. Hakuelewa anataka kwenda kufanya nini ingawa alijikuta akiingiwa na roho kali ya kisas



    “I don’t deserve this! Ooh My God! Save me from this hell fire.” ( Sistahili haya, Eeh Mungu wangu niokoe kutoka kwenye moto huu wa jehanum)

    Aliongea Kim huku akilia kwa uchungu.



    Kulipopambazuka tu, Kim alijihimu na kuelekea nyumbani kwa Alice. Ilikuwa bado ni asubuhi sana na Alice alikuwa bado amelala kwani alirudi usiku wa manane kutoka kwenye shughuli zake za kuuza mwili. Kim aligonga mlango kwa hasira, na muda mfupi baadae Alice akamfungulia. Alionekana kuchoka sana na alikuwa amejifunga kanga moja tu.



    “Aah kumbe ni wewe baby wangu! Karibu sweetie” Alice alionyesha uchangamfu wa kinafiki na akamshika Kim mkono na kumvutia ndani.



    Japokuwa Kim alikuwa amepania kumfanya kitu mbaya, kwa jinsi Alice alivyompokea, alijikuta akiishiwa nguvu na akawa anamwaga machozi kama mtoto. Alijihisi dhaifu sana mbele ya Alice, kuliko hata akivyokuwa akijihisi anapokuwa na Geneviv.



    Alice alimvuta mpaka kitandani na akamsogelea karibu kabisa. Akashtuka kumuona akimwaga machozi kama mtoto.

    “Jamani vipi tena mbona wantisha asubuhi yote hii, huyo mcharuko wako Geneviv ndio anakufanya ulie asubuhi yote hii”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kauli ile ilimpandisha sana hasira Kim, akainuka kwa jazba na kumkwida Alice shingoni. Alianza kumhoji kwa hasira kuwa ni kwa nini ameamua kumuua.

    “Mbona sikuelewi? Nimekuua kivipi! Au mcharuko wako ndio amekutuma uje kunifanyia fujo asubuhi yote hii, ntapiga kelele niseme unataka kunibaka”



    Aliongea Alice kwa jazba akijaribu kumtoa Kim mwilini mwake.

    Ilibidi Kim awe mpole kwani alikuwa amekutana na maji ya shingo, kisiki cha mpingo Alice. Alimuachia na kukaa kwenye stuli akiwa amejiinamia kichwa chini.



    Baada ya kuona ametulia Alice alimsogelea kwa upole na kuanza kumuuliza ni nini kimemsibu mpaka achanganyikiwe namna ile. Alice alikuwa fundi kisawasawa wa kubembeleza. Kim alijikuta akilainika na kuanza kueleza hofu yake baada ya kugundua kuwa kumbe Alice ni changudoa.



    Alice hakuwa na aibu hata chembe, akampasulia kuwa ni kweli yeye ni changudoa na anafanya vile sio kwa kupenda bali hali ya maisha ndio inamfanya awe vile. Alimtoa wasiwasi kuwa katika kazi yake, siku zote alikuwa akiujali sana uhai wake na hakuwahi kukutana na mwanaume yeyote bila ya tahadhari, na akazidi kumsisitiza kuwa yeye (Kim) ndio alikuwa wa kwanza kwenda nae bila Kinga, na kama ushahidi aliinuka na kufungua begi lake kisha akamtolea cheti cha daktari.



    “Nimeenda kupima wiki iliyopita tu, mimi ni mzima wa afya, sina ngoma kama watu wanavyonidhania, na ushahidi wa hili ni hiki cheti hapa.

    Kama bado huamini tuongozane hata sasa hivi tukapime upya, mi najiamini sana kwani siku zote niko makini”

    Aliongea Alice Kwa nyodo huku akiwa amemshikia kiuno Kim.



    Kim alishusha pumzi ndefu na kukichukua kile cheti kutoka mikononi mwa Alice na kuanza kukisoma. Ni kweli kilionyesha kuwa Alice hana maambukizi ya virusi vya UKIMWI kama walivyokuwa wakihisi. Hakutaka kuamini haraka akahisi kuwa labda ni cheti feki alichokinunua mitaani.



    Alice akazidi kumsisitiza kuwa kama haamini waongozane asubuhi hiyo hiyo mpaka Hospitali kurudia kupima. Kwa kiasi kikubwa imani ilimrudia Kim na akawa anapumua kwa nguvu kama ambaye haamini anachokisikia kutoka Kwa Alice. Akainuka kwa haraka na akawa anauendea mlango akitaka kutoka nje Alice alimuwahi na kumzuia mbele yake.



    “Kim naomba unisamehe kwa kitendo nilichokufanyia, sikupanga kukufanyia vile siku ile ila nilipitiwa tu, naomba unisamehe sana”

    Alikuwa akiongea Alice kwa lugha ya upole sana. Kim hakujibu kitu, akamsukumia pembeni na kutaka kutoka. Alice akamzuia tena na akamvaa mwilini kwa nguvu na kumrudisha ndani. Wakawa wanavutana kama majogoo yanayotaka kupigana.



    Bwana Magwaza aliwahi sana kuamka na kwenda kumuangalia mwanae Kim anaendeleaje. Alipofika chumbani kwake alikuta hakuna mtu, akajua labda Kim yuko uani. Alijaribu kuita lakini hakuitikiwa. Alienda mpaka kwenye chumba cha wageni na kuwaamsha Bi Patricia na mwanae waliokuwa bado wamelala.



    “Mwenzio yuko wapi?” Bwana Magwaza alimuuliza Geneviv kama anajua alipo Kim. Hakuna aliyekuwa na Jibu ni wapi alikoenda Kim asubuhi yote ile. Wakabaki kutazamana usoni. Walipoenda kuangalia mlango wa kutokea nje, ulikuwa wazi kuonyesha kuwa Kim alikuwa ametoka nje.



    Kengele ya hatari ikalia kichwani mwa Geneviv.Akahisi kuwa kwa vyovyote lazima Kim atakuwa amewahi kwenda kwa Alice kumfanyia vurugu kwa yale aliyomfanyia. Kwa jinsi alivyokuwa akimfahamu Alice, alijua lazima watafanyiana sana fujo na Kim. Akaingia ndani kwa haraka na kuvaa nguo, kisha akatoka kwa kasi akiaga kuwa anaenda kumuangalia nje.



    Alikimbia mpaka anakoishi Alice na muda mfupi baadae akawa ameshafika. Alianza kusogea kwa kunyata kusikia kama Kim alikuwa ndani… akaisikia sauti ya Alice akinong’ona chinichini kutokea ndani. Akajua lazima Kim yuko mle ndani.



    ****

    Baada ya Geneviv kuondoka kwa kasi, Bwana Magwaza na Bi patricia walibaki wakitazamana wakiwa hawaelewi nini kinachoendelea.

    “Achana nao hao, wanajuana wenyewe wala usiumize kichwa chako”

    Aliongea bwana Magwaza akimshika mkono Bi Patricia, wakaingia ndani.



    Walikuwa wamebaki peke Yao, Bwana Magwaza akaona huo ndio muda muafaka wa kujadili na Bi Patricia juu ya hatma ya maisha yao. Alirudia kauli yake aliyoitoa usiku wa siku iliyopita.



    “Patricia, naamini wewe ni mwanamke wa kipekee sana na bila shaka utaelewa vizuri ninachotaka kukwambia. Nimekuwa nikifikiria sana na nimeona itakuwa jambo la maana sana kuziunganisha familia zetu na kuwa kitu kimoja. Mke wangu alishafariki siku nyingi sana na kuniacha mpweke hapa duniani. Najua kuwa na wewe unajisikia upweke sana baada ya mumeo kutangulia mbele za haki… Kwa nini tusitoane upweke katika siku za maisha yetu yaliyobakia hapa duniani?”



    Bwana Magwaza alikuwa akimwaga sera za kiutu uzima. Bi Patricia alianza kujiumauma vidole kama msichana mdogo akikosa jibu la kumpa Bwana Magwaza. Ni kweli kabisa kuwa na yeye alikuwa akijisikia upweke sana baada ya kifo cha mumewe, lakini alishindwa kuelewa jamii ingemchukuliaje.



    ********



    Alice alihakikisha anaitumia nafasi ile ya Kim kumfuata chumbani kwake asubuhi ile kikamilifu. “Leo amejileta mwenyewe, ndege mjanja hunaswa katika tundu bovu!” Alice alikuwa akijisemea kimoyomoyo huku akitabasamu wakati wakitazamana na Kim. Zile hasira zote alizokuja nazo Kim zilikuwa zimeyeyuka kama barafu juani. Akajikuta kwa mara nyingine akiingia kwenye mtego wa mcharuko Alice. Alijaribu tena kutaka kutoka lakini Alice alimrudisha ndani na akawa anamfanyia vituko vingi ili kwa mara nyingine apate alichokitaka.



    “Kim bwana usiwe kama mtoto, mwenzio nakutaka uwe mume wangu! Ukinikubalia utakuwa umeyaokoa maisha yangu, ntaachana kabisa na biashara hii hatari ninayoifanya! Please Kim save my soul!” Aliongea Alice kwa sauti laini huku akiyalazimisha machozi kutoka machoni mwake na akapiga magoti mbele ya Kim. Wizi mtupu!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Miongoni mwa kasoro alizokuwa nazo Kim ni kuwa na huruma kupita kiasi. Alikuwa akimchukia Alice kwa aliyomfanyia, lakini kwa upande wa pili alijikuta akianza kumuonea huruma kutokana na aina ya maisha aliyokuwa akiishi. Aliogopa sana machangudoa kwani kazi yao ilikuwa ikiwaweka katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi.



    Kauli ile aliyoitoa Alice huku akipiga magoti mbele yake ilizidi kummaliza nguvu. Akaishiwa la kuongea akabaki kumtazama Alice kwa huruma. Alice naye hakutaka kulaza damu, akazidisha vituko na kuzidi kumtega Kim. Muda mfupi baadae wakawa wamekumbatiana wakirushana huku na kule juu ya kitanda. Alice alishavua kanga moja aliyokuwa ameivaa na kubaki akiwa mtupu, hali iliyozidi kumuweka Kim mtegoni. Akaanza kumsalaula Kim. Akiwa anamalizia kumvua bukta yake, walishtukia mlango ukisukumwa kwa nguvu na mtu akaingia kwa kasi ya Ajabu.



    “Kim! Kim! What are you doing with this bitch? Alice! Kwa nini unanitenda hivi lakini? Ooh my god! Why me?”

    Geneviv alikuwa akipiga kelele huku akilia baada ya kuwafuma Alice na Kim wakiwa kama walivyozaliwa juu ya kitanda cha Alice. Alijikuta akipatwa na uchungu mkali moyoni kiasi cha kuanza kulia kama mtoto mdogo akijitupa chini kwa fujo.



    Kim alipatwa na mshtuko mkubwa kupita kiasi. Alishindwa kuelewa ni nini kilichotokea, akawa kama yuko ndotoni. Kwa haraka alianza kutafuta nguo zake zilizokuwa zimetupwa chini na Alice. Alizivaa kwa upesi kisha akampigia magoti Geneviv aliyekuwa akigalagala chini akilia kwa uchungu mkubwa na kuanza kumuomba msamaha. Kuona vile Alice naye aliinuka na kufunga kanga yake kiunoni na kuanza kumvuta Geneviv kumtoa nje kwa madai kuwa alikuwa amemuharibia starehe yake.



    Ikawa ni zogo mtindo mmoja kwani Geneviv naye alicharuka na kuinuka kwa hasira akitaka kupigana na Alice. Ilibidi Kim atumie uanaume wake kutuliza mambo kwani hakika kama watu wangeshuhudia kilichokuwa kikiendelea mle ndani asubuhi yote ile, ingekuwa aibu ya mwaka.



    Geneviv alitoka kwa hasira na kupotelea kusikojulikana akiwaacha Alice na Kim wanazozana.Alice alikuwa akiporomosha matusi kwa Geneviv hali iliyomkera sana Kim, wakawa wanalumbana wenyewe kwa wenyewe. Kim alitaka kutoka kumuwahi Geneviv lakini Alice alimuwahi na kufunga mlango kwa funguo kisha akazitupia chini ya kitanda. Ikawa mshike mshike. Geneviv alikuwa ameumia mno kwani hakutegemea kuyaona yale aliyoyaona kwa Alice na Kim hasa ukizingatia jinsi alivyokuwa akimhusudu Kim. Akili yake iliacha kufanya kazi na akawa anafikiria kitu kimoja tu akilini mwake, kujiua.



    “Nitaificha wapi aibu hii mimi? Bora kufa! Siwezi kuendelea kuishi! Bora kufa!” Alikuwa akijisemesha Geneviv huku akilia kama mtoto mdogo. Hakutaka kurudi kwa kina Kim tena, akaona bora aende kufia kwenye nyumba yao. Alitembea kwa haraka akikwepa kuonekana na mtu yeyote. Muda mfupi baadae akawa ameshafika kwenye nyumba yao. Hakuogopa tena uchawi ambao ndio uliowasababisha wahame kwenye nyumba ile. Akasukuma mlango na kuingia moja kwa moja mpaka ndani. Alipitiliza mpaka chumbani kwake, akajitupa kitandani na kuanza upya kulia.



    Baada ya purukushani za muda mrefu, hatimaye Kim alifanikiwa kumzidi nguvu Alice na kutoka nje. Alianza kuhaha kumtafuta Geneviv akiwa hajui ameelekea wapi kwani ulikuwa umepita muda tangu alipoondoka na kuwaacha mle ndani na Alice. Alikimbia mpaka nyumbani kwao alikowakuta baba yake na Mama Geneviv wamekaa sebuleni.

    “Geneviv amekuja huku?” Aliongea Kim kwa sauti kubwa huku akiwa anahema kwa nguvu. Bwana Magwaza na Bi Patricia waliokuwa wamezama kwenye mazungumzo yao ya kiutu uzima walishtushwa ana Kim, wakabaki kumshangaa.



    Kilichowashangaza ni kwamba kwanza Kim aliyekuwa akilalamika usiku kuwa anaumwa kichwa alikuwa ameondoka hapo nyumbani Alfajiri na mapema bila hata kuaga, hali iliyowafanya wote wabaki roho juu. Kama hiyo haitoshi, Geneviv naye aliondoka katika mazingira ya kutatanisha akidai kuwa anaenda kumtafuta Kim. Sasa kitendo cha Kim kurudi mbiombio kiliwafanya wabaki wameduwaa.



    “Mi si nilikwambia, hawa waache wenyewe wanajuana. Aliyekuwa anatafutwa ndio huyu na yeye anamtafuta mwenzake, ujana unawasumbua!” Aliongea Bwana Magwaza kwa masihara akimueleza Bi Patricia.

    “Hapana! It seems ana tatizo huyu, hebu jaribu kuongea nae kwa upole utagundua kitu. Usipuuzie mambo namna hiyo”



    Aliongea kwa busara mno Bi Patricia, na Bwana Magwaza akaupokea ushauri ule. Bi Patricia alikuwa na saikolojia kali ya kuwaelewa vijana kwani alishajifunza mengi kutoka kwa mwanae Geneviv. Aliinuka na kumshika mkono mwanae Kim wakaelekea chumbani kwake.



    “Tell me Son! Whats wrong with you! You seems not to be alright. Tell me!” (Niambie mwanangu, una tatizo gani? Unaonekana hauko sawa. Niambie!) Bwana Magwaza alikuwa akizungumza na mwanae Kim kwa upole sana. Ilibidi Kim amueleze baba yake tukio lililotokea alfajiri hiyo. Alimueleza kila kitu maka jinsi Geneviv alivyowafuma wakiwa na Alice.



    “Come on son! Why do you hurt her while you know she is mentally stressed and she has not recovered fully?” (Kwa nini unamuumiza mwenzio wakati unajua fika kuwa akili yake bado haijatulia na bado hajapona vizuri?) Alihoji Bwana Magwaza huku akijishika mikono kichwani. Sio siri na yeye aliishiwa nguvu. Alitoka na kumuacha Kim chumbani, akaenda kumuelezea Bi Patricia.



    *****

    Baada ya kulia kwa muda mrefu, Geneviv aliinuka na kwenda kwenye duka la madawa lililokuwa jirani na pale nyumbani kwao. Alitaka kununua idadi kubwa ya vidonge vya dawa aina ya Quinine.

    “Dawa zote hizi za nini Geneviv?”



    Aliuliza yule muuzaji wa duka la madawa kwani alishtushwa na kiwango cha

    dawa alizokuwa anazitaka Geneviv.



    Ilibidi Geneviv adanganye kuwa bado yeye na mama yake wanaumwa kwa hiyo hizo dawa zilikuwa ni kwa ajili yao wote wawili. Yule muuzaji aliukubali uongo wa Geneviv, na akampatia dawa alizokuwa anazitaka. Baada ya kufanikiwa kupata vidonge Thelathini vya Quinine, Geneviv alirudi kwa haraka mpaka chumbani kwake. Akachukua kalamu na karatasi na kuandika ujumbe mfupi, kisha akauweka juu ya meza. Akajifungia kwa ndani.



    Baada ya Bi Patricia kusimuliwa na Bwana Magwaza kilichokuwa kinaendelea baina ya Kim na Geneviv, alijikuta akinyong’onyea mwili mzima. Kengere ya hatari ililia kichwani mwake na akajua kwa vyovyote lazima Geneviv ataamua kuchukua uamuzi wa kujidhuru kwani alikuwa akimpenda sana Kim.



    “Oooh My God! She may harm herself, She is real in love with Kim. I don’t know what to do! ( Mungu wangu! Lazima atajidhuru tu, anampenda sana Kim! Hata sijui nini cha kufanya). Aliongea Bi Patricia huku akianza kutokwa na machozi. Hakutaka kuona mwanae akiigia matatizoni tena.



    Aliinuka kwa haraka kutoka pale alipokuwa amekaa na kwa kasi ya ajabu akatoka na kuanza kukimbia kuelekea nyumbani kwake alikohisi lazima Geneviv ndio atakuwa amekimbilia. Njiani alikuwa akimuomba Mungu amkute salama Geneviv kwani alikuwa na uhakika kuwa lazima atajifanya kitu mbaya kwa jinsi alivyokuwa akimpenda Kim.

    ********



    Katika ujumbe aliouandika Geneviv, alisisitiza kuwa ameamua kuchukua uamuzi wa kujitoa roho baada ya kuumizwa na mtu aliyetegemea aje kuja baba wa watoto wake, Kim. Alizidi kusisitiza kuwa rafiki yake Alice amechangia kwa kiasi kikubwa yeye kufikia uamuzi ule wa kujitoa roho. Aliuweka ujumbe ule mahali ambapo ingekuwa rahisi kwa mtu yeyote kuuona kwa urahisi.



    Alichukua glasi ya maji na kumeza idadi kubwa ya vidonge, kisha akajilaza kitandani na kutulia kimya.haikupita muda akaanza kusikia kizunguzungu kikali kilichoambatana na maumivu makali ya tumbo na kichwa. Akawa anajinyonga nyonga huku povu jingi likimtoka mdomoni na puani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bi Patricia alikuwa akikimbia njia nzima kiasi cha kuwafanya watu waliomuona kuhisi amerudiwa na uendawazimu wake. Bwana Magwaza naye alitoka na kuanza kumfuata Bi Patricia kwa nyuma. Kim naye hakutaka kubaki nyuma. Kwa aibu kubwa akwa anawafuata kwa nyuma huku akijificha ficha kwani alitambua fika kuwa yeye ndio chanzo cha yote yale. Alijihisi mkosefu sana na akwa anamuomba Mungu wake wamkute Geneviv akiwa salama ili apate japo nafasi ya kumuomba radhi kwa mara ya mwisho.



    Muda mfupi baadae, Bi Patricia alikuwa ameshawasili kwenye nyumba yao. Alifungua mlango wa nje lakini akagundua kuwa ulikuwa umefungwa kwa ndani. Alijaribu kuutingisha kwa nguvu bila ya mafanikio. Akazidi kuchanganyikiwa. Muda mfupi baadae bwana Magwaza alikuwa ameshafika na kwa pamoja wakasaidiana kuuvunja mlango na kuingia ndani. Walipofika sebuleni walisikia sauti ya mtu akikoroma kwa nguvu kutoka kwenye chumba cha Geneviv.



    Waliusogelea mlango na kujaribu kuufungua lakini nao ulikuwa umefungwa kwa ndani. Ilibidi nguvu kubwa itumike kuuvunja kwani ulikuwa umefungwa kwa vitasa vyote kwa upande wa ndani. Baada ya purukushani nzito hatimaye walifanikiwa kuuvunja na kuingia ndani. Hakuna aliyeamini walichokiona. Geneviv alikuwa akijinyonganyonga kitandani kwa maumivu makali aliyokuwa anayasikia baada ya kunywa idadi kubwa ya vidonge kwa lengo la kujiua. Povu lilikuwa likimtoka kwa wingi mdomoni na puani na alikuwa akikoroma kwa nguvu kama anayetaka kukata roho.



    Wote walichanganyikiwa mno na wakawa wanatafuta mbinu ya kumuokoa haraka kabla hajakata roho. Muda mchache baadae, Kim naye aliingia na kujionea kwa macho yake kilichokuwa kikiendelea. Bwana Magwaza alimuinua Geneviv akisaidiwa na Bi Patricia na wakatoka nje na kuanza kutafuta usafiri wa haraka wa kuwawahisha Hospitali ili kunusuru maisha ya Geneviv.



    Wote walipotoka, Kim alibaki peke yake mle ndani akiwa haamini kuwa ni kweli Geneviv ameamua kujitoa uhai kwa ajili yake. Alijihisi ni mwenye hatia kubwa moyoni mwake na akabaki kujiuliza imekuwaje kwani kila kitu kilikuwa kikitokea kwa kasi sana kiasi cha kumfanya ashindwe kuelewa.

    Aliendelea kukitazama kitanda alichokuwa amelala Geneviv, huku idadi kubwa ya vidonge vikiwa vimetapakaa chini. Alipoendela kuchunguza huku na kule alikutana na ujumbe uliokuwa umeandikwa na Geneviv.



    Aliinama na kuanza kuusoma. Yalikuwa ni maneno mazito aliyoyaandika Geneviv kabla hajafikia uamuzi wa kunywa sumu. Alikuwa ameeleza wazi kuwa ameamua kujiua baada ya kusalitiwa na Kim na Alice. Kim alibaki ametoa macho akiwa haamini. Kama ingetokea Geneviv akapoteza maisha, basi yeye ndio angekuwa mhusika wa kwanza. Alijikuta akijilaumu sana moyoni mwake, alishidwa kujizuia kulia kwa uchungu mkubwa. Alipiga magoti na kuanza kumuomba Mungu wake ayanusuru maisha ya Geneviv.



    Bwana Magwaza na Bi Patricia walifanikiwa kumfikisha Geneviv kituo cha afya kilichokuwa jirani.

    “Emetic serum! Inject her on blood venules for quick feedback!”

    Daktari wa zamu alikuwa akiwaamuru manesi wake wampe haraka dawa ya kumtapisha sumu aliyokunywa kupitia mishipa yake ya damu. Wengine wakawa wanahangaika kumnywesha maziwa kwa nguvu ili kupunguza makali ya sumu ambayo sasa ilikuwa imeanza kukolea mwilini.



    Pamoja na kuhangaika kwa muda mrefu, hali ya Geneviv ilizidi kuwa mbaya na sasa uhai wake ukawa mashakani. Ilibidi yule daktari awape rufaa ya kwenda Hospitali kubwa kwani yeye pamoja na manesi wake walionekana kushindwa.

    Alipakiwa kwenye gari la wagonjwa (AMBULANCE) na akawa anakimbizwa kwenye Hospitali kuu ya Blaziniar. Ndani ya gari la wagonjwa, manesi wawili walikuwa wakizidi kuhangaika kuhakikisha wanaokoa uhai wa Geneviv.



    Baada ya safari ya kasi iliyochukua karibu nusu saa, wakawa wamefika kwenye Hospitali kuu ya Blaziniar. Ambulance iliyombeba ilipiga honi mfululizo na kwa haraka manesi wakatoka na kuja kumshusha. Aliteremshwa na kitanda chake cha kwenye gari na akawa anakimbizwa kuelekea wodini.



    Tofauti na mara zote, safari hii mama yake, Bi Patricia alikuwa ametulia kimya akitazama kila kilichokuwa kikiendelea. Hakulia wala kutoa hata tone la machozi. Alichukulia kama kila kitu ni cha kawaida, akawa anasubiri kuona nini hatma ya mwanae. Bwana magwaza ndiye aliyekuwa na wakati mgumu zaidi kwani alijua mwanae Kim ndio chanzo cha yote yale. Alijiapiza kuwa lazima afanye kila kinachowezekana kuhakikisha Geneviv anapona.



    Baada ya kuingizwa wodini, Geneviv aliendelea kupatiwa tiba ya haraka kunusuru maisha yake. Madaktari walikuwa wakipigana vikumbo wao kwa wao, kila mmoja akijitahidi kwa kadri ya uwezo wake. Walikuwa wakimhangaikia sana Geneviv kwani wengi walikuwa wakimfahamu vizuri Bwana Magwaza, ambaye aliwaambia kuwa Geneviv ni binti yake.



    “Usiwe na wasiwasi Mheshimiwa! Binti yako atapona tu. Tuachie kila kitu wala usiwe na hofu.” Daktari mmoja alikuwa akiongea na Bwana Magwaza, Bi Patricia akiwa nyuma yake. Aliwahakikishia kuwa atapona kwa kuwa alikuwa akipewa huduma ya uhakika. Bwana Magwaza alimshika mkono Bi Patricia na wakarudi kukaa kwenye viti vilivyokuwa pale mapokezi.



    “Hivi unafikiri Geneviv akipona, kile ulichoniambia asubuhi kitawezekana?” Alihoji Bi Patricia akimkazia macho Bwana Magwaza. Hakuwa na jibu la haraka kwa swali lile, akabaki kubabaika. “Mimi na wewe tukiwa mke na mume, inamaanisha kuwa geneviv na Kim watakuwa dada na kaka, wakati huyu anataka kujiua kwa kuwa anataka aolewe na Kim! Don’t you see this as a serial confusion?” Bi Patricia alitoa hoja nzito na ya msingi akimuacha Bwana Magwaza akimkodolea macho kama asiyeelewa anachoambiwa.



    “Mi nafikiri huu sio muda muafaka wa kulizungumzia hili. Tumuombee Geneviv apone kwanza mengine yatajiset baadaye.” Alijibu kwa Mkato Bwana Magwaza, kisha akageukia upande mwingine. Alichokisema Bi Patricia kilikuwa kimemuingia moyoni kisawasawa.



    Nyumbani kwa kina Geneviv, Kim alikuwa bado ndani ya chumba cha Geneviv, akiwa amepiga magoti chini na kujikunyata, akilia na kumuombea Geneviv apone. Alizidi kulia kwani hakika hatia ya maisha ya Geneviv ilikuwa juu yake. Alijilaumu sana kwa kitendo chake cha kumfuata Alice chumbani kwake kwani hicho ndio kilikuwa chanzo cha yote hayo. Ilifika mahali akajiapiza kuwa endapo Geneviv angepoteza maisha, basi na yeye angejiua.



    ****

    Baada ya tiba mfululizo, hali ya Geneviv ilibadilika na taratibu akaanza kupata nafuu. Madaktari waligundua tatizo kubwa sana kwenye mfumo wa fahamu wa Geneviv na wakawa wanahangaika kupunguza tatizo.



    “ Tumegundua tatizo kubwa, kuna uwezekano mkubwa binti yako akapoteza uwezo wa kuona na kusikia kwani sumu ya Quinine imeshambulia vikali milango yake ya fahamu. Tuanaendelea kujtahidi kupunguza tatizo”

    Whaaat? Ina maanisha Geneviv atakuwa ahwezi kusikia wala kuona? Oooh my God…”

    Bi Patricia ugumu ulimuishia na akajikuta akianza kulia.



    Kim aliendelea kuwaza kwa muda mrefu bila ya kupata jibu ya kilichotokea. Aliona kila kitu kama ni maluelue yanayotokea kwa kasi kubwa, akawa ni kama aliyechanganyikiwa. Aliendelea kukaa mle chumbani mwa Geneviv kwa muda mrefu akiwaza na kuwazua nini cha kufanya. Nafsi yake ilikuwa ikimsuta sana kwa kumsababishia Geneviv matatizo makubwa kama yale. Siku zote maishani mwake alikuwa akipigania kumuona Geneviv akifurahi na kusahau matatizo yote yaliyokuwa yanaiandama familia yao, lakini sasa alijikuta yeye ndio akiwa tatizo kubwa zaidi kwa Geneviv.



    Aliendelea kulia kwa muda mrefu lakini bado hakuhisi ahueni yoyote moyoni mwake. Mara alikumbuka kitu ambacho ndicho alichokiona kinafaa zaidi kwa wakati ule. Akiwa shule alizoea kuwasikia vijana wenzake wakimweleza jinsi ambavyo madawa ya kulevya huweza kumfanya mtu kusahau shida zake zote. Aliona hicho ndio kitu pekee kitakachomfaa kwa wakati ule.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakuwahi hata mara moja kufikiria kuwa ipo siku atawaza kutumia madawa ya kulevya, lakini sasa aliona ni lazima afanye hivyo akiamini atakuwa amepunguza kwa kiasi kikubwa hofu, woga na mawazo yaliyokuwa yakimuandama akilini mwake juu ya yaliyompata Geneviv. Kilichomuumiza zaidi nai zile hisia za kujiona yeye ndio chanzo cha kila kitu kilichompata Geneviv. Alijikuta akijiingiza kwenye mtego hatari zaidi.



    Bila ya kupoteza muda aliinuka na kuanza kutoka ndani ya ile nyumba ya kina Geneviv. Alienda mpaka kwenye kilinge kimoja walichokuwa wakishinda watoto wa mitaani wanaotumia madawa ya kulevya maarufu kama ‘mateja’ au ‘chokoraa’. Alipofika na yeye alijichanganya kati yao na akatoa pesa mfukoni mwake na kumpa kijana mmoja aliyekuwa anauza madawa, ambaye wenzake walikuwa wakimwita kwa jina lao walilozoea la ‘Pusha’.



    Wengine walikuwa wakiendelea kuvuta bangi na kula unga (Cocaine) huku wakipiga stori zao na kufurahi. Kwa kuwa Kim hakuwahi hata mara moja kujichanganya nao zaidi ya kuwapita kwa mbali akitoka shule, wote walikuwa wakimtazama na kunong’onezana maneno ya chinichini.

    Yule muuzaji wa dawa za kulevya, alikaa jirani na Kim na akawa anamfundisha namna ya kula unga baada ya kugundua kuwa alikuwa hajui kabisa.



    “Mwanangu, acha ukuda, inatakiwa ufanye kama mimi, niangalie vizuri! Unanisoma?” Yule kijana muuza dawa za kulevya alikuwa akiongelea puani akimwonyesha Kim namna ya kuvuta unga.



    Alimuelekeza namna ya kuvuta kwa kutumia pua, na taratibu Kim akawa anavuta. Kwa kuwa ilikuwa ni mara yake ya kwanza, baada ya kuvuta kidogo tu, alijikuta akiwa na hali ambayo hakuwahi kuihisi maishani mwake.



    ”Im flying without wings! Kumbe nilikuwa nikikosa vitu vizuri namna hii! Niongeze tena Bro!” Aliongea Kim kwa sauti ya kilevi kabisa. Akatoa hela na kumpa tena yule pusha, kasha akaongezewa mzigo. Wakiwa wanaendelea kupata dozi ya Cocain, Kim alishangaa kumuona mtu kama Alice akija kwenye lile kundi la wale vijana na kujichanganya nao.



    Kwa kuwa tayari alikuwa ameshalewa, Alishindwa kuzingatia alichokiona, lakini aligundua kuwa ni kweli yule aliyemuona alikuwa ni Alice naye akija kununua madawa ya kulevya. Alijipenyeza katikati ya wale vijana ambao walionekana kuwa na uswahiba nae kwani wote walikuwa wakimuita kwa jina lake.



    Akafika mpaka kwa yule muuzaji ‘Pusha’ na wakasalimiana kihuni kisha akakaa na kuagiza dozi yake. Alikuwa bado hajamuoana Kim kuwa yuko pale pale. Kim ambaye sasa alianza kuhisi mwili wote ukikosa nguvu na kuzingirwa na usingizi mzito hukufahamu zikimtoka. Aliinama na akawa anasinzia kutokana na kuzidiwa na dawa za kulevya.



    “Oyaa, huyu si Kim mtoto wa mama?, ameanza lini kutumia mambo ya kikubwa kama haya, asije kutuletea msala hapa”

    Alisikika kijana mmoja akiongea kwa kumdhihaki Kim ambaye sasa alikuwa amehama kwenye ulimwengu wa kawaida na kuzama ulevini. Hapo Ndipo Alice alipogundua kuwa Kim naye alikuwepo eneo lile, jirani kabisa na pale alpokuwa amekaa akiwa hoi kwa madawa ya kulevya.



    Licha ya kushtushwa na uwepo wake pale, alijiona kama mshindi kwani aliona huo ni muda mwingine mzuri wa kumfaidi Kim, tena safari hii akiwa hajitambui kwa kula unga.

    Alimsogelea pale alipokuwa amejiinamia, akamshika mkono na kumnyanyua, akawa anaondoka naye kumpeleka nyumbani kwake huku wale vijana wa kihuni wakishangilia kwa nguvu. Kim alikuwa hajielewi tena, akawa anamfuata Alice kama kondoo anayepelekwa machinjioni. Muda mfupi baadae wakawa tayari wamefika kwa Alice.



    ***

    Hali ya Geneviv ilikuwa bado sio ya kuridhisha kwani licha ya kuendelea kupewa tiba mfululizo hakuweza hata kufumbua macho yake. Akawa amelala kama mfu, ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi kwenye Hospitali kuu ya Blaziniar. Madaktari waliendelea kumhangaikia lakini bado hali yake haikubadilika.



    “Tulia mama Geneviv, unavyozidi kulia unamkosea Mungu wako, Amini yeye ana uwezo wa kumuokoa mwanao. Mangapi ameshakufanyia Ndio atashindwa hili! Tuliza moyo mpendwa.”



    Bwana Magwaza alikuwa akimbembeleza Bi Patricia ambaye baada ya kuambiwa kuwa mwanae hatakuwa tena na uwezo wa kuona wala kusikia alianza kulia kama mtoto mdogo. Bwana Magwaza aliendelea kumbembeleza kwa upole wakiwa pale kwenye sehemu ya mapokezi. Bi Patricia alimuelewa na akaacha kulia akiamini kuwa lazima hilo jaribu nalo litapita kama mengine yote yalivyopita.



    “Lakini Roho inaniuma sana mimi! Kwanini kila siku ni mimi tu, likiisha hili linaanza lingine, nimekuwa mtu wa kushinda Hospitali kila siku, mwisho wake si itakuwa ni uhai wangu kutoka! Eeh Mungu, kama kweli upo, nyoosha mkono wako kwangu na uniokoe.”



    Alikuwa akiongea Bi Patricia kwa uchungu mno. Bwana Magwaza aliendelea kumfariji kwa karibu sana. Masaa yalizidi kwenda na hali ya Geneviv ikawa bado sio ya kuridhisha, ikabidi Bwana Magwaza amshawishi Bi Patricia waende kupumzika kidogo halafu wangerudi baadae kuendelea kumuuguza Geneviv. Bi patricia hakuwa mbishi tena kwani moyo wake ulionekana kufa ganzi. Wakatoka na kurudi nyumbani kwa Bwana Magwaza.



    ***

    Baada ya Alice kumkuta Kim akiwa katika kijiwe cha watoto wa mitaani wanaotumia madawa ya kulevya, alifanikiwa kumchukua na kwenda naye nyumbani kwake. Kwa kuwa Kim alikuwa hajitambui baada ya kuvuta dozi kubwa ya madawa ya kulevya kwa mara ya kwanza, Alice alipata nafasi nyingine ya kufanya alichokitaka kwa Kim. Alimuingiza mpaka ndani na kuanza kumwagia maji ya baridi kupunguza nguvu ya madawa aliyobwia. Baada ya Kim kurudiwa kidogo na fahamu zake, alimvua nguo zote na kumlaza juu ya kitanda chake, kisha naye akavua za kwake.



    Ilivyoonyesha, Alice alikuwa amenogewa na mchezo waliokuwa wakiufanya na Kim kwani kama lengo lake lilikuwa ni kulipa kisasi kwa Geneviv, tayari hilo alishalifanikisha lakini bado aliendelea kumganda Kim kama Ruba, akitumia udhaifu wake kama silaha ya kumnasa kirahisi. Waliendelea na mchezo wao kwa muda mrefu mpaka jioni kabisa, Kim akiwa hana fahamu za kutosha baada ya kula unga mwingi. Fahamu zilipokuja kumrudia kisawasawa alijikuta akiwa amekumbatiwa kwa nguvu na Alice, wote wakiwa watupu. Akajua kwa mara nyingine tena amenasa mikononi mwa Alice na kuangukia dhambini.



    Safari hii hakuwa mkali tena kama ilivyokuwa awali, kwani alijua kupanic kwake badala ya kupunguza matatizo, mara zote kulikuwa kukimwongezea matatizo.



    “Kim, najua nakufanyia kitu ambacho hukifurahii kabisa, lakini ukweli ni kwamba na mimi sipendi kukufanyia hivi ila moyo wangu ndio unaonituma Kim. Najua kwa tabia zangu sistahili kuwa mpenzi wako, lakini nilishakwambia Kim, ukinikubali nitaacha kila kitu nilichokuwa nakifanya.”



    Alice alikuwa akiongea kwa hisia kali akiwa amelala kifuani kwa Kim. Aliyalazimisha machozi kutoka kwenye macho yae ili Kim aamini kile alichokuwa anamwambia. Alizidi kulalama kimahaba…

    “Namimi nina haki ya kupendwa Kim hata kama nilikuwa changudoa! Naahidi nitalitunza penzi lako kwani umenionyesha ulimwengu tofauti maishani mwangu, sikuwahi kumpenda yeyote, nilikuwa natafuta pesa tu Kim, ila kwako nakiri kuwa nakupenda kwa dhati na nataka nikuzalie watoto”



    Maneno yale yote aliyokuwa anayatoa Alice, hayakumwingia Kim ambaye sasa alikuwa akiwaza hatma ya Geneviv huko Hospitali. Madawa ya kulevya aliyoamini yangemsahaulisha matatizo yake, yalimfanya aangukie tena mikononi mwa Alice na kujikuta akirudia mchezo ule ule uliomfanya Geneviv akafikia uamuzi wa kujitoa roho. Alikuwa akikumbuka jinsi Geneviv alivyoumia alipowakuta alfajiri wakiwa ndani ya chumba hicho hicho. Kumbukumbu zile zilimfanya ashindwe kuyazuia machozi. Alice akawa anamfuta na kuzidi kumbembeleza akihisi alikuwa akitokwa na machozi baada ya kuguswa na kile alichokuwa anamueleza.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Im sorry Geneviv, I didn’t intend to hurt you! Forgive me my Queen! I will never do this anymore” ( Nisamehe Geneviv, sikukusudia kukuumiza, nisamehe malikia wangu! Sitarudia tena) Alikuwa akilalamika Kim kwa uchungu, hali iliyomkasirisha sana Alice. Alitambua fika kuwa Kim alimpenda Geneviv kuliko yeye. Hakukata tamaa, akawa anajiapiza kuwa lazima ayabadili mawazo ya Kim mpaka amsahau Geneviv.



    Masaa yalizidi kuyoyoma na giza likaanza kuingia, Kim akiwa bado ndani ya chumba cha Alice. Alitamani kupata tena dozi nyingine ya madawa ya kulevya kwani hisia zilizokuwa zinapita akilini mwake zilikuwa zikimuumiza sana. Alice alilitambua hilo na akainuka na kwenda kumletea unga (Cocaine) aliyokuwa ameificha kwenye kimkoba chake kidogo. Walisaidiana kuvuta na baada ya sekude chache, wakapitiwa na usingizi mzito.



    Baada ya Bwana Magwaza na Bi Patricia kufika nyumbani kwao, walianza kazi nyingine ya kumtafuta Kim ambaye haikufahamika yuko wapi kwani tayari giza lilishaingia.

    “Huyu ni mtoto wa kiume, achana nae atarudi mwenyewe nyumbani.” Aliongea Bwana Magwaza kumtuliza Bi Patricia ambaye alishaanza kuingiwa upya na wasiwasi. Waliandaa chakula cha mgonjwa, kisha wakajiandaa na kurudi tena Hospitali. Bwana Magwaza alikuwa bega kwa bega na Bi patricia na alijitahidi kwa kadri ya uwezo wake wote kumsahaulisha matatizo yake.



    Baada ya kupitiwa na usingizi mzito kwa muda mrefu, Alice alikuwa wa kwanza kushtuka kabla ya Kim aliyekuwa bado anakoroma. Akawa anapanga mikakati ya kufanya ili kuhakikisha Kim hamkumbuki tena Geneviv. Aliona njia bora ni kwenda kummaliza kulekule Hospitali ili kuwa na uhakika wa kumpata Kim kwa asilimia mia moja kwani aliamini Geneviv ndio kikwazo pekee kwake. Akawa anapanga mkakati wa jinsi ya kwenda kutekeleza azma yake hiyo.

    ********

    Bi Patricia na Bwana Magwaza wanaendelea kukaa Hospitali kwa muda mrefu wakimuuguza Geneviv ambaye bado ana hali mbaya kwani tangu alipofikishwa Hospitali hapo, alikuwa bado hajarudiwa na fahamu zake na madaktari walishasema kuwa hata kama angepona, angepoteza kabisa uwezo wa kuona na kusikia. Waliendelea kujadiliana nini cha kufanya ili kunusuru hali yake na Bwana Magwaza akawa na wazo jipya.



    “Inawezekana bado nguvu za kichawi za ndugu zenu zinawaandama, mi nafikiri kitu muhimu nikafuatilie taratibu za kuwatoa Bwana Magafu na ukoo mzima gerezani kwani naamini kwa siku hizi walizokaa lupango, hawataweza kurudia tena kufanya ujinga wao, nikishakamilisha hili itabidi tumpeleke Geneviv kanisani pamoja na wewe mkaombewe ili mikosi kama hii isiwarudie tena.”

    Bi Patricia alikubaliana na wazo lile na akamruhusu Bwana Magwaza aendelee na taratibu zote.



    Bwana Magwaza aliaga na kuondoka akimuacha Bi Patricia akiendelea kumuangalia mwanae pale wodini. Alikuwa akiendelea kusali kimoyomoyo ili apone, na zaidi alifurahia kitendo cha Bwana Magwaza kwenda kuwatoa gerezani ndugu zake kwani aliamini mikosi yote ingeisha. Muda mfupi tangu Bwana Magwaza aondoke, Kim alifika Hospitali huku akiwa na wasiwasi mkubwa. Aliuliza mapokezi na akaelekezwa wodi aliyokuwa amelazwa Geneviv, na kwa unyonge mkubwa akawa anatembea kuelekea wodini.



    Bi Patricia aliwahi kumuona kabla yeye hajawaona, na kwa kumtazama tu, alitambua kilichokuwa ndani ya mawazo yake. Alimuona jinsi alivyokuwa akisutwa na nafsi yake kwa matatizo aliyomsababishia Geneviv. Ilibidi Bi Patricia ageuke kuwa mshauri nasaha kwani aliamini Kim hakufanya vile kwa makusudi, na hata kama ilitokea basi ilikuwa ni bahati mbaya kwani siku zote yeye ndio alikuwa mfariji mkuu wa Geneviv.



    “Usiumie sana mwanangu! Mungu ana kusudi lake kwa kila jambo. Geneviv atapona na haya yote yatapita. Usijiumize nafsi yako bure, muombe Mungu wako akusamehe na muombee mwenzio apone.” Bi Patricia alikuwa akizidi kumpa somo Kim ambaye kila neno lililotoka kwa Bi Patricia lilikuwa likiuchoma mno moyo wake. Akawa anabubujikwa na machozi kwa wingi wakati akimtazama Geneviv aliyekuwa amelala kama mfu juu ya kitanda cha wagonjwa.



    Hakuweza kufumbua macho wala kugeuka, mwili wake ulikuwa umetulia tuli. Hali ile ilizidi kumtia uchungu mkali na akajikuta akilia kwa sauti, hali iliyomlazimu Bi Patricia amshike mkono na kutoka nae nje. Walienda kukaa kweye Bustani ya maua iliyokuwa ndani ya ile Hospitali na Bi Patricia akawa anazidi kumfariji Kim.



    ***

    Baada ya Kim kuwahi kuondoka asubuhi bila kuaga, Alice naye alijitayarisha haraka na akawa anamfuata nyuma nyuma bila ya Kim kufahamu kuwa anafuatiliwa. Aliamini kuwa kwa vyovyote atakuwa anaenda Hospitali kumuona Geneviv, akaona huo ndio muda muafaka wa Kwenda kummaliza Geneviv.



    Alichukua bomba la sindano kisha akaweka kiasi kikubwa cha Cocaine aliyokuwa nayo ndani ya chumba chake. Aliamini kabisa kuwa kwa kiwango kile alichokuwa amekiweka kwenye bomba la sindano, endapo angepata nafasi ya kumchoma Geneviv lazima angekufa haraka kwani madawa ya kulevya na dawa za Hospitali vikichanganywa pamoja vilikuwa vikitengeneza sumu hatari.



    Aliendelea kumfuata nyuma nyuma Kim mpaka walipofika Hospitali. Akawa makini kumtazama angeingia wodi gani. Baada ya kumuona akiuliza pale mapokezi, naye alijichanganya kwa watu akijificha Kim asije akamuona. Alimsindikiza kwa macho mpaka alioingia wodini. Akajua kazi yake inaelekea kukamilika. Aliendelea kukaa pale mapokezi kwa muda, akikodolea macho mlango wa ile wodi aliyoingia Kim. Roho ya kishetani ilikuwa imemuingia na hakuwa na huruma tena.



    Baada ya muda mchache, alimuona Kim akitoka akiwa ameshikwa mkono na mwanamke ambae alimtambua mara moja kuwa ni mama yake Geneviv. Alishusha pumzi ndefu kisha akageukia upande mwingine kujificha asionekane usoni. Aliendelea kuwatazama kwa jicho la wizi mpaka walipopita jirani kabisa na pale alipokuwa amekaa, wakielekea nje. Aliendelea kuwasindikiza kwa macho mpaka alipowaona wakikaa kwenye bustani ya maua iliyokuwa nje ya ile wodi.



    Alipohakikisha wametoka kabisa, aliinuka kwa haraka na kuanza kuelekea kwenye ile wodi aliyokuwa amelazwa Geneviv. Alifungua mlango ambao ulikuwa umeegeshwa na moja kwa moja macho yake yakatua juu ya kitanda alichokuwa amelazwa Geneviv huku dripu za dawa zikiendelea kutiririka kuingia mishipani mwake. Alishusha pumzi ndefu na akawa anakisogelea kile kitanda taratibu. Alisogea mpaka jirani kabisa, akawa anamtazama Geneviv aliyekuwa hana fahamu kabisa juu ya kilichokuwa kinaendelea. Alitoa bomba la sindano kutoka kwenye kimkoba chake kidogo na kuanza kulitikisa kwa nguvu kuchanganya ile sumu iliyokuwa ndani yake.



    “Wewe ni rafiki yangu kipenzi Geneviv, roho inaniuma sana lakini sina cha kufanya. Ni lazima ufe ili nipate nafasi ya kuwa na Kim. Nampenda sana Kim na nataka awe baba wa watoto wangu. Buriani Geneviv!” Aliongea Alice kwa sauti ya chini, kisha akatoboa sehemu ndogo ya dripu ya dawa iliyokuwa ikitiririka kuingia mwilini mwa Geneviv. Aliichanganya ile dawa na Cocaine iliyokuwa kwenye bomba la sindano. Akaitingisha kwa nguvu kuhakikisha imechanganyikana vizuri, mchanganyiko ule hatari ukawa unatiririka kuingia mishipani mwa Geneviv.



    Kwa kasi ya ajabu akatoka wodini na kuanza kuharakisha kutafuta njia ya kutokea nje ya Hospitali ile bila ya kushtukiwa na mtu yeyote. Alifanikiwa na muda mfupi baade akawa kwenye geti la nyuma la kutokea nje. Mlinzi alimsimamisha na kumuuliza kwa nini alikuwa akipitia mlango wa nyuma wakati geti la mbele lilikuwa wazi.



    ***

    Bi Patricia hakuwa na habari juu ya kilichokuwa kikiendelea wodini alikomuacha mwanae Geneviv. Alikuwa akizidi kumbembeleza Kim ambaye naye alikuwa akizidi kulia kwani hali aliyomuona nayo Geneviv ilimuumiza sana roho yake. Baada ya kubembelezwa na kupewa faraja kwa muda, alianza kurudi kwenye hali yake ya kawaida. Mara walishtukia kuona manesi wakikimbia kuelekea kwenye chumba alicholazwa Geneviv. Wakainuka kwa haraka na kuanza kukimbia kuelekea kule wodini, lakini walizuiwa mlangoni.



    Geneviv alikuwa akitapatapa kitandani akiwa ni kama anayetaka kukata roho baada ya sumu iliyowekwa kwenye dripu yake ya dawa kusambaa mwilini. Manesi walikuwa wakihangaika kumuokoa wakiwa hawajui ni nani aliyefanya unyama ule. Cha ajabu ni kwamba, wakati Geneviv akitapatapa, aliweza kutoa sauti na kufumbua macho yake, hali ambayo haikuwezekana kabla ya hapo. Madaktari walitoa amri ya Geneviv kurudishwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi na kwa haraka aliwekwa juu ya kitanda chenye magurudumu na akawa anakimbizwa ICU.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Its wonderfull that instead of killing her, it makes her recover her mental ability” ( Ni maajabu kuwa badala ya kumuua, sumu aliyowekewa imemrejeshea fahamu zake). Madaktari walikuwa wakijadiliana wakati wakichunguza ni aina gani ya sumu ilichanganywa kwenye dripu la mgonjwa Geneviv. Waliendelea kuua makali ya ile sumu, na katika hali ya kushangaza zaidi, makali ya sumu yalipoisha, Geneviv alikuwa amefumbua macho na akawa analia akiomba mama yake aletwe. Kila mtu mle wodini alibaki kuduwaa kwani hali kama ile haikuwahi kutokea.



    Alirudishwa kwenye wodi aliyokuwa amelazwa awali, lakini safari hii ulinzi uliongezwa mara dufu. Bi Patricia alizuiwa kabisa kuingia wodini na akawa amekaa eneo la mapokezi akiwa na Kim. Bwana Magwaza alipigiwa simu na muda mfupi baadae alifika Hospitali akiwa anahema kwa nguvu kwani alihisi mambo yameharibika. Alipofika aliwakuta Bi Patricia na Kim wakiwa pale mapokezi na wakamueleza kila kitu kilichotokea. Wote walibaki kushangaa kwani hawakuelewa ni nani aliyefanya kitendo kile.



    Baada ya muda mfupi, daktari aliwaruhusu waingie wodini kumuona mgonjwa wao kwani alikuwa amepata nafuu kubwa ndani ya muda mfupi.



    “Geneviv my queen, forgive me please! I will do this no more, ni shetani alinipitia…nisamehe tafadhali.” Alikuwa akilia Kim akiwa amepiga magoti pembeni ya kitanda cha Geneviv. Hakumjibu kitu zaidi ya kuendelea kumwaga machozi.

    “Mwenzio anakuomba msamaha, maandiko matakatifu yanasema samehe saba mara sabini”. Bi Patricia alikuwa akimsaidia Kim kuomba msamaha kwa Geneviv, akiwa amemkumbatia mwanae. Bwana Magwaza alikuwa amesimama pembeni akisikiliza yote yaliyokuwa yanaendelea. Hakuwa na neno la kuongeza zaidi.



    Wakiwa wanaendelea kuombana radhi, daktari aliiingia wodini na akawapa taarifa kuwa kuna binti amekamatwa na walinzi akijaribu kutoroka kupitia mlango wa nyuma, na ilivyoonyesha yeye ndiye aliyehusika kumuwekea mgonjwa sumu.



    “Yuko hapa kwenye jengo la walinzi. Njooni mumuone labda mnaweza kumtambua.” Aliwataarifu daktari na wote wakatoka kwenda kumuona muuaji wao, wakiwaacha Kim na Geneviv peke yao wodini.



    *****

    Alipanga kuwalaghai walinzi hata ikibidi kwa kuwapa penzi lake, ilimradi tu wamuachie. Ilikuwa ni kama bahati kwake kwani wale walinzi waliondoka wote na kumuacha akiwa chini ya ulinzi wa mtu mmoja, ambaye naye alianza kuonyesha masihara kwa Alice. “Hapa hapa sifanyi makosa” Alijisemea kimoyomoyo Alice wakati akijiandaa kuanza kumtega yule mlinzi.



    Baada ya kumfanyia vituko vya hapa na pale, mlinzi alijikuta akiingiwa na shetani na kutamani kuvunja amri ya sita na binti Alice. Kwa muonekano wa nje, usingeweza kumdhania Alice kuwa ni changudoa. Alionekana kama bado ni mwanafunzi tena ambaye bado ni mbichi kabisa. Alimzidishia vituko mlinzi mpaka akili yake ikawa imehama, akiwaza kitu kimoja tu akilini mwake, kumfaidi Alice.



    Alice alijirahisisha kama kawaida yake, yule mlinzi akamkumbatia kwa staili ya kutaka kuvunja amri ya sita. Hakulaza damu, akili yake ikawa inacheza kama Kompyuta. Mikono yake aliingiza kiufundi mifukoni mwa mlinzi na akawa anatafuta funguo za mlango wa kutokea nje. Baada ya mlinzi kuzidiwa, alimuomba Alice ampe hisani, naye bila ya hiana akakubali kwa sharti moja tu, la kuachiwa huru.



    Mlinzi ambaye sasa alikuwa amerukwa na akili kabisa, alimvutia Alice kwenye chumba cha walinzi na kuanza kulifaidi tunda la mti uliokatazwa. Alice aliutumia vizuri muda ule na akafanikiwa kumchomoa funguo yule mlinzi kutoka kwenye mfuko wake. Wakati akiwa amezama kwenye huba la shetani, Alice alikurupuka kwa nguvu na kumrusha yule mlinzi pembeni. Alivaa nguo yake na ndani ya dakika chache baadae akawa kwenye mlango wa kutokea.



    Aliingiza funguo kwenye kitasa na akafanikiwa kufungua na kutoroka akimuacha yule mlinzi akiwa bado hajitambui baada ya kuonjeshwa sumu ya penzi la Alice. Baada ya kufanikiwa kutoka, alikimbia mpaka ng’ambo ya pili ya barabara na kuanza kutimua mbio kwa kasi kurudi nyumbani kwake. Alimshukuru Mungu wake kwa kumuwezesha kutoroka na kuukwepa mkono wa Sheria.



    Kwa kuwa hakuna aliyemuona kati ya Geneviv , Kim au wazazi wao, aliamini hawataweza kuja kugundua kuwa ni yeye ndiye aliyamfanyia Geneviv kitu kile. Akilini aliendelea kuamini kuwa sumu aliyomchoma Geneviv lazima ingemuua muda mchache baadae na yeye angepata nafasi ya kujivinjari na Kim kwa uhuru.



    Kwa mara ya Kwanza alijikuta akiwa mtumwa wa penzi la Kim kiasi cha kuwa tayari kufanya lolote ili ampate. Alijishangaa kwa nini anase kimapenzi kwa Kim namna ile wakati tayari alikuwa ameshakutana na kulala na wanaume karibu wa kila aina. Alijiapiza kuwa atafanya lolote lile aliwezalo mpaka Kim awe wake na alijiapiza kuwa endapo Kim angemkubalia kabisa basi alikuwa tayari kuachana na biashara yake ya uchangudoa.



    “Hata kama mimi ni changudoa, nahitaji kupendwa! Na mimi ni binadamu kama wengine ila ni hali ya maisha ndio iliyonilazimisha niwe hivi. Nikubali Kim uyaokoe maisha yangu.”



    Alice alikuwa akiongea peke yake baada ya kufanikiwa kufika salama nyumbanii kwake. Alikuwa amejilaza kitandani huku machozi yakimtoka. Penzila kijana mdogo Kim lilikuwa limempagawisha kabisa na sasa akawa anamuwaza yeye tu akilini mwake. Alijua itakuwa ngumu sana kwa Kim kumkubali lakini alijipa moyo kuwa hakuna lisilowezekana.

    *****

    Bwana Magwaza akifuatana na Bi Paricia na mwanae Kim walitoka na kuelekea kwenye chumba cha daktari mkuu wakitaka kuonyeshwa mtuhumiwa aliyekamatwa kama wangeweza kumtambua.



    “Kwani mlikuwa bado hamjaenda kumuona tangu muda ule?” Alihoji Daktari kwa mshangao kwani alishaagiza wapelekwe wakamuone muda mrefu uliopita. Aliinua mkonga wa simu yake ya mkononi na kumpigia mlinzi aliyekuwa zamu, ambaye kwa hofu kubwa alimwambia kuwa mtuhumiwa wao ametoroka katika mazingira ya kutatanisha na haifahamiki amekimbilia wapi.



    Taarifa zile ziliwafanya wote wabaki wameduwaa. Ikabaki kuwa siri sirini juu ya mtu aliyetaka kumtoa Geneviv uhai. Akilini mwake Kim alishajua kuwa lazima ni Alice aliyafanya kitendo kile, akajikausha kama na yeye hafahamu kitu.



    “Basi tumuachie Mungu, labda ni miujiza yake kwetu. Tumshukuru kwa kumbadili muuaji kuwa mponyaji” Aliongea Bi Patricia na wote wakatabasamu kwa furaha kutokana na kauli ile . Wakatoka na kurudi wodini ambako Geneviv alikuwa amelazwa. Walimkuta akiwa amekaa juu ya kitanda chake, akionesha kurudiwa na nguvu zake zote.



    Taratibu za kutoka Hospitali zilifanywa na baada ya muda mfupi wakaruhusiwa. Daktari alimpa maelekezo Bi Patricia kuwa mgonjwa alitakiwa kupumzishwa kwa muda mrefu na akaonya kumuepusha na mambo yote ambayo yangeziumiza tena hisia zake. Daktari alisisitiza kuwa lazima akae mbali kabisa na mtu aliyemfaanya akataka kujiua vinginevyo angerudia tena jaribio lake kwani tayari akili yake ilishaathirika kisaikolojia.



    Bi Patricia aliukubali ushauri wa daktari mbele ya Bwana Magwaza na akaahidi kuwa atafanya kila liwezekanalo ili kumlinda mwanae mpaka apone kabisa. Baada ya kutoka Hospitali, Bi Patricia alienda na mwanae Geneviv nyumbani kwake. Alimshukuru Bwana Magwaza kwa msaada mkubwa aliowapa ila akamuomba kuwa anahitaji kuwa na muda wa kukaa na binti yake ili wayaanze maisha mapya.



    Bwana Magwaza alikubaliana na Bi Patricia na akamruhusu kwa moyo mkunjufu akiamini kuwa baada ya yote kupita na kusahaulika, lazima ndoto yake ya kuishi na Bi Patricia kama mkewe ingetimia. Kim hakutaka kabisa kuendelea kumuona Geneviv machoni kwa kuhofia kumuumiza tena. Alijiapiza kuwa huo ndio mwisho wake kukutana na Geneviv. Roho ilimuuma sana lakini hakuwa na jinsi, aliukubali ukweli na kujitenga mbali na Geneviv.



    Geneviv na mama yake wakawa wameyaanza maisha mapya ndani ya nyumba Yao, huku Kim na baba yake nao wakiendelea na maisha yao kama kawaida.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Pamoja na Geneviv na mama yake kuamua kuanza ukurasa mpya wa maisha na kusahau kila kitu, bado akili ya Geneviv ilikuwa haitulii kila alipomfikiria Kim, ambaye sasa alikuwa amebadilika kabisa. Kim hakuwa tena yule aliyemfahamu. Hakuenda tena kumtembelea nyumbani kwao na hakupata hata muda wa kuagana naye. Alikuwa ameamua kuyaanza maisha mapya kivyake, maisha tofauti kabisa na aliyozoea kuyaishi.



    “Mwanangu we tulia na Mshukuru Mungu kwa kila kitu. Huenda Mungu hakupanga wewe uwe na Kim na ndio maana haya yote yakatokea. Wewe ni mzuri na endelea kujitunza utampata tu atakayekufaa maishani.” Bi patricia alikuwa akimpa moyo mwanae baada ya kuona alivyoanza kuhangaika kumtafuta Kim. Alishindwa kuzidhibiti hisia zake, hali iliyomfanya mama yake awe na kazi ya ziada.



    Siku zilizidi kwenda na taratibu Geneviv akaanza kumsahau Kim mawazoni mwake. Baada ya mama yake kuona kuwa ameshaanza kurudi kwenye hali yake ya kawaida, alianza kumfanyia mipango ya kuanza shule ikiwa ni njia ya kumfanya asahau kabisa matatizo aliyopitia masihani mwake.



    “Cant Believe it that im going to start Secondary education! very funny! (Siamini kama ni kweli naenda kuanza sekondari mimi! Furaha iliyoje!) Aliongea Geneviv kwa furaha wakati mama yake akimpa taarifa kuwa anatakiwa kujiandaa kujiunga na kidato cha kwanza siku chache zijazo.



    Kwa upande wa Kim, mambo yalikuwa tofauti sana,kwani hisia za kushtakiwa na dhamira zilizidi kumsumbua na kumfanya ajione kama mkosaji sana hapa duniani. Hali hiyo ilimfanya aanze kuonesha mabadiliko makubwa sana ya kitabia ambayo baba yake, Mzee Magwaza aliweza kuyagundua waziwazi.



    Alianza kuchelewa kurudi nyumbani na akawa akirudi anapitiliza kwenda kulala. Hakuwahi kuwa na tabia kama hiyo hata siku moja. Mabadiliko haya yalianza siku Geneviv alipotaka kujiua kwa ajili yake.



    “Son!, you seems not to be alright! You come back home in mid-nights and you behave like a hooligan. Tell me what is weighing in your mind” (Mwanangu, unaonekana hauko sawa! Unarudi nyumbani usiku wa manane na umeanza kuwa kama mhuni hivi. Niambie nini kinachokusumbua mawazoni mwako.”



    Bwana Magwaza alikuwa amemkalisha mwanae Kim akimdadisi sababu za kubadilika kwake kitabia. Kim hakuwa na jibu zaidi ya kuinama chini akionekana kuzama kwenye dimbwi la mawazo. Akawa kila anapoulizwa kuhusu mienendo yake na kinachomsumbua akilini mwake, haelezi chochote zaidi ya kujiinamia chini.



    Bwana Magwaza alitambua haraka kuwa mwanae amepatwa na msongo mkali wa mawazo na kulikuwa na kila dalili kuwa tukio la Geneviv kutaka kujiua kwa ajili yake lilikuwa limemuathiri sana kisaikolojia. Akawa anatafuta namna ya kumsaidia. Hakusikika kumtaja tena Geneviv kama ilivyokuwa hapo awali, hakutaka hata kwenda tena kumtembelea kwao. Ikawa muda wa mchana akitoka shuleni anajifungia chumbani kwake na jioni ikifika anaondoka kuelekea anakokujua mwenyewe mpaka usiku wa manane.



    Ilibidi Bwana Magwaza kwa kushirikiana na Bi Patricia waanze kumfuatilia Kim kujua huwa anaenda wapi. Kazi haikuwa ngumu kwani siku chache baadae waligundua kuwa huwa anajichanganya na kundi la vijana wa mtaani kwao ambao wanafahamika vizuri kwa matumizi ya madawa ya kulevya,ikiwemo Cocaine na Marijuani.



    “Kim is Dopping? Cant believe! This is a reason behind his behavioural changes…Oooh my God, he is finished.” (Kim anatumia madawa ya kulevya? Siamini! Hii ndio sababu ya kubadilika kwake kitabia…eeeh Mungu wangu, amekwisha).



    Bwana Magwaza aliongea kwa kustaajabu mno baada ya kugundua kuwa kumbe mwanae alikuwa ameanza matumizi ya madawa ya kulevya. Bi Patricia alimtuliza sana na akamtahadharisha kuwa akitumia ukali kamwe hataweza kupata ufumbuzi wa tatizo lile la mwanae.



    Kwa Bwana Magwaza hili lilikuwa jipya kabisa. Kwa haraka akaanza kutafuta njia ya kumnusuru mwanae kutoka kwenye tabia hatarishi kama ile. Baada ya kumbana sana, Kim alikiri kuwa ni kweli anatumia madawa ya kulevya na akaeleza wazi kuwa anafanya vile kwa sababuya Geneviv.

    “Kwa sababu ya Geneviv kivipi? Yeye yuko salama kwao na wewe uko kwenu. Niambie kwa nini unafanya hivi?”



    Kim aliendelea kusisitiza kauli yake kuwa Geneviv ndio sababu ya yeye kufanya vile. Bwana magwaza akaona njia bora ni kumhamishia mbali na pale nyumbani kwao ili amsahau kabisa Geneviv. Alifanya mipango haraka na akamtafutia shule ya Bweni nchini Kenya na baada ya siku chache taratibu zote zikawa tayari. Alisafirishwa kimya kimya mpaka jijini Nairobi kuyaanza maisha mapya kwenye shule ya bweni ya wavulana ya Kasarani Boyz Camp iliyoko katikati ya jiji la Nairobi. Hakupata hata nafasi ya kuwaaga marafiki zake.



    Taratibu naye akaanza kumsahau Geneviv na akaachana na tabia ya matumizi ya madawa ya kulevya. Kwake ilikuwa rahisi kuacha matumizi ya madawa ya kulevya kwani yalikuwa vado hayajamkolea mwilini. Akabadilika na kurudi kuwa kama alivyokuwa zamani. Alisahau kila kitu na akawa akiutumia muda wake mwingi kujisomea. Baba yake alimwambia kuwa hatarudi nyumbani mpaka kipindi cha likizo ya mwezi Desemba na itakuwa hivyo mpaka atakapohitimu masomo yake.



    Siku chache baada ya Kim kupelekwa jijini Nairobi, Geneviv alianza rasmi masomo yake ya sekondari, kidato cha kwanza kwenye shule ileile aliyokuwa anasoma Kim kabla hajahamishiwa Nairobi. Ilikuwa ni furaha ya aina yake kwa Geneviv kuungana na rafiki zake waliosoma pamoja shule ya msingi. Akawa anajihisi ni kama amezaliwa upya.



    Bi Patricia naye aliamua kuanza kazi tofauti kabisa maishani mwake. Alifungua kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu kwa kushirikiana na Bwana Magwaza. Baada ya muda mchache wakaanza kampeni maalum ya kuwakusanya watoto wote wenye shida. Walianza na Alice ambaye mwanzoni aliwasumbua sana lakini baadae wakafanikiwa kumtoa katika ajira mbaya ya uchangudoa na wakawa wanamfanyia utaratibu wa kuanza shule.



    Bi Patricia hakusahau kijiji wanachoishi ndugu wa ukoo wa mume wake ambao kipindi cha mwanzo walitaka kumuua yeye na mwanae. Uhasama wao ulimalizwa kabisa baada ya wale wote waliokuwa gerezani kuachiwa huru. Waliendelea na maisha yao kama kawaida. Walianza kumuogopa na kumheshimu Bi Patricia baada ya kugundua kuwa ni mwanamke shupavu ambaye hayuko tayari kuyumbishwa na mtu. Migogoro yote ikamalizwa kwa tambiko maalum la kijadi na wakaanza ukurasa mpya kama hakuna kilichotokeaa kati yao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maisha yakarudi kuwa ya furaha na amani kama zamani. Uzuri wa Geneviv ukaanza kuchanua upya, safari hii akiwa ameongezeka na kuwa mkubwa. “Im now a beatiful lady” (Sasa nimekuwa binti mrembo). “Hebu niangalie mama” Geneviv alikuwa akimuonesha mama yake jinsi nguo zake za shule zilivyokuwa zinampendeza.Sitalia tena! I will shed no more tears! Aliongea Geneviv kwa hisia kali, wakakumbatiana kwa nguvu na mama yake.

    ******

    Mwisho wa Season 1



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog