Simulizi : Sikutegemea
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kabla hata sijakaa vizuri manyunyu madogo madogo yakaanza kudondoka, nilirudi ndani huku bado nikiwa na wasiwasi sana. Moja kwa moja nilielekea mpaka katika chumba cha kuongozea chombo hichi. Huko niliwakuta wote wakiwa wameshughulika na computer, “Capatain tumebakiwa na muda gani mpaka kufika Afrika kusini” nilimuuliza Capatain Sadick. “Kwa makadirio ya kawaida tumebakisha wiki mbili tu” alinijibu lakini sura yake ilionekana kujawa na hofu. Wakati tunaendelea kuongea ghafla meli ilipigwa na wimbi kubwa sana mpaka kupelekea vitu kadha kuanguka.
“Capatain, upepo umezidi kuwa mkali na mawimbi pia yamezidi kuwa makali”aliongea mtu mmoja. “kwa makadirio mawimbi yana ukubwa gani” aliuliza Capatain Sadick. “Kwa sasa yana ukubwa wa mita kumi kwenda juu lakini kadri muda unavyokwenda yanazidi ukubwa” alijibu huku akiweka sawa kifaa maalum alichoweka sikioni kwake. “Unataka kunambia mpaka usiku yatakuwa yashakaribia mita kumi na sita” aliuliza Captain Sadick huku akiwa amekodoa macho. “Nina wasiwasi huenda yakazidi ukubwa huo, hii ni kutokana na kuwa upepo unavuma kwa kasi sana” alifafanua.
Capatain Sadikck aliniangalia kisha akasema, “usiku wa leo utakuwa mkubwa sana”. Aliinuka sehemu aliokuwa amekaa na kuelekea katika sehemu yake husika. Alivyoongea hivyo sikuwa tena na la kuuliza maaana nilishafahamu kitakacho tokea. Nilitoka katika chumba hicho na kuelekea chumbani kwangu ambako nilikaa kitandani huku nikisikilizia chombo hicho kinanvyopambana na mawimbi. Wakati nikiendelea kusikilizia,nilisikia king’ora kikilia na kufahamu kuwa tulikuwa tunahitajika kwa kikao cha dharura. Nilinuka kitandani na kutoka ndani ya chumba hicho.
Nilipofika sehemu tunayokutana, wengine wengi walikuwa wameshafika. Baada dakika kama mbili hivi Capatain Sadick aliingia huku akiw na mavazi ya kazi kabisa. Mara nyingi alikuwa akivaa nguo za kawaida tu lakini siku aliingia akiwa na gwanda zake za unahodha. “Kila mtu asikilize kwa makini zaidi, tutakuwa na siku kama tatu mpaka nne za pepo na mawimbi makali mble yetu hasa nyakat za usiku. Hivyo basi ndani ya kipindi chote hicho tunatakiwa tushirikiane kikamilifu ili kuvuka hilo balaa mbele yetu” aliongea. “Aye Captain” tulijibu kwa pamoja na mimi nikiwemo.
“Kila mtu avae nguo zake za kazi, maana kazi ndio kwanza imeanza” alimalliza na kusema kwa nguvu “MV KANTANA” wengine wote wakajibu kwa nguvu “King of the ships, we lead others follow (mfalme wa meli, tunaongoza wengine wanafuata)”. Kisha kila mtu akatawanyika na kurudi sehemu yake ya kazi. Kama kawaida nilifuatana na Mzee Jackson mpaka katika kile chumba cha mashine na kuvaa gwanda za buluu alizonipa. “Kijana karibu katika mapambano” aliniambia na kunikabidhi kifaa maalum cha mawasiliano kisha akaniambia niweka sikioni na mimi nikafanya hivyo.
Kifaa hicho kilituunganisha watu wote ndani ya chombo hicho kikubwa, ikitolewa amri yeyote au tangazo basi watu wote tunasikia. Tayari kiza kilishaachukua nafasi yake huku kikisindikizwa na upepo pamoja na mvua kali sana yenye radi za kutosha.. Pamoja na kuwa Mzee Jackson alikuwa ameshaanza kukonga lakini alikuwa mwepesi sana kucheza na mashine hizo. Maana alikuwa kama Dj wa club anavyochezea ile mashine yake ya kuongezea mziki. “Chief engineer Jackson niongeze miguu miwili ya ziada” nilisikia kwa ufasaha zaidi kupitia kifaa nilichoweka sikioni. “Aye Captain” Mzee Jacksona aliongea na kusogea kwenye mashine moja kubwa na kubonyeza vitufe kadhaa na mashine hiyo ikaanza kunguruma.
Tulizidi kupambana na mawimbi makali sana, “Henry na Seif nendeni juu, nataka taarifa kamili” aliongea mzee Jackson na vija na aliowataja walitoka ndani ya chumba hicho n kuelekea walipoelekezwa. Baada ya dakika kumi walirudi wakiwa wamerowa sana. “Mkuu huko nje hali ni mbaya sana, mawimbi ni makubwa kuliko kawaida. Kwa muenekano tu yana urefu wa mita kati ya kumi na tani na kumi na saba” aliripoti Henry huku akihema. “Haya mawimbi ni makubwa sana kwa mashine nane” alijisemea mwyenywe kisha akabonyeza kitufe na kuongea “Captain, nguvu inahitajika zaidi”. “Fanya mambo” alijibu captain Sadick na mzee Jackson akaamsha mashine mbili za mwisho za kati.
Yaani tulikuwa chini katika chumba hicho lakini tulihisi kabisa kama meli hiyo ilikuwa inapanda wimbi kubwa sana. Maana mpaka siki kule chini tulianguka na kila mtu akatafuta sehemu ya kushika. Kadri muda ulivyokwenda hali ilizidi kuwa mbaya. “Capatain sehemu ya deki yote imejaa maji” mkaguzi wa nje wa meli hiyo aliongea, “fungua njia maalum na ziache wazi” Captain aliongea lakini sijui nini kiliendelea kwa sababu mimi nilikuwa ndani. Safari iliendelea huku chombo hicho kikizidi kukabana koo na bahari iliokasirika na pepo zilizonuna bila kusahau radi na mvua kali kupita maelezo.
Kwa mbali tulianza kuhisi meli ikianza kutiulia na hatimae mawimbo yakaacha kabisa na mvu ikakata. Mzee Jackso alizima mashine zile alizoziongeza na kuacha itembelee na mashine sita kama kawaida. Kila mtu huko tulipokuwa sisi alifurahi sana na wengine walikumbatiana. “Tukutane mara moja” Captain Sadick aliongea kupitia kile kifaa cha mawasiliano. Kwa pamoja tulitoka na kuelekea katika sehemu ya kukutana. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwanza niwashukuru kwa kufanya kazi bega kwa bega na kufanikiwa kuvuka hatari iliotukabili. Lakini huu ni mwanzo tu na huenda siku zinazofuata hali ikawa mbaya zaidi, kama tutafanya kazi bega bega bila kusahau kuwa Mungu ndio muweza wa yote basi tutvuka majanga haya kwa rehemza zake” aliongea Captain Sadick kisha tukaomba dua ya kushukuru na kupewa ruusa ya kupumzika. Niliekea chumbani kwangu na kujilaza kitandani, ilikuwa ni saa tisa usiku. Tulipambana na mawimbi kwa muda wa masaa zaidi ya saba. kutokana na uchovu usingizi ukanichukua na kunihamisha kabisa ulimwengu.
Nilikuja kushtuka saa tano asubuhi, nilinyanyuka kivivu na kuingia chooni. Baada ya kumaliza haja zangu huko, nilitoka na kuvaa overall langu kisha nikatoka chumbani. Niliwakta baadhi ya mabaharia wakiongea mawili matatu lakini zaidi waliongelea kuhusu mshike mshike wa usiku wa kuamkia siku hiyo. Kitu kilichonishtua zaidi ni pale waliposema kuwa, kutokana na mitambo yao ya kusoma hali ya hewa. Kutakuwa na mawimbi makali zaidi ya yale ya usiku, sikutaka kuuliza kitu zaidi ya kusalimia. Kisha nikachukua kikombe kujiwekea kahawa kidogo kwa ajili ya kuchangamsha damu.
Nilipomaliza niliondoka hapo na kuelekea chumba cha kuongozea meli. Huko nilimkuta Captain Sadick akiwa kajiinamia huku ameshika picha mkononi. “Mbona unaonekana una majonzi hivyo” nilimuuliza na swali langu hilo ndilo lilimshitua, “ah hakuna kitu” alinijibu huku akijaribu kukwepesha macho yake. “Usijali kwa uwezo wa Mungu tutafika salama, yote ni mitihani ya kutuma ni kiasi gani tunamuamini” niliongea kama njia ya kumpoza. “Adam mambo mengi haya kwako ni mageni na laiti ungeelewa dhoruba zitakazofuata basi ungejifungia ndani kwako ukasubiri matokeo” aliniambia na kunishangaz kidogo.
“Yaani mimi nimepitia mengi sana kiasi kwamba sasa siogopi tena hata kufa” nilimjibu kwa sauti iliojaa ukakamavu. “Mimi nakuamini sana tena sana, na nina imani na uwezo wako” nilimpa moyo. Aliniangalia kisha akatabasamu sana na kusema “kweli mzee Jackson hajakosea” aliongea na kuniacha njia panda. Aliinuka na kuelekea kwenye usukani mkubwa kisha akageuka na kuniangalia na kuongea “unasubiri nini sasa, nenda kanipe mambo tuchape mwendo”. “Aye Captain” niliitika kwa nguvu na kutoka ndani ya chumba hicho.
Nilikwenda kwenye chumba cha mashine na kufanya yangu, “tayari kuondoka” niliongea kupitia kile kifaa cha mawasiliano baada ya kubonyeza kitufe fulani hivi. Honi kali ilisikika na nanga iliokuwa imeachiwa ilipandishwa na safari ikaanza tena. Nilikaa huko huko kwenye chumba hicho huku nikifuata maelekezo yote alioyatoa Captain. Baada ya saa moja Mzee Jackson alifika na kuchukua nafasi yake kama kawaida. “Tusikilizane kwa makini, leo usiku tunategemea tena kukumbana na dhoruba lakini hii ya leo huenda ikawa nzito kuliko ya jana hivyo ushirikiano unahitajika kwa nguvu zote” mtu wa mamlaka ya hali ya hewa aliongea.
“Chief engineer kwanini tusiokoe muda kipindi hichi cha mchana ili kama usiku hali itakuwa mbaya kama ilivyosemwa tuwe angalau tmeopiga hatua” niliongea nikiwa karibu na mzee Jackson. “Wazo lako zuri sana” alinijibu kisha akawasiliana na Capatain Sadick kupata ruhusa ya kufanya hivyo nae captain aliunga mkono. Hapo sasa mashine zote kumi ziliwashwa na kuanza kutekeleza majukumu yake. Kwa mara ya kwanza niliona meli ikitembea kasi kiasi kile.
Nilitoka nje kabisa ili kuthibisha mwendo huo, kweli waliposema MV KANTANA inaongoza wengine wanafuata hawakukosea kabisa. Meli hio ilikuwa inakwenda kasi si mchezo, tulitembea kwa muda wa masaa matano mfululizo kwa kasi hiyo na kufanikiwa kutembea masafa marefu kweli kweli. Jioni ilipoanza kuingia tu mawingu yalianza kununa na taratibu yakaanza kulia, upepo nao ukaungana na mvua na kuizidisha makali. Hata hivyo mwendo ulikuwa ule ule wa mwanzo.
Usiku sasa ndio shughuli yenyewe ilianza, ile ya jioni ilikuwa na trela tu. Nilirudi katika chumba cha mashine na kuungana na mzee Jackson pamoja na wanamitambo wengine. Henry na Seif kama kawaida yao walikwenda nje na kuangalia hali ya mawimbi, walirudi na kuripoti kuwa mawimbi hayana tofauti na ya jana kwa urefu lakini yana nguvu zaidi kuliko ya jana. “Captain unamaamuzi yeyote” aliuliza mzee Jackson, “Yeah, Give me full power (ndio nipe nguvu yote)” alijibu capatain Sadick. “Vijana kaeni kwenye siti zeni na kila mtu acheze na mashine yake, utakuwa usiku mkubwa leo” aliongea Mzee Jackson na wale wanamitambo wengine waliitika na kila akasogea kwenye kiti chake na kukaa. “Adam kaa kweny kiti hichi” aliniambia huku akionesha kiti cha pembeni yake huku yeye akifunga mkanda wake vizuri. Wala sikutaka kujua zaidi nilisogea kwenye kiti na kukaa kisha nikafunga mkanda kabisa. “Okay pirates, make the baby cry” aliongea kwa nguvu na kila mtu katika nafasi yake alibonyeza kitufe. Hapo sasa mpaka mlio wa mashine ukabadilika, niliviangalia vile visahani vya kwenye zile mashine na kuona mishale yake ikigonga kwenye alama nyekundu.
Nilianza kusikia honi moja kali sana na ndefu ikiambatana na honi ndogo ndogo kadhaa, mimi nilekuwepo huko chini nilihisi kasi ya meli hiyo. Sasa sikupata picha waliokuwa juu. Nilihisi kabisa meli hiyo ikichapana na mawimbi na mara kadhaa nilihisi ikiinuliwa juu na kupiga chini kwa nguvu. Iliendelea na mchezo huo ila kwa bahati mbaya mara moja ilikumbana na wimbi zito sana. Wimbi hilo lilipelekea baadhi ya vyuma katika chumba hicho kuchomoka. Na bahati mbaya zaidi kimoja kilitua kchwani mwa Mzee Jackson na mabaharia wengine wawili wakakumbana dhahama kama hiyo. Masiki Mzee Jackson alipoteza fahamu papo hapo kwenye kiti chake.
“May day, may day we have man down” mwanamitambo mmoja aliongea huku akijifungua mkanda na kuwasogelea wenzake wawili ambao walikuwa hawajitambui na hilo ndio kosa alilofanya maana meli ilikumbana na wimbi kali sana lilipelekea yule mwanamitambo kupigizwa katika ukuta kwa nguvu. “Kaa hapo hapo ulipo usifungue mkanda” niliongea kwa nguv baada ya kumuona Seif akihangaika kufungua mkanda. “Lakini huyo mwenzetu tukimuacha hapo atazidi kuumi” alilamika, “nafahamu lakini kwa sasa hatuna jinzi mpaka tumalize hili balaa kwanza” nilimjibu na yeye akakubali japo kwa shingo upande.
“Tuliendelea kupepetwa kama mchele ungoni lakini hakukuwa na njia nyingine zaidi ya kuomba amani tu. Baada ya matano ya dhoruba hizo hatimae bahari ilitulia na kubakiwa na mawimbi madogo madogo tu ya kawaida. Tulizima mashine na kubakisha zile sita kamakawaida, nilifungua mkanda na bila kuuliza nikafungua mlango na kupeleka salamu kuwa tuna majeruhi. Mabaharia kadhaa walifuatana na mimi mpaka katika chumba cha mitambo na kuwabeba majeruhi wote na kuwapeleka chumba cha huduma ya kwanza na kuanza kuwapatia matibabu.
“Huvu umepata wapi ujasiri wa aina ile” aliniuliza Seif, “unajua kuna muda inabidi binaadamu ufanye maamuzi magumu kwa manufaa ya wengine, hivi unadhani wanamitambo wengi mungeumia chombo kingesimamiwa na nani” nilimjibu huku nikijiwekea barafu katika sehemu ya juu ya paji la uso ambako kulikua na kauvimbe kadogo. Kauvimbe hicho nilikipata baada kupigwa na nati ilioruka kutoka sehemu yake iliofungwa. Wakati huo pia tulikuwa katika sehemu ya kukutana tukiongea mengi wakati tukisubiri majibu kutoka kwa mtabibu ambae alikuwa anawahutubia wale waliokutwa na majanga.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya robo saa alitoka huku akiwa kajiinamia, jambo lilitujulisha kuwa taarifa zilikua si nzuri. “Captain na wenzangu kwa ujumla, nina taarifa mbili moja mbaya na nyingine nzuri. Mbaya ni kuwa tumempoteza mwanamitambo msaidizi engineer Ayoub na taarifa nzuri ni kuwa waliobakiwa wote wako salama ila sidhani kama Frank na Isham wataweza kufanya kazi kwa kipindi hichi kutokana na majeraha makubwa kichwani” alituambia na taarifa hizi zilikuwa kama mwiba kwetu. “Bwana ametoa na bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe” aliongea mzungu mmoja huku na wenzake wote wakaitika “Amen”. “Innaa lilaahi wa innaa ilayhi rajiuun” maneno hayo yalituto kwa pamoja mimi na captain Sadick pamoja na waislamu wengine katika chombo.
Mwili wa engineer Ayoub ulisafishwa vizuri na kuwekwa katik friji maalum kwa ajili ya kuhifadhiwa mpaka tutakapofika na kuupeleka kwa familia yake. “Jamani yaliotokea yametokea bado tunasafari ndefu sana mbele yetu” Captain Sadick alisimama na kuongea kama mkuu wa chombo hicho. “Kwani tumebakiwa na siku ngapi mpaka kufika Afrika kusini” aliuliza Seif, “kutokana kasi tuliokuwa tunatembea nayo tumebakisha kama siku kumi tu” alijibu bwana mmoja. “Capatain inabidi tuendeleee na safari usiku na mchana wote ili tuzidi kupunguza masafa” mshauri mmoja wa captain Sadick aliongea.
Seif alipewa nafasi ya kukaimu pengo la Mzee Jackson na Henry akakaimu nafasi ya engineer Ayoub. Mimi nilipewa nafasi ya seif na James akachukua nafasi ya Henry, “kila mtu kwenye nafasi yake, Seif nipe nguvu yote” alitoa amru captain Sadick na pia kuumpa amri Seif. Tuliondoka na Skuelekea katika chumba cha mitambo, Seif alifanya kama alivyoambiwa na kuwasha mashine zote kumi. Safari iliendelea japo haikuwa tena na furaha kama mwanzo lakini tungefanyae na kazi ya Mungu haina makosa.
Hakuna aliepumzika mpaka kufikia jioni ambako mvua kama kawaida yake ilianza tena, japo mwanzo haikuwa na upepo mkali.
Lakini kadri muda ulivyoyoyoma ulizidi kuwa mkali, nikiwa katika chumba kile cha mitambo alikuja mtu mmoja na kunambia kuwa Mzee Jackson ananihitaji. Niliacha kila kitu na kuelekea chumbani kwake ambako alikuwa amepumzika. “Kijana nataka nikupe jukumu zito” aliongea punde tu nilipofika, “jukumu gani tena” nilimuuliiza huku nikikaa kwenye kiti.
“Unajua katika maisha yangu nimefanya kazi na kukutana na wengi lakini sijawahi kukutana na mtu mweny kichwa chepesi kama chako. Pia napenda sana na unavyochukua maamuzi mazito” aliniambia huku akiniangalia. Nilijifanya kama sijafurahi lakini kichwa kilikuwa kama dunia kwa ukubwa. “Sasa jukumu lenyewe ni hili, hii meli sasa inataka mtu mwenye maamuzi kama yako. Nikiwa na maanza maamuzi magumu. Siku za nyuma zote tumekutana na dhoruba lakini zote zilikuwa cha mtoto kulinganisha tutakayo kutana nayo leo. Hivyo hichi kikipata mtu mwenye kushindwa kuchukua maamuzi ya haraka huenda tukaangamia wote. Leo tunakatiza katika moyo wa bahari ya Pasifiki, kawaida sehemu hiyo kunakuwa na mawimbi makali sana hata kama hali ya hewa ni nzuri” alinieleza na kunifanya nimeze funda kubwa la mate.
“Leo kuna mvua na upepo mkali sana, jiuliza hali itakuaje. Baada ya kukuambia hayo nakiacha chombo hichi mikononi mwako rasmi. Maamuzi yeyote utakayoamua ndio yatakuwa hatima ya meli hii” alimaliza kuongea na kunikabidhi funguo ya chumba cha mashine za dharura. Zile nne za pembeni. Kisha akaniambia niende nikaendelee na kazi niliopewa. Maneno yake hayakuacha kuzunguka kichwani mwangu, maana mwanzo sikuifahamu maana kamili aliokusudia. Nilifika katika chumba cha mashine na kukaa kwenye kiti changu huku bado nikiwaza.
“Captain tunatizo” aliongea Seif kupiti kifaa kile cha mawasiliano na hivyo watu wote kwenye meli walisikia vizuri.
“Tatizo gani” Captain Sadick aliuliza, “mashine nambari mbili na sita zinapungua nguvu” alijibu. Aliposema tu maneno hayo ndio nikakurupuka sasa na maana ya maneno alioniambia mzee Jackson nikaanza kuipata. “Moyo wa Pacific, maamuzi magumu na funguo za chumba cha mashine za ziada” nilijisemea maneno hayo, huku nikijaribu kuyaleta katika uhalisia na ndipo nikapata maana kamili. “Captain, Adam hapa naongea” niliongea bila kufikiri mara mbili, “Adam subiri kwanza tunashughulikia mambo muhimu” Captain aliongea kwa nguvu. Kabla hata sijataka kuongea neno jingine, nilitahamaki nikohewani na kujipigiza katika ukuta wa vyuma wa meli hiyo.
Ghafla ndani ya chumba hicho mabomba yakaanza kutoa maji yalioruka kwa kasi sana, “Captain, chini kumepasuka” Seif aliongea kwa nguvu huku akikimbilia mlangoni, “tokeni huko kabla mfumo wa dharura wa kufunga milango haujapanda hewani” Captain Sadick aliongea na ghafla wanamitambo wote wakaanza kukimnbilia mlangoni. Lakini mimi kila nilipotaka kukimbilia mlangoni maneno ya mzee Jackson yalinijia kichwani “maamuzi yeyote utakayoamua ndio yatakuwa hatma ya meli hii”.
“Adam twenzetu kaka huku hapafai tena huku” Henry alinipita huku akinipigia kelele, na mimi sikusita nikaungana nae lakini nilipofika mlangoni baada ya kutoka niliufunga mlango na mimi nikabakia ndani ya chumba hicho peke yangu. Kidogo nikasikia “Emergency system online (mfumo wa dharura umewaka)”.
Niliudi kwenye kiti changu na kukaa, wakati huo tayari maji yalikuwa magotini. “Adam huko chini utakufa” Capatain Sadick aliongea kwa msisitizo. “Nimechoka kuona kila mtu wangu wa karibu anakufa na kuniacha peke yangu” nilijibu huku nikiwakumbuka kina Latifa na wenzake. “Kama kifo changu kitakuwa pona yenu, basi niko tayari kufa” nilijibu na kutaka kutoa kile kifaa cha mawasiliano sikioni mwangu. “Ata Boy, tupeleke nyumbani” mtu alieongea alikuwa ni mzee Jackson, sauti yake ilinipa ujasiri wa hali ya juu sana.
“Nakuahidi mwalimu wangu tutakwenda nyumbani” nilimalizia kuongea na kutoa kile kifaa cha mawasiliano kisha nikakitupa pembeni. Nilisogea kwenye mashine zote na kuzipeleka mpak mwisho “kasi ya mwisho kabisa”. Haikuwa kazi rahisi kuzimaliza mashine zote kumi kutokana na kurushwa sana, nilipigwa ukutani mara kadhaa. Lakini nilisimama na kuendelea na kile ninachoamini ni maamuzi magumu. Wakati nikielekea katika ngazi ya kushukia chini ambako ndiko kulikuwa na chumba cha mashinie za dharura, nilirushwa kwa nguvu na kupiga kichwa katika chuma.
Niliposimama nilihisi maumivu makali sana huku nikisi kitu chenye asili ya umotomoto kikichuruzika usoni. Nilipogusa ndio nikagundu kuwa ilikuwa damu lakini sikuwa na muda wa kutafuta sehemu niliomia. Nilijikokota mpaka kwenye ile ngazi ambayo ilionekana kwa juu kidgo kutokana na njia hiyo kujaa maji kabisa. “Ukishuka huko chini kuna, mashine maalum initwa PRESSURE WATER WAY P.W.W, ukiwasha tu maji yote yatanyonywa kupitia mabomba maalum na kumwagwa nje kupitia sehemu ya juu kabisa ya meli hii” nilikumbuka maneno hayo vizuri kabisa. Ila kabla sijaingia, bomba moja kubwa likapasuka kabisa na kuanza kuingiza maji kwa wingi zaidi. “Hata maji yakiingia vipi, meli hii itachukua masaa mawili kabla ya kuanza kuzama” nilikumbuka tena.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilitabasamu na kuvuta pumzi kwa nguvu kisha nikapiga mbizi na kuelekea chini kwenye chumba cha mashine za ziada. Lakini kwanza ilibidi niende kwenye ile mashine ya P.W.W, ili nipunguze maji yaliongia. Na ilikuwa mbali kidogo lakini sikuwa na jinsi la sivyo ningekufa kabla hata sijawasha mashine za ziada. Nilijitahidi kuogelea kwa kasi sana huku nikiachia pumzi taratibu kabisa, nilifanikiwa kufika lakini pumzi ilikuwa ishaanza kuniacha mkono. Nilijikaza kiume tu maana tayari nilikuwa nimeshaanza kuona giza. Nilipeleke mkono mpaka kwenye kitufe cha kuwashia mashine hiyo na kukibonyeza. kisha nikashika chuma pembeni ili nisije nikavutwa na mimi.
Mashine ilianza kufanya kazi yake kwa kasi sana na maji yakaanza kunyoywa kupitia vitundu maalum vilivyounganishwa na mabomba hayo. Baada ya sekunde kadhaa maji yalianza kupungua kwa kasi na mimi nikapata sehemu ya kupumua. Baada ya kupata pumzi nzuri niliogelea mpaka kwenye chumba cha mashine za ziada ambacho hakikuwa mbali na sehemu hiyo. Mlango wa chumba hicho ulikuwa kwa juu na ulikuwa unalindwa na mipira maalum ambayo hairuhusu maji kuingi. Nilitoa fungua na kufungua kisha nikajivuta na kuigia ndani. Palikuwa pakavu kabisa, mimi ndie nilieingia na maji.
Nilisogea kwenye kiti na kutoa fungua nyinginie kisha nikafungua sehemu na kuingiza na kuwasha “Emergence engine are coming online in 3,2,1(mashine za dharura zinawaka ndani ya sekunde 3,2,1)”. Ndani ya chumba kuliwakana taa nyekundu na ghafla kukaanza kunguruma kwa nguvu. Nilihisi kabisa kama mwendo wa chombo hicho uliongezeka, nilicheka kwa nguvu na kufunga ya vizuri maana nilielewa kwa mwendo huo lazima nitapata mshike mshike. “Mzee Jackson sasa kazi namuachia captain, nimetimiza ahadi yangu” nilijisemea mwenywe na kuegemea kiti hicho.
Sikujuwa hata nini kiliendelea kwani nilianza kuhisi maumivu makali sana sehemu za kichwani na bila hata kuwaza nifanye, nulikumbwa na kiza kizito sana. “Mbona umechelewa sana kufika” Latifa aliniuliza, “dah tulikuwa tunakusubiria sana mtu wangu” Louise aliongezea. Karibu hapa ndio nyumbani, watu niliona wananichanganya kwanza kwa jinsi walivyovaa. Pili nilikuwa siwaelewe elewi maana walikuwa kama mizuka. Walinisogelea kwa pamoja na kunishika mkono kisha tukaanza kutembea taratibu. “Nyie huku ni wapi” niliwauliza kwa sintofahamu, “we twende tu utajua mbele ya safari” Latifa aliniibu lakini safari hii sauti ilikuwa nzito kidogo.
“Hebu niachieni mimi sitaki kwenda huko” niliongea na kujitoa mikononi mwao, walinigeukia wote wawili na kuniangali kwa macho makali sana. Nilijua tayari kishanuka nikaanza kurudi nyuma na nilipogeuka tu, nilianza kutimua. Kila nilipoangalia nyuma niliwaona wakija taratibu kabisa lakini cha ajabu walikuwa wakinikarbia kwa kasi sana. Nilijitahidi lakini nikashangaa ghafla wamenikata. Nilikurupuka kutoka usingizini huku nikihema kama kitu gani sijui. “Adam tulia kijana” mzee Jackson alikuwa pembeni yangu huku akitabasamu. Wakati nikiendelea kushangaa huku bado nikihema, captain Sadick na baadhi wa mabaharia wengine waliingia. “Vipi hali yako” aliniuliza lakini nilishidwa hata kujibu. “Amepata mshtuko huyo mwacheni kidogo” yule mtoa huduma ya kwanza aliongea, Mzee Jackson alinipa maji ya kunywa kisha akanambia nipumzike kidogo. Nilikunywa yale maji kwa pupa kisha nikamkabidhi glasi na mimi nikajilaza kama alivyonambia.
Nilipojilaza kitandani tu usingizi ulichukua nafasi yake na kunisindikiza katika ulimwengi mwengine. Nilikuja kushtuka tena baada ya kusikia honi ikilia, niliinuka na kukaa kitandani kwa dakika kama tano hivi. Baada ya kukusanya nguvu za kutosha nilinyanyuka na taratibu na kuanza kutembea kuelekea mlangoni. Niliungua na kutoka ila nilishangaa kuona mji kwa mbali, nilibaki nimekodoa macho kweli kweli. “Vipi mbona umekodoa macho” nilishtushwa na sauti ya Juma aliekuwa akitokea nyuma yangu. “Hapa ni wapi” nilimuuliza, “kijana karibu kwa Madiba au Afrika kusini” alinijibu huku akichanua tabasamu. Niliona kama ananitania hivi, bila kupoteza muda nilielekea chumba cha kuendeshea chombo hicho.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Captain Sadick aliponiona aliacha alichokuwa anakifanya na kunifata, “unajisikiaje Adam” swali la kwanza lilikuwa hilo. “nashkuru Mungu najisikia vizuri saa hivi” nilimjibu, “hivi ni kweli tushaakaribia Afrika Kusini” nilimuuliza. “Ndio kwenyewe, ila bandarini tutaingia wiki ijayo” alinijibu, unajua nilitamani niruke kwa furaha lakini nilijizuia. “Adam kabla hujaondoka, nashkuru kwa ujasiri wako uliounyesha. Bila ya jitihada zako labda saa hivi ingekuwa hadithi nyingine” aliongea huku akinipiga begani. “Halafu kitu kingine, ni kuwa bosi atakuja keshokutwa na timu yake nzima”, “sasa itakuaje akinikuta” niliongea kwa hofu kidogo.
“Usijali kila kitu kimeshapangwa, sisi tutajua tutamalizana vipi na bosi hata hivyo ni mtu mzuri tu” alinihakikishia usalama wangu. Maana nilikuwa nishaanza kuhisi mambo yale yalionitokea mwanzo, baada ya kuniambia hayo nilitoka na kuelekea deki ambako nilisimama juani huku nikiangalia mji huo unaavyoonekana kwa mbali. Tulitegemea kufunga gati Cape town, baada ya kuota jua kwa muda mrefu kidogo huku nikishangaa mameli mengine makubwa tena sana kuliko hata MV KANTANA. Nilirudi ndani na kuungana na wenzangu. Tuliongea mawili matatu na kisha nikarudi chumbani kwa ajili ya kupumzika.
Siku zilipita na hatimae siku ya bosi wao kuja ilifika, nikiwa chumbani kwangu nilikuwa kugongewa. Nilipofungua nilikutana na mzee Jackson. “Usiogope Adam” aliniambia kisha yeye akaongoza njia, tulielekea mpaka katika sehemu ya kukutana. “Bosi kija mwenyewe ndio huyo hapo” Captain Sadick alimwambia huku akinyoosha kidole nilipokuwa nimesimama. Alisimama mzee mmoja mpana sana na kunisogelea nilipokuwa nimesimama. Aliniangalia kwa makini “wewe ndio Adam” aliuliza ila sauti ilikuwa nzito sana. “Ndio” nilijibu kwa kujiamini, “kijana asante kwa kunirudishia chombo changu salama” aliongea huku akitabasamu. Kidogo ndio nikashusha pumzi na mabaharia pamoja na timu aliokuja nayo yule walipig makofi.
“Captain tutakutana mjini kwa ajili ya maongezi zaidi” alimgeukia Captain na kuongea, baada ya hapo aliaga na kuondoka. Nilibaki kimya maana kijasho kilikuwa kikinitoka kweli kweli, baada yule mzee kuondoka nilirudi chumbani kwangu na kujibwaga kitandani. Wiki ilikwisha na zamu yetu kuingia bandarini iliwadia. Tuliingia bandarini, mimi nikashuka na Captain Sadick na kuelekea katika hoteli ambayo walikuwa wakifikia pindi wanapokuwa nchini Afrika Kusini. Nilioneshwa chumba changu, mchana nilikuja kuchukuliwa na kupelekwa madukani ambako nilichaguliwa suti moja kali sana tena iliokamilika. Baada ya nilirudishwa hotelini na kukabidhiwa kikaratasi kidogo kilichoandikwa “saa kumi na mbili jioni uwe chini”.
Niliangalia saa ya ukutani iliokuwemo katika chumba hicho na kugundua kuwa ilikuwa ni saa kumi na moja kasoro kidogo tu. Sikulaza damu niliingia chooni na kuoga, nilipotoka nilitulia kidogo mpaka ilipotimia saa kumi na moja na nusu. Niliinuka kitandani na kutoa ile suti kweye mfuko wake wa plastic na kuvaa. Kisha nilisimama kwenye kioo, nilipohakikisha nimependeza niliangalia tena saa na kukuta ikinambia saa kumi na mbili kasoro kidogo. Nilitoka chumbani humo na kuelekea kwenye lift ambako nilishuka hadi chini. Nilikutana na Captain Sadick na baadhi ya mabaharia wakinisubiri, tulitoka nje ya hoteli hiyo na kuelekea kwenye basi moja kubwa sana lililoandikwa MV KANTANA.Tuliingia na safari ikaanza, basi hilo lilitembea kwa mwendo wa wastani huku nikipata wasaa wa kushaangaa majengo makubwa yaliokuwepo katika mji huo . Basi lilikuja kusimama mbele ya hoteli moja kubwa sana na ya kisasa inayoitwa ONE&ONLY CAPE TOWN.
Tulishuka na kuingia ndani, tulipofika tu tu ndani tulipokewa na wahudumu wa hoteli hiyo na captain kutoa maelezo kidogo. Tulipilekwa mpaka katika ukumbu wa mikutano uliokuwepo katika hoteli hio na kuoneshwa sehemu za kukaa. Kila mtu aliagiza kinywaji chake alichokitaka, baada ya dakika tano aliingia yule bosi na kamat yake na kukaa sehemu zao. Ukumbi huo ulisindikizwa na muziki laini wa kiafrika nikiwa na maana nyimbo zilizokuwa zikipigwa humo ni za wasanii wakiafrika tu wakiwemo wasanii wa nyumbani Tanzania.
Baada ya kimya kidogo kupita alinyanyuka msemaji mkuu wa kamati hiyo na kuomba kipaza sauti. “Habari za jioni mabibi na mabwana, ni matumaini yangu kuwa mutakuwa salama kabisa. Naam kutokana na ufinyu wa muda na kwa sababu bosi anasafiri usiku huu kuelekea Amerika sina budi kumkarisha aongee kile alichokusudia kukiweka wazi usiku huu” alimaliza kuongea na kumgeuka bosi wake “Mr Michael karibu sana”. Mzee huyo alisimama na kusogezewa kipaza sauti, alionekana mtu smart sana kwa sababu ukumbi mzimwa watu walikuwa wamependeza lakini yeye alikuwa aking’ara.
“Kabla sijaanza kuongea nina waomba capatain Sadick na Mr Adam wapite huku kwanza” aliongea na watu wakaanza kupiga makofi. Capatain Sadick alisimama na kunipa ishara tufanye kama alivyotaka bosi wake. Tulisogea mpaka mbele ambako alikuwa akihutubia mzee huyo, “munawaona hawa watu wawili, hawa ni baraka kutoka kwa Mungu.
Watu hawa ndio mashujaa waliojitolewa kuileta MV KANTANA bandarini wakisaidiana na vijana wangu wengine. Mmoja ni nahodha madhubuti na mwengine mpambanaji mzuri na mwenye kujali sana. Mimi sina cha kuwalipa maana hata nikisema niwape fedha bado itakuwa haijatosha, capatain Sadick nitakuachia uchague mwenyewe kitu gani unataka. Ila Adam nitamsemea mimi” alimaliza na kumkabidhi kipaza sauti Captain.
“Nashkuru Mungu kwa kunipatia bosi mwenye upendo kama wewe, sina la kuomba zaidi. Chochote utakachotoa mimi nitapokea lakini na wote waliokuwepo chini yangu nao wapate kama hicho” Captain alimaliza kuongea na kumrudishia kipaza sauti bosi wake. “Nimepokea maomb yako na nakuahidi nitayafanyia kazi” alijibu kisha akaweka tai yake vizuri na kunigeukia. “Adam, kuna meli mpya inakuja inaitwa MV KANTANA : MAJESTIC ISLANDER. Itakuwa tayari ndani ya miaka mitano ijayo. Hivyo basi nataka uwe nahodha mkuu wa chombo hicho, chagua chuo unachotaka duniani kusomea ubaharia na mimi nitakusomesha bure na nitakuwa nakulipa pia. Pia chagua na wanafamilia wako wawili wowote na wao pia nitawaajiri katika chombo hicho” aliongea kwa sauti iliojaa upendo.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alikabidhi kipaza sauti hicho nijibu kama nimekubali ofa yake hiyo, kwa mara kwanza nilijikuta nikikosa cha kuongea zaidi ya kuruhusu machozi yatengeze njia yake katika mashavu yangu. Captain alinigusa begani na kunipa ujasiri wa kujibu. “Nimekubali na nashkuru kwa moyo wako wa upendo Mungu akubariki na akupe miaka mingi zaidi duniani” nilijibu na kumrudishia kipaza sauti. “Nashkuru kwa kukubali ofa yangu” alimaliza kuongea na kurudisha kipaza sauti kwa muongeaji mkuu kisha alituruhusu turudi sehemu zetu za mwanzo.
Muongeaji alimalizia maongezi mingine na watu wakala na kunywa mpaka wakasaza, wakati wa kutoka bosi aliniita. “Kijana hii ni card yako ya bank, huna haja ya kuwek hela katika account hii, nitakuwa nakutilia kila mwezi. Mwaka huu utapumzika na jipange upya na maisha, sahau machungu yote yaliopita. Nimesikia mkasa wako na nimesikitika sana kuona kijana mwenye uwezo kama wewe unafanya maamuzi ya ajabu kama yale. Kijana “MATATIZO HAYAKIMBIWI” unapambana nayo kiume tena kifua mbele” aliongea na kuniusia kisha akanikabidhi kadi ya bank. Nyuma ilikuwa imeandikwa nambari za siri. Niliipokea na kumshukuru kisha nikaagana nae na mimi nikarudi walipo wenzangu.
Ukweli niliona kama ndoto kila kilichotokea lakini ndio hivyo maisha yangu yalianza kubadilika hapo, tulumaliza kupakuwa mzigo unaotakiwa kushhushwa nchini hapo na safari ya kuelekea nyumbani ikaanza.
Baada siku kadha tulitia nanga bandari ya Dar-es-salaam, nilikuwa siamini amini kama nimerudi nyumbani. “Adam, karibu tena nyumbani” Captain aliniambia, “kwa sasa mimi na wewe tutaachana hapa, kesho nasafiri kuelekea Tanga. Tutakuwepo hapa kwa miezi mitatu kwa hiyo unakaribishwa sana” alikuwa akilengwa na machozi lakini hakutaka kuonesha.
Nilimshukuru sana na baada ya kumaliza harakati niliwaaga na kuondoka, moja kwa moja hadi mbezi kwa rafiki yangu kipenzi Frank ambae hata sijui alikuwa kaitika hali gani. “Oi James niaje mtu wangu”, James aligeuka na kuonekana kama haamini hivi. “mwangu kipindi chote ulikuwa wapi, mwanao Frank juzi kati hapa kapata ajali mbaya sana na hivi sasa yuko muhimbili lakini hapati matibabu kisa hela ndugu” habari hiyo ilinishtua sana. Bila hata kusubiri nilimwambia awashe pikipiki na safarui ya muhimbili ikaanza.
Tulifika muhimbi na moja kwa moja tulienda mpaka katika chumba alicholazwa Frank, “Frank ndugu yangu nini kimekukuta” nilimuuliza nilipofika tu. “Wee ni Adam” aliniuliza huku akiwa haamini kabisa, “ndugu yangu mimi na maisha ya udereva ndio basi tena wamesema watanikata miguu yote miwili eti nimeumia sana” aliniambia huku akilia. Nilitoka chumbani humo na kwenda kuanza utaratibu wa kumuhamisha hospitali. Nilitoka nje na kukodi gari na kumuhamisha, wanadhani kukata kitafutia riziki cha mtu ni rahisi sana. Moja kwa moja hadi Regency ambako nililipia kila kitu na punde matibabu yakaanza. Nilimuaga kuwa mimi sitakuwepo kwa siku kadhaa, lakini sikutaka kumwambia nilipokuwa naenda.
Nilisafri na kuelekea nyumbani Unguja, huko nilikuta mengine mapya. Kakaangu alikuwa masikini sana na mke alibeba kila kitu na kutoweka pasipojulikana. Niliumia sana kutokana na hali hiyo na yeye alinilaumu sana kwa kumtelekeza kipindi alichokuwa ananihitaji zaidi. Sikuwa na lia kusema wala kujitetea, nilibeba lawama zote. Baada ya kumueleza kila kitu kilichonikuta, alibaki ameduwaa tu lakiini nikamuhakikishia kuwa maisha ya kuunga unga ndio yamekomea siku hiyo.
Sikukaa sana Unguja nilirudi Dar na kakaangu na kuanza maisha mapya, Frank pia baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali alikuja kusihi na sisi. Nilinunua nyumba maeneo ya Mbezi Beach na kufungua biashara nyingine. Sikutaka kabisa kufanya ujinga eti kisa nina pesa nyingi, baada ya mwaka huo kuisha. Mimi na Frank tulisafiri kuelekea nchini Netherland ambako tulisomea ubaharia, huku biashara zikiwa chini ya kakaangu.”
Ndugu Tariq au Mr Fun-tastic na huo ndio mwisho wa mkasa wangu mkubwa ulionikuta na kunipa funzo la maisha.
Mr Fun-tastic: Hapa kuna mtu ametuma swali, anauliza vipi kuhusu Latifa, unajua chochote .
Adam: Ukweli siju mara ya mwisho kuonana ni siku ile tuliokuwa kwenye ile boti tukijaribu kutoroka, lakini kama yuko hai popote pale duniani na kama ananisikia. Mimi namtakia maisha mema.
Mr Fun-tastic: Na kwanini umeamua kushare na watu historia yako ya maisha.
Adam: Nimeamua kufanya hivi ili kuwaonya na kuwahusia vijana wenzangu, ujana ni maji ya moto. Na mtu hakimbii matatizo. Ama kweli SIKUTEGEMEA: MATATIZO HAYAKIMBIWI.
Mr Fun-tastic: Swali hili ni la kwangu, Hapa uwanja wa ndege unafanya nini maana kwa unavyoonekana hutki kusafiri.
Adam: Namsubiria mke wangu anakuja kutoka Jamaica, ah yule pale.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Adam akainuka na kumfata Delila ambae alikuwa na watoto wawili mmoja mkubwa wa kiume na mwengine mdogo wa kike.
Adam: Mr Fun-tastic huyu ni mke wangu Delila, Delila huyu muandishi na mtunzi wa riwaya anaitwa Tariq Haji au Mr Fun-tastic. (huku tukifuatana kuelekea nje ya uwanja wa DIA)
“Captain Adam gari iko pale” aliongea kijna mmoja pale Adam alipofika tu nje.
Adam: Mr Fun-tastic huyu ni Frank na pia nashukuru kwa kujitotelea kuufikisha ujumbe wangu kwa jamii. Na pia unakaribishwa katika harusu yangu itakayofanyika Serena Hotel.
Mr Fun-tastic: Captain Adam kabla hatujaagana, hivi huu ni mwaka wa ngapi tokea upate mikosi.
Captain Adam: Huu ni mwaka wa saba.
Mr Fun-tastic: Asante sana kwa muda wako ulionipa na
kunisimuliza mkasa huu wenye mafunzo mengi sana.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment