Simulizi : Sikutegemea
Sehemu Ya Nne (4)
"Na kwa bahati nzuri nahodha mkuu wa meli hiyo ni mtanzania kama wewe, ni mtu mkarimu sana na kila akipita hapa hunipa vyakula mbali mbali vinavyotoka nchini Tanzania" aliendelea kuongea na kidogo nikashusha pumzi. "Nikitaka kufika nyumbani hiyo ndio njia pekee ilikuwepo mbele yangu kwa sasa" nilijisemea moyoni, lakini nilipokumbuka kilichonikuta kabla ya kufika hapo moyo ulisita kabisa kukubali kutumia usafiri wa wa meli. "Huwa anapita kila baada ya muda gani" nilipiga moyo konde na kuuliza.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Meli yao inapita hapa kila baada ya miaka miwili, bado miezi tisa ipite tena tokea ilivyopita mara ya mwisho" aliniambia, "duh inamaana niake nchini kwa watu kwa mud wa miezi tisa" nilijisemea moyoni. Hata hivyo hakukuwa na njia nyingine ya kufanikisha mpango wangu wa kurudi Tanzania, pia nilimini Mungu linifikisha Jamaica kama sehemu ya kunifnza. Baada ya kufikiria sana nilimuomba Delila nikae kwake kwa kipindi chote cha miezi tisa wakati nikiisubiri hiyo meli ambayo itanisaidia kufika nyumbani, nae alikubali bila kinyongo na maisha yangu mapya yakaanza rasmi nchini Jamaica.
Baada ya wiki moja kupita nilikuwa nimepona kabisa na afya yangu ilianza kutengemaa. Pia ndani ya wiki hiyo hiyo nilipata rafiki mpya, aliitwa Geroy. Alikuwa jamaa mmoja mcheshi sana, pia alikuwa amefuga rasta nyingi sana. Huyo jamaa ndo alikuwa rafiki yangu wa tatu baada ya Delila na mwanae. "Ata boy, nambie mtu wangu mchongo gani unaweza sana maana si unajua mjini mipango" Geroy alipendelea kuniita jina hilo. Nilimueleza sehemu zote ambazo niko vizuri, na tulizidi kupatana hasa baada kugundua kuwa nimepitia uvuvi kwa sababu hata yeye alikuwa akifanya kazi za uvuvi.
Namimi nikaona kuliko kukaa nyumbani kutegemea nguvu za Delila kula, ni bora niingie baharini kutafuta riziki. Nilimuelea Geroy kuwa nataka kwenda nae baharini nae alinikubalia na kunipeleka katika kambi yao ya uvuvi. Huko nilipata mwaliko wa moto maana kila mtu alinichangamkia na kunirabisha vizuri. Usiku wa siku hiyo tukaelekea baharini kuvua, tafauti na mashua nilizozoea nyumbani kwetu unguja. Mashua zao zilikuwa za kisasa zaidi tena kubwa kiasi cha kuhimili mawimbi mazito.
Usiku huo bahari ilikuwa inavurugu kidogo lakini hakuna hata mmoja kati ya wenzangu alieonesha wasiwasi. Na mimi pia sikutaka nionekana mtoto wa mama, nilijikaza kiumbe na kuendelea kushirikiana na wenzangu. Tulirudi mapema alfajiri, na kuanza kuuza samaki pale pale baharini na wateja walikuwa wengi sana. Mpaka inatimia saa mbili kamili asubuhi tulikuwa tumeshauza samaki wote. Baada ya hapo tuliweka pesa ya mafuta pembeni kisha kila akachukua pesa kidogo kwa ajili ya mahitaji yake binafsi na kuelekea nyumbani kwao.
Mimi sikuwa na cha kutumia huko maana nilikuwa mgeni hivyo pesa hiyo nilimkabidhi Delila ili itumike katika mahitaji ya nyumbani. Kutokana na ucovu wa kukesha baharini usiku mzima nilioga kisha nikapanda kitanda nikalala. Nikiwa usingizini niliota ndoto mbaya sana, nilikurupuka kutoka usingizini huku nikihema kwa nguvu. Hata hamu ya kulala iliisha, niliinuka kiandani na kutoka chumbani nikaelekea sebuleni ambapo nilikuta chakula ndio kinaadaliwa.
"Umeamka muda muafaka kabisa" aliongea Delila, nilitabasamu tu na kusogea mezani kwa ajili ya kupata msosi. Sifa moja kubwa ya Delila alikuwa ni mpishi mzuri na mama bora, hakuwa na mume lakini mwanae alipata kila alichohitaji. Baada ya kumaliza kutengwa chakula, tulikaa mezani wote watatu yaani mimi, Delila na Noah na kupata kile kilichoitwa starehe ya tumbo. Tulikula huku tukiongea mambo mengi sana, kwa kweli nilisahau shida zote zilizonikumba.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Maisha yaliendelea kusonga mbele huku nikizidi kujulikana sehemu hiyo niliokuwa nimeibuka badala ya kwa Obama. Kutokana na kuwa na nywele ndefu na mimi niliamua kuweka dredi, miezi miwili ilikata bila kupata shida yeyote ile kila kitu kilikwenda vizuri. Kama kawaida usiku uliwadia na kuelekea baharini, "Ata Boy, leo bahri mbaya sana" Karlus aliniambia nilipofika tu. "Hata mimi naiona inavyotisha" nilimjibu huku nikikaa pembeni. Ukweli kulikuwa na upepo sana siku hiyi lakini tulipiga moyo konde na kuelekea bahrini hivyo hivyo maana ndipo tulipokuwa tunapata riziki yetu ya halali.
Kadri muda ulivyokwenda bahri ilizidi kuchafuka na mawimbi yalizidi kuwa makali, "Brian bora tugeuze kabla hali haijawa mbaya zaidi" niliongea kwa nguv kutokana na upepo kuwa mkali sana. "Mbona huu upepo ni wa kawaida tu" Brian alijibu bila kuonesha wasiwasi. "Brian, Ata Boy anasema kweli ndugu bora tugeuze. Kwanza tumeshapata samaki wa kutosha" Geroy alisistiza lakini bado Brian alikuwa mbishi. Wakati tukiendelea kubishana nae ghafla mashua yetu ilipigwa na wimbi kali sana, wimbi lilimkuta Brian akiwa hajashika sehemu hivyo alitupwa katika maji.
"Geroy nipe kamba kaka" niliongea kwa nguvu, Geroy nae hakuuliza mara mbili. Alitoa kamba kubwa na kunipa. Nilijifunga kiunoni kisha nikamwambia aifunge sehemu maana kuishika kwa mikono ingekuwa shughuli pevu. Baada ya kuongea maneno hayo, sikusubiri nilipiga mbizi majini na kuanza kumfuata Brian ambae alikuwa anapambana na maisha yake. Nilifanikiwa kumfikia na kumpa mkono kisha nikanyanyua mkono juu kama ishara ya msaada. Wenzangu waliokuw kwenye mashua waliuona na kuanza kuivuta ile kamba. Tulifika mpaka kwenye boti na kupanda, wala sikupumzika nilijifungua kamba na kuelekea zilipo mashine.
Niliwasha na safari ya kurudi ikaanza, bahari ilikuwa imechafuka kweli kweli maana tulipigwa na mawimbi balaa. Kama umewhi kuwasikia vijana wa mitaani wakisema "leo bahari imechomoka" basi siku hiyo ilikuwa ni zaidi. Nilitumia ufundi wangu wote kuokoa chombo hicho ambacho ni ndio chanzo cha riziki yetu. "Ata Boy, unadhani tutaokoka leo" Geroy aliniuliza, "usijali kaka Mungu yu pamoja na waja wake" nilimjibu huku macho yangu yakiwa yanaangaza mbele tu ambako chombo hicho kilikuwa kinaelekea. "Jamani shikeni sehemu kwa nguvu maana sasa hatunabudi kuyavaa uso kwa uso mawimbi" niliongea baada kuona kasheshe imezidi kuwa kubwa na kama ningeendelea kuyakwepa yapige pembeni basi ningezamisha mashua hiyo.
Kila mtu alitafuta sehemu ya kushika kwa ajili ya maisha yake, "Eeh Mungu ni katika mikono yako nakabidhi maisha yangu, naomba uniongoze mja wako" niliongea maneno hayo na kuongeza uvutaji wa mafuta. Sasa nilikuwa sikwepi tena mawimbi, nilijitolea tu lolote kama liwe na liwe, baada ya purukushani za muda mrefu hatimae bahari ilitulia na upepo ulipungua. "Aisee hii kitu ya leo si mchezo, katika maisha yangu yote ya uvuvi sijawahi kukutana na ghoruba ya aina hii" aliongea mwenzetu mmoja huku akiachia sehemu alioshika. Furaha zilirejea tena katika nyuso zetu, nilitoa pumzi ndefu na kumshukuru Mungu kwa msaada wake aliotupa.
Safari ya kurudi nyumbani ikaanza, tukiwa njiani tuliona mbao kadhaa za mashua nyingine. Ilibidi nipunguze mwendo kwa ajili ya kutafuta kama mtu yeyote alienusurika na ajali hiyo. Maana kuona mbao hizo kuliashiria ajali, "Ata boy unasikia kelele" Geroy aliniuliza. Ilibidi niachie kuvuta mafauta ili kusikiliza kama ni kelele kweli. "Ndio tena zinatokea upande huu" nilijibu huku nikionyesha ishara upande wa kushoto. Niligeuza mashua na kuelekea upande tuliosikia kelele, na kweli tulikuta watu sita wakiwa wanaelea katika maboya maalum. Tuliwasaidia na kuwaingiza katika mashua yetu, wakati tunawapakia hao tuliona watu wengine watatu wanaelea.
Tulisogea walipo lakini kwa bahati mbaya tukagundua kuwa walikuwa wameshaaga dunia tayari. Hata hivyo hatukuwaacha, tuliipakia miili yao kwenye mashua na safari ikaendelea. Tulifika kisiwani saa mbili asubuhi, na tulishuhdiia umati mkubwa wa watu ukitusubiri. Tulipokaribia tu walikuja kwenye mashua haraka na kuanza kuivuta mpaka ilipokaribia kabisa na sehemu ya mchanga. Tulisaidiana kushusha ile miili ya wenzetu waliofariki, watu wa chini walitusaidia kwa kuwapokea na kuwalaza mchangani.
Baada ya kufanya hilo na sisi tuliosalimika tulishuka, kitendo cha kukanyaga tu chini nilishangaa nimevamiwa na nilipoangalia vizuri alikuwa ni Delilah. "Nilidhani sitokuona tena" aliongea kwa sauti ya kilio. Nilipata kazi nyingine ya kubembeleza maana Delilah alikuwa akilia kama mtoto mdogo. "Delila twende nyumbani basi" nilimnong'oneza kwa sauti ya chini, nae alikubali. Niliwaaga wenzangu na kuondoka eneo hilo, lakini njia nzima bado Delila alikuwa akilia tu na hata nilivyomnyazisha hakunisikiliza.
Tulipofika nyumbani tulikaa ukumbini lakini bado Delila alikuw akilia sana, "sasa kwanini unalia ya kushukuru nimerudi salama unalia" nilimuuliza huku nikiwa nimemshika mikono, "Adam, kwanini usiache kazi ya uvuvi na utafute kazi nyiningine ya kufanya" na yeye aliniuliza swali ambalo liliniacha kinywa wazi. "Nitaachaje kazi ya uvuvi wakati pesa nilioipata na kuchanganya na pesa zako kidogo ndio tumeweza kumrudisha Adam shuleni" nilimjibu huku nikimuangalia usoni. "Tafut kazi nyingine bwana hiyo achana nayo, kazi ya kuuz roho kila siku" lizidi kusisitiza. Nilimuambia anipe muda nifikirie kwa makini sana kabla ya kufikia uamuzi.
Baada ya mazungumzo hyo niliinuka na kuelekea chumbani kwangu ambako nilivua nguo na kuelekea bafuni kwaajili y kujitoa chumvi mwilini. Niliingi chooni na kufungua bomba la mvua kish nikakaa tu chini ya bomba hilo kuacha maji yatalii mwili wangu. Nikiwa nimezama sana katika dimbwi la mawazo, nilianza kuhisi mitu laini kikitambaa mgongoni. Niligeuka kwa haraka na kukutana na sura ya Delila aliekuwa akiniangala kwa macho yaliojaa huba. "Wewe unafanya huku chooni" nilijikuta nikiropokwa, "Adam nimevumilia sana, kwa kweli nimeshindwa. Nimetumia mbinu zote kukuonyesha jinsi ninavyokupenda lakini hukunielew" aliongea huku akiendelea na mchezo wake wa kunisugua sehemu mbali mbali katika mwili wangu.
Unajua hata ukiwa mgumu vipi kuna sehemu ukigusa, kama mtoto wa kiume unakuwa mnyonge tu. Basi ndicho kilichonitokea siku hiyo, mwanzo nilijifnya mgumu lakini na Delila siku hiyo alikuw amenikusudia na alikusudia kufanya kile alichokitaka. Baada ya purukashani za muda mrefu, alnizidi ujanja na na kujikuta nikizama kichwa kichwa. Mambo yalianza huko lakini hayakushia huko, tulirudi chumbani na shughuli ikaedelea mpaka pale tuliporidhika. Delila aliinuka kitandani na kuelekea chumbani kwake. Tokea siku hiyo maisha yetu ndani ya nyumba hiyo yalibadilika na tukawa tunaishi kama familia. Nikiwa na maana kuwa mimi ni baba wa familia hiyo japo sikuwa nimefunga ndoa na mwanamke huyo.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku zilizidi kukatika huku Delila alizidi kusisitiza niache kazi ya uvuvi lakini ukweli sikuwa tayari kufanya hivyo. Hatimae miezi tisa ilikamilika na kweli ile meli niliombiwa itakuja ilifika, "bado unataka kuondoka" aliniuliza Delila. "Ndio, nataka kurudi nyumbani ili kuwatoa wasiwasi" nilimjibu angali nilijua kabisa kuwa jibu hilo lilimuumiza sana Delila. "Sawa mi nitakukutanisha na huyo nahodha" alikubali lakini machozi yalikuwa yameshaanza kumtoka. "Nakuahidi tutaonana tena kwa uwezo wa Mungu" niliongea na kumsogeza karibu kish nikamkumbatia.
Siku iliofuata mapema tulielekea ambapo walikuwa wanakaa na mabaharia wa meli hiyo ambayo ningeondoka nayo. Tulipofika Delila alitoa simu yake na kumppigia Nahodha Sadick ambae hakukaa sana alitoka nje. "Delila, habari za siku nyingi" aliongea Nahodha huyo, "Safi tu captain, pole na safari" Delila alijibu huku akilazimisha tabasamu. "Huyu anaitwa Adam, Adam huyu ni Captain Sadick" alitutambulisha na sisi tukapeana mikono. "Mhh hiyo sura mbona kama sura za nyumbani hivi" aliongea nahodha huyo baada ya kuniangalia usoni. "Hujakosea kabisa" nilimjibu, "ama kweli watanzania ni kiboko maana hakuna nchi niliopita nikakosa kuonana na watanzania"aliongea Nahodha Sadick huku akionekana mwenye furaha sana.#
Tulitafuta sehemu na kukaa kisha tukaanza kuongea, nilimueleza kila kitu kilichonikuta na kumueleza nia yangu ya kutaka kurudi nyumbani. Alinisikiliza kwa makini sana na kuoenekana alikuwa amenifahamu vizuri. "Kwanza pole kwa kila kilichokukuta" aliongea kisha akaendelea "hakuna shida kabisa ila unachotakiwa ni kutengeza kitmbulisho kitakachokupa nafasi ya kuingia ndani ya meli tu kisha kila kitu nitamalizia mimi" aliongea maneno hayo ambayo yaliamsha fyraha ndani ya moyo wangu. "Kiasi gani kinahitajika kutengeza kufoji kitambulisho" nilimuuliza kwa shauku huku nikiwa kama paka mtoto alieona sufi. Alinitajia kiwango cha fedha kinachohitajika na bila kumuuliza nilimkabidhi kiwango hicgo kisha tukakubaliana kukutana baada ya wiki moja.
Baada ya kikao hicho kifupi tuliagana na kila mtu akaelekea upand wake, Delila alikuwa mnyonge sana tena kupita maelezo. "Delila nakuomba usiwe mnyonge kiasi hicho" niliongea punde tu baada ya kufika nyumbani. "Adam unataka niweje sasa, au unataka nifurahi kumuona mwanaume ninaempenda anaondokoa bila mategemeo ya kuonana nae tena" aliongea huku machozi yakimtoka. "Nataka ujue tu kuwa hata mimi nakupenda na inaniuma sana kuondoka kukuacha peke yako lakini nitafanyaje wakati hapa sio nchini kwangu na ikitokea siku wakaamua kukamata wahamiaji haramu unadhani nitasalimika. Wacha niende na mambo yangu yakikaa sawa nitarudi kuja kukuona kwa njia halali kabisa" nilimueleza lakini hata mimi mwenyewe niliuhisi moyo ukichanika tena taratibu.
Kwanza Latifa, Louise na Linda, sasa ni Delila, Noah na Geroy. Lakini ningefanyaje wakati hata ukiishi miaka mia nchini kwa watu utabakia kuwa mgeni tu. Wiki moja ilikatika kama mchezo na hatimae nilikutana na Nahodha Sadick na kunikabidhi kitambulisho changu na kunipa tarehe ya kukutana kwaajili ya safari. Nahodha huyu alinielewa kutokana na kuwa yeye mwenyewe mtanzania, hiyo ndio sababu kubwa ya mambo yangu kwenda kirahisi sana. Na namshukuru sana popote pale alipo kwa kuwa msaada mkubwa wa mimi kurudi katika nchi yangu japo hiyo safari nayo ilikuwa ni balaa jingine ambalo sikutegema kukutana nalo katika maisha yangu.
Baada ya kukabidhiwa kila nilirudi nyumbani kwangu kwaajili ya maandalizi ya safari, siku ya safari ilifika na kila kitu kilikuwa kimekamilika. Delila na mwanae Noah walinisindikiza hadi baharini ambako nilkutana na Capatain Sadick na kuungana nae, niliwaaga ilia kabla sijaingia ndani ya bahari Delila alinipa bahasha ndogo na kunambi nisiifungue mpaka boti itakapotia nanga Hudson Texas nchini Marekani. Niliichukua barua hiyo na kuitia kwenye begi langu dogo la mgongoni na kumpiga busu la kuagana. Baada ya maagano hayo nilielekea getini ambako Captain Sadick alikuwa akinisubiri, tuliongozana moja kwa moja mpaka kwenye kwenye meli hiyo kubwa kweli. Pembeni iliandikwa kwa maandishi makuwabwa ya rangi ya maziwa "MV KANTANA".
Juu kabisa ilikuw na bendera nchi kadhaa ikiwemo Tanzania nchi yangu nilioitoroka kwa sababu ya shida na kutumbukia katika matatizo zaidi. Na kwa sababu nilifuatana na Nahodha mkuu wa chombo hicho, hata sikuulizwa na mtu yeyote yule. Tuliingia ndani ya chombo hicho na mabaharia wengine wote walisimama na kutoa ishara ya salamu ya heshima kwa mkuu wao. "Oya Juma, mpeleke mwana kwenye chumba chake" aliongea Captain, "ay Captain" Juma aliitika kwa staili ambayo ni mara yangu ya kwanza kuisikia tokea siku niliozaliwa. "Oya we ndio Adam sio" alinifuata huku ametunisha misuli yake mikubwa na kuongea kisha akaendelea "karibu kambini kijana" alitabasamu.
"Asante" nilimjibu huku na mimi nikibasamu, "nifute huku" aliongea huku akitingisha kichwa kuonesha ishara ya upande tunaolekea. Tulitembea kwa dakika kama moja huku tukishuka ngazi kama mbili hivi mpaka tulipofika katika koridoo moja kubwa sana yenye vyumba vingi sana. Alifungua mlango wa chumba kimoja na kunambia kuwa hicho nfio kitakuwa chumba changu. Nilimshukuru na kuingia, niliweka begi langu pembeni na kujitupa kitandani. "Hatimae naelekea nyumbani" nilijisemea moyoni huku nikiwa na furaha sana. Baada kuweka kila kitu sawa nilitoka kwenye chumba hicho na kuelekea juu, haikuwa kazi sana kupajua kwa sababu nilikariri njia zote tulizopita wakati naelekea chumbani.
Nilipofika juu, Captain Sadick alitambulishwa kwa mabaharia wengine ambao walikuwa ni wajamii tofauti. Kulikuwa na wazungu, wasomali, watanzania sita na mimi wa saba pamoja na watu wa jamii nyingine mbali mbali. Dakika chache tu nilianza kuwazoea marafiki zangu wapya, na hio ilitokana na ucheshi wangu mkubwa sana niliozawadia na muumba wa mbingu na ardhi. Baada ya saa moja meli ilipiga honi na kung'oa nanga, safari ikawa imeanza rasmi.
Kila mtu alielekea upande wake wa kazi na kuanza majukumu yake, "Adam nifuate" nilimsikia Captain Sadick akinambia. Niliinuka kwenye kiti na kumfuata, tuliekea mpaka kwenye chumba cha kuendeshea meli hiyo. Kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni, nilikaribishwa ndani ya chumba hicho kwa makopyuta makubwa sana na vitufe vingi sana. "Hivi umevikariri vitufe vyote hivi" niliropoka swali bila kutarajia. "Na ndio maana nikapewa unahodha mkuu katika chombo hichi" alinijibu kwa mkato. Nilibaki nimekodoa mcho tu maana niliwahi tu kusikia kuwa kuna vifaa vingi sana katika mameli makubwa lakini sikutegemea kama vitakuwa vingi kiasi hicho.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Unajua" alianza hivyo "ukijiona wewe unashida waangalie wale wenye hali ngumu kuliko wewe. Afadhali wewe umepata kusoma mpaka kufikia kidato cha nne chini ya uangalizi mzuri wa wazazi, mimi sikupata bahati hiyo" aliongea maneno hayo huku akiniangalia kwa macho yaliojaa majonzi. Aliniambia nikae kwenye kiti na mimi nikafanya hivyo, kishaa na yeye akakaa na kuanza kunisimulia maisha yake. Hapa wacha nikuelezee historia ya mtu huyu, huenda ukajifunza kitu kupiti kwake.
Namnukuu "Leo mpaka kuwa hapa, nimetoka mbali sana tena sana kuliko hata shida ulizozipata kabla ya kujitakia matatizo. Mimi ni mzawa wa sehemu moja huko Kisiwani Pemba Zanzibar, ndio ni mzanzibari kama wewe tu. Nimezaliwa sehemu moja inaitwa Kojani, kwa bahati mbaya nikiwa na miaka mitano niliwapoteza wazazi wangu wote wawili kwa kisingizio cha kuwa eti ni wachawi. Kutokana maneno hayo kusambaa sana kila mtu aliamua kunitenga, hakuna kitu kibaya kama kutengwa na jamii inayokuzunguka ungali unahitaji msaada wao katika maisha yako.
Jambo hilo liliniumiza sana, ingawa nilikuwa mdogo lakini nilielewa kila kitu kilichoendelea. Kutokana na manyanyaso kunizidi niliamua kukimbia huko, ndipo katika tembe tembea yangu na kimbia kimbia nilijikuta nimefika katika bandari ya Wete ambako kulikuwa na majahazi yanayoenda Tanga. Nilifanikiwa kujipenyeza katika moja kati ya majahazi yanayoondoka siku hiyo, niliacha kila kitu nilipotoka na kuelekea sehemu ambayo sikuw nikijua hata mtu mmoja. Usiku wa siku hiyo jahazi lilianza safari na Mungu alinisaidia mpaka nafika tanga sikukamtwa.
Nikiwa na miaka sita ndipo nikapata wazo la kutafut ndoana ili niingie baharini nitafute riziki kupitia samaki. Nilinunua kila kitu kilichohitajika na kunza kazi punde tu baada kukamilisha vitu hivyo. Kwa siki nilipata vibuwa wawili watatu na kuuza, niliendelea na kazi hiyo kwa muda wa mwaka mzima. Mungu hakuwa mbali na harakati zangu kwani alinisaidia muda wote huo, maisha yangu niliaendesha kwa shilingi elfu moja kwa siku. Na yalikuwa yakienda vizuri tu na nashukuru Mungu sikuingiwa na tamaa za wizi japo wenzangu wengi walinishauri nijiunge na vikundi vyao vya uhalifu lakini nilikataa kata kata.
Mimi niliamini hata mtoto alianza na hatua moja mpaka akachanganya kutembea, hivyo niliamini tu ipo siku Mungu atafungulia milango ya ridhiki. Na kweli siku hiyo ilifika, nakumbuka siku moja nilikuwa sehemu moja inaitwa Raskazoni. Sehemu hiyo mara nyingi familia nyingi hufika kwa ajili ya kuburudika hasa kipindi cha za mapumziko yaani namaanisha jumamosi na jumapili. Kama kawaida familia nyingi zilimiminika siku ya jumapili katika bahari hiyo safi kabisa na yenye mandhari nzuri ya kuvutia. Miongoni mwa watu kulikuwa na mzee mmoja mwenye asili ya kiarabu, alifika pale na familia yake yote.
Alifika na mkewe pamoja na watoto wake wawili wa kike ambo kiumri mmoja alikuwa mkubwa kuliko mimi lakini mwingini alikuwa mdogo. Walionekana kuwa ni familia yenye furaha sana maana hata nyuso zao zilieleza hivyo na hukuhitaji kutafuta ushahidi zaidi kugundua hilo. Nilitamani sana kuwa na familia kama hiyo lakini wapi yangu mimi ilikuwa imeshatangulia mbele za haki. Ndio mipango ya Mungu ningefanyaje japo kuwa wamekufa vifo vya fedheha sana. Kila mtu alikuwa amezama katika furaha ya kuchezea bahari mpaka pale jua lilipoanza kutua.
Watu walianza kutawanyika nikiwemo na mimi miongoni mwao, nilifika sehemu ya walinzi na kuchukua baskeli ambayo nilikodo siku hiyo na kupandisha juu. Nilipofika juu nilimuona yule mzee wa kiarabu akipakiza vitu kwenye gari yake na kufunga mlango. Ila kwa bahati mbaya kuna mfuko mdogo wa kaki ulidondoka na yeye hakuona. Alipanda kwenye gari yake na kuondoka eneo hilo, mimi nilisogea ulipo mfuko huo na kuunyanyua. Lahaula nilipoufungua nilion makaratasi fulani hivi mengi mengi tu, nilitoa moja na kuliangalia ndipo nikakutana na kitu kilichonishtua. Japo sikwenda shule lakini niliweza kusoma kutoakana na kuwa nilisoma madrasa tokea nikiwa na miaka minne.
Niliirudisha karatasi hiyo na kuunyanyua mfuko huo wa kaki na kuutia kwenye begi langu kisha nikaanza safari ya kulifuata lile gari ikaanza. Nilijiatahidi kunyonga kadri ya uwezo wangu, na kwa sababu nilikuwa nimeikariri nilifanikiwa kuipata kuiona. Tatizo jingine lilijittokeza, alikuwa amefunga vioo vyote vya gari. Sikuwa na njia nyingine zaidi ya kuifuata gari hio na kwa bahati nzuri alikuwa akiendesha mwendo mdogo hivyo haikunipa shida kuifuatilia.
Niliifuatilia mpaka tulipofika barabara ishirini, ambapo aliacha barabaa kubwa ya Taifa Road na kuingia barabara ya mtaa huo. Alitembea kidogo mpaka katika nyumba moja ya kisasa na kusimamisha gari hiyo kisha akapiga honi. Geti lilifunguliwa na kisha akaingiza gari ndani, ila kwa bahati mbaya nilipofika mlinzi alikuwa tayari ameshafunga mlango. Hio ilitokana na kuchoka sana kiasi cha kushuka baiskeli na kuikokota ndicho kilicho nichelewesha.
Nilisogea mlangoni na kugonga, hazikupita sekunde nyingi mlinzi alifungua lakini aliponiona tu alionesha dharau na kunionyeshea kirungu chake cheusi alichokuwa ameshika mkononi. Kisha akanambia "We chokoraa potea haraka kabla sijakutwanga kirungu cha kichwa", nilijaribu kumuelezaa kuna kitu muhimu nataka nimpe tajiri yake lakini bado hakunielewa. Na mimi sikuwa tayari kuondoka kutokana na umuhimu zile karatasi nilizozikuta ndani ya mfuko ule. Mara kadhaa mlinzi huyo alinisukuma kwa nguvu na kupelekea nianguke chini. Hata hivyo nilisimama na kurudi tena na kuendelea na kile ambacho nimekisimamia.
Wakati tunaendelea kubishana tulisikia sauti ya mtu akiongea kw nguvu huku akija getini, yule mlinzi aliingia ndani haraka na baada ya sekunde kadhaa alitoka yule mzee. "Kijana unataka nini mbona ulikuwa unabishana na mlinzi wangu" aliniuliza swali hilo. "Samahani kwa usumbufu mzee lakini kuna nimeona nikukabidhi mkononi mwako kabisa kutokana na uzito wake" nilimjibu. "Kitu gani hicho kijana" aliniuliza, "wakati unaondoka kule Raskazoni uliangusha mfuko huu" niliongea na kumkabidhi ule mfuko" Captain Sadick alinyamaza kidogo na kuangalia saa yake ya mkononi.
"Adam ni muda wa kula" alinambia kisha yeye akainuka na mimi nikafuata, lakini sikuwa hata na hamu ya kula. Nilitamani aendelee kunisimulia historia yake ambayo ilinivutia sana, basi tulielekea sehemu ya maakuli na kupta kile kilichoitwa chakula cha mchana. "Hivi tutaingia Hudson lini" nilimuuliza wakati tunaendelea kula, "baada ya siku nne ndio tutatia nanga Hudson" alinijibu. Tuliendelea kupata chakula huku tukiendelea na soga nyingine.
"Hivi Adam imekuaje mpaka ukafanya maamuzi ya kijinga kiasi kile" aliniuliza mzungu mmoja miongoni mwa mabaharia wa kizungu. "Ni ujinga tu na tamaa za kipumbavu ndio sababu kuu" nilimjibu na wengi walicheka kidogo. "Hivi unadhani huku ulaya kuna maisha mazuri kama unavyoyaona kwenye runinga au" mzungu mwengine alitupia swali.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilibaki nimeshangaa tu nisijue nini cha kusema, maana ingekuwa vigumu kuamini kama angenambia mswahili mwenzangu lakini ni mzungu ndie alieniambia mambo hayo. Waliendelea kunieleza mambo mengi sana kuhusu nchi hizo za magharibi, yaani mpaka hamu ya hata kwenda kutembea ilinitokana hata kama ni kwa njia za halali. Tulimaliza kula na kila mtu akaelekea sehemu yake ya kazi. Mimi nilifuata na Nahodha mkuu mpaka katika chumba kile cha kuendeshea.
Tulipofika tulikaa tena sehemu ile ile na akaendelea kunisimulia historia yake ya maisha. Naendelea kumnukuu “ niliongea na kumkabidhi yule mzee ule mfuko wa kaki, bila hata kutegemea alinisika mkono na kuniingiza ndani ya geti kisha akampa ishara mlinzi wake alifunge haraka. “Kijana umeona kitu ndani ya mfuko huu” aliniuliza huku akihema juu juu. Nikamueleza kile nilichokiona, masikini mzee wa watu alishika kichwa na kukuna nywele zake ndefu zilizoja mvi. “Kijana unajua kitu ulichokiona ukimwambie mtu yoyote kitakuhatarishia maisha yako?” aliongea. “Hilo nilikuwansijui lakini kutokana na umuhimu wa nilichokiona ndio maana nikaamua kukufatilia hadi hapa kwako” nilimjibu na kuendelea “na mimi natumaini kazi yangu imekwisha hivyo naomba niondoke”.
Aliniuliza ninapo kaa, nilishindwa kumjibu kutokana na kuwa na pa kuishi. Nilikuwa nikilala vibarazani tu. “Mbona hunijibu”aliniuliza, “mimi naishi mtaani tu, sina familia wala ndugu ninae mjua” nilimjibu. Kilichofuata hata mimi ilinichukua muda kukiamini, siku zote watu husema wema hulipwankwa kwa wema tu na mtegemee Mungu katika maisha yako yote.
Yule mzee aliniomba niishi kwake na aliniahidi kunilea na kunisomesha kama mtoti wake wa kunizaa. Na hapo ule msemo usamao “mchumia juani hulia kivulini” ukachukua nafasi yake katika maisha yangu. Kuanzia siku hiyo nikapata familia iliojaa upendo na maisha yangu yalibadilika moja kwa moja mpaka leo hii unaponiona hapa nimekuwa nahodha mkuu wa chombo hichi ni kwasababu tu ya kuamini Mungu alikuwa pamoja na mimi na bado anaendelea kuwa pamoja na mimi”
Hapo ndio ulikuwa mwisho wa historia yake ambayo ilijaa mapito magumu sana hasa ukizingatia umri wake ulikuwa mdogo sana. Hata hivyo aliamua kukabiliana na matatizo yote yaliomkuta na kufanikiwa kuyatatua kwa neema za muumba wa mbingu na ardhi. “Adam, siku zote ridhika na kile Mungu anachokupa kwani ndicho ulichotakiwa ukipate kwa muda husika. Jaribu kufikiria ungekuwa katika umri wangu na ukakutwa na matatizo kama yangu, unadhani ungekuwa hai mpaka leo. Uvumilivu ni muhimu sana katika maisha, ukiona hali ni mbaya. Usikimbilie kule unapodhani utapata maisha mazuri bali tafuta sehemu ambayo itakupa muda wa kupambanua matatizo yako” aliniambia maneno hayo kwa kuyasisitiza sana.
Baada ya historia hiyo nilitoka katika chumba cha kuongozea chombo hicho na kuelekea nje kabisa katika deki ya meli hiyo. Kulikuwa na upepo mzuri sana kutokana na kuwa chombo hicho kilikuwa kikisonga mbele kwa mwendi mdogo. Niliiangalia ile deki kwa makini sana na kuvuta kumbukumbu za siku ile tuliokamatwa katika ile meli nlioamini inhenofikisha nchi za ulaya. Matukio yote yaliotokea siku yalijirudia katika akili yangu. Pia niliikumbuka ile pesa yote ambayo niliitoa kama rushwa, laiti kama isingekuwa tama zangu za kijinga. Leo hii ningekuwa namiliki pikipiki yangu mwenyewe, na pia ningekuwa nimejiajiri mwenyewe.
Moyo wangu uliandamwa na majonzi makubwa sana, maumivu niliokuwa nayapata yaliniuma sana kila nilipokumbuka watu ambao nimewapoteza. Wakati nikiwa nimezama katika dimbwi hilo la mawazo nilihisi mtu akinigusa bega. “Unaonekana una mawazo wazo” yule jamaa alieitwa Juma aliniuliza, “ndugu yangu we acha tu, laiti kama ningejua yatanikuta yalionikuta basi nisingethubutu kuondoka Tanzania” nilijibu huku nikihisi maumivu hasa mwilini mwangu. “Ndugu Mungu hutupa elimu pale tunapokosea na chukulia mambo yote ulioyapitia kama sehemu ya elimu hiyo” Juma alinijibu huku akitabasamu kidogo. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tuliendelea kuongea mambo mengi sana, alinambia kuwa yeye ameanza kazi ya ubaharia miaka miwili nyuma. Aliipata kazi hiyo baada kukutana na Captain Sadick na kwamba yeye ndo aliemkomboa kutokana na umasikini wa hali ya juu sana na kumpa kazi hiyo. Kumbe bado watu wema wapo duniani na sio kama watu wanavyosema.
Baada ya maongezi mafupi tulirudi ndani maana kiza kilishaanza kuingia na baridi ilizidi kuwa kali. Nilielekea chumbani kwangu na kujilaza kikitandani, nilianza kupanga mambo mengi sana ya kufanya nikifika nyumbani Tanzania.
Wakati nikiendelea na kupanga mipango yangu, nilisikia mlango ukigongwa. Niliinuka kitandani na kwenda kufungua. Alikuwa mzungu mmoja hivi, alikuja kunambia kuwa muda wa kula ulikuwa umewadia, niliitika na kurudi chumbani ndani. Nilivaa tisheti yangu ikiandamana na koti zito kidogo kisha nikatoka. Waliponiona tu walianza kucheka, na nilipowauliza kilichokuwa kinawachekesha mmoaja akanijibu kuwa hakuna hata baridi halafu mimi nimevaa koti.
Nilishangaa maana mimi nilihisi baridi mpaka kwenye mifupa lakini wao walikuwa wamevua kawaida tu na wengine walikuw wamevaa vest tu. Hata nilielewa kuwa watu wao walishaizoea baridi, niliungana nao kwenye meza na kupata chakula cha usiku. Tulikula huku tukipiga stori za hapa na pale, “Captain kwanini usitupe huyu kijana tukaenda nae chumba cha mashine, maana anaonkana ana akili sana” aliongea mzungu mmoja mzee kidogo. “Vipi Adam unataka kujifunza kitu” Captain Sadick aliniuliza. “Itakuwa vizuri kama nitajifunza kitu cha kufanya kuliko kulala na kuamka kama mwari anaesubiri mume” nilimjibu na kumfanya acheke.
Basi baada ya kula yule mzee aliniambia nimfuate, tulielekea mpaka katika chumba kimoja kilichoandikwa “Engine room”. Alikifungua na sote tukaingia, punde tu baada kuingia nilihisi mwili ukipata joto la ajabu sana kutokana na hali ya hewa iliokuwemo ya joto iliokuemo katika chumba hicho. Alinikabidhi nguo maalum za buluu ambazo ni overrall na kuniambia nzivae, hizo ndio zilikuwa sare za kukaa katika chumba hicho. Nilizivaa kisha tukaanza kutembea kwa mwendo mdogo huku akinionyesha mashine kadhaa na kuniambia kazi zake.
Kulikuwa na mashine nyingi sana huko ndani ya hicho chumba, tena zilikuwa kubwa kupita maelezo, Na kizuri zaidi kila mashibe ilikuwa na kazi tofauti na ile ya kukisukuma chombo hicho cha kisasa kabisa. “Kijana meli hii ni meli ya kisasa kuliko meli zote kubwa duniani” aliniambia, akanieleza kuwa inasukumwa na mashine kumi za kati akiw na maana mashine hizo ni mbili. Lakini mara nyingi husukumwa na mashine sita tu badala ya kumi. Kutumika zote kumi ni mpaka pale bahahri itakapokuwa na mawimbi makubwa na makali.
Ukiachilia hizo kumi, kulikuwa na mashine nyingine nne za pembeni. Alinieleza kuwa mashine hizo ni mashine za dharurua na zitatumika pindi tu pale mashine nyingine zitakaposhindwa kuhimili uzito wa mawimbi. Aliendelea kunielekeza mamb mengine mengi tu, baada ya ziara kama ya nusu saa hivi tulitoka ndani ya chumba na mimi nikaelekea chumbani kwangu. Niliingia chooni na kujisafisha na baada ya hapo nilirudi chumbani ambako nilivaa nguo nyepesi na kulala. “Adam ndio ukaamua kunisaliti, kisa nimekufa si ndio. Adam si nakuambia wewe, mapenzi yoe yale niliokuonyesha bado ukaamua kuala na mwanamke mwengine. Lazima na wewe utalipa kwa hilo” nilikurupuka kutoka usingizini huku nikihema kwa nguvu.
Niliemuota hakuwa mwengine isipokuwa Latifa, lakini cha ajabu alikuwa kapendeza sana japo katika ndoto hiyo aliongea maneno makali sana. “Hivi ni ndoto au” nilijiuliza maana nilihisi kama alikuwa kaismama pembeni yangu ndani ya chumba hicho kidogo. Niliangalia saa iliokuwa ikining’inia ndani ya chumba hicho na kugundua ilikuwa ni saa kumi na moja alfajiri. Niliinuka na kuingia chooni kwa ajili ya kupunguza maji mwilini. Kisha nilivaa tracksuit yangu pamoja na koti zito na kutoka chumbani.
Nilielekea deki ambako niliwakuta baadhi ya mabaharia wakifanya mazoezi, “kijana naona mapema sana” aliongea mmoja wao. “Ah si unajua ukishakuwa na majanga katika maisha yako hata usingizi hauji vizuri” nilijibu na mimi nikaungana nao kwa ajili ya kupasha mwili. Tulifanya mazoezi kwa masaa nawili kisha kila mtu alielekea chumbani kwake kwa ajili ya usafi. Baada ya hapo tulikutana mezani na kupata kifungua kinywa. Kwa siku moja nilikaa nao watu, tayari nilikuwa nimeshazoea sana. Tulikuwa tukiongea kama watu tuliokuwa tunajuana kwa muda mrefu.
Tulipomaliza kula nilifuatana tena Mzee Jackson, ambae ni yule mzee anaenielekeza kuhusiana na mashine za chombo hicho. Jackson ndio lilikuwa jina lake, tulifika katika hicho na kama kawaida nikavaa sare zile alizonipa na ziara ikaanza tena. Siku hiyo alionionyesha mashine nyingine kabisa, tunaposema akili ya binaadamu inanguvu kuliko komputer si uongo. Kutokana na wingi wa mashine hizo na kazi zinazofanya basi kama mtu angekuwa hajasoma basi asingejua kufanya chochote. Tafauti na mzee huyo alionekana ameshaakula chumvi kiasi, yeye alizifahamu kinaga ubaga kuanzia ndogo hadi kubwa.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku hiyo alinipa kidaftari kidogo kilichondikwa kwa nje, "MV KANTANA" na kunambia nirikodi kitu ambacho nitahisi kitakuwa na umuhimu kwangu. Sio kwamba kulikuwa hakuna watu wengine katika chumba laa, walikuwepo na kila mtu alikuwa na jukumu lake. Mzee Jackson alikuwa ni engineer mkuu wa kitengo hicho. Baada ya ziara ya muda mfupi ndani ya chumba hicho, tulitoka na tulipofika tu nje aliniambia nimpe kile kidafatari alichonipa. Sikujua alikuwa akikitaka kwa sababu gani lakini nilimkabidhi na akaanza kuangalia kile nilichokiandika.
Alipomaliza aliniangalia kisha akatabasamu, "yaani na akili yako ilivyokuwa nzuri ukathubutu kukimbia kwenu eti kisa matatizo" aliongea maneni hayo kisha akatabasamu. Sikumjibu kitu, nilimuomba anipe kile kidaftari kisha nikaelekea chumbani kwangu. Nilipofika nilikaa kwenye kitanda na kuanza kurudia kile nilichokiandika wakati ananielezea. Baada ya kurudia kwa muda mfupi nilikiweka pembeni na kujilaza. Kutokana nauchovu wa mazoezi asubuhi nailikuwa si kawaida yangu, usiingiz haukucheza mbali na ulichukua nafasi yake.
Siku ya tatu jioni tulitia nanga Hudson, Texas. Walishuka watu kadha akiwemo na nahodha Sadick, baada kama robo saa hivi walirudi na kutuambia kuwa usiku tutaruhusiwa kutokana katika chombo na kuelekea hotelini ambapo tutapumzika kwa siku nne kabla ya kuanza safari yenyewe kuelekea Tanzani kupitia Afrika Kusini. Nilitamani usiku uingia muda huo huo kutokana na kuwa na hamu ya kuona jiji hilo la Texas ambalo nilikuwa nililiona kwenye runinga na filamu za kiingereza tu. Hata kukaa niliona tabu maana nilihisi viti labda vimepakwa gundi na nikikaa tu nitaganda.
Kama yalivyo masaa hayagandi, usiku ulichukua nafasi yake na bila kuchelewa tulishuka wote na kuelekea katika gari ambayo ilikuwa inatusubiri. Tulielekea katika hoteli moja kubwa sana na ya kisasa, ilikuwa mara yangu ya kwanza kuingia katika hoteli kubwa kama hiyo japo kule kisiwani niliingia. Lakini haikuwa kubwa kama nilioingia mjini Hudson Texas. Kila mtu alipewa chumba chake kwa ajili ya kuupitisha usiku huo mwanana kabisa katika vyumba vilivyopambwa na hita(heater) kwa ajili ya kukifanya chumba hicho kiwe na hali ya hewa nzuri sana.
Siku hiyo hata ndoto mbaya sikuota kabisa, nililala fofofo kama mtoto mdogo alieshiba ziwa la mamae. Siku ya pili mapema kila mtu alitawanyika na kuelekea katika harakati zake anazozijua mwenyewe. Pale hotelini tulibaki watu wawili tu, mimi na nahodha Sadick. "Twendezetu tukazurure mitaani huko" aliniambia na mimi nikakubali bila kusita. Tulitoka nje ya hoteli hio na kuchukua gari maalum ambayo hupewa watalii hotelini hapo kwaajili ya matembezi kipindi chote watakachokuwepo.
Yaani mambo nilioyashuhudia yaliniacha kinywa wazi, yaani kila nilichoambiwa na yule mzungu katika meli ni kweli tupu. Maana asubuhi mapema tayari omba omba walikuwa washajipanga njiani kupigania riziki, hilo halikutosha ukahaba ulikuwa unafanyika kweupe na sio kama Bongo ambapo ukahaba ni usiku pekee. Kiufupi nchi kama Amerika ikiwa kwa siku unashindwa kupata hata dola mbili au tatu basi siku hiyo jiandae kula makombo ya hotelini baada ya kuosha vyombo. Wakati huku Tanzania ukiwa na elfu moja tu basi unapata japo mlo mmoja.
Ule tunaoita "pasi ndefu", tulizunguka sana na tulikula katika migahawa tofauti tofauti.
Jioni tulikutana hotelini ambako kila mtu aliingia chumbani kwake na kutoa kaptula, tulielekea sehemu ya nyuma ya hoteli hiyo ambako kulikuwa na mabwawa makubwa sana ya kuogelea. Tulipofika huko hakuna aliogeajambo, kila mtu aliingia katika bwawa hilo na kuanza kuogelea. Nilijiuliza mara mbili mbili kwanza kabla ya kuingia katika bwawa hilo maana baridi ilikuwa imeshaaza kuwa kali. Wakati naendelea kuwaza na kuwazua nilishangaa ghafla niko angani na kutua ndani ya maji.
Wengine wote walinicheka, niliona hakuna haja ya kujishauri tena maana tayari nilikuwa nimeshaivaa baridi. Niliungana na kufurahia jioni hiyo, kumbe wenzangu walikuwa hawaogelei tu. Walikuwa wakifanya mazoezi humo, mazoezi kama yale ya kuzamia na kukaa chini ya maji kwa muda mrefu. Tena walikuw na pumzi maana aliekaa muda mfupi kuliko wote alikaa dakika moja na sekunde thalathini. "Adam hutaki kujipima upepo" wakati nikindelea kushanga nilisikia mtu akionge nyuma yangu. "Mimi na kuzamia wapi na wapi, mazoezi hayo yana wenyewe akina nyie" nilijibu, sio kwamba nilikuwa siwezi laa, sikutaka tu.
Nilikuwa na uwezo wa kubana pumzi ndani ya maji kwa muda mrefu sana, kitu kimoja ambaocho sijawaambia. Kipindi kile nafanya kazi ya uvuvi, kuna siku wakati natega nyavu mguu wangu mmoja ukaingia katika nyavu hiyo na kujizonga. Nilihangaika sana kuutoa maana nilikua mbali kidogo uso wa maji. Nilipapatua mpaka nilipokuja kuutoa nilikua nishaanza kuhisi kifo, nilipofika juu wenzangu wakaniuliza nilikuwa nafanya nini huko chini kwa dakika tatu nzima. Niliwaeleza kilichonikuta na wakacheka. Hivyo kwa sisi wavuvi ni kawaida yetu kukesha chini kwenye maji.
Basi walinilzamisha namimi niajaribu kwa kunitolea sababu tofauti, mwisho niliona isiwe kero nilikubaliana nao na kuzamia. Lakini wakati huu uwzo wangu wa kukaa ndani ya maji kwa muda mrefu ulikuwa umepunguwa sana. Nilikaa kwa dakika mbili na sekunde kumi tu nikaibuka maana mapafu yalikuwa yashaanza kuwaka moto. Wengi waliniangalia kwa macho ya mshangao hasa wale ambao nilikuwa nimewazidi uwezo. Basi baada ya hapo kila mtu alirudi chumbani kwake na kujisafisha kisha tukapata chakula cha jioni kwa pamoja.
Tulipomaliza kula kuna baadhi waliondoka na kuelekea viwanja kama vile macasino na wengine madisco. Mimi na baadhi ya mabaharia tulibaki hotelini na kila mtu akajifungia chumbani kwake kwa ajili ya kuupitisha usiku huo mwanana kabisa katika jiji hilo la watu lililonofanya niuze roho yangu kwa tamaa. Nililala fofofo na usiningizi ulikuwa mzuri sana na wala haukuwa na ndoto zozote za ajabu ajabu.
Siku ya pili mapema niliamka na kutoka nje kwa ajili ya kunyoosha mwili, wakati natoka nikakutana na baadhi ya mabaharia ambao walikwenda viwanja usiku wakirudi huku wakikokotana. Walikuwa wamelewa chakari, niliwasilimu na kuelekea sehemu ya mazoezi ambako nilimkuta captain Sadick akiwa tayari ameshafika na alishaanza mazoezi. Na mimi niliungana nae na kufanya mazoezi huku tukiongea mambo kadhaa wa kadha.
Baada ya mazoeiz nilirudi chumbani kwangu na kujisafisha kisha nikaelekea sehemu maalum na kupata kifungua kinywa. Baada ya hapo nilitoka na captain Sadick na kuelekea mizungoni kama kawaida yetu. Hiyo ndio ilikuw starehe kubwa kwetu, pia nilipata kuona na kujifunza mengi sana kupitia mizunguko hio. Maisha magumu si Afrika tu hata huko wanapopaita kwa Obama kuna watu wana hali mbaya sana ya maisha kupita maelezo.
Tukiwa njiani nilimuuliza Captain Sadick kwanini yeye hajaenda viwanja, “Kwanza imani yangu hainiruhusu mimi kwenda katika sehemu kama hizo. Lakini pili mimi nina mkea nyumbani na naithamini ndoa yangu sana na kumthamini mke wangu. Kuwa mbali na mke wangu haimaanishi nifanye mambo ya kijinga. Kwa sababu kwenda sehemu kama macasino, kuna uwezekano mkubwa wa kulala na mwanamke mwenigine pasi na mke wangu” alinieleza hayo na mimi wala sikutaka kuendelea kuhoji kitu.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mchana tulirudi hotelini na kuunganika na wengine kwa ajili ya chakula cha mchana, maisha mjini Hudson yaliendela hivyo mpaka pale siku za mapumziko zilipokoma na maandalizi ya safari ndefu ya kurudi nyumbani yakaanza. Tulinunua vyakula vya kutosha pamoja na madawa mengi tu na nilipouliza dawa zote zile za kazi gani. Nikaambiwa kuwa ni za dharura tu ikitokea kama mtu ataumwa au kuumia kipindi chote cha safari. Maana safari hiyo ni ndefu sana na kuna wakati inachukua hadi miezi miwili mpanga meli kuti nanga bandari ya Dar-es-salaam Tanzania.
Baada ya kila kitu kukamilika, tulifungasha mizigo yetu na safari ya kurudi melini ikaanza. Tulipofika kila mtu alikwenda chumbani kwake huku tukikubaliana tukutane baada ya dakika kumi. Niliingia chumbani kwangu na kuweka kila kitu changu sawa kisha sikukaa niltoka na kuelekea katika sehemu ya kukutania. Baada dakika kidogo wengine walifika na kuongea mambo kadhaaa. Baada ya hapo kila mtu akaelekea katisa hemu yake ya kazi. Mimi sikwenda pahali kwa sababu sikuwa mfanyakazi wa chombo hicho. Nilibakia pale pale ukumbini huku nikiwaza mambo mengi ambayo nimeifunza kipindi chote hicho.
Baada kama nusu saa hivi nilizinduliwa kutoka katika mawazo hayo kwa mngurumo mkubwa sana mashine zilizopata uhai baada ya muda mrefu sana kulala. Na baada ya muda kidogo walikuja tena mabaharia wote na kuomba dua ya pamoja. “tutaondoka saa saba usiku” Captain Sadick aliongea na kila mtu akatawanyika na kuelekea sehemu anayoijua yeyey. Mimi nilielekea chumbani kwangu ambako nilijibwaga kitandani na usingizi haukuchukua muda ukanipitia.
Nilikua kushtuka baada kusikia mlio mkali na mkubwa sana wa honi ya meli hiyo, ilikuwa ni ishara kuwa chombo hicho kilikuwa kinang’oa nanga. Hapo sasa safari ya kurudi nyumbani Tanzani ikawa imeanza rasmi. Nilipata furaha sana moyoni mwangu baada kuhisi kuwa nareje a sehemu ninayostahiki kuwepo, nyumbani. Nikiwa katika furaha hiyo ndipo nikaikumbuka bahasha niliopewa na Delila. Nilikurupuka kutoka kitandani na kulisogelea begi langu, nilifungua na kutoa bahasha kisha nikardi kitandani na kuifungua kisha nikaanza kuisoma.
Kwako mwanaume niliekupenda na kukukabidhi moyo pamoja na mwili wangu, najua wakati utakapokuwa unaisoma barua hii utakuwa mbali na mimimi. Lakini kuwa na amani popote pale utakapokuwa na nataka ufahamu tu kama kuna mwanamke anakupenda kwa moyo wake wote. NAKUPENDA SANA ADAM na baada yako ndio nimefunga mlango wa upendo kwa mwanaume yeyote mwingine. Lengo la barua hi fupi si kukueleza ni kiasi gani nakupenda bali ni kwamba. Ulikuja ukakutuka wawili mimi na mwanangu Noah na ukatulea kama familia yako pasi na kutaka kujua chochote kile. Umemlea Noah kwa kipindi kifupi sana na kumfanya ahisi amepata baba aliekuwa akimtaka kwa muda mrefu. Wakati unaondoka hujatuacha kama ulivyotukuta, umetuacha watu watatu. Umetuachia alama ya upendo wako wa dhati, nina mimba ya miezi miwili sasa lakini nilishindwa kukuambia kutokana na nia yako ya kurudi nyumbani kwenu. Na nakuahidi kuwa nitamlea mtoto wetu na kumpa upendo kama ulionipa na nitamueleza babaake ni baraka ya pekee katika maisha yangu. Ishi kwa amani mpaka pale Mungu atakapotukutanisha tena kwa mapenzi yake. WAKO AKUPENDAE KWA DHATI DELILA.
Barua iliishia hivyo na ilikuwa inamatone kadhaa ya machozi yalioashiria kuwa alikuwa akilia wakati anaandika. Najua utakuwa na swali juu ya kuwa nimejuje kama yale ni machozi wakati yangekuwa yashakauka. Kulikuwa na alama nyeusi zilizotokana na wanja aliokuwa amepaka na ndio maana nikatambua kuwa alikuwa analia wakati anaandika. Moyo wangu uliingiwa na simanzi kuliko hata lililonipata baada ya kumpoteza Latifa. Niliuhisi unachanika na kuacha maumivu makali sana.
Machozi yalianza kunitoka bila kupenda, nilijiona mtu mwenye mikosi kuliko watu wote duniani. Maisha yangu niliyaona ya ajabu sana maana kila mtu niliempenda alitoweka katika maisha yangu. “Nitarudi kwa ajili yako tu” nilijisemea moyoni na kujiapiza kuwa lazima nirudi Jamaica, niliirudisha barua ile kwenye bahasha na kuiweka kwenye vizuri kwenye begi. Kisha nikarudi kitandani ili kujaribu kutafuta tena usingizi lakini wapi. Picha ya Latifa, louise, Linda na Delila zilikuwa zikipishana kwenye ubongo wangu kwa zamu.
Mpaka kunakucha sikufanikiwa kufunga hata jicho, nilinyanyuka kitandani na kuelekea chooni kwa ajili ya usafi kisha nikaelekea sehemu ya kupata kifungua kinywa ambako nilikutana na wenzangu. Baada ya kupata kifungua kinywa hicho, nilifuatana na Mzee Jackson mpaka katika kile chumba cha mashine ambako niliendelea kupata elimu ya moja kwa moja kutoka kwa bingwa huyo wa mitambo ya chombo hicho. “Hivi hujiuliza kwanini nakupa elimu hii” aliniuliza wakati tunatoka katika chumba hicho.
“Nilitaka kukuuliza muda mrefu lakini nikahisi muda muafaka bado, kwa vile umeniuliza wewe waweza niambie ni kwasababu gani unanifundisha mambo haya wakati hata hadhi ya kusomea sina” nilimjibu na kumafanya atabasamu kidogo kisha akasuuza koo na kusema “Huenda Mungu akawa amekuteuwa kurithi nafasi yangu katika chombo hichi baada ya kustaafu”. Nilibaki nimekodowa macho tu nisijue nini la kuongea, “katika chombo hichi wengei wanakuona kama mtu wa kawaida sana, mimi ninapokuangalia naona uwezo mkubwa sana wa akili umesimama mbele yangu” aliendelea.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kivipi” nilimuuliza, “unakumbuka mara ya kwanza nilipokupa kile kidaftari” aliniuliza nikamjinu kuwa nakumbuka vizuri tu. Hapo ndio akaniambia kuwa alinipa kile kidafatari kupima uwezo wangu wa kuchanganua na kuandika mambo muhimu. Na alifanya hivyo kwa wengine wote isipokuwa Captain Sadick. Lakini wote hawakufikia pale anapopataka ila mimi ndio nikamkonga moyo wake.Na ndio maana akaamua kunifundisha. Na alionesha kabisa kama alikuwa hatanii hata kidogo, sikuwa na la kujibu zaidi ya kutabasamu tu.
Siku zilipeperuka kama vumbi katika upepo mkali huku bahari ikiendelea kuwa tulivu kabisa bila kuleta shida yeyote ile. Mawimbi madogo madogo yalikuwepo lakini hayakukitisha chombo hicho kutokana na ukubw na uimara wake. Mwezi ulikuwa umekatika tayari huku mimi nikiwa nimeshaanza kuwa mzoefu na kucheza na mitambo. Nakumbuka siku hiyo nikiwa deki nimekaa napunga upepo ghafla hali ya hewa ilianza kubadilika na mawingu mazito yakatanda angani. Upepo nao haukuwa nyuma ukaanza kuonesha makeke yake kwa kuvuma kwa kasi sana jambo ambalo lilianza kunitia hofu.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment