IMEANDIKWA NA : HUSSEIN O. MOLITO
*********************************************************************************
Sehemu Ya Kwanza (1)
Ni upope mwanana ulioanza kuvuma kila kona ya jiji huku mawingu meusi yakutuliza joto lililokuwa dakika chache zilizopita. Watu walionekana wakiendelea na shughuli zao, huku baadhi ya wakina mama wakionekana kuanua nguo zao kwa kuhofia mvua ambayo dalili zake zote zilishaonekana.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Dadika ishirini baadae ilianza kunyesha mvua taratibu. Mvua hiyo iliwawezesha watu kuendelea kutembea bila miamvuli kwa muda. Lakini baadae mvua iliongeza kasi na kufikia kuwa hakuna mtu anayeweza kutembea barabarani hata kama utakuwa na mwamvuli.
Radi kali zilanza kutishia amani kwa waishio maeneo hayo. Mvua hiyo iliyoanza kimasihara iliendelea kunyesha kwa kasi ya ajabu huku upepo ukiendelea kuvuma kwa kasi hali iliyofanya baadhi ya paa za nyumba kuanza kuezuka.
Mvua hiyo ya ajabu ilidumu kwa muda wa masaa sita tu, lakini ilileta maafa makubwa sana huko Mbeya na kusababisha mafuriko makubwa na nyumba nyingi kubomoka.
Watu walioishi kwenye kijiji hicho walipata hasara kubwa kutokana na kuharibika kwa mazao yao yaliyokuwa ghalani.
Vilio vilisikika karibu kila nyumba kutokana na baadhi ya watu kufa kwa radi na wengine kuondoka na maji yaliyobomoa nyumba zilizokuwa karibu na mkondo wa maji.
Vilio hivyo vilidumu kila nyumba. Vilio vilivyokuwa vya kusikitisha sana ni vya wanandoa waliopata mtoto uzeeni huku mume akiwa na miaka arobaini na tano na mama akiwa na miaka Thelathina na saba.
Waliamini kuwa kupata mtoto huyo wa uzeeni alikuwa ni zawadi kutoka kwa Mungu kutokana na kukesha macho kwa miaka mingi wakiomba mtoto.
Wao kilio chao kuliuzidi msiba kwakua wao hawakuiona maiti ya mtoto wao. Zaidi ya taarifa tu ya kuondoka na mafuriko hayo.
Hakika ilikuwa ni zaidi ya majonzi kwa familia hiyo iliyokuwa na mtoto huyo wa miaka mitatu tu na nusu.
Wengi waliwaonea huruma wazee hao na kuwapa moyo kuwa Mungu yupo pamoja nao.
Hawakuweza kusahau japo kuwa miaka miwili imepita toka tukio lile la kihistoria kutokea mkoani kwao. Daima walimkumbuka mtoto wao na kila siku walikuwa wanalia kila wakiziangalia picha za mtoto wao.
Uwezo wa kupata mtoto mwengine illikuwa ngumu sana kutokana na umri wao pia vizazi vyao vilikuwa mbali kwa uthibitisho wa daktari wa kijiji hicho.
*********************
ABDUL ni mtoto aliyeokotwa katika maafa hayo yaliyotokea huko Mbeya na kupelekwa Dar na watu waliyemuokoa na kupelekwa kwenye kituo cha kulelea watoto yatima .
Mtoto huyo alifikisha umri wa miaka saba na kuazishwa shule pamoja na wenzake waliokuwa na umri unaolingana.
Hakua mzuri sana shuleni, ila kipaji cha kuimba kilikuwa nyota shuleni hapo baada ya kushiriki sherehe mbali mbali na kuwa mtumbuizaji mzuri sana.
Matokeao ya darasa la saba yalipotoka, Abdul hakuchaguliwa kujiunga na secondary. Hivyo kupelekwa shule ya mziki inayomilikiwa na Mr. Zungu.
Mzee huyo alijitolea kuanzisha chuo hicho cha muziki na kuandaa bendi iliyowakusanya vijana wapatao kumi walikuwa kwenye vituo mbali mbali vya watoto yatima.
Kundi hilo walilipa jina la DREAMZ kutokana na kuwakusanya vijana waliokuwa na ndoto za kuwa ma super star baadae.
Abdul alfanya mazoezi kwa juhudi kubwa na kufanya kujua kupiga vyombo vingi vya muziki kwa muda mfupi.
Walijifua kwa muda wa mwaka mmoja chini ya uongozi wa tajiri huyo aliyetoa nyumba kwa ajili ya wanamuziki hao ambao aliamini watakuja kuiteka Tanzania na hata Afrika nzima kwa kupiga muziki live na kufanya mziki kisomi.
Walimu wamuziki kutoka nje ya nchi walitua na kuwapa elimu hiyo ya kujua ala za muziki na kuwafundisha tone zote za muziki na sheria zake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walipata muda wa kufundishwa lugha takribani tatu kuu. Pia walipata elimu ya jinsia na kujitambua na kuwaaambia jinsi ya kuishi ki super star kwakua ndoto zao ilikuwa ni lazima kufanikiwa iwapo watamaliza miaka yao mitatu chuoni hapo.
Baada ya kumalliza elimu hiyo, bendi hiyo ilirekodi nyimbo yake ya kwanza chini ya mtunzi Abdul ambaye alikuwa kama kiongozi wao kutokana na sauti yake pamoja vionjo vyake vya kipekee.
Kila kona ya jiji zilibandikwa posterz za bendi hiyo kwa ajili ya uzinduzi. Watu walikusanyika kwa wingi na kuwashuhudia watu hao waliobeba vichwa vya habari kila sehemu.
Shoo ya kufa mtu ilifanyika na kila mtu akajikuta amekubali uwezo wa hali ya juu ya bendi hiyo mpya yenye kila sifa ya kuitwa bora.
Hakika waliifanya kazi iliyowaduwaza mpaka mastaa waliokuwa wanaangalia shoo hiyo.
Jina la DREAMS BAND lilikua kila siku iendayo kwa mungu na kuwa moja kati ya bendi zinazoongoza kwa shoo hapa Tanzania.
Kundi hilo lililopata tenda nyingi hasa mahotelini kwa ajili ya uwezo wao wa kutandika vyombo live na sauti murua walizojaaliwa na mungu ukijumlisha na elimu ya muziki waliyoipata.
Jina la Abdul lilienda sawa na umaarufu wa Bendi hiyo. Alijulikana kama mtunzi mahiri wa mashairi, pia sauti yake ilipenya kila sehemu ya mwili wa mpenda muziki na kujikuta ana muweka moyoni.
Bendi hiyo iliyokuwa na wasichana wawili na wanaume nane wenye umri mdogo tu wa chini ya miaka ishirini, walizikonga nyoyo za watu na kuwa tishio kwa mastaa waliokuwa wakishikilia chati muda huo.
Ni kawaida yao kwenda beach kila mwisho wa wiki kwa ajili ya mazoezi ya sauti, walipomaliza walijumuika pamoja kuoga. Kasoro Abdul. Yeye alikua muoga sana wa kuuogelea kutokana na kumbu kumbu yake iliyoganda ubongoni baada ya kunusurika kufa na maji kwenye mafuriko yaliyotokea miaka kumi na saba iliyopita.
Wengi walimpenda Abdul, si mashabiki tu. Hata wanakikundi wenzake hakuna aliyemchukia kutokana na kutokuwa mchoyo kwa kila wazo atakalolipata.
Hali hiyo iliwafanya wale wasichana wawili walikuwa katika lile kundi kumzimikia Abdul. Walipeda kuwa karibu nae na walipopata nafasi hata ya kukumbatiwa na yeye walifurahi sana.
SAPNA ni msichana ambaye alitoka nae Abdul katika kituo kimoja. Yeye na Abdul walikua pamoja toka utoto wao. Walisaidiana kwa mengi hususani katika maswala ya chakula. Ingawaje waliishi kifamilia kama kaka na dada, ila walishabiina sana hali iliyowafanya walezi kuwa makini nao kwa kuhofia kuvunja miiko ya familia hiyo.
Sapna afanyapo kosa. Abdul humtetea kwa nguvu zote. Na wakati mwengine alidiriki mpaka kiyanunua yeye yale makosa ya mwenzake. Hali kadhalika na Sapna hivyo hivyo. Alidiriki kusema yeye ndiye aliyefanya kosa Fulani ilimradi tu kumtetea Abdul kama ni yeye ndiye muhusika wa kosa lile.
Hata matokeo yao shuleni yalifanana kwa asilimia kubwa. Ilionyesha kuwa hata katika masomo walikuwa wanashirikiana sana.
Sifa ya upole na kuwajali wenzao ziliwaangukia wote wawili. Hali iliyowafanya kuwa watoto pendwa kuliko watoto wote pale kituoni.
Maisha yaliendelea kwa kila mmoja kupeleka ndoto zake kwenye muziki baada ya kufeli shule ya msingi. Hata huko pia, walipangwa tone moja kutokana na sauti zao kushabiina. Juhudi zao kwenye muziki ziliwafanya kuwa wataalamu na kujua kupiga chombo chochote cha muziki huku wakiwa wanaimba.
Mr. Zungu alipata umaarufu mkubwa juu ya bendi yake ya yatima aliyoianzisha na sasa kuwa top in Africa.
Shoo za nje ya nchi zilimiminika kama mvua. Shoo ya kwanza ya nje ya nchi ilifanyika nchini Kenya katika jiji la Nairobi. Na baade wakaenda Uganda katika jiji la Kampala. Shoo hizo mbili ziliwapa umaarufu mkubwa na kutanua wigo kwa kupiga shoo Rwanda,Zimbabwe,Nigeria na shoo kali kuliko zote walifanya kwa marehemu mzee Madiba. Afrika kusini.
Shoo hiyo ilifunika na kupata mualiko kwa malikia wa Uingereza nyumbani kwake. Mualiko huo wa heshima ambao Bendi yoyote Afrika na ulaya haijawahi kutokea, uliwafanya kundi lao kujulikana Dunia nzima.
Nyota zao ziling`aa na kuanza kupiga shoo nyingi nje ya bara la Afrika.
Baada ya mafannikio hayo kupatikana kwa kipindi cha mwaka mmoja tu, kila mmoja wa kundi hilo alikua na fedha za kutosha kumiliki mjengo na magari kadhaa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Utajiri wa Mr.Zungu uliongezeka mara mbili yake na kuwa mtu mwenye fedha nyingi sana.
Mtoto wake anaeshi huko marekani, alikuja Tanzania kwa ajili ya likizo kutokana na kuikumbuka Familia yake. Alipokelewa vizuri na familia yake uwanja wa ndege wa mwalimu nyerere.
Alipelekwa mpaka nyumbani kwa msafara maalumu. Hakika mapokezi yake yalifananishwa na msafara wa raisi kutokana na Benzi nyeusi zilizokuwa zinaongozana takribani tisa. Zote zikiwa na rangi sawa.
DIANA JEZBEL ndio jina halisi la mtoto huyo mwenye kila aina ya sifa za kuitwa mrembo. Alikua zaidi ya malikia kwa baba yake Mr. Zungu kutokana na kuwa wa pekee na aliyempata akiwa na umri mkubwa.
Ni binti mdogo aliyekuwa na umri wa miaka kumi na nane, lakini alikuwa na umbo kubwa kiasi kutokana na maisha mazuri aliyokuwa anaishi toka anazaliwa. Hajawahi kula ugali toka amezaliwa na wala hajui ugali ni nini. Hajawahi hata kusogeza sahani yake aliyokula yeye na kupeleka sehemu ya kuoshea vyombo achana na kuiosha kabisa. Hajawahi kuambiwa hapana kwa kila kitu alichokihiitaji kutoka kwa baba yake aliyempenda kuliko chochote..
Ameishi Tanzania kwa miaka Tisa na baadae kuhamishiwa ulaya kwa ajili ya masomo yake. Hivi sasa ni mwanafunzi wa chuo kikuu na amerudi Tanzania kwa ajili ya likizo tu.
Furaha ya Mr. Zungu ilikuwa kubwa sana. Nyumbani aliandaa sherehe kubwa sana iliyohudhuriwa na watu wenye hadhi zao na matajiri wakubwa wa hapa Africa.
Bendi ya Dreams na wasanii wengine wakubwa waliitwa kwa ajili ya burudani katika Sherehe hiyo adhim. Wafanya kazi zaidi ya sabini walipewa kibarua cha kusanbaza wine na vyakula katika meza za waalikwa.
Kulikua na Red capet iliyotandikwa vizuri kuelekea kwenye jukwaa kuu lililonakshiwa na wapambaji mashuhuri Afrika mashariki.
Wasanii walianza kuingia mmoja mmoja na kutumbuiza nyimbo zao kali. Hamu ya watu wote pale waliohudhuria ilikuwa ni Bendi ya Dreams ambayo ilikuwa ina muda mrefu kidogo haijafanya shoo yoyote hapa Tanzania.
Vyombo vyote vya habari vilirusha live sherehe hiyo na kuwapa watu fursa ya kuangalia sherehe hiyo ya ukaribisho wa mtoto wa tajiri mkubwa Mr Zungu.
Hatimaye kundi la Dreams lilipanda kwenye jukwaa na watu karibu wote waliohudhuria walisikika wakishangilia sana.
Walianza kwa kuimba nyimbo za taratibu na baadae wakachanganya na nyimbo zilizowaacha watu wafurahie kile walichokitarajia kutoka kwao.
Ufundi na uhodari wa kucheza aliokuwa nao Abdul, ulikua kivutio kikubwa kwa watu waliohudhuria ile sherehe. Alilitumia jukwaa vizuri na mara kadhaa alimsogelea mpaka malikia wa Mr Zungu. (Diana)
Ushawishi wa sauti murua na ujuzi wa hali ya juu wa kukun`guta gitaa, ulimfanya Diana kunyanyuka na kwenda kujumika nao kwa kucheza nao pamoja.
Furaha kubwa sana aliipata Diana na kukiri kuwa Bendi ya baba yake ilikuwa ya kimataifa.
Baada ya sherehe hiyo kuisha, watu waliondoka na kila mmoja katika kundi la Dreams aliondoka na kwenda kwake.
“umefurahi mwanangu.” Aliongea Mr. Zungu baada ya kuingia ndani na kukaa kwenye meza ya chakula cha usiku.
“ahsanre sana baba kwa surprise yako. Nimefurahi sana.” Alijibu Diana huku akionyesha wazi kufurahia tukio lile.
“kipi ambacho umekifurahia zaidi?” aliulkiza Mr.Zungu huku akinyesha wazi kufurahia uwepo wa mtoto wake pale.
“ile bendi yako ni soo baba. Kweli ina hadhi ya kuwa bendi ya dunia. Maana nilisisimkwa mwili na kujikuta naingia kati na kucheza. Hususani yule aliyekuwa anaimba na kucheza sana. Anaitwa nani yule?” aliongea Diana na baadae akauliza swali.
“anaitwa Abdul.” Alijibu Mr.Zungu.
“wooooh… anakipaji cha ajabu sana. Nimempenda ghafla.”
Aliongea Diana maneno yaliyowafaya wazazi wake watazamane na kumuangalia yeye ambaye hakuonyesha kuwa alikua ana nia yoyote mbaya kama walivyomaanisha wao. Walitabasamu na kumuangalia mtoto wao ambaye nae alikuwa anawatazama kwa zamu huku akishangaa kidogo kutokana na mabadiliko ya mapokeo ya wazazi wake kwa kile alichokiongea.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“vipi kwani?... mbona hivyo?” aliuliza Diana baada ya kuto wasoma wazazi wake.
“hamna kitu.” Alijibu Mr.Zungu huku akimuangalia mke wake.
Usiku huo ulipita na kuingia siku nyengine. Jioni ya siku hiyo, Diana aliomba apelekwe kwenye nyumba ambayo wanafanyia mazoezi Bendi ya Dreams.
Alipelekwa na baba yake na kuwakuta watu wote wakiwa wametimia wakiendelea na mazoezi kama kawaida. Alipoingia Mr.Zungu, vyombo vyote vilizimwa kutokana na kumuheshimu sana mzee huyo. Alifika na kuanza kuwatambulisha mwanae huyo wa pekee na kumwagia sifa kibao. Pia ilifika zamu ya Diana kumtambua mmoja baada ya mwengine. Alipofika kwa Abdul, moyo wake ulimuenda mbio sana kutokana na muonekano wake uliomvutia ghafla. Jina lake halikufanana na mwili wake. Alikua yupo kawaida tu, ila alikuwa na maajabu kwenye sauti yake pindi anyanyuapo kipaza na kuanza kuimba.
Walipiga nyimbo mpya kadhaa ambazo bado hazijarekodiwa, na baadae wakapiga nyimbo zao zinazo bamba.
Sauti na mitindo ya uchezaji vilizidi kumuacha hoi Diana. Alikua bize sana kumuangalia Abdul kwa kila anachokifanya, alijikuta anashangilia hovyo na kuonyesha wazi kuwa alikua anaburudika vya kutosha kuwaangalia vijana hao waliopikwa na kuiva na baba yake.
Utaratibu wa kwenda mazoezi kwa bendi hiyo ya baba yake haukukomea siku hiyo. Sasa alikua anaenda kila siku ya mungu akiwa na gari lake.
Mara kadhaa alikua anamuangalia Abdul na kumkonyeza. Lakini Abdul alikua haonyeshi dalili zozote za kukubaliana na yeye au kuwa tofauti naye.
Kadri siku zilivyozidi kwenda, ndipo Abdul alizidi kuziteka hisia za Diana. Alishamuota kwa mara kadhaa kuwa yupo nae karibu. Hali hiyo ilizidi kumtesa sana Diana juu ya mtu ambaye hakua na hata wazo nae.
Uzalendo ulizidiwa na tamaa, baada ya kumtamkia Abdul kuwa alikua anahitaji kuonana nae baada ya Shoo yao iliyofanyika hapa Dar.
Ilikuwa ni shoo kabambe iliyohudhuriwa na watu wengi katika viwanja vya Dar live.
Ingawaje kulikuwa na wasanii wengi waliopanda jukwaani, lakini kiu ya watu waliokuwa wamehudhuria pale ni juu ya kushuhudia mambo mapya kutoka kwa kundi la Dreams.
Waliingia na kushangiliwa na umati mkubwa wa watu walikuwa pale. Huku Diana akiwa ni mmoja wao. Walifanya yale ambayo watu walitarijia kufanywa na wao. Baada ya shoo hiyo, walikusanyika tayari kwa ajili ya kuondoka na Bus lao lililoandikwa Dreams Band.
“Abdul. Twende kwenye gari yangu.”
Aliongea Diana kwa sauti iliyosikiwa na kila mtu pale. Sapna aligeuka na kumuangalia Diana kwa macho makali kidogo kwa kuwa alianza kuhisi kuwa Diana Alisha
muhusudu Abdul ambaye yeye yupo moyoni mwake. Abdul aliwaangalia wenzake kwa zamu kama vile alikua anahitaji ushauri juu ya kukataa au kukubali ombi lake.
“poa.” Alijibu Abdul baada ya kuona amekosa msaada kutoka kwa wanakikundi wenzake.
Alishuka kwenye basi hilo na kuelekea kwenye gari ndogo aina ya marcides benz iliyokuwa inamilikiwa na mtoto huyo mdogo kabisa.
Sapna alikua anaangalia tu dirishani huku akijiona kama vile alikua hafanyiwi haki. Ila upande wa pili wa shilingi, aliumia rohoni na kujikuta anajilaumu mwenyewe kwa kutoweka hisia zake wazi juu ya mwanaume huyo.
Gari aliyopanda Abdul, iliondoka kwa kasi na kuelekea upande ambao haukuwa njia ya kuelekea kwenye kambi yao. Abdul alishangaa, lakini hakuuliza chochote kutokana na hadhi ya mtoto huyo kwa bosi wake.
Safari iliishia kwenye hotel kubwa ya kifahari. Na Diana alipaki galri hapo na kumuamuru Abdul ashuke. Abdul alisita kwa mara kadhaa, na baadae akanyanyuka na kumfuata dada huyo ambaye alikwenda mpaka mapokezi na kuchukua chumba.
“noo… siwezi kwenda kulala na wewe. Huu ni utovu wa nidhamu mbele ya Mr. Zungu.” Aligoma Abdul baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu na kuwa maamuma tu wa kufuata kila kitu akifanyacho Diana.
“sina nia mbaya na wewe… nilikuwa natafuta sehemu tulivu tu ili nizungumze na wewe Abdul.” Aliongea Diana maneno hayo kwa sauti Fulani hivi iliyosikika kimahaba hata kabla hajaongea hiyo shida yake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“kama kweli una maongezi na mimi ya amani, ni bora twende tu kule kwenye viti. Kuliko chumbani. Najua huko lazima kuna mtu ataanza ushawishi na ni vigumu kutoka salama wakati una heshima kubwa kama dada yangu kwa jinsi ninavyomuheshimu baba yako.” Aliongea Abdul maneno ambayo hayakumuingia akilini maramoja Diana.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment