Search This Blog

Thursday, July 14, 2022

I FAIL TO FORGET YOU (NASHINDWA KUKUSAHAU) - 5

 







    Simulizi : I Fail To Forget You

    Sehemu Ya Tano (5)





    “Dokta! Dokta msaada,” ilikuwa ni sauti ya Mama Andrew akiomba msaada kwa wakati huo hali ya mwanaye ilionekana kubadilika na kuwa si nzuri, Andrew alionekana akivuta pumzi kwa tabu huku akitapatapa kitendo kilichomuweka Mama yake katika hofu kubwa.



    Selestine alikuwa ndani ya chumba cha hoteli aliyokuwa amefikia, akili yake bado iliendelea kumfikiria Andrew kwa wakati huo. Hakutaka kumuona akiwa bado hai, alipoambiwa na Derick kuwa hakufa na bado alikuwa akiendelea kuteseka alisijikia vibaya sana, aliamini Andrew kuwa alifahamu kila kitu kilichokuwa kimetokea na kama angeweza kupona angesababisha kuifufua kesi ambayo ilikuwa imeshatupiliwa kapuni. Hilo likazidi kumuweka katika wakati wa mawazo sana, kila alilokuwa akilifikiria kwa wakati huo kuhusu Andrew lilizidi kumuumiza kichwa chake. Wazo lililomjia lilikuwa ni la mauaji, alipanga kumuua kabisa Andrew ili apoteze ushahidi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliamua kumpigia simu rafiki yake na kumueleza kile alichokuwa amekipanga kukifanya kwa Andrew.

    “Unasemaje?” aliuliza Derick kwa mshangao mara baada ya kupokea simu ya Selestine na kumsikia kuwa alipanga kumuua Andrew.

    “Hivyo ndivyo niliyopanga, inabidi nimuue kabisa ili nipoteze ushahidi,” alisema Selestine huku akionekana kutokuwa na wasiwasi wowote ule.

    “Unataka kumuua?”

    “Ndiyo.’

    “Sasa utamuua kwa kutumia nini halafu ujue unayataharisha maisha yako?”

    “Hapana wala usiogope, nitamuua kwa kutumia sumu,” alijibu Selestine.

    Hakutaka kupoteza muda, siku iliyofuata aliamua kufanya uchunguzi wake wa haraka na kugundua wodi aliyokuwa amelazwa Andrew. Hakuacha kuchunguza muda ambao alikuwa akiachwa mwenyewe na mama yake wakati alipokuwa akienda kutafuta chakula pamoja na muda aliyopewa kwa ajili ya kupumzika. Kila kitu alihakikisha anakifahamu ili pindi atakapoamua kufanya mauaji asikamatwe.

    “Kila kitu kipo kwenye mstari,” alisema Selestine huku akionekana kuwa na furaha iliyopitiliza.

    “Una uhakika utafanikiwa?” aliuliza Derick huku akionekana kuwa na wasiwasi juu ya tukio la mauaji alilokuwa amepanga kulifanya Selestine.

    “Ondoa shaka lazima nihakikishe namuondoa hapa duniani,” alijibu Selestine kisha akacheka kuashiria kufanikiwa katika mpango wake.

    Ulikuwa ni mpango wa mauaji ya kweli aliokuwa ameupanga Selestine kuhakikisha anafanikiwa kumuua Andrew ambaye bado alikuwa akiendelea kuteseka kitandani miaka yote.

    “Kwanini aendelee kuteseka, asumbue watu wakati kuzimu kupo?” alijiuliza Selestine usiku mmoja alipokuwa katika chumba chake hotelini, wakati huo alikuwa akiiandaa sumu ambayo alipanga kwenda kumuulia Andrew.

    Siku iliyofuata alipanga kwenda kufanya mauaji. Kama alivyofanya uchunguzi wake ndivyo ambavyo alienda katika chumba alichokuwa amelazwa Andrew, akaingia wakati huo hakukuwa na mtu yoyote. Akamvutisha Andrew ile sumu aliyokuwa ameiweka kwenye kitambaa, alipohakikisha kuwa alikuwa ameivuta yote akatoka nje, akaamua kuondoka huku akijifanya kuwa raia mwema kumbe tayari alikuwa ametimiza azma yake ya kufanya mauaji.

    ****

    Mama Andrew aliporejea ndani ya chumba alichokuwa amelazwa mwanaye alishangaa kumuona akitapatapa huku akionekana kushindwa kuvuta pumzi vizuri hali iliyomfanya aonekana kuhangaika pale kitandani. Ilibidi aanze kupiga kelele kuomba msaada kwa daktari ili aweze kuyaokoa maisha ya mtoto wake. Dokta Masawwe alifika haraka kisha akaanza kumuangalia ni nini kilichokuwa kimemtokea Andrew. Mama yake Andrew bado alikuwa katika hofu kubwa moyoni.

    ****

    “Mpango umekamilika.”

    “Umefanikiwa?”

    “Nilikwambia hakuna kinachoshindikana.”

    “Umemuua?”

    “Ndiyo nimempa sumu.”

    “Mmh! Una roho ngumu aisee.”

    “Acha afe.”

    Yalikuwa ni mazungumzo yaliyofanyika kwenye simu kati ya Selestine na Derick, wakati huo Selestine alikuwa akitabasamu kwa kufanikiwa kazi yake, aliamua kujipongeza kwa kunywa pombe usiku huo na kwenda kuchukua Malaya waliyokuwa wakijiuza mtaa wa Malindi na kwenda kulala nao usiku kucha. Aliamua kufanya yote hayo ikiwa ni kama sehemu ya kujipongeza kwa kazi nzuri aliyokuwa ameifanya.

    ****

    Mzee Antony alikuwa na kisasi na Selestine, hakutaka kumsamehe kirahisi kwa uwizi ule aliyokuwa amemfanyia. Kitu alichokuwa amekipanga ni kuwatafuta vijana ambao aliwapa kazi ya kumkafuta Selestine popote pale alipokuwepo na aliwaahidi kuwalipa pesa ambazo alitegemea kulipwa kutoka na biashara ya madawa ya kulevya aliyokuwa akiifanya kwa wakati huo kutoka Afrika Kusini kuyaleta Tanzania ambapo alikuwa akiyauza.

    “Popote pale mtakapo muona hakikisheni mnamuua,” alisema Mzee Antony akiwaamuru wale vijana wake, walikuwa ni vijana watatu waliyoonekana kuwa na miili iliyojengeka kimazoezi.

    “Sawa Mkuu haina tatizo,” alisema mmoja wa wale vijana kisha msako wa kumtafuta Selestine ulianza, walipanga kumuua endapo wangeweza kumpata.

    ****

    “Ooppss Mungu Wangu, Mwanao hawezi kupona tena,” alisema Dokta Masawwe mara baada ya kumuangalia Andrew ni nini kilichokuwa kimemtokea, aligundua kuwa alipewa sumu ambayo ndani ya muda na siku yoyote ilikuwa inakwenda kumuua.

    “Unasemaje dokta?” aliuliza Mama Andrew kwa mshangao mkubwa sana, alihisi kama masikio yake yalisikia vibaya, akaamua kumuuliza dokta Masawwe kwa mara nyingine.

    “Mwanao inaonekana amepewa sumu kali sana na muda wowote itaweza kumuua,” alisema Dokta Masawwe maneno yaliyomshtua Mama Andrew kisha hapo hapo akaanguka chini na kupoteza fahamu.



    Taratibu za kujaribu kuyaokoa maisha ya Andrew ziliendelea wakati huo Mama yake alikuwa amepoteza fahamu, alipelekwa katika chumba maalumu kwa ajili ya kupumzika.

    Hakukuwa na daktari au nesi ambaye alionekana kuwa katika uso wa furaha, kila mtu alionekana kuwa makini na kazi yake. Walijitahidi kwa hali na mali katika kuyaokoa maisha ya Andrew lakini uwezo na nguvu zao ziligonga mwamba, walikuwa wameshachelewa kwani sumu ilikuwa imeshamuathiri Andrew sehemu kubwa ya mwili wake na mpaka kufikia wakati huo ilikuwa imeshaingia kwenye ini.

    “Ooopssss,” alivuta pumzi ndefu na kuziachia dokta Masawwe huku uso wake ukionekana kushindwa kufanikiwa kuyaokoa maisha ya Andrew.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nini dokta?” aliuliza nesi huku akionekana kuwa na wasiwasi mkubwa sana.

    “Hawezi kupona,” alijibu dokta Masawwe kwa sauti iliyopoteza matumaini kabisa.

    “Unasema kweli dokta?”

    “Ndiyo inaonekana sumu aliyopewa imemuathiri kwa kiasi kikubwa sana.”

    “Kwani hakuna njia nyingine ya kuyaokoa maisha yake?”

    “Hakuna sumu imeshasambaa mpaka kwenye ini.”

    “Mmh! Kwahiyo tutafanyanye?”

    “Vipi mama yake ameshapata fahamu?”

    “Bado hajapata fahamu.”

    “Sijui akiamka tutamueleza nini?” aliuliza dokta Masawwe swali ambalo hata yule nesi alishindwa kujibu. Kwanza ilionekana kuwa ni uzembe mkubwa sana kwa kitendo cha mgonjwa kama yule kupewa sumu na mtu ambaye hakufahamika mpaka kufikia wakati huo.

    Kichwani yalimjia maswali mengi sana juu ya mtu ambaye alihusika kumpa sumu Andrew, hakujua alifananaje na kwanini aliamua kumpa sumu hiyo. Hayo yalibaki kuwa maswali bubu yaliyozidi kukiumiza kichwa chake, hakujua ni nini alitakiwa afanye tena ili kuyaokoa maisha ya Andrew.

    Tangu hapo siku za uhai wa maisha ya Andrew zilihesabika, hakukuwa na uwezakano wa kupona tena. Dokta Masawwe alikuwa ameshakata tamaa, kuna muda machozi yalikuwa yakimdondoka hapa ni baada ya kumfikiria Mama yake Andrew ambaye alihangaika usiku na mchana katika kuyapigania maisha ya mtoto wake lakini kwa wakati ule alikuwa anaenda kumpoteza.

    “Itabidi tumueleze ukweli tu,” alisema nesi mara baada ya kimya kirefu kilichotawala.

    “Unajua sio kazi rahisi sana kama unavyodhani,” alisema dokta Masawwe.

    “Sasa dokta unafikiri tutafanyaje wakati huu ndiyo ukweli.”

    “Ni kweli lakini ni ukweli ambao utaenda kumuumiza sana.”

    “Tumdanganye?”

    “Sidhani kama hiyo itakuwa ni suluhisho,” alisema dokta Masawwe huku akionekana kuchanganyikiwa kwa kiasi fulani.

    Hakujua alitakiwa amuambie vipi Mama yake Andrew pindi atakapokuwa amepata fahamu. Alihisi kuwa katika wakati mgumu sana hasa wa kumueleza ukweli.

    ****

    Herieth bado aliendelea kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Steven mwanachuo mwenzake ambaye alitokea kumpenda sana, hakukuwa na mwanaume mwingine ambaye alimpenda chuoni zaidi ya Steven. Moyoni aliamini Steve ndiye aliyekuwa mwanaume wa maisha yake. Hisia za kimapenzi zikamteka haswaa na kila kitu alichokuwa akikifanya alikifanya kwasababu ya Steven.

    Siku ziliendelea kusonga mbele za uhusiano wao huku kila mmoja akiufurahia uwepo wa mwenzake, walionekana kupendana sana hata baadhi ya wanachuo wenzao walikiri hilo na mara kadhaa walipopata wasaa wa kupiga soga hawakuacha kuuzungumzia uhusiano wao.

    “Wanapendana sana,” alisema mwanachuo mmoja wa kike.

    “Kweli wanapendeza kuwa pamoja,” alisema mwanachuo mwingine.

    Licha ya wazazi wao kuwa matajiri lakini utajiri aliyokuwa nao Baba yake Steven uliweza kumfunika Baba yake Herieth ambaye alitamba kwa utajiri wake Kilimanjaro tu! lakini kwa utajiri wa Baba yake Steven ulikuwa ni wa kidunia, hilo lilizidi kumfanya Herieth apagawe na penzi la mtoto wa bilionea huyo ambaye aliamini kwa vyovyote vile katika maisha yake angeweza kuishi kama malkia.

    ****

    Selestine bado alijiona kuwa mshindi kwa tukio alilokuwa amelifanya, alijiona kuwa na kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kumsaidia kufanikisha dhamira yake aliyokuwa ameikusudia.

    Aliendelea kuishi maisha ya furaha hotelini huku moyo wake ukiwa katika furaha kubwa sana, kila alipomkumbuka Andrew pamoja na matukio ya kipindi kile walipokuwa wakisoma alibaki akicheka peke yake kama mwendawazimu.

    Hakutaka kuendelea kubaki Kilimanjaro, aliamua kupanga safari ya kurudi Daresalaam japo alijua kuwa alifanya makosa na alifahamu fika alikuwa akitafutwa kwa wakati huo lakini hilo halikumtisha hata kidogo. Alipanga kurudi lakini ilikuwa ni katika mpango wake wa kumuangamiza Mzee Antony, alipanga kumuua, aliamini kama akishindwa kufanya hivyo basi maisha yake yangekuwa hatarini.

    ****

    Alipopata fahamu Mama Andrew kitu cha kwanza kilichomjia katika ufahamu wake alikuwa ni mwanaye kipenzi, alianza kumuita huku akiyaangaza macho yake huku na kule alipokuwa amelazwa kitandani, alikuwa akionekana kutokukumbuka kitu chochote kilichokuwa kimetokea. Ilibidi dokta Masawwe anaanze kumtuliza kabla ya kumueleza kitu chochote kile.

    “Mwanangu yuko wapi?”

    “Yupo usijali.”

    “Yuko wapi?”

    “Amepumzika subiri akiamka utaenda kumuona.”

    “Nataka nikamuone hivyohivyo mwanangu tafadhalini.”

    “Utaenda kumuona usijali.”

    “Nataka sasa hivi,” alisema Mama Andrew huku akionekana kujawa na wasiwasi mkubwa sana.

    Ilibidi dokta Masawwe afanye kama Mama yake Andrew alivyotaka, aliamua kumpeleka katika chumba alichokuwa amelazwa Mwanaye kwa wakati huo alikuwa amelala. Alipomfikia alipiga magoti chini na kuanza kumuita huku akijaribu kumtingisha mwili wake, Andrew hakuweza kuamka.

    “Mbona haamki?” aliuliza huku akionekana kuingia na hofu.

    “Amelala,” alisema dokta Masawwe.

    “Dokta kwe….” alisema Mama Andrew lakini kabla hajamalizia kutamka sentensi yake alishangaa akikumbwa na kigugumizi hapa ni baada ya kumuona mwanaye akiwa haonyeshi dalili zozote za kuvuta pumzi. Hapo hapo akaanza kulia kama mtoto mdogo pindi anapomkosa Mama yake pale anapomuhitaji.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mama Andrew hakutaka kuamini kama kweli mwanaye alikuwa amefariki dunia, aliendelea kulia huku machozi yaliyokuwa yakimbubujika mashavuni mwake yakimgusa kila mtu aliyekuwemo mule ndani.

    “Usilie Mama Andrew,” alisema nesi huku akijaribu kumbembeleza Mama Andrew ambaye alikuwa akilia kama mtoto mdogo, wakati huo dokta Masawwe alikuwa akimtazama huku akilengwalengwa na machozi, alikosa neno la kumwambia kwa wakati ule, kila alichokuwa akikifiria kichwani mwake kwa wakati huo alikiona hakina maana tena na ni hapa ambapo alizidi kuchanganyikiwa.

    Hakutaka kuendelea kuwa mtazamaji kwa kumwangalia Mama Andrew ambaye alikuwa katika kilio, aliamua kwenda kuchukua jukumu zito la kumbembeleza na kumwambia juu ya hali ile halisi iliyokuwa imetokea kwa mwanaye. Lilikuwa ni jukumu zito sana hasa la kumwambia ukweli Mama Andrew.

    “Pole sana Mama Andrew najua ni vigumu sana kuweza kukubaliana na hili lililotokea kwa mwanao ila ninachokuomba jikaze,” alisema dokta Masawwe huku akijaribu kumsihi Mama Andrew asiendelee kulia.

    Machozi bado yaliendelea kushika hatamu yake katika uso wa Mama Andrew, yaliendelea kumbubujika bila kukoma.

    “Andrew mwanangu amka, amka mwanangu unione Mama yako, amka baba, amka mwananguuu,” alisema Mama Andrew kwa sauti iliyosindikizwa na kilio.

    Hakutaka kukubaliana na kile kilichokuwa kimetokea kwa mwanaye lakini ukweli ni kwamba Andrew alikuwa amefariki dunia.

    ****

    Mzee Antony bado aliendela kuishi maisha ya chuki huku moyo wake ukiwa umehifadhi kisasi dhidi ya Selestine ambaye alipanga kumuua kabisa. Alikuwa amewapa kazi vijana watatu ya kumtafuta Selestine mahali popote pale alipo na endapo wangeweza kumkamata walitakiwa kumuua. Hilo ndilo alilokuwa amedhamiria kulifanya kwa Selestine kwani hakuona thamani yake tangu alipoweza kumuibia pesa zake. Alipofanikiwa kusafirisha madawa ya kulevya na kuyauza nchini aliweza kupata pesa nyingi sana, huo kwake ulikuwa ni zaidi ya ushindi mkubwa sana, alizidi kujiona kuwa bora.

    Baada ya kupita siku kadhaa aliweza kuletewa habari na wale vijana wake ambao aliwapa kazi ya kumtafuta Selestine, hawakuweza kumpata Selestine kwa wakati. Mzee Antony aliwaona kuwa wazembe kwa kazi aliyokuwa amewapa, kwa hasira alizokuwa nazo aliamua kuwaua wote watatu kwa kuwapiga risasi kisha maiti zao akaenda kuzitelekeza ufukweni mwa bahari ya Hindi ‘Coco beach’. Hakudhamiria kufanya mauaji yale ila kutokana na hasira alizokuwa nazo dhidi ya Selestine alijikuta akiwaua na baadae kujutia maamuzi yake.

    Alichokuwa akikiwaza ni kuitengeneza kesi ya mauaji ambayo mwisho wa siku alipanga Selestine ndiye aonekane kuwa amefanya mauaji yale, alijikuta akifurahi mara baada ya kufanikiwa kupata wazo ambalo kama kweli lingefanikiwa kutimia basi Selestine angeweza kufungwa jela kwa kifungo cha maisha.

    ****

    Nchini Afrika kusini katika chuo cha Pretioria Herieth aliendelea kufurahia maisha yake ya kimapenzi na Steve mtoto wa bilionea wa Marekani. Maisha yalionekana kuwa mazuri sana hasa ukizingatia hakukuwa na tatizo lolote kati yao. Licha ya kuwa walikuwa wakifanya vizuri katika mitihani yao pale chuoni lakini waliishi maisha ya starehe, waliutumia muda mwingi sana katika kufanya starehe.

    “Leo unataka twende wapi mpenzi?” aliuliza Steve huku akimtazama Herieth kwa jicho la huba.

    “Twende popote,” alijibu Herieth.

    “Wapi?” aliuliza Steve.

    “Popote.”

    “Nimekupa nafasi ya kuchagua.”

    “Sawa basi twende Cape Town”

    “Sawa mimi sina tatizo,” alijibu Herieth kisha kilichofuata mahali hapo ilikuwa ni kujiandaa na kwenda huko Cape Town kwa lengo la kufanya starehe katika fukwe za bahari.

    Mpaka kufikia wakati huo Herieth alikuwa hajui hali ya Andrew wala hakutaka kusikia lolote kuhusu kiumbe kilichokuwa kikiitwa jina la Andrew, alimchukia sana na kwa wakati huo alikuwa amezama katika kina kirefu cha mapenzi ya Steve, alikuwa haoni wala hasikii.

    ****

    Mzee Antony aliamua kuwatafuta waandishi wa habari na kuwaeleza juu ya habari zile za mauaji yaliyotokea ambapo kwa wakati huo zilikuwa zimepamba moto katika vyombo vya habari mbalimbali, kwenye magazeti ya udaku hakukuwa na habari nyingine zaidi ya habari hiyo ya mauaji ya watu watatu waliyokutwa ufukweni mwa bahari. Kila mtu alikuwa katika hali ya sintofahamu, hakukuwa na mtu aliyekuwa akifahamu lolote kuhusu muuaji aliyefanya mauaji yale. Jeshi la polisi liliingilia kati na halikutaka kufumbia macho mauaji hayo, walikuwa katika uchunguzi maalumu wa kumtafuta muuaji ambaye alikuwa amefanya mauaji yale.

    “Nina dili nataka kukushirikisha na wewe,” alisema Mzee Antony alipopata nafasi ya kukutana na mwandishi wa habari mmoja wa magazeti aliyejulikana kwa jina la Novatius. Wakati huo walikuwa katika hoteli ya Seashells Millennium iliyokuwepo Mikocheni.

    “Dili gani hilo?” aliuliza Novatius huku akionekana kuwa makini kusikiliza.

    “Kuhusu huyu muuaji anayetafutwa na jeshi la polisi,” alisema Mzee Antony huku akijitoa ufahamu na kuuvaa uhusika wa ushuhuda wa ukweli bandia aliyokuwa ameupanga kichwani mwake.

    “Muuaji?”

    “Ndiyo muuaji wa wale vijana watatu miili yao iliyokuwa ufukweni mwa bahari.”

    “Unasema ukweli?”

    “Ndiyo,” alijibu Mzee Antony huku akionekana kujiamini.



    Hakutaka kupoteza muda mahali pale, alichoamua kukifanya alianza kumueleza ukweli Novatius juu ya muuaji aliyekuwa akitafutwa na jeshi la polisi. Alionekana kufahamu kila kitu kuhusu muuaji huyo, hilo alilidhihirisha kupitia mazungumzo yake, alionekana kumaanisha kila neno alilokuwa akilitamka jambo ambalo halikuwa na ukweli wowote, ulikuwa ni ukweli bandia wenye lengo la kumuangamiza Selestine.

    “Unayosema ni kweli?” aliuliza Novatius huku akimtazama Mzee Antony kwa macho ya wasiwasi.

    “Ndiyo namfahamu muuaji,” alijibu Mzee Antony huku akiendelea kumkazia macho Novatius ambaye alionekana kutomuamini kabisa. Kitendo hicho kiliweza kumshtua Novatius na sasa akajikuta akianza kumuamini Mzee Antony.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Anaitwa nani?” aliuliza Novatius.

    “Anaitwa Selestine,” alijibu Mzee Antony.

    “Picha yake unayo?”

    “Ndiyo lakini ni passport.”

    “Haina shida kama unauhakika ni yeye kweli muuaji basi hakuna kilichoharibika itabidi nifanye kazi yangu ya uandishi kama inavyoniagiza halafu kitu kitakachofuata ni kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi.”

    “Mimi sina tatizo isipokuwa lengo langu ni kuona huyu muuaji anakamatwa maana anazidi kututishia amani,” alisema Mzee Antony huku akijifanya kusitikika.

    Kama alivyozungumza Novatius ndivyo ambavyo mambo yalienda kama yalivyopangwa. Kwa ushirikiano wa Mzee Antony juu ya ushuhuda wake wa muuaji ambaye alikuwa akitafutwa aliweza kulisaidia jeshi la polisi na mpaka kufikia wakati huo alikuwa ameshawapelekea vithibitisho vyote juu ya matukio ya mauaji aliyokuwa akiyafanya. Alikuwa amedhamiria kumuangamiza Selestine wala hakutaka kuwa katika wakati wa masihara hata kidogo, kitu kilichompelekea mpaka akawa katika hali hiyo zilikuwa ni pesa zake alizoibiwa.

    “Lazima uangamie,” alijisemea Mzee Antony huku akitabasamu, wakati huo alikuwa nyumbani kwake.

    Hakuishia tu! kwa kumsingizia kesi ya mauaji bali alifika mbali na kumzushia kuwa alijihusisha na biashara haramu za uuzaji na ununuaji wa madawa ya kulevya, kila kitu alichokuwa akikizungumza polisi alikuwa na ushahidi nacho na hivyo polisi hawakuweza kumpinga kwa lolote.

    “Kumbe hili li jamaa ni jambazi sugu kabisa linauza mpaka madawa ya kulevya?”aliuliza polisi mmoja mwenye lafudhi za watu wa kanda ya ziwa.

    “Ndiyo afande,” alijibu Mzee Antony kwa kujiamini.

    Hakukuwa na kitu kilichoshindikana kwa Mzee Antony, pesa ilishika nafasi yake katika kuhakikisha mambo yote aliyokuwa ameyapanga yanatimia. Alitumia pesa nyingi mno katika kuwanunua mawakili na mashahidi wa uongo juu ya kesi hiyo iliyokuwa ikimuandama Selestine.

    Vyombo vya habari vilianza kuripoti habari za muuaji Selestine, kila aliyekutana na habari hizo aliweza kulaani na wengine waliyonyimwa roho ya uvumilivu walijikuta wakitokwa na matusi ya nguoni bila kutarajia.

    ****

    Alipofanikiwa kufika Daresalaam hakutaka kila mtu afahamu ujio wake, aliamua kutafuta hoteli maeneo ya Sinza na kama kawaida yake akajificha huku akiendelea kufanya uchunguzi wake. Hakujua ni nini kilichokuwa kikiendelea kwa wakati ule.

    Kichwani mwake bado taswira ya Mzee Antony ilikuwa ikimjia, alipanga kumuua kabisa, hilo ndilo lilikuwa lengo lake na kadri siku zilivyokuwa zikisonga pale hotelini alipokuwepo aliona kama lengo lake linachelewa kutimia.

    Baada ya siku tatu kupita alianza kupanga mipango ya kumuangamiza Mzee Antony. Aliamua kujipanga kisawasawa kwani aliamini mtu ambaye alikuwa anakwenda kumuua hakuwa ni mtu wa kawaida, alikuwa ni mtu hatari sana.

    Kipindi ambacho aliamua kwenda kuifanya kazi yake ndipo ambapo Mzee Antony alikuwa amefanikiwa kumchafua Selestine katika vyombo vya habari na tena kibaya zaidi alikuwa amemuuzia kesi ya mauaji na kwa wakati huo alikuwa akitafutwa kwa udi na uvumba na jeshi la polisi.

    Selestine hakutaka kuamini macho yake kwa kile alichokuwa akikiona katika magazeti. Picha yake pamoja na kichwa cha habari kilichosomeka kwa maandishi ya herufi kubwa "MUUAJI ANAYETAFUTWA.

    "

    Alihisi kuchanganyikiwa baada ya kuona hivyo, nguvu zikaanza kumuishia, mauaji aliyokuwa amepanga kufanya aliamua kuyakisitisha. Skendo ile ilionekana kumshtua sana, akaamua kubaki hotelini akiendelea kujificha kuhofia kukamatwa na Polisi.

    ****

    “Kwanini hutaki kunielewa mpenzi?”

    “Nikuelewe nini Steve wakati kila kitu nakiona hapa.”

    “Mpenzi wangu kwanini unakuwa sio muelewa?”

    “Hakuna utakachoniambia nikakuelewa hivi kweli wewe leo wakunifanyia mimi hivi?”

    “Niamini mpenzi wangu hakuna kitu chochote kibaya nilichokufanyia hii ni picha tu.”

    “Steve umekosa nini kwangu?”

    “Hakuna nilichokosa.”

    “Niambie ni nini umekosa?”

    “Hakuna mpenzi wangu.”

    “Kwanini umeamua kunichanganya kiasi hiki?”

    “Herieth.”

    “Naomba unijibu kwanza tafadhali.”

    “Ni kweli nimekosea ila naomba unisamehe mpenzi wangu sitarudia tena nakuahidi.”

    Yalikuwa ni mazungumzo kati ya Herieth na Steve, wakati huo Herieth alikuwa akibubujikwa na machozi mashavuni mwake huku mkononi akiwa ameishika simu yake, alikuwa akiitazama picha katika simu yake hiyo. Hakutaka kuamini kile alichokuwa akikishuhudia katika picha hiyo. Alimuona mpenzi wake Steve akiwa sanjari na msichana mwingine mwenye asili ya kichina ambapo walionekana kuwa katika hali ya kimapenzi.

    Picha hiyo ilizidi kumuumiza sana Herieth na kila alipokuwa akiitazama moyo wake ulikuwa katika maumivu makali mno. Steve ndiye alikuwa mwanaume wake wa kwanza ambaye alimpenda na kumkabidhi dhamana ya mwili wake wa mapenzi lakini vilevile ndiye alikuwa mwanaume wake wa kwanza kumuumiza kimapenzi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kila siku Herieth aliendelea kuteswa na mapenzi, hakukuwa na mwanaume mwingine ambaye alikuwa akimtesa pale chuoni zaidi ya Steve. Steve alikuwa ni mwanaume ambaye alishiriki kwa kiasi kikubwa katika kuupondaponda moyo wa Herieth bila kujali maumivu aliyokuwa akiyapata. Tabia yake ya upole na ukarimu ilianza kubadilika pale ambapo alifanikiwa kufanya mapenzi na Herieth, hakuiona thamani yake tena. Aliutumia utajiri wa Baba yake katika kumteka Herieth. Hiyo ndiyo silaha kubwa aliyoitumia pia katika kuwateka kimapenzi wasichana wengine pale chuoni. Uzuri wa kumuona msichana mrembo hakuishia kumuona Herieth ambaye kila kukicha alikuwa akimsifia na kukiri katika maisha yake hakuwahi kukutana na msichana mrembo kama yule. Ni kweli katika maisha yake hakuwahi kutembea na msichana kutokea bara la Afrika tena katika nchi ya Tanzania lakini ilikuwa ni mazoea kwake kubadilisha wanawake kama nguo. Awali tabia yake ilifichika, alionekana kuwa mpole, mkarimu kiasi kwamba kila msichana aliyemuona alitamani kuwa naye kimapenzi. Hilo lilikuwa ni kosa kubwa ambalo walikuwa wakilifanya na kila mwanachuo ambaye alionekana kujirahisisha hakuachwa salama.

    Mtandao wa kuwapanga wasichana pale chuoni uliendelea, alikuwa ni mtu wa kupenda wanawake sana wala hakukuwa na mtu wa kushindana naye katika hilo.

    Ugomvi wake na Herieth ulianzia katika picha alizokuwa amepiga na msichana mwenye asili ya kichina, walionekana kuwa na ukaribu ule wa kimapenzi. Herieth alizidi kuumia hapa ni pale alipoanza kusikia tetesi kuwa Steve alikuwa akimchanganya na wasichana wengine pale chuoni, alikuwa akitembea mpaka na marafiki zake kitendo ambacho kilimuweka katika maumivu makali sana, muda wote alikuwa akilia.

    Alijutia mambo mengi sana ambayo alikuwa amefanya na Steve, alimuamini sana kupita maelezo na hiyo ndiyo sababu ambayo ilimfanya hata pale alipomuhitaji kufanya naye mapenzi aliamua kufanya huku akiamini kuwa kuna siku ingefika angekuwa mke halali wa Steve. Hayo yalikuwa ni sawasawa na mawazo ya kufikirika kamwe yasingeweza kutokea.

    “Kwanini umenifanyia ukatili huu Steve kwanini?” aliuliza Herieth huku akilia machozi ya uchungu.

    “Labda nikwambie kitu kimoja Herieth mimi sijakupenda kwa moyo wangu wote, nilikutamani tu na nilichokuwa natafuta nimekipata hivyo naomba huu ndiyo uwe mwisho wa mahusiano yetu,” alijibu Steve kisha akaondoka eneo lile, hakutaka kuendelea kuzungumza na Herieth ambaye alianza kumuona kama kero kwake, hakumpenda tena na kwa wakati ule alichokuwa amehifadhi katika moyo wake ni chuki. Alimchukia sana Herieth.

    Yalikuwa ni zaidi ya maumivu katika moyo wa Herieth, hakutaka kuamini kwa kile alichokuwa amekisikia kutoka kwa Steve mwanaume ambaye alimpenda na kumuamini kwa kila kitu, hakutaka kuamini hata kidogo akabaki ameduwaa kwa muda asiamini kama kweli ni yeye alikuwa ameambiwa hivyo. Wakati huo Steve alikuwa ameondoka na kumuacha peke yake. Steve hakuonekana kujali lolote kuhusu Herieth. Huo ndiyo ulikuwa mwisho wa mahusiano yao.

    ****

    Mzee Antony aliendela kutumia nguvu ya pesa zake katika kumuangamiza Selestine, aliamini kwa kile alichokuwa amekifanya ni lazima angeinuka na kuwa mshindi.

    Huo ulikuwa ni ukweli kwani mpaka kufikia wakati huo Selestine alikuwa hajui ni nini ambacho alitakiwa kufanya ili aweze kujiokoa, picha zake zilisambaa kila kona. Alikuwa akitafutwa kwa udi na uvumba.

    Baada ya kupita siku kadhaa kutokana na ushirikiano wa muhudumu wa hoteli aliyokuwa amefikia Selestine aliweza kulisaidia jeshi la polisi ambapo walifanikiwa kumkamata.

    Hatimaye Selestine akajikuta mikononi mwa jeshi la polisi huku akituhumiwa kwa kesi ya mauaji na uuzaji wa madawa ya kulevya nchini. Ilikuwa ni kesi ambayo kama angepelekwa mahakamani na kuhukumiwa basi angehukumiwa kifungo cha maisha.

    ****

    Herieth hakutaka kumuamini Steve kama alikuwa salama kiafya, alichoamua kufanya ni kwenda katika hospitali ya Zuid Afrikans iliyokuwepo Pretoria, Afrika kusini na kupima afya yake. Aliamua kupima maradhi yote huku akionekana kutojiamini, alihisi wenda alikuwa na tatizo lolote la kiafya.

    “Why if you seem to be afraid?” (Mbona kama unaonekana kuogopa?) aliuliza dokta mara baada ya kumuita Herieth ofisini kwa lengo la kumpa majibu yake.

    “I’m right,” (Nipo sawa) alijibu Herieth.

    “So are you ready to receive your answers?” (Kwahiyo upo tayari kupokea majibu yako?)

    “Yes.” (Ndiyo.)

    “We’ve been able to prevent all illnesses while there is only one thing you have.” (Tumekupima maradhi yote upo salama ila kuna kitu kimoja unacho.)

    “What’s that?” (Kitu gani?)

    “You’re Pregnant.” (Una mimba.)

    “What do you say?” (Unasemaje?)

    “You’re Pregnant,” (Una mimba,) alijibu dokta.

    Herieth hakuamini kile alichokuwa akikisikia kutoka kwa dokta ambaye alikuwa akimpa taarifa za ujauzito wake, hakutaka kuamini kama alikuwa amebeba ujauzito wa mwanaume huyo ambaye alitoka kuachana naye siku chache zilizopita. Majibu hayo yaliweza kumshtua sana.

    Aliporudi chuoni aliamua kumtafuta Steve ili aweze kumwambia habari zile, hakuweza kumuona kwa wakati ule hasa ukizingatia usiku ulikuwa tayari umeshaingia, alichoamua kukifanya ni kumpigia simu ili aweze kumwambia. Hakuwa akipatikana kwenye simu yake. Hakutaka kujiuliza sana, aliamua kumsubiri huku akionekana kuwa na wasiwasi uliyochanganyika na maumivu ya kusalitiwa. Hakujua kama Steve angeweza kuukubali ujauzito ule.

    Baada ya kupita masaa kadhaa iliweza kuja taarifa kuwa Steve alikuwa amepata ajali ya gari alipokuwa akitoka Club usiku ule akirejea chuoni, ilikuwa ni ajali mbaya sana ambayo ilisababisha kifo chake. Kwa mshtuko Herieth alijikuta akianguka chini na kupoteza fahamu.

    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Selestine alikuwa akituhumiwa kwa kesi ya mauaji aliyokuwa ameyafanya jambo ambalo halikuwa na ukweli wowote, kila alipokuwa akihojiwa hakuweza kukiri kwa kosa hilo alilokuwa amelifanya, hali hiyo ya kukataa ilimfanya apokee kipigo kikali sana na kumuacha na maumivu ya kutoyatarajia.





    “Jamani sijaua mimi,” alisema Selestine kwa sauti iliyomaanisha ukweli wa alichokuwa akikisema lakini hakukuwa na polisi aliyemsikiliza. Kadri alivyokuwa akiendelea kukataa ndivyo alivyozidi kupokea kipigo kikali sana. Maumivu aliyokuwa akiyapata alishindwa kuyavumilia mwisho akabaki akilia, alilia kilio kikali sana kilichokuwa na maumivu mno.

    “Jamani msinipige mimi sihusiki na hayo mauaji,” alisema kwa sauti iliyokosa ustahimilivu wa kipigo alichokuwa akikipata lakini ni kama alikuwa akipigia mbuzi gitaa kwani ndiyo kwanza wale polisi waliendelea kumpiga bila kujali maumivu yake.

    ****

    Alipopata fahamu kila kitu kilionekana kuwa tofauti na matarajio yake, alipanga kumueleza Steve kuhusu ujauzito aliokuwa nao, ulikuwa ni wake lakini kwa wakati ule alikuwa ameshakufa. Hakutaka kuamini kirahisi kama Baba halali wa ujauzito wake alikuwa amefariki dunia, alilia sana tena kwa uchungu.

    Baada ya kupita siku kadhaa tangu Steve alipofariki dunia maisha yaliendelea huku akiwa amekubaliana na hali halisi iliyokuwa imetokea. Mwanzoni alipanga kuitoa mimba hapa ni baada ya kukumbuka mateso na maumivu aliyoyapata kwa Steve, alimchukia sana lakini punde kumbukumbu za mapenzi yao ya dhati kipindi cha uhai wa Steve zilipomjia kichwani alijikuta akimkumbuka sana, moyo wake ulirudisha mapenzi, alihisi kumpenda sana Steve ambaye mwisho wa siku alikuwa kivuruge wa moyo wake. Alimuumiza mno

    ****

    “Shida yako ni nini?” aliuliza polisi ambaye alikuwa amepewa dhamani ya kusimamia kesi iliyokuwa ikimuandama Selestine.

    “Nataka apotee kabisa,” alisema Mzee Antony huku akimtazama polisi aliyekuwa akizungumza naye.

    “Kuhusu hilo ondoa shaka lazima sheria ifuate mkondo wake,” alijibu polisi.

    “Ukifanya kama nilivyokwambia nitakupa pesa nyingi sana.”

    “Usijali.”

    “Nimeshapanga mipango yote ya kumuandalia kaburi lake,” alisema Mzee Antony. Aliamua kutoa kiasi cha pesa cha shilingi milioni ishirini kisha akampatia yule polisi. Furaha yake ilikuwa ni siku moja aone Selestine amekufa.

    Baada ya upelelezi kufanyika polisi walimjua muuaji ambaye alikuwa amefanya amuaji yale, hakuwa Selestine kama walivyokuwa wakidhani ila kutokana na pesa alizokuwa akitumia Mzee Antony katika kumkandamiza Selestine alionekana kuwa muuaji. Ukweli ulijulikana kuwa Mzee Antony ndiye mtu pekee aliyekuwa akihusika na mauaji hayo hata katika upande wa vyombo vya habari chanzo cha kutoa habari kuhusu muuaji Selestine alikuwa ni yeye, alikuwa akiwanunua waandishi wa habari na kisha kuwauzia habari za muuaji ambazo hazikuwa na ukweli wowote. Aliamua kufanya hivyo kama kulipa kisasi kwa kuibiwa pesa zake na Selestine.

    Kutokana na nguvu walizokuwa nazo Jeshi la polisi waliweza kumkamata Mzee Antony na kumpeleka moja kwa moja Mahakamani huku akiwa ni mtuhumiwa wa kesi ya mauaji pamoja na uuzaji wa madawa ya kulevya.

    Kwa upande wa Selestine aliamini ule ndiyo ulikuwa mwisho wake wa mateso lakini katika hali ya kushangaza Mama yake Andrew pamoja na Derick waliweza kujitokeza na kutoa ushahidi kuhusu mauaji aliyokuwa ameyafanya Selestine mkoani Kilimanjaro. Walikuwa na ushahidi uliyokamilika mpaka rekodi ya sauti ambayo Selestine alikuwa akizungumza na Derick kwenye simu kipindi kile alipokuwa akimwambia kuhusu lengo lake la kumuua Andrew. Hakukuwa na mtu ambaye mtu aliyeweza kuamini kwa kile kilichokuwa kikisumulia, Mama Andrew machozi yalikuwa yakimbubujika mashavuni.

    Hatimaye Selestine na Mzee Antony waliweza kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani baada ya kukutwa na hatia ya mauaji.

    Mama Andrew alipata mdhamini ambaye aliahidi kumsaidia katika maisha yake baada ya kuguswa na simulizi ya maisha yake iliyomtoa machozi.

    ****

    Baada ya kupita miezi sita Herieth aliamua kuacha chuo Afrika Kusini kisha akaamua kurudi nchini Tanzania kwa malengo ya kuja kuilea mimba yake, wazazi wake baada ya kugundua alikuwa ni mjamzito na kwa wakati ule alikuwa ameacha chuo waliamua kumfukuza nyumbani, hawakutaka kumuona tena, walipoteza pesa nyingi sana katika kumsomesha nchi mbalimbali lakini pesa zao ni kama vile walikuwa wakizitupa katika shimo la choo, hazikuonekana thamani yake na kwa wakati huo mtoto waliyokuwa wakimsomesha alikuwa ameacha chuo huku akiwa ni mjamzito. Tangu hapo maisha ya Herieth yalibadilika na kuwa ni mtu wa kutangatanga mitaani, hakuwa na sehemu maalumu pa kula wala pa kulala. Joto, baridi, mbu vyote vilikuwa ni sehemu ya maisha yake.

    Baada ya kutimia miezi tisa hatimaye Herieth alifanikiwa kujifungua mtoto wa kiume katika wakati wa mateso sana, alikuwa ni mtoto aliyefanana kila kitu na baba yake, aliamua kumuita jina la Steve huku akiamini ilikuwa ni njia pekee ya kutomsahau Steve mwanaume aliyemfunza mambo mengi sana katika ulimwengu wa mapenzi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Herieth alipata bahati ya kusaidiwa yeye pamoja na mtoto wake katika kituo cha kulelea watoto yatima na hapo ndipo aliufungua ukurasa mpya wa maisha yake.



    Herieth aliishi maisha yake yote lakini alishindwa kumsahau kabisa Steve.



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog