Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

JELA NI HAKI YANGU - 1

 







    IMEANDIKWA NA : MODEL TEDDY



    *********************************************************************************



    Simulizi : Jela Ni Haki Yangu

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Mbaramwezi iliweza kukubali kuwa wakati wa utawala wake umekisha , japo nyota nao walikuwa wakijitahidi kutoa mwanga ili kuuchukua ufalme wa jua lakini nao walishindwa kutokana na ukali wa miale ya jua , wote waliondoka eneo hilo wakiwa wamezivuta sura zao si kwa bwana mkubwa mbaramwezi au wadogo zake waliokuwa wabishi wa kukubali kuwa mda wao umefika mwisho hivyo wamkabidhi utawala mheshimiwa jua aliekuwa ameanza kujitapa kwa kuanza kutoa miale michache lakini ilikuwa ikiathili afya za wapizani wake .

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Miale hiyo iliendelea kuchukua nafasi tena kwa fujo sana na hali ya kujitapa kuwa huo ulikuwa utawala wao , hawakuwa nyuma katika swala la kuchekelea ushindi wao , uliokuwa umeanza kusaidiwa na kusherekewa na viumbe wengine kama jogoo waliokuwa wakiwika kuashilia kuwa siku nyingine imewadia , ndege nao hawa kuacha kuimba nyimbo tofauti tofauti zenye mashairi ya kuisifu siku hiyo mpya waliruka kutoka mti mmoja hadi mwingine .

    Kadri mda ulivyozidi kuongezeka ndivyo bwana jua aliendelea kuiruhusu miale yake iendelee kutoka kwa kasi sana hali iliyopelekea anga kuwa jeupe na hiyo ikawa teyari imeitwa asubuhi ya siku nyingine .



    Kila kiumbe kilichokuwa kimepewa utukufu wa kutawala wakati wa utawala wa bwana jua kiliamu kuziondoa mbavu ama migongo yao iliyokuwa imelazwa kwenye vitanda vyenye magodoro ama sehemu isiyokuwa na magodoro binadamu ndio hasa watawala wa kila kiumbe walianza kutoka majumbani kwao na kuelekea sehemu zenye kujipatia riziki zao muhimu , purukushani mbalimbali zilikuwa zinaendelea mijini watu walikuwa wakigombania vyombo vya usafiri ili wawahi sehemu hizo , vijijini nako wananchi walikuwa wakitoka majumbani kwao, hawakuacha kubeba siraha za mapambano kama vile panga , majembe begani ama mkononi kuelekea shambani hakika kila mtu alikuwa bize na jukumu lake , kila mkazi wa nchi ya BUSOGA alikuwa ameipania siku hiyo kuwa iwe ya baraka kwake .



    Shughuli mbalimbali zilizidi kuendelea huku jua nalo likizidi kupanda juu zaidi , wafanyabiashara , wafanyakazi walikuwa wameshafungua biashara zao , wanafunzi hawakuwa nyuma katika swala la kuongeza elimu na ujuzi vichwani mwao kwa ujumla shughuli zilikuwa zimepamba moto .



    Matumaini ya kila mkazi wa nchi hiyo yalivunjika mnamo saa 4:39, asubuhi , hali ya hewa ilibadilika furaha na tabasamu zilizokuwa zimetanda kwenye mioyo na nyuso za wakazi wa nchi hiyo ziliyeyuka ghafla kama barafu ndani ya maji , shambulio la ghafla na la kusitukiza lilifanyika ndani ya dakika hizo , majengo mbalimbali ya taifa yalilipuliwa na kusababisha uharibifu mkubwa sana , watu wengi walipoteza maisha yao achilia mbali majeruhi na waliopata ulemavu hawakuhesabika watoto na wanawake ndo hasa walioathilika zaidi , hali ikiwa bado mbaya katika mji mkuu wa nchi ya BUSOGA uliokuwa ukifahamika kwa jina la MISSION , makazi ya Raisi wa nchi hiyo alimarufu kama ikulu yalilipuliwa dakika kumi na moja mbele hali iliyopelekea wanajeshi wengi kupoteza maisha yao . Haikuishia hapo tu makao makuu ya jeshi nayo yalipata madhara mda huo huo hakika ilikuwa hali ya kutisha sana .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Japo machafuko hayo yalifanyika ndani ya dakika kumi na moja tu lakini yalikuwa makubwa sana na ya kutisha idadi kubwa ya watu waliopoteza maisha ilikuwa haielezeki .

    ********

    "shit!!! mmefanya nini???, kwanini mmemuacha yule kenge aendelee kupumua!?" Rambo kiongozi mkubwa wa kundi la kigaidi la Al-kida alikuwa akiongea kwa hasira sana huku mapovu mdomoni yalikuwa yakimtoka , sura yake nayo ilibadilika na kutisha sana japo alikuwa na sura ya mvuto kwa wanawake lakini siku hiyo ilibadilika , mwili wote ulikuwa ukimtetemeka kwa hasira kali sana japo kulikuwa na panga boy ndani mle lilionekana kama halifanyi kazi yake kutokana na jasho jingi kuendelea kumtoka ,

    " wewe hebu niambie kwanini hamkutekelezaaaaaaa" alikuwa teyari ametembea na kusimama mbele ya mmoja ya vijana wake , mkono wake Wa kulia ulikuwa umeshika kola la shati la kijana huyo aliekuwa akitetemeka baada ya kutupia macho mkono huo uliokuwa umevimba na kujichora misuli misuli, " bo..oss wa ....wali....tuzidi...ujanja" aliongea kwa tabu sana kutokana na kukabwa shingo yake sawasawa , macho yake nayo yalikuwa yakiona nyota nyota zikipita na kumzomea " kiaje mmmmh!?"aliuliza Kwa sauti ya juu sana , macho nayo yalikuwa yametoka na kuwa makubwa" mheshimiwa Raisi hakuwemo katika msafara huo!"

    " mjinga sana , sina raisi mimi sema kenge hakuwemo pumbafuu" aliongea maneno hayo makali huku akimsukuma Carlos chini na kuanguka chini kama mzigo " puuuuu!".



    " kenge hakuwemo" alisema kama alivyoamriwa maana ilikuwa ni lazima kutekeleza kile alichokiongea la sivyo kichwa chako kitazawadiwa risasi

    " alipita wapi !????, nawauliza wote humu ndani hakuna mwanamke nyote jibuni haraka !" aliendelea kuongea huku akizunguka zunguka ndani humo ." nilivyosikia kuwa alishukia Bulogwa "

    David aliongea huku akiwa anatetemeka kiasi " oky kumbe Jesca mbwa hivi !" aliongea huku akiweka bastora yake kiunoni na kutoka kwa hasira sana , akiwaacha vijana wake katika mawazo .



    " lakini ilikuwaje hadi akashukia Bulogwa ili hali ndege yake nayo ilikuwepo uwaja wa ndege!?"

    " hata nami sijui tu " Carlos alijibu huku akijifuta futa michanga katika midomo yake , hawakuweza kuongea zaidi maana walikuwa hawajui nini kilitokea hivyo walimuachia jukumu hilo boss wao Rambo.walichukua sigara na kuzivuta taratibu .



    Purukushani zilikuwa hazielezeki , kila mtu alikuwa akikimbia sehemu salama ili kuiokoa roho yake , wanaume hawakujali wake na watoto wao hivyo waliondoka wao kama wao, baada ya kupita saa moja na nusu hali ilitulia kila sehemu kukawa kumebakia na askari pamoja na raia wachache waliokuwa wakisaidiana kusomba majeruhi pamoja na wale waliokuwa wamepoteza maisha , mji kuu wa Mission ulikuwa hautamaniki kila kona palionekana viungo vya binadamu , nyumba zilizokuwa nzuri ziligeuka na kuwa magofu , watoto wengi walipotezana na wazazi wao , yalikuwa machafuko makubwa sana yaliyosababisha madhara na hasara kubwa sana sio tu kwa taifa hilo hata kwa wananchi walipoteza mali zao.



    Baada ya miji kutulia ndipo mheshimiwa Robson raisi wa nchi hiyo alisikika akitoa salamu za pole kwa wananchi wake kupitia vyombo vya habari baada ya mawasiliano kurudi " kwanza napenda kutoa pole Kwa wananchi wote , Wa BUSOGA pole nyingi ziende kwa zile familia zilizoondokewa na wapendwa wao , nchi yetu sasa imejipanga na kujizatiti kwa kila kono na naahidi kitu kama hiki hakitatokea tena na mda mchache tunaenda kuwakamata wote waliofanya ukatili huu , poleni sana wanabusoga , tutajitahidi kukabiliana na magaidi hao kwa njia yeyote ile na kuwapa moyo zaidi ndani ya siku saba tutakuwa tumewatia mkononi endeleeni na kazi kama kawaida kuanzia mda huu hakuna tena kitu kibaya kitakachotokea, alimaliza hotuba fupi .

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Robson Kamega alikuwa rais wa nchi ya BUSOGA japokuwa alikuwa na madaraka makubwa ya kuongoza nchi yake lakini cheo hiko kilikuwa kama kivuli cha kufanyia maovu yake , alikuwa muuzaji mkubwa wa madawa ya kulevya , pili alikuwa akitembea na watoto wadogo sana na baada ya kuwapa mimba aliwalazimisha kutoa ukikataa tu kifo ni harali yako , alikuwa na vituo mbalimbali vya wanawake Kwa wanaume waliokuwa wakichezeshwa move za ngono na kuuzwa nje ya nchi hata baadhi ya wasichana walikuwa wakitekwa na kuuzwa nje za nchi , japo baadhi ya raia walikuwa wakilifahamu hilo lakini hakuna aliedhubutu kufungua mdomo wake wakihofia maisha maisha.

    ******

    Baada ya Rambo kutoka hofisini kwake akiwa na hasira na jaziba zisizo elezeka alichukua pikipiki iliyompeleka moja kwa moja JAWITA HOTELI iliyopo katika ya mji huo wa mission akiwa ndani ya hotel hiyo alimpigia simu Jesca kwa kigezo cha kumpatia nusu ya malipo Kwa kazi yake yaliyokuwa yamesalia katika yake ya kutoa siri na ratiba ya ujio wa raisi huyo .

    Jesca alikuwa ameingia mkataba na kundi la kigaidi la Ali- kida kwa malipo ya dola million 15 ili amsaliti raisi huyo , na Kwa upande wake lilikuwa ni swala jepesi sana maana alikuwa akijua ujio wa raisi huyo kutokana na cheo alichokua nacho , hata mda aliufaham hivyo magaidi hao walifika uwaja wa ndege saa moja kabla.



    Jesca alikuwa na hamu sana na pesa hizo hivyo alitoka hofisi kwake mbio mbio hadi hotelini hapo , aliegesha gari lake aina ya Nadia katika maegesho maalum " hello mpenzi habari yako , kuna mgeni wangu chumba namba 240" teyari alikuwa amefika mapozi na kupokelewa na sura nzuri ya dada aliekuwa akitabasamu

    " oooh nzuri !," yule Dada alijibu huku akiangalia majina ya wageni waliofika siku hiyo " ooooh yaaa Mr Jakobo ?"

    " mmmmh !!!!?" alisitika kidogo baada ya kutajiwa jina hilo lakini alijikuta akikubali maana alijua huenda ni vijana Wa Rambo " yaaa ndio huyo huyo " alijibu huku akianza kuondoka eneo hilo maana hakiri yake ilikuwa ikiziwazia dora million saba na nusu na teyari zilikuwa zimeshaanza kufanya mipango lukuki ndani ya ubongo wake .



    " madom ! je unapafahamu?"

    " hapana !" alisimama kidogo " floo ya pili kata kushoto kwako" hata kabla ya maelezo hayo kumalizika alikuwa teyar ameshaondoka " mmmh !!! hizo sio haraka daaah!" alijiongelesha peke yake Dada wa mapokezi " mmmh chumba ndo hiki " alisema Jesca na kuanza kugonga , Rambo aliekuwa amejilaza chali akiongea na bastora yake huku machozi yakimtoka alinyanyuka haraka na kuuendea mlango alishika kitasa huku mkono uliokuwa na bastora ukitetemeka kwa hasira sana.

    *****

    " hello bwana mkubwa uko salama !?" ulikuwa ni ujumbe mfupi wa simu ulioingia katika simu ya mheshimiwa Robson raisi Wa nchi ya Busoga , bila kuchelewa aliondoka eneo hilo alilokuwa na viongozi kadhaa , alijifanya kama anaenda msalani lakini lengo lake halikuwa hilo " nipe habari bwana Mdogo ?"

    " tafuta sababu yeyote itakayokufanya usifike uwaja wa ndege wa JISANGU tutakuwa hapo !"

    Japo aliingia humo hakuwa na lengo la kujisaidia alijikuta haja kubwa ikimbana na tumbo kuanza kumuuma vibaya .



    Rambo aliuendea mlango ule kwa tahadhali sana huku kifua chake kikizidi kujaa hasira na macho yakisaidia hasira hiyo kwa kutoa maji yaliyochanganyikana na chumvi nayo yakapewa jina la machoji , japo jochi la mwanaume ni adimu sana kuliona lakini la Rambo lilionekana , alinyonga kitasa huku akiufuata mlango ulikokuwa unaelekea na kumuacha mngeni wake kuingia kabisa ndani

    " bro stop joking niko na haraka , tumalizane fasta ili kila mtu afanye chake" Jesca aliongea hayo baada ya kuingia ndani na kumkosa mwenyeji wake akiwa bado ameganda katikati ya chumba alistukia akikabwa shingo yake kwa nguvu huku mdomo wa bastora ukiwa umewekwa sawasawa na kichwa chake " Nieleze kwa nini ulinindanganya " alisema Rambo huku akiendelea kutetemeka kwa hasira kali sana " we can talk mr( tunaweza tukaongea. bwana)" alijibu huku akitetemeka sana

    " sina mda wa kuzungumza tena " Rambo hakutaka kufanya ujinga wowote maana alimjua fika Jesca kuwa ni moja wa magaidi na makomado hatali kulegea kwake kungeweza kuibadili story .



    " usiniue niache nikuelezee " aliendelea kujitete ili tu aachwe hai

    " mie sipendi mtu acheze na maisha yangu , tulikupenda sana lakini hii imekupenda zaidi , wasalimie wote " alitamka maneno hayo Kwa uchukungu huku akiyasindikiza na risasi sita ndani ya kichwa cha mwanamke huyo , alimsukumia kitandani kisha aliibusu bastora yake " thanks my friend( asante Rafiki)" aliondoka humo huku akiuacha mlango wazi alifanya hivyo ili watu waweze kutambua mapema maana bastora yake ilikuwa ya kimya kimya.

    Dakika tatu baada ya tukio hilo alipita mhudumu aliekuwa akipeleka vinywaji chumba jirani alijikuta akidondosha sinia la vinywaji baada ya kumuona mtu alipasuliwa vibaya kichwa chake huku damu zikitapakaa ndani humo , alipinga kelele zilizosababisha watu kujaa eneo hilo .Uongozi wa hotel hiyo ulitoa taarifa polisi ndani ya dakika saba zaidi ya denffender tatu zilifika hapo ,haraka hataka askari wale waliingia ndani na kuanza kuchunguza huku wengine wakimhoji Dada aliekuwa mapokezi baada ya kila kitu kuwa sawa waliondoka eneo hilo wakiwa na mwili wa Jesca pamoja na Dada Wa mapokezi Kwa maelezo zaidi



    Mda mfupi taarifa za kuuawa kwa naibu Wa waziri wa ulizi na usalama mheshimiwa Jesca Japhet zilisikika kupitia radio ya taifa alimalufu kama BSG F.M, pamoja na radio mbalimbali .Ilikuwa ni habari ya kusikitisha sana Kwa taifa hilo , hivyo siku hiyo kukawa na matukio mengi zaidi .



    *****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mheshimiwa Robson Kamega alitoka msalani humo huku miguu ikiwa haikanyangi vizuri chini kutokana na kutetemeka kwa woga , kila mala alikuwa akigeuka nyuma kuangalia kama kulikuwa na adui , alirudi chumbani humo huku moyo ukimwenda mbio , " safari yangu haitawezekana kuelekea mission nimepata dharula ya ghafla sana hivyo nitashukia bulogwa na ninyi mtaenda na ndenge yangu hadi mission" alitoa maelezo hayo huku akijiandaa kwa safari kwani mda wa kuwa katika kikao cha asubuhi hiyo ulikuwa umekisha , japo baadhi ya wakuu wa nchi walishitushwa na taarifa hiyo lakini hawakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana na maneno ya kiongozi wao ,kutokana na kuchanganyikiwa alijikuta akisahau hata kutoa taarifa nchini mwake hivyo akawa amewapa nafasi magaidi hao kutekeleza adhima yao .



    Ndivyo ilivyokuwa baada ya ndege zote kutua uwanja wa jisangu magaidi nao walikuepo hivyo walikuwa wakiona kila kitu kilichokuwa uwajani hapo na baada ya kujihakikisha kuwa raisi hakuepo hasira iliwaka sana kwa Rambo aliekuwa eneo la mbali kidogo hivyo aliamuru waanze kupiga kila sehemu iliyohusika na mambo ya serikali ili tu kuiponesha hasira yake ,na mwisho kabisa alimalizia ikulu kwa mkono wake, hakujua kama aliefanya mpango huo Wa kuvujisha siri yake ni mmoja wa vijana wake tena aliekua akimuamini kupita maelezo si mwingine alikuwa Carlos , Carlos nae alikuwa dumila kuwili kama ilivyokuwa Kwa Jesca aliekuwa akila huku na huku na matokeo yake yakawa yeye kuuliwa .



    Alikaa bulogwa humo hadi hali ilipotulia mjini mission ndipo alipoamua kulejea tena baada ya kupewa taarifa ya usalama na Carlos

    " hivi huyu anaweza akapambana na mimi kweli amri jeshi mkuu na isitoshe ni kitoto cha chokora sasa naenda kukimaliza Kwa mkono wangu , nikizembea kitaniharibia sifa zangu , Rambo!!, Rambo !!! " alikuwa Robson raisi wa nchi hiyo akiongea peke yake ndani ya chumba cha siri huku akiwa ameinamia chupa ya konyangi na pembeni pakiwa na zaidi ya chupa za vilevi mbalimbali,.

    Hakutaka kuwa na mazungumzo siku hivyo alikuwa akipanga namna ya kumkamata Rambo.-





    baada ya Rambo kutoka hotelini humo alielekea moja kwa moja kijijini kwao mwalusangu " mama najua hupendi Mimi kufanya haya ninayoyafanya na ulikuwa ukinikataza kulipiza kisasi Kwa yeyote lakini kwa haya siwezi ," alikuwa Rambo akizungumza juu ya kaburi la mama yake Theopista aliekuwa amefariki dunia zaidi ya miaka kumi na tisa huku kichwa chake kikiwa kimelala juu ya kaburi hilo, machozi yalikuwa yakitiririka taratibu kutoka machoni na kuchora barabara nyingi usoni mwa Rambo na kufanya magari ya hudhuni kupita kwenye barabara hizo , akiwa hapo alijikuta akumbuka miaka mingi iliyopita.



    Ilikuwa imepita miaka kumi na tano tangu Rambo azaliwe, maisha yake na mama yake alikuwa magumu sana na ya taabu sana, siku hiyo alikuwa amekaa chini ya mti alikaa hapo kutokana na kuzidiwa na ukali wa jua , hakuwa amekula chochote toka jana yake na mchana huo hakuwa akijua namna ya kupata chakula , mfukoni hakuwa na chochote zaidi ya bisibisi , kisu na kiwembe , huku siku tano zilikuwa zimepita bila kusalimiwa na maji katika mwili wake, nguo alizokuwa amevaa zilikuwa hazitambuliki lini zilikuwa zimefuliwa mala ya mwisho hivyo zilifanya rangi yake ya asili kutokutambulika kutokana na uchafu uliokuwa umekithili.

    aliiruhusu hakiri yake kumrudisha kijijini kwao mwalusangu , alimuona jinsi marehemu mama yake alivyokuwa akimpenda , akimjali, akimthamini kupita maelezo , hasira zake zilizidi kuongezeka baada ya kukumbuka maongezi ya siku moja akiwa na mama yake.



    Siku hiyo Rambo alikuwa na furaha sana baada ya kupata zawadi toka shule baada ya kufanya vizuri katika mtihani wake wa mwisho wa kutoka darasa la nne " aaaaah!!! mwanangu hata siamini umefanya vizuri sana umekuwa wa pili"

    " ndio mama na mwaka ujao lazima niwe wa kwanza na nitasoma sana hadi niwe mbunge kama Robson" aliongea Rambo huku akitoa tabasamu la kitoto na kufanya uso wake upendeze kwa vishimo vilivyojichora mashavuni mwake.

    " kweli mwanangu" Theopista alijibu Kwa kivivu sana huku furaha yake ya mwanzo ikiondoka ghafla " hivi mama mimi sina baba!??" aliuliza Rambo huku akiwa amemkazia macho mama yake aliekuwa amelala juu ya jamvi chakavu akiuguza mguu wake .



    Theopista alimtazama mwanae kwa macho yenye maumivu na machozi ndani ya moyo wake , alitazama chini kwa mda kisha aliponyanyua uso wake alianza kwa kusema

    " nimekuwa nikiwaza kwa mda mrefu sana namna ya kuzungumza na wewe jambo hili ambalo ni maumivu na machungu ndani ya moyo wangu, ila leo sina jinsi kukueleza ukweli wa mambo yote maana nafahamu siku si nyingi nitakuwa sipo na wewe , na ningependa usipaniki ama kulipiza kisasi kwa wale walionitendea.." aalinyamaza kidogo na kumtazama usoni kisha aliendelea "baba yako yupo na ni mtu mkubwa sana hapa nchini na mwenye uwezo mzuri sana , nilipewa mimba yako nikiwa darasa la saba Kwa kulazimishwa kwani nakumbuka siku hiyo nilikuwa natoka shuleni nikakutana na watu waliokuwa wamesimama njiani walinikamata na kuniingiza ndani ya gari , waliondoka na mimi wakiwa wamenifunga kitambaa usoni , walinipeleka mbali sana na nyumbani na walipokuja kunifungua kitambaa nilijikuta nipo ndani ya jumba mbovu huku pembeni pakiwa na mwanaume aliekuwa akimbaka mtoto mdogo sana , baada ya kumaliza zoezi hilo alimtoboa macho na kumtupa pembeni CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwili wote ulikuwa ukinitetemeka Kwa woga wa hali ya juu maana nilijua kua na Mimi naenda kifanyiwa vile nililia sana lakini machozi yangu hayakuwazuia kunitendea unyama huo , yule mkubwa wao alinivuta na kunibaka bila huruma baadae alianza kunichana chana na viwembe mwili wote hawakuwa na haruma hata robo , pia walichukua moto na kuanza kunichoma vidole vyangu si unaona hapa ...." Theopista alimuonesha mwanae moja ya kovu lilokuwa mkononi mwake " mwanangu hutakiwi kulia " alizungumza hayo baada ya kuona machozi yakitiririka machoni Kwa Rambo ,

    " aaah! hahaha silii mama!" alisema Rambo huku akicheka cheka juu juu lakini moyoni alikuwa na maumivu sana " mmmmh ! Mama ikawaje!?"

    " sikujua kilichoendelea maana fahamu zilipolejea nilijikuta nipo polini huku nikiwa na maumivu mwili mzima na isitoshe palikuwa teyari usiku , sikujua ni wapi hapo hivyo ilinilazimu kuendelea kuwa hapo hapo hadi siku ya pili yake.



    Niliondoka eneo hilo asubuhi sana huku nikichechemea nilitembea umbali mrefu nisijue wapi naelekea ndipo nilipojikuta natokezea barabarani , haikuchukua mda mrefu alipita mwanaume aliekuwa akielekea gurioni nilizungumza nae na kumueleza wapi naishi alisikitika sana alipotambua umbali wa kutoka kijiji hicho hadi chetu lakini aliingiwa na huruma ya kunipeleka nyumbani kwetu.

    Nilifika nyumbani saa sita mchana baba aliponiona alianza kunitukana sana akinizuia nisikanyange uwaja wake na mbaya zaidi alichukua panga na kuanza kunikimbiza , japo nilikuwa nachechemea nilimzidi kukimbia kutokana na uzee wake , katika kukimbizana huko baba alijikwa na kuanguka hapo hapo akawa ametulia.



    Nilibaki nimesimama eneo nililo kuwa nimefikia wakati wa kukimbia , mwili wangu nao uliendelea kunitafuna kwa maumivu kwani ilikuwa kama nimeyachochea , sikujua kama baba alikuwa amefariki hapo hapo chini maana hata kurudi eneo hilo nilihofia kupigwa na kaka zangu , waliokuwa wameshafika eneo hilo walimnyanyua baba na kumpeleka ndani mda mfupi nilisikia kilio kikitoa ndani , kengere ya hatari iligonga kichwani kwangu mala nilimuona mdogo wangu akija eneo nililokuwa nimesima huku akilia , nilimuuliza nini kinamliza alisema eti mama nae amefariki baada ya kungundua kua baba alikuwa amefariki na kilichochangia mama kufariki ni plesha hakika yalikuwa maumivu makali sana nilijikuta nikipona ghafla.



    Nikiwa hapo nawaza na kuwazua alitokea kaka mkubwa akiwa na panga , alikuwa akija usawa wangu huku akinilaani vikari sana eti Mimi nimesababisha vifo vyao , nilikimbia sana maana nilikuwa namfahamu kaka , sikuwa na pa kwenda nilishinda naranda randa kutwa nzima huku njaa nayo ikilishambulia tumbo langu ndipo jioni shangazi aliniona alinichukua hadi kwake .

    Niliishi Kwa shangazi kama miezi mitatu nae alinifukuza kutokana na kumsumbua sana na magonjwa yaliyokuwa hayaishi nadhani yalisababishwa na mimba .Sikuwa na pa kwenda niliamua kutafuta moja ya nyumba ambayo watu walikuwa wamehama ndipo hapa hadi leo....." Theopista alikatishwa " ndo maana wanatukataza kulima hapa eeeh!" " niliishi hapa hadi nilipokuzaa wew...." Aliendelea bila kujibu swali la Rambo " namshukru mungu nilijifungua salama japo nilikuwa peke yangu..." alishindwa kujizuia alipofika hapo taswila halisi ililejea upya mateso yote yalilejea upya

    " nyamaza mama " aliongea Rambo Kwa upole huku akimfuta machozi kwa mkono wake wa kulia.

    " je ndugu zako wapo??aliuza Rambo huku nae machozi yakichungulia nje " ndio wapo ila hawataki kuniona na wala wewe wanadai Mimi ndie chanzo cha wao kuwa yatima katika kipindi walichokuwa hawatarajii". Rambo aliuma meno Kwa hasira huku akikipiga piga kifua chake kwa hasira "Rambo mwanangu hutakiwi kuwa na hasira kiasi hicho utakuwa mtu hatari sana".

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mawazo yake yalihama eneo hilo na kumpeleka siku ambayo mama yake alizidiwa sana hali iliyosababisha Rambo kutokwenda shule " mwanangu najua Mimi nitakufa " aliongea mama yake kwa taabu sana kutokana na kuzidiwa na maumivu

    " hapana mama huwezi kufa , sasa mama ukifa nitabaki na nani!???"

    " mungu mwema atajua pa kukuweka ila ninachokuomba kuwa mtu mwema , wapende rafiki na adui , usiterekeze wanawake utakao wapa mimba "

    " mama acha kusema hivyo ". " ndio amini ninachokuambia Mimi siponi ungonjwa huu lazima uniue tu " , Theopista alizidi kuzungumza mane no makali na machungu kwa mwanae , alijua kua yanamuumiza lakini alitakiwa ayatoe tu. " kwani zile dawa hazipo !??" Rambo aliuliza huku akiwa amechanganyikiwa baada ya kumuona mama yake akianza kujigeuza geuza kitandani hapo '" zile hazina uwezo Wa kutibu TB ni panadol za kutuliza maumivu " aliongea Kwa sauti ya chini zaidi " ni...fa..tie ...maaa..khooo!!, khooo!! khoooo!.... jiii ninyweeee" safari hii hali ilikuwa imebadilika kwani maneno hayo yalichanganyikana na kikohozi kikali zaidi , Rambo hakupoteza mda alikimbia hadi mtungini na kulejea na maji , miguu yake ikiwa inatetemeka sana .



    " maaaamaaaaa!!!!" Rambo alianza kulia huku akitamka jina hilo , alipomkuta mama yake amedondoka chini huku damu kidogo zikitoka mdomoni mwake , alikitupa kikombe haraka sana kisha alimsogelea mama yake aliekuwa teyari ameshafariki alijaribu kumtingisha tingisha lakini hakuamka alilia sana tena Kwa sauti ya juu hali iliyopelekea majirani kukusanyika " jikaze Rambo wewe ni mwanaume hutakiwi kulia sana , chozi lako acha litokee ndani " alizungumza mmoja Wa majirani baada ya kumweleza ukweli Rambo " hapanaaaa namtakaa mama nitaishije Mimi , mama njooo usiniache mwenyewe , kwanini umeenda , nitakula nini , nani atanipenda tena jitokezeeee... ,nakupenda sana , njooo njoooo mama , nichukue na Mimi twende wote, nihurumie mamaaaaa!!" yalikuwa ni maneno ya uchungu sana kutoka Kwa Rambo aliekuwa akilia huku akigara gara chini, hakika yalikuwa maumivu makali sana .

    . Akawa yatima akiwa na miaka tisa tu , picha ya kumbukumbu iliendelea kufanya kazi macho yake yalishuhudia jinsi mama yake akiwekwa ndani ya kaburi hakika aliumia sana .hakuwa na sehemu ya kuishi hivyo aliondoka kijijini hapo hadi mji wa Bulogwa baadae aliingia mission mji mkuu na kuyaanza maisha ya mtaani akiwa mtoto wa miaka Tisa tu.



    " oooooooh! Oshiiiiiii! lazima nilipize kisasi " alitamka maneno hayo kisha alitoa kipisi cha sigara ndani ya suruali yake chafu alikiwasha na kupuliza moshi hewani "Theopista !Theopista !!, nakupenda sana " aliyatamka moyoni lakini alijikuta akiyatoa hadharani akiwa pale pale kivulini .



    " mpenzi mama uliniachia maagizo ya kutolipa kisasi lakini kwa hili aaah!, mama tazama ni mala sita sasa nalawitiwa mbaya zaidi na baba yangu nae amehusika katka kunifanyia hayo ,sijui kama Mimi mzima lazima niwaue wote " alinyanyuka hapo na kuanza kuondoka huku njaa ikilitafuna tumbo lake .



    Kutokana na uzuri wa sura yake Rambo alijikuta akipata shida sana baada ya kuingia mjini vijana waliokuwa wakimzidi umri walimgeuza mwanamke kila walipomkuta sehemu yenye kificho ama nyakati za usiku hakika alipata mateso sana hakukuwa na mtu wa kumsikiliza ama kumsaidia mtaani humo ubabe wako na ukorofi wako ndo njia ya kuepukana hayo , baada ya mda mrefu kupita Rambo alianza kuwa mbabe sana kutokana na kuivua sura ya woga na upole hivyo akawa anapambana nao na ili kujimalisha zaidi alikuwa akipenda kuangalia move za ngumi .

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " boss hebu cheki yule kijana anaekuja huku daaah!! kizuri hatari , macho na kila kitu "

    " kweli mfatilie nataka nikamle leo Leo tu" aliongea Robson mbuge wa mwalusangu akiwa ndani ya cassino , tamaa yake ilikuwa teyari imeshawaka japo alikuwa na hadhi kubwa sana selikarini lakini tabia yake ya kubaka watoto wadogo na kuwalawiti watoto wa kiume hakuiacha .

    " oyaa! dogo mambo !"

    " poa nikusaidie nini??" alijibu Rambo huku akiwa anaendelea na safari yake " simama basi " " toa us*** ge " neno hilo lilichochea hasira za wapambe wa Robson walimkamata kwa nguvu na kumpakia ndani ya gari lao aina ya NISSAN na kuondoka nae , nusu saa baadae Robson nae aliondoka eneo hilo akiwafuata wapambe wake , hakuwa na mda wa kupoteza baada ya kufika eneo hilo alimfanyia uchafu huo bila huruma kisha akawaamuru vijana wake nao wamfanyie na kumuua kabisa ili kupoteza ushahidi.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog