Simulizi : Jela Ni Haki Yangu
Sehemu Ya Pili (2)
" huyu hatapona hakuna haja ya kumtoboa macho tumtupe huku huku ataliwa na fisi" wazo hilo likawa limepitishwa Rambo akawa ametupwa polini , alikuja kuzinduka siku tatu akiwa kitandani hakujua yuko wapi japo alijaribu kukumbuka lakini hakupata jawabu la maana hadi alipokuja kuelezewa na msamalia huyo .Alilia sana baada kuambiwa kuwa aliokotwa polini ." kwani hapa wapi !?"
" kijiji cha mwalusangu"
" heee!!!!huku kwetu nilishi na mama kabla hajafariki" alishangaa sana kujikuta yuko hapo " mama yako aliitwa nani ?"
" Theopista "
" mmmmh!" alishusha pumzi ndefu na kutulia kwnza huku akimtazama Rambo kwa makini kisha aliendelea " mama yako alikuwa mtoto Wa kaka yangu Mimi ni shangazi yake"
" okay sawa nashukru kukufahamu " alimjibu huku akiwa hana amani na furaha tena aliyakumbuka maneno ya mama yake ya kuwa hata ndugu zake walikuwa hawampendi aliumia sana lakini hakuwa na jinsi ilibidi avumilie hadi atakapo pona ndo achukue uamzi
" je mama yako alikueleza kuhusu baba yako!?" " hapana"
" yaani unateseka hivi wakati baba yako yupo na tajiri sana "
" yupo wapi ?" aliuliza Kwa mshangao na furaha sana aliona tumaini la maisha sasa limelejea upya aliamini akimpata baba yake yote hayo yatakwisha
" si huyu mbuge wetu na huyu huyu aliechukua fomu ya kugombea uraisi uchanguzi ujaoo , mtafute ni mtu mzuri sana "
" heee! Robson ndo baba agu !!??, nitamtafuta nikienda mjini tena" aliongea kwa furaha sana hakujua kuwa mtu huyo ndo aliemlawiti na huyo huyo ndo alietuma watu wakamuue polini .
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wiki tatu teyari hali yake ilikuwa imetengamaa alimuaga bibi yake na kulejea mjini tena kumtafuta baba yake bahati ilikuwa yake siku hiyo hiyo aliweza kumuona baada ya kuulizia Kwa vijana wenzake , alishituka sana baada ya kumtabua kuwa huyo nae alimlawiti hakutaka hata kumsogelea zaidi ya kumtumia ujumbe kupitia Kwa rafiki yake " baba Kwa mkono wangu nakuua " maneno hayo yaliyokuwa yameandikwa katika kipande cha box yalimshitua sana Robson na kujikuta akipoteza furaha yote japo aliulizia wapi ulitoka hakupata jibu .
Huo ndo ukawa mwanzo wa uhasama wao japo Rambo alikuwa akimfahamu vyema Robson lakini Robson alikuwa hamfahamu .
*****
Aliiruhusu miguu yake impeleke kokote ipendako ila hakiri yake haikuwepo habisa , mawazo hayo yalisababisha mvurugano mkubwa katika kichwa chake " dogo!, dogo !!" sauti hiyo ndo iliyomuamsha kutoka katka lindi la mawazo bila kuitika alipiga hatua hadi alipokuwa amekaa
" niambie mtoto mzuri , umependeza kweli sura yako nzuri , macho kama yamelishwa kungu daaah ! ungekuwa mwanamke nigekusaidia hadi ukawa miss BUSOGA."
Japo yalikuwa maneno machafu sana masikioni Kwa Rambo lakini hakuwa na nguvu za kuamsha shali kutokana na njaa ya mda mrefu.
" Kanigei basi " jamaa aliongea bila kupepesa macho wala kuona aibu alizima sigara aliyokuwa akivuta Kwa kuichoma chini kisha alinyanyuka na kumsogelea Rambo
" Kwa bei gani?"
" hee Dogo siku hizi unauza !"aliuliza huku akianza kuipeleka mikono yake katika kiuno cha Rambo,Rambo hakupendezwa na hali hiyo lakini alijiona hana nguvu za kupigana japo alikuwa na dhana za mapambano " moyo kuwa mvumilivu , hasira tulia nawe hakiri fanya kazi " Rambo aliviamrisha viungo hivyo vimpe mwanga.
"Sikia mshua hapa kweupe!"
" sasa wapi !?"jamaa yule alikuwa teyari keshatekwa na shetani wa ngono " kwani huna gheto" Rambo aliuliza huku akijaribu kujinasua mikononi mwa jamaa huyo aliekuwa yuko vibaya hatari
" ninalo vipi twende"
" ndio twende" jibu hilo kutoka Kwa Rambo lilimfanya afurahi kupita maelezo , hakuamini kama alikuwa anaenda kulala na Rambo maana alikuwaga keshapewa story za Rambo kuwa ukiingia kichwa kichwa lazima akutoe meno ya mbele.
Jiani kila mtu alikuwa akiwaza ya kwake upande wa Rambo alikuwa akiwaza jinsi atakavyo mpola pesa na baadhi ya vitu , hakuwa na huruma hata kidogo kwa vijana hao, jamaa yule alikuwa akiwaza jinsi atakavyo mpa kichapo cha nguvu hadi akome kulinga na alikuwa amempania hatari ,
" Dogo karibu gheto"
"Asante " hata kabla hajamalizia kuitika vizuri uchokozi ulianza baada ya kuvuta mikupuo mitatu ya bangi ili kuamsha midadi " subili kidogo "
" aaaah!!! dogo mizenguo hiyo , midadi ishapanda kitu cha taka kula bhana" aliongea huku akianza kuvua shati kabla ya suruali
" mikono michafu wangu Chakula huwa hakinogi , kaoge kwanza nami nikaoge "
"Aaaah! dogo". " mie nipo ondoa wasi wasi mpenzi" Rambo alizidi kumlaghahi ili tu atimize lengo lake " poa kaanze ww " " okay"Rambo alielekea bafuni huku akijipongeza Kwa kuona mwanga wa mafanikio ulikuwa umeanza kuonekana " fanya fasta Mimi nikitoka tu bafuni nikute kitu cheupe "aliongea jamaa yule huku akiwa anaelekea bafuni , Rambo hakutaka kupoteza mda alianza kupekua pekua mle ndani na bahati ilikuwa yake alikutana na noti ya elfu kumi ndani ya suruali alichukua na kutokomea.
" oyaaa teyali " alilopoka baada ya kutoka bafuni " Dogo!, Dogo !" alianza kuita baada ya kumkosa Rambo , alitupa ndoo na kukimbilia suruali yake hakuamini macho baada ya kuikuta pesa yake haimo aliyokuwa ameipata Kwa njia za kumkaba mama muuza mboga mboga mchana hiyo.Alitoka ndani mle akiwa amechanganyikiwa huku akimlaani vikali Rambo na kumtolea matusi mazito.
Rambo hakutaka kupoteza mda alielekea Kwa mama ntile alikula , kisha alishuka ziwani huko alioga na kufua nguo zake , huku akifanya mazoezi magumu sana ya kunyanyua mawe na kupiga ngumi zake katika mawe hayo , baadae alingia tena mtaani kuangalia usawa wa chochote kitakachopatikana .
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Maisha ya Rambo yalikuwa ya hatari sana makazi yake yalikuwa mtaani yalikuwa ya hatari sana kuiba , kukaba na kufanya ukorofi wa aina yeyote ile roho ya huruma ilikuwa imeshatoka kutokana na matendo machafu aliyokuwa amefanyiwa Kwa mda mrefu , mikono iliyompokea kutoka kijijini ilikuwa si mikono salama iliyosababisha nae awe na roho ya kikatili unywaji pombe kali , uvutaji bangi na sigara vyote hivyo alijifunza .
Japo alikuwa kijana wa miaka kumi na tano tu hakuna kituo cha polisi ambacho hakuwahi kufikishwa kutokana na matendo yake machafu , hata polisi wenyewe walimchoka mtu akipeleka lalamiko kuhusu Rambo askari walikuwa hawashughuliki nalo .
Siku moja akiwa katika pilika pilika zake alikutana na jamaa yule aliemchukuliaga pesa yake
"Duuuh!!! afadhali dogo leo nimekudaka " sauti hiyo ilizibua ngoma za masikio ya Rambo aliekuwa makini kumfatilia dada du hivi " mse*** ge" alijisemea neno hilo moyoni baada ya kukatishwa mipango yake
":afadhali nini kama upo safi niguse nikupasue !?"
" hiii !! dogo unavimba chukua hii" teyari alikuwa amemrushia ngumi ambayo Rambo alidaka kama mpira na kumchapa teke la mbavu lililo mfanya ajikunje na kabla hajakaa vizuri alilishwa bisi bisi tatu za haraka haraka mgongoni kisha Rambo alikimbia kama umeme huku akiacha watu katika hali ya sintofahamu japo baadhi yao yalikuwa wameshaanza kupiga makelele ya muuaji huyoooo.
" Huyoooo!, huyoooo ! kamata ameuaaaa , kamata" zilikuwa ni kelele za wananchi waliokuwa wakimfukuza Rambo wengi wao walibeba siraha na hata mawe ili tu wamfikiapo Rambo wamfanye kitoweo , Rambo aliwachanganya kwa kupita vinjia vya uchochoro na kutokezea Tanesco kisha alinyosha kama anaelekea wizara ya aridhi lakini hakufika huko, alikata kushoto na kuelekea ikulu " bado huyo mbwa !, mse***ge lazima nimuoneshe ushenzi wangu" alizungumza peke yake baada ya kufika eneo la ikulu ya nchi hiyo.
" atakoma kulinga kudadadeki nina hamu naye sema tu maf*** la wenzake wanamchunga sana" alizidi kuongea peke yake huku hasira zikijaa kifuani mwake " tena kuanzia leo mimi sio mwanao adui namba moja nakuua".Akiwa bado amegada eneo hilo mala walitokea vijana wanne waliokuwa wakijulikana kama wababe wa ikulu
" oyaaa! msela mbona unashangaa sana wa kuja nini!?" aliuliza mwenzao na kuwafanya kucheka karibia wote
" nani msela acha mambo ya kike kike " aliongea huku sura yake ikianza kukuja ndita za hasira
" dogo unatujibu hivyo mbuzi kabisa !" mmoja wao alimpiga teke la kifuani ambalo Rambo alilikwepa na kugusa bega lake kisha aliruka kama mmasai aliposhuka aliwazungushia watatu mateke ya pua yaliyowafanya wadondoke chini
" heee!!! dogo mgumu!?"
"Achaneni na mimi nitawaueni bure " aliogea huku akianza kupiga hatua za kuondoka taratibu
" oyaaaa mwanangu usisepe tubonge kwanza mimi nimekukubali , kama vipi join nasi !"
" sipendi magroup Mimi jeshi la mtu mmoja na nina mipango yangu" huku akizidi kupiga hatua.
" sikia bro mimi nimekulike sana kama vipi kubali , kwanza unaitwa nani !?" alimuuliza huku akiwa amemzuia kuondoka " Rambo" alijibu kwa kifupi huku akiwa bado na hasira usoni na moyoni dhidi ya Robson na wala sio hao jamaa
" hahaha mchizi na mboge la mjina hatari duuu! kweli wewe Rambo genster tunakupa namba eti machizi!?"
" huyu mwana sasa !" hata wale waliokuwa wamezawadiwa miteke na Rambo walikuwa wakicheka .
" oyaa sisi tupo wanne kubali uwe nasi halafu wewe utakuwa master Rambo " walizidi kumbembeleza sana hadi akakubali .CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mie naitwa Dan ama Daniel , huyu Danis , victor na peter ila kuna boss wetu Mr Carlos alisafili kitambo hadi tulishamsahau " Daniel aliendelea kuongea huku wakiondoka eneo hilo , na huo ukawa mwanzo wa urafiki wao na hata Carlos alipolejea alijiunga nao na walipendekeza Rambo awe kiongozi wao japo alikuwa Mdogo , kutokana na ubabe wake , umakini na alikuwa si mwepesi wa kukata tamaa akidhamilia kitu lazima akitekeleze . Walikaa nchini kama miezi sita toka urafiki wao uanze kisha walizamia nchi jilani huko ndo walikojiunga na kundi la kigaidi la Ali- kida na hayo yalikuwa mapendekezo ya Rambo alifanya hivyo ili ajifunze mambo mengi yatakayo msaidi kulipiza kisasi , .
*********
Hakika ilikuwa kumbukumbu ndefu sana iliyomfanya Rambo kujisikia maumivu makali ndani ya moyo wake taratibu alikinyanyua kichwa chake juu ya kaburi la mama yake kisha alisimama na kupiga hatua chache "mama sijui kama tutaweza kuonana tena , yawezekana hii ikawa safari yangu ya mwisho kuja huku kama nikikamatwa baada ya kutekeleza adhima yangu ...." alinyamaza kidogo nakuelekea upande wa kichwa katika kaburi hilo aliinama na kuanza kuongea tena " usihudhunike sana nafanya haya Kwa ajili yako alikubaka na kukutupa polini , japo Mimi alinilawiti lakini hainiumi sana kilio changu na hasira kipo dhidi yako na wanawake wenzako ambao mmenyimwa sauti wacha niwatetee , nakupenda mama pumzika Kwa amani mwaaaaaaah!" yalikuwa maneno ya uchungu sana aliyoyazungumza Rambo juu ya kaburi hilo utadhani alikuwa akiongea na mtu alie hai ila aliamini yamefika .
Aliondoka eneo hilo akiwa na nguvu mpya alifungua begi lake na kutoa mzinga wa konyangi na sigara aina ya sigar na kuanza kijiburudisha huku akiendelea kutafakari nani aliemsaliti
" anaecheza na hakiri yangu hakika atanitambua tu " alizidi kuwaza akiwa ndani ya gari alilokuwa ameliiba JAWITA HOTEL baada ya kutekeleza mauaji ya Jesca naibu waziri wa ulizi na usalama " tena atakuwa ni Denis huyu ni mwoga mwoga sana " alizidi kuwaza huku akikanyaga mafuta , aliingia mission jioni sana na kuliterekeza gari hilo na kuelekea kambini .
Siku zilizidi kukatika huku serikali ya BUSOGA ikijipanga kutekereza jambo lilokuwa mbele yao , uchunguzi ulikuwa umeshakamilika kupitia kwa mpelelezi wa serikali Mr Steven ambaye alikuwa akishrikiana na waziri wa ulizi na usalama Mr Andrew akiongozwa na mheshimiwa raisi wa nchi hiyo Robson ambaye hakiri yake ilikuwa haifanyi kazi kutokana na maneno ya vitisho kutoka kwa Rambo , alichofanya baada ya kunusurika siku ile ni kuichukua familia yake nchini humo hadi nchi za nje.
" hee! hebu niambie atakuepo mda gani ili tukija tumkamate kabisa "
" juzi aliondoka kwenda Jamaica ila alisema atakuepo kesho mchana kama itawezekana mnaweza kumkamatia hata uwanja wa ndenge"
" hapana Rambo ni mtu hatari sana anaweza akachafua tena hali ya hewa na sipendi tena hilo litokee sitakuwa na hakiri za maana tena ww tupe ramani ya kufika hapo basi na nadhani kesho lazima tutekeleze hilo" .
Yalikuwa ni mazungumzo ya siri sana yaliyokuwa yakifanyika ikulu nyakati za usiku katika chumba cha siri ambacho kilikuwa hakina camera yeyote na wala mtu hovyo hovyo alikuwa haruhusiwi kuingia huma wala kugusa komeo la mlango zaidi yake , kati ya Carlos mmoja wa vijana wa Al- kida na mheshimiwa Robson raisi wa nchi ya BUSOGA .
" hii ndo ramani ambayo mtaitumia kuingia kambini" Carlos alitoa ramani ya kufika kambini kwao ambapo palikuwa polini kabisa " sehemu hii msipite kuna mabomo , huku nako yapo ila ni machache sana " alizidi kuelekeza tena Kwa kitendo hali iliyomfurahisha sana Robson na hata aliweza kupata usingizi siku hiyo akiwa teyari ameshazungumza na wizara ya ulizi .
Asubuhi ya saa tatu kulikuwa na kikao cha dharula kwa mahofisa wote , mkuu wa jeshi mheshimiwa Rodric pamoja na kamanda wa jeshi la polisi BUSOGA mheshimiwa Simon .Madhumuni ya kikao hicho kilichoitishwa na mkuu wa nchi ni kujadili namna watakavyoweza kukivamia kukivamia kikundi cha Ali- kida kilichokuwa kikiongozwa na master Rambo kijana Mdogo sana lakini alikuwa akiumiza akiri za viongozi wa nchi yake , kila mtu alifurahishwa kupata taarifa nzuri sana na walipanga siku hiyo hiyo majira ya saa kumi wavamie kambi hiyo , hivyo waliondoka sehemu hiyo wakiwa na nyuso zenye tabasamu na midomo iliyojaa vicheko , baadhi yao waliishia bar kutafuna jasho la wananchi waliokuwa wakiteseka kwa ukosefu wa huduma za muhimu zikiwemo shule , vituo vya afya ambavyo vingi vilikuwa vimebakiza majina tu bila huduma lakini hakuna aliyeyaona hayo .
********
Upande wa Al- kida ambao makazi yao yalikuwa yamehamishiwa polini katika msitu wa Igamba nje kidogo ya mji mkuu wa nchi hiyo kulikuwa na kikao maarumu na mikakati ya kuivamia tena ikulu na kuondoka na raisi kama si kumuua kabisa endapo angeleta ubishi
" nyie sikieni kuna mtu humu anacheza na hakiri yangu ," alianza kuzungumza Rambo huku akiwa amekaa juu ya meza " laiti mgejua ni kiasi gani naumia ninapomuona yule msh*** zi anaendelea kutumbua mali za wanyonge hakika nazidi kuumia sana , na huyu mjinga mwenzao anaesambaza habari zangu kwa hao ma** la nitakipasua kichwa chake mapema sana na hamtaamini nyote " aliendelea kutoa maneno ya uchungu sana , alitoa sigara na kuiwasha kisha alipuliza moshi hewani na kufanya ndani kote paenee moshi kisha aliendelea " tambueni kuwa Robson ni baba yangu mzazi na ni adui yangu namba moja ..." alinyamaza kidogo na kuwaangalia wenzake waliokuwa wameshikwa na mshangao wa ajabu kisha aliendelea
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" najua nyote mtashangaa sana kiasi cha kutaka kujua mengi ila ukweli ndo huo " Rambo aliwaeleza yote tangu upatikanaji wa mimba yake , mpaka kifo cha mama yake uchafu aliokuwa akiufanya mheshimiwa huyo na hata uuzaji wa watoto wa kike nje ya nchi , madawa ya kulevya na hata tabia yake ya kurecord mikanda ya ngono na mengi mengi aliyokuwa akiyafahamu
" hata Mimi aliniomba nimpe dada yangu duuu!"yalikuwa ni mawazo ndani ya kichwa cha Carlos hakika alianza kujilaumu Kwa usaliti wake alimuona Rambo kuwa ni mtu mbaya kutokana na kujazwa maneno na mkuu huyo lakini alipoujua ukweli nae alipandwa na hasira na kujiapiza kuwa angemuua hata kabla ya Rambo , picha ya dada yake akisurubiwa kitandani na mianaume kibao huku kamera ikifanya kazi yake na pesa ikiongezea Kwa mtu huyo aliejivika ngozi ya kondoo kumbe mbwa mwitu aliumia sana .
Wakiwa katika mazungumzo hayo walisitukia kambi yao imevamiwa na wanajeshi zaidi ya hamsini wakiwa na siraha mikononi " wote mikono juu na mtulie " wanajeshi zaidi ya kumi waliokuwa wamewazigira Kwa dharau Rambo alinyanyuka sehemu aliyokuwa amekaa na kumtwanga ngumi moja mwanajeshi mmoja iliyosababisha kutoka Kwa meno mawili.
" paaa!, paaa! , paaaa!, risasi zaidi ya tatu zilitua kifuani Kwa Rambo na kumfanya atulie tuli chin.
" msh***zi sana huyu kijana tena sijui nimpasue na kichwa chake mda huu!" alizidi kuongea na kujitapa mwanajeshi aliekuwa amempiga Rambo risasi , hawakuwa na mda wa kupoteza eneo hilo zaidi ya kuwafunga pingu magaidi hao na kuwapakiza ndani ya gari maarumu lililokuwa linafanana kama la magereza na safari ikawa imeanza kutoka polini humo huku nyoyo zao zikiwa na furaha ya ajabu , walijiona washindi sana hata taarifa zilipomfikia kiongozi wa nchi alifurahi sana na kuahidi kuongeza robo ya mishahara yao , achilia mbali mualiko wa jioni hiyo wa chakula cha usiku nyumbani kwa raisi.
" hivi lile gaidi mliliweka wapi !?" " liko huko nyuma na wenzake " yalikuwa maongezi ya wanajeshi waliokuwa wakiendesha gari lilokuwa limewapakia magaidi hao na likiwa nyuma ya magari yote .
" shiiiii!"ilikuwa sauti ya Rambo akiwatuliza wenzao waliopatwa na mshangao baada ya kumuona akinyanyuka eneo hilo huku akiwa mzima kabisa , hakuwa nà mda wa kupoteza zaidi ya kutoa bastora yake iliyokuwa imehifadhiwa kiunoni na kulipiga kufuri lilokuwa limefungwa mlangoni hapo kisha aliwamuru wote waanze kuruka , haikuwapa shida sana kutokana na mazoezi waliyokuwa wakiyafanya achilia mbali mafunzo ya kivita waliokuwa wamejifunza nchi jirani , baada ya wote kuruka Rambo alitegesha Bomu ambalo lingeweza kulipuka ndani ya dakika tano tu nae aliruka huku akiancha gari hizo zikiwa zimelimaliza poli hilo.Rambo alikuwa amevaa kifaa maarumu cha kuzuia risasi hivyo walipompiga hazikumdhuru hata kidogo.
" gari lipo wazi jamani !"zilkuwa ni sauti za watoto waliokuwa wakikatsha barabara ndo zilizowashitua wanajeshi hao waliokuwa wamestarehe bila kuelewa nini kilikuwa kimetokea ndipo walipoamua kusimamisha magari yao matatu na kulizunguka gari lilokuwa limepakiza magaidi hao huku wakiwa na siraha zao mikononi wakiwa bado wanashangaa shangaa mlipuko wa ghafla ulitokea uliosababisha wanajeshi wengi kupoteza maisha yao na wengine kupoteza viungo hakika yalikuwa maafaa makubwa sana na hiyo ikawa mala nyingine ya Al- kida kufanya maafa ndani ya nchi yao .
Kwa wale waliokuwa wamenusurika waliweza kuwasiliana na makao makuu ya polisi ya nchi hiyo pamoja na jeshini kuhitaji msaada ndani ya dakika arobaini na tatu teyari. walikuwa wameshafika hapo na kuanza kutoa msaada kisha taarifa zilisambazwa nchini kote hali iliyowastua sana wananchi achilia mbali raisi Robson aliekuwa amepata gonjwa la moyo bila kusahau plesha iliyokuwa ikipanda na kushuka , hakuwa na amani tena ya kuwa hapo hata ulizi uliokuwepo alikuwa hauamini tena
Radio ya taifa BSG f.m pamoja na radio zingine bila kusahau Television hazikuwa nyuma kutangaza habari hiyo iliyokuwa imesisimu mioyo za wakazi wa nchi hiyo . " hatuna budi kuwafatilia tena inabidi tuanze mda huu kwa kumtumia ramani hii tutaweza kuwakamata kabla ya kesho "
" hapana mkuu Mimi naona kazi hii ifanyike kesho tu asubuhi kwanza tuwasiliane na Carlos nadhani atatueleza wapi waliko " yalikuwa ni maongezi kati ya viongozi kadhaa wa serikali waliokuwa wakiongozwa na mkuu wa jeshi usiku huo huo , kweli pendekezo hilo likawa limepitishwa na kesho asubuhi sana wanajeshi 29 waliianza safari ya kuwafatilia magaidi hao huku waziri wa ulizi akiwa ametoa agizo la kufungwa kwa mipaka yote .
******
" hapa ni kurudi kambini haraka sana na kuchukua siraha zote za muhimu kisha tutokomee polini usiku huu " aliongea Rambo huku akimalizia kumkatia victor pigu Kwa kutumia bastora yake iliyokuwa na kiwabo cha kuzuia sauti " duuuh !" Danis aliishia kutoa neno hilo lilomfanya Rambo amtazame Kwa jicho Kali sana .
Kweli wote sita walilejea kambini na kubeba kila kitu walichoona cha muhimu na kuingia ndani ya gari walilokuwa wakilitumia na safari ya kutoroka nchi ikaanza mala moja .
Mbwa sita walikuwa makini sana na njia hiyo walikuwa hawakosei kutokana na mafunzo dhabiti waliokuwa wampetia ,wanajeshi nao hawakuwa nyuma ilikuwa ni patashika kila mmoja alipania kuwakamata kabla ya mwenzie wakiwa wamependeza na sare zao za jeshi , begi mgongoni zikiwa na kila aina ya siraha huku mikononi nako wakiwa wame kamatila siraha zao .
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ulikuwa ni mwendo mfupi sana kwao kutokana na mafunzo waliyokuwa wameyapitia walijikuta wameanza kuona ishara za mikanyango ya viatu vya mda mfupi hapo hapo mbwa walianza kubweka kwa fujo sana wakizunguka zunguka eneo hilo , wanajeshi wote walilala chini na kuanza kutambalia tumbo huku mkuu wa msafara akikenua meno baada ya kummuona mmoja wa magaidi akiwa amesimama umbali wa kama kilomita tatu kwa kutumia darubini ama kiona mbali ,alitoa ishara ya kujikata kata makundi huku wakisonga mbele kwa mwendo wa tahadhali sana na siraha zao zikiwa begani teyari kwa lolote .
*****
"unaweza kufanya hivyo boss" Carlos alijibu kwa kujiamini na hakuwa na woga hata chembe aliamini hata kama angeuliwa angekuwa huru maana ukweli wote aliutoa ,Rambo alimtazama carlos kwa macho yenye maswali yasiyokuwa na majibu pale chini alipokuwa amesimamia magoti huku mikono yake ikiwa hewani .
"Carlos" Rambo aliita huku sauti yake na uso ukiwa umebadilika ile hasira yake ya mwanzo ilianza kuyeyuka na roho msambaza amani na pendo ndani ya mioyo ya wanadamu akichukua nafasi yake baada ya kumuondoa roho mchafu aliekuwa ameanza kumnyemelea hayo yote yalitokea baada ya kukumbuka umuhimu wa Carlos na hata mengi waliyokuwa wameyafanya huko nyuma istoshe aliwahi kumsaidia siku moja alipotakaga kulawitiwa na kundi lilokuwa hatari sana , hakuna sababu ya kumuua kisa kosa moja
" naam boss" Carlos aliitika huku akiwa anatetemeka tetemeka japo hapo mwanzo alikuwa jasiri " nyanyuka " alisema Rambo neno hilo ambalo Carlos hakuliamini na hata wengine , alimfaham fika Rambo hakuwa mtu wa kubadili nia akiaamua ameamua ,
" nakupa kazi moja !" Rambo alisema hayo baada ya Carlos kusimama .
" ndio "
" wasiliana na huyo mwehu wako , mweleze sehemu ulipo na umwambie unataka kuzungumza nae ila mwambie aje peke yake !"
" itakuwa ngumu hawezi kuja peke yake "
" kwanini ???". Aliuliza Rambo huku akitengeneza tengeneza bastora yake " najua hatakuja peke yake ". " ndogo acha kujijibu mwenyewe hujui kama hadi dakika hii tunatafutwa na ikitokea umewaeleza itakuwa rahisi wao kujileta huku , hebu piga"
Hakuwa na maswali mengi zaidi ya kuchukua simu yake na kutafuta jina la Robson kisha akaweka simu sikioni
" Mmmmmh! hakuna mtandao eneo hili " aliongea hayo baada ya kuambiwa simu haipatikana na hata zile alama za kuonesha mtandao kwenye simu yake hazikuepo .
Wakiwa bado eneo hilo walisikia sauti za mbwa Kwa mbali haraka haraka Carlos , na peter walitoa viona mbali ( dalubini ) na kuanza kuangaza huku na huku Kwa mbali waliweza kuona kundi kubwa la wanajeshi likija usawa huokwa kasi ya ajabu
" duuuh!!!!!, wanakuja huku huku "
" waache waje wauone ush** zi wangu " hara haraka Rambo alianza kutoa mabomu na kuanza kuyapandikiza eneo hilo wakisaidiana na Daniel alikuwa bingwa wa kuyaseti kiaina " fanyeni fasta tusepe eneo hili , tuelekee mlimani tikishuka tu mlima huo tutakuwa tumeingia nchi ya Tanzania " aliongea Rambo huku akimalizia kuchomeka bomu la mwisho kisha wote walianza kuondoka eneo hilo wakiwa wanakimbia kuelekea mlimani
" Mimi ndo master Rambo , mafia mhuni na jeuri nitawaua sana , mama Cheka ukombozi wako umefika patamu " yalikuwa ni mawazo ya Rambo yakizunguka zunguka kichwani mwake alipokuwa akipanda mlima.
" master huku nako wajinga wamegadi njiani hebu cheki mwenyewe!" Carlos alimkabidhi kiona mbali Rambo " hatari ila msijari ikibidi tunaanzisha vita ya msituni au vipi ???"
" ndio ooo" wote walijibu Kwa pamoja " watanzania wakileta ujinga wa kumtetea mhuni wetu nao nawamaliza " wakiwa bado wanatafakari mala walisikia mlipuko wa maana wote walichekelea na kugonga tano za maana , nusu saa kupita waliona helkopita tano zikizunguka zunguka hewani bila kutoa sauti .
*****CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kutokana na ukaribu waliokuwa wamewaonea magaidi wa kundi la Al- kida , wanajeshi walizidisha kasi ya kusogea eneo hilo bila hata kuchukua tahadhali , kadri walivyozidi kusogea ndipo walipoingia eneo lilokuwa limepandikizwa mabomu na dakika tano wote walikuwa wamezagaa eneo hilo hatari ndipo mlipuko wa maana ulitokea baada ya mmoja wao kugusa bomu moja liloyaamsha na yote , Daniel aliyaseti kimtindindo wa kuguswa moja yote yanalipuka ,na kufanya eneo lote kuwaka moto hakuna alieweza kuonekana zaidi ya kuona moto .
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment