IMEANDIKWA NA : TATU KIONDO
*********************************************************************************
Sehemu Ya Kwanza (1)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilikuwa siku ya jumatatu majira ya asubuhi zikisikiaka sauti za ndege na wanyama kwa mbali, ikiashilia kuchomoza kwa jua na, kuanza siku nyingine tena.Kijiji cha Busale kilikuwa katika pilikapilika za hapa na pale,watu wengi walionekana wakiwa na shughuli zao za kila siku. wapo wanakweda kazini wangine mashambani kujitafutia riziki kwa mwenyezi Mungu ili kuwawezesha kupata mahitaji ya msingi waweze cha kuingiza mdomoni na familia zao. Siku hiyo nikiwa bado nimelala , nikijizoazoa na kujigeuza geuza pale kitandani kutokana na uchovu wa usingizi. Bi.Maria aliingia chumbani nilipolala na kuniamsha ili niamke na nijiandae kwa ajili ya usafi wa kinywa ili kwenda shuleni, lakini sikuamka niliona usingizi umenikolea,macho yalikuwa mazito mno hata kufumbua yalikua shida. Nikaona kabisa taabu iliyokuwa mbele yangu, kuamka kwenda shuleni kukawa kichwani mwangu,sikutaka kabisa usumbufu huo nikaendelea kulala. Bi.Maria alijitaidi kuniamsha bila mafanikio, akanitingisha tingisha wee! mpaka akachoka kwani nilikuwa nimefumba macho yangu pima wala katu sikuyafumbua,alipoona sihamki akaniacha na kuamua kuondoka zake na kuniacha niendelee kulala mpaka nitakapojisikia kuamka nitahamka, hiyo ilikuwa ndio tabia yangu kuchelewa kuamka mapema.Hata usingizi ukiwa umepaa lakini kwangu nilijifanya ninao tena nimelala fofofo ili kuepukana na bugudha nilizokuwa nazipata kutoka kwa Bi.Maria.
Siku zote nilikuwa mchelewaji kufika shuleni, hata pale Bi.Maria alipojitaidi kuniamsha kwa nguvu zake zote ili nihamke, sikuonesha dalili ya kuamka ingawa sikuwa na usingizi,nilijigeuza geuza tu kitandani mwishowe niliendelea tena kulala.Tabia hiyo ilimchosha sana Bi.Maria,akaamua kuniacha kama nilivyo nami sikuchoka katu niliendelea kuuchapa usingizi kwa raha zangu mpaka pale nitakapojisikia kuamka.Nilipata adhabu nyingi sana shuleni lakini hazikunifanya kuacha tabia yangu ya kuchelewa kuamka mapema.Nilichimba mashimo na kusaficha uwanja kila mara,hata viboko navyo vilikuwa sehemu ya maisha yangu pale shuleni lakini sikukukoma.Nilipenda sana kulala lala hivyo bila sababu ya msingi,muda mwingine niwapo darasani mwalimu afundishapo nakua napata wakati mgumu sana kwa sababu ya usingizi.Mpaka Wazazi wangu Baba na Mama wakajua mtoto wao nimejiingiza kwenye makundi yasiyofaa,wakajua kwamba nimejiingiza kwenye makundi ya uvutaji wa bangi na sigara zenye madawa ya kulevya.siku moja nikiwa nimepumzika nyumbani Mama yangu ambaye ndio Bi.Maria mwenyewe aliniuliza .
"Fred mwanangu mbona siku hizi umebadilika sana?"
"Kwanini mama nimebadilika nini?” nilijibu
"Mimi nakuuliza na wewe unaniuliza, maana yake nini? Bi.Maria alimhoji
" sio hivyo mama sijabadilika kitu"nilimjibu
" Fred mwanangu unavuta madawa nini?
" Hapana mama sijawai na wala siijui kuvuta mama"nilimjibu Bi Maria
" Kweli?
“Kweli mama!”nilimjibu
"Sasa kwanini unalala sana asubuhi una tatizo gani?”Aliniuliza
"Mi sijui mama ila nikiamka macho yanakua mazito,naona raha nikilala”nilimjibu
"Basi mwanangu! Kesho uwai kuamka!”Aliniambia
"Sawa mama"nilijibu ungawa moyoni sikuwa na uakika
" Si umeyaona pale mayai, kuku anapotaga?”Mama aliniuliza kwa kunitega
“Ndio nimeyaona mama kesho ntawaii kuamka kuliko wewe kisha utanipa mayai”
Bwana mwaipopo na Bi.maria wanaishi katika kijiji cha busale wilaya ya kyela mkoani mbeya. Nilikuwa ni mtoto pekee katika familia hiyo, wazazi wangu wananipenda sana mtoto wao.Kipindi tangu nikiwa tumboni mwa Bi.Maria,Bwana mwaipopo alimkataza mkewe kufanya kazi ngumu,kama kuchota maji kupika na kuchanja kuni kwa ajili ya mapishi.Kipindi cha ujauzito wake bi.maria kazi yake ilikuwa kulala tu mumewe ndio alikuwa msaidizi kwake.Mnamo mwaka 1989 nilizaliwa nikiwa na afya bora, wazazi wangu walinilea na kunipa matunzo mema.mpaka pale nilipotimiza umri wa miaka saba, nikaanza darasa la kwanza katika shule ya msingi kasango.Bwana mwaipopo na Bi. Maria walikuwa ni wakulima wa zao la kakao na mpunga,kwa kiasi zao la kakao limewapatia manufaa makubwa, kuweza kuwaingizia kipato cha kujikimu kimaisha ndani na nje katika familia yake.
********
Wasiojua zao la kakao ni tunda mfano papai lenye radha maridhawa, ndani ya tunda ilo kuna mbegu ndogo ndogo zenye unyevunyevu.Wakati linapoliwa tunda hilo, mbegu zake hizo uifadhiwa ndani ya mfuko laini wa plastiki kwa muda wa siku tatu,baada hapo, uhanikwa tena kwa muda wa siku tatu kisha zikikauka upelekwa sokoni kuuzwa au kiwandani kusagwa na kukobolewa kabla ya kuwa kiungo cha chai hata kama huna majani ya chai basi utumia kakao kupata radha ya chai. Bwana mwaipopo na familia yake wanapendelea kulima sana zao hilo kutokana na kuwaongezea kipato kikubwa cha kijikimu kimaisha.
********
Siku moja majira ya asubuhi nikiwa bado nimelala Kama kawaida yangu, Nlishtuka gafla na kujizozoa kitandani kisha nikatoka nje huku nikinesa nesa na kumuita Mama, lakini sikuitikiwa niliendelea kumuita bila kuitikiwa, nilielekea chumbani kwake pia sikumuona,nikatoka chumbani kwake huku nikiongea peke yangu.niliendelea kuita bila mafanikio.Nilitoka nje na kuelekea msalani,nilichukua kopo lililokuwa pale sebuleni na kumimina maji kisha nikatoka na kufuata mswaki wangu uliokuwa juu ya ukuta wa choo hicho chakavu.Niliufikia na kuchukua kisha kuweka dawa ya meno aina ya witdent na kuingiza mdomoni.Nilisugua meno yangu, huku moyoni nikiwa na mashaka na wazazi wangu,baada ya muda nilimaliza kujisafisha kisha na kujiandaa kisha kuchukua begi kuelekea shuleni.Kabla sijatoka nilikumbuka ,Mama anapokwenda sehemu uwaga anananiachia ujumbe wa maandishi kwenye kalatasi, nilikurudi ndani moja kwa moja mpaka sebuleni,nikalifuata kabati la vyombo na pembeni yake kulikua na kimeza chakavu sana juu yake kukiwa na redio ndogo aina ya jock kutoka china. macho yangu yaliona kikalatasi juu ya redio alichukua na kuanza kusoma maneno machache yaliyokuwa yameandikwa na Mama.Kalatasi hile ilisomeka hivi "habari za kuamka mwanangu? Nategemea umeamka salama sisi wazazi wako tumekenda shamba, nimekuamsha hukuamka Kama kawaida yako nikaamua kukuacha, na kukuandikia ujumbe huu ili utakapoamka usipate shida kututafuta.Uamkapo nenda shuleni salama salmini mwanangu nakupenda sana baba angu" Nilisoma mara mbili mbili kalatasi hiyo kisha nilipoona inatosha nilimalizia kusoma na nikakiacha kile kikalatasi pale pale juu ya meza hiyo na kuelekea shuleni. Nilikimbilia shuleni kwa kasi ya ajabu, nikijua fika kama muda umekwenda nikiwa nimechelewa sana, kama robo saa nilifika shule na kuendelea na masomo.siku hiyo nilimkuta mwalimu mkali sate kupita wote..........
Shule ya msingi kasango ni shule ya miaka mingi yenye walimu wachache, walimu wengi wameama wengine kuacha kazi sababu ya ubovu wa miundominu na mazingira ya shule hiyo. Vyumba vya majengo ya madarasa katika shule hiyo vilikiwa chakavu tena sana, ata baadhi ya vipande vya bati kutoka juu ya paa umomonyoka na kuanguka ndani ya madarasa hayo.Kipindi cha mvua wanafunzi pamoja na walimu wao upata shida pale wanapomwagikiwa na maji ya mvua na kulowana chapa chapa bila kuwa na sehemu ya kujikinga na hadha hiyo. Ndani ya madarasa hayo hakukuwa na madawati wala meza kwa ajiri ya kuwafanya wanafunzi kukaa na kusoma vizuri.Tangu kuanzishwa kwa shule hiyo miaka ya nyuma kulikuwa na uhaba wa madawati mpaka sasa kuwafanya wanafunzi wengi kukaa chini na wengine kukalia mawe.
*******CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilipofika shuleni niliingia moja kwa moja darasani, nikakaa juu ya kipande cha mbao chakavu, maana siku zote ndipo nilipokuwa anakaa. Wakati naingia darasani kuna mwalimu pale nje aliliniona nilipokuwa naingia, lakini Mimi sikumwona wala kujua kama kuna mwalimu aliyekuwa ananiangalia,kwa wakati huo sikustuka wala kuweweseka kama mwalimu huyo aliniona.Kipindi nikiwa nipo darasani zilipita kama dakika tano mbele akaonekana msichana mrefu, mweupe kidogo, Mwenye macho ya makubwa ya ulegevu si mwingine huyu ni mwalimu Irene, kabila lake mchaga aliyezaliwa na kukulia marangu mkoani Moshi.Mwalimu huyu alikuwa macheshi hasiyeishiwa na tabasamu muda wote yeye alionekana mwenye furaha,ukimuona amekasilika ujue kuna jambo baya sanaalilofanyiwa. Yupo mbeya kwa ajiri ya kazi ya uwalimu,kufundisha katika shule ya msingi kasango, mwalimu Irene ni mama wa mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Nemes.Wanafunzi wengi wanampenda Mwalimu Irene kutokana na ukaribu,ucheshi na huruma kupita maelezo,hata hivyo Mwalimu Irene hakuonesha kujali kama alikuwa akiishi katika mazingira mabaya shuleni hapo.Nyumba walizokuwa wakiishi zilikuwa mbovu kiasi kwamba hata ukimkaribisha mgeni ndani ataomba atoke nje maana juu kulikuwa na mapopo na buibui katika makazi yao.Hivyo waliamua kutafuta vyumba nje ya shule na kufanikiwa kupata katikati ya makazi ya watu hivyo waliamisha vitu vyao na kuanzisha makazi mapya huo ukawa unafuu kwao.
Kipindi naingia darasani nilikuta ubao karibia wote ukiwa umeenea maandishi, mwalimu Irene alikuwa amekwishafundisha kipindi kilichopita, ndio maana nilipoingi tu darasani nikawakuta wenzangu wakiwa wanaandika, sikutaka kuwauliza maana nilikuwa nimeshapata uwakika kwa kile nilichokiona ubaoni. Tangu nilipoingia darasani hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyeniogelesha ingawa nina marafiki wengi darasani humo, hata mwenyewe sikudhubutu kuufungua mdomo wangu kumuuliza wala kumuongelesha mwanafunzi mwenzangu yeyote yule.Kuhusu suala la mwalimu Irene kuingia darasani na kufundisha nilikuwa na uhakika nalo kwa asilimia mia moja, maana nilikuwa nimeshapata ushahidi kwa mwandiko uliokuwepo ubaoni ulikuwa ni wa kwake .Nilichokifanya kwa wakati huo nilichukua daftari langu la sayansi na kuanza kuandika kilichopo ubaoni.Niliandika kwa haraka haraka maana muda ulikuwa umeshakwenda na kipindi cha somo la sayansi ambapo mhusika ni Mwalimu Irene ulikuwa umekwisha .Baada ya dakika kama saba kupita nilikuwa nimeshamaliza kuandika kazi iliyokuwa ubaoni,sasa nikawa nacheza na wenzangu darasani ghafla mwalimu Irene aliingia, ndio alikuwa mwalimu wangu wa darasa la tatu. Siku zote kama ilivyozoeleka Mwalimu wa darasa ufuatilia maudhulio ya wanafunzi wake, kwangu mimi alikuwa ameshanizoe kwa uchelewaji wangu wa kufika shuleni, naweza siku nisifike kabisa lakini alijua na kunionya au kinipa adhabu.
Kipindi naingia darasani nilikuta ubao karibia wote ukiwa umeenea maandishi, mwalimu Irene alikuwa amekwishafundisha kipindi kilichopita, ndio maana nilipoingi tu darasani nikawakuta wenzangu wakiwa wanaandika, sikutaka kuwauliza maana nilikuwa nimeshapata uwakika kwa kile nilichokiona ubaoni. Tangu nilipoingia darasani hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyeniogelesha ingawa nina marafiki wengi darasani humo, hata mwenyewe sikudhubutu kuufungua mdomo wangu kumuuliza wala kumuongelesha mwanafunzi mwenzangu yeyote yule.Kuhusu suala la mwalimu Irene kuingia darasani na kufundisha nilikuwa na uhakika nalo kwa asilimia mia moja, maana nilikuwa nimeshapata ushahidi kwa mwandiko uliokuwepo ubaoni ulikuwa ni wa kwake .Nilichokifanya kwa wakati huo nilichukua daftari langu la sayansi na kuanza kuandika kilichopo ubaoni.Niliandika kwa haraka haraka maana muda ulikuwa umeshakwenda na kipindi cha somo la sayansi ambapo mhusika ni Mwalimu Irene ulikuwa umekwisha .Baada ya dakika kama saba kupita nilikuwa nimeshamaliza kuandika kazi iliyokuwa ubaoni,sasa nikawa nacheza na wenzangu darasani ghafla mwalimu Irene aliingia, ndio alikuwa mwalimu wangu wa darasa la tatu. Siku zote kama ilivyozoeleka Mwalimu wa darasa ufuatilia maudhulio ya wanafunzi wake, kwangu mimi alikuwa ameshanizoe kwa uchelewaji wangu wa kufika shuleni, naweza siku nisifike kabisa lakini alijua na kunionya au kinipa adhabu.
“Fred una matatizo gani?”Mwalimu Irene aliniuliza baada ya kuingia ofisini
“Hapana Mwalimu sina tatizo lolote”nimlimjibu
“Mbona unalia sasa?”Mwalimu Irene alizidi kuhoji
“Hamna kitu mwalimu! “Nilimjibu
“Kama hutaki kuniambia kinachokuliza, nakupa adhabu sasa”Mwalimu Irene aliniambia
Sikujibu badala yake niliendelea kulia tena safari hii kwa sauti kubwa. baadhi ya waalimu waliokuwepo ofisini mle waliacha kazi zao na kuniangalia kwa mshangao.Sikujali macho yao wala kejeli kutoka kwa walimu hao, nilichokuwa akilini mwangu kwa wakati huo ni adhabu iliyokuwepo mbele yangu, mwalimu Irene anataka kunipa adhabu kwa kosa gani?nilijiuliza,kulia ndio kumemfanya mpaka kuniadhibu,haiwezekani. Niliendelea kumwangalia kwa macho yenye kuomba msamaha.mwalimu Irene alinisogelea kisha akaniambia,
“Nakupa adhabu kwa makosa yafuatayo”Mwalimu Irene alisema
“Nisamehe mwalimu”niliomba msamaha huku nikipiga magoti
“Kwanza umechelewa kufika shuleni,pili utaki kuniambia kinachokuliza”Mwalimu Irene alisema
“Nisamehe Mwalimu kesho sitachelewa tena”nilimjibu,
Mwalimu Irene alijikuta akinionea huruma kwa jinsi nilivyokuwa analia kwa uchungu, utadhani nimepigwa, alininyanyua pale chiki kisha akanishika mkono na kumrudisha darasani. Mwalimu Aisha na maimuna walimshangaa mwalimu Irene kwa hururma aliyokuwa nayo kwangu.walimu wale waliniona mwanafunzi nisiye na mbele wala nyuma, nisiye na utihifu wala nidhamu katika maendeleo yangu.walinichukia sana walio hao, ila tofauti kwa mwalimu Irene, yeye alinipenda sana kutokana na matatizo ya familia yangu,hali duni tuliyokuwa nayo.
Mwalimu Irene alikuwa kipenzi cha kila Mwanafunzi pale shuleni,wengi wao wenye matatizo kama yangu walimpenda pia, kutokana na ukalimu na busara zake viliwasaidia wengi.Hakuwa mchoyo wa fadhila umsaidia kila mtu anapoitaji msaada kutoka kwake,alikuwa ni mwalimu mwenye cheo kizuri shuleni.Kitendo cha mwalimu Irene kuwa na cheo kazini iliwapa wivu na majungu waalimu wenzake, kati ya walimu hao ni Mwalimu Aisha na Mwalimu Maimuna ndio waliokuwa na chuki za ajabu ajabu na kumfanyia visa vya wazi.Walimu hawa hawakupenda kumuona mwalimu Irene akiwa Mwalimu Mkuu Msaidiziaki,waliona Mwalimu Irene amependelewa kupewa heshima hiyo.Sababu wao ndio waliotangulia kufanya kazi katika shule hiyo,alafu Mwalimu Irene akafuatia.wakati mwalimu Irene ananirudisha darasani huku nyuma mwalimu Aisha aliubinua mdomo wake kwa kejeli ya hali ya juu kisha kumwambia mwalimu Maimuna”Yaani huyu anajishauwa Kama nini “Mwalimu Aisha alisema kwa kejeli,”Umeona hee! Sasa hapa kamletea nini huyu mwanafunzi, naona labda anatafuta kiki sioni cha maana alichokifanya, sasa alichomletea hapa kitu gani? wakati hata hiyo kossa hakuwa nalo Fred”Mwalimu Maimuna nae alidakia “Yaani ukisikia mwalimi mashauzi basi ndio huyu shoga”Heheee! Halooooo! Walicheka kwa pamoja kisha kugongeshana viganja vya mikono yao juu...........
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati walimu hao wanaonge na kutoa kejeli kwa mwalimu mwenzao, baadhi ya walimu waliokuwepo ofisini hapo walichoshwa na kashfa za walimu hao. Siku zote walikuwa na tabia ya kumsema Mwalimu Mwenzao, Mwalimu Juma aliamua kuvunja ukimya wao kwa kuwatolea uvivu na kuwaambia “nyamazeni si vizuri kumkejeli na kumsimanga Mwalimu Irene, mwenzenu hana muda na nyie lakini bado tu mnamuandana kwa vijembe, hacheni hizo!”Mwalimu Juma aliongea maneno hayo kwa hasira tena hisiyokuwa na chembe ya mzaa hata kidogo,kweli alikuwa ameshawachoka kwa bugudha zao aliona kabisa hawakupenda maendeleo ya Mwalimu Irene.
Mwalimu Aisha na Maimuna wakanyamaza na kumuangalia mwalimu Juma kwa jicho kali, lakini mwalimu Juma hakujali maana ameshawazoea hasa akitambua tabia za wanawake kuoneana wivu katika maendeleo ni jambo la kawaida kwao.Wakati mwalimu Irene anarudi ofisini mwalimu Aisha alijifanya kumshangaa kisha akajichekesha chekesha na akamwuliza kilichomtokea mwanafunzi yule mpaka akawa katika hali ile. Walimu Irene alimhadithia kisha alivuta kiti chake akaa, akaendelea na kazi. Walimu Aisha na Maimuna walikuwa na maswali kibao kutokana na kitendo kile cha Mwalimu Irene kumpeleka mwanafunzi ofisini bila kuwa na sababu maalum.Hata pale walipoendelea kumhoji,Mwalimu Irene hakutaka maongezi mengi zaidi akaamua kukaa kimya.
*******
Mwalimu Aisha na Maimuna ni marafiki wa siku nyingi tangu wakiwa chuoni, walipenda kuwa pamoja muda wote wakiwa nyambizi, club, kantini na kwengineko. Lazima utawaona wameongozana hiyo ndio desturi yao mpaka walipomaliza chuo kisha kufanikiwa kuhitimisha masomo yao na kupangiwa sehemu za kazi. Bahati nzuri walijikuta wamekutana tena kufundisha shule moja na ndio hapo Busale kwa mara ya kwanza kuanza kazi ya uwarimu katika shule hiyo..Mwalimu Aisha akiwa Mama wa mtoto mmoja wa kike mwenye miaka mitatu anayeitwa Neema, mwalimu Maimuna yeye bado hajabahatika kupata mtoto ingawa tayari ameshaolewa yapata Miaka miwili sasa ndani ya ndoa yake akiwa na mumewe Abdul.Urafiki wao ulikuwa na kustawika na ukashamili kutokana na familia yao kuwa pamoja kwa ujirani mwema .Wazaazi wao walisaidiana kwa shida na raha,hata pale watoto wao walipokuwa wamemaliza pamoja elimu ya sekondari, wazazi hao walishauriana jinsi gani watoto wao wa kike kuwaacha katika mazingira hayo.Waliongea mengi na mwishowe waliafikiana kuwapeleka chuo cha uwalimu kwa vile wote walikuwa wamepata daraja la tatu A kama taratibu za chuo cha ualimu Zinavyotaka.Chuo cha Tumaini Makumira tawi la Mbeya, hapo awali kilijulikana kama Mbeya Lutheran Teacher’s Collage ndipo walipokubaliana wazazi hao kuwapeleka watoto wao.Aisha na Maimuna walisoma katika chuo hicho kwa muda wa miaka mitatu,kupata diploma katika chuo hicho.Baada ya muda wa masomo kumalizika walirejea nyumbani ili kusubili posti zitakapotoka na kwenda kufundisha sehemu mbalimbali.Kipindi walipokuwa wanasubili majibu ya kupangiwa sehemu ya kazi,walijikuta wamepangiwa sehemu moja ya kufanyia kazi kufundisha shule ya msingi Kasango. Walifurahi sana kufuatia kwa majina yao kupangwa sehemu moja ya kufanya kazi katika shule ya msingi kasongo.Baada ya miezi mitatu majina yao kutangazwa, Aisha na Maimuna walikwenda kuripoti katika shule hiyo kisha siku iliyofuata wakaanza kazi wakiwa waalimu wa shule ya msingi kasongo.
*******
Ilikuwa majira ya asubuhi ni siku ambayo Bwana Mwaipopo na mkewe walikuwa shambani wakipanda na kupalilia kakao, wakati wakiendelea na shughuli zao, ghafla bwana mwaipopo alianguka chini huku mapovu yakimtoka mdomoni macho yakiwa juu kama mtu anayeugua kifafa. Bi.Maria alishtuka kumuona mumewe katika hali hiyo, alimwangalia mara mbilimbili pale chini, alimsogelea na kujaribu kumuamsha lakini Bwana mwaipopo hakuamka wala kupepesa macho, Bi.Maria alizidi kuchanganyikiwa, akapiga kelele za kuomba msaada, baadhi ya watu waliokuwepo eneo lile wakajitokeza kumsaidia.Huduma ya kwanza akapatiwa kuvuliwa shati alilokuwa amevaa na viatu aina ya mabuti yale wanaovaa wakulima kisha kumpepea. Baada ya huduma hiyo walimchukua na kumpeleka hospitali. Hospitali ya busale ni hospitali ya kata iliyopo maeneo ya kijiji hicho.Baada ya mwendo uliochukua nusu saa nzima, kupanda na kushusha vilima vya hapa na pale wakafika hospitali. Wahudumu na Manesi wa hospital hiyo walimpokea mgonjwa na kumlaza kwenye kitanda cha magurudumu na kumpeleka moja kwa moja mpaka chumba cha daktari.Wakati wote Bi.Maria na wasamalia wema wanatoka shambani mpaka wanafika katika hospitali hiyo hospitali, Bwana Mwaipopo alikuwa hoi bin taabani hajitambui.
Baada ya masaa kadhaa kupita, Bi.Maria na Majirani wakiendelea kusubiri ripoti kutoka kwa daktari, Bi. Maria alikuwa amekaa chini akiwa hajiwezi kwa Pressure kumpanda, machozi nayo yaliendelea kumtoka na kulowanisha uso wake ingawa hajui kilichomkumba na kilichomfanya Mumewe kuwa katika hali ile.Mawazo aliyokuwa nayo kichwani mwake hakika hayapimiki aliwaza mengi mno maana hakuwai kumuona Mumewe akiugua ugonjwa kama huo, yapata miaka sita ndani ya ndoa yao.Kipindi hicho tangu wafunge ndoa na Bwana mwaipopo hakuwai kumwambia jambo linalohusiana na ugonjwa huo uliokumba akiwa shambani, hakika ilikuwa mtihani mkubwa kwake. Baada ya nusu saa kupita Daktari alitoka ndani chumba walichokuwa wamekaa,kisha kumtaka ndugu wa karibu na mgomjwa amfuate ofisini kwake, Bi.Maria aliinuka kwenye ile sakavu alipokuwa amekaa na kumfuata Daktari, walipofika ndani ya chumba cha Daktari aliangaza macho yake huku na kule ,yakatua juu ya kitanda kilichukuwepo. Habadi moyo wake ukapiga paa! Na kuanza kudonda kwa kasi ya ajabu,alipoona juu ya kitanda hicho kukiwa hakuna mtu kama alivyodhania kuwa aingiapo atamkuta mumewe juu ya kitanda hicho lakini haikuwa hivyo alianza kuishiwa nguvu na kujizoa zoa pale alipokuwa amesimama na kukaa kwenye kiti kilichopo pembezoni mwa meza kubwa ya Daktari.Wakati Bi.Maria akiweweseka Daktari alimuona na kumuwai hasije hanguka na kumsaidia kukaa kwenye kiti huku akihema midhili ya mtu aliyekimbizwa na simba.Baada ya kukaa Daktari alimtoa wasiwasi Bi.Maria na kumtuliza ili waongee,Punde walianza mazungumzo,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Habari yako mama?”
“Salama, Bi.Maria aliitika kwa ufupi
“Mama Mgonjwa ni nani yako? Daktari alimwuliza
“Mume wangu, Bi.Maria alijibu huku akiwa na wasiwasi Daktari aliendelea kumwambia,
“Mgonjwa wako anasumbuliwa na shinikizo la damu, hivyo basi tunajitaidi juu ya uwezo wetu kuokoa maisha ya mumeo maana hali yake sio nzuri”,Daktari aliendelea
"Kwa hiyo mume wangu atapona kweli?"Bi.Maria aliuliza
"Kwa uwezo tuliokuwa nao tuna hakika atapona na kurejea kama zamani"Daktari alisema
"Nawashukuru sana kwa msaada wenu"
"Sasa naomba ukanisubili nje kisha baadae nitakuita ili nikupe haabari za hatua tuliyofikia"Daktari alisema
“Nitashukuru daktari Kama mume wangu atapona”Bi.Maria alijibu huku machozi yakimtoka
“Usijali mama, hali ya mjonjwa wako itakuwa sawa”Daktari alisema,
Bi.Maria alivyosikia hivyo alifajirika moyoni mwake,aliona sasa mumewe anaweza kurudi katika hali yake ya kawaida kama zamani. Alitoka nje na kuwaambia majirani hali ya mgonjwa inavyoendelea, walifurahi na kumtaka hasiwe na wasiwasi Bwana Mwaipopo atapona..............
Bi.Maria alikaa pembeni kusubili, huku ndani ya moyo wake akiwa na amani,ilipita kama dakika kumi bila daktari kutokea walisubili kwa muda mpaka wakachoka.Kama dakika ishirini kupita nao wakiwa wanamsubili mara kaka yake Bi.Maria alifika hospitalini hapo, Bi.Maria alipomuona alimkimbilia na Kakaye alipomuona dada yake akilia kwa uchungu alimshika begani kisha kukumbatiana.Bi.Maria aliendelea kulia tena safari hii kwa kwikwi iliyosikika kumkaba kooni kama vile alisokomezwa kitu katika koo lake jinsi lilivyokuwa likikoroma.Kaka yake alimtaka kutulia ili yeye aende kwa daktari kufuatilia anavyoendelea mgonjwa wao,alikubali kwa shingo upande na kunyamaza kisha wakakaa chini na kumsubili Daktari.
Mashaka ndio jina lake ni kijana mrefu mweusi mwenye ndevu nyingi zilizozunguka mdomo na mashavu yake, huyu ni kijana mwenye umri wa miaka therathini na tisa, ingawa muonekano wake unaweza ukafikiri ni Bwana mwenye miaka Hamsini kwa jinsi anavyojiweka na hata mavazi yake na muonekano wake kwa watu ni wa kiutu uzima. Huyu ni kaka wa Bi. Maria ambaye mimi upendelea kumwita Anko Mashaka.Katika udugu wao wamechangia Mama Baba tofauti, mwenye mke ila hakubahatika kupata mtoto hata mmoja,pia Anko Mashaka ni mfanya biashara ndogo ndogo mjini kyela.Bi.Maria na Mbwana Mashaka ni ndugu waliopendana na kushibana, kila jambo usaidiana sababu ndio ndugu pekee walioshikamana.Miaka ya sabini iliyopita wazazi wao wote wawili kupata ajari ya ndege walipokuwa safarini wakitokea mjini Mwanza. Baada ya hapo ndugu hawa wakajikuta kwenye maisha ya kutangatanga mitaani kisha baadae Mashaka alipata msaada wa rafiki wa baba yao anayeitwa Mzee Mkumbila kumpeleka kulelewa katika kituo cha watoto yatima na dada yake Maria kubaki katika familia hiyo kufanya kazi za ndani katika familia ya Mkumbila.Mwaipopo alikuwa ni mpwa wa Mkumbila hivyo kipindi hicho Maria alipokuwa anafanya kazi za ndani kwa mjomba wa Mwaipopo hivyo ilikuwa si jambo la kushangaza kwa wawili hao kukutana mara kwa mara.Maria aliendelea kusaidiwa na ukoo Mkumbila, mpaka pale David Mwaipopo alipoamua kumuoa na kumtoa mikononi mwa Mjomba wake.
*******
Baada ya kusubiri kwa muda mrefu bila daktari wala manesi kutoka katika chumba hicho,Bi.Maria akaanzaa kuingiwa na wasiwasi, akawaza na kuwazua uenda kuna jambo baya limetokea na kumkumba mumewe.Aliendelea kusubilia kwa muda huku kaka yake Mashaka akiwa pembeni yake akimbembeleza na kumfariji kwa maneno mawili matatu,lakini Bi.Maria aliendelea kunung’unika moyoni mwake .Akiwa kwenye mawazo mengi ghafla daktari alitoka katika chumba hicho,Anko Mashaka alipomuona haraka alinyanyuka pale chini na akamfuata Daktari hakumjua Anko Mashaka hivyo yeye alichofanya kumuita na kumtaka, Bi.Maria aende.Lakini kabla ajanyanyuka pale chini ili kwenda Anko alamuwai na kumwambia “Dada ngoja mimi niende wewe pumzika kwanza.Bi.Maria akakubalia kisha Kaka yake akamfuata daktari.Anko Mashaka na Daktari wakaongozana moja kwa moja mpaka chumba cha daktari,waliingia ndani sawia waliketi vitini na daktari akaanza kumwambia Anko Mashaka,
“Nadhani wewe ni ndugu wa karibu kwa mgonjwa kama sikosei?
“Kweli kabisa,”Anko Mashaka alijibuCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ni nani yako? Daktari aliuliza
“Ni shemeji yangu, Mume wa dada yangu!” Anko alijibu
“Okey, kwa bahati mbaya mgonjwa wenu hali yake sio nzuri!kwa uchunguzi wa hapa haitawezekana ”, daktaria aliendelea
“Aiyaaah! Mungu wangu, unamaana gani daktari, nini kinachomsumbua shemeji yangu?”Mashaka aliendelea kuhoji kwa mshtuko
“Tumefanya uchunguzi tukabaini mgonjwa anasumbuliwa na shinikizo la damu kitaalamu uitwa (hypertension).
“Hivyo basi mgonjwa hatoweza kuruhusiwa leo ataendelea kubaki hospitali kwa uchunguzi zaidi,
“Sawa daktari nashukuru sana kwa hilo”,
“Unaweza kuwaambia waingie tu kumuona mgonjwa”Daktari alisema
“Sawa ‘Mashaka alisikitika akatoka na kumwita dada yake ili naye aende kumuona mumewe.
Bi.Maria aliingia wodini macho yake yakiwa Pima kutazama kitandani alipolala mumewe.Alipomuona tu moyo wake ulijawa na mshtuko, hakuamini kama aliyekuwepo kitandani pale ndiye Mwaipopo kipenzi cha roho yake, mlezi wa familia yake.Bwana Mwaipopo alionekana akiwa amebadilika na kuwa rangi ya ngozi yake kuwa mweupe kama kalatasi, macho nayo yakiwa juu mithili ya mtu aombaye toba na mdomo wake ukiwa umepinda kwenda upande wa kushoto. Bi.Maria akaanza kulia akiisi miguu kumwishia nguvu,alijikaza na kumsogelea mumewe pale kitandani,alipomfikia alikumshika mkono na kubusu shavuni, Kitendo hicho alichokifanya alitegemea Mumewe angetingishika au kuamka lakini wapi Bwana Mwaipopo hakutikisika wala kupepesa macho, alikuwa ametulia vile vile kama maji mtungini.Daktari alipoona hali ya Bi.Maria ilivyobadilika na kuwa ya majonzi akaona sasa yaweza kuwa matatizo makubwa kwa mgonjwa.Bila kupoteza muda aliwataka watoke nje, Mashaka alimuona dada yake kazubaa pale kitandani na kumshikilia vilivyo mumewe, alimshika mkono kisha wote wakatoka nje.
**************
Siku iliyofiata Hali ya mgonjwa ilizidi kuwa mbaya,Daktari akashauri mgonjwa kuamishwa katika hospitali ile ya kijiji busale kwenda hospitali ya wilaya kyela kutokana kukosekana kwa vitendea kazi katika hospitali ile.ilipotimu saa kumi jioni walikamilisha taratibu zote za hospitali mgonjwa akapakiwa kwenye gari la wagonjwa na safari ya kupelekwa kyela ikaanza.ilichukua masaa mawili kufika katika hospitali hapo,mgonjwa alipokelewa kisha taratibu za matibabu ziliendelea,muda wote bi.Maria alikuwa akimlilia mumewe alikumbuka jinsi alivyomuona mara ya mwisho akiwa kama mfui,akawaza mumewe tayari ameshamuacha katika majonzi makubwa lakini moyo wake ulikataa kata kata kukubaliana na hali hiyo aliamini mumewe bado yu hai angali hajitambi.
Baada ya nusu saa Daktar alitoka chumba alicholazwa mwaipopo, Anko mashaka alimfuata kisha akamuuliza hali ya mgonjwa wake, lakini daktari hakumjibu badala yake alimtaka amfuate ofisini kwake.
“Poleni sana, ninasikitika mgonjwa wenu hatunaye tena duniani!”Daktari alisema baada ya kukaa kitini mwake
“Aisee! Nini kilichomuua hasa shemeji yangu?”Anko Mashaka alihoji huku akiwa na simanzi..............
“Mgonjwa alikuwa anasumbuliwa na shinikizo la damu ujulikana kama Pressure, ugonjwa huu wa hinikizo la damu huanishwa na namna damu inavyopiga kwenye kuta za mishipa ya damu. Kwa kawaida shinikizo la damu la mtu hupanda na kushuka kila siku, kwa baadhi ya watu hubakia juu na hapo ndipo huambiwa kuwa wana shinikizo la juu la damu”Daktari alijibu kwa ufafanuzi
“Aisee! Sasa inakuwaje mpaka mgonjwa akazidiwa kwa ugonjwa huu kupelekea kifo chake?”Anko Mashaka aliendelea kuhoji, daktari alimuangalia kisha akaendaelea
“Ugonjwa huu kwa kawaida huitwa muuaji wa kimya kimya kwa maana kuwa, mtu anaweza akawa na ugonjwa huo kwa miaka kadhaa lakini bila kujua, huku ugonjwa huo ukimletea madhara makubwa hapo baadae”
“Sasa nimepata kuelewa, maana shemeji yangu sikuwai kumuona wala kusikia akiugua ugonjwa huo hata dada pia hakuwai kuniambia kama mumewe anasumbuliwa na ugonjwa wa pressure ndio kwanza nakusikia wewe daktari!”Anko aliendelea kudadisi nae daktari akaendelea kumjuza
“Njia ya pekee ya kujua iwapo una ugonjwa huu, ni kwenda kupimwa shinikizo lako la damu. Hii ni kwa sababu shinikizo la damu lisilodhibitiwa huathiri na kuharibu moyo, macho na figo na huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa moyo na kiharusi”.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sawa, sasa nimekuelewa daktari kwa yote uliyonieleza kuhusiana na ugonjwa uliomuua shemeji yangu”Anko Mashaka alisema kisha Daktari naye akaendelea
“Shinikizo la damu au presha huonyeshwa kwa muhtasari wa vipimo viwili vya sistoli na dayastoli, ambapo tumempima marehemu. Sistoli ni kipimo cha damu kinachopima nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa ya damu wakati moyo ukidunda kwa mbali, na diyastoli ni kipimo cha damu kinachopima nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa ya damu wakati moyo umesimama kati ya mapigo ya moyo, hivyo ndio tulivyobaini kwamba mgonjwa amekata roho muda mfupi baada ya msukumo wa damu kusimama!”Daktari alisema kwa hitimisho huku akimuangalia Anko Mashaka kwa umakini.Lakini Anko Mashaka yeye alikuwa mbali kimawazo kutokana na msiba huo, alimuonea huruma sana dada yake.Baada ya muda, Anko Mashaka alitoka ofisini mwa daktari, Bi. Maria alipomuona alichanganyikiwa alimfuata Kakaye na kumtaka amwambie nini kimetokea kwani hakuwa katika hali ya kawaida lakini Anko hakudhubutu kunyanyua mdomo wake kumuambia dada yake kilichotokea, alijikaza kiume na kumtaka dada yake warudi nyumbani kuandaa chakula cha mgonjwa na maitaji mengine kwa ajiri ya siku hile.Bi.Maria alimkubalia kaka yake kwa shingo upande na safari ya kurudi ikafuata.
**********
Njia nzima Anko Mashaka alikuwa mtu mwenye mawazo mengi,msiba huo ulimchanganya kiasi kwamba,hakufahamu jinsi gani angemwambia dada yake kuhusu kifo cha mumewe.Hakujua kama Bi.Maria hangezipokea vipi taarifa hizo, zaidi kwake ulikuwa mtihani sana,uweza kusababisha mfadhaiko wa moyo kwa dada yake.Baada ya safari iliyochukua muda mfupi, hatimaye walifika nyumbani,Anko Mashaka akajikaza kiume kumkabili vilivyo dada yake,akamuelekeza na kumpeleka moja kwa moja mpaka ndani ya nyumba.Anko hakutaka kumsimulia kitu kwa wakati huo alimsogea pale kochini alipokaa dada yake na kumsihi ahache kulia badala yake alimtaka kumuombea mume wake kwa mola.Bi.Maria alimsikiliza kaka yake na mara moja akanyamaza na kutulia tuli,Anko Mashaka alitumianafasi hiyo kumueleza dada yake ukweli wa kifo cha mumewe.
“Dada yangu unajisikiaje kwa sasa?”Anko alianzisha mazungumzo
“Najisikia vizuri tu kaka, ila sina uhakika kama mume wangu atapona kweli”Bi.Maria alimwambia kakaye
“Husiwaze hivyo dada yangu isipokuwa nataka nikwambie ukweli ndugu yangu, kuhusu hali halisi ya mumeo, je uko tayari?.”Anko Mashaka alimwuliza dadaye, huku akimuangalia kwa udadisi
“Hee! Niambie kaka angu, nipo tayari”Bi.Maria alijibu akiwa tayari kumsikiliza kaka yake
“Bwana Mwaipopo hatunaye duniani! “Mashaka akamaliza kusema akainuka na kumshika bega dada yake
“Unasema! Sijakusikia vizuri kaka….. haiwezekani?”Bi.Maria alisema mfululizo
“Ni kweli dada Bwana Mwaipopo amefariki dunia!”Anko Mashaka alisisitiza
“Hapanaa……Aaaah…Jamani Mume wangu, kwanini umeniacha peke yangu nitakaa na nani mie sitawezaa kuishi bila wewe!”Bi.Maria alilia kama mtoto mdogo mikono kichwani
“Dada nyamaza kwanza, hacha kulia mshukuru mungu dada angu kwa kila jambo yeye ndio muweza wa yote “Anko Mashaka alisema kwa majonzi na kumbembeleza dada yake
Bi.Maria hakuweza kuendelea kuongea, kwikwi ilikuwa limemkaba Pima pasipo kupumua, muda huo huo akaanza kulia na machozi yakalowanisha uso wake. Hakika hakuamini kama kweli mumewe kipenzi amefariki na kumuachia pengo kubwa maishani mwake.Anko Mashaka alipata wakati mgumu kumbembeleza na kumtuliza dada yake ilikuwa pigo kubwa sana kwake kuondokewa na mume tena ndio ubavu wako siku zote mnalala na kuamka pamoja lei hii mwenzako hakuache hakika ni pigo takatifu lisilo kipimo.Majirani walisikia kulio cha Bi.Maria wakafika nyumbani kujulia kilichotokea, taharuki imewaandama hakikika hawakuamini pale Anko Mashaka alipowaambia kuhusu msiba uliotokea .wengi walilia wake kwa waume, kuomboleza msiba huo.baada ya muda taarifa zikasambaa kila kona ya kijiji cha busale, kuondokewa na shujaa Mwaipopo.Siku hiyo nyumbani kurifulika mafuriko ya watu ,ndugu jamaa na marafiki, wengi wao wakiwa wanachana wenzake, walimpenda kutokana na uongozi wake katika chama chao cha ushirika,alikuwa kiongozi aliyejiaminisha akaaminika.Bwana Mwaipopo alikuwa mwingi wa bashasha,ujasiri ucheshi na ukalimu na haiba si haba.Siku ya pili ilikuwa ni siku ya kuzishi yake, hakika watu walikuwa wengi sana kuliko siku iliopita .Bi. Maria alikuwa hajiwezi hata kunyanua mguu kusimama vyote vilimshinda. Majirani walimsaidia na kusimama ili aweze kupita mbele ya jeneza na kutoa heshima za mwisho Kwa mume wake kipenzi. Ilikuwa siku ya majonzi makubwa Kwake kuondokewa na mume ingawa bado anamuitaji.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***************
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment