Simulizi : Kisasi Ndani Ya Nafsi Yangu
Sehemu Ya Pili (2)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sijui Kama ilikuwa saa Saba au nane wakati wa mchana. Ninachokumbuka ni kwamba ulikuwa mwaka 1993 nikiwa na umri wa miaka kumi na mbili.Niliondoka shuleni baada ya kuruhusiwa kurudi nyumbani nikiwa na Musa rafiki yangu wa dhati na Dada yake Asha, njia moja kurudi nyumbani.tunaporudi nyumbani au tunapokwenda shuleni upendelea kufuatana.hiyo ilikuwa ndio desturi yetu.Wakati tukiwa njiani kitahamaki nakutana na mwanafunzi wenzangu juma, ninayesoma nae dalasa moja. Siku hiyo hakuja shuleni kwa sababu anazozijuia yeye.Aliponiona tu nilistahajabu kumuona akiwa mikono kichwani akanifuata na kunisabahi nami nikamuitika kisha kumuuliza kwema nyumbani hatoko, nae hakusita kunijulisha.akaniambia safari yake ilikuwa anakuja shuleni kunifuata, nikamuuliza shida yake naye bila hiyana akaniambia,
“Fred nimetumwa na Anko Mashaka nije nikufuate!”Aliniambia
“Kuna shida gani aliyokutuma Anko Mashaka “Nikamuuliza
“Ameniambia urudi nyumbani haraka”
“Kuna nini nyumbani? Nilimuuliza huku moyo wangu ukidunda,
“Hajaniambia kitu ila amesema ufike nyumbani sasa hivi!”juma alisisitiza sikuwa na pingamizi nae,nilitimua mbio kuwai nyumbani huku nikiwaacha Musa na Asha nyuma,wala sikuwajali, kwa wakati huo akili yangu ikiwa nyumbani.nikiwaza na kuwazua, Anko Mashaka amekuja nyumbani leo kuna nini kama amekuja kimatembezi mbona amemtuma mtu aje kunifuata, na kama kuna tatizo limetokea Juma hasingenificha.nilikimbia mpaka karibu kabisa ilipo nyumba yetu nikasimama huku nikitweta kama mwizi, kutahamaki naona watu wengi wamezunguka nyumba yetu nilipata mshtuko usio na mfano, nguvu ziliniishia pale pale.bila kujiuliza nikaingia moja kwa moja mpaka ndani, nikamkuta mama analia, nami nikaanza kulia pasipo kujua kinachomliza mama. Anko Mashaka alikuja kunichukua na kunipeleka chumba cha pili.nikajikuta namuuliza kilichotokea pale nyumbani anko Mashaka akaniambia kilichotokea.niliumia niligafirika kumpoteza Baba yangu Kipenzi Mzee Mwaipopo .Nilikuwa nimesikia mara nyingi kuhusu kitu hiki kiitwacho kifo hasa redioni na runinga ilipotangazwa kwenye matangazo ya vifo ,twasikitika kutangaza kifo cha furani binti furani na furani kipindi hicho ilikuwa kifo nje ya upeo na uwelewa wangu.Sikujua ilimaanisha nini maana ya kifo.
Siku mbili zikapita hatimaye ya tatu ikafika ya matanga kumaliza, ndugu na jamaa wakaanga kurudi makwao Bi.Maria alikuwa mnyonge kubaki nyumbani pekee, nilimuona kabisa mama yangu alivyobadilika lakini sikuwa na jinsi ya kumshawishi arudie hali yake ya kawaida .Anko Mashaka alibaki nyumbani takribani wiki mbili kumuangalia dada yake.ingawaje mama alizidi kudhoofika mwili ulikondeana kutokana na mawazo.Mama ali chakula akashiba,anywi akakata kiu yake,hacheki akafurahi,alikuwa kama pingili muda wote yeye kulia sijui ilikuwaje na usingizi kumpitia....
********
Nilipata wakati mgumu nikawa siendi tena shuleni, muda mwingi nashinda nyumbani nikimuhudumia Mama. Ilikuwa mtihani kwa Anko lakini hakujali alizidi kuwa karibu na nduguye .Siku zilipita wiki kukatika hatimaye mwezi ukatimia tangu Baba kuaga dunia. Sikujali tena kwenda shuleni, akili yangu kwa wakati huo ilikuwa kwa Mama yangu mpendwa Bi.Maria,sikuelewa kilichokuwa kinamsumbua Mama,nikajiuliza au kutokana na msiba wa Baba,lakini mwezi mzima bado Mama hajasahau tu?,niliwaza na kuwazua kuhusu hali aliyokuwa nayo.Hatimaye miezi miwili ikafikia,Mama akaanza kukosa nguvu akawa akionekana kama aliyeweuka huku akishindwa kufanya shughuli zake kama kawaida.Ikafikia kipindi akawa hata kunyanyuka kitandani ilishindikana haja zote umtoka pale pale, akashindwa ata kuongea.Niliumia sana moyoni, kumuona Mama yangu akiteketea na mwili wake kudhoofika kweli Mama yangu aliteketea mpaka ikawa nikimuangalia nalia,sikuelewa kitu gani kilichomsibu na kumfanya awe katika hali hiyo . Bi.Maria alikonda na kukondeana akawa ukimwangalia pale kitandani alipolala utadhani kama mtoto mchanga.Majirani wakatoa ushauri wa Mama Kupelekwa Hospitali, lakini Anko hakuafiki alikataa kata kata, akadai Dada yake amefanyiwa mambo ya kishirikina. Maamuzi akajichukulia kumpeleka Mama Kwa mganga wa jadi.
***********
Ilikuwa siku ya jumatatu tulivu majira ya saa sita mchana, nikicheza na watoto wenzangu nilimuona Anko Mashaka aliingia nyumbani,akiwa ameongozana na Mzee mmoja wa makamo.Nilijitaidi kumdadisi na kumwangalia vizuri ili kumjua Yule mgeni lakini sikumtambua hata kwa sura sikumfahamu, nikaamua kumfuata ndani niliwakuta katika chumba alicholazwa Mama, Mzee Yule alishtuka kuniona nilipoingia bila hodi, akaamaki na jaza ikamjaa Anko akamtuliza kisha kunitambulisha kwa mzee Yule anayeitwa Joazar.Nilipomdadisi vizuri Mzee Yule nikaja kumjua alikuwa mganga wa kienyeji, aliyeletwa kwa ajiri ya kumtibu Mama.Pasi na shaka kutaka kujua atamfanya nini Mama kwa utaalamu wake wa mazingaombwe .Nikajisemea moyoni lazima nijue anachokifanya mtu huyo, maana nimesikia vitu vingi wanavyofanya watu hao sasa leo najionea kwa macho yangu, tena nyumbani kwetu nilipata shauku hisiyoisha hamu.Baada ya muda nikamuona Mzee Joazari akiinuka alipokaa na kumwambia Anko Mashaka “Nipe mfuko niliokuja nao!,Anko akatii na kumkabithi mfuko wa Rambo,Mzee Joazar akaupokea kisha akatoa vitu vilivyomo ndani ya mfuko huo, nilimuona akitoa kofia nyeupe aina ya bagashia,pembe ndefu ya mnyama sikosei tembo iliyovishwa shanga nyekundu na nyeupe,msinga mweusi na nazi mbili zilizokuwa maandishi ya kiarabu.Nikapatwa na dukuduku kutaka kujua vitu hivyo amevipatia wapi ,maana vilikua vya maajabu kwangu .hakika nilipata mshangao tena hamaki ya mwaka nilikodoa macho pima kuviangalia, hasa nilivutiwa zaidi na ile pembe ndefu iliyozungushiwa shanga. Nilikumbuka kwenye runinga niliwai kumuona mtu akiipuliza kwa mdomo pembe kama filimbia akiwa mbugani, nikavutiwa nayo ile ya mganga, nilitamani nichukue kisha niijalibu lakini nikaogopa vya mganga.
Nikagutushwa kutoka katika lindi la mawazo na Mzee Joazari, akimtaka Anko amletee maji ,Anko alipofuata maji mganga Yule alinikazia macho nami sikupepesa nikamkodolea pia,nikamuona akinionyeshea kidole akinitaka kutulia,nikaitikia huku nikitikisa kichwa ishara ya kumkubalia.Anko alirudi na beseni kubwa lenye maji,Mzee Joazar akayachukua kisha akayaweka katikati ya miguu yake.Nikamsikia akianza kuongea maneno ambayo mpaka sasa siyakumbuki ,nilipata kusikia mganga akiongea uwa anaongea na majini yake, sasa sijui kama Mzee Joazari aliongea na hayo majini hama sivyo, yote sifahamu sababu ya upeo wangu mdogo.Akayangalia yale maji kisha akayachanganya na damu iliyokuwa katika kichupa kidogo alichokificha mfukoni mwake,maji yote yalichanganyika na ile damu na kuwa langi nyekundu tupu.Nilihamaki kumuona mganga akimtaka Anko ampe Mama ile damu anywe,Anko bila kusita akaipokea na kumnyweshwa, Mama akanywa yote.Nilimuona Mama ameinamisha kichwa chini, sura yake iliyokuwa na urembo wa urimbo ikaanza kupoteza mvuto, kuwa na makunyanzi usoni mwake ,ghafla nikamuona Mama amesimama nilishangaa nikajiuliza aliwezaje kusimama mwenyewe au ndio maajabu ya mganga.
Mama akawa anatembea kuelekea alipokaa mzee joazar,nikamuona akikaa chini, nilizidi kushangaa ata Anko nae sasa nilimuona akiwa amepigwa na butwaa akimuangalia dadaye .Mzee Joazar akaanza kuchakacha msinga wake na kumchapa nao Mama, nikamuona Mzee Joazar akipuliza na kuizungusha ile pembe. Hakika ilikuwa sinema ya bure, ingawa moyoni niliumia Mama yangu kufanyiwa vitendo vya kishirikina.......CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mganga Yule alipomaliza kuizungusha, aliweka ile pembe chini kisha akamlaza Mama chini akalala chali na akaanza kumchanja kwa kitumia wembe, sikujua ule wembe umetokea wapi ila nilimuona akiendelea kumchanja mguu wa kulia kisha kushoto, ubavuni wa kulia na kushoto mkono nayo vile vile akachanja, mpaka akamalizia juu ya paji la uso.Kila sehemu aliyokuwa amemchanja alimpaka dawa fulani hivi nyeusi mfano wa masizi ya mkaa.Mama alitulia tuli kama vile hakuhisi maumivu ya kiwembe hicho kilichokuwa kikipita ndani ya mwili wake, Mganga alipomaliza kumuweka dawa, akamuinua na kumlaza kitandani, nilimuona Mama akianza kuweweseka na kupiga kelele kama mtu aliyepata kichaa cha ghafla. Anko Mashaka akamtuliza lakini Mama aliendelea kubadilika, machozi yakamtoka na kuwalowanisha sura yake, iliyochafuka kwa dawa alizopakwa.Anko mashaka ikabidi amuulize kilichotokea, mpaka mgonjwa akawa katika hali hiyo,Mzee joazar akamwambia amuache vile vile Mama atakaa sawa.Nilimuona mganga akiweweseka alipomuona mama katika hali ile akamfuata na kumpaka dawa Fulani hivi sikuifahamu wala kuiangalia, wakati huo akili yangu yote ilikuwa kwa mama yangu kipenzi anavyoteseka.Nilipata wazo angali umri wangu ukiwa mdogo nikamwambia Anko Mashaka nini cha kufanya kwa wakati huo ,hatukutakiwa kubaki tukimuangalia tulitakiwa kufanya kitu ili kumnusuru mama na ugonjwa huo,maana hatukujua hasa ugonjwa gani unaomsumbua.
“Sasa Anko mbona mama anakuwa hivi?” wakati huo yeye alikuwa amechanganyikiwa kuona hali ya dada yake inazidi kuwa mbaya akajibu
“Anko hata sijui imekuwaje maana simuelewi”Anko alinijibu
“Basi tumepeleke hospital angalia hali yake inazidi kuwa mbaya“nilitoa wazo langu
“Hapana msimpeleke mgonjwa atatulia na kuwa sawa tu muacheni”mganga alidakia
“Haiwezekani tumuache dada yangu akateseka ndani, wakati zahanati ipo bora tumpeleke huko”Anko akasisitiza
“Lakini mnachanganya dawa, mnajua hapa bado sijamaliza kazi yangu!”Mzee joazar alisema
“Potelea mbali Kama ujamaliza utajua wewe “Anko alimjibu kwa kejeli huku akiwa amechanganyikiwa
Baada ya mabishano hayo Anko alimbeba Mama begani kisha tukatoka nje kuelekea zahati ya busale iliyopo mita chache kutoka nyumbani kwetu, tulimuacha Mzee joazar akiwa mle chumbani wala hatukumjali.Baada ya mwendo uliotumia kama dakika kumi tulifika hospitali,wauguzi walipotuona walichukua kitanda na kumlaza Mama kisha wakaelekea kwa dakitari.ghafla nilimuona Anko akianza kulia,nilishtuka na kumuuliza kulikoni lakini akunijibu badala yake alinikumbati, machozi yakanidondoka roho ikiniuma pasi na moyo kwenda mbio. Kwa mbali sauti ya Anko ikaniingia ndani ya ngoma ya masikio yangu nikasikia akisema,
“Masikini Dada yangu” sikumuelewa anachomaanisha nikatoka niongoni mwake na kumuangalia usoni, alikuwa akilia kama mtoto nilizidi kuchanganyikiwa mawazo yangu yakakumbuka kifo.Kifo kilimchukua Baba sasa kifo hicho hicho kinampata tena Mama. Nikasikia maumivu yasiyoelezeka ndani ya moyo wangu. Nikamkumbuka mzee Joazar Yule mganga tuliyemuacha nyumbani peke yake, anaweza fanya kitu bila sisi kujua, nilimlaumu sana Anko kumleta Yule mzee nyumbani.
*******
Ilikuwa usiku wa manane tukiwa bado hospitali tukimuuguza Mama ghafla nikashtushwa na vilio vya akina mama wale waliokuwepo karibu yetu, sikuelewa kilichokuwa kinawaliza mpaka pale nilipomsikia Anko akiwaambia wanyamaze ni mipango ya mungu. Nilipomuangalia vizuri kati ya kina mama wale mmoja nikamtambua, alikuwa Mama Juma jirani yetu kama unamkumbuka Yule mwanafunzi mwenzangu aliyetumwa na Anko kunifuata shuleni, basi Yule alikuwa Mama yake.ilipatwa na shauku kutaka kujua kinachomliza Mama juma na wenzake, nikamsogelea alipokuwa amekaa. Kabla sijamfikia Anko akaniwai kunishika mkono kisha akanitoa nje ya hospitali hiyo. Nilishangaa kwa kitendo hicho, lakini sikuwa na jinsi nikafuata Anko anavyotaka tukasogea pembeni
“Fred!
“Naam Anko? Nikamuitikia huku nikimkazia macho
“Unajua kiasi gani nimechanganyikiwa”Anko aliniambia
“Najua Anko!”Nikamjibu ingawa sifahamu kilichomsibu
“Naomba unisikilize kwa makini Anko”
“Nakusikiliza Anko”
“Bi.Maria hatunaye duniani!”
“Unasemaje Anko, Sijakuelewa”nilimjibu nikiwa nimechanganyikiwa
“Ndio hivyo Fred Mama yako amefariki dunia”Anko alisema niliposikia maneno hayo kwa mara ya pili nikaisi kuchanganyikiwa. macho yalinitoka pima moyo ukienda mbio pasipo kusimama kweli nilikuwa sijielewi miguu yangu ikiwa imeishiwa nguvu nikaa chini.Wala sikujali kama kulikuwa na uchafu wa kiasi gani pale sakafuni nilikaa na kutamani kulala kabisa maana nguvu zilikuwa zimeniishi mno.hakika kifo cha mama kilinichanganya sana sikutegemea ndani ya mwezi mmoja kuwapoteza wazazi wangu wote wawili hakika ilikuwa pigo kubwa sikuelewa wala kufahamu kilichoendelea baada ya kukaa pale chini kwa mawazo lukuki.
Ilipita wiki moja tangu kumaliza msiba wa mama,nikiwa nyumbani na Anko Mashaka.muda mwingi nikiwa mtu mwenye mawazo sana mpaka nikakonda sikuwa mtu wa kujichanganya na watoto wenzangu.kutwa nzima nilikuwa nashinda ndani, Anko alinitaka nichangamke ili niondoe mawazo lakini ilishindikana sababu nilimpenda sana Mama. Nilikumbuka mapenzi yake kipindi yupo hai, alikuwa akiniamsha ili niwai shuleni leo hii nitaamshwa na nani ili niwai shule,nikafikiria na kupata jibu mwisho wa kusoma utakuwa umefika tamati.Siku ya jumatatu nikiwa nimekaa sebuleni nikifuatilia kipindi redioni Anko Mashaka alifika nyumbani na mkewe. Nilishangaa kumuuona ugeni huo, ila sikuwa na jinsi nikamkalibisha bila pingamizi.tukasalimiana kisha kunipa pole ya msiba.Nikaona haina haja ya kumuuliza Shangazi kutokufika kwake msibani, nikaona labda atakuwa na sababu zake Maalumu.Anko alifahamu ila hakutaka kusema kwa sababu zake maalum.....
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku ya Jumatano katika kijiji cha busale, upepo ulikuwa ukivuma kutoka mashariki kwenda magharibi, hivyo kufanya eneo lile la Mbeya kuwa kivutio kwa wakazi wa mkoa huo.Watu walikuwa wengi nje ya nyumba yetu, ndugu na majirani walizunguka nyumba yetu kusikiliza hatima na hitimisho ya mali za wazazi.Ilifika muda ya wakubwa kuongea kutoa amri na hatima ya familia hiyo.Baba yangu Mkubwa anayeitwa Mzee Manjale alikuwepo pia katika mkotano huo,hivyo yeye ndio alikuwa kiongozi wa mahamuzi yatayoamuliwa.Baada ya muda kidogo Kikao kikaanza na Baba Mzee Manjale akasimama na kuanza kufungua kikao hicho kwa mbwembwe huku Wazee kwa Vijana walikuwa kimya kumsikiliza atakachosema Mzee huyo.
“Habari za majumbani kwenye ndugu zangu”alisalimia
“Salama……”wote waliitikia kwa pamoja
“Napenda kuwakaribisha na nimefurahi wote kwa pamoja kufika hapa ili kuhitimisha na kuchukua maamuzi ya nani wa kuishi katika makazi haya yaliyohachwa na marehemu”
“Naam, tunakusikiliza Mzee”
“Sasa ninachoomba kuuliza aliyekuwa tayari kuishi hapa ajitokeze na kumlea Fred mpaka atakapokuwa mkubwa”Baba mkubwa alisema
“Mawazo yangu ni kwamba anatakiwa mtoto mwenyewe ndio aseme anaitaji kukaa na nani?”Kaka yangu ambaye ni mtoto wake Baba mkubwa alitoa wazo lake
“Kweli….Kweli amchague tu mwenyewe”Sauti zilisikika kutoka upande wa pili kwa watu wale
“Sawia kabisa….Sasa tunamtaka Fred asimame ili aseme anayeona ona anafaa kukaa nae amtaje ili wote tuafiki maamuzi ya mtoto”
Baadhi ya ndugu zangu upande wa mama walitoa wazo na kupendekeza Mimi nisimame ili kumchagua mtu wa kuishi nae nyumbani, Nilishangaa kidogo maana sikuwai kuona mtoto akichagua mzazi wa kuishi nae badala ya mzazi kujitolea kumchukua mtoto na kumlea.Sikutaka kuumiza kichwa changu wala kufikilia namna ya kukabiliana na macho ya watu, nilisimama huku nikitafakari namna ya kuwajibu huku moyo wangu ukienda kasi, mwili ukaanza kutetemeka utadhani mtu aliyepatwa na homa ya ghafla. Nilimwangalia Baba mkubwa ambaye nae muda huo alikuwa bado amesimama akiniangalia,nilimuona macho yake hayajatulia sehemu moja,pale alipokuwa amesimama alionekana kuwa na mawazo tele kichwani mwake.Nikaachana nae macho yangu yakaangaza sehemu nyingine na kupepesa huku na kule na kumwangalia mmoja baada ya mwingine kisha nikaona kila mtu ika kikao hicho akiniangalia kwa shauku na kuachia tabasamu pana.Nikaanza kutfungua kinywa changu na kuzungumza maneno ambayo naisi yalikuwa mkuki kwa baadhi ya watu waliokuwepo “Namchagua Anko Mashaka na nitaishi nae huku akinilea katika maisha yangu yote”Baba Mkubwa aliposikia hivyo hakulidhika na uwamuzi wangu akanitaka nijifikilie alafu nimpe jibu lililo sahihi,sikuona sababu iliyomfanya mpaka kunitaka nirudie tena kuongea tena maneno hayo.Niliamua kushikilia msimamo wangu kwamba “Nimemchagua Anko Mashaka kuendelea kuishi nae nyumbani”hata Anko Mashaka mwenyewe, akamtaka kukubaliana na suala hilo sababu tangu awali tulikuwa pamoja kabla wazazi wangu hawajafariki dunia. Nilikuwa nimemchagua Anko Mashaka bila kushawishiwa na mtu yoyote yule, maaana nilimuona ni mtu aliyekuwa na huruma na mchango na msaada mkubwa kwangu.Ni kwamba kilichonishangaza siku hiyo ni kwamba Anko Mashaka hakuwa na wasiwasi aliona dhahiri kuwa ni jambo la kheri kwake kuendelea kuishi ndani ya nyumba ya dada yake Marehemu Bi.Maria.Walipenda sana na dada yake hata pale siku ya msiba Anko mashaka alilia ns kushinda siku mbili bila kula huku akiendelea kuomboleza kifo cha dada yake mpendwa Bi.Maria. Baba Mkubwa alinisema sana alinitaka nimchague yeye lakini sikuona umuhimu wa kumchagua mtu mwingine wakati kipindi hiki ni kigumu kwangu hivyokumchagua mtu mwingine itakuwa sio sawa hata kidogo,Anko ndio nilikuwa nimemzoea.Wageni wote ndugu na jamaa waliafikiana kisha wakaniaga na kila mmoja kuondoka kuelekea majumbani mwao.nikabaki nyumbani hapo nikiwa na Kuanzia siku hiyo nikaendelea kuishi na Anko, akiwa na mkewe Bi.Zuwena ndani ya nyumba ya Baba Mwaipopo na Mama yangu Bi.Maria.
Baada ya miezi miwili kupita Anko Mashaka, aliamisha kila kitu toka nyumbani kwake kyela na kuamia Kijijini Busale, kuanza makazi mapya nyumbani. nilifurahi kuendelea kuishi pamoja na Anko,alikuwa ni msaada mkubwa sana kwangu nilimuona kama Baba yangu Mzee Mwaipopo hakika alikuwa na msaada mkubwa kwangu.kwa kuwa anko alikuwa anajuana na mwalimu Mkuu katika shule niliyokuwa nasoma,akaenda kuniombea na nikarejea shuleni,ili kuendelea na masomo nikiwa darasa la sita.Siku nilipokwenda shuleni mwalimu Irene alifurahi sana kuniona akanipa pole na kunitaka niendelee na masomo kama kawaida.Nilimshukuru Mwalimu Irene, sababu alikuwa mkalimu na mnyenyekevu kwa kila mtu,kwa kifupi hana ubaguzi umpenda kila mwanafunzi pale shuleni.Siku zote nilizokwenda shuleni sikuwaona walimu Aisha na Maimuna, nilipowauliza wanafunzi wenzangu wakaniambia wameama.mwalimu Maimuna ameamia Kyela na Mwalimu Aisha ameamia Sumbawanga.Mpaka namaliza shule,sikubahatika kuwaona tena walimu hao.....
Katika nyumba ya wazazi wangu,Niliendelea kuishi na Anko, sababu nilikuwa kama mtoto wake wa kunizaa mapenzi yake hayana mfano, japo kwa shangazi ilikuwa tofauti.Shangazi alikuwa mtu tofauti sana, alikuwa Binadamu aliyevaa ngozi ya kondoo, hakika ukimuangalia huwezi mdhania kama ana roho ya fitna na majungu,juu yangu ilivyo moyoni mwake si sawa na machoni.Kadri siku zinavyozidi kwenda nami nikazidi kuzoea tabia yake Maana iliniladhimu kuzoea sababu sijawai kuishi na watu tofautitofauti zaidi ya kukaa na familia yangu yaani Baba na Mama tu.Wazazi wangu hawakuwa na tabia ya kunizoesha kunipeleka hata kwa ndugu kutembea,si likizo ndefu wala fupi hawakunipeleka wala kutembea tu mara moja popote pale. Hata kwa Anko Mashaka nyumbani kwake sikuwai kufika zaidi ya kumuona yeye akija tu kututembelea nyumbani, nilikuwa ni mtoto wa kudeka kulala na kuamka kwa Mama, sikumjua Mama Mdogo wala Mama Mkubwa zaidi ya kuwasikia tu wakizungumziwa kwamba walikuwa mbali na mji wetu lakini hata huku walipo sikufika.
*******CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mnamo mwaka 1997 nikiwa mhitimu darasa la Saba, nilikuwa nashinda nyumbani bila kazi yoyote.visa na vitimbi vya Shangazi Zuwena, vilizidi kuniandama.sikuwa na jinsi nilipambana navyo kama mwanaume, nikiwa sasa nimekuwa, kifkra na uwelewa vilienea akilini mwangu nilijua fika shangazi ananichukuia. Hata pale mumewe alipomkanya juu yangu naye aliambulia matusi ya nguoni mbele yangu.Siku zinavyozidi kwenda taratibu nikawa naanza kumchukia Shangazi, visa vyake anavyovifanya nyumbani vilinichukiza Sana.
Siku moja majira ya saa mbili Asubuhi nikiwa nimekaa na Anko Mashaka tukiongea mambo mbali mbali, Shangazi alikuja na kunitaka niende kufanya Usafi, sikutaka kubishana nae nilinyanyuka kwenda kufanya usafi kama alivyoniambia.Nikafanya usafi nyumba nzima kisha kuosha vyombo vilivyotumiwa usiku uliopita.Ilikuwa kawaida kwangu kuzoea kufanya kazi zote bila matatizo, niliumia moyoni hasa nilipowakumbuka wazazi wangu sijawai wala kudhubutu kufanya kazi kiasi kile.Nilikuwa nalala mpaka nachelewa shuleni bila Baba wala Mama kunibugudhi.kuwa katika mateso haya ikawa mtihana mkubwa kwangu.Nikiwa nimemaliza kufanya usafi nikajumuika na Anko Sebuleni.Kama nusu saa hivi tukiwaa tunaongea, Shangazi alikuja tena safari hii alionekana kuwa na jazba.Alisema maneno makali na kashfa juu yangu,Anko akaingilia na kuanza kumshambulia kwa vibao na mateke mkewe.lakini Shangazi hakuacha kuzungumza,
“Nakuona kila siku unamtesa Fred”Anko alimkalipia,
“Wewe unapenda akae tuu hasifanye kazi?shangazi alimjibu
“Sio hakae tu huyu mtoto wa kiume angalia na jinsi kazi unazompangia,
“ kwani mtoto wa kiume hafanyi kazi? Shangazi alimwuliza kwa kejeli
“Kazi zinazomfaha ni ndogo ndogo, lakini wewe kila siku unampangia majukumu, Fred hapumziki, mara kuosha viombo, kufagia mara kudeki, hauna hata huruma wewe umekaa tu hunakazi gani ya kufanya? Anko Mashaka alifoka kwa jazba.
“Sikiliza Kama unamuonea huruma, nenda kafanye wewe”shangazi alimjibu bila woga
“Sawa,sikiliza kwanza huyu mtoto anaitaji malezi mema kwa sababu yeye ni yatima, tambua mali zote ni za kwake, sisi tunaishi hapa kwa msaada wake,hivyo mpende na umlee vizuri kwa mapenzi mema mke wangu" Anko alimsisitiza
“Weee! Ishia hapo hapo hakuna cha Mali zake wala nini,mimi ndio mwenyewe hapa nimeshafika,”shangazi alisema kwa kujiamini
Muda wote wanagombana nilikuwa kimya kuwasikiliza kwa makini.Nilishanga sana kwa kauli ya Shangazi kusema kwamba sina cha mali wala nini,kauli hii ilinishangaza anamaana gani kusema maneno hayo.Sikuona umuhimu wa kuendelea kubaki pale sebuleni nilitoka na kuelekea chumbani kwangu nikajilaza kitandani huku moyo ukinienda kasi.Nilijifikiria nikawaza na kuwazua mpaka kichwa kuniuma lakini sikupata jibu, nikabaki nalia kwa uchungu kumbukumbu zikanijia kichwa kikajaa tele mawazo,wakati nikiwa na wazazi wangu sikuwai kugombezwa wala kufanyishwa kazi ngumu kama hizo hasa kwa mtoto wa kiume kama mimi, leo hii fred mimi Napata shida, wazazi wangu wameniacha nateseka tena kwenye nyumba walioniachia kama urithi wangu.......
Wakati nikiwa mwenye mawazo tele kichwani nikagutushwa na mtu anayegonga katika chumba changu, nikaenda kufungua mlango nikakukana uso kwa uso na Shangazi Zuwena.Kitu alichoniambia sikukitegemea kwa wakati huo, nguvu ziliniishia nilianza kumchukia,nikamuona adui yangu mkubwa na kumuona kama yeye ndio sababu ya wazazi wangu kufariki.Alichoniambia Shangazi ni kwamba nikachukue nguo chumbani kwake nikazifue.Nikaona sasa ananiletea dharau za wazi wazi, sikumjibu badala yake nikatoka nje na kukaa kwenye kiwambaza cha nyumba yetu.akanifuata safari hii akiwa na furushi la nguo mkononi, akanitaka nizipokee nguo zile nikazipokea kwa shingo upande.wakati nikiwa namuangalia kwa jicho baya mwanamke hasiye na haya, akasema
“Nataka ufue nguo hizo!
“Shangazi naomba nipumzike kidogo, najisikia kichwa kuniuma”nilimuambia
“Sitaki maneno mengi, ninachotaka ufue nguo hizo”alisisitiza shangazi
“Napumzika kwanza nitazifua baadae”nilimwambia shangazi
Gafla shangazi alisogea karibu yangu na kuanza kunipiga nami sikuwa nyuma tukaanza kujibizana kwa ngumi na mateke.shangazi alikuwa mwepesi kweli nililowa mvua ya matusi alinidhibiti villivyo.wakati huo kilio changu kikaongezeka mara dufu sasa nikajikuta nalia kwa sauti kubwa, ambayo ilimfikia Anko Mashaka akatoka nje na kuja,alipofika pale hakuzungumza kitu alimvamia mkewe na kumpeleka ndani.Shangazi alikuwa kafura kwa hasira nilimsikia akimtukana Anko Matusi mazito ingawa niliumia ila sikuwa na jinsi nikawaacha wayamalize wenyewe.Niliamua kuzifua zile nguo huku nalia,nilizifua kwa muda mrefu bila kuzimaliza nguo zilikuwa nyingi,baada ya muda nikachoka. Nilipokalibia kumaliza zikaletwa nyingine lakini sikusema kitu chochote, niliendelea kufua mpaka nilipomaliza zote na kuzianika kisha nikaingia ndani kupumzika. Nilipata mshangao wa mwaka, macho yalinitoka pima moyo ukinienda mbio mithili mbio za farasi, sikutegemea kama siku hiyo ningeona kitendo kile ambacho sikuwai kukiona katika maisha yangu.Nilimkuta Anko Mashaka akiosha vyombo, uso umemjaa baadhi ya mwili wake ukiwa na majeraha, hapo hapo nikamuuliza kulichomsibu,
“Vipi Anko Mbona hivyo?” nilimuuliza
“Hapana Anko
“Unakubali kufanyiwa hivyo kweli?, nilimuuliza
“Wewe acha tuu Fred”, alinijibu
“Yeye amekaa tuu, anakufanya mtoto mumewe? Niliendelea kumwoji huku nina maumivu moyoni
“Hapana Anko lakini…….!
“Lakini nini Anko, wewe viache atakuja mwenyewe kufanya kazi hiyo”nilimuambia
“Hapana ngoja nimalizie tu Anko”
“Sawa!”Nilimjibu.
Sikushangaa wala kutamalaki, ilikuwa ni kawaida yetu kupewa kazi kama hizo.Wakati nikiwa naongea na Anko Mashaka maneno hayo, shangazi alikuwa kiwambazani anatusikiliza.Nilipokuwa natoka ndio nilipokuta nae akiingia,alinifuata karibu na kuanza kumpiga,ikawa patashika nguo kuchanika mtindo mmoja kama ilivyokuwa ada yangu nikachomoka mikononi mwake mbio kuelekea mlango wa ukumbini ili nijitome nje.kwa bahati mbaya mlango ulikuwa umefungwa kwa ufunguo,wakati nilipokuwa najalibu kuufungua shangazi akaniwai na kunizaba kofi kali kwenye shavu langu,siku hiyo sikujalibu kuteteleka wala kupambana na nguvu za shangazi tena. Anko Mashaka aliposikia kukuru kakara alikuja kutuamulia, Kwa vile mlango wa uwani ulikuwa wazi hakupata shida kutufikia na kama angekuwa nje basi hasingeweza kuingia maana mlango wa ukumbini ulikuwa umefungwa, alimshika Mkewe na kumtoa maungoni mwangu, kisha kunitaka nitoke nje.Niliondoka nyumbani nikiwa sijui ninapoelekea mawazo tele kichwani yameenea ..........
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
********
Musa ni rafiki yangu kipenzi aliyekuwa anakaa kijiji kimoja cha busale, nyumba yetu na yao zinaangaliana, ilikuwa muda mwingi nashinda nyumbani kwao nikicheza na kufurahi pamoja.Kama utapata kukumbuka kipindi nipo shuleni nilisimulia nilivyokuwa narudi nyumbani na Musa, urafiki wetu ulikuwa wa kufa na kuzikana, tulipendana sana kwenye shida na usaidina kwenye raha ufurahia pamoja kiukweli urafiki wetu ulikuwa wa kushibana, waenda walisema akufahaye kwa dhiki ndiye rafiki. Baada ya kumaliza shule huku wote tukiwa tumefeli mitihani yetu, Musa akawa kaajiliwa kufanya kazi katika kiwanda cha kusaga na kukoboa mpunga akiwa na dadaye anayeitwa Asha. Pamoja na uyatima waliokuwa nao lakini Musa alikuwa na akili za uwelewa mkubwa, angali akiwa na umri wa miaka kumi na saba tu aliweza kujikumu kimaisha.Baada ya kuhitimu darasa la Saba Mama yao aliugua ghafla na kufariki dunia.Musa na Dadaye Asha wakiishi pekee. Siku moja Musa alinidokeza kuhusu maisha ya Baba na Mama yao, aliniambia Baba yao alikuwa mlevi kupindukia, akiludi amelewa na kufanya fujo nyumbani hali hisiyompendeza Mama yao alivumilia mwishowe akachoka akaamua kumfukuza nyumbani.
Aliendelea kuniambia Musa ni kwamba Baba yao Baada ya kufukuzwa aliondoka usiku wa manane,hawakujua alipoelekea wala hakuwaaga anapokwenda maana alikuwa amelewa chakali.Aliondoka huku akiyumba huku na kule, wakiwa hatujui aendako walimwangalia tu na kumkodolea macho akipotelea gizani.Baada ya siku mbili tukiwa tumekaa nyumbani tulisikia wanakijiji wakiongea habari za mtu aliyekutwa ameuawa maeneo ya kyela karibu na chuo cha tumaini tawi la mbeya ambacho awali ujulikana kama Mbeya Lutheren Teacher Corrage.
Siku hiyo walikuwa wametulia tu nyumbani wakiwa wanasikiliza redio ndogo aina ya Sing Sang kutoka china,kilichokuwa imewekwa juu ya meza ndogo pale sebuleni.Punde kipindi cha habari kiliwaadia na kusikika ndani ya redio hiyo Musa,Asha na Mama yao masikio yote yalikuwa kwenye redio hiyo “Mwanaume mmoja mkazi wa kijiji cha Busale Wilayani Kyela Mkoani Mbeya amefanyiwa ukatili wa kutisha kwa kukatwakatwa na Panga kichwani na kuondolewa kiganja, sikio na sehemu nyingine za mwili wake.Mwanaume huyo anayefahamika kwa jina la Joseph Mahenge amefanyiwa ukatili huo na mtu hasiyefahamika kwa madai ya kuwa mlevi na hasiyekuwa na maherewano mazuri na familia yake.Tukio hilo lilimkuta Bwana Joseph akiwa njiani akiwa navuka barabara ya Kyela. Alipofika hapo Musa akaendelea kunisimulia,Viongozi wa kijiji hicho wamekanusha kuwa hakuna uzembe uliofanyika kumkamata mtuhumiwa huyo kwani bado inaendelea kumtafuta ili kumtia hatiani.Taarifa hizo zilituchanganya sana hasa wanakijiji na watu waliofika maeneo hayo walipokuwa wakisema marehemu amefanyiwa kitendo cha kinyama, alikatwa mapanga na sime kutumbukizwa kichwani.Mama alikuwa anasikiliza kwa makini jambo lililokuwa ninasimuliwa alikurupuka ghafla kusikia jina la mumewe likitajwa alitoka nyumbani na kwenda Kyela.
Tulipofika mara moja Mama akatambua Maiti hiyo iliyotapakaa damu ikiwa sakafuni. wakati tukiwa hatuelewi cha kufanya Mama nae nguvu zikamuishia, wasamalia wema walitusaidia kutupakia kwenye gari kisha kuchukua Maiti na kurudi nyumbani busale.Siku iliyofuata mazishi yakafanyika kwa msaada wa ndugu na jamaa.Siku hiyo Musa alinisimulia mambo mengi sana kuhusiana na maisha yao, akiwa yeye na dada yake wanavyoishi maisha ya kifukara pasipo msaada kutoka kwa ndugu zao.Nilimuonea huruma sana musa ingawa sikuwa namna ya kumsaidia rafiki yangu kipenzi nilimpa tu pole na kumtaka hapunguze mawazo maana yote ni maisha...
Ulikuwa usiku wa manane mkesha wa January mosi mwaka 1985,kuhamkia siku inayofuata ambayo ilikuwa ni sikukuu ya kusherehekea kuingia kwa Mwaka mwengine.Nakumbuka alfajiri nilikuwa katikati ya usingizi mzito nimelala, ghafla nikakurupuka na kusikia sauti kutoka chumba alicholala Anko Mashaka ambapo ndipo chumbani mwao.Nikatega sikio langu ili kusikia kinachoendelea,niliahamaki kusikia sauti ya Anko aliugulia maumivu,tena ilikuwa maumivu makali mpaka akasikika akilia kwa uchungu nikatoka chumbani kwangu kuelekea ulipo mlango wa chumba chao.Nilitembea kwa tahadhali kubwa,kadri nilivyokuwa nakalibia kufikia chumba hicho ndivyo sauti hizo zilivyozidi kuongezeka.Nilipofikia mlango nikachungulia ndani kupitia kitundu cha funguo,Hamadi moyo ukapiga Paa!sikuamini macho yangu nilichokiona mle ndani hakika kiliniumiza akili yangu,nikajikuta hasira zikinipanda nilitamani nifungue mlango nikajionee lakini moyo ukawa mzito, miguu nayo ikakosa nguvu nikajikuta nimekaa pale mlango. Bila kutegemea mlango ukafunguliwa nikamuona shangazi akitoka akiwa na kifuko cheusi mkononi, aliponiona aliuficha ule mfuko pasipo kuongea kitu, nikajikuta uso kwa uso tunatizamana kila mmoja wapo pasipo kupepesa macho pembeni. Alipoona nimemkazia macho kama mjusi aliyebanwa na mlango alikenua mdomo wake kwa dharau na kuondoka zake nami nikapata mwanga kutaka kujitoma ndani ya chumba chao moyo wangu ulisita lakini nikaona nipige tu moyo konde na kutaka kujua Anko amepata matatizo gani nikajikuta nikiingia moja kwa moja mpaka ndani.
Nikamkuta Anko Mashaka akiangaika pale sakafuni povu likimtoka mdomoni pasipo fahamu kujitambua. Nikiwa natafuta namna ya kumsaidia nikaona kikombe kikiwa sakafuni, nilikisogelea na kukichunguza, nikaona ndani ya kikombe hicho kukiwa na mabaki ya uji yaliyosalia, ndio nikapata ushaidi wa tukio nililoliona,pasipo shaka shangazi ametumia uji ule wenye sumu kumnywesha Anko. Niliumia moyoni kumuona anko akiwa katika hali ile,alikuwa amelegea mno mdomo wake ukiwa umekaa upande povu lililochanganyika na damu likitoka kinywani wake .Sikuwa na namna ya kumsaidia badala yake nikatoka mpaka sebuleni nikachukua maji kwenye kikombe kikubwa na kunywesha Anko, lakini wapi hakuwa na nguvu kuyameza yale maji nikaamua kumwagia ili azinduke lakini wapi hakutikisika wala kupepesa. Nilizidi kuchanganyikiwa wazo likanijia nikachukua nguo iliyokuwa pembeni yake na kuanza kumpepe, mara shangazi akaingia mle ndani pasipo kuniongelesha akapanda kitandani na kulala bila kumhudumia Anko, aliniangalia tu nikiangaika bila msaada. Kiukweli nilichanganyikiwa sana wakati ananiona naangaika peke yangu yeye amelala tu bila wasiwasi.Wakati nikiwa kwenye taharuki nikamuona Anko akiweweseka pale sakafuni nikamshika na kumuegemeza miguuni mwangu kumwuliza kilichomsibu akanionesha kile kikombe kilichopo sakafuni pale nikakiangalia kile kikombe kisha nikamtupia jicho kali shangazi aliyekuwepo kitandani, nikaona Anko akinyoosha mkono na akinipa ufungua mdogo wa kabati nami nikaupokea haraka pasipo shangazi kuniona Nikautia mfukoni mwa bukta yangu yangu.Muda huo nikamsikia shangazi akinitaka nitoke chumbani mwake nilimkatalia lakini alinijia juu na kunifukuza kwa nguvu zake zote. Nikashindwa pambana nae nikajikuta nipo nje ya mlango wa chumba chao, nilimuonea huruma sana Anko, lakini sikuwa na jinsi kikajikongoja kurudi chumbani kwangu na kumuacha anko akiwa kwenye mateso makubwa.
Usiku ulikuwa mrefu kwangu niliwaza na kuwazua mambo mengi jinsi hali iliyokuwepo pale nyumbani. Nitaishi vipi bila malezi yao, Shangazi amemchukia Anko kwa sababu yangu nilijiuliza pasipo kupata majibu. Ghafla nikiwa nimejilaza kitandani mawazo yakanijia nikamkumbuka Musa, rafiki yangu kipenzi tumesaidiana mambo mengi nadhani anaweza kunisaidi.Nilijisemea moyoni “kesho asubuhi na mapema nitakwenda kwa rafiki yangu Musa, nitamueleza matatizo yangu yote labda anaweza akanisaidia”.wakati nikiwa kwenye mawazo nilipitiwa na usingizi nikalala fofofo sikuamka mpaka asubuhi.
*******CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment