Simulizi : Nimeipata Furaha Yangu
Sehemu Ya Nne (4)
“Wewe kijana ulipona?" Aliuliza mzee Hashim akiwa haamini.
"Ndio mzee tena kizuri sikuwa na Ebola."
"Kweli?"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ndio mzee." Ilibidi Rodrick amwelezee kila kitu toka mwanzo kisha wote walianza safari ya kuelekee nyumbani kwa Rodrick.
"Rhoda yuko wapi?"Akamuuliza huku akiwa anamtazama machoni.
Ilibidi naye mzee Hashim amweleze kila kitu kuhusu Rhoda toka alivyomuacha na hali yake ilivyozidi kuzorota kila kukicha.
"Je huyo mzungu atamponesha kweli?"
"Nina uhakika wa asilimia mia atapona na je umewezaje kufika huku wakati hakuruhusiwi mtu kuingia mwanza?"
"Kweli ila si kuna vipimo maalumu kila kituo cha usafiri."
Waliongea mengi sana siku hiyo kisha waliwekeana ahadi ya pindi Rhoda akirudi tu wanaenda kufungua kesi mara moja na baadae mzee Hashim alirejea kwake Butimba.
"Baba niko mwanza!"
"Nani baba yako mpuuzi wewe mbona hujihurumii mwenywe? Wewe unaona mwanza bado kunatisha kwa Ebola lakini unapeleka pua zako huko na ukiugua tena sitaki kukusikia ukinipayagia maneno tena una kichwa kigumu kama cha mama yako sijui huyo malaya amekuloga na nisisikie tena upuuzi wa ooooh! Namtetea nitakukata masikioooo tiiiii! Tiiiiiiiii!" Mzee Steven alimaliza kuongea bila kumpa nafasi mwanaye na kukata simu.
"Nini Rodrick?" Aliuliza Andrew huku akiandaa meza kwa ajili ya Chakula cha usiku.
"Aaaah! usijari nipo sawa."
"Mimi Rodrick Steven nahapa kwa kinywa changu kuitumikia kazi hii na kutetea haki za wanyonge kama mungu alivyoamuru eeeeh! Mwenyezi mungu nisaaidie!" Alijikuta akiyakumbuka maneno aliyowahi kuyatoa siku ya kihapo.
"Hapana lazima nikamilishe safari hiii nooo!” Alijikuta akilopoka kwa guvu hadi mwenziye akisikia kila neno alilokuwa akilizungumza.
****
Ndege ilishuka katika uwanja wa new York na teyari gari la wagonjwa mahututi arimafu kama ambulance lilikuwepo tayari uwanjani hapo safari ya kuelekea katika hospitali ya York Medical Center iliyopo katika ya mji mkuu wa marekani ilianza huku baadhi ya madaktari waliokuwemo ndani ya gari hilo wakianza kumshughulikia Rhoda kwa huduma ya kwanza.
"Ana tatizo gani mbona amefunikwa hivi?"
"Nilivyosikia ni Ebola!"
"What?" Alishangaa mmoja wa wauguzi ndani ya hospitali hiyo.
“That why i hate black people ( ndo maana nawachukia watu weusi ) alisikika akilopoka mmoja wa wagonjwa waliokuwepo hapo na kumfikia afande Marry aliyekuwa amekaa juu ya benchi
.
"Kwahiyo inatakiwa awekewe damu nyingine ili kuzuia maambukizi?"
"Aliuliza dokta Maycon kijana wa miaka 25 tu lakini alikuwa na uwezo mkubwa sana achilia mbali elimu kubwa aliyokuwa nayo.
Dokta Maycon ni raia wa Canada jimbo la califonia akiwa mtoto wa pekee katika familia yake ambayo baba yake alikuwa seneta wa nchi hiyo.
"Yaaa! Itakuwa vyema zaidi ila subili dakika 86 tutaona kama hali yake itakuwa ile ile tutaweka damu!" Dokta Collin alijibu akiwa anaendelea kumtundikia Rhoda dawa mbalimbali katika mwili wake huku wakiwa katika mavazi maalumu ya kuzuia maambukizi.
Baada ya wiki moja hali ya Rhoda ilikuwa inaendelea vizuri zaidi kwani aliweza kutembea mwenywe kula mwenyewe hata mwili wake ulikuwa umeanza kunawili ule ukurutu haukuwepo tena alianza kuvutia kwa kila aliyemtazama hiyo ilichangiwa na dawa zilizokuwa zimechanganywa na vyakula vyenye asili ya vimiminika lakini vikiwa na virutubisho ila alikuwa akisubili kipimo cha mwisho ambacho kingedhibitisha kama kweli alikuwa amepona kabisa.
"Rhoda!" Aliita Dokta Maycon akiwa anachomoa sindano ndani ya mkono wake wa kushoto.
"Unajua wewe ni mzuri sana!" Aliendelea baada ya kumuona Rhoda amenyamaza.
"Toka nizaliwe sijawahi kuona mwanamke wa kiafrika ambaye ni mzuri kama wewe japo umefungwa maisha yote jela ila nahapa kukupigania kutoka katika kifungo hicho ili uje kuwa mke wangu!" Daktari huyo hakuficha hisia zake kwa Rhoda ambaye alikuwa kimya muda wote.
"Nipe dakika kumi!"
Aliongea na kutoka na baada ya dakika hizo alirejea na kumpatia majibu ambayo yalionyesha hana virusi vya Ebola.
******
Ilikuwa jumatatu tulivu siku tatu baada ya Rhoda kurudi na teyari alikuwa ameanza tena kutumikia kifungo chake cha maisha , siku hiyo Rodrick alikuwa kituo kikuu cha pilisi akiadikisha kesi ya Rhoda , na kuomba kibali cha kwenda kumkamata mama mchepuko kwa mahojiano zaidi kuhusiana na kesi ya Rhoda .CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwakuwa alikuwa akifahamika hapo hakupata usumbufu hivyo alipatiwa askari watatu akiwemo wa kike kwenda kumkamata mama mchepuko ambaye alikuwa hajui nini kinaendelea
Defender lilokuwa na askari liliegesha nje ya nyumba iliyokuwa na geti jeusi kisha askari mmoja alienda kugonga geti hilo lakini kabla ya kufanya chochote alishangaa kuona geti likifunguliwa na mwanamke alikuwa amefungwa pingu alitokeza kisha mkuu wa polisi mkoa wa mwanza naye akiwa amefungwa pigu kisha wanajeshi kadhaa walitoka wakiwa wameba mfuko ambao mara moja haukujulikana ulikuwa na nini.
"Tunashida na huyu mama!"
"Njooni kituoni." Alijibu mmoja wa wanajeshi hao kisha walimpakiza mama mchepuko na mkuu polisi na safari ya kuelekea kituo kikuu cha polisi.
Gari tatu ambazo mbili ni za polisi na moja ikiwa ya jeshi zilisimama makao makuu ya polisi mkoa wa mwanza alimarufu kama centrol yalipo mkabala na jengo la mkoa Ccm. Wanajeshi saba waliruka kisha watu wawili ambao walionekana kama ni watuhumiwa kutokana na kufungwa pingu mikononi mwao walishushwa na kuamriwa kutangulia ndani ya kituo hicho cha pilisi . Ndani ya kituo hicho hakuna aliyeamini kama mkuu wao wa kazi alikuwa amekamatwa na kila askari alikuwa akiandaa masikio yake kusikia kisa cha mkuu wao.
"Vueni kila kitu kabla ya kufanya lolote!" Alliamru afande Matiku mwenyeji wa mkoa wa Mara kijiji cha kiabakari bila kuogopa chochote. "Lakini mimi boss wako matiku!" "Natekeleza kazi yangu, " alijibu huku akiandaa kalamu kwa nia ya kuandika maelezo yao. "Afande hawa wahuni tumewakuta wakiwa wanagawana madawa ya kulevya hilo ndo kosa la kwanza kwao," aliongea mmoja wa wanajeshi hao na kufanya kila askari kumtolea macho mkuu wao , "Na udhibitisho huu hapa." "Afande hivi ni kweli?" "Hapana !" "Hapana wakati kila kitu kipo wazi unabishana na hawa?" Matiku aliuliza kwa ukali "Ndio!" "Okay hebu mpelekeni kwanza selo akifika huko atakuwa ameshakubali tu. "Hawa wanaonishitaki wao wameambiwa na nani mimi nilienda pale kumkamata mama huyo!" Ilibidi mkuu huyo amtupie mpira mama mchepuko.
"Na kama si ukweli je hayo madawa mmeyakuta kwangu ama kwake?" "Kwake." "Basi tambueni nilienda pale kikazi na istoshe mmenidhalilisha sana," mkuu huyo alizidi kujitetea ili tu amkandamize mama mchepuko. "Jamaniii." "Kimya wewe mama kwanza unamakosa kibao bado na sakata la kuuza wasichana hebu muwekeni ndani huyu," ilibidi mkuu naye atumie nafasi ya kibabe kumkandamiza mama mchepuko aliyekuwa akishangaa shangaa. "Kabla hajapelekwa kokote nasi tuna mshitaki kwa mauaji ya Rhodina!" Ilisikika sauti ya Rodrick na kupenya sawia katika ngoma za mwanamke huyo. "Sijawahi kuua hata siku moja! Aliefanya hayo ni ndugu yake Rhoda na tayari yuko jela nyie vipi hahahaha!” Alijifanya kuongea huku akicheka kuashilia kuwa walikuwa wamebugi. "Mama usituone siye wajinga!.... Aliendelea Rodrick huku hasira za wazi zikiwa zimeanza kujitokeza. "Kijana hebu sogea hapa ueleze vizuri." Rodrick hakuwa na muda wa kupoteza alijipenya katikati ya watu na kuanza kuandikisha maelezo juu ya kifo cha Rhodina kisha alipewa nafasi ya kwenda Butimba kuonana na Rhoda ili aweze kuandika baarua ya kukata rufaa katika mahakamu kuu ya mjini dar es salam.
Rodrick aliegesha gari lake na kushuka akiwa na Andrew kwa kuwa walikuwa wameshatoa taarifa ya kufika hapo hawakupata shida kuonana na mkuu wa gereza hilo ambaye alikuwa ameshakuwa kama ndugu . "Shikamoo mzee." "Maharaba vijana vipi mmekuja kufanya mpango wa kuonana na Rhoda?" Aliongea huku akifungua mlango wa ofisi yake kisha wote waliingia na kuketi kisha mkuu wa gereza aliagiza kuitiwa Rhoda ambaye alikuwa hajui chochote.
"Mrembo wangu kwanza pole kwa kuugua,"aliongea Rodrick baada ya Rhoda kuingia ofisini humo akiwa katika mavazi ya rangi ya njano japo alikuwa mfungwa lakini uzuri wake haukutoweka tena ulikuwa umeongezeka sana hata Rodrick mwenyewe hakuamini kama Rhoda ni mrembo kiasi hicho. "Ahsante!" Alijibu kinyonge na kukaa kimya.
"Napenda ufahamu kuwa muda wako wa kukaa humu unahesabika." "Kiaje?"Aliuza huku akiwa ameyatoa macho juu juu teyari kichwani kwake alianza kujenga picha ya kwenda marekani kwa Dokta maycon. Ilibidi Mzee Hashim amwelezee jinsi mambo yatakavyokuwa kuhusu rufaa "Basi nipo tayari kuandika." Alisema Rhoda huku akiwa anacheka cheka kuashilia furaha imeanza kujitokeza. "Na akitoka tu ndoa hiyo!" Rodrick alijikuta akiwaza huku macho yake yakiwa juu ya paji la uso wa Rhoda ambaye naye mawazo yake yalikuwa marekani kwa mzungu ambaye alikutana naye hospitali nchini marekani.
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DAR ES SALAAM.
Shauri la Rufani ya jinai NO 284 la 07 la 2001. ( kutoka mahakama ya hakimu mwanza)
Kupinga hukumu ya mheshimiwa hakimu Marwa Wanjiku. Kati ya Rhoda Jackson........mrufani Na Jamhuri ......mrufaniwa
HATI YA KUKATA RUFAA. - Rhoda Jackson mrufani anakata rufaa kwenye mahakama kuu ya Tanzania dhidi ya hukumu ya hakimu Marwa Wanjiku ambapo alionekana na hatia ya kumuua dada yake Rhodina akahukumiwa kwenda jela miaka yote kwa sababu zifuatazo. - mshitaki ambaye ni mama mchepuko hakuwa na ushahidi wa mtaalam wa uchunguzi wa mtaalam wa afya unaodhibitisha kuwa marehemu Rhodina aliuawa na Rhoda . - ushahidi wa mshitaki mama mchepuko ama Regina alitaka kujitoa hatiani hivyo akatoa ushahidi wa kunisingizia kwamba nilimuua dada yangu kwa kumchoma chupa tumbani kisa mwanaume lakini haikuwa hivyo shahidi yangu bwana Andrew yupo tayari kuelezea kisa chote. -kwamba jamhuri haikuthibitisha mashitaki yake bila ya shaka ya maana dhidi yangu ( mrufani) -Mahakama ya mwanzo haikunipa muda wa kuleta shahidi. - Hakimu Marwa wanjiku alipokea rushwa ya shilingi laki tano ili anikandamize kutoka kwa Regina na Hamisi na hundi hiyo nimeambatanisha. Hivyo basi mrufani naomba mahakama yabatilishe hukumu ya mahakama ya mwanzo na kufutwa adhabu ilitotolewa dhidi yangu . R.Jackson Mrufani RHODA JACKSON. Gereza la Butimba , Mwanza, 23-07-2004. Nakala Kwa, Mkurugezi wa mashitaka.
Ilikuwa barua ya kukata rufaa kwa Rhoda aliyoiandika kisha aliiweka ndani ya bahasha ya kaki kisha alimkabidhi Rodrick ambaye aliondoka nayo kwenda kuituma mahali husika.
******
Baada ya Hamis kuwachomea akina mama mchepuko na mkuu wa polisi mwanza aliamua kutoroka na kuelekea Tabora lakini baada ya wiki moja alishangaa akitafutwa kwa kosa la kugushi uongo dhidi ya kesi ya Rhoda miaka miwili nyuma , Hakimu Marwa naye alikuwa ameshikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kutoa hukumu isiyostahili pia kupokea rushwa hali iliyomuumiza na kupanga njama za kumuua Rhoda kabla ya kesi yake kusomwa tena.
"Afande Josephne nakuomba tuonane kama itawezekana." Hakimu Marioba alimtumia ujumbe mfupi askari magereza huyo akiwa ndani ya chumba cha polisi kupitia simu ya mmoja wa askari polisi . Masaa mawili kupita afande Josephne alikuwa akiongea na hakimu huyo "Nataka ukamuue Rhoda usiku wa Leo!" "Hahaha !" Alicheka na kuendelea… " umemaliza mimi mwenyewe simpendi nilidhamiria kumuua kwa kumchoma damu ya virusi vya Ebola lakini amepona safari hii lazima afye." aliongea kwa kujiamini kisha alinyanyuka na kuondoka "Siku tano atakuwa ahela!"
"Hivi nani aliyetoa copy yangu ?"
Aliendelea kuwaza hakimu Marwa wanjiku akiwa ndani ya kachumba kadogo kalikokuwa kachafu na kenye uvundo.
"Itakuwa sekretali wangu aaaaaah! Kweli maana....daaaah! Alikumbuka kitu na kubaki akiyatumbua macho nayo yaliyokubali kutoka. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Shika hii bank slip mkuu hakikisha unamkandamiza huyo mtoto.”
"Hahaa haaha! Naenda kuchinja ila kabla ya kuendelea inabidi msaini hapa na hapa.”
"Hapana siye tunamkataba leteni niusain na nikitoka kukahukum nakuja kuwapa."
"Poa."
Hivyo ndivyo ilivyokuwa siku ya hukumu ya Rhoda miaka miwili nyuma na miezi kadha baada ya Hamis na mama mchepuko kupeana mkataba na karatasi ya malipo walitoka ndani humo na kuacha kila kitu juu ya meza na hiyo ikawa nafasi ya sekretali wake Angel kuingia na kuchukua kila kitu kisha kutoweka navyo maana aliumia kitendo cha ukandamizwaji wa Rhoda na aliahidi endapo atasikia kesi hiyo inazungumziwa lazima naye atoe ushahidi kweli siku ya Rodrick kwenda mahakamani kuomba nakala za kesi ya kwanza alibahatika kukutana na Angel ambaye nae alimkabidhi ushahidi huo.
"Nitamuua haraka sana mshenzi sana!" Wanjiku alijikuta akidhamiria kumuua.na Angel
"Afandeeeeee!" Aliita kwa sauti ya juu.
"Nini !?"
"Njooooo!"
"Aaaaah!" Japo alijibu kwa karaha lakini alikwenda
"Nipe simu."
"Yaa nini?"
"Nataka niongee na mwanasheria wangu."
"Poa !" Alijibu na kutoa bila kuelewa kuwa alikuwa akifanya kitu cha hatari tena kwa mara ya pili .
"John nendeni pansias sokoni nyumba no 125\ 12 muulizieni mwanamke anayeitwa Angel ni mrefu , mweupe muueni kabla ya kesho," aliongea na kukata simu hali iliyopelekea askari kutoelewa chochote kutokana na kuchengwa na lugha aliyokuwa akiinzungumza wanjiku .
"Jamani nimewafanya nini?" Sauti ya mwanamke ilisikika ikilalamika kutokana na mateso makali.
"Unaona hiki lazima kipasue tumbo lako!" Alijibu kijana huyo huku akitoa kisu chake na kuanza kumchoma choma nacho lakini alifanikiwa kukimbia hakujulikana ni wapi Angel alienda.
******
"Lazima afye mjinga sana yaani basi tu!" Josephne aliendelea kuwaza akiwa ndani ya daladala iliyokuwa ikifanya kazi zake Butimba na Igoma alipofika kona ya nyegezi alishuka na kuingia ndani ya duka la dawa za mifungo.
"Sipe super dipu."
"Saw dada."
Baada ya kuhudumiwa alienda duka la madawa na kununua sindano mbili kisha aliendelea na safari yake kuelekea gerezani.
"Hawa nataka unisaidie kitu kimoja."
“Kipi afande !?"
Aliuliza hawa huku akiwa na wasiwasi mwingi maana ilikuwa ajabu kuongea na afande Josephne kutokana na ukali wake achilia mbali ukorofi.
"Unamjua Rhoda?"
"Yupi yule wa kahama au yule mfungwa wa maisha?" Aliuliza Hawa huku akiwa anatazama chini.
"Yule wa maisha."
"Mmmh !"
"Nataka uumue leo!"
"Nini? Aaaah! Hapana! Mmmmh… siwezi kabisa."
"Sikiliza nawewe nitakupa pesa nyingi sana ambazo hujawahi kuziona!"
"Kwani kafanya nini?"
"Unajua alimuua dada yake mtoto wake na istoshe nimetumwa na mahakama hivyo usiwe na wasiwasi kabisa nitakupa hii sindano utamchoma kisha unaondoka hakuna ambaye atajua fanya hivyo sawa?"
"Naogopa afande." Japo alikuwa akizitamani pesa hizo ambazo zingetumika kuendeshea kesi yake lakini roho ya huruma ilikuwa ikimuingia pindi alipokumbukia upole wa Rhoda.
"Aya shika!"
"Hapana," hawa alijibu na kuondoka hakutaka tena kuua alihisi kufanya dhambi kubwa sana maishani.
"Mse****, kumbe hanijui na yeye nitamjumuisha !" Afande Josephne aliongea peke yake baada ya Hawa kuondoka ndani ya chumba cha kuhifadhia chakula.
"Kesho kutwa zamu yangu inaingia nitawaua wase*** hawa !" Alizidi kukiparua kichwa chake kwa mawazo yaliyochanganyikana na hasira.
****
Ulikuwa ni usiku wa saa nane ambao kila mfungwa alikuwa akikoroma kutokana na utamu wa usingizi , katika bweni la wafungwa wa kike alionekana mtu akiranda randa kuangalia usalama mara apite huku mara kule ilimladi alikuwa akihakikisha kazi yake inaenda vizuri .
"Wacha niende sasa!"
Aliongea na kuanza kutembea kuelekea usawa aliokuwepo amelala Hawa. "Naanza na huyu maana nikimuacha hai ataitoa siri hii!" Alitamka maneno hayo baada ya kufika sehemu aliyokuwa amelala Hawa , alichomoa sindano iliyokuwa imejaa sumu aina ya super dipu na kumchoma nayo Hawa , kisha alielekea upande aliokuwa amelala Rhoda napo hakufanya kosa alimchoma zaidi ya mara tatu na kuondoka.
"Afadhali daaa! Pumzikeni kwa maani." Aliyatamka maneno hayo huku akiwa anatoka nje ambako alipishana na mfungwa aliyekuwa akitoka chooni lakini hakuweza kumtambua kutokana na kiza tororo lilokuwa limetanda na kingine kilichichangia ni ule wasiwasi uliokuwa umejaaa ndani ya moyo wake.
"Huyu afande anafanya nini?" Alijiuliza mfungwa huyo baada ya kushuhudia kitendo cha Afande Josephne kuanzia mwanzo hadi mwisho lakini hakutaka kumshitua.
"Eeeeeeh! Humbeee!" Hawa alijisemea neno hilo huku akiwa ameuziba mdomo wake baada ya kushuhudia Rhoda akichomwa sindano na Afande Josephne aliumia sana kuona kitendo kile ila ilibidi atulie na kujifanya hajaona na alipomuona anatoka nje naye alijifanya kuingia ndani.
"Afandeeee! Afandeeeeee !Kunatatizoooo njoooo! Zilikuwa ni sauti kali za wafungwa zilizoyazibua masikio ya afande Marry aliyekuwa akikatisha asubuhi ya saa kumi na moja eneo wanalolala wafungwa.
"Kuna nini?"
"Kuna watu wamekufa!"
"Nini? Na ni akina nani?" Aliuliza huku akiwa amechanganyikiwa akipiga hatua ndogo ndogo kusogea eneo walilokuwa wamekusanyika wafungwa hao wa kike moyo wake ukiwa na wasiwasi sana.
"Hatujawafahamu vizuri kutokana na sura zao kubadilika ila itakuwa ni Rhoda na Hawa maana hawaonekani na istoshe sehemu hizo ndizo huwa wanalala!" Mnyapara wa wafungwa hao aliongea huku akiwa anatoa machozi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Oky wacha niongee na uongozi." Alitoka na aliporudi alirudi na msaidizi wa mkuu wa gereza hilo ambaye aliamrisha miili hiyo ipelekwe hospitali kwa uchunguzi zaidi .
Hakuna mfungwa ambaye hakuweza kutoa machozi pindi miili hiyo ilipokuwa ikipakiwa ndani ya gari la magereza wengi wao walikuwa wakimlila Rhoda .
Hakuna aliyendelea kulala tena ndani ya bweni hilo hadi kunapambazuka.
"Huna haja ya kunishangaaa mke wangu nimekuja kukusaidia kama nilivyokueleza huko Marekani!" Aliongea kwa kujiamini Dokta Maycon daktar aliyetoka nchini kwao kwa lengo moja tu la kuondoka na Rhoda baada ya kuisha kesi yake!
"Njooo unikumbatie!" Alizidi kuongea huku mikono yake akiwa ameitandaza lakini Rhoda hakumsogelea alibaki ameganda akimtazama kwa macho yake madogo huku moyo wake ukipiga mkumbo mkubwa sana.
"Rhoda nakupenda sana hebu ona nimetoka huko mbali kwa ajili yako! Kubali tuondoke wote!" Alizidi kuongea kwa lugha ya kingereza huku akiendelea kupiga hatua kuelekea usawa aliokuwa amesimama Rhoda ambaye alikuwa hajielewi elewi.
"Njooo mke wangu!" Dokta Maycon alimkumbatia na kufanya Rhoda aanze kuweweseka sana kutokana na joto la daktari huyo.
“Hellooooo! Rhoda!" Sauti kutoka kwa mwavita ndio iliyomzindua kutoka katika ndoto asubhi hiyo ambayo ndio alitakiwa kuondoka kuelekea Dar es salaam.
"Umenishtua!"
"Mimi nimekuona ukiongea peke yako basi amka ujiandae maana leo ndo unaondoka hivyo mpendwa"
"Nilikuwa naota!"
"Nini tena?"
"Si yule mtu !"
"Rodrick au mzungu maana nawewe hakauki mdomoni mwako."
"Rodrick ni kaka yangu bhana!"
"Akikupenda je ila mnaendana bora Rodrick shosti maana wazungu mmmmh!"
"Aaah! tuyaache hayo."
Kwakuwa kulikuwa kumeshapambazuka hakuwa na haja ya kuendelea kulala aliamka na kuanza kujiandaa kwa ajiri ya safari.
"Rhoda kwa kuelekea Dar es salam haitawezekana tena maana nina habari njema yako!"
"Ipi afande?"
"Tayari barua yako ya kesi imeshakuja na nzuri zaidi utakuwa mahakamani baada ya siku tano ,lakini kwa usalama wako leo mtaenda Kasungamile huko Sengerema na siku ya kesi utakuwa mahakamani kuna hakimu mzuri tu toka Dar es salaam na mwanasheria wako Rodrick atakusimamia hivyo una siku kumi ama zaidi za kuwa magerezani!" Alimaliza kutoa habari hiyo kwa Rhoda iliyomfurahisha zaidi.
"Waooo…. afadhali nikitoka tu naanzia kaburini kwa Rhodina kisha naanza kumtafuta Maycon , bora nikaishi mbali kuliko Tanzania hapa.
Saa nne kamili safari ilianza ya kuelekea gereza la Kasungamile.
******
Ilikuwa ni jumatano ya tarehe 02-08-2004 . siku hiyo ndio ilikuwa siku ya kuanza kusomwa tena kesi ya Rhoda Jackson aliyekuwa amehukumiwa kifungo cha maisha.
Majira ya saa tatu na nusu tayari watu walikuwa wameshafurika katika mahakama ya mkoa wa mwanza kuisikiliza kesi hiyo . Mara baada tu ya hakimu Emmanuel John kutoka Makao makuu ya mahakama Tanzania kuingia mwendesha mashitaka alianza kusoma historia ya kesi hiyo .
"Rhoda Jackson mrufani anayelalamikia hukumu ya hakimu Marwa Wanjiku ya tarehe 9-01-2001aliyohukumiwa kwenda kutumikia kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumuua dada yake kwa kumchoma chupa tumboni hadi kufa tarehe 25-12-2000 huko ilemela , mrufani anapinga kosa hilo kwa sababu zifuatazo......... " Mwendesha mashitaka alitoa sababu zote kisha Rhoda akapewa nafasi ya kuongea.
"Mtukufu hakimu nakiri kwa mdomo wangu mimi Rhoda sikuua na aliyefanya hayo ni mama mchepuko."
"Hukuua wakati kila kitu kilikuwa wazi na wewe ulikutwa ukiwa katika mwili wa Rhodina." Aliuliza mwanasheria akiyekuwa akitetea upande wa washitakiwa.
"Ni kweli nilikuwepo sikuweza kuvumilia baada ya kusikia kifo cha dada yangu nilichanganyikiwa sana hivyo nikajikuta napoteza fahamu mara baada ya kuona hali hiyo."
"Usitake kuidanganya mahakama binti…"
"Mbona unamnyanyasa sana mteja wangu hivi? Sina uhakika kama mtu anaweza kuua na kubaki ameulalia mwili wa mtu aliyemuua Rhoda alizimia na hata alipokuja kuzinduka alijikuta yuko hospitali" Rodrick aliingilia kati baada ya kumuona Rhoda akisua sua.
"Je maneno hayo yana ukweli gani bi Rhoda?" Hakimu alihoji ingali ukweli alikuwa ameshaujua kutokana na barua ya Rhoda ya kukata rufaa ila alitaka kujiridhisha zaidi.
"Kuna shahidi ambaye anaweza kueleza.".Mama mchepuko aliyekuwa kizimbani alianza kuangaza angaza macho lakini alipomuona Andrew aliishiwa nguvu, picha ya yeye kuwa ndani ya gereza ilianza kupenyeza ndani ya ubongo wake na kujiona jinsi alivyokuwa akihangaika na kazi za huko, akipata surubu ambazo hakuwahi kufikilia kama siku moja angeweza kuzipata.
"Nipo tayari kusema kila kitu hakimu ....!" Andrew aliaza kusema mara baada ya kwenda na kusimama sehemu sahihi ya yeye kuzungumza kila kitu alichokuwa akikifahamu pia hakuwa nyuma kueleze hira za Hamis kumuelezea mama mchepuko kuigeuza kesi.
"Je Regina una lipi la kujitetea hapo?"
Hakimu Emanuel aliuliza
"Oooih! Ha...pana..nali...!" Alishindwa kuongea na kubaki akitetemeka.Mapigo ya moyo wake yakizidi kwenda kasi sana asifahamu hatia ya kesi hiyo ambayo ilionekana kugeukia upande wake, lakini alipomfikiria mwanasheria wake ujasiri uliongezeka ndani ya moyo wake na hata akapata tabasamu usoni mwake.
"Regina ama mama mchepuko una lipi la kuieleza mahakama kuhusu tuhuma hi?" Lilikuwa ni swali kutoka kwa Rodrick ambalo lilimfanya mama mchepuko kutulia tuli. "Mimi naona hana cha kujitetea"
Baada ya hapo mwendesha mashita alianza tena kusoma kesi ya afande Josephne ambaye naye alipandishwa kizimbani baada ya mama mchepuko. "Josephne Japhet unamashitaka ya kuua watu wawili Chausiku na bi Ndaki ambao ni wafungwa katika gereza la Butimba baada ya kutofanikiwa kumuua Hawa na Rhoda kwa kutumia sumu aina ya super dipu je unalipi la kutetea jambo hili?" "Siyo Mimi!" "Siyo wewe wakati ulikamatwa na kidhibitisho?" "Nilitumwa na hakimu Marwa." "Kwa hiyo uliua ama hukuua?" "Niliua Kwa bahati mbaya na istoshe nilitumwa ;" "Jibu swali uliua ama hukua?" "Niliua!" "Basi sawa."CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya mahijiano hayo akipandishwa hakimu Marwa naye alisomewa mashitaka yake kisha alipewa nafasi ya kujitetea. "Aaah! Daaah! Hata sina cha kuongea naomba mahakama itekeleze kazi yake!" Hakimu Marwa hakuwa na la kujitetea kutokana na ukweli kuanikwa japo hapo mwanzo alikuwa ameshajitahidi kadri ya uwezo wake kuipigania kesi hiyo kwa kutafuta wanasheria lakini ilishindikana baada ya kumaliziwa pesa zake na mwisho wa siku hawakuonekana.
Siku hiyo lilikuwa fagio lililokuwa likifagia kila aliyekuwa adui wa Rhoda hali iliyopelekea hata Rhoda kuumia na kumshukuru sana Rhodrick macho yake hayakuamini idadi kubwa ya maadui aliokuwa nao . baada ya wote kupewa nafasi ya kutetea mashitaka yao, nyundo iligongwa na mahakama ikawa imeahirishwa kwa dakika tano.
"Regina ama mama mchepuko mahakama hii tukufu inakuhukumu kwenda jela miaka yote kwa makosa yafuatayo. Mauaji ya Rhodina. Uuzaji wa madawa ya kulevya. Unyanyasaji wa jinsia kwa watoto wa kike pamoja na utumiaji wa mavazi ya jeshi la pilisi kinyume na nataratibu .
Josephne Japhet unahukumiwa kwenda jela kwa miaka sitini kwa kosa la mauaji na kutaka kudhuru wengine likiwemo kosa la kuingiza sumu ndani ya gereza kinyume na taratibu za magereza na kuvulishwa rasimi heshima ya uaskari kuanzia leo.
Marwa Wanjiku kuanzia sasa heshima ya uhakimu umeondolewa rasimi na wewe unahukumiwa kwenda jela kwa miaka thelathini kwa makosa yafuatayo. Kupokea rushwa ya laki tano kutoka kwa mama mchepuko na Hamis ambaye bado anatafutwa na jeshi la polisi. Kukiuka kanuni na taratibu za mahakama. Kutuma mtu akafanye mauaji," hakimu Emanuel John alimaliza kutoa hukumu hiyo Mara baada ya kurudi ndani. "Rhoda Jackson kuanzia sasa upo huru" ilikuwa sauti iliyopenya katika masikio ya Rhoda na kumfanya asiami hali iliyompelekea kuzimia kutokana na furaha ambayo haikuelezeka .
"Jamaniii Mimi miaka sitini kweli? Marwa umeniponzaaaaa…….hakimu nipunguzie nina mtoto wa miaka miwili ambaye anahitaji malezi ya mama!" "Rhoda nisamehe kwanza najua nilikuumiza ila kabla ya kufa !". Yalikuwa maneno kutoka midomoni mwa wahukumiwa hao walipokuwa wakitolewa kizimbani na askari kwa safari ya kuelekea Butimba kabla ya mama mchepuko kupelekwa kigoma na Marwa kupelekwa Segerea ila Josephne alitakiwa kubaki Butimba hapo hapo.
******
Ilikuwa ni furaha isiyoelezeka kwa Rhoda, Rodrick ,mzee Hashim pamoja na Andrew ambao walikuwa kama ndugu baada ya kutoka mahakamani hapo Rodrick alimpeka Rhoda katika maduka ya Nguo kisha safari ya kuelekea Buswelu ilianza. Kesho yake Andrew aliondoka na Rhoda alimuomba Rodrick ampeleke kaburini kwa Rhodina kwa msaada wa Rose. Rhoda alishindwa kujizuia baada ya kuyaona maandishi yaliyokuwa katika msaraba alihisi anaota hata alipojaribu kupikicha macho aone kama alikuwa anaota ila haikuwa hivyo machugu yalianza tena ile furaha iliyokuwa imepatikana ilikufa ghafla .Taratibu alipiga magoti mbele ya kaburi hilo huku akiyaruhusu maneno yenye maumivu kutoka ndani ya mdomo wake.
"Dada ! Dada!!! Rhodina amka sasa tuwe pamoja haki imepatikana kaka Rodrick ametusaidia amka mpenzi njooooo! " Hayakuwa maneno matupu tu bali yaliambatana na kitendo cha kugaragara achilia mbali machozi yaliyokuwa yameulowanisha uso wake alitamani Rhodina awepo ili furaha hiyo waishelekee wote. "Rhoda acha kukufuru hii ni kazi ya Mungu jipe moyo kifo ni haki ya kila mtu leo kwake kesho kwetu." “Hapana Rodrick dada alikatishwa maisha hapana siwezi kumsamehe mtu huyu siweziiiii!" Rhoda alizidi kutoa maneno yenye kuumiza nafsi hata za wengine. "Sawa Rhoda mama mungu amekutendea mambo ya ajabu mtukuze kwa hayo na hata haya maumivu uyapatayo anajua namna ya kuyatuliza hajawahi kushindwa na daima ni mshindi siku ya mwisho utamuona tena Rhodina " Rodrick alijitahidi kumpa maneno yenye kumtuliza hali iliyopelekea Rhoda kuelewa kiasi .
Japo alikuwa akiishi maisha mazuri ambayo Rodrick alimpatia lakini chozi halikukauka machoni kwake kufiwa kwa dada yake kulianza upya alitumia muda mwingi kujifungia chumbani kwake na huko kilichokuwa kikiendelea ni kilio. Rhoda alilifanya kwa siri sana lakini Rodrick aliligundua ndipo alipoamua kumfungulia mradi utakao mfanya ajichanganye na watu , lakini napo hapakusaidia ikawa kama amempa nafasi ya kushinda katika kaburi la Rhodina akilia , kwani alikuwa akifunga ofisi hiyo na kuelekea huko ndipo alipoamua kumpeleka kwao.
"Kwawale wanaolekea Africa kutakuwa na ndege ya shilika la Qatar baadala ya ile ya mwanzo mliokuwa mmeambiwa mtapitia nchi kama Cameron ambapo mtabadili ndege itakayowapeka sehemu husika!" Ilipenya sauti ya mdada iliyokuwa nyororo ndani ya ngoma za masikio ya Dokta Maycon aliyekuwa anaingia ndani ya uwanja huo wa Las Vegas Marekani kwa lugha ya kingereza baadaye ilitafasiriwa kwa lugha mbalimbali ili kila mtu aelewe.
"Paki hapo!"
"Sawa boss," dereva wake aliegesha gari ndani ya uwanja huo uliokuwa mkubwa kupita kiasi kisha alizunguka nyuma ya gari na kufungua buti lilokuwa na begi mbili ndogo ndogo.
"Twende!" Wote walianza kutembea taratibu kuelekea ndani ya uwanja huo kisha dereva alimkabidhi begi zote baada ya kufika sehemu ya ukaguzi ambapo alifuata taratibu zote na kuruhusiwa kuingia ndani ya ndege hiyo.
"Mambo?"
"Safi." Alijibu msichana aliyekuwa karibu yake kwa lugha ya kifaransa ambayo haikuwa ngeni kwa daktari huyo kutokana na kusomea ufaransa akiwa kidato cha tano na sita kabla ya kwenda Chuo nchini kwao .
"Unaelekea wapi?"
"Nairobi."
"Oooih! Kumbe tupo safari moja mie Tanzania lakini sijawahi tembelea nchi yeyote ya Afrika ndo mara ya kwanza!" Kwa kuwa alikuwa amepata mwenyeji alijikuta akifurahi sana.
"Hebu niambie kuhusu Afrika husasani Tanzania."
"Kwaufupi Afrika ni moja ya mabara saba duniani lina watu wazuri na wakarimu sana kwa upande wa Tanzania sijui vizuri ila ninachokifahamu kuna mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu Afrika nzima kuna maziwa , mbuga za wanyama tofauti tofauti na inavivutio vingi sana." Alieleza Asnart raia wa ufaransa ila alikuwa akiishi nchin Kenya alikokuwa ameolewa na msanii wa mziki Jaguar.
"Na queen Elizabeth nationa park si ipo Tanzania maana ni mbuga kubwa sana kwa ukanda wa Afrika mashariki?"
Aliuliza Dokta Maycon akitaka kuijua vizuri Afrika ambayo alikuwa akiishia kuisoma tu katika majalada ama darasani hisusani alipokuwa primary na sekondari , sasa alikuwa akienda kujionea kwa macho yake.
"Hapana mbuga hii ipo nchini Uganda sehemu moja inayoitwa kasese na inapakana na maziwa kama Albert na Edward kusini mashariki mwa Uganda , ila kwa Tanzania kuna ngorogoro mbuga iliyopitiwa bonde la ufa , Serengeti , manyara na nyingine nyingi sana achilia mbali bahari ya Hindi ambayo ni moja ya bahari kubwa sana inayotenganisha bara la Afrika na Asia."
"Ooooooh!”Alishangaa sana kisha alichukua ramani aliyokuwaga amecholewa na afande Marry miezi mitatu iliyokuwa imepita akisaidiana na mtaalamu wa ramani Mr Briton kutoka Chuo kikuu cha Oxford America jinsi ya kufika Tanzania hususani jijini mwanza.
"Asnart nina ramani hapa hebu ona!"
"Okay hapa huwezi potea maana inajieleza yenyewe ukitoka Nairobi utafikia hapa ambako ni Dar es salam,"aksema huku akisonta eneo hilo kwa kidole chake cha shahada bila kumtazama mwenzake.
"Naenda mwanza." Alimkatisha
“Ndio lakini lazima ufikie Dar es salam maana hii ndege haitui mwanza."
"Kwa hiyo mwalimu Julius kambarage Nyerere intarnation airport ipo Dar es salaam?"
"Ndio baada ya hapo utakwenda hapa."
Hakika yalikuwa mazungumzo marefu sana yaliyokuwa yakihusu Afrika na Tanzania pia Dokta Maycon hakusita kumueleza Asnart adhima ya safari yake.
"Kwahiyo unafuata mke?"
"Ndio nampenda sana Rhoda mwaaaah!" Alijibu huku aikibusu picha ya Rhoda aliyokuwa amempiga kipindi cha nyuma akiwa hospitali.
"Ila nivizuri sana watanzania ni watu wakarimu wapole na wasiokuwa na majivuno umepata mke bora hongera!"
Hadi wanafika Cameroon walikuwa wametawaliwa na maongezi baada ya kutoka hapo waliingia nchini Kenya mbako Asnart alishuka na kumuacha Dokta Maycon akiimalizia safari yake iliyokuwa imebakia Fupi sana.
"Kwawale wanaelekea Tanzania waende katika ndege iliopo upande wa kushoto!" Sauti hiyo iliwafanya abiria waliokuwa wakisafiri kuiendea ndege hiyo akiwemo na Dokta Maycon aliyechukua vitu vyake na kuelekea humo.
Saa nne za usiku ndege hiyo ilitua katika uwanja wa mwalimu nyerere jijini Dar salam kisha abiria wote walianza kutoka akiwemo Dokta Maycon aliyekuwa anasukuma vibegi vyake baada ya kukabidhiwa vitu vyake ikiwemo bastola .
"Nitafutie hoteli nzuri sana!"
"Laki moja tu nitakupeleka Cate's hotel iko kariakooo." Aliongea dereva tax kwa kingereza cha kuunga unga baada ya kupokea mizigo ya mteja huyo na kuipaki sehemu maalum.
"Mbona kunajoto sana huku?"
"Aaaah! Kawaida tu mchizi,” japo alielewa swali hilo ila alishindwa kulielezea vizuri.
Kwakuwa kutoka uwanja wa ndege na kariakoo sio mbali sana walijikuta wakitumia dakika kumi tu kufika hapo na hiyo ilichangiwa kutokuwa na foleni njiani .alimlipa na kuingia ndani ya hoteli hiyo nzuri iliyopo mtaa wa Swahili.
******
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Rhoda mbona huoneshi furaha mama?" Aliuliza Rodrick wakiwa ndani ya ndege baada ya kumuona Rhoda akiwa kimya muda wote toka walipoianza safari yao mida ya saa kumi jioni.
"Noooo ! Nipo sawa tu ila nasikia tumbo likiniuma kwa mbali sana.
"Pole sana mke wangu!" Rodrick alijikuta akitoa neno hilo kwa mara ya kwanza baada ya kukumbukia tukio la jana usiku walilolifanya chumbani kwa Rhoda baada ya Rhoda kuumwa na nyigu hali iliyopelekea Rodrick kukimbilia chumbani huko akiwa na boksa tu.
"Aaaah! Oky sawa." Rhoda alijibu kwa sauti ya chini iliyobeba aibu ya kike kike ndani yake achilia mbali woga wa kumtazama Rodrick machoni.
"Tukifika nyumbani nitakupeleka hospitali,"akamweleza huku akimshika mkono na kumnyanyua kisha wakaanza kutoka nje.
Mishale ya saa mbili usiku ndege iliyokuwa ikitokea mkoani Mwanza ilionekana ikihangaikia kutafuta usawa wa kutua vyema katika uwanja mkuu wa mwalimu Nyerere mara baada ya kutolewa tangazo kwa abiria wote kufunga mikanda , iliinama upande wa mbele huku matairi yakiwa yameshaanza kuchomoza kwa kasi sana ilitua chini ikaanza kuseleleka taratibu kabla ya kusimama. "Tumefika mke mwema.”
“Mmh!" Rhoda aliishia kuguna kisha alinyanyuka taratibu akisidiana na Rodrick. Taratibu walitoka ndani ya ndege hiyo na kuiendea sehemu ya kuhifadhia mizigo yao walikabidhia na kutoka nje ya uwanja huo,mara baadaya ya taratibu husika kufuatwa.
"Waooooooo! Rodrick my bro," ilikuwa sauti ya Pamela dada yake mkubwa aliyekuwa anapatana sana na Rodrick alikuwa amekuja kumpokea. "Niambie?" "Poa mambo poleni na safari na karibuni sana." Baada ya salamu hizo wote waliongozana hadi kwenye gari la Pamela na safari ya kuelekea masaki nyumbani kwao Rodrick ikaanza iliyokuwa imetawaliwa na vicheko , utani na furaha kwa wanadugu hao. Hata walipofika nyumbani nako walikaribishwa na furaha ya ajabu iliyomshtua hata Rhoda maana toka akue hakuwahi kukutana na familia yenye upendo wa aina hiyo.
"Wazazi wangu huyu hapa mbele yenu ni mmoja wa rafiki yangu mkubwa sana na ndiye yule binti niliyekuwa nikihangaikia kesi yake mwanza." Rodrick alitoa utambulisho kwa ndugu zake mara baada ya kukaa.
"Oooh! Vizuri sana mwanetu na binti karibu nyumbani jisikie uko nyumbani." "Ahsante mama." "Pia ....." Rodrick aliendelea.
"Huyu ndie atayekuja kuwa mke wangu.” "Nini? Wewe mjinga hilo halipo na mtoto wa mzee makelele je?" "Nilishaga waambia simpendi hata siku moja huyu ndiye changuo langu," aliongea Ridrick kwa hasira akimanisha kile alichokuwa akikizungumza. "Sawa baba huyu binti anaelimu gani?" "Hana elimu lakini.." "Hakuna cha lakini hapo elimu yote hiyo unaenda kuoa mwanamke ziro kichwani! Hakufai naomba uachane naye na uwe na Alvia mwanamke msomi anauwezo na ni mzuri sio hiki kikaragosi chako!" Mzee Steven alizidi kutoa maneno makali bila kujali yanamaumivu gani ndani ya moyo wa Rhoda na Rodrick. "Nasema kwa hilo sitaki." "Lakini baba Pamela hali ilishabadilika je wewe ulichanguliwa?" Mama yake alidakia lakini alikatishwa. "Sitaki wewe binti achana na mwanagu na tena..,." kabla hajamalizia kuongea Rhoda alisimama kwa hasira na kutoka nje ya nyumba hiyo usiku huo huo na kuanza kukimbia asikokujua mbele kidogo aliona daladala ambalo hakujua linaelekea wapi alipanda na kutulia akili yake ikizidi kuvurugika sana. "Oyaaaa mdada toa mchango," koda wa daladala hilo alianza kukusanya pesa. "Nitakupa!" "Mie naishia kariakoo." "Nitakupa!" Rhoda alijibu kwa mkato huku kichwa chake kikiwa kimetawaliwa na mawazo chungu zima.
Kutokana na kutokuwa na foleni sana daladala hiyo ilitumia dakika ishirini tu kufika kariakoo. Haraka haraka Rhoda alishuka na kujichanganya katika abiria waliokuepo hapo hali iliyopelekea koda kutomuona kwakuwa hakuwa mwenyeji mji ule alijikuta akizunguka zungukuka hadi saa tano usiku asijue pa kwenda. "Acha nikakae pale," aliwaza hayo kisha alianza kulikatisha barabara bila kuangalia vyema hali iliyopelekea kugongwa vibaya na tax iliyokuwa ikija kwa kasi. "Ooh! Mungu wangu umeuaaa?"
Aliongea Dk. Maycon aliyekuwa ametoka kidogo ndani ya hoteli aliyokuwa amefikia. "Simama!" "Hapana siwezi niache," dereva tax alizidi kuongeza mwendo hali iliyopeleka daktari huyo kumkamata kwa nguvu akizuia gari hilo lisizidi kusonga mbele.
“Una akili gani wewe kwanini unakuwa na moyo wa kinyama namna hiyo?Huyo uliyemfanyia unyama huo si ni mtanzania mwenzako,”alizungumza kwa ukali kidogo akiwa amekimanisha kile alichokuwa akikizungumza.
“Nafahamu kaka ila nahofia kufungwa tafh…,”
“Kwahiyo wewe unajari uhai wako tu naomba usimame hapo nishuke huna akili kweli,”akazidi kuzungumza huku mkono wake wa kulia ukishika mlango wa gari hiyo kwa lengo la kuufungua. "Mungu wangu sijui atapona!" Alijikuta akiongea peke yake baada ya kumfikia Rhoda aliyekuwa hajitambui, sehemu kubwa ya mwili wake ikiwa imetapakaa kwa damu.
"Msaada..Nisaideniii.. ”Alianza kupiga kelele baada ya kuona gari likija upande wa kushoto. "Ridrick tumsaidie huyo." "Hapana Pamela nahitaji kumpata Rhoda usiku huu huu akiwa hai ama la!" Aliongea Rodrick na kuongeza mwendo bila kujua kama aliemuacha pale alikuwa Rhoda .
"Watu weusi bhana hawana hur...."hata hakumalizia sentesi yake aliona gari jingine alilisimamamisha."Tafadhali nahitaji hospitali ya karibu." "Sawa acha nikupeleke Regency hospitali,” aliongea mwarabu huyo huku akisaidiana na Dk. Maycon kumuingiza Rhoda ndani ya gari lake la kisasa .
"Ahsante sana naitwa Dk. maycon kutoka marekani nimefurahi kukutana na wewe,” aliongea Dk maycon baada ya kumfikisha Rhoda hospitali na kuandikisha kila kitu. "Usijali naitwa Abdullahman.”
Baada ya utambulisho huo Abdullahman aliondoka na kumuacha Dk maycon akiendelea kusubili majibu ya mgonjwa wake ambaye bado alikuwa hajamfahamu . Baada ya lisaa limoja mlango alioikuwa ameingizwa Rhoda ulifunguliwa na machela iliyokuwa imebeba mtu akiwa amefunikwa gubigubi tena ikiwa imelowa damu ilisukumwa kwenda chumba cha kuhifadhia miili hali iliyopelekea Dk kuingiwa na hofu.
"Tafadhali nesi nataka kujua mgo..."likatishwa. "Subili." Dakika tatu mlango ulifunguliwa tena na Dk. Rahman mwenye asili ya kiarabu alitokezea huku akiwa amesinyaa uso. "Niambie?” Aliongea Dk Maycon baada ya kumfikia. "Mmh... Pole.
”Akasema huku akizidi kutembea na kumuacha Dk.Maycon eneo hilo akiwa hafahamu cha kufaya.
"Pam!"Aliita Rodrick akiwa amekiinamisha kichwa chake katika usukani baada ya kupaki gari hilo maeneo ya Buguruni shel usiku wa saa nane,
"Abee kaka!"
"Kwanini baba aninifanyia hivi?"
"Hata sijui ila jipe moyo kama uliweza kumpigania Rhoda katika gumu lile hadi akashinda na leo yupo huru kwa nguvu zile zile endelea kulitetea penzi lako hata kwa kuutoa uhai wako!"
"Kwe...li..ila.."
Rodrick alishindwa kuvumilia na kujikuta akitoa machozi mbele ya dada yake ambaye hakuamini kuyaona machozi hayo.
"Usilie wewe ni mwanaume jikaze na lilia moyoni acha kutoa chozi lako hadhalani endelea na safari yako tena ikibidi uongeze kasi usikubali baba autumie moyo wako kama wake japo ana maamzi kama mzazi ila huwa yanamipaka ukizingatia wewe ni mtu mzima tayari una kazi yako na unajitegemea usilie washa gari tuendelee katika safari ya ukombozi ni muda wako sasa twendee!" Akamwambia huku akimiga piga mgongo wake na kukiinua kichwa cha kaka yake.
Rodrick alijikuta akipata nguvu mpya ndani ya moyo wake baada ya kusikia maneno hayo aliwasha gari na kuanza kumtafuta Rhoda ambaye hawakujua yuko wapi japo ilikuwa kama kuigiza kwa kitendo chao cha kumtafuta Rhoda ndani ya mji ule lakini walijipa moyo.
"Tumezunguka sana cha kufanya tutoe taarifa katika vyombo vya habari na tumalizie katika mahospitali!"
"Hilo la taarifa liko poa lakini la mahospitali mmmh!
"Kwanini Pam?"
"Rhoda hajafa bhana usiwaze hivyo."
"Ila acha tufanye tu!" Kweli usiku huo wa saa kumi na moja walianza kupita katika mahospitali mbalimbali wakianzia hospitali ya Temeke na hata zile ndogo ndogo za binafsi hadi inatimia saa nne asubuhi walikuwa wameshakangua hospitali zaidi ya kumi na tano.
"Ahsante dada acha niende nikalale kidogo kwa rafiki yangu."
"Kwanini usiende nyumbani?"
"Kwenda huko hadi Rhoda apatikane!"
"Haya."
Waliagana kisha kila mtu akaenda alikokujua wakiwa na miadi ya kukutana saa nane mchana kuendelea na zoezi lao.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
******
"Tafadhali Dokta nataka kujua anaendelea kabla sijaondoka ni." Dk. Maycon aliongea maneno hayo huku akiwa anamfaata Dk. Rahman kwa nyuma hadi ofisini kwake amabako aliketi na kumuonesha Dk. Maycon sehemu ya kukaa.
"Kabla ya yote ninaweza kusema pole mgo.” Alikatishwa
"Unataka kuniambia kwamba mgonjwa wangu amekufa?”
“Ndio, ilikuwa ajari mbaya sana kwake.”
Kwa mara ya kwanza Dk. Maycon alidondosha chozi mbele ya daktari huyo wa kiarabu roho ilimuuma sana kumpoteza msichana huyo ambaye hata sura yake hakuifahamu vyema.
"Usilie kila kitu ni sawa kwa mungu nakuomba umuombe,” japo Dk. Rahman alijitahidi kumbembeleza sana lakini hakunyamaza.
"Sawa daktari mwenzangu nakushukuru kwa yote uliofanya kwangu ,nikutakie maisha marefu."
Alionge Dk. maycon akiwa anaondoka ndani ya hospitali hiyo majira ya saa nane usiku.
Baada ya kutoka hapo alichukua tax iliyompeleka Cate's Hotel alionga na kupumzika huku kichwa chake kikiendelea kutawaliwa na zigo la mawazo hadi inatimia saa kumi na moja za asubuhi alikuwa bado hajapata hata lepe la usingizi.
"Ndio ilikuwa ajari mbaya sana kwake. " Kumbukumbu ya maongezi kati yake na Dk Rahman ilirejea tena.
"It might be she is not her ,my patient was a lady let me go there again(Yawezekana akawa sio yeye mgonjwa wangu alikuwa msichana),” aliwanza hayo na kunyanyuka kitandani alishuka ngazi mbili mbili kisha alichukua Tax iliyompeleka Regency hospitali.
"Dk Rahman bado yupo?"
"Ndio!"
"Nataka kuonana naye.”
"Subili kidogo anatazama wagonjwa.”
Yalikuwa ni maongezi kati ya nesi aliyekuwa mapokezi na Dk. Maycon aliyekuwa amerudi hospitalini hapo kujihakikishia kama aliyekuwa amekufa ndiye waliyemgonga usiku wake.
"Naweza nikakuliza msichana?”
"Uliza)"
"Jana ni..," kabla hajauliza swali lake Dk. Rahman alikatisha hapo hali iliyopelekea Dk. Maycon kumfuata.
"Wewe tena?”
"Ndio daktari nina swali dogo kwako”
" Kwanza keti”
Wote wakaongoza kuelekea ofosini huko ndiko mwenyeji wake alikodhamiria kuzungumza naye si njiani kama yeye alivyokuwa anataka. Akafika na kukaa kisha akamuonyesha sehemu yay eye kukaa lakini mwenzake akagoma alichotaka ni kuelezwa kile kilichomrudisha hospitalini asubuhi hiyo.
“Jana nilileta mgonjwa hapa wa ajari sijui unakumbuka?” Akasema huku akimtazama usoni macho akiwa ameyakaza, bila kupepesa hata ukope.
“Ndiyo!”
“Wakike ama wa kiume?”
“Wa kike.”
“Unauhakia?”
“Ndiyo.”
“Nisubili naje.”
Akamjibu na kutoka nje dakika mbili akarejea na faili, akalifungua na kuangalia watu walioandishwa usiku wa jana hususani wale waliopata ajari
“Kuna watu wawili hapa mmoja hajatambulika jina.”
“Wa kike?’
“Ndiyo.”
“Huyo huyu,”akajibu kwa harakaharak tena akisimama juu, aliamini huyo ndiye aliyekuwa mgonjwa wake.
“Ukimuoana utamfahamu?”
“Ndiyo!”
“Nifuate.”
Mbele Dk.Rahma nyuma Mzungu ambaye hakuwa na uhakika kama kweli mtu aliyekuwa akizungumziwa alikuwa yeye, ila kunakitu kilichokuwa kikimueleza kuwa huyo ndiye, hawakutumia dakika hata dakika nne wote wakasimama mbele ya kitanda, moyo wake ulilipuka mithili ya bomu mara baada ya uso wake kushuhudia sura ya Rhoda mtu aliyekuwa akimtafuta kwa udi na uvumba na ni huyo huyo aliyemgonga usiku wake.
“Kwanini ulinidanganya?”
“Kuhusu?
“Kuwa amekufa yet mzima!”
Akajiuma uma na kukosa cha kuzungumza akakumbuka kosa alilolifanya ni kuchanganya mafile hicho ndicho kilichokuwa kimetokea.
“Uhakika wa kupona lakini upo?”
“Ndiyo.”
"Inatosha kwangu."
Baada ya maogezi hayo wote walirudi ofisini kwa mazungumzo zaidi, Moyo wake ulifurahi sana aliamini ajari hiyo ilikuwa na maana yake, japo Rhoda alikuwa katika hali mbaya na yenye kutisha ila aliamini atapona tu
"Kwahiyo hapa hawezi akapona?" Mazungumzo yakaanza mara baada ya wote kufika ofisini.
"Ndio damu iliyovujia ndani ya ubongo ni nyingi sana tukipata msaada serikalini tutamsafirisha nje ya nchi!"
"Nipo ladhi kuondoka naye tena leo leo hii kama itawezekana!"
Aliongea Dk. Maycon akiwa hana utani kabisa baada ya kurudi ndani ya ofis ya Dk. Rahman.
"je ninaweza nikapata ndege ya kukodi kweli?"
"Mmmh! Tanzania yetu hii sidhani ila acha niongee na rafiki yangu!"Alimueleza huku akiitafuta simu yake na kupiga sehemu alikyokuwa ameikusudia.
Hapo hapo alichukua simu yake
"Hallo!"
Sauti nene ya kiume iliyokatishwa usingizi ilisikika upande wa pili.
"Juma kwa leo ninaweza nikapata ndege ya kukodi mpaka Nairobi?"
"Aah! sidhani kwani ni shida ya muhimu sana?"
"Ndio!"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilibidi Dk Rahman atoe sababu.
"Sasa nitaongea na mzungu aliyekodi kwenda somalia awasaidieni!"
"Tutashukuru sana!"
Baada ya maongezi hayo Dk Maycon aliondoka hospitalini hapo akiwa na miadi ya kuonana saa tatu ili kufatilia visa ya Rhoda aliyekuwa anapelekwa Marekani kwa mara ya pili.
******
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment