Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

NIMEIPATA FURAHA YANGU - 5

 







    Simulizi : Nimeipata Furaha Yangu

    Sehemu Ya Tano (5)



    "Rodrick mbona macho mekundu?"Aliuliza Maiko mwanafunzi aliyekuwa akisomea udaktari na alikuwa akifanya mazoezi ya kazi hiyo katika hospitali ya Regency baada ya kurudi nyumbani kwake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Acha tu Maiko unamuona huyu?"

    Rodrick alitoa picha ya Rhoda

    "Ndi..oo!"

    "Vipi?"

    "Namfananisha na msichana aliyeletwa siku tano nyuma hospitali akiwa amepata ajari na nimeacha akiwa anaandaliwa kwenda marekani kwa matibabu!"

    "Anaitwa nani?" Rodrick aliuliza kwa shauku.

    "Aliyemleta alidai anaitwa Rhoda Jackson na alidai kumfahamu."

    "Nipeleke,"akasema huku akisimama tayari kwa safari ya kuelekea hospitalini hapo kuzuia safari ya watu hao.

    Hawakuwa na muda wa kupoteza tena wote waliingia ndani ya gari la Rodrick na safari ya kwenda Regency ikaanza kumi na tano tu walikuwa hospitalini hapo.

    "Tunamulizia Dk, Rahman?"

    "Amelekea airport!"

    "Ameondoka na mgonjwa?"

    "Ndio!"

    "Mungu wangu!"Alisema Rodrick huku mikono yake yote ikikishika kichwa chake, mapigo ya moyo wake yakizidi kuongezeka na mwili wote ukiishiwa nguvu kabisa dalili za kumkosa Rhoda zilikuwa waziwazi.

    Walitoka mbio mbio hadi walikokuwa wamepaki gari lao wakiwa na lengo la kuizuia safari hiyo .

    Walijikuta wakitumia dakika thelathini kutoka hospitalini hapo hadi buguruni kutokana na foleni iliyokuwa imesababishwa na gari la mafuta lililokuwa limedondoka na kuziba njia hali iliyopelekea Rodrick kuchukua bodaboda ili awahi.

    "Wew kijana mbona hivyo?"

    "Nisamehe afande ninahitaji kuzuia safari nisaidie!"

    "Pole sana tegeneza bango!"

    Askari wa getini alitoa wazo hilo huku akimpatia karatasi kubwa na markpen alichora jina la Rhoda na kuanza kukimbia kuelekea ndani.

    "Hiyo inaelekea wapi?"

    "Nini?"

    "Ndegeee!"

    "Imekodiwa inaelekea Nairobi.”

    "Mungu wangu!" Aliiruhusu miguu yake kuikimbilia lakini kabla hajaifikia aliona inaseleleka huku ikiongeza mwendo na kupaaa mbele ya macho yake

    "Rhodaaaaaaaaaaaaa!"Aliita kwa sauti ya juu sana huku akikaa chini mwili wote ukiishiwa nguvu kabisa tumaini la yeye kumuona tena Rhoda likaanza kuyeyuka ndani ya moyo wake.





    Wakiwa ndani ya ndege hiyo Dk. Maycon alikuwa karibu kabisa na Rhoda akihakikisha kuendelea kumpatia matibabu madogo madogo , alihakikisha mashine ya oxygen ikifanya kazi yake vyema dripu za maji na damu nazo zilikuwa sawa.

    "Mie nitakuacha Nairobi!"

    "Haina shida nilishaandaa ndege."

    Masaa kadha ndege hiyo ilitua katika uwanja wa ndege wa nchini Kenya kwa kusaidiana na wafanyakazi wa uwanja huo walimshusha Rhoda ndani ya ndege na kumpakiza ndani ya ndege nyingine iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya safari hiyo kisha safari ilianza bila kupoteza muda.

    "Nataka upone haraka sana nifunge ndoa na wewe!"

    Aliwaza Dk. Maycon akiwa anamtazama Rhoda aliyekuwa amelala kama mfu lakini uzuri wake ulizidi kuongezeka. Ndani ya ndege hiyo hakukuwa na watu wengi zaidi ya Rhoda , Dk maycon na Rubani aliyekuwa bize na kazi yake.

    "Helooo!"

    "Yaah! Nakusikia hapo wapi?"

    "Sijui… sijui."

    Yalikuwa ni maogezi kati ya Rubani huyo na baadhi ya wafanyakazi wa uwanja wa ndege Cameron ambapo ndege hiyo ilikuwa ikitua kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya sana.

    "Please i need to reach America immeditely (Tafadhali nahitaji kufika marekani haraka sana)”

    “Lakini bwana ona..”

    "Acha kunitania , nina mgonjwa nitafanya nini hebu angalia utaratibu mwingine utakaonitoa mimi hapa,” aliongea Dk Maycon kwa jaziba na aliona anafanyiwa usanii.

    "Hapana bwana siwezi nikaendelea tusubili kwa muda.”

    "Okay acha mimi niondoke!”

    Japo idadi kubwa ya watu ilimzuia kuondoka lakini alilazimisha kuiogoza ndege hiyo bila kujali tatizo lilokuwa agani. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Wasinione mshamba ndege najua kuendesha kwetu ndo zilikuwa baskeli!" Dk. Maycon aliwaza hayo akiwa anaiselelesha taratibu baada ya kumfunga vyema Rhoda kabla ya kupaa taratibu ilianza kupaa na potelea angani huku nyuma kila mtu hapo Cameron akimsikitikia.

    Akiwa angani aliweza kuimudu vyema ndege hiyo na kujiona mshindi lakini ghafla hali ya hewa ilibadilika upepo mkali ukaanza kuiyumbisha yumbisha.

    "My God!( mungu wangu!)"

    Alishtuka sana baada ya bawa moja kugonga wingu zito hali ikiyopelekea ndege kuanza kushuka chini kwa kasi ya ajabu haukupita muda upepo huo ukaambatana na mvua kubwa sana iliyosababisha Dk. Maycon kutokuona mbele.

    "Am really sorry Rhodaaa!”



    Alitamka neno hilo baada ya kuona ndege hiyo ikiendelea kupoteza mwelekeo haraka haraka aliondoka sehemu ya kuiongozea na kukimbilia upande uliokuwa na maboya alichukua moja kubwa na kumfunga nalo vyema Rhoda lakini akiwa katika harakati za kujifunga na yeye ghafla aliona Rhoda akirushwa nje kupitia dirishani sehemu iliyokuwa imepasuka na kuacha uwazi mkubwa.

    "Rhodaaaa! " Aliita kwa sauti ya juu sana baada ya kushuhudia Rhoda akitumbukia ndani ya bahari ambayo hakujua ni bahari gani dakika mbili ndege nayo ilitumbukia ndani ya bahari hiyo.

    ******



    "Rhodaa!"

    Rodric aliita kwa sauti ya juu sana hali iliyopelekea kila mtu aliyekuwepo hapo kumshangaa.

    "Why me? Why?( kwani mimi? kwanini?)”

    "Vipi kijana?" Mwanaume aliyekuwa amevalia koti la kidaktari aliuliza baada ya kumuona Rodrick akilia hadhalani.

    " Rho.....Rhodaaaa!"

    Alishindwa kuongea vizuri baada ya kuzidiwa na kwikwi , hakujali kukusanya watu ama kutoa chozi lake hadhalani ukizingatia mwanaume taratibu alishindwa kusimama kutokana na miguu kuishiwa nguvu alishuka chini kama mzigo na kupoteza fahamu.

    "Ndugu wa nani?" Aliuliza Dk. Rahman aliyekuwa akiongea na Rodrick .Lakini hakuna aliejitokeza.

    "Ana tatizo gani?"

    "Ilikuwa ni plesha tu , ila tumemtundikia dripu ya glucouse atakuwa sawa muda si mrefu." Aliongea Dk Erick baada ya kutoka kumhudumia Rodrick aliyepelekwa hospitalini hapo na mwanaume huyo.

    "Acha niwasiliane na ndugu zake!"

    Dk. Rahman alichukua simu ya Rodrick na kutoa taarifa hiyo.

    "Yuko wapi?"

    " Eyes peace dispesary huku banana."

    "Nakuja sasa hivi !"

    Baada ya Pamela kukata simu alianza kuelekea banana baada ya kutoa taarifa hiyo kwa ndugu zake na kwa wazazi wake ambao walifika haraka sana hospitalini hapo.

    "Pole mwanangu ilikuwaje?"

    Mama yake aliuliza baada ya kufika hospitalini hapo.

    "Namhitaji Rhoda !"

    "Pole sana ipo siku utaonana naye tu muom.....?"

    "BBC Landon , habari zilizotufikia punde

    Msomaji wako ni Salim kikeke ndege moja kutoka nchini Kenya imedondoka katika bahari ya Altratic kusini mwa marekani na imesemekana kuua watu wote waliokuwemo mwana habari wetu Zuhura Venus anataarifa kamili."

    " ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la usafiri wa anga International Civil Aviation Oganization (ICAO) ikiwa chini ya nchi za Afrika mashariki na kusini mwa Afrika katika ofisi zilizoko Nairobi Kenya imedondoka katika bahari ya Altratic chanzo kikiwa ni hali mbaya ya anga iliyopelekea ndege hiyo kupigwa na wingu zito hali iliyopelekea rubani wa ndege hiyo Dk Maycon kushindwa kuiongoza , mbaye naye amefariki mwili wake tayari umehifadhiwa katka hospitali ya Misssipi kusini mwa marekani pia baada ya uchunguzi uliofanyika ndani ya ndege hiyo kumeonekana vyeti vya mwanamke aliyekuwa akipelekwa nchini marekani kwa ajili ya matibabu ambaye ni Rhoda Jackson Raia wa Tanzania."

    "Zuhura hebu tuambie huyo daktari ni raia wa wapi?"

    "Kikeke inasemekana ni raia wa marekani."

    "Je huyo mgonjwa wa Tanzania yupo wapi?"

    "Hadi muda huu haifahamiki aliko maana kitanda chake kimo ndani ya ndege na haijulikani kama yupo hai ama la! Ila kikeke tuombee uzima, maana tayari ndege hiyo imeshatolewa ndani ya maji na wazamiaji wanaendelea kumtafuta.

    "Ahsante sana Venus."

    "Okay "

    " Naam mpenzi mtazamaji na msikilizaji wa BBC endelea kutufatilia ili uweze kujua nini kinaendelea Salim kikeke BBC London."

    Ilikuwa ni taarifa iliyoishtua mioyo ya kila mmoja ndani ya chumba alichokuwa amelazwa Rodrick ambaye alikuwa akiendelea kulia na safari hii alikuwana maumivu yaliogezeka zaidi.

    "Rodrick kwanini umeamua kumua Rhoda?"

    "Hapana mzee Hashim nini Ba...!" Alijikuta akiitazama simu hiyo huku machozi yakiongezeka kulowanisha mashavu yake na kubaki kumtazama baba yake aliyengia ghafla akiwa ameivuta sura.



    "Triii! Triiii!" Simu ya Rodrick iliita tena na mpigaji akiwa yule yule mkuu wa gereza la Butimba akimshutumu Rodrick kwa kumuua Rhoda .

    "Ha haloo!"

    " Rodrick kwanini unamfanyia haya Rhoda si ni bora ungemuacha huku huku aaaaah!" Aliongea mzee Hashm kwa jazba.

    "Nipe nusu saa nitakujibu!" Kisha alikata simu na kumtazama baba yake kwa jicho la hasira.

    "Wewe kijana mbona unakuwa na kichwa kigumu kama nazi?"

    "Baba kwa hili acha nikudharau kama unaona nafanya hivyo ila siko tayari kumuoa Alvia na endapo Rhoda atakufa bora nitafute mwingine ila sio kutafutiwa kama ni radhi nipe !" Rodrick aliongea maneno hayo huku akinyanyuka kitandani.

    "Na kurudi kwako nitarudi nikiwa na Rhoda ama nikiwa ndani ya jeneza umenifanya nikaonekana katiri kwa Rhoda hata kwa mzee wangu Hashim,"alizungumza kwa hasira huku akimtazama mazazi wake huyo wa kiume mfano wa mtoto mwenzake.

    "Paaa!" Aliubamiza mlango na kuondoka huku akiacha kila mtu akiyazungusha mawazo yake ndani ya bongo zao.

    "Lakini mume wangu mbona unamnyima haki mtoto?"

    "haki ipi? Hujui mila na desturi zetu sisi ni wanyatunzu bhana lazima kila mtu afuate!"

    "Lakini dady ...mb..."

    "Funga kopo lako Pam na uondoke hapa!"

    "Lakini mzee mwenzangu unakosea!"

    Ilibidi Dk Rahman adakie. "Nyie hamjielewi kabisa !" Mzee Steven alinyanyuka na kuondoka

    "Nitamsaidia Rodrick!"

    "Hata mimi!!!!!" Kila mtu alimuunga mkono Dk. Rahman kisha walisambaratika hispitalin hapo.

    "Maiko kesho naenda kumtafuta Rhoda!"

    "Utampata wapi? Ungesubili kwanza taarifa zitolewe na ijulikane kama yuko hai ama la!"

    "Siwezi bora na mimi nikafie huko huko sioni sababu ya kuishi bila Rhoda nahitaji kumuomba msamaha!"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ni kweli ila vuta subila!"

    "Siweeeezi Maiko,mimi nakula na kulala vizuri sijui yeye yukoje na isitoshe alikuwa mgonjwa acha niende!" Alinyanyuka katika kiti alichokuwa amekalia na kuanza kuzunguka zunguka sebuleni hapo , mara simu yake iliita.

    "Dk. Rahman hapo hebu njoo huku kinodoni studio!"

    "Nakuja!" Hata hakujali kuoga alichukua gari lake na kuelekea huko.



    ****

    "Nimekuita hapa nikitaka kukusaidia!"

    Dk. Rahman alianzisha mazungumzo baada ya Rodrick kufika.

    "Ahsante sana na kesho naenda kumtafuta Rhoda awe mzima ama la!"

    "Ni vyema nikakupa mchango wa asilimia hamsini na kuhusu tiketi usijali acha niongee na rafiki yangu hivi." Hapo hapo alichukua simu na kuongea na mtu wake.

    "Usijali kesho ajiandae kwa safari mida ya saa mbili usiku," baada ya taarifa hiyo kupewa naye alimpatia Rodrick hali iliyopelekea furaha isiyo na kifani.

    "Habari wasafiri nawaomba mfunge mikanda !" Sauti ya msichana iliyokuwa ikitokea katika spika zilizokuwemo ndani ya ndege hiyo ilipenya moja kwa moja katika ngoma za masikio ya Rodrick aliyekuwa akiwaza na kuwazua ugumu wa safari yake lakini hakutaka kukataa tamaaa.

    "Mungu atanipigania na kunionyesha njia kama alivyowaonesha wana waisrael."

    Aliwaza hayo na kutulia.



    *******



    Boya alilokuwa amefungwa Rhoda lilikuwa kubwa sana hali iliyopelekea asiguswe na maji hata alipotua juu ya bahari hiyo kubwa , alibaki amelala akiwa hajui alikokuwa japo mvua ilikuwa ikiendelea kunyesha lakini maji yake hayakuweza kumfikia kutokana na kava la boya alilokuwa amevalishwa juu yake .

    Kasi ya maji ilikuwa kali sana hivyo alijikuta akipelekwa umbali mrefu sana kutoka hapo alipotumbukia.

    "Hebu oneni hapo!"

    "Kunanini ?"

    "Kitu kama mtumbwi kinaelea!" Yalikuwa maongezi ya wavuvi waliokuwa wakitoa nyavu zao usiku wa saa tisa waliongea kwa lugha ya kibrazilia.

    "Acha tukaone!" Hapo hapo waliwasha mashine yao na kuanza kufatilia kitu kilichokuwa kikielea.

    "mtu!Mtu!"

    “Kweli? Ndio!" Hawakuwa na muda wa kupoteza walimpakiza ndani ya chombo chao na kumkimbiza katika hospitali iliyokuwa ndani ya kijiji hicho ambacho kilikuwa cha wanaume hamsini tu kazi yao ikiwa uwindaji na uvuvi hawakuwahi kuishi na mwanamke zaidi ya miaka hamsini kutokana na kibuga kilicho ikumba nchi ya Brazil hali iliyopelekea wao kuwa pale , walikuwa wafupi na wenye nguvu nyingi sana , daima hawakuwa na desturi ya kuvaa shati walikuwa wakikaa kifua wazi na kufanya miili yao hasa sehemu ya vifua vyao kuonekana vyema ,hivyo kupatikana kwa Rhoda ilikuwa sherehe kwao na walihakisha anapona ili awazalie watoto

    "Akipona tu naanza mimi !"

    "Wapi hakuna kitu kama hicho mimi ndiye niliemuona!" Walibishana sana bila kupata mwafaka wakiwa ndani ya kihospitali kilichokuwa kikitumia matibabu ya dawa za kienyeji chini ya daktari Chan mchina aliyekuwa akiishi kisiwani humo.

    "Nice woman !" Dk Chan aliongea huku akitabasamu baada ya kumaliza kutoa huduma kwa Rhoda na kwa kutumia vipimo vyake hivyo aliweza kutambua tatizo la Rhoda .

    Kwa dawa zake ingechukua siku chache kupona

    "Sasa ninyi ondokeni kesho mtakuja asubuhi kumuona !"

    "Aya !!!" Walijibu kwa unyonge kisha walianza kutembea taratibu na wakitumia kuruzi kubwa zilizokuwa na mwanga mkali sana .

    Kila mmoja alijitupia juu ya kitanda chake kilichokuwa kimeshikiliwa na nguzo nne ambazo zilikuwa zimechomekwa aridhini na kuutafuta usingizi .

    ******



    Ndege aliyokuwa amepanda Rodrick ilitua nchi mbili tu Kenya na Cameron ambako alilala na siku iliyofuatia alitafuta helkopita aliyoitumia kusafiri hadi sehemu ya tukio.kwa kuwa lilikuwa tukio kubwa sana ilikuwa rahisi kufika hapo.

    Hakuamini macho yake baada ya kukuta idadi kubwa ya watu.

    "Am Rodrick brother to that girl who lost at this fly crushed (Naitwa Rodrick kaka yake na dada aliyepotelea kwenye ndege iliyodondoka,)” aliongea Rodrick na mmoja wa askari waliokuwepo eneo hilo.

    "Okay what should i do for you (Sawa nikusaidie nini ?)"

    "Am here to look her ( nimeku kumtafuta )."

    "Okay just wait a moment i do speak with those who are going to check her ( sawa subili kidogo nifanye kuongea na wanaoenda kumtafuta).”

    Askari huyo aliwafuata wazamiaji na kuongea nao na baada ya nusu saa walianza safari ya kumtafuta Rhoda lakini hadi inaingia jioni hawakubahatika kumpata kila siku walikuwa wakiendelea na zoezi hilo na jibu lilikuwa lile la Rhoda kutopatikana .

    Zilipita wiki tatu bila matokeo hivyo serikali ya Brazil ikaamuru kutoa wanajeshi maji na kila kitu na kumuacha Rodrick peke yake eneo hilo lilokuwa na kipori chenye wanyama wakali maana aligoma kuondoka .



    Hakika yalikuwa maumivu makali sana ndani ya moyo wa Rodrick akiwa anatazama jinsi helkopita zilivyokuwa zikijiandaa achilia mbali wanajeshi wote walivyokuwa wakiondoka kwa furaha eneo hilo , macho yake yalijaa machozi na gumi nzito ya maumivu ndani ya moyo wake.

    "Sitoweza kuondoka hapa bila Rhoda acha nifie huku huku kama ni kufa!" Aliwaza hayo huku akiendelea kuyatoa machozi ambayo alidhani yangeweza kumsaidia chochote ama kumrejesha Rhoda , mawazo nayo yalirudi nchini Tanzani kipindi cha nyuma akiwa na Rhoda mwanamke aliyetokea kumpenda na leo ameondolewa mikonini mwake tena na baba yake mzazi , hakuacha kumtupia lawama zote mzee wake kwa kitendo hicho .maneno yaliyokuwa hayana vipimo kutoka kwa baba yake ndio chanzo cha yeye kuwepo hapo porini alilia sana.

    Hadi helkopita zote zinapotelea hewani Rodrick alikuwa bado amesimama katika moja ya mti mkubwa uliokuwa na kivuli kikubwa wakati wa mchana , hakukuwa na kelele tena ama vurugu vurugu za watu kama ilivyokuwa muda mchache uliokuwa umepita , kelele zilizokuwa zikisikika zilikuwa za ndege ama wadudu tofauti tofauti ambao ndio walikuwa wameanza kutawala kwa kuzitoa sauti zao.

    Upepo mtulivu na mwanana nao ulichangia kupendezesha ,kijijua cha saa kumi jioni ambacho kilikuwa kikikimbia sana kuitafuta rangi ya kahawia , mkononi alishika picha mbili moja ya Rhoda akiwa gerezani na nyingine wakiwa airport wiki tatu nyuma , hakuacha kuzitazama macho yake yalikuwa yakitazama ile ya magereza hali iliyopelekea chozi kudondokea katika shavu la Rhoda

    "Hakika wewe ndo furaha yangu hapa duniani nakiri kwa kinywa changu kuwa nakupenda na sikuwahiwa kupenda hivi huko nyuma , nimekubali kuyapoteza maisha yangu kwa kuliwa na simba , chui ama kifo chochote nikitetea penzi langu kwako ambalo ni la dhati kokote uliko jua kuna mtu duniani anaekupenda ambae ni Rodrick acha nikutafute ili siku moja nije kuwa mshindi katika vita hii kali." CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikuwa kama anaongea na Rhoda kumbe alikuwa akiongea na picha

    "Acha niende!"

    Hapo hapo aliingia ndani ya hema na kuchukua kila kilichokuwa chake.

    “Safari ya ukombozi imeanza !" Aliwaza hayo huku akipaki darubini na bastola alizokuwa ameachiwa na mmoja wa wanajeshi ndani ya mifuko ya suruali , iliyokuwa na mifuko mingi mingi kuanzia mapajani kushuka chini pamoja na shati lake lenye rangi ya kaki kiatu kilichokuwa kikifanania na cha jeshi , begi mgongoni pamoja na kofia kichwani kisha alivaa na miwani ya jua alitoka nje.

    "Niende usawa upi?"

    Alibaki amesimama hapo kama dakika tano kisha alipata wazo ambalo lilikuwa mchezo wake wa utotoni alitema mate katika kigaja chake cha mkono wa kushoto na kuyapiga na kidole chake cha shahada akiwa na lengo la kuwa mate yatakakokwenda ndo aelekee.

    "Huku huku!"

    Hakupoteza muda alianza kuifuata njia iliyokuwa ikielekea kusini mwa bahari hiyo .

    Alitembea umbali mrefu sana bila mafanikio yeyote hadi kiza kinaingia alikuwa hajafanikiwa chochote , alipanda juu ya mti na kuutafuta usingizi ,na kesho yake alifanya hivyo hivyo hadi inakatika miezi nane hakuwa amempata Rhoda lakini roho ya kurudi nyumbani haikuwepo aliendelea kuamini kuwa yupo hai na anateseka sehemu fulani hata ngozi ya mwili wake ilikuwa imebadilika na kuwa nyeusi isiyokuwa na mvuto wowote ulaji wa matunda pori na mizizi tayari alikuwa ameshauzoea laiti ungemuona usingeamini kuwa alikuwa mwanasheria mkubwa nchini kwao.

    "Nitaishi huku huku porini nishazoea"

    Aliwaza siku moja asubuhi akiwa anaota kijua cha saa mbili.



    ******



    Dk Chan aliendelea kuhakikisha Rhoda anapona kwa muda mfupi sana tayari alikuwa ameshampatia dawa ya kutoa damu iliyokuwa imegandiana ndani ya ubongo wake , dawa hiyo ya kichina ilikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuponesha vidonda vyote mwili mzima hasa hasa kuulisha ubongo ili urudi katika hali yake ya kawaida.

    Pia hakuwa nyuma kwenye dawa za kurejesha kumbukumbu kwa haraka sana , siku tatu tu hali ya Rhoda ilianza kuleta matumaini kwani aliweza kutikisa baadhi ya viungo vyake vya mwili na baada ya wiki nne kupita alikuwa ameshapona kabisa na hata kumbukumbu zake zilianza kufanya kazi kama kawaida,

    "Niko wapi hapa?"

    "Yes?" Dk. Chan hakuelewa chochote alibaki kumtumbulia macho Rhoda aliyekuwa ameshikilia kikombe cha chai asubuhi moja.

    "Hili eneo gani ?

    “ Daduby nchini Brazil,”alijibu Dk chan naye akiwa anamimina chai ndani ya kikombe.

    "Heee!!!"Rhoda hakuamini ndipo hapo Dk. Chan alipoamua kumsimlia mazingira ya yeye kuwa eneo hilo.

    Waliendelea kuongea hadi wanakijiji walipokuja wakitaka kuondoka na Rhoda hali iliyopelekea Dk. Chan kuwakatalia kwani na yeye alikuwa ameshatokea kumpenda na tayari alikuwa ameshamzoea sana.

    "Bado hajapona endeleni kuleta nyama na samaki kwa wingi maana zitamsaidia sana!" Hilo ndilo lilikuwa jibu lake la kila siku .Rhoda naye hakuwa na jinsi alianza kuyazoea maisha hayo maana hakuona haja ya kurudi Tanzania na istoshe hakuwa na msaada wowte wa kumrudisha nchini kwake .pia Dk chan alikuwa akimfundisha mazoezi ya kuruka mito kupigana na wanyama na hata baadhi ya dawa alianza kumuelekeza.

    Baada ya miezi miwili kupita hali ya Rhoda ilianza kubadilika alianza kutapika usingizi wa kila mara ,uchovu na hata alianza tabia ya kubagua chakula ndipo hapo Dk. Chan alipoamua kumpima na kugundulika mjamzito.

    "Hii mimba ya nani?"Aliuliza Dk. Chan akiwa na hasira maana hakutarajia majibu hayo.

    "Mimbaa?"

    "Ndio.Tena ya miezi miwili!'

    "Sijui!" Alitoa jibu hilo huku taa nyekundu ikianza kuwaka ndani ya ubongo wake.

    "Mungu wangu itakuwa ya Rodrick !" Alikuwa ameshakumbukia tukio walilolifanya kipndi cha nyuma siku aliyoingiliwa na nyingu chumbani kisha Rodrick kukimbilia huko akiwa na nguo ya ndani tu.

    "Nitakupa dawa ya kuitoa!"

    "Hapanaa , acha nizae kisha nikuzalie na wewe usijali!" Ilibidi Rhoda atumie ujanja kwani mchina huyo hakuwa mtu wa mchezo kwenye maamuzi yake.

    Hivyo ndivyo walivyoamua kuishi hadi inakatika miezi nane walikuwa wakiishi katika hali hiyo hiyo.

    "Jamani kwanini mchina atuchukulie mke wetu!"

    "Mimi kila siku nawaelezeni kuwauwa hamtaki tumekwa mazoba kuwalisha na mbaya zaidi kampa mimba naenda kuwauwa ili tukose wote!"

    Alizungumza mmoja wa wanamume hao waliokuwa wameuzunguka moto usiku wa saa tano

    "Kweli twendeni!" Hapo hapo walinyanyuka na kuifuata nyumba ya Dk. Chan aliyekuwa hajui chochote.

    "Funguaaa!!!"

    Sauti hizo zilimshtua Dk. Chan alikuwa akilazimisha penzi kwa Rhoda.

    "Tumekufaa!"

    "Nini?"

    "Wanaka kutuua kisa niliwakatalia kuwa na wewe !" Aliongea Dokta kwa kunong'ona huku moyoni akiwalaani wanaume hao ambao walimkatili adhima yake.

    Alipofikiria uwezo wa watu hao alianza kutetemeka.

    "Tupee mkeee wetuuuu!!"

    "La sivyo tunakuuua!" Watu wale waliendelea kupiga kelele na safari hii walianza kuupiga mlango.

    "Nakupenda sana ila siko tayari kufa nakuomba uende kama utaweza kukimbia kimbia pitia mlango wa nyuma!" Aliongea Dk. Chan huku akimfungulia Rhoda mlango ambapo macho yake yalipokelewa nagiza tororo ambalo lilikuwa linatisha.

    "Nisaidie!"

    "Huo ndio msaada wangu kwako lasivyo nikutoe kwao!"

    "Siwezi ku..kukimbiaaa, tumbo linaniuma na nyonga zimebanaaa!" Aliongea Rhoda huku akianza kulia.

    "Okay naenda kuwafungulia nenda!"

    Hapo hapo alinyanyuka na kuueendea mlango mkubwa akiwa na lengo la kumkabidhi Rhoda mikononi mwa watu hapo.

    Rhoda alipoona hivyo alianza kukimbia asikokujua japo tumbo na nyonga zilikuwa zinasumbua lakini hakutaka kufia mikononi mwa watu hao , alijitahidi kukimbia lakini alijikuta akishindwa baada ya damu kuanza kuchuruzika huku akihisi kitu kigumu kutoka sehemu yake ya siri.

    "Rodrickkk!!!!"Alijikuta akitamka neno hilo huku akikaa chini ya mti mkubwa ambao juu yake alikuwemo Rod rick alikuwa amejipumzisha baada ya kutembea umbali mrefu .

    "nani ananiita!" Alijiuliza huku akiichukua bastola yake na kuikoki tayari kwa lolote, macho nayo hayakuwa nyuma kuanganza huku na huko lakini ilikuwa ngumu sana kutambua chochote kutokana na kiza.

    "Nani?"

    Aliuliza huku akimlika sehemu sauti hiyo ilikotokea sekunde kadhaa hakuamini macho yake baada ya kumuona mwanamke aliyekuwa na tumbo kubwa akilia kwa maumivu alishuka haraka sana juu ya mti.

    " Rhodaaaaaa?" Alitamka neno hilo baada ya kuhakikisha ni yeye.

    "Nakufaaa.. mpenziiiii.. mtotoooo.. anatokaaaa!" Baada ya Rhoda kujibu alijikuta akisukuma mtoto ambae alianza kulia kwa sauti hali iliyopelekea wale wanaume kuzidi kumfatilia Rhoda baada ya kumkosa kwa Dk. Chan hali iliyopelekea kumuua Dokta na kuanza kumfatilia Rhoda wakiwa na hasira sana.

    "Pole jikaze mama!"

    Aliongea Rodrick huku akimfunika mtoto kwa shati lake.

    "Mwingineee! Mara sauti ya kitoto kingine ilisikika na kumfanya Rodrick kuchanganyikiwa

    "Tulia hivyo hivyo!"

    Sauti ya wanaume zaidi ya arobaini ilisikika na wote waliwazunguka sura zao zikiwa na hasira sana







    Kelele za vilio vya watoto wa Rhoda zilizidi kuongezeka na kufika umbali mrefu sana hali iliyopelekea wabrazil kuzidi kuongezeka .

    "Tunakufaa Rodrick "CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliongea Rhoda akiwa bado amelala chini na damu zikiendelea kumtoka mapigo ya moyo nayo yalizidi kuongezeka.

    "Hapana tulia! Ondoa wasiwasi mungu yupo kama aliweza kuokoa maelfu kwa malaki na kulisha watu wengi hatashindwa kutuokoa sisi wachache!" Ilibidi Rodrick atumie maneno ya ujasiri na yenye faraja ili kumjengea moyo Rhoda ambaye hakuwa na tumaini lolote , kwani aliwajua vyema wabrazil hao kuliko Rodrick ambae alimuona kama anabwabwaja bwabwaja tu.

    "Mwamini mungu kwanza!". Walizidi kuongea kwa kunong' ona ili kuepuka kusikiwa na wabrazil hao.

    "Nipe maarifa mungu wangu!"

    Aliongea Rodrick huku akipeleka mkono mfukoni ilikokuwa bastola yake haraka haraka aliitoa na kuiseti tayari kwa kuanzisha mashambulizi lakini kabla ya kufanya chochote alishtukia kundi kubwa la simba likitokea eneo hilo na kuanza kuwashabulia wabrazil hao na kila simba alikuwa akiondoka na mtu mmoja mmoja hadi wote wanaisha hakuna simba hata mmoja aliyedhubutu kuwasogelea akina Rodrick japo kelele za vilio vya watoto zilikuwa zikizidi kupamba zaidi.

    "Haleluya ahimidiwe Mungu wa majeshi na mungu wa viumbe vyote hakika wewe ni Mungu na akili zako hazichunguziki!"

    Rodrick hakuacha kutoa shukuruni kwa mungu wake kutokana na muujiza aliokuwa amemfanyia hakuna aliyeamini kuwa wangesalimika kutoka mikononi mwa watu hao ambao walikuwa na siraha mbalimbali za kijadi zilizokuwa na uwezo mkubwa sana na hata Rodrick angetumia siraha yake asingeweza kuwateketeza wote ila mungu ndiye aliejitokeza mahali hapo.

    "Umeona?"

    "Kweli nimeamini mungu yupo nasi!"

    "Hakuna linaloshindikana kwake!"

    Japo walikuwa hawaamini kama simba wale hawaweza kurudi tena.

    “Ahsante Rhoda kwa watoto wazuri mke wangu ,lakini wa nani ?"

    Ilibidi Rodrick aulize maana kumbukumbu yake pindi Rhoda anapotea Dar es salam usiku ule hakuwa na tumbo lolote.

    "Wakwakwo !"

    "Mmmh! Sawa."

    Hakupenda kumbana sana kwa maswali kutokana na hali waliyokuwa nayo kwa furaha na kwa mapenzi ya dhati aliwafunika watoto wale na nguo zake na kuwalaza chini ya mti kisha alimkokoto Rhoda hadi sehemu iliyokuwa na maji alimsafisha na wote walirudi kwa watoto wao waliokuwa wamesinzia.

    "Niambie sasa kuhusu mimba hii nilikupa lini kweli?" Aliongea Rodrick huku akiwamlika watoto wale . Rhoda hakuwa na hiyana ilibidi amweleze ukweli wote na kweli Rodrick alipohesabu siku alijikuta ni sahihi.

    "Mwaaaaaah! Nakupenda sana na nipo radhi kufa kwa ajili yako niko radhi kwenda jela kisa wewe , umekubali kunitunzia watoto wangu katika hali ya mateso , sitakuacha milele najiona mwanaume wa pekee sana na tukirudi Tanzania kitu cha kwanza ni ndoa tu!"

    Maneno yaliyotoka mdomoni mwa Rodrck hayakuwa yenye utani hata kidogo.



    "Mzazi wako je?" Aliuliza Rhoda huku akilaza kichwa chake katika mapaja ya Roderick.

    "Na ili uhakikishe kuwa nakupenda nakuvika pete hii ya uchumba!"

    Rodrick alinyofoa nyasi chache zilizokuwa eneo hilo kisha alizitengeneza kitu kama mfano wa pete na kumvika Rhoda aliyekuwa akitoa machozi ya furaha.



    "Hili ndilo penzi langu kwako lisiloisha na sio la maneno tu , nakupenda sana asante kwa kunizalia watoto wazuri , huyu wa kiume atakuwa Lion au Rogers kwa maana mungu ametuletea wanyama hao acha naye tumtukuze na wa kike atakuwa Dorcas ama paa mnyama mdogo sana aishie porini na huwa anapenda kulala juu sana ya miti , nimeishi porini na kulala juu ya miti kama yeye !

    Kwakuwa walikuwa wamepunzika kwa muda mrefu sana ilibidi waianze safari ya kutoka ndani ya kisiwa hicho ,Rodrick alibeba mtoto mmoja, mgongoni akiwa na begi lake Rhoda naye alibeba mmoja.

    Hadi kunapambazuka walikuwa bado wamo ndani ya kisiwa hicho kila mara Rhoda alikaa hiyo ilisababishwa na maumivu makali katika mwili wake,

    "Nimechoka siwezi kutembea tena tazama nilivyochafuka miguu ilivyopasuliwa na miiba, pia nahisi njaa sana."

    "Jikaze mama lion!"

    "Nakuomba uwatunze watoto wangu ambao nawaacha muda si mrefu!"

    "Hapana hutokufa! "Japo Rodrick alikuwa akiongea kwa kujiamini ila hata yeye alianza kupoteza tumaini watoto nao hawakuacha kulia kutokana na njaa kali.

    "Wanyonyeshe watoto!"

    "Hakuna maziwaa nasikia njaaa sana !" Rhoda alianza kuongea kwa taabu sana. Rodrick hakutaka kuona Rhoda anafia mikononi mwake alimbemba na kuanza kutembea naye kama umbali wa mita mia mbili alimtua kisha aliwarudia watoto waliokuwa amewaacha nyuma huo ndio ukawa mwendo wa safari yake wa kuwatanguliza watoto ama Rhoda.

    Akiwa katika hatua ya kukata tamaa na hata nguvu nazo zilikuwa zimemwishia mara alisikia muungurumo mkali angani na alipotazama hakuamini macho yake kuona helkopita kubwa ikitafuta eneo la karibu na wao , hakujua malengo ya helkopita hiyo.



    Baada ya helkopita kutua wanajeshi watatu walishuka na kuwakimbilia akina Rodrick ambao walikuwa katika hali mbaya sana hasa hasa Rhoda na watoto ambao tayari walikuwa wamezimia.

    "Unafanya nini humu porini?" Aliuliza mmoja wa wanajeshi hao raia wa Brazil huku akiwa amekamata vizuri bunduki yake ya kijeshi.

    "Tusaidieni!

    "Hili eneo ni hatari sana lina simba wengi pia huko mbele kuna nyati wanaoingizwa humu sisi tumetumwa na serikali kuwaokoa wananchi waliokuwa wakiishi humu lakini tumekuta wameshaliwa na simba."

    "Tunashaanga kuwakuta mko hai?" Mwingine alidakia .

    Kwakuwa walikuwa na kazi ya kuokoa watu ilibidi wapunguze kahawa ( maneno mengi) na kuwachukua wao ila kabla helkopita hiyo haijaondoka simba kumi waliokuwa na njaa kali waliizunguka helkopita hiyo lakini hakuna aliejeruhiwa.

    "Ametoka damu nyingi anatakiwa aongezwe!"

    Nesi aliyechukua vipimo kutoka kwa Rhoda alitoa taarifa hiyo kwa daktari katika ndani ya hospitali ya Missisipi nchini Brazil .Kwakuwa Rodrick hakuwa na hali mbaya ilibidi ajitolee kumuongezea lakini damu ilipopimwa ilikuwa na tatizoo!.



    Moyo wa Rodrick ulizidi kuongezeka mapigo kadiri muda ulivyokuwa unakwenda , baada ya kupewa taarifa ya majibu ya damu yake , alibaki akizunguka huku na huko bila kupata jibu la maana wakati huo japo alikuwa katika muonekano wa kutisha kwa macho ya watu waliokuwa hapo na hata wengine walidiriki kumuita mwenda wazimu wa kiafrika kutokana na mavazi yake yalivyokuwa machafu , nywele ndefu na hata ngozi ya mwili nayo ikiwa haina mvuto hata kwa macho ya watoto , lakini hayo yeye hakuyajali , alichokuwa akitaka yeye ni uhai wa Rhoda pomoja na watoto wake Rogers na Dorica ambao afadhali hali zao zilikuwa zikianza kuridhisha baada ya kupewa huduma ya maziwa .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Majibu ya utofauti wa group la damu ndilo haswa swala lilokuwa likikiumiza kichwa chake , kila mara alikuwa akienda kumtazama Rhoda kupitia katika moja ya vioo vilivyokuepo katka wodi ya Icu aliyokuwa amelazwa.

    "Nesi nahitaji msaada wako tafadhali,”

    "Toka nje unaingiaje ofisini kwangu kama unaingia chooni!” Alifoka nesi aliyekuwa katika chumba cha kuhifadhia damu.

    "Nisamehe ni.....n...mke wangu ,,,,,”hakumalizia sentesi yake.

    “Najua lakini ulitakiwa ungonge mlango kabla ya kuingia sawa subili nje nakuja,”aliongea nesi yule safari hii akiwa amepunguza ukali kutokana na huruma ilimuingia baada ya kumtazama Rodrick aliyekuwa akitoa machozi kama mtoto mdogo na kulowanisha ndevu zake zilizokuwa zimejaa kidevuni na kuuzunguka mdomo.



    "Unatakiwa utoe damu ambayo itabaki hospitali na mkeo tutampatia ya group O ambayo imebaki chupa moja tu," aliongea nesi Sabrina baada ya kutoka chumba cha damu huku mkononi akiwa ameshikilia chupa ya damu.

    Miguu yake ilinyosha hadi chumba alichokuwemo Rhoda , alimtundikia damu hiyo.

    "Siku mbili tu mkeo atakuwa amepona.”

    Nesi Sabrina aliongea huku akiendelea kutoa damu katika mwili wa Rodrick iliyokuwa imetofautia na ya Rhoda ambayo ya Rhoda ilikuwa group O Rodrick akiwa na group A.

    "Nitafurahi sana!"

    "Lakini ilikuwaja hadi mkawa porini kwa muda mrefu?" Nesi Sabrina alizungumza huku macho yake yakiwa yanautazama uso wa Rodrick aliyekuwa amekaa juu ya benchi . Kwakuwa Rodrick hakutaka kuficha chochote ilibidi amweleze historia yote.

    "Nilisikiaga habari hiyo ya kuanguka kwa ndege! Daaaah! Pole sana na ninakupongeza kwa moyo wa upendo wa dhati uliomuonesha dada huyu, niwanaume wachache pia naahidi kuhuzuria harusi yako na kukusaidia kwa chochote kuanzia sasa!"

    "Ahsante sana dada!"

    Japo walikuwa wamekutana kwa muda mfupi sana lakini walitokea kuwa marafiki kama wa miaka mingi .Baada ya mazungumzo hayo nesi Sabrina alimpeleka saloon na kisha alimpeleka madukani alikonunua nguo zake , za Rhoda pamoja na za watoto kisha walirejea hospitali walikomkuta Rhoda amerejewa na fahamu hali iliyopelekea furaha kubwa kwa Rodrick .

    "Nipe watoto wangu niwaone!"

    Rodrick hakuwa mbishi alifanya utaratibu wa kuongea na Sabrina aliyekuwa akiwahudumia watoto hao.

    "Heeee! Ameongea?"

    "Ndio!" Alijibu Rodrick huku akipikicha pikicha macho yake yaliyokuwa yamezidiwa na usingizi mkali usiku huo .

    Haraka haraka nesi Sabrina alimkabidhi Rodrick watoto waliokuwa katika kitoroli cha watoto kilichokuwa kimenunuliwa siku hiyo na nesi Sabrina . Kwa mwendo wa taratibu sana na wa uangalifu Rodrick alikisukuma kitoroli hicho hadi chumbani kwa Rhoda.

    "Sasa furaha yangu imeanza kupatikana!"

    "Sio imeanza sema umeipata!"Alizungumza Rodrick huku akiwa anamkabidhi mtoto wa pili Rhoda alyiekuwa akitoa chozi la furaha naye Rodrick hakuwa nyuma kuungana na Rhoda katika furaha hiyo alizunguka mgongoni kwa Rhoda aliyekuwa amewakumbatia watoto wake kwa mikono yake miwili alimkumbatia Rhoda pamoja na watoto wao ambao walikuwa wakitabasamu tabasamu japo mwanzo Rodrick alikuwa na usingizi lakini alijikuta umeisha.



    "Penzi zuri.

    Sauti hiyo ndio iliyovuruga furaha za watu hao.

    "Ahsante Sabrina.” Sabrina alikuwa na kikamera kidogo alilazimika kuwapiga picha ambazo aliamini ni ukumbusho tosha kwao na hata kwake .

    "Am luck to meet with you ( Nina bahati kukutana na ninyi!)

    "Why?( kwanini ?)”

    "Hudhani watu weusi ni wabaya na hawana haki ya kuishi! Kweli watu wengi upande huu wanawachukieni! Lakini toka nimekutana na ninyi sijaona ubaya wowote kutoka kwenu , nakuahidi kumpatia Rogers mke miongoni mwa binti zangu ili kuulinda undugu wetu." Alizungumza nesi Sabrina huku akitabasamu kwa furaha.



    "Kama wao watapendana mie sina neno ila mimi siwezi nikalazimisha."

    "Kweli kabisa,” Rhoda naye alidakia

    Hadi kunapambazuka walikuwa wamezama katika mazungumzo wiku ya tatu kupita hali ya Rhoda ilikuwa imetegamaa hivyo akawa ameagwa hospitalini hapo .

    "Halooo!"

    "Yes Dk. Rahman , Rodrick hapa."

    "Rodrick?"

    "Ndio niko Brazil na Rhoda kesho tunakuja."

    "Hapana siamini!"

    "Tiiii! Tiiii!" Simu yake ilika kutokana na salio kuisha. Japo Rodrick alikuwa ana namba ya wazazi wake hakutaka kuwaeleza chochote , siku iliyofuata Rodrick na Rhoda watoto wao waliokuwa bado wachanga pamoja na nesi Sabrina walikuwa ndani ya gari wakielekea uwanja wa ndege wa nchi hiyo majira ya saa mbili usiku.

    "Nitawakumbukeni sana !"

    "Nesi vivyo hivyo na mungu akuzidishie moyo wa upendo zaidi ya huo nilikuwa nikiwaza jinsi ya kurejea Tanzania kutokana na kukosa nauli , lakini wewe um..,"

    Rodrick hakumalizia sentesi yake ghafla idadi kubwa ya wandishi wa habari kutoka vituo mbalimbali vya habari walianza kuongea naye hali iliyopelekea kukatisha mazungumzo yake kati ya Sabrina wakiwa uwanjani hapo .

    "Habari iliyotufikia punde!.

    Ni furaha ilioje! Ninaweza nikaaita hivyo ....!" mtangazaji wa Dira ya Dunia ama BBC SWAHILI Kaila alisikika katika mawimbi ya radio na Televisheni karibia dunia nzima

    ("Yule binti aliedhaniwa kufa maji katika ajari ya ndege huko kusini mwa marekani ameonekana akiwa hai tena akiwa na mume wake mtarajiwa Rodrick hebu msikilize mwenywe! "Hakika mungu ni mwema kwangu nilisalimika katika ajari ya ndege ile iliyomuua rafiki aliyekuwa amejitolea kwangu mungu ampumzishe , pia namshukru mpenzi wangu Rodrick aliyekubali kuishi porini kwa miezi tisa akinitafuta hakika nampenda sana!"

    "Pia tunarudi nyumbni tukiwa na watoto wetu wapendwa Rogers na Dorca ambao ni mashujaa!"Rodrick naye aliongezea naam mtazamaji na msikilizaji umewasikia wenyewe mimi sina la ziada ya kuwatakieni safari njema! Hii ni Dira ya Dunia mimi ni Kaila)”

    Taarifa hiyo pia ilimfikia Pamela dada wa Rodrick aliyekuwa bado akilia lia kutokana na upotevu wa kaka yake ambaye alidhani kuwa alikuwa amekufa naye alitoa taarifa nyumbani kwao ambako waliandaa sherehe kubwa sana , marafiki wa Rodrick nao walipanga kwenda kumpokea uwanja wa ndege .

    Walifuata taratibu zote uwanjani hapo likiwemo la kukabidhi siraha yake na mizigo yao kisha waliviendea viti vya ndege wakiwa na watoto wao wapendwa Rogers ama Lion pamoja na Dorca.Walikaa na kila mmoja alipakata mtoto huku vichwa vyao vikilaliana na ndege ikapaaa!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Japo ilikuwa ni safari ndefu na yenye kuchosha lakini hadi wanaingia Nairobi hakuna aliyekuwa amepata hata lepe la usingizi wote walizama katika maongezi yenye furaha sana na yaliyokuwa yakihusu ndoa tu.

    "Kesho naelekea kanisani kutoa taarifa hiyo na baada ya wiki tutakuwa tunakula wali wetu!"

    "Unaharaka mwanaume wewe!"

    "Haaa! Rhoda unataka nizembee tena kwanza ningekuwa na uwezo ningejifungisha ndoa mwenywe hahahaha!" Aliongea Ridrick huku akimalizia na cheko la furaha.

    "Nikuambie kitu baby?"

    "Sema nakusikiliza mke wa Rodrick."

    "Wewe mtanashati sana."

    "Kweli?" Aliuliza Rodrick huku macho yake akiwa ameyakazia usoni kwa Rhoda hali iliyopelekea Rhoda kuyakwepesh macho yake kutokana na aibu ya kike ambayo wanawake wengi huwatokea.

    "Nisikilize Rhoda !" Aliongea Rodrick huku mikono yake ikiwa imeshika mabega ya Rhoda na kufanya watazemane , aliendelea

    "Nashukru kwa kuniambia hilo ila tambua wewe ni mzuri sana katika wanawake ambao nimewaona hakuna anaekufikia , nikisema mzuri ni mzuri na sio uzuri tu bali uko malkia wa moyo wangu mwanamke wa maisha yangu nisipokuoa wewe nitakuwa nimeharibu kila kitu katika maisha yangu niahidi hutoniacha?"

    "Siwezi."

    "Kweli?"

    "Ndio."

    Hayo ndiyo yalikuwa mazungumzo yaliyokuwa yameitawala safari yao.

    Ndege aina ya PAK FA kampuni ya Emirates ilionekana ikihangaika kutua katika uwanja mkuu wa mwalimu Julius kambarage Nyerere ndio aliyokuwemo Rodrick na familia yake .

    Baada ya kutua chini abiria wote walianza kushuka na miongoni mwa hao alikuemo Rhoda aliyekuwa amebeba mtoto akifatiwa na Rodrick akiwa vilevile huku mkono wake ukisukuma kitoroli kilichokuwa na bengi mbili .

    "SHUJAA. WA MAPENZI AREJEA"

    Yalikuwa ni maneno makubwa sana yenye rangi nyeusi , yakiwa yameambatanishwa na picha ya Rodrick hakuamini idadi kubwa ya watu waliokuwa uwanjani hapo wenye nyuso za furaha, kila mmoja alikuwa na shauku ya kumuona Rodrick na Rhoda ambao walikuwa wakidhaniwa kufa , wandishi wa habari nao hawakuwa nyuma kila mmoja wao alitaka kupata habari.

    "Unaweza ukatueleza ni jinsi gani ulipona katika ajari ya ndege? Vipi kuhusu hawa watoto je ni wa wabrazil?" Ni baadhi ya maswali aliyokutana nayo Rhoda kutoka kwa wanahabari hao lakini hakuwajibu zaidi ya kuendelea kutembea.



    Msafara wa magari ulikuwa mrefu sana utafikiri wa kiongozi mkubwa wa nchi , huko nako alikuta watu wengi hatari.

    "Mbona baba haoneshi chuki na mimi?"

    "Itakuwa keshayapotezea!" Rhoda na Rodrick walikuwa wakinong'onezana usiku wa siku hiyo.

    Hakuna aliyepinga wazo la Rodrick la kufunga ndoa na Rhoda

    "Tena kesho nitaenda kuongea na padri Thadei !"

    "Nitashukru sana baba!'

    "Usijali tugange yajayo wanangu," Baada ya mazungumzo hayo kila mmoja aliingia katika chumba na kupumzika.



    ******



    Ilikuwa jumamosi tulivu sana ambayo kila mtu aliyekuwa ana kadi ya harusi ya Rodrick alikuwa akiigojea sana.

    Siku hiyo Rhoda alikuwa haamini kama kweli atakuwa mke harali wa Rodrck akiwa saloon mawazo yake yalikuwa ndani ya kanisa akila kiapo.

    Baada ya kutoka saloon humo akiwa na best wake mwavita aliyekuwa huru kutokana na msamaha wa raisi.

    Rodrick naye alitoka salon akiwa na hamu ya kutimiza nia yake alifika kanisani kabla ya Rhoda na kupitiliza ndani kabisa aliketi sehemu iliyokuwa imeandaliwa kwa ajiri yao kadri muda ulivyokuwa ukizidi kuongezeka ndivyo watu walivyoongezeka nesi Sabrina aliyekuwa ameingia Tanzania akiwa na ndugu zake hakuamini upendo uliokuwepo kati ya watu weusi ambao wao walidhani watu weusi ni wakorofi wenye roho mbaya lakini leo hii hakuiona tabia hiyo.



    Nyimbo nzuri na zenye maadili zilizidi kuongeza amsha amsha katika mioyo ya wahudhuliaji wa harusi hiyo mzee Hashim aliyekuwa amesimama kama mzazi wa Rhoda alikuwa hakaukiwi tabasamu usoni na kutokana na uwepo wake katika harusi hiyo ulichangia askari wengi kuwepo hapo ili kuhakikisha usalama hakika kila mtu alikuwa na hamu kubwa ya kuishuhudia ndoa hiyo ya shujaa wa mapenzi kama wengi walivyokuwa wakimuita.

    Milango ya kanisa katoriki la mtakatifu Peter lililoko chang'ombe jijin dar es saalam lilifunguliwa na mwanamke aliyekuwa ndani ya shela aliingia taratibu akitanguliwa na vitoto viwili alimarufu kama bibi harus na bwana harusi wadogo visichana vinne vilivyokuwa vikimwaga maua katika wasichana waliokuwa wakicheza cheza mitindo yao iliyokuwa ikiendana na mziki uliokuwa ukilia na nyuma alifuatia Rhoda akiwa ndani ya shela nzuri na la gharama kutoka Brazil .

    Hakuna alieshindwa kugeuza shingo yake kumtazama Rhoda na idadi kubwa ya watu walikiri kuwa Rhoda alikuwa mrembo.

    "Ni haki mchizi ukataka kufa kwa kifaa hiki mmh! ni shiidaa!"Emanuel John hakimu aliyekuwaga amemtoa jela Rhoda alimnong'oneza Rodrick alipokuwa akinyanyuka kwenda kumpokea .

    Shangwe na nderemo zilisikika baada ya Rodrick kumfikia Rhoda na kumfunua Rhoda kinguo kilichokuwa kimeziba uso wake kabla ya kumbusu kisha walitembea taratibu kuifuata altare

    "Umependeza."

    "Hata we we,"Japo walikuwa wakiongea na kupongezana lakini hakuna aliesikia kutokana na mikele ya furaha kutoka kwa watu

    "Rodrick Steven unakubali kumuoa Rhoda kuwa mke wa ndoa katika raha shida mpaka kifo kitakapowateganisha ?" Aliuliza padri Thadei na kumpa nafasi Rodrick kujibu.

    "Noooooo! Rodrick ni mume wanguuuuu!"Ilikuwa sauti ya mwanamke aliyeingia ndani ya kanisa hilo kabla ya wanadoa hao kukamilisha zoezi lililowapeleka.



    Sauti ya mwanamke huyo ilisikika vyema katika masikio ya kila mtu aliyekuepo eneo hilo , hakuna ambaye hakugeuza shingo yake uelekeo wa mwanamke huyo aliyekuwa akiendelea kupiga hatua kuelekea mbele ya altare.

    Macho ya Rodrick hayakuweza kumtambua vyema kutokana na mshtuko wa ghafla alioupata japo alikuwa akitumbua macho lakini hakuona vizuri .

    Akiwa katika hali ya kupigwa na butwaa alishangaa kumuona Rhoda akichomoka mahali hapo ila hakufika mbali baada ya mzee Hashim na hakimu Emmanuel ambaye alikuwa mshenga wa Rodrick walimkamata.

    "Niacheni… niachieni hawazi kunizalilisha hivi .....nia"

    "Rhoda tulia…tulia kwanza maamzi yako yanaweza yakakugharimu baadae! Mangapi umepitia ? Vuta subira ndoa lazima ifungwe!" CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Emmanuel alijalibu kumuasa Rhoda ambae alikuwa amepaniki huku machozi yakiendelea kumtoka bila kizuizi na kufuta makorobwezo aliyokuwa amepakwa usoni, minong'ono ya chini chini ilizidi kuongezeka.

    "Huyu mwanamke ametumwaaaa sio bule!"

    Sauti ya Pamela ilivunja minong'ono na kila mtu kumtazama haraka sana alimfuata Alvia ambae alikuwa akichekelea na kujiona mshindi.

    "Wewe kahaba wa mjini ume.....!"

    "Pam funga kopo lako!" Mzee Steven alidakia na kuzuia fujo iliyokuwa inaanza kutokea kati ya Alvia na Pamela ambae alikuwa amefika kama simba jike kifua chake kilikuwa kikipanda na kushuka kwa hasira za waziwazi.

    "Dady ndooo umee...amuuaa kunifanyia hivi?"

    "Kijana hebu acha wehu wako nilishaga kuambia uache kuvuta bangi hivi una akili kweli kumlopokea mzazi wako maneno kama hayo!" Mzazi wake aliwaka

    "Tumsifu yesu kristo!" Padri Thadei ilibidi anyamazishe kwanza kelele zilizokuwa zimetanda ndani ya kanisa hilo.

    "Milele Amina!!!!"

    "Ndugu zangu kwanza napenda kutoa pole sana kwa maharusi wetu pili sitoweza kufungisha ndoa hii kwa sasa mpaka tupate jibu la swali hili

    na tatu binti unaedai Rodrick ni mume wako unatakiwa useme mbele ya kanisa lini ulifunga ndoa na uoneshe vielelezo vya hiyo ndoa pia ulete mashaidi waliohudhulia ndoa hiyo achili mbali mikanda iliyorekodiwa katika harusi yako ukileta hivi utakuwa halali kuwa mke wa Rodrick."

    Padri Thadei alimaliza maneno yake na kumkaribisha Alvia kutoa ushahidi.

    Kila mtu alitulia na kuyatega masikio yake kusikiliza kipi Alvia alikuwa akienda kuongea mbele ya umati huo Rodrick alitamani kumrukia lakini ilibidi hasira yake aiweke kando.

    "Najiona ni mwanamke mpumbafu sana ...."alianza kuongea baada ya kufika mbele ya altare , hali iliyopelekea mzee Steven kuyatoa macho aliendelea.

    "Nahitaji sara ya toba kwanza toka mwanzo wazazi wangu na wazazi wa Rodrick walitulazimisha sisi kuoana ...." Alikatishwa

    "Bnti nitoe humo mimi simo alaa!" Mama yake Rodrick alidakia.

    "Mwanzo nilikataa sana ila kutokana naaneno makali ya wazazi wangu na mzee wake ikabidi nikubali kumvurugia Rodrick ndoa yake kwa kusingizia kuwa mimi mkewe na hata vyeti bandia wao ndo walionipatia roho wa huruma ameniingia ghafla naona natenda dhambi kubwa sana ingali simpendi Rodrick , Rodrick na Rhoda naombeni mnisamehe sana.”

    Alimaliza kuongea Alvia muda wote aliokuwa akiongea Alvia mzee wake Rodrick alikuwa ameinamisha kichwa chini kwa aibu na aliomba aridhi ipasuke atumbukia ili kuyakwepa macho ya kila mtu.

    "Kwahiyo wewe unatakaje?"

    "Sina bifu na mtu naomba wafunge ndoa yao na istoshe nawahurumia watoto wao." Aliongea Alvia na kuondoka kanisani humo akiacha ameyatupa na mavyeti yake ya kugushi.



    "Padri tunakuomba uifungishe ndoa hii na swala hili utuachie wanafamilia.”

    Maneno ya mzee Hashim yalikubalika kwa kila mtu na hata shangwe za mwanzo zikarejea tena Rhoda aliyekuwa ndani ya ofisi ya kanisa hilo akitulizwa ilibidi aitwe .

    Padri Thadei hakuwa na muda wa kupoteza tena baada ya maharusi kurudi alifungisha ndoa hiyo iliyokuwa imevamiwa na shetani kisha watu walisambaa na wengine walielekea kupiga picha pamoja na maharusi.

    "Ulilia sana Rodrick?"

    "Rhoda hutakiwi kuniita Rodrick tena nipe heshima yangu basi."

    "Hahahaha! Mume wangu ulilia"

    "Hata wewe eti ulisusa sema nilisahau tu ningesimama mbele na kusema ndio Alivia mke wangu!"

    Yalikuwa maongezi yenye furaha utani kwa mahurusi hao wakiwa bechi wakifurahia maisha mapya .baadae walijiandaa kwenda ukumbini baada ya kurejea hotelini walikoga kula na kumzika kwa muda.



    ******



    Baada ya wiki mbili kupita Rodrick na Rhoda kumaliza honeymoon yao.

    Familia nzima ilikuwa imekaa bustanini baada ya chakula cha mchana wakimalizana tofauti iliyokuwa imetokea kati ya Rodrick na baba yake.

    "Watoto wangu mnisamehe sana." Alianza kuzungumza mzee huyo.

    "Niliona niko sawa kumchangulia Rodrick mke kumbe nilikuwa sitendi haki na imekuwa aibu kwangu.”

    "Usijali baba tulishaga kusamehe,"Rodrck alimkatisha baba yake hakutaka maneno mengi tena maana tayari aliona yameshapita . Kwamoyo wa wazi kabisa familia hiyo ilisameehana na kuyaanza maisha mapya yenye upendo .

    "Nakuahidi Rhoda na Rodrick mbele ya wote nitahakikisha nasimamia masomo ya watoto wenu watakafikisha umri wa kwenda shule.”

    Nesi Sabrina alizungumza hayo akiwa uwanja wa ndege akirejea nyumbani kwake.

    "Tutashukuru sana." walijibu kwa pamoja Rodrick na Rhoda .Nusu saa baadae Sabrina aliondoka. .

    "Leo nataka nikuzungushe mji mzima hadi ukome."

    "Hata sikomi nikiwa na wewe furaha ya moyo wangu furaha iliyokuwa imejificha."

    "Kweli? Mke wa mimi."

    "Eeeh!"

    Mazungumzo hayo yalikuwa yakifanyika ndani ya gari la Rodrck baada ya kutoka uwanja wa ndege .

    Wiki mbili baadae walisafiri hadi mwanza yalikokuwa makazi ya Rodrick siku hiyo hiyo aliwasili kazini kwake alikokuwa amekuacha kwa muda mrefu kila mtu alimpongeza sana na kumkaribisha tena , siku hiyo alitafuta shule kwa ajili ya Rhoda ambaye aliishiaga darasa la pili alipanga kumsomesha tena maana aliamini elimu haina mwisho.



    Siku iliyofuata familia ya Rodrick iliamua kuwatembelea wafungwa katika gereza la Butimba ambako alikuwa amefungwa Rhoda hakuna aliyeamini kumuona Rhoda.

    "Mnisamehe sana Rhoda."

    "Usijali Josephne yalishaga pita tugange yajayo mpenzi,"Rhoda na Josephne walisameehana kisha walielekea lumara sehemu aliyokuwa amezikwa Rhodina.



    "Mpenzi Rhodina ndugu pekee wa Rhoda uliyekuwa umesalia niko hapa na ndugu wengine mungu alionipatia Rodrick mume mwema na Rafiki yangu Rogers na Dorica watoto wangu pia wanao ambao nimewaleta uwaone!"

    Japo alijitahidi kuyazuia machozi lakini haikuwezekana aliwakalisha watoto wale juu ya kaburi ishara ya kubebwa na Rhodina aliyekuwa amefukiwa ndani ya kaburi hilo.

    "Jikaze my love najua unaumia sana ila huna budi kuzoea na kazi ya mungu

    haina makosa amini siku moja mtaonana," aliongea Rodrick huku akimnyanyua Rhoda aliyekuwa amelalia kaburi la Rhoda akilia kwa uchungu.

    "Pole mama."

    Aliwabeba watoto waliokuwa wakilia kisha wote waliondoka kuelekea alikokuwa amelipaki gari lao na safari ya kuelekea MALAIKA BEACH ikaanza Rodrick alifanya hiyo ili kumuondolea mawazo Rhoda na hakupenda kumuona akiwa katika hali ya huzuni maana aliamini yeye ndiye furaha iliyokuwa imebaki .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jioni walirejea nyumbani kwao Buswelu alikokuwa amejenga wakiwa wenyefuraha .

    "Nitakupenda daima Rhoda mama watoto wangu."

    "Nami pia umenionesha mapenzi ya dhati na nuru angavu maishani mwangu umenisahaurisha yote umefuta sumu ndani ya moyo wangu uwepo wako umefanya nikapata ndugu wengine Rogers na Dorca nakupenda sana furaha yangu."

    Maneno yenye hisia kali iliyokuwa ikisindikizwa na machozi ya furaha.

    "Wewe furaha yangu njia yangu mwanga wa maisha yangu daima nitakupenda,”alizungumza Rodrick huku akiyafuta machozi ya Rhoda kwa ulimi wake wakiwa ndani ya bustani nyumbani kwao baada ya chakula cha usiku huo pembeni yao walikuepo watoto wao wakisikiliza maneno ya wazazi wao .

    "NIMEIPATA FURAHA YANGU!"

    Kwa pamoja walilitamka neno hilo kwa sauti hali iliyopelekea watoto kulia kutokana na mshtuko ila wao walicheka kwa furaha.



    MWISHO.



0 comments:

Post a Comment

Blog