Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

SIKUTEGEMEA - 1

 









    IMEANDIKWA NA : TARIQ HAJI



    *********************************************************************************



    Simulizi : Sikutegemea

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ama kweli mwanaume wa kweli hakimbii shida, kwa jina naitwa Adam. Ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto wawili, yaani mimi na kakaangu. Sio kwamba tulikuwa na maisha mazuri sana lakini kila nilichokitaka nilikipata kutoka kwa wazazi wangu. Wakati nikiwa kidato cha pili kakaangu alioa na kuondoka, aliishi na mkewe sehemu moja inayojulikana kama Kijichi kisiwani Zanzibar. Maisha yaliendelea kuwa mazuri huku nikiwa na ndoto za kuwa mtu wa maana sana katika jamii, lakini ndoto zote hizo zilizima baada ya wazazi wangu wote wawili kuaga dunia katika ajali ya meli.



     Wakati huo nilikuwa nimeshamaliza kidato cha nne na nilikuwa nasubiria majibu, lakini hata yalipotoka sikuweza kuendelea kusoma kwa sababu hakukuwa na mtu wa kunisomesha. Nilitegemea labda kaka angeniendeleza lakini yeye mwenyewe maisha yake yalikuwa duni sana. Nilikaa nyumbani nikisubiria fungu langu la urithi ambalo ndani ya akili yangu nilidhamiria nikilipata nijiendeleze mwenyew. Ama kweli dunia hadaa ulimwengu shujaa na na ukistaajabu ya Mussa utayaona ya firauni.



     Jamaa zetu walizigombania hizo mali kidogo zilizoachwa na wazazi wetu na kugawana wao kwa wao. Na hilo pia lilipelekea kufukuzwa nyumbani na nyumba ile kuuzwa. Kiufupi sikubakiwa na kitu chochote kile zaidi ya nguo nilizokuwa nimevaa. Taarifa zilimfikia kakaangu na hapo akaamua kunichukua nikaishi kwake, nilishukuru Mungu japokuwa sikujua kumbe huko nako kuna majanga mengine.



     Kaka alikuwa akijishughlisha na masuala ya uvuvi hivyo muda mwingi hakuwa nyumbani, nilibaki mimi na shemeji yangu tu. Nae alianza kunifanyia vitimbi, kuna wakati hakunipa chakula kutokana na sababu anazozijua yeye mwenyewe. Hilo halikuniumiza sana kwani kula hata  mtaani nilikuwa napata kutoka kwa marafiki zangu niliowakuta eneo hilo. "kaka kwanini na mimi usinichukue bahari usiku nikajifunze kuvua" siku kaka alikuwa nyumbani na nikapata muda wa kuongea nae. "mdogo wangu bahari isikie kama ilivyo" alinijibu, "ah unajua kukaa nyumbani kama mtoto wa kike nimeshachoka na mimi nataka niende baharini nikajifunze uvuvi, pia hio itasaidia na hapa nyumbani" nilijaribu kuwa mbishi mpaka mwisho akanikubalia.



     Maisha yangu mapya kama mvuvi yalianza, siku za mwanzo nilipata sana shida hasa ukizingitia uvuvi wetu ulikuwa ni wa usiku sana. Lakini kadiri siku zilivyokwenda nilianza kuzoea mpaka na mimi nikawa bingwa sasa. Miaka miwili ilipita kama upepo na vitimbi vya shemej yangu vilizidi ndani ya nyumba. Sasa alikuwa akinitaka kimwili jambo ambalo sikuwa tayari kulifanya, mara kadhaa alinitishia kuwa akirudi kaka atamwambia namtongoza.



     Nilivumilia mwanzo lakini mambo yalizidi kuwa mabaya maana alikuwa akinifata chumbani kwangu hata kama kaka yupo. Mshare wa hatari ukagonga kichwani mwangu na hapo ukawa umefika muda wa kufanya maamuzi magumu. Siku hiyo nilijifanya naumwa ili nibaki nyumbani, baada ya kaka kuondoka kuelekea baharini nilichukua begi langu na kuchukua nguo kadhaa. Kimya kimya bila hata kuaga nilitoroka nyumbani.



     Moja kwa moja mpaka bandarini, nilikata tiket ya meli ya usiku huo kuelekea jiji lenye heka heka za kila aina za maisha nalo si jingine bali ni jiji la Dar-es-salaam. Meli iling'oa nanga saa nne usiku na safari mpya ya maisha yangu ikaanza, "oi mwanangu niaje" wakati nikiwa nimepumzika nilisikia mtu akinisalimu. "shwari kama kawa" nilimjibu, "mimi naitwa Frank" alijitambulisha. "nashukueu kukugahamu Frank, mimi naitwa Adam" nilimjibu huku nkimpa mkono. Hapoo ndio ulikuwa mwanzo wa urafiki wetu.



     Tuliongea mengi sana na kumwambia kuwa mimi ni mgeni huko ninapo kwenda, "usijali ndugu yangu sisi wote tunakwenda huko kutafuta" aliongea Frank kisha akaendelea "mimi ni dereva wa bodaboda huko sehemu moja inaitwa mbezi makonde". "mimi hata sikuaham huko napasikia tu" nilimjibu, "tukishuka tufatane huenda ukapata shavu huko, kuna vibosile vingi tu vinatafuta vijana wa kazi hasa madereva wa bodaboda" alinijibu na kunipa moyo. "lakini ndugu yangu mimi hiyo pikipiki kuendesha sijui". "usijali ndugu nitakufundisha kisha ntakusaidia kutafuta ajira" aliongea huku akinipiga begani.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     "ama kweli dunia bado ina watu wenye huruma" nilijiesemea moyoni, meli ilitia nanga saa kumi na mbili asubuhi. Abiria wote tukashuka, niliongozana na Frank mpaka nje ya bandari na kuchukua kibajaji mpaka kariako. Huko tulipanda magari kuelekea tegeta na kushuka mbezi, 2karibu nyumbani aisee" Frank aliongea wakati tunaingia katika chumba kimoja kidogo sana cha kupanga. Hata hivyo nilishukuru sana maana sikujua hata nikifika nitakaa wapi lakini kama ilivyo Mungu hamtupi mja wake, akaniletea muokozi.



     Maisha yalianza hivyo hivyo japo yalikuwa magumu sana kutokana na mimi kutokuwa na kazi, wakati huo Frank alikuwa akinifundisha kuendesha pikipiki. Baada mwezi mmoja nilikuwa nimeiva vizuri sana, bila kuchelewa nilianza kufatilia mchakato wa leseni na kufanikiwa kuipata. Franka alinitembeza kwa mabosi anaowajua na kufanikiwa kupata ajira kwa mama mmoja hivi wa kizaramo. Kuanzia hapo maisha yangu yaliingia tumaini jipya, nilifanya kazi kwa bidii sana huku nikijathidi kuweka pesa kwa ajili kuja kununua pikipiki yangu mwenyewe.



     Kwa wakati huo nilikuwa na miaka ishirini na mbili, uaminifu wangu ulimpendezesha bosi na kuniacha pikipiki nifaye kazi hadi usiku. Maisha yalizidi kuwa mazuri huku mimi na Frank urafiki wetu ukizidi kuota mizizi, "oyaa, wewe mpemba kichaa"mtu mmoja aliniita. "halafu we si nmekwambia usiniite hilo jina" nilimlibu huku nikikaza macho. "ah wapi, mimi ntaendelea kukuita jina hilo hata kama hulipendi, we umesikia wapi mpemba akawa dereva wa bodaboda. Nyinyi kazi yenu uvuvi huko na si kuvamia kazi za watu" alizidi kuongea. "Jackson acha utani wewe, eti wapemba kazi yao uvuvi" Frank aliongea huku akicheka.



     Hayo yalikuwa ni matani ya kawaida kila siku, walizoea kuniita mpemba kichaa mpaka jina hilo likazoeleka maeneo yote ya karibu. Ukweli nilipata marafiki wengi sana tafauti na nilivokuwa nikifikiria kipindi niko kisiwani. Nilikuwa najua Dar kuna wezi na matapeli ile mbaya lakini kumbe zilikuwa stori tu japo zilikuwa na ukweli ndani yake. Lakini niliowapata mimi walikuwa marafiki wa kweli na kila siku nilikuwa nikimshukuru muumba wa mbingu na ardhi.



     Siku moja nikiwa kijiweni nasubiria, niliwasikia washkaji wakiongelea mchakato wa kuzamia nchi za magharibi. Maongezi yao yalinifanya nitege masikio vizuri maana na mimi nilikuwa nina hamu ya kuwa na maisha mazuri. Na nilidhani ukifika tu huko nchi za magharibi basi ndio unasahau kabisa shida. "unasikia mtu kuna meli huwa inakuja Tanzania kwa mwezi mara moja tu, na ktika hiyo meli kuna mzungu ukichinga nae fresh tu basi anakupenyeza halafu ndio kwa heri shida2 aliongea kijana mmoja. "mwanangu wasema kweli au watania wewe" James aliuliza kwa lafudhi yake ya kitanga.



     "sasa mtu wangu nikutanie vipi wakati mifano hai  ipo, si munamkumbuka yule mshkaji alikuja kutoka Tabora", "ndio halafu yule dogo kapotea mwaka wa pili huu". "ah kapotea wapi yule, dogo anakula shavu kwa Obama huko", "ebwnaee". "unataka kusema dogo kazamia mbele huko", "ndio mimi ndo nilimfanyia mpango". "sasa mbona wewe uko hapa leo", "ndugu yangu wee, nilikuwa sina hela ya muhonga mzungu". Kwa kweli mazungumzo hayo yaliniingia akilini kisawa sawa na kujikuta nikitamani na mimi niende huko wanapopaita kwa Obama sijui kwa malikia.



     Niliendelea kufanya kazi huku nikiwa nawaza ntampataje mshkaji ili anipe mchongo kama vipi na mimi nizamie kwa ngozi nyeupe huko nikale bata. Baada siku mbili wakati nasubiria wateja usiku nilimuona yule mshkaji alieongelea kuhusu kuzamia. Niliwasha pikipiki na kusogea alipo, nilimpa ishara apande kisha nikaondoka eneo hilo. Nilipofika sehemu ambao niliami tutaongea wa faragha nilisimamisha pikipiki. "mambo niaje mwanagu" nilimsalimu, "Shwari tu kama kawaida" alinijibu huku akishuka.



     "ebwana juzi wakati unaongelea kuhusu kuazamia aisee ulinivuta sana" nilimwambia bila kuficha, "kwa hiyo ndugu yangu unataka kuibuka kwa Obama sio" aliniuliza. "ndio maisha bongo magumu sana", "una hela ya kutosha kumuhonga huyo mzungu". "kwani ni kiasi gani?", "ah sio hela ndefu sana, ni milioni mbili na kidogo tu". "dah kwani hiyo meli inakuja lini?", "hiyo itaingia bandarini mwezi wa sita huko". "basi mpaka muda huo hela itakuwa ishakamilika", "hamna noma we ukiwa tayari unaweza kunishtua tu". Tulimaliza kuongea na kubadilishana namba za simu na kuahidi kuwa hiyo iwe siri kati yetu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Niliondoka hapo na kuendelea kazi yangu huku nikipania kufanya kazi ya ziada ili kutimiza kiasi cha fedha kinachotakiwa. Kwa wakati huo nilikua na kama milioni na nusu hivi, niliiweka pesa hio ili nije kununua pikipiki yangu. Lakini wazo hilo lilikufa baada ya kuingia tamaa ya kwenda huko kwa Obama. "ama kweli tamaa mbele mauti nyuma" niliusahau kabisa msemo huo, nilinza kupiga kazi kwa bidii mpaka Frank akawa ananishangaa lakini aliponiuliza nilimdanganya kuwa nataka kununua pikipiki yangu. Miezi ilikatika haraka na hatimae mwenzi wa sita nilimtafuta yule jamaa, "mzigo nnao wa kutosha sasa bipi kuhusu ile ishu tulioongea". "hakuna noma meli imeingia juzi na sasa hivi wanapakuwa mizigo, inabidi kwanza tukaongee na huyo jamaa maana haikai sana itaeleekea kwa Mandela".



     Nilikubaliana nae na kuchoma mafuta mpaka Oysterbay ambapo ndipo anapokaa huyo baharia wa kizungu, jamaa alitoa simu na kuwasiliana nae na baada ya muda alitoka na kutonyesha ishara tumfate. Tulitafuta sehemu iliotulia na kuanza kuongea, muda wote mimi nilinyamaza kimya kwasikiliza wao wakionge. Baada robo saa jamaa aliniita pembeni, "mwanang mchono umetiki" alipoongea hivo nilitamani kumkumbatia lakini si unajua tena. "sasa nipe hiyo bahasha nimkabidhi" aliongea na hapo nikatoa bahasha na kumkabidhi. yule mzungu alizito zile pesa na kuanza kuzihesabu, na alipomaliza alitabasamu na kunionyesha dole gumba akimaanisha zinatosha. Yaani niliztoa milioni mbili na laki sita ambazo nilizitolea jasho kuzipata kirahisi rahisi sana.



     Yule jamaa alienipeleka alirudi na kunambia tuondoke, niliwasha pikipiki na safari ya kurudi mbezi ikaanza. "safari lini?"nilimuuliaza, "jumamosi inayofuata, na unatakiwa ufike pale pale tulipokutana nae saa tatu usiku" alinambia na hapo nikafunga mdomo kuwa makini na barabara nisije kufa kabla sijafika nnapopataka. Tulifika mbezi na kumuacha jamaa sehemu ambayo ni mbali na kituo, niliendelea na mizunguko ya kawaida huku nikiwaza safari tu.



     Hatimae siku ya safari ilifika, siku hiyo nilirudisha pikipiki kwa bosi mapema kwa kisingizio nimepata simu ya ghafla kutoka kwa mtu ninae mfahamu kutoka Zanzibar. Alinielewa na kunipa laki tano kwa ajili ya safari. Nilijisikia vibaya sana lakini sikuwa na jinsi, akili yangu ilikuwa ikiwaza mambo mazuri yanayonisubiri nchi za magahribi. Niliaga nakuondoka kurudi nilipopanga, "oya mbona unapanga, vipi kaka?" Frank aliniuliza. "ah nakwenda Zanzibar kidogo, nimepakumbuka sana" nilimdangaja, "afadhali hata unataka kurudi kwenu, ni miaka takriban miwili sasa imepita hujapatia mguu" Frank aliongea huku akitabasamu.



     Nilimaliza kupanga nguo mbili tatu, nikafunga begi. Nilimuaga Frank na kuondoka, nilipanda boda boda mpaka maeneo ya Posta. Nilifanya hivo ili nisishtukiwe, baada yule jamaa kuondoka niliita bajaji na kuelekea Osterbay ambapo ndipo nilikubaliana nikutane na yule mzingu. Nilifika Osterbay na kushuka, nilimlipa mwenye bajaji na kuanza kutmbea. Na kwasababu ilikuwa saa tisa, ilibidi niatafute pahali nikae kwanza kwa ajili ya kuusongesha muda mbele. Nilikaa sana huku mara kadha nikizungunguka, nilikumbuka kuwa maji ni muhimu. Hivyo nilinunua chupa kadhaa za maji na kuzitia kwenye begi langu. Niliendelea kusubiri mpaka saa tatu ilipotimia, nilimuona yule mzungu akija upande wangu.



     Wala hakufika sehemu niliopo, alinipa ishara nimfate. Niliinuka haraka na kuanza kumfata, alitangulia mbele huku akiwa makini sana. Tulifika mpaka kwenye gari yake, tulipanda na safari ikaanza. Tulipofika katika geti la kuingia bandarini alinipa ishara niiname kujificha, nami nikafanya hivo. Baada ya maongezi ya sekunde kadhaa na walinzi pale getini, aliruhusiwa kupita. Moja kwa moja mpaka kwenye meli moja kubwa sana, aliipandisa gari mpaka ndani ya meli kuendelea mpaka sehmu moja ambayo nahisi ilikuwa ni ya kuwekea magari.



     Alishuka kisha akanambia na mimi nishuke, tulitembea kwa umakini mkubwa mpaka kwenye mlango mmoja hivi. Aliufungua na kuanza kushuka ngazi kuelekea chini, tulifika kwenye chumba fulani hivi na kufungua mlango. Macho yalinitoka kukuta vijana wengine kama mimi, wavulana kwa wasichana wakiwa wamejazana ndani ya chumba hicho. "kijana utakaa humu na wenzako" aliongea hivo na kunikabidhi box dogo la biskuti, "hichi ndio kitakuwa chakula chako, utakuwa unakula moja kila baada ya siku tatu na maji nitakuwa nawaletea mimi" alimaliza kuongea na kukifunga chummba hicho.



     Niliwaangalia wale wenzangu na kutabasamu kidogo, niliona tayari nimeshapata marafiki wa kuanza nao maisha tukifika. Mashine za meli ziliwaka mnamo saa nane usiku, na baada muda kidogo nilisikia ikipiga honi kuashiria kuwa ilikuwa inang'oa nanga. Moyo wangu uliingiwa na amani na kuhisi kuwa nimetuwa mzigo mkubwa wa dhiki. Ama kweli usilolijua ni sawa na usiku wa giza na ng'ombe wa masikini hazai. Meli hiyo ilikuwa ikitembea taratibu sana, kuna baadhi ya wakati vijana wengine walitapika kutoka na kuchafuka kwa bahari.



     Kuna wakati ilisimama na nilihisi kuna vijana wengine waliingizwa katika vyumba vingine, safari hiyo ilendelea huku kila siku nikipanga mipango mingo sana. Kuna wakati mawazo kama "nikifika huko niwe msanii au niwe muigizaji", "nikifika huko niwe muuza madawa ya kulevya maana ya hela sana" yalipita katika akili yangu. Meli ilisimama tena sehemu na baada masaa kadha nilisikia milango ikifunguliwa, hiyo iliashiria kuwa vijana wengine waliingizwa kwa siri.



     Kadri siku zilivyokwenda ndio hali ya bahari ilizidi kuwa mbaya, huku vijana wengi walitapika hadi kupoteza fahamu. Wengine walitapika mpaka kujisaidia haja ndogo na kubwa hapo hapo, ilimradi ilikuwa ni karaha ndani ya chumba hicho. Harufu ilikuwa mbaya sana, utasema tulikua tunaishi katika karo la mavi. Hata hivyo ilifikia wakati hiyo harufu sikuisikia tena, masikini mimi nilipojiangalia niligundua kuwa nilikuwa nimekonda sana.



     Hapo sasa nikaanza kujuta kwanini nimefanya maamuzi ya kijinga namna ile, lakini ningefanyaje na wakati maji nilishayavulia nguo na sikuwa na budi kuyaoga. Mwili wangu ulijaa ukurutu kutokana kutooga kwa muda mrefu sana. Yaani tulikaa ndani ya chumba hicho mpaka tukasahau siku zinaendaje huko duniani maana hata jua tulikuwa hatulioni.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Ukweli hali ilizidi kuwa mbaya katika vyumba hivi tulivyofichwa, isitoshe tulikuwa wengi sana lakini tungefanyaje na kila mmoja alikuwa ya kufika magharibi. Tukiwa humo ghafla meli ilisimama, tulidhani kuwa tushafika. Wengi tulianza kutabasamu lakini tabasamu hizo zilipotea baada ya kufunguliwa na kuingia wanaume watatu wakiwa na mitutu mkononi. Walituamuru tusimame na kuongoza njia kuelekea nje ya vyumba hivyo. walitupeleka mpaka juu kabisa kwenye deki na huko sasa nilipigwa na mshangao mzito baada kuona idadi yetu ilikuwa kubwa sana.



     "nyinyi ndio munaopenda kuzamia, si ndio?" aliongea mtu mmoja aliekuwa katika mavazi ya kinahodha. Moyo ulianza kunienda mbio na hapo nikaanza kukumbuka hadithi za mtaani, eti ukikamatwa na mabaharia aidha ufanywe mwanamke au wakutose majini uliwe na samaki au ufe mwenyewe. Na asikwambie mtu kifo cha maji kibya sana, kwasababu hufi mpaka pale utakapokuwa ushakunywa maji mengi sana na mwili hauna tena pumzi. Yaani unakufa taratibu huku unajiona kabisa lakini huwezi fanya chochote.



     "si nimewauliza nyinyi" alifoka tena kisha akaendelea "sasa ni hivi, hapa inadidi uchague kuwa mke wetu au tukutoe sadaka baharini ukaliwe na samaki". "halafu mimi huwa napenda sana makalio ya kiume" aliongea baharia mmoja amabe alionekana kuwa na uchu wa ngono. Ilikua ni rahisi kumjua kutokana na kuwa tayari suruali yake ilishatuna maeneo ya zipu. "eti mwanaume mzima nikubali kulawitiwa" nilijisemea moyoni, nilipoangalia pembeni nilmuona binti mmoja mrembo sana wenye asili ya kisomali. Alikuwa kitetemeka si mchezo, mimi mwenyewenilikuwa nikitetemeka lakini nilijikuta nikimuonea huruma. "masikini sijui amekimbia vita huko kwao, na huku anakutana na msala mwengine" nilijisemea moyoni.





    Nilianza kuangaza huko na kule kutafuta kama kuna kisiwa karibu, kutokana na uzoefu wangu baharini niliweza kugundu kuwa kipo kisiwa japo kuwa kilikuwa mbali kidogo. "ehe nani nani yuko tayari kuwa chombo chetu cha starehe?" aliuliza baharia mmoja. Hapo niliwaona wadada wawili wakisoge mbele kuashiria walikuwa tayari kutumika kama chombo cha starehe ili kuokoa maisha yao. Mabahria wawili walishaki wale wadada na kuwavua nguo kisha wakaanza kuwafanyia ushenzi wao mbele yetu. Na mbaya zaidi waliwaingilia sehemu zote mbili huku mmoja wao akiwa na camera akirikodi uchafu ule.



     Masikini wadada wa watu walipiga sana kelele na kulia kwa nguvu kutokana na maumivu wanayoyapata pale walipongiliwa kinyume na maumbile. Hata hivyo wale jamaa hawakuacha kuwafanyia walichokuwa wanakifanya mpaka pale walipofika mshindo mkuu. Waliwapiga risasi na kuwatosa baharini, "unapopakuliwa hutakiwi kulia" aliongea mmoja miongoni mwa wale washenzi wawili. "kama mbwai na iwe mbwai tu, mimi mtoto wa kiume siwezi kufanya shoga bora hata nife majini ili nipate kujitetea mbela za Mungu" nilijisemea moyoni na kumwangalia yule binti wa kisomali. Nilimfanyia ishara kama anajua kuogelea nae akatikisa kichwa kuashiria kuwa alikuwa anajua.



     Nilivuta pumzi kwa nguvu kwa maana nilielewa kitendo ninacho kwenda kukifanya kinaweza kunigharimu maisha yangu. Nilimshikia mkono yule binti na kukimbia nae, nilipofika mwisho sikujishauri, nilimvuta kwa nguvu na kuruka nae majini. kwa mbali nilisikia milio ya risasi lakini wala sikujali, kutokana na uwezo wangu mkubwa wa kuogelea pia na wa yule binti tulifanikiwa kufika mbali na kuibuka. Nilipoangalia kule kwenye meli niliwaona vijana wengine wenye roho za paka kama mimi wakijitosa majini.



     Sikutaka kupoteza muda hapo maana nilielewa tukiendelea kung'aang'aa macho macho sehemu hiyo huenda wale jamaa wakatufuata. Nilimpa ishara yule binti anifuate na kuanza kuogelea, tuliogelea kwa muda mrefu sana. "mimi nimeshachoka" aliongea yule binti, "jitahidi tu muda si mrefu tutafika" nilimjibu uongo ili mradi tu asikate tamaa. Alikubali na tukaendelea kukata maji, sasa kiza kilishaanza kuingia. "naomba niache nife wewe endelea na safari na nshkuru kwa msaada wako" yule binti aliongea kwa tabu sana na kabla sijamjibu alianza kuzama. "mimi sijakuokoa uje kufia mikononi mwangu" nilijisemea na kumshika kisha ni



     Sijui hata saa ngapi nilipoteza fahamu ila nilikuja kushtuka baada kuhisi kitu baridi kikinigusa mdomoni na kunisaidia pumzi, wenzetu wanaita busu la kuokoa maisha (kiss of life). Nilipoangalia vizuri niligundua kuwa nilikuwa ufukweni, na yule binti alikuwa pembeni yangu ananiangalia. "sijawahi kuona mtu mbishi kama wewe, yaani unathubutu kupambana na kifo" aliongea binti huyo huku akitabasamu. Tabasamu ambalo liliuchanua uso wake na kuuthibitsha urembo wake, "siku yetu ya kufa ilikuwa bado" nilimjibu huku nikijizoa zoa na kukaa kitako.



     "mimi naitwa Adam" nlijatmbulisha maana mpaka muda huo tulikuwa hatujuani majina,  "mimi naitwa Latfina au Latifa kama wengi walivyozoea kuniita Tanzania" alijibu akitabasamu. "hivi ulijuaje kama kuna kisiwa maeneo haya" aliniuliza, "ah niliwahi kuwa mvuvi huko nyuma, so nilijifunza kusoma mazingira ya bahari poja na mwenendo wa mawimbi na hicho ndicho kilichonisaidia kujua kama kuna kisiwa karibu japo sio karibu kama nnavyokusudia" Nilimjibu huku nikisimama. Lakini nilishanga kujikut sina nguvu hata kidogo, "pumzika kwanza, umechoka sana" Latifa alinambia.



     Tulikaa ufukweni kwa muda mrefu kabla kuanza kuona miili ya watu ikisukumwa ufukweni na mawimbi. Sijui hata nguvu nilito wapi, nilisimama na kukimbilia kwenye maji na kuanza kuwavuta mmoja mmoja na kuwaweka ufukweni. Nilishangaa kumuona Latifa akiwashika mikono chini kidogo kwenye kiganja, "unafanya nini?" nilimuuliza. "inawezekana wengine hawajafa hawa" alinijibu huko akisilizia kwa makini, ghafla alianza kumgandamiza kifua na kufanya kama anasukuma hivi. Ghafla alizinduka huku akikohoa na kutema maji.



     Basi tuliendelea hivo huku mimi nikijatahidi kuwaleta nchi kavu, Latifa akiwapatia huduma ya kwanza wale waliobahatika kuwa hai. Wakati nikiendelea kusubiri miili ifike nchi kavu kwa mbali nilimuona mmoja akiwa anapapatuana na maji, na alionekana kuchoka sana. Nilipiga mbizi na kumfuata alipo, nilimshika na kurudi nae nchi kavu. Tulipofika kwanza wote wawili tulilala chali huku tukihema kwa nguvu, baada ya mua kidogo niliinuka na kumpa mkono. kwa msaanda wangu alisemama na kuelekea walipo wenzetu. "kati ya watu mia waliokuja nchi kavu ni watu ishirini na mbili tu ndio wamepona, wengine wote wamepoteza maisha" Latifa aliongea kwa huzuni kidogo.



     "samahani bro, nashkuru kwa msaada wako, kwa jina naitwa Louise" aliongea yule kijana nilieenda kumuokoa, "usijali Louise tushukuru Mungu kwa kutupa uwezo wa kuwa hai mpaka saa hivi, mimi naitwa Adam na huyo nesi hapo anaitwa Latifa" nilimjibu na kujitmbulisha pamoja na kumtambulisha Latifa. Wakati huo njaa ilikuwa inanisumbua kweli kweli, taratibi nilianza kusogea kwenye miti. Niipofika nilianza kukata majani na kula, asikiwambie mtu njaa mwanakharamu. Wale wengine wote walivyoona nakula majani na wao walikuja mbio na kuanza kufakamia majani ya miti amabyo wengi wetu tulikuwa hatuijui.



     "unajua Adam kukaa hapa ufukweni ni hatari sana" aliongea Louise kunambia, "kwanini?" nilimuuliza. "bora tuingie humo msituni huenda tukawa salama zaidi" aliongea, na kwa upande mmoja wazo lake lilikuwa la msingi sana. Baada jushiba majani tuliitana wote na kushauriana kama vipi tuingie msituni. Wengi waliliunga mkono wazo hilo na bila kuchelwa tunajongea na msitu huo ambao hatukujua tungeishi kwa muda gani.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Tulitembea kwa dakika kama ishirini hivi mpaka tulipofika pahali kwenye uwazi kidogo, kwa kweli sikuwahi kuona sehemu nzuri kama ile. Kulikuwa na maporomoko ya maji safi yasio chumvi hata kidogo, kulikuwa na miti yenye matunda pamoja na ndege wa aina mbali mbali. Kila mtu alikimbili katika bwawa ambalo maji yalikuwa yakimwagika kutoka katika bonde la karibu. Wakati wenzetu wakifurahia maji; mimi, Louise na Latifa tulikaa tuli tunawaangalia. Wengi walionekana kufahamiana lugha tafauti na sisi ambao tulikuwa pekeetu. Mimi ndie mtanzania pekee niliokoka kutoka katika ile meli, Latifa ni msomali na Louise ni mnamibia. Tuliongea Lugha tatu tofauti lakini hawa wawili walikuwa wakikifahamu kiswahili japo si sana.



      Kiza kilianza kuingia na hapo tugawanyika katika makundi kadhaa, huku kundi letu ltukiwa sisi pekeetu. "unajua kwa hii hali ilivyo, huenda baadae ikanyesha mvua" aliongea Louise, "dah na hakuna hata sehemu ya kujikinga" aliongea Latifa. "msijali marafiki zangu mimi najua kutengeneza vibanda kwa kutumia vichaka na vina uwezo kutukinga na mvua bila tatizo" Louise aliongea hukua akiangaza huku na kule. Alipona kichaka kilichoshona miti mingi alikisogelea na kuingia ndani japo kwa shida kidogo, nipeni dakika kama ishirini hivi kitakuwa tayari" aliongea akiwa ndani ya kichka hicho.



     Tulianza kusikia miti ikikatika katika, kichaka hicho kilikuwa kikitingishikwa kwa juu. Lakini maajabu ni kwamba, haukuonekana hata mti mmoja ukikatika kwa juu. Baada kama dakika kumi na tano hivi alitoka na kuniambia nimfuate. Tulitembea mpaka kwenye miti fulani hivi inafanana na migomba, tulikata majani kadhaa na kurudi nayo kwenye kile kichaka. Aliingia ndani na kuendelea na kazi yake, baada muda kidogo alitoka na kutuamabia tuingie. Loo sikuamini macho yangu kwa jinsi kile kichaka alivyokichonga ndani. Kilikuwa kam kijichumba flani hivi kidogo kidogo, "mimi na wewe tutalala hapo" aliongea huku akininyooshe kidole. "na mimi je?" Latifa aliuliza, "wewe utaingia hapo kwenye hiyo kuna, ndio kuna kijisehemu chako. Wewe unahitaji uhuru wa kutosha so nimekuandalia hico kijisehemu ambacho utakuwa unaweza kufanya mambo yanayokuhusu wewe na kulala unavotaka" alijibu Louise.



     "hivi kweli maji hayawezi ingia humu?" nilimuuliza kwa mshangao kidogo, "ndio na kama huamini subiri mvua inyeshe" alinijibu. "sasa huko nje mtu si ataona mlango wa kuingilia ndani?" aliuliza Latifa, "hapana mtu hawezi gundua kama katika hichi kichaka kuna watu wanaishi labda aone alama za miguu. Na hilo ni gumu sana kutokana na kuwa mvua katika sehemu kama hizi hazikati hivyo hata hizo alama za miguu zitakuwa zinafutika" alijibu Louise. Wakati tukiendelea kuongea ghafla mvua ilianza kunyesha, nilisubiri kwa hamu ili kuthibitsha maneno ya Louise. Na kweli halikupa hata tone moja la maji ndani ya kichaka hicho.



     "hivi umewezaje kutengeza hivi?" ilibidi niulize ili kutoa dukuduku langu, "mimi ni mwanajamii wa jamii za kiwindaji zinazopatikana Namibia, kabila langu ni Khosa ama san kama wanavoita watu wengine. Pia vijana wengi wa siku hizi wanatuita Bushman baada ya kuona ile filamu ya the gods must be crazy" alipofika nilitamani kucheka lakini Latifa alinifinya na kunifanya nitulie. "wazazi wangu walitaka nijifunze mila zetu hivyo wakaamua kuniondoa mjini na kunipeleka kwa babu yangu ambae bado yeye alikuwa anaishi kimila zaidi, huko nilifundishwa kuwinda. Pia nilifundishwa jinsi ya kugundua miti ambayo ni dawa na miti ambayo ni sumu. Pia nilifundisha jinsi ya kutengeza makazi ya muda mfupi ikiwa usiku utanikuta porini na mambo mengine mengi tu" aliendelea kutusimulia. 



     "sasa kwanini umeamua kuzamia" ilibidi nimuulize, "ah si unajua tena kila mtu siku hizi anataka maisha ya kisasa yaliojaa starehe, na hicho ndicho kilichonifanya nitoroke kule kwa babu. Na mpaka sasa wazazi wangu wanajua niko kwa babu yangu kwa sababu hakuna njia ya mawasiliano isipokuwa kufika tu huko anapoishi babu. Kwa kweli najuta kwanini nimefanya maamuzu ta kipumbavu sana wakati kila kitu ninachokitaka nilikuwa napata" alipofika hapo alianza kulia, ilibidi tumnyamazishe na hapo ndio ukawa mwisho.



     Kwa vile kiza kilishaingia wala hatukutoka tena kwenye kichaka hicho ambacho ndicho tulikifnya kama nyumba yetu. Asubuhi na mapema tulitoka na kuelekea kwenye lile bwawa ambapo tulikuta wenzetu kadhaa wakiwa washaamka. Kila mtu alitafuta upande wake wa kuoga na kumaliza haja zake zote. "sasa hapa tatizo linabaki chakula" niliongea kwa sauti ndogo kama mtu aliekuwwa hataki kusikika. "ah na matunda na miti yote hii iliojaa ufe njaa kweli, utakua huna akili" Louise alinisikia na kunijibu.



     Wakati tukiendelea kuongea, Latifa alifika na kuunga maongezi. "Tuingie ndani zaidi huenda tukapata matunda mazuri" Louise aliongee na kusimama. Mimi na Latifa tuligate kwa nyuma, tulitembea huku tukichuma matunda aina tofuti na kubugia. Tuliposhiba tulibeba na mengine kisha tukarudi walipo wenzetu. Kwa kweli hata tulikuwa hatujui siku zinaendaje, maana sisi tulikuwa tunaishi tu ili kuokoka. Pia tulikuwa na matumaini kama huenda meli nyingine ikapita na kupata msaada wa kuondoka katika kisiwa hicho, hivyo hatukuacha kutembelea ufukweni.



     Wiki ilikuwa ishakata huku wenzetu wengi wakionekana kujisahau kama wapo kwenye dhiki, kuna wakati walikuwa wakifanya mapenzi kama wanyama tu. Walifanya kweupe huku wengine wakishuhudia na kushangilia. Tulijaribu kuwaonya kuwa huenda tukawa hatupo pekeetu kwenye kisiwa hicho lakini walionekana kutoelewa kabisa. Ilibidi tuwaache wafanye wanavyotaka maana ilifika wakati mpaka tukawa tunagombana.



    ` Siku moja wakati tukiwa tunaongea mawili matatu, nilianza kusikia harufu fulani hivi ya moshi. Harufu hio haikuwa ngeni puani mwangu, "tungieni ndani haraka" nilipiga kelele huku nikionesha ishara ya hatari. Bila kupoteza muda mimi, Louise na Latifa tuliingia ndani ya kichaka chetu na kujificha. Haukupita muda nilianza kuhisi maruweruwe na kuanganguka sehemu niliokaa na kupoteza fahamu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



     Nilishtusha na mangurumo mazito huku yakiambatana na mvua kali sana, niiangaza pembeni ambapo niliwaona Louise na Latifa. Kila mtu alikuwa amelala anavojua mwenyewe, "Louise, Louise...Latifa amkeni" niliwaita huku nikiwatikisa. Louise alikurupuka kama mtu aliechomwa na mweba, "kuna nini?" na kuuliza, "mimi mwenyewe sijui lakini nahisi tumelala muda mrefu sana" nilimjibu. "Latifa amka" nilimuamsha na Latifa ambae aliamka kwa kujizoa zoa na alionesha amechoka sana.



     "hivi imekuaje tukalala bila kujitambua" aliuliza Latifa punde tu baada ya kuamka, "ni ile harufu ya moshi" nilijibu na kuwafanya wote waniangalie. "ule moshi ni kemikali aina chlorofom au nusu kaputi, inavyoonekana katika hichi kisiwa kuna watu wengine" nilifafanua na kuongezea. "unamaanisha hatuko pekeetu?" Louise aliuliza huku ametoa macho, "ndio maana yake hiyo, na inavyoonekana hawa watu si wa kawaida" alijibu Latifa.



     "hapa hapatufai tena itabidi tuhame" Louise aliongea kwa msisitizo.



     "tusubiri pakuche kwanza tuangalie hali ikoje huko nje" niliongea na wote wawili wakakubaliana na mimi. Ila hakuna hata mmoja aliepata lepe la usingiz, kwanza kutokana na hofu, pili ni kwamba tulikuwa tumelala muda mrefu hivyo usingizi wenyewe ukagoma kuja. Palikucha na kwa umakini wa hali ya juu tulitoka kwenye kichaka chetu kama visungura hivi, tuliwakuta baadhi ya wenzetu wakilia na tulipowauliza kwanini wanalia. Wakasema kuwa kuna wengine wamechukuliwa na watu wasijulikana. Ilibid tutane wote ili tujue tumebakia wangapi, na ukweli kwamb wenzetu tisa walikuwa hawapo.



     "huu mtihani mkubwa" nilijisemea moyoni, wakati tukiendelea kujadili nini tufanye. Kwa mbali nilisikia kama mlio wa gari. "Louise unausikia huo mlio wa gari" nilimuuliza ili kuthibitisha, "shit! huo ni mlio wa gari tena kubwa" Louise alinijibu. "itabidi kwanza tujue hawa watu ni wa aina gani" nilisema kwa nguvu kidogo. "acha utani wewe" Louise aliongea, "kweli tena Louise bila kujua tunacheza na nani itakuwa vigumu sana kutoroka katika eneo hili" niliongea kwa msisitizo kuonesha kuwa sikukosea mwanzo.



     "haya master plan tueleze tunafanyaje sasa" Latifa aliongea na Louise akacheka kidogo, "inabidi tupande hilo bonde, huenda juu tukapata mwanya mkubwa kulijua eneo hili na kila kitu chake" nilitoa wazo ambalo Louise aliliongea kwa tena kwa lugha tatu tofauti ambazo zilikuwa kiingereza, kijerumani na kifaransa. Hapo wale wengine waliguna kidogo na hiyo ilikuwa ishara kuwa wamelielewa. Mmoja wao aliongea kwa jambo kwa kifaransa, Louise alinigeukia na kunambia "anasema ni wazo zuri lakini ni hatari pia, ila kama litapita basi yeye amejitolea kuwemo miongoni mwa watakaopnada hilo bonde"



     Tuliendelea kujadiliana huku Louise akinisaidia kuwatafsiria wale ambao hawanielewi, mwisho tulifikia lengo moja tu kuwa watoke vijana watatu miongoni mwetu wapande lile bonde. Nilijitolea mimi, Louise na yule jamaa mwengine ambae aliitwa Akinola. Alikuwa ni mtu wa Nigeria, tuliwaaga wenzetu na kuanza safari. tulitembea mpaka kwenye bonde kabisa na kuanza kupanda. Kwa kweli haikuwa kazi rahisi hata kidogo na mara kadhaa tlikosea kuteleza na kuangulka, hata hivyo tulipiga moyo konde na kuendelea kupanda.



     Ilituchukua takribani masaa matatu mpaka kufika juu huku tukipumzika mara nne njiani, tulitafuta sehemu na kujificha ili tupumzike. Maana ilikuwa balaa si dogo mpaka kufika juu, kama ingelikuwa si kupigania maisha yangu naapa kwa Mungu ningeishia njiani. Baada ya kupata mapumziko kama ya dakika kumi hivi, tuliinuka na kuanza kusonga mbele. Macho yalitutoka baada kuona mahoteli makubwa upande wa pili wa kisiwa hicho. "yaani sisi tunapigika huku, tunaishi kama ngedere kwa kushindia matunda. Lakini upande wa pili wa kisiwa hicho hicho kuna watu wanaponda starahe" nilijisema huku nikiuma meno.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Tuliendelea kusonga mbele kwa kuufata mto huo unapotoka lakini tukiwa makini sana tusije tukakamatwa. Kwa mbali tulianza kusikia miguno lakini hakuwa ya kawaida maana yote ilikuwa ya kiume. iliidi tusogee karibu zaidi ili tujue kitu gani kinaendela, La haula tulimuona mzungu mmoja akiwa anamuingilia kijana tena wakiume. Alikuwa amemfunga kamba katika mti kiasi cha kushindwa kujitetea, nilijikuta hasira zikianza kunipanda hasa pale nilipogundua kuwa yule mzungu ndio yule mpumbavu alienifanyia mchongo wa kuingia katika meli yao. Nilinyata kama simbi na kuokota gongo kubwa.



    Bila kusita nilipomkaribia, niliinua gongo juu na kumsindika nalo la kichwa. Alipigwa ukwenzi mara moja tu na kabla hajakaa sawa nikamtwanga la pili na kuendelea kumtandika magongo ya kichwa bila huruma hata kidogo. Mwisho Louise alilishika gongo na kunambia basi maana tayari alikuwa kashakufa, tulimfungua yule kijana lakini kwa aibu aliinuka kukimbilia gogo lenye ncha kali na kujichoma. Iliniuma sana kuona kijana mwenzangu kama yule amejiuwa lakini angefanyaje na ndivyo akili yake ilivyomtuma ili kueouka aibu. Wakati tukiendelea kushangaa eneo hilo, tulianza kusika mivumo ya gari ikija upande wetu.



     Haraka tulitafuta sehem ya kujificha kwa usalama wetu, lilipita gari moja kubwa kama yale yanayobeba petroli. Ilisimama mbali kidogo na tulipo sisi lakini tulifankiwa kusikia walichokuwa wanakiongea, "hii kemikali ni sumu na endapo mtu yoyote atakunywa haya maji baada kutia kemikali hii basi atakufa" nilisikia vizuri sana. Hapo akili yangu ikawa inamuwaza Latifa tu, nilijikuta nikichomoka kama mshale huku wenzangu wakinifata nyuma kwa lwengo la kunizuia kwa maana ilikuwa ni vigumu kufikisha ujumbe huo kwa wengine. Kwasababu hata nikifika huko chini basi watakuwa tayari wameshakufa kwa sababu tulikuwa tukinywa sana.



     Jambo ambalo hawakulijua wenzangu ni kwamba, sikuwa na mpango wa kushuka bonde hilo kama nilivyopanda. Nilipofika karibu na maporomoka, niliruka tu bila hata kufikiria huko chini ntakutana na nini. Nilichoma kwenye maji na nilipoibuka tu nilianza kupiga kelele watu watoke kwenye maji. Sekunde kadhaa baadae alichoma Louise na Akinola, nao pia walipoibuka walipiga kelele watu watoke kwenye maji.



     Baada wote kutoka kwenye maji, Louise alitupa ishara kuwa tuondoke eneo hilo haraka sana maana palikuwa si salama tena hata kwa dakika moja. Tuliongozana na kuzama msituni zaidi kwa lengo la kuokoa maisha yetu, tulikuwa tukikimbia tu bila kufata njia maalum. Mara kadhaaa baadhi yetu tulijikwaa lakini tuliokotana na kuendelea na safari huku tukihakikisha hatumuachi mtu nyuma. Tuliendelea kukimbia bila kusimama kwa muda kama wa nusu saa hivi, "jamani tupumzike kidogo" aliongea mschana mmoja huku akisogea kwenye mti na kuegemea.



     "Jamani inatosha tumekimbia sana na wenginie wamechoka sana" aliongea Akinola, "hakuna shida, tutapumzika hapa kwa muda kisha tutaendelea na safari" aliongea Louise na hapo karibu kundi zima tukakaa chini. "Tuelezeni basi mumekutana na nini huko juu na kutufanya tukimbia kama panya darini wakimkimbia paka" aliongea mtu mmoja. "Nyine acheni tu tulichokikuta huko ni hatari kabisa" niliongea kwa kiingereza ili kila mtu anielewe japo sikuwa nikikijua vizuri. Wala sikuogopa kwasababu hapo walikuwepo wengine ambao walikuwa wakiongea kingereza kibovu kuliko mimi.



     "Yaani tumejitahidi kutoroka kwenye ile meli tukiamini ndio salama yetu lakini haikuwa hivyo. Inaonekana hapa kisiwani ndipo tulipokuwa tunaletwa kwa ajili ya kutumika kama vyombo vya starehe. Upande wa pili wa kisiwa hichi kuna mahoteli makubwa sana tena ya kifahari kuliko tunavyofikiria. Yaani hawa jamaa wanazunguka katika nchi masikini na kutuchota watu kama sisi ambao tunajaribu kukimbia matatizo. Wanatudanganya eti watatufikisha nchi za magaharibi huku wakitupa matumaini yasiopingika. Lakini ukweli ni kwamba wanatuchukua kilaini sana na kuja kutfanya watumwa wa ngono huku katika kisiwa hichi" nilimaliza kuongea na kuwaangalia wenzangu. Wote waliokuwepo hapo walikuwa wamejiinamia na kujiona wajinga wa hali ya juu.



    "Lakini tukikaa pamoja na kusaidiana tunaweza tukaondoka hapa kisiwani" aliongea Louise na kuwa kama alirudisha uhai katika moto ulianza kuzima.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kila mtu alianza kunong'ona na mtu aliekaribu nae huku wakionekana kubadilishana mawazo. Wakati kila mtu akiwaza lake, ghafla Louise alishtuka na kulaza sikio lake la kulia kwenye ardhi. Hakuishia hapo tu, alichota tope kidogo mkononi na kuliramba kisha akawa kama anasikilizia utamu fulani hivi.



    "Shit! Adam hii sehemu si nzuri kabisa" aliongea hukua akisimama na kuanza kuangaza huku na kule.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog