Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

SIKUTEGEMEA - 2

 







    Simulizi : Sikutegemea

    Sehemu Ya Pili (2)



    "kivipi mbona sikuelewi Louise" niliuliza, "hii njia inavyoonekana kuna myama mkali anapita mara kwa mara" alijibu huku akizidi kuwa makini. Kwa kweli huyu jamaa alikua na kipaji cha uwindaji, mimi naweza sema yeye mwenyewe alikuwa kama mnyama katika kushtukia mambo. Aliinua kichwa na kuangalia miti iliotuzunguka, alionekana kama kupiga mahesabu yake bila kupepesa macho.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



     "Jamani kwa mazingira haya tumeumia" aliongea na kukata majani kadhaa kisha akauarusha juu kuangalia muelekeo wa upepo unapuliza wapi.



     "Adam nahisi mnyama anaepita njia hii ni jamii ya paka wa kubwa" aliongea huku akisogea kwenye mti na kuangalia kwa makini.



    "Na kama ni jamii ya paka wa kubwa, huenda akawa chui mweusi au chui mwenye mistari maana ndio mazingira yao haya" niliongea bila kutarajia. Kilichonifanya niongee hivyo ni baada ya kukumbuka filamu fulani hivi inaitwa apocalipto au vijana walikuwa wanaiita filamu ya Ronaldinho wa msituni.



    "Hapana chui mwenye mistari hawezi kusihi katika msitu huu ndani ya kisiwa kama hichi" Louise aliongea huku akirudi nyuma kwa woga kidogo. Hapo wenzetu wote walikuwa wakituangalia bila kujua nini kinaendelea maana tulikuwa tunaongea Kiswahili.



    "unataka kunambia hapa anapita chui mweusi au" niliongea huku nikimeza funda kubwa la mate.



    "ndio maana yake na kwa kukadiria hivi sasa kunaelekea jioni, kutokana na upepo unavyo vuma. Huyu kiumbe atakuwa anarudi kutoka mawindoni muda si mrefu" Louise aliongea.



    "umejuaje" niliuliza sasa wasiwasi wangu ukiwa wazi,



    "kawaida ya wanyama wanamna hii mara zote hutembea kupingana na upepo, hiyo inawasaidia harufu yao kutohisika na wanyama wengine" alijibu.



     Kutokana na nilivyomuangalia kwa haraka nikagundua kuwa alikuwa akijipanga kukimbia, niliwageukia wengine na kuwaonesha ishara kuwa wakimbie lakini kimya kimya sana. Nilipogeuka mbele Louise alipita pembeni yangu kwa kasi ya hali ya juu sana. Bil kuchelewa nilimshika mkono Latifa na kuanza kutimuka. Hapa sasa ilikuwa si kuwakimbia watu bali ni kuokoa maisha yetu, nyuma yangu vilifuata vishindo vilivyoandama na kelele za woga. Nilichokifanya ni kukaza mkono wangu niliomshika Latifa na kuongeza mwendo. Mbele yangu alikuwa Louise ambae alikimbia kadiri miguu yake ilivyotoa ushirikiano.



     Wakati tukiendelea kukata mbuga tulisikia ukwenzi mzito uliofuatiwa na ungurumo mzito sana. Hapo nilielewa kuwa tayari kuna mmoja wetu kashakamatwa na kiumbe hicho kilichokuwa nyuma yetu. Ungurumo ule ulikuwa ni kama gia kwa Latifa ambae alinichia mkono na kunipita kwa kasi hali ya juu sana, na mimi sikubaki nyuma niliongeza mwendo hasa ukizingatia sasa nimekuwa mwepesi zaid.  Louise alikibia mpaka sehemu yenye mlima wa mawe na kuanza kupanda, Latifa nae alifuata huku mimi nikiunga mkondo huo. Nyuma yangu nilisikia pumzi nzito na kunifanya niongeze kasi ya kupanda mlima huo.



     Tulipofika juu Louise alisimama ghafla na kumzuia Latifa ambae alionekana kukosa breki kabisa, mimi niliwapita kidogo na kusimama kwa mbele. Nilipogeuka nyuma nilimuona mschana mmoja akimalizia kupanda mlima huo. "Hapa tutakuwa salama, hawezi kutufata huku" Louise aliongea na kukaa kitako. "kumbe wewe ndo ulikuwa nyuma yangu" nilimwambia yule mschana huku nikicheka kidogo. "ndio" alijibu, "mi nilidhani ni yule kiumbe ndio maana nilikuwa nakaza mwendo tu. Tulipoteana na wengine na wala hatukujua hatma yao ilikuwa nini, tulibakia wanne tu yaani mimi, Louise, Latifa na yule mwanadada aliejitambulisha kwa jina la Linda.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Tulibaki kimya tunatazama kwa muda huku kila mtu akihema kama farasi aliesafiri masafa marefu. "Sasa tunaganyaje" aliuliza Latifa, "hakuna cha kufanya zaidi ya kutafuta sehemu ya kujificha kwa muda kabla kiza hakijachanganya" nilijibu. "Eneo hili halina hata maji, inabidi tutafute sehemu iliokaribu na chanzo cha maji" aliongea Louise akijikaza na kusimama. "Ah bora tupumzike tu, kesho ndio tutaanza kusaka sehemu yenye chanzo cha maji" nilongea kwa uvivu sana. Tulibishana sana ila mwisho alikubali tutafute sehemu ya kulala, siku ya pili ndio tutaanza safari.



     Tulitembea kwa nusu saa mpaka kufika sehemu ambayo tulihisi ni salama kwa kuupitisha usiku. Sehemu hiyo ilikuwa na majani makubwa sana kiasi cha kutoonekana kirahisi hata kama mtu angetokea ghafla. Louise alifanya mandingo yake ya kukunja majani hayo na kufanikiwa kutengeza vibanda viwili vidogo. Kimoja kilikuwa kwa ajili ya waschana na kimoja kwa ajili yetu sisi wavulana, tulikaa nje ya vibanda hivyo kwa muda huku tukipiga soga za hapa na pale. Tulifanya hivo ili kujaribu kuutoa woga uliokuwa umejirundika ndani ya mioyo yetu.



     Tuliongea sana mpaka tukaanza kusinzia, hapo sasa kila mtu aliingia kwenye kibanda kinachomuhusu kwaajili ya kuupitishwa usiku huo ambao ndani yake ulikosa amani kabisa. Wakati tukiwa tumejilaza mimi na Louise, tulisikia kibanda chetu kikitiswa. Louise alinipa ishara nitulie tuli kama maji mtungini,



    "jamani nyie mbona hamuitiki" tulisikia sauti ya Latifa. Kwa pamoja tukashusha pumzi kisha tukatoka.



    "Mnataka nini si mkalale" niliongea kwa uvivu kidogo, "sisi tunaogopa kulala pekeetu" aliongea Latifa huku akionesha wazi alikuwa akitetemeka.



    "Sasa tunafanyaje na kibanda kimoja hatutoshi sote" aliongea Louise akiwa ameshangaa kidogo.



    "Kama vipi mimi ntalala na Latifa na wewe lala na Linda" niliropokwa tu bila hata kufikiria maana usingizi ulikuwa umenishika vilivyo.



    "Bora hivyo" Linda aliniunga mkono, basi hatukuwa na jingine la kufanya. Louise aliingia kwenye kibanda kimoja pamoja na Linda na mimi nikalala na Latifa. Sikujua huko kwa mwenzangu mambo yameendaje lakini kwangu mambo yalikuwa magumu kuliko nilivyotegemea.



     "Wewe si ulale huko na mimi huku" niliongea baada kuhisi nimeguswa mgongo,



    "Adam mimi naogopa sana kwa kweli, kama ungekuwa shuka basi ningejifunika" aliongea Latifa huku akizidi kujisogeza kwangu.



    "Sasa wewe unaogopa nini wakati hapa tumejiridhisha pako salama kupumzikia" niliongea huku nikijaribu kumsukuma kwa sababu alikuwa tayari kashanibana sana.



    "Adam tafadhali bwana usinisukume, si nimeshaakwambia naogopa" aliongea Latifa huku akiishika mikono yangu nisiendelee kumsukuma. Bila kutarajia aliitanua mikono yangu na kurudi nyuma kwa nguvu kisha akauzungusha mkono wangu na kuulaza tumboni kwake. Hapo sasa tulikuwa tumegusana kabisa, niliona hakuna haja ya kuendelea kubishana nae wakati hapo na mimi ningepata faida ya joto. Nilichokifanya ni kuupenyeza mkono wangu kwa chini na kuukutanisha na mkono wangu ambao ulikuwa tumboni kwake. Kila mtu alifunga macho kwaajili ya kulala, kutokana na uchovu hazikupita dakika nyingi mimi nikalala.



     Usingizi huo uliambatana na vijindoto vitamu vitamu na vya kufurahisha sana, na hiyo ilitokana na joto liliyokana na kugusana kwa miili yetu. Nilikuja kushtuka baada kupigwa na mwangaza wa jua usoni. Nilimsogeza Latifa pembeni ambae bado alionekana yupo katika ulimwengu mwingine kabisa. Nilitoka kwenye sehemu niliolala na kujinyoosha kidogo, "Louise, Louise pamekucha mtu wangu" niliita na baada ya sekunde kadha alitoka. Alionekana ni mwenye kuchoka sana "vipi jamaa yangu mbona mapema sana" aliniuliza.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     "Sasa ulitaka tukae hapa mpaka saa ngapi wakati unaju kabisa bila shaka tutakuwa tunatafutwa" nilimjibu,



    "basi sawa tuwaamshe hawa waschana halafu tuondoke eneo hili". Niliingia nilipolala na kuamsha Latifa, alikuwa hataki kabisa kuamka lakini nilimkomalia mpaka akaamka. Tulitoka na kuwakuta kina Louise na Linda wakitusbiri, baada kapigwa na jua kidogo tulianza safari ya kuelekea tusipopajua. Tulitembea kwa muda mrefu sana mapaka tukafika sehemu ambayo tulihisi itakuwa salama kwa kupumzika kabla ya kuendelea na safari.



     "Jamani mimi nina njaa sana" Linda alilalamika, "hata sisi tunanjaa lakini hapa tulipo hatuwezi pata chakula" nilimjibu huku nikishika tumbo langu ambalo lilikuwa linakoroma kama paka.



     "Tukifanikiwa kufika sehemu yenye maji huenda tukapata na matunda ya kula" Louise aliongea, wote tulikubaliana nae japo njaa ilikuwa ikitula ndani kwa ndani. Baada ya mapumziko mafupi safari iliendelea, tulitembea karibu siku nzima huku mara kadhaa tukipumzika.



    "Jamani naona kama maporomoko ya maji kwa mbali" Louise aliongea. Wote tuliinuka na kuangalia na bila kuuliza kila mtu alianza kutimua kuelekea kwenye maporomoko.



     Tulikimbia kwa muda kidogo mpaka tukafika sehemu hiyo, mimi wala sikusimama nilipitiliza mpaka kwenye maji na kuanza kunywa. Nilikunywa mpaka niliporidhika ndio nikapumua, baada ya hapo niligeuka na kuingalia sehemu hiyo. Nilichogundua kuwa sehemu hiyo ilikuwa ni vigumu mtu kuiona akiwa karibu kutokana na kuzungukwa na miti miti mirefu sana. Miti hio ilikuwa na matunda ambayo wala sikuwahi kula hata siku moja. Niliokota jiwe na kurusha mara kadhaa, nilifanikiwa kupata matunda na kuanza kula.



     Yaani tulikuwa tukigombania matunda hayo utasema yalikuwa dhahabu, yaani mtu anakula hili akimuona mwenzake anakula jingine. Anaacha lile analo kula na kunyang'anyiana lile jingine. Ama kweli aliesema



    "njaa mwanaume hajakosea hata kidogo, wakati wengine wanaendelea kula. Mimi au Louise mmoja wetu aliangua mengine. Tulikula mpaka mwisho tukawa tunayaangalia tu matunda ambayo tulikuwa tumeyazunguka.



    "Sasa afadhali" nilisema huku nikiegemea mti ulikuwa nyuma yangu.



     "Tumepotezana na wenzetu wote na hatujui wako katika hali gani" Latifa alioengea baada ya kushiba.



    "Hilo lishatokea na tunachotakiwa kufanya saa hivi ni kuhakikisha tunakaa pamoja mpaka pale tutakapo pata msaada" Louise aliongea.



    "Sasa mkandarasi vipi mpango wa kulala" nilimuuliza kiutani. "Ahaa hakuna shida subiri kidogo chakula kishuke ndio tuanze kazi" alijibu huku akipapasa tumbo lake.



     Tulikaa kwa muda tukiongea huku tukisaidia na mwanga hafifu kwa mwezi kutokana na kiza kilishaachanganya.



    "Muda wa kutengeza vibanda vya kulala" Louise aliongea na kuinuka lakini ghafla alishika kichwa.



    "Kuna nini tena mbona unahika kichwa" nilimuuliza, "sasa unadhani tuanakataje miti ya kutengezea na miti yenyewe minene kweli kweli" alinijibu na kunifanya na mimi kushika kichwa pia.



    "Kwa nini tusitafute ilianguka tu" nilitoa wazo, "hilo wazo zuri lakini pia ina matatizo yake" alinijibu.



    "Matatizo gani" niliuliza,

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "vijidudu, si unajua imeshakaa chini na mengine ishakaa sana na wadudu washaanza kujenga nyumba zao".

     Nilikaa kidogo kidogo nikawa natafakari huku nikiangaza huku na huko, nilijikuta nikitabamua bila kutaka. "Mbona unacheka mwenzetu" aliuliza Latifa, "unajua nimeona miti ambayo itatusaidia kujengea" nilijibu. "Mti gani huo" Louise aliuliza, "ni hio minazi" nilijibu huku nikisogelea mnazi uliokaribu kabisa. Haukuwa mrefu sana kiasi cha kutishia amani kuupanda, nilipanda mpaka juu na kuanza kushindana na makuti yaliojishilikialia vizuri katika mti huo. Mara kadhaa nilikosea kuanguka lakini hilo wala halikuniogopesha kabisa.

     Baada kungo'a makuti kadhaa nilishuka na kupanda mnazi mwngine mpaka pale nilipohakikisha makuti yametosha. Unajua kitu kingine ambacho nimejifunza kipindi cha uvuvi na kusuka makuti na kutengeneza sehemu ya muda mfupi ya kuishi. Kwa utashi nilokuwa nao juu ya sanaa ya kucheza na makuti nilifanikiwa kujenga vijisehemu ambavyo tungeweza kuupitisha usiku huo mpaka sikui inayofuata. Kutokana na uchofu safari ndefu tuliokuwa nayo tulipoweka tu vichwa chini tulipitiwa na usingizi mzito.



     Siku ya pili mapema tulianza kazi ya kutafuta miti ya kujengea, japo tulikuwa wageni eneo hilo lakini kwasababu tulikuwa na Louise kazi haikuwa ngumu. Tulipata miti ya kutosha ya kujengea na tukaanza kazi, tulijenga kwa kasi sana maana usiku ukiingia ni shida. Kulikuwa na baridi kupita malelezo, tulufanikiwa kumaliza mapema tu. Tulipohakikisha vibanda hivyo vimesimama na vinafaa kuishi kwa binaadamu tulipongezana sana.



    "Jamani kwa sasa itabidi tuzoe mazingira kwanza maana kurudi ufukweni ni kujitafutia kifo tu" niliongea wakati tuna tunapata kula. Usije ukadhani ni kula ipi, tulikuwa tunakula matunda mwitu tu.



     "Ni kweli kabisa, kwa sasa itabidi tukae huku, baada ya muda kupita ndio tutarejea ufukweni kuangalia uwezekano wa kurudi uraiani" Louise aliniunga mkono.



    "Pia maisha hapa hayatokuwa magumu kwa sababu tunapata kila kitu, matunda na maji na ndivyo tegemezi letu kwa sasa maana hata kuwasha moto ni hatari" aliendelea kuongea. Tuliendelea kupiga domo, kwa muda tulisahahu kabisa kama tupo katika wakati mgumu sana wa maisha.





    Kasheshe ilikuwa kwenye kuoga sasa, sio kwamba maji yalikuwa hayatoshi. Laa, japo kulikuwa na maporomoko ya maji lakini hapakuwa na sehemu kubw sana. Hivyo ulipoika wakati wa kuoga kila mtu alikuwa anaona aibu kuvua nguo mbele ya mwenzake. Kutokana na hilo ilibidi sisi wanaume tuingia vibandani ili kuwaachia wanawake waoge kisha ndio tuende sisi. Si unajua kuoga ya wanawake, wanaoga utadhani hiyo ndio mara yao ya mwisho kuoga.

     Walipomaliza wao ndio tukaingia mimi na Louise, dakika kadhaa tu tulikuwa tumemaliza. Baada ya hapo tulikaa sehemu na kuanza kuongea mawili matatu. Kiza kilianza kuingia hivyo tulipata chakula cha usiku na kila mtu akaingia kwenye kibanda chake kwa ajili ya kupisha usiku huo ulioandamwa na rasha rasha za mvua. "Hivi tunalalaje" Latifa aliniuliza, "ah kama kawaida tunalala mzungu wa nne" nilimjibu kisha nikageuka upande wangu na kujilaza.

     "Adam mwenzio nasikia baridi" kabla hata sijafumba macho nilimsikia Latifa akiongea, "ah na huku hata blanket" nilimjibu bila kugeuka. Ghafla akaniwasha kofi zito, "sasa mbona umenipiga" niliongea huku nageuka. "Mimi nakwambia kitu cha maana wewe unadhani masihara" aliongea kwa sauti iliojaa deko. "Ah sasa mimi nakusaidi.." kabla sijamaliza hata kuongea, nilishangaa kashanivamia. Wakati nataka kumtoa aliniwahi mikono na hapo akasogeza midomo yake laini na kukutanisha na ya kwangu. Hapo mtoto wa kiume nikaishiwa ujanja kabisa na kumpokea kwa mikono miwili. Naam na baridi niliisahau kabisa na ulimwengu nikahama na kuelekea ulimwengu wa huba uliojaa rasha rasha za upendo na kibaridi cha kukonga moyo.

     "Adam nakupenda sana" alininong'oneza maneno hayo wakati tukindelea na starehe yetu ambayo ni haramu kuifanya kabla ya ndoa. Bila kusita nilimuekea kidolo mdomo kama ishara anyamaze na tuendelee na furaha yetu. Hata sijui saa ngapi nilipitiwa na usingizi baada ya kumaliza tendo hilo, nilikuja kushtuka asubuhi baada ya kupigwa na miale ya jua. Ndege pia walionekana kulifurahia jua hilo la asubuhi huku wakiimba kwa sauti zao walizoajaaliwa na muumba. Bado Latifa alikuwa maungoni mwangu na alionekana kuchoka sanan. Hivyo sikutaka hata kumuamsha na mimi nikafunga macho kwa ajili ya kuongeza masaa ya kulala.

     Maisha yetu yaliendelea hivyo huku tukiishi kama watu wa msituni, maana mwisho aibu ilitutoka kabisa. Kiufupi hatukua na tofauti na wanyama kwa sababu kuna wakati tulifanya mamabo ambayo hayaykustahiki kufanywa hadharani kabisa. Lakini tungefanyaje maana utu ulikuwa umeanza kutuvuka, hiyo ilitokana na kukaa ndanu ya pori hilo kwa muda mrefu huku tukihesabu masiku tu. Nakumbuka siku hiyo niliamka mapema kuliko wenzangu wote, nilitoka ndani ya kipanda changu na kuelekea mtoni kwa ajili kutimiza yale mahitaji yangu ya asubuhi. Wakati nikiwa katikati ya shughuli nilihisi kitu kama mwiba kikinichoma mgongoni na ghafla nilianguka na kupoteza fahamu na sikujua nini kilindelea.

     Wakati nikiwa katika usingizi mzito nilihisi kama watu wakipiga kelele huku wakicheza ngoma. Nilifumbua macho kivivu ili kuangalia ni kitu gani kinaendelea maana nilihisi niko ndotoni, lakini haikuwa hivyo kila nilichokiona mbele yangu kilikuwa kweli tupu. Niliona watu wengi wakicheza na kururuka huku wakizunguka moto mkubwa sana uliokuwa unawaka na kutoa mgurumo mkubwa kuonesha n jinisi gani ulivyokuwa mkali.

     "Kumbe ni kweli watu aina hii wapo duniani" nilijisemea mwenyewe huku nikiushidi kabisa moyo ukipiga kwa nguvu na kusababisha kifua changu kupanda na kushuka kwa kasi sana. Maisha yangu yote nilidhani kuwa jamii za watu wa aina hii haipo tena duniani. Najua utakuwa unajiuliza watu aina gani, usijali nitakwambia tu. Inasadikika zamani kulikuwa na watu wanaokula watu nyama za watu wengine, wanajulikana kama canibals. Kwa kweli siku hiyo nilidhani nimeshaageuka kitoweo maana kwa zile staili walizokuwa wakicheza, wazi kuwa walikuwa wakisheherekea kwa kupata kitoweo safi.

     Nilijaribu kuangaza huku na kule ili kutafuta kama kuna uoenyo wowote wa kutoroka hatari iliokuwa mbele yangu. Lakini hakukuwa na upenyo wowote ule, nilikuwa nimefungiwa ndani ya banda la miti. Nilivyogusa ilikuwa migumu kwelikweli, bila shoka kulikuwa hakuna uwezekano wa kutoroka eneo hilo. Nilihisi haja ndogo na kubwa zikitaka kutoka, tena zilitaka kutoka kwa wakati mmoja zote. Aisee japo kulikuwa na baridi usiku huo lakini kijasho chembamba kilikuwa kikinitoka usoni.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Wakati nikiwa katika dimbwi la mawazo ghafla niliskia mlango ukifunguliwa, waliingia wanaume wanne walioshiba. Walinishika kwa nguvu na kunifunga kamba mikononi na miguui, kisha wakanibeba na kunitoa nje ya banda kisha wakachukua gongo na kulipitisha miguuni mpaka mikononi na kunining'iniza. Yaani kama umewahi kuona wawindaji wa zamani wanavomuweka mnyama baada ya kumuwinda basi ndivyo hivyo hivyo nilivyokuwa nimening'inizwa.

     Nilijaribu kuomba msamaha waniachie lakini ilikuwa ni kama napigia mbuzi gita maana hata lunga niliokuwa naongea walikuwa hawaifahamu. Walinipeleka mpaka karibu na moto na kuniweka pembeni kabisa na moto huo. Baada ya hapo walikaa pembeni na kuinamisha vichwa vyao, hapo sasa nilimuona mmoja kati yao akiinuka kutoka katika kiti kikumbwa kilichotandikwa ngozi ya chui, Mtu huyo alikuwa na kofia kubwa iliosukiwa manyoya fulani hivi ya ndege nisiemfahamu. Alikuwa na mwili mkubwa kidogo, alikuwa mweusi tii kama nyungu inayopikiwa kwa kuni, alikuwa ni kiongozi wao.

     Aliinua mikono juu na kuongea kitu kwa nguvu sana, wengine wote walishangilia kwa nguvu. Hasa wanawake waliruruka kwa nguvu na kufanya vifua vyao vilivyoshiba chakula cha mtoto kutii miruko hiyo na kwenda chini na juu. Yaani mimi wakati huo nilikuwa nalia kama mtoto mdogo alienyimwa ziwa na mamae. Kilio hicho kiliambatana na kamasi laini iliotengeza njia yake na kutoka nje ua nuymba yake. "Ee Mungu wangu, niokoe na hili janga. Najua kama nimekukosea lakini sistahili adhabu ya aina hii" nilijisemea moyoni huku nikianza kuomboleza kifo changu mwenyewe.

     Lakini ghafla wakati akiendelea kuongea kile nisichokielwa, mvua ilianza kunyesha tena ilikuwa kubwa sana na kila muda ulivyozidi kuenda ndivyo ilivyozidi kunyesha. Moto ulianza kufifia na mwisho ukazima kabisa na hapo nikaanza kusikia vilio. Yule aliekuwa kiongozi wao aliongea kitu kwa nguvu na hapo wale jamaa waliokuja kunitoa kule bandani wakanabeba na kunirudisha tena kule kule. Yaani kunyesha mvua ndio imekuwa pona pona yangu, kweli Mungu alikuwa amesikia kilio changu.

     Walinifungia na wao wakaondoka, wakati huo machozi yalishakata. Nilitafuta kona katika banda hilo na kujikunyata kama paka aliemwagiwa maji ya baridi. Hapo sasa ndio mawazo ya wenzangu yakanirudia kichwani, picha ya Latifa mschana niliempenda  kuliko wanawake baada ya mamaangu mzazi ambae alikuwa tayari ni marehemu. Pia niliwakumbuka Louise na Linda, kwa kipindi kifupi ambacho nimekaa nao basi wameweza kutenengeza makazi yao ya kudumu.

     Nilihisi moyo wangu ukimenyeka na kukatika vipande, nikiwa katika hio usiingizi ulinipitia na kunihamisha ulimwengu. Nikiwa usnigizini nilianza kuota ndoto mbaya sana, ndoto ilionionesha nimekatwakatwa vipande na kupikwa vizuri. Watu walikuwa wakila nyama yangu huku wakifurahi sana, tena walikuwa wakicheka sana. Nilikurupuka kutoka usingizni huku nikihema kwa kasi sana, kitu cha kwanza nilijiangalia kama kuna kiungo chochote kimepungua mwilini mwangu maana ile ndoto haikuwa ya kawaida hata kidogo.

     Nilipoangaza vizuri tayari kulikuwa kumeshaanza kukucha, wanajamii wa sehemu hiyo walikuwa wakiendelea na shughuli zao za kawaida. Hawakunyesha kujali kabisa uwepo wangu eneo hilo isipokuwa watoto tu ndio walikuwa nje ya banda hilo wakinishangaa na kucheka cheka. Kiu ilikuwa imenibana sana na nilitani kuomba maji lakini nikawa sijui nianzie wapi maana ni sawa na kuku kuongea nabata kitu ambacho hakiwezekani. Mwisho nikaona bora ninyamaze tu maana sikuwa na jinsi.

     Siku hiyo iliisha kwa mtindo wa kushinda na kiu yangu, usiku uliingia na baridi siku hiyo ilizidi kuwa kali. Sitoweza kusahau nilivyoteseka na baridi siku hiyo, nilihisi ngozi kama inataka kuchanika. Wakati nikiwa nimejikunyata katika pembe moja wapo ya banda hilo, nilisikia mruzi wa sauti ya chini. Niliangaza kutafuta wapi mruzi huo ulipotoka, "Adam" nilisikia jina langu likiitwa. "Louise unafanya nini hapa" niliuliza baada ya kutambua kuwa sauti hiyo ni ya Louise. "Nimekuja kukutoa mtu wangu, marafiki hawaachani nyuma" Louise aliongea kwa sauti ya chini.

     "Hii miti migumu sana, na huwezi kuivunja kama huna silaha" nilimjibu huku nikisogea alipo. "Ah kuna sehemu itakuwa imelegea tu, tukiipata hiyo sehemu utaweza kutokan ndani ya banda" alinijibu na papo hapo tukaaanza kutafuta sehemu iliolegea. "Hii hapa nimeipata" nilimsikia Louise akiongea, nilsogea sehemu aliopo na tukasaidiana kuusogeza mtu uiolegea. Kweli nilpata nafasi ya kutoka, sijui nguvu niliizipata wapi. Yaani baada ya kutoka tu nilitoka mbio, hata kama kungekuwa na chui au simba au mnyama mwengine yeyote basi aingenikamata badala yake angeambulia vumbi tu.

     Louise alikuwa nyuma yangu na alijitahidi kuashikamana na mwendo wangu, kweli mlemavu kaponyoko meno ya simba usiulize kaponyokaje maana jibu utakalopewa halitokurdhisa kabisa. Baada ya kukimbia kwa muda mrefu hatimae nilisimama na huku nikihema kama mbwa, "duh, ndugu unakimbia" Louise aliniambia huku akiwa ameshika magoti kuashiria kuwa alikuwa amechoka sana. "Kina Latifa wako wapi" nilimuuliza, "nimwaacha kule tunapokaa" Louise alinijibu. "Ile sehemu haifai tena twende haraka tukawachukue tuondoke" nilimjibu nikijaribu kuchora ramani kichwani mwangu jinsi ya kufika kule tulipokuwa tunakaa.

     "Poa nifuate" Louise aliongea na kuongoza njia, tulitembea kwa muda kidogo. Latifa alikuwa amekaa karibu na mto, na aliponiona tu alikuja mbio kunikumbatia. Jamani kupendwa raha acheni kabisa, kwa sekunde kadhaa nilisahau kabisa kama nimechoropoka kifo. Tuliwaeleza hali halisi na wao waliubaliana na sisi na muda huo huo safari ikaanza. "Sasa tunaelekea wapi" Linda aliuliza, "tunaelekea ufukweni tujaribu bahati yeti kama itapita meli yeyote" nilimjibu huku nikikzana.

     "Hivi Louise umejuaje kama nilikuwa kule" lilinitoka swali hilo kinywani mwangu maana lilikuwa limenikaa sana. "Siku uliochukuliwa nilikuona, lakini nikashindwa kufanya chochote kutokana na wale watu walikuwa wengi. Hivyo nilianza kufatilia kwa siri mpaka ulipofikishwa kule kijijini. Hata hivyo ilibidi nitulie sikuwa na uwezo wa kufanya chochote kwa wakati ule. Nilirudini kambini kujipanga kwanza kabla kurudi tena kwa mara ya pili. Lakini usiku wake siku ile nikasikia ngoma, kwa kweli nilijua kabisa kuwa rafiki yangu unakuwa kitoweo. Lakini bado Mungu alikuwa upande wako, ile mvua ndio iliokuokoa.Nilirudi tena kijijini usku wa kuamkia leo na ndio nikafanikiwa kukutorisha" alimalizia hapo.

     "Yaani ndugu yangu nahisi kama usingeniokoa, saa hivi wale viumbe wangekuwa wanachezea matumbo yao huku wakimalizia kulamba mifupa yangu" niliongea na kuwafanya wote wacheke. "Kama si tamaa za kimaisha leo nisingekuwa hapa" nilijisemea moyoni, "Sikutegemea, ama kweli matatizo hayakimbiwi". Tulitembea kwa muda mrefu sana mpaka miguu ikaanza kugoma kutoa ushirikiano, "jamani tupumzikeni maana hii miguu nahisi inawaka moto" Linda aliongea na kukaa kitako kabisa. "Sawa tutapumzika hapa kwa muda kisha tutaendelea na safari" Louise aliongea na yeye akakaa. Mimi sikukaa tu bali nililala kabisa maana mwili wangu wote ulikuwa unauma kama kidonda.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Kwa bahati nzuri pia tuliondoka na matunda kadhaa, hivyo tukapata matunda kidogo ili kuyafurahisha matumbo yalioonekana kunguruma kama gari kwa njaa. Baada ya mapumziko ya kutosha, safari ilianza tena. Tulitembea siku nzima huku tukipumzika mara kadhaa, usiku nao ulianza kuonyesha nguvu zake kwa kusambaza kiza chake. Bila hata kufikiria tayari kiza kilishaatanda kabisa, hatukua na kipanda wala nini. Na sehemu tulikuwepo ilikuwa tambarare kabisa, "leo tutalala hapa, na tuombe mungu tu mvua isinyeshe" Louise aliongea. "Hata ikinyesha ntalala hivyo hivyo" nilijikuta nikisema kwa nguvu na kukaa kwenye nyasi.

     Latifa alikaa pembeni yangu na kunishika mkono, "tuombe Mungu tuokoke na hili janga" aliongea kwa sauti ya chini. Nilimsogeza karibu na kumkumbatia kisha tukajilaza chini kwaajili ya kuupitisha usiku. Kutokana na uchovu sikuwaza kufanya chochote zaidi ya kulala tu maana nilikuwa nimechoka kuanzia akili mpaka kiungo kidogo chao mwilini. Japo kulikuwa na baridi sana lakini sikuihisi kabisa, yaani nililala kama mtu aliepuliziwa dawa ya usingizi. Wakati nikiwa usiningizini nilihisi mtu akinitingisha.

     "Adam amka kaka, kuna msala unakuja" japo nilikuwa usingizini lakini niliifahamu fika kuwa asuti hiyo ilikuwa ni ya Louise. Nilifungua macho kivivu na kuuliza, "mbona tunakatiashiana usingizi". "Nasiki sauti za magari zinakuja upande huu" Louise aliongea kwa sauti ya chini, hapo sasa usingizi wote ukaniruka na kuinua masikio kama mbwa kusikiliza kama ni kweli. "Ni kweli kaka, waamshe hao tuondoke" niliongea huku nikisimama na kuanza kumuamsha Latifa. Louise nae alimuamsha Linda, walipoamka tuliwaonesha ishara watulie. "Kuna gari zinakuja upande huu, inabidi tuondoke sasa hivi" niliongea huku nikimshika Latifa mkono.

     Kwa mwendo wa haraka tulianza kutembea huku tukiwa makini sana, ghafla Linda alikaja mwiba na kutoa ukwenzi wa maumivu kabla Louise hajamuwahi. Lakini keki ilikuwa ishaingia mchuzi, maana tuliona taa za gari hizo zikija upande wetu. Gari hizo zilikuwa zinakuja kasi sana, huku mataa makali ya juu katika gari hizo zikimulika sehemu tulipo na kutufanya tuonekane vizuri zaidi. Ngoja nikueleze kitu ndugu msomaji, sifa yangu moja nzuri sana na nashukuru mungu kwa kunipa sifa kama hiyo, Mimi ni mwepesi sana wa kufanya maamuzi hasa nikishaona hatari inakuja.

     Kabla hata wenzangu hawajafikiria wafanye nini, niliukaza mkono wangu uliokuwa umeshika mkono wa Latifa na kuanza kuchapa ndala. Louise nae aliniunga akiwa kamshika Linda ambae alikuwa akilia kutokana na maumivu aliokuwa anayapata. "Simameni au tunafyatua risasi" tulisikia sauti hiyo lakini mimi sikuijali kabisa, niliendelea kuchanja mbuga tu. "Adam tusimame watatuua hawa watu" Latifa aliniongelesha wakati tunakimbia. "Mimi bora waniue kuliko kuniepeleka kule kambini kwao" niliongea kwa nguvu huku nikiendelea kuchana upepo.

     Wakati tunakimbia sikuwasikia kina Louise nyuma yangu, lakini hilo halikunifanya nisimame. Nilidhamiria kufanya maamuzi magumu sana ya kuendelea kutetea roho yangu. "Nyinyi ndio hamusikii, si ndio" nilisikia sauti ikiongea tena. "Wewe piga tu risasi lakini mimi sisimami" nilijisemea moyoni, lakini ghafla nilishangaa Latifa kuutoa mkono wake kwa nguvu jambo lililopelekea yeye kuanguka kutokana na kasi niliokuwa namvuta.

     Nilisimama ili kumrudia lakini nilimsikia akisema "Adam mimi siwezi tena kukimbia, nimechoka. Wewe endelea na safari". Na nilipoangalia vizuri wale jamaa walikuwa washamkaribia sana, "ni mwendo wa maamuzi magumu tu" nilijisemea moyoni na kugeuka na kuanza kukimbia tena. "Adam jitahidi kidogo tu, msitu huo hapo mbele yako. Hiyo ndio salama yako" sauti yangu mwenyewe iliniongelesha na kunifanya nizidi kuchochea miguu. Najua utajiuliza kwanini nilikuwa nawaacha mbali, hiyo ilitokana na sehemu hiyo kuwa na miinuko na mashimo mengi sana kiasi kwamba ukiendesha gari kasi lazima utapinduka.





    Nilifanikiwa kuingia msituni ndipo nikasimama kuvuta pumzi maana kifua kilikuwa kinawaka moto. Niliegemea kwenye mti huku nikihema kama chui alieukuza windo na kulikosa, kabla hata sijakaa sawa niliona miale ya taa ikija msituni. "Yule pale" nilimikia mmoja wo akisema, kabla hata sijafikiria nifanye nini ghafla nilisikia mlio wa risasi lakini haikunipa ilipiga kwenye mti. Akili yangu ikatuma taarifa miguuni kuwa ifanye kazi yake. Na bila kujishauri mara ya pili nilianza kutimuka tena, yaani kiukweli hasa sijui pumzi zile za kukimbia muda mrefu nilizitoa wapi.



     "Wewe si ndio nunda sio" nilimsikia mtu akiongea kwa mbali,



    "bora niliwe hata na mnyama kuliko kukamata na nyinyi mkanifanya shoga" nilijisemea na kuongeza mwendo. Wakati nazidi kuruka vihunzi na vituta, mashimo na mizizi ghafla nilishtuka nimekanyaga hewa na kuanza kuanguka. Kumbe nilikuwa nimefika mwisho wa bonde nililokuwa nakimbia, katika maisha yangu sijawahi kuanguka umbali kiasi kile. Nilitamani nitoke mbawa niruke lakini wapi, hata hivyo bahati ilikuwa kwangu. Maana chini kabisa kulikuwa kunapita mto, hivyo nilichoma ndani ya maji lakini kutokana na kasi niliofika nayo. Nilikwenda moja kwa moja mpaka chini kabisa na kupiga kichwa katika sakafu ya mto huyo japo haikuwa na mawe lakini nilikata mawasiliano na mwili mzima na kupoteza fahamu.



     Nilikuja kushtuka nimo ndani ya kipanda, niliangaza pande zote kuangalia kama kuna mtu yeyote. Na nilipojaribu kusimama nilishindwa kutokana na kichwa kuuma kama kinachogongelewa msumari. Hivyo sikuwa na budi nilirudi tu chini na kuendelea kulala, wakatia natafakari niko wapi. Ghafla aliingia mwanaume mmoja mzee sana, sura yake likuwa ina michoro kadhaa. "Tobaa nimerudi kule kwa wale wanaokula nyama au" nilisemea moyoni, lakini hofu ilinitoka baada ya yule mzee kunisogelea pale nilipolala na kunishika kichwa. "Unajisikiaje kijana" nilishtuka aliponiuliza hivyo, tena cha ajabu sana aliniuliza kwa kiswahili.



     "Hivi mimi naota ama vipi" niliongea kwa sauti kubwa kidogo mpaka yule mzee akanisikia, "hapana kijana wala huoti kila kitu unachokiona ni kweli" alinijibu na hapo nilithibitisha kuwa sioti. Baada ya hapo alitoka na nje kurejea baada ya dakika muda kidogo akiwa na bakuli mkononi. "Kunywa hii dawa itakusaidia kupunguza maumivu ya kichwa" alinikabidhi bakuli hilo na kuongea. Aisee sijawahi kuja dawa chungu kama ile tokea nizaliwe, ilikuwa chungu kiasi kwamba kila nlivykuwa nikipiga mbwewe uchungu niliuhisi mdomoni.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Na kweli baada ya muda kupita kichwa kiliacha kuuma kabisa na hapo ndio nikapata uwezo wa kusimama na kutoka nje. Nilishangaa kukuta watu wengi wakinisubiri hapo nje. Yule mzee aliongea kwa lugha nisioifahamu, alipomaliza baadhi yao walinifuata na kunishika mkono na kunisogeza kwenye kiti kizuri kilichotengenezwa kwa ngozi ya chui mweusi. "Unawitwa nani?" mmoja wao aliniuliza akimaanisha naitwa nani, "Naitwa Adam" nilimjibu na hapo aliangua kicheko na kumfata yule mzee na kumwambia kitu. "Amekwambia nini" nilimuuliza, "anasema anataka umfundishe kiswahili" alinijibu huku akicheka. "Kijana ilikuwaje ukafika huku?" swali hilo lilifuata, "kwa kweli mzee wangu ni hadithi ndefu sana inayonifanya nijione mjinga na mpumbavu mwenye PHd, sikutegemea ila kwa kweli matatizo hayakimbiwi. Laiti kama ningeliridhika na kipato alichonijaalia Mungu leo nisingekuwa hapa" niliongea huku nikitiririkwa na machozi.



     Nilimueleza kila kitu kilichonikuta mpaka nikafika pale, "kijana haya ndio maisha, usipofunzwa na mamayo basi utafunzwa na ulimwengu" alianza kwa methali hiyo. Ila kabla hajaendelea nilimkatisha kwa kumuuliza imekuwaje mpaka  yeye akawa sehemu ile kwa wakati ule. "Mimi sikufika hapa kwa kutaka kuzamia kama wewe, miaka takribani thalathani ilopita nilikuwa mwanafunzi wa chuo cha Muhimbili. Nilikuwa nikisomea udaktari, hakika niliupenda sana hivyo nikawa nashiriki semina nyingi sana za ndani ya nchi na nje ya nchi. Siku moja nilipata bahati ya kushiriki katika uchunguzi maalum, nakumbuka kipindi hicho nilikuwa nachukua shahada ya uzamili.



     Tulichaguliwa wanafunzi watatu kutoka Afrika Mashariki, tulisafirishwa mpaka nchini Marekani ambako tulipewa mafunzi kwa muda wa miezi mitatu kabla ya kuanza uchunguzi. Tulizunguka visiwa vingi sana kusaka miti mizuri ya kutenegezea dawa, na ndipo tukafika katika kisiwa hichi. Hapa ndipo tulipoupata mti tuliokuwa tunautafuta, na mimi ndie mtu wa kwanza kuugundua lakini kama unavyojuwa wenzetu hawataki wawe chini yetu. Hivyo walipanga mbinu za kutuuwa, mbinu hiyo ilifanikiwa kwa wenzangu wawili lakini mimi nilifanikiwa kutoroka.



     Baada ya hapo waliondoka kabisa kisiwani hapa na kuniacha nikiwa natanga tanga nisijue nini cha kufanya. Mwisho nilikata tamaa ya kabisa ya kurudi tena katika ulimwengu wa kawaida, hivyo nikaamua kuanzisha makazi yangu huku huku. Na kazi yangu kubwa ilikuwa n kutafuta miti shamba ambayo ni dawa. Baada ya miezi mingi sana kupita, siku moja wakati nazunguka msituni ndipo nakijikuta mikononi mwa jamii hii. Walinikamata na kunileta huku kijijini kwao, walikuwa na lengo la kuniua. Lakini kwa bahati nzuri au mbaya mtemi wao aliumwa ghafla na jitihada za kuokoa maisha yake ziligoma kabisa.



     Sijui hata ujasiri nilitoa wapi lakini niliwaomba kwa lugha ya ishara kwa sababu tulikuwa hatufahamiani lugha ya maongezi kuwa ninia uwezo wa kumtibu kiongozi wao. Walinikubalia na kweli kwa elimu alionipatia mungu nilifanikiwa kujua tatizo na kufanikia kumtibu. Alipopona tu alinifanya kuwa muuguzi mkuu wa jamii yao na kuniozesha binti yake. Walinifundisha tamaduni na miendendo ya  maisha yao na tokea siku hiyo nikiwa miongoni mwao" alimaliza kunieleza mzee huyo. Muda wote nilibakia mdomo wazi huku nikiwa na maswali kadhaa kichwani.



     "Hivi huku upo kwa muda gani sasa" nilimuuliza, "huu ni mwaka wa thalathini na tatu sasa" alinijibu. Nilibaki nimekodoa macho kama mjusi aliebanwa na mlango, hapo ndio nikathibitisha ule msemo wa kimtaani "hakuna sehemu ambayo wabongo hawapo". Msemo huo nilikuwa nikiusikia tu kwa vijana wenzangu lakini siku ndio siku niliothibitisha siku hiyo. "Samahani mzee wangu lakini sijakujua jina bado" nilimuuliza tena, "mimi naitwa Robert Augistino au wazee na wanafunzi wenzangu walipenda kuniita Robby" alinijibu huku akitabasamu.



     Katika vitu ambavyo sikutegemea kukutana navyo katika masiha yangu, moja ni hii safari ya kwa obama iliobadilika na kuwa ya mwituni. Pili ni kukutana na mtanzania anaeishi miongoni mwa makabila yanayosadikika kutokuwepo tena duniani. Kutokana na hali yangu kutokuwa nzuri sana niliamua kukaa na jamii hiyo bila kuuliza njia ya kuondoka katika kisiwa hicho. Maisha ndani ya jamii hiyo hayakuwa magumu kabisa, watu wake walikuwa wakarimu tofauti na wale walionikamata mara iwa kwana kutaka kunifanya supu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Baada ya muda kidogo kupita ndio nikaanza kumuuliza Mzee Robert kama kuna uwezekano wa kuondoka kisiwani hapo. "Kijana kuondoka katika kisiwa hichi ni kama ndoto" alinipa jibu lilikuwa mwiba moyoni mwangu. "Lakini kuna boti upande wa pili wa kisiwa hiki japo sina uhakika kama ni nzima au mbovu. Boti hiyo kama itakuwa nzima ndio itakuwa njia pekee ya kutoroka hapa kisiwani" alinipa maelezo hayo kidogo yakarudisha matumaini. Kichwa changu kilianza kupiga mahesabu ya kutoroka, lakini kabla sijafika mbali katika mipango yangu niliwakumbuka wenzangu ambao sijui maisha yao yakoje huko walipopelekwa baada ya kukamatwa.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog