Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

DUWA LA KUKU - 1

 







    IMEANDIKWA NA : MIRAM 3



    *********************************************************************************



    Simulizi : Duwa La Kuku

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Kuna mambo mengine ukihadithiwa unaweza kusema ni hadithi tu, au ni visa tu vya kutunga tu na wengine wanasema wewe unayaandika haya, umesaidia wangapi....kweli tuone tusiseme, kweli tumeona , tumesikia, tusiseme tukae kimia tu kwa vile hatuwezi kusaidia,..mimi naona kusaidia tuliojaliwa nako ndio huku kusema, kuyaelezea yale mabaya yanayotokea, huenda ikawa ndio sabau ya watu kubadilika...



    Na haya wengine hawaamini,...kutokana na mitizamo mbali mbali...lakini hakuna aliyeomba,..labda tusuibiria, yatukute ndio tutaamini maana ndio hulka zetu, tunaamini kwa mifani, tunasaidiki kwa kuona, na ndio maana mabeberu wanatunga uwongo, ili kutupumbaza akili zetu, si ndivyo tunataka kwa mifano ndivyo wanadamu tulivyo,  …watu wanafikia hata kutokumuamini mwenyezi-mungu kiukweli kutoka moyoni, wanaamini tu mdomoni, mpaka wapatwe na mitihani mikubwa ndio utamsikia mtu akisema mungu wangu nisaidie.



    Wakati naliwazia hili, nikakumbuka kisa cha binti, ambaye alikuwa mfanyakazi wa ndani, ambaye wakati ananihadithia kisa hiki, alikuwa kambeba mtoto mgongoni, sasa ni mama mlezi,…hajui watakula nini, lakini hajakata tamaa!

    Nilimuangalia yule mtoto aliyembabe, akahisi ninataka kusema nini, akatangulia kusema;



    ‘Sasa nina huyu mtoto, lakin mpaka sasa sijajua baba yake ni nani…’akasema



    ‘Kwanini, kwani huyu mtoto ulimpataje..?’ nikamuuliza.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Mungu ndiye shahidi yangu kwa kauli hiyo…, maana hata niongee nini, ni nani atanisikiliza, nimejionea nijinyamazie tu…, na kuna kipindi nilitaka kwenda mahakamani, lakini nilichokipata nikasema basi tena.., nimuachie mungu japokuwa duwa la kuku halimpati mwewe….’akasema aionyesha uso w majonzi.



    ‘Kwanini usinisimulie kisa cha matatizo yako, huenda ikawa ni sababu sio kwako wewe tu, bali na iwe ni sababu ya wengine kuliona hili jambo kwa ukweli wake, kutoka kwako, maana kwa hivi sasa watu hawalijua au sio..kama ulivyosema,…, na wanasema mengi ..si ndio hivyo, watu si wanasema mengi ambayo sio sahihi kuhusu huyo mtoto..?’



    ‘Ni kweli, na sitaki tena kuwaambia lolote nimewaacha waongee tu, lakin siri ya matatizo haya nayafahamu mimi mwenyewe, na nimeamua, nitahangaika na huyu mtoto, mpaka atakua mkubwa.., na ipo siku ataniuliza baba yangu ni nani, ndio hapo nitampa jibu ambalo hatalisahau..’ilikuwa kauli ya huyo mdada, aliyekuwa mfanyakazi wa ndani.



    ‘Haya niambia ilikuwaje, …huyo mtoto ulimpataje, na baba yake ni nani..?’ nikamuuliza.



    ‘Hivi uniamini….Nimeshakuambia baba yake mimi simjui,..hadi hii leo, sio kwamba naongea hili kwa kuogopa kumtaja, hapana, naongea hivi kwa vile kiukweli simjui hasa baba wa huyu mtoto ni nani….mungu mwenyewe ndiye anayemfahamu, na huenda kafanya hivi ili iwe mtihani kwangu na kwa hao walionifanyia hivi…’akasema.

    ‘Hao waliokufanyia hivyo, ina maana ni wengi, labda samahani,..walikubaka..au..?’ nikauliza



    ‘Walinibaka!!…Mhh,…hata sijui…nakuambia simjui,…na ..oh, tuyaache tu…’akasema



    ‘Sawa labda unisimulia ilikuwaje,..’nikasema, na yeye akaniangalia machoni, halafu akatizama chini, baadae akasema;



    ‘Naogopa sana kulisimulia hili,…nilitaka nije kumsimulia huyu mtoto akikua,…najua yeye atakuja kuniamini, wengine hawataki kuniambi…waliniona ni Malaya…niliipata kwa …wapiga debe , kama alivyosema huyo mama na mumewe….’akasema



    ‘Mama yulee, aliyekuchukua kwa mama yako na mumewe au sio…?’ nikamuuliza



    ‘Ndio….hata huwezi kuamini…yaani ni watu wema kabisa,…ukiwaona wakiongea hivi, huwezi amini, na hata mimi sikuamini hilo mpaka siku …ulipotokea huu mtihani…’akasema.



    ‘Sasa naanza kupata picha…huyo baba huyo anaweza kuwa baba wa huyu mtoto au sio..?’ nikauliza.



    ‘Hapana….siwezi kumuhukumu huyo baba wa watu..sijui, kama ningelijua ningelimtaja, kwanini nimfiche..lakini mama alinifundisha kitu, nisiwe muongo, na nisiseme jambo kama sina uhakika nalo,….’akasema



    ‘Sawa, ….nimekuelewa.



    ‘Mimi nitakusimulia, kisa hiki, ..nimekusikia sana kwa jinsi gani unavyoandika visa vyako vya kuwasaidia watu kama mimi, nitakusimulia kwa sharti moja, usije kunitaja jina langu, au la hao walionitendea hivi..’akasema.



    ‘Hilo usijali,…’nikasema.



    Kwanza akaanza kulia,…mmh, nikajiuliza kwanini tena, baada ya kuongea anaanza kulia, na nikaona nimuache kwanza alie..huenda itasaidia kumuondoa hicho kilichopo moyoni mwake, baadae akatulia, na kusema;



    ‘Jana alinitokea mama yangu, akaniuliza kwanini sijafanya alichotaka nikifanye…’akaanza kusema hivyo.



    ‘Oh, alikutokea mama yako mzazi, kwa vipi..?’



    ‘Mimi ni yatima, sina baba wala mama, baba yangu alifariki zamani kidogo, na baadae akaja kufariki mama, na tangia nianze matatizo mama amekuwa akinitokea, akitaka nilipize kisasi kwa haya yaliyotokea kwangu na kwake, lakini mimi mtu kama mimi nitafanya nini…’akasema.



    ‘Kwa vipi mama yako akutokee wakati alishafariki, … hizo si ndoto tu, ..’nikasema.



    ‘Ni ndoto tu eeh!.. hahaha,..wewe unasema tu kwa vile haijawahi kukutokea,…na kuna mambo aliwahi kunitokea akaniagiza, nikayafanya, na ikafanikiwa, nilitaka ku…..itoa hii mimba, akanizuia, kwa namna ya ajabu kabisa, siwezi hata kuamini..’akasema.



    ‘Unazidi kunipa hamasa ya kukisikia hiki kisa, …hebu tuanzie awali kabisa, ilivyoanzia, tuanzie, eeh, huko kwa wazazi wako ilikuwaje.



    ‘Nitaanzia, pale nilipoagana na mama yangu,..huko kijijini, siku ambayo alikuja, mama mmoja, yeye, ni mwenyeji huko kijijini kwetu…ila wao  mungu amewajalia kuwa na uwezo, wamejaliwa kuwa na maisha mazuri, huko kijijini na huku mjini halikadhalika, ..’akatuliza.



    ‘Basi huyo mama akaja kwa mama yangu kiwa hai, …huko kijijini tunajulikana sisi kama masikini wa mwisho ..hata ndala hatuna, nilikuwa natembea peku peku nikipita kuomba mitaani…, na siku alipofika huyo mama ndio alininunulia ndala,..nashukuru, kwani alininunulia ..sio ndala, kwangu nilikiona kama kiatu cha ufahari.., kwangu mimi nilikiona cha thamani kubwa sana, haijawahi kutokea au kuvaliwa kwenye huu mguu wangu…na alimnunulia mama pia.



    ‘Sasa mama nani hii,… nimekuja kukuomba jambo, najua nyie mpo wawili tu, na huyu binti ndiye anakusaidia sana…lakini hata akikaa hapa pembeni yako, anakusaidia nini, …’akasema akinitupia jicho.



    ‘Ndio hivyo, kuomba omba, mitaani, anachokipata ndio riziki yetu tutafanyaje…’akasema.



    ‘Na hivi kile kishamba chenu vipi..?’ akauliza huyo mama.



    ‘Watu wanakitaka, …lakini tukikiuaza si ndio basi tena,baba yake huyu binti yangu, alisema tusikiuze, kije kumsaidia huyu binti yetu,..lakini inafikia mahali hatuwezi,..hapa naumwa, sina pesa ya dawa, ni huyu binti apite pite mitaani akiomba ndio ..nipate dawa..’akasema kwa unyonge.



    ‘Sasa  sikiliza, je huyu binti akiondoka,…nataka akawe mfanyakazi wangu wa ndani, na atakuwa akikutumia pesa za matumizi , unaonaje..?’ akauliza.



    ‘Oh, jamani…mimi nitaishije,..lakini kama atanitumia pesa za matumizi,..si bora , kuliko kuomba omba hivi, sipendi kuomba, inaniumiza sana, lakini nitafanyeje… basi ni heri…..’akasema akiniangalia mimi, sikuamini kama mama angelikubali hivyo, walishafika watu wengi akawakatalia, sijui huyu mama alikuwa na bahati gani.



    ‘Mimi nitakusaidia dawa, na nitakuachia pesa za matumizi, kwa siku kadhaa.. na vyakula nimekuja navyo, nitakuachia, unga, maharage, ..na mchele kidogo, vya kukusaidia siku kadhaa,..angalau uweze kupata chochote wakati, huyu binti akiondoka, na kila mwisho wa mwezi huyo binti yako atakuwa akikutumia chochote alichokipata, unaonaje..?’ akauliza.



    Mama yangu alipoambiwa hivyo, akampigia magoti, huyo mwanamke, kwa kumshukuru, na kweli akapewa vyakula, na pesa, na usoni mama alionyesha ile furaha yake, ambayo sijawahi kuiona, japokuwa hiyo furaha yake,  ilikatika pale aliponiona sasa naondoka machoni kwake, aliniangalia kwa macho ya huzuni,..macho ambayo nayakumbuka hadi leo,…macho ya kuniaga macho ambayo, yananijia kila mama akinitokea,…’akasema.



    ‘Yaani mama, sitakuona tena, zaidi ya kunijia kama ndoto…mpaka leo nakuambia siamini..nahisi kama mama yangu yupo huko kijijini ananisubiria…’akasema.



    Hapo huyo mwanadada akawa analia, na mtoto wake , ni mdogo tu wa kukaa, hajaanza kutembea akawa anamfuta machozi, kile kitendo cha mtoto mdogo kama yule kumuonea mama yake huruma na kumfuta machozi, kilifanya hata mimi machozi yanilenge lenge., dunia hii jamani, kwanini…we yaache tu.



    ‘Sikujua kuwa siku ile mama ananiaga, na machozi yanamtoka, akiniambia binti yangu nenda, maana huenda ndivyo mungu alivyotupangia, nenda ukijua kuwa mimi mama yako nipoje, hapa nilipo ni masikini wa kutupwa…wa mfano,  na sina thamani yoyote  hapa kijijini, ..na kila mtu akitaja umasikini ananifananisha na mimi.



    ‘Binti yangu, huko unapokwenda ni mji wa watu una mitihani mingi …,..sijui hawa watu wapoje, mimi nimeona uende nao tu,  lakini moyo wangu unasita, nahisi,unakwenda kwenye mitihani ya maisha, kwa umri uliofikia, wanadamu wasio wema, wanaweza kukutia kwenye majaribu, ,,ila wewe nenda tu, muhimu mungu wako muweke mbele.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Sisi hatukuomba tuwe masikini,..likumbuke hilo, …ila umasikini upo, na sisi ndio zawadi yetu, usije ukaenda huko ukinilaumu mimi, kuwa mama, wazazi wangu ni uzembe wao….mimi nina imani kuwa umasikini wetu, sehemu yetu ya maisha, na mungu ndiye aliyotupangia…..



    ‘Kila siku nalia…kwanini sisi…maisha yetu ndio hivyo, tokea baba yako, atutoke, kila kitu kimeondoka, na maisha yetu yamekuwa,..ya jana ni bora kuliko ya leo..leo hii kwa mara ya kwanza tutaweza kula chakula cha kujipikia wenyewe…nataka nikupikie na mimi, ule chakula alichokupikia mama yako…’akasema.



    ‘Hapana hatuwezi kusubiria, yeye atakula huko mbele…’akasema huyo mwanamke.



    ‘Mwanangu usije kunisahau,..na safari ni hatua, sijui itakuwaje huko mbele, sijui itakuwaje ukiondoka nikabakia peke yangu, sijui…maana hata hicho kidogo tulichopata, kuna wengine wanakitamani, unakumbuka jana walituibia ile ndoo tuliyopewa, yaani hata sisi masikini wanatuibia,..’akasema .



    ‘Basi mama inatosha mimi sitakusahau mama yangu, nakupenda sana mama yangu..’nikasema na yule mwanamke alikuwa akinisubiri…niende yeye sasa alishatangulia kwenye gari lake.



    Mama, akanishika mkono, akaniangalia machoni, akasema;



    ‘Kwaheri mwanangu,..nahisi kama sitakuona tena…’



    ‘Kwanini unasema hivyo mama…’nikasema sasa nikiingiwa na wasiwasi.



    ‘Kwaheri mwanangu…’akasema na kuondoka kuingia kwenye kibanda chetu, ambacho kilikuwa mbavu za mbwa.

    .

    Basi nikaingia kwenye gari la huyo mama, kwa mara ya kwanza kuingia kwenye gari, nikawa nahangaika kumuangalia mama, lakini mama hakutoka nje, na ikawa mwisho wa kuonana na mama yangu.



    Kisa kipya kipya, je nikiendeleze.





    WAZO LA LEO: Masikini wapo, kama walivyo matajiri, haya yote sio kwa ujanja wetu, walijaliwa wengi wanaona labda kuwa hivyo ni kwa ujanja wao, wangapi wangapi wanajitahidi hawafanikiwi, au waliojaliwa wanakuja kukosa kabisa.., mola peke yake ndiye anayejua ni kwanini akaweka hizi hali mbili. Ilivyo, kama alivyotuagiza mwenyezimungu matajiri wanatakiwa wawasaidie masikini, na wawasaidia bila kuwanyanyapaa, wawasaidie wakijua ni wajibu wao, na masikini wasiwaonee wivu matajiri, kwani riziki zetu zimepangwa hivyo, muhimu ni kujitahidi, tusijipweteke, kwani vyote hivyo vinapatikana kwa jitihada,..na kumtegemea mungu!



    Kiukweli njiani kilichonifanya nimsahau mama yangu kwa muda ni kule kuona vitu vya kunishangaza, nilizoea maisha ya kijijini, ngedere, tumbili, ngombe na watu, sikuzoea kukutana na magari,  na nyumba za kisasa, ilikuwa mimi na watu, kunyanyapaliwa ndio ilikuwa maisha yangu mimi na mama yangu,…sasa naelekea mjini, kwangu mimi kila kitu nilichokiona ilikuwa ni kushangaa tu, mpaka nafika mjini,….sasa nikaingia kwenye jumba. Kwangu ilikuwa ni jumba.



    ‘Nililiona kama jumba ya mfalme, mnaingia kwenye geti mnakutana na walinzi, walinzi wanamnyenyekea bosi wao, na mimi nakajihisi ni miongoni mwa ..hahaha familia hiyo, lakini kwa mbali nikamuona yule mlinzi akiniangalia kwa jicho la dharau.



    ‘Hapa ni kama ulaya…’nikajikuta nakijisemea hivyo…huku nikizungusha macho huku na kule kuona mandhari ya nyumba.



    Hayo ya kushangaa yalikuwa ni mengi sana.., na siku baada ya siku nikaanza kuzoea, kwani pia pamoja na ushamba wangu, nilikuwa mwepesi sana wa kujifunza na kuelewa mambo, na nilijitahidi sana kutekeleza kila nilichoelekezwa, na kwa tabia hiyo, wenyeji wangu wakanipenda sana.



    Pale nyumba walikuwa wakiishi baba na mama, na alikuwepo kijana wao wakiume, kuachilia mbali wafanyakazi,..nilikuja kufahamu kuwa familia hiyo ilikuwa na watoto wengine lakini wao walikuwa nje ya nchi, wakisoma, kwahiyo muda mwingi nilikuwa na huyo kijana wa umri wangu…, lakini yeye alikuwa ni mwanaume.



    Alianza kunizoe kwa vile muda mwingi alikuwepo hapo nyumbani, na yeye ndiye alikuwa karibu kwa kunielekeza na kunifundisha kile nisichokijua, kwahiyo akawa ni mtu wangu wa karibu, japokuwa nilikumbuka usia wa mama.



    ‘Usipende kuwa karibu na wanaume, hawa watu wakiingiwa na hamasa, wakatawalia na matamanio yao ya nafsi huwa hawajali huyu ni nani, jichunge sana binti yangu…,na kaa mbali na  na wanaume…’mama aliniambia hivyo. Kwahiyo japokuwa kijana huyu alikuwa akinisaidia bado nilikuwa najaribu kuwa mbali na yeye kwa kadri nilivyoweza, mpaka yeye akaligundua hilo.



    ‘Mbona nakuona kama unaniogopa…?’ akaniuliza.



    ‘Ni kawaida ..sio kwamba nakuogopa natimiza wajibu wangu kama mwanamke..’nikamwambia hivyo.



    ‘Usiwe mshamba wewe…huoni nakusaidia ili ujue mambo mengi, ..ukiniogopa mimi, hutajua mambo mengi ambayo hujawahi kuyaona, au kuyasikia…’akaniambia.



    ‘Oh,…muda ukifika nitayaona na kujifunza kama ni ya lazima kujifunza…’nikasema na kuondoka.



    Lakini sikuwa na raha, maana nilianza kufululiza ndoto mbaya mbaya, na nyingi zilimlenga mama yangu,...ikawa hainipi raha, nikamuomba mama mwenye nyumba ajaribu kutafuta mawasiliano ya huko, yeye akasema;



    'Usiwe na wasiwasi, tulimuachia chakula cha kutosha, yeye peke yake kinaweza hata kumaliza mwezi...'akasema



    'Lakini alikuwa anaumwa...'nikasema



    'Kwahiyo unataka kwenda kumtibia...?' akaniuliza



    'Aaah, nataka kujua hali yake tu....'akasema



    'Nitatafuta mawasiliano ya huko,..nitakuambia...'akasema



    Hakuniambia kitu wiki, mwezi..nikamuulizia tena, na sasa akawa mkali, hataki kulizungumzia hilo, mpaka nikawa na mashaka, kuna nini, kwanini nikimuulizia maswala ya mama yangu yeye anakuwa mkali sana,..



     Siku zikawa zinakwenda, na kwa vile mimi nilitokea sehemu ya umasikini, na sasa nimeingia seheme ya matajiri, mwili wangu ulianza kubadilika, kunawiri, na ule uzuri wa usiichana wangu ukaanza kuonekana, na hata wenyeji wangu wakaanza kunitania;



    ‘Kumbe maskini na yeye mnzuri….’ Alisema baba mwenye nyumba na mama mwenye nyumba akacheka...lakini akaniangalia kwa jicho lenye ujumbe fulani, kwani baba alipoondoka, aliniita pembeni akasema;



    'Unasikia,...usijione umependeza ukakiuka mikataba yetu, hapa umekuja kufanya kazi, jichunge sana, wanaume watakuhadaa, ukiharibikiwa ujue ndio tiketi yako ya kurudi huko kwenu na sijui utakwenda kuishi nani huko...'



    'Nitakwenda kuishi na nani....'nilijiuliza hivyo, sikumuelewa huyo mama ana maana gani, kauli hiyo ilinizidisha mawazo, lakini sikuwa na la kufanya, aliyekuwa karibu wa kumuuliza ni kijana wao, na nilipomuuliza akasema;



    'Mimi sijui,...mama ndiye anawasiliana na watu wa huko, ningelijua namba za huko tungeliwapigia,...ngoja nitamuomba mama namba za huko utaongea nao...'akasema



    Siki ya pili yake nikamuuliza kama kaipta hiyo namba, akasema



    'Mama kasema haipatikani, ...tuachane na hilo swala...'akasema



    'Mimi nahisi kuna jambo wananificha...'nikasema



    'Hakuna, kwani wewe una wasiwasi gani, hapa unaishi vyema, unakula unashiba, una wasiwasi gani...'akasema



    'Mama yangu nampenda sana,..yeye ndiye tegemeo langu, sitaki nimkose,..kaniagiza nifanye kazi nimsaidia, tupate dawa, sasa ...siwezi nikawa na raha, kama sijui anaendeleaje..'nikasema



    'Sasa amua moja, urudi huko kwenu au uendelee kufanya kazi.....'akasema



    'Sawa ..nitafanyaje , mimi binti masikini nina nini tena,..ndivyo tulivyojaliwa tuwe hivyo, lakini naumia sana...'nikasema.



    Huko kijijini walizoea kuniita jina hilo ‘masikini,..’ kwahiyo likawa limezoeleka, hivyo sikukasirika, nilijionea sawa tu, maana ni kweli hali yetu ilikuwa hivyo!



    **************

    'Masikini mbona upo hivyo...'nilishtuka sauti ya kiume, alikuwa ni baba mwenye nyumba.



    'Hapana baba , hakuna kitu...'nikasema na kwa haraka nikakurupuka kwenda kuendelea na shughuli zangu.



    Baba mwenye nyumba alikuwa mara nyingi hashindi hapo nyumbani anarudi usiku labda siku za wikiendi ndio tunakuwa naye, na sikuzoeana naye sana, na hakuwa muongeaji, zaidi ya kunituma kile cha ulazima, kama mkewe hayupo vinginevyo, hakuzoea kunituma zaidi ya kupitia kwa mkewe au kijana wake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Muda ukapita nikaanza kuona mabadiliko fulani…., hasa kwa huyu kijana,…kwasababu nilikuwa naye muda wote, hata kwa baba mwenye nyumba, lakini kwa vile alikuwa anaonekana mara moja au mbili kwa wiki, sikuweza kumjali sana, tatizo ilikuwa kwa huyu kijana.



    Huyu kijana … nikaona ananiangalia kwa jicho lisilo kuwa la kawaida, na kuna muda nilimfuma akinichungulia, nikiwa labda chumbani kwangu, au hata nikioga, ananichungulia kwenye tundu za milango.



    ‘Wewe vipi mbona umekuwa hivi siku hizi,,,,?’ nikamuuliza.



    ‘Hahaha, wewe hujioni, umekuwa mnzuri, nashindwa kuvumilia….’akaniambia.



    ‘Acha ujinga huo, wewe ni ndugu yangu…hujasikia mama akituambia, sisi ni ndugu, tuheshimiane kama ndugu….’nikasema.



    ‘Hahaha mimi ndugu yako mimi, acha ushamba huo…hayo ni mambo ya kizamani, mama hawezi kusema tusipendane, mimi na wewe tunaweza kuwa wapenzi bila ya mama kujua, unajua mimi nakupenda sana…’akasema



    'Eti nini..unanipenda umejifunzia wapi hayo mambo ya kikubwa, ...'nikasema



    'Hahaha, eti ya kikubwa, kwani wakubwa walianzia wapi...'akasema



    'Sikiliza mimi siyataki hayo maneno yako, siyapendi, kama unataka tukosane endelea na hayo mambo yako...'nikasema.



    'Utajifunza tu, usijali...'akasema , uzuri wake, huyu kijana alikuwa hakasiriki, anaweza ukakuuzii , ukamsema vibaya, yeye anatabasamu tu,...lakini kwa mabadiliko hayo, nikaanza kumuogopa zaidi, nikikumbuka usia wa mama.



     Huyu kijana hakuacha kunisumbua, kuna wakati mwingine antaka nione anavyoangalia kwenye simu yake au laptop yake, nikiangalia na kuta kaweka mapicha mabaya, basi, mimi huondoka hapo yeye anaishi kunicheka na kuniita mimi ni mshamba,…na ikafikia muda akawa sasa hafichi dhamira yake, alisema ananitaka, na atajitahidi mpaka anipate.



    ‘Unanitaka nini,...nimeshakuambia, mimi itaki upuuzi, huo na ukiendelea hivyo sasa nitamuambia mama yako…’nikasema.



    ‘Ukimuambia mama yangu, nimjuavyo, basi ujiandae kurudi kwenu, mimi na wazazi wangu tunapendana sana, na lolote nikisema wataniamini, je wewe watakuamini zaidi yangu….’akasema.



    ‘Hata kama …ila mimi nimeshakuambua mimi sitaki huo ujinga wako…’nikasema.



    ‘Utautaka tu, upende usipende…’akasema na sikumuelewa ana maana gani.



    'Unataka kunifanya nini..?' nikamuuliza na yeye akacheka tu, na kusema;



    'Wewe mshamba,..mimi mtoto wa mjini, najua jinsi gani ya kukupata...'akasema.



    Basi nikaogopa, sikutaka kumtishia hivyo tena, ila nikajitahidi kuwa mbali na huyo kijana lakini huyo kijana hakuwa na raha bila ya kuja karibu yangu maana alishazoea kuwa name karibu kama mwalimu wangu.



    ************



    Ilikuwa siku ya wikiendi, nilibakia na baba mwenye nyumba, nikafanya usafi sehemu zote, lakini sikuweza kufanya usafi ndani kwa wenye nyumba, kwa vile baba mwenye nyumba yupo, na akiwepo mama huwa anafanya usafi peke yake huko chumbani kwao..., lakini leo mama alikuwa hayupo, …na kijana alikuwa katoka.



    Nikawa nimemaliza kazi ya usafi, na sasa nataka kwenda kuosha vyombo, mara nikasikia baba mwenye nyumba akiniita,…cha ajabu alikuwa akiniitia chumbani, nikashangaa sio kawaida yake.



    'Binti masikini....'akaniita, nikaitika...



    ‘Mbona huku chumbani hujafika kufanya usafi…’akasema.



    'Mama hayupo...'nikasema



    'Ina maana mpaka mama awepo ndio unaingia kufanya usafi huku ndani...'akasema



    'Nilikuwa nasubiria utoke...nisikusumbue umelalala...'nikasema.



    'Wewe ingia ufanye usafi...' akasema.



     Nikawa najiuliza nitaingiaje kufanya usafi huko ndani, na wakati baba mwenye nyumba yupo, na aliposisitiza hivyo, na kwa vile nilimuona yeye kama baba yangu, nikatii amri,  nikaingia ndani, ….



    Mungu wangu nilimkuta kavaa taulo tu kifua nje..na kakaa kitandani, sijawahi kumuona mwanaume katika hiyo hali, niliona kama nimemuona akiwa uchi...,..nikataka kutoka nje nihisi nimeingia kabla hajavaa shati, labda...akasema.



    ‘Fanya usafi, usijali, …kipi kigeni kwako hapa….’akasema yeye akiwa anaangalia lapotop yake aliyokuwa kaiweka, mapajani.



    Nikaanza kufanya kazi kwa haraka haraka sio kama ile inavyotakiwa ilimradi nitoke humo ndani, sijui ilikuwaje, nilikuwa nimeinama nakusanya uchafu, mara nikahisi mtu ananikamata, kwa nyuma, yaani ilitokea haraka.



    Nilipiga ukelele, unajua kupiga ukelele,..nahisi ulikwenda mbali sana, na huo ukelele ukamfanya jamaa aniachie kwa haraka,...na alipjaribu kunishia tena, kwa kuniziba mdomo...nikapiga tena ukelele na kwa haraka nikamtoka na kuanza kukimbilia nje....mbio,…mbio…



    Wakati natoka mbio…, nakutana na yule kijana akiwa katokea dukani, akaniangalia kwa macho ya kujiuliza, maana nilikuwa nahema, ninatetemeka kwa uwoga.



    ‘Vipi wewe umeanza mashetani yako…’akasema.



    ‘Baba..baba…’nikawa nasema hivyo tu..na yeye, kwa haraka akakimbilia ndani akijua labda kuna kitu kibaya kimetokea kwa baba yake, baadae akarudi na kusema;



    ‘Mbona baba kalala kitandani..tena fofo, yaonekana alikuwa kalala muda mrefu, mimi nahisi ni hayo majinamizi yako unayoota kila siku..?’ akasema, lakini sikusema kitu tena zaidi ya hapo, ila nina imani, mtu alinishika kwa nyuma, tena akiwa uchi…sizani kama nilichanganyikiwa,..labda, lakini..hapana…alinishika, mimi sijachanganyikiwa.



    ‘Hapana…sijaota ni kweli…’nikasema.



    'Ni kweli kwa vipi, kwani ilikuwaje,...?' akaniuliza, lakini sikumuambia kitu, nikabakia kimia tu.



    ‘Unajua wewe una tabia ya kuota na kupiga makelele, hasa usiku na hata mchana ukilala unakuwaga hivyo, sikujua kuwa hata ukiwa macho unapandwa na maruhani yako …’akasema.



    Ni kweli nimekuwa na tabia hiyo, huwa naota sana, na  kuna siku niliota ndoto mabaya sana haijawahi kutokea,……sitaweza kuisahau…



    *************



    Mama alikuwa kanituma dawa, yeye alikuwa kalala ndani, anaumwa hajiwezi, na tuliomba omba tukapata vijisent vya kununulia dawa..., mama akanipa pesa, na mimi nikakimbilia dukani kumnunula hizo dawa,..



    'Usichelewe mwanangu maana ukichelewa hutanikuta...'akasema hivyo.



    'Mama sichelewi, kwanini nisikukute utakwenda wapi, wakati unaumwa....'nikasema



    'Haya,..hujui mungu kapanga nini, nenda haraka, ....'akasema na mimi nikatoka kwa haraka nikakimbilia duka la dawa, lilikuwa mbali  kidogo, nikanunua, na  wakati narudi, nakaribia nyumbani, niona mosho umetanda juu, kama kuna kitu kinaungua, na hapo nikasema;



    'Mungu wangu huo moto sio nyumba imeungua, isije ikatokea kwetu..'nikasema na kuongeza mwendao, na nilipokaribia nyumbani kwetu, ndio naona moto, unatokea kwenye nyumba yetu,..moto umewaka, nakwa muda huo unatokea  dirishani na mlangoni..unaanza kushika na paa...



    'Mungu wangu ni mkosi gani huu...'nikasema nikikimbilia kutaka kujaribu kuzima, ..kitu ambacho hakiwezekani, moto ulishashika hatamu..



     Nikaanza kupiga kelele,..



    'Mama, mamaaa, toka nje nyumba inaungua..'



     Lakini mama hakutoka, moto ulikuwa mkali kweli kweli…, na pale mlangoni ukawa ni makali kupitliza, mtu huwezi kupita, kuingia ndani….na sikuwa na njia ya kuingia ndani , ili niweze kumsaidia mama, na mama hali yake sio nzuri.



     Nikawapigia majirani makelele ya kuomba msaada, … ili waje kusaidia kuzima moto lakini hakuna hata mmoja aliyejitokeza , ni kama vile tulikuwa tunaishie peke yetu.



    'Oh, mama yangu jamani,…’nikawa nalia, na sasa nikawa najaribu njia yoyote ili niweze kuuzima ule moto, nikaokota ndoo mbovu mbovu,  nikajaribu kutafuta maji, lakini hakukuwa na maji yoyote karibuni, maeneo ya kwetu maji ni shida, tunayafuatilia mbali sana, ..sikuweza kupata maji hata yale machafu, ...



     Moto sasa ulikuwa umezingira nyumba nzima, hakuna anayeweza kufanya lolote…na kwa maana hiyo mama atakuwa kaungua, na sizani kama angeliweza kupona kwa jinis moto ulivyo mkali.



      Kwa bahatio upande mmoja wa nyuma, nikaona sehemu hakujashika moto, naweza kupenya, nikajaribu kupaendea, japokuwa ni joto kweli, nilipokaribia tu, nikahisi mtu ananishika kwa nyuma,..kama kunizuia nisiende,…



    'Niache niache nikamuokoe mama yangu...'nikasema lakini huyo mtu akawa haniachii.



     Nikawa nasumbuana naye, aniachie lakini hakuniachia, na alivyonishika, ni kama ananikaba, nikawa najiuliza iweje badala ya kunisaidia, kuuzima moto yeye  ananikaba, anataka nini huyu anataka mama yangu ateketekee na moto…



     Sasa ikawa napambana na huyu mtu, huku moto unazidi kuwaka, nyumba sasa inazidi kuteketea!



    'Mama yangu jamani…’nikasema na huyu mtu akawa anaendelea kunikaba, na ..hata sijui alikuwa akinifanya nini…ila nilichohisi ni maumivu makali chini ya kitomvu,makali kama mtu aliyechomwa na kisu, hapo nguvu zikaniishia, sikuweza kupambana tena na huyo mtu, nikahisi kupoteza fahamu.



    Mara…...



    'Wewe vipi, mbona leo umelala kama gogo..’ ilikuwa sauti ya mama mwenye nyumba na mimi nikakurupuka kwa haraka kutoka kitandani, lakini mwili haukuwa na nguvu..



    ‘Nahisi vibaya mama,…’nikasema.



    ‘Wewe siku hizi umeanza uvivu, kila siku ukiamuka asubuhi hujisiki vizuri, una nini wewe..?’akaniuliza akiniangalia kwa mashaka.



    ‘Hata sijui mama, nimeota ndoto mbaya..mama yangu sijui …’nikasema na huyo mama akatulia kidogo halafu akasema;



    ‘Mama yako,…anakutegemea wewe ufanye kazi upate pesa umtumie, lakini kwa mtindo huu, sijui kamaa utaweza kufanya hivyo…’akasema.



    ‘Kwanini mama, najitahid, ila usiku inakuwa nishida kwangu,..naota ndoto mbaya,…sijui …nahisi mama hayupo sawa…’nikasema.



    ‘Kama hayupo sawa utafanya nini…bila ya kuwa na pesa, au unataka nikurudishe huko kwenu kijijini…’akasema.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ‘Mama hapana…ila nataka kujua hali zao tu, sijawahi kuongea na mama yangu, tangia nije huku sasa sijui …oh, mama yangu jamani, sijui yupoje…’nikasema nikihis kulia.



    ‘Hebu amka kule, ukafanye usafi…’akasema huyo mama, na mimi nikajikakamua kuamuka, lakini mwili wote haukuwa na nguvu, nikawa nahisi joto la homa,…na nikahisi maumivu makali tumboni  mara...nasikia kama kutapika,…



    'Nini hii tena jamani…’nikasema na kuhisi kichwa kikiniuma kweli kweli…tumbo, kichwa, na maumivu makali sehemu za siri…na hapo hapo, nikajiwa na kizunguzungu, na kupoteza fahamu.

     nilipozindukana nikajikuta nipo hosp nimelazwa….



    Nililazwa wiki, nikatoka, sasa leo nakutana na tukio jingine la aina yake, na baba mwenye nyumba !



    *********



    ‘Unajua wewe una tabia ya kuota na kupiga makelele, …’akasema yule kijana na mimi nikasema



    ‘Na nikiota kawaida ndoto zangu huwa kweli,….nahisi mama yangu hayupo sawa



    ‘Kwani hawajakuambia…’akasema huyo kijana



    ‘Kuniambia nini…?’ nikamuuliza na mara baba akatokea akiwa kavalia, …hakusema neno, akaelekea kwenye gari lake, na kijana akasema;



    ‘Kama unaumwa mwambie baba akupeleke hospitali



    ‘Niambia kwanza umesema kwani hawajaniambia , hawajaniambia nini..?’ nikauliza na baba akasikia, na kusema



    ‘Wewe nanihii..njoo…’akamuita kijana wake, wakawa wanateta, na baadae akarudi na kusema



    ‘Baba kanipa pesa nikakununulie dawa….’akasema



    ‘Dawa gani kwani anjua nina umwa nini…?’ akauliza.



    ‘Za maumivu…kasema unakuwa kama umechanganyikiwa,..unapiaga piga kelele ovyo...kasema akija atakupeleka hospitalini, anahisi una malaria, kama yale uliyopimwa kipindi kila ikaonekana malaria yako imepanda kichwani…’akasema.



    ‘Lakini , …..nina uhakika alitaka kunishika…’nikasema na mara mama akatokea



    ‘Ndio alitaka kukushika alipokuona ukipiga ukelele...alijua utaanza kukimbia ovyo,..usijali baba ni mtu mwema sana, atakusaidia sana, nilisikia akisema atakupeleka VETA kusomea ufundi,...ila usije kumuuzi baba.., ukimuizi baba,..ana hasira kali sana, na hawezi kusamehe, utarudi kijijini tu upende usipende..yaani mimi nasema ni bora ukosane na mama, kuliko kukosana na baba, mwenyewe si unamuona hana muda wa kuongea mara mbili…’akasema.



    'Lakini nina uhakika, alitaka kunishika  kwa-kwa nguvu..kwa nia mba-a.....'nikasema na nikakatisha maneno, kwani mama alishafika, na akasikia nikisema hivyo, na hapo hapo mama akauliza



    'Ni nani alitaka kukushika.....?' akauliza mama.



    NB: Mambo yalianza hivyo..





    WAZO LA LEO: Tuweni makini sana na wafanyakazi wa ndani, kuna visa vingi vinatokea, vingine ni wao wanakuja na tabia ambazo, zinakuja kuwaathiri watoto wetu,…kabla ya kumuachia mwanao jitahidi kuwa naye karibu, mchunguze kwa makini. Lakini pia kuna visa vingine vya wenye nyumba kuwazalilisha hawa wafanyakazi wa ndani,…haya ni madhaifu yapo na yanatokea, ewe baba, ewe mama, huyu ni mwanao kama watoto wako ana wazazi kama ulivyo wewe kwa watoto wako, mthamini kama mwanao…kwani ukimtendea mabaya, na wewe watoto wako watakuja kutendew hivyo hivyo, dhambi hizi hulipiziwa hapa hapa duniani.



    'Baba kanipa pesa nikakununulie dawa....'akasema na mimi kwa haraka nikauliza.



    ‘Dawa gani kwani mimi naumwa nini…?’ nikamuuliza yule kijana mwenzangu.



    ‘Kaniambie dawa za maumivu…kasema leo wakati unafagia ulikuwa kama umechanganyikiwa, ulikuwa unapiga makelele ovyo,…sasa kama hali hiyo itaendelea atarudi kazini aje akupeleka hospitalini, anahisi una malaria, kama yale uliyopimwa wakati ule wakasema malaria yako imependa kichwani…’akasema.



    ‘Lakini , mimi siumwi, najisikia vibaya tu, kwasababu usiku silali, napata shida sana…’nikasema.



    ‘Ndio…nakuonaga ukihangaika,…unapiga kelele sana usiku, kwani ukilala, huwezi kuamuka, ukaona kuna kitu gani karibu yako …’akasema.



    ‘Kuamuka kwa vipi wakati hayo yanatendelea nikiwa usingizini,..yaani ni kama mtu anakuja ananikaba, ananiifanyia mambo mabaya..yaani nashindwa hata kuelewa…’nikasema.



    'Anakufanyia mambo mabaya, mambo gani hayo...?' akaniuliza



    'Hata siwezi kusema,..mungu mwenyewe anajua...'nikasema.



    ‘Mhh…pole sana, baba kaondoka akiwa na wasiwasi sana….’akasema.



    ‘Lakini mimi  …..nina uhakika alitaka kunishika…’nikasema na ndio hapo mama akatokea



    'Kukushika, kwa vipi, ..si ndio hivyo alitaka kukushika usikimbie, wewe hujijui tu, ukiachiwa hapo ukiwa kwenye hiyo hali unaweza kukimbia, ukapotea....



    'Hapana sio hivyo....hisia zangu zinatuma vingine kabisa...'nikasema



    'Unataka kusema nini, ...kuwa baba,...'akakatisha



    'Wewe hujui tu,..tuyaache hayo, ila ..kiukweli, sijaota, sijachanganyikiwa, alitaka kunishika kwa..nguvu..au sijui alitaka nini, ila alikuja nyuma yangu wakati nimeinama, akataka kunishika...kwa..kwa nguvu....'nikasema na niliona kijana akitoa macho akiangalia mbele .



    Kumbe alimuona mama akiingia,..



    Tuendelee na kisa chetu..



    *************



    ‘Nani alitaka kukushika…kwa nguvu,..’mama akasema kwa ukali, mimi nikakaa kimia, sikutaka kusema lolote kuhusu hayo yaliyotokea, huko chumbani kati yangu na baba mwenye nyumba,  kwanza kama kweli alikuwa na nia mbaya, hakufanikiwa, na pili nikisema ninaweza kuleta kutokuelewana kwa wanandoa hao na ikawa mimi ndiye sababu, na hapo inaweza kuwa ndio mwisho wa kazi hapo nyumbani.



    'Jitahidi binti yangu, ujue dunia hii ina mitihani mingi, ukipatwa na shida, usikate tamaa, pambana na mikakati yako mpaka ufanikiwe...'nikakumbuka maneno ya mama.



    Huyo kijana yeye akatangulia kujibu kwa haraka haraka, kwa kusema;



    ‘Mama, naona huyu mdada apalekwe hospitalini, usiku anapiga kelele sana, humsikiagi mama, yaani mimi nakosa usingizi, … sijui anaota nini, na leo kapiga kelele kamsumbua sana baba, baba akahangaika kumshika, maana alionekana kama anataka kukimbia…’akasema



    ‘Oh,…sasa ni hayo malaria yamerudi tena..au kuna tatizo gani, najua pia inachanganyikana na mawazo uliyo nayo,…sasa nikuulize wewe kama unataka kwenda kumuona mama yake, oh...mama yako huwezi kumuona,…’akasema na ghafla akakatisha ni kama lijigundua kuwa kasema neno ambalo hakutakiwa kulisema.



    ‘Kwanini siwezi kumuona mama yangu…?’ nikauliza nikionyesha mashaka usoni, nikimuangalia moja kwa moja usoni, na yeye akaangalia pembeni na kusema;



    ‘Kwasababu hali ya huko ni mbaya…kuna njaa sana huko kijijini, watu wanaishia kula mizizi, sasa hebu fikiria kwa ujumla kupo hivyo, je mama yako na ile hali atakuwaje…yeye pale alipo, anahitajia misaada kutoka kwa wasamaria wema,…na …mimi sasa hivi nimetoka kupeleka misaada ya chakula , nimeagiza kwenye mabasi, lakini kikifika huko ni cha kugombea maana wengi wana hali mbaya..unanielewa..’akasema.



    ‘Oh, kumbe, ulimpelekea mama yangu chakula…oh ahsante sana mungu, ahsante sana mama, umemfaa sana mama yangu, mungu atakulipa zaidi….kwahiyo ulipata nafasi ya kuongea na mama?’ nikamuuliza, sas anikionyesha furaha.



    ‘Nilishakuambia mimi namjali sana mama yako, muhimu utulie, ufanye kazi, kilichokuleta hapa ni kazi, na kazi ndio itamfanya mama yako …awe….asiwe na shida,… na mwisho wa mwezi huu nitamtumia pesa, nitakata kiasi kwenye mshahara wako, na mimi nitaongezea za kwangu kidogo, sawa…’akasema.



    ‘Sawa mama za kwangu mtumie zote tu….’nikasema



    ‘Usijali, naona sasa umepona…’akasema, akimuangalia kijana wake, na kijana wake naye akawa anatabasamu aliponiona nipo na furaha.



    Kijana wake alionekana mwenye huruma sana, na unaweza kusema labda ndio huko kunipenda, japokuwa mimi sikuwa na uelewa huo, ….hata hivyo mimi sikumuamini, yeye na baba yake niliwaona kama wana tabia zinazofanana, hata hivyo sikuwa na mashaka na wao, zaidi ya kujitahidi kuwa mbali na wao.



    ‘Haya kafanye kazi,…au bado unajisikia vibaya,…kama unajisikia vibaya kapumzike  nitamalizia mwenyewe kazi zilizobakia,…usijali kuhusu huko kijijini,  nitajitahidi kadri niwezavyo kuwasaidia…’akasema huyo mama.



    Kauli hiyo ilinifanya niingiwe na faraja kidogo, lakini moyoni nilihisi kama kuna jambo, kuna kitu , sijui kwanini nafsi yangu ilikuwa inanituma  hivyo, kiukweli mimi nilimpenda sana mama yangu, wakati mwingine najuta kwanini niliamua kuja huku, na kuwa mbali na mama yangu, lakininingelifanyaje..niliona kuja huku kutafungua sura mpya ya maisha yetu,..huenda ningelijaliwa niweze hata kumchukua mama yangu…ndio ilikuwa ndoto zangu hizo.



    Siku hiyo ikapita hivyo…japokuwa usiku nilisikia mama na baba wakizozana kuhusu jambo, nahisi walikuwa hawaelewani, nikasikia mama akisema;



    ‘Na siki nikigundua kuwa ni kweli,…itakuwa mwisho wa ndoa yetu,..nakuambia hilo, yule binti wa kwanza ulijitetea, nikakusamehe, lakini huyi, hivi wewe una nini, binti wa watu masikini, hana mbele wala nyuma, ni nini umekikosa kwangu,…’



     Kauli hiyo ilinifanya nijua wananizungumzia, mimi, nikataka kutega sikio, lakini mara akatokea kijana wao, na yeye yaonekana alisikia, huo mzozani, kwani usoni alionekana hana raha..kiukweli, sikupenda kuingilia mambo yao. Na hilililitokea kwa bahati mbaya..



    ‘Kuna nini..?’ nikamuuliza



    ‘Hayakuhusu, hayo ni mambo ya wakubwa,…’akasema akinipita kuelekea nje.



    Niliamua kumfuata huko nje…, kwani nilikuwa na maswali mengi ya kumuuliza, kuna mambo mengi yalikuwa yakiendelea kichwani mwangu.



    ‘Eti samahani, nikuulize kitu….’nikasema



    ‘Uniulize nini, kama ni maswala ya baba na mama, usiniulize….’akasema



    ‘Hapana, nauliza hivi, …hapa nyumbani, …kulikuwa na mfanyakazi wa ndani kama mimi….?’ nikamuuliza.



    ‘Kwanini unauliza hivyo, umesikiliza maneno ya wakubwa au..? ni tabia gani hiyo mbaya…’akasema kwa hasira, kwa mara ya kwanza nilimuona akinikunjia uso.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Nauliza tu, maana ndani ninapolala, nimekuta nguo nyingi ndani, niliwahi kumuuliza mama, akasema zilikuwa za mfanyakazi aliyepita…’nikasema.



    ‘Sasa kama unajua hilo, kwanini unaniuliza tena…’akasema akionyesha kukerwa, nikajua ni hayo yanayoendelea kati ya wazazi wake, niliona ajabu sana, watu hawa wana maisha mazuri, kwanini wasiwe na furaha, kwanini inaonekana kama wana msigashano fulani…hiyo sio mara ya kwanza kusikia wakizozana.



    Naona huna raha, unajua wewe ni rafiki yangu, na nikikwazika najua wewe ndiye wa kunisaidia, sasa kama nakuuliza swali unakuwa mkali, basi, ngoja niondoke tu…’nikasema na yeye hapo akabadilika na kusema;



    ‘Haya uliza, unajua kun akitu kinanisumbua, nilitaka kuongea na mama, au baba, sasa naona hawapo vizuri,..aah, tuyaache hayo, ..niuliza, usijali…’akasema.



    ‘Nataka kukuuliza kuhusu huyo mfanyakazi,  aliondokaje hapa…?’



    ‘Aliamua tu mwenyewe, …’akasema sasa akiwa katulia, na mimi nikaona huo ndio wakati wakumdadisi mambo ninayoyaona humo nyumbani, sikupenda kumuuliza lakini kwa jinsi yanavyozidi nikaona kuna umuhimu kuyajua.



    ‘Mhh, hata sielewi…nahisi hakuondoka kwa kupenda, …’nikasema.



    ‘Ni uamuzi wa mtu, hata wewe ukijiskia kuondoka si unaondoka tu, hujalazimishwa, au sio, ..mimi ndivyo nijuavyo hivyo…’akasema.



    ‘Ndani kule chumbani, niliona kijitabu hiki  kidogo,…nahisi kilikuwa cha huyo msichana, na alipenda kuandika andika mambo, kuna sehemu nimesoma mpaka nahisi huenda kuna tatizo kwenye hii nyumba, nahisi …maana hata mimi sijielewi…’nikasema.



    ‘Aliandika nini…?’ akaniuliza akionyesha kushtuka.



    ‘Humu ndani kuna mashetani……’nikasema



    ‘Weee, nani kasema hayo, hakuna mashetani humu ndani…’akasema.



    ‘Ndivyo alivyoandia yeye…’akasema



    ‘Huyo muongo, alimzulia sana baba, na hata mimi, …unaona kumbe aliandika kuwa humu kuna mashetani, ole wake, …baba na mama wangelijua hilo, …’akasema



    ‘Lakini kwanini hata mimi sipati usingizi usiku,..kuna mambo yanitokea, ndio maana nahisi huenda nay eye yalimtokea hivyo hivyo…’nikasema



    ‘Wewe si malaria tu.. .sikiliza hayo aliyoandika ni uwongo, kama yapo mashetani mbona mimi hayajanigusa au wazazi, huoni kuna uwongo hapo…’akasema



    ‘Labda yapo kwa ajili ya wageni tu…’nikasema



    ‘Kwahiyo unaamini hayo maneno?' akaniuliza.



    ‘Sijasema nimeamini…ila nakuuliza maana yeye kaandika kuwa ikifika usiku akiwa amelala huwa anashikwa na majinamizi, yanamkaba, na sio kumkaba tu, yanafikia kumdhalilisha…’akasema na kijana akabakia kimia kama anawaza jambo.



    ‘Mbona hakusema…alikuwa analalamika tu, na kudhalilishwa kwa vipi, ni muongo huyo….’akasema



    ‘Kaandika kuwa aliwahi kumuuliza mama, mama akamfokea, na kumuambia anazusha mambo , na akiendelea na tabia hiyo atafukuzwa kazi,...na siku kadhaa akamuuliza baba, baba akasema hivyo hivyo,..ila baba alisema atafuatilia kuona kama maneno yake ni ya ukweli, mkamuita mtu wa dini, kweli si kweli…?’ akauliza



    ‘Kwanini aliandika hayo, ….hebu nipe hicho kijitabu….’akasema



    ‘Hapana siwezi kukupa hiki kitabu sio chako, nitamtafuta huyo msichana nimpe kijitabu chake..ila kwasasa nataka nikisome chote nikimalize…..’nikasema



    ‘Ole wako baba au mama wakiyasikia hayo maneno..., maana sisi hatuamini hayo mambo ya mashetani….’akasema



    ‘Hamuamini ndio , kwa vile nyie hayawasumbui….mimi usiku nalala kwa shida sana,..kama mama angelikuwepo, najua angelisaidia, lakini hapa nitamuambia nani anielewe….lakini kiukweli humu ndani kuna matatizo…’nikasema.



    ‘Huyo aliyeandika humo ni muongo…nimini mimi, alikuwa na yake , huenda alikuwa na mashetani yake, ndio yakawa yanamsumbua...kwanini huyo mtu wa dini alipokuja kuomba hakukuwa na tatizo lolote...’akasema,



    'Hamna shida, mimi nilikuuliza tu....'nikasema



    'Sasa kama wewe huamini ninayokuambia, basi itabidi yafike kwa baba na mama, na wakigundua kuwa una hicho kitabu kilichoandikwa uwongo, sijui kama watakuelewa, watakuona wewe ni mfitinishaji, watakufukuza..bora unipe hicho kitabu tukiharibu,….’akasema.



    'Hapana hiki kitabu kitarejea kwa mwenyewe..'nikasema



    'Utampata wapi..?' akauliza



    'Atakuja kuchukua vitu vyake...'nikasema



    'Mliongea naye...?' akaniuliza



    'Nilisikia akiongea na mama, kwenye simu, akasema atakuja, ndio mama akaniambia vivipange vitu vyake vizuri, akija asikae humu ndani muda mrefu...'nikasema



    'Sitaki hata kumuona....'akasema



    'Kwanini...?' nikauliza



    'Sio mkweli, muongo, mfitinishaji,..alitaka kuvuruga ndoa ya wazazi wangu...mtu anayewafany wazazi wangu wasiwe na raha, ni adui yangu...'akasema na mimi nikamuoangalia kwa jicho la pembeni, nilitaka kumuambia jambo, lakini nikasikia nikiitwa ndani.





    ********



    Siku moja wakati nafanya usafi chumbani kwa mabosi wangu hawa, baba alikuwa hayupo, kurudi kwake najua ni usiku,.. halikadhalika mama naye alikuwa hayupo yeye, hurudi saa kumi jioni,  na kijana wao, alikuwa kaenda chuo , huwa anasoma chuo cha ufundi, lakini anawahi kurudi, kama kwenye saa nane hivi…,



    Basi mimi nikawa nafagia ndani kwenye chumba cha waheshimiwa hao, nikiwa huru kabisa, nipo peke yangu, nafanya kazi kwa nafasi,..najua nina muda, nikimaliza kufagia napanga panga vitu…baadae naenda kuosha vyombo.



    Kawaida muda kama huo nina uhuru, nipo peke yangu, na wafanyakazi hawawezi kuingi ndani, huwa muda kama huo wafanyakazi, hawaruhusiwi kuingia ndani, mpaka nimalize usafi, kama wana jambo muhimu la kufuatilia ndani, inabidi wasubirie....ni amri waliyopewa na wenye nyumba,  na kwa vile kulikuwa na joto, nikawa nimejifunga khanga moja tu..,



    Mara wakati nainua kitabu, kuvuta mavumbi, kukadondoka karatasi, ilikuwa ni barua,…sina kawaida ya kupekua vitu vya watu…, huwa navipanga kama vilivyo, ila sijui ilikuwaje, wakati nataka kuirudisha hiyo barua, ikadondoka tena chini, na sasa ikafunguka,..Sijawahi kusoma vitu vya watu humo ndani,…mungu mwenyewe anajua ni kwanini, ila ile barua ilipofunguka, nikaona neno kijijini, moyo ukanilipuka, paah,…nikaacha kupanga vitu, na kuanza kuisoma hiyo barua, mungu nisamehe tu, kwa kosa hilo.



    Kumbe barua hiyo ilikuwa inatokea kijijini kwetu, kutoka kwa rafiki na jamaa ambaye ndio mama mwenye nyumba humtumia, kwa mawasiliano na huko kijijini. Mara nyingi wanawasaliana kwa simu, lakini nilishangaa kuwa kumbe wanaandikiana na barua.



    ‘Shoga, nimeona nikuandikie barua, ili iwe kumbukumbu kwak, huku kijijini hali ni mbaya sana, njaa, hali ngumu za kiuchumi, na zaidi, hivi sasa kumezuka tabia ya watu kuiba, na kufanya mauji, sijui dunia hii imekuwaje.



    Hutaamini, kuwa watu hawa hawajali wanyemfanyia hivyo ni nani, najua ni kutokana na hali ngumu za maisha,…kama nilivyokupigia simu, tukio lile la moto, kumbe lilitokana na kile chakula ulichomuachia yule mama masikini..inasikitisha sana.



    Vijana hao majambazi, sijui walijuaje kuwa umemuachia huyo mama chakula, na pesa, walimvamia usiku, na aheri wangeliiba tu hicho chakula, na pesa, kwani  hawakuishia hapo wakachoma na hicho kibanda cha huyo mama, na kuteketeza kila kitu.



    Mama wa watu hakuweza kuokolewa, aliungua vibaya sana, na alipofikishwa hopitalini akafariki dunia,..na kutokana na hali aliyokuwa nayo, hakucheleweshwa kuzikwa, inasikitsha sana…  sasa sijui mtamu….’

    Binti hakuweza kumalizia kusoma hiyo barua akadondoka chini na kupoteza fahamu.



    Siku hiyo baba mwenye nyumba aliwahi kurudi nyumbani, akiwa na furaha zake anapiga mrudi, akapiga hodi, akaona kimia.



    ‘Hawa watu wamehama…’akasema na kwanza akaingia chumba anacholala huyo binti, akijua labda huyo binti kajipumzisha, hakupiga hodi, akafungua mlango, huyo binti alikuwa hayupo chumbani, akaweka zawadi fulani juu ya kitanda cha huyo binti, halafu kwa haraka akaelekea chumbani kwake.



    Alipofika chumbani kwake, akakuta mlango upo wazi, akajua labda ni mkewe naye karudi kwa dharura, hapo akili ikamcheza, kwa haraka akageuka na kurudi kule chumba cha huyo mfanyakazi , nia ni kuichukua ile zawadi, isije ikaleta matatizo, lakini sasa alipofika kule chumbani akakuta ile zawadi haipo.



    ‘Huyu binti kaingia huku saa ngapi….’akasema hakutaka kuita, akijua mkewe atasikia, basi akageuka na kurudi kule chumbani kwake, ili akaongee na mkewe, huenda naye karudi hajisikii vyema.



    Alipofungua mlango, anashangaa, mtu kalala chini, ni yule binti, akiwa ka khanga moja,..na alivyolala,..sehemu kubwa na mapaja yapo wazi…kwanza ibilisi akamteka jamaa, lakini moyoni akahisi huyo binti hayupo sawa….



    Kwanza ikabidi amkague huyo binti kwa kugusa mapigo ya moyo, kama kuna uhai,…na alipoona kuna uhai, akaona ni vyema akaribu huduma ya kwanza, anayoifahamu yeye, …akamgeuka na kumlaza chali, akaweka mikono kifuani, kuminya taratibu, anajua mambo hayo…binti hakuamuka.



    ‘Oh,…sasa hili ni tatizo….’akasema.



    ‘Ngoja nifanye huduma nyingine, akasema, sasa akachuchumaa, nia ni kupanua mdomo wa huyo binti na kufanya huduma ya mdomoni, hapo, sasa….



    Ile anainama, na kushusha mdomo wake kukutanisha na mdomo wa huyo binti,  mlango wa chumbani kwake, ukafunguliwa, mama mwenye nyumba huyo akaingia…., jamaa akajikuta kanasa, kuinuka hawezi kuendeela na huduma hiyo hawezi, na binti alivyovaa , khanga moja, na sehemu kubwa ya mwili ipo wazi.



    Mama mwenye nyumba akabakia mlangoni haamini anachokiona jicho limemtoka, na alichosema baada ya muda kidogo;



    ‘Kumbe ni kweli…..’ilikuwa kauli ya mama.



    ‘Huyu binti nimemkuta kazimia,..ndio nataka kumpatia huduma ya kwanza…’akasema.



    ‘Kazimia, humu chumbani kwangu, na …akiwa hivyo, uchi…..hahaha, sikuelewi….’mama akawa kama anacheka na kwa muda huo, huyo binti akawa kazindukana,…

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Nilipozindukana, niliona nipo chumbani kwa watu, nikakumbuka nilivyokuwa nimevaa, na juu yangu yupo baba mwenye nyumba, kaniinamia… akili za kwanza zikanituma vibaya, nikajua huyu baba anataka kunifanyia kitu kibaya, nikakurupuka, na kuanza kupiga ukelele, nikisema;



    ‘Sitaki, sitaki…..’ na waki nakurupuka, nakimbilia nje,..ndio  nikakutana na mama mwenye nyumba kasimama mlangoni,… uso, kwa uso…na hilo jicho nililoangaliwa nikajua sasa kumeharibika, hata hivyo sikusimama, mbio mbio, nikakimbilia nje…na wazo langu la haraka ni kuondoka kabisa kwenye hiyo nyumba.



    NB: Kisa hicho kinaanza kasi yake.





    WAZO LA LEO: Ikitokea jambo baya, mfano kwenye mahusiano, au tukio baya katika jamii, …Kwanza tusikimbilie kuchukua hatua,..kulaumu, au kuhukumu, kwa kuhitimisha na kuhalalisha ubaya huo. Kwanza ni vyema kufanya uchunguzi kutegemeana na ukubwa wa jambo lenyewe, na kuona sababu za jambo hilo, huenda jambo hilo limetokea kwa bahati mbaya tu, au kuna sababu za msingi za kutokea jambo hilo.



    Wengi wetu , tunapenda kuchukulia mambo kwa pupa na hasira, na matokea yake, ndoa huyumba, au hata kuharibika, au mahusiano kati ya mtu na mtu au jamii, huja kuvurugika, na baya zaidi wengine hukataa hata kukaa mezani kuyaongelea matatizo hayo,  au kutafuta ni kwanini… Tukumbuke kuwa kila jambo hutokea kwasababu fulani, nahiyo sababu inaweza ikawa ni fundiasho kwetu, basi tulitafute hilo jambo kwa hekima ili tufundishike.



    Mimi nikakimbilia nje, kwa muda huo nilikuwa sijajitambua vyema, akili ipo kwenye ile hali kuwa baba mwenyenyumba alikuwa na dhamira mbaya dhidi yangu, ndivyo nilivyokuwa nafikiria hivyo, kwa wakati huo, lakini pia nilishaingiwa na woga kuwa mama mwenyenyumba hatanielewa,..atafikiria na mimi nilikuwa nina nia mbaya, kwa hali niliyokuwa nayo, nilianza kujilaumu kwanini sikuwa nimevaa vizuri, lakini ni kawaida wakiondoka navaa hivyo kwasababu ya joto, na kwa vile ninafahamu kipindi hicho huwa hakuna mtu.



    Na nikamuona yule kijana akiingia getini, hapo nikaharakisha kukimbilia chumbani kwangu kabla hajaniona, niliona ajabu na yeye kwanini amewahi kurudi hivyo, ...baba karudi mapema, na halikadhalika mama, na sasa kijana, kuna nini leo, sikutaka kufikiria zaidi, nikakimbilia chumbani kwangu.



    Kwakweli akili yangu ilikuwa imetekwa na mawazo hayo sikuwa nimefikiria jambo jingine, sikuwa na kumbukumbu za nyuma, hadi nilipofika huko nje, nikatulia kidogo, nikajikagua, ooh, hali niliyokuwa nayo, nilivyovaa, sio ya kuonekana na mtu, kwa haraka sasa nikageuka kuelekea ndani, hapo bado akili imeganda kwa tukio hilo.



    Nilipofika ndani, nikavaa nguo zangu za heshima, na wakati navaa,ndio akili ikaanza kurejea mahali pale, na hapo ndio nikakumbuka ile barua, kwanza sikuamini, nikahisi labda ilikuwa ni ndoto, nilitaka iwe hivyo, iwe ni ndoto sio kweli,…unajua huwezi kuamini, kufiwa ni kitu kingine jamani, …



    ‘Haiwezekani, …kwanini , kwanini lakini, kwanini sisi, kwanini jamani, sisi tumewakosea nini hawa watu jamani, na umasikini huu tena, bado, mama yangu kawakosea nini jamani…’ hapo sikuweza kuvumilia tena nikaanza kuangusha kilio, kilio cha kwikwi,….nililia hadi kichwa kikaanza kuniuma, na sijui ilitokeaje, maana nilihisi giza usoni, na kulala sakafuni.



    Nilizindukana mtu akinishika shika..nikakurupuka, na kusimama nikitaka kukimbia, lakini nikajikuta nikishikwa na mshangao, kwani aliyekuwa kasimama mbele yangu alikuwa ni mtu mgeni kwangu, ni mdada …mdada aliyekuwa kavalia vizuri tu, akaniangalia usoni, akatikisa kichwa kama kusitikia, akasema;



    ‘Oh, pole, sana…’ akasema akiniangalia kwa macho ya huruma, sikuweza kumjibu, machozi yakaanza kunitoka kama maji, akili haitaki kukubali, na japokuwa sikujua ananipa pole ya nini…lakini akilini nilihisi labda ananipa pole ya msiba, kama ni hivyo kajuaje…nikataka kumuuliza ila yeye akaanza kuongea;



    ‘Mimi nilikuwa mfanyakazi wa humu kipindi cha nyuma, najua nikwanini upo hivyo, ila mimi kwasasa nimekuja kuchukua mizigo yangu niliyoacha humu ndani natumai mama mwenye nyumba amekuambia …’akasema.



    ‘Kawaulize wenye nyumba, mimi sijui, naondoka zangu…’nikasema, sasa nikitaka kuanza kuchukua nguo zangu na kuondoka mbali kabisa na hiyo nyumba, sikujua nataka kwenda wapi.



    ‘Unaondoka,….!! Unataka kwenda wapi bibi wewe,…hahaha, naona umeshaanza kuionja joto ya jiwe au….! Nikuambie kitu, pambana na haki yako, …usikubali kushindwa, mimi niliondoka hapa kwa vile nilipata sehemu nyingine, vinginevyo, wangelinitambua mimi ni nani…’akasema akitikisa kichwa kwa majigambo.



    ‘Sasa kwanini uliamua kuondoka..?’ nikamuuliza hivyo, japokuwa sikutaka kuongea sana.



    ‘Kuna mengi yalitokea humu, ….nilivumilia sana, lakini ikafika muda, nikaona haina haja, hata hivyo, nilikuwa nimepata kazi sehemu nyingine,…ila kuishi humu inataka moyo,…kuna mambo mabaya sana humu ndani,…utajionea wewe mwenyewe…’akasema.



    ‘Kuna mambo gani…?’ nikamuuliza kwa mshangao, japokuwa nimekutana na mambo mambo..lakini kwangu mimi bado nilikuwa naamini ni ndoto tu.



    ‘Sijui mashetani, sijui….aah, utajionea wewe mwenyewe…’akasema na hapo nikakumbuka kale kakijitabu, nikajua huenda ni yeye alikiacha hicho kijitabu kidogo.



    ‘Kwani hayo mashetani yapoje, mimi siyajui………’nikamuuliza na yeye akaniangalia kwa macho ya kushangaa, halafu akaniuliza;



    ‘Kwani wewe umefika muda gani kwenye hii nyumba na je tangia uje humu huwa unalala kwa amani …?’ akaniuliza;



    ‘Mhh…sina amani kwakweli, lakini kwani hayo ni mashetani yapoje, yanaonakena, au…maana mimi nahisi kama naota tu, mtu ananikaba, ananifanyia mambo mabaya, ni hivyo tu…’nikasema.



    ‘Hahaha, wewe wa wapi,….mmh,… hayo ni majinamizi, na majinamizi kwa uelewa wako  ni nini…na baya zaidi, yanavyokufanyia vitu vibaya au sio…, si ukiamuka unajiona ni kweli umafanyiwa vitu vibaya, vibya kwa vipi,…?’ akaniuliza.



    ‘Aaah kwakweli mimi sijui kitu….’nikasema sikutaka kusema lolote, kwangu mimi bado niliamini ni ndoto, sikuwa na wazo jingine.



    ‘Hahaha, hujui kitu eeh…., ngoja ubebe mimba ndio hapo utajua kuwa sio ndoto..ni kweli, na ukibeba huo mzigo, utaanza kuina dunia, imeibeba wewe ….’akasema.



    ‘Mimba itaingiaje wewe, kupitia kwenye ndoto…’nikasema kwa mshangao.



    ‘Hahaha, ..hebu niondoke zangu naona naongea na mtu asiye-elewa, siku ukielewa utanitafuta….’akasema.



    ‘Mimi hata sijui…ni mtihani gani huu jamani, nimetoka kwetu nikijua nakuja kupata ahueni ya maisha, sasa tena nakutana na mambo haya,..sasa tena, mama yangu wamemuua…nitakwenda wapi mimi jamani , binti masikini…’nikasema.



    ‘Eti nini….!!!, wamemuua mama yako, akina nani hao…?’ akauliza kumbe alikuwa hajajua kwanini nipo na hali hiyo.



    ‘Nilikuwa sijui, walinificha, nimegundua baada ya kuona barua waliyoandikiwa, kutoka huko kijini..sijui kwanini walifanya hivyo…wangeniambia tu, angalau nihudhurie msiba wa mama yangu….nitawalaumu sana kwa hiki kitendo, ….ndio maana nataka niondoke kabisa humu ndani…’nikasema na kuendelea kulia.



    ‘Unajua hawa matajiri hawana moyo wa huruma kwa watu kama sisi,…wao kwa wao wanaoneana huruma kwa vile wanaweza kusaidiana, sasa wewe utamsaidia nini…., ndio wanaweza wakawa na huruma ya kujionyesha,…kwa vile…unanielewa hapo…., lakini kwa maswala yasiyowahusu, au kwa kuogopa sheria tu…ila kiukweli, kwa watu kama sisi, hawawezi kukutilia maanani hisia zako, kwao wao uwatimizie kazi zao tu, ..na ukiumwa, utaona watakavyokuchukia….’akasema.



    ‘Lakini kwani wao hawafiwi, hawaumwi…?’ nikamuuliza.



    ‘Wanafiwa, wanaumwa ten asana…, lakini wao si wao,…hisia zao kwao ni kwao, na kwa wengine hasa watu kama sisi, hawazijali sana, wanaju ukipewa ruhusa ya kwenda kwenu, utakaa huko mwezi, na nani atawafanyia kazi zao, na ukienda utwatia gharama, na gharama kwao, ni hasara, wewe utakuja kujionea tu….’akasema.



    ‘Lakini hawa watu hapa wanaonekana ni wema, wamekuwa wema kwangu, wamekuwa wakimtumia mama vyakula ....kiukweli mimi sijawahi kuona ubaya wao....kuachilia mbali haya yaliyotokea, na haya yametokea kwa bahati mbaya tu, mimi sikukusudia iwe hivyo…’nikasema.



    'Yapi yaliyotokea...?' akaniuliza



    'Aaah, ....'nikasema hivyo tu na yeye akasema;



    ‘Wema wanao, lakini …wema wao ni wa kumpatia ng’ombe majani ili upate maziwa, …chunga sana, humu ndani, utakutana na mambo mengi tu,…mimi niliondoka, ila…ipo siku, watanikumbuka…’akasema



    ‘Kwanini unasema hivyo…?’



    ‘Mimi nimetoka kwetu, nimeaga, walichonifanyia,…watakuja kunitafuta, …huo ni ujumbe kwao, kama utawaambia haya,…na umbea wako,… kama hutawaambia, yaache kama yalivyo, nimekuja kuchukua vitu vyangu, na kama hujaanza kupatwa na matatizo, basi, labda mwenzetu upo tofauti, lakini ..mimi ….nimekuja tu hapa kwa vile niliacha nguo zangu, vinginevyo, nisingelikanyaga tena hapa, mpaka wao wanitafute, najua watanitafuta tu….’akasema sasa akipanga vitu vyake vyema.



    ‘Utawafanya nini….?’ Nikauliza



    ‘Hahaha, nitawafanya nini, kama walivyonifanyia mimi, na wao nitawafanyia hivyo hivyo, na yoyote atakayekuwa upande wao, atakiona cha moto….’akasema.



    'Kwani wao walikufanyia nini...maana ...?' nikauliza



    'Mimi kwasasa sitaki kujiuliza uliza, humu kutawaka moto, yoyote aliye humu ndani atauonja ubaya wangu...sitakuwa na huruma na mtu ....mpaka moyo wangu ufurahi....'akasema



    ‘Ina maana….hata mimi…?’ nikauliza kwa mashaka.



    ‘Sikiliza ….nikuambie kitu, hapa kuna tatizo kubwa sana, siwezi kukuambia ni nani yupo nyuma ya haya matatizo, awali nilimshuku sana baba mwenye nyumba,…nilimtegea siku moja,…maana walijua mimi ni hivi hivi tu, baadae nikajiukuta nina mimba...aah, …lakini tuyaache kwanza, sitaki nikusimulie kwa hivi sasa kila kitu, muda utafika nitakusimulia, lakini sio kwa sasa hivi….’akatulia.



    ‘Lakini si umesema ni mashetani au…?’ nikauliza



    ‘Ndio ni mashetani, hujanielewa nikuambia mara ngapi….’akasema akiniangalia machoni.



    ‘Sasa hao watu, baba mwenyenyumba wanakujaje hapo?’ nikamuuliza.



    ‘Inawezekana wao wanayatumia, au wao wanajivika huo ushetani, au …hata sijui,ila mimi sijali kama ni wao au kuna mtu mwingine, hapa hapa nitapambana nao, nilipatia matatizo humu nikaharibiwa usichana wangu humu, nika...we aha tu, sitaki hata kusimulia tena, nashukuru kuwa leo nimefika na nimepaona vyema...'akaangalia huku na kule, na mimi sikusema neno, yeye akaendelea kuongea.



    'Siku ..., nilipoondoka hapa....niliondoka na giza usoni,..nalia, nasononeka.....hakuna aliyenionea huruma,.... sasa nimekuja na macho yangu mawili, macho yenye nuru ya ukatili, unasikia, unyama unyama..…’akasema akiangalia huku na kule kama kukagua.



    ‘Oh….mungu wangu, sasa nitaishije humu ndani, mbona unaanza kunitisha…, kwanza mimi naondoka, mama yangu, kafa…mmh, mama yangu hayupo tena duniani masikini mie..nitakua mgeni wa nani…ooh, mama umeamua kuniacha mama…’hapo nikaanza kulia tena, hadi huyo msichana akanionea huruma.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Kwani mama yako alifarikije..?’ akaniuliza akiniangalia na machoni nilimuona na yeye akilengwa lengwa na machozi.



    Nikamuelezea kama barua ilivyosema, halafu yeye akasema;



    ‘Nilisikia taarifa kama hiyo….mmh,  kuna mtu mmoja alitokea huko kijijini, sijui itakuwa ndio hiyo au la…, lakini mbona ilitokea siku nyingi, labda sio hiyo taarifa niliyoisikia mimi…ni mud asana…’akasema.



    ‘Sijui ilitokea lini,… mimi ndio niliona hiyo barua, sijaangalia iliandikwa lini…’nikasema.



    ‘Hiyo barua ipo wapi…?’ akaniuliza



    ‘Aaah, …..hata sitaki kuiona tena…nilitoka humo ndani kwa haraka, sijui ..itakuwa huko huko ndani…’nikasema.



    ‘Sasa utajuaje mama yako alifariki lini, maana huenda wasikuambie,...nikushauri kitu, ..jaribu kuwa mjanja,..uwe makini kwa kila jambo, usipoteze ushahidi,..unajua kuna kitu nataka wewe unisaidie, kama unataka uwe na amani..vinginevyo, na wewe yatakukuta hayo ninayotaka kuyafanya, …mmh, naona muda umekwenda,..siwezi kukuambia kwa leo….’akasema.



    ‘Oh, wala sitaki kukaa tena humu ndani….’nikasema.



    ‘Sikiliza mama yako ameshafariki, huwezi kumrejesha tena hapa duniani, hata ukienda huko kijijini, na kama ulivyonisimulia maisha ya huko kwenu, ina maana huna ndugu huna jirani atakuekuthamini tena, ina maana sasa wewe ni wewe, huna baba, huna mama, wewe ni yatima, masikini…unanielewa…’akasema.



    ‘Mungu mwenyewe anajua…’nikasema hivyo.



    ‘Sio mungu mwenyewe anajua,..... wewe kwa hivi sasa unatakiwa upambane kivyako….au  hebu niambie ukienda huko kijijini eeh,, utafanya nini, sana sana watakuonyesha kaburi la mama yako, halafu,..niambie hilo kaburi litakusaidia nini… utafanya nini, …muhimu kwasasa ni kuanza mapambano, kwanza jitahidi upate chako, pili hakikisha haki inatendeka, hao waliomfanyia hivyo mama yako, na wao uje kuwafanyia hivyo hivyo…kwa udi na uvumba…’akasema kwa kujiamini.



    ‘Nitawajuaje mimi…wewe unakijua kijiji chetu kilivyo..huko kuna watu watemi, wanafanya watakavyo…viongozi wa kijiji wenyewe wanawaogopa…..’nikasema.



    ‘Kwanini usiwajue, watakuwa ni wanakijiji au ni wageni, …sikiliza nikuambie kitu, hakuna kinachoshindikana chini ya hii dunia, ukiwa bado unapumua,…na ukiamua, lakini ukibakia kulia lia, haya lia, mpaka machozi ya damu labda yatakusaidia, ni kweli hata mimi nililia sana, lakini baadae nikazindukana, …wao kama wamekufanyia unyama, na wewe walipizie kwa unyama, kwa njia yoyote ile usijali ni njia gani…’akasema.



    ‘Sijui, …hata sielewi, hapa kichwa changu hakipo sawa..unayoniambia mimi sielewi…na sitaki kulipiza kisasi, mimi namuachia mungu tu…’nikasema.



    ‘Hahaha, haya muachie mungu, mungu humsaidia anyejisaidia…haya muachie mungu, siku yako nayo ifike, huko mbele utalipiziwa na mungu ..maana hao watu wakijua kuwa upo, na wakahisi unaweza kuwafuatilia na wewe watakuua..sasa kabla hawajaanza kufanya hivyo,wewe wawahi…mapema….’akasema kwa kujiamini.



    ‘Hapana mimi sitaki kufanya lolote baya…nitamuomba mungu tu inatosha….’nikasema.



    ‘Hahaha, toka lini duwa la kuku likampata mwewe, haya omba, omba usiku na mchana, tuone kama watakuja wakuambia ni sisi tumeua….hahaha, wewe vipi wewe….pambana nao, wapige kiini macho na wao wataabike…’akasema



    ‘Hapana…, mama yangu alinipa usia, kuwa..nisipende kulipiza kisasi, na pili, nisishndane na wenye pesa, kwani wao wameshikilia mpini,…na …aah, basi mimi sina nguvu tena, ..waache waje waniue na mimi, ni heri tu niende huko mbeleni, nikakutane na mama yangu..mimi sioni kama kuna umuhimu wa kuishi tena kwenye hii dunia, nimezaliwa masikini, nimekulia masikini, na…sizani kama kuna lolote nitafanya linisaidie….’nikasema.



    ‘Sikiliza wewe, usiwe mjinga,…mimi nitakusaidia kitu,… huyo mtu aliyenisimulia anasema kuna watu anawahisi na wamekimbilia huku huku dar, sasa kwa hivi sasa huwezi kufanya kitu huna mbele wala nyuma, hujaweza hata kuweka mtaji, ili ufanye kitu, unatakiwa uwe na pesa..kuna hata kusafiri, hadi huko kwetu, unakufahamu huko kwetu…kama unataka nikusaidie mimi…’akaniuliza.



    ‘Nitakujuaje huko kwenu na mimi ni mara ya kwanza kuonana na wewe…’nikasema



    ‘Kwetu ni ufipa, lyamba liya mfipa,..huko ndani ndani, ukitoka huko kwetu kuja huku, huagi, ..ila mimi sikukulia sana huko,…baada ya kupatwa na matatizo humu ndani, nilikutana na ndugu yangu mmoja, nikamsimulia wee, akaniambia hiyo ni kazi ndogo tu…, twende kijijini….haaah, nilipofika huko nikawekwa sawa, na bado, kazi haijaanza, hawa watu humu watanitafuta…’akasema.



    ‘Wewe jamani kwanini unataka kufanya hivyo, kwanza huna uhakika kuwa ni wao, umesema ni mashetani, je kama sio wao,..mimi niliona jambo jema ni kuwasamehe tu….’nikasema.



    ‘Wasamehe tu eeh….haaha….!, unajua walichonifanyia,…wewe unasema tu, niwasamehe tu, niwasamehe, kwanini wao hawakuliona hilo, wakanionea huruma, mimi nimepatwa na matatizo ndio niwasamehe, unajua sasa hivi sina kizazi….’akasema akishika tumbo.



    ‘Kwanini…?’ nikauliza nikionyesha mshangao.



    ‘Yatakuja kukuta na wewe…haina haja ya kukusimulia…kwasasa kaza buti, nakuonea huruma sana, lakini vita havina huruma, ama uwe upande wangu au uwe nao, na ukiwa nao, wewe ni adui yangu, kwaheri….’akasema sasa akiwa kachukua mzigo wake wa nguo zake.



    ‘Mimi hata sielewi kitu, hivi sasa akili yangu haipo sawa, natamani ninywe sumu tu..nimfuate mama yangu, …’ nikasema.



    ‘Utaelewa tu, dunia itakufunda, ….kama wataka kujiua kajiue…utamkomesha nani….’akasema akikagua humo ndani, kwa macho, halafu akatema mate chini, na kusema;



    ‘Humu, ilikuwa jela yangu, humu niliteseka, humu, nililia,. ….mpaka machozi ya damu, hakuna aliyenionea huruma, huyo kijana wao, anajifanya ana huruma, lakini moyoni kama baba yake….sasa tutapambana…na wao…’akaanza kuondoka.



    ‘Sasa mbona unaondoka…’nikasema nilipoona nabakia peke yangu.



    ‘Nitakufundisha kitu, lakini sio leo, …..ngoja niondoke wasije kunikuta humu ndani…’akasema.



    Mara nikakumbuka kitu,…



    ‘Wewe uliacha kijitabu kidogo hivi…?’ nikauliza



    ‘Ndio eeh kweli,….nimekitafuta wewe…yaani hicho ndio kumbukumbu zangu zote, nakiomba tafadhali..humu kuna mambo nilifundishwa huko kijijini, …sasa ok…nipe nipe…’akasema .



    Basi nikampa kijitabu chake, na kwa haraka akachukua mzigo wa nguo zake na kuondoka, na haikupita muda, mara mama mwenye nyumba akaingia, akiwa kaiva, kakunja uso, ..sijawahi kumuona akiwa katika sura hiyo kabla,…akashika kiuoni, ananiangalia machoni…macho yaliyojaa hasira…mkononi kashika mfuko wa zawadi.



    Na kwa nje, nikasikia gari liondoka kuonyesha kuwa baba mwenye nyumba anaondoka !



    **************

    NB : Ndio ilikuwa hivyo, je itakuwaje baadae



    WAZO LA LEO: Ukitendewa ubaya, usikimbilie kulipiza kisasi, kwani hujui ni kwanini ikatokea hivyo, mola wako hajakuacha, na huenda karuhusu huo ubaya ili upate fundisho fulani lenye heri mbele yake. Muhimu ni kuvuta subira, na kuelekeza maombo yako kwa mungu. Hakuna jambo lenye herii kama kusameheana. Kusamehe huvuta heri, na kulipiza kisasi huzaa kisasi kingine.



    Ile sura niliyoiona kwa huyo mama, ilinitosha kuwa ni ujumbe kwangu, mimi nikanywea, nikasubiria kauli itakayotoka, kiukweli nilishajiandaa kuondoka, lakini sikujua wapi pa kwenda, ila nilitamani tu kuondoka hapo,…na huko ninapokwenda nitaishije, hayo kwangu akilini yalikuwa hayapo, lakini kama tuliishi mimi na mama yangu kwa kuomba, kwanini nije kushindwa kuishi. Mungu mwenyewe anajua!





    ‘Hii ni zawadi yako, au sio…?’ huyo mama alianza kuniuliza hivyo, huku akiwa kainua mfuko wenye kitu ndani, ni mifuko unayowekewa kitu ulichonunua madukani hasa supermarket,…hata sikujua ni kitu gani, au kimetoka wapi.



    Nikajua labda ni zawadi ya kuondoka nayo, sikusema kitu wala kusimama kuipokea, nikawa nimetulia tu kimia, akilini nikiwa nashindwa hata kuwaza, mambo mengi yamepita akilini , na kichwa hapo kinaanza kuuma, lakini nikajitahidi kujituliza.



    ‘Nakuuliza hii zawadi ni yako, au unaogopa kusema sasa, hii zawadi amekuletea mume wetu, kakuletea wewe bi mdogo wake, ichukue, …’akasema akinirushia na mimi sikusogea kuichukua, nikawa nimetulia tu. Nilikumbuka maneno ya mama, akinikanya nisigombane na watu, aliwahi kuniambia;



    ‘Binti yangu, ukiona mwenzako kakasirika anaongea kwa jaziba wewe tulia mpe muda amalize jaziba yake, halafu akitulia ndio unaweza kufikiria jambo la kumjibu. Mara nyingi mtu kama huyo ukimjibu ghadhabu zake huongezeka, na inaweza kutokea madhara makubwa!



    ‘Utashangaa nimeipata wapi hii zawadi yako, na mletaji kashangaa nimeipataje,…mimi nilikuja mapema tu, nikijaribu kuchunguza kinachoendelea, …’akasogea ndani na kusimama, akageuka kuangalia mlangoni, huku anaongea.



    ‘Nimesikia mengi kutoka kwa majirani, ..sikutaka kuchukulia haraka, …nilijua ipo siku tu , nitawanasa,…sasa leo nimewanasa, na nimegundua kuwa ni kweli, wewe ni nyumba ndogo ya mume wangu,…unajua mimi ni mvumilivu sana, lakini uvumilivu una mwisho wake,  siwezi kuvumilia tena, maana haya yametokea mara nyingi,…sasa nasem basi, umesikia nitakuachia huyo mume, lakini sio kuwa nitawaachia, make humu, hapana wewe na yeye mkatafute wapi pa kuishi..huo ndio uamuzi wangu….’akasema na aliponiona nipo kimia, akanigeukia.



    ‘Unajua,…mama yako, alinikabidhi wewe, akasema nikulee kama mwanangu, nikulee kama binti yangu, kumbe nimechukua nyoka ndani ya nyumba yangu, siwezi hata kuamini,..unajifanya mpole, unajifanya hujui kitu, kumbe, umekubuhu….huwezi kusema kitu maana mimi mwenyewe, nimejionea kwa macho yangu..halafu ulipogundua kuwa nimewafuma, ukajifanya kukurupuka na kukimbia, ujanja w kitoto…’akasema.



    ‘Sasa nimekuambia mwenzako, afungashe, na wewe nimekuja kukuambia ufungashe…mkatafute pa kuishi, hii nyumba ni yangu ni mali ya wazazi wangu, …nina mamlaka nayo,…kama ulifikiri kuwa ni mali ya mume ..umenoa, huyo mume hana kitu hapa…unisikie vyema, mtaenda kutafuta sehemu ya kupanga, muanze maisha yenu, mjifunze maisha,….unanielewa…’akasema akiniangalia na mimi nikawa kimia, ni kama sikuyasikia hayo maneno.



    Machozi yalikuwa yakinitoka,..yanatiririka kama maji, lakini sikuweza kutoa sauti ya kulia, kilio kilikuwa ndani ya moyo, nasononeka, ..naomboleza, ..lakini ni nani atalijua hilo, ni nani atamuonea huruma binti masikini…



    Mara akatokea kijana wake,..akaja na kusimama mlangoni, akasema



    ‘Mama mbona unachukulia haya mambo kwa jaziba, ….’akasema na mama yake akamuangalia kwa macho yaliyojaa hasira,



    ‘Hayakuhusu haya,…’mama akasema.



    ‘Mama,…., kwanza naomba samahani, kuwaingilia …ila mama una uhakika na unachokisema, ….?’ Akauliza, sasa akiingia ndani kabisa.



    ‘Uhakika gani ninao-uhitajia mimi…., hebu niambie mwanangu, nimemfuma huyu Malaya akiwa chumbani kwetu na mume wangu, akiwa kavalia khanga moja, wapo wana, hapo unahitajia ushahdi gani mwingine, niambie wewe unayejifanya mkubwa sasa, …..yaani nasikia hata kutapika…’akasema.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Mama umuogope mungu, hivi kweli mama, huyu anaweza kufanya kitu kama hicho kweli mama, nakuomba mama urejeshe moyo wako nyuma, wewe ndiye uliyesema huyu ni binti wa kijijini hajui lolote, tumuongoze, leo hii unasema kayafanya hayo, mama mimi siamini hayo, hajafanya hayo unayoyasema….’akasema huyo kijana na mama yake akamuangalia huyo kijana usoni akiwa katahayari, akasema;



    ‘Ina maana mimi naongopa, ina maana mimi macho yangu hayaoni siku hizi, nimekulea nikakuonyesha njia, sasa umeota mapembe,…sikiliza wewe mtoto, wewe bado mdogo, haya hayakuhusu kabisa…, na hujui uchungu nilio nao mimi….subiria muda wako utafika, utaoa, na utafanyiwa hivyo ndio na wewe utajua ni kwanini ninasema haya…’akasema.



    ‘Mama nayasame haya kwa vile mimi namfahamu sana huyu mdada, hawezi kuyafanya hayo, na unakumbuka siku moja nilikuambia kuwa huyu mdada alishikwa na baba…alishikwa na  baba akitaka kukimbia….’akatulia akimuangalia mama yake.



    ‘Mama, huyu mdada ana matatizo makubwa, anapata shida, anaweweseka usiku, na wakti mwingine anadondoka na kupoteza fahamu….je ulimpa nafasi baba akuelezee kama huyo mdada hakudondoka akapoteza fahamu na baba alikuwa akijaribu kumrejesha katika hali yake, ..je mama angelikuwa ni binti yako, ungelifanyaje,…mama wewe ulitufundisha tumuogope mungu, kwa kusingiziana uwongo, je kama unachomsingizia mwenzako sio kweli, utasemaje mbele ya mungu...’kijana akasema.



    ‘Wewe mtoto, wewe unataka kusema nini kuwa mimi namsingizia uwongo huyu mwanamke…, kama namsingizia uwongo kwanini hajitetei…aseme yeye mwenyewe kama sio kweli…kama sio kweli sikumkuta akiwa kalala chini akiwa uchi, na mume wangu yupo juu yake, …asema yeye mwenyewe kama sio kweli….’akasema na mimi nikaendelea kukaa kimia.



    ‘Eti ni kweli hayo dada…?’ akaniuliza huyo kijana akiniangalia moja kwa moja, na mimi nikawa nimeinama chini, nikuendelea kukaa kimia, na mama akaonyesha ishara kama kusema



    ‘Unaona…’ lakini hakutamka neno….na kijana akaniangalia kwa mshangao, na kusema;



    ‘Sema ukweli wewe mdada, jitetee,  shauri lako…, ukikaa kimia ni nani atakusaidia….’akasema, na mama akasemaa;



    ‘Usimlazimishe kukana maovu yake, kukaa kwake kimia, inaashiria nini, kuwa ni kweli, na moyoni anaona haya….kwa uchafu walioufanya na ….huyo baba yako….’akasema mama.



    ‘Mama…usiseme hivyo, una uhakika….’akasema kijana



    ‘Si huyo hapo,….umemuuliza kakujibu nini, kakaa kimia, maana ukweli unauma…ni ..hata sijui niseme nini, ashukuru mungu siku hizi hasira zangu zimeenda likizo…’akasema mama.



    Na mimi kwanza nilikaa kimia, nikiwazia haya mambo kwa undani zaidi, sikuwa na la kujibu, nilishindwa nijubu nini maana hayo anayoyasema huyo mama, siyaelewi, na sijui yametoka wapi, baadae sijui ilikuwaje nikajikuta nasema haya maneno;



    ‘Mungu pekee ndiye anayejua ukweli wa hayo yote, kama umeamua kuamini hivyo, hata nifanyeje siwezi kubadilisha imani yako, ila mwenyezimungu peke yake ndiye anayeweza kufanya hivyo….’nilipotamka maneno hayo, nilihisi kichwa kikitulia maumivu, na hapo nikaingiwa na nguvu y akuongea zaidi, nikasema;



    ‘Mimi sina uwezo wa kuwafanya nyie muamini ukweli ulivyo…ila mungu anaweza. Lakini ni bora niseme ukweli,…, mimi sijui hicho ninachosingiziwa nacho,…sijui mama unaongea nini, mpaka sasa naona kama umeamua kunitungia uwongo, labda ili uweze kutimiza unachokitaka….’niliposema hivyo huyo mama akataka kunikatiza, lakini sikumpa nafasi nikaendelea kuongea.



    ‘Mama…kilichotokea,…. mimi nilidondoka, na kupoteza fahamu…’niliposema hivyo, mama akacheka kwa kebehi, akijua labda nimesema hivyo kwa vile kijana wake alisema hivyo.



    ‘Mimi nilidondoka, … baada ya kuisoma barua iliyotokea kijijini kuwa mama yangu amefariki….’niliposema hivyo, machozi yakawa yananitoka utafikiri maji yana mwagwa, na mama akabakia mdomo wazi, kanikodolea macho utafikiri kasikia jambo gani, hakutarajia hilo kabisa, huenda hata hiyo barua, labda aliiona mume wake na hakuweza kumuambia mkewe kuwa mimi nimeugundua ukweli.



    ‘Mama, wewe umesema kuwa umenichukua mimi kama muwe kama wazazi wangu, kwa vile mama alikuomba ufanye hivyo, ..je ungeyafanya haya kwa mtoto wako,…, najiuliza ni kwanini mkanifanyia mimi hivyo, au ni kwa vile, …’nikasema hivyo bila kumalizia.



    ‘Mama nyie  …mlipata taarifa hiyo mkakaa kimia…’nikasema na huyo mama sasa akabadilika sura. Kutoka kwenye hasira na kurejea kwenye kushangaa…binadamu sura hujieleza ukimuangalia kwa makini.



    Mama sasa akawa anatafuta njia ya kujitetea, kwanza akahema kama mtu aliyepo kwenye usingizi akibadili pumzi kwa nguvu. Akamtupia jicho kijana wake , na kijana wake akawa kainama chini, sasa ikawa zamu yao, kuhisi unyonge, maana ukweli huuma!



    Lakini kama ujuavyo, mwenye uwezo, tajiri, watawala hata wakikosa hawakosi neno la kujitetea, huyo mama akasema;



    ‘Ni nani alikuambia upekue pekue huko ndani kwangu..si nilishakuambia kuwa wewe kazi yako ni kufanya usafi tu huko ndani…na nilishakuambia kama baba yako yupo wewe usiingie kabisa huko ndani…kwanini sasa unajiamini mpaka unaanza kupekua pekua huko unatafuta nini, je nikipotolewa na kitu utakataa kuwa wewe hujahusika, na kumbe wewe ndiye unamtia mshawasho mume wangu kwa kuingi ahuko chumbani na khanga moja,…niambie ni kwanini ukafanya hivyo?’



    ‘Mama, mimi sikupekua pekua vitu vyenu nilikuwa nakung’uta vitabu mavumbi, na kwa bahati mbaya ndio hiyo barua ikadondoka, na kufunguka,…na mama sijawahi kuingia ndani akiwepo baba kwa utashi wangu, kama niliingia, ni kwa muito wa baba….’nikasema na hapo akakunja uso kama anataka kusema neno, na mimi sikumpa nafasi nikaendelea kusema;



    ‘Wakati nakugung’uta vitabu, ndio hiyo barua ikadondoka,…na ilipodondoka, ikafunguka,…na ndio nikaona maelezo ya kutoka kijijini, na macho hayana pazia,..kuona maneno hayo,…nikavutika kuyasoma yote,…na ndio hapo nikagundua hilo,… kama ni kosa, hapo nimefanya kosa, kwa kusoma barua yako,…naomba mnisamahe, lakini najua ni mungu alitaka kunifunulia ukweli,..mlitaka kunificha mungu akataka kunifunulia ukweli…. sasa nauliza ni kwanini mumenifanyia hivyo…’nikasema



    Huyo mama sasa akanywea, akahema, akageuka kumuangalia mwanae, kama vile anataka amsaidie kujitetea, lakini kama nilivyosema watu hawa wenye uwezo, hawakosi neno,…akasema;



    ‘Sikiliza, wewe binti, hatukuwa na nia mbaya kwako,…nia yetu ilikuwa ni njema kabisa, ya kuwa tukikuambia huo ukweli, kwanza utachanganyikiwa, utashindwa kufanya kazi, na wewe hujadunduliza kiasi cha fedha cha kukuwezesha maisha, na kwanini tulifanya hivyo, tulijua ukiambiwa utataka kwenda nyumbani, na ukienda huko unaweza usirudi kwa hali ilivyo...'akasema



    'Kwanini jamani....'nikasema hivyo.



    'Sisi tunaona mbali zaidi yako...hebu jiulize ungeenda hivyo kiharaka hivyo, nani angelusaidia, hpo kuna nauli..kuna matumizi, na huko je.... huko ungeenda kuishie, na maisha yalivyo huko sio kama ulivyoondoka, ..huko sasa hivi, huko kijijini eeh, we usikie tu, hali ni mbaya sana hakuna chakula watu wanakufa kwa njaa…, na isitoshe, hali ni hatari, watu wanauwawa ovyo, tuliogopa ukienda huko na wewe utauwawa…sasa nikuulize je hivyo tulifanya vibaya...’akatulia.



    'Mimi najiuliza kame ingelikuwa ni wewe umefiwa, na tena mama yako, ungelifanyiwa hivyo ungelifurahi...yaani hata..hapana mimi bado sijaridhika na hilo, lakini nitafanyeje, mimi naweza kusema nini kwenu, mliamua kwa vile....'hapo sikumalizia, na huyo mama akanidakia kwa kusema.



    ‘Mama yako alinikabidhi wewe akasema nikulinde, na nihakikishe upo mikono salama, na ndicho tulichokifanya,…hata kama hutaelewa,…na hata hivyo, kwa mfano tungekuambia, uende…ungeenda huko ungelifanya nini, maana hata sisi wenyewe taarifa hiyo tuliipata imechelewa walikuwa wameshazika kutokana na hali ilivyokuwa huko…, mama yako aliungua sana….umenielewa, pole sana, na tuliza kichwa chako…’huyo mama akasema alipoona mimi ninalia kwa kwikwi.



     ‘Sasa pamoja na hayo najua sasa hivi upo kwenye majonzi,….wenzako sasa wameshasahau wa kusahau…lakini ni lazima nihakikishe mambo fulani, japokuwa umeweza kujitetea kihivyo,..kwa hayo yaliyotokea, nataka uniambie ukweli, ..ukweli ndio utanifanya na mimi nitulize moyo wangu, nataka unijibu bila kuogopa, …je mume wangu amekuwa akikufanyia hivyo mara ngapi…?’ akauliza na kijana akataka kuingilia lakini mama yake akamuashiria anyamaze.



    ‘Kunifanyia hivyo kw vipi, sijakuelewa mama..?’ nikauliza nikimuangalia huyo mama naye akawa kanikazia macho, na kwa hali hiyo mimi nikatizama chini.



    ‘Nilimkuta anakuwekea mdomo wake kwenye mdomo wako….unaelewa ni nini maana yake hiyo, unieleze hayo anakufanyia, hivyo ….je ni mara ya ngapi kakufanyia hivyo…?’akasema na mimi nikashtuka na kusema;



    ‘Kwanini afanye hivyo,…mama, mimi sijui unachoongea, kwanini afanye hivyo, hata sielewi…mimi nilipozindukana nilimkuta baba kachuchumaa, kaniinamia, kama vile yupo juu yangu, akiwa hivyo, kwa haraka nilipozindukana,,..nilijua anataka kunifanyia kitu kibaya, ndio maana nikaanza kupiga ukelele na kukimbia…’nikasema.



    ‘Kwahiyo yote aliyokufanyia baba yako hukuyaona, unataka kunidanganya eeh?’ akaniuliza.



    ‘Kwani alinifanyia nini..mama mimi sijui hayo unayoyaongea, ..sikumuona akinifanyia hivyo, maana wakati nadondoka humo ndani nilikuwa peke yangu, hata sijui huyo baba alikuja saa ngapi…’ nikasema sasa nikiwa na hamu ya kutaka kujua.



    ‘Wewe…unajifanya hujui, nakuuliza ni mara ngapi kawahi kukufanyia hivyo, au vitendo kama hivyo…wewe sio mtoto mdogo utake nikuffanulie kila kitu, haya labda nisema, kakulazimisha hivyo, mara ngapi, ….?’ Akauliza.



    ‘Mama kwakweli sijui unachotaka kukisema, kama ni hivyo, kupoteza fahamu, na labda, mimi sijui kama alifanya nini, ..sijawahi kufikia hatua hiyo, …ni huo mshutuko ulionifanya nidondoke na kupoteza fahamu….sijua lolote baadae mpak niliposhituka na kumkuta hivyo…’nikatulia nikisita kuelezea tukio lile lililopita.



    ‘Nakuuliza tena, maana isije ikatokea tatizo ukajuta, ..mimi ni mtu mnzima, nawafahamu sana wanaume, leo na au kesho kutwa, nije kusikia kuwa una mimba, nakuapia, utatoka humu ndani ukiwa huna sura, nitakurarua, mpaka unijue kuwa mimi ni nani…’akasema kwa hasira.



    ‘Mimba !!!...mama mimba itoke wapi….mimi siwezi kufanya kitu kama hicho…, kwa vipi mama,..mimi sijui kitu,….mama mimi sijui hayo mambo…sijawhi na sitaki kujihusisha na mambo hayo , mama alinikataza kabisa…’nikasema na akanisogelea kama kuninong’onezea kitu ili kijana wake asisikie…, akaniuliza jambo, sikumsikia vyema, au sikumuelewa alikuwa na maana gani, lakini nikahisi tu, na kusema;



    ‘Mama mimi hayo siyafahamu kabisa,…mama alinikanya sana kufanya urafiki na wanaume, hayo unayoyaongelea kwangu ni mageni kabisa siyajui mama…’nikasema.



     Mama akaniangalia machoni kwa makini kama ananipa kuwa kweli niliyosema ni sahihi au najaribu kumuhadaa, halafu akasema;

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Sawa…ila nakuonya tena na tena, huo mwili na kupendeza usije kukudanganya, watakuambia wewe ni mnzuri, unapendeza na mambo kama hayo…..watafikia hata kukupatia zawadi,.. na ujanja wa wanaume, ili kukufanya ujione wana kupenda, wengi wao huanzia kwenye kukupa zawadi,….’akasema



    ‘Mama mimi sijachukua zawadi ya mtu yoyote, wakinipa huwa nakataa…’nikasema.



    ‘Na hiyo zawadi aliyokuletea mume wangu ilikuwa ni ya nini, kama sio mlishaanza urafiki…’akasema.



    ‘Zawadi gani mama, baba hajawahi kunipa zawadi nikiwa peke yangu, mara nyingi akileta zawadi, anakupa wewe ndio unanpa mimi,…kweli si kweli…?’nikasema na kumuuliza.



     Mama akahema kidogo, halafu akageuka kumuangalia kijana wake, kuna kitu alitaka kuniuliza lakini kuwepo kwa kijana wake, akashindwa kuongea, akaniangalia na kusema;



    ‘Haya mimi nakuambia tu…usije kudanganyika ukaingilia ndoa za watu, usije kudanganyika ukaanza mapenzi na kijana wangu, huyu kijana wangu, sio hadhi yako, usije kukudanganya kuwa anaweza kukuoa, hilo halipo na sitakukubalia hata siku moja, na…. usije kudanganyika ukaanza umalaya huko nje, ukaniletea mimba humu ndani au magonjwa, ukumbuke hayo, usije kunilaumu na kuniona mbaya,..’akasema.



    Mimi nikakaa kimia, aliponiona sisemi kitu akasema;



    ‘Nikuambie ili kama angalizo, kuanzia sasa hivi,  nitakuchunguza hatua kwa hatua, ole wako, unasikia ole-wako, nije kugundua kuwa kuna kitu kinachoendelea kati yako wewe na mume wangu au kijana wangu….’akasema kwa hasira.



    ‘Mama mimi naomba niondoke humu ndani, haya ya humu ndani siyawezi,…kwani yaonekana wewe huniamini tena…, nilijua nyie ni kama wazazi wangu, sasa nageukwa,…’nikasema.



    ‘Uondoke , uende wapi… na ni nani anakugeuka, unaona kauli yako, nahisi kuna kitu unanificha, sema ukweli, nikusaidie, je kuna lolote kakufanyia mume wangu..?’ akaniuliza



    ‘Hapana, mimi naona ni bora nirudi kwetu kijijini…’nikasema



    ‘Hahaha, eti urudi kwenu kijijini, wenzako huko wanapakimbia, wanakuja huku , wengine wanatafuta sehemu ya kwenda wewe..unataka kwenda huko , sawa kama unataka kurudi kwenu kijijini, mimi nitakupatia nauli yako uende, lakini ukiondoka hapa ndio bye bye…waulize waliokuwepo hapa mimi sina muda wa kubembeleza mtu,…’akasema



    ‘Kwanza usiku mimi silali…nateseka na …sijui kuna nini humu ndani…’nikasema na hapo akashtuka na kusema



    ‘Kuna nini kinatokea usiku…haya anza kuongea maana nilikuwa nasubiria hilo, usiku unaona kitu gani, kunatokea nini..?’ akauliza na mara kukasikika mngurumo wa gari, mume wa huyo mama alikuwa karudi na wageni, ..



    ‘Nona kuna wageni, tutaliongelea hilo baadae…nataka uje kunielezee vizuri kabisa, …kwasababu kuna mwenzako alikuwa akiishi humu ndani kabla yako, alivumisha mambo mabaya sana, eti humu ndani kuna mashetani, hayo mashetani aliyaleta yeye, mbona sisi hatuyaoni hayo mashetani, acheni mambo ya kishirikina….sasa jiandae kuniambia ukweli wote …’akasema akigeuka kuondoka.



    Alipoondoka, kijana wake akasema;



    ‘Kwanini umemuambia hayo mama yangu..?’ akauliza



    ‘Kwasababu ndio ukweli ulivyo, mimi usiku nateseka, silali, kwanini nisimuambie…’nikasema



    ‘Una uhakika kuwa kweli kuna mashetani humu ndani, mbona mimi sijawahi kuyasikia hayo mahetani …yapoje,…., au kunitokea nini…halafu kwanini iwe ni wewe, na huyo mwenzako aliyekuja leo na kuondoka…msitake kuwachanganya wazazi wangu…’akasema.



    ‘Mimi hayo siyajui kwasababu nimeanza kuyapatia hapa,…sijawahi kusikia hivyo nikiwa huko kwetu kijijini,…’nikasema.



    ‘Unasikia,….uwe makini na kauli zako, mama ni mjanja sana, anatafuta njia ya kumuona baba ana makosa, nina uhakika kuwa baba hana makosa mimi namfahamu sana baba yangu, na ikithibiti kuwa kuna kitu kinahusiana na baba, na mama akasikia kutoka kwako,…utavuruga ndoa yao,…na hapo hutapata mtetezi tena, baba ndiye mtetezi wako, na alipanga mambo mengi ya kukusaidia, …’akasema



    ‘Kwahiyo wewe ulitakaje,…kuwa mimi nikae kimia huku napata shida, ….hapana mimi nitasema ukweli, hata kama ukweli huo utaniumiza mimi,lakini siwezi kudanganya…’nikasema.



    ‘Mbona hujamuambia mama kuhusu hicho kijitabu cha huyo mdada, kama kweli wewe ni mkweli…, au kuhusu huyo mdada aliyekuja kuchukua mizigo yake, alikuambia nini..?’ akaniuliza.



    ‘Alinisimulia alivyopata taabu, akiwa humu ndani, mpaka akaamua kuondoka…’nikasema



    ‘Hivyo tu…?’ akaniuliza



    ‘Ndio, na kwanini na wewe unayaingilia haya, au na wewe una kitu kinakuhusu…?’ nikamuuliza



    ‘Mimi najaribu kukusaidia wewe, na kuisadia familia yangu, siwezi kunyamaza kama kuna tatizo linaigusa familia yangu, hao ni wazazi wangu, sitafurahi wakikosana, na mimi nimekuwa nikikusaidia hata wewe…tangia ufike hapa,mengine ..ya..ya… kukuomba urafiki ni kawaida tu, …wala usije kunifikiria vibaya…’akasema.



    ‘Ulisema utafanya juu chini mpaka unipate, nakumbuka sana kauli yako hiyo, nakutilia mashaka na kauli hiyo…’nikasema



    ‘Unanitilia mashaka, kwa nini unitilie mashaka, …najua huyo mdada kakuhadaa kwa maneno yake ya uwongo,….’akasema



    ‘Maneno gani ya uwongo….?’ Nikauliza.



    ‘Hayo, tuyaache kwasasa,… muhimu ni hali hii inayoendelea hapa, ni bora uwe makini na unachokiongea, ukiongea jambo la kumfitinisha baba, ukasababisha wao wakosane na mama. …sijui …na hata hivyo, huyo mdada alichokuambia, mimi simuamini, ..kuna mambo yake mengi alikuwa kiyafanya, na sikuwahi kuwaambia wazazi wangu, maana niliona hayana maana…’akasema



    ‘Kama mambo gani..?’ nikamuuliza.



    ‘Huyu mdada ni mshirikina..uwe makini sana na kauli zake, ukimuendekeza atakuharibu, na ukiishirikiana naye, ….utakuja kuingia kusipofaa, na mama atakugundua tu,………..’akasema.



    ‘Mimi sijui hayo, mimi nazungumzia hayo yanayotokea kwangu, na ambayo kumbe yalitokea na kwake, kwanini yanitokee hivyo kila siku kukabwa, kusumbuliwa, sipati usingizi….na yeye aliniambia hali ilikuw ahivyo hivyo, je hayo ni mambo ya kishirikina…?’nikasema.



    ‘Mimi nikushauri jambo…’akasema na mara baba na mama wakafika, na tukakatiza mazungumzo, na baba akasema;



    ‘Ni bora tukayaongelee chumba cha maongezi…sio huku chumbani…’akasema baba na kuondoka na mama akaingia na kusema;



    ‘Haya, sasa jiandae uje kuna maongezi, nataka uje uelezee kila kitu, ukinificha, basi shauri lako, ..yatakayokutokea usije kunilaumu..mimi nawafahamu sana hawa wanaume, ..unanisikia, mimi nataka nikusaidie wewe haya yasije kutokea tena…unanielewa…, kwahiyo sema kila kitu kinachotokea humu ndani, na kama uliwahi kufanyiwa jambo lolote na mume wangu, uliongee, huu ndio wakati wako…’akasema na kuondoka kumfuata mume wake.



    Na kabla sijaondoka kijana akaja ka haraka, akionyesha kuwa ana jambo anataka kuniambia, lakini kabla hajaanza kuongea mara mzee mwenyewe akatokea, na kwa nyuma yake nikamuona mama akiwa kasimama,...

    .

    NB: Haya mambo ya familia hayo, ngoja tuone itakuwaje kwenye hicho kikao cha familia.





    WAZO LA LEO: Matatizo yakitokea kukawa na msigishano, uwe wa wanandoa au uwe wa viongozi au ujirani nk… hekima na busara ni kila mmoja kukubali kushuka, na kukubali kukaa mezani na kuongea, ili muweze kujadili yale yenye sintofahamu. Kiubinadamu, tabia hutofautiana, kutokana na hisia na utashi wa kufikiri, na usipokubali kuwa kuna utofauti huo, utashindwa kushirikiana na mwenzako au kuvumiliana kwenye mambo ya kila siku. Hala hala, ili kuondoka mgongano, jambo jema ni kukubali kukaa na kuongea kwa kusikilizana, kila mmoja atoe duku duku lake, ili mwisho wake kuje kupatikana suluhu..Suluhu hujengwa kwa maridhiano, sio ubabe





    ‘Haya, sasa jiandae uje kuna maongezi, nataka uje uelezee kila kitu, ukinificha, basi shauri lako, ..yatakayokutokea usije kunilaumu..mimi nawafahamu sana hawa wanaume, ..unanisikia, mimi nataka nikusaidie wewe haya yasije kutokea tena…unanielewa…, kwahiyo sema kila kitu kinachotokea humu ndani, na kama uliwahi kufanyiwa jambo lolote na mume wangu, uliongee, huu ndio wakati wako…’



    Hiyo ilikuwa kauli ya mama mwenye nyumba



    .Unasikia,….uwe makini na kauli zako, mama ni mjanja sana, anatafuta njia ya kumuona baba ana makosa, nina uhakika kuwa baba hana makosa mimi namfahamu sana baba yangu, na ikithibiti kuwa kuna kitu kinahusiana na baba, na mama akasikia kutoka kwako,…utavuruga ndoa yao,…na hapo hutapata mtetezi tena, baba ndiye mtetezi wako, na alipanga mambo mengi ya kukusaidia....'alinionya huyo kijana



    Niliwazia hayo...na kunifanya niwe njia panda...



    Tuendelee na kisa chetu...





    ****************



     Nilifika kwenye hicho kikao nilichoitiwa, nilijua labda ni hao wanandoa wawili na mimi mwenyewe, lakini humo nikawakuta wazee wawili,….niliambiwa mmoja ni mzazi wa baba na mwingine ni baba mkubwa wa mama, wenye nyumba.



     Baadae yule kijana alikuja…kama nilivyosema huyu alikuwa na umri karibu sawa na mimi,kama kanizidi mimi ni kidogo tu…huyo kijana alipoingia, kwanza aliwatupia macho hao wazee, halafu akanigeukia mimi na kuniangalia kwa mashaka, kama ananionya kuhusu jambo fulani, mimi sikumjali, dhamira yangu ilikuwa kusema ukweli tu, sikutaka kudanganya tena, ila kwa mbali akilini nikawa nakumbuka onyo la huyu kijana..



    ‘….na uwe makini na kauli zako, mama ni mjanja sana, anatafuta njia ya kumuona baba ana makosa, nina uhakika kuwa baba hana makosa mimi namfahamu sana baba yangu, na ikithibiti kuwa kuna kitu kinahusiana na baba, na mama akasikia kutoka kwako,…utavuruga ndoa yao,…na hapo hutapata mtetezi tena, baba ndiye mtetezi wako, na alipanga mambo mengi ya kukusaidia…’

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilijiuliza kwanini huyo mama anatafuta makosa ya mumewe, ili ndoa ivunjike…au sikumuelewa vyema huyo kijana, ….na kwanini ukweli wangu uje uvunje hiyo ndoa, sasa nifanyeje, niseme ukweli au nikae kimia, na je ikijulikana kuwa mimi nasema uwongo,….hapana, mimi nitafuta ushauri wa mama yangu, mama yangu wakati wote aliniusia kuwa mkweli…hata kama ukweli huo utaniumiza.



    Nilisalimia kwa adabu halafu nikaambiwa nikae , nilikaa sehemu ambayo naangaliana uso kwa uso na huyo kijana, nilimuona akinitupia jicho la aina yake, na mara nyingi alikuwa kainamisha kichwa chini.



    ' Haya tuambieni mlichotuitia…’alianza mzee mmojawapo., na baba mwenye nyumba ndiye akaanza kuongea;



    'Wazee wangu, samahani sana, imebidi niwaite,..nilishawaita kabla lakini tukaweza kuyamaliza wenyewe, ila hili la sasa limeshindikana…nikaona ni bora, niwasumbue…lakini hata hivyo, nyie ni wazazi wangu, mara nyingi matatizo ya kifamilia yakifikia hatua mbaya, ni lazima tuyafikishe kwenu kuliko kukimbilia mahakamani kwanza….ili muweze kutusaidia…’akaanza kuongea na wale wazee wakatikisa kichwa kukubaliana, lakini hawakusema neno.



    ‘Wazee wangu ndoo yangu imeingiliwa na matatizo….’akasema na kumtupia mkewe jicho, mkewe alikuwa kaangalia pembeni.



     'Sawa, kuna tatizo gani…tuambie…’akasema mzee.



     ' Mke wangu haniamini, kafikia kunishuku ugoni, na hata kunitaka tuachane, kwasababu za kunishuku tu, hana ushahidi, maana sio kweli kwa hayo anayonishuku nayo….’akasema.



     'Hilo tu…?’ mzee akauliza na baba mwenye nyumba akamuangalia huyo mzee kwa macho ya kushangaa, na kutahayari, akasema;



     ' Wazee, hilo mwaliona ni dogo, ..jamani, mpka nimeamua kwuaita mjue kuwa mimi nimeshindwa kumshawsihi mke wangu, kang’ang’ania kuwa tuachane….na kuachana huko anataka mimi niondoke kwenye hii nyumba…’akasema.



    'Mimi nimeuliza kama kuna nyongeza ya hilo,nikitaka ufafanuzi zaidi, sina maana ya kuliona hilo jambo kama jambo dogo, udogo wake na ukubwa wake, unategemeana na maelezo yenu, maana hata sisi tumepitia huko…’akasema mzee.



    'Mengine ya ziada ni kiwa mke wangu kwa hivi sasa haniheshimu kama mume wake, amekuwa akitafuta mwanya wa kunichafulia heshima yangu….na kunidharau, sawa, mimi..labda kwa vile hii nyumba tumepewa na wazazi wake, ..lakini tulikubaliana na wazee wakaridha kuwa hii ni nyumba yetu sote, sikulipinga hilo nikijua haya ni maisha yetu ya mume na mke…’akasema.



    'Labda tuanza kulidodosa hili jambo, maana naona utakimbilia kutoa maelezo mengine ambayo hayayaweza kuleta suluhu, nikuulize kisa hasa nini nini..ndio huko kukushuku, kwanini akushuku, kuna tukio lilitokea, au …?’ akauliza.



     'Labda tumuulize yeye ambaye ananishuku mimi….’akasema baba mwenye nyumba, na mzee akasema;.



     'Kabla ya kumuuliza yeye…sisi kwanza tunataka tukukabili wewe baba mwenye nyumba, na kwa vile wewe ndiye umefikia kutuita sisi, yeye, atakuja kuulizwa, lakini kwanza tunataka kusikia kutoka kwako wewe, kichwa cha familia..swali  je ni kweli, kuhusu shutuma hizo…?’ akaulizwa.



    'Sio kweli wazee wangu, ndio maana nikaziita shutuma, ni hisia tu, na sijui kwanini anafikia kunishuku hivyo….’akasema.



     'Je mke wako kwa bahati mbaya, aliwahi kukufumania ukiwa na mwanamke mwingine…?’ akaulizwa na akamuangalia huyo mzee kwa uso wa kujiuliza ni kama vile anahisi mzee anamkandamiza, lakini huyo ni baba yake mwenyewe.



     'Hapana,..hiyo haijawahi kutokea,…ndio maana nashindwa kumuelewa…’akasema.



     'Sasa ilitokeaje mpaka akafikia kukushuku…maana yeye sio mtoto mdogo, kuna sababu kakuambia, au hamjawahi kuliongelea hilo…nakuuliza hili nikiwa na maana mpaka, wanandoa wanafikia hatua ya kuwaita wazee, ni lazima wameliongea, wakazozana, wakawa hawaweze kuafikiana, na katika kuzozana huko ni lazima mwenzako atakuwa kakuambia …na hata kukutokea ushahidi wake, au sio mzee mwenzangu…?’ akasema huyo mzee.



    Mzee mwenzake, akatikisa kichwa kukubaliana na maneno hayo.



     'Kuna matukio yalitokea, yeye akanihisi vibaya, lakini kiukweli sivyo hivyo kama ilivyoonekana…’akasema.

    'Ilikuwaje..tuambie, maana kama mumetuita, basi tunahitajia ukweli wote…’akasema huyo mzee.



    'Kwa tukio la hivi karibuni ambalo limevuka mpaka,…mimi nilirudi nyumbani na kumkuta mdada wa kazi akiwa kapoteza fahamu….’akasema na sasa aliyeuliza ni huyu mzee mwingine.



    'Kapoteza fahamu…!!, kwa vipi…hebu tuelezee hapo…’akasema huyo mzee mwingine.



    'Nilimkuta kalala sakafuni akiwa hajitambui, …akiwa kapoteza fahamu….’akasema.



    'Oh, kwanini awe hivyo, labda mnajua sababu yake, na je hiyo ni ara ya kwanza kwa tukio kama hilo..?’ akaulizwa.



     'Mhh, kuna kipindi ilitokea hivyo, na aliyekuwepo, na kumuona ni mke wangu, na wakawahi kumpeleka hospitalini….’akasema.



     'Kwani huyo bint ana tatizo gani hasa…?’ akauliza.



     'Hicho kipindi alipodondoka, na kupelekwa hospitalini walimpima na wakagundua kuwa aalikuwa na malaria,ana malaria hiyo ilikuwa imepanda kichwani….’akasema.



    ‘Kwahiyo wewe ulipomkuta kapoteza fahamu hukutaka kumpeleka hospitalini au…?’ akaulizwa



     'Kwanza ukimkuta mtu kapoteza fahamu si unatakiwa umkague, na kumpa huduma ya kwanza, si ndio hivyo wazee wangu…’akasema.



    ‘Kwahiyo wewe uliamua kumkagua kwanza kama ulivyosema awali….na ulipomkagua ukaona haina haja ya kumpeleka hospitalini au ulifanyaje..?’ akaulizwa.



     'Nilimkagua ndio nikahakikisha kuwa kapoteza fahamu…na ndio nikaanza kumpatia huduma ya kwanza…’akasema.



     'Ulifanyaje…?’ akaulizwa, wazee hawa ni wasomi, kwahiyo maswali yao yalikuwa ya ujanja ujanja, jamaa wakati mwingine aliona kama wazee hawa na wao wanamshuku vibaya, hata hivyo aliendelea kuwajibu bila kukasirika.



    ‘Kwanza nilimlegeza khanga aliyokuwa kajitanda mwilini….’akasema.



    ‘Kwanga, kwanza alivaaje, maana ukisema khanga, …..ok, alivaaje,…?’ akaulizwa.



     'Mhh,… alikuwa kafunga khanga moja, ile unafungwa shingoni, na kufunika mwili mnzima.



    'Kwanini akawa kavaa hivyo, ina maana alivaa khanga moja tu, …bila kitu kingine, ndio kawaida yake au…?’ akauliza huyo mzee kwa mashaka.



     'Hilo la kwanini, mimi siwezi kujua, labda atajieleza yeye mwenyewe….’akasema akimtupia mke wake macho, hakumuangalia huyo binti.



     'Kwahiyo wewe ulifanyaje….ulipomkuta huyo binti kapoteza fahamu baada ya kumkagua…?’ akauliza mzee.



    ‘Ina maana mnataka niongee kila kitu, mengine naona kama hayana umuhimu ….’akalalamika



    ‘Kijana, mwaneti, sisi ni wazee wako, tuna maana kubwa ya kukuuliza haya, fununu za hayo yanaytokea humu ndani tumeyasikia sana tukayapuuzia, sasa tunataka uyajibu maswali yetu, …kwani kuna ubaya ukituelezea…?’ akaulizwa.



     'Kwasababu alikuwa kapoteza fahamu, muhimu nijuavyo mimi ukimkuta mtu wa namna hiyo cha kwanza ni kumlegeza nguo alizovaa, kama zinambana, kabla ya kumfanyia huduma ya kwanza….’akasema.



     'Umesema huyo binti alikuwa kavaa khanga moja, na khanga tujuavyo sisi ni nguo nyepesi sana, je ilikuwa inambana, …..?’ akaulizwa.



     'Ndio kwasababu, ile kanga alikuwa kaifunga shingoni, huoni itakuwa imekaza mishipa ya damu shingoni..’akasema.



     'Haya,bwana, halafu..ukaifungua shingoni, na kumuacha uchi au…?’ akauliza na hapo akacheka ile yakuonyesha anakerwa na hayo maswali.



    ‘Hakubalia uchi, ililegea kwenye ule mkunjoa wa kufungwa shingoni,…..’akasema



    ‘Kwahiyo ukamaliza au ulifanya nini tena…?’ akaulizwa



     'Nikamminya kifuani, mara moja, …mbili….na tatu…ili kurudisha mapigo yake ya moyo…’akasema



    'Ok, huo ni utaalamu, unajua wewe,….hebu tukuulize tu, huo utaalamu wewe ulijifunza wapi..?’ akaulizwa



     'Huduma ya kwanza, nilijifunza chuoni…tunafundishwa, hata vitabuni ipo, kwenye mitandao ipo, ni kitu cha kawaida tu….’akasema.



     'Kifuani kulikuwa wazi…maana mfano khanga ikifningwa hivi, ukaifungua huku singoni, si inaacha kifua wazi, na kwa vile alikuwa hajavaa nguo nyingine ni …..atabakiwa huku wazi, au sio…?’ akauliza mzee.



     'Mzee hakubakia wazi, alikuwa kavaa khanga..kanga ilimfunika….’akasema.



     'Khanga tu, hakuvaa sidiria…hata sidiria….’akasema mzee.



    'Wazee, mbona mnauliza maswali hayo…mimi sioni kama yatasaidia….’akalalamika.



     'Mwanetu, sisi sio watoto wadogo, tunakudodosa tujue ukweli ulivyo, huyo ni mdada, mwili wake wote unatia hamasa kwa mwanaume, katika maelezo yako hatukusikia neno, kuogopa kumgusa,  nay eye kuna maelezo alimuelezea mama yake,…je hukumguza zaidi ya kumminya kifuani mara tatu, maana labda tutasema aliota…’akasema huyo mzee, na jamaa akamtupia mkewe jicho, lenye kuonyesha chuki fulani.

     'Mzee, huyu ni sawa na bint yangu, namuona kama mtoto wangu, na kwa hali niliyomkuta nayo, nisingeliweza kuwa na mawazo kama hayo mabaya…sijui kawaambia nini, au mke wangu kawaambia nini,…lakini mimi nilifanya kile kilichokuwa ni sahihi….’akasema sasa kwa ukali kidogo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     'Je ungemkuta yupo kwenye hali tofauti, ungefanyaje..labda kavaa kahanga moja kama hivyo, kama hujawahi, maana kama alivaa hivyo, yaonyesha ni kawaida,…au sio, …?’ akaulizwa.



    'Mimi kama mzazi, ningelimkemea kuwa haifai kuvaa hivyo, na mimi sijawahi kumuona akiwa kavaa hivyo kabla….’akasema.



     'Je ni mara ya ngapi umemkuta,akiwa katika hali kama hiyo…..?’ akaulizwa

     'Una maana gani mzee, unajua wazee, mimi huwa natoka asubuh, narudi usiku, huwa nipo nyumbani siku za wikiendi tu na mara nyingi, siku kama hizo, mke wangu yupo….’akasema.



    ‘ Ni mara ngapi...hivi umeelewa swali..?’ akaulizwa.



     'Sikuweza kujua hilo, kifupi, sijawahi kumuona akiwa katika hali hiyo kabla…, hiyo ni mara ya kwanza kwangu akasema na mkewe alionekana kutikisa kichwa kama kusikitika kuashiria kuwa mumewe anadanganya..

     'Una uhakika na hilo, je ukitolewa ushahidi kuwa hiyo sio mara ya kwanza kumuona hivyo utasemaje..?’ akaulizwa

     'Mzee…..’akataka kulalamika na mzee hakumpa nafasi, akamuuliza.



    'Hilo tuliache, nikuulize, japokuwa hili ni swali la nyie wote wawili, ni kwanini ulimkuta huyo binti huko chumbani kwenu…?’ akaulizwa, na kwanza akamtupia mkewe jicho, kama kutaka kumlaumu lakini akaona mkewe hamuangalii, akasema;



     'Labda alikuwa anafanya usafi…’akasema



    ‘Labda, huna uhakika…kwahiyo yeye huwa anafanya usafi hadi chumbani kwenu, anatandikia, ana…panga nguo zenu,..si ndio hivyo…?’ akaulizwa.



     'Mzee kwani hapo kuna ubaya gani, huyo ni kama binti yangu tu, yupo makamo sawa na huyu kijana hapa..kwahiyo hata akiingia akafanya usafi, kwangu mimi sioni kuwa ni tatizo…..’akasema.



    'Hahaha,…mwanetu…. eti unasema nini,…kuwa hilo sio taizo, labda niseme kwangu mimi na uzee wangu huu, na kwa mila na desturi, na…hata ukiangalia, kiuhalisia, na kiubinadamu , hilo kwangu ni tatizo, huwezi kumruhusa mfanyakazi wa ndani, kufanya usafi hadi chumbani kwenu, huko ni sehemu ya siri kati yenu wawili, hamjafundishwa hilo jamani, mtasema mnaishi kidhungu au sio…mwanetu, hilo ni kosa, …sisubirii kulisema huko mwishoni..hilo ni kosa..na adhabu yake ndio hiyo…’akasema.



     'Mzee..adhabu gani…?’ akauliza.



    'Msijitetee, mambo mengine mnajitakia nyie wenyewe..mimi hilo naliwekea alama ya kuuliza, nyie wananda mna matatizo, kama mumeiga,, kama mlifanya hivyo, kwa vile mnamuona huyo ni sawa na binti yenu,…lakini sio binti yenu huyo ndio maana hayo mengine yalitokea,….’akasema mzee



    ‘Mengine yapi mzee…?’ akauliza sasa akionyesha mashaka.



    ‘Mzee mwenzangu unasemaje kuhusu, wewe unona ni kawaida kumruhusu binti wa ndani afanye usafi ndani, chumbani, atandike,…na kuvaa kwenyewe ndio huko…hivi kweli mna akili nyie…’mzee akasema kwa hasira.



     'Mhh, hata mimi najiuliza, labda ndio usasa huo…na madhara yake ndio hayo, na watu hawataki kujifunza, wanaiga tu,….kiukweli sio sahihi, …’akasema mzee mwenzake.



     'Haya ulipomshika kifuani, ukakandamiza , mara tatu, halafu ikawaje…?’ akauliza huyo mzee sasa akicheka.



    'Mzee naona mnielewe, kama hili mwalichukulia mzaha, mimi ….’akasema



    ‘Mwanetu, hatukuja kupoteza muda hapa, sisi tunataka kuwaonyesha madhaifu yenu, ili mjifunze, msione sisi wazee tulikuwa tunafanya hivyo, tunayajua hayo sana, binadamu ni mdhaifu, nafsi ni kitu kingine,..msiige tu bila kujua madahara yake…..’akasema huyo



    ‘Haya atujibu Sali letu, hapa sasa mpo mahakamani, mnatakiwa mjibu maswali kama yanavyoulizwa, sisi ni wazazi, hata kama mumezaa mna watoto wakubwa, lakini mkiwa mbele yetu, nyie ni watoto tu…’akasema huyo mzee.



    ‘Hakuzindukana…’akasema sasa akiwa katahayari.



     'Ukafanyaje ulipoona hakuzindukana…?’ akaulizwa.



    'Mzee, kuna huduma ya kumpuliza mdomoni..kama hiyo ya kifuani haikufanya kazi….’akasema

    'Ehee..haya makubwa hayo, ya mdomoni...!!..’akasema huyo mzee, wazee hawa wawili wakaangaliana.



    'Ndio mzee, kwahiyo hayo si yanajulikana jamani….’akasema

    'Kwahiyo ukaifanya hiyo, au sio…?’ akaulizwa.



    'Hapana mzee..sikufanikiwa kuifanya….wakati najiandaa kuifanya hiyo, ndio mke wangu akatokea,…..’akasema kwa sauti ya kunywea kidogo.



    ‘Ukaacha kuifanya hiyo huduma, kwanini sasa….?’ Akaulizwa



    'Ndio nikaacha kwasababu….’hakumalizia.



    'Kwanini uliacha na wewe ulikuwa ukimuhudumia mgonjwa, hebu nikuulize docta akamuhudumia mgonjwa, je akitokea docta mwenzake ataicha hiyo kazi, kwa vile mwenzake katokea…?’ akaulizwa.



     'Nilisita,kwa jinsi mke wangu alivyoniangalia, macho yake yalionyesha kuhisi vibaya, yalimtoka kama vile kani..’akasita kumalizia.



    'Malizia..hilo neno ni muhimu sana tukalisikia…’akaambiwa.



    'Ni kama kaona kitu cha kutisha vile….na mimi nikashikwa na mshangao, kwanini ananiangalia hivyo….’akasema



    "Ni kama vile kakufumania au sio...?" akasema huyo mzee



    'Nahisi hivyo..lakini sio kweli….’akasema



    'Kwanini akuhisi hivyo, kwani alikukutaje, ulikuwaje, wakati unafanya hayo…?’ akaulizwa



     'Mimi Sijui kwanini alionekana kuniangalia hivyo, na hakunipa nafasi ya kujieleza…’akasema



    'Hebu nikuulize wakati unamfanyia huyo mdada huyo huduma ulikuwa umekaaje…?’ akaulizwa



     'Mzee kwa vyovyote nitakuwa nimepiga magoti, nimemuinamia….ningafanyaje ..?’ akaulizwa



    ‘Kwanini ulivua shati, …?’ akaulizwa na hapo akashtuka.



    ‘Mzee hapo ni chumbani kwangu,….nilipofika nilivua shati, nilihisi joto, na nilitaka nibadili nichukue jingine nilivua hilo hata kabla sijajua kuwa kuna mtu humo ndani…..’akasema.



    ‘Una uhakika kuwa ulimshika kufuani, tu ukambinya mara tatu tu….maana ukumbuke hilo tendo, hukulifanya ukiwa peke yako, kuna watu walikuona, na mtendewa mwenyewe …unajua..mwanetu, humu ndani kuna tatizo,….mna mataizo makubwa, mpaka sisi tunakubali kufika hapa, mjue kuna tatizo, na sio wajinga sisi kukuuliza maswali kama hayo….sasa kabla hatujaanza kumuhoji mkeo, ..kabla hatujaanza kumuuliza binti, na kabla hatujawaleta mashahidi kuwa..hapa ndani kuna tatizo, nakupa nafasi ya mwisho.



    ‘Mzee, unataka kusema nini, kuwa mimi …’



    ‘Mimi ni baba yako, nimekuzaa mwenyewe, na haya yaliyotokea humu ndani yalilifika hadi kwangu, awali nilikutetea sana maana sivyo nilivyokulea hivyo , na sikuamini nilipoambiwa hayo, nikataka kutafuta ushahidi, na..nimekuhoji maswali hayo nikiwa na maana…kijana, mimi ni baba yako nimemuangukia mzee mwenzangu ili haya yaishe,..lakini yataishaje kama hujauangama…ukakiri kosa yakaisha…



    ‘Baba….’akawa kakasirika sasa.



    ‘Nataka wewe ukiri ukweli, useme ukweli haya yaishe, mwenzako kasema ukikiri ukweli, yupo tayati kukusamehe, lakini kama utaendelea kuwa mkaidi, na wakati unajua ulitenda kosa, na yaliyashatendeka awali akakusamehe, …sasa ni mara ya pili…mimi nitanawa mikono, nimekudhamini kuwa wewe utasema ukweli na kukiri kosa, sasa nakupatia nafsi hiyo ya mwisho kabla hatujamuuliza bint ambaye ndiye mtendewa, najua ataelezea yote yaliyowahi kumtokea, na hilo, ulipojifanya unamfanyia huduma ya kwanza,..na kuna mashahidi wengine…..’akasema huyo mzee.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ‘Mwanetu, hebu fikiria hivi, wewe haupo duniani, una binti kama huyu, anafika kwenye nyumba za watu wanamfanyiwa mambo kama hayo..utajisikiaje…, hebu liweke akilini hivyo. Maana usiseme kwako haiwezi kutokea, mungu ni wajabu sana, wangapi walikuwa wanahali nzuri sana, lakini sasa wapo mitaani, wangapi walikuwa na hali nzuri, walipofariki, wakawaacha nyuma wanafamilia, wakaja kufirikisika hadi kufikia kuwa omba omba..hawa waliomba..hapana,…hii inaweza kumtokea yoyote, …liwazie sana hilo mwanangu…’akasema mzee



    ‘Kama unaona sio kweli, tutaanza kuitisha mashahidi…na hapo sijui utasemaje,…maana nimesikia mengi,..kuna binti alikuwa hapa awali, ilitokeaje,…utasema ni uzushi….ee , na huo ni uzushi…nakuuliza wewe….?  mwanangu ndivyo nilivyokulea hivyo, kuna tatizo gani….sasa ni muda wa kuniambia ukweli, kama umeniita hapa kuja kuikoa ndoa yako, sasa nahitajia ukweli, na…huyu binti wa watu apate haki yake, sipendi watu kama hawa wateseke, eti kwa vile masikini….je upo tayari kuusema ukweli…na …’akatulia.



    Baba mwenye nyumba akageuka kumuangalia kijana wake, halafu binti, kwa mara ya kwanza akamuangalia huyo binti,…sasa akiwa kakunja uso kwa hasira, baadae akainamisha kichwa chini, na alipoinua machozi yakawa yanamtoka…huku uso umejaa hasira.



    NB: Imebidi niliweke hili hivi…ili kufunua ukweli wa maisha katika familia.





    WAZO LA LEO: Ili uishi kwa amani,…jitahidi kuepuka,..kuweka visasi moyoni, kupenda kulalamika-lalamika, kulaumu wengine…, kufanya mambo kwa vile umefanyiwa, wewe fanya mema vile itakiwavyo bila kujali kuwa na wewe umefanyiwa au la…maana kufanya hivyo, kuna neema yake, kuliko kutokufanya, na ukifanya kwa vile umefanyiwa hiyo ni ria, na ria ni shrike ndogo,…wewe fanya ukijua ni wajibu wako, na Mola atakuzidishia baraka kwa kujitolea kwako kwa mema unayoyafanya.



     ‘Mwanetu, hebu fikiria hivi, wewe haupo duniani, una binti kama huyu, anafika kwenye nyumba za watu wanamfanyiwa mambo kama hayo..kiubinadamu utajisikiaje…, hebu liweke akilini mwako hivyo....'ilikua sauti ya mzee.



    'Kuna wengi walikuwa na uwezo wao, wakajua hali ngumu, na mitihani ya dunia haitaweza kuwafika, lakini ya mungu mengi sasa wapo mitaani! Wapo pia walikuwa na hali nzuri, mume akafariki, akawaacha watoto na mama yao huku duniani, wanafamilia hao wakaja kufirikisika hadi kufikia kuwa omba omba, na binti akafikia kwenda kuomba kazi za ndani, haya yapo hayapo....'akasema mzee, akimuangalia mzee mwenzake.



    'Yapo sana, na mifano kama hiyo ipo mingi tu....'akasema mzee mwenzake.



    'Unajua ukiwa na uwezo, nafsi hukudanganya, unaweza ukajawa na kiburi, na hata ukawadhulumu wengine, wakilalamika kwako na kukuomba, uwasaidie, unawadharau, na wengine wanafikia kumuomba mola wao, mbele ya wenye uwezo, na wenye uwezo kwa kiburi wanajibu, ..toka lini duwa la kuku likampata mwewe....'akasema mzee.



    'Ni kiburi kibaya sana hicho....'akasema mzee



    'Sasa mwanetu, tusipoteze muda, ubinadamu una madhaifu yake, na kukosa inatokea, na mwenye hekima akikosa huomba msamaha..umekosea, hata kama utajitetea vipi umekosea , sasa ni wajibu wako kuomba msamaha, hatutaki kujitetea, na kuongezea chuki zaidi, haina haja sasa gangeni yayajao,..na humu sasa mna mfanyakazi mwingine, yaliyotokea yametokea, yeye naye kama binadamu atakusamehe kama uliwahi kumfanyia lolote baya...



    'Mzee aliposema hivyo, baba mtu akamtupia jich huyo binti, binti alikuwa kainama chini, tu...



    'Sasa tuambie, upo tahari kwa hilo...na kulia ni dalili njema kuwa umekiri kosa, unajuta, na ujute basi na kauli yako, kututhibitishia kuwa kweli uliteleza...au sio...?' akasema mzee akimuangalia mzee mwenzake.....



    'Sawa tumalize tushikane mkono sisi tuondoke zetu...'akasema mzee mwingine.



    Tuendelee na kisa chetu.



    *****************





    Baba mwenye nyumba. alishika kichwa kwa mikono yote miwili akawa kaegemeza kichwa kwenye viganja vya mikono yake, ikachukua muda, akawa kama anawaza, na baadae akainua kichwa, na sasa akageuka kumuangalia kijana wake...



    Alimuangalia kijana wake kwa makini, na inaonyesha labda alikuwa akimuwazia kijana wake huyo huenda atakuwa miongoni mwa hao mashahidi wanaotakiwa kuelezea hicho kinachoendelea hapo nyumbani, yeye anamuamini sana kijana wake na mara nyingi yupo upande wake, lakini kwa namna nyingine hataki kumuumiza mama yake pia...., na huenda keshaongea na mama yake na amekubali kuelezea hayo anayoyafahamu yeye.



    ‘Mungu wangu, sijui itakuwaje…ni nini hiki, kwanini wananiandama hivi...’akasema kimoyo moyo.



    Sasa akageuka kumuangalia binti, tangia waingie hapo, alikuwa akikwepa sana kumuangalia huyo binti usoni,  sasa anawaza kumtafuta huyo shahidi akamtupia jicho kwa mara ya kwanza,…, akamgundua wanaangaliana na kijana wake, na baadae huyo binti akageuka na kuangaliana na baba mwenye nyumba, haraka baba mwenye nyumba akakwepesha macho yake, huku akiwa kakunja uso kwa hasira, alihisi huyu binti anaweza kusema neno ambalo litaiangamiza ndoa yake.



    Kilichomuumiza zaidi ni maneno ya baba yake pale aliposema, na kwa maswali aliyokuwa akiuliza alihis kuwa baba yake atakuwa kaamini kabisa hicho alichoambiwa kwa hayo yanayoendelea humo ndani, na kama ni hivyo, basi kwake yeye hana wa kumtetea, na mara akamkumuka yule binti aliyeondoka,…



    Binti huyo aliondoka, lakini akiwa kaacha doa kubwa kwenye familia yake, na hadi anaondoka ilisadikiwa kuwa yeye ndiye alimpachika mimba huyo binti, na mpaka ikafikia yeye kutafuta pesa kwa ajili ya kuitoa hiyo mimba mimba, na hapo ndio akakumbuka siku binti huyo alipofika kwake na kuanza kulia mbele yake.



    ‘Baba haya yote ni kwasababu yako, sasa nina mimba yako, na sijui nitafanya nini masikini wa mungu…’ aliambiwa.



    ‘Mimba, nani kakupa mimba?’ akauliza akionyesha uso wa mashaka.



    ‘Unasema nani kanipa mimba, ni wewe baba, umesahau yale yote, nikukanya lakini , ukajifanya huongei, na ukafanya upendavyo, sasa unaniuliza swali kama hilo….’akasema.



    ‘Wewe binti wewe una uhakika na unachokisema, nimesahau yale yote yapi, una wazimu wewe…?’ akasema kwa ukali, huku akiangalia huku na kule asije akatokea mkewe.



    ‘Baba,…kwanini unasema hivyo, mara ngapi umekuwa ukifika kitandani kwangu usiku tunalala wote, na matokea yake ndio haya…’akasema huyo binti.



    ‘Mimi, nahisi wewe umechanganyikiwa,…kwanza hebu toka nje, usiniletee kisirani humu ndani, kama umefanya umalaya wako huko nje, na sasa unatafuta sehemu ya kujitetea, sio mimi, na maneno yako haya inabidi nikufukuze kazi, naona huna nia njema na mimi…’akasema.



    ‘Unanifukuza kazi, wakati wewe ndiye umeniharibia maisha yangu…na kuapia kabla sijaondoka hapa nitahakikisha nimeongea na mama,..najua yeye ataniamini…kwasabau ipo siku nilimgusia, hakunisikiliza akasema atafanya uchunguzi,….’akasema.



    ‘Ulimgusia ukamuambia nini wewe, …uliongea naye kuhusu nini...kuwa mimi ndio nimekupa hiyo mimba, wewe binti wewe, unataka nini kwangu, sikiliza hata ukinisingizia, hutapata kitu, na …..’mzee akasikia mlango ukifunguliwa akajua ni mkewe.



    ‘Nilimuambia tabia yako, kuwa sikuamini na akaniuliza kwanini huniamini nikamwambia una tabia ya kuingia chumbani kwangu usiku, ..na kabla hatujaendelea kuongea, akatokea mgeni , tukakatiza mazungumzo,…kwahiyo usibishe, mimi na wewe tumekuwa tukifanya mausiano ya kujiiba, unabisha nini au kwa vile nina ujauzito wako,…’huyo bint alimuambia baba mwenye nyumba.



    ‘Mimi,… kwanini nifanye hivyo,…wewe binti wewe una nini lakini, unataka kufanya nini, nitakuharibu, kabla hujatimiza huo ushetani wako humu ndani, nimekuvumilia lakini hili sasa limevuka mpaka,..hebu toka mbele yangu….?’ Akauliza, na kusema kwa hasira.



    ‘Baba kwanini unanifanyia hivyo, angelikuwa binti yako ungelimfanyia hivyo, au kwa vile sisi ni masikini, mnatufanya mpendavyo,….na hata kama sisi ni masikini, ujue mungu anatuona…hii mimba ni ya kwako, na sitaondoka hapa mpaka kieleweke, umesikia, au niende polisi nikatoe taarifa…’akasema.



    Baba aliwaza sana, akajua hayo yakifika kwa mke wake, hataaminika, kwahiyo akatafuta njia nyingine, akili sasa ilishindwa kuwazia, zaidi, sasa akasema;



    ‘Wewe mimi sitaki huo uongo wako, sijui kwanini umefanya hivyo, nitakupatia pesa ukaitoe hiyo mimba, hata kama sio ya kwangu, na nakuapia baada ya hili sizani kama nitaweza kuishi na wewe humu ndani, utafute kazi sehemu nyingine uondoke, unasikia,…’akasema.



    ‘Kwanini niitoe hii mimba, unajua hatari yake wewe, au kwa vile….je nikifa, au nikiharibu kizazi changu, nataka unihakikishie jambo la kunilinda, kama lolote litatokea, basi uwajibike…?’ akauliza.



    ‘Kwani ni ya miezi mingapi hiyo mimba..?’ akaulizwa.



    ‘Mimi sijui ni ya miezi mingapi…nilianza kujisikia vibaya nikaamua, kwenda kupima, na nilipoona nina mimba, nikachanganyikiwa sikujua la kufanya, na mimi sina mwanaume yoyote niliyewahi kutembea naye zaidi yako wewe…’akasema



    ‘Nenda kahakikishe ni miezi mingapi, lakini muhimu uitoe hiyo mimba,  unasikia, na usije kuliongelea hili hapa nyumbani, na kwa kuondoa wasiwasi, na sijui kwanini unanifanyia hivyo, wema wangu wote wa kukujali kama binti yangu ndio umefikia hapa, ..sasa ukimaliza kuitoa, utafute sehemu ya kwenda haraka iwezekanavyo, maana na mimi nitatafuta cha kukufanya, hutaweza kunisahau…’akasema, na kumpatia huyo binti pesa za kuitoa hiyo mimba…na kazi ikafanyika.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Na kweli baadae binti akapata kazi sehemu nyingine, na huko akakaa huku akisumbuliwa na tumbo, akaenda kupima, akaambiwa asafishe kizazi, na alipopimwa zaidi akaonekana kizazi kimeathirika, ikabidi kitolewe kabisa.



    Binti huyo aikabidi amfuate huyu baba mtu akamuelezea hiyo hali, baba mtu, safari hii alitolewa kwa nguvu, na akaahidiwa kuitiwa polisi, siku akifika tena hapo.



    ‘Ndio unanifanyia hivyo,…mimi unajua nilipotoka….naahisi hutaishia kwangu, kila atakayekanyaga hapo ndani utamfia hivi, na ole wake ungelikuwa na binti, na yeye angelifanyiwa hivyo….’akasema



    ‘Nenda zako wewe…nimeshakuambia, nisije kukuona humu tena..unapewa mimba huko unakuja kunibambikia mimi, nimekusaidia bado hujali….kafaney utakavyo, hilo duwa lako ni la kuku tu…’akasema baba mtu kwa hasira.



    Baba mtu alipoliwazia hili, akahis machozi yakimtoka, hakujua hayo machozi yanamtoka kwa sababu gani ila alijikuta yakitoka tu….



    ************



    Pale nilipokuwa nimekaa, kichwa kilikuwa kikinawaka moto kwa mawazo, nikifikiria jinsi gani ya kuuongea huo ukweli, lakini huo ukweli usije kuathiri ndoa ya watu. Nilimkumbuka sana mama yangu aliwahi kunionya kuwa vyovyote itakwavyokuwa niwe makini sana kwenye ndoa za watu.



     Nilimuona baba mwenye nyumba akiwa hana amani, wazee walikuwa wakimuhoji kama vile wameshajua kosa lake, na nia yao ni kutaka akiri kosa lake na huenda mkewe akamsamehe.



     Nilijiuliza bila kupata jibu, ni kwanini huyo mbaba akafikia hatua ya kufanya hivyo, mke anaye, tena mke mnzuri tu, hata pamoja na utu uzima alio nao, bado alionekana mrembo, pesa inamfanya mtu asizeeka haraka.. ..na nilipoliwazia hilo nikamtupia jicho huyo mkewe nilimuona mara kwa mara akimuangalia mumewe wake kwa macho ya dharau fulani hivi…, kuonyesha kuwa ana uhakika kuwa mumewe ni mkosaji.



     Nikageuka kumuangalia kijana, macho yetu yakakakutana, kumbe huyo kijana mara kwa mara alikuwa akiniangalia mimi..niliogopa hiyo hali ya kuniangalia itaweza kuleta tafsiri mbaya kwa watu waliomo humu ndani…na tulipoangaliana niliona macho yake yakionyesha mashaka na huzuni…, sijui ni kwanini alikuwa akiniangalia mimi mara kwa mara, nikahisi kuwa huenda ni kwa vile labda mimi nitateuliwa kuwa shahidi wa matendo ya baba yake, na anajua kuwa mimi sitaweza kuficha kitu.



     Ndio ikafika muda baba mwenye nyumba akatakiwa akubali na kukiri kosa laki la sivyo, wataitwa mashahidi, na mama alisema sio masahidi tu, anao mpaka ushahidi wa video, na wazee waliposikia hivyo, walimkazia macho baba mtu ajitoe na kukiri, ili watumie hekima zao za uzee kulisawazidha hilo jambo.



    Mke wakati anasubiria mumewe aongee, akasema;



    'Wazee wangu, mimi kiukweli nashukuru kuwa mwenzangu ameamua kuwaita nyie wazazi wangu, sikulitarajia hili, nilijua yeye kama muungwana angekuja kwangu na kukiri kosa, aniombe msamaha, na mimi ningelifikiria jinsi gani ya kumsamehe,….sasa yeye kakimbilia kuwaita nyie, labda lengo lake ni zuri kuwa sasa anataka kukiri kosa lake kiukweli na kwamba hatarudia tena,…'akasema mama mwenye nyumba.



    'Na nitalifikiria hilo, kama kweli atakiri ukweli wa kukiri,...na itabakia kuamua, kiukweliwazee wangu, nimemvumilia sana, hebu jamani jiulizeni ni nani angelifanyiwa hivyo na bado andelee kuishi na …..hapana hili sasa limevuka mpaka,....siwezi tena, nahisi damu yake bado inachemka sana, akaoe vijana waendane sambamba, si ananiona mimi nimezeeka, yeye bado yumo au sio, sasa nafasi hii ni yake, aamua moja mbele yenu, na kuamua kwake, itategemea na ukweli wake, mimi naufaham ukweli wote, siwezi kumshuku mtu vibaya kwanini ...hapana, nimechoka…’akasema.





     'Unasikia mume mtu, hiyo ndio kauli ya mkeo, kasema yupo tayari kukusamehe, lakini anataka kuona ukweli wako, jinsi gani utakavyojikosha,….maana inavyoonekana kweli umefanya kosa, na waliotendewa wapo, na wamekiri kuwa watasema ukweli, sasa usitake kuumbuka zaidi.



    'Wazee wangu, ….hayo anayosema mke wangu, sio kweli, namfahamu sana mke wangu, yeye anachotaka ni mimi nikiri shutuma zake, na kitakachofuata hapo, ni kunifukuza mimi kwenye hii nyumba, alishaniahidi hivyo, sasa mimi siwezi kukubali shutuma hizo…’sasa mbaba akasema na kwuafanya wazee waangaliane tena.



     'Kwahiyo wewe nachoogopa ni hiyo adhima ya mkeo, kuwa takufukuza kwenye hii nyumba, na atakufukuza baada ya kuomba talaka yake, au sio….lakini ukweli ni kuwa umefanya makosa,..na mtu aliye mwema, alitakiwa kukubali makosa,..na kwenye wazee haliharibiki neno..’akasema mzee.



     'Nikiri kosa gani, mimi sijafanya kosa, ni yeye na dhana zake potofu..'akasema mbaba, sasa akimuangalia mkewe kwa uso wa hasira.



     'Ina maana hutaki kukiri kosa, wakati kweli mkeo kathibitisha na kasema yeye ana ushahidi wa kulithibitisha hilo, na ana video ya matendo yako machafu,…unataka nini mwanangu, unataka tuone madhambi yako, ayaonyeshe hapa mbele yetu,hiyo itavuka mpaka, siwezi kuliona hilo, kama kweli unanijali mimi kama baba yako, yamalize haya, kiungwana….’akasema baba yake.



     Mbaba akatikisa kichwa akionekana kusikitika,hakuna aliyejua dhamira yake ni nini..na machozi yalikuwa hayafutika machoni, na hakuna aliyejua kwanini aliyatoa hayo machozi.,machozi ambayo yalimuathiri sana kijana wake, kwa jinsi alivyoonekana akimuangalia baba yake kwa macho ya huruma.



     Kijana akamuangalia mama yake, na alipoona mama yake anamuangalia baba yake kwa kebehi, au dharau fulani, akainamisha kichwa chini na yeye….haikuchukua mdua machozi yakaanza kumlenga lenga, kijana huyu alimpenda sana baba, na sio baba yake tu, aliwapenda sana wazazi wake, hakutaka ndoa hiyo ivunjike, hakutaka kabisa baba yake na mama yake watengane.



     Tendo hilo la kijana kutokwa na machozi, aliliona mdada , na hapo akathibitisha ukweli kuwa kijana huyo kweli anawapenda wazazi wake, lakini swali ni kwanini aukumbutie uovu wa baba yaka kama kweli kayafanya hayo, na je kwanini hamuonei huruma mama yake kwani hali kama hiyo, inamtesa pia mama yake..



    Na mara mlango ukagongwa, na wote wakatizama mlangoni...macho ya kila mmoja yalionyesha wasiwasi, walijua labda ni ugeni wa jirani tu,...lakini kwa walengwa, mawao yao yalienda mbali zaidi, maana ugeni humo, ni nadra....



    Na aliyesimama kwenda mlangoni alikuwa kijana, ...alisimama kwa haraka na kwenda huko mlangoni, akahakikisha ameufunga mlango nyuma yake, sauti za maongezi huko nje hazikusikika, na baada ya dakika chache, mlango ukafunguliwa, na sasa aliyeingia sio yule kijana, alikuwa ni mtu mwingine..





    NB: Ni nani huyo..JAMANI LEO NIMETINGWA SANA NA MAJUKUMU, LAKINI KWA KUWAJALI NIKAONA SIKU ISIPITE HIVI HIVI..



    WAZO LA LEO: Wakati mwingine ukweli ukisemwa kwa papara unaweza ukaleta maangamizi, badala ya kusaidia, na kila jambo huwa halitaki papara, tuweni makini sana kuzitumia ndimi zetu, kwani ndimi zinaweza zikawa silaha kubwa zaidi ya bomu la nyukilia. Wenye hekima wanaona ni vyema kukaa kimia kuliko kuongea maneni yenye kuumiza wengine, maneno ambayo hayatakuja kujenga bali ni kubomoa.





    Tunaweza kujiona ni washindi wa kuongea, kutukana kudharau, kukebehi, na kuwazalilisha wengine kwa maneno ya kashfa, bila kujali hata umri wa tunayemfanyia hivyo,…jamani tujihadharini sana, kwani ulimi utatupeleka pabaya, ni heri kukaa kimia kuliko kuongea kama unachoongea ni kauli yenye ubaya na dharau  ndani yake. Hala hala sisi tunaotumia mtandao, kama vile tupo kijiweni, tunaandika tu bila kujua madhara yake baadae,..halahala jamani, wenzetu wengine walifikia kuuana kwasababu ya haya haya, na ushahid mmojawapo ni maandishi, ..chungeni sana maandishi yenu..tuache ulimbukeni wa kuandika kama tunavyoongea mitaani…, kwani maandishi ni kauli yako kwa lugha nyingine, yatakuja kukuhukumu wewe mwenyewe.



    Wakati kijana ametoka nje, mzee mmoja akaona asipoteze muda, akasema;



    'Ina maana hutaki kukiri kosa, wakati mkeo kasema kathibitisha hayo na kasema yeye ana ushahidi mpaka wa mkanda wa video,…sasa unataka nini mwanangu, unataka tuone madhambi yako, ayaonyeshe hapa mbele yetu,….’akasema baba yake.



     Mbaba akatikisa kichwa akionekana kusikitika,hakuna aliyejua dhamira yake ni nini..na machozi yalikuwa hayafutika machoni, na hakuna aliyejua kwanini aliyatoa hayo machozi.,machozi ambayo yalimuathiri sana kijana wake, kwa jinsi alivyoonekana akimuangalia baba yake kwa macho ya huruma.



    ‘Wazee wangu mimi sina cha kusema,….’akaanza kuongea na mara mlango ukafunguliwa na waliatarajia atakuwa kijana wao, lakini aliyeingia alikuwa mtu tofauti,…..



    Tangia awali, walitaka kikao hicho kiishie kama familia, na hakukutakiwa mtu mwingine aje, walimuhusisha binti wa kazi kwa vile naye analifahamu hilo tatizo na kwa namna nyingine yeye ni mhanga wa hilo tatizo, …akachukuliwa na yeye kama miongoni mwa familia.



    ‘Haya tuyaongee kama familia, tuna imani kuwa hakutakuwa na mtu wa kuja kutuingilia, kwahiyo mtajua wenyewe jinsi gani akija mgeni mtaweza kumuomba kuwa aje siku nyingine au…mtajua wenyewe….’hiyo ilikuwa kauli yam zee walipoanza kuongea.



    ‘Hatutarajii kuwa na mgeni…’akasema mama mwenye nyumba.



    Sasa mlangoni anaingia mgeni, na mgeni huyo sio mwanafamilia,…itakuwaje sasa….

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tuendelee na kisa chetu…



    ***************



    ‘Kiongozi umekuja,…’aliyesema hivyo, alikuwa baba mwenye nyumba, huku akimuangalia mgeni huyo kwa mashaka, hakutarajia ugeni huo, na hakujua kwanini mtu huyo amefika, lakini mgeni ni mgeni, hata kama hukumtarajia, na sasa keshaingia ndani mtafanyaje…



    Wakasalimiana, na wazee nao wakawa wanamuangalia mgeni huyo kwa shauku, na kuona jinsi gani wenye nyumba watamuondoa, ili waweze kuendelea na kikao chao, na hawakujua ugeni huo una maana gani, hata mama mwenye nyumba, akawa anamuangalia mgeni huyo kwa namna ya kujiuliza….



    ‘Naona wote hamukunitarajia…, macho yenu yanaonyesha kila kitu, niwaombe radhi tu, kuwa nimefika, na ujia  wangu ni mguu wenu, na mguu wa kikao hiki…na nilishaambiwa kipo kikao, na niliombwa nije mapema, tuendelee nikiwemo, lakini mnajua tena, majukumu, ukitaka kulifanya hili kunatokea hiki,…na mtajiuliza ni nani kanialika niwepo kwenye hiki kikao… lakini ujio wangu umetokana na kijana wenu, alinipigia simu, ….’akasema na wote sasa wakatulia, maana kijana yupo nje, na yeye ndiye alitakiwa kuulizwa ni kwanini akafanya hivyo.



    ‘Kijana wenu aliwahi kidogo kunielezea tatizo fulani a humu ndani,…na leo akanipigia simu mapema sana, akanielezea mambo yalipofikia, ambayo sasa, amehisi yanaweza kuleta matatizo kwenye familia yake, …’akatulia.



    ‘Sisi ndio tunafunga ndoa, lakini mara nyingi wanandoa wanafikia kubaya, na badala ya kurudi kwa wale waliofungisha ndoa, wao wanachukua hasira na kuivunja ndoa hata bila ya kutushirikisha, na huenda wangelitushirikisha, tungeliweza kutatua tatizo,…’akatulia



    ‘Kijana anakiri kuwa kafanya kosa, kunielezea hayo, na hajui wazazi wake watamfikiriaje, lakini ameona hakuna jinsi nyingine ila mimi niwepo nije nishirikiane na mababu zake, kulitatua hili tatizo..aliniuliza je alichofanya ni sahihi kama kakosea basi, ninyamaze tu kimia…mimi nikimwambia, mimi ni kiongozi wa dini, na moja ya kazi zangu ni kuwasaidia waumini wangu, na sio waumini wangu tu, na hata wale wanaoamini kuwa mimi kama kiongozi wa dini nitaweza kuwasaidia…’akatulia.



    ‘Unajua kuna mambo mengine hayana matibabu ya kihospitali, lakini ni maradhi, ila hayatambulikanai kama maradhi, na mambo hayo hayana ujanja ujanja wa kibinadamu, na hayana ujanja ujanja wa kishirikina, au uganga wa kienyeji, matibabu yake ni ya kiroho..'akashiko sehemu ya moyo.



    'Na kwa alichosema kijana japokuwa sio kwa uwazi,...naliona jambo hili linahitajia, dawa ya kiimani zaidi, ..kuzisafisha nafsi zetu zaidi,...ili dawa hiyo ya kiroho iweze kupenya ndani... unajua kuna mambo tupende tusipende, yanahitajia nguvu za mola wetu,...na  hatuwezi kufanikiwa kama hatujamfahamu mola wetu aliyetuumba, ambaye wakati mwingine anatupatia mitihani ya kutupima imani zetu, sasa kama huna imani ndio hapo unakimbilia kukufuru.....'akatulia, na kwa muda huo alikuwa bado kasimama.



    ‘Mimi kila siku napita hapo nje, nawasalimia, na kijana wenu huyu amekuwa ni mwanafunzi wangu, na najua hata kuja kwake hadi kuwa mwanafunzi wangu, ni kwasababu ya matatizo yaliyopo ndani ya familia yake,..hakuwahi kunieleza hayo bayana, lakini maswali yake mengi aliyokuwa akiniuliza yalijionyesha hivyo, ….kuwa kwenye familia yake kuna tatizo, sijui kama ni  kweli au si kweli..?’ akawa jana anauliza.



    ‘Ni kweli kiongozi, lakini hatukuwa tumefikia uamuzi wa kuyaweka matatizo yetu hadharani, tulitarajia kuyamaliza kifamilia tu…’akasema baba mwenye nyumba.



    ‘Safi kabisa, uwe na amani kuwa hilo tatizo limefika kwangu, na halitakuwa la hadharani, bali tatizo hilo litamalizwa ndani ya familia, na wanafamilia wenyewe, mimi nitakuwa kama mshauri wa imani, wa kuzisafisha nafsi zetu….’akatulia.



    ‘Karibu ukae…’aliyesema hivyo alikuwa mzee



    ‘Mimi naona raha nikiongea huku nimesimama…najihisi nipo kwenye majilisi yangu,…labda niwaulize, je nimewaingilia, na labda sihitajiki kwa sasa, maana ujio wangu nimeufanya kwa kushtukiza , baada ya kijana kufika kunipigia simu akionyesha yupo kwenye majonzi makubwa,..alikuwa kama analia kwa suati yake,  kwa vile anahisi baba na mama watafikia hatua ya kuachana, kitendo ambacho kwa kauli yake kitamfanya asiwe na amani tena hapa duniani…’akatulia



    ‘Mh…kwa vile umefika, na tunachotaka kukifanya hapa ni kuweka mambo sawa,..na itakuwa ni vyema ukitusaidia pia, kwani nyie mumejaliwa elimu hiyo ya dini, na ndoa ni nusu ya dini..sisi tulikuwa tukiangalia upande wa nusu nyingine, na sasa tunaona umefika basi utusaidia kwenye hiyo nusu nyingine ya upande wa dini..sisi wazee tunaona itakuwani heri kwetu….’akasema mzee.



    ‘Hewala…sasa labda mimi nikae, nisikilize muendelezo wake, na ikibidi na mimi nitaingilia katim niwie radhi wazazi wangu, maana wazee nyie ndio tunaowahitajia kutuongoza kwa kupitia hekima zenu…’akasema



    ‘Hapana, wewe sasa ingia moja kwa moja,..tunakuachia uongozi,...ila kwa kifupi ni kuwa wanandoa hawa wamefikia sehemu hawaaminiani tena..., na chanzo, kwa maelezo ya haraka ni kutokana na kuhisi kuwa huenda baba mwenye nyumba ana mahusiano na wafanyakazi wa ndani, ..naona niseme moja kwa moja hivyo, japokuwa tulikuwa hatujaingilia huko..kwa maoni na kauli ya mama mwenye nyumba ndio hivyo, yeye anahisi huenda mume wake anamsaliti,….’akasema mzee.



    ‘Anamsaliti kwa kupitia wafanyakazi wa ndani au sio…?’ akauliza kiongozi wa dini.



    ‘Sawa kabisa,…kwa kupitia kwa wafanyakazi wake wa ndani, hatujaweza kupata nyongeza kuwa ni kwa kupitia kwa wafanyakazi wa ndani tu au kuna wengine, ndio tulikuwa tunaelekea huko katika kudodosa dodosa, na kiukweli hatukutaka kuyafahamu yote hayo, tulipendelea kuwe na suluhu bila kupata mambo hayo kwa undani wake, haina haja, au sio mzee mwenzangu,…’akasema mzee na mzee mwingine akaongezea kwa kusema;



    ‘Ni kweli, jingine la ziada ni kuhusu hao wafanyakazi wa ndani, utaona hiki kiao kilikuw cha kifamilia, lakini humu yupo huyo mfanyakazi wa ndani, yeye kaingia humu moja kwa moja kwa vile, hao mabinti ni mayatima, wametokea kwenye familia zenye mitihani ya matatizo mbali mbali na kuwa wafanyakazi humu ilikuwa ni pamoja na kupata msaada awe kama mtoto wa familia, kwa namna moja au nyingine..’akafafanua huyo mzee mwingine.



    'Oh...ni vizuri sana kama wanafamilia wengi wangelifanya hivyo , kila mwenye uwezi amchukue yatima, au wale wasiojiweza waweze kuishi nao, wawalipe kama wafanyakazi lakini pia wawachukulie kama watoto wao, hiyo ingeleta baraka kwenye maisha yetu, na mola angelikuwa radhi na sisi....'akasema kiongozi wa dini.



    'Lakini sasa hilo limeleta mtihani...'akasema mzee na kiongozi wa dini akasema;



    ‘Basi vyema tuone tatizo hilo ni nini, au mumeshaliona taizo limetokea wapi...?' akauliza kiongozi wa dini.



    'Sisi tulitaka tutumie hekima za uzee, tuachane na msigishano, wao kwa kila mmoja wapo, ajione kakosea, maana katika kudodosa dodosa tumeona madhaifi yapo kwa pande zote mbili, kuacha hilo la kutokuaminiana..lakini kwanini wasiaminiane, tumeona kwa haraka kuwa kuna matendo waliyaruhusu na huenda ikawa ndio chanzo...'akasema mzee.



    'Mhh...lakini kwa vyovyote iwavyo, kuna hili la mayatima, hawa watu wana kosa gani, ...hapo naanza kupata kichefu chefu, labda tuendelee ....'akasema kiongozi wa dini.



    'Kifupi hapa kuna tatizo, na ni nyeti kidogo,…kwanza ni tatizo la ndoa, lakini pili ni haki za mayatima, ni kwasababu hiyo, ndio maana na sisi kama wazee likatuvuta na sisi tufike hapa kwa haraka, kabla adhabu ya mungu haijafanya kazi, ….maana japokuwa sisi sio wataalamu sana wa imani za dini, lakini uzee wetu unatupa hekima ya kuliona jambo hili kuwa ni kubwa, kuliko wenyewe wanavyofikiria..



    ‘Mfanyakazi wa ndani ni sawa na mfanyakazi mwingine maofisini, lakini hawa wametunikiwa mtihani mwingine mkubwa wa uyatima, binti huyu hapa, baba na mama yake wamefariki, na zaidi, kama nilivyosikia hali yao ya kiuchumi ilikuwa mbaya, na ninaweza kudiriki kusema kuwa walikuwa kwenye kundi lile la masikini..sasa ije itokee wanatendewa madhila mengine kama hayo tuliyoyasikia, inaumiza sana….’akasema mzee



    ‘Mzee samahani, unaongelea kuhusu huyu binti …au kuna mwingine kauli yako inaonyesha kuwa sio binti mmoja au..?



    ‘Yupo mwingine, lakini hayupo hapa kwa sasa, ila tulimweka tayari afike akihitajika, ili kutoa ushahidi, ikibidi, …



    ‘Na yeye sifa zake ni hizi hizo..au ?’ akauliza kiongozi huyo.



    ‘Ndio..kabisa, nimewafuatilia maisha yao huko nyuma, nimegundua kuwa wote wapo hivyo hivyo…’akasema mzee



    ‘Mungu ni mkubwa….’akasema huyo kiongozi wa dini.



    ‘Sasa kwa ujio wako, tunakuomba uliangalie hili tatizo kwenye uwanja wako, hasa kwenye nusu yako imani ndani ya ndoa, kama mlivyotuambia ndoa ni nusu ya dini, …..au sio, sasa utusaidie hapo, tutalitatuaje hili jambo, maana lina utata mkubwa sana..baba mwenye nyumba mpaka sasa hajataka kukubali shutuma hizo, hatujui, ni kweli au si kweli, japokuwa mama ana ushahid mnzito sana…’akasema mzee.



    ‘Ushahid wa kivipi..?’ akauliza kiongozi wa dini.



    ‘Mama mwenye nyumba anasema yeye ana uhakika wa shutuma zake kwani ana ushahidi wa watu na mwingine upo kwenye vifaa vya kisasa, yaani ana video…’akaambiwa.



    ‘Mungu ni mkubwa….’akasema huyo kiongozi



    ‘Sasa sijui tuanze vipi, maana sisi tulifikia sehemu ya kumuomba baba mwenye nyumba, akiri kosa na atubu hayo makosa, ili mambo yaishe kwa amani…, ili tusipekenyue pekenyue mambo yao ya ndani, haina haja tujue kila kitu kilichotokea, haina haja tukajua siri zao za ndani, siri zao za kindoa,…tumemuomba mume mtu aliokoe hilo kwa kukiri kosa na kutubu, na kuomba msamaha yaishe…’akasema mzee.



    ‘Kwa namna hiyo kumbe mlishafika sehemu nzuri tu ya kuhitimisha hayo, ili na mimi nije kutoa maneno ya mungu, ili kuwaweka sawa, au sio.....'akasema na kumgeukia baba  mwenye nyumba na kusema;



    'Kumbe kwahiyo baba mwenye nyumba ndio uwanja wako wa kukiri na kutubu, na hatimaye kumuomba mwenzako msamaha..kusameheana ni jambo jema sana, na hakuna kitu kibaya kama kukaa mkiwa na kinyongo, chuki, na visasi, hivyo ndio vinazidisha maradhi, maradhi ya moyo,..na shinikizo la damu, tusipende kufikia hapo, tuwe huru kusamehe, tuweze huru kuomba msamaha, na kwa kufanya hivyo, upendo utazidi, na neema za mola zitakuwa nyingi tu....sasa baba mwenye nyumba niambie...au wazee nimekwenda haraka kidogo…?’ akauliza kiongozi wa dini.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Ndio hivyo kiongozi, tuendelee…’akasema mzee, na kiongozi wa dini, akamgeukia tena baba mwenye nyumba, akamuuliza;



    ‘Je mkuu wa familia, upo tayari kwa hilo...?' akauliza



    'Kwa lipi, la kukiri au kuomba msamaha...?' akauliza



    'Kwa yote ..si mumeshamaliza au..?' akauliza



    'Hapana labda umeshtukiziwa tu, hatujamaliza, ...'akasema



    'Kwahiyo unataka kusema nini, kuwa  shutuma hizo sio za kweli, na hapo tayari kukiri kosa, ukatubu, na kumuomba mwenzako msamaha kuwa hutarudia tena, na mkayasahau yaliyopita mgange yajayo..kwa upendo na furaha, kwanini msifanye hivyo mkakumbukia enzi hizo, na watoto wakawa na amani, au mnafurahia hivyo watoto wanavyoumia, wakiwaona hamuishi kwa amani?’ akaulizwa baba mwenye nyumba.



    Baba mwenye nyumba hakutaka hata kutulia sasa akasema ;



    ‘Hizo shutuma sio za kweli, na siwezi kukiri kosa ambalo sijalifanya, …sio haki na imeniuma sana kushutumiwa jambo ambalo silijui, na kwa vile limefikia hapo, mimi kama mume nataka kuusikia huo ukweli, auseme, maana sasa nahisi nataka kupandwa kichwani…’baba mwenye nyumba akasema nakuwafanya wazee wote wawili wagune.



    Na mama mwenye nyumba akacheka, kicheko cha dharau fulani hivi, na mimi pale nilipokaa, nikawa najiuliza ni kwanini baba mwenye nyumba huyu afikie kusema hivyo, kwanini asikubali tu, mambo yakaisha na hizo shutuma na mambo yao ya ndani, yakafichika.



    ‘Oh, samahani kidogo, mimi nilijua mumeshafikia muafaka, mbona sasa yaonyesha ni kama vile tunaanza, wazee, mumelisikia hili, msije mkafukia fukia bora liende,, hili la shutuma, hili la kukiri kosa, naona bado haliwekwa sawa, ...kwa za baba mwenye nyumba au mimi nimekuja na kuchochea fitina...'akasema kiongozi wa dini.



    'Hapana kiongozi sisi tulinza kumuhoji baba mwenye nyumba ili tuone msimamo wake, tukamweka sawa, na tulitajia kuwa tungelifikia muafaka, sasa naona imekuwa tofauti na muono wetu...'akasema mzee.



    'Mnajua, watu sasa hivi wanapupia kwenye kusikiliza maneno ya kusikia, ...kauli za kusikia tu, watu wanachuklia kuwa ni kweli, ni hatari namna hii, sisemei hapa, au kuhusu hili, ila kiukweli kiuhalisia watu wanapenda sana kuhitimisha mambo yao kwa kauli za kusikia, ....tutahukumuwa kwa hili, sio vizuri usikie jambo na wewe ulihalalishe kuwa ni kweli....'akatulia.



    'Naomba mnielewe hapa, sio kwamba nimesema hivi kwa veile eti hili tatizo ni la kusikia tu, hapana, natoa u kama angalizo kwetu sisi sote, na naomba hili angalizo lisije kuwa ni kikwazo cha kuusema ukweli, sawa mama mwenye nyumba....'akasema kiongozi.



    'Mimi nimekuelewa sana, ndio maana kabla ya kulisema hili nilihakikisha kua nina ushahidi, na nilishafanya uchunguzi wa kutosha, ...sina shaka  na hilo...'akasema mama mwenye nyumba.



    'Lakini baba mwenye nyumba, unasema hujafanya , na shutuma hizo zipo mbali na wewe, je mnataka kulimalizaje hili, maana kuna njia rahisi tu, ya kukubaliana na kupotezea hayo yaliyopita, nna ni heri kwenu,...'akasema



    'Hapana, ..yeye kadai kuwa hana shaka na hilo, ina maana yeye anasema kuwa ana uhakika na shutuma zake, mimi nasema ni uwongo, hana uhakika, ni uzushi wa kusikia tu...siwezi kukubaliana nao,…’akasema baba mwenye nyumba.



    'Wazee mbona ...kumbe ilikuwa bado hamjaafikiana, na naona kuna ugumu wa kukiri kosa, sasa tufanyeje...?' akauliza kiongozi





    ‘Ndio maana tunakuomba wewe utusaidi hapo..tulitaka tutumia nguvu za wazazi, maana sisi ni wazazi wao, tunaweza kuhukumu, na kutumia rungu letu la wazazi,  tukayamaliza kwa nguvu, lakini je itakuwa ndio mwisho wake..’akasema mzee



    ‘Mtakuwa hamjamaliza tatizo, kwa hali hii, mngeliondoka hapa huku nyuma watu wanashikana mashati, na zitakazoumia ni nyasi,…’akasema kiongozi wa dini



    ‘Sasa tusaidie…’wazee wakasema



    ***********



    Kiongozi wa dini akamgeukia mama mwenye nyumba, na kusema;



    ‘Mama mwenye nyumba, na baba mwenye nyumba pia, katika mahusiano, ya mke na mume muwe makini sana, kwenye kutoa shutuma, …maana kama utamshutumu mwenzako kwa kosa ambalo hajafanya, ni dhambi kubwa sana , kwahiyo uwe makini sana,…na umakini huo utapatikana kwa nyie wawili kwanza kuelezana ukweli, kuwa mimi nakushuku hivi je ni kweli, na mwenzako ajitetee,..la sivyo, ndio tunapitia sehemu kama hizi…’akasema mkuu wa dini.



    ‘Lakini muwe makini sana kuchunga ndimi zenu, maswala kama hayo ya kushutumiana, na matatizo ya ndani kabisa ya ndoa, yasitoke nje, ikawa mnatanagaziana ubaya wenu kwa watu wengine, hilo ni kosa kubwa maaan hamjui ni nani atalipokea kwa wema, au kwa ubaya..sasa ni hivi, nikuulize wewe mama mwenye nyumba je una uhakika kuwa shutuma hizi ni kweli..?’ akauliza kiongozi huyo.



    ‘Nina uhakika….’akasema mama mwenye nyumba.



    ‘Mtihani….’akasema mzee mmojawapo.



    ‘Mtihani kweli…’akasema mzee mwingine.



    ‘Je hampo tayari, kusameheana bila ya kuingilia undani wa tatizo lenyewe, yaani kila mmoja akiri kosa, na amsamehe mwenzake, ili yashe, na muendelee na maisha ya ndoa kama kawaida, maana mengine yanatokea kama mtihani,na hapo ndipo shetani anapata mwanya wa kuleta fitina zake…?’akauliza kiongozi wa dini.



    ‘Mpaka ilipofikia hapa, hakuna kurudi tena nyuma, nataka ukweli ubainishwe la sivyo yeye akiri kosa, ili yaishe, lakini yeye kang’ang’ania kuwa sio kweli, ….mimi nilikuwa tayari kuyasamehe, lakini kwa hatua ilipofikia, mimi siwezi kusamehe tena,…kwasababu yeye anaona kuwa mimi ninamsingizia, nisimsingie ili iweje,….kwa hilo mimi sina jinsi , nitaanza kutoa ushahidi wangu, na kwsababu imefikia hapo, mimi nitajua la kufanya baada ya kutoa huo ushahidi wa kuonyesha uchafu wake…’akasema mama mwenye nyumba.



    ‘Unaona anavyonitishia, na ndio maana mimi sitaki kukubali kirahisi, najua ananitega,…ningelisema nikubali tu bora yaishe, lakini je ana dhamira gani baada ya hilo, kwa vile mimi namfahamu sana alivyo, basi mimi siwezi kukubali tu kwa nia ya kukubali, ili tu yaishe, hapana,..yeye sasa autoe huo ushaidi wake…nipo tayari kwa lolote lile…yeye si ana ushahidi autoe, ….’akasema baba mwenye nyumba akimkazia macho mke.



    ‘Kwa hali hiyo mpo tayari tuanze kuingilia mambo yenu ya ndani, ina maana mpo tayari mambo yenu ya ndani yawekwe hadharani, ujue baba mwenye nyumba mkeo kasema ana ushahidi wa watu na video, na watu watasema kwa vinywa vyao kwa hayo waliyoyaona au kutendewa, watu ni watu sio wote wenye nia njema kwenu, na video itadhirisha hata yale tusiyoyataka kuyaona,…huoni kuwa ni aibu kwako…?’ akaulizwa,



    ‘Ni aibu kama nilifanya, ni aibu kama shutuma hizo ni za kweli, lakini kama ni za kutengenezwa tu.., wenyewe mtajua la kufanya, ila kwa hatua hii basi na mimi nipo radhi nisikie huo ushahidi wake,……itakuwa ni vyema ili hatima ya haya yote ijulikane, mimi nashindwa kuelewa kwanini iwe hivyo, nimetoa machozi hapa, sikuweza kujizuia, maana mimi sijui hayo yametokea wapi, mangapi nimekuwa nikiyavumilia, ….sitaki kuongea mengi, ila namuomba mke wangu atoe huo ushahidi…’akasema.



    ‘Ndugu zanguni, maswala ya ndoa ni rahisi sana, kama wana ndoa wenyewe watakuwa radhi kukubaliana, na kukubaliana ni kuelezana mambo yao bayana, uzito unakuja pale kila mmoja anaposhikilia lake la moyoni, ubabe na kudharauliana vikatawala, na mambo hayo ya ubabe, na dharau, ni sumu ya ndoa, …niwaambie kitu, mwenyezi mungu alipanga hili la ndoa liwe ni raha kwa wanandoa…, kusaidiana na kuvumiliana iwe ni nyenzo ya kufikia malengo ya kimaendeleo, na hatima yake ni upendo, wenye kuleta neema,…sasa kama raha haipo na hakuna masikilizano ndoa zetu zitakuwa sio ndoa tena bali ni ndoana…’akasema kiongozi wa dini.



    ‘Mimi kwa kuliingilia hili kati…, sikupendelea hilo la kutoa ushahidi na kila kitu, nilitaka kwanza tuone chanzo cha tatizo, maana huko inawezakena ikawa ndio sababu kubwa sana, na haya mengine yakawa ni madhara ya hilo tatizo….ndugu zanguni, ndoa ni kati ya mke na mume wengine tunasaidia tu kuhakikisha wana ndoa wanafanikiwa kwenye malengo yao…, na tunashiriki kwasababu ya udugu, au ujirani mwema tu….nyie wawili ndio mnaoweza kuijenga ndoa yenu au kuibomoa ndoa yenu, na msikubali kamwe kuivunja ndoa yenu kirahisi hivyo….



    ‘Lakini imenisikitisha sana kuona kuwa ndoa yenu imevuka mipaka na kuvunja maagizo ya mwenyezimungu kuhusu kuwatendea wema mayatima, na kuwasaidia masikini, ..hapo mimi kama kiongozi wa dini, inabidi niliingilie kati na nione ni kwanini ikafikia huko, kwanini msiwaonee huruma hawa waliokutwa na mitihani hiyo, mayatima na masikini wametajwa sana kwenye vitabu vya mungu, kwanini, kwasababu wao kama wao hawakulipenda hilo, sasa tuziwaongezee mzigo, bali tuwasadie kuwapunguzia huo mzigo….’akatulia.



    ‘Je matatizo haya yalianzaje….?’ Akauliza na mama mwenye nyumba sasa akaomba yeye aanze kuongea, na baba mwenye nyumba naye akataka yeye aanza kuelezea..na kiongozi wa dini akasema;



    ‘Hebu kwanza tumsikia mlalamikaji, mama mwenye nyumba, yeye alianzaje kuliona hili tatizo, ili tuone kama ndio chanzo cha tatizo au la….’akasema kiongozi wa dini, na mama akaanza kuongea.



    NB: Leo jamani  naishia hapa ili msabe-sabe vyema!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    WAZO LA LEO:  Ni kosa kubwa kujiona wewe upo sahihi kwa kila jambo, na hata kama wewe ni kiongozi, au mkuu wa kaya, au bosi, inatakiwa uwasikilize na wengine waliopo chini yako, kuwa na wao wana mawazo gani kuhusiana na hoja au jambo linalizungumziwa. Kuna mambo ambayo sio ya kisayansi, ni mambo ya nadharia tu, mambo ambayo kila mtu ana hoja zake, ili kufikia lengo. Kama kiongozi uwe ni mwepesi kutoa uwanja wa mawazo, hata kma unajua hitimisho la mawazo hayo ni lipi. Usiwadharau wale waliopo chini yako, kwani ukiwapa nafasi ya kutoa mawazo, unakuwa umewashikirisha kwenye lengo, na kwenye utekelezaji kila mmoja atajiona anafanya kile alichokubaliana na wenzake.





    Mume wangu nilimpenda sana,…utaniuliza kwanini natumia neno ‘nilimpenda,..kwanini sasa nashindwa ‘Ninampenda…’…sijasema simpendi, lakini kama binadamu kuna matendo ambayo yakitokea ukayashuhudia hata kama ulikuwa na moyo wa chuma, utabadilika tu…yanaumiza na kutesa sana, na baya zaidi ni pale unapomuuliza mwenzako, akakataa, na hata kukufanya wewe umechanganyikiwa.



    ‘Sijasema hivyo, ni wewe tu mke wangu…’mume akasema lakini mke hakutaka kubishana naye akaendelea kuongea.



    ‘Wazee wangu ,…sijui niseme nini, najua mungu anajua kilichopo moyoni mwanagu na machungu ninayoyapitia, maana mwanzoni nilipoona hayo kwa macho yangu,  niliumia sana, ikafika muda nikasema basi labda,..labda,..nisamehe tu, na nikajitahidi kufany ahivyo…, japokuwa moyoni nilikuwa naumia, lakini ilipojirudia tena na tena, nikasema sasa basi, kama mimi nina moyo wa chuma basi chuma hicho kimeshashika kutu….mimi siwezi tena kuvumilia…’akasema.



    ‘Mume wangu nampenda sana haya yeye, analifahamu hilo…’ akatulia pale mume wake aliposema



    ‘Hata mimi nakupenda sana ni wewe….’akasema na kutilia.



    ‘Kumpenda kwangu huko kulinifanya nikosane na wazazi wangu, hadi hii leo, ni wao kwa tatazo kama hili wangelifika hapa kunisaidia, lakini wapo wapi, huko walipo wakisikia haya, watasema, ‘’tulikuambia,..’ lakini ningefanyaje, na ili hali mtu nilishampenda. Namshukuru sana baba yangu huyu mkubwa, alinielewa, na mpaka sasa ananilewa..yeye ndiye aliyesimamia ndoa yangu, baada ya wazazi wangu kunisusia.



     Pamoja na yote, wazazi ni wazazi tu, wao walitupatia hii nyumba, na uone ajabu baba aliindikisha kwa sote wawili, ndio maana mwenzangu nikimtishia kumfukuza, ananijibu kwa jeuri kuwa nyumba hii ni yetu sote, lakini anasahau kuwa nyumba hii ilitolewa na wazazi wangu, na wao wanaweza kumuondoa yeye, kama…haya watakuja kuyafahamu, hilo halijui…sawa kisheria ipo hivyo, nyumba imeandikishwa kwa sote wawili,  lakini sheria nayo inaangalia sheria za ndoa, huwezi ukavunja sheria za ndoa, na sheria ikakubeba tu….’akasema.



    ‘Lakini nani kavunja sheriza ndoa mke wangu…?’ akauliza na mkuu wa dini akasema;



    ‘Usimuingilie muache aongee….’akasema.



    ‘Samahani wazee, haya ngoja tumsikilize…’akasema.



     ‘Najua baada ya haya yote, anajua nitamfukuza humu ndani…, lakini hata hivyo, ni nani angeliweza kuyavumilia hayo yote… natamani nisiyaongee maana kuyaongea zaidi ndio nazidi kujiumiza, lakini kwanini niendelee kunyamza wakati mwenzangu ananiona mimi ni ninaota tu, eti naota, sio kweli…hivi kweli mimi nimzushie uwongo mtu niliyempenda ikafikia hadi nitengane na familia yangu, kwanini nifanye hivyo…’akasema na kutulia kidogo.



    Mwenzangu amesahau tulipotoka, amesahau, nilivyojitolea kwa ajili yake, nilifikia hadi kuiba pesa kwa wazazi wangu au kudanganya, ili tu nimpatie ada aendelee kusoma, na hata alipofika chuo kikuu, tukiwa pamoja naye, alikuwa hana mbele wala  nyuma, mimi nilikuwa namfadhili, aseme ukweli wake kama sikutafanya hayo kwa ajili ya upendo wetu, leo hii kafanikiwa, maana hana tatizo, tena, ana kazi nzuri, kipato kizuri, na nasikia kaanza kujenga nyumba yake, haniambii, nasikia kwa watu tu, mimi siwezi kumuingili huko.



    ‘Hilo nalo jipya….’akasema mume wake, na alipokumbuka kuwa kaambiwa asiingilie akatulia kwa haraka.



    ‘Hayo sio muhimu sana kwa leo, maana anaweza kusema hayo yliyokuwa ya kale, zilipendwa, sasa umezeeka, nataka damu mpya, kwasababu mume hazeeki, sawa, ..ni kweli mimi nimezeeka, hayo ya mapenzi ya ujana mimi sina tena, sina …nasema kweli sina..na sitaki tena kuendekeza mambo hayo.., ndio maana nilimpa uhuru wa kufanya pendavyo, lakini sio ndani ya nyumba yangu…’akatulia



    Hayo nilimuambia mapema tu, akasema mimi mzushi, …nikamwambia ipo siku nitakuthibitishia hilo, na kweli nikaja kuyaona , sasa ndani ya nyumba yangu mwenyewe, kaamua kunikomoa …hivi kweli mimi ni binadamu gani wa kuvumilia haya, na bado namuuliza hataki kusema ukweli, nitamsaidiaje mtu kama huyu…’akawa kama anauliza



    ‘Haya basi kama kaona mimi simtoshelezi, kama kaona anahitajia damu changa, basi aniambie tu…mimi  nitamsaidia hata kumtafutia mke mwenza anayefaa, sio kutembea na wafanyakazi wa ndani,…’akatulia pale mume wake alipotaka kuingilia . Mume akatulia hakusema neno.



    ‘Mimi naweza kukubali aoe tu…lakini iwe kwa utaratibu mnzuri na makubaliano…, yeye akasema hayo najitungia tu mimi mwenyewe kwa vile simtaki, kwa vile nataka yeye aondoke kwenye hii nyumba, kwanini kila kitu anarefaa kwenye hii nyumba, hii nyumba ni nini jamani...’akasema akionyesha nyumba.



     ‘Siyasemi haya kwa kujionyesha kuwa sisi tupoje, labda nafanya makosa kutoa siri hizo, lakini sasa nifanyeje, ni lazima niwaambie nyie wazazi wangu ili mfahamu hiki kinachoendelea humu ndani,  ili muone je hii ndoa kweli ipo au ni geresha tu…’akawaangalia wazee wake.



    ‘Huyu mume wangu nilimpenda sana, nay eye alionyesha kuwa ananipenda kwa vile, sasa naanza kufahamu ni kwa vile alihitajia kitu, na sasa kakipata, …sasa sina thamani tena kwake, naomba mnisaidia sana, kwa hili, labda mimi nimkosaji, kama nimekosea, basi mje mniambie, lakini hapa ilipofikia, siwezi kuvumilia tena…’akatulia

    ‘Mke wangu jamani..usiseme hivyo….’mume mtu akasema kwa sauti ya huruma.



    ‘Sisemi hivi kwa vile utasema mimi najivunia wazazi wenye uwezo, hapana, mimi sasa hivi sitegemei wazazi wangu, nilishajitoa kwao, na nilishajipanga kuishi maisha yangu bila kuwategemea wao, na ndio maana pale tulipopewa hii nyumba nilikataa,….unakumbuka mimi nilikuambie tutafute chetu, tuanzie nyumba ya kupanga, wewe ukanishauri nikubali tu, mpaka hapo tutakapojenga nyumba yetu, sasa…kipowapi,….’akageuka kumuangalia mume wake.



    ‘Ongea tu, ongea kila kitu, ila mimi nataka ushahidi, maana umeamua kunivua nguo mbele ya watu, haya endelea….’akasema mume wake kwa sauti ya huzuni.



    ‘Ni mimi nakuvua nguo au ni wewe umejivua nguo mwenyewe kwa tamaa zako za mwili, umejishushia hadi wewe mwenyewe japokuwa hutaki kuukubali ukweli….’ akauliza

    ‘Samahani wazee wangu, ngoja nimuulize swali…?’ akasema na wazee wakakaa kimia tu, nay eye akasema.



    ‘Mke wangu wewe unasema niimejitakia kwa vipi fafanua hapo ili na mimi nielewe,…wewe unazunguka, unaelezea mengi ya zamani, nia yako ni nini,kuwa mimi nilikuwa mtoto wa mitaani, ukanisaidia, na kufikia hapa, au sio, sawa ni kweli, nakubali hilo, na nakushuruku sana, lakini hili la kuniambia mimi nakusaliti, siwezi kulivumilia, niambie wapi , na nani nilifanya naye hivyo…, hilo tu…tusizunguke saana…’akasema.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Huko nitafika, maana hata mimi nashangaa baada ya kuongea na wewe na kukuelezea kuwa ninao ushahidi bado huamini, bado unaniona nakusingizia, hapo natilia mashaka,…wewe una tatizo, haupo sawa, sio yule mume niliyemfahamu kabla… ningekuwa mshirikina ningelisema wewe kuna kitu wamekuwekea, lakini mimi sio mshikirina na siamini mambo hayo, huo ni ulimbukeni wako tu…’akasema.



    ‘Sawa..sasa si useme,…unaogopa nini…unajua mke wangu kwanini hujiulizi, kwanini mimi nijiamini kiasi hicho, ..utakuja kuumbuka mwenyewe, …nakuatahdharisha mapema..’akasema.



    ‘Nitasema, leo nitasema kila kitu, na ..ushahidi ukitaka nitauonyesha, kama upo tayari wazazi hawa wauone uchafu wako mimi nitauonyesha, kwasababu mimi nilishauona, unatia kinyaaa…sasa sijui baada ya hilo utakwenda wapi, utaficha wapi hayo macho yako yenye aibu, nakuonea huruma jinsi gani utateseka…’akasema.



    ‘Hahaha, mimi au wewe…wewe ndio utaumbuka, kwa kuwapotezea hawa wazee muda wao,..maana sijafanya kitu jamani, wewe unakisia tu,…kama kweli huo mkanda wa video ulichukua hali halisi iliyokuwepo,…kuwa mimi nilikwenda mle ndani kuhakiki…maan nina haki, kelele zilisikika na mimi nakaenda kuhakiki, ..hao ni watoto wangu, …haya onyesha, labda uwe umetengenezwa huko mitaani…’ akasema kwa kujiamini.



    ‘Mume wangu nakuomba tena utubu madhambi yako, tuone ni nini cha kufanya, nakuuliza tena mbeel ya hawa wazee je hukufanya hayo madhambi…?’ akaulizwa.



    ‘Sijafanya ndio maana mpaka sasa naendelea kupinga, mimi sijafanya hayo madhambi unayoyasema wewe, huo uwongo na uzushi…kama ni kweli toa huo ushahidi wako..’akasema.



    ‘Kwanza, kabla sijaendelea na hilo, niwaulize nyie wazee, na kiongozi wetu wa imani, je nikifanya hivyo nitakuwa nimekosea…?’ akauliza mama mwenye nyumba.



    ‘Ukifanya vipi..?’ akauliza kiongozi wa dini.



    ‘Nikitoa huo ushahidi unaonyesha ukweli wa haya yote, maana unaonyesha matendo yasiyofaa, kwa mume kama huyu , mzee kama huyu,..…maana sio mnzuri kuangalia, na ..sikupenda iwe hivyo, kama angelikubaliana na mimi, basi ningeona jinsi gani nyingine ya kufanya, ili ajifunze, na dunia ingemfunza tu…’akasema.



    ‘Kwanini unazunguka kwanini mpaka uwaulize hao wazee kuwa utoe au la…wa kuulizwa ni mimi, kama ni aibu si zangu mimi au sio..,..nimeshakuambia mimi nipo tayari, kuuona na kuwasikia hao mashahidi wako, waite mmoja mmoja waseme ukweli hapa mbele ya wazee, kama kweli watasema ukweli, lakini kama ni wao ni waongo, haya tutawasikia…’akasema.



    ‘Mhh…haya, kwanza nimuulize huyu binti ambaye yupo hapa, asema ukweli wake, yaliyotokea humu ndani, je ni kweli hajawahi kufanyiwa mambo yasiyo faa, maana nisiende mbali, wewe binti, unamuogopa mungu wako,niambie ukweli kinachoendelea humu ndani..na ukumbuke, kama utaficha na ikatokea tatizo, ujue mimi sitakuwa nawe tena,….’akasema akimuangalia huyo binti.



    ‘Je ulishawahi kufanyiwa matendo yasiyofaa..?’ nikaulizwa , nilitarajia hivyo, lakini hapo akawa kaniwahi , bila kujiandaa, hapo nikajikuta natokwa na jasho jingi mwilini nikakaa kimia kwanza na yaliyokuja kichwani ni yale maneno ya kijana ya kunitahdharisha nisije kuvunja ndoa ya watu.



    ‘Binti hebu ongea ukweli, usiogope..’akasema mzee



    ‘Mhh..hapana mimi sipo tayari kuongea lolote, nahitajia muda hivyo..’nikasema.



    ‘Kwanini..unahitajia muda gani, wa kusema ukweli, sema ukweli kilichokutokea, unaogopa kusema ukweli, au unamuogopa baba mwenye nyumba..?’ nikaulizwa.



    ‘Kwasababu yote nayaona kama ndoto, sina uhakika…na naogopa kuja kusema uwongo, kumbe ni ndoto tu, mimi sijui, ..’nikasema.



    ‘Kwani hiyo ndoto ilitokeaje..?’ nikaulizwa



    ‘Kiukweli tangu nifike hapa nyumbani nimekuwa nikitokewa na vitu vya kutisha…’nikasema



    ‘Ukitokewa kwa vipi..?’ akaulizwa.



    ‘Huwa naota ndoto za kukabwa, na….’hapo nikasita kuendelea kuongea kwa kuogopa kuelezea mambo kama hayo mbele ya watu wazima.



    ‘Mnasikia, anafanya nini..anaota, ndoto zinatokea wapi…jamani tusaidianeni hili ndoto hutokea kichwani akilini, sio matendo…..’akasema baba mwenye nyumba.



    ‘Tulia,….’akasema kiongozi wa dini



    ‘Ongea ukweli, sisi tunataka kusaidia hili jambo…tumekupa nafasi hiyo, usiogope kutuvunjia wazee heshima kwa maneno yasiyofaa kuongelewa,…nia hapa ni kuwasaidia hawa wana ndoa wawili na nyie pia…, hatutakubali ndoa hii ivunjike, tunajua jinsi gani ya kuliweka hili jambo sawa sawa, nimegundua kitu hapa, lakini siwezi kukisema mpaka nipate maelezo zaidi yenye uhakika….’akasema mkuu wa dini.



    ‘Mimi kwakweli nashindwa kuongea maana naota tu, kuna vitu vinanikaba, mwili unaisha nguvu kabisa siwezi hata kugeuka, siwezi kufanya lolote ….ni majinamizi sijui….nahisi kama kuna mtu ananishika kwa nguvu, ananikaba, nakosa pumzi, hata kupiga kelele siwezi, nalegea mwili mnzima, nahangaika wee, na ..inafikia sehemu nahisi kama nazalilishwa,..nafanyiwa vitendo vibaya…’nikasema



    ‘Unazalilishwa kwa vipi, usiogope kufafanua …?’ akaulizwa



    ‘Nafanyiwa vitendo vibaya,…’akasema



    ‘Na nani…?’ akaulizwa



    ‘Simjui , maana simuoni, nahisi tu, sioni kitu, nahisi kwenye njozi tu….’akasema



    ‘Je kwa hali kama hiyo ya kuzalilishwa, ukiamuka unajiona kweli umefanyiwa vitendo kama hivyo..?’ akaulizwa



    ‘Aaah…,mimi siwezi kujua, maana ni vitu nimekuja kuvionea huku,…na sijui una maana gani kwenye hilo swali,…, na wala sijui nijibuje..…naona kama ndoto tu ndicho ninachoweza kukisema, lakini nateseka, sijui kwakweli…’akasema.



    ‘Imetokea hivyo mara ngapi..?’ nikaulizwa



    ‘Kwa kuzalilishwa, mmh, mara nyingi tu, sijaweza kupata amani labda nikiwa kwenye siku zangu, mara nyingine naweza kukabwa tu, nikasumbuliwa wee, aah, hata sielewi ni kitu gani na kinataka nini .…’akasema



    ‘Na ndio maana yule binti wa kwanza, ilimtokea hivyo mpaka akapata mimba, huyu mume wangu mwenyewe akamsaidia kuitoa, anabisha na hilo…’akasema mama mwenye nyumba.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Nani..mimi, wewe….hebu sema ukweli hapo…wewe mwenyewe unajua ni kwanini tulifanya hivyo, na wewe ndiye ulinishauri tufanye hivyo…., kama ningelikuwa na nia mbaya kwanini nikakushirikisha..?’ akauliza baba mwenye nyumba kama anashtuka!



    ‘Ulinishirikisha kwa vile alishaamua kuja kuniambia ukweli, ukaona ili ujikoshe, uje kuniambia kuwa mumesingiziwa wewe na mtoto wangu, nikaona sasa hayo yatakuwa makubwa, na sifa ya familia yetu itaharibika, ndio maana nilikukubalia ombi lako…’akasema mke wake



    ‘Mke wangu, mke wangu, ombi langu au ombi letu,..usikwepe hapo kabisa, umeamua kulisema hilo , basi liseme vyema, wewe ndiye ulipendekeza hilo la kutoa mimba, kweli si kweli, tutakubaliana tufanye hivyo, kweli si ikweli, sasa unajifanya kuogopa kusema ukweli eeh, sema ukweli wako, unaogopa nini sasa, muone jinsi mke wangu alivyo…’akasema.



    ‘Ninajua ni wewe uliyempa mimba binti wa watu, kwasababu nilikupenda, nikaona tuhakikishe hilo jambo halisambai, na wewe ukaniahidi kuwa utajitunza, ukasema kama ni kweli hutarudia tena…’akasema mke wake.



    ‘Wewe mwanamke sema ukweli wote, mimi nilikuambia kama ni kweli,…nilitamka hivyo,…mimi nilikuambia sio mimi, na kama ni kijana wetu basi amuoe, wewe ukasema kijana wetu hawezi kumuoa mtu kama huyo,  kweli si kweli…na kijana wetu kuna kipindi alikuwa hana raha, tulipomuhoji alionekana kuwa na mashaka, tukahisi ndio yeye kafanya hivyo, ndio maana tukakubaliana na hilo..inatakiwa hapa useme ukweli wote, muogope sana mungu kwa kuzua uwongo....’akasema mumewe.



    ‘Wewe ndio umuogope mungu wako, hutaki kuukubali ukweli ukasaidiwa…wewe una tatizo, mume wangu wewe una tatizo, kwanini usikubali ukasaidiwa,…mimi nahsi kuna kitu kimekutokea, sio bure…’akasema



    ‘Hahaha, huna jipya wewe…mimi ndio mwenye tatizo au ni wewe…wewe una tatizo, unaingiwa na akili ya kuzua mambo, unahitajia kusaidiwa, ….na kauli yako hiyo naona inaanza kukugeuza mtizamo wako, wa kuamini mambo kishirikina,…umempata wapi mganga wa kukudanganya, ?’ akauliza



    ‘Mimi naona tunapoteza muda hapa…’akasema mkewe.

    ‘Wewe ndio unapoteza muda,  na nakuambia sasa,  mimi leo hatumalizi hiki kikao mpaka uutoe huo ushahidi wako unaosema unao,…nimechoka kuzalilishwa na kauli zako zisizo na ukweli, …’akasema.



    ‘Ushahidi si ndio huo kwanza kwa huyu binti anapatwa na kitu gani, …na ni nani anamfanyia hivyo,na sisi tupo humu ndani wa ngapi…?’ akauliza.



    ‘Kwahiyo na hili pia, unataka kumsingizia hata mwanao au sio,..?’ akauliza.



    ‘Sijamsingizia mtoto wangu, na kama na yeye anafanya hivyo, ni wewe umemfundisha, maana alishaniambia…yanaoyoendelea humu, ila anakutetea, sasa umemsikia huyu binti alivyosema, kuna mtu anamkaba usiku, na kitendo hicho kinafanyika lakini anashindwa kujigeuza,…au kuona kuwa ni nani, sasa ni nani angeliingia humu ndani na kufanya hivyo, wakati tumefunga mlango, ni nani kama sio wewe…?’ akaulizwa.



    ‘Na mwanangu sio..?’ akauliza



    ‘Sijamsema mtoto wangu maana hata ushahidi huu nilio nao, unakuonyesha wewe peke yako, ukiwa na huyo binti…..’akatoa kanda ya video kwenye mfuko.



    ‘Unakuonyesha wewe….ukiwa na yule binti aliyeondoka mkifanya uchafu wenu,…si unataka tuuonyeshe huo uchafu wako mbele ya wazazi,..na utaabika kweli ukionekana…’akasema na hapo mumewe akabakia kimia akikodoa macho kuaangalia huo mkanda.



    ‘Wewe mwanamke umefikia hapo..umeupatia wapi huo mkanda?’ akauliza



    ‘Kufanya nini, si unataka ushahid wa video, wewe ulifikiria natania, sasa mkanda ni huu hapa, nionyeshe wauone wazazi wako…?’ akaulizwa



    ‘Kwanini nilikuambia unionyeshe huo ushahidi awali, ukakataa, ..sasa unautoa mbele za watu…’akasema mme mtu sasa akionyesha mashaka.



    ‘Swali je ni kweli ulifanya..?’ akaulizwa



    ‘Sijafanya..sio kweli na huo mkanda kama ni kweli utakuwa umeutengeneza huko na hao watu wako,…mimi nayafahamu hayo sana..siku hizi vitu kama hivyo vinafanyika…ila mimi bado nasema sio kweli, …kama ulichukua matendo halisi, basi hakuna cha maana kitakachoonyeshwa, mimi sijafanya madhambi hayo..’akasema, lakini sasa sauti ilikuwa sio ya kujiamini kama awali.



    ‘Nakuuliza tena mume wangu ..nakupenda sana, kwani  hayo yatakayotokea baadae hutaaamini, baada ya hili, basi tena, …maana ni aibu kuonyesha mbele ya wazazi hawa, kitu kama hicho…na mimi sitakuwa radhi kuendelea kuishi na wewe…’akasema.



    ‘Kwanini unanitisha maswala ya kuachana…, kwanini hutaki kuutoa huo ushahidi, huyu binti hapa ulisema ni shahidi yako kakataa, kasema ni ndoto tu, sasa hebu niambie ninaingiaje kwenye huo ubongo wake,…akilini mwake… na kuyafanya hayo anayosema anayaota, au unanishuku mimi ni mchawi, niambie…’akasema



    ‘Huyu binti, hawezi kusema maana hana uhakika, yeye anahisi kaota, lakini sio kweli, hayo yaliyomtokea ni kweli,..nilimdadidi akasema aliona hiyo athari mwilini mwake..hawezi kuyasema hayo hapa.. ninachojiuliza iweje,…ifanyike na yeye ashindwe kuzindukana, ina maana kuna kitu anafanyiwa, mpaka anashindwa kuzindukana, sasa ni nani anamfanyia hivyo…’akasema



    ‘Kwahiyo mimi ndio namfanyia hivyo…?’ akauliza baba mwenye nyumba kwa sauti ya kutahayari.



    ‘Hapo mimi sijui ni wewe au ni nani, ndio maana nikakuuliza na kama hutaki kukubali ukweli, basi tutafute njia za wewe kukubali, na kama hawa mabinti wengekubali kushirikiana, basi tungelishalimazlia hili,…’akasema na mumewe akatikisa kichwa, na kugeuka kumuangalia huyo binti, akauliza akimuangalia huyo binti;



    ‘Wewe binti uliwahi kuniona nikiingia chumbani kwako usiku kama anavyodai huyo mama yako, sema ukweli wako wala usiogope, maana kikao hiki ni cha kusaidiana, na ukisema ukweli, siwezi kukufany alolote, mbele ya wazee hawa, sema uliwahi kuniona nikiingia chumbani kwako usiku na kukufanya hivyo, inavyodaiwa, kuingia sikatai, niliwahi, lakini je niliwahi kukugusa, …?’ akauliza



    ‘Hapana….mimi sijawahi kumuona....hata kukuona ukiingia kama unavyodai kuwa unaingia usiku, kiukweli tangia nifike hapa sijawahi kukuona ukiingia chumbani kwangu usiku, nasema hilo kiukweli wangu,…, maana huwa nimelala,..huwa ninakuwa na usingizi mnzito, isingelikuwa ni hayo majinamizi.. kwahiyo mimi …siwezi kulithibitisha hilo…’nikasema na wazee wakamgeukia mama mwenye nyumba ili aendelee



    Na baba mwenye nyumba akasema;



    ‘Umesikia…..jamani mumesikia wenyewe, ….shahidi wa kwanza kakukana, haya tafuta ushahidi mwingine, au unataka kuonyesh hiyo kanda kwanza, mimi ningelishauri, …tunampigie huyo binti mwingine au sio..mimi nataka tulimalize hili kwa amani,  ili tuone ni nani mwenye matatizo, ni mimi au ni wewe….’akasema mume mtu huku akianza kupiga simu kumuita huyo binti mwingine.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    NB: Ushahidi utaendelea sehemu ijayo..je binti atakubali kuja, au utaonyeshwa ushahidi wa video,



    WAZO LA LEO: Kila mtu ana udhaifu wake, na udhaifi mwingine unakuja kuwa ni ugonjwa mtu asipokubali kusaidiwa, kuna watu wanaingia kwenye ulevi wa pombe au sigara, au kwenye matatizo fulani,  kumbe ni kutokana na misongo ya mawazo!



    Wengi wao, wangelikubali kusaidiwa huenda matatizo hayo yasingelifikia huko. Kama wewe ni mke wa mtu, au mume wa mtu, jaribuni kukaa na mwenzako, muongee matatizo yenu, kuliko kuyaweka kichwani, au kuanza kutafuta njia zisizo halali , eti kuondoa mawazo…ikishikindikana watafuetni wazee wenye busara, mpate mawazo ye hekima na busara!





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog