Simulizi : Nisamehe Grace
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya Afande Sophia kumaliza kutoa Maelezo Afande Koboko alikuwa anatetemeka mbaya. Muda ule Baridi ya Mkoa wa Arusha ilikuwa haitii Dafu Maana Usoni Afande Koboko alikuwa Ameenea Jasho Utafikilia amejimwagia Maji. "Nauwezo wa kufanya vile Kama Ulivyoniambaia ila Tafadhari naomba Unipe ahadi kuwa Mimi hutanifunga. Ni kweli nilikuwa natumwa na Watu Wangu Wakubwa hivyo Sikuwa na Jinsi. Naombeni Mnisaidie Mimi Sasa hivi nitaenda kukamilisha Ushaidi wenu"Aliongea Afande Koboko huku bado alikuwa anatetemeka mbaya. Wakati Afande Koboko akiwa Anaongea vile huku Suzani alikuwa anatetemeka mbaya. Muda ule hadi Machozi yalikuwa yanamtoka hasa alipomuona Mtu ambaye alimkita mume wake kisu mara mbili akiwa anaongea upumbavu wa kuomba Asamehewe. Suzani alikumbuka Jinsi ambavyo alikuwa anaishi maisha ya raha na Mume wake Afande Joshua ndio hasira zilizidi kumbana na Hamu ya kutaka kuua ilikuwa inamwijia. Kwa Kasi ya ajabu Suzani aliamka chini utafikilia hakuwa amepigwa Risasi kwenye bega. Alipoamka alijongea kwa kasi ya ajabu hadi kwa Goodlucky na kwenda kumuondolea Bastora ambayo alikuwa nayo Good na Kumnyooshea Koboko. "Koboko mimi kwa kweli nipo tofauti na Mawazo ya Afande Sophia, ulimuua Mpenzi wangu makusudi tena kwa kumchoma visu mbele ya macho yangu na watu wengine walikuwepo kwenye kile chumba cha hospitalini. Sasa na mimi nitakuua mbele ya watu ambao wapo kwenye hiki chumba. Baada ya Mume wangu kufa nilimwambia kuwa lazima nimuue mtu ambaye alisababisha yeye kufa sasa naona huu ndio Muda wako wa kufa. Afande Sophia naomba utanisamehe Sana maelezo uliyotoa ya kumsamehe huyu mtu ili akuletee ushaidi mimi nayapinga. Huyu mtu ndio amemuua mume wangu wala siyo Mkuu wa jeshi la Polisi. Amemua mume wangu na amekuja kuniua na mimi hadi sasa kanipiga risasi ya begani leo nimwache kweli haitawezekana mtanisamehe sana leo Koboko lazima ufe ili nitimize kile ambacho nilimuhaidi Mpenzi wangu"Aliongea suzani Huku akiweka Bastora yake tayari kwa kumpiga Kaboko. Afande Sophia aliposikiliza yale Maneno ya suzani kweli aliona akichelewa Suzani atampiga koboko risasi hali ambayo itaharibu kazi yake ambayo alikuwa anataka kuifanya. Sasa aliwaza kitu gani ambacho angemwambia Sophia ili asimshambulie Koboko lakini alishindwa kukipata. Kwa haraka ambacho aliamu ni kwenda mbele ya Koboko kumzuia Suzani asifanye hivyo. "Suzani naomba usimuue Koboko maana hana hatia kweli alimuua mume wako lakini alitumwa na Shawali pamoja na Mkuu wa Jeshi la polisi. Kama unataka kumuua huyu mtu naomba niue kwanza mimi"Aliongea Afande Sophia huku akiwa amekaa mbele ya Koboko. Afande Sophia alijua koboko kuwa alikuwa na hatia na lazima angemfunga ila muda ule alitaka kumtumia koboko kupata ushaihidi alafu baadae anamgeuka. "Afande Sophia kumbe na wewe ni Mjinga kiasi hiki inamaana kumbe na wewe unaungana na huyu mtu ambaye alimuua Mume wangu ili kutetea maiasha yake. Sasa mimi sitajari nitawaua wote, ndio lazima niwaue tu wote si umesema nianze na wewe basi mimi nitafanya tu. Wewe afande Gani mtu ameua kwa kuzamilia kabsa leo unaniambia hajaua alitumwa. Ngoja nikwambia huyu Mtu alimpiga Mume wangu risasi kipindi tukiwe Hotelini alipompiga Risasi hakufa lakini aliamua kumfuata hadi hospitalini na kuja kumuua na mimi nikiwa naona leo hii unaniambia nimsamehe. Namuua mungu wangu na wewe afande Sophia kama ukiendelea kumzuia utakufa naye"Aliongea Suzan huku hadi machozi yalikuwa yanamtoka. Goodlucky alipomwangalia Suzani aliona kweli alikuwa na lengo la kuua kabsa. Alichofanya alimnyemelea Suzani kwa Nyuma na kumuondolea ile Bastora. Kitendo cha Good kumuondolea Bastora suzani kilileta purukushani kali mle ndani kwani Suzani hakuwa tayari kumuona mtu ambaye alimuua Mume wake anatoka salama kwenye kile Chumba. Baada ya kubembelezwa kwa Muda mrefu ndipo Suzani aliamua kutulia kwa Muda ule ila aliendelea kuapa moyoni Mwake lazima atamuua tu Koboko. Baada ya Maongezi ya Muda wa Dakika tano Koboko na Afande wengine Waliruhusiwa kuondoka kwenye nyumba ya Suzani ili kwenda kuchukua ushaidi mwingine kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi. Huku nako Sophia walimchukua Suzani na kumpeleka Hospitalini ili kwenda kutibiwa. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Shawali baada ya kwenda kwa kina Sophia na kumkuta sophia yupo mzima wala Frank hajamzuru aliamua kuondoka kwenda kwa Mkuu wa jeshi la polisi ili kwenda kuomba afande wa kumlinda Grace kama mama yake na Grace alivyomwambia. Alipofika kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi alimuelezea kwanza Jinsi ambavyo alishindwa kutimiza kazi yake ya kuwaua wale watu. Pia alimpa taarifa kama Frank katoroka Gerezani. Mkuu wa jeshi la Polisi aliposikia kuwa Frank katoroka Gerezani ndio alichanganyikiwa kabsa. Baada ya Maongezi mengi Mkuu wa kituo alimpa walinzi wa wanne Shawali ili kwenda Kumlinda Grace huku wakiapa lazima wamtafute Frank hadi Wampate. Huku kwa Frank ambako alikuwa Amewekwa ndani alipanga lazima atoke ili kwenda kuongea na Grace kwa Mara ya Mwisho aone kweli alimkataa kama alivyofanya Gerezani au vipi
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kabla ya Frank kuondoka ili kwenda kuonana na Grace alihitaji kupata Ruhusu kwanza kwa Mzee Ramadhani maana yeye ndie ambaye alimuweka mle ndani na alimwambia kuwa atakuwa anapata huduma zote ndani na Asitoke nje ovyo hadi Siku ya Harusi itakapofika ambayo bado hata ilikuwa haijapangwa itakuwa lini. Muda wa Saa Kumi na Moja Jioni mzee Ramadhani alikuja kumuona Frank kama Kawaida yake Maana kwa siku alikuwa anamuona mara mbili Asubuhi anapoenda kazini na Jioni anaporudi kazini. Ndani ya kile Chumba Mzee Ramadhani alikuwa na mlizi wake ambaye ndio alikuwa anampatia Frank chakula kwa siri. "Mzee Samahani kuna kitu nahitaji kukuomba, Kitu chenyewe nahitaji kukifanya kesho. Mzee Nahitaji kuonana na Grace kwa Mara ya Mwisho niongee naye maana bado sijaamini kama kweli Grace anitaki"Frank alimwambia Mzee Ramadhani baada ya kusalimiana "Frank unakumbuka nilivyokwambia kuwa kwenye hii nyumba unatakiwa usiwe unatoka sana. Maana kama Mwanangu atakuona na Kugundua kama Mimi ndio nimekuweka hapa dili ambalo tunataka kulicheza litakuwa Gumu. Frank mimi najua kabsa kama Mwanangu amekudhurumu haki yako ndio maana nahitaji kukutimizia. Ila Sawa hiyo kazi ya wewe Kuonana na Grace niachie Mimi, Kesho Mimi Muda wa Saa nne nitakuja kukuchukua na kukupeleka hadi kwa Grace uwezo kuonana naye"Aliongea Mzee Ramadhani. Yale Maneno ambayo Aliongea Mzee ramadhani kwa kweli yalimpa Faraja Frank. Ambacho alikuwa anahitaji Frank ni kumuona Grace alafu amuone akitamka tena kwa Mara ya pili kuwa Hamtaki na yeye yupo tayari kuolewa na Shawali. Baada ya Stori za hapa na Pale Mzee Ramadhani alimuaga frank na Kumwambia Wataonana kesho. Shawali baada ya kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi aliwapeleka Walinzi Hadi nyumbani kwa kina Grace na kuwapa Jukumu la kumlinda Grace. Kile kitendo kwa kweli kiliwafurahisha Familia ya kina Grace hata Grace Mwenyewe alikuwa na Furaha mbaya. Maana kitendo kile kilimfanya Grace kuamini kama Shawali alikuwa anampenda mbaya. Alipowakabizi wale Walinzi Shawali waliongea Kidogo na Grace kisha alirudi nyumbani kwao. "Baba kwa kweli nahitaji kumuoa Grace Haraka iwezekanavyo. Baba nafanya hivyo kwa kuwa Frank ametoroka Gerezani na anampango wa kumuua Grace. Sasa nahitaji nimuoe Haraka Grace ili nimlinde maana Grace kama akiwa karibu na mimi ulinzi utakuwa Mkubwa zaidi"Aliongea Shawali baada ya kufika nyumbani bila kujua kama mtu ambaye alikuwa anamwambia habari za kutoroka kwa Frank ndio ambaye alimtorosha Frank. "Mwanangu hata Mimi hilo ndilo ambalo nilikuwa nahitaji kusikia. Unajua Mwanangu upinzani wa wewe kumuoa Grace unazidi kuongezeka siku hadi siku. Hivyo kama tutazidi kuchelewa unaweza ukashindwa kabsa kumuoa Grace kitu ambacho itakuwa aibu kwetu sote. Watu tajiri na pesa zetu tushindwe kumpata mtoto wa masikini. Hivyo mimi nakuunga Mkono na Maandalizi yataanza Mara Moja wewe Pendekeza tu lini unahitaji ndoa yako ifanyike"Alijibu Mzee Ramadhani huku akionyesha tabasamu. Mzee Ramadhani Ingawa alikuwa anatabasamu ila Moyoni alikuwa na hasira sana na Mwanae maana alikuwa anafanya mambo ya kinyama. "Ndio maana Mimi huwa Nakupenda baba yangu maana huwa unapanga vitu kama mimi mwanae ninavyowaza. Mimi mzee Nahitaji Juma tano ya wiki Ijayo nifunge Pingu za Maisha na Mpenzi wangu Grace hivyo nahitaji tuanze Maandalizi kama Kawaida"Aliongea Shawali huku akiwa na Furaha mbaya. "Sawa Mwanangu wewe anza kufanya Maandalizi na kama Wageni anza kuwaalika na waliopo mbali waanze kuja maana Juma tano ya wiki ijayo siyo mbaya. Mimi pia Mwanangu nahitaji kuja kukufanyia Surprise babukubwa siku ya Harusi yako ambayo itakufanya uamini ni kiasi gani nakupenda. Pia Kesho nahitaji kutoka na Mkwe wangu Wa kwanza wa kike Grace. Nahitaji kutoka naye mimi na yeye tu nahitaji kumpeleka Super Maketi ili niweze kwenda kumnunulia zawadi yangu kabla ya ndoa yake. Nafanya hivi Mapema kwa kuwa nahitaji niwe mtu wa kwanza kumpatia zawadi Grace. Lakini mtoto wangu wewe fundi sana wa kuchagua watoto wazuri yani umenirithi mimi baba yako"Aliongea Mzee Ramadhani na kuongeza utani ili kuweza kumtoa wasiwasi Mwanae. Mzee Ramadhani alikuwa anahitaji kutumia huo upenyo ili kuweza kumkutanisha Grace na Frank kama Frank alivyomwambia "Baba Bwana!! Ila nashukuru kwa Kumjali Mke wangu na Kesho mimi nitamleta asubuhi kwako ili uje umtoe out. Ila Sasa hivi Nimemwekea walinzi kwa usalama zaidi" Aliongea Shawali. "Asante Mwanangu kwa kunielewa ila mimi sihitaji umlete asubuhi sana. Nataka umlete muda wa saa tano kwangu na sitaki waje na walinzi maana Mimi mwenyewe najiamini"Aliongea Mzee Ramadhani.
Yale Maneno ya Mzee Ramadhani kusema kuwa Anaitaji Grace aletwe kwake na amtoe out bila Walinzi Yalimfurahisha Sana Shawali. Yeye hakujua kama Mzee Wake alikuwa anahitaji kumkutanisha Grace na Frank ili kuja kuongea naye. "Baba Bwana yani wewe huwa Unajiamini Sana. Ok mimi nitamleta tena bila Walinzi ila uwe makini baba usije kumkosa Mkwe maana Frank naye anaawinda"Aliongea Shawali kumwambia Baba yake huku akicheka bila kujua mtu ambaye alikuwa anamtilia Mashaka alikuwepo ndani ya Nyumba yao. Baada ya Maongezi mengi Frank aliondoka huku akiwa na Furaha mbaya. Kitendo cha baba yake kukubali ndoa yao ifungwe Juma tano ya wiki ijayo kilimfurahisha Sana. Hapo alihisi sasa Muda wa Kuhangaika kuhusu Grace ndio unaenda kuishia pale pale. Yeye Hakujua kabsa Game ambayo ilikuwa inachezwa na baba yake kuwa ilikuwa hatari. Baba yake alikuwa anahitaji kumuonyesha mwanae Maovu yake ambayo alikuwa anafanya tena mbele ya watu. Afande Koboko Baada ya Kuachiwa na Afande Sophia kwa kweli Alimshukuru Sana Mungu huku akiapa lazima atafute Ushaidi ambayo utamfanya Sophia kumuachia na kumfunga Afande Mkuu wa jeshi la Polisi. Yeye alihisi kama atapaata Ushaidi na Kumpelekea Sophia basi ile Video ambae sophia alichukua hata ipeleka na yeye atakuwa Huru. Mawazo ya Afande Koboko yalikuwa yanautofauti Mkubwa na Mawazo ya Afande Sophia. Sophia yeye alikuwa anahitaji kuwa Funga wote kuanzia Shawali , koboko, afande Rama pamoja na Mkuu wa Mkoa. Ila alitumia ile mbinu ya kumshawishi Afande Koboko kuwa atafute Ushaidi ili yeye Amsamehe kwa kurahisisha tu kazi ya kupata Ushahidi wa Kumfanya Mkuu wa Jeshi la Polisi kuwa na Hatia. Baada ya kutoka nyumbani kwa Suzani huku tayari akiwa Amefeli mtihani wa kuwauawa suzani na Aisha Afande Koboko moja kwa moja aliondoka kuelekea kwa Mkuu wa jeshi la Polisi. tayari Camera yake Ndogo Mfano wa Saa ambaye alikuwa amepewa na Sophia ilikuwepo Mkononi mwake. Alichokuwa anataka ni siku hiyo hiyo kukamilisha mchezo wala hakutaka kuchelewesha maana alihisi isije dili likayumba na Sophia akabadilisha maamuzi. "Naona Umekuja kijana Wangu mwenzako mpango wake wa kumuua Frank na baba yake Umeshindikana Vipi wewe umefanikiwa"Aaliongea Mkuu wa Jeshi la Polisi baada tu yakuona Koboko karudi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Yeye alikuwa Anaongea hakujua koboko alikuja kivingine na tayari camera yake alikuwa ameitegesha. "Hapana Mkuu mimi sijafanikisha kuna Upinzani Mkubwa umetokea lakini Mkuu hivi kwa nini wewe unataka hawa watu wafe"Aliongea Koboko yeye wala hakuwa na wasiwasi maana alijua sauti kamwe haiwezi kumfunga mtu na alikuwa na uwezo wa kukataa kama ile haikuwa sauti yake maana ile camera mkononi wakati anaongea alikuwa ameielekeza kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Arusha. "Kijana hivi unataka niongee Mara Ngapi, Naahitaji Wafe hao kwa Sababu ya pesa, Pesa nyingi Sana tunapewa na Shawali. Pia Frank nataka Afe maana atakuwa anajua kama na mimi nahusika kwenye mipango ya yeye kuwekewa Madawa ya kulevya. Nakuomba Kawauwe hawa watu haraka kabla Mpango haujaharibika. Wewe kama unaashindwa kuwaua niambie ili hiyo kazi nikafanye mimi hivi unafikili mimi nitashindwa kuwaua. Labda nikwambie kitu Kimoja ambacho hukijui hivi unafikilia kwa nini mimi nimekuwa tajiri haraka na unafikilia kwa nini Wanajeshi wengine wanawahi kutajirika na wengine hakuna. Wakati nikiwa mwanajeshi wa kawaida niliua watu wengi sana na kujipatia pesa. Pia wanajeshi ndio tunaongoza kwenye matukio makubwa hasa ya wizi wa pesa nyingi kuvamia maduka na bank zenye pesa. Hivyo usinione hivi ninakitambi na nabadilisha Gari kila Muda zamani niliua sana. Hivyo basi na wewe unatakiwa kuua ili uwe kama mimi Ua kijana wangu wala usiogope sisi ndio tunashikilia Sheria hivyo lazima itakulinda na ipo siku utakuja kuwa Mtu mkubwa sana. Unajua hata Mimi hadi kuwa mkuu wa jeshi la Polisi arusha kuna kazi ya mauaji nilifanya tena nilitumwa na Kigogo wa Serikali. Sasa hata wewe endelea kumaliza watu kila unapotumwa na watu wakubwa ipo siku utakuja kutoboa"Aliongea mkuu wa jeshi la polisi kwa Urefu kabsa bila kujua kama alikuwa anajichoma. Yale Maneno ya Mkuu wa mkoa yalimfanya Koboko kuanza kucheka kwa Furaha maana alijua picha ngumu yenye majambazi hatari ameweza kuekti bila hata kushituliwa bega. "Mkuu haya Maneno ambayo umeyaongea ni matamu sana kwangu nazani nitakulipa kwa wema huwezi Amini. Kitu ambacho nitakufanyia kwa kweli mwenyewe utakuja kufurahi huku ukishangaa huu uwezo nimeutolea wapi"Aliongea Koboko kimafumbo huku akicheka. Afande Mkuu alipoona Koboko kaongea vile yeye alifurahi labda alihisi Koboko ndio anaenda kumaliza kazi yake. Alichofanya alimsogelea akampiga piga kwenye bega lake kisha alimwachia mpunga kama milioni mbili ili kumpa motisha wa kufanya ile kazi na yeye aliondoka. Kesho yake Asubuhi muda wa Saa mbili shawali aliamka na kuanza kujiandaa ili kwenda kumchukua Grace kumleta kwa Baba yake Kama alivyoambiwa na Mzee. Wakati Shawali akiwa anajiandaa huku nako mzee alikuwa anajiandaa Maana alikuwa na Mapango Mwanae akitoka tu na yeye anamtoa Frank na kumpeleka sehemu kisha anarudi anamsubilia Mwanae shawali amlete Grace kisha anamchukua na Grace anaenda kuwakutanisha na Frank. Kichwani mzee alikuwa anawaza ni mbinu Gani atumie ili Grace asigundue kama yule Mzee wapo pamoja na Frank. Maana kama Grace angegundua kama yule mzee alikuwa na ushirikiano na Frank lazima angemwambia mume wake kitu ambacho kingefanya Mtego wake kufyatuka kitu ambacho alikuwa hataki kitokee. Muda wa saa tatu kamili tayari Shawali alishamaliza kujiandaa alimuaga baba yake na kutoka huku akimwahidi saa nne na Nusu atakuwa ameshamleta Grace nyumbani. Ili kumuhakikishia baba yake alimwambia kabsa kama walishaongea na Grace na amekubali kutolewa out leo. Baada ya Shawali Kuondoka Mzee alienda kumchukua Frank na kwenda Kumpakia kwenye Gari kisha waliondoka kumpeleka Selena Hotel. Huko ndiko alipanga kwenda kumkutanisha na Frank ila bado hakujua atawakutanisha vipi. "Sasa Mwanangu Mpango wa kumuona Grace umeshakamilika na Saa tano kamili ndio utamuona. Sasa mimi bado sijajua Njia gani utatumia kumuona ili asigundue kama wewe upo na mimi maana akigundua kitaharibika"Aliongea baba yake na Shawali huku akiongeza speed ya Gari amfikishe haraka Frank selena hotel ambayo ndani ilikuwa na super maketi ili awahi kurudi. "Hilo Mzee wala lisikupe wasiwasi wewe kama unabastora naomba nipe"Aliongea Frank maneno ambayo yalimshitua mzee Ramadhani. Mzee Ramadhani alimwangalia Frank kwa makini kisha hakuwa na Wasiwasi na yeye hivyo alimpa frank bastora. "Unajua mwanae hana Kosa Mzee Ramadhani ila wewe ndio unamAkosa maana hukumfunza mwanao kuwa na nidhamu. Unajua wahenga mimi nahisi walikosea sana methali yao waliosema asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na Ulimwengu. Mimi nahisi mzazi anatakiwa kuwa makini kuhakikisha Mwanae anakuwa na tabia nzuri. Sasa kama wewe umeshindwa kumfunza Mwanae shawali tabia nzuri na kufikia kutuzurumu sisi wannyonge unaonaje nikaanza na wewe. Ndio nahitaji kukuua kwanza wewe ili kumuonyesha Shawali ni kiasi gani ninahasira na yeye"Aliongea Frank Kisha alikoki pisto ambayo alipewa na Mzee Ramadhani kisha alielekeza kwa mzee Ramadhani tayari kwa kutaka kumpiga.
Kwa kweli yale Maneno ya Frank yalimshitua Sana Mzee Ramadhani. Mzee Ramadhani alimwangalia Frank kweli alimkuta yupo Siliasi na Amekunja uso kabsa tayari kwa kutaka kumpiga Risasi. "Ni kweli Mwanangu hata Mimi Najua kama Mwanangu sijamlea katika Malezi Bora. Hicho ambacho unataka kukifanya Mwanangu Upo sahihi. Wewe si Unataka kunipiga Risasi kumuonyesha Shawali Kuwa ni kiasi Gani Unahasira naye. Basi ngoja nipaki Kabsa Gari ili unipige Risasi taratibu wala watu wasisikie pia Wewe usipate Madhara yeyote"Aliongea Mzee Ramadhani huku kweli alipunguza Gari Hatimae alipaki na kuinamisha kichwa chake chini kusubilia kupigwa risasi na Frank. "Wewe Mzee Hebu Amka bwana nitakupigaje Risasi mzee wa watu waakati huna hatia yeyote. Umeniuliza ni Mbinu Gani tutatumia kuweza kunikutanisha na Grace bila Grace yeye kugundua hii ndio mbinu natakiwa kutumia"Aliongea Frank Maneno yaliyomfanya Mzee Ramadhani kuamka na kumwangalia Frank kwa mshangao. Mzee Ramadhani yeye kwa njinsi ambavyo alimuona Frank aliamini kabsa anataka Kumpiga Risasi. Hivyo hata alipomuona Frank akiongea huku akicheka ilibidi kushangaa. "Bado Sijakuelewa Mwanangu Frank hiyo mbinu gani sasa mbona mimi bado Giza"Aliongea tena Mzee Ramadhani kutaka Ufafanuzi zaidi. "Wewe twende Mimi ukanishushe Selena Hotel kama Ulivyosema. Ukinishusha Pale wewe utarudi kwenda kumchukua Grace. Ukienda kumchukua Grace na Kuja naye mimi nitatokea pale selena kama mtu mwenye shida nahitaji kukuuliza kitu ukifungua tu kioo cha Gari nitakuteka na kukwambia ushuke kwenye Gari. Wewe Utaashuka kwenye Gari na kuniacha mimi na Grace. Ukishashuka kwenye Gari wapigie simu polisi kisha utakuja nae pale. Ila uhakikishe unaniacha muda wa dakika kumi na tano ndio Utakuja na hao Polisi. Ukifika pale utakuta mimi nimeshaongea na Grace pia nitakuwa nimeondoka hivyo Grace hataweza kugundua kitu chochote. Atahisi mimi nilitokea tu wala na wewe hukujua"Aliongea Frank kumueleza yule mzee. Yale maneno ya Frank yalimfanya mzee Ramadhani kuanza tu kucheka maana ilikuwa ni mbinu babkubwa. Baada ya Mzee Ramadhani kumuelewa Frank ambacho alikuwa anamanisha aliwasha Gari na kuliondoa kuelekea Selena Hotel. Baada ya muda wa dakika kumi na tano tayari Mzee Ramadhani alishamfikisha Frank Selena hotel na kumchukulia chumba kisha aliondoka tena kumfuata Grace. Koboko baada ya kuhakikisha Ushaidi alikuwa naye Mkononi kesho yake Asubuhi sana alimtafuta Sophia ili kumpa. Kwa kweli hakutaka kabsa kuchelewesha maana alijua kama Sophia wakibadilisha mbinu atakuwa kwenye wakati Mgumu. Alichofanya alimpigia Simu na kumwambia Wakutane nyumbani kwa Suzani na walipokutana alimkabizi ile video na Sophia alimpongeza kwa kazi nzuri na kumwambie yeye amejitoa kwenye kesi anatakiwa kuwa huru. Kwa kweli Koboko alivyosikia vile alifurahi sana maana kile kitu kilikuwa kinamtesa sana. Siku hiyo Aliamua kurudi nyumbani kwake Mapema kwenda kujipumzisha wala hakutaka kabsa siku hiyo kwenda hata kituoni kazini. Sophia alipopata ile camera moja kwa moja alienda nyumbani kwake na kwenda kuwasha na kuanza kungalia. Kwa kweli yale Maneno ya Mkuu wa jeshi la Polisi mkoa wa Arusha ambayo alikuwa anayaongea kwenye ile move yalitisha. Kile kitendo kilimfurahisha sana Sophia na kujua sasa huu ndio Muda wa kuwafunga hawa watu wote. Kupitia ule ushaidi kwa kweli angepeleka Mahakani hata Wangehonga pesa kiasi gani ilikuwa Vigumu kuweza kuachwa. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Mzee Ramadhan aliporudi nyumbani kwake alikuta Bado Shawali alikuwa hajarudi. Kile kitendo kilimfurahisha maana alitaka Shawali Amkute nyumbani Ili asimshitukie hata Kidogo. Alipofika nyumbani wala hata dakika kumi hazikupita Shawali walishafika na Grace. Walipofika kwa kweli Shawali alikuwa na Furaha mbaya alimkabidhi Grace kwa baba yake na yeye aliwasha gari na kuondoka kuelekea Kazini kwake. Mzee Ramadhani alimchukua Grace na yeye wakaenda hadi kwenye Gari na Kupanda Safari ya kuelekea Selena Hotel ilianza
Ndani ya Gari Mzee Ramadhani Walikuwa wanapiga Stori na Grace. Grace Muda wote alikuwa anamsifia Mume wake Shawali bila kujua kama Mzee Ramadhani alikuwa amechukia kabsa. Mzee Ramadhani yeye hakutaka kumzuia binti kuongelea lile Jambo maana alikuwa anajua kabsa kama binti yule dawa za kienyezi ndizo zinamfanya vile kama alivyowahi kuongea na Grace. Hadi Muda ule Mzee Ramadhani bado alikuwa hajapata Uhakika mzee Mwenzake Oska aliuawa au bado alikuwa Mzima maana kuna Muda alikuwa anampigia Simu na alikuwa hapatikani. Ambacho Aliamua ni kuchukua Simu yake na Kumtafuta Tena Mzee Oska. "Mzee Ramadhani Unataka kuniingiza tena kwenye mtego wa kufa siyo. Muda ule umenipigia Simu tukutane kumbe ulikuwa na Mpango wa kumtuma Mwanao aje kuniua. Tena Mwambie Mwanao mimi haniwezi na akiendelea kufatilia Maisha yangu atakuwa wa kwanza kufa na kuniacha mimi. Unajua Mimi Bindamu wananishangaza Sana Mwanao Kamuondolea Mwanangu Mke kisha Kampeleka gerezan lakini watu tumetulia. Hata Kutulia sijui anaona tunafaidi sasa ameanza kutafuta na roho zetu. Tena Mwambie Shawali bado mtoto hana Uwezo wa kutoa Roho ya Mzee Oska"yalikuwa ni Maneno ya Mzee Oska ambayo yalikuwa yanasikika kwenye simu. Yale Maneno kwa kweli Yalimchoma Mzee Ramadhani maana hakupewa hata Muda wa kuongea. Baada ya kuona Mzee Mwenzake anatema cheche sana alikata simu huku tayari alishapata Jibu sahihi kama Mwanae alienda kwenda Kummaliza baba yake na Frank. Alipogundua vile alihitaji kuhakikisha kama Mwanae alienda kituoni tena kwenda kumtafuta Frank. Alitaka kufanya hivyo ili kuthibitisha usemi wa Frank kama ulikuwa wa kweli Maana Frank alishawahi kumwambia kuwa Shawali anataka Kumuua baba yake pamoja na yeye mwenyewe Frank. Ili kupata Majibu Sahihi aliamua kumpigia Mkuu wa Magereza kuulizia kama mwanae Shawali alifika pale. "Kama Ulivyoota Mzee Wangu baada tu ya wewe kuondoka na Frank Mwanao Shawali alikuja huku akisema anahitaji kumuona Frank waongee naye Anahitaji Kumsaidia. Mimi hilo Deal nilishalisoma hivyo nilimwambia kuwa Frank katoroka. Huwezi Amini baada ya kumwambia vile Mwanao alishituka na kunyong'onyea sana. Sasa mimi nikawa nashangaa kama mtu ulikuwa unahitaji kumsaidia kutoka ndani na umekuta katoroka si ulitakiwa kufurahi na siyo kushituka. Sasa baada ya kumpa taarifa zile huwezi Amini Dakika kumi mbele Mkuu wa Jeshi la Polisi katia Team na kutoa Amri Frank atafutwe popote pale na aletwe akiwa Mzima au amekufa. Hivi ninavyokamwimbia Mzee Wangu muweke Frank vizuri ili watu wasimuone maana kama wakimuona wakamkamata ikajulikana kama mimi na wewe tulimtoa maisha yangu yatakuwa hatarini. Wewe sawa hutakuwa hatarini kwa kuwa anayefanya si Mwanao upande wangu naweza kumfuata afande Mwenzangu Joshua kitu ambacho sipendi kabsa kitokee"Alieleza Mkuu wa Gereza kwa upana. Yale Maneno kwa kweli yalizidi kumchanganya Mzee Ramadhani na kuanza kuona kazi ambayo ilikuwa mbele yake ilikuwa hatari. Mwanzoni alikuwa anaona kazi rahisi ila kwa muda ule alianza kuona kazi iliyopo mbeleni kwake siyo ya kawaida. Pia yale Maneno ya Mkuu wa Gereza yalianza kumtia Wasiwasi maana muda ule Frank alikuwa nje na kama anasakwa huenda angekuwa hatarini zaidi. Mzee Ramadhani alichofanya ni kuongeza Mwendo kasi wa Gari ili kuwahi sehemu ambayo alikuwepo frank wafanye alichokita kisha amrudishe Frank Nyumbani kwake kwa Usalama zaidi. "Baba Naona upo busy Sana Simu za Ofisini hizo"Aliongea Grace baada ya kumuona mzee Ramadhani kafululiza kuongea na Simu huku wakati wanaongea sura yake na Furaha ilikuwa inatoweka. "Ndio Mwanangu biashara hizi si unajua biashara usipokaza kila siku utakuwa unalia shoti tu"Alijibu mzee Ramadhani kwa Umakini kuhakikisha Grace hatamuhisi kwa kitu chochote kile kibaya. Baada ya mwendo kama wa daki kumi hivi tayari Mzee Ramadhani alishaiigia Selena Hotel. Alipofika Selena Hotel kama Kawaida alisimamisha kwanza Gari na kushusha Pumzi kabla ya kushuka kwenye Gari. Aliposimamisha tu Gari Frank tayari alikuwa ameshawaona hivyo aliondoka kwa kasi na kwenda kwenye lile gari. Muda ule Frak alikuwa amevaa kofia kubwa na miwani miusi hali ambayo ingekuwa ngumu mtu kumfahamu. Alipofikia kwa mzee alichungulia kama anataka kuongea naye kitu. Mzee Ramadhani alipoona mtu anachungulia Moja kwa Moja alijua ndio Frank hivyo alishusha kioo kumsikiliza. Aliposhusha kioo palepale Frank alitoa pisto yake na kumnyoshea Mzee Ramadhani. Kile kitendo Grace alikiona na kumfanya kuanza kutetemeka. "Jamani naomba usimuue Baba yangu chukua kitu chochote unachotaka ila Mwache mzee wangu akiwa hai"Aliongea Grace huku akitetemeka. "Mzee Kama unahitaji Usalama Wa Maisha yako nakuomba Shuka kwenye hii gari haraka"Aliongea Frank huku akiwa kama mtu ambaye anataka kufyatua Risasi. Mzee Ramadhani na yeye alipoambiwa vile alianza kushuka Taratibu na kujifanya anatetemeka ili kumfanya Grace asiisome ile picha. Baadae mzee Ramadhani alishuka na kutoka Nduki kumwachia Frank kuzama ndani kuongea na Grace.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya Mzee Ramadhani Kukimbia na Kumwacha Frank pale Moja kwa Moja Frank alipanda kwenye Gari na kufunga mlango wa Gari ili Kuongea Vizuri na Grace. Muda ule Grace kwa kweli alikuwa anatetemeka sana maana kasi ambayo aliingia nayo Yule Mtu haikuwa ya Kawaida. Baada ya Kuingia Kwenye Gari Frank alivua ile kofia ambayo alikuwa amevaa na Miwani yake Miusi ndipo Grace alimuona na kumfahamu. "Umekuja kufanya nini Humu, umekuja kuniua haya Niue basi. Maana taarifa nimeshapewa Kitambo na Mume Wangu Shawali kuwa Umetoroka Gerezani unahitaji kuniua"Aliongea Grace kwa Kujiamini kabsa. Sijui kwa nini Wakati akiwa bado hajamfahamu yule mtu alikuwa anatetemeka Sana ila alipomuona kuwa ni Frank woga wote uliyeyuka na kuanza kuona hali ya kawaida sana. "Grace nitakuuaje wewe Wakati Unajua wewe ndio Malkia wa Moyo wangu. Grace nini kimekukuta mpenzi wangu maana umebadilika sana mke Wangu. Kumbuka tulipotoka Grace mimi na wewe enzi zile tunasoma shule ya Sekondari Sanya Juu. Kumbuka ahadi ambayo ulinipa kuwa nitakuja kukuoa. Mimi Bado nakupenda Grace nahitaji kukuoa. Sawa Bikra ambayo nilikuwa Naaisubilia Mimi Goodluck amekuzibua ila Nitakuoa hivyo hivyo Maana nakupenda Tafadhari naomba Rudisha Moyo wako nyuma na kumbuka tulikotoka"Aliongea Frank kwa Sauti ya Huruma huku dhahili akionekana ni mtu ambaye kama akiendelea kuongea si Muda machozi yataanza kumtoka. Cha ajabu yale Maneno ambayo Frank alikuwa anaongea kwa Grace ilikuwa kama anasikiliza comedy maana frank alipoacha kuongea kusubilia Grace Angejibu nini alishitukia Grace akicheka sana. Kicheko cha Grace kilionyesha kuwa Frank ambacho alikuwa anakiongea ni Komedy tupu. "Yani Frank wewe unanichekesha kweli bado tu Unaamini kuwa Mimi nitakuwa mchumba wako hivi ulivyo. Hivi inamaana Maneno ya Wazazi wangu wewe Hukusikia kuwa wanaitaji Mtoto wao aolewe na mtu tajiri. Sasa wewe kiribatumbo utanipeleka wapi mimi kama siyo kwenda kunichakaza tu. Shoping moja ya Shawali inawalisha mwezi mzima kwenye ukoo wenu alafu uniambie eti kumbuka tuliko toka. Hiyo ya kukumbuka tulikotoka nenda kaandike historia watakuja kusoma kizazi kijacho. Frank kama huelewi Falsafa ya Mapenzi inavyosema acha mimi nikueleweshe, Siku zote Mpenzi wako wa Kwanza ni Mpenzi wa kukulea na kukuonyesha Uzuri wa kupendana na Kufanya mapenzi kwa Jumla ingawa wewe hukufanya mapenzi na mimi. Hivyo kamwe mchumba wako wa kwanza hawezi kukuoa. Mchumba mzuri ambayo hutimiza malengo ni wapili au watatu ndio maana karata ya Mwisho uliyoramba kwenye mchezo wa kujitoa ni Jokel na mwenzako shawali karamba A hivyo acha kunifatilia acha niolewe na Shawali"Aliongea Grace kwa kirefu zaidi kisha alianza kumcheka tena Frank. Yale Maneno ya Grace kwa kweli yalizidi kumuumiza Frank hakutegemea kama Grace yule ambaye mwanzo alikuwa anampenda hadi kufikia kulia leo angeongea maneno ya upuzi kama ule. Wakati moyo ukiwa unamuuma Pale alikumbuka Maneno ya Goodlucky kuwa mama yake alimwendea Grace kwa Mganga ili ampende shawali na kukuchukia wewe. Yale Maneno kwa kweli yalimfariji kidogo Frank na kuelewa huenda hapa siyo Grace anaongea. "Grace nahitaji kumaliza Mchezo hapa hapa naomba utanisamehe Sana kwa hiki ambacho nitakifanya. Grace natambua sana kama unanipenda ila sasa hivi dawa ambazo mama yako alikuendea Kwa Waganga ndio zimekufanya uwe hivi. Inaniuma Sana na sikutaka kufanya hivi ila Sina jinsi. Grace sipendi nione ukiolewa na mtu yeyote yule ndio maana nafanya hivi. Maisha yangu siwezi kuishi huku nikiwa nakuona Grace ukiwa unaishi na mtu Mwingine. Nakupenda Grace pia Utanisamehe Sana kwa hiki ambacho nitakifanya. Sina Jinsi Grace nahitaji kukuua na mimi nijiue ili Tuondoke pamoja kama kuna maisha kule mbeleni tukaendeleze. Hapa Duniani Mapenzi yetu yamekuwa na Upinzani mkubwa. Mama yako hanipendi na hanitaki hadi anafikia kukuendea kwa Mganga. Sasa Ngoja nimuonyeshe Mama yako kuwa alichokuwa anakifanya ni Ujinga maana atakukosa. NISAMEHE GRACE kwa hiki ambacho naenda kukifanya nataka nikuue wewe na mimi nijiue"Aliongea Frank na kutoa tena pisto yake huku machozi yakiwa yanamtoka na amechanganyikiwambaya mbaya. Muda ule kwa kweli Frak ambacho alikuwa anawaza ni Kumuua Tu Grace maana aliona Grace kamwe hawezi kumuelewa maana Dawa zilikuwa zimemzidi. Upande wa Grace alipoona Frank kachomoa pisto huku akisema yale maneno kuwa atamuua Woga ulimtawala mbaya. Dalili ambayo aliiona kwa Frank alihisi kweli frank anataka kumuua
Muda ule grace alikuwa anatetemeka mbaya maana alihisi kifo anakiona vile vile kinakuja. "Frank nakupenda tafadhari naomba Usiniue kweli Mimi ni Mjinga ila nilikuwa nakupima kuona kiasi gani unanijali hivyo please naomba usiniue nakupenda"Aliongea Grace. Grace alikuwa anaongea yale Maneno siyo kwamba alimpenda Frank bali alikuwa anataka kunusuru maisha yake maana aliona kama akileta mchezo atakufa. Frank aliposikia yale Maneno ya Grace naye alicheka kwa Dharau kama Mwanzo Grace alivyomcheka. Aliona Grace anaongea yale Mambo kama njia ya kujitetea Asife. Frank hakutaka kurudisha Mawazo yake nyuma kile ambacho alikuwa Amepanga ni Kumuua Grace na yeye kujiua. Alikoki kwa Mara ya Mwisho Vizuri bastora yake na kumuelekezea kwa Grace. " Najua hayo unayoongea hayatoki ndani ya Moyo wako yanatoka kwenye ncha ya ulimi tena Machungu. Unaongea hivyo ili kuweza kujiokoa kufa siyo. Ok kama unanipenda acha tukaendeleze mapenzi yetu sehemu nyingine ila siyo kwenye hii dunia iliyojaa watu wabaya kama mama yako pamoja na Shawali"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Aliongea Frank kwa mara ya Mwisho huku Muda ule tayari alikuwa ameshika bastora yake imara tayari kwa kutaka kumua Grace. Muda ule Frak Jasho Mwili mzima lilikuwa linamtoka utafikilia alikuwa anacheza mpira. Hapo kweli Alikubali kama kutoa roho ya mtu siyo kitu cha Mchezo. Wakati Frank alipotaka kufyatua tu risasi kumpiga Grace alianza kusikia Vingora vya Gari la Polisi Moja kwa Moja aliona mzee anakuja kama alivyokubaliana. Ile hali ndio ilimfanya Frank kusita kidogo Kumuua Grace maana alihisi huenda akampiga na yeye akajipiga wakaokolewa na Wasife au yeye akafa na kumuacha Grace Duniani kitu ambacho alikuwa hataki kitokee. "Umepona Grace ila nitarudi kwa Mara nyingine sitaki kabsa uolewe na shawali"Aliongea Frank kisha alirudisha Pisto yake kiunoni akavaa kofia yake pamoja na miwani na kushuka. Aliposhuka kwenye Gari Moja kwa Moja alitoka hadi nje ya ile hotel nakupotea kabsa pale. Mzee Ramadhani alipokimbia pale kwa Frank yeye alitoka hadi nje ya ile hotel na kumpigia Simu Mkuu wa Magereza na kumueleza mpango mzima wa hali halisi. Hivyo alimwambia amtafutie kijana wake ambaye anamwamini waje huku ili awapeleke kwa Grace kama kwenda kumkamata Frank ili Grace asishitukie. Mzee Ramadhan alikuwa anajua watakapo mkosa Frank wale Askari hawatamfatilia zaidi pia yeye alikuwa anajua Frank chumba ambacho alikuwepo hivyo angemrudisha Grace nyumbani na yeye angekuja kumchukua Frank. Kweli yule mkuu wa Magereza baadaa ya kupewa Zile Taarifa alimtafuta kijana Wake siwema kwa njia ya Simu maana askari Magereza hawafanyi kazi ya kukamata waharifu wao ni kulinda wafungwa. Hivyo alimtafuta siwema ambaye alikuwa Mkuu wa kituo Majengo kwa Muda ule na kumpa hiyo kazi huku akimwambia Aende Selena hotel kwa kwa lengo la kumkamata Frank lakini akifika kule ahakikishe hamkamati Frank anamsikiliza mzee Ramadhani ambacho alikuwa anakitaka. Siwema alivyoambiwa vile na yeye aliandaa Askari wenzake na kupanda kwenye Defender na kuondoka. Kumbe Moja ya Askari waliokuwepo Pale alikuwa anaafanya kazi kama Mpelelezi Wa mkuu wa Jeshi la Polisi Arusha. Hivyo alipojua kama Wanaenda kwenye Deal la kumkamata Frank yeye alimpa taarifa mkuu wa Jeshi la Polisi. Mkuu wa Jeshi la Polisi aliposikia vile yeye aliandaa kikosi mara moja na kuelekea Selena Hotel. Yeye aliondoka kwa kasi ili kuwawahi Siwema ingawa alikuwa hajui kama Siwema wao walikuwa wanaenda kutia kama Ushahidi wa kumfanya Grace asimshitukie mzee Ramadhani. Mzee Ramadhani baada ya kuona King'ora cha Polisi alijua tayari Vijana wale Wamefika hivyo aliwafuata kuwapeleka kwenye Gari.cha Ajabu alibaki akiwa anashangaa alipomkuta Mkuu wa Jeshi la Polisi wapo kwenye ile Misheni. Wakati akiwa anashangaa ile Hali Alimuona Muona na Mwanae Shawali akishuka kwenye hiyo Defender
Kwa kweli kitendo cha Shawali na Mkuu wa Jeshi la Polisi kufika wa Kwanza kwenye Eneo la tukio kilimshangaza sana Mzee Ramadhani. Alishindwa kuelewa hawa Watu wamefahamu vipi kama kuna tukio hili la Frank kumteka Grace lilikuwa limetokea hapa. Upande Mwingine Mzee Ramadhni alihisi huenda Mkuu wa Magereza nayo kamsaliti maana yeye Alimwambia kuwa Siwema ambaye alikuwa Mkuu wa kituo Majengo ndio anakuja kuja kutia Ushaidi leo vipi waje Wakuu wa Jeshi la Polisi tena mbaya zaidi na Mwanae Shawali akiwepo. Upande Mwingine Mzee Ramadhani alihisi huenda tayari Sasa hata Mwanao atakuwa ameshajua mchezo hali ambayo itamfanya kazi yake kuwa Ngumu. Tayari Mzee Ramadhani alishacheza nusu ya kazi yake hivyo alihisi anaenda kushindwa kumalizia kama kweli Mkuu wa Gereza atakuwa amesanua Dili. "Baba yangu upo Salama, niambe Grace yupo wapi na huyu Mjinga kajuaje kama upo huku. Baba nilikwambia uje na Walinzi unaona sasa huyu mtu anaweze kuja kuawau wote pumbavu zake nikimshika sitakuwa na muda wa kumucha hai tena"Aliongea Shawali kwa hasira kumwambia baba yake. Yale Maneno ya Shawali yalimfanya baba yake Kugundua kuwa bado dili lilikuwa halijasanuka. Ila bado hakuelewa nani sasa kawaambia hawa watu waje pale kama siyo Mkuu wa Magereza. Muda ule Mzee Ramadhani alikuwa anaomba Frank awe ameshakimbilia kwenye chumba chake maana tayari Afande walikuwa wanaliendea Gari ambalo Grace alikuwepo pamoja na Frank. Wakati Afande wakiwa wanaliendea lile Gari kwa kasi Ving'ora tena vilianza kusikika na Hata Dakika mbili hazikupita Tayari waliingi Afande ambayo wale Sasa ndio walikuwa wamepewa Dili na Mkuu wa Magereza. Mzee Ramadhani alipoangalia kwenye Zile Defender na Kumuona Afande Siwema ndio alizidi kushangaa na kujiuliza Maswali hawa Afande waliokuja na Shawali pamojo na Mkuu wa Jeshi la Polisi waliambiwa na nani. Hata Afande Siwema alipofika na kuona mkuu wake wa kazi yupo na ndio anasimamia hiki kitengo alibaki akiwa anashangaa. Hakutaka kushangaa sana zaidi alienda kwa Mkuu wake wakepeana salamu kisha hakuwa na jinsi na yeye aliruhusu afande wake washirikiane na Afande wa Mkuu wa Jeshi la Polisi kumtafuta Frank. "Siwema lakini mbona kama sielewi hii taarifa ni nani ambayo amewapa hawa. Unajua mnaniweka wakati Mgumu Frank anaweza kukamatwa tena. Frank akikamatwa anaweza hata kuuawa maana hata Mkuu wenu kuna vitu anavifanya na Frank anajua hivyo frank yupo kwenye hatari"Aliongea Mzee Ramadhani. "Mimi Mwenyewe nimeshangaa ila Mchezo mimi tayari nimeshausomo kuwa ninamtu kati ya hawa Afande Wangu Wanafanya kazi chini ya mkuu wangu. Yani huyu mtu amepewa apeleleze sehemu yeyote ambayo atasikia frank yupo atoe taarifa. Kuna Afande Nilimuona anaongea na simu huyo huenda ndio kaharibu. Mkuu wa Magereza kwa kweli wewe usimuhisi msaliti hata kidogo. Hapa kilichopo tuombe tu Wasimkamate Frank"Aliongea Siwema. Yale Maneno ya Siwema ndio yalimfungua akili hata mzee Ramadhani na kujua kweli kuna afande atakuwa alimzunguka siwema. Wale afande walipolifikia Gari walimkuta Grace akilia tu Frank hakuwepo. Hata walipomtafuta kwa Makini lakini bado hawakumuona. Baada ya kutafuta bila Mafanikio Shawali na Mzee Ramadhani wakiambatana na Grace walipanda Gari na Kurudi nyumbani kwao. Huku nako Afande waliamua kuondoka maana tayari frank hakuwepo. Baada ya Frank kutoka pale yeye Moja kwa Mjoa alinyooka Uwanja Wa Ndenge kwenye nyumba ambayo walikuwa wanaishi na Mpenzi wake Grace. Huko ndio alijua kuna Usalama maana alikuwa na uhakika kamwe Afande hawawezi kuhisi kama Frank ataenda huko. Frank alikuwa anatembea huku akiwa analia kabsa na alikuwa amechanganyikiwa mbaya. Kitendo cha Grace kumkataa mara ya pili ndio kilikuwa kinamchanganya sana. "Mzee Wangu Ramadhani utanisamehe kwa kwendo kinyume na Matakwa yako. Wewe unataka siku ya harusi ya Grace na mwanao Shawali ndio mimi nimuoe grace. Nahisi hilo kwangu limekuwa gumu maana siwezi kumuoa Grace huku akiwa hanipendi. Kuna kitu nahitaji kumfanyia Grace ili iwe Surprise kwa Mwanao maana yeye si anamtaka Grace kwa Nguvu zote. Siwezi kurudi tena kwako mzee Ramadhani ila kwenye Misheni yako ya harusi nitakuja. Najua utaumia Sana utakaporudi kwenye hicho chumba na kunikosa ila jua sasa na mimi nipo malindoni tena Namwinda Mkuu wa Jeshi la Polisi pamoja na afande Ambaye alimua Afande Joshua"Aliwaza Frank kisha alitoa pisto yake tena na kuibusua. Baada ya kutembea Mwendo Mrefu kutoka Selena hotel alikutana na boda boda ambaye alipanda na kumwambia amepeleke hadi Uwanja wa ndege. Alipompeleka Uwanja wa ndege alishuka kisha alianza kutembea kwa Mguu kuelekea nyumbani kwake. Hakutaka yule Dreva bodaboda ampeleke Moja kwa moja hadi nyumbani kwake maana alihisi huenda dili likaharibika. Alipofika nyumbani kwake alivunja kufuri mlangoni na kuingia. Alipoingia cha ajabu alikuta ile Nyumba ikiwa kwenye mazingira ya usafi sana ambayo ilionyesha kama kuna mtu alikuwa anaishi. Nyumba ambaye tangia atoke akiwa anamkimbilia Grace hakuwahi kurudi kuikuta ipo kwenye usafi ule alihisi kuna mtu anaishi. Upande Mwingine alihisi huenda Grace atakuwa anakuja nini lakini hakuwa na uhakika hata kidogo. Akiwa yupo pale anashangaa ile hali ya nyumba yake alihisi kama mlio wa Gari Unasikika nje ya nyumba yake kisha ngurumo za watu kama wanaongea zilisikika. Ile hali kwa kweli ilimshitua Frank na Kuhisi huenda afande walimuona hivyo wanakuja kumkamata. Kama siyo afande basi mtu ambaye alikuwa anaishi kwenye ile nyumba atakuwa amefika-CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Frank baada ya kusikia vishindo vya watu wakitembea nje na kuonekana kama wanakuja kuingia kwenye ile nyumba ndio wasiwasi ulizidi kumuongezeka. "Basi mimi ngoja niondoke aisha ila jitaidi kuwa makini maana Shawali anahitaji kukuua hivyo usipende kutoka toka sana hadi mimi nikupitie"yalikuwa ni Maongezi yakiendelea nje ambayo frank alifanikiwa kufahamu Sauti kuwa ilikuwa ya Goodlucky. Hapo sasa alipumua na kuanza kusogea mlangoni. Frank Muda ule hakutaka watu wengi wajue kama yupo mle zaidi ya yule ambaye angekuwa anaishi naye mle. Hivyo alisogea mlangoni makusudi ili Aysha akifikia ule mlango yeye amfungulie. Maana kama asingefanya hivyo na aisha aufikie mlango lazima angeshangaa huenda na kupiga kelele za kumuita tena Goodlucky maana Frank wakati anaingia si alivunja mlango. Baada ya Goodlucky kuagana na Aysha kweli aisha alisogea hadi mlango. Aliposogea aliona komeo la Mlango limevunjwa wakati akiwa anashangaa ile hali aliona mlango ukifunguliwa na Kubaki akishangaa kumuona mtu aliyefungua Mlango kuwa ni Frank. Kwa kweli Aysha alishangaa sana maana yeye alikuwa anajua kuwa Frank bado atakuwa yupo Magerezani. Frank na aisha waliingia hadi ndani na Frank alimuelezea hadi Mwisho Aysha hadi mbinu ambaye Mzee Ramadhani anahitaji kumuabisha Mwanae. Yale Maelezo ya Frank kwa kweli yalimfurahisha sana Aysha na kuhisi sasa Frank anaenda kumuoa Grace. Hata Frank alipomuelezea kuwa Grace hataki kabsa kuolewa naye lakini Aysha alimwambia Frank asijali hizo ni Dawa za kienyeji zitaisha na Mambo yataenda sawa. Aiysha naye alimueleza Frank mambo yote ambayo yanaendelea. Alimueleza Jinsi ambavyo wameshakusanya ushaidi wa kutosha kumfunga mkuu wa Jeshi la Polisi pia wanaushaidi wa kutosha wa Kumfunga Koboko ambaye alimuua Afande Joshua. Alimueleza kila kitu na namna ambavyo afande Sophia anafanya kazi yake kwa kutumia akili ya hali ya Juu. Baada siku tatu Tangia Suzani apelekwa Hosipitalini baada ya kujeruhiwa kwa Risasi aliweza kuruhusiwa. Afande Sophia wakishilikiana na Goodluck walimpeleka Suzani hadi Nyumbani kwake. Walipomfikisha Walimsihi asiwe na wasiwasi kabsa kazi ya kuwakamata watu ambaae walihusika na kifo cha Mume wake siyo muda itatimia. Wakati afande Wakiongea yale Maneno Upande wa Suzani mawazo hayakwepo kabsa pale. Yeye kwa kweli kichwani hakuwaza kabsa kuwakamata watu wale ambacho alikuwa anawaza ni kuhakikisha anawaua watu wawili ambae ni shawali na koboko. Yeye alihisi shawali ndio ambaye alituma watu kumuua mume wake hasa baada ya kugundua kama mume wake alikuwa anamsaidia Frank. Yeye kichwani hakuna kitu kingine ambacho alikuwa anakiwaza zaidi ya kumuua Shawali pamoja na afande koboko. Alihisi hawa watu kukamatwa na kufikishwa mahakani huenda hata kufungwa ipo siku watatoka na kamwe hatakuwa ameutendea haki moyo wake. Yeye aliamini kama watu watakufa basi atakuwa amelipiza kisasi kikubwa kwenye moyo wake na atalizika. Baada ya Afande Sophia na Goodlucky kukaa muda mrefu kwa Suzani hatimae wote waliondoka na kumuacha Suzani na walinzi tu. Afande Sophia alikuwa anaelekea Ofisini kwake kukamilisha Ushahidi wa kupeleka Mahakani kesi ya Frank upya na kupitia hiyo hiyo kesi wataonekana watu ambae walikuwa na hatia Frank atakuwa Huru na Shawali, mkuu wa Jeshi la Polisi naKoboko wao watakutwa na kesi ya kuua hatimae watafungwa. Goodlucky yeye alipotoka pale kwa Suzani yeye alinyoosha Moja kwa Moja kuelekea Sanya Juu Kilimanjaro. Goodlucky yeye kwa kweli alishajitolea kumlinda baba yake na Frank maana aliona kama Asipofanya Hivyo Mzee Oska anaweza kuuawa kitu ambacho hakupenda kitoee kingemuumiza Frank. Baada ya Sophia na Goodlucky Kuondoka Suzani naye aliamka na kuelekea chumbani ampo walikuwa wanalala na mume wake. Tangia Mume wake afe kwa kweli hakuwahi kuingia kwenye kile chumba. Hata walipokuja na kina Aisha alienda kulala chumba ambacho alikuwa analala mtoto wake ambae tangu baba yake afariki yule mtoto alichukuliwa na ndugu wa baba yake maana suzani na yeye si alitekwa. Alipoingia kwenye Chumba chake picha ya ukutani ambaaye alipiga na Mume wake wamekumbatia ilitua kwenye macho yake. Ile pichwa kwa kweli ilimkumbusha mbali na kujikuta akitoa machozi "Mume wangu Afande Joshua lazima nilipieze kisasi yani wewe usiwe na wasiwasi kabsa hawa watu nitawaleta kwako. Nikihakikisha hawa watu wamekuja kwako basi na mimi nitakuja kwako maana nimekumisi sana mpenzi wangu Afande Joshua"Aliongea Suzan huku akitaja jina la utani ambalo alikuwa anapenda kumwita mumewe. Suzani alijivuta na kwenda hadi kwenye Droo za kabati huko ndiko alijua mumewe alikuwa anahifadhi bastora hivyo lazima angekuta. Kweli alipovuta droo ya kwanza alikuta kuna bastora huku pembeni kukiwa na karatasi. Alichukua ile Bastora na karatasi ile ili kuisoma. Alifungua karatasi na kuanza kusoma ambayo ile karatasi iliandikwa hivi. "Mke wangu Sasa hivi maisha yangu yapo hatarin maana namsaidie Frank kumtoa kwenye kesi ambayo hahusiki. Kama nitakufa mke wangu unaatakiwa kuelewa kuwa kifo changu atakuwa amekifanya Mkuu wa Jeshi la Polisi pamoja na shawali maana wao ndio wanataka frank afungwe na wananiwinda kweli. Hivyo nikifa naaomba endelea kumsaidia Frank na karatasi hii mpelekee wakili wangu Mzee Maguma atakusaidia. Pia nimekuachia hiyo hapo na Bastora kwa ajili ya ulinzi wako si unakumbuka nilikufundisha nama ya kujilinda na kutumia hiyo bastora"Ile sms fupi iliisha. Ile Sms ilimfanya Suzani kulia zaidi kumbe mume wake alikuwa anajua kama atakufa lakini hakumwambia.
Kwa kweli Suzan muda ule alikuwa na huzuni ambao ulikuwa hauelezeki. "Mume wangu kwa nini hukuniambia kama kuna watu wanataka kukuua huenda ningekulinda. Wewe mwenyewe ulikuwa umenifundisha kutumia bastora ili nikulinde kwa nini sasa hukuniambia. Hivi Unajua ni kiasi Gani nimekumis Mume wangu. Nimekuelewa Mume Wangu nitafanya kile ambacho unataka hii Karatasi nitampelekea Wakili wako Mzee Maguma. Pia frank mimi nitamsaidia ili kutimiza kile ambacho umeniambia. Ndio nitamsaidia na Msaada ambao nitampa kamwe hatateseka tena Duniani maana naaenda kuwamaliza hawa watu wote ambao wanamsumbua Frank na waliokufanya uwe mbali na Mimi. Nikishawamaliza hawa watu sitakubali kuishi Maisha ya kipweke Gerezani nitakufuata huko uliko mume wangu"Aliongea Suzan kwa Huzuni huku akiwa ameikumbatia Bastora ambayo aliachiwa na Mumewe. Kwenye kichwa cha Suzan Muda ule alikuwa anawaza kuua tu. Yani muda ule alikuwa ni Mtu ambaye alikuwa amechanganyikiwa bila kuua mtu yeye aliona kamwe maisha yake hayataenda vizuri. Ambacho alikuwa Amepanga ni kuweza kuwaua watu wote ambao walimfanyia ubaya Frank pamoja na Mume wake kisha na yeye anafuata anajiua. Baada ya kulia kwa muda huku akiwa amekumbatia bastora baadae alirudisha tena kwenye Droo ile Bastora na kwenda kitandani akajitupia apumzike na baadae apange namna ya kuweza kuwamaliza hawa watu. Nyumbani kwa Mzee Ramadhani Shawali alikuwa hajamshitukia kabsa Mzee Ramadhani. Tangu Grace waonane na Frank zilikuwa zimepita kama siku tatu hivi. Polisi ambao walikuwa wanashirikiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi walishamtafuta Frank hadi walichoka lakini hata kuhisi tu kuwa Frank alikuwa mitaa flani ilikuwa hakuna. Muda ule kwa Mzee Ramadhani Maandalizi ya Harusi ya Mwanae Shawali CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Pamoja na Grace ilikuwa imepamba moto. Ndugu mbalimbali wa Mzee Ramadhani pamoja na Marafiki wake walishaanza kuingia nyumbani kwa Mzee Ramadhani maana zilishabaki siku tatu tu harusi ifanyike. Hivyo wale ndugu wa mbali kama Omani, Saudi arabia walishanza kuingia. Harusi ya Shawali na Grace kwa kweli ilikuwa Gumzo kwenye Jiji la Arusha na Tanzania kwa Ujumla. Watu wengine ambao walikuwa wapo mikoa mingine na walikuwa hawamjui shawali wala Grace ilikuwa kero kwao maana kila Muda kwenye vyomba vya habari haijalishi Redio, Magazeti Television ilikuwa ni Matangazo kuhusu ndoa ya Shawali. Pesa ambazo Shawali alikuwa Amemwaga kwenye vituo vya habari vile ndio vilifanya karibia kila Saa moja lazima Tangazo lake lisikike mara mbili. Mzee Ramadhani kwa kweli yeye alikuwa busy sana tayari mambo yake alishaweka vizuri. Tayari kwenye ile ndoa ukiacha Shekhe wa Mkoa wa Arusha ambaye alipanga kufungisha hiyo ndoa pia alishamuandaa Mchungaji ambaye alimueleza kuwa ataenda kufungisha ndoa tena kwenye hiyo hiyo harusi ya Mwanae. Alimwambia tu mchungaji kuwa kwenye ile harusi ya Mwanae pia kutakuwa kuna harusi ndogo ya Mwanae wakike anaolewa na mtu Mkristo hivyo ataenda kufungisha ndoa na yeye. Alichokuwa amekiongea mzee Ramadhani ilikuwa ni tofauti kabsa pale palikuwa na ndoa mbili sawa ila mwanamke alikuwa mmoja. Ambacho alikuwa anakitaka Mzee Ramadhani baada ya watu kukusanyika kushuhudia ndoa ya Mwanae Shawali angesimama na kuongea mabaya ya mwanae yote kisha Anamwambia Shekhe hii ndoa ya Shawali na Grace haipo tena na atampa ruhusua Mchungaji kumfungisha Ndoa ya Frank na Grace huo ndio Mpango ambao aliupanga Mzee Ramadhani. Licha ya mambo yake Kuwa Mazuri lakini bado alikuwa na Wasiwasi Mkubwa wa Kutokutimiza hiyo kazi Maana Tangia Frank waongee na Grace hakuonekana tena. Mzee Ramadhani alienda hadi Chumba ambacho alikuwa amempangishia Frank lakini hakumuona. Hata alipomtafuta kwenye simu bado hakupatikana. Kitendo cha Frank kutokupatikana ndicho ambacho kilikuwa kinamchanganya Mzee Ramadhani. Upande Mwingine alianza kuhisi Huenda Frank tayari alishakamatwa na Askari na huenda alishauawa maana ukimya ulianza kumshitua Mzee Ramadhani
Hakuwa na Njia Nyingine ile zaidi ya kuchukua Simu yake ambayo alizima tangia atoke Selena Hotel na kuiwasha Kwa lengo la Kuwasiliana na Mzee Ramadhani. Mzee Ramadhani kwa kweli baada ya kuona zimebaki siku mbili bila Mafanikio yoyote ya Kumpata Frank alikuwa amechoka na kukata tamaa kama vile alikuwa anaumwa. Mambo yote ambayo alikuwa amepanga aliona yanaenda kufel kitu ambacho alikuwa hataki kitokee kabsa. Bila kukamilisha kile ambacho alikuwa amekipanga alijiona mkosefu mkubwa kwa Mungu. Ili moyo wake uwe na amani na kujiona hana kosa Kwa Mungu mzee Ramadhani alipanga siku ya Harusi ya Mwanae Shawali ndio angetobao mabaya yote ambayo mwanae Shawali alikuwa anafanya pamoja na kuamuru Frank amuoe Grace. Wakati yeye akiwa anawaza yale tayari kulikuwa na watu wawili walikuwa na mawazo tofauti ingawa mmoja alikuwa angalau na mawazo ambayo yalikuwa yanafanana na mzee ramadhani. Huyu alikuwa ni Suzani yeye alikuwa anataka kwenda kwenye ile Harusi kwa ajili ya kumwaga Damu za watu wawili Koboko na Shawali kisha kumwacha Frank huru aweze kumuoa Grace ndio maana mawazo yake kidogo yalikuwa yanafanana na Mzee ramadhani ingawa utofauti ulikuwa kuua. Laiti Mzee Ramadhani angelijua kitu ambacho Suzani angefanya kamwe hata ile Harusi bora angesitisha au mwanae angefunga ndoa na Grace wakiwepo ndugu zake tu pamoja na Mchungaji. Mtu mwingine ambayo alikuwa na mawazo tofauti na Mzee ramadhani alikuwa ni Frank. Frank kwa kweli baada ya Kumuuliza Grace Mara mbili na kujibiwa kuwa hataki kuwa na yeye hakuona umuhimu wa kumuoa tena Grace kama Mzee Ramadhani alivyomwambia. Yeye aliamua kufanya kitu cha surprise kwa Shawali, Grace pamoja na watu wote ambao walitakiwa kuhudhulia hiyo harusi. Hicho kitu hakuna ambaye alikijua maana ilikuwa ni Siri ya Frank. Hata Aisha ambaye ndio alikuwa anajua kama Frank ametoka jera hakuwa anajua zaidi Frank alimwambia tu kuwa anaenda kwenye hiyo Harusi kwa kwenda kukamilisha hatua za kumuoa Grace kama walivyopanga na Mzee Ramadhani. Mzee Ramadhani akiwa hana Raha kabsa huku akiwa yupo kwenye meza akipata kahawa ili kupunguza mawazo na wasiwasi aliyonayo mara Simu yake ilianza kuita. Muda ule kila Simu ambayo ilikuwa inaita mzee Ramadhani alikuwa anatoa kwa Kasi ya ajabu kuangalia kama ni Frank kapiga. Alipotoa ile Simu na Kuangalia kwa kweli moyo wake ulishituka mbaya alipoona mtu ambaye alikuwa amempigia ni Frank. "Mzee naomba kwanza unisamehe kwa kujificha bila kukupa taarifa. Labda nikwambie kitu kimoja ile siku niliona kama nitakaa kwenye kile chumba ambacho ulinilipia ningekamatwa. Hivyo mimi niliamua Kujificha ili nisikamatwe hadi siku ya harusi ambayo wewe unataka. Najua utakuwa umehangaika sana kunitafuta na kuanza kuhisi vingine lakini amini sasa mimi nipo mzima. Sikutaka kuongozana na wewe tena kwa kuwa nilijua huenda ningekamatwa na kukuletea matatizo. Sasa kwa hizi Siku mbili ambazo zimebaki waweza kuonana na mimi na kupanga kama wewe unavyotaka"Aliongea Frank kwenye simu. Kwa kweli Mzee Ramadhani aliposikia kabsa kama yule ambayo alikuwa anaongea kwenye simu alikuwa ni Frank alijihisi Raha hadi Mchozi ya Furaha yalianza kumtoka. Moja kwa Moja aliona kazi Ngumu ambayo alikuwa ameifanya anaenda kuimaliza. "Usiwe na wasiwasi mimi sina neno na wewe ila sasa hivi usinifanyie tena hivyo utaniua na Pressure. Kwa kweli nashukuru sana Frank kwa kunitafuta na mimi nahitaji tuonane sasa hivi Meridian Roge ili niweze kukuchukua na kukupeleka Shoping nikununulie vitu vyote vya harusi na pia tuje tuongee mambo kadha wa kadha. Mimi Frank nahitaji haki yako ambayo umedhurumiwa na mwanangu irudi kwako hicho tu ndio nataka mwanangu"Aliongea Mzee Ramadhani kwa huzuni ulioambatana na Furaha kali. Yale maneno ambayo aliongea mzee Ramadhani yalizidi kumuuma Frank maana Mzee ramadhani kile ambacho alikuwa anataka kilikuwa hakiwezi kufanikiwa. Baada ya Maongezi ambayo kila mtu aliamini amelizika walikubaliana kuonana Meridian Roge. Mzee Ramadhani walipomaliza tu Kuongea na Frank alitoka Moja kwa Moja chumbani kwake na Kwenda hadi Nje. Huko Nje kwa kweli alikutana na Umati wa Watu ambae ulikuwa busy kuanda ukumbi ambayo harusi ile Ingefanyika. Mzee Ramadhani hakutaka ndoa ya Mwanae sijui ikafanyikie msikitini maana alikuwa hataki mambo ambayo alipanga yatokee yafanyikie kwenye nyumba ya ibada ingekuwa siyo vizuri. Watu walikuwa wamendelee na kazi mbali mbali maana kuanzia hiyo siku ambayo zilikuwa bado siku mbili Harusi kufanyika watu wangelikesha mle kwa kula na kunywa maana watu wengi wa mbali walikuwa wameshafika hivyo Huduma zote wangelizipata mle ndani. Alipotoka nje na kushangaa kidogo hakutaka tena kuendelea kupoteza Muda alipanda kwenye Gari kuelekea Meridian Hotel ambako ndiko walipanga kwenda Kuonana na Frank. Huku Sanya Juu wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro baba yake na Frank mzee Oska wakiwa na Mke wake pamoja na Goodlucky walikuwa kwenye maandalizi ya Mwishoni tayari kwa Safari ya kuja Arusha kuja kusherekea ndoa ya Mwanao Frank. Yani Mzee Ramadhani tayari alishaenda hadi kwa Mzee Oska na kumuelezea kama ndoa ambayo inaenda kufanyika kwake siyo ya Shawali bali ni ndoa ya Frank na Grace hivyo aliwaambia Waje kwenye Harusi hiyo. Ili kuwahakikisha aliwatumia hadi Gari kwa ajili ya kwenda kubeba ndugu wote wa Frank kuanzia wazazi wajomba binamu yani ukoo wote ulikwepo hadi babu yake na Frank. Hivyo Siku hiyo Sanya Juu walikuwa wapo kwenye Maandalizi ya Mwisho maana kuna Gari nje ilikuwa inawasubilia. Ndugu wengine wote ambao walipanga kwenda kwenye hiyo Harusi walikuwepo wameshafika nyumbani kwa Mzee Oska wakijiandaa kwa ajili ya kuondoka kuelekea Arusha kwenye Harusi ya Mwanao Frank. "Aisha naondoka na nazani hatutaonana tena labda hadi kwenywe Harusi yangu. Ila mimi ningependa Sana kama utakuja kuolewa na Goodlucky maana ni Mwanaume mwenye mapenzi ya dhati na wewe ni Mwanamke mwenye mapenzi ya dhati. Naondoka leo naenda kuonana na Mzee Ramadhani tayari kwa kwenda kujiandaa kwa ajili ya ndoa"Aliongea Frank akimuaga Aisha. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Yale Maneno ya Frank kwa kweli yalimpa Raha Aisha maana Aisha alikuwa anahangaika hadi zamani kuhakikisha Frank anamuoa Grace maana alihisi kitendo cha Grace kumkuta wakifanya mapenzi na Frank kimesababisha kiasi kikubwa ndoa yao kutokufanyikiwa. Hivyo alipanga kufanya kila ambalo linawezekana Frank amuoe Grace. Hivyo alipoagwa kuwa Frank anaenda kwenye Maandalizi ya Mwisho kwa ajili ya ndoa yake hakuwa na Budi ya kuwa na furaha mbaya. "Ok kwa kuwa na mimi natoka acha leo nikupeleke hadi huko maana kutembea kwa miguu au boda boda siyo vizuri. Najua siku nyingi Sana hujapanda Gari yako tangia uitelekeze kule kwenye foleni ukimfukuzia Grace. Leo naomba nikupakie kwenye Gari yako nikupeleke hadi kwa Mee huyo kisha n Mimi niende kwa suzani kwa ajili ya Maandalizi ya kuwafunga hawa wajinga milele"Aliongea Aisha. Baada ya aisha kuongea vile Frank hakuwa na kipingamizi Walitoka hadi Nje wakapanda kwenye Gari lake na kuanza safari ya kuelekea Meridian hotel.
Frank akiwa ndani ya Gari alikuwa Mkimya Sana huku akitafakari mambo kadha wa kadha ambayo amewahi kupitia katika maisha yake. Kwa kweli maisha ambayo alikuwa amepitia baada ya kuanza kuishi na Grace asilimia kubwa yalikuwa yanatisha. Miaka mingi muda wote alikuwa Gerezani akitumikia kifungo ambacho hakuwa na hatia. Kwa kweli kila alipokuwa anakumbuka haya Mambo kichwa kilikuwa hadi kinamuuma na kuamini kama binadamu hana utofauti na Mnyama mkali kama Simba. Japokuwa binadamu hawezi Kung'ata lakini anaweza akakufanyia Jambo baya hafadhari ya kung'atwa na Simba. Maisha ambayo aliisha Frank yalikuwa yanatisha na haya yote yalisababishwa na binadamu mwenzake. Alienda Gerezani bila hatia kwa kusababishwa na binadamu mwenzake. Mke wake kipenzi ameondolewa na binadamu Mwenzake. Hivyo kwa yale Mambo ambayo alifanyiwa aliamini kabsa bora kuishi kwenye kundi la wanyama wanaotisha kama simba na Chui kuliko kuishi kwenye kundi la Watu lenye watu kama kina Shawali na Mkuu wa wa Jeshi la Polisi. "Mbona Frank upo kimya Sana unatafakari kitu gani"Aliongea Aisha baada ya kuona kimya kimetawala kwenye gari. "Nakumbuka Mengi sana Aisha, Unajua hii Gari ambayo wewe leo unaniendesha ni Gari ambayo baba yangu alininunulia kama zawadi ya kuelekea kumuoa Grace ambayo ingenisaidia kupiga misele ya hapa ha pale. Sasa unapiniona nipo kimya nakumbuka mbali sana aisha. Pia kitu chochote kibaya ambacho kitatokea kwenya Harusi yangu naomba hili Gari litakuwa mali yako pia vitu vyote nyumbani kwangu vitakuwa mali yako"Aliongea Frank. "Frank naomba Usioongee hivyo kwani hata sasa ndio unaenda kumuoa Grace na kuishi maisha ya kawaida. Pia hakuna kitu kibaya ambacho kitakukuta kwani kuna ulinzi wa kutosha kwenye hiyo Harusi ambaye tena walinzi ambao watakuwepo watakuwa wa Afande Sophia ambae wapo upande wetu wa kuhakikisha Shawali na Mkuu wa Jeshi la Polisi wanakatwa. Hivyo kuhusu usalama wako wala usiwe na wasiwasi kabsa"Aliongea Aisha. mwendo kama wa Dakika kumi hivi ndio walifika Meridian Roge. Walipofika hapa tayari walikuta mzee Ramadhani ameshafika. Aisha yeye hakusimama zaidi alimshusha Frank na kuondoka. Nyumbani kwa Suzani Maandalizi ya Mwishoni Mwishoni yalikuwa yanafanyika. Mkuu wa kituo cha Kambi ya pili cha Polisi Sophia alikuwa na afande wake mia moja ambao walitakiwa kwenda kulinda kwenye harusi ya Shawali. Wale Afande alishawakabizi kwa Koboko ambaye yeye angewapeleka kwenye jumba la mzee shawali tayari kwa ulinzi maana Koboko ndio ambaye alipewa kazi ya kuhakikisha ulinzi unakuwa Shwali kwenye nyumba ya Mzee Ramadhani na ndoa ifanyike vizuri. Kwa upande Wa Suzani yeye mambo yake yalikuwa yapo sawa maana Muda ule tayari bastora yake aina ya revolver ambaye ilikuwa na Risasi za kutosha ilikuwa kiunoni kwake kusubilia siku ya harusi. Kwa Upande wake kwa kweli siku alikuwa anaona haziendi maana alikuwa na hamu ya kulipiza kisasi. Kwa Bastora yake aina ya Revolver alikuwa na uhakika wa kuweza kumaliza mchezo mapema. Maana alikumbuka maelezo ya mume wake ambayo alikuwa anamuelezea kuwa ile Bastora huwa na Nguvu sana. Kama ukimpiga Mtu kwa kutumia ile Bastora hususani maeneo ya kwenye Kifua huwa Vigumu Sana kupoana maana hiyo Risasi ambayo inatoka kwenye Bastora inapoingia kwenye mwili wa binadamu husambaza kabsa sehemu hiyo ya mwili. Sophia yeye kwa kweli alikuwa na uhakika wa kumaliza kazi yake Vizuri. Yeye kwa kuwa walikuwa na mawasiliano vizuri na Mkuu wa Jeshi la Polisi kutokana na ufanyaji bora wa kazi yake basi alimualika na yeye kuja kwenye Harusi ya Shawali huku akisema kuwa mtu ambaye alikuwa anaolewa alikuwa ni mtoto wa mama yake Mdogo. Afande sophia walifahamiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kupitia baba yake ambaye alimualika Mkuu huyo kwenye Sherehe yake ya kustafu kazi ya kijeshi ambaye yeye alikuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha. Hiyo hiyo Siku wakati baba yake anastafu hiyo kazi ndio siku ambaye Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini alimwambie Mkuu wa Jeshi la polisi mkoa wa Arusha Amfanye sophia kama mkuu wa kituoa cha kambi ya Pili kama Shukrani yake ya kumtunuku baba yake na Sophia zawadi. Baada ya Sherehe kwisha Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini walipata muda wa kuongea Zaidi na Sophia na kufikia kumtongoza na kumtaka awe mke wake huku akimueleza mke wake wa kwanza alikuwa ameshakufa. Sophia hakukataa ombi la Mkuu wake zaidi ya kukubali na kuwa na Mahusiano ila alimuomba amuache kwanza miaka minne ndipo angemuoa. Hivyo Sophia alikuwa na uhakika kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania angekuja maana si alikuwa mchumba wake na alikuwa na Uhakika anampenda hivyo asingemwangusha. Hivyo kama Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini angekuwepo na kuja kuona mambo ambayo yalikuwa yanafanywa na Mkuu wa jeshi la Polisi Arusha basi asingepona. Hadi Muda ule tayari Sophia alishapewa taarifa kuwa Siku ya Harusi Asubuhi atakuwa ameshafika. Baada ya Frank kuonana na mzee Ramadhani walienda hadi kwenye Maduka ya nguo na Mzee Ramadhani alienda kumnunulia Frank Suti safi ya Harusi. Baada ya Shoping Hiyo waliondoka na Frank hadi nyumbani kwake ambapo alifanikiwa kumuingiza ndani kisiri bila mtu yeyote kuona. Baada ya kumuingiza ndani Frank yeye alitoka nje kusalimiana na Wageni mbalimbali ambao walifika. Moja ya Wageni ambayo mzee Ramadhani alikuwa anawasubilia kwa Hamu alikuwa mzee Oska baba yake na Frank. Shawali yeye hata alipomuona mzee Oska hakuwa na wasiwasi walisamiliana vizuri na kuomba msamaha huku akisema siku ile hakupanga kuwauawa alikuwa anawatishia tu. Shawali alikuwa hana wasiwasi na mzee Oska maana baba yake alishamwambia kama Mzee Oska naye atakuja maaana anataka ndoa yake shawali ifanyike vizuri hata wabaya wake wawepo. Laiti kama Angejua kama wale watu wamekuja kushuhudia Frank akimuoa Grace angeshawatimua. ..,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Ilikuwa siku ya Juma tano ambayo hiyo siku ilikuwa ya aina yake. Hiyo siku ndio ilikuwa siku ya Harusi ya Shawali akimuoa Grace kama watu wengi walivyokuwa wanajua pia ilikuwa siku ya Frank kumuoa Grace kama watu wachache ambao walikuwa wanajua. Pia hiyo Siku ndio ilikuwa siku ya Suzani kumuua Koboko pamoja na Shawali na hiyo Siri alikuwa anaijua yeye tu. Pia hiyo Siku ndio ilikuwa siku ya Frank kufanya Surprise kwa Grace, Shawali pamoja na watu wote ambao walikuwepo kwenye hiyo Sherehe na hiyo siku ndio ilikuwa siku ya Mzee Ramadhani kuvunja ndoa ya Mwanaw shawali na kuamua Frank amuoe Grace. Pamoja na Nyumba ya Mzee Ramadhani kuwa na pango Pana na ukumbi mkubwa ambao ulikuwa umetengenezwa lakini watu walijaa mpaka nje. Kila mtu alikuwa na hamu ya Kushuhudia ndoa ambayo ilikuwa inawasumbua kila Muda kwenye vyombo vya habari. Walinzi ambae waliwekwa kwa ajili ya kulinda wao wala hawakukagua hata mtu mmoja hivyo walisaidia kwa watu kama kina Suzani kuingia na vitu vyao vya moto aina Revolver kwa ajili ya kwenda kumwaga damu za watu. Sophia alikuwa amekaaa kwenye kiti cha mbele wakiwa na mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania akiwa anasubilia kwa Hamu boomu ambalo alitaka lilipuke lifanikiwe. Wakati Huku Harusi ikiwa inakaribia kuanza huku Wakili mzee Magumu alikuwa ndani ya Gari kuelekea Mahakani kwenda kufungua kesi upya ya Frank huku akiwa na Ushahidi wa kutosha. Alikuwa anajua kama akienda kufungua kesi upya ya frank na kuonyesha ushahidi wa kufungua ile kesi upya lazima Shawali , mkuuu wa jeshi la Polisi pamoja na koboko wangekamatwa na kuwekwa ndani. Alikuwa na uhakika na ule ushahidi wa video hivyo alikuwa anajua hadi kitu ambacho kingetokea
Kwa kweli Watu walikuwa wengi sana kwenye ule Ukumbi na Wote ambao walikuwa wamekaa walikuwa wamepigilia Suti mbaya na walikuwa wamependeza mbaya. Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini ambaye alikuwa Mpenzi wake na Afande Sophia hakuwa na Uzito kwenye ile Sherehe maana alialikwa na Sophia kwa Kudanganywa kuwa ambaye anaolewa ni Mdogo wake na Sophia ili tu ashuhudie kimbwembwe ambacho Kingetokea kwenye ile Harusi. Alipofika Ukumbini alipokelewa kwa Heshima ya hali ya Juu na Mkuu wa jeshi la Polisi nchini na kwenda Kukaa viti vya mbele. Ujio wa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ulimfanya Shawali kujiamini zaidi na kuhisi kutakuwa na Ulinzi imara. Grace na Shawali kwa kweli walikuwa wamependeza mbaya na kila Muda walikuwa watu wa kutabasamu tu kuonyesha ni kiasi gani walikuwa na furaha siku hiyo. Mama yake na Grace pamoja na baba yake mzee Mambo walikuwa wamekaa na wao kwenye meza ya kifalme kusubilia ndoa ya Mwanao kufanikiwa. Frank yeye alikuwa amekaa kwenye viti vya mbele huku akiwa amepigilia Suti safi miwani mieusi pamoja na ndevu za bandia ambazo zilitengenezwa lengo tu asifahamike. Kwa kweli kwa jinsi zile ndevu ambazo zilikuwa ndefu zilimfanya Frank mtu yeyote asimfahamu. Tayari Frank kwenye kiuno chake alikuwa na Bastora ambayo kama unakumbuka alipewa na Mzee Ramadhani kwa lengo la kwenda kumteka Grace na kuweza kuongea naye. Harusi ilianza kwa Mbwembwe Sana Huku Mtangazaji Michael Donald Maliga akianza kwa Mbwembwe Kwa Utambulisho. Kwa kweli ilikuwa ni Hurusi ya kuvutia Sana na kila Mtu alipendezeshwa nayo. Baada ya Utambulisho ndio CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Sasa Shekhe mkuu wa Mkoa wa Arusha alitakiwa Kufungisha ile Ndoa Rasmi na Sherehe ndio ingendelea zaidi. Baada ya Mtangazaji kumaliza Utambulisho alitaja tukio ambalo lilifuata kwenye ratiba yake kuwa ni Muda wa kufungishwa ndoa kwa Shawali na Grace, lakini kabla ya Shekhe kuamka ili kuweza kufungisha hiyo ndoa baba yake na Frank alienda kwa Mc na kumwambia kuna kitu ambacho anataka kukiongea kabla ya ndoa hiyo kufungwa. Mc hakuwa na shida ukiangalia na mtu aliyoomba hiyo nafasi alikuwa ndio muhusika mkuu wa harusi hiyo hivyo aliamua kumpa nafasi hiyo. "Nashukuru Sana Ndugu zangu kwa Kujitokeza kuja kushuhudia ndoa ya Mwanangu. Hii inaonyesha ni kiasi Gani mzee Ramadhani mnampenda. Kwa kweli hata mimi nawapenda Sana na Mungu awabariki. Nimeamua kuongea Maneno machache kabla ya ndoa kufungwa kwa kuwa ninamaana yangu. Katika maisha yangu kwa kweli huwa Sipendi kuona Mtu anadhurumiwa haki yake hata kidogo. Nikiona Mtu anadhurumiwa haki mimi moyo wangu huwa unauma Sana. Hata kama mdhurumaji atakuwa ni Mwanangu huwa sipendi kumficha namwambia aachane na tabia hiyo. Nazani kabla ya Mwanangu kumuoa Grace kulikuwa na matangazo ya harusi ambayo huyu mwanamke ambaye anaitwa grace ndio alikuwa anatakiwa kuolewa na Kijana ambaye anaitwa frank. Hadi baba yake alikuja hadi kwangu kumnunulia Mwanae Gari. Kwa kuwa mzee Oska nilikuwa najuana naye nilimwambia Lazima nitahudhulia kwenye hiyo harusi. Cha ajabu hiyo harusi iliyeyuka juu juu na mtu ambaye alikuwa anahitaji kuoa akaishia kusingiziwa kesi na kufungwa"Aliongea Mzee Ramadhani maneno ambayo yaliwafanya watu kutulia huku na wengine wakivuta kumbukumbu kama watakumbuka chochote kuhusu yale Maneno ya Mzee Ramadhani. Pia yale Maneo ya Ramdhani yaliwachanganya sana Shawali, Grace pamoja na wazazi wake na Grace maana hawakujua kwa nini yule Mzee alikuwa anakumbushia mambo ambayo yalikuwa yamepita. "Nazani watu wengi mtakuwa mnashangaa na kujiuliza naongelea kwa nini mambo haya wakati yalikuwa yameshapita. Naongelea haya Mambo kwa kuwa mimi napenda haki na sipendi mtu kuonewa hata siku moja. Sababu za ndoa ile kuvunjika ilikuwa ni Mwanangu. Mwanangu ndio alitumia pesa kuwashawisha wazazi wake na Grace ili yeye amuoe Grace. Hata yale Matangazo ya Husuri hayakuwa ya kweli bali ilikuwa ni mtego wa kuweza kumuua Frank. Yani walijifanya wanakubali mwanao kuolewa na Frank ila kabla ya ndoa Wamuue Frank na kwa kuwa wao walikuwa wameshakubali mwanao kuolewa hivyo Grace asingegundua. Hii kazi ya mauaji ambayo ilitakiwa kufanyika msimamizi alikuwa ni Mwanangu Frank. Mimi najua yote na lazima leo niongee maana mimi mpenda haki na sitaki mwanangu atumie mali zangu kuwanyanyasa wale ambao hawana. Sasa baada ya mtego wa kumuua Frank kushindikana kwa sababu walipoenda kumuua walimkosa na kulikuwa na hitirafu kati ya Frank na Grace na Grace kukimbilia nyumbani kwao ndipo Sasa waliamua kumuingiza Frank kwenye mtego wa kesi. Mimi sitaelezea sana ila muhisika Frank ambayo watu wengi manjua yupo gerezazi na polisi wengi mnajua katoroka Gerezani yupo hapa atawaelezea na ndio ataokea mambo ya unyama zaidi hafi kifo cha mkuu wa kituo cha Majengo bwana Joshua. Ila Mimi hapa nimesimama kusitisha ndoa ya mwanangu pamoja na Grace na ndoa ambayo itafanyika hapa ni ndoa ya Frank pamoja na Grace kama haki ambayo inasema. Ndio lazima Frank aoe leo maana ndio ahadi ambayo nilimwahidi Mungu wangu ili kujisafisha kwa dhambi za mwanangu. Tayari nilishaandaa hadi mchungaji wa kuifungisha hii ndoa na ndia sababu iliyonifanya hii ndoa kufungishwa maeneo haya na siyo kanisani. Naomba mchungaji ambae nilikudanganya kuwa kutakuwa na ndoa mbili unatakiwa kufungisha moja simama pia Frank ambae watu wanajua kuwa upo gerezani na askari wanajua umetoroka simama na uongee maneno machache na watu"Aliongea Mzee Ramadhani.
Kwa kweli yale Maneno ya Mzee Ramadhani yalizidi kuwachanganya watu. Hafadhali sasa watu walikuwa kama wanashangaa kile ambacho alikuwa anakiongea ila Shawali ndio alikuwa amechanganyikiwa na kushindwa kuelewa baba yake alikuwa anaongea nini. Kwa kweli hakutegemea kama baba yake angeongea maneno kama yale, hata aliposema kuwa kuna frank pale na alikuwa anamkaribisha bado Shawali alihisi huenda ni utani baba yake alikuwa anafanya. Mkuu wa jeshi la polisi Mkoa wa Arusha aliposikia yale Maneno kwa kweli na yeye Roho yake ilianza kuwa Juu maana alihisi kama Frank atasimama na kuongea ukweli basi Maisha yake yangekuwa matatani. Maana alijua Frank alikuwa anajua Siri zake zote hivyo angemuumbua tena Mbaya zaidi na Mkuu wake wa Kazi alikwepo pale. "Baba unaongea maneno gani mbele ya watu, hebu acha utani wako bwana. Kweli unathubutu kumtetea huyu Mnyama mbele za watu"Aliongea Shwali maama alishindwa kuvumilia maana miguno ya watu huku wakiteta chinichini ilizidi kuongezeka. "Mimi sina Utani shawali, tena Nakuita Shawali maana najivua Gamba mbele za watu wewe siyo Mwanangu tena. Mimi sina Mwanangu mwenye roho ya kinyama kama wewe. Mtu muuaji usiyejari ubinadamu wa mwenzako. Nazani hii kesi yako itakuwa nzuri sana na sitaki mtu yeyote akuwekee zamana maana matendo yako yanatisha pia uzuri hadi Mkuu wa Jeshi la nchi upo hapa utajionea na mambo wanayofanya maafande wako. Hivi unafikili shawali mimi Sijui kama Ulienda kumteka rafiki yangu Mzee Oska wakiwa na Goodlucky ili umuue. Unafikili Sijui kama wewe ndio chanzo hata cha Frank kutoroka Jela maana ulipanga kumuua Mzee Oska pamoja na Goodlucky kisha unaenda kumuua Na Frank Gerezani ili ndoa yako iende vizuri unafikili mimi sijui hilo. Tena naomba usiniite tena baba ukithubutu kunyanyua mdomo wako tena na kuniita baba utanifanya na mimi niwe na Dhambi maana nitakuua mbele za watu"Aliongea Mzee Ramadhani kwa Hasira maneno ambayo yaliwafanya hadi watu wote Ukumbini Kuguna. Yale maneno kwa kweli yalizidi kumchanganya shawali na kubaki akiwa amesimama huku hali ya hewa kwake ikizidi kuwa mbaya. Maana ilikuwa haitabiriki ilikuwa hali gani ya hewa ilikuwa inapita kwake maana muda ule shawali alikuwa anaonekana anatetemeka kama anaona baridi na cha ajabu jasho lilikuwa linamtoka. Baada ya Mzee Ramadhani kumaliza kuongea yale maneno ya kumjibu Shawali mchungaji ambaye aliitwa kuja kufungisha ndoa alisimama na kuwapungia watu mikono kisha sasa watu walikuwa wametulia kimya na kuangalia Frank ambaye alikuwa anatajwa angetokea wapi. Cha ajabu watu walibaki wakishangaa mtu akisimama kutoka kwenye viti vya Wageni maalumu huku akiwa amebobea ndevu kisha alianza kupita mbele. Alipofika mbele ya Ukumbi alitoa miwani yake na kuvua kofia ambayo alikuwa amevaa pamoja na kutoa ndevu za bandia. Alipotoa vile vitu Shwali, mama yake na Grace pamoja grace mwenyewe walibaki wakiwa wanashangaa. Mkuu wa Jeshi la Polisi alipomuona kweli yule mtu alikuwa ni Frank ambaye alikuwa anamtafuta kwa kutoroka Jela aliamka na kutoa pisto yake ili kwenda kumkamata lakini Sophia naye aliwahi na kumwambia atulie arudi kukaa. Yale Maneno ya Sophia wala hakutaka kuyalewa alizidi kuelekea mbele ili kwenda kumkamata Frank hapo ndipo Mkuu wa Jeshi la Polisi na yeye aliamua Kuingilia kati na kusimama kumzuia Mkuu wa Jeshi la Polisi arusha kwenda kumkamata Frank. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini baada ya kusikiliza maneno ya Mzee Ramdhani kwa kina pia kumuoa frank ambaye alikuwa anamfahamu kama aliwahi kuhukumiwa kwa kumuua Mkuu wa Kituo bwana joshua alihisi huenda kuna kitu kilijificha akiongea Frank anaweza kukielewa. Mkuu wa Jeshi la Polisi Arusha alipoona Mkuu wake amesimama na kumwambia Arudi alipokuwa amekaa aliamua kurudi huku akiwa anatetemeka maana alikuwa anajua moto unaenda kuwaka siyo muda. Kwa kweli Fank alipovua miwani yake pamoja na kofia kitu cha kwanza alimwangalia Grace kwa Umakini kwa muda kama wa dakika mbili hadi machozi yalianza kumtoka. "Najua Grace siyo moyo wako umependa wewe kuwa na Shawali ila ni moyo wa mama yako. Nauhakika maana siku Nikiwa nasomewa kesi mahakani ulikuja huku ukiwa unalia na kuniambia utakuja kunisaidia. Mama yako mimi nahisi siyo binadamu yeye labda ni hafu caste yani nusu binadamu alafu nusu fisi. Grace mama yako alikuendea Kwa Mganga ndio maana sasa hivi unampenda Sana Shawali. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Mama yako ndio aliyofanya kuuhamisha moyo wangu kwako ambao ulikuwa unaupenda na kumpa Shawali ndio maana upendo umehamia kwa Shawali. Hivi Unakumbuka tulipotoka lakini Grace. Unakumbuka kama Mimi nilikupenda kutoka wewe ukiwa unasoma kidato cha pili na Mimi nikiwa nasoma kidato cha kwanza. Nilivumialia kwa Muda wa Miaka saba bila kuwa na mwanamke kwa kuwa nilikupenda wewe"Aliongea Frank na uvumilivu ulimshinda na kulia zaidi. Yale Maneno ambayo Frank alikuwa anaongea kwa kweli yahakumuingia kabsa Grace akilini yeye alibaki akitabasamu tu maana alijua Frank anaongea uongo mtupu. Hata Frank alipomuangalia Grace na kuona akitabasamu yeye hakumuona mbaya lakini alizidi kumlaani mama yake na Grace. Kitendo cha watu kusikia yale Maneno ya Frank akiongea kwa huzuni kwa kweli walitulia kimya huku wengine huzuni wa hali ya juu ukiwakumba. "Mama Grace hivi Kwa nini uliamua kunihukumu hivi, ulifikia hadi kunitengenezea kesi ya kuekti mwanao kafa ili mimi nipelekwe jela. Yani Baada Ya Grace kuondoka huku akiwa analia alikuja kwako wewe uliamua kukusanya watu na kuanza kulia Kama Grace amejiua. Nilipofika kwako tayari ulishawaanda Askari wapenda Rushwa na kunipakia kwenye Gari kunipeleka kituoni. Hivi Unajua kilichotokea kituoni wewe? Mwenzako nilipofikishwa kituoni sikusonewa kesi ya kumuua Mpenzi wangu grace bali nilisomewa kesi ya kuwa nimekamatwa na Madawa ya kulevya uwanja wa ndege na safirisha wala siyo kusababisha mke wangu kujiua. Shawali rafiki yangu hivi wewe unamoyo wa namna Gani?"Aliongea Frank huku sasa akipiga hatua tatu kusogea kwa Shawali hapo ndipo alipokuwa anataka kuanza kuongea yote mambo ya Shawali
Wakati Frank akiwa Anaongea huku Shawali alikuwa na wakati Mgumu sana Muda ule Jasho lilikuwa linamtoka kupita kiasi. Siyo Shawali tu Hata Mkuu wa Jeshi la Polisi alikuwa na Wasiwasi mbaya maana alijua sasa siri yake ndio inaenda kuvuja. Alitamani kuondoka pale kwenye harusi ili asisikie kitu chochote lakini upande Mwingine wa moyo wake ulimwambia Asiondoke ili asikie kama Frank atamuhusisha na yeye. Pia wakati Frank akiwa anaongea huku machozi yakimtoka huku Suzani na yeye alikuwa anapanga namna ya kuingia pale katikati ya Ukumbi ambapo alikuwepo Frank. Pale alihisi angefika ilikuwa rahisi maana watu ambae alikuwa anawatafuta walikuwa karibu kabsa. Shawali ambaye alihisi ndio kisababishi cha mume wake kufa alikuwepo mbele tu pale. Afande Koboko ambaye ndio alimuua mume wake hospitalini baada ya kumchoma kisu huku akishuhudia kwa Macho yake na yeye alikuwepo mbele kumlinda Shawali. Hivyo kama Angefanikiwa kupita mbele basi aliona itakuwa rahisi Sana kumaliza kazi yake. Alichofanya Taratibu alianza kujisogeza mbele ili kwenda kumaliza kazi yake Maana aliona ndio Muda Mwafaka umefika. "Shawali Mimi nilikukosea nini hadi uliamua kuniadhibu hivi? Hivi ni kweli mimi kuwa na Mahusiano na Grace ndio umeamua kuniadhibu namna hii. Ungeniambia tu kuwa nimwache Grace ila siyo kunipeleka Jela kisa Mwanamke. Kweli unathubutu hadi kutuma watu ili kuja Kumuua Afande Joshua ambaye alikuwa ananisaidia mimi kwa nini lakini"Aliongea Frank tena Maneno ambayo yalimfanya Shawali kuamka kwa hasira maana aliona Sasa anataka kuchafuliwa jina lake. Alipoamka Shawali hata kabla hajamfuata Frank koboko alimuwahi na kumrudisha akae maana ndio alipewa kazi ya kuhakikisha ulinzi unakuwa salama pale pamoja na kumlinda shawali. "Shawali Najua utakuwa na Hasira sana ila huo ndio ukweli na mimi sijaja hapa kwa lengo la kuja kugombana ila nimekuja kufanya Surprise kwako kwa Grace pamoja na watu wote ambao wapo hapa. Ila kabla ya kufanya hii Surprise nataka niwathibitishie watu kuwa mimi sina hatia yeyote ile ndio Maana Mzee Ramadhani ameamua kunisaidia ili mimi Nimuoa Grace. Shawali akishirikiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ndio ambao wamemua Mkuu wa kituo cha Majengo Joshua na Mtu waliomtuma kufanya hiyo kazi ni Afande koboko ndio ambaye amemuua kwa kumchoma na kisu mbele ya macho yangu. Huku pia Mke wake Suzan, Goodlucky pamoja na aisha wakiwa wanashuhudia. Baada ya kumuua mimi walinichoma sindano ya Usingizi wakishirikiana na Dactari ambaye alikuwa anapenda Rushwa na wenzangu waliwateka na kwenda kuwatupia kwenye shimo ili wafe huko. Ndio maana baada tu ya Afande Joshua kufa mke wake Suzani alipotea mazima maana walitupiwa kwenye shimo. Huko kwenye shimo walipokuwa wanaenda kutupiwa kumbe Afande Sophia alikuwa ameona ndio aliwaokoa na kuwatorosha kuwapeleka moshi maana kama wangegundua hawa watu bado wazima wangewatafuta wawaue ili kufuta ushahidi. Walipomaliza hiyo kazi ndio sasa wakanisingizia mimi ndio nimeua. Nina mambo mengi sana ya kuongea ila nazani nikizidi kuongea yatazidi kuniumiza, ila nazani sasa hivi ndio Muda wa kufanya surprise"Aliongea Frank huku akiwa analia kwa hasira kisha ghafla alipeleka mkono kwenye kiuono chake na kutoka na Bastora aina ya Renover. Kitendo cha Frank kutoa Bastora kiliwashitua sana watu ambao walikuwepo pale Ukumbini. "Jamani hakuna haja yeyote ya kuogopa kwani hii ni hali ya kawaida sana mtu kuwa na bastora. Mzee Ramadhani kwanza ningependa kutoa shukrani kwa msaada wako ulionipa pia nakuomba msamaha kwani kile ulichokipanga hakitaweza kutimia. Ndio mimi sitaweza kumuoa Grace maana hanitaki. Kwa kuwa Grace hanitaki na wazazi wake walikuwa hawataki nimuoe kisa mimi masikini basi mimi nataka niondoke na Grace ili iwe funzo kwa wazazi wengine. Grace najua hapo ulipo siyo akili yako bali umetekwa na madawa ya Kiganga hivyo NISAMEHE GRACE kwa hiki ambacho nataka kukifanya. Nahitaji kukuua ili tuende mbinguni huenda nitakuoa huko bila kipingamizi chochote. Pia kabla ya kukua ningeomba Goodlucky umlee mtoto wako ambaye yupo kwa Grace na ningependa huko ambako ningeenda ningeona umemuoa aisha hata aisha nilishamwambia hivyo"Aliongea Frank maneno ambayo yaliwafanya watu kuzidi kushangaa. Muda ule ulinzi ulianza kuongezeka ili kwenda kumlinda Grace ili Frank asije kumuua. Wakati watu wakiwa wanasikiliza maneno ya Frank tayari Suzani aliweza kujipenyeza hadi kupita mbele ya ukumbi ambapo alikuwa amesimama Frank. "Ni kweli kabsa Koboko ndio ambaye alimuua mume wangu na sisi walituteka. Pia Frank nakuomba usifanye tukio lolote baya maana watu ambao walikufanya wewe maisha yako kuwa mabaya ndio naenda kuwamaliza"Aliongea Suzani kwa haraka haraka kisha alichomoa bastora yake kiunoni kwa style ya kasi ambayo alifundishwa na mume wake na kuinyoosha kuelekea kwa Shawali. Aliponyoosha ile bastora hakutaka kuchelewesha alifyatua na kwenda kumtandika shawali risasi mbili za kifuani kisha alitembea kwa kasi kuelekea mbele alipomuona Koboko vizuri alifyatua na nyingine ambayo ilienda kupiga kichwa cha koboko na kwenda chini mzima mzima na Damu zilitapakaa. Wakati tukio lile likiwa linatokea watu walianza kupiga kelele huku wakiwa wanaomba msaada. Kitendo cha watu kuanza kukimbia ovyo kilifanya Frank na yeye ashike Bunduki yake kumfuata Grace. Ambacho alikuwa anahitaji Frank ni kuhakikisha anamuua grace tu na yeye anajiua maana alishachoka mateso ya hapa duniani. "NISAMEHE GRACE NAOMBA UNISAMEHE GRACE, NISAMEHE GRACE Nahitaji kwenda kuishi maisha marefu ulimwengu mwingine"Aliongea haya Maneno huku akiwa anawasukuma watu kuwafuata watu ambae muda ule walikuwa wanamtorosha Grace huku wakiwa na mama yake na Grace. Hatua kama kumi mbele kwa kuwa yeye alikuwa yupo kwenye mwendo wa kasi alishawafikia Grace hivyo alichofaanya alimwita Grace kwa Sauti ya Nguvu Grace alipogeuka tu Frank alifyatua Risasi na kwenda kumtandika Grace kwenye kifua kisha alimuongeza na nyingine iliyomfanya Grace kutapika Damu Mdomoni na kwenda mzima mzima hadi Chini
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Frank alipohakikisha Sasa amempiga Risasi Grace za kutosha ambazo alikuwa na Uhakika lazima atakufa aligeuza Bastora yake na yeye alijipiga Risasi mbili za kifuani na kwenda mzima mzima hadi chini. Huku kwa Suzani baada ya kumaliza Tukio lake kumpiga Shawali Risasi pamoja na Koboko hata yeye alijipiga Risasi ya kichwani ambayo ilifanya hadi kichwa kisambaratike na ubongo kusambaa chini. Yani kwa Upande Wa Suzani yeye pale pale alikuwa ameshakufa maana Silaha ambayo alikuwa anatumia ilikuwa ya hatari kuliko hata ya Frank. Bastora aina ya Revorlver ambayo alitumia kuwapiga Koboko na Shawali ilikuwa na Nguvu sana hivyo kitendo cha kujipiga yeye huku akiwa Karibu zaidi ndio kilifanya kichwa chake kusambaa zaidi. Watu kwa kweli walikuwa wamechanganyikiwa Sana kutokana na ile Milio ya Bunduki na Walikuwa wanasukumana mbaya ili kutoka nje na kila Mtu alikuwa anaokoa maisha yake. Kwenye ile Harusi wapo Watu ambao walikuwa Wamekuja na watoto wao au Mume na Mke ila kwa Muda ule kila Kunguru Muoaga alikuwa anaponyesha Bawa lake. Muda ule hakuna ambaye alikuwa na kumbukumbu kama alikuwa na watoto au mwanamke na alihitaji kuokoa maisha yake zaidi kila mtu alijitaidi kukimbia na Kusukuma watu ili apite. Ile hali kwa kweli kwa watoto wadogo ilikuwa shida maana walikuwa wanasukumwa akianguka mtu anapita juu wala hajali kama chini kuna mtoto mdogo kaanguka. Hakuna kitu ambacho kinamlio mbaya Kama Bunduki kikilia kwa kweli huwa kinachanganya vibaya akili za watu. Kwenye ule Ukumbi wenye watu kama Mia tano hivi ni Watu kama kumi tu hivi ambao walikuwa hawajashituliwa na ile milio ya Bunduki bali wao walikuwa wanashangaa kile ambacho kilikuwa kinatokea maana wengine walihisi kama wanaangalia picha ya Mauaji wala haikuwa ni ukweli. Wapo ambao walisubutu hata kufikicha macho ili kuhakikisha kile ambacho kilikuwa kinatokea ni kweli au ndoto. Hawa watu alikuwa Mzee Ramadhani, Mkuu wa Jeshi la Polisi wazazi wake na Frank pamoja na Grace, Aisha, Goodlucky, Afande Sophia pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini. Upande wa Mzee Ramadhani kwa kweli yeye alishindwa kuelewa vile vitu ambavyo vilikuwa vinatokea tangia asimame pale alipokuwa amekaa wala hakutoa hata Mguu. Alimuona Mwanae akipigwa Risasi, frank akimpiga Grace risasi kisha na yeye kujipiga risasi. Yale matukio ndio yalimfanya kubaki njia panda na kushindwa kuelewa kwa nini frank alimsaliti na kuchukua maamuzi ambayo yalikuwa siyo Mazuri. Baada tu ya Frank kujipiga Risasi wala hakukaa Hata dakika Moja huku nako Defender Ziliingia. Hizi ndio Gari ambazo zilikuwa zimetoka kwenye Makao makuu ya kituo cha Polisi arusha kuja kumkamata Mkuu wa Jeshi la Polisi Arusha. Tayari Mzee Maguma alishapeleka mashitaka kule na walipoangalia Ushahidi ulikuwa wa kutosha ndipo waliambiwa kuja kuwakata wote ambao walihusika kufanya lile tukio. Mkuu wa Jeshi la polisi alipoona defender zikiingia alitaka kukimbia maana alihisi lazima zimekuja kumkamata lakini Sophia alimuwahi na Kumuweka chini ya Ulinzi hivyo alikuja kuchukuliwa kizembe na kupakiwa kwenye Defender. "Mwanangu hebu amka bwana nakuomba amka huwezi kufa maana Shawali anakusubilia Ukafunge ndoa. Grace hebu acha Utani wako bwana utalalaje hivi chini tena mbele za watu huoni kama unanitia aibu"Yalikuwa ni Maneno ambayo alikuwa anaongea Mama yake na Grace huku akiwa anamtingisha grace ambaye Muda ule alilala chini huku akiwa kimya na damu zilikuwa zinamtoka. Baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Arusha kukamatwa Huku nako Shawali, Koboko, Grace na Frank walipakiwa kwenye Gari na kukimbizwa hospitali kwa ajili ya kwenda kupatiwa matibabu. Lakini hadi Muda wanawapakia Grace, koboko na Suzani wao walishakufa zamani. Walipowafikisha Hospitalini haraka haraka waliingizwa kwenye Vyumba vya Wagongwa maututi. Walipoingiwa Huduma ilifuata na Baada ya Dakika kama tano hivi na Wahusika wa wagongwa walishafika. Muda ule tayari Shuka za njano zilikuwepo kwenye vitanda vitatu ambavyo ilikuwa ni Kwa Grace, Suzani na Koboko huku kwenye vitanda vingine viwili Madactari walikuwa wapo busy Kuhakikisha frank na Shawali wanapona. Mzee Oska wakiwa na Mzee Ramadhani wao walipofika waliambiwa wasubiri nje maana huduma ndio zinaendelea. Walikaa pale kwa Muda kama wa Saa moja ndipo Dactari alitoka na kuanza kuuliza Ndugu wa Wagonjwa ambao walikuwa wameletwa mle ndani. "Jamani kwa kweli ni huzuni ambao unatisha, sina Muda wa Kumvuta mtu mmoja mmoja na kumueleza hali ya Mwanae au nduguye maana matukio yote yaliyowakuta watoto wenu yanafanana. Hivyo hiki ambacho nitakiongea hapa kinanafanana kwa wote. Najua mtakuwa kwenye wakati Mgumu sana kwa wote ila hakuna Jinsi hii ni Mipango ya Mungu. Hivyo basi Wagonjwa Wote ambao waliletwa humu kwa kweli hakuna hata Mmoja ambaye amepona wote wamekufa"Aliongea Dactari maneno ambayo kila mtu pale alikuwa hataki kuyasikia. "Hapana Mwanangu hawezi Kufa Grace hawezi kufa sasa Grace akifa na mimi si nitakuwa Matatizoni. Mume wangu naomba unipeleke kwa Mganga Sasa hivi maana nilimwekea Mwanangu Dawa ili ampende Shawali ila wakati napewa zile Dawa Mganga aliniambia mwanangu asipatwe na tatizo lolote hadi aolewe. Hivyo kama akipatwa na tatizo hususani afe zile Nguvu za dawa zitaniru..."Aliongea Mama yake na Grace hata kabla hajamalizia Maongezi alianguka chini na kuanza kurusha rusha Miguu kama mtu mwenye Kifafa. ................................................... Watu wengi walikuwa wamekusanyika mahakani Kuu ya Mkoa arusha kusubilia Hukumu ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Arusha. Matukio ya Kinyama ambaye alifanya hadi kupelekea kifo cha Mkuu mwenzake bwana Joshua ndio kilikuwa kimewatia watu Hasira na kufika kuja kuangalia Hukumu yake. Tayari ilishapita kama wiki mbili tangu vifo vya watu watano. Muda ule pia mama yake na Grace yeye alishapoza upande Mmoja wa mwili wake na alikuwa hawezi kuongea tayari alikuwa kama bubu. Pamoja na kuwa bubu hata yeye alifikishwa mahakamani pamoja na Mume wake Mzee mambo maana wao nao ilikuwa chanzo cha Matatizo ya Frank na Mwanae maana waliekti kama Mwanao kafa na kumuingiza matatizoni frank. Jazi wa ile kesi alisimama na kusoma vizuri kesi zote tatu kisha kutoa Hukumu. Mkuu wa Jeshi la Polisi yeye alihukumiwa kwenda kifungo CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/cha Maisha Jera. Mzee Gambo yeye kwa kuwa mke wake alipoza hukumu ya mke wake aliibeba yeye. Na kwa kuwa hawakuwa na mtoto wa kuwasaidia na walitengwa na ndugu kutokana na matukio ambayo alifanya mke wake Jaji alimuonea Huruma na kumuhukumu miaka mitatu Jela au atoe Fani ya milioni Saba. Baada ya Hukumu hiyo Mkuu wa Jeshi alianza kifungo Rasmi huku nafasi yake ikichukuliwa na Afande Sophia. Wiki moja mbele Mzee Mambo aliuza nyumba yake na kwenda kutoa faini mahakamani kisha walitoka na kwenda kuanza kuishi maisha ya Shida na Mkewe. Miezi Miwili ilipita tangu matukio yale ya kutisha yatokee ndio Goodlucky walioana Rasmi na Aisha kutimiza yale Maneno ambayo Frank aliwaambia. Mtoto wake Goodlucky ambaye alikuwa ameshakuwa na miaka mitatu walimchukua na kuanza kuishi naye. Mzee mambo pamoja na Mkewe kwa kweli wao walipouza nyumba Maisha ya Mjini yalikuwa Magumu sana hivyo walirudi kijijini kwao Himo kilimanjaro na kwenda kuanza maisha upya huku ndugu wa pande zote mbili yani mke na mume walikuwa wamewatenga kwa matukio ya kinyama ambayo walifanya
**********MWISHOOO***
0 comments:
Post a Comment