Search This Blog

Friday, July 15, 2022

JULIETH - 5

 







    Simulizi : Julieth

    Sehemu Ya Tano (5)

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ndani ya buti Jullieth aliendelea kupigania roho yake lakini nguvu yake ilikuwa ndogo kuliko roho ya mauti. Na ndani ya dakika hiyo hiyo Roja alifunga buti na kukaa juu ya gari lile akihesabu sekunde na dakika akingojea Jullieth awe maiti na mwili wake utolewe kisha utupwe katika bahari. “Oyaa Kuna kitu gani katika buti” sauti kali ilitokea nyuma yake..almanusura Roja ajikojolee namna alivyo pata mshituko…Aligeuza shingo yake na kutizama sauti iliko tokea., na hapo akakutana na askari kutoka katika kampuni ya ulinzi akiwa na mbwa pamoja na bunduki aina ya gobole. Roja alibaki amebung’aa kwa nukta kadhaa akiwa haelewi afanye nini mapigo ya moyo yakamwenda mbio, Mwili wake ukawa unachuruzisha jasho jepesi. “Nimekuuliza katika buti kuna kitu gani?...jibu upesi..kwanza fungua buti la gari..” alisema tena yule askari na wakati huo huo asakri mwingine alyevalia magwanda kama yale ya mwenzie aktokea na kusogea eno lile. Kengele ya hatari iligonga kichwani mwa Roja. Chuse aliyekuwa katika uskani aligutuka baada ya kuona mzozo huko nyuma, alipotizama kupitia kioo cha kutizamia pembeni ndipo moyo wake ulipo patwa na mshtuko mkubwa kwa kile alicho kiona. Aliamini sasa maisha yake yaniangia katika hatari ya kuhusihwa na kesi ya mauwaji. Hakuwa tayari kuona anakwenda jela kirahisi kiasi kile. “Mungu wangu tumekwisha” chuse aliwaza wakati huo akijiweka sawa ndani ya gari tayari kwa makabilano yoyote pale itakapo bidi. Akiwa anajishauri afanye nini dhidi ya kile kilicho kuwa kinaendela nyuma ya gari .,kupitia kioo kilicho mwezesha kuona nyuma alishuhudia Roja akiachia ngumi kali ya shigo kwa yule askari mwenye bunduki na mbwa pigo lililo mpeleka chini, lakini wakati huo huo mbwa alimrukia Roja na kumpalula kwa makucha na meno ila kwa wepesi wa ajabu Roja alichomoa kisu kilicho kuwa chini ya kiatu chake na kukididimiza katika tumbo la mbwa yule..mbwa alitoa kilio kikali cha uchungu huku damu zikiruka na kutapakaa hovyo. Lakini wakati huo huo yule askari wa pili alimrukia Roja mzima mzima na kubingirishana nae chini katika mchanga huku yule askari aliyepigwa ngumi kali ya shingo akiamka na kuungana na mwenzake kukabilana na Roja. Ilikuwa ni kitimtim Roja hakuweza tena kakabilana na watu wawili. Alidhibitiwa.

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yote hayo Chuse alikuwa akiyashuhudia kupitia katika kioo cha gari. Na hata wakati hayo yakijili alibaki akiwa ameganda kama kwamba yupo katika theluji kali. Lakini katika hali ambayo hata yeye haukuitegemea alishuhudia Roja akijivuta kwa nguvu zake zote kutoka katika mikono ya wale maafande wawili na kurukia kisu chake kilicho kuwa ardhini sentimita chache kutoka mahala walipo kuwa wamemkwida na kwa wepesi mwingine wa ajabu alikididimiza kwa nguvu zake zoote kisu kile katika tumbo la askari yule wa awali.. lakini wakati huo huo sauti kali ya risasi kutoka katika gobole la askari wa pili ilisikika na ndani ya nukta hiyo hiyo yowe la uchungu lilimtoka Roja



    huku damu nyingi kutoka katika tumbo lake ikimiminika kama bomba. Ni hapo ambapo akili ya Chuse alipo zinduka na kumwambia kuwa mahali pale hapakuwa sahihi kwa usalama wake na anacho takiwa kufanya ni kuliondoa gari eneo lile na kukimbia. Alikanyaga krach kisha akatoa handblek na kuliwasha kisha akilindoa kwa spidi kubwa akiacha taharuki isiyo na kifani eneo lile. Alishika njia ya kuelekea mbagara akiamini uelekeo ule ulikuwa sahihi na salama kuliko njia ya kivukoni…naam mahesabu yake yalienda sahihi, kasi aliondoka nayo ilimuwezesha kufika mbagara Kongowe kwa muda wa dakika zisizozidi kumi na tano. Sasa aliingia katika barabara ya kilwa {kilwa road} bahati nzuri siku hii foleni haikuwa kubwa sana alikanyaga mafuta kwa kasi na ndani ya dakika nyingine kumi na tano zilitosha kabisa kumfikisha keko…alikunja kushoto na kushika uelekeo wa keko magulumbasi.. Sasa akawa mbele ya kijumba cha chumba kimoja...giza tayari lilikwisha meza nchi...akili yake ilikuwa ikizunguka..ubongo wake haukupata utulivu hata kidogo..aliamini fika Roja alikuwa katika masaibu makubwa mno..hatua ya Roja kutiwa nguvuni hiyo inatoa maana watakuwa wanakabiliwa na kesi ya mauawaji japo hakujua hali ya mtu aliyekuwa ndani ya buti la gari lile aliyepewa sumu na Roja kabla ya kuibuka kwa patashika kule mikadi beach. “Mungu wangu nifanye nini sasa” aliwaza akiwa ndani ya gari akiwa hajui afanye nini..kwa nukta kadhaa alibaki ameganda..alikurupuka kama kwamba amemwagiwa maji ya baridi. Na kuzunguka nyuma ya gari kisha akafungua buti na kumtoa Jullieth.. *********************************** Hatimae mtiririko wa kumbukumbu za Chuse ukakoma baada ya kustushwa na kikohozi cha mfululizo kilichotoka kwa mwanamke aliyekuwa amelala pale mbele ya kitanda. Pumzi ndefu ilimtoka Chuse baada ya kuona hali ya binti yule ikiimarika..alichukua kikombe kilicho kuwa na maziwa nusu na kumnywesha tena binti yule. “Wajionaje wewe?” Chuse aliuliza kwa sauti ya chini akiwa sentimita chache karibu na sikio la Jullieth. Lakini kabla binti yule hajtoa jibu mara ghafla suti kali ya kishindo kutokea mlangoni kwakwe ilisikika huku sauti kali za mamia ya watu zikihamasisha kukamatwa kwa mtu zilirindima masikioni mwake.. Moyo wake ulipiga paaaaa tumbo likaingia ubaridi.. “Mungu wangu nimekwisha!!” alijikuta akibwabwaja kibwege na akiwa tayari kutiwa mbaroni.. “Sasa hawa watu wamejua vipi yale yaliyo tokea huko mikadi” Chuse aliwaza,lakini wakati huo huo sauti kutokea nje ikasikika ikisema, “mtoe mwizi.”…“Ndiyo mtoeee” sauti ya mtu mwingine ilijibu kwa nguvu. Atimae Chuse alifungua mlango. Hamadi!!. Alikutana na mlundo wa watu wenye fimbo mawe na malungu.na hapo hapo baada ya kuonana ana kwa ana na wale watu kundi la watu lilijichoma ndani mwake pasina ruhusa tayari kwa kumtoa mwizi wao walie amini amekimbilia mule ndani. “Jamani huyo mwizi humu hajaingia” Chuse alisema kwa mahamaniko huku roho ikimdunda,vipi yule mwamnamke ambaye yumo mule ndani akisema kwa wale watu juu ya kile alicho tendewa!.Aliogopa. “Oyaa kibaka humu ndani hayupo naona jamaa alikuwa na demu wake tu” mtu mmoja alisema kutokea mule ndani. Na hapo lile kundi la watu waliondoka pale kwa Chuse na kumtafuta kibaka mahala pengine. Alishusha pumzi ndefu kisha akarejea kwa yule mwanamke pale kitandani,.alimkuta anakodoa kodo.********************

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Niko wapi hapa?” “Keko magulumbasi” “Toka lini?” “Siku ya tatu leo” “Kwanini niko huku…na nimekuja lini?” “Kwani wewe unajua ulikokuwa kabla ya kuwa hapa?” “No hata” “Sasa kwanini unauliza umekuja lini hapa inaonyesha unahisi kuna mahali ulikuwa kabla ya kuwa hapa?” “Ndio nahisi ila sina uhakika..kwani mimi ni nani..eti kaka?..na jina langu naitwaje?” Masikini Jullieth msichana mrembo alikuwa amepoteza kabisa kumbukumbu zake.kila kitu katika kichwa chake kilikuwa kitupu. “Ni habari ndefu kidogo,.ila kwa sasa unahitaji uendelee kupumzika” Alisema Chuse boy, wakati kwa upande wa Jullieth alibaki kuangaza angaza mazingira ya mule ndani maswali yakiwa mengi japo hakujua vipi ayapangilie katika kuuliza..hakuwa na kumbukumbu na hata moja. Matukio yote yaliyo tokea siku chache za nyuma yalikuwa yameyeyuka katika ubongo kwa kiasi kikubwa madawa ya kulevya yalikuwa yamevuruga kabisa akili ya binti yule mrembo. Tokea hapo Jullieth alikuwa ni kama mtoto aliyezaliwa,.hakuwahi kujua hata moja katika maisha yake ya nyuma. Kila kitu katika maisha yake ya nyuma ilikuwa ni historia isiyoweza kusimulika,. Tangu hapo Hakuna aliye hangaika na maisha ya Julleth, hakuna aliyejali maisha ya binti huyo, na kwa muda mfupi Jullieth alichakaa na katu usingeweza kumtofautisha na mwendawazimu wengine wa mtaani.,kama angetokea mtu akakwambia binti yule ndiye alikuwa mtangazaji maarufu wa televisheni kamwe usingeweza kumkubalia.. Aliishi tandika huko katika mitaa ya mango na alifanya lolote, kwa wakati wowote, na kwa mtu yeyote, ilimradi apate pesa ya kununua unga{cocain} hakuwa na kitu muhimu katika maisha yake zaidi ya kupata unga, hakujua thamani ya uhai kwakuwa kwakuwa hakuogopa mauti. Wewe ungeweza kusema binti huyu anaishi maisha magumu. Lakini kwakwe yeye, yale yalikuwa ni maisha bora zaidi, pengine kuliko maisha yote ambayo aliwahi kuishi..madawa ya kulevya yalimfanya ajione yupo katika pepo ya fildausi, pamoja na nakwamba kuna wakati akili yake ilimwambia kuwa madawa ya kulevya yanamadhala lakini burudani ya dope {cocain} ilishinda akili yake. Hata siku moja hakuwahi kujua kama aliwahi kuwa na mchumba wa dhati aliyempenda aitwae Chacha. Giza zito lilitawala Utashi wake..hadi siku moja alipojikuta ameingia katika ulimwengu mwingine. ***************

    SOBA CLINIC; BAGAMOYO.

    Ilikuwa ni ndani ya jumba la wahanga na watumiaji wa madawa ya kulevya,.mtu mmoja mrefu mweusi muda wote alionekana sura yake ni yenye matumaini makubwa.wahaka ulikuwa mwingi usoni mwake, alikuwa pembeni ya kitanda alichokuwa amelala mwanamke ambaye dripu za maji zilikuwa zikiingia taratibu katika mishipa yake ya damu, kimwenekano usingeweza kumtofautisha na kichaa,.nywele zake zilikuwa zimetimka timtim, nguo zake pia zilikuwa zimechakaa lakini uzuri wake ulikuwa haujapotea. Ni Jullieth. “Julieth mama..” yule kijana aliyekuwa pembeni ya kile kitanda aliita. “Julleth mke wangu” jamaa aliita tena safari hii akimtikisa kidogo. Lakini Jullieth hakuitika wala kufumbua macho. Kijana yule aliendelea kumsemesha binti yule ambaye alilowea katika bahari kubwa ya usingizi nap engine ingechukua muda mrefu kabla ya kufumbua kope za macho yake. Chacha alipatwa na jazba kali, kila ambavyo alivyo kuwa akikumbuka namna mwanmke yule alivyoteseka huko mtaani, kila mara taswira ya Jullieth akiwa amelala mitaloni ilimjia akilini. Swali ambalo alikuwa akijiuliza kichwani na kujipatia majibu ambayo hakutaka kabisa ukweli wa kile alichokuwa akimini,.ni vipi pale ambapo binti yule alipokuwa amelewa madawa ya kulevya kiasi cha kulala katika mitaloni, je wahuni wangeweza kumwacha hivi hivi bila kumbaka? Jibu lilikuwa ni NO lazima angefanyiwa uhuni na wahuni pale tu ambapo inatokea madawa ya kulevya yamemlevya.. Alisimama wima na kumtizama yule mwanamke macho yake yakiwa mekundu. Alitoka nje ya clinic ile hasira yake ikizidi kuwa kuu.alingia katika prado lake na kuliondoa kwa kasi kuelekea Dar es Salam Dakika arobaini alikuwa nje ya geti lake pale mbezi jogoo na kujitoma ndani. Alingia hadi katika sebule kubwa iliyokuwa imesheheni vitu vyote vya thamani unavyo vifahamu, kisha akavua shati lake na kubaki na singrendi nyeupe. Alingia chumbani sekunde zisizo zidi thelathini akatoka akiwa amekamata bastola kubwa iliyounganishwa na bomba ambayo kazi yake ni kuzuia mlio wa risasi. Kabla ya kufanya lolote alitizama picha kubwa ya Jullieth iliyokuwa imebandikwa pale ukutani, sura nzuri ya mwanamke aliyekuwa akimtizama kwa macho maregevu yenye kutia huruma huku midomo yake ikiwa na bashasha ya tabasamu. Hakika hasira ya Chacha ilizidi kuongezeka mara dufu zaidi. Alitoka nje ya ngome ya ile nyumba na kuingia katika banda alilokuwa akitumia kufugia mbuzi.. Watu wanne walikuwa wamefungwa kamba ngumu katika mikono yao nyuma ya mlingoti mpana na mgumu ndani ya zizi la mbuzi, kimwonekano sura za wale watu zilikuwa zimechakazwa kwa kipigo cha haja. Chacha alingia mule ndani na kusimama mbele yao. “ninyi watu” aliita kwa ukali akiwa ameikamata bastola yake kwa nguvu. Jamaa hawakuitika zaidi ya kugumia maumivu, “nawauliza kwa mara nyingine tena kwanini mlitaka kumuua Jullieth” alisema chacha kwa kunong’ona lakini kwa sauti ya ukali kidogo. “Unataka ujibiwe mara ngapi we fala” Jamaa mmoja miongoni mwa wale watu, sura yake ikiwa na majeraha mengi pengine kuliko wote, alisema kwa kujiamini sura lake baya likijaa kiburi na kufanya mikunjo mikunjo katika paji lake la uso. Chacha aliuma meno hasira ikizidi kujaa kifuani mwake alinyanyua bastola yake na kumwelekezea yule jamaa. “Haki ya mama nakulipua blood fool” alisema chacha kwa hasira. “Mbona

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    unakawia we fala..lipua tena on the spot na ole wako nikipata bahati ya kukukamata..sintokupa nafasi ya kujutia kosa.” Yule mtu alisema tena kwa kujiamini zaidi.CHacha alitetemeka,.na hakuwa na chakufanya zaidi ya kukiruhusu kidole chake kifyatue kitufe cha kuruhusu risasi kutoka. Kichwa cha yule mtu kilisambalatishwa vibaya na risasi ya chacha Tundu kubwa katika paji la uso lilimwaga damu zinto iliyochanganyikna na ubongo huku macho ya yule jamaa yakibaki yamekodoa kama kwamba labda aliona jini kabla ya kufa, kwakweli taswira iliyoonekana katika sura ya ule mwili usio kuwa na uhai ilitisha. “Nauliza kwa mara nyingine, kwanini mulitaka kumuaa yule mwanamke” Kimya.. “Ninyi watu..hamnijbu sivyo?” “Kimya tena” “Alaa! Kumbe mnaona mimi mjomba wenu mafala ninyi” alisema tena Chacha na papo hapo alifyatua risasi mbili zilizo fumua kifua cha jamaa wa pili, Chacha alikuwa kama nyati aliyejeruhiwa zile hasira za kikulya zilipamba moto. “Mmebaki wawili..nawauliza tena kwanini mlitaka kumua Jullieth,. jibu upesi ninyi watu” “piga risasi yako katika paji langu la uso kunguru wee” “Paaaaaaa” mlio mdogo wa risasi ulisikika tena, yule jamaa alikuwa amefumuliwa tena kichwa chake.. “Sioni hatari mimi kuwaua wote,.kwani sina faida na hata mmoja wenu kati yenu..” Alisema Chacha akiwa amechanganyikiwa kwa kiwango kikubwa, na sasa alikuwa akishindilia risasi nyingine katika ile bastola tayari kwa kumaliziz yule mmoja.. Basi.,basi basi bwana nitakueleza kila kitu..tafadhali usiondoe roho yangu tafadhali nipo tayari kusema lolote utakalo.



     “Sema upesi pusi wee” Chacha alikoroma kwa ukali. “Huyu ni mbunge” Alianza kusema yule jamaa mwenye kuitwa Doni, “na huyo jamaaa hapo ni meneja wa wa redio ambayo mkeo alikuwa akifaya kazi” alisema tena huku akisonta kwa jamaa aliyekuwa amefumiliwa kifau chake kwa risasi mbili. “Na huyu hapa ndio bigger pusher wetu. Kwakweli ninacho jua ni kuwa mkeo kuna siku alikaribia kujua biashara za madawa ya kulevya ambazo zoimekuwa zikifanywa na mabosi wangu hapa,.hivyo walicho dhamilia ni kumchezesha picha la ngono na kumua…” “Nini!!” chacha aliuliza kwa mshangao macho yakiwa yamemtoka pomoni. “Ndio..ukweli ndio huo..” “Kwahiyo mlimvutisha madawa mchumba wangu?” “Ndiyo” “Halafu mkafanya nae mapenzi kwa zamu?” “Ndivyo” “Na mbona hamkumuua..mliamua kumdhalilisha au siyo”Roja ndiye alikuwa mtu wa mwisho kuwa na mkeo ila baada ya hapo siku iliyofuatia ulikutwa mwili wa Roja akiwa amepigwa risasi na walinzi wa fukwe za mikadi beach huku mkeo akiwa hajulikani mahala alipo.na toka hapo sikuwa na taarifa yoyote juu ya huyo mtu hadi leo unaponiuliza juu ya maswali hayo. “Roja ni nani?” “Alikuwa ndiye ichaji wa hiyo inshu” “Nataka kujua kila mtu aliyehusika na mateso ya Jullieth” “Comredi Chuse boy” “Ndiyo nani?” dereva tax na bajaji anapaki ilala boma ila anishi huko keko magulumbasi wilaya ya temeke. “Wewe pia ulimbaka mke wangu?”Chacha aliuliza swali ambalo kwa upande mwingine ungeweza kuona lilikuwa la kipuuzi, yule jamaa alibaki akibabaika hata siweze kujibu lolote. Wakati akiwa bado anababaika juu ya swali lile,Chacha alikoki ile bunduki ndogo yenye kuitwa bastola na kuielekeza kichwani mwa yule mtu. “Usije ukajidanganya hata siku moja katika maisha yako kuwa nitakusamehe mshenzi wa tabia wewe” Jamaa macho yalimtoka pima..akiwa bado hajajua atumie aina gani ya maneno yenye kuweza kulainisha moyo wa yule kijana wa kikulya aliye wahi kuwa na ndoto kubwa katika maisha,tayari risasi moja ilitoka katika mdomo wa bastola na kumtwanga katika paji lake la uso, alihisi chuma kigumu kikipenya katika kichwa chake huku giza zito na la ajabu lililindima machoni mwake na ndani ya sekunde mbili tayari yule mtu ulikuwa maiti.**********************



    1/1/2004 saa sita kamili usiku Ilikuwa ni siku ya mwaka mpya zilisikika kelele nyingi huko nje ya jengo la Soba house clinic Bagamoyo. Chacha alikuwa amemkumbatia kwa nguvu zote Jullieth., machozi ya furaha yalimtoka,kamwe hakuamini kama atimae mwanamke yule aliyempenda siku zoote katika maisha yake yupo katika mikono yake. Kubwa kuliko vyote afya ya Jullieth alikuwa imerejea na hata zile kumbukumbu zake pia kwa sasa zilikuwa sawa. “Jullieth” “Abee” “Atimae tumekuwa pamoja tena” “Ndio Chacha Mwenyezi Mungu ni muweza” “Hakika Jullieth” alijibu Chacha akilaza kichwa cha Jullieth katika kifua chake. “Chacha” Jullieth alita akiwa kifuani mwa Chacha. “Naam” “Umepona miguu yako iliyokuwa imepooza?” “Ndiyo Jullieth kama ulivyo sema Mungu ni muweza” “Ilikuwaje?” Jullieth aliuliza. “Ni habari ndefu inayo hitaji tukae pamoja kisha tuzungumze karibu kila siku” “Nieleze tu japo kwa ufupi” Jullieth alinga’nga’nia. “Baada ya kuwa umepotea kusiko julikana nilamua kwenda kijijini huko Musoma makutano, ambako nilikuwa na

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ng’ombe wengi tu.,niliuza wote na kurejea Dar kwa matibabu…lakini pia visenti vilivyo salia nilinunua nyumba na mabasi ya kusafirisha abilia hapa mjini pamoja na bastola” “Bastola!!” Jullieth aliuliza kwa mshangao,alipatwa na hisia kwa kusikia neno bastola kuliko yote aliyo yasema Chacha. “Ndio, hii bastola ndio imesaidia kuwakamata watu wote walikufanyia ushenzi na nimewaua wote kasoro mmoja wa huko keko” Chacha alisema tena. “Heee!!” Jullieth alishangaa maneno ya yule mtu, kila neno liliibua hisia mpya moyoni mwake, lakini vilevile moyoni alikuwa akijiuliza “inamaana Chacha amepambana na kundi lote la akina doni na wenzake na kuwashinda kiasi cha kuwaua wote!”. Lakini halikuwa hilo lililomshangaza kubwa ni kuwa vipi Chacha awe na roho ngumu kiasi cha kuweza kuondoa uhai wa mtu, kuua mtu aone ni kama kumkanyaga mende kwa kandambili. “Umeua wangapi chacha?” “Wanne ila bado mmoja wakati wowote naweza kumuibukia na kumaliza kisasi changu” “Mungu wangu wee!!. Na ulijuaje kama hao watu ndio walio nifanyia unyama?” “Hiyo pia ni habari ndefu mno tutaongea siku nyingine Jullieth”.Alisema tena Chacha, “Walikuwa ni akina nani?” Mbunge wa viti maalum, meneja wa kampuni uliyokuwa ukifanya kazi, na walinzi wao wawili. “Kwahiyo umewaua wote?!” “Ndiyo,sijabakiza mtu pale” “Kwanini walinifanyia mimi haya” Jullieth aliuliza tena machozi yakimtoka, hakuwa tayari kuamini kama meneja wake mr Robert pia alikuwa ni miongioni mwa watu waliokuwa nyuma ya tabu na mateso. aliyoyapata katika maisha yake. “Niambie tafadhali” alisema tena Jullieth machozi yakimlenga. “Nitakueleeza mpenzi wangu kwani kidogo ni habari ndefu ila nitakueleza.” Ilikuwa ni furaha kubwa mno kwa hawa watu wawili, Jullieth afya yake ilikuwa njema kwa mhujibu wa vipimo vya kitababu hakuwa ameambukizwa magojwa ya zinaa hivyo usiku huu wa mwaka mpya, walijikuta wanaikutanisha miili yao, na joto la miili yao ikisukuma hisia ya kila mmoja kutamani kiungo cha uzazi cha mwenzake.



    “Krii,kriiii, krii, krii,” sauti kali ya simu ya mkononi ilikuwa ikiita kwa kasi, ilirudia rudia kuita kwa kasi bila kukoma, mtu aliyekuwa anakoroma katika kitanda, hakuwa na dalili ya kuamka kwa wito wa simu ile ya mkononi.

    Mpigaji wa simu ile hakuchoka, ni wazi alikuwa na shida muhimu na mmiliki wa simu ile, aliendelea kupiga ile simu ilihali mmiliki akiwa amezama kabisa katika usingizi mzito wa pono. Yapata saa tisa za usiku, joto lilikuwa kali ndani ya chumba hiki ambacho ndani yake kulikuwa na mwanamke aliyelala fofo akiwa mtupu, huku mwili wake ukiwa umeloa mijasho itokanayo na joto kali lililokuwa likifukuta mule ndani. Ilikuwa ni chumba kidogo, ambacho hakikuwa na vitu vingi vya thamani, ungeweza kuona kitanda cha tano kwa sita, meza ndogo, stuli mbili za kukalia,kiruninga kidogo aina ya sony na beseni lililo beba vyomba vingi vya plastiki. Katika kuta za chumba kile, kulikuwa na mapicha ya wasaniii wa ughaibuni wa muziki aina ya hihop, hadi hapo ungeweza kuhisi mwenyeji wa chumba hiki alikuwa ni kijana, lakini sio kijana tu bali ni kijana wa kileo mwenye mapenzi na muziki. Simu ile iliendelea kuita pasina kupokelewa na binti aliyekuwa amelala chali kihasara huku akiwa kama alivyo kuja duniani. Simu ilikatika na katika kioo cha simu ilionyesha missed call kumi na nne. Binti yule alizidi kukoroma. Huku mwili wake wenye shepu ya kuvutia ukiwa bado umeloea katika bahari ya usingizi. Lakini wakati huo huo, nje ya nyumba ile kulikuwa na mtu aliyekuwa akimwaga mafuta ya petroli kuzunguka nyumba ile ya chumba kimoja, ambayo ndani yake alikuwa amelala msichana yule aliye uchi wa mnyama. Jamaa aliyekuwa akimwaga mafuta yale ya petrol alionekana ni mtu mwenye hasira na donge kubwa kifuani mwake, alidhamilia kabisa kuua mtu, hakuwa na utani na kile alicho kuwa akikifanya. Hatua hamsini kulikuwa na kijana aliyekuwa akihaha huku na kule kama kuku mwenye kutaka kutaga, alikuwa akipiga simu yake kila mara, lakini alionekana kutopata majibu kutoka upande wa pili, na kadri alivyokuwa akikosa majibu ya kupokelewa kwa simu yake ndivyo alivyo zidi kuwa na wahka mkubwa mno. Muda huo yule jamaa aliyekuwa akimwaga mafuta ya petrol alikuwa amekwisha maliza zoezi lake, sasa alitoa kiberiti cha gesi na kuwasha moto. Jamaa aliyekuwa umbali mdogo alipo ona lile tukio alitoa ukulele mdogo wa fadhaa huku mikono yake akishika kichwa chake. Macho yamemtoka pomoni. Moto mkubwa ulilipuka ghafla, na kijumba kile cha chumba kimoja kikashika moto, jamaa aliyekuwa mita hamsini alipagawa vibaya mno, alihaha huku na kule, alitamni akimbie eneo lile lenye kuwaka moto, lakini alikuwa mwingi mno wa hofu. Binti aliye kuwa ndani amelala uchi akiwa ameloea katika usingizi wa pono hakujua nini kiinaenda kutokea katika maisha yake. Moshi mwingi na mzito ulizagaa ndani ya chumba.hakuna kilicho salia*************

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku ya pili vyombo vya habari vililipoti juu ya taarifa ile.Chacha na Jullieth walikuwa ni miongoni mwa watu walio kuwa wakifuatilia taarifa ile kwa kina.,.ambacho Jullieth hakujua ni kuwa tukio lile lililoteka hisia za watu wengi aliyefanya yote hayo ni Chacha,.lakini hata Chacha pia hakujua kuwa aliyekuwa muaji usiku wa kuamkia siku hii Alikuwa ni mtu mmoja tena mwanamke mrembo asiyekuwa na hatia huku akimwacha mbaya wake akiwa hai. Wakiwa wanendelea kufatilia taarifa katika televisheni ghafla waliingia watu sita mule ndani walionekana kuwa ni askari polisi wakiwa wameongozana na kijana aliyekuwa amejaa hofu kubwa machoni mwake. Chuse boy Mr Chacha upo chini ya ulinzi na utatakiwa katika vyombo vya sheria kwa makosa ya mauwaji. Alisema askari mmoja aliyeonekana kuwa ni kiongozi wa wale polisi. Jullieth alibakia amekodoa macho asiamini kwa kile kilicho kuwa kinatokea mbele yake.



    TAMATI..



0 comments:

Post a Comment

Blog