IMEANDIKWA NA : NYEMO CHILONGANI
*********************************************************************************
Simulizi : Darkness Of Comfort (Giza Lenye Faraja)
Sehemu Ya Kwanza (1)
YUNNAN, China.
Lilikuwa ni moja ya matukio ya kuhuzunisha, vilio vilitawala kila kona, idadi kubwa ya watu walikuwa wamepoteza maisha na wengi kujeruhiwa,
Wachina hawakuamini kile kilichokuwa kimetokea, japokuwa matetemeko ya ardhi yalikuwa yamezoeleka nchini China, ila la siku hiyo lilikuwa kiboko.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jimbo la Yunnan lilikuwa limetetemeshwa, majengo mengi yakaanguka huku barabara zikiharibiwa vibaya, mabomba ya maji yaliyokuwa yamechimbiwa ardhini yakafukuliwa na kuanza kumwaga maji hovyo.
Madereva waliokuwa barabarani, wakashindwa kuyakontro magari yao na kujikuta wakipata ajali, majengo yaliyokuwa yamewekwa vioo, vyote vikavunjika na hata majengo mengine kudondoka.
Tetemeko hilo la ardhi ambalo lilidumu kwa zaidi ya dakika moja lilileta maafa makubwa jimboni hapo.
Miongoni mwa nyumba zilizokuwa zimepata maafa makubwa kutokana na tetemeko hilo la ardhi lilikuwepo jengo la umma lililojengwa na serikali ya China kwa ajili ya kuwasaidia watu wasiokuwa na kazi yoyote ile, jengo la ghorofa kumi lililokaliwa na watu zaidi ya elfu moja.
Hakukuwa na tofali lolote lililosimama, jengo zima lilikuwa limedondoka chini. Hakukuwa na mtu aliyeweza kumpa pole mwenzake kwani asilimia sitini ya watu, majengo yao yalikuwa yamedondoshwa na tetemeko hilo kubwa kuwahi kutokea nchini China.
Kila mtu alionekana kuwa bize mahali hapo, utoaji wa vifusi ulikuwa ukiendelea huku kwa wale waliokuwa na makoleo au vyombo vyovyote vile walikuwa wakiendelea kufukua kwa ajili ya kuzitoa maiti na watu waliojeruhiwa vibaya.
“来帮我们” (njooni mnisaidie) alisikika jamaa mmoja huku akijitahidi kutoa vifusi vya jengo hilo.
Watu waliokuwa pembeni wakaanza kusogea kule alipokuwa jamaa yule, vifusi vikubwa vya matofali vilikuwa chini huku vikiwa vimeifukia miili ya watu waliokufa na wale waliokuwa majeruhi, wakaanza kuitoa miili hiyo hata kabla magari ya serikali hayajafika.
Miili ilijawa vumbi, matofali makubwa na mazito yalikuwa yamewafunika. Miili mingine haikuweza kutolewa kwani vifusi vilivyokuwa vimewafunika vilikuwa vikubwa na vizito. Kwa miili waliyoweza kuitoa, waliitoa lakini ile ambayo kwao ilionekana kuwa vigumu kuitoa, wakaachana nayo na kusubiri magari ya serikali.
Kila mmoja kwa wakati huo alikuwa bize kumsaidia mwenzake, wale wasiokuwa na nguvu, walikaa pembeni huku wakiangalia kazi iliyokuwa ikiendelea kwa wenzao. Baada ya dakika chache, magari makubwa ya serikali yakafika mahali hapo na kuanza kutoa vifusi vile.
Picha ambayo ilionekana mahali hapo ilimtisha kila mtu, watu wengi walikuwa wamekufa kwa kudondokewa vibaya na vifusi vile, wapo waliokuwa wamepasuka vichwa na damu kuwatoka nyingi huku wengi wakiwa wamevunjwavunjwa viungo vyao.
“我找我的朋友” (namtafuta rafiki yangu) alisikika msichana mmoja wa kichina.
Kwa kumwangalia tu, naye alikuwa mmoja wa waathirika wa tetemeko lile, mwili wake ulikuwa umejaa vumbi huku ikiwa ni vigumu kumtambua kwa kumwangalia mara moja.
Naye alikuwa amesogea hapo na kutaka kumuona rafiki wake ambaye hakuwa akijulikana na watu waliokuwa bize wakiondoa vifusi.
“舒押嗯,这边走” (Shu Yan, sogea huku) alisema mwanamke mmoja na kumvuta msichana yule ambaye alikuwa na miaka kumi na sita.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Muda wote msichana huyo alikuwa akilia, kila mwili uliokuwa ukitolewa mahali hapo alikuwa akiusogelea na kuanza kuuangalia ili apate kujua kama alikuwa ndiye huyo rafiki yake au la.
Miili iliendelea kutolewa lakini hakumuona mtu aliyemhitaji hali iliyomuongezea kilio zaidi.
Kutokana na maafa makubwa yaliyotokea siku hiyo kutokana na tetemeko kubwa lililokuwa limetokea, jioni ya siku hiyo taarifa rasmi ikatolewa na kuonyesha kwamba zaidi ya watu elfu sitini walikuwa wamefariki dunia, ilikuwa ni idadi kubwa zaidi ya tetemeko lililotokea mwaka 1822.
Shu Yan, msichana masikini asiyekuwa na ndugu, msichana aliyekuwa akiishi ndani ya jengo lililokuwa limedondoka, alijikalia chini pembeni huku akilia, kila alipokuwa akiyaona majengo mengine yaliyokuwa yamedondoka kutokana na tetemeko lile la ardhi, alibaki akilia tu.
“李察,你在哪里?” (Richard, upo wapi?) aliuliza Shu Yan huku akijifuta machozi yake.
Swali lake hilo halikupatiwa jibu, alibaki akilia tu, machozi yaliendelea kububujika mashavuni mwake huku akiyafuta kwa kutumia nguo yake chafu aliyokuwa ameivaa.
Usiku mzima Shu Yan hakulala, alikuwa akilia tu huku akihitaji kumuona rafiki yake huyo. Mara ya mwisho kabisa kuonana naye, alikumbuka kwamba alikwenda chooni mara baada ya kumuacha Richard akiwa koridoni na watoto wengine, kipindi hicho ndicho ambacho tetemeko hilo la ardhi likatokea na hakujua kama rafiki yake huyo alikufa au la.
Urafiki wake na Richard ulikuwa ni wa karibu mno. Wote walikuwa watoto masikini waliokutana ndani ya jengo hilo, walisaidiana kwa kila kitu na hata walipokuwa wakitoka kwenda kuomba mitaani, bado waliambatana pamoja.
Watu waliwashangaa mitaani, halikuwa jambo la kawaida kumuona msichana wa kichina akiambatana na mtu mweusi. Kwa Shu Yan, hakutaka kujali, kwake, urafiki huo ulikuwa ni zaidi ya kila kitu maishani mwake, hakuangalia rangi, urefu au ufupi, kitu pekee alichokuwa akikiangalia, moyo wake ulisemaje.
“Ninataka kukuona Richard, umeniacha peke yangu, ninahitaji kukuona, upo wapi Richard wangu,” alisema Shu Yan lakini maneno yake yalikuwa si kitu, ni kama machozi ya samaki, kila alipolia, yalichukuliwa na maji.
Serikali ya China ikatoa msaada mkubwa kwa ajili ya watu walioathiriwa na tetemeko lile la ardhi. Wakatenga sehemu maalumu ambayo ikafanywa kama kambi ya muda kwa ajili ya watu hao.
Shu Yan hakuonekana kuwa na furaha, bado shauku yake ilikuwa ni kumuona rafiki yake aliyekuwa akimpenda kwa mapenzi yote, Richard ambaye alipotea na hakujua kama alikuwa hai au alikuwa mfu.
Usiku mzima mawazo yake yalikuwa kwa Richard tu. Hakulala, usiku mzima alikuwa akimfikiria rafiki yake huyo. Machozi yalikuwa yakimbubujika kwani moyo wake ulimuuma mno.
Mpaka asubuhi inafika bado alikuwandani ya kambi ya watu walioathiriwa na tetemeko lile, bado hakujua mahali alipokuwa Richard. Siku hiyo hakutaka kubaki hivyohivyo tu, alichokifanya ni kuanza kumtafuta katika kambi hiyo.
Alitumia muda wa dakika zaidi ya arobaini na tano, hakufanikiwa kumuona na hata alipoulizia, hakukuwa na mtu aliyekumbuka kama alimuona baada ya tetemeko lile.
“最后一次见他,他就在走廊” (Mara ya mwisho kumuona alikuwa koridoni) alisema jamaa mmoja, mkono wake ulikuwa umevunjika na alifungwa POP.
“他在哪里?” (Yupo wapi?) aliuliza Shu Yan.
“我不知道” (Sifahamu) alijibu jamaa yule.
Shu Yan alihisi kuchanganyikiwa, hakuamini kwamba mpaka muda huo hakuwa amemuona rafiki yake aliyekuwa akimpenda kwa mapenzi ya dhati ambaye aliamini kwamba mpaka jengo lile linaanguka usiku, Richard alikuwa ndani ya jengo hilo palepale koridoni.
Siku hiyo hakutaka kukaa kambini, alichokifanya ni kuondoka na kuelekea katika Hospitali ya HKM (Hospital of Kunming Medical) iliyokuwa katikati ya Jimbo la Yunaan.
Alipofika huko, akamuulizia mtu huyo, majina yalipoletwa mikononi mwake na kutazama kama kulikuwa na jina la Richard, hakuweza kuliona.
Hapo ndipo alipochanganyikiwa zaidi, hakujua mahali alipokuwa rafiki yake huyo, moyo wake ukawa kwenye majonzi makubwa. Kila alipokuwa akijifikiria mahali ambapo Richard angeweza kuwepo, hakupata jibu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Moyo wake ukagubikwa na majonzi mazito, hakujua ni kitu gani alichotakiwa kufanya mahali hapo. Kilio chake kikaongezeka, machozi yakaendelea kumbubujika mashavuni mwake.
Hakuwa na wazazi, mtu pekee ambaye aliamini kwamba angempa faraja ya moyo alikuwa mtu mmoja tu, huyu aliitwa Richard ambaye mpaka katika kipindi hicho hakujua mahali alipokuwa.
“Nitamtafuta tu, siwezi kumuacha, ninampenda Richard, ni ndugu yangu, rafiki wangu pia, siwezi kumuacha, ni lazima nimuone tena, na hata nisipomuona, nataka kuiona maiti yake tu niridhike” alisema Shu Yan huku akijifuta machozi yake.
Kumpoteza Richard lilikuwa pigo kubwa maishani mwake.
Watu walikuwa wamekusanyika nyumbani kwa bwana Walusanga Ndaki kwa ajili ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ya kufikisha miaka arobaini na mbili. Kelele za shangwe zilikuwa zikisikika nyumbani hapo, watu walikula na kunywa mpaka kusaza.
Bwana Walusanga alikuwa Mtanzania aliyekuwa akiishi nchini China ndani ya jiji la Chuxiong. Alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa matajiri ambao walimiliki kiasi kikubwa cha fedha katika akaunti yake.
Japokuwa kulikuwa na ugumu kujenga nyumba nchini China hasa kwa wageni, kwa bwana Walusanga wala hakupata tatizo lolote lile, alifanikiwa kujenga nyumba zake mbili za kifahari ambazo zilikuwa karibu na Bahari ya Sicbuan.
Alikuwa mwanaume wa Kitanzania lakini kutokana na biashara zake kuwa nyingi, akahamia nchini China ambapo maisha yake yaliendelea kuwa huko huku akiwa na mke wake aitwaye Diana na mtoto wake wa kiume aliyeitwa Richard.
Fedha zilikuwa zikiongezeka kila siku, hakukoma kufanya biashara na Wachina, mara nyingi alikuwa akifungua biashara zake na kuwaajiri Wachina na kuwalipa vizuri tu.
Jina lake likawa kubwa, watu wengi waliokuwa wakiishi katika Jimbo la Kunming ndani ya Jiji la Chuxiong walimfahamu kutokana na ukaribu wake, mapenzi yake kwa watu wa China na hata ajira alizokuwa akizitoa tofauti na wachina matajiri ambao wengi wao hawakutaka kutoa ajira.
“Ningependa kumshukuru mke wangu kwa kunifanya niwe hivi nilivyo, ninampenda sana,” alisema mzee Walusanga, watu wote wakaanza kupiga makofi ya shangwe.
“Mke wangu, hebu sogea hapa kwanza,” alisema bwana Walusanga, mke wake akaanza kusogea pale alipokuwa amesimama, akaupitisha mkono wake begani kwa mkewe.
“Huyu ndiye kila kitu kwangu, ninafanya mambo mengi kwa ajili yake, toka nilipokuwa masikini mpaka katika utajiri huu, bado nilikuwa naye, ninampenda na kumthamini. Kama ningeulizwa ni nani ninayetakiwa kumshukuru katika maisha yangu, ukiachilia Mungu, ningemshukuru huyu mrembo,” alisema bwana Walusanga huku akiachia tabasamu pana.
Makofi yakaongezeka mahali hapo, kila mmoja alionekana kuwa na furaha isiyo kifani. Mara baada ya kumsifia sana mke wake, akamuita mtoto wake aliyekuwa na miaka kumi na saba, Richard na kuanza kumsifia mbele ya wageni wale.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Huyu naye hayupo nyuma, ni kijana mcheshi sana, ana akili nyingi na pia anafahamu mengi sana, ninapenda kuchukua nafasi hii kumwambia kwamba ninampenda sana, baada ya kifo changu, yeye ndiye atakuwa mrithi wa kila kitu,” alisema bwana Walusanga, kama kawaida watu wakaanza kupiga makofi.
Siku hiyo ilikuwa ni shangwe tu. Muda wa muziki ulipofika, ukafunguliwa na watu kujumuika pamoja.
Hayo ndiyo yalikuwa maisha yake, kila siku akaunti zake ziliingizwa fedha kutokana na biashara mbalimbali alizokuwa akizifanya nchini hapo, jina lake likawa kubwa, alikuwa akipendwa kila kona.
Kama ilivyo kwa matajiri wengine kuwa na maadui, basi hata kwake ilitokea pia. Matajiri wengi hasa Wachina hawakuwa wakimpenda kwa sababu alizifanya biashara zao kuwa ngumu kufanyika jambo lililowapelekea kuandaa fitina.
Kitu cha kwanza wakaanza kuwatumia viongozi wa serikalini kwa ajili ya kuchunguza mwenendo wake mzima wa biashara zake.
Wakaanza kumchunguza kuhusu ulipaji wake wa kodi, kila kitu kilikuwa poa, hakuwa na tatizo lolote. Walipoona hapo wameshindwa, wakaanza kuchunguza bidhaa zake, kwa kila kitu kilichokuwa kimefanyika, bwana Walusanga alikuwa makini kupita kawaida.
Walipoona wameshindwa, mikakati mipya ikaanza kupangwa kwamba walitakiwa kumuua na kuchukua fedha zake zote zilizokuwa benki. Mpango mzima ukasimamiwa na tajiri mkubwa ambaye alikuwa kwenye ushindani naye, huyu aliitwa Tai Peng.
Pamoja kwamba alikuwa na fedha nyingi lakini kitendo cha kukaa nyuma ya bwana Walusanga kilimuuma, hakumpenda hata kidogo, alimchukia kupita kawaida.
“Ni lazima auawe,” ilisikika sauti ya bwana Tai Peng simuni.
Mkakati mzito ukapangwa, ilikuwa ni lazima bwana Walusanga auawe hata kama alikuwa na ulinzi kiasi gani. Mchakato wa kwanza kabisa kufanyika ilikuwa ni kumuwekea sumu katika kahawa yake ofisini.
Wakacheza mchezo na sekretari kwa ajili ya kukamilisha mpango wao huo, cha kushangaza, sekretari hakufanikiwa kwani hata kahawa hakuwa akinywa, yaani alionekana kama alijua kilichokuwa kikiendelea.
Hawakuishi hapo, walichokifanya ni kumuandalia ajali ya gari, mpango kabambe ukaandaliwa na ulitakiwa kufanyika ndani ya siku chache. Kweli ajali ikatokea, kitu cha kushangaza, hakuwepo ndani ya gari hilo zaidi ya dereva wake na wakati alipokuwa akipanda, walimuona.
Kila kitu walichokuwa wakikifanya, ikashindikana, hapo ndipo walipoamua kumuua kwa kumpa taarifa, kwamba ajiandae kufa, labda kuishi kwa presha kwa kuogopa kufa kungemfanya kuweweseka na hatimae kumuua.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
****
“Mke wangu!” aliita bwana Walusanga, alikuwa akitetwa na jasho.
“Kuna nini mume wangu? Mbona upo hivyo?” aliuliza bi Diana.
“Nimepokea ujumbe simuni mwangu.”
“Unasemaje?”
“Umeandikwa kwa kichina, sijajua umeandikwa nini.”
“Sasa umeuelewa? Kwa nini uogope?”
“Nahisi ni wa kitisho, sijawahi kutumiwa meseji ya kichina.”
“Usihofu mume wangu. Inawezekana ukawa ni ujumbe wa kawaida au kuna mtu kakosea namba,” alisema bi Diana.
“Inawezekana kweli?”
“Ndiyo. Lala kwa amani bwana, ukiwa na wasiwasi, utatutia wasiwasi na sisi pia,” alisema bi Diana.
“Ila sina amani.”
“Kwa nini?”
“Huu ujumbe, kila nikiuangalia, nakosa amani,” alisema bwana Walusanga.
“Achana nao, hebu tulale mpenzi,” alisema bi Diana.
Japokuwa alikubaliana na mkewe lakini bado alikuwa na wasiwasi tele, kila alipokuwa akifikiria kuhusu ujumbe ule moyo wake uliendelea kukosa amani. Alijua fika kwamba halikuwa jambo rahisi kwa mtu kukosea meseji kwake, tena mbaya zaidi ujumbe ulikuwa umekuja kwa kichina.
Alichokifanya mara baada ya kuamka ni kumtafuta wakili wake, msichana aliyeonekana kuwa mrembo, mwenye asili ya kizungu, huyu aliitwa Stacie Alexander ambaye alikuwa na uwezo mkubwa wa kuifahamu lugha ya Kichina.
“We are coming to kill you,” (tunakuja kukua) alisema Stacie alipokuwa akiisoma meseji ile.
Hapo ndipo bwana Walusanga akapata uhakika kwamba hofu yake juu ya meseji ile ilikuwa sahihi kabisa, kulikuwa na watu ambao walijipanga kwa ajili ya kumuua.
Hakutaka kujiuliza sababu, alijua kwamba kutokana na utajiri mkubwa aliokuwa nao ndiyo uliowafanya watu kumtafuta na kutaka kumuua, hivyo, akaandaa ulinzi mkubwa.
Kila alipokuwa akienda, ulinzi wake ulikuwa mkubwa zaidi ya kipindi cha nyuma. Alitembea na watu watatu, wote walikuwa na bastola viunoni huku yeye mwenyewe akiwa amevalia vazi kwa ndani lenye uwezo wa kuzuia risasi.
Ulinzi huo haukusaidia kitu, baada ya siku mbili, alijikuta akiwa katikati ya watu waliovaa vinyago huku walinzi wake wote wakiwa wamepigwa risasi.
Bwana Walusanga alikuwa akitetemeka kwa hofu, hakuwa akijua watu hao walihitaji nini mpaka waliamua kumtafuta kwa kiasi hicho. Kitu cha kwanza kabisa, akapakizwa ndani ya gari lenye vioo visivyoonyesha ndani na kupelekwa sehemu ambayo ilikuwa karibu na ule Ukuta wa China.
Akalazwa sehemu iliyokuwa na nyasi nyingi zilizoloana na kisha kuelekezewa mdomo wa bunduki. Alizidi kutetemeka kwa hofu, hakujua watu hao walikuwa wakina nani na walitaka nini kutoka kwake.
Baada ya dakika chache, bwana Tai Peng akatokea mahali hapo. Kwanza akashangaa, alimwangalia mzee huyo kwa macho yenye maswali mengi lakini mwisho wa siku akapewa jibu kwamba alitakiwa kufa mahali hapo kama asingefanya kitu kimoja tu, kuwakabidhi utajiri mkubwa aliokuwa nao.
“Haiwezekani, fedha na mali zangu ni kwa ajili ya mke wangu na mtoto wangu,” alisema mzee Walusanga.
“Unasemaje?”
“Siwezi kutoa kila kitu nilichokuwa nacho.”
Kilichofuata ni kupiga ngumi mfululizo. Japokuwa alisikia maumivu makali lakini msimamo wake ulikuwa uleule, mali na fedha zake zilikuwa ni kwa ajili ya familia yake tu.
“Tufanye nini?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ninaitaka familia yake hapa,” alisema Tai Peng.
Hilo wala halikuwa tatizo, vijana wakaondoka mahali hapo, maagizo waliyokuwa wamepewa ni kwamba ndani ya dakika thelathini wawe wamekwishafika hapo huku wakiwa na familia hiyo.
Hiyo wala haikuwa kazi kubwa, kwa kutumia uwezo wao mkubwa, dakika arobaini baadae walikuwa mahali hapo huku wakiwa wameongozana na mke wake, bi Diana.
Alipomuona mumewe tu, akaanza kulia, hakuamini kama mwanaume mtanashati alikuwa vile kama alivyokuwa. Moyoni aliumia, akaanza kulia mfululizo, akamfuata mume wake na kupiga magoti.
Shati lake lilikuwa limetapakaa damu na uso umevimba, mateso makubwa aliyoyapokea kutoka kwa watu hao yalimpa wakati mgumu mno. Hakuweza kuongea vizuri, kila alipokuwa akimwangalia mke wake, alitamani kuongea lakini sauti haukutoka.
“Mtoto wake yupo wapi?” aliuliza Tai Peng.”
“Hatujafanikiwa kumuona.”
“Acheni utani. Nendeni mkamlete mahali hapa, nataka asikie uchungu juu ya kile kitakachokwenda kutokea kwa familia yake,” alisema mzee Tai Peng.
“Sawa mkuu,” waliitikia vijana wale na kuanza kwenda huko, mikononi walikuwa na bunduki zao, walijiandaa kwa kila kitu, ilikuwa piga ua, lazima Richard aletwe mahali hapo. Hawakujua kwamba kila kitu kilichokuwa kikitokea, bwana Walusanga alikifahamu, hivyo alijipanga vilivyo kwa ajili ya kuzilinda mali na fedha za familia yake.
Je nini kitaendelea?
Je Richard ataweza kupatikana?
Nini kitatokea akipatikana?
Je bwana Walusanga na mkewe, bi Diana watauawa?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment