Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

SITOISAHAU MBEYA - 5

 





    Simulizi : Sitoisahau Mbeya

    Sehemu Ya Tano (5)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Evelyne Gando alikuwa kayeyuka mithili ya upepo. Niliangaza macho yangu huku na huko kumtafuta Evelyne Gando. Lakini sikumuona kabisa. Nikaachana nae, akili yangu iliacha kumtafuta mwanamke yule msaliti, Evelyne Gando. Macho yangu sasa yalibadili uelekeo, sasa yakaelekea katika gari kubwa aina ya fuso, gari ambayo ilikuwa wanashuka wanafunzi wa shule ya sekondari Sangu. Walishuka, wakashuka. Mwanafunzi wa saba kushuka katika gari ile, macho yangu yalivutika nae, yakawa yameganda kwake, yakifata nyendo zake. Nilimuona mwanafunzi yule



    akitua chini salama. Akiwa na begi dogo mkononi. Akasimama kidogo, akageuza shingo yake upande wa kulia, akaangalia upande huo kama nusu dakika, akageuza shingo yake kuangalia upande wa kushoto, nako aliangalia kama nusu dakika. Akapiga hatua moja ndogo kwa mguu wake wa kulia, mguu wa kushoto nao ukafata kupiga hatua ukipishana na ule mguu wa kulia. Alikuwa anafanya kitu kinachoitwa mwendo. Kutembea. Baada kama ya hatua sita mwanafunzi yule alisimama. Aligeuka upande wa kushoto haraka. Alitabasamu. Alitanua mikono yake huku akiwa na tabasamu tele usoni mwake. Mara, nilimuona msichana akikirukia kifua cha kijana yule, na kupata kumbato la nguvu. Macho yangu yalihama ghafla toka kwa watu wale waliokumbatiana, na kutua katika ile gari ya fuso ambayo bado wanafunzi walikuwa wanaendelea kushuka. Sasa Ilikuwa zamu ya mwanafunzi wa kiume kushuka katika gari ile. Kwa bahati mbaya kabisa kijana yule alikuwa akishuka huku akiangalia wale vijana waliokumbatiana katikati ya uwanja. Kijana alipoteza kabisa umakini. Alikuwa analishangaa kumbato. Bila kutegemea yule kijana aliporomoka toka kule juu ya gari hadi chini. Unajua lile kumbato lilikuwa la kina nani? Lilikuwa kumbato la mwanamke msaliti, anayesaliti mtu na baba yake kwa pamoja. Mwanamke anayeishi kwa wakati mmoja na mtu na mwanae. Sasa Evelyne Gando alikuwa kifuani kwa mwanaume aitwae Philimon Uvambe,



    mchezaji bora wa mpira kwa shule ya Sekondari Sangu. Lilikuwa ni kumbato la mwanamke msaliti ndilo lililomdondosha kijana yule toka garini. Evelyne Gando alikuwa kamuacha Richard Chali pale chini, na sasa yupo na mwanaume mwengine.



    Yule mwanafunzi aliyeanguka aliinuka huku akichekwa na wanafunzi wenzie. Macho yangu yalitoka kule kwenye gari na kurudi katika kumbato la mwanamke msaliti, Evelyne Gando. Sasa alikuwa anaachiana na yule mwanaume, Philimon Uvambe.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mkono wa kushoto wa Evelyne Gando na mkono wa kulia wa Philimon Uvambe ilishikana kwa nguvu na miili iliyokuwa inamiliki mikono ile ilijongea na kuelekea pembeni ya uwanja. Upande tofauti na ule aliokuwa amekaa Richard Chali. Walichagua sehemu waliyoiona wao sahihi na kukaa chini. Nami nilisimama toka pale nililokuwa nimekaa, na kwenda kujichanganya na wanafunzi wenzangu.



    Majira ya saa kumi na nusu mpira ulianza. Ilikuwa ni mechi ngumu sana. Iliyokutanisha shule mbele mahasimu jijini Mbeya. Shule ya Sekondari Sangu na shule ya Sekondari Meta. Shule hizi mbili zilikuwa mahasimu kweli, mahasimu katika michezo, mahasimu katika taaluma. Hadi mpira unamalizika mpira ilikuwa sare ya moja kwa moja. Kutokana na mwingiliano wa



    watu baada ya mpira kumalizika sikuwaona wale maadui zangu wawili. Siku hiyo niliyogundua mambo mabaya sana kuhusu Evelyne Gando ilipita. Tangu siku hiyo sikukutana tena Evelyne Gando wala Richard Chali. Ni miezi takribani sita ilipita tangu mambo hayo yatokee.



    *****



    Mimi ni mpenzi mkubwa sana wa kuangalia mpira. Napenda sana kuangalia mpira wa miguu. Siku moja ya mwisho wa wiki ilimikuta katika uwanja wa Sokoine. Uwanja mkubwa na maarufu zaidi katika Jiji la Mbeya. Nakumbuka kulikuwa na mechi kati ya timu ya Magereza ya Prisons, timu yenye maskani yake katika gereza la Luanda walikuwa wanacheza na timu ya Yanga, timu yenye maskani jijini Dar es salaam. Niliwahi kufika uwanjani ili nipate mahali pazuri pakukaa. Maana mara nyingi inapokuja kucheza Simba au Yanga uwanja wa Sokoine hufurika sana. Nilikaa upande unaoangalia geti kuu la kuingilia uwanjani. Upande ambao unatazamana na mahali wanapokaa viongozi ama watu mashuhuri. Ndipo niliwaona! Evelyne Gando akiwa na Mzee Chali walikuwa katika jukwaa hilo la VIP. Toka pale nilipokuwa niliziona vizuri sana tabasamu zao za furaha. Kwa mara nyingine tena nilithibitisha kwamba wale watu walikuwa ni zaidi ya mtu na mkwewe.



    Nilithibitisha kwamba Mzee Chali na Evelyne Gando walikuwa mtu na mpenzi wake. Sikutaka kabisa kuimezea ile habari ya kusikitisha. Habari ya aibu. Shida sasa ilikuwa nitaiambia vipi jamii ili inielewe. Je jamii haitohusisha ugomvi wangu na Richard ndio sababu iliyofanya nitunge mambo hayo. Nilitatizika sana.



    Ilikuwa asubuhi na mapema. Wiki moja baada ya tukio la kule katika uwanja wa wa mpira wa Sokoine. Nakumbuka ilikuwa siku ya jumamosi, na nilipanga siku hiyo iwe siku ya kufichua ukweli. Kumwaga mchele hadharani. Kumuonesha Richard Chali kwamba Evelyne Gando ni nani. Niliamua ile inaitwa liwalo na liwe!



    Siku hiyo nilitoka asubuhi na mapema sana na kuelekea nyumbani kwa kina Richard. Nilipanga kwenda kumwambia kila kitu mama mzazi wa Richard, mke wa mzee Chali. Nusu saa baadae nilikuwa nje ya geti la kina Richard, niligonga mlango na kusubiri kufunguliwa. Nilisikia kelele za miguu ya mtu zikija kufungua mlango. Na geti lilifunguliwa taratibu. Nilimuona mtu aliyekuja kufungua mlango.

    Adui yangu!



    Tulikuwa tunatazamana uso kwa uso na Richard Chali. Rafiki yangu wa zamani ambaye sasa ni hasimu wangu mkubwa!



    "Nambie we domo zege, umepotea njia?" Richard aliniuliza kwa kejeri na dharau kubwa sana.



    Niliposikia hilo jina hasira zilinishika maradufu. Jazba zilinipanda hasaa. Nilikasirika. Sikulipenda hilo jina hata kidogo. Lilikuwa ni jina baya zaidi kusikiwa na masikio yangu. Nilianza kumwangalia kwa jicho la chuki!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ghafla nikamshika Richard shingoni na kumsukumia ndani kwa nguvu. Kilikuwa ni kitendo cha ghafla sana ambacho Richard hakukitegemea kabisa. Alijikuta akidondoka chini huku mimi nikiwa nimesimama mbele yake.



    "Nyi watoto vipi tena!" Nilisikia sauti ya mama Richard Chali ikiuliza toka bustani, iliyokuwepo ndani ya uwa.



    "Nina shida na wewe mama.." Nilisema huku nikielekea upande wa bustani. Nikimuacha Richard pale chini. Akiwa pale chini Richard aliniangalia kwa jicho lenye hasira sana. Nilisikia akinitukana tusi



    kubwa la nguoni kwa sauti ndogo, nilisikia lakini mama yake hakusikia. Lakini mimi wala sikujari.



    "Hivi mna nini hivi nyi watoto?" Kwa sauti ya kulalamika mama Chali aliuliza tena.



    "Evelyne, Evelyne Gando mama!" Nililitaja jina la Evelyne kwa nguvu. Jina ambalo lilimtoa mbio baba yake Richard huko alikokuwa na kutoka nje. Sasa tulikuwa watu wanne nje ya nyumba ya kina Richard, uwani. Richard alijitahidi kujizoazoa pale chini na kutufuata kule upande kulikokuwa na bustani, na mzee chali na alikuja upande huohuo. Mzee Chali akiwa anahema vibaya mno, Richard akiwa anahema vibaya sana, mama Chali akiwa na mshangao mkuu usoni mwake. Hakuwa anaelewa kabisa jinsi mambo yalivyokuwa yanaendelea pale uwani.



    Ghafla katika mlango wa geti alisimama mtu mwengine wa tano, alikuwa ni mtoto wa kike aliyeumbwa ukaumbika. Alikuwa ndani ya suruali ya njano ya jeans na blauzi fupi nyeusi. Alikuwa amesimama huku mkono mmoja akiwa kalishikia geti. Kwa majina mwanamke aliyesimama getini alikuwa anaitwa Evelyne Gando!



    'Evelyne!" Richard na baba yake waliita kwa pamoja. Kilikuwa ni kindumbwendumbwe!





    Pale mlangoni Evelyne Gando alipigwa na butwaa. Alikuwa anatazamana na wapenzi wake wawili kwa mpigo. Alisimama wima huku mkono wake wa kulia ukiwa unaliachia geti sasa.



    "Evelyne Gando" Niliita hilo jina huku nikielekea pale mlangoni alipokuwa.



    Macho sita toka kwa watu watatu yalikuwa yanauangalia mgongo wangu. Macho ya mzee Chali, Mama Chali na Richard.



    "Nimepatikana leo!" Evelyne alitamka kwa nguvu.



    Alikuwa anadondoka chini. Nilikimbia kwa kasi na kumuwahi kabla hajafika sakafuni. Mikono yangu ilimshika mwanamke yule mrembo niliyekuwa nampenda sana hapo kabla. Nilijisikia wa thamani sana, ilikuwa kama nimeshika dhahabu. Evelyne aliniangalia kwa jicho lilionesha kukata tamaa.



    "Naombea unisaidie" Nilimsikia akitamka kwa sauti ndogo sana. Richard na wazazi wake walikuja mbio pale mlangoni. Wote wakiwa wamechoka na mambo yale.

     CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Na mimba yako mzee" Evelyne alithubutu kusema huku akilia, alisema huku macho yake yakimwangalia mzee Chali.



    "Unasemaje Eve, una mimba ya baba?" Richard aliuliza huku machozi yakimtoka. Nakwambia alilia. Kauli ile ya Evelyne haikuweza kuvumiliwa na mama Chali, alianguka chini vibaya sana, yeye hakukuwa na wa kumdaka. Mzee Chali alivyoona vile alichanganyikiwa sana. Lakini hakuwa na la kufanya, chozi la majuto lilimdondoka.



    "Richard kaite Tax?" Nilisema kwa nguvu. Richard alikuwa ananiangalia tu huku akitetemeka, hakuwa na la kufanya. Machozi yalikuwa yanatiririka toka machoni mwake.



    Niliona hatari iliyokuwa inatukaribia mahali pale. Taratibu nilimuweka Evelyne chini na kukimbilia nje ya geti. Dakika kama kumi na tano baadae nilirejea pale, nyumbani kwa mzee Chali.

    Niliyoyakuta!

    Lile eneo lote lilikuwa limetapakaa damu. Damu tupu! Mzee Chali alikuwa amelaliana na mkewe, wamekumbatiana, wote wakiwa wametapakaa damu vibaya mno. Evelyne Gando hakuwepo pale. Nilijaribu kumtafuta kwa macho lakini sikumuona. Huku



    Richard Chali akiwa amelala pembeni kabisa ya bustani akigugumia kwa maumivu.

    Eneo lilikuwa na damu, damu ambayo bila shaka ilisababishwa na mapenzi. Mapenzi yalifarakanisha ile familia, familia yenye kila sababu ya kuitwa familia bora. Mapenzi, mapenzi mabaya sana. Mapenzi yana nguvu sana. Nguvu ya mapenzi haina kifani. Baba na mwana waliokuwa wanapendana sana bila shaka walipigana kwa sababu ya mapenzi. Sijui kilikuwa kimetokea nini na kwa muda gani. Lakini mwili wa mzee Chali ulikuwa umetapaa majeraha ya kisu. Mwili wa Richard Chali nao ulikuwa una majeraha makubwa ya kisu. Cha ajabu Evelyne Gando haukuwepo eneo lile.

    Sikumuona.



    Baada ya nusu saa askari Polisi waliwasili pale nyumbani. Sikujua nani aliyewaita. Baada ya kupekua ndani na nje ya nyumba walifanikiwa kuukuta mwili wa Evelyne Gando ukiwa bustanini, ukiwa na majeraha mengi sana, ukiwa hauna uhai. Wale majeruhi wawili walipakiwa katika gari la Polisi na kupelekwa hospitalini, lakini hawakufika, walifia njiani. Baba na mwana walikufa kwa sababu ya mapenzi.



    Saa tano mbele mama Chali alizinduka. Kumbe hakuwa ameumia hata kidogo. Damu alizokuwa nazo



    zilitoka kwa Mzee Chali. Nilimsimulia kila kitu kilichotokea hadi kutokea kwa mambo yale. Alilia sana. Alisikitika sana. Lakini hakuwa na jinsi, mambo yalikuwa yashatokea. Baada ya siku tatu maiti ya Richard Chali na baba yake zilisafirishwa kwao. Na Evelyne Gando alizikwa katika makaburi yaliyopo nyuma ya Shule ya Sekondari Mbeya. Nililia sana wakati tunamzika Evelyne Gando. Nilikumbuka ile siku ya kwanza tunaonana ndani ya basi. Nilikumbuka ile siku ya 'debate'. Siku ya kwanza kumkumbatia Evelyne. Mwanamke aliyezitesa sana hisia zangu. Tulimzika Evelyne. Nikikuwa mfu wa mwisho kutoka katika tuta la kaburi lake. Nikipiga magoti. Nilinyoosha mikono juu nikimuombea kwa Mungu apumzike kwa amani Evelyne. Mara askari walinivamia na kuninyanyua pale. Baada ya utambulisho, nilitambua kwamba natakiwa niende Polisi nikaelezee juu ya mambo yale. Ndani nyuma ya gari ya Polisi nililia kwa nguvu huku nikisema kwa sauti kubwa. Kwa mkasa huu kamwe SITOISAHAU MBEYA!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *****



    Jitihada za baba. Ushahidi wangu na wa mama Chali na maombi yangu kwa Mwenyezi Mungu ulifanya niachiwe huru baada ya kukaa mahabusu kwa muda wa mwezi mmoja.



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog