IMEANDIKWA NA : ERICK SHIGONGO
*********************************************************************************
Sehemu Ya Kwanza (1)
Septemba 9, 1990
Monrovia - Liberia
Hali ilikuwa imetulia, hakuwepo mtu hata mmoja aliyefikiria kwamba saa chache zijazo zingebadili kabisa maisha ya familia ya bwana na bibi Davis Kanyon na mkewe Christine Steven pamoja na watoto wao wawili, Dorah mwenye umri wa miaka kumi na tisa na kaka yake, Harvey, mwenye umri wa miaka kumi na saba. Jioni hiyo, walikuwa wameketi sebuleni wakipata chakula cha jioni huku mzee huyo akisimulia jinsi familia yake ilivyohamishwa kutoka Marekani mpaka Liberia. Ni historia hiyo ndiyo iliyoonekana kuwavutia zaidi watoto hao, wakataka kupata simulizi yote juu ya nini kilitokea mpaka wakawa hapo.
Huo ndiyo ukweli wanangu, asili yetu sisi ni Marekani.
Nini kilitokea baba? Harvey aliuliza akijiweka vyema kitini.
Ni historia ndefu sana kuisimulia hapo nimeeleza kwa ufupi?
Mh! watoto wakaguna.
Kwa hiyo ina maana tungekuwa Wamarekani? Dorah aliuliza.
Huo ndiyo ukweli wanangu.
Baba kwa nini tusirudi huko? Harvey aliuliza.
Haa! Haa! Haaa! mzee Kanyon akaachia kicheko kikali.
Mbona sasa unacheka?
Nimefurahi lakini ukweli ni kwamba hatuwezi kurejea tena huko, alimaliza mzee huyo.
Vijiko vikaendelea kuingia mdomo kwa kasi wakicheka na kutaniana na mara kadhaa wakiongea mambo mengi kuhusu maisha ya baadaye lakini ghafla mzee Davis akatupa macho yake kwenye televisheni iliyokuwa pembeni kidogo, habari ya kushtusha ilikuwa ikisomwa, taratibu bila kusema kitu akaweka kijiko chake chini na kunyanyuka kitini kisha kuisogelea televisheni.
Mungu wangu! ndiyo kelele pekee iliyosikika.
Mke na watoto nao wakasogea karibu kuangalia ni kitu gani kilikuwa kimetokea.
Kwa masikio yao yote huku wakisikia na kuona ilikuwa ni habari juu ya machafuko yaliyoikumba Liberia, rais wao Samuel Doe, alikuwa amepinduliwa na kundi la waasi la Independent Nationa Patriotic Front lililoongozwa na Prince Johnson kisha kukatwa kichwa chake na kuzungushwa mtaani.
Tumekwisha! Liberia imeingia katika machafuko makubwa, Davis aliongea huku machozi yakimbubujika.
Kimetokea nini? mkewe alihoji, yeye pia alikuwa akilia.
Hata mimi sijui, ndiyo kwanza habari hii naiona hapa sasa hivi.
Tufanye nini sasa?
Haraka tuondoke vinginevyo aliongea Davis na haraka bila kusema tena neno akatoka mbio kuelekea chumbani huku akiwataka watoto wake nao pia wafanye maandalizi na kuchukua vitu vilivyokuwa muhimu.
Wakakubaliana na baba yao, wao pia wakaingia kwenye vyumba vyao na haikuchukua hata dakika tatu wakatoka mbio sebuleni hapo wakimkuta mama na baba wakiwasubiri.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tuombe Mungu wanangu, tunatoroka kukimbilia... aliongea Davis lakini kabla hajamalizia sentensi yake mlango ukasukumwa na kundi la watu waliovalia kijeshi likaingia, mitutu ya bunduki, mapanga na mashoka vikiwa vimetangulia mbele. Ishara tosha ya kuonesha hatari.
We are going to die! (Tutakufa) alisema Davis huku akiwa katika hali ya kutaharuki. Kwa macho yake, bila watu hao kusema kitu, alishuhudia panga likitua kichwani kwa mtoto wake mpendwa Dorah na kuanguka chini huku akivuja damu nyingi kupita maelezo.
Akatupa kila kitu kilichokuwa mikononi mwake ili aingie kazini kupambana lakini tayari alishachelewa wauaji walishamkata mkewe Christine na kumpiga kwa panga kama walivyofanya kwa mtoto wake, akashuhudia kelele moja tu ya mkewe akilalama kwa maumivu kisha kuanguka chini na kukata roho.
Davis akaelewa hivyo vilikuwa ni vita vya kuangamiza familia yake hivyo akajitoa mhanga kama ni kufa basi naye aifuate familia yake. Akiwa na hasira nyingi, akapigana kiume kufa na kupona huku mapanga kadhaa yakiendelea kupita ndani ya mwili wake na akisikia maneno kutoka kwa waasi kwamba ilikuwa ni lazima afe kwani yeye pia alikuwa ni mmoja wa wafuasi wa Samuel Doe.
Lazima afe huyu hakuna kumwacha akiwa hai, ni mmoja wao! alisema mmoja wa waasi.
Ua! Ua! Piga panga ! zilikuwa ni sauti za waasi na sauti ya panga likitua juu mwili wa mtu ikasikika.
Paaa ! ilikuwa sauti ya kipigo ikiambatana na kilio kikali.
Mwili wa Davis ulijaa majeraha makubwa na damu nyingi kuvuja lakini bado aliendelea kujikaza kiume akipambana na kundi la watu wasiopungua kumi lakini mwisho akaonekana kuzidiwa nguvu kwa kushushiwa panga moja kwenye paji lake la uso, ni jambo hilo ndilo lililompeleka chini na kupoteza uhai wake.
Hureee! Hureeee! Hapa kazi tumemaliza twendeni mbele ! zilikuwa ni sauti za waasi ndani ya nyumba wakishangilia ushindi kwa kufanya mauaji ya familia ya David Kanyon.
Wakati waasi hao wakifurahia ushindi kwa mauaji ya kikatili Harvey pekee ndiye aliyekuwa amesalia ndani ya nyumba hiyo kwa kujificha nyuma ya mlango huku akishuhudia ukatili na unyama wote jinsi waasi walivyoitendea familia yake. Moyo wake ukauma kupita kiasi, akalia na kuomboleza huku akimwomba Mungu amnusuru na balaa hilo baya, akailaani siku hiyo kutokea katika maisha yake huku akiapa kutosahau mpaka siku atakapoingia kaburini.
Mara kadhaa taswira ya ndugu zake ilimjia hasa wakati baba yake akisimulia kwamba wao walikuwa ni Wamarekani waliohamishwa kwa nguvu kuja nchini Liberia. Akiwa katika mawazo hayo ghafla akaisikia sauti ya baba yake ndani ya kichwa chake ikijirudia.
Huo ndiyo ukweli wanangu, asili yetu sisi ni Marekani.
Harvey akalia machozi ya uchungu.
Walipohakikisha kwamba kila kitu kimekwenda kama walivyopanga, bila kufahamu kwamba kulikuwepo na mtu mwingine ndani ya nyumba hiyo, waasi wakashangilia na kuanza kutembea kutoka ndani kuelekea nje huku wakiimba nyimbo za ushindi, vishindo vyao vikasikika vikipotea, ishara kwamba walikuwa wakitokomea kuondoka eneo hilo.
Taratibu alipohakikisha kwamba waasi wameondoka eneo hilo, akatoka sehemu aliyokuwa huku akinyata na kusogea karibu na mahali baba yake alipoangukia, akainama na kumtingisha huku akimwita kwa sauti ya kunongona lakini hakuonyesha kuwa na majibu, kwikwi ya kulia ikiwa imemkaba Harvey, akainama na kumbusu baba yake juu ya paji lake la uso huku akitamka maneno.
Shujaa wangu umekwenda, najua umetangulia nami nitafuata muda si mrefu, aliongea kwa uchungu na akafanya vivyo hivyo kwa mama na dada yake na alipomaliza akatembea kuuelekea mlango huku akigeuka nyuma kuangalia maiti zilizokuwa chini, akaishia kuangua kilio.
Moyo wake ukiwa umejawa na hofu kubwa, akatoka mpaka nje ya nyumba na kuangaza huku na kule bila kumwona mtu yeyote, hapo akapiga moyo konde na kuanza kutembea taratibu huku akinyata kuingia barabarani kukiwa na ukimya wa ajabu.
Huku akilia, Harvey hakufanikiwa hata kupita hatua tano mbele, akakutana na maiti za watu zikiwa zimetapakaa njia nzima, hofu ikazidi kuugubika moyo wake, akashindwa kuelewa hatima ya maisha yake lakini akajipa moyo na kuendelea kukimbia kutokomea kusikojulikana. Ukimya aliokutana nao ndiyo uliozidi kusumbua ubongo wake. Eneo lote alilofanikiwa kupita hakukutana na mtu yeyote, hata alipojaribu kutupa macho yake kuangalia ndani ya nyumba hizo hakuambulia kitu zaidi ya maiti nyingi zilizokuwa zimezagaa chini.
Kwa mwendo wa nusu saa nzima bado aliendelea kukimbia peke yake lakini ghafla akiwa amekata tamaa kabisa, kwa mbali alimwona mtu ambaye naye pia alionekana kukimbia kitu fulani. Kwa ishara akamwita na alipogeuka aligundua alikuwa ni kijana ambaye hawakutofautiana naye umri, hivyo bila kuongea kitu chochote wote kwa pamoja wakaanza kukimbia kusonga mbele.
Waliendelea kusonga mbele wakikutana na vijana wengine zaidi, hatimaye kufanya idadi yao kufikia watano lakini bado waliendelea kukuta maiti nyingi zaidi, jambo lililozidi kuwatia hofu ndani ya mioyo yao. Hatimaye mbio hizo ziliwafikisha pembezoni mwa bahari huku hali zao wote zikiwa mbaya.
WAKATI wanalifikia jahazi tayari watu wengine walishaanza kupanda ndani yake, muda mfupi baadaye nao wakalipa fedha zilizohitajika kisha wakaanza kuingia mmoja baada ya mwingine. Ndani yake wakapanda vijana wanne, mmoja
waliyeongozana naye akakosa nafasi kutokana na fedha zake kuwa kidogo. Ni hapo ndipo walipolazimika kumwombea msaada kwa mmiliki ambaye alisita kwa muda lakini walipombembeleza sana hatimaye akawa amekubali, akaungana na wenzake huku furaha ikitawala kati yao.
Safari ikawa imeanzia hapo, ndani ya mioyo yao wote walifikiria kufika walikokuwa wanakwenda na walipozungusha macho yao huku na kule ndani ya jahazi walishuhudia watu wengi wakiwa katika hali kama zao, wao pia walikuwa wamekutwa na matatizo kama ya kwao japo hakuna mtu aliyeongea na mwenzake.
Jahazi likaanza kukatisha bahari na kutokomea, hatimaye wakawa wameondoka. Ndani ya moyo kwa Harvey hali ilikuwa ni tofauti kabisa, muda wote machozi yalionekana kububujika mashavuni mwake, taswira ya familia yake ikiuawa kinyama mbele ya macho yake ikawa inajirudia, moyoni akajilaumu kwa kutoweza kufanya jambo lolote kuokoa maisha yao.
Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi. Mimi nimenusurika na mauaji, nimeondoka Liberia kuingia nchini Marekani nikiwa ndani ya jahazi lakini sina uhakika na huko niendako kama nitafika salama. Ikitokea hivyo basi nitamshukuru Mungu wangu lakini nikiri wazi kwenu ndugu zangu kama kweli kuna sehemu nyingine tutaonana basi na iwe hivyo kwikwi ya kulia ikamkaba Harvey, akashindwa kujizuia na kuangua kilio kikali kilichowafanya watu wote ndani ya jahazi kugeuka na kumwangalia.
Harvey wewe sasa umeshakuwa mkubwa unatakiwa uwe na moyo wa uvumilivu, jikaze bwana wewe ni mwanaume wa shoka mmoja wa vijana aliosafiri nao ndani ya jahazi aliongea akijaribu kumtuliza.
Inauma! Hapa nilipo nimempoteza mama, baba na dada, wote wamekufa nimebaki mimi peke yangu, nimebaki yatima nikiwa sina msaada wowote, ninaichukia hii dunia kwa ukatili wake
Harvey hii ndiyo dunia, sote tumepata majeraha kama yako lakini tunavumilia.
Hakujibu kitu tena, akainamisha kichwa chake chini na kutulia kimya, alionekana kuwa na mawazo mengi kichwani mwake na hata wenzake walipomwangalia waliligundua jambo hilo, wao pia pamoja na kuwa na maumivu ndani ya mioyo yao wakamgeukia Harvey na kumfariji, hakika dunia ilikuwa imemtenda kitu kibaya.
SAFARI ya kuingia nchini Marekani ilikuwa imeanza, watu wote ndani ya jahazi pamoja na kwamba walikuwa na huzuni walikuwa na furaha ya kuondoka nchini Liberia kukimbia vita. Wakalishuhudia jahazi likiyakata maji na kutokomea lakini kwa Harvey hali ilikuwa tofauti kabisa. Muda mwingi alikuwa ameinama chini akigugumia kwa maumivu na kuilaumu dunia kwa unyama iliomtendea.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Taswira za baba, mama na dada yake wakiuawa kinyama mbele ya macho yake ilikuwa ikijirudia mara nyingi ndani ya kichwa chake. Ni hali hiyo ndiyo iliyouumiza zaidi ubongo wake, akayaona maisha kwake hayana maana tena kwani alipoteza nguzo muhimu. Jahazi lilizidi kupasua mawimbi na kusonga mbele.
Wote wamekufa, wameniacha peke yangu! Hivi ni kwa nini dunia haina usawa? alijiuliza swali hilo mara kadhaa ndani ya kichwa chake bila kupata majibu. Aliponyanyua uso wake na kuzungusha macho yake huku na kule ndani ya jahazi, hakumfahamu mtu hata mmoja zaidi ya vijana wanne aliokutana nao njiani wakati wakikimbia kunusuru roho zao, hao ndiyo walikuwa ndugu zake kwa wakati huo.
Siku ya kwanza ilikatika wakiwa bado ndani ya maji, watu wengi walionekana kuchoka na wengine kulalamika njaa lakini hiyo ndiyo ilikuwa safari, nahodha wa jahazi hilo aliwataka kuwa wavumilivu kwani safari ingechukua muda mrefu.
Kama nahodha wa jahazi alivyokuwa amewaeleza mwanzo kwamba safari yao ilikuwa ngumu na iliyohitaji uvumilivu, ndivyo
ilivyotokea. Wiki ya kwanza ilikatika, hatimaye ikaja ya pili wakiwa bado ndani ya bahari. Walipojaribu kudadisi ni lini safari yao ingefika mwisho, walipewa jibu moja tu, kwamba bado safari ilikuwa ni ndefu.
Ikatimu wiki ya tatu na siku nne, watu ndani ya jahazi wakaanza kuchoka. Njaa na kiu viliwasumbua huku wengi wakiugua maradhi mbalimbali, vyakula vilivyokuwa vimechukuliwa ili kukidhi mahitaji ya safari zao vilikuwa vimekwisha. Si hilo tu, hata dawa za huduma ya kwanza nazo zilikuwa zimekwisha, watu wakaanza kupata hofu kama watafika salama, wengi afya zao zilikuwa mbaya kwa kukosa huduma muhimu.
Nakiona kifo mbele yetu, sijui kama tutafika salama huko tuendako? alisema Harvey kwa sauti ya chini.
Mungu ni mkubwa, ukimwomba kitu hawezi kukunyima.
Najua hilo lakini , Harvey alijibu mbele yake aliiona hatari kubwa.
Kwa nini unasisitiza jambo hilo kila mara? rafiki yake mmoja aliuliza.
Mimi mwenyewe nashindwa kuelewa ni kwa nini lakini hivyo ndivyo moyo wangu unavyonieleza.
Hebu achana na hayo mawazo mabaya, unajiumiza moyo bure.
Kwa muda waliendelea na mazungumzo yao, hatimaye usiku ukaingia wakiwa bado safarini. Ni hapo ndipo usingizi ulipowapitia wote, wakalala fofofo huku kelele za watu wachache waliokuwa macho muda huo zikiendelea kusikika, hizo ndizo zilizowaamsha.
Nini kinataka kutokea? aliuliza Harvey akiyafikicha vyema macho yake ili aone vizuri.
Dhoruba!
Dhoruba?
Mh!
Mungu wangu, yametimia.
Kelele nyingi zilitawala ndani ya jahazi, watu wakawa wanalia na kuomba msaada ili kunusuru maisha yao kwani kwa jinsi hali ilivyokuwa, hatari kubwa ilikuwa mbele yao na ingewakumba ndani ya muda mfupi. Bahari ilikuwa imechafuka, upepo na mawimbi makubwa ulikuwa ukivuma kutoka pande kuu nne za dunia, hali ilikuwa imebadilika kabisa.
Abiria wote wakaanza kumwomba Mungu awasaidie kwani kama jahazi lingepinduka tu, basi asingesalia mtu hata mmoja. Watu wote mia moja na ishirini wangekufa maji na miili yao kuliwa na samaki wakubwa baharini.
Mungu ninakuomba unisamehe kwa kila dhambi niliyoitenda na uipokee roho yangu na kuilaza mahali pema peponi, amina! alisema Harvey huku akishuhudia dhoruba hiyo.
Kwa muda wa saa nzima watu wote walishaamka na walionekana kufanya jitihada kubwa ili kujiokoa lakini dhoruba ilikuwa imewashinda. Tayari ndani ya jahazi kulishaanza kuingia maji na taratibu lilianza kupoteza mawasiliano.
Wakati wakifikiria nini wafanye, sauti ya nahodha ikasikika ikiwatangazia kwamba jahazi lilikuwa katika hali ya hatari hivyo kungeweza kutokea kitu chochote, akawataka watu wavae makoti maalum (life jackets) ambayo yangewasaidia wasizame ili kuokoa maisha yao mara jahazi litakapozama.
Hali ya hewa ilishachafuka, hakukuwa na mawasiliano tena ndani ya jahazi, kila mtu alikuwa akifikiria kuokoa nafsi yake na si vinginevyo. Wengi walilia na kujilaumu kwa kuamua kuchukua uamuzi wa kuondoka nchini kwao kukimbia mauaji. Waligundua kuwa kumbe walikuwa wameruka majivu na kukanyaga moto na sasa walikuwa wakifa kwa maumivu.
Harvey alikuwa kimya kabisa, taswira za ndugu zake zilikuwa zikijirudia ndani ya akili zake, akaamini kwamba muda si mrefu angeungana nao huko walikokuwa.
Ninakuja kuungana nanyi muda si mrefu alisema maneno hayo na akashuhudia wimbi kubwa likilipiga jahazi huku watu wakipiga kelele nyingi bila mafanikio. Akiwa hapo akashuhudia wimbi la pili nalo likija kwa nguvu na kulipiga jahazi lao, maji mengi yakaingia ndani. Watu wakaanza kutapatapa huku na kule, wengi wakionekana kuzimia.
Akashuhudia pia watu wakijirusha kutoka jahazini na hadi baharini huku wakizidi kupiga kelele za kuomba msaada bila mafanikio. Harvey akauona mwisho wake, hakutaka kuamini kuwa atakufa kifo cha uchungu cha kuzama bahari na mwili wake kuliwa na samaki wakubwa. Machozi yakawa yanambubujika, pamoja na maumivu hayo alifurahi kwamba alikuwa anakwenda kuungana na baba, mama na dada yake, akajikuta akiachia kicheko.
Wimbi la tatu likapiga tena, safari hii kwa nguvu zaidi. Harvey akashuhudia jahazi likipinduka na hatimaye kuzama huku kelele za watu zikisikika. Ghafla ukimya wa ajabu ukatanda eneo lote.
KELELE nyingi zilitawala ndani ya jahazi, watu wakawa wanalia na kuomba msaada ili kunusuru maisha yao kwani kwa jinsi hali ilivyokuwa, hatari kubwa ilikuwa mbele yao na ingewakumba ndani ya muda mfupi. Bahari ilikuwa imechafuka, upepo ulioandamana na mawimbi makubwa ulikuwa ukivuma kutoka pande kuu nne za dunia, hali ilikuwa imebadilika kabisa.
Abiria wote wakaanza kumwomba Mungu awasaidie kwani kama jahazi lingepinduka tu, basi asingesalia mtu hata mmoja. Watu wote mia moja na ishirini wangekufa maji na miili yao kuliwa na samaki wakubwa baharini.
Mungu ninakuomba unisamehe kwa kila dhambi niliyoitenda na uipokee roho yangu na kuilaza mahali pema peponi, amina! alisema Harvey huku akishuhudia dhoruba hiyo.
Kwa muda wa saa nzima watu wote walishaamka na walionekana kufanya jitihada kubwa ili kujiokoa lakini dhoruba ilikuwa imewashinda. Tayari ndani ya jahazi kulishaanza kuingia maji na taratibu lilianza kupoteza mawasiliano.
Wakati wakifikiria nini wafanye, sauti ya nahodha ikasikika ikiwatangazia kwamba jahazi lilikuwa katika hali ya hatari hivyo kungeweza kutokea kitu chochote, akawataka watu wavae makoti maalum (life jackets) ambayo yangewasaidia wasizame ili kuokoa maisha yao mara jahazi litakapozama.
Hali ya hewa ilishachafuka, hakukuwa na mawasiliano tena ndani ya jahazi, kila mtu alikuwa akifikiria kuokoa nafsi yake na si vinginevyo. Wengi walilia na kujilaumu kwa kuamua kuchukua uamuzi wa kuondoka nchini kwao kukimbia mauaji. Waligundua kuwa kumbe walikuwa wameruka majivu na kukanyaga moto na sasa walikuwa wakifa kwa maumivu.
Harvey alikuwa kimya kabisa, taswira za ndugu zake zilikuwa zikijirudia ndani ya akili zake, akaamini kwamba muda si mrefu angeungana nao huko walikokuwa.
Ninakuja kuungana nanyi muda si mrefu , alisema maneno hayo na akashuhudia wimbi kubwa likilipiga jahazi huku
watu wakipiga mayowe bila mafanikio. Akiwa hapo akashuhudia wimbi la pili nalo likija kwa nguvu na kulipiga jahazi lao, maji mengi yakaingia ndani. Watu wakaanza kutapatapa huku na kule, wengi wakionekana kuzimia.
Akashuhudia pia watu wakijirusha kutoka jahazini hadi baharini huku wakizidi kupiga mayowe ya kuomba msaada bila
mafanikio. Harvey akauona mwisho wake, hakutaka kuamini kuwa atakufa kifo cha uchungu cha kuzama bahari na mwili wake kuliwa na samaki wakubwa. Machozi yakawa yanambubujika, pamoja na maumivu hayo alifurahi kwamba alikuwa anakwenda kuungana na baba, mama na dada yake, akajikuta akiachia kicheko.
WIMBI la tatu likapiga tena, safari hii kwa nguvu zaidi. Harvey akashuhudia jahazi likipinduka na hatimaye kuzama huku kelele za watu zikisikika. Ghafla ukimya wa ajabu ukatanda eneo lote. Ilikuwa ni ajali mbaya katika jahazi hilo lililokuwa na watu mia moja na ishirini. Hakika lilikuwa tukio la kuhuzunisha kupita maelezo.
Ni wakati wimbi la tatu linapiga na Harvey kulishuhudia kwa macho yake likija kwa kasi, akasogea karibu na kijana mmoja kati ya wale waliofanikiwa kukimbia vita pamoja na kumshika mkono huku akimweleza maneno ya uchungu.
Sasa ni wakati wa sisi kufa lakini kabla hatujafa ni lazima tujaribu kufanya kitu, sogea karibu yangu na wote tushikane mikono kwa nguvu, aliongea Harvey na kwa pamoja huku wakitetemeka wakaruka na kuliacha jahazi likizama.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walizama na kuibuka mara kadhaa baharini na walipojaribu kutupa macho yao kuona kama wangepata msaada hawakufanikiwa kuona kitu zaidi ya giza nene lililokuwa limetanda kila upande, wakalia machozi ya uchungu kwamba nao pia wangekufa muda si mrefu.
Harvey?
Mh!
Sidhani kama tutapona.
Tutapona nishike mkono vizuri usiniachie.
Siwezi nimechoka naona nguvu zinaniishia.
Hapana usifanye hivyo kamata vizuri tutapata msaada muda si mrefu.
Akaushika vyema mkono wa Harvey na kwa pamoja wakaanza kusonga kwenda mbele wakijaribu kuokoa maisha yao. Ni juhudi za Harvey akimfariji mwenzake ndizo ziliwafikisha juu ya mgongo wa jahazi wakapanda kwa pamoja na kumshukuru Mungu.
Ahsante Mungu kwa ukombozi wako, hakika huu ni muujiza! aliongea Harvey huku jahazi likisukumwa taratibu na upepo kwenda mbele.
Tunayo kazi kubwa mpaka kufika tunakokwenda.
Kwa neema za Mungu tutafika tu.
Harvey alizidi kumpa moyo mwenzake ambaye alionekana kukata tamaa waziwazi. Wakati jahazi likisukumwa na upepo taratibu walijaribu kuangaza huku na kule kuona kama wangefanikiwa kuona mtu mwingine lakini haikuwa hivyo, wakatoka eneo moja kwenda jingine bila mafanikio.
Wakiwa hawajui muelekeo wa maisha na hatima yao, njaa, kiu na baridi kali viliendelea kuwasumbua lakini hawakupoteza tumaini.
Nasikia homa, aliongea rafiki wa Harvey.
Pole lakini huna budi kuvumilia rafiki yangu, tunachotaka sisi ni kufika Marekani basi, Harvey alizidi kuongea akimpa moyo rafiki yake.
Unachozungumza ni kweli tupu rafiki yangu lakini sijui
Waliongea wakiwa juu ya jahazi hatimaye mchana ukaisha na usiku ukaingia bila kupata msaada wowote ule huku bado wakiendelea kuteseka kwa njaa na baridi kali ambayo ilizidi kudhoofisha miili yao.
Wakiwa juu ya jahazi, bado waliendelea kuona machafuko ya bahari, upepo mkali ukivuma na kulisukuma jahazi. Wakiwa juu yake, waliendelea kumwomba Mungu anusuru maisha yao. Hakika kwao ilikuwa ni safari ndefu na yenye machungu mengi lakini
hawakuwa na jinsi, ilibidi waikubali kwani huko walikokuwa wakitoka hakukuwa na amani, vita ndivyo vilivyotawala na kupoteza ndugu, jamaa na marafiki. Walitaka wafike Marekani, kuanza maisha upya na kutafuta ndugu wengine. Huko ndiko yangekuwa maisha yao yote kama wangefanikiwa kufika wakiwa hai.
Wiki ya kwanza ikakatika, ya pili, hatimaye ya tatu wakiwa bado wako juu ya jahazi bila msaada wowote na hatimaye nao wakaanza kuchoka na kukata tamaa ya kufika Marekani salama, wakakiona kifo mbele yao, afya zao zilikuwa mbaya, wakakonda kupita maelezo na nguvu nazo zikaisha, tumaini la kufika salama likapotea, wakati huo wakakitamani kifo zaidi kuliko uhai.
Harvey!
Unasemaje?
Mimi ninakufa muda si mrefu, nimevumilia vya kutosha naona sasa niachie na kuzama baharini.
Usiniache peke yangu bado nakuhitaji ni wewe ndiye ndugu yangu tafadhali jitahidi.
Siwezi, hali ni mbaya, njaa inanisumbua.
Sikiliza! Piga moyo konde amini kwamba Marekani tutafika.
Lini? Wakati hakuna hata dalili ya kisiwa wala meli baharini ambayo itaweza kutuokoa?
Mungu ataleta muujiza, Harvey aliongea.
Jahazi likazidi kusukumwa na upepo kadiri siku zilivyozidi kusonga mbele ambapo hali ikazidi kuwa mbaya.
Harvey acha mimi nitangulie, hakika siwezi kuendelea tena nimechoka, Mungu akipenda tutaonana.
Nasema hapana, huwezi kufa nitakulinda.
Najua unanipenda kweli lakini si mimi, ni moyo ndiyo umetamani kuwa hivyo, hakika siwezi kuendelea na safari hii ninakufa.
Harvey akageuka na kumshika vyema rafiki yake huku akiongea maneno ya faraja lakini bado hayakuonekana kumwingia kichwani mwake kwani bado aliendelea kusisitiza kwamba ni bora afe. Akajitahidi kwa nguvu zake zote mwisho naye akachoka kubembeleza na kumwachia Mungu aamue.
Akiwa pembeni tu akashuhudia rafiki yake mpendwa, ndugu pekee aliyebaki naye akilegea taratibu na mikono yake kuachia sehemu aliyokuwa amejishikilia, mwisho akasikia kilio kikali kikiambatana na mlio.
Dubwi!
Harvey akalia huku akimwomba Mungu amnusuru rafiki yake na kifo, akiwa juu ya jahazi akashuhudia kwa macho yake akizama mara ya kwanza na kuibuka, mara ya pili ya tatu pamoja na kwamba giza lilishaanza kuingia hakumwona tena akiinuka juu akajua tayari ameshakufa maji.
Akaangua kilio kwani tayari alikuwa amebaki peke yake bila mtu yeyote, kwake tumaini la kufika alikokuwa akielekea lilishaanza kutoweka ndani ya moyo wake.
Nguvu zikiwa zimemwishia taratibu akajilaza juu ya jahazi akiendelea kumwomba Mungu amtendee muujiza. Mara kadhaa alikumbuka familia yake akaziona taswira za baba, mama na dada yake zikimwita awafuate, akashindwa kujizuia na kwikwi ya kulia ikamkaba.
Akaliona giza nene machoni mwake, mwili wake pia ulikuwa ukichemka kwa homa kali, mwisho wake naye ulikuwa umekaribia taratibu akashuka na kujilaza juu ya jahazi akayafumba macho yake na kumwomba Mungu amsamehe dhambi zake zote na ikiwezekana amkaribishe kwenye ufalme wake. Alipomaliza tu salama hiyo usingizi mzito ukamchukua.
Ilikuwa ni ajali mbaya mno ambayo ilichukua maisha ya watu wengi katika kipindi hicho na kuyavuruga kabisa maisha ya kijana Harvey ambaye alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wakisafiri na jahazi hilo lililopinduka likiwa safarini kuelekea Marekani ambako angeanza upya maisha yake akiwa hana ndugu, jamaa wala rafiki. Alikuwa amebaki yatima asiyejua nini kingetokea mbele ya maisha yake, akakiona kifo waziwazi mbele yake.
Kwa muda wa saa tatu mfululizo alilala juu ya boti akiwa kati hali ya kutojitambua, hatimaye saa ya nne upepo mkali ukaanza kuvuma. Huo ndiyo uliomuamsha kutoka katika usingizi mzito aliokuwa amelala, akanyanyua kichwa chake na kuangaza huku na kule akijaribu kuvuta kumbukumbu. Taswira za mauaji pamoja na ajali ya jahazi vikamwijia kichwani mwake, uchungu mkali ukamgubika ndani ya moyo wake. Hakika dunia ilikuwa imetenda kitu kibaya sana maishani mwake, akaapa kutosahau maumivu hayo mpaka mwisho wa uhai wake.
Kadiri muda ulivyozidi kusonga ndivyo hali ya Harvey ilivyozidi kuwa mbaya zaidi huku akijitahidi kwa nguvu kidogo zilizokuwa zimebaki kuendelea kukaa juu ya jahazi. Akawa anamwomba Mungu amtendee muujiza pengine hata wa meli au boti ambayo ingekatisha baharini hapo na kumpa msaada lakini haikuwa hivyo, usiku ukaingia na hatimaye mchana bila kupata msaada Harvey akachoka kabisa.
Homa kali ilizidi kumsumbua, baridi na njaa navyo vilichangia kumweka katika hali mbaya. Akiwa hapo akapata wazo ndani ya kichwa chake la kumkumbuka Muumba wake. Alitaka kufanya sala ya toba pengine kama ikitokea akafa basi aende mahali pema, taratibu akajiweka vizuri na kuanza kusali.
"Mungu wa Mbi .nguni tege meo pekee amba lo ninalo ni wewe, na omba usiniache na ka ma ita to kea basi yata kuwa ni ma takwa yako pu mzisha roho yangu mahali pema lakini pia nitafu .rahi zaidi ni..kiku tana na wape ndwa wangu walio tangulia ahsa nte kwa sababu utanijibu sawa sawa na maombi yangu Ami n..." alisali Harvey.
Kabla hajamalizia sentensi hiyo, nguvu zikamuishia kabisa, pamoja na kwamba muda huo kulikuwa na baridi kali akahisi jasho mwili mzima, mapigo yake ya moyo nayo yalizidi kupotea, kibaya zaidi macho yakaingia kiza, akawa anakiona kifo mbele yake. Akajaribu kufungua mdomo wake angalau kupaza sauti ili kama kuna mtu anapita karibu na eneo hilo aweze kumpa msaada lakini haikuwa hivyo, taratibu akalegea na mwisho akalala juu ya jahazi na kutulia kimya.
***
Madaktari na wauguzi walikuwa katika hekaheka nzito, wakikimbia huku na kule ndani ya wodi, kila mmoja akitumia uwezo wake wote kuhakikisha wanafanikiwa kuokoa maisha ya kijana aliyeletwa hapo muda mfupi akiwa katika hali ya kufa. Baada ya uchunguzi, madaktari wakashauri kwamba ni vyema mgonjwa huyo akapelekwa chumba cha wagonjwa mahututi kwani hali yake haikuwa nzuri.
"Mtundikieni dripu haraka imsaidie kuongeza maji mwilini mwake, halafu pamoja na kuwa katika hali ya kuzimia anaonekana yu katika njaa kali, asaidiwe haraka, mmenisikia?"
"Ndiyo daktari," muuguzi mmoja aliitikia na haraka dripu ikaletwa na mgonjwa akawekewa.
"Mkimaliza hapo apelekwe chumba cha wagonjwa mahututi kwanza mengine yatafuata baadaye"
"Mh!"
Machela ikasukumwa kuelekea chumba cha wagonjwa mahututi, juu yake kijana mzuri alilazwa akionekana kuwa katika hali ya kuzimia, hakuwa akijitambua hata kidogo.
"Masikini wa Mungu, sijui ni nani, ametokea wapi na amekutwa na balaa gani?" muuguzi aliyekuwa anasukuma machela kupeleka chumba cha wagonjwa mahututi alijiuliza maswali kichwani mwake.
Baada ya muda yule muuguzi alifika wodi ya wagonjwa mahututi, mlango ukafunguliwa kisha mgonjwa akaingizwa ndani ambako madaktari wengine walikuwa tayari wameshafika wakimsubiri.
"Tunaweza kuwafahamu ndugu zake?" daktari mmoja aliuliza.
"Kuna mtu amemleta hapa."
"Yuko wapi?"
"Hapo nje?"
"Haraka tunamhitaji hapa ili atusaidie zaidi," alisema daktari na muuguzi akatoka mbio kuelekea nje ya wodi na kumwita mwanaume ambaye ndiye haswa alikuja na kijana huyo.
"Tafadhali tunakuomba wodini," muuguzi alisema na wote kwa pamoja wakatoka eneo hilo huku wakikimbia kuingia ndani.
"Karibu sana"
"Ahsante," alijibu mwanaume huyo huku akionekana kutweta kwa hofu.
"Ah! Tunahitaji jambo moja tu kutoka kwako juu ya mgonjwa."
"Amefariki?" aliuliza mwanaume huyo.
"Hapana"
" Hali yake ni mbaya!"
"Mh! Sina cha kueleza, mimi ni msamaria mwema tu niliyemsaidia na kumleta hapa?'
"Si ndugu yako?"
"Simfahamu hata kidogo, nikiwa baharini katika kazi zangu za uvuvi ndipo nilipomwona akiwa katika hali ya kupoteza fahamu," alijieleza mwanaume huyo kwa ujasiri.
"Inamaana hana ndugu huyu?"
"Ndiyo."
"Basi tunakushukuru kwa msaada wako, unaweza kuondoka sasa."
Kazi ikabaki mikononi mwa hospitali, kwa ushirikiano madaktari na wauguzi wakaapa kufanya kila walichoweza kuhakikisha maisha ya kijana huyo yananusurika na kifo.
"Tutajitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kuhakikisha anapona, pengine anaweza kueleza historia ya maisha yake nini kilimpata."
"Kweli kabisa."
Wakati wakiongea hayo, dripu bado ilionekana kuingia mwilini mwa mgonjwa huku muuguzi maalum akiwepo pembeni ya kitanda chake kumwangalia. Ghafla wakiwa katika majadiliano, sauti ikasikika.
"Daktari dripu yake imesimama kabisa, haiingii tena mwilini."
"Unasema?" tayari walikifikia kitanda cha mgonjwa na daktari mmoja akajaribu kutingisha ili kuangalia kama ilikuwa inatembea au la!
"Ni kweli imesimama kabisa."
"Sasa?"
"Hebu angalieni mapigo yake ya moyo yanakwenda au yamesimama?"
Wakafanya kama alivyoshauri, mapigo ya moyo nayo hayakusikika kabisa.
"Hili ni tatizo, tafadhali mashine ya hewa ya oksijeni iletwe hapa haraka huku tukisubiri jambo hilo apewe msaada wa kushtua moyo "
USHIRIKIANO mkubwa ulikuwa ukionyeshwa ndani ya wodi ya wagonjwa mahututi, kijana ambaye hakufahamika alikuwa ameletwa na msamaria mwema baada ya kumwokota baharini hali yake ilikuwa mbaya, na madaktari walitakiwa kufanya kila walichoweza kuhakikisha wanaokoa maisha yake.
Hebu pimeni mapigo ya moyo yanakwenda sawa hivi sasa?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mh! Hebu tuangalie tena, alijibu muuguzi na ukimya wa takriban sekunde mbili nzima ndani ya wodi ukajitokeza.
Majibu tayari? daktari aliuliza.
Sasa nayasikia japo kwa mbali.
Vizuri nitapenda kupewa majibu kila baada ya dakika kadhaa kuhusu mapigo hayo ya moyo.
Sawa daktari hakuna shida, muuguzi aliyekuwa ameketi pembeni alijibu, huyo ndiye alikuwa amepewa jukumu la kumwangalia mgonjwa huyo.
Kila kitu kilikwenda sawa kabisa na jinsi walivyopanga, mashine ikafungwa na kuendelea kufanya kazi, dripu nazo zilikuwa zikishuka kwa kasi kuingia mwilini, zote hizo zilikuwa ni harakati za kuokoa maisha ya kijana aliyekuwa katika hali ya kufa.
Kama kutakuwa na tatizo lolote basi nipewe taarifa, sawa?
Tutafanya hivyo daktari, muuguzi akajibu na kushuhudia mlango ukifunguliwa na daktari kuondoka ndani ya wodi.
Kazi ya muuguzi ikawa ni moja tu, kupima na kuandika ripoti ya mapigo ya moyo ya mgonjwa kama kumbukumbu ili daktari atakapoingia aweze kumpatia na kuiangalia.
Saa zikazidi kusonga hatimaye jioni ikawadia hali ya mgonjwa ikiwa bado tete madaktari wakibadilishana zamu huyu akitoka mwingine anaingia, lilikuwa ni zoezi gumu mno lakini liliwalazimu kulifanya kwani hiyo ndiyo ilikuwa kazi yao.
Tiiii! Tiiiii! Tiiii! sauti ilisikika ndani ya chumba, ni hiyo ndiyo iliyomzindua muuguzi aliyekuwa pembeni mwa kitanda ambaye alionekana kupitiwa na usingizi.
Nini? aliuliza akinyanyua kichwa chake, akazungusha shingo yake huku na kule ndani ya chumba akijaribu kutafuta ni wapi sauti hiyo ilitokea, ghafla akatupa macho yake kwenye mashine ya hewa ya oksijeni iliyokuwa imefungwa kumsaidia kupumua mgonjwa.
Mungu wangu! alitamka maneno hayo akisogea karibu, akiwa hajui nini cha kufanya akaishuhudia mashine hiyo ikielekea kusimama akapata wazo la kupiga kelele kuomba msaada.
Daktari! Daktari! aliongea muuguzi huyo akifungua mlango na kutoka nje mbio kuelekea ofisini.
Nini tatizo?
Mashine imesimama tafadhali njoo!
Unasema? muuguzi mwingine aliuliza akiwa haamini kama alichokisikia kilikuwa ni sawa.
Naona huna msaada wewe, tafadhali mwite daktari haraka aje, vinginevyo tutamko aliongea muuguzi huyo na kabla hajamalizia
sentensi yake tayari alishaufikia mlango wa chumba cha daktari, akausukuma na kuingia ndani.
Tafadhali twende ukaokoe maisha ya mgonjwa, mashine inayomsaidia kupumua inaonekana kusimama.
Mh! Daktari akaguna tayari naye ndani ya kichwa chake taa nyekundu ilishawaka kuashiria hatari.
Wote wawili wakatoka mbio kueleka chumba cha wagonjwa mahututi hofu nyingi ikitawala ndani ya mioyo yao.
Kimetokea nini kwani?
Kwa kweli sijui daktari, nimeshtuka tu na kukuta hali hiyo.
Hujagusa kitu kweli wewe?
Naapa kwa Mungu imegoma tu yenyewe.
Lakini lazima kutakuwa na tatizo, tayari walishaufikia mlango wa wodi na wote wakaingia ndani huku daktari akitupa macho yake kuangalia mashine.
Hebu tujaribu kushtua tena mapigo yake, aliongea daktari na zoezi hili likaanza mara moja.
Moja mbili tatu zilikuwa ni harakati za kuushtua tena moyo wa kijana aliyekuwa amelala juu ya kitanda akiwa hana fahamu kabisa.
Kwa ushrikiano mkubwa waliendelea kumpa mgonjwa huduma ya kuushtua moyo wake kwa muda wa saa moja bila mafanikio nao pia kama madaktari wakaanza kuingiwa na hofu na kuhisi pengine alikuwa ameshaaga dunia.
Hapana daktari hebu tuendelee kwa muda tuone, muuguzi alitoa wazo ambalo lilikubaliwa na kuanza kufanyiwa kazi.
Zoezi hilo likaendelea madaktari wote wakiwa ndani ya chumba kila mmoja akihakikisha anachangia ipasavyo lakini haikuwa hivyo, mwisho wake wakaanza kukata tamaa kwani walikuwa wamefanya zoezi hilo bila mafanikio yoyote.
Ameshakufa.
Hapana mimi ninaamini ataamka.
Kwa nini unasema hivyo daktari?
Ninazo hisia zote kwamba ataamka hata kama si leo basi kesho.
Jambo la mgonjwa kufa likazua mtafaruku mkubwa ndani ya chumba, makundi mawili yakagawanyika, baadhi wakisema amekwishafariki na wengine wakisema alikuwa katika hali ya kuzimia na muda si mrefu angezinduka.
Wakajipa moyo na kusubiri kwa muda kadhaa wakiamini muujiza ungetokea na mgonjwa angeamka lakini haikuwa hivyo.
Uchunguzi wa mwisho ukaonyesha wazi kwamba tayari alishaaga dunia na hakukuwa na haja tena ya kuendelea kumweka ndani ya chumba hicho hivyo daktari akaandika ripoti ya kifo na kuikabidhi kwa wauguzi ambao wangechukua mwili na kwenda kuuhifadhi chumba cha maiti.
Muuguzi!
Ndiyo daktari!
Mfunikeni vizuri na kumwondoa hapa kumpeleka chumba cha maiti, sawa?
Sawa daktari, wauguzi wakaitika na bila kuchelewa huku wakiwa na sura za majonzi wakafanya kama walivyopewa maelezo na bosi wao.
Wakafanya maandalizi na walipohakikisha kwamba kila kitu kilikuwa sawa wakaubeba mwili na kuulaza juu ya kitanda maalum ambacho kingesukumwa mpaka chumba cha kuhifadhia maiti.
Kwa mwendo wa pole wakaisukuma, hawakuwa na uhakika kama kweli mgonjwa wao alikuwa ameaga dunia lakini wakalazimika kukubaliana na ripoti ya daktari kwani huyo ndiye alikuwa msemaji wa mwisho.
Maskini wa Mungu kijana mzuri kama huyu amekufa kweli?
Ni kweli daktari hawezi kukosea.
Mh!
Lakini wamejitahidi kadiri ya uwezo wao wote nadhani ilikuwa imepangwa hivyo.
Ni kweli kabisa, kibaya zaidi hana ndugu sijui itakuwaje?
Atazikwa na serikali, yalikuwa ni maongezi ya wauguzi wawili wakisukuma machela kuelekea chumba cha kuhifadhia maiti, wao pia walikuwa wakilengwalengwa na machozi.
"KHO!Kho!Kho!"
"Mh!"
"Marehemu amekohoa"
"Nini?"
Tayari wauguzi waliokuwa wakiisukuma machela kuelekea chumba cha kuhifadhia maiti walishaiachia na kutimua mbio huku wakipiga kelele.
"Kimetokea nini?"
"Yule mtu amekohoa wakati ameshafariki kitambo."
"Mnasema kweli?"
"Hakika daktari sisi wenyewe jambo hilo limetustaabisha."
"Hebu twendeni."
Wauguzi wakamtaka daktari atangulie mbele kisha wao wangefuata nyuma kwani bado walikuwa na hofu ya jambo walilolishuhudia muda mfupi uliopita. Kwa mwendo wa haraka daktari alitembea na kuifikia machela ambayo juu yake alionekana kulala mtu akiwa amefunikwa na shuka kuanzia kichwani hadi miguuni.
Huku akionesha hofu machoni mwake, haraka akalivuta shuka na kulifunua huku macho yake yote yakikodoa kumwangalia mtu ambaye aliaminika kufa na sasa alikuwa ameonyesha ishara ya uhai kwa kukohoa.
Kwa takriban dakika tano nzima aliendelea kusimama hapo kuchunguza mwili huo lakini hakufanikiwa kuona kitu, kwa ishara akawaita wauguzi waliokuwa pembeni kidogo na kuwaeleza kwamba mtu huyo alikuwa amekufa kwani hakukuwa na dalili yoyote ya uhai kwake.
"Daktari sisi tunakuambia amekohoa huyu!"
"Hapana, pengine mlikuwa na mawazo vichwani mwenu."
"Tulichokisikia ndicho daktari wala hatujakosea."
"Haraka pelekeni maiti ikahifadhiwe vizuri."
Wakati wakiongea hivyo umati mkubwa ulishafurika eneo hilo, wengi walishapata taarifa kwamba kulikuwa na kijana aliyefariki dunia muda mfupi uliopita na alikuwa akipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti lakini akiwa mlangoni alikohoa.
"Pengine ni kweli jamani labda hajafa!"
"Wewe mtu akishafariki harudi tena."
"Na hao waliosema kakohoa?"
"Ah! Mbona daktari kaja na kumwangalia amethibitisha tena kwamba amekufa kitambo." Yalikuwa ni majibishano ya wagonjwa waliokuwa eneo hilo la hospitali wakionyesha kushangazwa na tukio lililotokea.
Baada tu ya daktari kutoa kauli, wauguzi walisogea tena karibu na machela huku wakitetemeka wakaanza kuisukuma kuiingiza ndani ya chumba lakini hawakufanikiwa kutembea hata hatua mbili, sauti ikasikika kutoka ndani ya shuka.
"Chafya! Chafyaaa!"
"Daktari! Daktari huyu mtu hajafa vizuri hebu mpimeni tena jamani safari hii amepiga chafya tumesikia kwa masikio yetu…" aliongea muuguzi mmoja huku akipaza sauti kumwita daktari.
Ni tukio hilo ndilo lililofanya madaktari wote waliokuwa ndani ya ofisi zao, wengine wodini kutoka mbio kuelekea eneo la tukio kujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea hapo.
"Nini kimetokea tena?"
"Amepiga chafya"
"Mnasema kweli"
"Hakika daktari"
"Mh!" Nao pia wakapigwa na butwaa iweje mtu aliyekufa apige chafya? Hilo likabaki kuwa swali ndani ya vichwa vyao.
"Hebu mrudisheni chumba cha wagonjwa mahututi haraka tukamwangalie kwa ukaribu pengine hajafa amezimia tu!" daktari mmoja alitoa wazo ambalo lilipokelewa na kufanyiwa kazi bila kuchelewa.
Machela ikageuzwa haraka na kurejeshwa chumba cha wagonjwa mahututi, madaktari wote wakifuata kwa nyuma huku kila mmoja ndani ya kichwa chake akijiuliza maswali mengi bila majibu.
Dakika tatu tu tayari machela ilishafikishwa chumba cha wagonjwa mahututi ikaingizwa ndani na mtu aliyeaminika kufariki dunia akateremshwa na kulazwa juu ya kitanda ambacho alikuwa awali, bila kuchelewa madaktari wakakizunguka na kuanza kumchunguza upya.
"Hebu pimeni mapigo yake ya moyo," daktari mmoja aliongea na haraka zoezi hilo lifanyika.
"Mh!"
"Vipi?"
"Mapigo yake nayasikia kwa mbali sana,"
"Hebu mwingine apime naye tusikie atasemaje?"
Daktari mwingine akasogea karibu na kupima mapigo ya moyo naye alitoka na jibu kama la daktari wa kwanza.
"Kama hivyo ndivyo basi leteni mashine ya oksijeni ifungwe tena kisha tuangalie tuone."
"Sawa"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi kila kitu kikafanyika kama ilivyotakiwa na jopo la madaktari na wauguzi wote walikuwa hapo kutoa msaada ambao ungehitajika.
Kadiri muda ulivyozidi kusonga ndivyo hali ya mgonjwa aliyeaminika kufa ilivyoendelea kuwa nzuri, mapigo yake ya moyo yakaendelea kuongezeka na hewa ya oksijeni nayo aliyoyofungiwa ikisaidia kumpa hewa safi.
"Tumwangalie kwa muda wa siku nzima leo tukimchunguza kwa ukaribu ili tuone ataendeleaje lakini kikubwa ni kupima mapigo yake ya moyo kila mara na muuguzi atakayefanya kazi hii ashirikiane na daktari kwa ukaribu tusije tukafanya kosa kama tulilolifanya mwanzo la kumuua mtu wakati bado yuko hai, hili lisitokee tena madaktari wenzangu, sawa?" aliongea daktari mkuu wa hospitali.
"Tutakuwa makini daktari," kwa pamoja walijibu na wakaanza kutoka ndani ya wodi wakimwacha daktari mmoja na wauguzi wawilia ambao wangekuwa hapo kumsaidia mgonjwa muda wote.
Kwa muda wa wiki nzima mfululizo madaktari waliendelea kumhudumia mgonjwa ambaye hali yake ilionekana kuwaridhisha wengi, kikubwa walichotamani kitokee kwa wakati huo ni mgonjwa huyo kuamka na kueleza historia yake kwamba alikuwa nani na alitokea wapi ili kama kungekua na uwezekano basi ndugu zake watafutwe na kupewa taarifa juu ya ndugu yao huyo.
Muda ukazidi kusonga mgonjwa akiwa bado kitandani, kibaya zaidi bila fahamu kama hali yake ilionekana kubadilika siku hadi siku.
"Akiamka tu aeleze ni wapi walipo ndugu zake ili tuwape taarifa haraka."
"Hilo ndilo suala la muhimu kwetu tunamwombea uzima," yalikuwa ni maongezi ya madaktari ndani ya wodi asubuhi ya wiki ya pili walipokuwa wakifanya mzunguko wao wa kila siku.
***
Miezi miwili ilishakatika na mgonjwa alikuwa akiendelea vizuri kabisa, mashine ya hewa ya oksijeni ilishaondolewa na alikuwa akipumua kwa njia ya kawaida jambo lililowafurahisha madaktari waliokuwa wakimpatia matibabu, pamoja na hayo yote tatizo moja kubwa lilikuwa limebaki ambalo lilileta hofu na shaka kwa madaktari, mgonjwa hakuweza kuongea kitu chochote hata walipojaribu kumuuliza wakimdadisi kwamba alikuwa nani na alitokea wapi hawakupata ushirikiano ni kama vile hakuwa na kumbukumbu ya kitu chochote.
"Hili ni tatizo."
"Pengine ni bubu?"
"Hapana inawezekana hii ajali aliyoipata ndiyo imesababisha kuwa hivi"
"Sasa tufanye nini?"
"Mimi naona tumwangalie kwa muda huku tukijaribu kuongea naye kwa upole na upendo ataongea tu," ulikuwa ni ushauri wa Dk. Lewis ambaye alijitolea kuwa karibu na kijana huyo kwa kila kitu. Hali hiyo iliendelea hivyo siku nazo zikizidi kwenda mbele tumaini la madaktari kuona kijana huyo akifungua mdomo kuongea kitu chochote zaidi sana alipoletewa chakula alikipokea na kula kisha kurejea tena kitandani bila kusema kitu chochote.
alikufa na uamuzi wa kumpeleka chumba cha kuhifadhia maiti ukafikiwa, alikuwa amezinduka baada ya kukohoa na kupiga chafya. Akarejeshwa tena wodini, kwenye chumba cha wagonjwa mahututi kuendelea na matibabu, watu wengi wakifika kumwangalia ili kuthibitisha kama habari zilizokuwa zimezunguka kila pembe ni za kweli.
Pamoja na kuzinduka, kijana huyo hakuwa na uwezo wa kuongea chochote, walijitahidi kumsemesha lakini hakuitika wala kujibu maswali yao, ikadhaniwa yawezekana alikuwa ni bubu. Hakuna aliyefahamu kijana huyo alikuwa nani, alitokea wapi zaidi ya kujua tu kwamba baharia mmoja aliyemwokota majini wakati meli yake ikikata maji kuelekea Marekani ndiye aliyempeleka kwenye hospitali hiyo kubwa.
JACKSON Memorial Hospital, ndiyo ilikuwa hospitali kubwa kabisa katika Jiji la Miami, ilitibu watu wote wa maeneo hayo na wengine waliletwa kutoka hata Jacksonville kwa sababu ya huduma zake kuwa nzuri hasa kwa wagonjwa wa majeraha.
Ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi cha hospitali hii ndimo alimokuwa amelazwa kijana huyu, kitanda chake kilikuwa kimezungukwa na madaktari saa moja na nusu asubuhi wakijadili juu ya hali yake.
Do you think he is dumb? (Je, mnadhani ni bubu?) Dk. Lewis .. bingwa wa magonjwa ya wanadamu au kwa Kiingereza taaluma yake huitwa physician, aliwauliza wenzake katika mjadala huo.
I dont think so! aliitikia Dk. Clara Thomas, akimaanisha hakufikiria hivyo kama mgonjwa huyo alikuwa bubu.
Why? (Kwa nini?)
One of the nurses told me yesterday that, he had some hallucinations and spoke some words in the African language. (Mmoja wa wauguzi aliniambia jana kwamba, mgonjwa alipatwa na maluweluwe na kujikuta anasema maneno katika lugha moja ya Kiafrika.)
Sure? (Ni kweli?)
Yeah! (Ndiyo).
Then, he might probably had hit his head somewhere and caused a concussion to his brain, which resulted into memory
loss. (Basi inawezekana alipiga kichwa chake sehemu fulani na kusababisha mtikisiko wa ubongo ambao matokeo yake yakawa kupoteza kumbukumbu.) Dk. Lewis alifafanua akijaribu kutafuta chanzo cha mgonjwa huyo kutoongea.
Or he is just probably depressed! (Au inawezekana ana mfadhaiko wa akili tu.)
May be, we need a CT Scan of the brain urgently. (Tunahitaji kupiga picha ya ubongo haraka.)
Wote wakakubaliana na jambo hilo, Dk. Lewis katika hali isiyo ya kawaida alikuwa ametokea kumpenda sana mgonjwa huyo
mpaka wauguzi na madaktari wengine wote wakagundua kilichokuwa kikiendelea. Hisia zao ziliwatuma kuamini pengine ni kwa sababu alikuwa ni mtu mwenye asili ya Afrika kama yeye.
He is tall, you never know, he might play for the Miami Heat basketball team when he recovers! (Ni mrefu, huwezi kujua, pengine anaweza kupona na kuchezea timu ya mpira wa kikapu ya Miami Heat!)
Wote wakacheka wakiondoka kuelekea ofisini, huku machela ikisogezwa ili mgonjwa abebwe na kupelekwa chumba cha kupigia picha ya ubongo. Hawakwenda hata hatua kumi wakasikia kelele, haraka wakarudi wakikimbia mpaka kando ya kitanda tena na kuwakuta wauguzi wakiwa wamejawa na tabasamu badala ya huzuni.
What happened? (Kimetokea nini?)
He has spoken some few words! (Amezungumza maneno machache.)
Really? (Kweli?) Dk. Clara aliuliza kwa mshangao huku Dk. Lewis akimsogelea mgonjwa kwa karibu kama vile alikuwa hakusikia kilichosemwa.
What is your name? (Jina lako nani?)
Ha rve y!
How old are you? (Una miaka mingapi?)
Kijana huyo hakujibu, alibakia kimya akiangalia tu, ndipo Dk. Lewis akionyesha furaha akaongeza swali jingine la ni wapi alikotokea, akitaka kufahamu historia ya mgonjwa wake ambaye mpaka wakati huo alikuwa hafahamiki vizuri asili yake.
Liberia!
Liberiaaaa!?
Yes.
How?
I am hungry, give me some food then I will be able to narrate my entire story. (Nina njaa, nipe chakula baada ya hapo nitakuwa na uwezo wa kuwasimulia historia yangu yote.)
Hapakuwa na chakula wodini wakati ule, kwani ilikuwa bado ni asubuhi, alichokifanya Dk. Lewis ni kutoka akikimbia hadi nje ambako aliingia ndani ya gari lake na kuendesha kwa kasi hadi kwenye mgahawa wa KFC, uliokuwa umbali wa kama
kilomita tatu kutoka hospitali ya Jackson Memorial. Hapo alinunua chips, baga na vipapatio vya kuku kisha kurejea haraka hadi wodini, ndani ya dakika ishirini, tayari Harvey alikuwa akila na kuendelea kwa takriban saa nzima ndipo akamaliza.
Tueleze sasa.
Kwanza machozi yalianza kumtoka alipokumbuka namna wazazi na dada yake walivyouawa kinyama, picha yote ilionekana akilini mwake, akalazimika kuihamisha kutoka humo na kuiingiza masikioni kwa watu waliokuwa wakimsikiliza. Ilikuwa ni simulizi ya kutisha, ni kweli wote waliona kwenye vyombo vya habari namna ambavyo mauaji yalifanyika huko Liberia lakini kumbe hawakuwa wamepata picha halisi mpaka walipomsikia Harvey.
Hakukomea hapo, akaendelea jinsi yeye na wenzake walivyojaribu kutoroka kuelekea Marekani nchi ambayo baba yake mzazi alimwambia ndiko walikotokea, mateso ya njiani yaliwasikitisha wote waliosikiliza. Harvey akaendelea kuongea huku machozi yakimtoka, namna wenzake wote walivyokufa na yeye kupoteza fahamu kisha kujikuta akiwa hospitalini hapo.
Nani alinileta hapa?
Baharia mmoja.
Anaitwa nani?
Tutaliangalia jina lake na kukuambia baadaye. Dk. Lewis alijibu akijifuta machozi, kwa mara ya kwanza tangu aanze kazi hospitalini, siku hiyo alilia mbele ya mgonjwa jambo ambalo kitaaluma lilikuwa halitakiwi.
Ni muujiza, Mungu alipanga nisife.
Mshukuru sana Mungu, Harvey.
Mungu ni mwema.
Kila mtu alikuwa amefurahishwa na kilichotokea, habari za Harvey zikazidi kuenea, mpaka waandishi wa habari wakawa wanafika wodini kumpiga picha na kuzungumza naye juu ya namna alivyonusurika kifo kimaajabu. Hata hivyo, wiki mbili baadaye, aliruhusiwa kutoka hospitali, akiwa hajui mahali pa kuelekea.
Watu karibu wote waliokuwa ndani ya chombo hicho wanapoteza maisha lakini Harvey kwa mara nyingine tena ananusurika kimiujiza. Anaokotwa akiwa na hali mbaya baharini na msamaria mwema aliyekuwa akijishughulisha na shughuli za uvuvi. Anapelekwa mpaka Miami, kwenye Hospitali ya Jackson Memorial.
Kutokana na hali yake ilivyokuwa mbaya, kila mtu anamkatia tamaa akidhani atapoteza maisha muda wowote, lakini haiwi hivyo. Roho yake inapambana na roho ya mauti na hatimaye anazinduka akiwa wodini na kueleza yeye ni nani, ametoka wapi na nini kilichomsibu. Historia ya maisha yake inawasisimua wengi, akiwemo Dk. Lewis. Anaendelea kupatiwa tiba ya hali ya juu na hatimaye afya yake inaimarika.
BAADA ya hali ya Harvey kuwa ya kuridhisha, madaktari wa Hospitali ya Jackson Memorial, Miami walikubaliana kuwa wamruhusu aondoke hospitali. Cheti maalum cha kumruhusu kutoka hospitali (Discharge Form) kikaandaliwa na kusainiwa na daktari aliyekuwa akisimamia matibabu ya Harvey tangu alipofikishwa hospitalini pale, Dk. Lewis.
Unatarajia kuelekea wapi baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali? Dk. Lewis alimuuliza Harvey wakati akimsindikiza kutoka wodini alikokuwa amelazwa. Katika hali ambayo ilimshangaza Dk. Lewis, Harvey alimueleza ukweli kuwa japokuwa anatoka hospitalini, hajui wapi kwa kwenda kwa sababu hakuwa na ndugu wala mtu yeyote anayefahamiana naye katika Jiji la Miami,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
akamwambia kuwa alikuwa akisali kimoyomoyo kuwa angalau madaktari wachelewe kumruhusu kutoka hospitali kutokana na hali ile.
Sina mtu hata mmoja anayenifahamu kama nilivyokueleza, ni mgeni kabisa hapa Miami na Marekani kwa jumla, natamani Mungu aichukue roho yangu ili nikapumzike na wazazi wangu ahera kuliko haya mateso ninayoyapata, alisema Harvey huku akilengwalengwa na machozi.
Kauli ile iliuchoma sana moyo wa Dk. Lewis, ikabidi amchukue Harvey mpaka kwenye bustani ya maua, jirani na lango la hospitali ile, wakakaa kwenye viti vya kisasa vilivyokuwa vimepangiliwa kinadhifu eneo hilo, wakaanza kuzungumza kwa kirefu. Dk. Lewis alimhoji maswali mengi Harvey, akataka kufahamu kwa kina historia ya maisha yake na mambo yote
aliyokutana nayo maishani mwake. Harvey alizungumza kama alivyoongea mara ya kwanza akiwa wodini. Hakupindisha neno.
Alisimulia kila kitu kuanzia jinsi alivyokuwa akiishi na wazazi wake nchini Liberia kabla hali ya amani haijachafuka na kusababisha mapigano makubwa yaliyozigharimu roho za ndugu zake wote na maelfu ya wananchi. Nimebaki peke yangu,
mimi peke yangu! Nguzo zangu zote zimeanguka hata sijui wapi pa kukimbilia, eeh Mungu, kwa nini mimi?
Usilalamike sana Harvey, umri wako bado ni mdogo na una nafasi ya kuyaanza upya maisha yako kwa kufungua ukurasa mpya, ukiendelea kulalamika mwisho utamkufuru Mungu, amini kila jambo huja kwa sababu limepangwa, jifunze
kumshukuru Mungu kwa kila jambo, alisema Dk. Lewis huku naye akilengwalengwa na machozi. Hali ya maisha aliyokuwa nayo Harvey ilimsikitisha sana, akaamua kwa moyo mmoja kumchukua na kwenda kuishi naye nyumbani kwake.
Kuanzia leo utakuwa ukiishi na mimi, nitakupeleka nyumbani kwangu ambapo nitakutambulisha kwa mke na motto wangu na kuanzia hapo na wewe utakuwa sehemu ya familia yangu. Nimeamua kuyabadili maisha yako na naamini hilo litawezekana, alisema Dk. Lewis huku akiinuka na kumkumbatia Harvey ambaye bado alikuwa akibubujikwa na machozi.
Taarifa ile ilimfanya Harvey apigwe na butwaa kwa muda, masikio yake yakawa kama hayaamini kile alichokisikia kutoka kwenye mdomo wa daktari yule. Hakutaka kuamini kuwa kumbe duniani kuna watu wenye roho nzuri, wenye upendo na wanaoyachukulia matatizo ya wengine kama ilivyokuwa kwa Dk. Lewis. Alimkumbatia kwa nguvu, akazidi kulia kwa
kwikwi, safari hii kwa furaha kwani hatimaye aliamini maisha yake yatabadilika. Baada ya kusimama wakiwa wamekumbatiana kwa muda, hatimaye walianza kuondoka eneo lile hadi nje, Dk. Lewis akamuongoza mpaka eneo alipokuwa amepaki gari lake, wakaingia na safari ya kuelekea nyumbani ikaanza.
Njia nzima hakuna aliyemsemesha mwenzake, Dk. Lewis alikuwa akifikiria namna ya kumfanya Harvey kuwa kijana mwenye
furaha tena kwani ilivyoonesha matukio aliyoyapitia maishani mwake yalimfanya aathirike kabisa kisaikolojia. Lazima nitampeleka shule na kumhudumia kama mwanangu, nahitaji kuwa chanzo cha furaha yake, aliwaza Dk. Lewis wakati gari likizidi kukata mitaa kuelekea nyumbani kwake.
Wakati Dk. Lewis akiwaza hayo, Harvey alikuwa akifikiria yake. Bado kumbukumbu za matukio ya kutisha yaliyozigharimu roho za wazazi wake zilikuwa zikimtesa akilini mwake. Kuna wakati alisikia sauti ikimwambia ndani ya moyo wake kuwa ni
lazima siku moja arejee kwao Liberia na kulipa kisasi kwa wote waliohusika. Hakutaka kuipa nafasi sauti hiyo, nasaha za Dk. Lewis kuwa kila kitu amwachie Mungu zikawa zinamfariji. Akawa anaisanifu mitaa ya Jiji la Miami kupitia dirisha la gari lile.
Baada ya takribani dakika 20, gari liliwasili mbele ya nyumba kubwa ya kifahari, Dk. Lewis akapiga honi ambapo mlinzi
alitoka kufungua geti haraka, gari likaingia hadi eneo la maegesho, wakashuka huku Dk. Lewis akimtaka Harvey kujisikia yupo nyumbani.
Hapa ndipo ninapoishi na familia yangu na ndipo yatakapokuwa makazi yako kuanzia leo, tafadhali kuwa huru kunieleza jambo lolote, nitakuwa pembeni yako kukupa msaada kila utakapohitaji, alisema Dk. Lewis huku akimpigapiga mgongoni
Harvey, wakaelekea kwenye ngazi za kuingilia ndani na kuongoza moja kwa moja mpaka sebuleni.
Kila kitu kilikuwa kama miujiza kwa Harvey. Maisha aliyozoea kuishi kwao Liberia yalikuwa tofauti kabisa na pale Miami. Mandhari nzuri kuanzia nje hadi ndani ya nyumba ile, vilimfanya ajihisi anaingia peponi hapahapa duniani. Dk. Lewis
alilitambua hilo, akawa na kazi ya ziada ya kumchangamsha na kumfanya aone kila kitu ni cha kawaida. Unatumia kinywaji gani? Maji tu yanatosha, alisema Harvey kwa sauti ya kubabaika, Dk Lewis akamwambia kuwa kwa sababu ametoka hospitali, ni bora anywe juisi ya matunda, wazo ambalo aliliunga mkono. Akainuka na kuelekea kwenye friji, akatoa juisi na kuimimina kwenye glasi mbili, wakaanza kunywa taratibu huku wakibadilishana mawazo.
Muda mfupi baadaye, honi zilisikika nje ya geti la nyumba ile, mlinzi akaenda kufungua haraka. Kwa kupitia dirisha la vioo, Harvey aliliona gari la kifahari aina ya Range Rover jekundu likiingia na kwenda kupaki. Mwanamke mrefu wa Kizungu, mwenye nywele ndefu zilizofika mpaka mabegani akateremka na kwenda kufungua mlango upande wa pili, akamteremsha mtoto mdogo aliyekuwa na mchanganyiko wa baba na mama (chotara), akamshika mkono, wakawa wanaelekea ndani huku nyuso zao zikionesha kuwa walikuwa na furaha.
Huyo anayeingia ndiyo mke wangu, ametoka kumchukua mwanangu wa kipekee shuleni, nitakutambulisha vizuri usiwe na wasiwasi, alisema Dk. Lewis, wale watu wakawa wanaelekea pale walipokuwa wamekaa. Dadiiii! I miss u, alisema yule mtoto wa kike, akamkimbilia baba yake na kumrukia, wakakumbatiana kwa muda huku kila mmoja akifurahi, yule
mwanamke akawa anamkazia macho Harvey kama anayejiuliza huyu ni nani? Baada ya hapo, Dk. Lewis alikumbatiana na mkewe na kupigana mabusu, akaanza kumtambulisha mgeni.
Anaitwa Harvey, amekuja kuungana na sisi hapa nyumbani. Oooh! Ndiyo yule kijana uliyekuwa ukinisimulia habari zake, karibu sana na jisikie upo nyumbani, alisema yule mwanamke kwa uchangamfu, akapeana mikono na Harvey.
Harvey, huyu ni mke wangu, anaitwa Suzan Lewis na huyu ni mwanangu wa kipekee, anaitwa Skyler, alisema Dk. Lewis, Harvey akailazimisha furaha machoni mwake, akapeana mikono na Skyler kisha wakaketi. Mke wa Dk. Lewis akaanza kumpa pole upya kwa yaliyomsibu na kumsihi amuachie Mungu kwani yeye ndiye anayepanga hatima ya kila mwanadamu
hapa duniani. Kwa mara nyingine, Harvey alijikuta akishindwa kuyazuia machozi, yakawa yanatiririka kwa wingi na kuyalowanisha mashavu yake.
Licha ya ukweli kwamba karibu watu wote waliokuwa ndani ya chombo hicho kilichopata ajali baharini wanapoteza maisha, Harvey kwa mara nyingine ananusurika kimiujiza na kuokotwa na msamaria mwema akiwa hajitambui. Anapelekwa mpaka Miami, nchini Marekani kwenye Hospitali ya Jackson Memorial.
Baada ya kutibiwa kwa muda mrefu, hatimaye anarejewa na fahamu zake akiwa wodini ambapo anaeleza yeye ni nani, ametoka wapi na nini kilichomsibu. Historia ya maisha yake inawasisimua wengi, akiwemo Dk. Lewis. Baada ya kupata ahueni, anaruhusiwa kutoka
hospitalini lakini anakosa mahali pa kwenda. Hali hiyo inamfanya daktari aliyekuwa akisimamia matibabu yake, Dk. Lewis kujitolea kumchukua na kwenda kuishi naye nyumbani kwake.
Anamtambulisha kwa mkewe, Suzan na mwanaye Skyler ambapo wanampokea kwa mikono miwili. Anayaanza maisha mapya akiwa na familia ya Dk. Lewis.
DK. Lewis na mkewe, walikuwa na kazi ya ziada kumfariji Harvey kwani kuna wakati alishindwa hata kuendelea kula nao chakula cha usiku, kilio cha kwikwi kikawa kinambana mara kwa mara. Kilichomliza zaidi, ni kuona Skyler amekaa katikati ya wazazi wake, huku wote wakiwa na furaha.
Kumbukumbu za wazazi wake zikawa zinamjia, akatamani yeye ndiyo awe amekaa katikati ya baba na mama yake huku ndugu zake wengine wakiwa pembeni, lakini hilo halikuwezekana. Taswira za jinsi wapiganaji walivyoivamia nyumba yao na kuwatoa roho kikatili wazazi na ndugu zake, zilikuwa zikiendelea kupita ndani ya mawazo yake kila baada ya muda mfupi, akawa mtu wa machozi muda wote.
Baada ya kumbembeleza sana, hatimaye Harvey alitulia, wakamalizia kula chakula kisha mke wa Dk Lewis, akawaongoza katika sala maalum. Wote walifumba macho, Suzan akaanza kumuomba Mungu wao.
Baada ya kumaliza kumuomba Mungu wao, wote waliweka mikono yao juu ya kichwa cha Harvey, wakafumba macho na kuendelea kumuombea kwa Mungu amsahaulishe matatizo yote katika maisha yake na kumwezesha kufungua ukurasa mpya.
Skyler, licha ya umri mdogo wa miaka tisa tu aliokuwa nao, alionekana kuimarika sana kiroho kwani alikuwa akisali na kumuombea Harvey kama mtu mzima.
Angalau maombi yale yalisaidia kwani walipomaliza, Harvey alitulia, wakawa wanaangalia runinga kubwa iliyokuwa sebuleni pale. Akili zao zikachukuliwa na mechi ya Ligi Kuu ya Mpira wa Kikapu ya Marekani (NBA) kati ya Miami Heats na Memphis
Grizzlers iliyokuwa inaoneshwa runingani. Mechi hiyo ilipoisha, wote walienda kulala, Harvey akasindikizwa na Dk. Lewis mpaka kwenye chumba chake.
Alimpa nasaha chache, akamuuliza kama atapenda kuendelea na masomo au la, Harvey akajibu kwa shauku kubwa kuwa yupo tayari. Japokuwa mfumo wa elimu kati ya nchi aliyotoka, Liberia na Marekani ilikuwa tofauti sana, Harvey alimhakikishia Dk. Lewis kuwa atajitahidi kukazania masomo ili hatimaye ndoto zake zitimie. Kwa kuwa ilikuwa ni Ijumaa, Dk. Lewis alimwambia kuwa atasimamia mambo yote ili aanze masomo Jumatatu.
Kesho yake kulipopambazuka, Dk. Lewis alienda kumuamsha Harvey asubuhi na mapema, akampa nguo za mazoezi na kutoka naye, wakawa wanafanya mazoezi mepesi kwa kukimbia huku na kule kwenye barabara safi za Jiji la Miami.
Unapenda mchezo gani Harvey?
Napenda sana basketball ila kule kwetu Liberia hakuna viwanja vizuri wala mashabiki wengi wa mchezo huo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hapa Marekani ndiyo penyewe, kuna viwanja karibu kila mtaa, wengine wamejijengea viwanja ndani ya nyumba zao hata mashabiki wengi wanapenda basketball kuliko hata soka au rugby.
Natamani sana kuwa mchezaji hodari wa mchezo huo, naamini Mungu atanisaidia.
Yaah! Kila mwomba Mola hupata. Mtangulize Mungu kwa kila jambo naamini utafanikiwa. Hata umbo lako limekaa ki-
basketball, si unaona ulivyo mrefu ukikazana unaweza kuja kuwa staa kuliko hata Kobe Bryant, Dk. Lewis na Harvey walikuwa wakizungumza huku wakikimbia taratibu pembeni ya barabara kupasha misuli ya miili yao.
***
Jumatatu ilipofika, Dk. Lewis kama alivyokuwa amemuahidi Harvey, aliongozana naye hadi katika shule ya sekondari ya Miami Elementary School, akaingia naye katika jengo la utawala na kwenda kumsajili kwa mkuu wa shule. Kwa kuwa Dk.
Lewis alikuwa akifahamika shuleni pale, hasa ukizingatia kuwa mwanaye Skyler naye alikuwa akisoma palepale, zoezi la kumsajili Harvey halikuwa gumu.
Akapokelewa na kusajiliwa rasmi kama mwanafunzi halali wa shule ile. Ilikuwa ni siku nyingine ya miujiza kwa Harvey. Alishindwa kuzificha hisia za moyo wake, akadondosha chozi la furaha wakati Dk. Lewis akimkabidhi kwa mkuu wa shule, akawa anajiandaa kuondoka kuelekea kazini.
Usilie Harvey, jikaze wewe ni mtoto wa kiume, jitahidi kuishi vizuri na wanafunzi wenzako kama utakuwa na tatizo lolote mtafute Skyler, anasoma hapahapa ila yeye bado yupo shule ya msingi, madarasa yao yapo upande wa kule juu, naamini atakusaidia, alisema Dk. Lewis huku akimpigapiga mgongoni Harvey. Akaondoka na kumuacha shuleni pale ambapo Mkuu wa shule alimuita mwalimu wa darasa wa kidato cha kwanza na kumkabidhi Harvey.
Umekuja na vifaa vyako vyote? aliuliza mwalimu Wisconsin Myler, mwanaume mrefu mwenye upara.
Ndiyo mwalimu, alijibu Harvey kwa nidhamu huku akijitahidi kuyaficha machozi yake.
Haya twende darasani, alisema mwalimu huku akimshika mkono Harvey, akamuongoza mpaka darasani ambapo alimpanga mkondo C. Akayaanza masomo rasmi. Kila kitu kilikuwa kigeni kwake. Mazingira aliyokulia kwao Liberia, shule aliyosoma,
marafiki zake, majengo, nyenzo za kufundishia na vinginevyo, vyote vilikuwa tofauti sana kwa Harvey. Akawa na kazi ya ziada kujitahidi kuendana na maisha mapya pale shuleni.
Jambo ambalo liliwashangaza wanafunzi wenzake na walimu, Harvey muda wote alikuwa kimya kabisa, huku akionekana kuwaza mambo mazito ambayo hakuna aliyeyajua. Hali ile ilifanya wanafunzi wenzake washindwe kujenga naye urafiki kwa urahisi, akawa ni mtu wa kujitenga muda wote huku uso wake ukipambwa na huzuni.
This black dude seems to be so strict like a guerrilla, many students are scared of him,
(Huyu jamaa mweusi anaonekana kuwa siriasi kama mpiganaji wa vita vya msituni, wanafunzi wengi wanamuogopa)
Im scared of him too! He might be with weary historical background and wounded soul.
(Hata mimi namuogopa. Lazima atakuwa na historia mbaya ya maisha ya zamani na nafsi iliyoumizwa).
Wanafunzi wawili walikuwa wakimjadili Harvey bila mwenyewe kujua, muda wa mapumziko baada ya kumuona akiwa amekaa peke yake kwenye bustani za maua, akionekana kuzongwa na mawazo.
Akiwa amekaa katika hali ya huzuni, Harvey alishtukia mikono laini ikimziba macho kutokea upande wa nyuma. Alishtuka
kwani hakutarajia kuna mwanafunzi anaweza kuwa amemzoea kiasi cha kumfanyia masihara kiasi kile. Alimwachia, akageuka kumtazama, macho yake yakagongana na ya Skyler aliyekuwa amejawa na tabasamu pana usoni mwake.
Jamani kaka Harvey! Mbona umekaa peke yako kinyonge namna hii? Nimekutafuta sana, nimeingia madarasa yote sijakuona kumbe umetulia huku? Vipi unayaonaje maisha mapya ya hapa shuleni, alihoji Skyler kwa bashasha za hali ya juu huku akikaa pembeni ya Harvey.
Kwa kiasi fulani, Harvey alichangamka baada ya kumuona Skyler, akainuka pale alipokuwa amekaa na wakaanza kutembea taratibu huku wakibadilishana mawazo.
Maisha mapya ni mazuri, shule nzuri, wanafunzi wazuri na kila kitu kizuri, nafurahi kusoma hapa kwani hapafanani kabisa na shule niliyokuwa nasoma kule kwetu Liberia.
Sasa kama ni hivyo mbona bado unaonekana kuwa na mawazo na muda mwingi umejiinamia kwa huzuni?
Usijali dadaangu, unajua matukio niliyoyashuhudia maishani mwangu yamenifanya niwachukie binadamu wote. Roho inaniuma sana nikiwakumbuka wazazi wangu, ningekuwa na uwezo ningewafuata huko waliko ili na mi Harvey alishindwa kumalizia sentensi yake, kilio cha kwikwi kikambana.
BAADA ya chombo alichokuwa anasafiria Harvey pamoja na maelfu ya watu wengine waliokuwa wanakimbia vita nchini Liberia kupinduka, watu karibu wote waliokuwa ndani ya chombo hicho wanapoteza maisha lakini Harvey kwa mara nyingine ananusurika kimiujiza na kuokotwa na msamaria mwema akiwa hajitambui.
Continued after the jump ....
Anapelekwa mpaka Miami, nchini Marekani kwenye Hospitali ya Jackson Memorial ambapo baada ya kutibiwa kwa muda mrefu, hatimaye anarejewa na fahamu zake na kueleza historia ya maisha yake ambayo inamsisimua kila mtu, akiwemo Dk. Lewis. Baada ya kupata ahueni, anaruhusiwa kutoka hospitalini lakini anakosa mahali pa kwenda.
Dk. Lewis anajitolea kumchukua na kwenda kuishi naye nyumbani kwake, Miami nchini Marekani. Anamtambulisha kwa mkewe na
mwanaye na anayaanza maisha mapya akiwa kama mwanafamilia kwenye familia hiyo. Anafanyiwa mpango wa kurejea shuleni na siku chache baadaye anaanza rasmi masomo ya sekondari kwenye shule ya Miami Elementary School. Hata hivyo, bado jinamizi la huzuni kali linamshambulia.
WAKATI Harvey na Skyler wakiendelea kuzungumza, kengele ya kuingia madarasani iligonga, ikabidi waachane kwani madarasa waliyokuwa wanasoma yalikuwa sehemu mbili tofauti. Harvey aliyekuwa kidato cha kwanza, majengo yao yalikuwa upande wa Kusini wakati Skyler aliyekuwa anasoma shule ya msingi, madarasa yao yalikuwa upande wa Kaskazini wa shule ile ya Miami Elementary School.
Muda wa kurudi nyumbani ukifika unisubiri getini, mama atakuja kutuchukua, alisema Skyler huku akimpungia mkono Harvey, kila mmoja akaelekea darasani kwake. Harvey akawa anajifuta machozi kwa kutumia kitambaa cha mkononi akikwepa kujulikana kuwa alikuwa akilia.
Vipindi vilipoanza, somo lililokuwa la kwanza lilikuwa ni Baiolojia lililokuwa linafundishwa na mwalimu Wisconsin Myler ambaye pia alikuwa ndiyo mwalimu wao wa darasa.
Ok guys, today we are going to discuss about human endocrine system. First of all let us start to discuss a hormone known as Adrenaline. Adrenaline is a natural stimulant made in the adrenal gland of the kidney. Adrenaline is carried in the bloodstream and affects the autonomous nervous system, which controls functions such as the heart rate and secretion of sweat and saliva.
(Leo tutajadili kuhusu mfumo wa homoni wa mwili wa binadamu. Kwa kuanzia tutajadili homoni iitwayo Adrenaline. Hiki ni kichocheo cha asili ambacho kinazalishwa na tezi ya Adrenal kwenye figo. Adrenaline husafirishwa kwenye mkondo wa damu na kuathiri mfumowa neva za fahamu, zinazodhibiti kazi mbalimbali kama mapigo ya moyo,uzalishwaji wa jasho na mate)
Mwalimu Wisconsin alikuwa akifundisha mbele ya wanafunzi wa kidato cha kwanza, akawa anatumia mfumo wa maswali na majibu ili kuwafanya wanafunzi wazingatie alichokuwa anawafundisha.
Aliendelea na somo kwa zaidi ya nusu saa, kabla ya kugundua kuwa kuna mwanafunzi ambaye kimawazo hakuwa pamoja na wenzake.
Harvey, what is Adrenaline? alimuuliza Harvey kwa sauti kubwa, wanafunzi wote wakageuka na kumtazama Harvey ambaye licha ya kuulizwa, alionekana kujiinamia kama ambaye hajasikia kile alichoulizwa.
Harvey? alisema mwalimu Wisconsin kwa sauti kubwa, safari hii akiwa amemsogelea kabisa Harvey.
Kwa mshtuko mkubwa, aliruka pale alipokuwa amekaa, almanusra aanguke lakini mwalimu wake akamuwahi na kumkalisha vizuri. Akachukua karatasi aliyokuwa ameishika na kuanza kuiangalia.
Kumbe wakati mwalimu Wisconsin akifundisha, yeye alikuwa akichora picha za mauaji ya watu wengi vitani na wengine waliokuwa wanazama baharini. Licha ya kuwa hakuwa mchoraji mzuri, kile alichokuwa anakimaanisha kilijidhihirisha kwenye karatasi lile.
Why are you drawing massacre pictures while Im teaching?
(Kwa nini unachora picha za mauaji ya halaiki wakati mimi nafundisha?
That is the only memory I have in my brain, im sorry.
(Hiyo ndiyo kumbukumbu pekee niliyonayo ndani ya kichwa changu, samahani).
Whats is your home country?
(Unatokea nchi gani?) mwalimu Wisconsin alimuuliza Harvey kwa sauti ya chini kiasi kwamba hakuna mwanafunzi aliyesikia.
Liberia, alijibu Harvey.
Go and wait for me at my office,
(Nenda kanisubiri ofisini kwangu) alisema mwalimu Wisconsin baada ya kumuona Harvey ameanza kulengwalengwa na machozi. Alitii maelezo aliyopewa, akakusanya vifaa vyake na kwenda kumsubiri mwalimu yule kwenye ofisi yake.
Baada ya kumaliza kipindi, mwalimu Harvey alifanya mazungumzo marefu na Harvey na kujaribu kumdadisi kwa undani juu ya matatizo yaliyokuwa yanamsumbua. Historia ya maisha yake ilimhuzunisha hata mwalimu yule, lakini akamsisitiza kuwa kwa sababu kilichompeleka pale
shuleni ni masomo, hakukuwa na maana ya kuendelea kukumbuka na kuumia moyoni kwa sababu ya matukio ambayo yalishapita.
Muda mfupi baadaye, kengele ya kuhitimisha muda wa vipindi vya darasani iligonga, wanafunzi wakakusanyika kwenye eneo la mkusanyiko (assembly) na kupewa matangazo machache kabla ya kuruhusiwa kila mmoja kurejea nyumbani kwao.
Harvey! Harvey! Im here (Nipo hapa) alisema Skyler kwa sauti huku akimkimbilia Harvey, akamuongoza mpaka sehemu ambayo mama yake huwa anakuja kumchukua na gari. Muda mfupi baadaye, Range Rover nyekundu iliwasili eneo lile la maegesho, mama yake Skyler akateremka na kwenda kuwachukua Skyler na Harvey. Aliwashika mikono kwa upendo, akawaongoza hadi kwenye gari ambapo safari ya kuelekea nyumbani ikaanza.
Licha ya kila mmoja kuendelea kujitahidi kumfariji Harvey aone kila kilichotokea ni cha kawaida, bado aliendelea kuwa vilevile. Muda mwingi akawa anajitenga na kukaa peke yake akiomboleza vifo vya wazazi na ndugu zake.
Siku ziliendelea kusonga, akafanya mtihani wake wa kwanza ambapo alikuwa mwanafunzi wa mwisho kati ya 45 waliokuwa wanasoma kidato cha kwanza. Matokeo yale yaliwasononesha sana Dk. Lewis, mkewe na mtoto wao Skyler sambamba na walimu wake.
Labda ni kwa sababu ya tofauti kubwa ya mazingira kati ya kwao Liberia na hapa Marekani.
Wala tatizo siyo hilo. Bado anasumbuliwa na msongo wa mawazo na huzuni kali.
Mimi nina wazo, labda tuanze kumpeleka kanisani huenda neno la Mungu likamsahaulisha matatizo yake.
Nilishawahi kuzungumza naye kuhusu suala hilo, akasema hayupo tayari kwenda kanisani kwa sasa kwa sababu haamini kama Mungu yupo. Anasema kama kweli Mungu angekuwepo asingeruhusu wazazi wake wauawe na binadamu waendelee kuteseka kama anavyoteseka yeye.
Mh, kama ndiyo hivyo basi tatizo lake ni kubwa zaidi, alisema mama Skyler, wakabaki kutazamana na mumewe wakiwa hawajui namna ya kumsaidia.
Muhula wa kwanza ulipomalizika, maendeleo ya Harvey shuleni yakawa bado hayaridhishi. Akawa anapata alama za chini katika mitihani kuliko mwanafunzi yeyote. Mwalimu wake wa darasa akawa na kazi ya ziada kuhakikisha anamrejesha Harvey kwenye mstari.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Unaona? Nilikwambia sahau hayo matatizo yako na elekeza nguvu kwenye masomo ukawa huelewi, matokeo yake kila siku unashika nafasi ya mwisho kwenye mtihani, una nini Harvey kisichoisha? mwalimu Wisconsin alikuwa akizungumza na Harvey ofisini kwake.
Alianza upya kazi ya kumshauri lakini wakati akiendelea na zoezi hilo, Harvey alikuwa akitiririkwa na machozi, hali iliyosababisha akatishe mazungumzo naye. Akamwambia aende darasani atazungumza naye siku nyingine.
Siku zilizidi kusonga mbele, Harvey akawa anazidi kuboronga kwenye masomo mpaka wanafunzi wenzake wakawa wanamtania kwa kumuita jina la Bogus. Akaingia kidato cha pili, hali bado ikawa ileile, muda wote akawa ni mtu wa machozi na maombolezo. Furaha ikaendelea kuwa msamiati mgumu kwake.
LICHA ya matatizo anayoyapitia kijana mdogo Harvey, bado Mungu yupo upande wake. Licha ya chombo alichokuwa anasafiria pamoja na maelfu ya watu wengine waliokuwa wanakimbia vita nchini Liberia kupinduka na watu karibu wote waliokuwa ndani ya chombo hicho kupoteza maisha, Mungu anamnusuru, anaokolewa na msamaria mwema anayempeleka Jijini Miami, nchini Marekani kwenye Hospitali ya Jackson Memorial.
Continued after the jump ....
Baada ya kutibiwa kwa muda mrefu, hatimaye anarejewa na fahamu zake na kueleza historia ya maisha yake ambayo inamsisimua kila mtu, akiwemo Dk. Lewis. Baada ya kupata ahueni, anaruhusiwa kutoka hospitalini lakini anakosa mahali pa kwenda. Dk. Lewis anajitolea kumchukua na kwenda kuishi naye nyumbani kwake, Miami nchini Marekani.
Licha ya kuyaanza maisha mapya na kutafutiwa shule, bado huzuni kali inamsumbua Harvey kila anapokumbuka jinsi wazazi wake na ndugu zake walivyouawa kikatili, jambo linalosababisha hata maendeleo yake shuleni kuwa ya kusuasua. Muda mwingi anajitenga na kujiinamia kwa huzuni.
SIKU zilizidi kusonga mbele, maisha ya Harvey shuleni pale yakawa yanazidi kudorora kila siku. Hakuwa na marafiki zaidi ya Skyler, muda wote akawa ni mtu wa kujiinamia huku akionekana kuwa na huzuni kali na majonzi.
Mwaka ulipoisha, aliingia kidato cha pili, bado akawa anafanya vibaya kwenye mitihani yake, jambo lililozidi kuwakatisha tamaa Dk Lewis na mkewe.
Mara kwa mara, Dk Lewis alilazimika kuwa anamtembelea shuleni pale na kumfariji, akimtaka ajitahidi kusahau yote yaliyopita na nguvu zake zote kuzielekeza kwenye masomo. Dk Lewis alizungumza pia na mwalimu wake aliyempokea siku ya kwanza, Wisconsin na kumweleza kuwa kijana wake huyo anahitaji uangalizi wa karibu kwa sababu ya tatizo la msongo na huzuni kali lililokuwa linamkabili.
Najitahidi sana kumuweka sawa lakini haelewi, inaonekana ameathirika kwa kiasi kikubwa sana. Hapendi kuzungumza na mtu zaidi ya Skyler na wenzake wanapomtania, amekuwa akitishia kuwaua.
Sasa unafikiri tutafanya nini mwalimu?
Hatuna cha kufanya zaidi ya kuendelea kumsisitiza akazanie masomo. Muda husahaulisha hata yale ambayo katika hali ya kawaida ni vigumu kuyasahau.
Baada ya mazungumzo yale kati ya Dk. Lewis na mwalimu Wisconsin, alizungumza kidogo na Harvey, akaendelea kumpa ushauri nasaha, kisha akaondoka na kurejea kazini kwake.
Matokeo ya nusu muhula wa mwaka wa pili yalipotoka, bado Harvey aliendelea kuburuza mkia, akashika tena nafasi ya mwisho. Hali iliendelea hivyo hata mwishoni mwa mwaka wa pili, akaingia kidato cha tatu na hatimaye, akaingia kidato cha nne huku historia ya maendeleo yake darasani ikizidi kudorora.
Harvey mwanangu, huu ni mwaka wako wa mwisho, inabidi ujitahidi baba ili angalau upate alama zitakazokuruhusu kuendelea na masomo ya juu, Suzan Lewis, Mke wa Dk Lewis alikuwa akimpa ushauri mwanaye huyo wa hiyari.
Nitajitahidi mama ingawa bado kumbukumbu mbaya zinanisumbua ndani ya kichwa changu.
Kumbukumbu gani zisizoisha Harvey? Kumbuka wewe ni mwanaume, miaka michache baadaye utakuwa na familia yako na itabidi wewe ndiyo uwe kiongozi wa kila kitu. Utaweza vipi kuimudu familia kama hujiamini na badala yake unaumizwa sana na mambo ambayo yalishapita miaka mingi?
Anachokisema mama ni kweli Harvey, jitahidi kakaangu, alidakia Skyler, akaenda kukaa kiti kimoja na Harvey na kumlalia miguuni.
Muda mfupi baadaye, mama Skyler alitoka na kwenda kuandaa chakula cha jioni, akawaacha wakiwa wawili tu sebuleni.
Unajua kaka Harvey wewe ni mzuri sana, yaani kama ungekuwa unazingatia masomo na kuachana kabisa na mawazo juu ya mambo ambayo yalikutokea miaka mingi iliyopita maishani mwako, tayari ungeshakuwa na mchumba mzuri pale shuleni kwani kila siku wasichana unaosoma nao wananiuliza kuhusu habari zako.
Siyo kwamba napenda kuwa hivi Skyler, hata mimi nina moyo, hebu vuta picha kama ndiyo ungekuwa wewe umewapoteza wazazi wako wote wawili pamoja na ndugu zako huku ukishuhudia, ungeweza kusahau kweli?
Ningejitahidi kusahau kaka Harvey, lakini wewe umezidi, yaani kuna kipindi hata mimi naogopa kukaa jirani na wewe. Jitahidi kakaangu, alisema skyler huku akijilaza vizuri miguuni kwa Harvey.
Siku zilizidi kusonga kwa kasi na hatimaye siku ya kufanya mtihani wa mwisho wa kuhitimu elimu ya sekondari iliwadia, Harvey na wanafunzi wenzake waliokuwa wanasoma kidato cha nne, wakaingia chumba cha mtihani. Kwa kuwa walikuwa wakisoma masomo tisa, iliwachukua wiki nzima kumaliza mitihani yote, walipomaliza, ikabidi Harvey arudi nyumbani kwenda kusubiria matokeo.
Miezi miwili baadaye, matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, yalitoka. Katika hali ambayo kila mmoja aliitegemea, Harvey alipata divisheni ziro baada ya kupata alama F katika masomo yote.
Si nilikuambia mwanangu? Unaona sasa umevuna ulichokipanda! alisema Dk Lewis kwa masikitiko.
Mimi mwenyewe kila siku nilikuwa namwambia kuwa elimu ndiyo itakayoziba mapengo ya wazazi wake lakini hakuwa akitilia maanani, sasa wazazi kawakosa na elimu kaikosa pia, aliongezea mkewe.
Unanihuzunisha sana Harvey, sasa unafikiri tutakupeleka wapi ikiwa umeshindwa kufanya vizuri kwenye mtihani?
Nataka kurudi nyumbani kwetu Liberia, lazima nikalipe visasi kwa wote waliohusika kuwapoteza wazazi na ndugu zangu, alijibu Harvey huku akilengwalengwa na machozi.
Yaani mpaka leo bado unafikiria kulipa kisasi? Wewe ni binadamu wa namna gani usiyesahau? alihoji kwa jazba Dk Lewis.
Huyu bwana anajiendekeza, mi nishamchoka, tumtafutie tu nauli aondoke zake, alisema mke wa Dk Lewis.
Hapana mke wangu, tusifanye hivyo, tulishakula yamini ya kuhakikisha tunafanya kila liwezekanalo kuyabadilisha maisha yake, hatutakiwi kukata tamaa.
Mama usimuache kaka Harvey akaondoka, mi nimeshamzoea na nampenda sana kakaangu, mpe nafasi nyingine atajirekebisha, alisema Skyler katika kikao maalum cha wanafamilia kilichowakutanisha Harvey, Dk Lewis, mkewe na Skyler.
Kwa jinsi ilivyoonesha, mama Skyler alishachoka na hali aliyokuwa nayo Harvey lakini bado Dk Lewis na mwanaye Skyler walikuwa na matumaini makubwa kuwa ipo siku atabadilika.
Mimi nina wazo lakini sijui kama Harvey mwenyewe atalikubali.
Wazo gani mume wangu?
Kwa kuwa ameshindwa kufanya vyema katika masomo ya darasani, nafikiri itakuwa busara kama tukimpeleka katika chuo cha ufundi.
Wazo zuri sana mume wangu, hata mimi naliunga mkono.
Hata mimi baba naliunga mkono, alisema Skyler, kwa pamoja wakamtazama Harvey kusikia atasema nini.
Harvey, baba yako ametoa wazo kuwa uende kusomea masomo ya ufundi, mbona unanyamaza kimya bila kujibu chochote? Au hutaki? alihoji mama Skyler, Harvey akafikiria kwa muda mrefu bila kusema kitu chochote, baada ya ukimya wa zaidi ya dakika tatu, akafumbua mdomo wake na kusema kuwa yupo tayari.
Mbona umefikiria kwa muda mrefu kiasi hicho? Kama haupo tayari ni bora useme mapema, tusije tukaharibu fedha zetu ukaishia kufeli kama ulivyofanya kwenye masomo ya sekondari, alisema mama Skyler, Harvey akawahakikishia kuwa yupo tayari kwa moyo wake wote na kwamba atajitahidi kwa kadiri ya uwezo wake wote
Baada ya mazungumzo yale yaliyochukua zaidi ya saa tatu, walimshukuru Mungu wao kisha kila mmoja akaelekea chumbani kwake kulala.
Kulipopambazuka, Dk Lewis alianza kufanya taratibu za kumtafutia Harvey chuo cha ufundi kama walivyokuwa wamekubaliana.
Akaenda kuulizia nafasi katika Chuo cha Miami Engineering College kilichokuwa ndani ya Jiji la Miami, nchini Marekani. Kutokana na kufahamika kwake, Dk. Lewis alipata nafasi haraka katika kitivo cha Mechanical Engineering (Ufundi Makenika).
Kwa kuwa alitembea na kiwango cha fedha kilichokuwa kinatosha kulipia karo, alimaliza kila kitu. Akalipa ada ya mwaka mzima na kurudi nyumbani akiwa na furaha. Akamuita mkewe, Harvey na mwanaye Skyler ambapo walikaa tena kikao cha familia na kuwaeleza alipokuwa amefikia.
Kila mmoja alifurahi sana, hata Harvey mwenyewe kwa mbali alionesha kutabasamu ikiwa ni ishara ya kufurahishwa na jinsi familia ya Dk. Lewis ilivyokuwa inamjali.
MCHUMA janga hula na wa kwao! Tabia ya kuendekeza huzuni na kumbukumbu zenye kuumiza inamfanya Harvey ashindwe kuzingatia masomo yake. Hali hiyo inasababisha apate matokeo mabaya kwenye mitihani yote, tangu akiwa kidato cha kwanza hadi cha tatu. Hatimaye anaingia kidato cha nne, licha ya ushauri anaopewa na walezi na walimu wake mara kwa mara , bado anashindwa kuzingatia masomo na matokeo yake anapata divisheni ziro kwenye mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari.
Continued after the jump ....
Matokeo hayo yanawasikitisha sana Dk Lewis na mkewe, wanajadiliana nini cha kufanya kwenye kikao cha familia lakini Harvey anangangania kuwa anataka kurejea kwao Liberia na kulipiza kisasi kwa wote waliohusika kuwaua wazazi na ndugu zake. Hata hivyo, baadaye anabadili msimamo ambapo anakubaliana na wazo la kupelekwa kwenye chuo cha ufundi.
Ari mpya inaamka ndani ya moyo wake, anajiapiza kuwa atafanya kila liwezekanalo kushindana na huzuni kali na mawazo mabaya yaliyokuwa yanamtesa, anaweka nadhiri ya kuhakikisha anasoma kwa bidii na kuwafuta machozi walezi wake ambao matokeo yake ya kidato cha nne yaliwavunja sana nguvu. Dk Lewis anaanza taratibu za kumtafutia chuo, anaenda kumuandikisha Miami Polytechnic and Engineering College ambapo anamtafutia nafasi katika kitengo cha Mechanical Engineering.
HARVEY alifarijika sana kwa namna Dk Lewis na familia yake walivyoendelea kuwa naye katika hali zote. Kitendo cha wao kuanza kufikiria nini watamfanyia baada ya kufeli mtihani wa kidato cha nne, kuliamsha ari mpya iliyokuwa imepotea ndani ya moyo wake. Akatambua fika kuwa walikuwa na nia ya kweli ya kumsaidia hivyo hakutaka kuendelea kuwavunja moyo.
Akaahidi kufanya kila linalowezekana ili afaulu masomo yake ikiwa kama malipo ya fadhila alizokuwa anafanyiwa. Kwa kuwa chuo kile kilikuwa na nafasi za bweni pekee, maandalizi ya vifaa vyote muhimu vilivyokuwa vinahitajika, yalianza kufanyika. Dk Lewis akamchukua Harvey na kwenda kufanya shopping ya vitu mbalimbali vilivyokuwa vikihitajika shuleni.
Baada ya kuzunguka kwenye maduka mbalimbali kwa siku mbili mfululizo, vifaa vyote muhimu kwa ajili ya Harvey vilipatikana, akawa anafanya maandalizi ya mwisho kabla ya kuondoka kuelekea chuoni.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jamani kaka Harvey, unaondoka unaniacha na nani? Mi nishakuzoea jamani, alisema Skyler huku akifungua mlango wa chumba cha Harvey, akaingia na kwenda kujitupa kitandani kwa Harvey. Alimjibu kwa kifupi kuwa atakuwa akienda kuwatembelea pale nyumbani kwao mara kwa mara kwa kuwa chuo hakikuwa mbali, akaendelea kupanga vitu vyake.
Licha ya kumwambia vile, Skyler hakuridhika, akainuka pale kitandani alipokuwa amelala na kusimama, akamsogelea Harvey huku machozi yakimlengalenga. Harvey alizitambua hisia zake, naye akamsogelea na kumkumbatia kwa nguvu, Skyler akajilaza kifuani kwake kama mtoto afanyavyo anapobebwa na mama yake huku machozi yakiulowanisha uso wake mzuri.
Usijali dadaangu, kimwili tutakuwa mbali lakini kiakili tutaendelea kuwa pamoja, wala usiwe na wasiwasi.
Hapana kaka Harvey, mi najisikia wivu mwenzio najua huko unakoenda utakutana na wasichana wazuri watakaokushawishi uanzishe nao uhusiano wa kimapenzi.
Hapana Skyler, mimi sipo hivyo, we mwenyewe unanijua. Lakini hata hivyo, kwani we hupendi kaka yako nikuletee wifi mzuri?
Sitaki, sitaki kabisa kusikia hizo habari kumbe hunipendi kaka Harvey.
Basi nisamehe dadaangu, nakupenda sana na sitaki kukuudhi! Si unajua we ndiyo dadaangu wa ukweli? alisema Harvey, lakini
katika hali ambayo hata yeye ilimshangaza, Skyler hakutaka kumuachia, aliendelea kumkumbatia kwa nguvu kifuani kwake huku machozi yakiendelea kumtoka.
Basi usilie Skyler, nenda chumbani kwako kalale si unajua tayari ni usiku na kesho unatakiwa kuwahi shuleni? alisema Harvey lakini Skyler akawa ni kama hasikii. Aliendelea kumkumbatia kwa muda mrefu mpaka aliporidhika, akamuachia huku macho yake yakizungumza lugha ambayo hakuielewa.
Baada ya Skyler kuondoka, Harvey aliendelea na maandalizi yake, alipomaliza akaenda kuoga na kurudi chumbani kwake kulala. Vitendo alivyofanyiwa na Skyler vilimfanya ajiulize maswali mengi kichwani mwake bila majibu. Akajipa moyo kuwa hakuna chochote kibaya alichokuwa anakiwaza kwani alimchukulia kama mdogo wake waliyezaliwa tumbo moja.
Kulipopambazuka, familia nzima ilimsindikiza Harvey mpaka chuoni. Saa moja za asubuhi juu ya alama, Range Rover nyekundu iliyokuwa inaendeshwa na mke wa Dk. Lewis, Suzan iliwasili kwenye lango la kuingilia kwenye Chuo cha Miami Polytechnic and
Engineering College, pembeni yake akiwa amekaa mumewe na siti ya nyuma wakiwa wamekaa Harvey na Skyler.
Baada ya kukamilisha taratibu za pale langoni, waliruhusiwa kuingia mpaka ndani, gari likaenda kusimama mbele ya jengo lililokuwa na maandishi makubwa yaliyosomeka Adminstration Block, wakateremka na kuanza kushusha mizigo. Baada ya kukabidhiwa kwa wakufunzi wa chuo kile, waliagana tayari kwa kuondoka.
Kaka Harvey nakuomba uniweke mimi kwenye kumbukumbu zako muda wote. Usinisahau jamani, nakupenda sana kakaangu, alisema Skyler huku akiwa amemkumbatia Harvey wakati wakiagana. Skyler alimkumbatia Harvey kwa muda mrefu huku akionekana kuvuta hisia nzito, mpaka mama yake alipopiga honi na kumwambia kuwa atachelewa shule, akamuachia huku akijifuta machozi.
Mwanao kamzoea sana Harvey, atajisikia vibaya sana kuishi naye mbali, hebu mtazame anavyolia, Dk Lewis alikuwa akiongea na mkewe wakati Skyler akitembea kinyonge na kuingia ndani ya gari. Gari likaanza kuondoka huku wakipungiana mikono na Harvey. Skyler alishindwa kujizuia, akawa analia kwa kwikwi.
Walimfikisha mpaka shuleni kwao, akateremka na kuelekea darasani huku akionekana kuwa mnyonge kuliko siku zote. Baada ya hapo, mama Skyler alimpitisha mumewe kazini kisha na yeye akaelekea ofisini kwake.
Harvey akawa ameyaanza maisha mapya chuoni kwani muda mfupi baada ya familia yake kuondoka, alipelekwa kwenye bweni walilokuwa wanaishi wanachuo wenzake wa mwaka wa kwanza, akapewa chumba ambacho tayari kulikuwa na wanachuo wengine watatu, yeye akawa wa nne.
Alipoanza rasmi masomo, kidogo alijitahidi kujirekebisha, akawa siyo mtu wa kukaa na kujiinamia peke yake, nguvu zake zote alizielekeza kwenye masomo ingawa bado hakupenda kujichanganya na wenzake, muda mwingi akawa anautumia darasani baada ya masomo akawa anapenda kwenda kufanya mazoezi ya mpira wa kikapu kwenye uwanja wa chuo.
Taratibu akaanza kuuelewa mchezo huo kuliko mwanzo, siku zikawa zinazidi kusonga mbele, akayazoea maisha ya chuo na wanachuo wenzake wakaanza kumfahamu na kupenda kufanya naye mazoezi ya mpira huo.
Ebwana kuna yule mwanafunzi mgeni wa mwaka wa kwanza anaitwa nani sijui, mweusi hivi halafu mrefu, anacheza basketball huyo, sijapata kuona.
Anaitwa Harvey lakini tatizo lake huwa hapendi kabisa kujichanganya na wenzake, hata mazoezi huwa anafanya peke yake.
Nasikia hata alipokuwa anasoma sekondari alikuwa anapenda kujitenga hivyohivyo, sijui ana matatizo gani?
Lakini licha ya kujitenga kwake, mi namkubali sana kutokana na jinsi alivyo na kiwango kikubwa, akibadili tabia zake anaweza kuja kuwa mtu maarufu sana hapa Marekani na duniani kote. wanafunzi wawili, Mike na Angelus waliokuwa wanasoma chuo kimoja na Harvey, walikuwa wakimjadili.
Si hao tu, uwezo mkubwa wa Harvey kwenye mchezo wa basketball ulimfanya awe gumzo chuo kizima, kila mahali akawa anazungumziwa yeye ingawa wengi walikuwa wakishangazwa na tabia yake ya kupenda kujitenga. Mabinti nao walichanganywa sana na jinsi Harvey alivyokuwa na umbo zuri la kimazoezi. Kifua chake kilikuwa kimejengeka vizuri kimazoezi, mikono yenye
nguvu na urefu wake, vilikuwa ni miongoni mwa vitu vilivyowachanganya sana wanachuo wa kike.
Japokuwa Harvey alikuwa akiishi chuoni hukohuko, karibu kila mwisho wa wiki Skyler alikuwa akienda kumtembelea na kumpelekea zawadi mbalimbali yakiwemo maua, kadi, chokleti na vitu vingine vizuri kwa lengo la kumfariji na kumsahaulisha matatizo aliyokuwa nayo.
Kila mwisho wa wiki hakukosa kufika chuoni pale mpaka wanachuo wengine hasa wa kike wakaanza kumchukia kwani waliona kama anawanyima nafasi ya kuongea na Harvey. Wachache waliufahamu ukweli kuwa alikuwa mdogo wake ingawa wengine walikuwa wakihisi kuwa huenda wana uhusiano mzito wa kimahaba.
HARVEY! Harvey! Tafadhali simama nahitaji kuongea na wewe, nipe nafasi ya dakika tano tu zitatosha kabisa, ilikuwa ni sauti nyororo ya msichana mrembo aliyeitwa Suzan ambaye walisoma darasa moja na Harvey.
Sawa, Harvey alijibu.
Tunaweza kusogea pembeni kidogo?
Bila shaka
Taratibu wakajikongoja na kusogea pembeni.
Harvey tafadhali nipe muda wako kidogo, ni siku nyingi nimehitaji kuongea na wewe jambo fulani lakini moyo wangu umekuwa na kigugumizi.
Nieleze tu wala usiogope.
Kwanza kabisa nahitaji kujua hivi kweli Skyler ni dada yako?
Ukimya wa dakika kama tatu ukatokea, wote wawili ni kama vile walishikwa na vigugumizi.
Suzan! Harvey aliita.
Mh!
Niwie radhi kwa swali langu nahitaji kujua tu.
Uliza tu usijali.
Unajua ukweli kutoka moyoni mwangu wewe kama mwanaume umeshasoma macho yangu ukaelewa nini nataka kutoka kwako, Harvey ni siku nyingi tu nimekupenda na mara nyingi joto la penzi limekuwa likinitesa ndani ya moyo wangu aliongea Suzan.
Harvey akanyanyua macho yake na kumkodolea Suzan akijaribu kuyasoma macho yake kwa umakini wa hali ya juu, alitaka kuona dalili zilizokuwa ndani ya macho yake kwamba kweli alimpenda kama alivyomaanisha.
Akayashuhudia machozi yakitiririka mashavuni mwa msichana huyo mrembo, akashawishika kunyoosha mikono yake na kumkumbatia kisha kumsihi aache kulia na amjibu swali alilokuwa amemuuliza.
Sikiliza Suzan, mimi na Skayler ni mtu na dada yake huo ndiyo ukweli wangu na ninaomba uupokee.
Ni kweli?
Hakika.
Lakini watu wanasema ninyi ni wapenzi?
Si kweli hata kidogo, ninachokueleza mimi ndicho hicho.
Mh! Suzan akaguna huku akimwangalia Harvey .
Basi naomba mimi niwe mpenzi wako kama kweli Sklayer ni dada yako?
Suzan sijawaza wala kufikiria kuwa na mpenzi ingawa umri wangu unaniruhusu kufanya hivyo nataka nisome mpaka nitimize
malengo na ndoto zangu zote ndipo mapenzi yafuate, aliongea Harvey machozi yakimbubujika. Alikuwa katika kipindi kigumu katika maisha yake, mara kadhaa alipoikumbuka familia yake na maisha aliyowahi kuishi huko nyuma yalikuwa yakimuumiza sana, alitamani kuwa na wazazi wake wote pamoja na dada yake lakini bahati mbaya walikuwa wametangulia mbele ya haki.
Harvey kwa nini unalia? Nimekuudhi? Basi naomba unisamehe halikuwa kusudio langu ni mapenzi ndiyo yamenipeleka huko, Harvey ninakupenda tangu siku ya kwanza nilipokuona na ningependa uwe wangu.
Hapana Suzan kwa sasa siko tayari nipe muda kwanza nitakujibu.
Mpaka lini?
Sijui ila ninaomba muda ahsante na naomba sasa tuagane mimi niende bwenini kupumzika.
Basi sawa lakini weka jambo hili kichwani mwako kwamba mimi Suzan ninakupenda ningependa siku moja niwe wako, alimaliza Suzan na kila mmoja akashika njia yake.
Ni kweli kabisa tangu Harvey aingie chuoni hapo siku ya kwanza tu Suzan alipomwona alihisi mapigo yake ya moyo yakienda kasi, alimpenda kijana huyo kupita maelezo na alikuwa akitafuta ni namna gani angeweza kumwingia kijana huyo ampate na kuwa wake
lakini maneno ya watu wengi chuoni humo yalimvunja moyo kwamba kijana huyo asingekubali kuwa mpenzi wake kwa sababu tayari alishakuwa na wake tangu mwanzo na hata yeye mwenyewe Suzan pamoja na kusikia aliona kwa macho yake jinsi Harvey alivyopendwa na Skayler ndiyo maana baada tu ya kupata wasaa wa kuongea naye alijaribu kutupa ndoano yake bila woga wowote.
***
Nitaendelea kumpatia zawadi mfululizo bila kuchoka na mwisho nitamwingiza kwenye mtego wangu, siko tayari kumkosa Harvey, nataka awe wangu kwa gharama yoyote ile, eti kaka nani kasema, hiyo ni danganya toto tu nadhani hata yeye mwenyewe hajagundua kwamba ninahisi penzi ndani ya moyo wangu, nitahakikisha ninampata aliwaza Skyaler siku moja akiwa chumbani
kwake akitazama albamu ya picha na kuiona picha ya mwanaume aliyempenda na kuapa kumpata.
Alipoingia ndani ya nyumba yao na kutambulishwa kwake kama kaka yake, Skyaler alimpokea lakini kadiri siku zilivyozidi kusonga
alihisi hali ya tofauti, uzuri wa kijana huyo uliichanganya akili yake pamoja na kwamba alikuwa katika hali ya ugonjwa lakini uzuri wake hakika haukujificha hata kidogo, moyoni mwake akaapa kumfanya mpenzi wake wa maisha pamoja na kufahamu kwamba hilo lilikuwa ni kosa la jinai kwani wazazi wake wasingekuwa tayari kukubali jambo hilo.
Najua itakuwa ngumu lakini nitaufanya kwa siri kubwa uhusiano wangu mimi na Harvey na nitamweleza wazi kwamba muda mwingi nimekuwa nikimtaka mapenzi najua hata yeye hatakataa, atakubali kwa uzuri nilionao, aliwaza Skyaler akivuta shuka lake na kujifunika gubigubi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ndani ya kichwa chake alifahamu wazi kwamba alikuwa akicheza mchezo hatari lakini ambao pengine ungeleta shida au matatizo katika maisha yake lakini alitaka kujaribu bahati yake kwa kuwa na kijana mzuri kama Harvey.
Nitasubiri akirudi tu likizo nimweleze ukweli naye nitamtaka afanye siri kubwa sihitaji baba wala mama afahamu uhusiano wetu, lakini pia nitahakikisha anapata mahitaji yote muhimu kama ilivyo kwangu ninampenda kuliko maelezo
Wanakaa kikao cha familia kujadili nini cha kufanya baada ya Harvey kufeli, mwenyewe anasisitiza kuwa anataka kurejeshwa nchini kwao Liberia kwa ajili ya kazi moja tu, kulipa kisasi kwa wote waliohusika kuiangamiza familia yao. Dk Lewis, mkewe na mtoto wao, Skyler wanajaribu kumbadilisha mtazamo ambapo baadaye wanafikia muafaka kuwa apelekwe kwenye chuo cha ufundi.
Anaandikishwa katika Chuo cha Miami Polytechnic and Engineering, katika kitengo cha Mechanical Engineering. Anayaanza masomo huku akiahidi kurekebisha makosa aliyoyafanya awali. Anaelekeza nguvu zake zote kwenye masomo huku akiutumia muda wa ziada kufanya mazoezi ya basketball. Kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele, anazidi kungara katika mchezo huo, hali inayosababisha wanachuo wengi wa kike waanze kumtamani kimapenzi.
Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO
KAKA Harvey mbona siku hizi nikija kukusalimia nakukuta unazungumza na wasichana unajua mi sipendi Harvey, sipendi nasema, alilalamika Skyler na kumfanya Harvey awe na kazi ya ziada kujitetea mbele yake.
Lakini Skyler nilishakwambia kuwa sihitaji kuwa nao kimapenzi kwa sasa, naomba uniamini, usimwambie baba au mama, sina uhusiano wowote nao, alisema Harvey kwa kujitetea, akiamini anafanya yale mbele ya mdogo wake, kumbe haikuwa hivyo kwa upande wa Skyler, kichwani mwake alikuwa akiwaza mapenzi.
Wivu wa kimapenzi ulikuwa ukimsumbua ndani ya mtima wake. Japokuwa hakuwahi kumtamkia jambo lolote la kumtaka kimapenzi, aliamini ishara alizokuwa anamuoneshea zinatosha kufikisha ujumbe aliokusudia. Jambo hilo lilimfanya ajisikie vibaya kila alipokuwa anaona wasichana wanamshangilia Harvey anapokuwa kwenye mazoezi ya basketball.
Baada ya Harvey kutumia muda mwingi kumbembeleza, hatimaye Skyler alitulia, wakawa wanapiga stori na kukumbushana mambo mbalimbali ya nyumbani.
Yaani siku hizi hadi najiona kama nakonda, nilikuzoea sana kaka Harvey napata sana shida kwa kuwa muda mwingi upo mbali nami.
Usijali Skyler, bila shaka utafurahi sana kusikia kaka yako nimefaulu masomo ya chuo, nakumbuka jinsi ulivyoumizwa na matokeo yangu ya kidato cha nne, jikaze bado miezi michache nitarudi nyumbani kwa likizo fupi, alisema Harvey huku akimpigapiga Skyler mgongoni kumbembeleza.
Baada ya kukaa pamoja kwa saa zaidi ya mbili, Harvey alimsisitiza Skyler umuhimu wa kuwahi nyumbani. Kwa shingo upande Skyler akakubali kuondoka kwa ajili ya kwenda kufanya maandalizi ya shule siku inayofuatia kwani siku ile ilikuwa ni Jumapili.
Kwani mimi nina kasoro gani mpaka Harvey hanitamkii kuwa ananipenda? Kwa nini anavutiwa na kina Suzan na wanachuo wengine wa kike kuliko mimi, alijisemea Skyler muda mfupi baada ya kuwasili nyumbani kwao, akiwa nyuma ya kioo kikubwa chumbani kwake.
Akavua nguo moja baada ya nyingine na kubaki na skin-tight pekee, akawa anageuka na kujishika kiuno kama wafanyavyo warembo wanapokuwa kwenye mashindano ya umiss. Alifanya vile kwa muda mrefu, akawa anajikagua kila kiungo katika mwili wake kuona kama hana kasoro.
Sura yangu nzuri na inawavutia wengi, hata mama huwa ananiambia kila siku kuwa mimi ni mzuri sana kifua changu bado kichanga, rangi ya ngozi yangu inafanana na chokleti kwa nini Harvey hanipendi lakini? Kwa nini? Roho yangu inauma sanaaa, alisema Skyler huku akilengwalengwa na machozi, akazibana vizuri nywele zake ndefu na nyeusi, zilizokuwa zinakaribia kufika kiunoni.
Harvey I love you baby, please be mine, come and show me the meaning of love come and teach me how to love
(Harvey nakupenda mpenzi, nakuomba uwe wangu, njoo unioneshe maana ya mapenzi njoo unifundishe namna ya kupenda )
alisema Skyler kwa sauti ya kunongona huku ameikumbatia picha ya Harvey kwenye kifua chake kilichokuwa na vifuu vyenye ukubwa wa wastani na ngozi laini kama sufi, akajilaza chali taratibu akiwa bado ameikumbatia picha ile, machozi yakawa yanatiririka kupitia kona za macho yake na kulowanisha shuka.
***
Harvey alizidi kupata umaarufu pale chuoni kwao, idadi ya marafiki zake ikaanza kuongezeka kwa kasi. Japokuwa hakuwa mwepesi wa kuwachangamkia watu wengine, kutokana na jinsi alivyokuwa anacheza vizuri mchezo wa basketball, alijikuta wanachuo wenzake wakianza kumchangamkia kila wanapomuona, jambo lililomfanya taratibu aanze kuachana na tabia ya kujitenga.
Siamini kama Harvey mimi naweza kuheshimika kiasi hiki, tazama kila ninapopita nasikia wanachuo wenzangu wakilitaja jina langu siamini kabisa. Hata darasani kila mtu anapenda kukaa karibu na mimi, naona kama muujiza mkubwa eeh Mungu nisimamie, bado safari yangu ni ndefu, Harvey alijisemea akiwa amejilaza juu ya kitanda cha double decker, ndani ya bweni
kwenye chuo cha Miami Polytechnic and Engineering College alipokuwa anasoma.
Kumbukumbu za mambo yaliyomtokea zamani zikawa zinamezwa kwa kasi na faraja na sifa alizokuwa anazipata kutoka kwa wanafunzi wenzake kwa sababu ya kiwango kikubwa cha mchezo wa basketball alichokuwa nacho.
Harvey, tunakuomba uwe unafanya mazoezi na timu ya chuo ya basketball kwani siku chache zijazo mashindano ya NCCA yataanza na hatutaki chuo chetu kipate aibu tunaamini utakuwa mchango mzuri kwetu, nahodha wa timu ya mpira wa kikapu ya chuoni pale, Cazzard Emmert alikuwa akimwambia Harvey.
Harvey alikubali, habari ambazo zilipokelewa kwa furaha na wanachuo wengi, kila mmoja aliamini ataibeba timu yao kutokana na kipaji kikubwa alichokuwa nacho.
Kama alivyoahidi, siku iliyofuatia Harvey akaanza rasmi mazoezi na timu ya chuo ikiwa ni maandalizi ya michuano mikubwa ya mpira wa kikapu kwa wanafunzi wa vyuo nchini Marekani iliyopewa jina la National Collegiate Athletic Association au kwa kifupi NCAA.
Michuano ya NCAA, kwa kawaida ilikuwa ikizishirikisha timu za mpira wa kikapu kutoka vyuo zaidi ya 68 ambapo kwa miaka mingi, Vyuo Vikuu vya UCLA, Kentucky, Indiana, North Carolina na Duke ndivyo vilivyokuwa vikibadilishana ushindi na kushika nafasi za juu.
Mwaka huu ni zamu ya Miami Polytechnic and Engineering College kuchukua ubingwa, tumejifua vya kutosha na nawaomba wapenzi wa mchezo huu wa basketball waishangilie timu yetu kwani tuna wachezaji wenye ari, nguvu na kila sababu ya kuchukua ubingwa kama Harvey, nahodha wa timu ya mpira wa kikapu ya chuo kile, Cazzard alikuwa akitoa tambo kwenye runinga wakati
akihojiwa na kituo maarufu cha CBS kilichokuwa kinasifika kwa kuonesha vizuri mechi zote za mashindano hayo.
Shamrashamra za maandalizi ya mashindano hayo ambayo yalipangwa kuzinduliwa rasmi kwenye makao makuu ya NCCA yaliyopo White River State Park, Indianapolis katika Jimbo la Indiana nchini Marekani ziliendelea kwa nguvu, Harvey akazidisha
kasi ya kufanya mazoezi ambapo kila baada ya kumaliza ratiba ya mazoezi na timu ya chuo alikuwa akitenga muda wa mazoezi binafsi.
Harvey bwana mi sipendi uwe unafanya mazoezi kifua wazi, si unaona wale wasichana wanavyokuangalia kichokozi, umbo lako limejengeka vizuri sana, usilioneshe ovyo, cheki kifua kilivyotanuka, alisema Skyler jioni moja baada ya kumtembelea Harvey chuoni pale na kumkuta akifanya mazoezi na timu ya shule huku wasichana wengi wakiwa wamekaa makundi-makundi pembeni ya uwanja.
Wote walionekana kumkazia macho Harvey na alipokuwa anafunga magoli walikuwa wakimshangilia kwa nguvu. Harvey alimjibu Skyler kuwa amemuelewa alichokisema, akaahidi kuwa hatakaa kifua wazi tena.
Siku zikawa zinasonga kwa kasi, hatimaye siku ya ufunguzi wa mashindano hayo ikawadia. Harvey na wanachuo wengine wakasafiri kwa basi la shule hadi Indianapolis, mahali ufunguzi wa mashindano hayo ulipokuwa ukifanyika. Timu yao ikawa miongoni mwa ambazo zilipanga kuanza mechi siku ya ufunguzi.
Licha ya kupata matokeo mabaya kwenye mtihani wa mwisho wa kuhitimu kidato cha nne, Dk Lewis na familia yake bado wanaahidi kumsaidia Harvey kwa uwezo wao wote. Hali hiyo inamfanya aamue kuwatoa kimasomaso kwa kukazana kwenye masomo na kuendelea na mazoezi ya mpira huo wa kikapu.
Nyota ya umaarufu inaanza kumuwakia kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza mpira wa kikapu. Anaanza kuwa gumzo miongoni mwa wanachuo wenzake na anaitwa kuichezea timu ya chuo kwenye mashindano makubwa ya mchezo wa mpira wa kikapu kwa wanafunzi wa vyuo nchini Marekani (NCAA).
Upande wa pili, Skyler anaanza kuonesha dalili za mapenzi kwa kaka yake huyo wa hiyari lakini Harvey anakuwa mgumu wa kumuelewa kwani anamchukulia kama mdogo wake. Wanachuo wa kike nao wanazidi kuchanganywa na uzuri na kipaji alichokuwa nacho Harvey.
Michuano mikubwa ya mpira wa kikapu kwa wanafunzi wa vyuo nchini Marekani iliyopewa jina la National Collegiate Athletic Association au kwa kifupi NCAA, ilizinduliwa rasmi katika makao makuu ya NCAA yaliyopo White River State Park, Indianapolis katika Jimbo la Indiana nchini Marekani.
Wanafunzi kutoka kwenye vyuo vipatavyo 68 vikiwemo UCLA, Kentucky, Indiana, North Carolina na Duke walifurika kwa wingi kwenye uzinduzi huo. Chuo cha Miami Polytechnic an Engineering nacho hakikuwa nyuma.
Ratiba ikaonesha kuwa timu ya chuo alichokuwa anasomea Harvey kitafungua mashindano hayo kwa kucheza na timu ya UCLA, mechi ambayo ndiyo ilikuwa ya kwanza kabisa. Vuguvugu la sintofahamu likatanda miongoni mwao kwani UCLA ndiyo walikuwa mabingwa watetezi.
Muda mfupi baadaye, wachezaji waliokuwa katika kikosi cha kwanza na wale wa ;reserve' wa Chuo cha Miami Polytechnic Engineering and College walishabadilika kimavazi ndani ya chumba cha kubadilishia mavazi, wakatoka wakikimbia mpaka kwenye
uwanja, wakaanza kufanya mazoezi mepesi mepesi ya kupasha misuli moto huku wakishangiliwa na mashabiki wao.
Muda mfupi baadaye, pambano lilianza rasmi ambapo Harvey alikuwa ni miongoni mwa wachezaji walioanzia benchi. Mtifuano mkali uliendelea huku wanafunzi wa vyuo hivyo wakishangilia kwa nguvu kila mchezaji wa timu yao alipokuwa akigusa mpira.
Baada ya muda, chuo cha akina Harvey kikawa kimeelemewa kimchezo, hali iliyosababisha wafungwe vikapu vingi mfululizo.
"Kocha muingize Harvey," alisikika Cazzard akimwambia kocha wao ambaye alikuwa ni mwalimu wa michezo pale chuoni kwao. Bila kupoteza muda, Harvey akasimama na kuanza kupasha misuli yake, mabadiliko yakafanyika haraka, Harvey akaenda kuongeza nguvu kwenye timu yake ambayo sasa ilikuwa ikifungwa pointi nyingi.
Kama wengi walivyotarajia, Baada ya Harvey kuingia, alianza kuonesha uwezo wake kwa kuwakimbiza sana wachezaji wa timu pinzani na ;ku-score' mfululizo kuisawazishia timu yake. Dakika chache baadaye, timu yao ambayo ilikuwa nyuma kwa pointi nyingi, ikaanza kuwakaribia wapinzani wao na hatimaye matokeo yakawa sawa.
Harvey akawa anajitahidi kuwachezesha wenzake kwa kasi, hali ya mchezo ikabadilika mara moja, wakawazidi wapinzani wao kimchezo na kuanza kuwaelemea. Wanachuo wa Miami Polytechinic, wakawa wanashangilia kwa nguvu huku wakilitaja jina la Harvey kama shujaa wao.
Hali hiyo ilizidi kumpa morali Harvey, akazidi kuwachangamsha wenzake na baada ya muda kupita, timu yao ikawa inaongoza kwa pointi nyingi. Waandishi mbalimbali wa habari za michezo wakawa wanasubiri kwa hamu mchezo uishe ili wapate kumfanyia mahojiano Harvey, ambaye kwa hakika alionekana kuwa nyota wa mchezo.
Mchezo ulipoisha, Harvey alizungukwa na waandishi wa habari kutoka vituo mbalimbali vya runinga na redio, akawa anaulizwa historia fupi ya maisha yake, wazazi wake na namna alivyojiingiza kwenye mchezo. Licha ya furaha aliyokuwa nayo Harvey kwa kuweza kupigana kiume kuiokoa timu yake, bado hakufurahishwa na maswali ya waandishi wa habari
"Natokea Miami Polytechnic and Engineering College, " alikuwa akijibu kwa ufupi Harvey huku akiondoka na kuelekea chumba cha kubadilishia nguo. Waandishi wengi wa habari walipigwa na butwaa kwani Harvey hakuwapa ushirikiano kama walioutegemea, wakahisi kuwa huenda ni mara yake ya kwanza kufuatwa na vyombo vya habari kwa wingi namna ile.
"Mbona unalia Harvey! Wenzako tunafurahi wewe umejiinamia unalia, nini tatizo?" nahodha wa timu yao, Cazzard alikuwa akimuuliza kwa upole Harvey, baada ya kumuona anatokwa na machozi ndani ya chumba cha kubadilishia nguo. Wenzake karibu wote hawakuwa na habari naye, wakawa wanaendelea kusherehekea ushindi mnono walioupata.
Baada ya Cazzard kujaribu kumbembeleza, Harvey alinyamaza, akabadilisha jezi na kuvaa nguo zake alizokuwa amezivaa awali, akavaa na miwani ya jua kuficha macho yake ambayo yalishabadilika na kuwa mekundu kutokana na kulia.
Baada ya mchezo ule, jina la Harvey likapaa maradufu, kila mmoja akawa anamzungumzia yeye. Hata wanafunzi wa vyuo vingine walishangazwa na uwezo mkubwa aliouonesha siku ya kwanza tu ya michuano hiyo. Baada ya mechi nyingine za ufunguzi kuisha,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Harvey na wanachuo wenzake waliingia ndani ya basi lao la shule na safari ya kuelekea chuoni kwao ikaanza.
Walipofika chuoni, Harvey alipitiliza bwenini kwao na kwenda kulala. Maswali aliyoulizwa na waandishi wa habari kuhusu historia yake yakawa yanajirudiarudia kichwani mwake. Akaona ni kama wamemtonesha donda ambalo lilikuwa bado halijapona. Baada ya muda usingizi ukampitia, akalala na kuwaacha wanachuo wenzake wakizidi kusherehekea ushindi mnono walioupata siku ya kwanza tu ya michuano ile.
***
"Anaitwa nani?"
"Harvey."
"Urefu wake ukoje?"
"Unafaa sana kwa mchezo wa mpira wa kikapu, hebu angalia hii video ya mechi ya ufunguzi, mhusika ni huyu mwenye kitambaa mkononi," maafisa wa timu ya mpira wa kikapu ya Miami Heat walikuwa wakijadiliana jioni ya siku ile, baada ya kurejea kwa wawakilishi wao waliowatuma kwenda kufuatilia michuano ya NCAA na kujaribu kutafuta vipaji vipya vya mchezo huo kwa ajili ya timu yao.
"Tunatakiwa kutafuta vijana wenye uwezo na vipaji vikubwa kama huyu Harvey, si mnaona wapinzani wetu wa Chicago Bulls wanavyotishia kutupokonya ubingwa wetu msimu huu?"
"Ni kweli meneja… huyu kijana atatufaa sana, nashauri mazungumzo ya awali yaanze kufanywa kati yetu na uongozi wa chuo anachosoma."
Kikao kilimalizika, viongozi wakakubaliana kuendelea kumuangalia kwa karibu mchezaji huyo huku wengine wakianza mchakato wa mazungumzo na chuo alichokuwa anakisomea.
Siku ya mechi ya pili ya Chuo cha Miami Polytechnic dhidi ya Chuo cha Arkansas iliwadia. Watu wakawa wanasubiri kwa shauku kumuona Harvey kwani habari zake zilizotangazwa na vyombo vya habari baada ya mechi ya ufunguzi, ziliwashtua wengi. Kama kawaida, Harvey na wanachuo wengine wakasafiri kwa basi la chuo mpaka kwenye Chuo cha Arkansas kwani walipangiwa mechi ya ugenini.
Tofauti na mechi ya awali, Harvey alipangiwa kuanza katika kikosi cha kwanza, Cazzard akamkabidhi ukapteni wa timu, jambo ambalo angalau lilimpa faraja Harvey. Akapania kuhakikisha anafanya maajabu kwa mara nyingine.
Mchezo ulipoanza tu, Harvey alifunga kikapu cha kwanza ndani ya sekunde chache na kuipa timu yake ushindi wa mapema, akaongeza kasi na kuwachezesha vilivyo wenzake, jambo lililofanya wapate pointi nyingi ndani ya dakika tatu za mwanzo. Uwanja mzima ukawa unalipuka kulitaja jina la Harvey kila alipopata mpira.
"Harvey! Harvey! Harvey!" uwanja mzima ulilipuka, mpaka mashabiki wa timu pinzani ambayo ndiyo ilikuwa mwenyeji wakawa wanamshangilia.
Skyler alikuwa akimalizia kufanya ;homework' aliyopewa shuleni kwao. Akaamua kuwasha runinga kuangalia kilichokuwa kinajiri, macho yake yakatua kwenye mechi ya mpira wa kikapu ambapo alimuona mtu kama Harvey akiruka na ;kudank' kwenye goli la wapinzani, akakimbilia chumbani kwa baba na mama yake ambapo aliwaita harakaharaka, wote wakakimbilia sebuleni kumuangalia.
MAISHA ya Harvey, kijana mdogo kutoka nchini Liberia aliyekimbia mauaji ya halaiki yaliyozigharimu roho za wazazi na ndugu zake, yanaanza kubadilika akiwa katika Chuo cha Miami Polytechnic and Engineering College nchini Marekani ambapo taratibu anaanza kusahau maumivu ya kuwapoteza wazazi wake na yote yaliyotokea akiwa njiani kukimbia mapigano nchini kwao.
Licha ya kupata matokeo mabaya kwenye mtihani wa mwisho wa kuhitimu kidato cha nne, Dk Lewis na familia yake bado wanaahidi kumsaidia Harvey kwa uwezo wao wote. Hali hiyo inamfanya aamue kuwatoa kimasomaso kwa kukazana kwenye masomo na kuendelea na mazoezi ya mpira huo wa kikapu.
Nyota ya umaarufu inaanza kumuwakia kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza mpira wa kikapu. Anaanza kuwa gumzo miongoni mwa wanachuo wenzake na anaitwa kuichezea timu ya chuo kwenye mashindano makubwa ya mchezo wa mpira wa kikapu kwa wanafunzi wa vyuo nchini Marekani (NCAA).
Upande wa pili, Skyler anaanza kuonesha dalili za mapenzi kwa kaka yake huyo wa hiyari lakini Harvey anakuwa mgumu wa kumuelewa kwani anamchukulia kama mdogo wake. Wanachuo wa kike nao wanazidi kuchanganywa na uzuri na kipaji alichokuwa nacho Harvey
Ingawa Harvey alipata matokeo mabaya kwenye mtihani wa mwisho wa kuhitimu kidato cha nne, Dk Lewis na familia yake bado wanaahidi kumsaidia kwa uwezo wao wote kumjengea maisha bora. Anaandikishwa katika Chuo cha Miami Polytechnic and Engineering College nchini Marekani.
Taratibu anaanza kusahau maumivu ya kuwapoteza wazazi wake na yote yaliyotokea akiwa njiani kukimbia mapigano nchini kwao na anaelekeza nguvu zake zote kwenye masomo na mazoezi ya mpira wa kikapu.
Nyota ya umaarufu inaanza kumuwakia kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza basketball. Anakuwa gumzo kwenye mashindano makubwa ya mchezo wa mpira wa kikapu kwa wanafunzi wa vyuo nchini Marekani (NCAA) ambapo anaiongoza timu yake kupata mafanikio makubwa.
Timu kubwa ya mpira wa kikapu nchini humo, Miami Heat inavutiwa na uwezo wake na sasa imeshaanza taratibu za kumshawishi ajiunge nayo. Fungu kubwa la fedha linatengwa kwa ajili ya usajili wake.
Mama ona ona, yule si kaka Harvey yule?
Ni yeye jamani hata siamini macho yangu.
Mi nilijua tu huyu Harvey ana kitu kikubwa alichojaaliwa na Mungu ila bado hajaanza kujitambua, alisema Dk Lewis na kukumbatiana na mkewe na Skyler.
Ni fahari kubwa kwetu, ila bado kuna jambo anatakiwa kusaidiwa sitakata tamaa kumtafutia washauri wa kisaikolojia ili kumsahaulisha kabisa yote aliyowahi kuyapitia maishani mwake, alisema Dk. Lewis, wakakaa kwenye viti na kukodolea macho runinga.
Kila mmoja alinyamaza kwa muda, lakini baadaye Skyler alishindwa kuvumilia, akawa anashangilia kwa nguvu na kurukaruka mbele ya baba na mama yake. Furaha aliyokuwa nao iliwazidi wote, akajikuta akizidi kumpenda ndani ya moyo wake na kumfanya muda wote achekecheke mwenyewe. Waliangalia runinga mpaka kipindi kile cha michezo kilipoisha, kila mmoja akaondoka kuelekea chumbani kulala huku wakiwa na furaha tele.
Skyler alipofika chumbani kwake, alichukua picha ya Harvey na kuikumbatia, akawa anakimbiakimbia mle chumbani huku akiwa na furaha ambayo sasa ilionekana kupitiliza.
We Skyler si ulale, furaha gani isiyo na mwisho?
Hapana mama, niache nifurahie mafanikio ya kakaangu mpendwa Harvey, nampenda sana, alisema Skyler akiwa chumbani kwake, akaendelea kufurahi kwa muda mrefu mpaka usingizi ulipompitia. Akawa anaweweseka na kuzungumza maneno asiyoyaelewa akiwa usingizini.
Mwanao ana nini leo? Mbona mpaka muda huu anaongea peke yake na kucheka?
Atakuwa anaweweseka huyu, ni kawaida yake kuweweseka kila anapolifikiria jambo moja kwa muda mrefu.
Hebu nenda kamlaze vizuri, anaweza kupata madhara usiku, alisema Dk Lewis, mkewe akaamka na kuelekea chumbani kwa mwanaye ambapo alimkuta akiwa amelala huku amekumbatia picha ya Harvey, jambo lililomfanya ajiulize maswali mengi kichwani. Hata hivyo aliamua kupuuzia, akaichukua ile picha na kuiweka mahali pake, akamlaza vizuri Skyler na kumfunika, akazima taa na kurejea chumbani kulala.
Unajua mume wangu lazima tuwe makini sana na uhusiano wa Skyler na Harvey, wanazidi kukua na kama unavyomuona mwanao Skyler ameshakuwa mwali sasa.
Ni kweli mke wangu, lakini kwa namna tunavyowalea watakuwa wanachukuliana kama kaka na dada na si zaidi ya hapo.
Ni sawa lakini si unajua akili za vijana wanaovuka kipindi cha mpito na kuingia utu uzima? Mi nafikiri itabidi nitafute siku ya kukaa na Skyler na kuzungumza naye mambo kadhaa nampenda sana mwanangu na sipo tayari kuona maisha yake yanaingia dosari kwa namna yoyote ile, alisema mama Skyler huku akijifunika vizuri, wakaendelea kulala.
***
Wakati kila mtu akiendelea kuyafurahia mafanikio makubwa aliyoyapata Harvey, kwa upande wake bado hakuwa na furaha kama ile waliyokuwa nayo wanachuo wengine.
Hivi nitaendelea kuteswa mpaka lini na historia ya maisha yangu? Nafikiri ni muda wa kuwa mkweli kwa nafsi yangu na waandishi wa habari ili kila mtu ajue historia halisi ya maisha yangu, nitaeleza kila kitu kilichonitokea, alijisemea Harvey akiwa amelala chali na kutazama juu ya dari la bweni.
Licha ya kuwa ilikuwa ni usiku sana, bado Harvey hakuwa amepata usingizi hata chembe. Alidhamiria kueleza kwa waandishi wa habari kila kitu kuanzia jinsi alivyokimbia mapigano nchini kwao Liberia mpaka alivyopokelewa na Dk Lewis.
Siku iliyofuatia, kama kawaida Harvey aliwahi kuamka na kwenda kufanya mazoezi kwenye viwanja vya mpira wa kikapu shuleni pale. Baada ya kumaliza, alianza kujiandaa kuingia darasani kwani siku hiyo alikuwa na kipindi cha kwanza kinachoanza asubuhi na mapema.
Nakuomba ukimaliza kipindi chako cha kwanza uje kwenye ofisi ya Dean of Students, kuna jambo la muhimu nahitaji kuongea na wewe, mlezi wa wanachuo au maarufu kama dean, alimwambia Harvey asubuhi na mapema wakati akiingia kwenye kipindi cha kwanza.
Harvey alimjibu lakini akawa anajiuliza maswali mengi juu ya sababu za kuitwa kwa dean asubuhi yote ile. Hata wakati profesa wa kipindi cha kwanza akiendelea kufundisha, Harvey hakuwepo kabisa kimawazo, akawa anafikiria kwa kina bila kupata majibu juu ya alichoitiwa.
Kipindi kilipoisha, wanachuo walianza kutoka, Harvey bila kuchelewa akaongoza moja kwa moja kwenye ofisi ya mlezi wa wanachuo.
Kuna ujumbe wako kutoka kwa uongozi wa Miami Heat, wanahitaji kuja kuzungumza na wewe ana kwa ana kuhusu kuingia nao mkataba wa kuichezea timu yao nje ya muda wa masomo.
Whaaat? Miami Heat? Mbona mimi ndiyo kwanza nimeanza kucheza mpira siku mbili hizi, nitawezaje kumudu kuwa na timu kubwa kama ya Miami Heat?
Jiamini kijana, una sifa zote anazotakiwa kuwa nazo mchezaji bora wa mpira wa kikapu, ukiona mpaka viongozi wa Miami Heat wamekuja hapa kukufuata, ujue neema ipo jirani kukufikia.
Hakuna timu inayolipa vizuri wachezaji kama Miami Heat, ukifanikiwa usinisahau na mimi kwenye ufalme wako, alisema yule mlezi wa wanachuo na kumtoa wasiwasi Harvey, wakawa wanacheka kwa furaha huku akimtaka ajenge moyo wa kujiamini.
Habari ile ilimfanya Harvey ajihisi kama yupo kwenye njozi tamu, akawa anaomba kimoyomoyo kuwa kile alichoambiwa na mlezi wao kisiwe ndoto bali ukweli utakayoyabadilisha kabisa maisha yake.
Mechi mbili tu za mpira wa kikapu alizoiongoza timu yake ya Miami Polytechnic and Engineering College dhidi ya timu za Vyuo vya UCLA na Arkansas zilimfanya ageuke gumzo kila mahali. Hakutaka kuamini kuwa uwezo ule wa siku mbili tu aliouonesha unaweza kuwachanganya watu kiasi cha kuwaniwa na timu kubwa kama Miami Heat.
Kutwa nzima ya siku ile alishinda akichekacheka mwenyewe, akawa anavuta picha kichwani mwake akiwa amevaa jezi za timu kubwa kabisa ya mpira wa kikapu nchini Marekani, Miami Heat iliyokuwa inatetea ubingwa wa Ligi ya NBA.
Mechi yao ya tatu walipangiwa kuchezea pale chuoni kwao dhidi ya timu ya Chuo Kikuu cha Duke. Baada ya kusikia habari juu ya kuwaniwa na timu ya Miami Heat, alipania kwa moyo wote kuonesha kuwa hawakuwa wamekosea kumchagua ajiunge na kikosi hicho.
Mazoezi makali aliyokuwa anayafanya yalisababisha awe na nguvu nyingi na pumzi za kutosha kama faru dume, mchezo ulipoanza tu, akaanza kucheza kwa kasi kubwa na nguvu. Kwa mara nyingine alifanikiwa kuonesha uwezo mkubwa kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mchezo huo, tena akiwa katika uwanja wao wa chuo.
Kwa muda wote wa mchezo, Harvey alikuwa akishangiliwa kwa nguvu huku baadhi ya wanachuo wakiwa wamebeba mabango makubwa yaliyokuwa na ujumbe wa kumhusu. Akazidisha juhudi na kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi mnono dhidi ya wapinzani wao wa Duke.
Baada ya mechi ile ambayo ilikuwa ya tatu kwa mzunguko, wanaume wawili waliokuwa wamevalia suti nadhifu, mikononi wakiwa na briefcase, walimfuata na kujitambulisha kuwa wao ni maafisa kutoka timu ya Miami Heat, wakamwambia wana mazungumzo naye hivyo watafute sehemu ya kukaa na kuzungumza kwa kina.
Michuano ya mpira wa kikapu kwa wanafunzi wa vyuo nchini Marekani, almaarufu NCAA yanayovikutanisha vyuo vingi vya elimu ya juu, ndiyo yaliyofanya uwezo na kipaji kikubwa alichokuwa nacho Harvey kijulikane. Mechi za awali alizoshiriki akikichezea chuo chake cha Miami Polytechinic and Engineering College, zinamtangaza vyema kutokana na jinsi alivyoonesha uwezo mkubwa kwenye mchezo huo.
Uwezo mkubwa anaouonesha unawavutia viongozi wa timu kubwa mbalimbali zilizokuwa zinashiriki ligi kuu ya mpira wa kikapu nchini Marekani, NBA ikiwemo Miami Heat. Timu hiyo kubwa iliyokuwa inatetea ubingwa wa ligi hiyo, inaanza kumuwania Harvey. Taarifa zinatumwa chuoni kwao na mipango ya kumsajili inaanza kufanywa mara moja.
Upande wa pili, tamaa ya mapenzi kwa Harvey inazidi kumuwakia Skyler lakini anashindwa kumwambia moja kwa moja kwani wanaishi kwenye familia moja kama kaka na dada. Mafanikio anayoyapata yanamfanya Skyler azidi kumpenda Harvey na anajiapiza kuwa lazima atakuja kuwa na uhusiano naye.
BILA shaka wewe ni Harvey? aliuliza mmoja kati ya wanaume wale ambao walijitambulisha kama maafisa kutoka timu ya mpira wa kikapu ya Miami Heat. Harvey aliwapa ushirikiano mzuri kwani tayari alishakuwa na taarifa za ujio wao, alizozipata kutoka kwa mlezi wa wanachuo (dean of students) pale chuoni kwao.
Waliingia katika chumba maalum kilichokuwa katika jengo la utawala, wakaenda kukaa kwenye meza ya duara iliyotengenezwa kwa vioo na wale wanaume wakaweka briefcase zao mezani na kutoa ujumbe waliotumwa na timu yao ya Miami Heat.
Vipi kuhusu masomo yangu ya chuo?
Utaruhusiwa kuendelea na masomo kama kawaida lakini pale tutakapokuwa tunakuhitaji hususani jioni baada ya muda wa masomo, utakuwa unakuja kuchukuliwa kisha kurejeshwa chuoni mapema, tutayapa kipaumbele masomo yako, alisema mmoja kati ya wale wanaume, mwenzake akawa anamuunga mkono kwa kutingisha kichwa.
Waliendelea kuzungumza mambo kadha wa kadha, wakamfafanulia kila kipengele kilichokuwa katika mkataba ambao Harvey alitakiwa asaini. Baada ya kusaini angepewa kiwango kikubwa cha fedha kama malipo ya usajili wake na mishahara yake ya miezi mitatu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nahitaji kwenda kujadili na familia yangu kwanza, wao ndiyo wenye mamlaka ya kusema cha kufanya, alijibu Harvey, wakakubaliana na wazo lake, wakaahidi kurejea tena siku inayofuata.
Walipoondoka tu, Harvey alienda kumpa taarifa mlezi wao (dean of students), akamweleza kila kitu walichozungumza na maafisa wale wa Miami Heat, akamuonesha na nakala ya mkataba waliokuwa wanataka ausaini na fedha ambazo angelipwa.
Dean akawa anaupitia juujuu, akakutana na kipengele kilichokuwa kinasomeka $45 million as per advance salary of three month. (Dola milioni 45 kwa ajili ya malipo ya awali ya mshahara wa miezi mitatu).
Duuh! Watakuwa wanakulipa dola milioni 15 kwa mwezi? Yaah wamemaanisha hivyo kwa sababu hapa wanasema watakupa kianzio cha mishahara ya miezi mitatu ambayo ni dola milioni 45... achilia mbali mamilioni ya kusaini mkataba mnono kama huu... ama kweli Mungu yu mwema, alisema Dean na kumshika mkono Harvey.
Bila shaka Dk Lewis atafurahi sana, inatakiwa uende nyumbani sasa hivi kumfikishia taarifa, alisema. Bila kupoteza muda, Harvey akaenda hostel kujiandaa haraka kisha akaianza safari ya kuelekea nyumbani kwao. Dakika 30 baadaye tayari alishawasili nje ya geti, akasalimiana na mlinzi na kuingia mpaka ndani.
Kwa kuwa muda ule ilikuwa bado ni mapema, Dk Lewis na mkewe walikuwa kazini huku Skyler akiwa shuleni. Nyumba ilikuwa imepoa kwa ukimya. Harvey akapata wazo kuwa ni bora amfuate Dk Lewis kazini na kumfikishia taarifa zile, wakubaliane nini cha kufanya mapema. Akiwa anajiandaa kutoka alisikia sauti ya mtu kama Skyler akizungumza na mlinzi getini.
Mh hapa leo kazi ipo, alijisemea Harvey huku akichungulia dirishani kuangalia upande wa mbele kwenye geti. Alitambua fika kuwa Skyler alikuwa na hisia za mapenzi lakini hakutaka kuruhusu hilo litokee.
Baada ya muda alimuona Skyler akiingia huku akiwa amebeba begi lake la shule mgongoni, akiwa amejishika mikono tumboni. Kwa jinsi alivyokuwa anaonesha, Skyler alikuwa akihisi maumivu makali ya tumbo. Harvey akatoka nje kumsaidia kuingia ndani.
Whaooo! Harvey kumbe umekuja? Kwa nini hujanitaarifu? Mbona mlinzi hajaniambia kama upo ndani... oooh come on! alisema Skyler na kuchangamka ghafla, akamkimbilia Harvey na kumkumbatia kwa nguvu.
Kwa nini umewahi kurudi shule?
Naumwa Harvey, tumbo linaniuma sana, alisema Skyler kwa kudeka, wakaingia ndani na kwenda kukaa sebuleni. Kwa jinsi Skyler alivyokuwa na bashasha baada ya kumuona Harvey, hata maradhi ya tumbo aliyokuwa nayo yaliisha ghafla.
Akawasha runinga na kuanza kumsimulia jinsi walivyomuona akicheza mpira wa kikapu usiku uliopita.
Nilirekodi kwenye VCD, nilifurahi sana, alisema Skyler na kuuchukua mkoba wake wa DVD, akaanza kuitafuta kwa lengo la kumuonesha Harvey. Muda mfupi baadaye, runinga kubwa ya kisasa iliyokuwa pale sebuleni ilikuwa ikionesha kipande cha mchezo kati ya chuo alichokuwa anasoma Harvey na timu nyingine.
Umeshakuwa superstar Harvey... im so proud of you (najivunia sana kuwa na wewe) alisema Skyler, akajilaza kwenye miguu ya Harvey aliyekuwa ametulia juu ya sofa, akiendelea kukodolea macho kwenye runinga. Kwake kila kitu kilikuwa kama miujiza, hakuwahi kudhani anaweza kupata umaarufu mkubwa kiasi kile.
Kaka Harvey naomba unikumbatie kifuani kwangu, alisema Skyler kwa sauti ya kudeka huku akimsogelea Harvey pale juu ya kochi.
No Skyler... tumeshakuwa wakubwa sasa, hatuwezi kukumbatiana mwilini kama zamani, lazima tutaingia kwenye vishawishi tu, alisema Harvey lakini Skyler hakutaka kumuelewa.
Harvey hakuwa na ujanja tena, akaamua kutulia na kufanya kile dada yake alikuwa anakitaka. Walikumbatiana kwa nguvu, kwa kuwa Harvey alikuwa akifanya mazoezi, hakupata shida, wakakaa pale juu ya sofa kwa dakika kadhaa.
Kaka Harvey mi nasikia usingizi, nataka unipeleke chumbani nikalale, alisema Skyler huku akimtazama Harvey kwa macho yaliyokuwa na ujumbe mzito.
Harvey aliamua kujikaza na kuonesha uvumilivu hadi hatua ya a. Akamuinua Skyler pale kwenye sofa na kumsindikiza mpaka chumbani kwake, akamlaza kitandani na kumfunika.
Utapona usijali umesikia Skyler!
Ahsante Harvey, naomba ukae hapa pembeni ya kitanda changu, alisema Skyler huku akiupitisha mkono wake mmoja na kumgusa Harvey kiunoni, akamganda kama ruba. Walikaa katika hali ile kwa muda mrefu, Skyler akaanza vituko vingine, akawa anamwambia Harvey kuwa anasikia joto kali.
Nikuwashie feni?
Hapana... nataka unisaidie kuvua nguo za shule, alisema Skyler na kujilegeza mwilini mwa Harvey. Hali ile ilimpa wakati mgumu sana Harvey lakini akaamua kujikaza kiume, akamvua shati na kumuacha akiwa amevaa blauzi nyepesi ndani, akamwambia hataweza kumvua sketi bali afanye vile mwenyewe na yeye atamsaidia kuzitundika ukutani.
Kwa makusudi Skyler alisimama na kuanza kutaka kuvua sketi mbele ya macho ya Harvey, hali iliyomfanya afungue mlango na kutoka nje. Akamuacha Skyler kule chumbani.
Hivi huyu Skyler kwa nini ananifanyia hivi? Si ameshakuwa kama dada yangu wa kuzaliwa tumbo moja huyu? Kwa nini anataka kuleta hisia za kimapenzi? alijiuliza Harvey bila kupata majibu, akaamua kutoka nje kabisa ili kuepusha kile kilichokuwa kinataka kutokea.
Kwa bahati nzuri, muda mfupi baadaye mama Skyker aliwasili nyumbani pale akitokea kazini. Harvey akampokea na kumweleza kwa kifupi kilichomfanya arudi nyumbani.
Skyler naye yupo chumbani kwake anasema tumbo linamuuma, alisema Harvey, mama yao akapitiliza moja kwa moja mpaka chumbani kwa mwanaye na kumuacha Harvey akiteremsha baadhi ya vitu kwenye gari.
Mum im sick, my stomach is aching,
(Mama naumwa) alisema Skyler huku akijigalagaza huku na kule. Baada ya kubaini kuwa ni tumbo ndiyo lilikuwa likimsumbua mwanaye, alienda chumbani kwake na kutoka na sanduku maalum la huduma ya kwanza. Akaanza kumtafutia dawa za kutuliza maumivu ya tumbo.
Baada ya kupewa dawa, Skyler alitulia, akalala na kuwaacha mamake na Harvey wakiendelea kuupitia ule mkataba. Waliendela kupitia kifungu kimoja baada ya kingine na kutafuta tafsiri ya kila kilichokuwa kimeandikwa. Baada ya saa kadhaa kupita, Dk Lewis alirejea nyumbani na kuwakuta wakiendelea na zoezi lile.
Akiwa na watu wengine wengi, wanatoroka nchini kwao kukimbia machafuko na kuelekea nchini Marekani. Wakiwa njiani, balaa jingine linatokea ambapo chombo walichokuwa wanasafiria baharini kinapinduka.
Harvey anakuja kurejewa na fahamu na kujikuta akiwa hospitali, jijini Miami nchini Marekani. Baada ya kueleza kilichomsibu, Dk Lewis anajitolea kumsaidia, anamchukua na kwenda kuishi naye nyumbani kwake.
Anayaanza maisha mapya nchini Marekani ambapo anapelekwa shule ya sekondari lakini anashindwa kufanya vizuri kutokana na msongo wa mawazo.
Dk Lewis na familia yake wanaamua kumtafutia chuo cha ufundi na hapo ndipo nyota yake ya mafanikio inapoanza kung'ara kupitia uwezo mkubwa wa kucheza mpira wa kikapu aliokuwa nao.
Ligi ya mpira wa kikapu kwa wanafunzi wa vyuo nchini humo maarufu kama NCAA inamfanya apate fursa ya kuonesha kipaji chake na sasa anageuka gumzo nchi nzima huku timu kubwa ya Miami Heat ikiwania kumsajili.
Viongozi wa timu hiyo maarufu wanaenda kuonana na Harvey chuoni pale na kumpa mkataba ambao wanamwambia aupitie kwa makini na akiridhika asaini. Harvey anaamua kurejea nyumbani kwenda kuomba ushauri kwa walezi wake, Dk Lewis na mkewe.
BAADA ya Dk Lewis kuwasili, ilibidi Harvey aanze kuelezea kila kitu kilivyokuwa, kuanzia jinsi alivyopewa taarifa na mlezi wao pale chuoni, jinsi alivyokutana na maafisa wa ngazi za juu wa timu ya mpira wa kikapu ya Miami Heat na mazungumzo yote waliyoyafanya pamoja.
Kwa Dk Lewis, ile ilikuwa ni zaidi ya habari njema. Japokuwa alitoka kazini akiwa na uchovu sana, aliposikia habari ile, moyo wake ulifurahi kupita kawaida. Mkewe hakuwa na tofauti naye. Mara kwa mara walikumbatiana kwa furaha, wakawa wanamshukuru Mungu wao kwa kumfungulia Harvey njia ya mafanikio.
Waliendelea kuupitia mkataba ule kifungu kimoja baada ya kingine na walipojiridhisha kuwa kila kilichokuwa kimeandikwa kina manufaa kwa Harvey, walimsaidia kuujaza. Dk Lewis akaweka sahihi sehemu ya mzazi au mlezi pamoja na anuani yake ya makazi.
Baada ya kumaliza kazi ile, waliagana na kutakiana usiku mwema, Dk Lewis akatoka na mkewe hadi chumbani kwa mtoto wao, Skyler kumjulia hali kwani alikuwa akilalamikia maumivu ya tumbo. Harvey alienda chumbani kwake huku akiwa na furaha ya ajabu moyoni mwake.
Kilichomfurahisha zaidi ni kwamba Dk Lewis na mkewe waliyafurahia sana mafanikio yake na kuahidi kuwa naye bega kwa bega. Wakamfanya asione pengo la wazazi wake kwa muda ule. Kwa furaha aliyokuwa nayo, alipoingia chumbani kwake hakukumbuka hata kufunga mlango, akaenda kufungulia muziki na kujitupa kitandani, hisia za furaha zikawa zinapita ndani ya kichwa chake, hali iliyomfanya muda wote uso wake ujawe na tabasamu pana.
Hakuelewa usingizi ulimpitia saa ngapi lakini alikuja kushtuka baadaye baada ya kusikia kitu kikimpapasa mwilini. Alifumbua macho na kutulia, akawa anataka kujua ni kitu gani. Kilichomshtua, wakati anapitiwa na usingizi hakuwa amezima taa, kufunga mlango wala kujifunika lakini aliposhtuka kutoka usingizini, alijikuta akiwa amefunikwa na shuka huku taa ikiwa imezimwa na mlango kufungwa.
"Harvey!" alisikia sauti ya mtu akinong'ona jirani kabisa na sikio lake la upande wa kushoto. Mshtuko alioupata ulimfanya akurupuke pale kitandani na kukimbilia kwenye swichi, akawasha taa na kukodolea macho pale kitandani. Alipatwa na mshangao mkubwa kumuona Skyler akiwa pale juu ya kitanda chake, tena akiwa amevaa ‘night dress' pekee.
Mapigo ya moyo yalianza kumwenda mbio kuliko kawaida kwani alijua endapo wazazi wake wangeamka ghafla na kuwakuta wakiwa katika hali ile, wangehisi tayari wameanza kushiriki mchezo haramu.
"Kumetokea nini Skyler… kwa nini upo hapa muda huu," aliuliza Harvey kwa sauti ya chini akiogopa asije kusababisha kelele ambazo zitawaamsha Dk Lewis na mkewe. Skyler hakujibu kitu zaidi ya kumuoneshea ishara kuwa asipige kelele, akainuka kutoka pale kitandani alipokuwa amelala na kumsogelea Harvey mwilini.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akiwa bado haelewi cha kufanya, Harvey alishtukia Skyler amemkumbatia kwa nguvu na kumganda kama ruba, akawa analalamika kuwa ameshindwa kulala chumbani kwake kutokana na baridi aliyokuwa anaisikia, hasa ukizingatia kuwa bado tumbo lilikuwa linamuuma.
"Huoni kama utanisababishia matatizo makubwa? Hivi ikitokea baba na mama wametukuta huku chumbani tukiwa katika hali kama hii unafikiri watatuelewaje?" aliuliza Harvey kwa sauti ya chini huku akijaribu kujinasua kutoka mwilini mwa Skyler bila mafanikio.
"Harvey please… nasikia baridi sana nahitaji unikumbatie," alisema Skyler huku akizidi kumganda. Alijaribu kutumia ujanja wake wote kumuweka sawa ili amuachie lakini haikuwezekana.
"Hata baba na mama wakitukuta mi nitawaambia nakupenda na nataka unioe."
"Skyler… hujui tunaishi kama kaka na dada, unafikiri nani atatuelewa? Utanisababishia matatizo makubwa, tafadhali nakuomba rudi chumbani kwako ukalale."
"Sirudi… nimeshakwambia nasikia baridi, hunionei huruma wakati mwenzio naumwa?" alilalama Skyler huku akijikamua ili machozi yamtoke. Alipoona Harvey hataki kumuelewa, ikabidi amtolee vitisho:
"Ukikataa kufanya ninavyotaka nitapiga kelele niseme ulikuwa unataka kunibaka," alisema Skyler na kubenua midomo yake mizuri kwa jeuri. Harvey alimsihi sana asifanye vile, akamwambia kuwa yupo tayari kufanya kila alichokuwa anakitaka lakini asifanye kile alichokusudia.
"Basi nakukumbatia kidogo, ukiacha kusikia baridi utarudi chumbani kwako," alisema Harvey huku akivua shati lake na kumsogeza Skyler kifuani kwake. Wakakumbatiana kwa dakika kadhaa wakiwa wamesimama wima katikati ya chumba cha Harvey.
"Kwa nini tusisogee kitandani? Nimechoka kusimama," alisema Skyler huku akimsukumia Harvey kitandani. Harvey akaona atakuwa amevuka mipaka ya maadili, akamkatalia kufanya vile alivyotaka. Wakiwa bado wanavutana, walisikia mlango wa chumba cha baba na mama yao ukifunguliwa, Skyler akamuachia Harvey haraka na kukimbia kwa kunyata kuelekea chumbani kwake.
Harvey alishindwa kuificha hofu iliyokuwa ndani ya moyo wake, moyo ukawa unadunda kwa nguvu. Aliyajua madhara ambayo angeyapata endapo baba au mama yake wangegundua kuwa alikuwa na Skyler chumbani kwake usiku ule.
"Eeeh Mungu nisaidie," alisema Harvey huku akiurudishia mlango wake taratibu, akazima taa na kurudi kitandani kimyakimya huku masikio yake yakiwa makini kusikiliza kilichokuwa kinaendelea.
Alisikia mlango wa maliwatoni ukifunguliwa, akashusha pumzi ndefu na kutulia, angalau akawa na imani kuwa hakuna anayeweza kugundua kilichotokea muda ule. Baada ya muda, alisikia mlango ukifunguliwa tena, akasikia hatua za mtu akitembea kuelekea chumbani kwa Skyler.
"Mbona unatetemeka sana mwanangu halafu jasho linakutoka," alisema mama Skyler baada ya kumkuta mwanaye katika hali ile. Skyler alijibu
kwa sauti ya kuigiza kuwa alikuwa anahisi baridi kali na ndiyo iliyomfanya awe katika hali ile. Harvey alikuwa akisikiliza kwa makini kila kilichokuwa kinaendelea.
"Basi ngoja nikamuage baba yake nije tulale wote," alisema mama Skyler huku akitoka. Muda mfupi baadaye alirejea na kulala na mwanaye, hiyo ndiyo ikawa ahueni kwa Harvey. Akaenda kuufunga mlango wake kwa ndani na kujilaza taratibu kitandani. Hata ile furaha aliyokuwa nayo kwa mafanikio aliyoyapata, ilitoweka na sasa akawa analifikiria tukio lile.
Baada ya muda akapitiwa na usingizi. Kulipopambazuka, Harvey ndiyo alikuwa wa kwanza kuamka, akajiandaa tayari kwa kuondoka.
"Mbona umewahi sana kuamka?" aliuliza Dk Lewis baada ya kumkuta Harvey sebuleni akiwa ameshajiandaa.
"Leo tuna kipindi cha asubuhi, inabidi niwahi sana," alisema Harvey, Dk Lewis akamuunga mkono. Wakakubaliana kuwa ampeleke kwa kutumia
gari lao la familia mpaka chuoni kisha ndiyo arudi kwa ajili ya ratiba nyingine. Harvey akaondoka kabla Skyler hajaamka. Wakiwa njiani, akawa anaendelea kufikiria kwa kina juu ya kile kilichotokea usiku uliopita.
Kipaji kikubwa cha kucheza mpira wa kikapu alichojaaliwa na Mungu wake, kinamfanya awe maarufu ndani ya muda mfupi, akiwa ni mwanafunzi katika Chuo cha Miami Polytechnic and Engineering College. Dk Lewis na familia yake ndiyo waliompeleka kwenye chuo hicho, baada ya kushindwa kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha nne aliofanya.
Mafanikio yake yanamfanya angalau aanze kusahau machungu aliyopitia maishani mwake. Ule msongo wa mawazo uliomtesa kwa kipindi kirefu, sasa umekwisha na kipaji chake cha kucheza mpira wa kikapu kinazidi kujidhihirisha kwenye michuano ya NCAA, iliyokuwa inawahusisha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali nchini Marekani.
Kutokana na kipaji kikubwa alichokionesha kwenye michuano ya NCAA, timu kubwa ya mpira wa kikapu ya Miami Heat inavutiwa naye na sasa viongozi wake wanafanya mipango ya kumsajili. Upande wa pili, Skyler anachanganywa na hisia kali za mapenzi alizokuwa nazo kwa Harvey. Anaanza kumtega akitaka awe mpenzi wake bila kujali kuwa wanaishi kama kaka na dada.
BAADA ya kuona mbinu yake ya kumnasa Harvey imeshindikana kwa usiku ule, Skyler alianza kuandaa mtego mwingine. Kwa hatua aliyokuwa amefikia, alikuwa tayari kufanya jambo lolote kuhakikisha anamnasa Harvey kimapenzi. Ile heshima aliyokuwa anampa kama kaka yake tangu wakiwa wadogo, sasa iliisha na jambo pekee lililokuwa ndani ya kichwa chake, lilikuwa ni mapenzi.
Cheki alivyo na kifua kizuri cha mazoezi, itazame mikono yake ilivyojazia vizuri, sura yake ya kitanashati, urefu wake oooh! Lazima awe mpenzi wangu, Skyer alikuwa akijisemesha mwenyewe wakati akiitazama picha ya Harvey chumbani kwake.
Wakati akiendelea kuitazama ile picha, alisikia mlango wa chumba chake ukigongwa, akaificha ile picha haraka chini ya mto na kwenda kufungua mlango. Alikuwa ni mama yake, Suzan.
Unaendeleaje mwanangu, alisema Suzan huku akimbusu Skyler kwenye paji la uso.
Bado tumbo linaniuma sana mama, naona zile dawa za jana hazijanisaidia.
Utaweza kwenda shule kweli?
Hapana, nataka nipumzike tu nyumbani, nikizidiwa kaka Harvey atanipeleka hospitali.
Mwenzio ameshaondoka kurejea chuoni, kwani hakukuaga? Labda aliogopa kukusumbua mgonjwa, ameondoka alfajiri na mapema, alisema Suzan, kauli ambayo ilipenya kwenye mtima wa Skyler na kumfanya aduwae kwa muda.
Basi pumzika mwanangu, sisi tunaenda kazini, ukiona hali inazidi kuwa mbaya utanipigia simu kunitaarifu, alisema mama Skyler huku akitoka na kuufunga mlango wa chumba cha Skyler. Kauli ya mama yake kuwa Harvey tayari alishaondoka, ilimmaliza kabisa nguvu Skyler.
Mpango kabambe aliokuwa ameupanga ndani ya kichwa chake, ambao alitaka kuutumia kwa Harvey muda mfupi baada ya wazazi wao kuondoka kwenda kazini, ulivurugika akawa anajilaumu kwa kushindwa kuitumia vizuri nafasi aliyoipata usiku uliopita.
Alipohakikisha wazazi wake wameshaondoka kwenda kazini, harakaharaka aliinuka pale kitandani, akaenda kujimwagia maji
bafuni na kuanza kujiandaa kutoka. Alipanga kwenda kumfanyia Harvey shopping ya vitu vidogovidogo ambavyo angevitumia kuwasilisha ujumbe wake wa mapenzi kwa Harvey. Alipokuwa tayari, alitoka na kuingia mtaani.
Aliongoza moja kwa moja mpaka kwenye supermarket kubwa ya Miami Mall iliyokuwa mtaa wa tatu kutoka pale nyumbani
kwao. Akanunua kadi nzuri iliyokuwa na ujumbe mzito wa kimahaba, chokleti, vanilla, nguo za ndani za kiume, pafyumu nzuri na maua mazuri, akaomba kufungiwa vitu vyote katika boksi la zawadi. Wahudumu wa ile supermarket wakafanya kama alivyotaka.
Alipohakikisha kila kitu kipo safi, alilipa fedha na kutoka kurejea nyumbani kwao. Alipofika alipitiliza mpaka chumbani kwake,
akaingia tena bafuni kwa mara ya pili na kuoga. Alipomaliza, akaanza kujipamba na kujipodoa mwili mzima. Alitumia zaidi ya nusu saa akiwa kwenye dressing table yake.
Aliporidhishwa na namna alivyopendeza, alisimama na kuelekea kwenye kabati la nguo. Akawa anachagua nguo nzuri ambazo aliamini zitamvutia Harvey. Baada ya kuchagua nguo karibu kabati zima, hatimaye aliipata iliyompendeza zaidi.
Alichagua gauni la kisasa la rangi ya pinki alilonunuliwa na mama yake kwenye siku yake ya kuzaliwa, wakati akitimiza miaka 19. Alipolivaa alijipitisha mara kadhaa mbele ya kioo, akawa anageuka huku na kule kama wafanyavyo mamisi, alipohakikisha amependeza vya kutosha, alichukua boksi lake la zawadi na safari ya kuelekea chuoni kwa akina Harvey ikaanza.
***
Baada ya kufikishwa chuoni na Dk Lewis, Harvey alipitiliza moja kwa moja mpaka bwenini kwao. Kwa kuwa ilikuwa bado ni asubuhi sana, aliungana na wanachuo wenzake waliokuwa wanajiandaa kwa ajili ya kuhudhuria kipindi cha asubuhi ile.
Ulilala wapi Harvey? Usiku tulikuwa na wasiwasi kweli baada ya kuona hutokei, tukahisi labda umepatwa na tatizo.
Dah! Mtanisamehe kwa sababu niliondoka bila kuwaaga, nilikuwa nimeenda nyumbani kujadiliana na familia yangu kuhusu mkataba wa kuichezea Miami Heat.
Mkataba wa kuichezea Miami Heat? Kwani wanataka kukusajili?
Ndiyo, na tayari wameshanipa mkataba wao, nilienda nyumbani kuwaonesha ili wanisaidie kuujaza. Leo wakija tena nitawapa halafu nitasubiri kuona hatua inayofuata.
Daaah! Hongera sana mtu wangu, watu wengine mna bahati zenu bwana! Umepata dili la kucheza kikapu kwenye Timu ya Miami Heat? Basi siku chache zijazo utakuwa bonge la milionea, kumzidi hata Lebron James.
Kweli kaka, lakini nahitaji dua zenu zaidi, si unajua wewe ndiyo umekuwa mshauri wangu mkubwa kwenye haya mambo, Harvey alikuwa akizungumza na mwanachuo mwenzake, Cazzard huku wakiendelea kujiandaa kwa ajili ya masomo.
Muda wa masomo ulipowadia, Harvey na wanachuo wenzake waliingia katika ukumbi maalum wa kufundishia wanachuo (Lecture Hall). Kipindi kikaanza kama kawaida. Wakati mhadhiri akiendelea kufundisha, kila mtu akiwa kimya kumsikiliza, Harvey aliona kitu kilichomshtua.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa kupitia madirisha ya vioo ya ukumbi ule, alimuona Skyler akija huku mkononi akiwa amebeba boksi lililoonekana kuwa na mzigo ndani yake.
Huyu Skyler si alisema anaumwa tumbo jamani halafu mbona leo amenifuata asubuhi namna hii? Nisipokuwa makini shetani atanizidi nguvu kwani simuelewi kabisa anachotaka kutoka kwangu, alijisema Harvey huku akili zake zikiwa zimeshahama darasani. Akawa anawaza atakavyokabiliana naye bila kumuudhi, huku kumbukumbu za tukio lililotokea usiku uliopita zikipita kwa kasi akilini mwake.
Aliendelea kumtazama Skyler kwa mbali mpaka alipopotelea kwenye majengo mengine ya chuo kile. Bila kusubiri kuja kutafutwa, aliinuka mwenyewe na kukusanya kila kilichokuwa chake, akatoka kwa kupitia mlango wa nyuma bila mtu yeyote kugundua.
Aliongoza moja kwa moja mpaka kwenye jengo la utawala, akamkuta Skyler akiwa amekaa kwenye sehemu ya wageni, huku usoni akiwa amejawa na tabasamu pana. Alipomuona Harvey tu, aliinuka haraka na kumkimbilia, akamkumbatia kwa nguvu huku akimmwagia mvua ya mabusu usoni.
Nimependeza eti eeeh! Mbona hunisifii? alisema Skyler huku akizidi kumkumbatia Harvey kwa nguvu.
Umependeza sana dadaangu, nimekuona tangu nikiwa darasani, alisema Harvey huku akijilazimisha kuchangamka.
Sitaki unite dada Harvey, niite jina zuri kama darling, honey, sweet, dear au lolote zuri utakalolipenda, alisema Skyler huku akizidi
kumkumbatia Harvey kifuani. Baada ya Skyler kumkumbatia Harvey kwa dakika kadhaa, aliporidhika alimuachia na kumshika mkono, akamwambia kuwa amemletea zawadi nzuri ambazo anataka akazifungue chumbani kwake na yeye akiwepo.
Twende ukafungulie kwenye chumba unacholala, wenzako si wapo madarasani muda huu, alisema Skyler na kumkabidhi Harvey lile boksi la zawadi. Wakawa wanatembea taratibu kuelekea kwenye chumba alichokuwa analala Harvey.
Walipofika na kuingia ndani, Skyler aliufunga mlango kwa ndani, akaenda kujitupa kitandani huku akiuficha uso wake kwa aibu za kikekike. Harvey akaanza kulifungua boksi la zawadi.
Mtoto wa Dk Lewis, mwanaume wa makamo aliyempokea Harvey na kujitolea kuyabadilisha maisha yake aitwaye Skyler, anaanza kuonesha hisia za mapenzi kwa kaka yake huyo wa hiyari. Anatumia mbinu mbalimbali kuwasilisha
ujumbe wake wa kimapenzi kwa Harvey lakini anakuwa mjanja na kujitahidi kuvishinda vishawishi.
Bado Skyler hakati tamaa na anajiapiza kuwa atafanya kila linalowezekana kuhakikisha analipata penzi la Harvey, ambaye sasa umaarufu wake ulikuwa ukizidi kuongezeka siku baada ya siku, kutokana na kiwango kikubwa cha
kucheza mpira wa kikapu alichokionesha kwenye mashindano ya NCAA, yaliyokuwa yanawahusisha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali nchini Marekani.
HARVEY alifungua boksi la zawadi, akakutana na harufu nzuri ya manukato yaliyokuwa yamepuliziwa vizuri. Akaanza kutoa zawadi moja baada ya nyingine. Kwa kiasi fulani alifurahishwa na zawadi zile, akajilazimisha kuamini kuwa kwa sababu zimetoka kwa dada yake, hakutakuwa na tatizo lolote.
"Umezipenda?"
"Nimezipenda sana Skyler, nashukuru kwa kunijali."
"Hizo zinakutosha? Hebu ijaribu hata moja nione inavyokupendeza," alisema Skyler huku akinyoosha kidole kwenye nguo za ndani alizokuwa amemletea Harvey kama zawadi.
"Nitazijaribu nikiwa peke yangu… naamini zitanipendeza sana," alisema Harvey akiwa tayari ameshaugundua mtego wa Skyler.
"Hapana bwana, mi' nataka uzijaribu sasa hivi ili nione kama nimechagua nzuri," alisema Skyler na kusimama, akamsogelea Harvey na kuushika mkanda wa suruali yake, akawa anajaribu kuufungua lakini Harvey akatumia ujanja wa hali ya juu.
"Subiri kwanza nikazibadilishie bafuni halafu nitakuita uje unione nilivyopendeza," alisema Harvey na kuzichukua, akaelekea kwenye bafu lililokuwa ndani. Alipofika aliingia na kujifungia mlango kwa ndani, akawa anahema juujuu huku akifikiria namna ya kumkwepa Skyler.
"Kwani akiniona nitapungua nini, potelea mbali, liwalo na liwe," alisema Harvey huku akianza kuivua suruali yake na kuzijaribu zile nguo za ndani alizoletewa na Skyler. Wakati akiendelea kubadilisha, alisikia sauti ya mwanachuo mwenzake, Cazzard akimuita na kugonga mlango.
"Nipo huku bafuni, nakuja," alisema Harvey huku moyoni akishukuru kwa kitendo cha rafiki yake huyo kumfuata. Harakaharaka alivaa suruali yake na kutoka, akamfungulia mlango. Alipomtazama Skyler, alimuona akikunja sura kuashiria kuwa hakufurahishwa na ujio wa Cazzard.
"Nimetumwa kuja kukuita, kuna wageni wako pale utawala," alisema Cazzard, Harvey akaweka vitu vyake vizuri na kuzifungia zile zawadi zake kwenye kabati.
"Twende mara moja halafu tutarudi kuja kuendelea," alisema Harvey huku akimshika mkono Skyler na kumuinua, kwa shingo upande akakubali kuongozana naye. Walikwenda mpaka kwenye ofisi za utawala wa chuo kile ambapo Harvey aliwaona wanaume wawili waliokuwa wamevalia suti nadhifu na kubeba ‘briefcase' mikononi mwao. Aliwakumbuka vizuri kuwa ni wale maofisa wa timu ya Miami Heat, akatabasamu.
Aliwasalimu kwa heshima, wakaenda kukaa kwenye chumba cha mazungumzo ambapo walianza kumuuliza juu ya hatua aliyofikia kuhusu mkataba waliomuachia siku iliyopita. Aliwajibu kuwa kila kitu kilienda vizuri, akawaomba wamsubiri kidogo akaulete ukiwa tayari umeshajazwa. Skyler naye alisimama, wakaongozana hadi kwenye hosteli ya akina Harvey.
"Nina furaha sana Skyler, wale ndiyo mameneja wa Miami Heat walioleta ule mkataba niliokuja nao jana nyumbani, naamini siku chache zijazo na mimi nitakuwa mchezaji maarufu sana duniani," alisema Harvey kwa furaha akitegemea Skyler atamuunga mkono lakini haikuwa vile.
"Wee ukishakuwa maarufu si utatafuta wanawake wengine maarufu kama wewe? Mi' sitaki uwe maarufu," alisema Skyler huku akijikamua machozi, Harvey akamsogelea na kuanza kumbembeleza. Skyler aliitumia vyema nafasi ile kwani alijilaza kwenye kifua cha Harvey kwa kudeka, mikono yake akaipitisha kijanja na kuanza kumpapasa mgongoni.
"Harvey… nifanye nini ili uelewe hisia za moyo wangu? Nakupenda sana na nakuhitaji uwe wangu wa maisha," alisema Skyler huku akizidi kumpapasa Harvey mgongoni.
"Nakupenda pia Skyler lakini hatuwezi kuwa wapenzi, sisi ni ndugu… tafadhali naomba unielewe dada'angu."
"Ndugu? Kwani mimi na wewe tumezaliwa tumbo moja? Halafu si nilishakukataza kuniita dada? Harvey nakuomba utibu maradhi ya moyo wangu, naomba unielewe… Nakupenda sana," alisema Skyler kwa sauti iliyojaa huba, akamsogezea mdomo wake na kutaka kumbusu lakini Harvey akamkwepa na kumwambia kuwa wafanye haraka kwa sababu wanasubiriwa na watu muhimu kule nje.
"Kwa hiyo hao mameneja wa Miami Heat ni muhimu kuliko mimi? Kwa nini hutaki kunielewa Harvey? Nifanye na mimi nijione ni mwanamke niliyekamilika, naomba niwe mpenzi wako," alilalama Skyler huku akizidi kumkumbatia Harvey kwa nguvu.
Harvey aliamua kutumia nguvu kumtoa Skyler mwilini mwake. Akaenda kwenye kabati lake la kuhifadhia vitu na kuutoa ule mkataba ambao tayari ulishajazwa. Akamuinua Skyler ambaye alikuwa amejiinamia huku akilia, akampa moyo kuwa suala lile watalijadili kwa kina baada ya kumaliza taratibu za kukabidhiana ule mkataba na maafisa wa Miami Heat.
Skyler alikubali kwa shingo upande, wakatoka na kurudi kule utawala ambapo waliwakuta wale maafisa wa Miami Heat wakiwasubiri. Alipowapa mkataba uliojazwa, walimpa kitabu maalum cha kusaini kisha mmoja akafungua briefcase yake na kutoa hundi.
"This cheque worth ten thousand dollar for you! Registration allowance,"
(Hundi hii ina thamani ya dola elfu kumi kwa ajili yako! Posho ya usajili)
alisema afisa mmoja huku akiigeuza na kuisaini upande wa nyuma. Kwa Harvey, ule ulikuwa kama muujiza. Dola elfu kumi kama posho, nje ya malipo ya mkataba na mshahara wake, hakutaka kuamini haraka. Baada ya makabidhiano yale, wale maafisa waliaga na kuondoka, wakamuahidi kuwa watawasiliana naye na kumpa maelekezo ya nini cha kufanya baada ya kusaini mkataba.
Kwa furaha aliyokuwa nayo Harvey, alijikuta akimkumbatia Skyler kwa nguvu, akambusu kwenye paji la uso wake na kumnyanyua juujuu. Kitendo kile angalau kilirejesha furaha kwenye mtima wa Skyler. Wakakubaliana kuwa waondoke asubuhi ileile mpaka benki kwa ajili ya kwenda kuzitoa fedha zile.
"Nisubiri hapahapa nikajiandae, nakuja muda si mrefu," alisema Harvey, akaondoka mbiombio hadi chumbani kwake ambapo alibadilisha nguo tayari kwa kutoka kwenda kuchukua fedha zake benki. Muda mfupi baadaye, tayari alishakuwa amejiandaa.
Wakaondoka na Skyler mpaka kwenye benki kubwa ya Miami Corporate, Harvey akatoa ile hundi na taratibu za kibenki zikaendelea. Baada ya muda mfupi, noti mpya za dola miamia zilipangwa mbele ya Harvey, akazichukua na kuzihakiki kisha wakaondoka na Skyler mpaka nyumbani kwao.
"Si umefurahi sana Harvey."
"Nimefurahi mno Skyler, yaani hata sijui niseme nini," alijibu Harvey bila kuelewa sababu za Skyler kumuuliza vile, akamshika mkono na kumwambia amfuate.
"Unataka kunipeleka wapi?"
"Wee nifuate bwana, unaogopa nini," alisema Skyler huku akizidi kumvuta Harvey mkono, akampeleka mpaka chumbani kwake na kumsukumia kitandani, akafunga mlango kwa funguo kisha akazitupia chini ya kitanda.
"Kwa kuwa leo umefurahi nataka na mimi unifurahishe, nimechoka kuteseka kwa ajili yako," alisema Skyler huku akianza kutupa nguo mojamoja mwilini mwake. Akavua gauni lake zuri alilokuwa amelivaa na kubakia na nguo za ndani. Umbo lake changa likajionesha vizuri mbele ya Harvey.
"Sijawahi kumruhusu mwanaume yeyote kuujua mwili wangu, nilikutunzia wewe hii zawadi, naomba uitumie na mimi nijione ni mwanamke niliyekamilika," alisema Skyler huku akijinyonganyonga kiuno chake kama dondora na kurembua macho yake kimahaba. Harvey alikuwa ameduwaa pale kitandani akiwa ni kama hayaamini macho yake. Taratibu uzalendo ukaanza kumshinda, hisia za mapenzi zikaanza kumpanda.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
LAKINI Dk Lewis akigundua kuwa natembea na mwanaye wa kipekee si nitakuwa matatizoni sana? Mama Skyler naye... aliwaza Harvey ndani ya kichwa chake, mawazo yale yakamfanya hisia za kimahaba ambazo sasa zilikuwa zimeshapanda, zikatike ghafla. Akaamka na kwenda kujaribu kuufungua mlango lakini hakuweza kwani Skyler aliufunga kwa funguo walipoingia.
Niache niende Skyler, leo sijisikii vizuri, nitakutafuta mwenyewe siku nyingine na kukupa hicho unachokitaka mpaka utosheke.
No Harvey, huwezi kuondoka humu ndani bila kunitimizia haja zangu.
Please Skyler, nimekwambia sijisikii vizuri leo, tumbo limejaa gesi na linauma sana, naomba nielewe tafadhali, haraka za nini?
Nimeshasema, kama hutaki tutakaa humuhumu chumbani kwangu mpaka mama arudi, na akiuliza nitasema unataka kunibaka.
Mungu wangu! Skyler kwa nini unataka kuniharibia maisha kiasi hicho? Nimekukosea nini? Hupendi kuniona nikiwa na furaha, alisema Harvey huku machozi yakianza kumlengalenga lakini Skyler hakuelewa kitu.
Sasa sikiliza, kama unanilazimisha hatuwezi kufaidi raha ya mapenzi, kwa leo niache lakini nakuahidi siku nyingine yoyote tutakayokutana, nitatii kila utakachoniambia? Kwa nini hutaki kunielewa Skyler? alilalama Harvey, safari hii michirizi ya machozi ikianza kuulowanisha uso wake.
Skyler, baada ya kumuona Harvey anatokwa na machozi, alienda kumkumbatia kwa nguvu, akamwambia kwa sauti ya kunongona kuwa amemuelewa alichokisema lakini akamuomba siku nyingine wakikutana asikatae tena kama siku ile.
Harvey alishukuru Mungu kuona Skyler amemuelewa, naye akamkumbatia huku akijifuta machozi, akavaa vizuri nguo zake na kumuomba Skyler afungue mlango. Alipofanya hivyo, alitoka harakaharaka huku akimuahidi kuwa atarudi siku nyingine. Bila hata kugeuka nyuma, Harvey aliondoka kasi hadi nje, akapanda basi hadi chuoni kwao huku mawazo tele yakiendelea kukisumbua kichwa chake.
Alimuona Skyler kama kikwazo kingine maishani mwake, akajiapiza kuwa atafanya kila awezalo kumkwepa binti yule kwani kiukweli hata yeye alishaanza kuingia kwenye mtego wa kutaka kuvunja naye amri ya sita, jambo ambalo hakutaka kabisa litokee.
Baada ya muda, aliwasili chuoni kwao huku akiwa na kiwango kikubwa cha fedha kwenye begi lake. Akapitiliza moja kwa moja mpaka hostel ambapo alienda kuzihifadhi zile fedha kwenye kabati lake. Kwa jinsi kichwa chake kilivyokuwa kimezongwa na mawazo, alijitupa kitandani na muda mfupi baadaye, usingizi mzito ukampitia.
***
Oyaaa amka twende mazoezini, si unajua kesho tuna mechi ngumu dhidi ya wanafunzi wa chuo cha New Hampshire, Cazzard alimuamsha Harvey aliyekuwa amezama kwenye dimbwi la usingizi wa pono. Harvey alishtuka kutoka usingizini, harakaharaka akaamka na kuanza kutafuta nguo zake za mazoezi. Muda mfupi baadaye akajumuika na wanafunzi wenzake kwenye mazoezi ya mpira wa kikapu.
Leo unaonekana kuwa na mawazo sana, kuna tatizo nyumbani ulikoenda?
Hapana Cazzard, nipo sawa lakini si unajua nimetoka kulala. Uchovu wa usingizi ndiyo umenifanya niwe hivi, Harvey alijaribu kudanganya baada ya mwanachuo mwenzake kumuuliza swali lile. Ukweli ni kwamba kichwa chake kilikuwa kimezongwa na
mawazo kutokana na tukio lililotokea nyumbani kwao ambapo Skyler alikuwa akimlazimisha kufanya jambo ambalo hakutaka kabisa litokee.
Baada ya muda wa mazoezi kuisha, Harvey alirejea hostel na baada ya kuoga, hakutaka hata kula chakula cha jioni wala kwenda kujisomea, akapitiliza kulala. Muda uliyoyoma hatimaye siku ya pili ikawadia. Kwa kuwa siku hiyo chuo chao kilikuwa kikishiriki kwenye mzunguko wa pili wa ligi ya NCAA, pilikapilika zilianza tangu asubuhi, hali iliyomfanya Harvey angalau asahau matatizo ya Skyler.
Wanachuo wengi walikuwa wakimpa moyo Harvey kuwa wanamtegemea sana siku hiyo kwani bila yeye, wasingeingia kwenye mzunguko wa pili wa ligi hiyo. Muda ulipowadia, wanachuo wengi akiwemo Harvey, walisafiri kwa basi la shule hadi katika Mji wa Hampshire, wakanyoosha moja kwa moja mpaka kwenye chuo kikuu cha mji huo, mahali ambapo pambano la mpira wa kikapu lingefanyika.
Kama kawaida yake, Harvey alijiandaa vya kutosha na muda wa mechi kuanza ulipowadia, aliwapanga wachezaji wenzake vizuri, kazi ikaanza. Ndani ya dakika chache za mwanzo, Harvey alifanikiwa kufunga pointi nyingi mfululizo, wanachuo wenzake wakawa wanamshangilia kwa nguvu huku waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nao wakimzungumzia kama mchezaji nyota aliyengara siku ile.
Mpaka mchezo unafikia mwisho, timu ya chuo chao ilikuwa inaongoza kwa pointi nyingi, shangwe zikaendelea ambapo wanachuo wenzake walimbeba Harvey juujuu kama shujaa wao. Waandishi wa habari nao wakawa na kiu ya kumfanyia mahojiano lakini walishindwa kutokana na wanachuo wenzake kumshangilia kwa nguvu na kumbeba hadi kwenye basi walilokuja nalo. Muda mfupi baadaye wakaondoka na kurejea chuoni kwao.
Timu yao ikawa imefuzu kuingia hatua ya robo fainali kwa juhudi kubwa za Harvey. Kila mmoja alimuona kama shujaa anayestahili kushangiliwa, wanachuo wenzake wakambatiza jina la Lebron, mchezaji nyota aliyekuwa anaichezea timu kubwa ya Miami Heat.
Siku mbili baadaye, timu yao ilijitupa tena uwanjani kupambana na chuo cha Illinois kilichokuwa na historia ya kuchukua ubingwa wa ligi hiyo mara kadhaa. Pambano lilikuwa la kukata na shoka kwani chuo hicho nacho kilikuwa na wachezaji nyota ambao walimsumbua sana Harvey, wakawa wanamkaba watatuwatatu ili asipate nafasi ya kufunga magoli.
Kwa kiasi fulani, walifanikiwa kumpunguza kasi lakini mpaka mwisho wa mchezo, timu yao ilikuwa imewazidi wapinzani wao kwa pointi chache. Wakaibuka washindi ingawa Harvey alipata majeraha kadhaa kutokana na kubanwa sana na wachezaji wa timu pinzani.
Leo walikukamia sana, si unaona walikuwa wanakukaba watatu watatu, lakini bado wameshindwa kukuzuia, we jamaa ni hatari sana, yaani chuo chetu hakijawahi kufuzu kuingia nusu fainali ya NCAA hata mara moja, leo ndiyo mara ya kwanza, mwanachuo mmoja alimwambia Harvey wakiwa njiani kurejea chuoni kwao. Wote wakacheka na kushangilia kwa nguvu wakati daktari wa timu akiendelea kumpatia Harvey huduma ya kwanza.
Timu ya chuo cha Miami Polytechnic and Engineering College, kwa mara ya kwanza ilivuka hatua zote hadi ikafanikiwa kuingia katika hatua ya mwisho ya fainali, ambapo ilipangwa kucheza na timu ya Chuo Kikuu cha York College cha jijini New York.
Hatimaye siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa ya fainali ya michuano hiyo iliwadia. Akina Harvey na wenzake wakasafiri hadi jijini New York wakiwa na matumaini makubwa ya kunyakua ubingwa. Pambano hilo lilivuta hisia za watu wengi, kila mmoja akawa na hamu kubwa ya kuiona timu mpya ya Miami Polytechnic and Engineering College ikichukua kombe kwa mara ya kwanza, chini ya kiongozi wake, Harvey.
Kilichotabiriwa na wengi ndicho kilichotokea kwani pambano lilikuwa kali na la kusisimua. Mpaka mwisho wa mchezo, Harvey kama kawaida yake akafanikiwa kufunga magoli mengi peke yake, na kuvunja rekodi ya mchezaji aliyepachika vikapu vingi kuliko wote tangu ligi hiyo ianze.
Furaha waliyokuwa nayo wanachuo wenzake ilikuwa haielezeki, muda wa kutolewa kwa zawadi ulipowadia, chuo hicho kikakabidhiwa kombe pamoja na fedha taslimu, huku Harvey akichukua tuzo tatu kwa mpigo. Tuzo ya kwanza ilikuwa ni ya mchezaji bora aliyechipukia kwenye mashindano hayo, tuzo ya pili ikawa ni mfungaji bora wakati tuzo ya tatu ikawa ni mchezaji bora.
Alikabidhiwa tuzo tatu pamoja na fedha taslimu, tukio lililorushwa na vituo karibu vyote vya runinga nchini humo. Jina la Harvey likaingia katika orodha ya wachezaji bora kabisa wa mchezo wa kikapu kwa wanachuo kuwahi kutokea.
Unajisikiaje kunyakua tuzo tatu kwa mpigo na kukiwezesha chuo chako kwa mara ya kwanza kunyakua kombe la NCAA? Larry Clarkson, mtangazaji wa michezo wa runinga ya CNN alikuwa akimhoji Harvey, muda mfupi baada ya shamrashamra za fainali hiyo kumalizika jijini New York.
Najisikia fahari sana, sikuwahi kutegemea kuwa ipo siku nitakuwa na uwezo mkubwa kiasi hiki kwenye mchezo wa mpira wa kikapu. Namshukuru Dk Lewis na familia yao kwani bila hivyo nisingekuwa hapa nilipo. Zaidi namshukuru Mungu wangu kwa kuninusuru na yote yaliyotokea mpaka leo nimefika hapa nilipo, alisema Harvey huku akijifuta machozi ya furaha.
Licha ya ugumu aliokumbana nao mwanzo kutokana na kuzongwa na msongo mkali uliosababishwa na kumbukumbu za kuhuzunisha za jinsi wazazi wake walivyouawa mbele ya macho yake kisha kunusurika kufa baharini wakati akitoroka na wenzake, nyota ya jaha inaanza kungaa maishani mwake.
Kipaji kikubwa cha mchezo wa mpira wa kikapu alichojaaliwa kinamfanya awe maarufu haraka nchini Marekani. Michuano ya mpira wa kikapu ya NCAA iliyokuwa maalum kwa wanafunzi wa vyuo nchini humo, inamtangaza na sasa kipaji chake kinaonekana na kila mtu.
Wakati akianza kusahau machungu aliyopitia maishani mwake, kikwazo kingine kinaanza kuibuka. Mtoto wa Dk. Lewis, Skyler anaonesha hisia nzito za mapenzi kwa Harvey na kuanza kumtega ili akubali kuvunja naye amri ya sita lakini anakuwa makini na kumzidi shetani nguvu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
HARVEY aliendelea kupamba vyombo mbalimbali vya habari nchini Marekani na sehemu nyingine kwa wiki kadhaa huku kila mmoja akimtabiria kuja kuwa mtu mwenye mafanikio makubwa kupitia kipaji kikubwa cha mpira wa kikapu alichokuwa nacho.
Siku zilizidi kusonga mbele huku jina lake likizidi kuwa gumzo kila mahali. Akaendelea na masomo huku safari hii akipewa heshima ya kipekee kutoka kwa wanachuo wenzake, wakufunzi na watu wa kila aina, akawa anaishi kama waishivyo watu maarufu nchini humo.
Licha ya yote aliyokuwa anayapitia, kwake heshima kwa wakubwa na wadogo ilibaki kuwa nguzo yake muhimu. Kamwe hakujisikia wala kuwadharau wengine, akaendelea na masomo yake huku kila mwisho wa muhula, matokeo yake ya mitihani chuoni hapo yakizidi kuwa mazuri.
Hakuacha kuwaheshimu Dk Lewis na mkewe ingawa alipunguza sana safari za kwenda kuwatembelea nyumbani kwao akihofia kukutana na Skyler. Alitambua fika kuwa itakapotokea akakutana na Skyler wakiwa wawili tu, lazima shetani atamzidi nguvu na kumsukuma kufanya jambo ambalo mwisho wake utakuja kuwa mbaya.
Badala ya kuwatembelea nyumbani kwao, akabadili utaratibu ambapo alikuwa akimfuata Dk Lewis kazini kwake na kufanya naye mazungumzo hukohuko kisha kurejea chuoni. Hata alipohitaji kuzungumza na mama Skyler, alikuwa akimfuata kazini kwake na kumalizana naye.
Kila Skyler alipokuwa anamtembelea chuoni, alikuwa akiwaita marafiki zake wawili au watatu na kumfanya ashindwe kumfanyia vituko vya kimapenzi, jambo lililoonekana kumchukiza Skyler, akapunguza safari za kumfuatafuata huku moyoni akiweka nadhiri kuwa ipo siku yale aliyokuwa anayataka yatatimia.
Hatimaye Harvey alimaliza mwaka wa pili chuoni pale kwa mafanikio makubwa, kipindi cha likizo hakurudi nyumbani kama ilivyokuwa kawaida, badala yake akaomba ruhusa kwa walezi wake ya kwenda kuimalizia likizo yake (vacation) kwenye Jiji
la Bridgetown kwenye Visiwa vya Barabados kujipongeza kwa mafanikio makubwa aliyoyapata.
Alihitaji muda wa kukaa mbali na watu wote ili apate fursa ya kuyatazama upya maisha yake na kuangalia alipotoka, alipo na anapolekea. Wazo lile liliungwa mkono na Dk Lewis na mkewe kwani hata washauri wa kisaikolojia waliokuwa wanamtibu Harvey siku za mwanzoni, walishauri jambo kama lile.
Hakuongozana na mtu yeyote katika safari ile, akachukua vitu vichache zikiwemo nguo na baadhi ya vitabu vyake. Akasafiri kwa ndege mpaka kwenye Jiji la Bridgetown. Kwa kuwa fedha hazikuwa tatizo tena kwake, alifikia kwenye hoteli yenye hadhi ya nyota tano ya Bajan Grenadines iliyokuwa kwenye ufukwe wa Bahari ya Atlantic iliyokuwa inakizunguka kisiwa hicho.
Alikaa kisiwani humo kwa siku 28 huku kila siku asubuhi na jioni akitumia muda mwingi kufanya mazoezi ya mpira wa kikapu, ikiwa ni maandalizi kabla hajaenda kuripoti rasmi kwenye timu ya Miami Heat. Kwa siku zote alikuwa bize kiasi cha kumfanya asihisi upweke wa aina yoyote. Baada ya wiki nne kuisha, alijiandaa kwa safari ya kurejea Miami, Florida nchini Marekani.
Baada ya maandalizi yote kukamilika, alisafiri kwa ndege ya American Airline hadi Marekani na bila kupitia nyumbani kwa Dk Lewis alipitiliza moja kwa moja chuoni japokuwa bado muhula wa masomo ulikuwa haujaanza. Kilichomfanya apaone nyumbani kwa Dk. Lewis kama kituo cha polisi ni vituko vya Skyler. Aliona njia pekee ya kuepusha shari iliyokuwa inataka kutokea ni kujiweka mbali na binti huyo.
Siku chache tangu arejee kutoka Barbados, alipigiwa simu na viongozi wa timu ya Miami Heat wakimtaarifu kuwa siku inayofuata, viongozi wa juu wa timu hiyo walikuwa wakihitaji kuzungumza naye.
Alijiandaa na siku iliyofuatia akafunga safari mpaka kwenye makao makuu ya timu hiyo yaliyokuwa katika Mtaa wa Miami Chini (Downtown) kwenye Jimbo la Florida. Alipofika, alipokelewa kama shujaa na watu ambao tayari walikuwa wameandaliwa kwa kazi ile bila mwenyewe kujua. Ikawa ni kama sapraizi kwake ambapo alibebwa juujuu hadi kwenye chumba cha mikutano katika jengo la American Airways Arena lililokuwa linatumika kama ofisi za timu hiyo.
Harvey, karibu sana Miami Heat, kutana na Micky Arison, huyu ndiye mmiliki wa timu hii, utamfahamu zaidi ukianza kushiriki mazoezi na timu yetu, alisema meneja wa timu hiyo, Pat Riley, Harvey na Arison wakapeana mikono huku kila mmoja akiwa na furaha ya kukutana na mwenzake.
Akatambulishwa pia kwa kocha mkuu wa timu hiyo, Erik Spoelstra ambaye walipopeana mikono alijaribu kumpima nguvu kwa kuusukuma mkono wake kwa kushtukiza.
Safi sana, hapa nilikuwa nakufanyia jaribio jepesi, unaonekana una nguvu za kutosha kwenye mikono yako, jambo ambalo ni muhimu sana kwa wachezaji wa mpira wa kikapu, alisema kocha Spoelstra huku akicheka, ukumbi mzima uliokuwa umejaa maafisa wa juu wa timu hiyo, ukalipuka kwa vicheko.
Utambulisho uliendelea ambapo alikutanishwa na maafisa wengine waliokuwa wanaunda menejimenti ya timu hiyo. Baada ya kumaliza utambulisho huo, Harvey alielekezwa sehemu ya kukaa ambapo mmiliki wa timu hiyo alianza kutoa hotuba fupi ya kumkaribisha Harvey kwenye timu yake.
Tutakulipa mshahara mnono kila wiki na utakapomaliza chuo tutakupa nyumba ya kuishi pamoja na usafiri. Tunataka uitumikie timu yetu kwa uwezo wako wote kuhakikisha tunatetea kombe la NBA tunalolishikilia na kunyakua mengine zaidi, alisema Arison kwenye sehemu ya hotuba yake na kupigiwa makofi na wote waliokuwa ukumbini mle.
Akakabidhiwa jezi namba yenye namba 11 mgongoni ambayo aliambiwa ndiyo atakuwa akiitumia awapo na timu hiyo. Wakafuatia viongozi wengine ambao kila mmoja alitoa hotuba fupi akionesha matumaini makubwa kwa mchezaji huyo.
Kwa Harvey bado alikuwa anaona kama yupo ndotoni, hata alipopewa nafasi ya kusema chochote, aliishia kumwaga machozi ya furaha na kuahidi kuitumikia timu ile kwa moyo mkunjufu. Baada ya kikao kile kumalizika, Harvey alienda kutambulishwa kwa wachezaji wenzake waliokuwa wanaendelea na mazoezi kwenye viwanja vya timu hiyo.
Akakutanishwa na mchezaji nyota wa timu hiyo, Lebron James ambaye alianza kumtambulisha kwa wachezaji wengine kama Ray Allen, Joel Anthony, Shane Battier, Chris Bosh, Mario Chalmers, Norris Cole, Eddy Curry, Justin Hamilton, Terrel Harris na wengine wengi.
Ilikuwa siku ya kipekee sana kwa Harvey kwani alizoea kuwaona wachezaji hao kwenye runinga na vyombo vya habari lakini siku hiyo alipeana nao mikono laivu na kuzungumza nao mawili matatu. Baada ya muda, akaambiwa abadilishe nguo zake na kuvaa jezi mpya alizokabidhiwa kisha aungane na wenzake kwenye mazoezi.
Waandishi mbalimbali wa habari wakiwemo wapiga picha na watangazaji wa redio na runinga walishaataarifiwa kuwa Harvey atatambulishwa rasmi siku hiyo, hivyo wakamiminika kwa wingi kwenye viwanja vya timu hiyo. Baada ya Harvey kuvaa jezi nadhifu za timu hiyo, aliingia uwanjani huku akishangiliwa kwa nguvu, akaanza kufanya mazoezi huku kila mtu akiwa makini kumtazama.
Aisee hatujakosea kumsajili huyu kijana, hebu cheki anavyowakimbiza wenzake na ku-dunk, yaani hata Lebron James hapa itabidi afanye kazi ya ziada kulinda namba yake, alisema mmiliki wa timu hiyo, Arison na kuungwa mkono na wenzake. Mazoezi yakaendelea ambapo kwa mara nyingine Harvey alifanikiwa kuthibisha uwezo wake kwa vitendo.
Baada ya kukaa na kupambana na ugumu aliokumbana nao mwanzo kutokana na kuzongwa na msongo mkali uliosababishwa na kumbukumbu za kuhuzunisha za jinsi wazazi wake walivyouawa mbele ya macho yake, Harvey anaanza kusahau yote na mafanikio yanaanza kuelekea upande wake.
Kipaji kikubwa cha mchezo wa mpira wa kikapu alichojaaliwa, kinamfanya awe maarufu haraka nchini Marekani na kusajiliwa na timu kubwa ya Miami Heat, iliyokuwa inashikilia ubingwa wa NBA nchini Marekani. Harvey ambaye aliibukia kutoka kwenue michuano ya mpira wa kikapu ya NCAA iliyokuwa maalum kwa wanafunzi wa vyuo nchini humo, anakuwa gumzo kila sehemu.
Wakati maisha yakimnyookea, kikwazo kingine kinaanza kuibuka. Mtoto wa Dk. Lewis, Skyler anaonesha hisia nzito za mapenzi kwa Harvey na kuanza kumtega ili akubali kuvunja naye amri ya sita lakini anakuwa makini na kumzidi shetani nguvu.
HARVEY aliendelea kufanya mazoezi na wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya Miami Heat, huku benchi la ufundi la timu hiyo, likiangalia mambo kadhaa kwa mchezaji huyo waliyekuwa tayari wamesaini naye mkataba mnono.
Viongozi wa juu wa timu hiyo, akiwemo mmiliki, meneja, kocha na maafisa wengine wa ngazi za juu, wote walikuwa uwanjani huku wachezaji wote wakiendelea na mazoezi kwa nguvu. Kwa kuwa Harvey alikuwa na mazoea ya kufanya
mazoezi magumu kila siku, kwake ile ilikuwa nafasi ya kuonesha uwezo wake mwingine. Akaendelea kujitahidi kwa uwezo wake wote, huku akishangiliwa kwa nguvu.
He was born to succeed through basketball,
(alizaliwa ili afanikiwe kupitia mpira wa kikapu)
alisema meneja wa timu hiyo, wakati akibadilishana mawazo na mmiliki pamoja na maafisa wengine. Waandishi wa habari nao waliendelea kufanya kazi yao, Harvey akapigwa picha nyingi kuanzia zile za kawaida (still) mpaka za video. Kwa kipindi chote alichocheza, hakuna hata dakika moja ambayo alionekana kupunguza kasi, akawa anawachangamsha wenzake na
kuwaonesha ufundi wa kila aina, kila mmoja alimpigia makofi huku wengine wakiendelea kumshangilia kwa nguvu. Mpaka muda wa mazoezi unamalizika, jina la Harvey lilikuwa mdomoni mwa kila mtu, watu wakawa wanaulizana alikuwa wapi siku zote kujitokeza.
Safi sana, naamini hapa ndipo ulipopangiwa kuja kufanikiwa maishani mwako. Nimefurahishwa na uwezo wako, na nakuahidi utakapoendelea kuongeza juhudi kila siku na malipo yako yatakuwa yanaongezeka, alisema mmiliki wa timu ile, Micky Arison. Wakazungumza mambo mengi ambapo pia walikubaliana Harvey aendelee kubaki na timu ile kwa siku chache ambazo zilikuwa zimesalia kabla ya muhula wa masomo kuanza.
Kwa kuwa Harvey bado alikuwa na siku chache kabla ya kuanza masomo, alikubaliana na wazo lile, akaendelea kukaa kwenye makao makuu ya timu hiyo, Miami Downtown akifanya mazoezi ya asubuhi, mchana na jioni kulingana na ratiba ilivyokuwa inaeleza.
Aliendelea kuonesha kipaji chake muda wote huku wenzake wengi wakitamani nao wangekuwa na uwezo kama wa Harvey. Siku moja kabla ya tarehe ya kuanza rasmi kwa masomo chuoni ilipowadia, Harvey akiwa tayari ameshafanya mambo mengi na wachezaji wenzake na angalau kuanza kuzoeana nao, alianza kujiandaa kwa ajili ya kurejea chuoni siku inayofuatia
Usiondoke Harvey, endelea kufanya mazoezi na sisi, ukiondoka tutapooza kabisa, tumeanza kukuzoea, alisema Lebron James, nahodha wa timu hiyo iliyokuwa inashikilia ubingwa wa kombe la ligi kuu ya mpira wa kikapu nchini Marekani (NBA). Hakutaka kabisa kusikia taarifa za Harvey kurejea chuoni.
Ahsante kaka, najua mnavyojisikia , lakini ni lazima nihitimu kwanza masomo yangu, tupo pamoja wala msijali, alijibu Harvey huku akiwa ameshikana mkono na Lebron, wakaendelea kuzungumza mambo kadhaa yaliyowafanya wazidi kuzoeana.
Wachezaji wengi hawakutaka Harvey aondoke kwani mbinu, nguvu, ubunifu na kasi alivyovionesha kwa muda mfupi aliokuwa amekaa na timu ile, viliwafanya wachangamke sana, tofauti na walivyokuwa mwanzo.
Nguvu ya kujiamini ikaongezeka kwa kila mmoja. Hata hivyo, Harvey ilikuwa ni lazima arejee chuoni kumalizia mwaka wa mwisho kama mkataba ulivyokuwa unaeleza. Akawaahidi kuwa angeendelea kushirikiana nao siku za mwisho wa wiki au baada ya muda wa masomo.
Ikabidi iandaliwe hafla nyingine fupi ya saa zisizozidi tatu, ambapo wachezaji na viongozi wote, walimshukuru Harvey kwa kujumuika nao kwa siku zile chache, wakakubali kuwa uwezo na kipaji alivyokuwa navyo, ni hazina kubwa kwa timu ile.
Walimsihi asikubali kurubuniwa na timu nyingine kwani pale ndiyo kwao na mkombozi waliyekuwa wanamsubiri kwa muda mrefu kwenye mpira wa kikapu, alikuwa amewadia.
Baada ya hafla ile fupi iliyojumuisha watu kula, kunywa na kucheza muziki kumalizika, Harvey alisindikizwa na msafara mkubwa wa wachezaji na viongozi wa timu ya Miami Heat mpaka chuoni kwao, shamrashamra za kujiunga kwake na timu hiyo zikalitikisa jiji lote la Miami na Jimbo la Florida kwa jumla. Shangwe zikapamba moto kwenye mitaa yote msafara wa kumsindikiza chuoni ulipopita.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mpaka wanawasili chuoni kwao, Miami Polytechnic and Engineering College, wanachuo wenzake walikuwa wameshajipanga, wakampokea kwa shangwe na kupitiliza mpaka kwenye ukumbi mkubwa wa Hall 7, uliokuwa unatumika kufanyia sherehe na matamasha ya wanachuo, burudani kubwa ikaendelea chuoni pale.
Najisikia fahari sana, mafanikio haya niliyoyapata ni yenu na nayatoa kwa ajili yenu, namshukuru Mungu wangu na wote mnaoniunga mkono, naheshimu sana wema wa Dk Lewis na familia yake kwangu, sina cha kusema zaidi ya ahsanteni sana, alisema Harvey huku akishangiliwa kwa nguvu.
***
Siku ile ya kipekee kwenye maisha ya Harvey ikapita, usiku akalala usingizi wa ajabu, ambao hakuwahi kuulala tangu azaliwe, akawa anajiona anaelea kwenye mbingu ya saba kwa mafanikio yale. Kesho yake, alfajiri na mapema aliamka kama kawaida, akavaa nguo zake za mazoezi na kwenda kwenye gym ya chuo kwa ajili ya kujifua.
Siku zote hakutaka kubweteka, japokuwa kila mtu alikuwa akiukubali uwezo wake awapo uwanjani, mwenyewe bado hakuwa akiridhishwa na kiwango chake, akapania kufanya mazoezi ya nguvu mara kwa mara ili kuongeza uwezo wake maradufu. Aliendelea na mazoezi mpaka saa moja kasoro za asubuhi, akaenda kujiandaa na wenzake kwa ajili ya kuhudhuria masomo kulingana na ratiba yao ya chuo ilivyokuwa.
Wakati akiendelea kujiandaa, mwanachuo mwenzake, Cazzard alimfuata na kumweleza kuwa jana yake, wakati yeye akiwa bado hajarejea kutoka kwenye utambulisho wa timu ya Miami Heat, mdogo wake, Skyler alifika chuoni pale na kumkosa.
Alikusubiri kidogo, baadaye akaondoka na kuahidi kuwa leo atakuja tena kwa sababu ana ujumbe muhimu sana kwako.
Aaah! Huyu dadaangu naye anataka kuniharibia future hivihivi.
Kwa nini unasema hivyo Harvey?
Mh! Najisikia aibu kusema lakini ndiyo ukweli dadaangu huyu anataka tuwe na uhusiano wa kimapenzi.
Whaaaat? Mapenzi? Huyu si mdogo wako kabisa huyu, halioni hilo?
Yaani mi sina la kusema, amenikosesha raha kwa kipindi kirefu sana.
Ndiyo maana siku ile nilipokuja kukugongea mlango mkiwa naye ndani alinitazama kwa jicho baya sana? Una msala
mwanangu lakini mtoto mzuri kama yule siku moja unafumba macho na kuuweka undugu pembeni then unaonja asali lakini mara moja tu teh teh teh! Im just kidding! (natania tu), alisema Cazzard na kumfanya Harvey amkazie macho.
Sipendi utani huo, be serious Cazzard, hili ni tatizo lingine kwenye maisha yangu, alisema Harvey, ikabidi rafiki yake abadili mazungumzo haraka akikwepa kumkasirisha zaidi.
Muda mfupi baadaye, wakati vipindi ndiyo vikikaribia kuanza, Harvey alishtuka kumuona Skyler akija mbiombio. Kwa kuwa safari hii alikuwa anapafahamu mpaka kwenye chumba alichokuwa analala Harvey pale chuoni, aliongoza moja kwa moja.
Harvey akaishiwa nguvu, ikabidi akubali kumpokea, wanafunzi wengine wakaanza kuelekea kwenye vipindi vya masomo yao, kila mmoja kulingana na ratiba yake ilivyokuwa inasema.
Skyler, naomba niende darasani tutazungumza baadaye.
Noo Harvey, naomba uahirishe vipindi vya asubuhi, nina ujumbe mzito kwa ajili yako, please, fanya hivyo kwa ajili yangu, alisema Skyler kwa kubembeleza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment