Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

QUEEN OF THE GORILLAS ( MALKIA WA MASOKWE ) - 3

 







    Simulizi : Queen Of Gorillas ( Malkia Wa Masokwe )

    Sehemu Ya Tatu (3)





    MTOTO wa Skyler, Harrison anazidi kukua vizuri licha ya kwamba alizaliwa katika mazingira magumu. Kwa kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele, ndivyo mtoto huyo



    anavyozidi kuwa mkubwa, huku utundu ukiwa umemtawala. Anapotimiza miaka mitatu, anaandikishwa shule ya chekechekea.



    Ile huzuni iliyokuwa imetanda kwenye maisha ya Skyler, sasa inaanza kupungua kwa jinsi alivyokuwa anafarijika akimtazama mwanaye huyo. Mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo kwa Harvey, sasa anayahamishia kwa Harrison.



    Kumbukumbu juu ya wazazi wake, Dk Lewis na Suzan zinaanza kukisumbua kichwa chake. Anajiambia kuwa ameshawasamehe kwa yote yaliyotokea na anaanza kufikiria kurudi nyumbani kwao na kuwapelekea mjukuu wao, Harrison.



    Upande wa pili, familia mpya ya Charwe na mkewe Anganile, inajaliwa kupata mtoto mzuri wa kike, Charlotte. Mwanaume anaendelea kufanya kazi Geneva, Uswisi na mwanamke anafanya kazi kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Hali hiyo inafanya



    wawe wanasafiri kwa ndege mara kwa mara kwa ajili ya kutembeleana, hasa kipindi cha likizo au sikukuu.



    MSIMU mwingine wa sikukuu uliwadia, Anganile akawa anajiandaa kwa safari ya kuelekea Geneva kwa mumewe, akiwa na mwanaye kipenzi, Charlotte ambaye alikuwa akizidi kukua, huku urembo na shani alivyojaliwa na Mungu vikizidi kujidhihirisha.

    Baada ya maandalizi yote kukamilika, Anganile aliwasiliana na mumewe, akamtumia tiketi ya ndege. Anganile akamchukua mwanaye pamoja na



    zawadi nyingine walizomuandalia baba Charlotte, wakafunga safari mpaka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.



    Walipofika kwenye ofisi za Shirika la Ndege la Uswisi (Swiss Airways), mhudumu aliyekuwepo aliwapa taarifa juu ya mabadiliko ya ratiba za ndege yaliyosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyozikumba nchi za Ulaya.



    “Ukungu mwingi umetanda kwenye anga la nchi mbalimbali za Ulaya hususan Ufaransa, Sweden, Uholanzi na Uswisi mnakotaka kwenda. Kuepusha ajali za ndege zinazoweza kuzuilika, safari zote kuelekea Ulaya moja kwa moja kutoka Afrika zimesitishwa.



    “Kampuni yetu imeamua wateja wote wanaosafiri kuelekea nchi za Ulaya waende mpaka New York, Marekani na baada ya hapo watahamishiwa kwenye ndege nyingine itakayowapeleka mpaka barani Ulaya. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza,” alisema yule mhudumu, Anganile akashusha pumzi ndefu na kusogea pembeni na mwanaye.



    Habari zile zikawa zinaendelea kutangazwa pale uwanja wa ndege kwa kutumia vipaza sauti vilivyokuwa kwenye kila kona. Abiria wengi walikumbwa na taharuki, wakawa na wasiwasi mkubwa juu ya usalama wao na mali zao

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Taarifa zile zilimchanganya sana Anganile, ikabidi awasiliane na mumewe Charwe kwa njia ya simu na kumueleza hali halisi.

    “Ni kweli kuna ukungu mzito huku, ndege nyingi zimesimamisha safari zake, ningeweza kusema muahirishe safari mpaka wakati mwingine lakini kwa kuwa nimewakumbuka sana na sikukuu zimekaribia, fuateni mlivyoambiwa na wahudumu wa ndege, kampuni yao ndiyo itakayogharamia kila kitu,” alisema Charwe.



    Mkewe alienda kubadilisha tiketi ya ndege kama walivyoambiwa na baada ya kusubiri kwa saa moja, ndege kubwa ya Swiss Airways iliyokuwa inaelekea Marekani, ilianza kupakia abiria. Anganile na mwanaye wakawa ni miongoni mwa abiria walioingia kwenye ndege ile. Baada ya muda, safari ikaanza.



    Baada ya safari ndefu iliyochukua takribani saa kumi angani, ndege ile iliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa John F. Kennedy jijini New York, Marekani. Abiria wakaanza kuteremka mmoja baada ya mwingine, Anganile na mwanaye nao wakawa miongoni mwao.



    Kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya zaidi kwenye nchi za Ulaya, ukungu ukiendelea kuwa tishio, ilibidi abiria wote waliokuwa wanaendelea na safari wapelekwe kwenye hoteli walizokuwa wanazitaka kwa gharama ya Kampuni ya Swiss Airways mpaka asubuhi ya siku ya pili.



    Anganile na mwanaye walienda kupumzika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, New York ambapo asubuhi walikuja kuchukuliwa na kupelekwa tena uwanja wa ndege. Wakapandishwa kwenye ndege kubwa ya kisasa, Herpa Lufthansa Premium, toleo jipya namba C-47B-DK 1:200 iliyokuwa na uwezo wa kusafiri hata kwenye ukungu mzito.



    Kwa kuwa kulikuwa na abiria wengine kutoka sehemu mbalimbali za dunia ambao nao walikuwa wamekwama kwenda nchi za Ulaya kutokana na hali ya hewa, ndege ilijaa yote. Ghorofa zote mbili, ya juu na ya chini zilishona abiria, muda mfupi baadaye safari ya kuelekea Geneva ikaanza.

    Ndege ikaanza kujongea taratibu na kugeuka kuelekea kwenye njia za kurukia (run ways), ikaanza kuongeza kasi huku injini zikizidi kuchanganya, sekunde chache baadaye ikapaa na kuiacha ardhi ya Marekani.



    Muda mfupi baada ya ndege hiyo kuruka, marubani walianza kuhangaika kwani ukungu ulikuwa mzito kuliko walivyotegemea, hali iliyosababisha mawasiliano yawe magumu.

    Ndege ile, licha ya kuwa ilikuwa ni toleo jipya, ikiwa na taa maalum za kumulika kwenye ukungu na uwezo mkubwa wa kuhimili hali mbaya ya hewa, ilianza kuyumbayumba.



    Abiria wakakumbwa na hofu kubwa, hali ya sintofahamu ikatanda kila mahali huku wakianza kusali kwa imani zao wakimuomba Mungu awanusuru na janga kubwa lililokuwa mbele yao.



    Hali iliendelea vile kwa muda mrefu, hatimaye ndege ile ikapoteza mwelekeo na kuanza kuzunguka angani. Maafisa wa Uwanja wa Ndege wa John F. Kennedy kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Marekani, walipokea taarifa za ndege hiyo kupoteza mwelekeo, haraka wakaanza kuhangaika kuitafuta angani.



    Mitambo iliyokuwa inaongozwa na satellite sambamba na wataalamu wa usafiri wa anga na wale wa vikosi vya uokoaji, walisaidiana na baada ya kuhangaika sana, walifanikiwa kutambua mahali ndege hiyo ilipokuwepo.



    “Tunaiona ikiwa inazunguka kwenye ukungu mzito, juu ya msitu mkubwa wa Tongass, Kusini Mashariki mwa Jimbo la Alaska karibu na mpaka wa Marekani na Canada lakini tumepoteza kabisa mawasiliano na marubani,” alisema Kamanda wa Kikosi cha Uokoaji, Russel Winans, harakaharaka ndege za kijeshi za uokoaji zikaanza kuondoka kwa kasi kubwa kuelekea kwenye Msitu wa Tongass kuiokoa ndege ile kabla haijaanguka.

    ***



    Harrison alizidi kuwa mkubwa, masomo ya shule ya awali aliyokuwa anasoma yakamfungua upeo wake wa kuelewa mambo kwa kiasi kikubwa. Akawa anaweza kuhesabu vizuri, kuwatambua wanyama na vitu mbalimbali.

    “Huyu mtoto anapenda sana kucheza na wanyama, atakuja kuwa daktari wa wanyama akiwa mkubwa.”

    “Akuu, mwanangu awe daktari wa wanyama? Mi nataka aje kuwa mtaalam mwenye kazi yake ya maana, siyo hiyo,” alisema Skyler wakati akizungumza na Scolastica.



    Scolastica alimwambia Skyler ni vizuri kumtazama mtoto mapema na kumuongoza katika kipaji au karama aliyokuwa nayo. Waliendelea kuzungumza mambo mengi kuhusu mtoto yule. Kila Skyler alipokuwa akimtazama mwanaye, alikuwa akifarijika sana ndani ya moyo wake. Ile furaha iliyokuwa imetoweka kwa kipindi kirefu, ikawa inarejea na kumfanya ajione shujaa.



    Siku zilizidi kusonga mbele, mawazo ya Skyler juu ya wazazi wake yakawa yanazidi kumsumbua kichwani.

    “Inabidi nirudi nyumbani,” aliwaza Skyler, akazungumza na Scolastica ambapo alimueleza mambo mengi kuhusu familia yao ambayo awali hakuwahi kuyasema. Scolastica alimsubiri mumewe Bill ambapo alimueleza kila kitu alichozungumza na Skyler. Wakakubaliana kuwa watamsindikiza ili nao wakafahamiane na wazazi wake kwani tayari walishakuwa kama ndugu.



    “Kesho tunaenda kwa bibi na babu wengine, si kila siku unanisumbua,” Skyler alimwambia mwanaye wakati wakijiandaa kulala. Harrison alichekelea sana, japokuwa alikuwa mdogo, alikuwa akiweza kutofautisha na kuelewa mambo mengi.



    Asubuhi na mapema, Skyler na mwanaye sambamba na walezi wake, Bill na Scolastica waliingia ndani ya gari la familia, safari ya kuelekea Miami ikaanza. Walisafiri kwa muda mrefu, hatimaye wakaanza kukaribia kufika.



    “Hii ndiyo shule niliyokuwa nasoma,” alisema Skyler huku akiwaonesha Bill na Scolastica majengo ya shule iliyokuwa pembeni ya barabara. Aliwaelekeza njia za kupita na baada ya muda, wakawa tayari wameshaingia kwenye mtaa aliokuwa anaishi Skyler na wazazi wake.

    “Simama kwenye hilo geti hapo mbele,” Skyler alimuelekeza Bill aliyekuwa akiendesha gari. Gari likasimama ambapo Skyler ndiyo alikuwa wa kwanza kufika. Mazingira aliyoyakuta, yalimshtua kuliko kawaida.



    Nyumba ilikuwa imechakaa, madirisha na milango vikiwa wazi kuonesha kuwa hakukuwa na watu waliokuwa wanaishi kwenye nyumba hiyo. Majani yalikuwa yameota karibu kila sehemu kuzunguka nyumba. Zile bustani za maua ambazo kipindi cha nyuma zilikuwa zikihudumiwa na kutunzwa vizuri, sasa ziligeuka na kuwa vichaka vya kutisha.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    FAMILIA mpya ya Charwe na mkewe Anganile inaingia kwenye msukosuko mkubwa baada ya ndege waliyokuwa wanasafiria Anganile na mwanaye Charlotte, Herpa Lufthansa Premium wakati wakiwa njiani



    kwenda Geneva, kupoteza uelekeo ikiwa angani kutokana na ukungu mzito uliokuwa umetanda.

    Licha ya vikosi vya uokoaji kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wao wote kuiokoa ndege hiyo kabla haijapata ajali, ukungu unafanya zoezi liwe gumu. Inazidi kupoteza uelekeo, ikiwa kwenye anga la Msitu Mkubwa wa Tongass, kwenye Jimbo la Alaska nchini Marekani.



    Upande wa pili, Skyler, mwanaye Harrison na walezi wake, Bill na Scolastica wanasafiri mpaka nyumbani kwa akina Skyler, Miami lakini wanapofika, wanakuta eneo lote likiwa kimya kabisa na kutawaliwa na upweke, hali inayoonesha kuwa hakuna mtu aliyekuwa akiishi ndani ya jengo hilo.



    LICHA ya marubani wa ndege ile kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wao wote kupambana na hali mbaya ya hewa, bado hawakufanikiwa kuirudisha ndege kwenye mstari. Walizidi kusukumwa na upepo mkali ulioambatana na ukungu juu ya Msitu wa Tongass, Kusini Mashariki mwa Jimbo la Alaska karibu na mpaka wa Marekani na Canada.



    “Injini moja ya kushoto imepoteza uwezo wake wa kufanya kazi. Lazima itakuwa imeingia maji kutokana na ukungu.”

    “Mungu wangu, sasa itakuwaje? Mi’ nashauri tutafute sehemu yenye uwazi tutue.”

    “Hatuwezi kutua, kuna ukungu mzito sana, tukiteremka mita chache kutoka hapa tulipo injini nyingine zote zitazima.”

    “Hebu tujaribu kuongeza joto kwenye injini ili kukausha ukungu unaosababisha maji kujaa,” marubani wa ndege ya Herpa Lufthansa Premium, toleo



    jipya namba C-47B-DK 1:200 walikuwa wakijadiliana cha kufanya ili kuiokoa ndege ile ambayo sasa ilipoteza kabisa uelekeo.

    Muda mfupi baada ya injini ya kwanza kuzima, nyingine ilizima na kusababisha ndege nzima iwe inaendeshwa kwa injini mbili zilizosalia, tena zote zikiwa upande mmoja wa kushoto.



    Vikosi vya uokoaji vikiongozwa na Kamanda wa Kikosi cha Uokoaji wa Anga, Russel Winans, vilikuwa vikiendelea kuhaha huku na kule kuitafuta ndege ile. Ndege za kijeshi zilizotumwa eneo la tukio kujaribu kuiokoa ndege ile, nazo zilimezwa na ukungu mzito, zikashindwa kuendelea na safari ya kuifuata ndege ile.



    Mawasiliano pekee yaliyokuwa yamesalia, yakiwa yanaongozwa na satellite, nayo yalianza kusuasua, hali ya sintofahamu ikazidi kutawala kila sehemu. Baadhi ya vyombo vya habari vilianza kurusha habari ile, wananchi wengi wa Marekani na nchi jirani ambao ndugu zao walikuwa kwenye ndege ile wakazidi kuchanganyikiwa.



    Charwe, akiwa ofisini kwake, alishtushwa na habari iliyokuwa inarushwa na kituo cha runinga cha CNN iliyoeleza juu ya ndege kubwa ya Herpa Lufthansa Premium iliyokuwa na zaidi ya abiria mia mbili, wakiwemo mkewe Anganile na mwanaye wa kipekee, Charlotte.

    “Mungu wangu, balaa gani tena hili,” alisema Charwe huku akiongeza sauti kwa kutumia rimoti, akasogea kwenye runinga huku akijishika mikono kichwani.



    “No! Haiwezekani, haiwezekani,” alisema Charwe huku akizidi kuitumbulia macho runinga iliyokuwa ofisini kwake.

    Habari ile iliendelea kurushwa mara kwa mara, watu wengi wakawa wanaelewa kilichokuwa kinaendelea, huku kila mmoja akimuomba Mungu kwa imani yake ili kuzuia janga lile lisitokee.



    “Tunawaomba watu wote watulie, kikosi cha uokoaji wa anga kinajitahidi kufanya kila linalowezekana ili kuiokoa ndege kabla haijapatwa na tatizo lolote. Tunaendelea kushughulika na bado abiria wote wapo salama ndani ya ndege,” alinukuliwa Kamanda wa Kikosi cha Uokoaji wa Anga, Winans wakati akizungumza na mtangazaji wa runinga ya CNN.



    Licha ya kujaribu kuwapa moyo watu waliokuwa na ndugu zao ndani ya ndege hiyo, bado hali ya taharuki ilizidi kutawala, watu wakaanza kujikusanya kwenye vikundi mitaani, huku wakiwa makini kusikiliza kilichokuwa kinaendelea.



    “Tangazo! Tangazo! Tangazo! Abiria wote tunaomba usikivu wenu. Ndege yetu imepatwa na hitilafu na hivi sasa inapita kwenye mkondo wa hewa unaokwenda kasi kutokana na ukungu. Tunaomba kila mmoja akae kwenye kiti chake na kujifunga mkanda ili kuipa ndege uzito unaotakiwa. Tunaomba kila mmoja afunge mkanda na kutulia,” mhudumu wa ndege ile alikuwa akijaribu kuwatuliza abiria.



    “Mwanangu Charlotte, nakupenda sana mwanangu… sipo tayari kuona unapoteza maisha yako ukiwa na umri mdogo kiasi hicho. Ni bora nife mimi lakini nikuokoe wewe,” alisema Anganile huku akilengwalengwa na machozi. Alishakata tamaa ya kusalimika kwenye ajali ile, akajua kifo kipo mbele yake.



    Muda mfupi baadaye, wahudumu wa ndege ile walianza kupita kwa abiria na kuwagawia maparachuti maalum ambayo wangeyatumia kutoka ndani ya ndege baada ya kukaribia kufika ardhini.

    “Tumelazimika kutua kwenye msitu wa Tongass kwa dharura, tukikaribia kufika ardhini milango itafunguliwa na abiria wote mtaruka na kutoka nje mkiwa kwenye maparachuti yenu,” alisikika rubani wa ndege ile akitoa maelekezo. Abiria wakayashika maparachuti yao na kusubiri maelekezo mengine.



    Anganile aliamua kumvalisha mwanaye parachuti lile na kumfunga vizuri, Charlotte ambaye hakuwa akielewa chochote kutokana na umri wake mdogo, alikuwa akichekelea kuvalishwa parachuti na mama yake.

    Kufumba na kufumbua, ndege iligeuka kwa kasi kubwa na kuanza kulalia upande mmoja.



    “Ooh shit! Injini zote zimezima, hatuna ujanja… eeeh Mungu onesha miujiza yako,” rubani mmoja alisema baada ya kugundua kuwa zile injini mbili zilizokuwa zimesalia, nazo zilikuwa zimeingia maji na kuzima. Ndege ikaanza kujigeuzageuza huku abiria wakichomoka kwenye viti vyao na kuanza kugongana wao kwa wao.



    Kufumba na kufumbua, Anganile alikanyaga kioo kilichokuwa jirani na pale alipokuwa amekaa na mwanaye, alirudia kukanyaga kwa nguvu, kioo kikachomoka na kuachia nafasi, kwa ujasiri wa hali ya juu akalishika parachuti alilokuwa amemvalisha mwanaye Charlotte na kulisukumia pale kwenye uwazi, likatoka nje na kufunguka, akamsukumia mwanaye nje, akawa anaelea kwenye ukungu mzito. Charlotte akiwa ananing’inia kwenye parachuti, alisukumwa na upepo mkali kuelekea Magharibi mwa msitu huo.



    Alipomaliza tu kufanya vile, Anganile alijaribu kusimama ili atafute parachuti lingine na kuvaa ili na yeye aruke nje ya ndege kama mwanaye lakini alichelewa kwani kufumba na kufumbua moto mkubwa ulianza kuwaka kutokea kwenye vyumba vya marubani, abiria wakawa wanakimbia huku na kule, ndege ikazidi kubiringika angani.



    Moshi mzito ukatanda ndani ya ndege yote, abiria wakawa wanakohoa huku wengine wakianza kuzirai na kupoteza fahamu. Muda mfupi baadaye ndege yote ikalipuka, moto mkubwa ukawa unaonekana juu ya anga la Msitu wa Tongass.

    “Oooh Mungu wangu, ule moshi kule ni wa nini?” alisema Kamanda Winans aliyekuwa ndani ya ndege ya kijeshi iliyokuwa jirani na pale ndege ile kubwa ilipokuwepo. Alipotoa darubini yake iliyokuwa na uwezo wa kupenya hata kwenye ukungu, alishuhudia ndege hiyo ikiteketea kwa moto mkubwa.



    “Herpa Lufthansa Premium inateketea kwa moto, hatuna la kufanya kwani ipo kwenye mkondo wa hewa inayosafiri kwa kasi, moto mkubwa umetanda angani,” alisema Kamanda Winans wakati akitoa taarifa kwa wenzake waliokuwa ardhini.

    Habari zikasambaa kwa kasi, taifa la Marekani likaingia kwenye maombolezo makubwa. Hakukuwa na uwezekano wa abiria hata mmoja kuokolewa kutoka kwenye ndege ile.



    Ndege iliendelea kuteketea kwa moto mkubwa, baadhi ya vyuma vya ndege vikaanza kujiachia na kudondoka mpaka kwenye msitu mnene wa Tongass. Baada ya kuungua yote, vyuma na majivu viliendelea kudondoka ardhini. Hapakuwahi kutokea ajali mbaya ya ndege kama ile nchini Marekani.



    Vyombo vya habari viliendelea kuripoti habari ile ambayo ilitangazwa kama janga la kitaifa, bendera zote za Marekani zikashushwa nusu mlingoti kama ishara ya maombolezo.



    Charwe alishindwa kuamini macho yake wakati Kituo cha Runinga cha CNN kilipokuwa kikirusha picha zilizopigwa kutoka ardhini, zikiionesha ndege ile wakati ikiteketea kabla haijageuka kuwa majivu.

    “Nooo! Haiwezekaniii, mke wangu na mwanangu jamaniii!” alipiga kelele Charwe, akadondoka na kupoteza fahamu.



    AJALI mbaya ya ndege ya Herpa Lufthansa Premium iliyosababishwa na ukungu mzito uliokuwa umetanda angani, inasababisha pigo kubwa kwa Charwe kwani anampoteza mkewe kipenzi na mwanaye, Charlotte waliokuwa njiani kuelekea Geneva kumfuata Charwe.



    Jitihada za vikosi vya uokoaji zinashindwa kuzaa matunda na watu wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo, wanapoteza maisha na kuteketea ndani ya ndege hiyo.

    Upande wa pili, Skyler anaamua kurejea nyumbani kwao akiwa na walezi wake, Bill na Scolastica na



    mwanaye Harrison lakini tofauti na alivyotegemea, anakuta nyumba yao ikiwa imetawaliwa na upweke wa hali ya juu. Inavyoonesha, hakuna mtu aliyekuwa akiishi ndani ya nyumba ile.



    LICHA ya vikosi vya uokoaji kufika eneo la tukio, hakuna mtu wala kitu chochote kilichookolewa kutoka kwenye ndege ile, vyuma, mafuvu ya binadamu na mifupa vikawa vinadondoka kutoka angani na kuangukia kwenye msitu mkubwa wa Tongass.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Tangu nianze kazi ya uokoaji wa anga sijawahi kuona ajali mbaya kama hii. Yaani abiria wote wameteketea kwa moto wakiwa angani? Hii imevunja rekodi,” Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Uokoaji wa Angani, Russell Winans alisema wakati akitembea kwa miguu na kikosi cha askari waliokuwa wa kwanza kufika eneo la ajali, ndani kabisa ya msitu wa Tongass.



    Vyombo vya habari viliendelea kuripoti hatua kwa hatua juu ya kilichokuwa kinaendelea, maombolezo yakaendelea huku watu waliopoteza ndugu zao wakielekezwa kuelekea kwenye Ukumbi wa Madison Square ambapo mabaki yaliyokuwa yanaendelea kuokotwa eneo la tukio yalipelekwa.



    Maelfu ya waombolezaji wakiwa wamevalia mavazi meusi wakawa wanaongozana kuelekea katikati ya Mtaa wa Manhattan jijini New York. Maombolezo yakaendelea, bendera zote zikawa zinapepea nusu mlingoti.



    Baada ya kurejewa na fahamu, Charwe alijikuta akiwa kwenye chumba chenye mashuka meupe, huku pembeni yake akiwa amezungukwa na wafanyakazi wenzake.

    “Hapa ni wapi na nimefikaje?”

    “Upo hospitalini Charwe, umekutwa ukiwa umedondoka na kuzimia nyumbani kwako.”

    “Ahaaa,” alisema Charwe huku akionekana kuanza kuvuta kumbukumbu ya kilichotokea.

    “Kwani umepatwa na tatizo gani?”

    “Mke wangu na mwanangu, oooh! Mungu wangu, kwani haya yanitokee mimi?”

    “Unamaanisha nini Charwe? Tuambie ili kama ni msaada tujue tunaanzia wapi.”

    “Mke wangu na mwanangu ni miongoni mwa abiria waliopata ajali na ndege ya Herpa Lufthansa Premium, wote wamekufaaaaa,” alisema Charwe huku akilia kwa uchungu, wafanyakazi wenzake wakawa na kazi ya ziada kumtuliza.



    Ilibidi taratibu za kiofisi zifanyike haraka, Charwe akakatiwa tiketi ya ndege kutoka Geneva mpaka jijini New York kuungana na waombolezaji wengine kwenye Ukumbi wa Madison Square.

    Akasindikizwa na wafanyakazi wenzake wawili mpaka New York, wakaungana na maelfu ya waombolezaji waliokuwa wanaendelea kumiminika kuangalia mabaki ya ndugu zao Madison Square.



    Baada ya mabaki karibu yote yaliyokuwa yametapakaa kwenye eneo la tukio kukusanywa, makaburi ya halaiki yalianza kuchimbwa nje kidogo ya Jiji la New York. Siku tatu baadaye, mazishi ya pamoja yakafanyika, majina ya watu wote waliokuwepo ndani ya ndege yakaandikwa na kubandikwa kwenye kuta zilizojengwa kuzunguka makaburi yale.



    Baada ya taratibu zote za mazishi kukamilika jijini New York, Charwe alilazimika kusafirisha msiba mpaka Tanzania na kwenda moja kwa moja mkoani Mbeya, nyumbani kwa mkewe Anganile. Kwa kuwa tayari alishawasiliana nao kwa njia ya simu, msiba ulikuwa ukiendelea.



    Alipofika, alipokelewa kwa vilio na maombolezo na ndugu wa mwanamke sambamba na ndugu zake waliosafiri kutoka Bukoba, msiba ukawa ndiyo kama umeanza upya. Pigo lilikuwa kubwa sana kwa Charwe kwani mbali na mke, alimpoteza mwanaye kipenzi Charlotte kwenye ajali hiyo.



    Kwa jinsi alivyokuwa akimpenda mkewe na mwanaye, Charwe aliweka nadhiri ya kukaa siku arobaini nyumbani kwa marehemu mkewe. Alitimiza nadhiri yake na baada ya siku arobaini kuisha, walimsomea marehemu dua kisha akasafiri mpaka nyumbani kwao Bukoba alikokaa siku tatu kisha akapanda ndege kurejea kazini kwake, Geneva nchini Uswisi.

    ***

    Baada ya kuona mazingira ya pale nyumbani kwao jinsi yalivyokuwa, Skyler aliwashauri Bill na mkewe wajaribu kwenda kazini kwa baba yake ili kujua kama kuna taarifa zozote zilizokuwa zinamhusu Dk Lewis na mkewe.



    “Watakuwa wamepatwa na nini?” alijiuliza Skyler wakati gari walilokuwa wanasafiria likikatiza mitaa kuelekea Miami Hospital, alipokuwa anafanya kazi Dk Lewis. Walipofika, Bill na mkewe walibaki ndani ya gari pamoja na mtoto wa Skyler, Harrison. Akateremka na kuanza kutembea harakaharaka kuelekea mapokezi.



    Kila mtu aliyekuwa anakutana naye, alikuwa akimshangaa Skyler, akajikaza na kutoonesha mshtuko wowote. Alipofika mapokezi, alimkuta msichana ambaye ilionesha kuwa ndiyo kwanza anaanza kazi. Skyler akashusha pumzi ndefu kwani alijua kuwa endapo angemkuta mtu anayemjua, angeanza kumhoji maswali ya mahali alipokuwa siku zote hizo, jambo ambalo lingemkasirisha.

    “Namuulizia Dokta Lewis.”

    “Wewe ni nani?”



    “Mwambie naitwa Skyler,” alijibu huku akikwepesha sura yake. Hakutaka yule dada aendelee kumtazama usoni. Alinyanyua mkonga wa simu na kuzungumza na upande wa pili kisha akakata.

    “Mbona ameshtuka sana nilipomtajia jina lako?”

    “Sijaonana naye siku nyingi.”



    “Anasema anakuja sasa hivi,” alijibu yule dada, Skyler akasogea pembeni na kukaa huku muda mwingi akiwa amejiinamia chini.

    Sekunde chache baadaye, mwanaume wa makamo aliyekuwa amevalia kidaktari alikuja huku akiwa anakimbia. Alikuwa ni Dokta Lewis ambaye taarifa za uwepo wa Skyler hospitalini pale alizipokea kama muujiza.



    “Yuko wapi? Yuko wapi Skyler wangu?” Dokta Lewis alimuuliza yule dada wa mapokezi huku akigeuka huku na kule.

    “Babaaaaaa,” alisema Skyler baada ya kumuona baba yake, akasimama na kumkimbilia. Dokta Lewis aligeuka, akakutana na Skyler aliyekuwa anakuja mbio, wakakimbiliana na kukumbatiana kwa nguvu. Kila mmoja akawa anatokwa na machozi.



    “Nisamehe mwanangu, nisamehe kwa yote, nakupenda sana Skyler,” alisema Dk Lewis huku akiwa bado amemkumbatia mwanaye Skyler.

    “Nilishakusamehe baba na wewe naomba unisamehe kwa yote.”



    “Nilishakusamehe mwanangu… vipi mjukuu wangu yuko wapi? Au hukujifungua?” aliuliza Dk Lewis huku akimtazama mwanaye tumboni.



    “Sikwambii chochote mpaka uniambie mama yuko wapi na siku hizi mnaishi wapi kwani nimepita nyumbani nimekuta hali ya ajabu sana,” alisema Skyler huku akijifuta machozi yaliyokuwa yanaulowanisha uso wake.



    Dokta Lewis alishusha pumzi ndefu, akamtazama mwanaye na kurudia kumkumbatia, wakashikana kwa muda mrefu bila kuzungumza chochote. Dokta Lewis alimshika mwanaye mkono, akamuongoza kwenda kwenye bustani za maua zilizokuwa jirani na pale walipokuwa wamesimama, ndani ya Hospitali ya Miami.



    “Ni stori ndefu mwanangu, kutoweka kwako kulisababisha matatizo makubwa kwenye familia yetu. Namshukuru sana Mungu kwamba umerejea, naamini bado nina nafasi ya kuisimamisha upya familia yangu.”

    “Unamaanisha nini baba? Mbona sikuelewi?”



    “Mimi na mama yako tumetengana, ilibidi nimpe talaka mahakamani. Mama yako alikuwa anakupenda sana hivyo ulipoondoka, alinichukia mno akiamini mimi ndiyo chanzo cha matatizo. Alinipa masharti ya kuhakikisha nakupata na hilo liliposhindikana akanipeleka mahakamani na kudai talaka.



    “Vitu vyote tulivyochuma pamoja maishani ilibidi tugawane, vingine tukauza na kubakiza kitu kimoja tu, nyumba ambapo hata hivyo tulikuwa kwenye mipango ya kuiuza lakini tukakosa mteja kutokana na bei yake kuwa kubwa. Hivi sasa mimi naishi mwenyewe na mama yako alirudi nyumbani kwao,” alisema Dokta Lewis huku naye akibubujikwa na machozi.



    Skyler hakujibu wala kuchangia kitu, akampeleka baba yake kwenye gari la Bill na mkewe lililokuwa limepaki nje ya hospitali ile.

    “Hawa ndiyo walezi wangu walioniokota nikiwa kwenye hatua za mwisho za maisha yangu na kunitunza mpaka leo,” alisema Skyler



    lakini kabla hajamaliza kumtambulisha, macho ya Dokta Lewis yalitua kwa mtoto aliyekuwa amekaa siti ya nyuma.

    “Mh! Hii sura mbona imefanana sana na Harvey? Huyu ndiyo mjukuu wangu nini?”

    “Mbona una haraka baba? Tulia nikutambulishe mwenyewe. Huyo ndiyo mjukuu wako, anaitwa Harrison.



    “Mbona amekuwa mkubwa hivi? alisema Dokta Lewis, Skyler akafungua mlango wa gari na kumtoa mwanaye, na kumtambulisha kwa babu yake.



    “Harvey ‘copyright’! Kweli Mungu ana miujiza yake… naamini bibi yake akimuona hasira zake zote zitaisha na atakubali kurudiana na mimi,” alisema Dokta Lewis huku akimrusharusha Harrison. Lile tabasamu ambalo lilipotea kwa kipindi kirefu kwenye maisha yake, sasa lilichanua upya kama lichanuavyo waridi.



    AJALI mbaya ya ndege ya Herpa Lufthansa Premium iliyolipuka angani baada ya kupoteza mwelekeo kutokana na ukungu mzito uliokuwa umetanda, inasababisha pigo kubwa kwa Charwe aliyewapoteza mke na mwanaye waliokuwa njiani kumfuata jijini Geneva ili washerehekee pamoja Sikukuu ya Krismasi.



    Abiria wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo wanapoteza maisha na hakuna kinachookolewa zaidi ya mabati na vyuma vya ndege sambamba na mafuvu ya binadamu yaliyokuwa yanaangukia kwenye Msitu wa Tongass. Msiba mkubwa unalikumba taifa la Marekani na nchi nyingine ambazo raia wake walipoteza maisha kwenye ndege hiyo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande wa pili, Skyler, mwanaye Harrison na walezi wake, Bill na Scolastica, baada ya kukuta mazingira yasiyoeleweka nyumbani kwa akina Skyler, wanafunga safari mpaka kwenye Hospitali ya Miami, alikokuwa anafanyia kazi Dk Lewis na wanafanikiwa kukutana naye. Haamini macho yake kama kweli amekutana tena na Skyler, tena akiwa amemletea mjukuu wa kiume aliyefanana kwa kiasi kikubwa na Harvey.



    BAADA ya kuzungumza mambo kadhaa, Dk Lewis alirudi ofisini kwake na kuomba ruhusa, akatoka hadi pale nje alipokuwa amewaacha Skyler, Harrison, Bill na mkewe Scolastica. Akawachukua Skyler na mwanaye na kuwapakiza kwenye gari lake, akawataka Bill na mkewe Scolastica nao waingie kwenye gari lao na wamfuate.



    Msafara wa magari mawili ukatoka kwenye lango kuu la Hospitali ya Miami na kukata kona upande wa kushoto. Wakaingia kwenye barabara na kusafiri umbali wa takriban kilometa tano, Kaskazini mwa Jiji la Miami. Ndani ya gari, Dk Lewis aliendelea kuchekacheka mwenyewe akiwa kama haamini kilichotokea.



    Mara kwa mara alikuwa akimtazama mwanaye na mjukuu wake huku akiwa na tabasamu pana kwenye uso wake.

    “Naitwa babu sasa! Hongera sana mwanangu kwa kumleta upya Harvey! Nisamehe kwa yote yaliyotokea, naamini Mungu alikuwa na makusudi yake kuacha haya yote yatokee,” alisema Dk Lewis huku akikata kona na kuingia upande wa kulia, akazipita nyumba

    kadhaa kabla ya kuegesha gari mbele ya nyumba ndogo iliyokuwa na rangi ya bluu.



    “Hapa ndipo ninapoishi tangu nilipotengana na mama yako, nimepanga,” alisema Dk Lewis wakati akipaki gari vizuri, akateremka na kuwaelekeza Bill na mkewe Scolastica namna ya kupaki gari lao. Alipomaliza, aliwafungulia mlango Skyler na mjukuu wake Harrison, akambeba juujuu huku akiendelea kumrusharusha.



    “Karibuni sana, hapa ndiyo ninapoishi,” alisema Dk Lewis wakati akiwakaribisha Bill na mkewe, akafungua mlango mkubwa na wote wakaingia. Ilikuwa ni nyumba ndogo lakini yenye kila kitu muhimu. Wakaingia na kukaa sebuleni, Dk Lewis akafungua friji na kutoa jagi lililokuwa na juisi, akawatolea glasi na kuwamiminia kila mtu ya kwake.

    “Baba nani kakutengenezea juisi?”



    “Nimetengeneza mwenyewe, mbona hata chakula huwa napika mwenyewe na kuosha vyombo!” alisema Dk Lewis huku akiendelea kucheza na mjukuu wake Harrison, wote wakacheka kwa furaha na kumsifia kutokana na kutengeneza juisi nzuri kiasi kile. Waliendelea na mazungumzo, Dk Lewis akisimulia jinsi alivyohangaika baada ya mwanaye kutoweka bila kutoa taarifa.



    Baada ya mazungumzo marefu, Bill na mkewe Scolastica waliaga na kuondoka, wakaahidi kuendelea kuwatembelea mara kwa mara. Waliwasindikiza mpaka getini kisha Dk Lewis, mwanaye Skyler na mjukuu wake Harrison wakarudi ndani.

    “Hapa kazi kubwa iliyobaki ni kumfuata mama yako nyumbani kwao, naamini akikuona atabadilisha uamuzi wake na kukubali kuishi tena na mimi,” alisema Dk Lewis, bila kupoteza muda wakaanza kujiandaa tayari kwa safari ya kuelekea Wisconsin, nyumbani kwa wazazi wa Suzan.



    Walitoka hadi nje na kuingia ndani ya gari la Dk Lewis, safari ikaanza. Dk Lewis alikuwa makini kwenye usukani, kila mmoja akawa kimya ndani ya gari isipokuwa Harrison ambaye alikuwa akiendelea kucheza na midoli iliyokuwa ndani ya gari lile.

    Baada ya muda, waliwasili nyumbani kwa wazazi wa mama Skyler, wakapokelewa kwa ukarimu huku kila mmoja akimshangaa



    Skyler na mwanaye. Waliambiwa kuwa mama Skyler alikuwa bado hajarudi kutoka kazini ingawa huo ndiyo ulikuwa muda wake.

    “Sasa hivi atakuja, wala msiwe na wasiwasi, alisema mama mwenye nyumba na kuungwa mkono na mumewe ambao kwa pamoja umri ulikuwa umewatupa. Dk Lewis akaanza kueleza kilichomkuta Skyler na jinsi walivyokutana upya baada ya kupotezana kwa kipindi kirefu.

    Akiwa anaendelea kusimulia, wote walisikia honi ya gari kutoka getini.



    “Huyo anakuja,” alisema bibi yake Skyler huku akitoka mbiombio kwenda kumfungulia mwanaye. Geti lilipofunguliwa, Suzan aliingiza gari mpaka eneo la maegesho na kulipaki, akatoka na mkoba wake na kwenda kusalimiana na mama yake.

    “Kuna wageni ndani, sikwambii ni akina nani nataka ukajionee mwenyewe,” alisema huku akimshika mkono Suzan, akaingia naye ndani.



    “Whaaat? Naota au ni kweli? Nooooooo!” alipiga kelele Suzan baada ya kumuona Skyler amembeba mtoto, huku pembeni yake akiwa amekaa mtalaka wake, Dk Lewis. Kutokana na mshtuko mkubwa alioupata, mama Skyler alianguka chini kama mzigo na kupoteza fahamu, wote wakainuka na kukimbilia pale alipokuwa ameangukia, wakaanza kumpepea ili azinduke.



    Licha ya kumpepea kwa muda mrefu, bado hakuzinduka, Skyler na bibi yake wakawa wanalia huku Dk Lewis na babu yake Skyler wakihangaika kumuinua na kumpeleka kwenye gari, tayari kwa safari ya kuelekea hospitali iliyokuwa jirani.

    Muda mfupi baadaye, tayari wote walikuwa ndani ya gari wakielekea hospitali. Dk Lewis ndiyo alikuwa akiendesha huku mkwe wake akiwa amekaa pembeni. Skyler na bibi yake walikuwa wamekaa na mgonjwa wakiendelea kumpepea.



    Baada ya kuwasili hospitali, walipokelewa na wahudumu wachangamfu, Suzan akapandishwa kwenye kitanda cha magurudumu na kukimbizwa wodini.



    “Hana tatizo kubwa, vipimo vinaonesha amepatwa na mshtuko, msijali atakuwa sawa,” alisema daktari aliyekuwa anamhudumia. Akalazwa wodini huku dripu za maji na dawa zikiendelea kutiririka mishipani mwake.

    Baada ya kulazwa kwa zaidi ya saa tatu, Suzan alipiga chafya na kuzinduka, akawa anapepesa macho huku na kule kama anayejiuliza pale ni wapi na amefikaje. Ilibidi watu wote watolewe wodini wakihofia anaweza kupata mshtuko mwingine, akabakia mtu mmoja tu, mama yake.



    “Pole mwanangu, usijali, utapona tu,” alisema mama yake huku akimpapasa shingoni kwa upendo, Suzan akawa bado anavuta kumbukumbu na kujaribu kukumbuka kilichotokea mpaka akawa na hali kama ile.

    “Mama, ni kweli nimemuona Skyler akiwa na mtoto au nilikuwa naota?”

    “Ni kweli mwanangu, mwanao hakufa kama ulivyokuwa unahisi, ni stori ndefu lakini ukweli ni kwamba Skyler amerudi, tena akiwa na mtoto wa kiume.”



    “Ooh! Ahsante Mungu, nilishamhukumu mume wangu bureee! Ningesikiliza ushauri wako huenda mpaka leo tungekuwa tunaishi pamoja.”



    “Wala hakijaharibika kitu, talaka iliyotolewa mahakamani inaweza kubatilishwa kwa wahusika kula viapo na kuthibitisha mahakamani kama mmemaliza tofauti zilizofanya mpeane talaka. Kama upo tayari nitalisimamia hili.”

    “Mi siwezi kusema kitu kwa sababu sijazungumza chochote na mume wangu na sijui kama hakuoa tena baada ya kuachana na mimi.”



    “Mumeo kasema bado anakupenda na ndiyo maana ameamua kumleta Skyler na mwanaye ili uwaone na kubatilisha uamuzi wako. Ukipona utamsikia mwenyewe akisema kuwa bado anakuhitaji,” alisema mama Suzan huku akiendelea kumpapasa mwanaye shingoni.

    ***



    Baada ya kurushwa dirishani na mama yake, muda mfupi kabla ajali haijatokea, huku akiwa amevaa parachuti, Charlotte alipulizwa na upepo mkali na kupelekwa upande wa Magharibi ya msitu wa Tongass, mbali kabisa kutoka eneo ilipotokea ajali ya ndege ya Herpa Lufthansa Premium.



    Aliendelea kuelea angani kwa saa nyingi, sauti ikamkauka kutokana na kulia kwa muda mrefu na kupulizwa na upepo mkali ulioambatana na ukungu mzito. Kutokana na umri wake mdogo, tena akiwa hajazoea kukaa kwenye baridi kali, Charlotte alipoteza fahamu akiwa angani, hakuelewa tena kilichoendelea.



    Alikuja kushtuka saa nyingi baadaye na kujikuta akiwa amelala kwenye nyasi ndefu, huku parachuti lake likiwa limeanguka mita chache kutoka pale alipokuwa. Licha ya umri wake mdogo, Charlotte alisimama na kujifikicha macho, akajivua kamba za parachuti na kukaa pembeni, akawa analia huku akimtaja mama yake.



    Akiwa anaendelea kulia, alisikia sauti za wanyama wa porini ambao hakuwatambua, zile sauti zikawa zinazidi kusogea huku nyasi na vichaka vilivyokuwa jirani na pale alipokuwa amesimama, vikitingishika. Alijaribu kuinua shingo yake ili aone ni wanyama gani



    lakini hakufanikiwa kuona chochote kutokana na ufupi wake. Zile sauti zilizidi kusogea, vichaka vikawa vinazidi kutingishika, mara akajikuta amezungukwa na wanyama ambao kutokana na umri wake mdogo, hakuweza kuwatambua.



    BAADA ya kutengana kwa miaka kadhaa kutokana na kupotea kwa mtoto wao wa kipekee, Skyler, hatimaye Dk Lewis na Suzan wanakutana na kuanza kupanga mikakati ya kuijenga upya familia yao. Kupatikana kwa



    Skyler, tena akiwa na mtoto aliyekuwa akifanana kwa kiasi kikubwa na marehemu baba yake, Harvey kunaonekana kuwa faraja kubwa kwa wote.



    Mama Skyler ambaye awali alipatwa na mshtuko uliosababisha apoteze fahamu baada ya kumuona mwanaye katika mazingira ambayo hakuyategemea, anapelekwa hospitali na baada ya muda anapata

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    nafuu na kurudishwa nyumbani. Mwanaye anamsimulia kila kitu kilichotokea baada ya kuondoka nyumbani.

    Wanaombana radhi na sasa wanakubaliana kufungua ukurasa mpya wa maisha yao. Suzan anakubaliana na Dk Lewis kwenda kuvunja talaka mahakamani na kula kiapo kipya cha kuishi pamoja kama mume na mke.



    KWA kutumia gari la Dk Lewis, walisafiri mpaka kwenye Mahakama ya Miami County High Court na kwenda moja kwa moja kwenye kitengo cha viapo. Wakaeleza shida yao ambapo karani waliyemkuta aliwaelekeza kwenda chumba namba 7113.



    “Karibuni sana, niwasaidie nini?”aliuliza mwanamke wa makamo aliyekuwa amekaa nyuma ya meza kubwa ya mapokezi.

    “Mimi na mwenzangu tulipeana talaka lakini sasa tumeamua kurudiana,” alisema Dk Lewis huku akimpapasa Suzan mgongoni kimahaba.



    Yule mwanamke aliwatazama mmoja baada ya mwingine kisha akawaelekeza kwenye ofisi ya Jaji Valentine Powell aliyekuwa akishughulika na viapo vya ndoa, talaka na kadhalika.

    Waliongozana na baada ya muda mfupi waliingia ndani ya ofisi hiyo, wakapokelewa na mwanaume mzee mwenye mvi nyingi kichwani. Dk Lewis akaanza kueleza kilichowapeleka.



    “Kitu gani kilichosababisha muachane na sasa kitu gani kinachowafanya mtake kurudiana?”

    “Tulikuwa na matatizo ya kifamilia lakini tayari tumeshayamaliza na hayawezi kujirudia tena,” alisema Dk Lewis kwa kujiamini.

    “Kwa kawaida ili kuvunja talaka inabidi mle kiapo mbele ya mashahidi halafu baada ya hapo mtakula kiapo kingine cha ndoa ya mkataba.”

    “Ndoa ya mkataba?”aliuliza Suzan kwa mshangao.



    “Ndiyo, mkishapeana talaka sheria ya ndoa inasema mkirudiana inabidi ndoa yenu iwe ya mkataba na mtakuwa mkiuongeza kwa kadiri mtakavyokuwa mnaishi kwa maelewano,” alijibu Jaji Powell, Suzan na Dk Lewis wakatazamana kwa sekunde kadhaa kisha wakatingisha vichwa vyao kuonesha kuwa wameridhia.



    Walitoka kwenda kutafuta wadhamini na baada ya muda wakarudi na kula kiapo cha kuvunja talaka, wakapewa fomu maalum ya kusaini wao na wadhamini wao. Walipomaliza walipewa fomu nyingine ya ndoa ya mkataba, Jaji Powell akawaongoza kula kiapo kisha wakasaini kwenye zile fomu.



    “Sasa mmehalalishwa kuwa mke na mume kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1972, kipengele kidogo cha 3b,” alisema Jaji Powell.



    Baada ya shughuli ile, Suzan alimrukia Dk Lewis, wakagonganisha ndimi zao na kuanza kuelea kwenye ulimwengu wa mahaba. Walikaa kwenye hali ile kwa zaidi ya dakika mbili, wakaachiana na kuanza kutazamana kama majogoo yanayotaka kupigana.



    “Siamini macho yangu kama umerudi kwenye mikono yangu,”alisema Dk Lewis huku akilengwalengwa na machozi.

    “Mimi mwenyewe siamini, naahidi nitalilinda penzi lako mpaka siku nafukiwa kaburini, tusahau yote yaliyopita na tufungue ukurasa mpya,” alijibu Suzan huku naye akitokwa na machozi ya furaha. Akatoka huku wakiwa wamekumbatiana mpaka kwenye gari lao.



    Safari ya kurudi nyumbani kwa Dk Lewis ilianza na baada ya muda wakawa tayari wameshawasili. Walipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani wakajifungia.



    Baada ya kukaa chumbani kwa saa nyingi wakiwa peke yao, baadaye walitoka wakiwa wamechoka na kuingia ndani ya gari, wakaondoka na kurejea nyumbani kwa wazazi wa Suzan ambapo waliwakuta wote wakiwasubiri kwa hamu.



    “Vipi mmefikia wapi?” aliuliza mama Suzan, mwanaye akamjibu kuwa kila kitu kimeenda kama kilivyopangwa na tayari wameshakuwa mume na mke halali. Kila mmoja akashangilia kwa nguvu, wakawakumbatia na kuanza kuimba nyimbo za furaha. Shangwe ziliendelea mpaka usiku sana.



    Wakaruhusiwa kuondoka pamoja lakini Skyler na mwanaye Harrison wakalazimika kubaki palepale. Kesho yake kulifanyika sherehe ndogo ya kuwapongeza, wakafungua ukurasa mpya wa maisha ya ndoa.



    Sherehe ilipoisha, waliwachukua Skyler na mwanaye Harrison na kurudi nao mpaka pale Dk Lewis alipokuwa anaishi.

    Kwa kuwa nyumba ilikuwa ndogo, walikubaliana kwenda kuikarabati nyumba yao waliyokuwa wanaishi kabla hawajatengana. Mafundi wakatafutwa ambapo kazi ya ukarabati ilianza haraka. Madirisha na milango ambavyo vilikuwa vimeharibika vikarudishiwa upya, kuta za ndani na nje zikapakwa rangi na kuifanya nyumba ionekane mpya.



    Dk Lewis aliomba likizo ya dharura kazini kwao, mama Skyler naye akafanya hivyohivyo, siku chache baadaye wakahamia kwenye makazi mapya na kuyaanza maisha ya kifamilia, safari hii wakiwa na mtu aliyeongezeka, Harrison.



    Kwa kuwa Harrison tayari alikuwa ameanza masomo ya chekechea wakiwa nyumbani kwa Bill na mkewe, ilibidi taratibu zifanyike za kumhamishia jirani na pale nyumbani kwao, akaendelea na masomo kwenye shule ya Miami Kindergaten.



    “Sikuwahi kutegemea kuwa familia yangu inaweza kurudi na kuungana pamoja kama hivi, namuomba Mungu hii furaha tuliyonayo iendelee miaka yote,” alisema Dk Lewis jioni moja wakati wakipata chakula cha usiku.



    “Hata mimi sikutegemea mume wangu, naamini sote tumejifunza jambo kwa haya yaliyotokea,” alisema Suzan, wakaendelea kula chakula cha usiku.



    Siku zilizidi kusonga mbele, maisha yao yakazidi kutawaliwa na amani, upendo na furaha. Baada ya muda, likizo zao ziliisha, wakalazimika kurudi kazini huku Skyler akibaki nyumbani. Harrison akawa anazidi kukua huku akili yake nayo ikipevuka kutokana na masomo ya chekechea aliyokuwa anafundishwa.

    “Mume wangu, mi nilikuwa na wazo.”

    “Wazo gani mke wangu kipenzi?”



    “Huyu Skyler mi sifurahishwi na yeye kuendelea kukaa nyumbani. Kwa nini tusimtafutie shule ili aendelee na masomo yake?”

    “Hata mimi nilikuwa nawaza hivyo mke wangu, nafikiri ni jambo la msingi sana. Ila umeshazungumza naye na kumsikia anasemaje?”

    “Hapana, lakini kwa sababu wote tupo, nafikiri huu ndiyo muda muafaka wa kumuita na kumuuliza,” alisema Suzan, akainuka na



    kwenda kumuita Skyler aliyekuwa akiendelea kucheza na mwanaye Harrison. Walikaa naye na kumweleza walichokuwa wamekiamua, naye akaonesha kufurahishwa sana na uamuzi ule wa wazazi wake.



    “Nataka niendelee na masomo ya sekondari kuanzia pale nilipokuwa nimeishia, bado nina ndoto kubwa kwenye maisha yangu na elimu pekee ndiyo itakayonifanya niweze kuzitimiza,” alisema Skyler huku akionesha kufurahishwa sana na uamuzi ule.



    Taratibu za kumrudisha shuleni zilifanyika, akatafutiwa shule ya kulipia, tofauti na ile aliyokuwa anasoma awali. Baada ya wiki kadhaa, akaendelea na masomo ya sekondari, safari hii akiwa na uchungu na elimu kuliko kawaida. Harrison naye aliendelea na masomo na baada ya miezi kadhaa, aliandikishwa kuanza darasa la kwanza.

    ***



    Charlotte aliendelea kupiga kelele na kumuita mama yake lakini hakuna mtu aliyemsikiliza, wale wanyama wakamzunguka na kuanza kumshangaa. Waliendelea kumzunguka lakini hawakumdhuru, baada ya kumshangaa kwa muda mrefu, mnyama mmoja aliyeonekana kuwa mkubwa kuliko wengine alimshika Charlotte kama afanyavyo mama kwa mwanaye na kumuweka mgongoni.



    Wakaondoka kundi zima na kutokomea ndani kabisa ya Msitu wa Tongass, wakawa wanaruka kwenye matawi ya miti huku mnyama yule mkubwa akiwa makini kuzuia Charlotte asidondoke.



    Licha ya awali kujawa na hofu juu ya usalama wake, taratibu Charlotte alianza kuwazoea wale wanyama, ile hofu aliyokuwa nayo ikaisha hasa baada ya kugundua kuwa wanyama wale hawakuwa na lengo la kumdhuru. Akaanza kuzoea kushinda nao, siku zote akiwekwa katikati yao, akilishwa mizizi na matunda ya porini kama wao walivyokuwa wanakula.



    Kilichomtesa ni kwamba hawakuwa na nyumba au pango la kujisitiri wakati wa mvua au baridi kali, akawa anateseka lakini taratibu alianza pia kuzoea hali ile. Akaanza kujifunza kuruka kwenye matawi ya miti kama viumbe wale, akaanza kujiona kama hana tofauti yoyote. Hayo ndiyo yakawa maisha yake mapya.



    Siku zilizidi kusonga mbele, Charlotte akawa anazidi kukua huku haiba na tabia za kibinadamu zikitoweka kwenye maisha yake na kuishi kama wale wanyama. Kilichompa faraja ni kwamba kila kulipotokea hatari yoyote, wale wanyama walikuwa wakimthamini yeye kuliko kitu kingine chochote. Akawa anazidi kuwa mkubwa.



    HAKUNA marefu yasiyo na ncha, walinena wahenga. Baada ya familia ya Dk Lewis kuvurugika hadi kufikia hatua ya daktari huyo kupeana talaka na mkewe kutokana na kupotea katika mazingira ya kutatanisha kwa



    mtoto wao wa kipekee, Skyler, hatimaye mambo yanatulia.

    Baada ya Skyler kupatikana, tena akiwa na mtoto Harrison aliyefanana kwa kiasi kikubwa na marehemu

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    baba yake, Harvey, Dk Lewis anamfuata Suzan aliyekuwa anaishi na wazazi wake baada ya kupeana talaka. Suzan anashtuka mno baada ya kumuona Skyler na anapoteza fahamu kwa muda. Baada ya kupewa huduma ya kwanza anarejea kwenye hali yake ya kawaida.



    Baadaye wanaenda mahakamani na Dk Lewis kuvunja talaka waliyopeana. Zoezi hilo linakamilika ambapo familia inaungana upya na kufungua ukurasa mpya.



    MAISHA yalizidi kusonga mbele, Skyler akaendelea na masomo huku akizidisha juhudi kuliko ilivyokuwa awali. Mwanaye naye alizidi kukua, akawa



    mchangamfu, hali iliyozidi kuleta faraja ndani ya nyumba ya Dk Lewis.

    “Unataka ukiwa mkubwa usomee nini mwanangu?”

    “Nataka kusomea tabia za wanyama.”

    “Kuna somo linaitwa tabia za wanyama?”



    “Aah, nimekosea mama, nataka kuwa mtaalam wa Bailojia, kipengele cha Zoology, mwalimu ametufundisha kuwa Zoology ni sehemu ya Bailojia lakini yenyewe inazungumzia zaidi wanyama.”



    “Mh! Yaani wewe ndiyo huna akili kabisa, badala ya kuchagua masomo yanayoendana na ulimwengu wa kisasa kama Teknolojia ya Mawasiliano (IT) au ufundi wa kompyuta (Computer Science) kama mimi mama yako wewe unataka kusomea mambo ya wanyama, kwa hiyo utakuwa unaishi porini?”



    Unakosea Skyler, hata wewe tulikupa nafasi ya kuchagua masomo unayoyataka na ndiyo maana muda si mrefu utakuwa mtaalam wa IT mwenye sifa na vigezo vyote, usimlazimishe mjukuu wangu awe kama wewe, mpe anachokitaka,” mama Skyler alilazimika kuingilia kati mazungumzo ya mwanaye na mjukuu wake, Harrison.



    “Mama, yaani na wewe unakubali mjukuu wako aje kuwa daktari wa wanyama? Nimemzaa ili aje kuwa shujaa hapa duniani, siyo mtaalam wa wanyama!”



    “Anaweza kuwa shujaa hata kwa kusomea Ethology (somo la tabia za wanyama), cha msingi ni kumsikiliza anachokitaka na kumsaidia atimize malengo yake, tena anaonesha somo la Baiolojia analiweza sana, si unaona matokeo yake yanavyoridhisha?”

    “Hapana mama, sipo tayari kuona hilo linatokea, lazima asomee masomo ambayo atapata kazi na mafanikio kwa urahisi,” alisema Skyler, kauli ambayo haikuwafurahisha mwanaye Harrison na bibi yake.



    Licha ya Skyler kuonekana kumpinga, bado Harrison ambaye alikuwa akizidi kukua kwa kasi, alishikilia msimamo wake kuwa anataka kusomea masomo hayo.



    Maisha yalizidi kusonga mbele, miaka miwili baadaye Skyler akahitimu masomo ya sekondari na kuendelea na elimu ya juu ambapo alijiunga na Chuo cha Teknolojia cha Oregon alikosomea Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Information and Communication Technology).

    Harrison naye aliendelea na masomo ya shule ya msingi, akazidi kukua kimwili na kiakili huku malezi mazuri aliyoyapata kutoka kwa mama yake pamoja na bibi na babu yake, yakimjengea uwezo mkubwa wa kujiamini.



    Japokuwa awali mama yake, Skyler alikuwa hataki Harrison asomee elimu ya viumbe hai na tabia za wanyama, baada ya kuona mwanaye anazidi kuyakazania masomo hayo, huku matokeo ya kila mtihani akifaulu kwa alama za juu, ilibidi akubaliane na hali halisi. Akamruhusu kwa moyo mkunjufu aendelee huku akimpa msaada wa kila alichokuwa anakihitaji.



    Skyler baada ya kumaliza masomo yake, alipata ajira kwenye Kampuni ya Microsoft Limited, tawi la Miami ambapo alikuwa akifanya kazi kwenye kitengo cha ICT. Akawa analipwa mshahara mzuri uliomfanya auchukue mzigo wa kugharamia masomo ya mwanaye Harrison kutoka kwa wazazi wake.



    Akawa anamlipia ada mwanaye na kumnunulia vitabu ikiwa ni pamoja na kumtafutia twisheni ya masomo aliyokuwa anayapenda. Fedha nyingine alimfungulia akaunti benki, ikawa kila mwisho wa mwezi anaenda kumuwekea akiba ya kumsaidia siku za baadaye.

    ***

    MIAKA 15 BAADAYE

    Harrison aliendelea vizuri na masomo yake, akahitimu shule ya msingi na kujiunga na Shule ya Sekondari ya Miami Academy, akasoma kwa miaka minne akiwa amechagua mchepuo wa masomo ya sayansi na kuhitimu kwa mafanikio, akapata alama za juu na kuwa miongoni mwa wanafunzi kumi bora.



    Kutokana na kufaulu vizuri, hususan masomo ya Botany na Zoology, Harrison alipata nafasi ya kuendelea na masomo ya juu, akajiunga na chuo cha Michigan State University, School of Ethology. Akiwa chuoni hapo, alisomea Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Zoolojia (Bachelor Degree of Science in Zoology).



    Mwaka wa kwanza uliisha, matokeo ya mwisho wa mwaka yalipotoka, Harrison alifaulu vizuri, hali iliyofanya wanachuo wenzake pamoja na wakufunzi kuanza kuulizana juu ya mwanachuo huyo kwani wengi walikuwa hawamjui.



    “Unamjua bwana, ni mkimya sana na anapenda kukaa nyuma kabisa. Ukimuona utasema haongei lakini ana utundu wa chinichini huyo!”

    “Mpenzi wake ni nani?”



    “Mh! Sijawahi kumuona na msichana, muda mwingi yupo bize na masomo, anapenda kubeba vitabu vikubwavikubwa vya Baiolojia,” wanachuo wawili walikuwa wakijadiliana pembeni ya ubao wa matangazo, baada ya kuona jina la Harrison Harvey likiwa la kwanza kwenye matokeo ya mtihani wa mwisho wa mwaka chuoni pale.



    Habari zake ziliendelea kusambaa, watu wengi wakawa na hamu ya kumjua na kwa kadiri siku zilivyozidi kusonga mbele, akapata marafiki wengi, wa kike na wa kiume. Likizo alirudi nyumbani kwao, akapokelewa kwa shangwe na mama yake, babu na bibi yake ambao walimuandalia sherehe ndogo ya kumpongeza kwa kufaulu vizuri masomo yake.



    “Umeamini sasa kwamba kila mtu na kipaji chake? Ungemlazimisha asomee masomo kama ya kwako, ungempoteza Harrison, tazama anaongoza chuo kizima.”



    “Mh! Unayoyasema mama ni ya kweli, siamini kama mwanangu anaweza kuongoza kwa matokeo ya mwaka mzima, tena kwa chuo kama Michigan State kilichojaa watu wenye vipaji kutoka sehemu mbalimbali!” Skyler na mama yake walikuwa wakijadiliana wakati wakiwa jikoni kuandaa chakula cha jioni.



    Harrison na babu yake walikuwa wakitazama runinga sebuleni, wakawa wanaelekezana mambo kadhaa yaliyokuwa yanaoneshwa kwenye kituo cha runinga cha Discovery walichokuwa wanatazama.



    “Mto Amazon ni wa pili kwa urefu duniani, umeanzia Brazil na unakatiza nchi nyingi mpaka kwenye Bahari ya Pacific unakomwaga maji, unafahamu nini kuhusu Amazon?” aliuliza Dk Lewis.



    “Karibu theluthi moja ya viumbe vyote duniani, wanyama wa porini, ndege, samaki na wengineo, wanaishi kwenye misitu minene inayozunguka mtu huo.”



    “Ni kweli kabisa, inaoesha upo makini sana na masomo yako. Unafahamu kuhusu nyoka wakubwa waitwao Anaconda wanaopatikana kwenye mto huo?”



    “Ndiyo babu, Anaconda ndiyo nyoka wakubwa kuliko wote duniani na wanapatikana kwenye Mto Amazon pekee. Maisha yao yote huishi kwenye maji na huacha vichwa vyao vikielea juu ya maji wanapowinda.”

    “Vipi kuhusu pomboo wakubwa wa Amazon?”



    “Ahaaa, unazungumzia kuhusu samaki aina ya dolphin? Wapo tena wakubwa haswaa! Tofauti na dolphin wa baharini, wale wa Amazon huwa wanabadilika rangi, wakiwa wadogo huwa na rangi ya kijivu, baadaye huwa na rangi ya pinki na wakikomaa hubadilika na kuwa weupe.



    “Pia naujua msitu wa Tongass na viumbe wote waliomo ndani yake, kuna sokwe wakubwa, ndege, swala na wanyama kibao,” alijibu Harrison, babu yake akawa anakuna kipara chake kwani mjukuu wake alikuwa na uelewa mkubwa sana wa viumbe hai na mazingira.





    BAADA ya kutengana kwa miaka kadhaa kutokana na kupotea kwa mtoto wao wa kipekee, Skyler, hatimaye Dk Lewis na Suzan wanakutana na kuanza kupanga mikakati ya kuijenga upya familia yao.



    Kupatikana kwa Skyler, tena akiwa na mtoto aliyekuwa akifanana kwa kiasi kikubwa na marehemu baba yake, Harvey kunaonekana kuwa faraja kubwa kwa wote.

    Mama Skyler ambaye awali alipatwa na mshtuko uliosababisha apoteze fahamu baada ya kumuona



    mwanaye katika mazingira ambayo hakuyategemea, anapelekwa hospitali na baada ya muda anapata nafuu na kurudishwa nyumbani. Mwanaye anamsimulia kila kitu kilichotokea baada ya kuondoka nyumbani.



    Wanaombana radhi na sasa wanakubaliana kufungua ukurasa mpya wa maisha yao. Suzan anakubaliana na Dk Lewis kwenda kuvunja talaka mahakamani na kula kiapo kipya cha kuishi pamoja kama mume na mke.



    KWA kutumia gari la Dk Lewis, walisafiri mpaka kwenye Mahakama ya Miami County High Court na kwenda moja kwa moja kwenye kitengo cha viapo. Wakaeleza shida yao ambapo karani waliyemkuta aliwaelekeza kwenda chumba namba 7113.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Karibuni sana, niwasaidie nini?”aliuliza mwanamke wa makamo aliyekuwa amekaa nyuma ya meza kubwa ya mapokezi.

    “Mimi na mwenzangu tulipeana talaka lakini sasa tumeamua kurudiana,” alisema Dk Lewis huku akimpapasa Suzan mgongoni kimahaba.



    Yule mwanamke aliwatazama mmoja baada ya mwingine kisha akawaelekeza kwenye ofisi ya Jaji Valentine Powell aliyekuwa akishughulika na viapo vya ndoa, talaka na kadhalika.



    Waliongozana na baada ya muda mfupi waliingia ndani ya ofisi hiyo, wakapokelewa na mwanaume mzee mwenye mvi nyingi kichwani. Dk Lewis akaanza kueleza kilichowapeleka.



    “Kitu gani kilichosababisha muachane na sasa kitu gani kinachowafanya mtake kurudiana?”

    “Tulikuwa na matatizo ya kifamilia lakini tayari tumeshayamaliza na hayawezi kujirudia tena,” alisema Dk Lewis kwa kujiamini.



    “Kwa kawaida ili kuvunja talaka inabidi mle kiapo mbele ya mashahidi halafu baada ya hapo mtakula kiapo kingine cha ndoa ya mkataba.”

    “Ndoa ya mkataba?”aliuliza Suzan kwa mshangao.



    “Ndiyo, mkishapeana talaka sheria ya ndoa inasema mkirudiana inabidi ndoa yenu iwe ya mkataba na mtakuwa mkiuongeza kwa kadiri mtakavyokuwa mnaishi kwa maelewano,” alijibu Jaji Powell, Suzan na Dk Lewis wakatazamana kwa sekunde kadhaa kisha wakatingisha vichwa vyao kuonesha kuwa wameridhia.



    Walitoka kwenda kutafuta wadhamini na baada ya muda wakarudi na kula kiapo cha kuvunja talaka, wakapewa fomu maalum ya kusaini wao na wadhamini wao. Walipomaliza walipewa fomu nyingine ya ndoa ya mkataba, Jaji Powell akawaongoza kula kiapo kisha wakasaini kwenye zile fomu.



    “Sasa mmehalalishwa kuwa mke na mume kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1972, kipengele kidogo cha 3b,” alisema Jaji Powell.



    Baada ya shughuli ile, Suzan alimrukia Dk Lewis, wakagonganisha ndimi zao na kuanza kuelea kwenye ulimwengu wa mahaba. Walikaa kwenye hali ile kwa zaidi ya dakika mbili, wakaachiana na kuanza kutazamana kama majogoo yanayotaka kupigana.



    “Siamini macho yangu kama umerudi kwenye mikono yangu,”alisema Dk Lewis huku akilengwalengwa na machozi.

    “Mimi mwenyewe siamini, naahidi nitalilinda penzi lako mpaka siku nafukiwa kaburini, tusahau yote yaliyopita na tufungue ukurasa mpya,” alijibu Suzan huku naye akitokwa na machozi ya furaha. Akatoka huku wakiwa wamekumbatiana mpaka kwenye gari lao.



    Safari ya kurudi nyumbani kwa Dk Lewis ilianza na baada ya muda wakawa tayari wameshawasili. Walipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani wakajifungia.



    Baada ya kukaa chumbani kwa saa nyingi wakiwa peke yao, baadaye walitoka wakiwa wamechoka na kuingia ndani ya gari, wakaondoka na kurejea nyumbani kwa wazazi wa Suzan ambapo waliwakuta wote wakiwasubiri kwa hamu.



    “Vipi mmefikia wapi?” aliuliza mama Suzan, mwanaye akamjibu kuwa kila kitu kimeenda kama kilivyopangwa na tayari wameshakuwa mume na mke halali. Kila mmoja akashangilia kwa nguvu, wakawakumbatia na kuanza kuimba nyimbo za furaha. Shangwe ziliendelea mpaka usiku sana.



    Wakaruhusiwa kuondoka pamoja lakini Skyler na mwanaye Harrison wakalazimika kubaki palepale. Kesho yake kulifanyika sherehe ndogo ya kuwapongeza, wakafungua ukurasa mpya wa maisha ya ndoa.



    Sherehe ilipoisha, waliwachukua Skyler na mwanaye Harrison na kurudi nao mpaka pale Dk Lewis alipokuwa anaishi.

    Kwa kuwa nyumba ilikuwa ndogo, walikubaliana kwenda kuikarabati nyumba yao waliyokuwa wanaishi kabla



    hawajatengana. Mafundi wakatafutwa ambapo kazi ya ukarabati ilianza haraka. Madirisha na milango ambavyo vilikuwa vimeharibika vikarudishiwa upya, kuta za ndani na nje zikapakwa rangi na kuifanya nyumba ionekane mpya.



    Dk Lewis aliomba likizo ya dharura kazini kwao, mama Skyler naye akafanya hivyohivyo, siku chache baadaye wakahamia kwenye makazi mapya na kuyaanza maisha ya kifamilia, safari hii wakiwa na mtu aliyeongezeka, Harrison.



    Kwa kuwa Harrison tayari alikuwa ameanza masomo ya chekechea wakiwa nyumbani kwa Bill na mkewe, ilibidi taratibu zifanyike za kumhamishia jirani na pale nyumbani kwao, akaendelea na masomo kwenye shule ya Miami Kindergaten.



    “Sikuwahi kutegemea kuwa familia yangu inaweza kurudi na kuungana pamoja kama hivi, namuomba Mungu hii furaha tuliyonayo iendelee miaka yote,” alisema Dk Lewis jioni moja wakati wakipata chakula cha usiku.



    “Hata mimi sikutegemea mume wangu, naamini sote tumejifunza jambo kwa haya yaliyotokea,” alisema Suzan, wakaendelea kula chakula cha usiku.



    Siku zilizidi kusonga mbele, maisha yao yakazidi kutawaliwa na amani, upendo na furaha. Baada ya muda, likizo zao ziliisha, wakalazimika kurudi kazini huku Skyler akibaki nyumbani. Harrison akawa anazidi kukua huku akili yake nayo ikipevuka kutokana na masomo ya chekechea aliyokuwa anafundishwa.



    “Mume wangu, mi nilikuwa na wazo.”

    “Wazo gani mke wangu kipenzi?”



    “Huyu Skyler mi sifurahishwi na yeye kuendelea kukaa nyumbani. Kwa nini tusimtafutie shule ili aendelee na masomo yake?”



    “Hata mimi nilikuwa nawaza hivyo mke wangu, nafikiri ni jambo la msingi sana. Ila umeshazungumza naye na kumsikia anasemaje?”



    “Hapana, lakini kwa sababu wote tupo, nafikiri huu ndiyo muda muafaka wa kumuita na kumuuliza,” alisema Suzan, akainuka na kwenda kumuita Skyler aliyekuwa akiendelea kucheza na mwanaye Harrison. Walikaa naye na kumweleza walichokuwa wamekiamua, naye akaonesha kufurahishwa sana na uamuzi ule wa wazazi wake.



    “Nataka niendelee na masomo ya sekondari kuanzia pale nilipokuwa nimeishia, bado nina ndoto kubwa kwenye maisha yangu na elimu pekee ndiyo itakayonifanya niweze kuzitimiza,” alisema Skyler huku akionesha kufurahishwa sana na uamuzi ule.



    Taratibu za kumrudisha shuleni zilifanyika, akatafutiwa shule ya kulipia, tofauti na ile aliyokuwa anasoma awali. Baada ya wiki kadhaa, akaendelea na masomo ya sekondari, safari hii akiwa na uchungu na elimu kuliko kawaida. Harrison naye aliendelea na masomo na baada ya miezi kadhaa, aliandikishwa kuanza darasa la kwanza.

    ***



    Charlotte aliendelea kupiga kelele na kumuita mama yake lakini hakuna mtu aliyemsikiliza, wale wanyama wakamzunguka na kuanza kumshangaa. Waliendelea kumzunguka lakini hawakumdhuru, baada ya kumshangaa kwa muda mrefu, mnyama mmoja aliyeonekana kuwa mkubwa kuliko wengine alimshika Charlotte kama afanyavyo mama kwa mwanaye na kumuweka mgongoni.



    Wakaondoka kundi zima na kutokomea ndani kabisa ya Msitu wa Tongass, wakawa wanaruka kwenye matawi ya miti huku mnyama yule mkubwa akiwa makini kuzuia Charlotte asidondoke.



    Licha ya awali kujawa na hofu juu ya usalama wake, taratibu Charlotte alianza kuwazoea wale wanyama, ile hofu aliyokuwa nayo ikaisha hasa baada ya kugundua kuwa wanyama wale hawakuwa na lengo la kumdhuru. Akaanza kuzoea kushinda nao, siku zote akiwekwa katikati yao, akilishwa mizizi na matunda ya porini kama wao walivyokuwa wanakula.



    Kilichomtesa ni kwamba hawakuwa na nyumba au pango la kujisitiri wakati wa mvua au baridi kali, akawa anateseka lakini taratibu alianza pia kuzoea hali ile. Akaanza kujifunza kuruka kwenye matawi ya miti kama viumbe wale, akaanza kujiona kama hana tofauti yoyote. Hayo ndiyo yakawa maisha yake mapya.



    Siku zilizidi kusonga mbele, Charlotte akawa anazidi kukua huku haiba na tabia za kibinadamu zikitoweka kwenye maisha yake na kuishi kama wale wanyama. Kilichompa faraja ni kwamba kila kulipotokea hatari yoyote, wale wanyama walikuwa wakimthamini yeye kuliko kitu kingine chochote. Akawa anazidi kuwa mkubwa.



    MAISHA ya familia ya Dk Lewis yanarudi kwenye mstari na anafanikiwa kuiunganisha upya familia yake kufuatia kupatikana kwa mtoto wake wa kipekee, Skyler ambaye alitoweka kipindi kirefu kilichopita. Skyler



    anakuja na mtoto wa kiume, Harrison ambaye amefanana vitu vingi na marehemu baba yake.

    Siku zinasonga mbele kwa kasi na Harrison anazidi kuwa mkubwa. Anamaliza elimu ya msingi na kuanza shule ya sekondari anakohitimu kidato cha nne. Baadaye anajiunga na chuo cha Michigan State University



    anakosomea masomo ya tabia za wanyama, Ethology. Anahitimu masomo yake na kuwa mtaalamu wa tabia za wanyama.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kuhitimu masomo, anaenda kufanya utafiti kwenye msitu wa Tongass, lengo lake likiwa ni kujua mambo mbalimbali yahusuyo wanyama, hususan sokwe wengi wanaopatikana kwenye msitu huo mkubwa.



    ILIBIDI akajibanze kwenye mti mkubwa na kuangalia ni wanyama gani, macho yake yakatua kwenye kundi kubwa la sokwe wakubwa waliokuwa wanaruka kutoka tawi moja kwenda jingine kwa kasi kubwa, wakawa wanaelekea pale alipokuwa amejibanza.



    Kelele zilizidi kuongezeka, utulivu uliokuwepo ndani ya msitu ule ukatoweka, Harrison akazidi kujibanza pale kwenye mti huku bastola yake iliyokuwa inatumia risasi za mpira ikiwa mkononi, tayari kwa kujihami endapo lolote lingetokea.



    “Mungu wangu, mbona wakubwa hivi? Halafu mbona wengi kiasi hiki?” alijiuliza Harrison huku akiichukua kamera yake kwenye begi kwa mkono mmoja, akakaa vizuri na kuanza kupiga picha kwa mbali. Alipiga picha kadhaa, akawa anaendelea kushangaa jinsi sokwe wale walivyokuwa wakubwa na wengi.



    Kundi lile la masokwe lilipotoweka, alishusha pumzi ndefu na kuweka vifaa vyake vizuri. Ilibidi arudi kwenye hema lake, akaenda kuweka kumbukumbu za alichokiona. Akawa anaandika baadhi ya mambo kwenye kijitabu chake cha kumbukumbu.



    Siku zilizidi kuyoyoma Harrison akiwa bado ndani ya msitu wa Tongass, kila siku akawa anaendelea na kazi ya utafiti juu ya tabia za masokwe na viumbe wengine katika msitu ule, pamoja na kuchunguza uoto wa asili. Taratibu alianza kuwazoea masokwe wale wakubwa na wa kutisha.



    Tofauti na wanyama wengine, sokwe wa msitu wa Tongass walikuwa wakitembea kwa makundi makubwamakubwa, huku moja likionekana kuwa kubwa zaidi. Kila alipobahatika kuwaona, walikuwa kwenye makundi, wakiruka juu ya matawi ya miti kwa namna ambayo ilimshangaza sana Harrison.



    Baada ya kukaa kwa muda wa wiki mbili ndani ya msitu ule, Harrison aliamua kuondoka na kurejea nyumbani kwao kwenda kufanyia kazi taarifa mbalimbali za kiuchunguzi juu ya tabia za wanyama hususan masokwe wa Msitu wa Tongass alizozipata.



    Alijiandaa kwa kufungasha vitu vyake vyote, akalikunjua hema na kulibana kwa namna ambayo ilikuwa rahisi kubebeka, alipohakikisha amechukua kila kitu, aliianza safari ya kuelekea kwenye ofisi za msitu ule kwa ajili ya kukabidhi baadhi ya vifaa alivyokuwa amepewa.



    “Umefanikiwa?”

    “Nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa na namshukuru Mungu sijapata madhara yoyote.”

    “Unawaonaje masokwe wa Msitu wa Tongass?”



    “Mh! Sijawahi kuona sokwe wakubwa kama hawa, halafu wanatembea kwa makundi makubwa sana, lazima nitarudi tena kwani nadhani ndani ya msitu huu nitajifunza vitu vingi ambavyo awali sikuwa navifahamu.



    “Ngoja nikafanyie kazi hizi data nilizozipata,” alisema Harrison wakati akizungumza na askari wa wanyama pori aliyemkuta kwenye ofisi za msitu ule.



    Baada ya makabidhiano, Harrison alitembea kwa miguu kwa kilometa chache kabla ya kuifikia barabara kuu. Akasimamisha gari na safari ya kurejea nyumbani kwao, Miami ikaanza.



    ”Ooh! Karibu baba, umekuwa mweusi kweli, inaonesha kuna baridi sana huko ulikotoka.”

    “Ahsante sana, kuna baridi kali kwenye Msitu wa Tongass lakini namshukuru Mungu nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa,” alisema Harrison wakati akipokelewa na bibi yake.

    “Mama yupo wapi?”

    “Ameenda kazini lakini muda si mrefu atarudi. Mh! Habari za huko?”



    “Nzuri kabisa mama, nimeifurahia sana safari yangu kwenye Msitu wa Tongass, nimewaona sokwe wakubwa haooo! Yaani hata wewe nikikuonesha picha utashangaa,” alisema Harrison.



    Baada ya kuingia ndani na kupumzika kwa muda, Harrison alienda kuoga na kubadilisha nguo, akachukua kamera zake mbili alizokuwa anazitumia kupigia picha na kwenda kuziunganisha kwenye kompyuta kwa lengo la kuzitoa zile picha na kuzihifadhi vizuri.



    Alichomeka waya maalum kutoka kwenye kamera na kuunganisha kwenye kompyuta, akaanza kutoa picha, zoezi lililomchukua zaidi ya nusu saa. Alipomaliza alianza kuzichunguza vizuri moja baada ya nyingine. Aliendelea na zoezi lile



    huku akizitenganisha katika mafaili mbalimbali, kuanzia zile za mazingira, za uoto wa asili mpaka zile za makundi ya sokwe.

    Wakati akiendelea kuzifuatilia, aligundua jambo ambalo lilimshangaza. Kila alipokuwa akizichunguza kwa makini picha alizopiga makundi yale ya sokwe, aligundua kama kuna kitu katikati yao ambacho hakikuwa kikionekana vizuri.



    Alibaini pia kuwa sokwe wale walikuwa wakitembea kwa mtindo wa kuweka duara, hata walipokuwa wanaruka kutoka mti mmoja kwenda mwingine, katikati kulikuwa na kitu ambacho walionekana kukilinda kwa nguvu kubwa.

    “Hiki ni nini?” alisema Harrison huku akijaribu kuivuta picha karibu kwenye kompyuta, ‘akai-zoom’ mpaka mwisho, hali



    iliyomsaidia kuona vizuri, akagundua kuna kitu kilikuwa katikati ya sokwe wale ingawa hakuelewa mara moja ni kitu gani.

    Aliendelea kufuatilia picha zile kwa muda, akajikuta akisisimka mwili mzima kutokana na kitu alichokuwa anakiona.

    “Lazima nirudi Tongass, nitaenda kufuatilia kwa makini ili nijue ni kitu gani,” alijisemea Harrison huku akiendelea kuzitazama zile picha. Aliifanya kazi ile kwa muda mrefu mpaka muda wa kulala ulipowadia.



    Kesho yake, alfajiri na mapema Harrison aliamka na kuaga kuwa anarudi tena kwenye msitu wa Tongass kuendelea na kazi.

    “Wewe si ulisema utapumzika kidogo? Kinachokufanya uwahi kurudi bila kukaa nasi hata kidogo ni nini?”

    “Mama kuna kazi ya muhimu nilikuwa sijaimalizia, ni muhimu sana,” alisema Harrison bila kutaka kufafanua ni kazi gani.



    Mama yake hakuwa na hiyana, alimruhusu lakini akawa anajiuliza maswali mengi ambayo hayakupata majibu.

    Harrison akasafiri kwa mara nyingine kurudi kwenye msitu wa Tongass. Safari hii hakupanda treni bali alisafiri kwa mabasi, akaunganisha safari mpaka alipofika Tongass.



    “Mbona umerudi tena? Kuna kitu umesahau?” askari wa wanyama pori aliyemuacha jana yake, alimuuliza Harrison, akamweleza kuwa kuna jambo la muhimu alisahau kulifanyia kazi. Hata hivyo, hakumueleza ni jambo gani, akapewa vifaa na kurudi msituni, akaenda kuweka kambi pembeni kidogo ya pale alipokuwa amesimamisha hema lake.



    Kwa kuwa tayari muda ulikuwa umeenda huku uchovu wa kuunganisha safari ukimsumbua, Harrison aliamua kupumzika mpaka kesho yake. Kulipopambazuka tu, aliwahi kuamka na kwenda nje ya hema, akawa anaangaza macho huku na kule akitegemea kuliona tena lile kundi la sokwe.



    Muda ulianza kwenda lakini masokwe hawakutokea, ikabidi aanze kuwatafuta sehemu mbalimbali za msitu ule. Kuna wakati alisikia kelele, akahisi watakuwa ni wenyewe lakini alipofuatilia, alikuta kundi la tai likiufaidi mzoga wa mnyama aliyekuwa amejifia.



    Akaendelea kuzunguka huku na kule, akijipenyeza katikati ya miti iliyokuwa imefungamana ndani ya msitu huo. Baada ya kuhangaika sana bila mafanikio, Harrison aliamua kurudi kwenye hema lake kupumzika. Akiwa mita chache kutoka kwenye hema, alianza kusikia kelele upya, alipoangaza macho yake juu ya miti, aliwaona sokwe wakiruka kwa kasi, akatafuta sehemu na kujibanza, akawa anaangalia kwa makini katikati ya lile kundi.



    Kamera yake nayo ilikuwa mkononi, akiwa tayari kupiga picha endapo angekiona kile kitu alichokuwa anakisubiri. Hata hivyo, kazi haikuwa nyepesi, kila sokwe wale walipokuwa wanaruka, walikuwa wameweka duara huku wakiwa makini kuziba kitu kilichokuwa katikati yao.



    HARRISON aliendelea kusubiri ili aone ni kitu gani kilichokuwa katikati ya kundi lile la masokwe kwa muda mrefu lakini hakufanikiwa. Akiwa bado amejibanza pale pembeni ya mti, alishtukia akipigwa na jiwe mgongoni, akadondoka na kuangusha kamera yake.

    Ghafla alishtukia sokwe mkubwa akiruka kutoka kwenye tawi la mti huku mkononi akiwa ameshika fimbo ndefu, akaanza kumcharaza Harrison



    aliyekuwa bado amelala pale chini. Masokwe wengine wakubwa nao wakawa wanaporomoka kutoka kwenye matawi ya mti na kumzunguka Harrison pale chini huku wakitoa milio ya kutisha.



    Kwa kasi ya ajabu aliiokota kamera yake na kuanza kutimua mbio lakini wale masokwe waliendelea kumkimbiza kwa kasi huku lile kundi lingine likizidi kutokomea ndani kabisa ya Msitu wa Tongass. Alipoona wale masokwe wakubwa wanakaribia kumdhuru alikumbuka kuwa mfukoni alikuwa na bastola inayotumia risasi za mpira.



    Harakaharaka alichomoa ile bastola na kufyatua risasi moja hewani, wale masokwe wakatawanyika na kuanza kukimbilia mahali lile kundi lingine lilipoelekea hiyo ndiyo ikawa ponapona yake. Alitafuta sehemu ya kukaa akawa anajitazama alama za fimbo na jiwe alilopigwa mgongoni.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hawa wanyama ni hatari sana, nisipokuwa makini naweza nikafia huku porini,” alisema Harrison huku akiugulia maumivu aliyokuwa anayapata. Aliikagua kamera yake na kugundua kuwa haikuwa imeharibika, akamshukuru Mungu kimyakimya na kurudi kwenye hema lake kupumzika.

    ***

    “Mume wangu, Harrison ameshakuwa mkubwa sasa. Aina ya kazi aliyoichagua inamfanya ajitenge na binadamu wengine, jambo ambalo linaweza kumsababishia matatizo hapo baadaye.”

    “Ni kweli mke wangu, wataalamu wengi wa mambo ya wanyama pori hujikuta wakiutumia ujana wao mwingi porini wakifanya tafiti mbalimbali matokeo yake hujikuta wanazeeka bila ya kuoa wala kuwa na watoto. Sitaki hali hii imtokee mjukuu wangu.”

    “Kwa mtazamo wako unataka tumsaidiaje?”

    “Mimi nashauri tumtafutie mke wa kuoa.”

    “Hata mimi nilikuwa nawaza hivyohivyo.”



    “Hayo mawazo yenu ya kizee mtayaacha lini? Hakuna mtu mwenye haki ya kumchagulia mume au mke mtu mwingine. Ndoa ni jambo la hiyari, nataka mwanangu aamue mwenyewe,” Skyler aliingilia kati mazungumzo ya wazazi wake.



    Dk Lewis na mkewe walitazamana kwa sekunde kadhaa kisha wakamgeukia Skyler, mama yake akawa anazungumza: “Mwanangu Skyler, wewe umeshakuwa mtu mzima, hata kama hujaolewa najua unafurahi sana kumzaa Harrison na kumlea mpaka hapo alipofikia. Hutaki na yeye aje kuwa na watoto?”



    “Isitoshe mjukuu wangu huyu sijawahi kumuona hata akiwa na rafiki wa kike, akiendelea hivi anaweza asione umuhimu wa kuoa. Ni wajibu wetu kumsaidia,” alikazia Dk Lewis lakini bado Skyler aliendelea kushikilia msimamo wake.



    Mazungumzo yaliendelea kwa muda mrefu, Skyler akawa anasisitiza kuwa mwanaye apewe uhuru wa kujiamulia mambo yake mwenyewe lakini wazazi wake hawakuafikiana naye. Wakajiapiza kuwa ni lazima wamtafutie mjukuu wao mke hasa kwa kuzingatia kuwa alishamaliza masomo yake.

    Skyler alipoona wanang’ang’ania msimamo wao, aliamua kuondoka na kuwaacha peke yao sebuleni.

    ***



    Baada ya siku ile ya kwanza kupita, kesho yake Harrison aliwahi kuamka na kujiandaa kuendelea na kazi yake na akachukua vifaa vyake vyote muhimu na kuingia porini. Alipanga kuendelea kulifuatilia kundi lile la masokwe mpaka ajue ni kitu gani kilichokuwa katikati yao.



    Alielekea upande wa Magharibi mwa msitu ule lilipoelekea kundi lile jana yake. Akiwa anaendelea na kazi yake, mara alishtukia miti ikianza kutingishika huku kelele za ajabu zikisikika, akajua ni lile kundi kubwa la masokwe, akajibanza kwenye mti mkubwa na akaanza kujipanga tayari kwa kupiga picha.



    Ugumu alioupata jana yake uliendelea kuwa vilevile kwani hakupata hata upenyo wa kutazama vizuri kilichokuwa katikati ya kundi lile, ikabidi abadilishe lenzi ya kamera na kutumia yenye uwezo wa kuona mbali, akawa analifuatilia wakati likiruka kutoka tawi moja hadi lingine.

    Bahati mbaya mvua ilianza kunyesha na kumfanya airudishe kamera yake kwenye mkoba akihofia kuiharibu kwa maji ya mvua, akakubali kuendelea kuloana na mvua mpaka atakapojua ni kitu gani kilichokuwa katikati ya masokwe wale.



    Mvua iliendelea kunyesha kwa muda mrefu lile kundi likawa linatafuta sehemu ya kujibanza ili lisinyeshewe na mvua, likakimbia mpaka mahali palikuwa na pango kubwa. Masokwe wote wakaingia ndani ya pango lile.



    “Hapahapa, nitakaa mpaka nione mwisho wao,” alisema Harrison huku akitafuta sehemu nzuri ya kujibanza. Akasubiri mpaka mvua ilipoanza kupungua, wale masokwe wakaanza kutoka mmoja baada ya mwingine. Baada ya dakika kadhaa kupita, Harrison hakuamini alichokiona mbele ya macho yake.



    Kiumbe ambaye alikuwa tofauti kabisa na wale sokwe alitoka kwenye lile pango,Harrison akaiweka vizuri kamera yake na kupiga picha kadhaa mfululizo. Akamuona yule kiumbe akiingia katikati ya kundi la wale sokwe na kuanza kuparamia matawi ya miti kama wanyama wale.



    “Mungu wangu mbona amefanana na binadamu lakini mbona anaruka kwenye miti kama sokwe? Kwa nini analindwa kiasi hicho,”Harrison alibaki amepigwa na butwaa kwa sekunde kadhaa kabla ya kushtukia akidondokewa na kitu kizito kutoka juu ya mti.



    Alikuwa ni sokwe mkubwa ambaye kumbe alimuona Harrison akipiga picha. Akaanza kumrarua kwa meno na kucha huku akipiga kelele zilizo washtua wenzake. Ikabidi Harrison atumie uwezo wake wote kujinasua kutoka kwenye makucha ya yule sokwe, akatimua mbio huku akijitahidi kuweka vizuri kamera yake.



    Kundi lote lilianza kumfukuza kwa kasi akatimua mbio mpaka kwenye hema lake na kuingia ndani na kujifungia. Lakini katika hali ambayo hakuitegemea, sokwe wakubwa wakaanza kuchanachana lile hema hali iliyomfanya atokee upande wa pili na kutokomea vichakani huku akijitahidi kuiweka vizuri kamera yake .



    Kutokana na kuhofia usalama wake hakutaka kurudi nyuma alikimbia mpaka kwenye ofisi za msitu huo na kukabidhi vifaa alivyopewa, akaaga na kuondoka huku askari wa wanyama pori aliyekuwa zamu akawa anamshangaa kutokana na hali aliyokuwa nayo.

    “Vipi kuna tatizo?”

    “Hapana afande,nimeamua kurudi nyumbani.”



    “Na hizo alama za kucha mwilini ni za nini? Umevamiwa na chui? Mbona mizigo yako hujachukua?” aliuliza yule askari lakini Harrison hakumjibu chochote akaondoka zake kwa kasi.



    MWILI wake wote ulijaa majeraha yaliyotokana na mashambulizi ya sokwe lakini Harrison hakujali, alitaka kurejea zake Marekani haraka iwezekanavyo ili akautangazie ulimwengu juu ya kiumbe cha ajabu alichokiona katikati ya pori kikilindwa na sokwe kama malkia wao. Hakuwahi hata mara moja kusikia kama kulikuwa na sokwe aliyefanana na binadamu kiasi hicho.



    Akiwa amechoka baada ya kutembea umbali mrefu katikati ya pori aliamua kuketi kando ya njia na kutoa kamera yake kwenye mfuko, akaiwasha na kuanza kubonyeza huku akiangalia picha moja baada ya nyingine, mpaka akazifikia alizozipiga kabla ya mapambano yake na sokwe.



    “Mungu wangu, sijapata kuona mwanamke mrembo kama huyu maishani mwangu, ona nywele zake, matiti yake, hips zake, makalio yake na hata urefu wake. Rangi yake ya ngozi ndiyo kabisaa inavutia mno, ni nani huyu? Aliyeamua kuja kuishi porini na sokwe na akaelewana nao kiasi cha wao kumlinda? Nahitaji kumjua, bila shaka sitakiwi kurejea Marekani bila kuikamilisha kazi hii ambayo ninajua siku moja nikiichapisha



    itanijengea heshima kubwa sana duniani, hili si jambo la kawaida hata kidogo,” aliwaza Harrison akiendelea kuitazama picha ya msichana huyo, tayari alikuwa na uhakika wa asilimia mia moja kuwa be huyo hakuwa sokwe.

    Baada ya kutuliza mawazo yake vizuri, aliiweka kamera yake kwenye begi, akaitoa bastola yake kiunoni na kuhakikisha iko sawa, ndipo akaamua kugeuza kurejea tena porini, alipofika kwenye eneo la ofisi za msitu, askari wa wanyamapori yuleyule alikuwepo.



    “Vipi tena?”

    “Ninarudi porini.”

    “Kufanya nini?”

    “Kazi yangu haijakamilika.”

    “Kibali chako hakijaisha?”

    “Bado.”

    “Hebu.”

    Harrison akaingiza mkono mfukoni na kukitoa kibali kisha kunyoosha mkono wake kumkabidhi askari ambaye alikisoma na kuthibitisha kilikuwa na mwezi mmoja na nusu mbele, hivyo kilifaa kutumika, hata hivyo alimweleza Harrison kuhusu usalama wa porini, kuwa sokwe walikuwa wamekasirishwa na jambo ambalo hakuna mtu aliyelijua mpaka wakati huo askari wengi wa wanyamapori walikuwa wamejeruhiwa vibaya.

    “Nakushauri usiende!”

    “Niache tu.”

    “Lakini kumbuka ukipatwa na matatizo sisi hatuwajibiki!”

    “Hakuna tatizo. Najua jinsi ya kujilinda.”

    “Una silaha?”

    “Ndiyo.”

    “Iko wapi?”

    “Hii hapa,” aliongea Harrison akionesha bastola yake.

    “Ha! Ha! Ha!” badala ya kufurahi, askari alicheka kwa dharau.

    “Mbona unacheka?”



    “Huwajui sokwe wakikasirika? hiyo siyo silaha, watakunyang’anya halafu watakuchomoa hiyo shingo mwilini.”

    “Bwana litakalokuwa na liwe, lazima niikamilishe kazi niliyoianzisha, aliyesema ‘Never start something you can’t finish’ (Kamwe usianzishe



    jambo ambalo huwezi kulikamilisha) hakuwa mjinga,” Harrison aliongea akianza kuchapa mwendo kurejea porini; kamera mkononi.

    Masaa mawili baadaye alikuwa katikati ya pori akitembea kwa uangalifu, macho yakiwa chini kutafuta nyayo za sokwe na wakati mwingine



    kusikiliza milio yao, hakwenda umbali mrefu sana kabla hajasikia mlio wa sokwe uliomaanisha kutoa taarifa kwamba kulikuwa na adui ili sokwe wote wa kiume wakusanyike, aliuelewa mlio huo ulikuwa na maana gani kwa sababu ndiyo elimu aliyoisomea.



    “Mungu wangu!” alisema maneno hayo baada ya kushuhudia sokwe wakikusanyika makundi kwa makundi na kumuweka katikati huku wakitoa milio iliyomaanisha “ ua” moyo ulimdunda, jasho likamtoka na akahisi nguo ya ndani ikilowana, hakuhitaji elimu kubwa sana kutaka kufahamu kama huo ulikuwa ni mkojo.



    Baada ya kama nusu saa hivi, zaidi ya sokwe wasiopungua elfu mbili walikuwa wamemuweka katikati, wakionekana kama walikuwa wakisubiri amri kutoka mahali fulani ili waweze kumaliza kazi iliyokuwa mbele yao. Harrison akawa mwenye uhakika kabisa kuwa huo ulikuwa mwisho wake, hakuwa na namna yoyote ya kujiondoa eneo hilo, risasi za plastiki alizokuwa nazo kwenye bastola yake zisingeweza kumsaidia, akaamua kuachana nayo.



    “Ningejua ningemsikiliza yule askari wa wanyamapo…” hakumalizia sauti yake baada ya kusikia sauti nyembamba ya kike ikiwaamuru sokwe wavamie na kuua adui, sauti ilitokea kwa nyuma na sokwe wote waliokuwa na ukubwa kama wa ng’ombe wakaanza kukimbia kwenda mbele kwa kasi lakini kabla hawajamfikia alisikia tena sauti ileile ikiwaamuru waache kuua, sokwe wote wakafunga breki na kuanza kurudi kinyumenyume kumpisha aliyetoa sauti.



    Huku akitetemeka Harrison alimshuhudia msichana yuleyule aliyemuona katikati ya sokwe akitokea, usoni amejawa na tabasamu, mashavuni kukiwa na vishimo vilivyoitwa dimpoz. Chini ya pua yake, mkono wa kushoto kulikuwa na kidoti cheusi kilichomfanya azidi kuonekana mzuri.

    “My God, what a chick! Am I dreaming? What is she doing in this thick forest?” (Mungu wangu, msichana mrembo ajabu! Ninaota? Anafanya nini kwenye msitu huu wa kutisha?) aliwaza Harrison akinyanyuka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Cha kwanza alichokifanya ni kuikamata kamera yake na kuanza kupiga picha za mfululizo, sokwe wakataka kumvamia lakini msichana akanyosha mkono wake juu, sokwe wote wakatulia kabisa na kulala chini wakionesha utiifu wa hali ya juu, Harrison akazidi kupiga picha.



    “Who are you?” (Wewe ni nani?) aliuliza.

    “What are you doing here?” (Unafanya nini hapa?)

    “Tell me.” (Niambie.)



    Harrison alizidi kuuliza maswali mfululizo lakini hakuna hata moja lililojibiwa, msichana huyo aliendelea kutabasamu tu huku akimpapasa Harrison mwili wake kama vile alikuwa akishangaa. Ilionekana wazi ilikuwa ni mara yake ya kwanza kukutana na kiumbe cha aina hiyo, Harrison aliligundua hilo kutokana na mshangao ulioonekana machoni mwake, alipoanza kuzungumza alizungumza kwa lugha ya sokwe, Harrison akashangaa lakini hakuweza kumjibu chochote.



    Akatoa mlio fulani, sokwe wakanyanyuka na kusimama wima kisha kuanza kutembea wote wakiwa wamemuweka katikati, Harrison alizidi kupiga picha, kichwani mwake akijisemea maneno; Yes, she is the queen of the gorillas, too beautiful to live here though. I am going to do



    whatever I can to bring her to civilization.” (Ndiyo, ni malkia wa masokwe, ingawa ni mzuri mno kuishi hapa. Nitafanya kila linalowezekana kumuondoa hapa na kumpeleka kwenye maisha ya ustaarabu.) aliwaza Harrison akishuhudia kundi kubwa la sokwe likiondoka mbele yake, haikuwa rahisi kuamini kama alikuwa amenusurika kuchanwachanwa.



    HARRISON, mtafiti wa wanyama ambaye mara baada tu ya kumaliza masomo yake ya chuo kikuu aliamua kuzama kwenye msitu wa Tongass kuwafanyia utafiti sokwe na maisha yao, amefanikiwa kupiga picha ya ajabu ambayo hakutarajia kabisa kukutana nayo kwenye msitu huo.



    Ni picha ya msichana mrembo mno, ambaye yeye amembandika jina la Queen of the Gorillas kwa sababu msichana huyo aliishi na sokwe porini na walimlinda kama malkia wao, uzuri wake ulitisha, alikuwa mrefu, mwenye umbile zuri, nywele ndefu alizozivuta kwa nyuma, ngozi laini ya mwili wake na miguu minene yenye kuvutia.



    Picha hiyo imemchanganya kabisa akili Harrison, mara ya kwanza aliamua kuondoka kuokoa maisha yake baada ya kupokea kichapo kutoka kwa sokwe ambao hawakutaka kupigwa picha lakini akiwa njiani alikata shauri kurejea ili akamilishe vizuri uchunguzi wake kwa msichana aliyempiga picha.



    Safari ya pili alijikuta amezingirwa na kundi kubwa la sokwe waliokuwa tayari kumuua, bila msichana huyo kujitokeza na kuwazuia sokwe wasitekeleze amri aliyokuwa ametoa, ni wazi Harrison angechanwachanwa kiasi kwamba hakuna kipande cha nyama yake kingeonekana.



    Baada ya sokwe kuzuiliwa, aliwashuhudia wakiondoka na malkia wao na kumwacha yeye akiendelea kuwapiga picha. Hakika alikuwa amepigwa na butwaa, akabaki eneo hilohilo akiwashuhudia sokwe wakipotea porini.



    “OH, Mungu wangu, lazima niondoke, nimepata kitu nilichokuwa nakitafuta, nitarudi tena siku nyingine kumfuata huyu msichana niende naye Marekani, hafai kuishi hapa! Acha kwanza nirejee nyumbani nikaueleze ulimwengu juu yake, najua hakuna atayenianimi lakini kwa ushahidi nilio nao kila mtu atakubali na lazima nitapata hata tuzo ya upiga picha, kwani hakuna mtu amewahi kufanya kazi ya aina hii, ningekwishaiona



    mtandaoni!” aliwaza Harrison akibeba mabegi yake na taratibu akaanza kuondoka kuelekea kwenye kituo cha maaskari wa wanyamapori.



    Hapo alibahatisha ndege iliyoleta watalii kutoka Marekani, akaomba msaada wa usafiri na hakuna aliyemkatalia. Saa moja baadaye alikuwa angani na kuruka kwa masaa matano mpaka San Francisco ambako ndiko ulikuwa mwisho wa safari ya ndege hiyo. Akashuka na kutaka kulipa l



    akini pesa yake ilikataliwa na kuambiwa alichopewa ulikuwa ni msaada, Harrison akashukuru akaondoka hadi stesheni ya treni huko alipanda treni iliyoondoka San Francisco kuelekea Los Angeles, akaingia saa tano za usiku na kutafuta nyumba ya wageni ya bei rahisi maeneo ya Pasadena na kupumzika mpaka siku iliyofuata asubuhi.

    “Sasa ndiyo wakati wa kutengeneza pesa maishani mwangu,” aliwaza akiziangalia picha alizokuwa nazo na kuipitia upya taswira ya mambo yote aliyokutana nayo.



    Siku hiyohiyo alitafuta kampuni ya uchapishaji wa vitabu iitwayo Modern World Publishing na kuzungumza nao juu ya kuchapisha kitabu chake ambacho alitarajia kukiandika juu ya maisha ya malkia wa sokwe. Wote walionyesha mshangao, wakishindwa kuelewa ni nani angetaka kununua kitabu cha namna hiyo.



    “Najua ninachokiongea.”

    “Tuelezee kidogo.”



    “Nitawaelezea kwa mdomo lakini sitawaonyesha picha.”

    “Hakuna shida.”

    Akasimulia kila kitu juu ya msichana aliyemwona bila kutaja msitu alikokuwa na hata kuwaonyesha picha, kila mtu alivutiwa na wote wakakubaliana naye kuhusu kukichapisha kitabu hicho, wakimtaka haraka sana aandike muswada na kuwapelekea ofisini kwao ili waanze kuupitia.

    “Itakuchukua muda gani?”

    “Mwezi mmoja, si maneno mengi sana, zaidi itakuwa ni picha.”

    “Sawa.”



    Mkataba ukasainiwa na Harrison akaondoka kwenye ofisi za kampuni hiyo akiwa mwenye furaha kupindukia, tangu siku hiyo alianza kazi ya kuandika kitabu na mwisho alipomaliza, wiki tatu baadaye badala ya mwezi mzima alikwenda kwenye ofisi za kampuni ya uchapishaji, wote



    wakashangazwa na kasi yake lakini wakashangazwa zaidi na picha alizokuwa nazo, hawakuwahi kuona picha za aina hiyo, wote waliamini kitabu hicho kingeuzwa kuliko kingine chochote ambacho kimewahi kuchapishwa katika historia.

    “Mwanzoni nilifikiri ni uongo, lakini kwa picha hizi nimekuamini. Huyu msichana yupo?”



    “Ndiyo.”

    “Wapi?”

    “Kwenye msitu wa Tongass, nitakueleza kwa sababu nimesaini mkataba na wewe, vinginevyo nisingesema.”

    “Alifikaje huko?”

    “Hata mimi sijui, hakunieleza chochote zaidi ya kutabasamu, tabia zake ni za sokwe kabisa.”

    “Du!”

    ***

    Dk. Charwe Rwegoshora hakuipenda kabisa Geneva tena, kifo cha mke na mtoto wake kwenye ajali mbaya ya ndege iliyolipuka kilimwumiza mno. Kifupi maisha yake hayakuwa sawa baada ya tukio hilo, kazi ilimshinda, akawa ni mtu wa kunywa pombe masaa ishirini na nne akiamini alikuwa anapoteza mawazo kumbe alikuwa anazidi kujididimiza.



    Aliishi kwa msaada wa serikali ya Uswisi na hakutaka kurejea nyumbani Buzilayombo ambako aliamini moyo wake ungemuuma zaidi, mara mbili alishajaribu kukatisha maisha yake lakini akaokolewa.



    Kwake msiba ulikuwa haujaisha, alimlilia mke na mtoto wake kila siku na kutamani angalao kungekuwa na makaburi ambako wangezikwa na yeye angewatembelea na kuzungumza nao, lakini haikuwa hivyo.



    Kila mwezi wa kumi na mbili alisafiri hadi mahali ambako ndege iliangukia na kufanya ibada maalum peke yake akiwaombea mke na mtoto wake, hakuna mtu wa kumweleza kwamba miaka mingi baadaye mtoto wake alikuwa yu hai, akiishi na sokwe katikati ya msitu wa Tongass na sokwe waliomwokoa wala hakuwa na taarifa kabisa kwamba eti alikuwa na familia sehemu fulani.



    Charwe alishakata tamaa kabisa, wala hakutaka kuoa tena na kupata mtoto mwingine. Kifupi hakuhitaji mke maishani mwake, kwake kufanya hivyo ilikuwa ni sawa na kumsaliti mkewe, jambo ambalo hakutaka kabisa kulifanya. Watu wengi walimwona kama mtu asiye na akili timamu



    kwa jinsi alivyotembea na kuongea peke yake njiani, bila kufahamu kila alikokwenda alisikia sauti za mwanaye Charlotte na mke wake Anganile zikimsemesha.

    NDEGE aina ya Air Bus iliyokuwa na abiria zaidi ya 415 inaanguka karibu kabisa na Msitu wa Tongass na watu wote waliokuwemo ndani yake wanaaminika kufa bila kufahamu kwamba mwanamke mmoja



    aliyekuwa na mtoto wake (Charlotte) alivunja kioo cha dirisha na kumpitisha mtoto wake hapo kabla ndege haijajatua chini, kwa msaada wa parachuti mtoto huyo alifanikiwa kutua porini na sokwe wakamuokota, kisha kutokomea naye porini.



    Baadaye taarifa zilitangazwa kwamba watu wote wamekufa! Ndipo Dk. Charwe Rwegoshora, aliyekuwa akimsubiri mke na mtoto wake Charlotte katika Uwanja wa ndege wa Geneva alikokuwa akiishi kuchanganyikiwa na kuvurugikiwa kabisa na maisha yake kuharibika, kwani familia yake ndiyo ilikuwa kitu muhimu kuliko kazi na fedha zote alizopata.



    Sokwe wakamchukua mtoto yule na kuishi naye msituni kama mtoto wao hadi akakua akijiona ni sehemu yao na wakamfanya kuwa malkia wao, hakujua alikotokea na aliishi na kuwa na tabia za kisokwe. Hakuwahi kuwa na mawasiliano na binadamu mwingine yeyote mpaka mpiga picha mmoja (Harrison)



    ambaye pia alikuwa mtafiti wa wanyama alipompiga picha msituni, siku hiyo ndiyo binti huyo alipogundua tofauti aliyokuwa nayo kati yake na sokwe.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Picha alizozipiga Harrison alisafiri nazo hadi Los Angeles ambako lengo lake lilikuwa ni kuzichapisha katika kitabu na kuelezea maisha ya msichana wa ajabu aliyemuona msituni, akasaini mkataba na kampuni ya uchapishaji ya Modern World Publishing ili wakachapishe na kukisambaza kitabu hicho duniani kote.



    KWA Dk. Charwe maisha hayakuwa na maana tena, simanzi ilimsumbua, hakuna mtu aliyemuona ambaye aliamini alikuwa ni daktari. Uchafu ulimfunika na burudani yake kubwa ikabadilika na kuwa pombe ambazo baada ya muda zilionekana kutompa furaha aliyoitafuta, hapo ndipo akavamia dawa za kulevya aina ya cocaine, akazidi kudidimia na hakuwa na mtu yeyote wa kumgeuza.



    Ndugu zake walishajitahidi kadiri ya uwezo wao kumshawishi arejee Tanzania lakini hakuwa tayari, jibu lake liliendelea kuwa moja tu; “Haya ni maisha yangu, niachiwe mwenyewe.” Hakuna siku iliyopita bila kutumia pombe au madawa ya kulevya kwenye damu yake, alitisha na hakuna



    aliyemuamini kwani alifikia mpaka hatua ya kuiba vitu ndani ya nyumba za rafiki zake ili tu aweze kupata fedha za kunywea pombe au kununua cocaine, hili lilifanya azidi kutengwa.



    Baada ya kuuza kila kitu ndani ya nyumba yake na kodi ya nyumba kuwa tatizo, hatimaye aliamua kuingia mitaani ambako aliishi na mateja wengine wa madawa ya kulevya wasio na makazi, juhudi za kumuondoa huko kumpekeka kwenye vituo vya kuwasaidia waathirika wa madawa ya kulevya mara kadhaa zilishindwa kuzaa matunda, kwani alitoroka huko na kurejea mitaani ambako aliendelea kubwia unga.



    “Mungu wangu ajali ile,” dereva wa gari moja alisikika akisema baada ya kushuhudia mkusanyiko wa watu katikati ya barabara, kukiwa na msongamano mkubwa wa magari, taratibu akashuka na kutembea hadi eneo hilo.

    “Amegongwa tena vibaya sana!” Mtu mwingine alisema akitokea eneo hilo.



    “Kagongwa na nini?”

    “Gari la kuzoa taka!”

    “Duh! Imekuwaje mpaka akagongwa?” dereva aliuliza.

    “Nimeshuhudia kwa macho yangu.”

    “Umeshuhudia nini?”

    “Aliyegongwa nadhani ni mteja wa unga, alikuwa anabembea barabarani bila ya kuangalia kushoto wala kulia kwenye ile kona, si akaja yule dereva wa gari la taka akiwa mwendo wa kasi, wakati anakata kona ndiyo yule mteja naye akawa amefika, pale pale …..”

    “Hebu na miye nikaone.”

    “Hutaweza kuangalia, kaumia sana.”

    “Ngoja…”



    Dereva alisogea mbele akipita katikati ya watu mpaka akafika mahali alipolala mtu aliyegongwa, hakuonekana kuwa mzima, akazidi kumuangalia kwa umakini ili aone kama angeweza kumtambua. Ghafla akapiga kelele alipoviangalia viatu vyake, akatamka kwa sauti kwamba huyu alikuwa ni daktari Mwafrika aliyeamua kuingia kwenye matumizi ya haramu ya madawa ya kulevya.



    “Mungu wangu! Huyu si Dk Charwe?” Alipouliza hivyo tu watu wote walifumbuka macho kwani Dk. Charwe alikuwa maarufu katika Jiji la Geneva kwa kuwa alishaandikwa sana na Magazeti ya Udaku kutokana na tabia yake ya ulevi wa kupindukia ambayo madaktari wengi walidai, bila kujua tatizo lililokuwa likimsumbua, kwamba aliidhalilisha taaluma yao.



    Wakati Dk. Charwe ananyanyuliwa na kupakiwa kwenye gari la wagonjwa, watu wote walikuwa na uhakika kwamba alishakata roho lakini alipofikishwa hospitali na kupimwa, aligundulika kwamba moyo wake ulikuwa bado ukipiga kwa mbali, hivyo akakimbizwa chumba ha upasuaji



    ambako alishonwa sehemu zote zilizokuwa zikivuja damu, kisha akapigwa picha za X-Ray, MRI na CT- Scan ili kuona kama alikuwa na maumivu kwa ndani, majibu yalipotoka, kila mtu alisikitika.



    “Kwa hali ilivyo, inawezekana akanusurika kifo lakini maisha yake yote atakuwa mtu wa kitandani, maana ameumia mgongo na uti wa mgongo kuanzia shingoni, sehemu yote ya chini kuanzia mikono hadi miguuni hazifanyi kazi.”



    “Atarejewa na fahamu kama kawaida?” Muuguzi aliuliza.

    “Zitarejea baada ya muda ila kitu ambacho hakiwezi kurejea ni fahamu za kwenye miguu.”

    “Basi tena, ataishi maisha ya shida sana.”

    “Ana ndugu?” Daktari aliuliza.

    “Hapa Uswisi?”

    “Ndiyo”



    “Hana ndugu, nasikia tu mke na mtoto wake walikufa katika ajali ya ndege wakisafiri kutoka Afrika kuja hapa, hicho ndicho chanzo cha yeye kuvurugikiwa na akili na kuamua kunywa pombe na hatimaye madawa ya kulevya.”



    “Namkumbuka sana huyu daktari, itabidi muwasiliane na watu wa kitengo cha Ustawi wa Jamii ili waweze kuwapigia simu ndugu zake huko Afrika juu ya tatizo lililomtokea.”

    “Sawa daktari tutafanya hivyo.”



    Daktari akaondoka na matibabu ya Dk. Charwe yakaendelea huku mawasiliano ya ndugu zake waliokuwa Tanzania yakiendelea kwa kutumia anuani za barua pepe ambazo walizipata kwenye ofisi aliyokuwa akifanyia kazi kabla mambo hayajamharibikia.



    Mwezi mmoja baadaye, fahamu zikiwa zimemrejea, ndugu zake walifika na taratibu zikafanyika, Dk. Charwe akasafirishwa hadi Tanzania ambako safari iliendelea hadi kijijini kwao Muleba, Bukoba kwenye nyumba aliyoijenga na kuanza maisha akiwa na bibi yake tu, kila mtu alijua hakuwa na muda mrefu wa kuishi duniani.



    “Ogu Omwana owo mwandetela ndamkolaki?.” (Nitamfanya nini mtoto huyu, mmeniletea mimi?) Alisema bibi yake baada ya kumpokea.



    ***

    “Sifanani nao, nafanana na yule waliyetaka kumuua!” aliwaza msichana huyo akiwa katikati ya kundi la sokwe waliokuwa wakimlinda.

    Kulikuwa na tofauti kubwa sana kati yake na viumbe aliokuwa akiishi nao, hakufanana nao kwa kitu chochote, aliowaona ni wazazi wake ambao

    alijitambua akiwa mikononi mwao walikuwa ni wanyama wenye sura mbaya na miili iliyojaa manyoya, vivyo hivyo ndugu zake wawili waliomfuatia nao pia walikuwa na sura hizohizo tofauti na ya kwake.



    “Hapa lazima kuna tatizo! Haiwezekani mimi peke yangu ndiye niwe tofauti na wengine wote, ningependa kujua.”



    Mawazo haya yalimfikisha Charlotte kwenye hali ya kutaka kuufahamu ukweli, mtu pekee wa kumuambia ukweli huo hakuwa mwingine bali ni yule aliyefanana naye, hivyo ndivyo alivyoamini baada ya kuwauliza sokwe wote mpaka wazazi wake bila kupata ukweli. Akaamuru mtu huyo atafutwe na Sokwe, kama angepatikana basi aletwe kwake mara moja, kazi ikaanza.



    Hayo yakitokea porini Tongass, tayari kitabu cha Harrison chenye sura na historia ya msichana mrembo wa ajabu aliyeishi na sokwe kilikuwa kimetoka chini ya kichwa cha habari “THE QUEEN OF THE GORILLAS” yaani Malkia wa Masokwe na watu dunia nzima walikuwa



    wakikigombania kwa dola ishirini kwa kitabu kimoja, hii ilikuwa ni dalili kuwa kitabu hiki kingemtajirisha Harrison ndani ya muda mfupi na ndivyo ilivyotokea, kwani katika kipindi cha miezi mitatu tu, nakala milioni kumi zilishauzwa kila pande ya dunia na kilikuwa kikitafsiriwa



    katika lugha nyingine mia moja na moja (101), wataalamu wa mambo walianza kusema hapakuwa na kitabu kilichowahi kuuza nakala nyingi kiasi hicho.



    MAISHA ya Dk. Charwe, baba wa Charlotte (msichana aliyeko msituni akiishi na sokwe) yanaharibika baada ya kuamini mke na mtoto wake walikufa katika ajali ya ndege iliyoanguka na kuua abiria wote waliokuwemo ndani yake, hakuna aliyejua kwamba mtoto alinusurika na



    kuokotwa na sokwe ambao waliishi naye msituni na kumfanya kuwa malkia wao.

    Harrison, ni kijana wa Kimarekani mtafiti wa wanyama ambaye alifika kwenye msitu wa Tongass na kufanikiwa kupiga picha za msichana huyo



    akiwa katikati ya kundi la sokwe wengi waliomlinda na kumheshimu.

    Picha hizo anazitumia kuandika kitabu kiitwacho The Queen of Gorillas ambacho baadaye alikichapisha na kupata mamilioni ya dola kilipouzwa dunia nzima. Maisha yake yakabadilika kabisa.



    Tayari Harrison alikuwa maarufu kuliko alivyowahi kufikiria maishani mwake, utajiri wake ulitisha, kitabu kimoja tu, The Queen of Gorillas kilikuwa kimebadilisha kabisa maisha yake, mamilioni ya dola yalikuwa yakimiminika kwenye akaunti yake, akiwa na umri wa miaka ishirini na nane tu.



    Karibu kila chombo cha habari cha Ulaya na Marekani kiliandika habari zake, alifanya mahojiano katika vipindi mbalimbali vya televesheni, vikiwemo vya Oprah Winfrey Show, Larry King, Friday Night Show na vingine vingi tu, kifupi ndani ya miezi sita alikuwa maarufu sawasawa kabisa na wachezaji sinema wa Hollywood, jambo lililomfanya aalikwe sehemu mbalimbali ambako watu maarufu walikutana.



    “Hi! Are you Harrison?” (Salama! Wewe ni Harrison?) aliuliza msichana mmoja wakati Harrison akiingia kwenye Ukumbi wa MGM Grand, siku ya utoaji wa tuzo ya Cliff Edom’s New American Award, ambayo inawahusu watu waliofanya mambo ya kuheshimika nchini Marekani.

    “Yeah! Can I know who is this friend of mine?” (Ndiyo! Naweza kujua huyu rafiki yangu ni nani?)

    “I am Linda Morris!”(Naitwa Linda Morris)

    “You look good in that dress!”( Gauni ulilovaa limekupendeza sana)

    “Thank you, you look handsome too in that black suit and red tie!”(Ahsante, unaonekana mzuri pia ndani ya hiyo suti nyeusi!)

    “Thank you!”(Ahsante)

    “Are you here alone?”(Uko peke yako?)

    “Yeah!”(Ndiyo)

    “I am alone too, can we give each other some company?”(Niko peke yangu pia, tunaweza kuwa pamoja?)

    “No problem!”(Hakuna tatizo)



    Wakashikana mikono na kuanza kutembea kuingia ndani huku wakikanyaga zulia jekundu, kamera zote ziliwafuata wao. Hivyo ndivyo ilikuwa katika maisha ya Harrison tangu apate umaarufu, pati zote alizoalikwa, wasichana wa kila aina walimtaka kimapenzi, hisia zake zilimfanya ealewe walichokipenda si yeye bali fedha na umaarufu wake.



    Wakaketi kwenye kiti cha watu wanne, muda mfupi baadaye mcheza sinema maarufu Chuck Norris na mkewe walifika na kuketi kwenye meza hiyohiyo, Harrison hakuamini kwamba hatimaye siku moja alikuwa ameketi meza moja na mtu aliyemuona kwenye sinema tu. Wakasalimiana na mazungumzo yakaendelea.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Linda alijaribu kadiri ya uwezo wake wote kuwa karibu na Harrison, akimtega kwa kila mbinu ili aingie kwenye mstari wake, jambo ambalo Harrison aliligundua mapema. Isitoshe hakuwa tayari hata kidogo kuwa na uhusiano na msichana mwingine kwa wakati huo, mwanamke pekee aliyemuwaza kichwani mwake ambaye alimtaka ampate kwa udi na uvumba na kumuoa hakuwa mwingine bali ni yule aliyemuona msituni.



    “Nampenda sana yule msichana, laiti ningefanikiwa kumpata kutoka porini, basi ningefunga naye ndoa ya ajabu. Sijui kama nitafanikiwa lakini lazima nirudi tena msituni kumsaka na kujaribu kumuondoa katika mazingira hayo, watu watashangaa sana na pengine anaweza kuja kukutana na familia yake,” aliendelea kuwaza Harrison bila kujua kilichoendelea ukumbini kwa jinsi alivyokuwa amezama kwa mawazo.



    “And the winner of this year’s Cliff Edom’s New American Award is Harrison Harvey for his book the Queen of the Gorillas which has transformed many people’s lives!”(Na mshindi wa tuzo ya mwaka huu ya Cliff Edom’s NewAmerican Award ni Harrison Harvey kwa kitabu chake kiitwacho Malkia wa Masokwe ambacho kimebadilisha maisha ya watu wengi.)



    Ukumbi wote ukalipuka kwa shangwe na nderemo watu wakimshangilia Harrison ambaye alipigwa na butwaa baada ya kusikia jina lake likitajwa, ilikuwa ni heshima kubwa mno kwake kupata tuzo hiyo ambayo kwa kawaida ilichukuliwa na watu waliofanya mambo makubwa hata katika masuala ya vita n.k.



    Taratibu alinyanyuka mahali alipoketi na kuanza kutembea akiongozana na Linda, watu waliowaona walidhani alikuwa mpenzi wake, ingawa hakufurahia tabia hiyo, Harrison hakuwa na jinsi ikabidi amuache Linda afanye kilichomfurahisha. Akapokea tuzo kisha akapewa muda mfupi wa kuongea kutoa shukrani.



    “Thank you very much, this award goes to my mom and dad wherever he is, my grandparents, for their support and lastly, thanks to all Americans and the girl I love…” (Ahsanteni sana, tuzo hii iende kwa mama na baba yangu popote alipo, babu na bibi yangu kwa kuniunga mkono na mwisho ni kwa Wamarekani wote na msichana nimpendaye…) Harrison akasita na kumwangalia Linda



    ambaye sura yake ilijaa tabasamu, meno karibu yote yakiwa nje, kama jinsi ambavyo watu wote ukumbini walivyodhani aliyekuwa akiongelewa hapo ni Linda, ndivyo msichana huyo pia alivyowaza. Alibaki kimya akisubiri tu jina lake litajwe ili ashangilie.

    “…who is in the forest living with gorillas, without her photographs, I wouldn’t be here today. She is pretty and beautiful, hope one



    day she will be my wife living here with us.” (aliyeko porini, akiishi na masokwe, bila picha zake mimi nisingekuwa hapa. Msichana mzuri wa kuvutia, tumaini langu ni kwamba siku moja awe mke wangu na aishi hapa mjini pamoja na sisi) alimaliza Harrison akimsifia malkia wa masokwe, Linda akainamisha kichwa chake kwa aibu.



    Sherehe ilipomalizika kwenye majira ya saa sita usiku hivi, watu walisambaa kila mmoja kwenye gari lake na kuondoka, Harrison alikuwa akiendesha gari aina ya Audi New Model yenye thamani kubwa, nyuma yake alikuwepo Linda ndani ya Escarade mpya,



    akiangalia kupitia kioo cha pembeni, Harrison alishindwa kuelewa msichana huyo alikuwa ni nani hasa mpaka kuendesha gari la kifahari kiasi hicho.

    Badala ya kuendelea na safari yake msichana huyo alimfuata Harrison kwa nyuma mpaka nyumbani kwake maeneo ya matajiri yaitwayo Bel Air, gari likaingizwa ndani na ya Linda ikafuata nyuma. Alipoegesha Harrison alishuka na kumfuata Linda kwenye gari lake.



    “What’s up?”(Vipi?)

    “I wanna talk to you.”(Nataka kuongea na wewe)

    “About what? It is midnight baby, we all need to go to bed, call me tomorrow!”(Juu ya nini? Ni katikati ya usiku, wote tunahitaji kupumzika, nipigie kesho.)

    “It is important!”(Ni muhimu)

    “What is it about?”(Juu ya nini?)

    “It about us!”(Ni juu yetu)

    “I don’t have any deal with you.”(Sina biashara yoyote na wewe)

    “You just don’t know, give me time to explain!”(Hujui tu, nipe muda nikueleze)

    “Meeen! I need to go to bed, get the hell out of here!”(Hapana! Nahitaji kupumzika, ondoa upuuzi hapa!)

    “Let me be open!”(Acha niwe muwazi)

    “About what?”(Juu ya nini?)

    “I love you so much, please accept me in your life!”(Nakupenda sana, tafadhali kubali niwe maishani mwako)

    “You know what?”(Unajua nini?)

    “I don’t know!”(Sijui)

    “I hear that word ‘I love you’ about one hundred times a day, so you better go home, this is a wrong number.” (Nalisikia hilo ‘nakupenda’ karibu mara mia moja kwa siku, hivyo nakuomba tu uondoke, hapa siyo mahali sahihi.)



    WAKATI Malkia wa Sokwe (Charlotte, binti anayeishi Msituni na Sokwe, ambaye baba yake anaamini alikufa ndege ilipoanguka miaka mingi kabla lakini kumbe alinusurika na kuingia kwenye himaya ya Sokwe) akiwa amewaagiza Sokwe wamtafute mvulana aliyempiga picha porini



    (Harrison) baada ya kugundua hakufanana na wanyama hao ila kijana huyo, tayari Harrison yupo Los Angeles, amekwishachapisha kitabu chake kiitwacho Queen of the Gorillas na kujipatia mamilioni ya dola kutokana na mauzo dunia nzima.



    Hivi sasa Harrison si yule wa zamani tena, ni mtu maarufu sawasawa na wacheza sinema wa Hollywood, akiishi Beverly Hills, maeneo ya watu matajiri, hajaoa na siku zote anatamani kurudi porini kwenda kumtafuta msichana mrembo aliyemwona, akiamini huyo ndiye alitakiwa kuwa mke wake.



    Akiwa katika fikra hizo, amejitokeza msichana aitwaye Linda Morris, ambaye walikutana kwenye pati ambayo Harrison alipokea tuzo Cliff Edom’s New American Award kutokana na kitabu chake. Msichana huyu anamng’ang’ania Harrison hadi nyumbani kwake baada ya sherehe hiyo kuisha ingawa Harrison hataki kabisa uhusiano naye, alishaapa kutokuwa na uhusiano na msichana mwingine yeyote kabla hajamuoa Malkia wa Sokwe.



    “I don’t care how many times you do hear the word ‘I love you’, all I know is I love you truly, please accept me!” (Sijali unalisikia neno ‘nakupenda’ mara ngapi kwa siku, ninachojua mimi ni kwamba ninakupenda mapenzi ya kweli. Tafadhali nikubali.) aliongea Linda tena akilengwalengwa na machozi, jambo lililoashiria wazi kuwa alimaanisha alichokisema. Harrison alimwonea huruma lakini hakuwa na cha kufanya, kwani moyo wake ulikuwa kwa mtu mwingine kabisa na mtu huyo alikuwa ni Charlotte, Malkia wa Sokwe.



    “I can read your eyes and understand your heart, but…” (Naweza kuyasoma macho yako na kuuelewa moyo wako, lakini…)

    “But, what darling… I love you.” (Lakini, kitu gani tena mpenzi…nakupenda.)

    “I am committed to someone else and I promised my heart to love only one woman!”(Nimekwishajiweka kwa mtu mwingine na niliuahidi moyo wangu kumpenda mwanamke mmoja tu!)

    “Who is that luck woman?” (Huyo mwanamke mwenye bahati ni nani?)

    “Do you wanna know?”(Unataka kujua?)

    “Yeah!”(Ndiyo)

    “Won’t you be hurt?”(Hutaumia?)

    “Just tell me, whether I will be hurt or not is non of your business!”(Wewe niambie tu, nitaumia sitaumia, siyo shughuli yako!)

    “Why are you so fierce?” (Kwanini ni mkali hivyo?)

    “I love you and for really I don’t want loose you.”(Nakupenda na kwa hakika sitaki kukupoteza.)

    “So I shouldn’t tell you?”(Kwa hiyo nisikuambie?)

    “Ok, go ahead and tell me.”(Sawa, niambie tu.)

    “I don’t know her name, but she is the Queen of the Gorillas!”(Simjui jina lake, lakini ni Malkia wa Sokwe.)

    “The one in your book?”(Uliyemwandika kwenye kitabu chako?)

    “Yeah!?”(Ndiyo)

    “Oh my God! That sucks!” (Mungu wangu! Hiyo ni mbaya)

    “Why?”(Kwa nini?)

    “She is too dirty and shabby!” (Ni mchafu na shaghalabaghala!)

    “Don’t say that, do not call my girl that name.”(Usiseme hivyo, usimwite msichana wangu jina hilo.) Harrison aliongea machoni



    akionyesha kukerwa, Linda hakuwa na namna zaidi ya kuomba msamaha.

    Waliendelea na maongezi mpaka saa tisa na nusu usiku, Linda akibembeleza na Harrison akiwa ameweka msimamo, hatimaye



    usingizi ukawashika. Alichokifanya Harrison ni kumchukua Linda hadi nje ya nyumba kulikokuwa na nyumba ya wageni, akafungua mlango na kumkaribisha ndani ambako alimpeleka hadi chumbani na kumwonyesha bafu pamoja na choo kisha kumtakia usiku mwema.



    “Why can’t I sleep in your room?”(Kwanini nisilale chumbani kwako?)

    “No! We might fall into temptations! Good night Linda” (Hapana! Tunaweza kuingia majaribuni usiku mwema Linda)



    “Ok!”(Sawa!) Linda aliitikia kwa shingo upande na Harrison akaondoka kuelekea nyumbani kubwa ambako aliingia chumbani na kuanza kusoma kitabu chaQueen of the Gorillas akiangalia picha za Malkia wa Masokwe, alimpenda mno, hakuamini kama

    kungekuwa na mwanamke mwingine wa kumchanganya akili yake kama ilivyotokea.



    Baadaye alipitiwa usingizi bila hata kuoga wala kuvua nguo alizokuwa nazo, aligutushwa usingizini na kengele ya mtu akitaka kufunguliwa mlango, alipotupa macho kwenye saa yake aligundua tayari ilikuwa ni saa kumi na nusu usiku, karibu kabisa na asubuhi. Haraka akanyanyuka na kufungua mlango kisha kuanza kushuka ngazi hadi chini.



    “What’s up?”(Vipi tena?) Aliuliza baada ya kufungua mlango na kukutana na Linda.

    “I can’t sleep!”(Siwezi kulala)

    “Why?”(Kwa nini?)

    “There are so many ants inside there!”(Kuna wadudu wengi sana huko ndani.)

    “Ants? In my compound? No way! We do fumigate every week, please Lind stop your funny jokes!(Wadudu? Ndani ya eneo langu? Hapana! Tunapuliza dawa ya kuua wadudu kila wiki, Linda acha utani wako!)



    “Yeah!”(Ndiyo!) aliitikia Linda akiwa tayari amekwishaingia ndani na kumwacha Harrison amesimama nje. Hakuwa na jinsi zaidi ya yeye pia kuingia ndani na kufunga mlango.



    “So what do you want us to do?”(Kwa hiyo unataka tufanye nini?)

    “Let’s just go and sleep in your room.”(Twende tu tukalale chumbani kwako)

    “I have told you that can’t happen!”(Nimekwishakuambia hilo haliwezi kutokea)



    “Please!”(Tafadhali!) Linda alizidi kubembeleza, huku akilia tena kwa uchungu kabisa, taswira hiyo ilimwingia Harrison moja kwa moja moyoni mwake na kujikuta akimwonea huruma.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Linda what do you want from me?”(Linda unataka nini kutoka kwangu?)

    “I don’t need anything, I am Linda Morris Ford, descendant of the Ford family, I so rich Harrison, I do not need a single penny



    from you, all I need is your love, period!”(Sihitaji kitu chochote, acha nikuambie, ninaitwa Linda Morris Ford, kitukuu cha familia ya Ford, sihitaji hata senti yako, ninachohitaji ni penzi lako tu!) alisisitiza Linda huku akimsogelea Harrison na kumkumbatia.



    Kilichotokea baada ya hapo ni watu wawili kupandisha ngazi hadi ghorofa ya kwanza ambako walinyoosha moja kwa moja hadi chumbani kwa Harrison, uso wa Linda ukiwa umeanza kurejewa na tabasamu, sehemu fulani ndani ya moyo wake alijisikia mshindi na kuamini kweli hakuna mwanamume alikuwa mjanja mbele ya mwanamke kama mitego ikiwekwa sawasawa.



    “You are in this room under one condition.”(Uko ndani ya chumba hiki kwa sharti moja tu.)

    “What is that condition?”(Sharti hilo ni lipi?)

    “NO SEX!”(hakuna ngono)

    “I don’t need it either.”(Hata mimi sihitaji pia.)

    “Ok! Let get in bed now.”(Haya tulale.)



    Harrison akajitupa kitandani na nguo zake vivyo hivyo Linda na gauni lake refu kama la bibi harusi, wakategana migongo na kuanza kutafuta usingizi, jambo ambalo lilikuwa gumu sana kutekelezeka. Kila mmoja alifikiria kimya akifikiria mambo yaliyokuwa



    yakitokea, Harrison akimfikiria Malkia wa Sokwe na Linda akiwaza namna ambavyo angelifanikisha zoezi la kumfanya Harrison amvue nguo na wafanye tendo la ndoa.



    “Kwa shepu yangu lazima atalegea tu, acha nicheze mchezo wa sitaki nataka kwanza asije akaniona rahisi.” Aliwaza Linda akiwa kimya.



    Nusu saa baadaye alianza kumsikia Harrison akikoroma, akagundua kweli mwanaume huyo alikuwa mgumu na alidhamiria kutofanya tendo hilo.Akamsogelea karibu na kumwekea paja lake kubwa kwa juu kisha kusogeza mdomo wake karibu kabisa na sikio la Harrison, taratibu akaanza kumhemea sikioni akiamini kitendo hicho lazima kingemsisimua, lakini Harrison aliendelea kukoroma kama vile hapakuwa na kilichokuwa kikiendelea.



    “Harrison!Harrison!” aliita akimtingisha baada ya kuona kile alichofanya kilikuwa hakiwezekani.

    “Vipi tena?”

    “Hebu nifungulie zipu mgongoni, hili gauni linanipa joto sana!”

    “Lakini kuna kiyoyozi? Tena mimi nasikia baridi sana.”

    “Nataka kwenda kuoga.”

    “Sawa!”



    Harrison alimfungua zipu, akiwa amefumba na kufumbua macho yake nusu sababu ya usingizi, kisha kurejea kitandani na Linda akanyoosha moja kwa moja ambako alivua gauni lake na kuoga.Haukupita muda mrefu sana akaibuka na gauni lake mkononi, akiwa kama alivyozaliwa, shepu yote nje! Harrison alikuwa usingizini akasogea hadi karibu yake kabisa na kumgusa.

    “Harrison! Harrison!”

    “Naam.”

    “Niweke wapi hili gauni?”

    “Kwenye kabati!”

    “Liko wapi?”

    “Hapo kushoto.”

    “Sioni.”



    Harrison aliketi kitako na kumwangalia Linda, ilikuwa ni kama ndoto kwa alichokuwa akikiona mbele ya macho yake, hakuwa na uhakika kama katika maisha yake yote aliwahi kukutana na mwanamke mwenye umbile la namna hiyo.

    “Mungu wangu!”Ndilo neno pekee alilosema wala hakukumbuka swali ambalo Linda alikuwa ameuliza.



    KIJANA maarufu Harrison ambaye umaarufu wake umetokana na kuandika kitabu kiitwacho Queen of the Gorillas ambacho kimeuzwa mamilioni ya kopi duniani na kumfanya awe miongoni mwa matajiri anajikuta katika mapenzi mazito na msichana wa msituni ambaye aliandika kitabu juu yake.



    Msichana huyu ni Charlotte, ambaye miaka mingi kabla alikuwa akisafiri na mama yake kwenye ndege kuelekea Uswizi, ndege ikaanguka na watu wote kufa isipokuwa yeye, akaokotwa na Sokwe ambao walimlea mpaka akakulia msituni akiwa hajui chochote na sokwe walimfanya Malkia wao.



    Harrison alipomwona msichana huyu alikuwa akifanya utafiti wa Sokwe porini na baada ya kuuza kitabu chake alitamani kurejea porini kwenda kumtafuta, akijiandaa kufanya hivyo, anakutana na msichana mwingine mrembo aitwaye Linda ambaye amedhamiria kumpata kwa gharama yoyote.



    Pamoja na kukataa, Harrison anajikuta amemkaribisha Linda nyumbani kwake na wanakubaliana kulala na nguo ili wasifanye mapenzi lakini usiku wa manane Linda ameanza vituko, yupo kama alivyozaliwa na Harrison anashuhudia.





    MACHO ya Harrison yalitua moja kwa moja kwenye maumbile ya Linda, akamwangalia kutoka kichwani, akaridhika kabisa kwamba sura ya Linda haikuwa ya kuvutia sana lakini kilichompa pointi ni ile ambayo vijana wengi huiita ‘Figa’. Hakika Linda aliumbika.



    Kifuani alikuwa na vilima viwili vilivyonyanyuka vyenye ncha kali, kushuka tumboni hakuwa na tumbo kabisa, wala yale ambayo huiitwa ‘sanamu la michelini’ chini ya tumbo kulikuwa na kiuno chembamba ambacho chini yake kidogo tu mtoto alipanuka mithili ya mtungi wa maji, halafu chini ya hapo akaanza kupungua na mwisho kabisa kulikuwa na mguu mzito.



    Huyo ndiye alikuwa Linda, hakika Harrison alihitaji nguvu ya ziada ili kuweza kukishinda kishawishi kilichokuwa mbele yake, kwani kila dalili ilishaonekana kwamba alichohitaji msichana huyo ni tendo la ndoa na alikuwa amedhamiria. Bila kutarajia Harrison alianza kusikia suruali yake ikimbana kwa mbele chini ya mkanda.



    “Nitaweza? Mimi mwanaume bwana lazima nionyeshe uwezo, nilishaahidi sitatembea na mwanamke kabla ya ndoa na mwanamke pekee ninayemtaka maishani mwangu ambaye atatakiwa kunibikiri kama hata wanaume huwa wanabikiriwa ni Malkia wa Sokwe, basi! Ee Mungu nisaidie,” aliwaza Harrison akimwangalia Linda mbele yake.



    Alichokifanya ni kufumba macho na kumwelekeza Linda mahali pa kutundika nguo yake, kisha msichana huyo akaja moja kwa moja na kupanda kitandani akiwa kama alivyozaliwa. Harrison alivuta shuka na kujifunika, kisha kuzihamisha kumbukumbu zake kwa msichana huyo na kuzipeleka msituni; akaanza kumfikiria Malkia wake wa Sokwe.



    Hakuchukua muda mrefu sana, fahamu zikampotea, alikuwa katikati ya usingizi, wala hakukumbuka kwamba kando yake alikuwepo Linda akihema kwa nguvu sababu ya tamaa za mwili wake. Kilichomshtua usingizi ni kitu kizito kikimgandamiza ubavuni.

    “Nini tena Linda?”

    “Siwezi!”

    “Huwezi nini?”

    “Kuvumilia.”



    “Lakini tumekubaliana hakuna tendo la ndoa kati yetu.”

    “Naelewa, lakini nimezidiwa sana, nihurumie Harrison, leo tu, wala haitatokea tena siku nyingine.”

    “Haiwezekani Linda, nilishaweka kiapo.”



    Linda akaanza kulia akimbembeleza Harrison akubali lakini haikuwezekana mwisho akaanza kujieleza kuhusu lengo lake, kwamba hakuwa na nia yoyote ya mali alizokuwa nazo, wala alikuwa havutiwi na umaarufu wake isipokuwa alimpenda kutoka moyoni.

    “Harrison”

    “Naam.”

    “Hivi unajua mimi natoka familia gani?”

    “Ndiyo, familia ya Ford.”

    “Kwa hiyo sina shida na pesa, tunazo nyingi za kutumia mpaka wajukuu zetu.”

    “Najua.”



    “Kwa hiyo sikufuati kwa sababu ya fedha zako bali ninakupenda kutoka moyoni!”

    “Najua lakini hatuwezi kufanya tendo la ndoa, nakubali tuwe marafiki.”



    Linda akajibwaga pembeni kwa hasira na kuanza kulia, Harrison alimbembeleza lakini haikusaidia ikabidi aendelee mpaka asubuhi akililia penzi.Harrison alidamka asubuhi na kuandaa kifungua kinywa, wakanywa pamoja baada ya kuamka na kuoga, kilichofuata



    hapo ikawa ni mazungumzo, Harrison akijaribu kumpa mwenzake ushauri juu ya maisha na kufanya maamuzi sahihi.

    Saa nne kamili Linda aliondoka, wakiwa wamekubaliana kuendelea na urafiki wa kawaida badala ya mapenzi na hivyo ndivyo



    ilivyotokea, kila mwisho wa wiki walikuwa pamoja kiasi cha watu kufikiri kulikuwa na uhusiano zaidi ya kawaida kati yao.

    Harrison alitambulishwa kwenye familia ya Ford na Linda akatambulishwa kwenye familia ya Harrison, wote walifurahia na



    waliwashawishi hata wafikirie kufunga ndoa ili kuimarisha zaidi uhusiano wao lakini kwa Harrison jambo hilo lilionekana haliwezekani.



    “When is your birthday?”(Siku yako ya kuzaliwa ni lini?) Linda alimuuliza Harrison wakiwa wameketi ufukweni maeneo ya Santa Monica wakipunga upepo.

    “Tenth August every year!”(Tarehe kumi mwezi wa nane kila mwaka.)

    “Do you celebrate?”(Huwa unasherehekea?)

    “Yeah, but not too much! And when is yours?”(Ndiyo, lakini siyo sana na yako ni lini?)

    “April twenty eighth! ”(Tarehe ishirini na nane mwezi wa nne.)

    “Do you celebrate?”(Huwa unasherehekea?)

    “So much.”(Sana.)



    Linda alikuwa amefahamu siku ya kuzaliwa Harrison mwanzoni tu mwa urafiki wao baada ya kuchunguza mtandaoni, hakumwambia Harrison chochote na siku hiyo wakiwa wameketi ufukweni ilikuwa ni tarehe kumi mwezi wa nane, kwa sababu ya shughuli nyingi alizokuwa nazo Harrison alikuwa hakumbuki chochote.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya mazungumzo yao yaliyoisha kwenye saa nne hivi usiku, ndipo Linda alishauri wahame kutoka mahali walipokuwa na kuingia ndani sababu ya baridi kali. Wakanyanyuka na kuingia ukumbini ambako Harrison alishangazwa na idadi ya watu kuwa kubwa, jina lake likiwa limeandikwa ukutani na watu wote wakanyanyuka na kushangilia huku wakiimba wimbo wa ‘Happy



    Birthday’ Harrison akapigwa na butwaa, kumbe Linda alishaandaa kila kitu na familia zote mbili zilikuwepo.

    Hakuamini alipomwona mama yake katikati ya watu, akasogea karibu na kumkumbatia kwa furaha huku mama yake akimtamkia maneno ya kumtakia afya njema na maisha marefu. Baadaye watu wote walifika na kumkumbatia wa mwisho kabisa akawa ni



    Linda ambaye alipata nafasi ya kuzungumza ili kuanza rasmi sherehe.

    “Nakupenda Harrison, sikupendi kawaida tu, nakupenda isivyo kawaida na ningefurahi mambo yangekuwa tofauti na yalivyo sasa!



    Hongera kwa kutumiza miaka ishirini na sita.” Alimaliza Linda na kumsogelea Harrison, akampiga busu usoni.



    “Ahsante Linda, nakupe…” Harrison alishindwa kumalizia maneno hayo, machozi yakamlengalenga, upande fulani wa moyo wake ulikuwa unaanza kumpenda Linda lakini alikuwa akipambana nao kwa nguvu zote kwani hakutaka kumsaliti mwanamke aliyempenda ambaye wala hakuwa na habari juu ya penzi hilo.



    “Kuna kitu kidogo kama zawadi yako, ningependa nikupe sasa hivi kabla ya chakula rafiki yangu mpendwa, mabibi na mabwana, wazazi wangu, ndugu na marafiki nimejitahidi kutunza fedha kidogo kidogo kwa muda mrefu ambazo nimezitumia kumnunulia



    Harrison zawadi yake ya siku ya kuzaliwa…” Linda aliongea akiwa amejawa na tabasamu watu wote uwanjani wakageukia upande alikoelekeza mkono wake. Pazia likafunguka.



    Lilikuwa ni gari jeusi, lenye matairi makubwa na likiwa limepambwa vyema ambalo liliendeshwa taratibu kuingizwa katikati ya ukumbi, kila mmoja wao akayasoma maandishi ubavuni “Ranger Rover” mpyaaaaa! Harrison hakuamini, akiwa katika mshangao, Linda alimsogelea na kumkumbatia, kisha kuusogeza uso wake karibu kabisa na wa Harrison.



    HARRISON amepata mafanikio makubwa sana baada ya kuchapisha kitabu kiitwacho Queen of Gorillas ambacho kinamhusu msichana mrembo aliyempiga picha katikati ya pori akiwa amezungukwa na sokwe, alionekana ni kama mnyama wa porini kwa tabia zake zilivyokuwa, hakika msichana huyo alifanana na sokwe kwa kila kitu isipokuwa maumbile.



    Harrison hivi sasa ni milionea wa dola za Kimarekani, anaweza kulinganishwa kabisa na wacheza sinema wa Hollywood. Ameingia kwenye orodha ya watu maarufu wa nchi hiyo na hivi sasa kinachomsumbua sana ni mabinti ambao wengi wanampenda na wanataka kuwa wapenzi wake ili baadaye waolewe naye.



    Akili yake yote ipo kwa msichana aliyemwona porini ambaye ndiye alimwandikia kitabu na kujipatia utajiri, huyu ndiye anataka kurudi porini kwenda kumtafuta ili baadaye aweze kuwa mke wake. Anamuota kila siku, kumuwaza kila mara na anaamini ndoto yake itatimia.

    Akiwa katika fikra hizo anaibuka Linda, msichana kutoka familia tajiri ya akina Ford ambao utajiri wao hauwezi kuisha mpaka kwa wajukuu.



    Msichana huyu anampenda Harrison na amedhamiria kumpata kwa gharama yoyote, anaamini huyu ndiye atakuwa mume wake. Harrison hataki sababu ya mwanamke wake wa msituni.



    Linda anabembeleza kwa muda mrefu lakini anakataliwa na kuombwa awe rafiki wa kawaida, akakubali, ukaribu ukaongezeka siku hadi siku na mwisho wakajikuta wamekuwa kama wapenzi huku Linda akiingia moyoni mwa Harrison taratibu.



    Ni siku ya sikukuu ya kuzaliwa Harrison, Linda anampa zawadi ya ajabu ya gari aina ya Ranger Rover Sport, ya thamani kubwa. Harrison haamini anachokishuhudia na ghafla moyo wake unaanza kumpenda Linda ambaye sasa amemkumbatia, amemsogezea uso, pua zimegusana na baadaye midomo tena mbele za watu, Harrison anakielewa kinachotaka kutokea lakini hana jinsi, ameanza kumpenda Linda.



    “NO!”(hapana) ilikuwa ni sauti ya Harrison kabla ndimi zao hazijagusana, akili yake ilikuwa imerejea tena msituni kwa Malkia wa Masokwe, bado alimpenda msichana huyo kuliko alivyompenda Linda pamoja na utajiri wa familia yake.

    “Why?”(Kwa nini?)

    “We can’t do that before our parents.”(Hatuwezi kufanya hivyo mbele ya wazazi wetu.) Hilo ndilo lilikuwa jibu la Harrison ambalo kwa Linda lilimaanisha kulainika kidogo, kwani tafsiri yake ilikuwa kama wazazi wasingekuwepo walichotaka kufanya kingetendeka.

    “Can we go outside?”(Tunaweza kwenda nje?)

    “Not now, may be later!”(Siyo sasa! Labda baadaye.)



    Linda akasinyaa, hata hivyo alijikaza na kumshika Harrison mkono ili watu wasigundue na kwenda naye moja kwa moja hadi kwenye gari ambako alitamka maneno: “Hii ndiyo zawadi yako” kisha wote wawili wakaingia ndani ya gari, watu wakishangilia na kurudi kinyumenyume wakitoka ukumbini huku MC akiendelea.



    Nje ya ukumbi, kwenye giza kidogo, alichokifanya Linda ni kumwambia Harrison asimamishe gari, akajinyoosha hadi upande wa dereva na kumshika mabegani huku gia ikimuumiza kiunoni lakini hakujali, akamvuta karibu yake na hatimaye midomo yao ikagusana, kilichofuata baada ya hapo ni ambacho Harrison kwa kipindi kirefu alikuwa amekipinga; mabusu.



    “I love you Harrison!”(Nakupenda Harrison.)

    “Nakupenda pia Linda.”

    “Kweli?”

    “Kabisa.”

    “Vipi juu ya yule mwanamke wa msituni?”

    “Nimebadilisha mawazo.”



    Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa penzi lao, Linda akawa amemzidi Harrison ujanja na kumwingiza mtegoni. Alifahamu kabisa alikuwa hapendwi lakini moyoni aliamini kwamba penzi kama ulivyo mmea mwingine wowote, hukua iwapo litaendelea kumwagiliwa na kuwekewa mbolea.



    Kazi ya Harrison sasa ilishakuwa ni utunzi wa vitabu, maana hivyo ndivyo vilikuwa vimempa jina na kipato ambacho hakuwahi kutarajia kuwa nacho, akaanzisha kampuni iitwayo Upgraded Publishing Company Ltd yeye akiwa mkurugenzi. Pamoja na kuandika vitabu pia aliwasaidia waandishi wengine wachanga waliokuwa na miswada yao ambayo ilikuwa haijachapishwa, kuiandaa na hatimaye kuichapisha.



    Linda alifanya kazi kwenye kampuni ya magari ya familia yao, lakini kila siku jioni ilikuwa ni lazima waonane na mara nyingi alilala nyumbani kwa Harrison hasa siku za mwisho wa wiki, mapenzi yalizidi kupamba moto na kila mmoja akamtambulisha mwenzake kwa familia yake, watu wote waliwafurahia na kuwataka wafunge ndoa haraka iwezekanavyo.



    “Lini mnatarajia kufunga ndoa?” Baba wa Linda alimuuliza Harrison siku moja.

    “Bado kidogo.”

    “Fanyeni haraka, kwa muda mrefu nimesubiri sana harusi ya Linda.”

    “Haitapita miezi sita!”

    “Eti Linda ni kweli?”

    “Ni kweli baba.”



    Nusu ya mawazo ya Harrison yalianza kutawaliwa na Linda, lakini nusu yalibaki msituni, karibu kila siku alimfikiria Malkia wa Masokwe akiwa na uhakika kabisa kwamba wala msichana huyo alikuwa hamkumbuki. Ni kweli alitaka kumuoa Linda lakini



    upande mwingine bado alitaka kumuoa Malkia wa Masokwe, mawazo hayo yakamweka njia panda akiwa ameshindwa kabisa kuelewa nini cha kufanya.



    Wakati huohuo, Linda alikuwa taaban kimapenzi, hakuwa tayari kusikia habari ya mwanaume mwingine yeyote, akili yake alishaihamishia kwa Harrison. Hakuwa msichana mwenye tabia mbaya, alijiheshimu na wanaume wengi walitaka kumuoa lakini aligundua kilichowafanya wengi wachukue uamuzi huo ilikuwa ni utajiri wa familia yake, walifikiria mali zaidi kuliko yeye ndiyo maana alipokutana na Harrison alizama moja kwa moja.



    “Sijui nitafanya nini siku ukiniambia unaniacha.”

    “Siwezi kukuacha Linda.”

    “Unasema kweli?”

    “Kabisa.”

    “Mwanamke wako wa msituni je?”

    “Huyo…”

    “Huyo nini?”



    “Tuachane naye!” alijibu Harrison ingawa ukweli wa mambo ni kwamba bado msichana huyo alimtesa, kuna wakati hata alifikiria kumkimbia Linda lakini alishindwa akijua lazima msichana huyo angejiua na familia ya Ford isingemwacha Harrison hai kama tukio hilo lingetokea.



    Miezi saba baadaye, Harrison akiwa katikati ya fikra kati ya wanawake hao wawili, maandalizi ya harusi yalianza, michango kutoka kwa marafiki na familia ikafanyika. Maelfu ya dola yalikusanywa, kampuni maalum ya kuandaa na kusimamia harusi iliyoitwa Los Angeles Wedding Planners ndiyo ilipewa tenda ya kusimamia harusi hiyo haraka ambayo watu wote maarufu nchini Marekani walitarajiwa kuhudhuria ikiwa ni pamoja na rais wa taifa hilo kubwa na lenye nguvu duniani.



    Kwa Linda ilikuwa furaha kubwa lakini kwa Harrison ilikuwa nusu furaha ingawa hakutaka kuonesha wazi akiwa hataki kumvunja moyo mke wake mtarajiwa, bado akili ilikuwa msituni lakini alikosa jinsi ya kujinasua kwa jinsi mambo yalivyokuwa yamepelekwa maana harusi hiyo ilikuwa gumzo kwenye vyombo vya habari, hasa taarifa ziliposambaa kwamba hata mwana wa Mfalme wa Uingereza ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa familia ya Ford alihudhuria.



    “Hivi nampenda kiasi cha kumuoa kweli? Nitaishije maisha ya taabu miaka yote? Kwa nini nisiachane na hili jambo nikaingia msituni kumtafuta mwanamke nimpendaye?” aliwaza Harrison.



    Hakuwa na uwezo wa kuchukua hatua hiyo kwa kuhofia Linda angejidhuru na hilo lingemletea matatizo, hivyo akaendelea kutulia na kuacha mambo yaendelee mpaka siku ikawadia ambayo watu zaidi ya elfu tatu walijaa ndani ya Kanisa la Los Angeles Baptist



    Church kushuhudia harusi hiyo kubwa na ya kifahari ikifungwa.

    Linda aliingia akiwa na msafara wa magari ya kifahari zaidi ya kumi na kuongozwa moja kwa moja kuingia kanisani, Harrison alikuwa hajafika, mpaka nusu saa kabla ya muda wa kufunga ndoa hakuwa ameonekana kanisani. Linda na watu wengine wakaanza kuingiwa na wasiwasi, wazazi wakachanganyikiwa na watu mbalimbali walimfuata mama yake aliyekuwepo kanisani kumuuliza.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Anakuja, nimemwacha nyumbani.”

    “Kweli?”

    “Kabisa.”



    Hali iliendelea kuwa hivyo mpaka zilipobaki dakika tano ndipo muungurumo mkubwa wa pikipiki ukasikika, alikuwa ni Harrison na suti yake nyeusi, jasho likimtoka. Maelezo yake yakawa ni kwamba alikutana na foleni, hivyo kuamua kukodisha pikipiki. Linda alipomwona kanisani, alifuta machozi na furaha ikamjaa.



    Watu wakaanza kuimba nyimbo za sherehe ya ndoa, walinyamaza mchungaji alipoingia na kuanza kuiendesha sherehe hiyo mpaka sehemu ambapo wawili hao walitakiwa kula kiapo na kuvishana pete. Kwanza aliuliza kama kulikuwa na mtu mwenye pingamizi, hakuna aliyejitokeza, hapo ndipo mchungaji akamgeukia Linda.



    “Linda unakubali kuolewa na Harrison awe mume wako katika shida na raha, katika mateso na chuki, umpende na kumheshimu siku zote za…”

    “Ndiyo nakubali.”



    Kanisa likalipuka kwa shangwe na nderemo pia vifijo, kabla mchungaji hajamgeukia Harrison na kumuuliza swali lilelile, badala ya kujibu ili watu washangilie, alibaki kimya kwa kama dakika tatu, ikabidi mchungaji aulize tena huku kanisa zima likiwa kimya.

    “Sikubali!”

    Linda akaanguka chini, Harrison akatoka mbio hadi nje ambako muungurumo wa pikipiki ulisikika akiondoka kwa kasi.





    HARRISON, mtoto wa marehemu Harvey na Skyler, amepata mafanikio makubwa sana baada ya kuchapisha kitabu kiitwacho Queen of Gorillas kinachomhusu msichana mrembo anayeishi na masokwe ndani ya msitu mkubwa wa Tongass.



    Alifanikiwa kumpiga picha msichana huyo mrembo katikati ya pori akiwa amezungukwa na sokwe, akiwa na haiba zote kama mnyama wa porini, hakika msichana huyo alifanana na sokwe kwa kila kitu isipokuwa maumbile.



    Baada ya kuupata utajiri huo, Harrison anaingia kwenye orodha ya watu maarufu wa nchi hiyo na hivi sasa kinachomsumbua sana ni mabinti ambao wengi wanampenda na wanataka kuwa wapenzi wake ili baadaye waolewe naye.



    Miongoni mwa mabinti hao ni Linda, msichana kutoka familia ya kitajiri anayetokea kumpenda sana Harrison na kutaka awe mume wake. Licha ya kumweleza mara kadhaa kuwa hampendi, Linda anamng’ang’ania mpaka baadaye wanakubaliana kufunga ndoa kanisani.



    Siku ya harusi inafika, Linda anatangulia kanisani akiwa amerembwa kama bibi harusi, watu mashuhuri kutoka sehemu mbalimbali wanamiminika kanisani kushuhudia ndoa hiyo lakini mambo yanageuka na kuanza kwenda mrama baada ya Harrison kumkataa binti huyo madhabahuni.



    WAPAMBE wa bwana na bibi harusi pamoja na wazazi wa pande zote mbili walikuwa na kazi ya ziada ya kumpepelea Linda ili arejewe na fahamu huku taratibu za kutafuta gari la kumkimbiza hospitalini zikifanywa kwa kasi.



    “Mlegezeni mkanda wa gauni, mvueni viatu na vitu vyote vinavyombana,” alisema mchungaji, wapambe na wazazi wake wakafanya kama walivyoelekezwa. Kila mmoja alikuwa akihaha kuokoa maisha ya Linda.



    Wakati hayo yakiendelea, kanisa zima lilikumbwa na hali ya sintofahamu, kila mtu akiwa haamini kilichotokea. Minong’ono na sauti za watu wakilia chinichini zilisikika kutoka kila kona ya kanisa, wengine wakilifananisha tukio hilo na filamu ya kusisimua.



    Muda mfupi baadaye, ving’ora vya gari la kubebea wagonjwa (ambulance) vilianza kusikika nje ya kanisa. Manesi wanne waliokuwa na kitanda cha kubebea wagonjwa, walipandisha ngazi za kanisa na kuingia ndani haraka baada ya kupigiwa simu na wazazi wa Linda, waumini wakawapisha wafanye kazi yao ambapo walipitiliza mbiombio mpaka madhabahuni, eneo Linda alipodondokea na kupoteza fahamu.



    Wakasaidiana kumuinua Linda na kumlaza kwenye kitanda cha magurudumu, sekunde chache baadaye wakawa wanakisukuma kitanda kile kwa kasi, Linda akiwa amelala katika hali ya kupoteza fahamu. Walitoka mpaka nje, milango ya ambulance ikafunguliwa, mpambe wa bibi harusi na mama mzazi wa Linda pamoja na wale manesi, wakaingia na safari ya kuelekea hospitali ikaanza kwa kasi kubwa.



    Waumini waliosalia kanisani walitoka nje na kulisindikiza gari lile kwa macho mpaka lilipopotea kabisa, wakajikusanya vikundivikundi na kuanza kujadili kilichotokea.



    “Jamani namuonea huruma binti wa watu! Kweli fedha haiwezi kununua mapenzi.”



    “Huyu si juzijuzi tu alimtunukia zawadi ya gari la kifahari aina ya Range Rover mumewe mtarajiwa siku ya ‘birthday’ yake?”

    “Ndiyo! Bibi harusi kwao mambo safi, si unamjua vizuri baba yake? Anatisha kwa utajiri.”

    “Sasa kwa nini amemkimbia bibi harusi? Si bora angekataa tangu mapema?”

    “Inawezekana Linda ndiyo alikuwa analazimisha mapenzi.”

    “Hamna kitu kama hicho, yule bwana harusi atakuwa amerogwa, siyo bure.”

    “Wanaume wabaya sana, sasa kama alikuwa hamtaki kwa nini alikubali kuja kanisani?”



    Kila mtu alikuwa akizungumza lake kanisani pale lakini hakuna aliyeweza kuubadili ukweli kuwa Harrison alimkimbia Linda madhabahuni.

    ***

    Muungurumo wa pikipiki kubwa ulisikika nje ya nyumba ya Rogers Presley, kijana wa Kimarekani aliyekuwa akifanya kazi kwenye Hospitali ya Oklahoma Medics.



    “Nani tena huyo anayekuja kwa kasi kama yupo kwenye mashindano ya pikipiki?” alijiuliza Rogers wakati akifunua pazia la sebuleni kwake na kuchungulia nje.

    “Haaa! Harrison? Ni wewe?”

    “Ni mimi Rogers, yaani hapa sijielewi kabisa.”

    “Kwani vipi? Leo si ndiyo siku yako ya kufunga ndoa na Linda?”

    “Ndiyo Rogers lakini mambo yamekuwa ndivyo sivyo, ngoja nitakusimulia kila kitu,” alisema Harrison huku akihema kwa nguvu. Rogers akamshika mkono na kuingia naye hadi ndani, wakakaa sebuleni huku Rogers akiwa na hamu kubwa ya kutaka kujua kilichotokea.



    Harrison na Rogers walikuwa ni marafiki tangu wakiwa watoto wadogo, walisoma pamoja shule ya msingi na baadaye sekondari ingawa baadaye walitengana baada ya Rogers kwenda kusomea uuguzi katika Chuo Kikuu cha Havard nchini humo. Urafiki wao uliendelea hata baada ya kila mmoja kumaliza masomo na kuanza kazi.



    “Rogers! Wewe ni rafiki yangu mkubwa sana.”

    “Ndiyo najua Harrison.”

    “Nadhani unafahamu kila kinachoendelea kati yangu na Linda.”

    “Ndiyo najua Harrison lakini niliposikia unafunga naye ndoa, nilijua umeamua kurudisha moyo wako nyuma.”

    “Nimejitahidi sana kuulazimisha moyo wangu lakini kiukweli simpendi kabisa Linda.”

    “Ni sawa Harrison, lakini bado hujaniambia nini kilichotokea.”

    “Nimefanya dhambi kubwa sana leo, ooh! Linda nisamehe,” alisema Harrison huku akianza kutokwa na machozi. Ilibidi Rogers amsogelee na kuanza kumtuliza huku akimsihi amueleze kilichotokea ili wajue nini cha kufanya.

    “Nimemkana Linda madhabahuni na kumkimbia.”

    “Whaaaaat? Are you out of your mind?”

    (Niniiii? Umechanganyikiwa?) aliuliza Rogers huku akiwa amemtumbulia macho Harrison.

    “Nimefanya kosa kubwa sana, najua kila mmoja atanichukia lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kufanya hivi nilivyofanya,” alisema Harrison huku akizidi kububujikwa na machozi.

    “Sasa kwa nini umefanya hivyo Harrison?”

    “Rogers, nampenda sana malkia wa masokwe, nadhani hata wewe unalijua hilo. Sipo tayari kumpoteza na kumuoa mwanamke mwingine yeyote. Naomba msaada wako.”



    Rogers alikaa kimya kwa zaidi ya dakika mbili, akawa anatafakari kwa kina kile alichokisikia, mwisho akashusha pumzi ndefu na kumgeukia Harrison.



    “Najua jinsi unavyojisikia Harrison lakini kwa kuwa wewe ni rafiki yangu, nipo tayari kukusaidia.”

    “Utanisaidiaje Rogers? Nataka kwenda kuishi na malkia wa masokwe.”

    “Najua familia ya akina Linda haiwezi kukubali jinsi ulivyomdhalilisha binti yao. Baba yake anaweza hata kutuma watu waje kukuua. Namjua vizuri yule mzee. Sasa hapa inabidi tucheze mchezo wa kimafia.”

    “Nipo tayari kwa lolote utakalolisema Rogers, nakutegemea wewe.”



    “Inabidi tupate maiti moja ya kiume inayoshabihiana na wewe kisha nitakuelekeza nini cha kufanya.”

    “Maiti? Halafu itakuwaje?”



    “Nitakuelekeza cha kufanya, ngoja niende kuzungumza na mtu wa mochwari pale hospitalini ninapofanyia kazi kisha nitakuelekeza nini cha kufanya,” alisema Rogers na kusimama, akamuaga Harrison na kutoka nje mpaka mahali anapopaki gari lake. Akaliwasha na kuondoka kwa kasi.



    Harrison alibaki ameduwaa akiwa hajui rafiki yake huyo alikuwa amefikiria mpango gani kichwani mwake. Baada ya takriban dakika thelathini, Rogers alirejea na kuliingiza gari lake mpaka sehemu ya maegesho, akatoka na kumuita Harrison wasaidiane kubeba maiti iliyokuwa kwenye buti.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kuiingiza ndani, Rogers alimwambia Harrison avue kila kitu, kuanzia suti yake ya harusi iliyonunuliwa kwa bei mbaya mpaka viatu. Akapewa nguo nyingine za kuvaa kisha wakaanza kusaidiana kuivalisha maiti ile zile nguo za Harrison. Baada ya muda wakawa wameshamaliza.



    UTAJIRI mkubwa alioupata Harrison, mtoto wa marehemu Harvey na Skyler, umekuja baada ya kijana huyo kuchapisha kitabu kiitwacho Queen of Gorillas kinachomhusu msichana mrembo anayeishi na masokwe ndani ya msitu mkubwa wa Tongass.



    Harrison anafanikiwa kumpiga picha msichana huyo mrembo katikati ya msitu wa Tongass akiwa amezungukwa na masokwe, akiwa na haiba zote kama mnyama wa porini.



    Hata hivyo, licha ya kuwa na tabia kama mnyama, Harrison ambaye sasa ameshaingia kwenye orodha ya watu maarufu wa nchi hiyo, anatokea kumpenda sana kiasi cha kuwakataa wasichana wote waliokuwa wanataka kuolewa naye.



    Penzi alilonalo Harrison kwa malkia wa masokwe, linamfanya amkatae Linda, msichana kutoka familia tajiri aliyetokea kumpenda sana. Anamkana madhabahuni siku ya harusi yao kisha kukimbia kuelekea kusikojulikana kwa kutumia pikipiki kubwa.



    “NIWEKE wazi Rogers, unataka kufanya nini?”

    “Tulia Harrison, si unataka msaada kutoka kwangu?”

    “Ndiyo.”

    “Basi tulia uone nitafanya nini, wasiwasi wa nini?”

    “Inatakiwa tufanye haraka, ndugu zake Linda wanaweza kuja hapa ikawa balaa,” alisema Harrison kwa hofu, Rogers akaendelea kushikilia msimamo wake wa kumtaka atulie.

    Baada ya kumaliza kuivalisha maiti ile nguo alizokuwa amevaa Harrison, Rogers alimwambia kuwa inatakiwa lipatikane gari la kununua au la kukodi haraka iwezekanavyo.

    “Sasa tutapata wapi gari?”

    “Kwani wewe huna fedha za akiba?”

    “Ninazo lakini kadi zangu za benki na nyaraka zote nimeviacha nyumbani na siwezi kurudi.”

    “Basi usijali, kwa kuwa nimeamua kukusaidia nitakupa lile gari langu ambalo silitumii.”

    “Halafu nini kitafuata?”

    “Nataka tutengeneze ajali ambayo itawafanya watu wote waamini kwamba umekufa.”

    “Nimekufa? Rogers! Huoni kama ni hatari?”

    “Hiyo ndiyo mbinu pekee itakayokufanya uendelee na maisha ambayo umeyachagua wewe mwenyewe.”

    “Sasa mbona sura yangu na hii maiti hazifanani?”

    “Hiyo mbona kazi ndogo sana,” alisema Rogers huku akivaa ‘gloves’ mikononi mwake. Akafungua kabati lililokuwa ukutani na kutoa chupa kubwa iliyokuwa na maandishi yaliyosomeka Concentrated Hydrochloric Acid.

    Rogers alisogea mpaka pale kwenye ile maiti, akafungua mfuniko wa chupa iliyokuwa na tindikali na kuimwagia ile maiti usoni. Katika hali ambayo Harrison hakuitegemea, ndani ya sekunde chache alishangaa kuona sura ya ile maiti ikiharibika kiasi cha kutotambulika.

    Rogers alipomaliza, alimwelekeza kuwa wasaidiane kuibeba ile maiti mpaka kwenye gari. Harrison alifanya kama alivyoelekezwa, wakaibeba na kuitoa mpaka sehemu ya maegesho ya magari, wakaiingiza na kuikalisha ndani ya gari dogo aina ya Corolla lililokuwa na vioo vyenye rangi nyeusi (tinted). Wakaipakiza na pikipiki ya Harrison.

    “Tutakwenda mpaka kwenye daraja la Miami, pale nitakuelekeza cha kufanya,” alisema Rogers huku akikanyaga mafuta na kuingiza gia, gari lao likawa linasafiri kwa kasi kubwa kuelekea Miami. Safari haikuwa nyepesi kutokana na umbali uliokuwepo kutoka Oklahoma mpaka Miami.

    Baada ya kusafiri kwa saa nyingi, hatimaye walifika kwenye daraja kubwa la Miami lililokuwa likipita juu ya bahari na kuunganisha upande mmoja na mwingine. Rogers alitafuta sehemu nzuri, akapunguza mwendo na kusimamisha gari. Akamuelekeza Harrison nini cha kufanya.

    “Inabidi tusaidiane kuiteremsha pikipiki na kuiweka katikati ya barabara, kisha tutapita na gari juu yake ili ionekane umegongwa na gari ukiwa unaendesha pikipiki.”

    “Halafu hii maiti tutaifanyaje?”

    “Tutaiburuza kidogo barabarani kisha tutaitupia baharini.”
“Watu wakituona si itakuwa balaa?”

    “Muda huu hakuna watu wengi wanaoitumia hii barabara.”

    Baada ya kusema vile, waliteremka haraka garini na kuishusha pikipiki.

    Rogers akarudi ndani ya gari na kukanyaga mafuta kwa nguvu, akaenda kuigonga ile pikipiki na kuifanyaiharibike vibaya.

    “Zoezi la kwanza limekamilika, bado la pili,” alisema Rogers huku akifungua mlango wa nyuma wa gari. Wakasaidiana kuitoa ile maiti, wakaiburuza kwenye kingo za barabara na kuifanya ipate majeraha mengine, walipomaliza wakasaidiana kuitosa baharini. Kishindo kikubwa kikasikika; chubwii!

    Harakahara walirejea kwenye gari, wakaingia na kuondoka kwa kasi kubwa bila kuonekana na mtu yeyote.

    ***

    “Hapa ni wapi?” aliuliza Linda baada ya kurejewa na fahamu zake na kujikuta akiwa ametundikiwa dripu ndani ya chumba kilichokuwa na rangi nyeupe, akiwa amefunikwa mashuka meupe.

    “Hapa ni wapi na nimefikaje?” aliuliza tena Linda, mama yake aliyekuwa amekaa pembeni yake akitokwa na machozi, alimsogelea na kumshika shavuni kwa upendo.

    “Upo hospitalini mwanangu. Ulipatwa na mshtuko ukiwa kanisani.”

    Baada ya kusikia kauli ile, Linda alianza kuvuta kumbukumbu, akakumbuka vizuri kuwa siku hiyo alikuwa kanisani akijiandaa kufunga ndoa na Harrison.

    “Mama, mume wangu Harrison yuko wapi? Leo si ndiyo siku ya harusi yetu?” aliuliza Linda huku akionekana kama asiyekumbuka vizuri kilichotokea.

    Mama yake alishindwa cha kumjibu, akawa anajifuta machozi kwa uchungu. Hali ile ilimfanya Linda atulie kwa dakika kadhaa, akakumbuka vizuri kilichotokea.

    “Harrison! Harrison kipenzi changu, kwa nini umenikimbia kanisani? Kwa niniii?” alisema Linda huku akianza kuangua kilio upya kama mtu aliyeletewa taarifa za msiba.

    Licha ya mama yake kujitahidi kumbembeleza, Linda hakutulia, aliendelea kulia kwa nguvu, mara akachomoa sindano ya dripu aliyokuwa amechomwa mkononi, akasimama wima kama mwendawazimu.

    “Namtaka Harrison wangu, nataka anioe! Bila hivyo naenda kujiua,” alisema Linda huku akianza kutimua mbio kuelekea upande kulipokuwa na lifti ya kupandia ghorofani.

    “Simama Linda, bado haujapona mwanangu, utapata matatizo zaidi,” alisema mama yake Linda lakini binti yake huyo hakumsikia.

    Alilishika gauni lake la harusi kwa mkono mmoja ili apate uhuru wa kukimbia vizuri. Kelele alizokuwa anapiga mama yake, ziliwashtua manesi na madaktari, wote wakaanza kutimua mbio kuelekea kule Linda alikokuwa anakimbilia.

    Walichelewa kwani Linda alishaingia kwenye lifti na kujifungia, akabonyeza kitufe ukutani, lifti ikaanza kupanda kuelekea juu.

    Ilimpeleka mpaka kwenye ghorofa ya 33, juu kabisa ya jengo lile la hospitali. Alipoteremka kwenye lifti, alipanda ngazi chache na kutokezea upande wa juu kabisa, kwenye paa la ghorofa lile refu.

    Baada ya dakika chache, mama yake akiwa ameongozana na manesi na wauguzi, nao walipanda mpaka kule Linda alikokimbilia.

    “Ishieni hapohapo, mkisogea hata hatua moja mbele najirusha mpaka chini nife,” alisema Linda kwa sauti ambayo haikuwa na masihara hata kidogo.

    Ilibidi wote wasimame huku wakiwa hawaamini walichokuwa wanakiona mbele ya macho yao. Linda alikuwa amesimama ukingoni kabisa mwa ghorofa lile, mahali ambapo hata upepo wenye nguvu ukipiga, ungeweza kumuangusha mpaka chini.

    “Noo! Noo Linda, tupo tayari kufanya chochote unachokitaka,” alisema mama yake huku akipiga magoti.

    “Namtaka Harrison wangu, nataka mkamtafute mahali popote alipo na kumleta hapa, vinginevyo najirusha mpaka chini.”

    “Harrison atapatikana mwanangu lakini nakuomba usogee huku tulipo, hapo ni hatari sana mwanangu, nakuomba Linda,” alisema mama Linda huku akizidi kulia kama mtoto mdogo.

    Linda hakutaka kuelewa chochote, alishikilia msimamo wake kuwa Harrison atafutwe mahali popote alipo na kuletwa pale juu ya ghorofa, vinginevyo atajirusha hadi chini.

    Muda mfupi baadaye, wanausalama na madaktari wengine walifika kule juu ya ghorofa, wakawa wanamsikiliza Linda anachokitaka.

    “Kwa hiyo tukimleta Harrison utakubali kurudi huku tulipo na kuteremka hadi chini kwa usalama?”

    “Ndiyo! Nampenda sana Harrison, sipo tayari kuishi bila yeye,” alisema Linda huku akilia kwa uchungu.



    HALI ya sintofahamu imetanda kwenye Hospitali ya Oklahoma Medics baada ya Linda, mtoto wa tajiri maarufu nchini Marekani kutishia kujiua kwa kujirusha kutoka juu ya ghorofa refu akishinikiza Harrison, mchumba wake aliyemkimbia kanisani wakati wakitaka kufunga ndoa, atafutwe.



    Linda amedhamiria kujiua na haoneshi masihara hata kidogo, jambo linalozidi kuwatia hofu mama yake, manesi, madaktari na watu waliofika eneo la tukio. Anataka kitu kimoja tu, Harrison atafutwe na kuletwa pale alipo ili wafunge naye ndoa, sharti linaloonekana kuwa gumu kwani mwanaume huyo alishaonesha kwamba hamhitaji na ndiyo maana alimkimbia kanisani muda mfupi kabla ya kufunga ndoa.



    Upande wa pili, Harrison kwa kushirikiana na rafiki yake Rogers, wanatumia mbinu za hali ya juu na kutengeza ajali ili ionekane kwamba mtunzi huyo wa kitabu cha malkia wa masokwe amefariki kwenye ajali wakati akimkimbia Linda. Akili ya Harrison ipo kwa msichana mrembo anayeishi na masokwe ndani ya msitu mkubwa wa Tongass.



    Kwa mara ya kwanza alifanikiwa kumpiga picha msichana huyo mrembo katikati ya msitu wa Tongass akiwa amezungukwa na masokwe, akiwa na haiba zote kama mnyama wa porini. Moyo wake ukatokea kumpenda licha ya hali aliyokuwa nayo na sasa anawakataa wasichana wote wanaotaka kuolewa naye, akiwemo Linda. Ndoto zake ni kumuoa malkia wa masokwe.



    “HAPA tukitaka kutumia nguvu tutaharibu kila kitu.”

    “Sasa tutafanyaje?”

    “Mimi nafikiri tumtimizie anachokitaka. Inawezekana kabisa Harrison akapatikana na kuletwa hapa,” maafisa wawili wa usalama wa Hospitali ya Oklahoma Medics walikuwa wakijadiliana wakiwa eneo la tukio, juu kabisa ya ghorofa.

    Bado Linda alikuwa amesimama kwenye ukingo wa ghorofa lile, akiwa sentimeta chache kutoka mwisho wa ghorofa. Wakati wakiendelea kujadiliana, waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, zikiwemo runinga na redio waliwasili juu ya ghorofa lile baada ya kupata taarifa juu ya tukio lililokuwa linataka kutokea.

    Wakati waandishi hao wakianza kuandaa vifaa vyao zikiwemo kamera na vinasa sauti kwa ajili ya kunasa tukio lile, baba mzazi wa Linda, mzee Ford naye aliwasili huku akitiririkwa na jasho mwili mzima. Mkewe alipomuona alimkimbilia na kuanza kulia kwa sauti.

    “Linda anataka kujiua, fanya chochote kumuokoa mwanangu,” alisema mama Linda huku akiwa amekumbatiana na mumewe. Ilibidi mzee huyo aliyekuwa anasifika kwa kumiliki utajiri mkubwa ajaribu kuzungumza na mwanaye.

    “Nakuomba mwanangu, rudisha moyo nyuma. Maisha yanawezekana hata bila Harrison, chondechonde Linda.”

    “Siwezi baba, nataka Harrison akatafutwe haraka iwezekanavyo, bila hivyo nitajirusha mpaka chini,” alisema Linda huku naye akibubujikwa na machozi.

    Baba yake alipojaribu kupiga hatua moja kumsogelea, Linda alizidi kusogea ukingoni mwa ghorofa, hali iliyofanya wote waliokuwa eneo lile kupiga kelele kwa woga huku wakiwa wameshika vichwa vyao.

    “Linda!”

    “Abee baba.”

    “Harrison akipatikana hutajiua?”

    “Nakuahidi baba, nataka japo nimuone tu na anitamkie kwamba ananipenda, bila hivyo maisha yangu hayana maana yoyote.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati akisema hivyo, tayari waandishi wa habari walikuwa wakimrekodi huku picha nyingi zikipigwa. Lilikuwa ni tukio la aina yake lililozigusa hisia za wengi nchini Marekani.

    “Harrison! Harrison! Mahali popote ulipo, nakuomba uje haraka kwenye Hospitali ya Oklahoma, mwanangu anataka kujirusha kwenye ghorofa kwa ajili yako, nakuomba sana uyanusuru maisha ya binti yangu, nipo tayari kukupa chochote unachokitaka,” alisema baba Linda mbele ya kamera za waandishi wa habari kutoka vituo mbalimbali vya runinga.

    Mkewe naye alipewa nafasi ya kuzungumza lakini kutokana na uchungu aliokuwa anauhisi, alishindwa kuongea na kuishia kulia kwa kwikwi. Habari zile zikasambaa kama moto wa kifuu, runinga ya CNN ikawa ya kwanza kuirusha habari ile moja kwa moja kutoka eneo la tukio. Hali ya sintofahamu ikatawala kila sehemu.

    Baba Linda aliendelea kuzungumza kwenye vyombo vya habari huku akiahidi donge nono la dola za Kimarekani milioni hamsini kwa yeyote atakayefanikiwa kumshawishi Harrison afike eneo lile. Watu katika mitaa mbalimbali walijikusanya kwenye vikundi vidogovidogo wakijadiliana juu ya tukio lile.

    “Kuna watu wengine wana mapenzi mpaka shetani anayaogopa. Yaani huyu binti yupo tayari kufa kwa sababu ya mwanaume?”

    “Alimpenda sana lakini bahati yake mbaya. Unajua jamaa amemkimbia kanisani?”

    “Kamkimbia kanisani kivipi?”

    “Walikuwa wafunge ndoa leo, si unamuona huyu binti amevaa gauni la harusi? Sijui kumetokea nini jamaa kamuacha kwenye mataa.”

    “Sasa amefikaje juu ya ghorofa la hospitali?”

    “Baada ya kukimbiwa kanisani alipoteza fahamu ndiyo akaletwa hapa, alipozinduka ndiyo akakimbilia huku juu ya ghorofa.”

    “Aisee! Tukio linasisimua sana hili, utafikiri filamu?”

    “Wasipokuwa makini anaweza kweli kujiua huyu, ameshachanganyikiwa,” watu waliokuwa wanatazama runinga walikuwa wakijadiliana wakati wakiendelea kutazama tukio la Linda kutaka kujirusha kwenye ghorofa.

    ***

    Einsten Duke, mwanaume wa makamo aliyekuwa akiyaendesha maisha yake kupitia kazi ya uvuvi kwenye Bahari ya Atlantic, alikuwa akitegesha nyavu kwenye bahari tayari kwa kazi ya uvuvi. Kwa kuwa ilikuwa ni majira ya joto, hakuwa akienda mbali na ufukwe kwani samaki walikuwa wengi sana pembezoni mwa bahari.

    Wakati akiendelea na kazi ya kutega nyavu jirani na daraja la Miami, alishtuka baada ya kuona kitu kinaelea kwenye maji.

    “Yule siyo mtu kweli? Hebu nisogee,” alisema Duke huku akigeuza boti ndogo ya uvuvi na kusogea jirani na pale alipoona kile kitu mithili ya mtu kikielea.

    “Mungu wangu! Ni binadamu! Inaonesha amepata ajali na kuangukia huku,” alisema huku akiuchunguza mwili ule. Haraka alitoa simu yake na kupiga namba 911! Aliwaeleza polisi kila kitu alichokiona ambapo baada ya dakika chache ving’ora vya magari ya polisi vilianza kusikika sambamba na boti za uokoaji.

    Wakiwa juu ya daraja, polisi walistuka baada ya kuona pikipiki kubwa ikiwa imeharibika vibaya katikati ya barabara. Haraka walisimamisha magari yao na kuteremka, wakaanza kuangalia kilichotokea.

    “Inaonesha kuna mwendesha pikipiki amegongwa na gari,” alisema askari mmoja akiwaambia wenzake, harakaharaka eneo lote la ajali likazungushiwa utepe maalum wa kuzuia watu wasiohusika kusogea.

    “Msamaria mwema aliyepiga simu ameelekeza kuwa ameona mwili wa mwanaume ukielea baharini jirani na daraja hili.”

    Wakati wakiendelea kujadiliana, walisogea kwenye kingo za daraja na kuchungulia chini ambapo waliwaona wenzao wa kikosi cha uokoaji majini wakisaidiana na yule msamaria mwema, Duke kuopoa mwili uliokuwa unaelea baharini.

    Waandishi wa habari nao tayari walishapata taarifa zile, wakafika eneo la tukio haraka na kuanza kurekodi kila kilichotokea. Kilichowashangaza wengi, mwili wa mwanaume yule ulikutwa ukiwa umevaa suti ya harusi, harakaharaka watu wakaanza kuunganisha matukio.

    Kilichofanya kazi ya kuutambua mwili ule iwe ngumu ni kuharibika vibaya kwa sura ya marehemu. Hata hivyo, pikipiki iliyokutwa barabarani ilisaidia kupata mwanga wa taarifa za marehemu yule.

    “Haaa! Ile si ndiyo pikipiki aliyokuwa anaitumia Harrison?”

    “Mh! Mi mwenyewe nahisi ndiyo aliyoitumia kumkimbia bibi harusi kanisani.”

    “Unataka kusema Harrison amepata ajali na kufa?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog