Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

CHOZI LA MWISHO - 3

 





    Simulizi : Chozi La Mwisho

    Sehemu Ya Tatu (3)



    nikutanapo na wewe...nipe japo kwa leo tu, " jirani yangu alionesha amedhamilia.

    "Haiwezekani kwanza naomba utoke ndani mwangu kwa hiyali

    yako, lakini ukikaidi nitakutoa kwa nguvu," nilimtisha ili aondoke.

    "Jaribu kama aibu haijakurudi kila mtu mtaani atajua na nitajinadi

    kwa sauti ya juu kuwa umetembea na mimi na kunidanganya

    kunipa hela lakini umeninyima. Sijui mume wangu utamwambia nini

    na mkeo anayekuamini utamwambia nini na hao majirani

    utawaambia nini, jaribu uuone moto wa tipa," Sabina alikuja juu mpaka akanitisha.

    "Lakini jirani mbona unataka kuniadhiri tatizo nini, sema unataka

    kiasi gani ili tulimalize," ilibidi niwe mpole kuona mke wa jirani

    yangu amepania alikuwa hatanii.

    "Baba Shikilwa ningekuwa na shida ya fedha ningekwambia wala

    nisingekuja na nguo moja, lakini kumbuka ni wewe ndiye uliyenikubalia sasa iweje unigeuke au ulitaka kunipima?"

    "Hapana jirani, nilijua ni utani wetu wa kila siku."

    "Basi leo si utani ni kitu kilichokuwa kweli, nipe haki yangu niwahi kabla usiku haujawa mkubwa usisababishe nikalala hapa itakuwa habari nyingine usitake kuyafanya mambo yawe makubwa. Jambo la watu wawili lisiwe la wengi najua aibu itakuwa kwetu wote. Kwangu mimi nipo tayari kwa lolote hata kuachika la muhimu nalinda hadhi yangu huwezi kuuona mwili wangu uniache hivihivi."

    Mmh! Mambo yalikuwa mazito nilishindwa nifanye nini nilijikuta nakumbuka matukio mengi ya wanawake tokea dunia ilivyoumbwa. Ni mwanamke ndio aliyesababisha wanadamu tuishi maisha ya tabu, hata sababu ya baba yetu Adamu kufukuzwa kwenye bustani ya Aden kwa ajiri ya mwanamke ambaye ni mama yetu Hawa.

    Pia hata Samson mwanamume mwenye nguvu kuliko wote waliowahi kuishi chini ya jua, alidanganywa na mkewe Delila na kumsababishia matatizo makubwa na ndio sababu ya mauti yake. Hata mwelekeo wa bondia mashuhuri duniani Mike Tyson alipoteza mwelekeo sababu ya hao hao wanawake.

    Nilijiona nipo kwenye mtihani mzito juu ya kuyashinda majaribu

    ya shetani. Nilijaribu kumbembeleza ninavyojua lakini hakuna kilichoeleweka. Niliona heri lawama kuliko fedhea nilimkubalia ili aniondokee kwa kuwa nilikuwa sina jinsi. Nilizungumza kwa sauti ya chini ya huzuni:

    "Sina jinsi, lakini naomba iwe siri."

    "Nimekwisha kueleza labda siri hii uiseme wewe."

    Ndani ya miaka miwili toka nimuoe mke wangu kipenzi Minza nilijikuta nikivunja kiapo cha ndoa cha kwenda nje ya ndoa kwa shinikizo. Kweli nimeamini wanawake wengine ni mashetani wenye sura za kibinadamu wanaojali matamanio ya miili yao bila kuangalia utu wa mtu hata

    kutoziheshimu ndoa zao.

    Nilijikuta nikiivunja amri ya sita na mke wa jirani yangu huku

    moyo kwa ndani ukilia.Nilikuwa sina tofauti na baba yetu Adamu

    pale alipolazimishwa kula tunda walilokatazwa na Mungu.Tukiwa katikati ya dimbwi la mahaba mara mke wa jirani yangu alinisukuma, nijikuta nashtuka na kumuuliza:

    "He! Nini tena?"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Tumbo...tumbo....tumbo...mama nakufa," kilio kile kilinifanya nione nimeimgia kwenye balaa lingine.

    “Vipi?” Nilimuuliza huku nikitetemeka.

    “Jirani nakufa tumbo linanikata kama nimekatwa utumbo kwa ndani, niwahishe hospitali nakufa miye jamani…”

    Nilinyanyuka haraka na kupitia bukta hata bila nguo nyingine ya ndani na kukimbilia dukani. Saa ya ukutani ilionyesha ni saa tano na nusu usiku.

    Kila sehemu iliyokuwa na duka la dawa palikuwa pamefungwa,

    sikuwa na jinsi nilikimbia kwenye hospitali ya kulipia. Nilikuta

    wamerudisha mlango, niligonga huku jasho likinitoka na kutweta.

    "Ingia sukuma mlango," sauti ilitoka ndani ya hospitali, nilisukuma

    mlango na kuingia ndani. Niliwakuta kina dada wakiwa wamejiegemeza kwenye meza.

    "Karibu kaka tukusaidie nini! Mbona unahema hivyo?"

    "Nimetokea mbali kidogo."

    "Ehe! Una shida gani?"

    "Nataka dawa ya tumbo."

    "Nani anaumwa?"

    "Mmm..ke..hapana...dada yangu," nilijikuta nikibabaika.

    “Kwa nini usimlete hospitali?”

    “Kwanza nilitakiwa nimpe huduma ya kwanza ndipo nimlete hapa,” nilidanganya.

    "Tumbo linauma vipi?"

    "La kukata," nilijibu bila kujua tumbo la jirani linauma vipi.

    "Mpatie dawa ya tumbo la kukata," dada aliyekuwa amekumbatia

    kitabu kikubwa alimwambia mwenzie.

    "Dozi au nusu dozi?"

    "Jamani mbona maswali hivyo nyinyi nipeni dawa mnayoona

    itanisaidia."

    Nilipewa dawa na kulipa pesa niliondoka mbio kurudi nyumbani. Nilijikuta nikitweta ovyo njiani na kusikia vichomi, yote ilitokana na kutokupenda kufanya mazoezi. Lakini sikusikiliza kichomi, niliendelea kukimbia kuwahi nyumbani. Nilikimbia bila kupumzika hadi nyumbani, nilipofika kabla ya kuingia ndani

    nilisimama nje nikiwa nimeinama nikihema na jasho liliendelea

    kunivuja kama maji.

    Baada ya kifua kutulia kidogo nilingia ndani hadi chumbani

    nilipomuacha Sabina mke wa jirani yangu juu ya kitanda. Nilimkuta

    katulia nikiamini amepitiwa na usingizi labda tumbo limetulia.

    Nilijua kama tumbo limetulia ni muda muafa wa kumuamsha ili kumtoa

    akalale kwake hata kama litamrudia atakuwa nyumbani kwake. Alikuwa

    amelala akiwa bado amejitandaza kitandani akiwa mtupu kama

    nilivyo muacha.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilimsogelea na kumwita jina lake kwa sauti ya chini karibu na sikio lake:

    "Jirani...jirani...Sabina...Sabina...amka nimeisha leta dawa."

    Hakukuwa na jibu lolote wala kujitikisa, nilipomtikisa alikwenda mzima mzima kitu kilichonishangaza. Nilipatwa na wasiwasi amekuwaje nilipo mshika mkono nimkalishe ili mniomnyeshe dawa. Lakini ajabu mkono ulikuwa wa baridi na umelegea kama mlevi aliyelishwa dawa za kulevya.

    Shingo ya Sabina ilikuwa imeangukia pembeni, kitu kilichozidi kunipa wasiwasi. Wazo liliniijia nimpime mapigo ya moyo, niliweka sikio kifuani hapakuwa na mapigo ya moyo. Sikuamini wazo lililoniijia huenda Sabina amefariki, lakini sikukubaliana nalo.

    Mwili ulikuwa umepoa kabisa nilipojaribu kuangalia macho yake yalikuwa yamepoteza nuru. Ukweli uliokuwa mbele yangu haukuwa mwingine zaidi ya kutambua Sabina mke wa jirani yangu amefariki. Nilijikuta nivuja jasho kama nimenyeshewa na mvua, nilijikuta nikitetemeka na kujiuliza nitafanya nini ili kuuficha ushahidi.

    Sauti ya mke wangu niliisikia masikioni ikisema maneno ambayo

    alinieleza siku niliyokuwa nikimsindikiza akienda kwao, siyo jana ila

    ilikuwa wakati akienda kujiandaa kujifungua mtoto wetu Shikilwa:

    "Mume wangu nakuamini kwa asilimia mia, lakini angalia wanawake wana hila mbaya, yashinde majaribu ya shetani. Sipendi kusikia kuondoka kwangu umekosa uaminifu, napenda nilivyokuacha ndivyo nitakavyo kukuta nakupenda sana mume wangu.

    “Nitaendelea kukupenda hata ukiwa mbali nami upendo wangu ni wa moyoni si wa mdomoni. Nitaendelea kuwa muaminifu ndani ya ndoa yetu nikiwa mbali au karibu.

    “Naomba uniahidi mpenzi wangu kunilindia mwili wangu na moyo wangu na heshima yangu ili niwe juu siku zote mbele ya wanawake wenzangu."

    Nilijikuta nikipayuka kwa sauti:

    "Naomba unisamehe mke wangu kweli nimekubali wanawake wana hila mbaya, leo nimekuwa kama Samson mauti yananisubiri. Nitahukumiwa bila kosa ...Oooh maskini mke wangu...Oooh, maskini mwanangu kitanzi kinaiita sina ujanja hila zilizo mshinda baba yetu Adamu na Samsoni ndizo leo zinanihukumu leo."
    ***
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Nilijikuta nikitangatanga kama kuku anayetaka kutaga, muda ulikatika bila kujua nitafanya kitu juu ya mwili wa jirani yangu uliokuwa umelala kitandani. Nilijifikiria nitakaa na maiti ya mke wa mtu mpaka saa ngapi? Nilijiuliza akitafutwa nitasemaje?

    Wasi wasi wangu inawezekana kuna mtu alimpa siri yake kuwa anakuja kwangu, akichelewa kurudi lazima atajua amelala kwangu. Na zikipita siku lazima maiti itaanza kualibika na kutoa harufu kibaya, kingine mke wangu atarudi siku ya tatu toka siku ile.

    Nilijikuta nakuwa kwenye mtihani mzito usio na majibu nilijua maiti kama ikikutwa ndani mwangu lazima nitanyongwa. Sikuwa na ujanja nilijiuliza nitamueleza nani siri ile ili anielewe, bora asingekuwa mke wa mtu ningeweza kwenda polisi kutoa taarifa za tukio lile ambalo lazima lisingenitia hatihani. Lakini mke wa mtu nitaeleza nini wanielewe, aliingiaje ndani mwangu tena usiku. Wazo lililoniijia ni kuichukua ile maiti na kwenda kuizika nyuma

    ya nyumba yangu ambako kuna uchocholo. Wazo lile nililiona linafaa

    sikuwa na njia nyingine zaidi ya hiyo. Nilipanga baada ya kufanikiwa kumzika

    bila kuonekana ninauza nyumba na kuhamia sehemu nyingine.

    Saa ya ukutani ulionyesha ni saa nane kasoro usiku, nilikwenda hadi stoo na kuchukua jembe na koleo. Nilipeleka kitu kimoja kimoja kwa umakini mkubwa huku nikiangalia huku na huko na kupata uhakika hakuna mtu yeyote aliyekuwa akiniona.

    Nilianza kuchimba shimo kwa mahesabu makumbwa kwa kupiga jembe bila kutoa kishindo kikubwa. Muda wote moyo ulikuwa ukinienda mbio kwa hofu, kama angetokea askari ningekufa kwa mshtuko.

    Nilifanikiwa kuchimba shimo bila mtu yeyote kutokea, niliingia ndani kwanza na kutulia kusikilizia kama kuna hatari yoyote, nilitulia ndani kama nusu saa mpaka ilipotimu saa tisa, ndipo nilipotoka akili na mwili haukuwa wangu.

    Niliangalia eneo lote hali ya usalama nilikaa nje muda wa robo saa, ndipo nilipo hakikisha kuwa hali ni shwari. Nilirudi ndani na kuufunga mwili wa Sabina mke wa jirani yangu kwenye shuka na kuubeba kwa taadhari kubwa na kumpeleka nyuma ya nyumba kwenye shimo.

    Niliutua ule mwili kwenye shimo huku nikitetemeka na kumuomba Mungu wangu anisaidie kuuvuka ule mtihani aliobeba maisha yangu. Baada ya kuutua shimoni nilianza kuufukia, nilichota koleo la kwanza na kutumia udongo shimoni, wakati nachota udongo kwa mara ya pili, nilitamani ardhi ipasuke inimeze baada ya kusikia sauti kali nyuma yangu ikinihoji:

    “Tulia ulivyo unafanya nini?”

    Nilijikuta haja ndogo ikinitoka bila kutegemea na kuanza kutetemeka na kujikuta nikitamka kwa sauti:

    "Nimekwisha," koleo nililokuwa nimeshikilia liliniponyoka na kuanguka chini.

    Bila kutegemea nilijikuta nimekaa chini bila kujijua.

    Sauti ile ambayo ilikuwa bado ipo nyuma yangu ilizidi kusogea na kuuliza:

    "We muheshimiwa unafukia nini usiku wa manane?"

    Sikuwa na jibu kama ungekuwa wewe ungejibu nini? Mdomo

    ulikuwa mzito kila nilililolifikiria kulisema lilikataa kutoka.

    Mbele yangu walisimama askari waliokuwa wameongozana na mbaya

    wangu jirani tunaye gombea mpaka wa nyumba. Alikuwa amejifunga msuri

    nilimsikia akisema:

    "Lazima atakuwa anazika uchawi ili anidhuru, mtu huyu mbaya sana najua

    anataka kunimaliza."

    "Eti muheshimiwa unazika nini?" Askali aliniuliza kwa upole.

    Bado mdomo ulikuwa mzito, ndipo askari mmoja alinyanyua chini kwa kunishika kwenye pindo la bukta.

    “Ndugu unatuletea kiburi, tueleze unazika nini?”

    Bado sikuwa na jibu nilibakia nimebung’aa kama mchawi niliye shikwa na tego la kiganga.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog