Simulizi : Chozi La Mwisho
Sehemu Ya Nne (4)
“Huyu
lazima anazika uchawi ili animalize kwa vile tunagombea mpaka,” Jirani yangu
aliongezea.
“Huyu hanijui siyo, hebu tueleze unazika nini?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Bado sikuwa na jibu nilijikuta nikizidi kutetemeka huku nikijichafua na haja ndogo. Baada ya kukosa jibu langu walinisukuma pembeni na kuanguka chini kama dafu toka juu ya mnazi.
Nikiwa bado chini nisijue cha kufanya hata kukimbia sikuweza kutokana na mwili kukosa nguvu. Askali mmoja alichukua kolea na kuanza kufukua ili wajue nilikuwa nazika nini? Kila alivyo kuwa akichimba nilivyo nafsi ilivyo acha mwili na kubakia ganda tupu chini. Nilitamani kabla ya kugundua kuna nini ardhi ipasuke na kunimeza. Baada ya kufukua kidogo nilimsikia mtu akisema kwa sauti ya mshtuko:
"We mutu hiki nini?" Sauti ya kuonesha mshtuko iliwafanya askari wenzake
wasogee na kuhoji:
"Afande john kwa umeona nini?"
"Naona kama hili rijamaa lilikuwa linazika mtu peke yake."
"Oooh! Hiri rijamaa rijasiri kweli rinazika peke yake, eti muheshimiwa
ulikuwa unamzika nani usiku wote huu tena peke yako kama richawi?"
"Ooh! Kama maiti ya mtu lazima itakuwa alitaka kunimaliza ni
uchawi mbaya sana," jirani alichangia akionesha kuchanganyikiwa baada ya kujua nilikuwa nazika mtu.
"We mzee hatukuja kusikiliza maswala ya uchawi hapa, serekali haijui uchawi...Hebu tusaidie kuitambua maiti hii maana muheshimiwa amegeuka bubu."
Jirani yangu mzee Masanyiwa aliisogelea ile maiti ya mke wa jirani yangu huku akitetemeka wakati huo ilikuwa umefunuliwa sehemu za uso. Aliitazama kwa makini akisaidiwa na mwanga wa tochi. Nilimsikia akisema kwa mshtuko:
"Maaaaamaaa," kauli ile iliwashtua wale askari na kuhoji kulikoni. Nilijua nimekwisha, sikuwa na ujanja tena zaidi ya kusubiri kupelekwa mahakamani na kuhukumiwa kwa kosa la mauaji na kitanzi kuhitimisha safari yangu ya duniani.
Ajabu yule jirani yangu mzee Masanyiwa badala ya kuelezea ile maiti ni ya nani aliangua kilio mikono kichwani:
"Ooh! Mungu wangu yaani umemuua mke wa Mathayo na kutaka kumzika usiku, maskini amekukosea nini mpaka kumuua na kutaka kumzika bila ndugu fa mumewe kujua?"
"Mzee hukutuita ili uje utulilie, vile vile hatuhitaji kujaziwa watu usiku huu. Swali letu huyu ni nani, je, unamfahamu?"
"Ndio namfahamu ni Sabina mke wa jirani yetu Mathayo ambaye kwa sasa
hayupo, amekwenda kwenye semina mkoani, na ameondoka kama sikosei juzi."
"Haloo muheshimiwa una mahusiano gani na marehemu?"
Sikuwa na jibu mdomo bado ulikuwa mzito, askari mmoja alinifuata na kuninyanyua huku akinikazia sauti ambayo ilionyesha kupandwa na hasira.
"Muheshimiwa kukubembeleza kutakwisha utaongea kwa lazima na sisi hatutaki kufanya hivyo si vizuri kumpiga mtu aliyekuwa akimuhifadhi mwenzake. Lakini bado tuna wasiwasi na uzikaji wako wa usiku tena peke yako, kingine kinachotufanya tuwe na mashaka ni mahusiano yako na huyu mwanamke, hebu tuweke wazi ili tuendelee na shughuli zingine."
Pamoja na kubembelezwa kama mtoto mdogo bado nilikosa la kusema mbele yao ili wanielewe, nauliza tena, kama ungekuwa wewe ungejibu nini? Kitendo cha mimi kukaa kimya kiliwaudhi askari na kuanza kunipiga kipigo ambacho
niliona kama kuchungulia kaburi niliwasikia wakisema:
"Hili litakuwa riuaji tu."
Kipigo kilipokuwa kikali nilijikuta nikiwaomba waniache niseme ukweli. Japo nilikuwa sina jinsi ya kusema ukweli, lakini hawakunielewa na kuendeleza kipigo mpaka nikapoteza fahamu.
Nilizinduka siku ya pili na kujikuta nimelazwa hospitali nikiwa na pingu mkononi, mwili wote ulikuwa ukiniuma kama kidonda na kuwa na majeraha kila kona ya mwili. Niliamini ile kauli siku zote shetani huwa pamoja kukushawishi utende maovu na akiisha kukuingiza kwenye matatizo hukuacha peke yako ukijutia ulichokitenda. Kweli shetani hakushikapo hutenda kwanza ndipo hufikiri wakati huo umeisha halibikiwa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilijiuliza ule ulikuwa mkosi gani alionikumba, sikujuwa mke wangu
nitamueleza kitu gani ili anielewe. Ushahidi mwingine ulioonesha kweli nilidhamilia kutenda yale kanga za marehemu zilizokutwa ndani
mwangu. Kumbe wapo waliomuona akiingia ndani japo yeye aliona ni siri.

****
Nilisubiliwa
nipone majeraha ili nifunguliwe mashitaka ya kuua kwa kukusudia. Sikuwa na jinsi
nilijua yote mipango ya Mungu kama kufa au kuokoka, siku ya tatu mke wangu
alirudi nyumbani na kuelezwa niliyoyafanya. Baada ya kuelezwa vile alilia mpaka
akapoteza fahamu.
Jioni alikuja kuniona hosipitali na kunikuta nikiwa sitamaniki kutokanana kipigo nilichokipata toka kwa polisi. Nilipo muona moyo ulinipasuka na kuanza kulia kwa majuto.
"Oooh! Mke wangu nisamehe sana."
"Masikini mume wangu, nini kimekusibu mpaka ufanye unyama huu?”
"Yaani sijui nikuanzie wapi kweli kila lililopangwa na Mungu hutimia, humpata hata asiye na makosa."
"Una maana gani?" mke wangu aliniuliza.
Sikuweza kumficha nilimueleza ukweli wote bila kuacha hata moja, mke
wangu aliinama huku machozi yakimtoka na kusema kwa sauti ya upole:
"Japo kuzini na mke wa mtu ni dhambi lakini kwa hili tumuachie Mungu hakuna jinsi."

Mke wangu aliondoka akiwa mnyonge kama mgonjwa roho iliniuma kila nilikumbuka jinsi mke wangu anavyo teseka kwa ajili ya matatizo yangu, nilimuangalia mwanangu aliyekuwa amelala mgongoni kwa mama yake. Machozi yalinibubujika kama chemuchemu itokayo juu ya mlima wa kilimanjaro.
Nilijiuliza nini hatima ya maisha ya mwanangu na mke wangu pindi nitakapo nyongwa au kufungwa kifungo cha maisha. Nilijikuta kila dakika maumivu ya moyo yalizidi kuwa makubwa. Ndoto yangu ya kumsomesha mwanangu Shikilwa niliiona ikimezwa na wingu zito jeusi lililoshindwa kusukumwa na upepo ili kuifanya anga ipendeze.
Siku alizokuwa anakuja mke wa kuja kuniona ndivyo hali yake ilivyozidi kudhoofu. Kila alipokuja hakuwa na la kusema zaidi ya kulia tu kitu kilichokuwa kikiniumiza. Nilimuuliza kuhusu pesa zangu kidogo ajaribu kutafuta wakili ili anitetee huenda nikapona kwa sababu nikumuua labda nihukumiwe kwa kutembea na mke wa mtu adhabu yake si kubwa sana zaidi ya kulipa faini.
Ajabu jibu alilonipa mke wangu lilinikata maini pale aliposema, eti sababu ya kifo kile siku ile Marehemu alikuja kunijulisha kuwa ana mimba yangu kutokana na mchezo ule mchafu kuuanza muda mrefu. Wanadamu hutafuta chanzo ya kumalizia wanayajua wenyewe.
Walimjaza maneno mke wangu eti siku ile baada ya mimi kuelezwa vile kuwa ana mimba yangu nilimlazimisha aitoe lakini yeye alikataa na mimi ndipo nilipoanza kumpiga nikimlazimisha aitoe wakati yeye akisema hataito. Ndipo kipigo kilipozidi walisikia kimya, yaani Sabina aliyekuwa akilia kwa kipigo changu alinyamaza.
Walimwengu bwana waliendelea kumlisha uongo mke wangu eti baada ya Sabina kunyamaza walijua tumepatana ndipo walipoondoka. Waliongezea kuwa mchezo wetu walikuwa wanaujua siku nyingi lakini walishindwa kumwambia mke wangu, kwa kuogopa kuivunja nyumba yangu.
Nimeamini dunia ya sasa unapo tumbukia shimoni wao hufurahi badala ya kukutupia kamba wao ndio kwanza wanakutupia udongo ili wakufukie kabisa. Kila nililomueleza mke wangu juu ya uongo ule hakuniamini na kuniona ni
msaliti wa ndoa yetu na Mungu ameniadhibu kwa tabia zangu chafu nilizokuwa nazifanya kwa siri lakini Mungu kaliniumbua.
Nilijua kamwe kwa maneno ya uongo aliyolishwa mke wangu hata ningejitetea vipi hasingeweza kunisikiliza. Kweli wakati wa matatizo utamjua rafiki wa
kweli na wa uongo. Baada ya kupona kidogo majeraha nilihamishiwa gerezani
kusubiri kusomewa mashtaka ya mauaji. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mke wangu hakuchoka kuja gerezani hali yake ya kiafya ilikuwa mbaya kila nikimuangalia alikuwa akinizidishia machungu. Nilipomuuliza kuhusu kutafuta wakili wa kunitetea alisema maneno mazito yaliyo nikatisha tamaa na kujiona nasubiri siku ya kuhukumiwa kunyongwa.
Mke wangu alinielezea kuwa:
" Hizo fedha za nini kuzipoteza bora nimlelee mtoto japo haitamtosha
kuliko kuipoteza kwenye kitu kilicho na ushahidi kamili.Tumuombe
Mungu usihukumiwe kunyongwa lakini hakuna njia nyingine ya kukuokoa."
Niliamini kila aliae ushika kichwa chake, yaani hata kipenzi changu alinigeuka. Kweli wanadamu wabaya lakini nilijua yote yanapandikizwa na adui yangu mzee Masanyiwa ili kunipoteza aidhurumu familia yangu eneo langu.
Niliendelea kukaa gerezani kwa miezi sita nikisubiri ushahidi ukamilike ili
nihukumiwe. Wazazi wangu kila walipokuja nao niliwaona wananiongezea machungu. Pale walipo niambia mkosi wote umesababishwa na mke wangu ambaye hakuwa na nyota na mimi.
Haya nayo kwa upande wangu niliyaona mapya kila mtu alikuwa akija na lake.
Niliwashangaa kwa kauri ile kwa kuwa hawakuwahi kusema kipindi cha nyuma iweje siku ile nimetokewa na matatizo waseme yale. Niliwapuuza na kuwaona hawana msaada na mimi. Badala ya kufikiria jinsi ya kunisaidia wao ndio wameona muda wa kulaumiana.
Siku zilizidi kukatika kazi yangu ilikuwa siku ikifika ya kupandishwa kuzimbani nilisomewa shtaka bila kujibu na kurudishwa
gerezani. Dhamana yangu ilikuwa imefungwa kwa hiyo niliendelea kusota mahabusu. Nikiwa nimejiegemeza kwenye kona ya mahabusu kichwani nikiwa na mawazo tele juu ya hali ya mke wangu na wanangu ilivyozidi kudhoofika kila kukicha.
Kwa upande wangu sikuwaza lolote kwa vile nilikuwa nimekwisha jikatia tama kwa kuogopa kumlaumu mtu kwa vile nilijitakia mwenyewe. Sina wa kumlamu familia yangu kila mmoja maisha yake anayajua mwenyewe akila leo kesho
majaliwa ya Mungu. Mwenye uwezo katika familia yangu nilikuwa mimi peke yangu na ndiye niliye kuwa tegemeo lao.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
***
0 comments:
Post a Comment