Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

NDOA ILIVYOTETERESHA IMANI YANGU - 1

 





    IMEANDIKWA NA : IRENE MBOWE



    *********************************************************************************



    Simulizi : Ndoa Ilivyoteteresha Imani Yangu

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    MAISHA NA FAMILIA YA FRORA.



    Nilizaliwa kwenye familia ya wazazi wasomi, wenye kujua nini maana ya familia, mama yangu na baba yangu siku zote walikuwa wakinuia mamoja, walipenda na kutulea kwa upendo wa hali ya juu. Tulijikuta sisi watoto tukiwa watoto wenye adabu sana na kusifiwa sana mtaani kwetu, wengi walifikiri baba yetu ni mchungaji lakini ukeli hakuwa mchjungaji ila alikuwa kama mchungaji kutokana na matendo yake na utu wake na namna anavyoishi kwa upendo na mkewe na wanawe.. Hiii ndiyo ilikuwa familia yetu familia ya mzee george maliki. Tulipenda sana imani yetu, tulipendana sana sisi kwa sisi, na kwa vile tulikuwa tumelelewa kimaadili kila mmoja alipata elimu nzuri sana, mama yetu alikuwa ni nesi na baba yetu alikuwa ni mfanyakazi serikalini, hivyo pesa zao kwa pamoja zilitulea kwa kuhakikisha tunapata huduma na malezi bora, kipindi cha kumaliza mitihani ya kidato cha nne mama yangu na baba yangu waliniambia endapo nitafauli vyema basi wangenizawadia zawadi nono sana, wakati huo kaka yangu na dada zangu walikuwa tayari wako vyuoni, na mimi kama binti wa miwho kwa kudeka sana walifikiri singefanya vizuri. Lakini nilijitahidi sana kuhakikisha nafauli masomo yangu vyema. Haikuwa hivyo baada ya matokeao, nilifeli na kupata devision 0. Mwaka 1991. Nilijisikia vibaya sana, kwani mama yangu alilia. Baba yangu alinitia moyo sana, vijana wenzangu kanisani walinicheka na kuniambia kwa nini skuwa makini kwenye masomo? Dada zangu hali kazalika walinicheka sana, lakini kaka yangu aliniambia nikisoma tena na kurudia kidato cha nne nitafaulu, na

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    alimshauri baba yangu na mama yangu nirudie mitihan yangu. Na hivyo sasa nilisubiri mwaka unaokuja ili nirudie mitihani yangu. Kaka yangu aliniambia nikiomba mungu nitafaulu na kikitia nia nitafaulu kikubwa nisome na kuatia nia. Alinitia maoyo sana, na kuanzia hapo nikaona ninaweza. Hivyo nilianza tena kidato cha nne katika shule nyingine. Maombi yangu siku zote yalikuwa mungu ifungue akili yangu nielewe vyema, ahivi ndivyo niliomba kila siku. Na kweli nilifunguliwa akaiali na kuelewa kwa haraka sana, lakini pia niliomba kukumbushwa nisiwe msahaulifu na nikawpewa kumbu kumbu mzuri sana. Nilifanya maajabu kwenye mtihani wa kufunga shule mitihani ya pre natinaonal mama yangu na baba yangu hawakuamini kuona report yangu, nilipata devision 2. Hesabu ambayo nilikuwa napata f, sasa nilipata c. Ilikuwa ni maajabu kwa familia nzima. Kaka yangu aliniambia ninaweza kufanya maajabu zaidi kwa kusoma, kutia nia na kuomba mungu akaniusia nisiache kuomba kwani yeye ndiye ambaye imemsaidia sana. Nilirudi shule kama mfalme,, nilifungashiwa kila kitu nilichotaka,, nilipewa kila kitu kizuri na wazazi, babayangu alinifurahia sana, mama pia alikuwaakailia machozi ya furaha sana, nilirudi shsuleni kwa ajili ya mitihani yangu, kipindi hicho nilikkuwa naona wanafunzi wenzangu wakiwa na boyfriiends, niliwashangaa sana. Wanawezaje kuwa na wachumba ili hali ni wadogo vile, wengi wlinicheka na kuniita mteule ama mlokole ama sister,, jina lililojulikana kulkiko jina langu halisi la flora. Kipindi cha mitihani kilipofika sikuwa nafanya lolote zaidi ya kuomba tu, kwani nilishasoma sana, hivo niliamua kufunga siku 11 kwa ajili ya mitihani yangu niliyokuwa naifanya. Nilishangaa sana, mar ya kwanza niliingia kwenye mtihani wa siasa,, nilishangaa nilivyoweza kuufanya vyema mpaka nikawa ninacheka.. Kisha kwenye mtihani wa biology nao hali kazalika nilishangaa sana na kujiuliza je ni mtihani ama ni mchezo? Mitihani ya mwanzo ilinipa roho ya kutoogopa mitihani ijayo, hivyo nikaendelea akuomba mungu anikumbushe yote niliyosoma na hivi ndivyo kaka yangu alinipa maelezo kwambna nisisome ila niwe namuomba mungu kwani nilishasoma sana kipindi cha nyuma, na hii ilifanya wengi waone kama nimechanganykiwa na kuonekana mpumbavu,, lakini sikujali. Nilimaliza mitihani yangu yote na kurudi nyumbani. Niliwaeleza wazazi wasijali nitafanya maajabu,, walikwua wakicheka sana, mkesha wa krismas tukiwa tunatoka kanisani, kijana mmoja alinifuata na kuonekana kunihitaji, niliogopa sana nikijua ni dhamabi kubwa na nilikumbuka amitihani yangu na kusema nikifanya hii dhambi nitafeli mitihani yangu, hivyo nilikataa kabisa nilionekana kusichana aliyekomaa lakaini sikutaka kujiingiza kwenye mahusiano ya mapenzi, nilirudi nyumbani nikiwa na hofu ya kutenda dhambi hiyo. Imani ya kufunga na kuomba iliniingia sana na kuona ni jambo lenye ukweli na mafanikio, hiviyo kila kitu changu nilichotaka nilifunga na kuomba na kilifanikiwa kwa asilsimia zote, na sasa nilianza kuombea matokeo yangu kwa kufunga na kuomba na siku zote niliomba kwa kufunga kwa siku 11 mfululizo nikiwa nafunga tu. Na nilipomaliza maombi baada ya muda matokeo yalitoka, kila ndugu yangu alikuwa na shauku ya matokeo yangu, kla mmoja alitaka kuona matokeo yangu, kaka

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    yangu aliyekuwa karibu na matokeo ndiye ambaye alikuwa ana shauku kubwa mno. Siku ya jumatano nikiwa natoka kwa fundi kwa ajili ya kuchukua nguo yangu ya sherehe kwa maandalio ya pasaka, nilifika nyumbani na kumkuta baba yangu akinisubiri kwa hamau, alinikumbatia na kuniambia binti maajabu… Nilimwambia enhe baba niambie,,,, kisha kaka yangu mama yangu na dada yangu mmoja aliyekkuja likizo kwa pamoja walitoka kwa pamoja wakiaimba ule wimbow a “mungu amenihuruumir tendo hili kubwa ssana sikustahilii jambo hili nimelipata bure tu,, sasa na iamba…………. Nasifu ni huuuruma tu, nasifu ni huruma tu….. ” nisingeweza kuzuia mahcozi yangu kwani kila mmoja alikuwa analia zaidi sana mamaa, lakaini baba na kaka walikuwa wakicheka,, na kisha aliniambia wewe ni binti maajabu, umefaulu sanaa nilianza kupata shauku ya kutazama matokeo yangu,,, na mara niliyaona,, sikuamini nilifurahia sana, nilipata devition one.. Iliyonyooka,,, nilimsifu sna mungu na kumshukuru kwa upendo wake na huruma zake,, na sasa kujiona msomi kama ndugu zangu na baba yangu na mama yangu. Nilichaguliwa kwenda kwenye shule ya vipaji maalumu, kutokana na kufaulu kwangu. Kaka yangu aliniambia nikiendelea kuogopa dhambi akisisitiza auzinzi aliniambia nitafanya maajabu katika elimu yangu. Na kujulikana sana, na kweli niliamua kusimamia elimu yangu, na nilimaliza elimu yangu ya kidato cha sita na kuchakugliwa kwenda chuo. Nilikaa miaka yote chuoni kwa heshima ya hali ya juu, na nilimaliza masomo yangu na kuanza kazi kwani niliomba pia nipate kazi nzuri na niipendayo, kama kawaida yangu nilifunga na Kuomba kwa ajili ya kazi na ilikuwa hivyo.





    UCHUMBA NA NDOA.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikiwa msichana mrembo sana, mcha mungu na msomi, nilipendwa na wanaume wengi wenye pesa zaoa na elimu zao , lakini niliogopa sana kumtenda mungu dhambi. Na sasa nilisema kijana atakayenifuata nitakubali kuolewa. Naye endapo nitamridhia, na sasa nilianza kuwa na mahusiano an kijana mmoja niliyempenda sana. Nilimuamini, nilimpnenda kwa shati, kila mmoja alimwambia umepata mchumba mwema. Na mrembo na msomi. Kwa vile wazazi wangu waliishi kwa upendo nilijua hizo ndizo ndoa. Lakini sikuwahi kuwa na marafiki wengi ambao wangrnifanya niogope ndoa. Marafiki zangu wote ni wasichana wataratibu wenye mahusiano ya heshima ma matokeo ni ndoa. Hivyo hili lilinifanya nijue naolewa kwa salama na si kashi kashi. Elimu ya mchumba wangu ilikuwa juu sana. Na aliniambia atanioa kisha anapaswa kusoma tena miaka 5 kwa ajili ya kukiendeleza kielimu apate mshahara mnono na maisha mazuri. Na akasema anataka kuoa kisha ndo aingie kwenye elimu. Na tulikubaliana hivyo. Haraka sana deusi mpenzi wangu wa moyotulioana naye. Baada ya kuolewa nilipendeza sana. Na kuona haya ndiyo maisha. Raha ya ndoa. Mapenzi moto moto. Tuna elimu pesa na kila uzuri wa maisha. Na haraka sana nilibahatika kubeba ujauzito. Hapo ndipo niliona ndoa ni paradiso. Nilipendwa sana na deusi. Tuliitwa kumbi kumbi. Na baada ya kujifungua wanangu mapacha alinisaidia kwa hali na mali. Na kuniwekea wasichana wa kazi 2. Ambao ni ndugu zao huko kijijini. Nilipendeza sana na uzuri wamgu kuchanua. Sura yangu iling’aa sana na kuoneka a mrembo wa haja. Deusi alianza kupata wivu jui yangu na kunichunga sana. Na sasa safari ya shule pole pole alianza kuipotezea. Lakini akiamini nitamuacha. Hivyo hakuliongelea tena. Bado haikunisumbua. Nilikuwa mwema sana kwa mume wangu nilimpenda nilimheshimu na kumhudumia sana. Nilifanya kama mama yangu alivyokuwa akifanya. Niliendelea na maombi yangu kama kawaida. Sikuacha hata kimoja. Kanisani nilipendwa na kuanza kupewa vyeo mbali mbali. Nilikuwa mwenyekiti wa uwt… Nilikuwa mlezi wa vijana.. Nilikuwa kjongozi wa maombi ya wanawake waombolezaji. Niliheshimika na kuonekana nyota ing’aayo. Wengi mtaani walinipenda sana na kunitaka niwashauri na kuwasaidia kwa mambo mengi. Nilikuwa mwanamke kijana wa nguvu. Nilivalia mavazi ya heshima ya hadhi. Mavitenge ya bei ghali ndiyo nilivalia. Nilikuwa na pesa ya kutosha kununua kila nilichotaka. Nyumba nzuri gari ya kutembelea ya mume wangu nzuri watoto wazuri na maisha ya kifahari mazuri. Kila rafiki yangu alisema flora na deusi mmebarikiwa. Mume wangu alipendeza sana. Na kunipenda pia. Ndugu zake deusi walisema mke wa deusi anadeka.. Kadekezwa na kunionea wivu. Lakini sikuwa ninadeka ila nilipendwa tu. Maisha yalisonga sana. Mume wangu hakuwa mlevi kabisa. Na hanywi kileo chochote. Siku moja akanitaka tutoke. Tena sherehe ya kikazi kama boss yeye. Tulienda shereheni na kuanza kula na kunywa. Wanaume wengi walinikodolea macho. Nilianza kuogopa mume wangu angeona. Kisha alimiambia flora kumywa wine kidogo… Mh… Nilishangaaa nikakataa. Yeye akanywa glass mbili kisha tatu kisha nne. Na kuamza kulewa. Na sasa hali ya ulevi ikawa inamshawishi anipe na mimi. Nilikataa kata kata. Akiwa kasimama huku anaongea kilevi na maneno ya kejeli aliniwasha kibao kimoja shavuni cha nguvu mpaka nikaona cheche… Nilimtazama na kushangaaa… Kisha akarudia kingine na ndipo nikaamini si yeye bali kuna shetani ndani yake. Nililia ma kuanza kuondoka huku marafili wakinisihi nibaki. Naarafiki ma wake zao nao ni walevi. Niliamua kuondoka kuepusha shari. Nilifika home na luanza kulia lwa uchungu wa hali ya juu nisijue nifanyeje. Uso ulibakiza alama za vidole. Nilioga niliomba mungu na kulala. Saa saba usiku kwa mara ya kwanza nilishtuka na kujikuta niko mwenyewe. Kisha honi ya gari iliita. Nilienda kufungua mlango na kumpokea nikiwa na hasira ya hali ya juu. Na alipoingiza gari aliniburuza ndani kwa kipondo cha hali ya juu na kuniambia nilikuwa najionyesha kwa wanaume ili wanitongoze. Majaribu

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kwa flora yanaanza: Nilipigwa kama nyanya. Nilishangaa sana. Sikulala chumbani bali jikoni kwa kujibanza banza ili watoto wasinione. Asbh nilijitazama kwenye kiyoo na kujishangaa nilivyokuwa nimeumia. Aliamka asbh na kujiandaa akaondoka na kuniambia haishi na malaya. Niliumia sana. Niliomba ruhusa kazini na kwenda kwa mama yangu kumuelezea kisa kizima. Mama alinishangaa na majeraha. Baba aliumia sana na kusema nisiondoke ila atamuita na kumkanya alichofanya ni hatari. Na baadae baba alinituma kwa wadhamini ili nikae huko mume aje. Jioni mume alipigiwa simu na wadhamini na hakuonyesha kujali. Baadae sana alikuja na kusema alilewa nimsamehe. Kirahisi tu hivyo. Nilishangaa. Nilirudi nyumbani kwa makubaliano akinipiga tena basi. Kwa vile nilikuwa na hasira ilikuwa ngumu kumchekea. Alimiambia anatola akacheke na wengine. Na kweli aliondoka. Alirudi saa sita usiku akiwa kalewa. Nilianza kuogopa kupigwa na hivyo niligungua mlango na kunyamaza kimya kuepusha kupigwa. Aliingia ndani na kusema hataki maswali. Sikumjibu nilinyamaza. Asbh kama kawaida aliondoka zake bila salamu wala kutaka kujua lolote. Ilikuwa ni siku ya maombi. Nilienda kanisani kuongoza kipindi. Nilikuwa na mzigo mzito moyoni . Sikuona upako wala njia kufunguka. Kipindi hakikuwa kizuri kama siku zote. Na hivyo sasa ilibidi niwe wazi kwa wenzangu. Niliwaelezea kila kitu. Na waliniambia tuombe. Tuliomba ila bado sikuweza kububujika. Nilikuwa na hasira sana. Na chuki moyoni. Wenzangu walinihurumia na kuniambia hilo ni jaribu kwa kazi njema niifanyayo. Na hivyo lazima nilishinde. Sikuwa nawaelewa… Umsamehe akupigaye how?mume mlevi how?roho iliingia chuki mbaya. Nilirudi nyumbani na kumkuta mume amekaa sebuleni. Ilikuwa ni saa kumi na mbili jioni. Alianza kuniambia nimetoka wapi. Nilimjibu kanisani…. Kisha akarudia kwa kejeli kanisaniiii.. Na kunifyonza. Nilichukia sana na kupitiliza jikoni. Alinifuata huko huko na kunipiga sawa sawa. Niliumia sana. Nililia sana. Nilikumbuka nilivyojiyltunza usichana wangu na kumtukuza mungu iweje aniache?nililia. Hakujali. Alioga na kuondoka na kuniacha. Tena safari hii kwa kuchukua kibegi kidogo na kuondoka. Niliumia sana. Nililia sana. Haraka nilimueleza mama kila kitu. Mama aliniambia tukutane mahali tuzungumze tena kanisani kwani hakutaka mume ajue tunazungumza. Usiku kucha nililala peke yangu. Mawazo. Nilikesha kwa kuwaza. Nilimchukia deusi vibaya mno. Haswaaa. Sikumpenda kabisa. Asbh nilielekea kanisani tulikutana na mama. Nililia mno. Nilimuelezea mama kila kitu. Ndani kanisani wenyewe. Mama aliniambia mwanangu wewe umekuwa muaminifu sana. Shetani anakuonea wivu. Anataka kukuvuruga. Na kaona hapa nfipo pa kukuvuruga. Msamehe mumeo na muombee. Akaniambia mwanangu usiposamehe unazaa chuki na kisasi. Kisasi ni kibaya sana hakitendi haki ya mungu. Hivyo samehe kwa faida yako kwanza. Kisha faida ya wanao alafu mumeo. Sikuwa namuelewa mama. Niliona anaongea pumba. Aliniambia mwanangu samehe. Nilikataa kata kata. Alijaribu kunisihi sana lakini sikumuelewa kabisa. Nililia mno. Aliniombea sana. Kisha akaniangalia na kuniambia flora umekomaa. Wewe ni mwanangu. Ni mke na rafiki yangu. Je unaweza kutofikiria ubaya nikupe kisa changu?nilimtazama kisha nikamuona akidondosha machozi.. Nilipata hofu na kutamani kumsikiliza mama. Nilitaka kujua ataniambia nini juu ya kisa chake.. Je alipigwa na baba?kama ndio aliwezaje kusamehe?je alifanyajwe na baba ili hali walipendana hivyo?nilimtazama mama ambaye bado alikuwa akilia sana na kudondosha machozi mengi na kujifuta na khanga yake makamasi. Kisha nikamwambia mama ndio nataka kukusikiliza. Niambie. Moyo wangu ulianza kuingia baridi na chuki ya jambo nisilolijua.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog