Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

NDOA ILIVYOTETERESHA IMANI YANGU - 2

 





    Simulizi : Ndoa Ilivyoteteresha Imani Yangu

    Sehemu Ya Pili (2)



    MAISHA YA MAMA YAKE FLORA.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    TULIKUWA TUMEKAA TU KANISANI MIMI NA MAMA YANGU. TULIONGEA KWA SAUTI YA CHINI SANA . KANISA LILIKUWA NA MWANGWI. KILA MAMA ALIPOPENGA MAKAMASI SAUTI ILISIKIKA SANA. KISHA AKANIGEUKIA NA KUNIAMBIA…”Flora ndoa ni kitu kingine na kumtumikia Mungu ni kitu kingine. Ndoa yako unaipenda sana. Ila kumtumikia Mungu ni jambo jengine kabisa. Mimi nilitumika sana kanisani nilipokuwa msichana. Miaka hiyo wazazi hawakujua thamani ya elimu. Nilikaa kanisani kwa uaminifu sana. Kazi yangu kanisani ilikuwa ni kufanya usafi na kufuma vitambaa vya Madhabahu ya Bwana. Niliimba kwaya pia. Sauti yangu nzuri sana kwa kwaya. Nakumbuka miaka hiyo hakukuwa na vyombo vya muziki kama sasa hivi. Tulitumia ngoma kinanda na makopo ya mawe. Lakini niliiomba vyema sana na kubariki wengi sana. Na kama unakumbuka wimbo unaoimbwa sasa hivi kanisani na kwaya kuu ni mimi niliutunga. Ule usemao… Mama alianza kuuumbia nao ulisema hivi…



    Verse 1:

    Umeanza safari ya mbinguni usigeuke nyuma… ukiwa nayo nia njema mbinguni utafikaaaa



    Solo:

    Mbinguni hakitaingiaaa.

    Mbinguni eeeeee

    Wote: kinyonge wala kidhaifuuuu katika mbimbu ya Utukufu watakuwepo waluotakaswa..



    Solo:Mbinguniiiiiiiiiii

    Wote:Mbinguni…..



    Verse2

    Mke wa lutu aliiianza safari kwenda Soari

    Lakini aligeuka nyuma akawa jiwe la chumvi..



    Chorus…..



    NILIKUMBUKA WIMBO HUU NA SAUTI YAKE NZURI. MAMA HAKUWAHI KUNIAMBIA ALIWAHI KUWA MTUMISHI KANISANI WALA MUIMBA KWAYA. NILISHANGAA ALIWEZAJE KUTUNGA WIMBO MZURI NAMNA ILE. SAUTI YAKE NZURI NA YENYE MVUTO WA HALI YA JUU. NILIVUTIWA SANA. KISHA MAMA AKAENDELEA.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mama aliendelea kuniambia…. Niliimba sana mwanangu. Nilifanya kazi nzuri kanisani. Walikuja wamisionari na kunipeleka shule ya unesi. Nilisoma vyema na wakanipeleka nje ya nchi kwa masomo na kupata degree huko. Kisha nikaolewa na baba yenu. Sikuwahi kuacha kazi ya kuhudumia kanisa kila nilipopata nafasi mara baada ya kazi yangu. Mungu alinibariki sana. Baba yenu alianza vituko baada ya kupandishwa cheo kazini. Na baada ya muda alifukuzwa kazi. Nilimlilia Mungu na akanisaidia sana na kunipandisha cheo kazini nikawa mkubwa wa manesi. Na mkunga mkuu niliyejulikana sana. Lakini ni kwa sababu nilimuamini Mungu na shetani alinimatisha tamaaa. Kanisa lilifungua hospital na nilienda kusoma tena kwa ajili ya kusimamia hospital hiyo. Nilifanya vyema. Nilikaa ulaya miaka 2. Kisha nilituma nauli baba yako na ndugu zako wakaja tukakaa kwa miaka mingine 2. Na kisha tukarudi na baba kunishukuru sana na kuanza kutafuta kazi kwani kule alisoma kozi mbali mbali na kuwa msomi mzuri sana. Sikubesabu ubaya wake ila nilisema nafanya huruma kwani Mungu alinihurumia mimi kuwa nesi niwaangalie ninyi…



    Mama aliendelea kuongea huku akibubujikwa na machozi…. nilimsikiliza lakini bado sikuona unyama wa baba. Na sasa nilitaka kusikia unyama gani baba alimfanyia mama… bado niliona baba hana tatizo kama deusi. Mama alisita kidogo kuendelea kuzungumza… kisha akalia sana kwa sauti ya juu. Na baada ya hapo mama alinitizama na kuniambia Flora narudia tena je una nguvu za kutoweka kisasi? Nilimtazama mama na kumwambia ndio. Mama Aliniangalia kisha akaniambia nimfunue mguu wake. Nilimfunua mguu wake mpaka kwenye paja lake.. nilishtuka kuona nilichoona… sikuamini…. nilimtazama tena mama kwa makini sana na kumuuliza mama ni nini hiki?aliniambia umeona nini?nilimwambia mama nimeona kama sijaona…. Niliona kitu cha ajabu sana. Mama alikuwa na mguu wa bandia.. nilisimama kwa mshangao… kwa miaka yangu 26 sikuwahi kulijua jambo hili. Tuliamini mama yetu alizaliwa akichechemea kumbe hakuwa na mguu.. nilishtuka… nilimuuliza mama ni nini hiki?mama alifuta machozi na kuniambia je unajua jina baba yako analoniita?nilimwambia ndio najua. Akaniuliza ananiita nani?nilimwambia anakuita NYOTA…ndio mwanangu. Mimi ni nyota. Nang”aaa duniani na Mbinguni.Baba yenu nilipomuita ulaya alikuja na kisha aliendeleza ubabe wake. Na siku moja akiwa kalewa alinipiga na nilidondoka kwenye ngazi na mguu kuvunjika. Na kwa kuogopa atafungwa kutokana na sheria za kule baada ya kuniomba msamaha sana nilificha kosa na mguu ukaoza. Na hivyo ulikatwa. Lakini nilimsamehe. Tulirudi Tanzania hakuna aliyejua. Hata mchungaji wala wazazi wala watoto. Nilitoa msamaha wa moyoni. Na leo hii nimekuambia ukweli ili ukusaidie. Nataka uwe nyota kwa Mumeo. Na ninakusihi toa siri zote ila hii kamwe usimwambie mtu tafadhali mwanangu. NILILIA SANA KWA MAELEZO YAKE. KISHA MAMA AKANIKUMBATIA NA KUNIAMBIA NIAHIDI HUTASEMA. nilimtazama nikilia sana na nikamwambia Sitasema.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baba yenu aliporudi Tanzania alipata mafanikio makubwa sana. Alikuwa boss mkubwa sana serikalini. Alipata pesa nyingi sana. Lakini hakuwahi kuwa mlevi wala mzinzi. Wengi walimuita luther.. alionekana mtanashati sana. Na mwanaume mzuri sana. Lakini alinipenda vibaya mno. Alikuwa muaminifu vibaya mno. Niliishi kama Nyota. Kwa furaha na amani. Alinisaidia kila kazi ngumu. Na hakuna aliyewahi kujua sina mguu. Wote niliwaficha. Ilikuwa ni rahisi sana. Nilisema nina ugonjwa wa visigino hivyo muda wote nilivaa soks na raba nzuri sana. Na ninyi hamkuwahi kulijua hilo. Nilipotaka kupumzika tulifunga chumba na kuvua mguu na nilikaa kwa muda ndani na baba tukizungumza na hamkuruhusiwa kuingia. Na hata mlipoingia mlinikuta kitandani nimejifunika na hamkujua lolote. Hivi ndivyo niliishi. Na ilawa siri kubwa sana. Wengi wanajua nina matatizo ya kisigino kama ulivyojua na wewe na wenzako. Je unaweza kumsamehe mumeo kwa kosa la kukupiga na kulewa?Nilimtizama mama nikamwambia naumia kwa nini anipige naumia. Mama alisisitiza nimsamehe na nisisimulie tena mtu matatizo ya mume wangu. TULIMALIZA KUONGEA. MAMA AKANIAGA. NJIA NZIMA NILILIA. NILISHANGAA JINSI AMBAVYO MAMA AMEWEZA KUFICHA SIRI HII. KWELI ALIMSAMEHE BABA. KWELI ALIMSAMEHE. NILIFIKA NYUMBANI NIKIWA HOI NIMECHOKA KWA MAWAZO AKILINI.





    NILIFIKA NYUMBANI AKILI IKIWA IMENIVURUGIKA. NILIMTAZAMA MAMA YANGU NA KUKUMBUKA SIKU MOJA ALIANGUKA AKIWA ANATOKA KAZINI. NILIMUONA ILA ALINITUMA KUITA JIRANI. NA SIJUI ALIJIBURUZAJE NA NILIMKUTA CHUMBANI NA ALISEMA BABA AKAITWE HARAKA SANA. ALIJIFUNGIA CHUMBANI NA JIRANI ALIVYOKUJA ALISEMA ANAOGA YUKO OKAY. KISHA BABA ALIITWA NA WALIKAA CHYMBANI KAMA KAWAIDA YAO. SASA NILIANZA KUPATA PICHA ALIKUWA MBOVU WA MGUUU NA HAKUTAKA NIONE. NILIKUMBUKA PIA NAMNA ANAVYOPENDA KUDANCE NA MOTION YAKE ILIVYO.. NILIANZA KUPATA PICHA ALIVYPKUWA AKIDANCE TENA NA BABA AKIMSHILA NA WAKICHEZA KWA FURAHA. NILIPATA PICHA SIKU YA MAHARI YANGU ALIVYOKUWA AKICHEZA KWA FURAHA SANA. NILIENDELEA LUSHANGAA. NILIKUMBUKA KITU KIMOJA… MAMA ALIMSAIDIA SANA MKE WA KAKA YANGU KWA UZAZI NA MKE WA KAKA YANGU ALIWAHI KUKAA CHUMBANI NA MAMA WAKIZUNGUMZA KWA MAMBO YAO YA KUSULUHISHA UGOMVI… JE WIFI YANGU ANAJUA?JE DADA YANGU ANAJUA?DE DADA YANGU ANAJUA?JE KAKA YANGU ANAJUA?NILIWAZA MENGI. NILITAMANI KUONGEA NAO MMOJA MMOJA. NA NILITAMANI PIA KUMWAMBIA BABA KWAMBA NIMEJUA UPENDO WAKE NI WA KINAFIKI NI KWA VILE ALIMUUMIZA MAMA NA SI UPENDO WA DHATI…. NILIPATA HASIRA GHAFLA NA KUPANGA SAFARI YA KUMUONA BABA.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilikumbuka sauti ya Baba ikiita Nyotaaaaa.. na mama aliitika kwa furaha sana na kuachia tabasamu lake na kufanya mwanya wake uonekane. Kisha baba alimsogelea na kumbusu mama yangu katika paji la uso… picha hii ilinijia na kuona busu lile ni la usaliti. Kama la Yida Eskariote aliyemsaliti Yesu kwa Busu. Nilimchukia Baba kuanzia hapo. Niliumia sana. Nilijuta nimejua ya nini. Nikiwa yumbani mume wangu alikuja na hakunisemesha lolote. Na mimi kwa kiburi sikumsemesha lolote. Nilinyamaza. Tulanuniana. Asbh nilienda kazini. Sikuwa na furaha. Mume aliondoka na yeye. Kila mtu kwa namna yake. Mchana nikiwa kazini baba yangu alikuja lumiyembelea. Alitaka kujua naendeleaje. Moyo ulinipasuka kumuona… kisha aliingia ofcn kwangu akiwa na tabasamu. Baba alinipenda sana. Alishangaa sijamchangamkia nilikuwa namuona kama sijui nini. Nilitamani kumtemea mate.Baba alinisogelea na kuniambia mwanangu samehe. Msamehe mumeo. Mungu atakusamehe na kikujalieni mafanikio mengi. Kuna baraka za mafanikio tele kwenu msamehe mumeo. Kidogo simanzi ikaniingia. Nikaanza kupata huruma. Nikamkumbatia baba. Nikamuona alivyo na upendo kwa kuweza kuacha uzinzi na ulevi kwa ajili ya mama. Niliona sasa sura mpya. Alijinyima starehe na anasa kwa ajili ya mke wake. Nilimuona hodari sana . Kwanza nilihisi mama alipokosea ilikuwa ni lazima amsamehe ili asikumbuke mguu. Sasa nilitaka kujua baba naye aliwahu kumsamehe mama?nilimuuliza baba je umewahi kuuziwa na mama ukamsamehe?baba alinitizama na kuniambia mwanangu hakuna mwanadamu asiyekosea ila kusamehe ni lazima. Nilimuuliza ni nini ambacho mama alikukosea na ukamsamehe ili niweze kupata nguvu ya kusamehe.Baba alinitizama. Kisha akaniambia mwanangu nakupenda na nitakueleza. Ila iwe siri yako tu. Usimwambie yeyote yule. Nilimwambia sawa baba. Baba aliniambia kwamba mama alikuwa mvivu sana. Hakuweza kufanya kaxi za mikono. Na alikuwa akigombana na wasichana kila siku. Na alifukuza wasichana wote. Na hivyo kwa uvivu wake niliweza kumvumilia kumpenda na nilifanya kazi zote. Niliitwa mume bwege lakini nilimsamehe mke wangu na sikujali. Miaka yetu mwanamke hakuwa na sauti. Lakini mama yenu alikuwa na sauti . Ila kwa upendo nilimvumilia sana. NILIMTAZAMA BABA YANGU. NIKAKUMBUKA ALIVYOKUWA AKIMFULIA MAMA YANGU NGUO ZAKE NA SARE ZA KAZINI. NILIJUA KWELI NDOA NI SAFARI NDEFU NA KILA MMOJA ANA VHA KUELEZA NA KIKASISIMUA. NANI ANGEJUA HAYA YOTE KWA NDOA ILE ILIYOKUWA IKISIFIKA VILE?Nilimwambia baba nitamsamehe mume wangu. Nitamsamehe. Baba aliniambia sio utamsamehe msamehe sasa hivi ndo utoke nje. Nilicheka kisha nikamwambia baba nitamsamehe.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog