Simulizi : Niache Nilie
Sehemu Ya (2)
Ilipoishia..
Nilianza kuchimba mpaka nilipofika kwenye msingi wa ile nyumba na kukutana na kimfuko cheusi kilichofungwa vifundo vitatu na kilikuwa ni kirefu.
Songa nayo…CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Basi mama mdogo aliniambia nikichukue. Nilikibeba na alinionyesha sehemu ya kwenda kukichoma. Alinipa kiberiti na kwenda kukichoma na wakati nachoma moshi ulikuwa mwingi sana na mweusi nilisogea pembeni kidogo na aliponiona nasogea aliniambia rudi nisimame pale pale mpaka nimalize kuchoma. Nilisimama pale hadi vikamalizika kuungua. Cha ajabu palikuwa kama hapajachomwa kitu chochote palikuwa kama nilivyopakuta yaani hapaonyeshi kama kuna kitu kimechomwa. Moshi wote uliniishia na nilianza kusikia maumivu makali ya kichwa huku mwili nao ulianza kuchoka na kuuma kila mahali. Baada ya muda niliwaona wale watumishi wa kanisani wanakuja nyumbani. Walipofika mama aliwapokea na kuwakaribisha na kuwaeleza kuwa tayari nimeshachimba na kuutoa uchawi wangu.
Nao walisema kuwa, mchungaji aliwaagiza waje wachimbe kama nimekataa kuchimba. Baada ya kuambiwa maneno hayo walianza kuchora alama za misalaba kwa kutumia mafuta waliyokuja nayo na walianza pale pale mlangoni.
Walipaka nyumba nzima mafuta hukuwa wakiwa wanaongozana na mama mdogo na walipomaliza waliondoka. Kipindi chote hicho nilikuwa najisikia maumivu makali na mara ghafla mwili ulianza kubadilika nikadhofika sana. Nilikuwa mwembamba kwa muda wa saa chache. Mama mdogo na wanaye walizidi kunisengenya na kila waliponiangalia walicheka kwa dharau. Niliwaza mengi, nilitamani hata ardhi ifunguke niingie ili nisionekane katika uso wa dunia hii. Kana kwamba hilo halitoshi, akili zangu zilianza kupoteza mwelekeo na kujikuta nipo kwenye tatizo jingine la kuanza kusahau vitu. Ikawa kila nikiambiwa nifanye kitu flani ikawa inanipasa nifanye wakati uleule kwani nisipokifanya kwa muda huo nasahau. Basi baba alirudi kutoka kazini na tulipata chakula cha usiku na wakati tunakula stori zilizungumziwa kwa wingi na zinazo nihusu, mama mdogo aliniangalia na kucheka sana. Ghafla nilianza kulia.
Mama mdogo: Baba Recho mwanao leo amechimba ule uchawi wake (Recho ni mwanaye kwa huyo mama).
Baba: Yaani huyu shetani amekubali kuchimba?
Mama mdogo: Amechimba kwa jina la Yesu.
Baba: Kulikuwa na kitugani humo?
Baba alianza kucheka bila kujua umuhimu wangu na wala hakunionea hata huruma mimi mwanaye licha ya kupata manyanyaso makubwa. Nilikonda nikatisha. Amani ya kuishi ilitoweka ndani yangu nilizidi kulia kila palipokucha, nilikuwa ni mtu wa machozi zaidi kwani sikuwa na mtetezi kwa upande wangu hata mmoja kila mtu alijitenga mbali nami hata kwa ndugu wa baba sikuweza kwenda kwani baba alishanikataza. Siku zilizidi kwenda na hali ikizidi kuwa mbaya zaidi kwangu. Nilianza kwenda kanisa ambapo siku moja nilienda na mama mdogo tulipofika niliabudu hadi ibada ilipoisha. Baada ya ibada kuisha niliitwa na yule mchungaji. Niliingia ofisini kwake na kukutana naye na kuanza kunieleza kuwa; “leo naomba iwe ni mwisho wa kukuona kanisani kwangu, usije tena hapa kanisani kwa sababu wewe ni mchawi.” Niliondoka na tulianza safari ya kuelekea nyumbani na mama mdogo, tulipofika mama alinieleza kuwa:
“Uchawi wako ndiyo uliosababishwa ufukuzwe kanisani, sasa utakaa hapa nyumbani na uwe mlinzi wa hii nyumba. Muda ulifika baba alirudi kutoka kazini na mama mdogo alimuelezea hali halisi iliyotokea kule kanisani. Baba alijibu; “atajua mwenyewe na ushetani wake, muache akae hapa nyumbani.” Basi hali ilizidi kuwa mbaya na tena nilizidi kukosa amani zaidi kwani nilijua hata kama nitakuwa na hali ya tofauti kwa kuwa nyumbani wananichukia basi mchungaji atanitia moyo lakini cha ajabu mtumishi wa Mungu huyo huyo ndiye anayezidi kuniumiza zaidi ya wale ninao ishi nao. Niliumia sana kwa kile kitendo cha kunifukuza kanisani na nilizidi kuumia zaidi kwani yule ni mtumishi wa Mungu najua asingepaswa kunitendea kitendo kama kile. Nilianza kukwazika moyoni na kuwachukia wachungaji bila sababu. Ilikuwa kila mchungaji anayekuja mbele yangu nilijua kuwa ni wale wale wenye moyo mbaya.
Mchungaji huyo aitwaye Mathayo ambaye kanisa lake lilikuwa Ngulelo Arusha hakika naye alichangia kuweka majeraha makubwa moyoni mwangu. Nilitegemea kuwa hata kama nilikuwa na tumiwa na nguvu za giza bila mimi kujua yamkini angeniombea na kutokwa na uchawi huo. Nilianza kuhisi kwamba, mchungaji alikuwa anashirikiana na wazazi wangu kunifanyia unyama huo. Nilikaa nyumbani mpaka nilianza kupachoka. Baba alikuwa akisali katika kanisa la Kristo Ufalme Ngarenaro kwa Father Babu na ni mara chache sana alikuwa akienda kwenye lile kanisa alilokuwa anaabudu mama mdogo. Baba alianza kunielezea ndoto mbaya anazoota usiku na zinanihusu mimi. Siku moja aliniambia ameota mimi natembea kwenye fensi ya nyumbani nikiwa nimevaa gauni jeupe lakini sikanyagi chini yaani natembea kwa kupaa juu juu. Alianza kunikalipia na kuniambia naacha kulala na kufanya kazi yako ya kuzunguka zunguka usiku. Nilinyamaza siku jibu chochote. Maisha yalizidi kuwa magumu sana kwangu kwani hata hamu yakumuona huyo baba yangu iliisha badala yake niliendelea kuumia kila nilipomuona. Mama mdogo alisema kuwa atamfuata baba yake aje atushonee kwenye riblauzi vya ndani yaani sing’lendi hilizi zenye ngozi. Nikamwambia vinasaidia nini akanijibu kama mtu ni mchawi au ni mbaya akipita atajulikana kwa kupitia vingozi hivyo (hilizi). Moyo wangu ulijaa wasiwasi huku nikijiuliza kama mtu kweli ameokoka itakuwaje aamini hilizi? Lakini sikupenda kumuuliza. Alituonya na alituambia tusimwambie mtu yeyote na hiyo ni siri yetu. Basi siku moja mama mdogo akaniambia pamoja na kunifunga hili hiyo atanipeleka kanisani kwa ajili ya maombi. Nikamwambia sawa kisha nikamuuliza ni wapi huko atanipeleka naye akasema kuwa tutaenda kwa mama Sia aliyekuwa anaishi Mbauda. Siku ilifika tulienda hadi Mbauda kwa huyo mama na tulipofika tulimkuta akiwa anafanya shughuli zake za nyumbani tulimngoja hadi alipomaliza. Niliingia ndani nikamsalimia kisha wao wakaendelea na maongezi. Maongezi yalipoisha nakumbuka waliweka kanda ya wimbo wa kuabudu kwenye redio na ule wimbo ulipoisha ndipo walianza maombi. Walinipaka mafuta kwa kunichora alama ya mlasaba wakati maombi yanaendelea. Binafsi mimi niliyaona kama ni mafuta lakini ukweli waliujua wao waliokuwa wakinichora misalaba kwa kutumia mafuta hayo. Nasema hivyo kwa sababu kabla ya kufanya maombi yule mama aliingia chumbani kwake na kutoka na kikombe cheupe chenye hayo mafuta. Walinivua nguo na kuanza kunichora misalaba kwa kutumia yale mafuta huku akisema kwa jina la Yesu katika jina la Yesu huku mimi nikiendelea kulia kwa kuonyesha sijafurahishwa na kitendo kile. Nilipakwa yale mafuta kila sehemu katika mwili wangu hakuna mahali ambapo waliacha na manisha hadi sehemu zangu za siri kwa kutumia jina la Yesu huku wakiendelea kukemea na kusema kwa jina la Yesu Kristo shetani toka tunakuamuru toka. Basi walipomaliza walinipa mengine ninywe lakini nilikataa ndipo walipoanza kunishika kwa nguvu na kunilazimisha nilizidi kukataa ndipo yule mama alipotoka nje na kuwaita vijana wawili hivyo wakawa wanne pamoja na wao. Waliniminya mdomo nami sikuweza tena kujizuia yale mafuta yaliingia ndani yam domo wangu mara nikapoteza fahamu kwa hiyo yaliyoendelea siyafahamu hadi leo. Nilipozinduka nilimuona mama mdogo na wadogo zangu pamoja na yule mama wamekaa wanaongea. Nilimwambia mama mdogo naomba kwenda msalani nikajisaidie. Niliposimama naye akasimama na kuniambia twende pamoja, nikamwambia tangu lini ulishanipeleka msalani? Akaniambia twende basi nilielekea huko huko yeye akiwa nyuma yangu. Nilipofika mama mdogo akaniambia niache mlango wazi nilifanya hivyo kisha nikaanza kujisaidia haja ndogo lakini sikufanikiwa kutokana na maumivu makali sana sehemu za siri. Nilizidi kujikamua kwani mkojo ulikuwa umenibana sana ingawa hautoki, baada ya muda ulianza kutoka huku nikisikia maumivu makali na ulikuwa unameremeta kana kwamba umechanganywa na mafuta. Nilipomaliza kujisaidia tulirudi ndani na kuendelea na maombi na tulipomaliza tuliondoka kuelekea nyumbani lakini kabla ya kuondoka yule mwenyeji wetu alimpigia simu baba yangu na kuanza kuongea naye.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Basi tulirudi nyumbani huku mwili wangu ukiwa na maumivu makali. Kanisani sikuruhusiwa tena kwenda. Mama mdogo aliniiambia kuwa nikiona siku zangu nimwambie. Kauli hiyo iliendelea kunichanganya tangu lini nikamwambia juu ya suala hilo. Nilijaribu kuziba pamba masikioni, baada ya kuziona siku zangu sikumwambia lakini yeye cha ajabu yeye alijua. Niliona siku zangu majira ya jioni nakuanza kujiweka sawa kama inavyotakiwa, nililala na palipokucha nikiwa naelekea chooni kutupa ule uchafu ndipo mama aliponizuia kuelekea chooni. Aliniambia niingie ndani nami nilifanya hivyo na kuelekea chumbani kwake. Tangu nikanyage nyumbani hapo nilikuwa sijawahi kuingia chumbani kwao. Niliingia na akaniambia nikikamue kile kitambaa cha uchafu wa siku zangu. Alinipa kikombe ambacho huwa natumia kunywea chai ili nikamulie damu hiyo humo. Nilifanya kama nilivyoagizwa, nilikamua na zile damu zikajaa kwenye kile kikombe. Tendo hilo lilifanyika asubuhi, mchana na jioni na ililala chumbani kwao. Siku iliyofuata palipombazuka wadogo zangu walielekea shuleni na baba kazini tulibaki mimi na mama mdogo tu. Na ndipo aliniita kule chumbani na kufunga milango yote na kunipa dakika mbili niinywe uchafu huo. “Nakupa dakika mbili tu nisiione hiyo damu kwenye hiki kikombe,” aliniambia.
Hakika ulikuwa wakati mgumu sana kwangu kwani nilipouangalia huo uchafu tena ukiwa na harufu kali nilianza kulia. Nilimkumbuka shangazi yangu Elizabeth, marehemu bibi yangu Martha huku sura ya mama yangu mzazi Ruthi ikinijia kichwani lakini haikusaidia chochote. Juhudi zangu za kugoma kunywa hiyo damu ziligonga mwamba na kujikuta naiywa damu hiyo mpaka nikamaliza kikombe kimoja. Hakika inauma sana na mara baada ya kumaliza kunywa aliniambia kuwa;
-Huta soma
-Huta zaa
-Wewe ni wakufa tu
Alipomaliza kunieleza maneno hayo aliniambia niondoka mbele yake. Niliondoka na kuelekea nje huku roho ikiuma na machozi yasiyoisha yaliendelea kunitoka. Baada ya tukio hilo nilikaa wiki moja nikiwa siwezi kuongea kabisa, siku moja nikiwa nyuma ya mlango, mama mdogo aliniita na ndipo sauti ilitoka. Vituko vya kila aina vilizidi kujitokeza kwangu, hakuna aliyekuwa akinipenda. Nilizidi kumkumbuka shangazi yangu japo naye alikuwa ananitesa lakini ya mama mdogo yalikuwa makali zaidi. Ilifika wakati baba akawa anatoka kazini kwa lengo la kuja kula chakula cha mchana na alikuwa anakuta chakula hakijaiva na kila alipouliza kwa nini hadi mida hiyo chakula hakijaiva mama mdogo alimwambia muulize mwanao. Nilizidi kuonekana mbaya kadiri siku ilivyozidi kwenda. Wakati wote huo nilikuwa siendi shule. Siku moja nilimwomba baba ruhusa ya kwenda shule na palipokucha nilijiandaa kuelekea masomoni. Wakati wote huo mdogo wangu Raheli kwa jina lililozoeleka ‘Recho’ alikuwa anaenda shule na tulikuwa tunasoma pamoja lakini aliambiwa asiwe anaongozana na mimi. moja lakini alishanyimwa asitembee na mimi. Nilienda shuleni na muda wakutoka shule ulipofika niliitwa ofisini na mwalimu wangu wa darasa, nilipofika nilimkuta mama yangu mzazi na nilipomwona machozi yalinitoka nililia sana na kwa uchungu. Nilimueleze,a mama hali halisi ya pale nyumbani kwa baba nayale yote waliyokuwa wakinitendea ingawa mama nae aliamua kusema, mwanangu siwezi kukuchukua hadi nikaonane na ndugu zako yaani kaka wa baba yangu, ndipo nitakuja kukuchukua. Nilikataa na kumwambia mama siendi leo kwa baba naenda na wewe, mwalimu wangu walimsii na kumwambia nenda na mwanao. Basi tuliondoka na mama na kuelekea kazini kwa baba yangu mkubwa tulipofika mama yangu alimuelezea na kumwambia nimeamua kumchukua mwanangu. Baba mkubwa alimwambia kwani ulikuwa ujui kuwa mtoto ni mama? Ndipo niliondoka na mama na kuelekea nyumba kwa mama, yangu ,nilifika na kuwakuta wadogo zangu wawili kwa upande wa baba yangu mdogo yaani baba wa kambo, kwa lugha nyingine. Niliingia hadi ndani na ndipo niliendelea kuishi kwa mama yangu mzazi kwa amani, na upendo kwani baba mdogo hakuwa ananichukia alinipenda kama wanae na alinijali na pale nilipokuwa na shida nilimwambia mama na ma kumuelezea baba mdogo na kupewa msaada, nilianza kuishi kwa amani ingawa yale ya kule kwa baba ilikuwa nikiyasahau na kila nilipoyakumbuka nilizidi kulia tu. Mwili wangu ulikuwa umedhoofika sana hali ilikuwa mbaya, mama yangu alijitaidi na kuirudisha afya yangu ingawa ilimgarimu sana na kupoteza fedha nyingi kwa ajili yangu. Kwa kuwa alikuwa ndiye mzazi halali hakuona shida kunigharamia. Ndipo nilipojua kuwa nina ndugu wengi kwa baba ninawadogo zangu wawili, msichana mmoja na mvulana mmoja ingawa kwa sasa sijui kama kuna mwingine. Na kwa mama nina wadogo zangu wanne, wasichana wawili na wavulana wawili na mimi niwatano. Maisha yaliendelea kuwa mazuri, amani, furaha, na upendo nilizidi kuona kwa wale wazazi nilioishi nao. Ulifika muda ilibidi mama aanze kunitafutia shule ya karibu na nyumbani na alipofanikiwa kupata aliomba nafasi na alipata nilianza kwenda shule kwa amani ingawa nilisoma bila uhamisho kwani hata baba yangu hakufuatilia ule uhamisho kule moshi. Ilibidi mama yangu aanze safari ya kufuatilia ule uhamisho hadi alipofanikiwa na shangazi yangu aliendelea kuwa nae bega kwa bega kwa kuwa alikuwa ni mwalimu wa hapo shuleni nilipokuwa nikisoma. Hivyo walishirikiana sana ingawa shangazi yangu kwa mara ya kwanza ilikuwa ni vigumu sana kusikilizana na mama yangu kwa ajili ya Yule baba aliyoyatenda lakini baadae shangazi alimuelewa mama yangu na kuanza kusaidiana nae hadi walipokamilisha. Mama alirudi Arusha na kupeleka ule uhamisho katika shule ya msingi. Burka Primary School iko Arusha. Niliishi maisha ya furaha na ya amani na nilitimiziwa kila anachostahili kutimiziwa mtoto. Mama alikuwa ameokoka siku nyingi nae baba mdogo, na walisali katika kanisa la Elerai kwa Pasta Haule. Nilianza kusali nikiambatana na wazazi wangu hao. Niliendelea, kusoma darasa la sita lile lile hadi nilipo maliza ule mwaka. Nilifurahi sana kuishi na wazazi wangu hao kwa amani isiyo na kifani, nilipendwa na ndugu zangu na hata na jamii iliyokuwa imenizunguka. Nikajua mama ni mama tu na mama nitofauti na mtu yeyote Yule mtu asikudanganye, mama ni mama tu na uchungu wa mwana anaujua mama. Mama yangu mzazi aliishi Mbauda Kerai Olasiti.
****
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Baba yangu anaishi Ngarenaro Matejoo wote wako Arusha sehemu tofauti siku zilisogea na maisha yaliendelea nilimaliza darasa la sita na kuingia la saba na nilifanikiwa kumaliza darasa la saba salama na kufaulu vizuri.
Nilifaulu katika shule ya sekondari Olgori lakini sikuwahi kwenda hata siku moja katika shule ila nikiwa nangoja Januari ifike ili niende shule, baba mdogo akaniambia ile shule uliyofaulu iko mbali sana na nyumbani cha kufanya nitakusaidia nikutafutie shule nyingine.
Ni kweli shule ilikuw ani mbali sana na nyumbani nilipoishi kwani kwa wanao ifahamu Arusha iyo shule, iko chini ya kwa Mrumboo hicho nikisehemu tu kinaitwa hivyo ni sawa na kusema natoka kinondoni naelekea Tabata.
Baba mdogo alinisaidia sana na kupata shule nyingine ambayo nilianza atu baada ya shule kufunguliwa na kuingia fomu wani katika shule ya sekondari Kaloleni chiniya mkuu wa shule kwa jina la Mungu mwaka 2006.
Nilimshukuru sana baba mdogo kwa msaada mkubwa aliyojitolea kwa ajili yangu na kwa ajili ya maisha yangu pia. Nilimaliza darasa la saba mwaka 2005 katika shule ya msingi Burka Primary school, na kuendelea na masomo ya sekondari Kaloleni Sekondari school Arusha nilipoanza elimu ya sekondari hali ilianza kuwa mbaya nilianza kuugua ovyo bila sababu.
Nilianza kujisikia vibaya mwili ulianza kudhoofika tena ingawa hakuna nilichokuwa nikikosa pale nyumbani damu zilianza kutoka masikioni na puani hali hiyo ilizidi kuendelea kwa muda mrefu nilianza kukosa amani tena ingawa wazazi walijitahidi sana kuwa karibu na mimi na kunitia moyo na walizidi, kuendelea na maombi chini ya mchungaji Kasesa kwani baada ya muda kuendelea kanisa lilifunguiwa pale mtaani kwetu kwani hapakuwa na kanisa la Kiroho katika eneo lile.
Hivyo kanisa lilifunguliwa pale na mchungaji aliitwa Kabesa na mama akiwa Shemasi na baba akiwa mzee wa kanisa. Hilo likiwa ni tawi la Elerai. Maombi yaliendelea kwa wshirika wa kanisa la Elerai na kanisa la Chemchem Olasiti kwa mchungaji Kabesa niliendelea kufanyiwa maombi kil akona kutokana na ile hali iliyoanza kujitokeza kwangu.
Wazazi walinijenga katika hali ya kuzidi kumjua Mungu na kunikwepesha na yale mawazo ya kule kwa baba yangu mzazi. Hali ilizidi kuwa mbaya damu ziliendelea kunitoka bila kukatika, niliendelea kuombewa na hali ikizidi kubadilika. Nililazwa katika hospitali ya Mount Meru Arusha kwa muda wa wiki moja.
Baba yangu alipewa taarifa na baba yangu mdogo mume wa mama yangu. Baba mdogo alimwambia mwanao ni mgonjwa na amelazwa hospitali ya Mount Meru. Baba alifika hospitali na alipofika pale kwenye kile kitanda nilicholazwa lakini cha ajabu akiwa kama mzazi alikuja mikono mitupu na cha ajabu kabisa alinisalimu hivi.
Emy Mambo?
Huyo ni baba aliyenizaa, haoni uchungu wangu haoni thamani yangu hata kidogo. Nilimwangalia roho iliniuma nilianza kulia kwa uchungu kwani akiwa kama mzazi angepaswa kunisalimia vizuri na kuuliza, tatizo, lakini cha ajabu aliniambia mambo na kugeuka na kuondoka sikuwahi kumuona tena akija, kuniangalia hospitali, lakini nilijua kitu na kujismea moyoni anajua alichotenda kwa hiyo ajui thamani yangu hayo niliyasema moyoni mwangu.
Nilitoka hospitali na kurudi nyumbani lakini cha kushangaza hakuna walichoniambia kunachonisumbua zaidi nilitundukiwa maji tu. Nilirudi nyumbani na kuendelea kuuguziwa nyumbani mama na baba yangu mdogo naliendelea na maombi bila kuchoka hli alianza kuwa katika hali nzuri na baadae nilindelea kwenda shuleni.
Muda uliendelea kwenda ile hali ilipotea nilisoma vizuri na matumizi kama mtoto kwa wazazi niliendelea kupewa muda siku zilizidi kwenda. Baada ya muda nikiwa shuleni nilianza kutapika damu na hiyo yote ilitokea pale nilipohisi tumbo kuuma.
Hali hiyo ilitokea nikiwa shuleni hivyo walimu wangu walinisaidia na kunipeleka tena hospitali ile ile ya Mount Meru nililazwa tena kwa muda mrefu nilizidi kutapika damu zaidi. Baada ya muda madaktari walinipima na kukuta, naupungufu wa damu na kuniambia tunakuongezea damu lakini mama yangu alikataa.
Zaidi mdogo wa mama yangu kwa jina la Judith Mwakalinga alinitafutia matunda na kunitengenezea juisi ambayo aliniambia kunywa ili damu iongezeka kwani hizi damu za kuongezewa si nzuri nilijitahidi na kuendelea kutumia ili juisi. Nilitoka hospitali na kwenda moja kwa moja kwa babu yangu mzaa mama nilikaa kwa muda huku nikiendelea. Baada ya muda nilirudi nyumbani kwa mama yangu. Niliendelea kufanyiwa maombi hadi ile hali ilipopotea.
Babu yangu alikuwa akiishi Tengeru Arusha na hivyo nilipotoka pale bado hali yangu ilizidi kuwa mbaya hadi nilipofika nyumbani kwa mama ingawa babu yangu alijitahidi kunpa dawa za kila aina lakini haikuwa tiba kwangu.
****
Hadi nilipofika nyumbani na baba mdogo na mama yangu kuendelea na maombi hadi ile hali ilipotea tena. Niliondoka nyumbani kwa mama yangu na kwenda kuishi na mama yangu mdogo Judith ambae ni mdogo wa mama yangu na hali yangu ikawa nzuri na niliendelea kwenda shule vizuri nikiwa kwa mama yangu mdogo hadi nilipomaliza kidato cha kwanza.
Na nikiwa kwa mama yangu mdogo niliendelea na maombi chini ya mchungaji kipara kanisa la Lutherani na kila nilipoenda kwenye maombi hali ilizidi kuwa ile ile. Nilimaliza kidato cha kwanza vizuri na kurudi kwa mama yangu nilikaa kwa muda mrefu bila kuugua tena na nilizidi kwenda kwenye maombi ya Mwakasege na kwa wengine wengi.
Likizo ilifika na baba mdogo na mama walizidi kunipenda hawakuchoshwa na ile hali yangu walizidi kunitia moyo ingawa kwa upande wangu ilikuwa nikikosa sana amani kutokana na ile hali. Mwaka uliisha na niliingia kidato cha pili salama nilisoma vizuri baada ya muda kidogo hali ikaanza tena, niliugua kwa muda mrefu nilitamani kujiuwa kwani hata hamu ya maisha ilinishia.
Nilianza tena kukaa nyumbani shule siendi tena hali ilikuwa mbaya. Ndipo mama na baba mdogo alichukua hatua ya kwenda kumshtaki baba yangu mzazi kutokana nayale maelezo ambayo niliwaelezea, maana shuleni mwalimu aliniambia nikae nyumbani hadi nitakapopona ndipo nirudi shuleni, roho iliniuma sana sikusoma kwa raha na sikuishi kwa raha kutokana na ile hali.
Tulienda hadi kituoni na mahakama iliamua kesi ile ikaishie kanisani, ilibidi twende hadi kanisani na tulipofika kanisani tulikutana na Padri Moleni wa kanisa la Ngarenaro kwa Father Babu na ndiye aliyeanza kunisaidia tena nilianza kuombewa maombi mengine tena ya kikatoliki na padre aliendelea kunihoji maswali kila tulipoona na nilimwambia padri nilikuwa ni mkatoliki na nilishapata komunyo ya kwanza na kipaimara na tangu, nilipofika kwa baba sikuwahi kuja kanisani kwani mamdogo alinipeleka kanisani kwake na baada ya muda kanisani kwake nilifukuzwa akaniambia kwanini wakufukuze nikamwambia hali halisi iliyonikuta hadi kufukuzwa kanisani hapo. Padre aliumia sana na kuniambia maneno haya:CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Emmy mwanangu si kila asemaye Bwana atakaye urithi ufalme wa mbinguni. Na usichukie makanisa mengine kwa ajili ya mtu mmoja,na pia siku hizi watu wengi wanachagua makanisa mengine kwa kufungua makanisa na kuyapa majina kama ya makanisa mengine,” Nikamwambia kwa nini amesema hivyo Padre akanijibu.
“Unaweza kwenda kanisa lingine, kama hilo hilo na zikawa na utofauti na wakakuombea ukapokea uponyaji kabisa, kwa hiyo kaa ukieleza kuwa wapo wanaochafua makanisa kwa kufungua makanisa yao na kuyapa majina ya makanisa mengine lakini mambo wanayokuwa wakiyafanya ni tofauti kabisa.
“Kuwa, hiyo usije ukakutana na kanisa lingine kama hilo ukajuana na wenyewe wako hivyo hapa na kwanza muombe Roho mtakatifu akuongoze na akufunulie na akuonyeshe mahali salama pakumwabudu,” nikamwambia asante Padri.
Tuliondoka na kuelekea nyumbani kesi ikiwa mikononi mwa Yule Padri: Siku ziliendelea na tulirudi tena kanisani ndipo Padri aliniuliza baba yako anaitwa nani? Nikamwambia anaitwa Ernest Tairo.
Padre alikaa kwa muda bila kuongea lolote. Baada ya muda akaniambia pole sana mwanangu, baba yako nimeshaonana nae na alikuja hapa kanisani kwani nilikuwa na maongiezi nae na aliniambia kuna kanisa ambalo, mke wake anamshawishi aende uko na alienda na alipoenda wakamwambia amtoe kafara mtoto wake wa kwanza ili awe tajiri, kwani wewe ni mtoto wake wa ngapi? Nikamwambia mimi ni mtoto wake wa kwanza. Basi mama yangu alianza kulia kwa maumivu na mimi nibaki nalia padre alizidi kuumia lakini padre alisema haya. Nimemwambia tuonane na hiyo siku atakayo kuja nitawaambia na nilimwambia aje na mkewe.
Basi siku zilizidi kwenda hatukuweza kuonana. Tulienda tena kanisani na tulipofika tulikaa kikao tukiwa mimi Shangazi yangu Yule niliyekuwa naishi nae, Baba yangu mzazi, mama yangu mzazi, baba yangu mdogo, na wengine wengi tukiwa pamoja na padre na baadae maamuzi yakatolewa baba yangu akaletwe na maaskari kabla ya kufika kwake.
Askari walienda hadi nyumbani kwa baba na kuja nae akiwa na mkewe. Na walipofika kikao kiliendelea. Padre akamwambia mama yangu wa kambo naomba usome hii sehemu ya biblia hapa, na ukimaliza tutaendelea na mengine. Mamdogo alikataa na kumwambia Padri niambie ni sehemu, gani ya biblia nisome kama naweza.
Padre akamwambia chukua biblia hii usome. Akamwambia ninayo biblia yangu sema nisome wapi. Walizidi kuwa tofauti, mumewe akamlazimisha asome lakini akiisukuma ile biblia na baadaye padri akamwambia sasa msalaba huu hapa kama ni kweli ujamfanyia chochote kile huyu mtoto gusa huu msalaba. Mama wa kambo akajibu hivi mimi siabudu misalaba padre akamwambia siulikuwa mkatoliki wewe na sijakwambia uguse msalaba kwa kukwambia uuabudu hapana nataka uguse tu kudhibitisha kuwa si wewe uliyeyafanya haya.
Padre alimwambia baba yangu mzazi aanze na baba akagusa na alipomaliza, mama wa kambo akaambiwa auguse lakini alikataa katu katu na ndipo walipomlazimisha kwa nguvu lakini mamdogo (mama wa kambo) alisema hahabudu misalaba na kuchuku aule msalaba wa padari na kuuvunja kati kati. Ndipo baba akampiga mkewe kwa kitendo kile alichokifanya mkewe. Maongezi yaliisha na kuchukua majukumu mengine.
Padre akamwambia baba yangu mzazi tunaenda hadi kwako kufanya ibada fupi ya upatanisho na utoe na nguo za huyu mtoto. Kwani nilipoondoka kwa baba sikuchukua chochote na niliondokea shuleni.
Baba alikubali na tuliondoka pale kanisani wote na kuelekea nyumbani kwa baba matejoo. Tulifika na padre alimwaga maji ya Baraka Yule mama alikuwa akikemea.
Tuliingia ndani na tulianza ibada fupi na tulipomaliza, padre alituambia tushikane mikono kwa ishara ya kusamehana na tulipomaliza padre alimwambia baba na yule mama tunaomba nguo za huyu binti ndipo mama wa kambo aliposema hivi hizo nguo zilikaa hapa kwa muda mrefu na nilipoona haji kuchukua hadi niakaenda kuzigawa kijijini, padre akamwambia uliendaje kugawa nguo za mtu ambae yupo na utagawaje nguo za mtu bila idhini yake kwani amekufa? Yule mama hakujibu chochote kile alinyamaza kimya ndipo baba aliposema kuwa nguo ziko kwenye dari.
Padre akauliza kweli mnaziweka, nguo za mtu ambae yuko hai mnaziweka dari ni kweli? Yaani hapo nyumbani kwa baba nyumba, yake vinasing board kwa hiyo wameziweka ufa juu. Padre akasema basi zitoeni lakini haikuwa hivyo baada yake baba alisema tulishazitoa tulizigawa kwa hiyo hapakueleweka. Tulimaliza Ibada na kuondoka, na nguo zangu hadi leo hii sijajua zilipoenda.
Mama yangu mzazi Ruth Mwakalinga, akawaambia basi kama mmeamua kugawa hizo nguo, naomba nguo zile za ndani, paliendelea kuwa kimya hakuna chochote kile walichojibu kuhusu nguo zangu za ndani: Tuliachana na padre, na padre alituahidi kuendelea kutuombea. Hali ilizidi kuendelea kuwa, mbaya kwa upande wangu, hivyo basi kwa padre ilishindikana hivyo kesi iliendelea mahakamani.
Niliumia sana kwani shule siendi na hali yangu kwa ujumla inaendelea kuwa mbaya zaidi hivyo basi kesi iliendelea mahakamani nikiwa mimi, baba mlezi ambae ni mume wa mama yangu mzazi kwa jina la Stephen Ngome na mama mzazi Ruth Mwakalinga.
Kesi iliendelea katika mahakama ya Mwanzo pale Ngarenaro na mwisho wa siku kesi iliisha na hatimae baba yangu mzazi kushinda ksesi na kutaka kulipwa shilingi elfu thamanini hivyo ililazimu baba mlezi kutoa elfu themanini hizo ili kuweza kumlipa baba yangu mzazi, yule aliyenitendea mabaya yote bila huruma yoyote ule.
Tulimpa kiasi hicho cha fedha na kesi kuisha na tuliachana nae kila mmoja kuendelea na mambo yake. Tuliendelea kutafuta suluwishi la uponyaji wangu bila mafanikio.
Ilitokea siku moja mama yangu mzazi alipata safari ya kwenda Mbeya, kwa dada yake kwani kwa wakati huo mama yangu alikuwa ni mjamzito na hivyo alipendelea zaidi kwendakujifungulia mwanae mbeya.
Nilibaki na uwangalizi wa baba mlezi na mama zangu wadogo, wadogo wa mama yangu mzazi hali yangu ilizidi kuwa mbaya zaidi kila palipokucha.
Siku moja nikiwa nyumbani hali ilibadilika ghafla na baba yangu mlezi alikuwa kazini nyumbani nilikuwa na ndugu zangu tu, watoto wa baba mlezi.
Baba alipigiwa simu na kurudi nyumbani hali yangu ikiwa bado ni mbaya alikuwa na rafiki yake kwa jina la Ntwale aliyezoeana nae kama baba yake.
Hivyo alimpigia simu na walikutana nyumbani kwetu na walipeana ushauri wakiwa wawili. Waliamua kunipeleka Kisongo Arusha kwa Ngurumo wa upako kwa jina lingine aliitwa mchungaji Soderi tulienda hadi anapofanyia huduma lakini hatukumkuta, tulielekezwa nyumbani kwake, baba yangu mlezi yule mzee Ntwale hawakukata tama tulielekea hadi nyumbani kwake bila mafanikio yoyote.
Tulifika na kuwakuta watumishi wake na walituambia saa hizi kwali mtumishi hamtaweza kumuona labda mje kesho au tuachie namba zenu za simu. Baba aliwapa na hivyo tulirudi nyumbani bila kupata huduma yoyote. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hali yanguilizidi kubadilika kila siku maajabu ya kila aina yakiendelea kuonekana kwenye mwili wangu. Niliendelea kukaa nyumbani huku nikiendelea kuombewa na kila mtu. Mungu alishusha huruma zake na hali yangu ikaanza kuwa nzuri shuleni niliitwa ofisini na mazungumzo yalikuwa hivi.
Mwalimu : Emiliana kuna mzazi wako ameleta madaftari hapa na amesema tukukabidhi na hayo mengine usiyatumie.
Emiliana : Mwalimu mzazi yupi huyo?
Mwalimu : Kwa taarifa alitokea hapa amesema ni baba yako
Emiliana : Mwalimu kwa nin amesema haya mengine nisiyatumie kwani yana nini?
Mwalimu: Sielewi
Niliachana na mwalimu na kuelekea darasani, kichwani mwangu nikielewa aliyeleta hayo madaftari na kusema ni baba yangu atakuwa ni baba yangu mzazi.
Nilipotoka shuleni nilifika nyumbani na kuwaelezea wazazi wang hali halisi na waliendelea kulifuatilia mwenyewe. Niliendelea kwenda shuleni vizuri lakini siku moja nikiwa naelekea shuleni nilipanda gari vizuri na nilipofika kituoni nilishuka na wakati naelekea na njia ya kwenda shule alitokea, mwanamke mmoja akiwa amevaa kininja alinipiga ngumi ya mgongo na damu ziliruka mdomoni, mwangu na nilipoanza kuomba msaada kwa watu waliokuwa wakipita walinisaidia na niliweza kuwaonyesha muhusika aliyenipiga lakini walidai hawamuoni.
Sikwenda tena shuleni ilibidi nirudi nyumbani. Nilirudi nyumbani hali ikizidi kuwa mbaya zaidi na niliendelea kutapika damu tu. Niliendelea kukaa nyumbani kwa huduma zaidi, niliendelea kuombewa hadi hali ilipojirudi katika hali yake. Mungu alinisadia na niliendelea tena kwenda shule kama kuwaida.
Na safari ya mama yangu ya kutoka Mbeya na kurudi Arusha ilifika na alirudi salama na kuendelea kunipa huduma. Niliendelea kwenda shule vizuri bila tatizo,lolote lile.
Baada ya muda tena nikiwa natoka shule nilikutana na vijana watatu wakiwa wamevaa kininja na walikuwa katika kituo cha kupanda gari. Nilifika na nilikuwa nasubiria usafiri na hao walikuwa na tax nyesi isiyokuwa na namba yoyote, walinifuata na kuniambia haya.
Wao Wewe unaitwa Emiliana
Mimi: Hapana mimi siitwi Emiliana
Wao: Wewe ni Emiliana kwani baba yako si anaitwa Ernest?
Mimi: Siitwi Emiliana jamani na sina baba anayeitwa Ernest?
Walichukuwa uwamuzi wakuninyang’anya madaftari yangu mawili na biki yangu moja. Na walipochukua yale madaftari na kusoma jina waliniambia hivi
“Tumekuuliza unaitwa Emiliana ukakataa mbona hapa umeandika Emiliana?” Sikujibu chochote zaidi nilizidi kulia uku nikiendelea kuomba msaada kwa watu waliokuwa kituoni hapa na kila niliyemuomba msaada alikuwa akicheka na kusema malaria imenipanda kichwani ingawa nilijaribu kuwaonyesha wale vijana lakini walidai hawamuoni mtu yeyote Yule aliyekuwa akiniletea vurugu na kuzidi kuniambia niende hospitali labda malaria imenipanda kichwani.
Nililia sana ingawa sikupata msaada kwa wale watu wote waliokuwa katika eneo lile. Vijana wale waliamua kunitemea mate kwenye banda la uso na walipomaliza waliondoka na walienda na yale madaftari yangu na ile kalamu yangu, kichwa kilianza kuniuma paleplae na alitokea kijana mmoja ambae ni kondakta wa magari yakuelekea nyumbani akanishika mkono na kuniiingiza kwenye gari nakuelekea nyumbani.
Nilifika nyumbani salama huku nikiwa na maumivu makali sana kichwani, nilimuelezea mama yangu hali halisi iliyonikuta na akaniombea niijipumzisha hali ikiendelea kuwa mbaya.
Usiku uliingia maumivu yakiendelea kuwa makali zaidi, kichwa kiiendelea kuuma sana haswa kwa panda la uzo, ndipo damu zilizidi kutoka utosini na nilipozidi kulia yalitoka macho toka utosini na nilipozidi kulia yalitoka machozi ya damu hali ilizidi kuwa mbaya kiafya.
Mama aliendelea kuniombea bila kukata tamaa niliendelea kutiwa moyo na watumishi mbalimbali na rafiki zangu maombi yaliendelea kila sehemu waliokuwa Mbeya ambao ni ndugu wa mama yangu mzazi waliendelea kuniombea, waliokuwa Moshi waliendelea na maombi na hata kwa ndugu wa mama walioko Iringa walindelea na maombi na kwa watumishi wote walioko Arusha waliendelea na maombi bila kukata tamaa, hali ilizidi kuwa mbaya kwa upande wangu. Ilifika mahali mama yangu alikata tamaa nakusema haya.
Ruth Ee Mungu kama ni mtoto ni wewe ulinipa, na nimemlea hadi umri huu wa miaka 18, kama ni mapenzi yako naomba yatimizwe. Na kama si yako naomba uzima kwa mtoto wangu.
Aliyaongea kwa uchungu na kwa machozi ya uchungu. Ndugu na waumini wenzake wakiendelea kumtia moyo kwa wakati mgumu uliomfika.
Na wengineo, walijua ni lazima nife tu chakushangaza baadhi ya wengineo waliokuwa ni majirani wa mama yangu walizungumza maneno machafu mtaani bila kuwa na huruma.
Waliongea haya:CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
- Inawezekana mama yake anaficha siri yamwanae, uenda katoa mimba sasa ndiyo hayo.
- Wengine wakasema haya uenda mama yake mwenyewe anamuuwa mwanae kila mmoja alitamka analoweza kutamka na kwa walio mzarau Mungu walisema Mtu gani huyu ambae anaombewa na watu wote hao lakini haponi alafu eti ni walokole, walokole si wanasemaga, wanaponya mbona huyo haponi ni maneno yaliyoendelea kutolewa na binadamu ambao hawakuwa na hofu ya Mungu ndani yao Nilizidi kuumia zaidi kwa maneno makali na yasiyokuwa na uzima ndani yake.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment