Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

NIACHE NILIE - 5

 





    Simulizi : Niache Nilie

    Sehemu Ya Tano (5)



    Ilipoishia…

    Palikucha na mimi kama kawaida nilielekea shule na kuwaeleza baadhi ya marafiki na waalimu pia. Nilimwambia kwa lengo la kuwaomba wamuombee zaidi.

    Songa nayo…



    Shule ilipotoka niliendelea moja kwa moja hadi hospitalini nikiwa na rafiki zangu. Tulipofika tulimwombea baba na baada ya hapo rafiki zangu waliniomba waende niliagana nao na baba pia aliwashukuru na kuwaaga nao waliondoka. Baada ya muda mfupi mama alikuja na chakula cha mgonjwa alimhudumia na muda wa kutoka ulipofika tuliondoka.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku ziliendelea na hali yangu ikawa imetulia ingawa bado damu zinanitoka puani lakini sehemu nyingine nilikuwa sawa kabisa siku moja nikiwa nyumbani mama alinipigia simu na kuniambia baba yako ameruhusiwa lakini ameambiwa apumzike mahali na asipande gari kwa mwendo mrefu kutokana na moyo kwa hiyo nitakuwa kwa Paul. Baada ya hapo nilimwambia basi kama ni hivyo kesho nikitoka shule nitakuja kukaa huko ili tusaidiane. Mama aliniambia Ester na hiyo hali yako utaweza kweli, nilimjibu nitajitaidi mama. Siku iliyofuata nilienda shule na baada ya masomo nilielekea KCMC kwa mjomba wangu Paul ambapo ndipo baba alipoenda kupumzika nilifika salama na niliwakuta, wote niliwasalimia na kumuuliza baba, baba unaendeleaje? Alinijibu naendelea vizuri kabisa naamini kesho nitaamka salama kabisa na nitarudi nyumbani Arusha kwani nimewakumbuka sana watoto wangu.



    Nikamwambia hata mimi naamini kesho utaamka salama kabisa na ninaamini hata sasa ni mzima. Alimjibu kesho nitaamka mzima na nitakapoenda Arusha itabidi niende kazini moja kwa moja kwani ninakazi nyingi na kuna ndege za kwenda kupaka rangi. Naamini Ester nikifanya kazi kwenye ndege moja tu nitakulipia ada yote na kukununulia mahitaji yako ya shule. Sawa nilimjibu sawa baba lakini katika kujibu kule moyo ni nilikuwa na uchungu na nilitamani kulia pia.

    Muda ulisogea siku ziliendelea kwenda na mkuu wa shule bado akawa anaturudisha ada ya shule. Niliumia sana kwa wakati ule kwani wa kumwambia suala la ada yuko kitandani. Nilizidi kumuomba mwalimu na alinielewa. Tuliendelea kumuuguza baba na watumishi wa Mungu waliendelea na maombi kila kukicha. Aliombewa na mchungaji kabese ambae ni mhumini wake na tena ni mzee wake wa kanisa na pia aliombewa na mchungaji Masalu aliyeishi Mbauda Kerai Arusha aliombewa pia na waumini wa makanisa mbalimbali na Paster Haule ambae ndiye alikuwa mchungaji wake wa kwanza kabla ya kufunguliwa kwa tawi la chemchem chini ya Paster Kabese ambae ndiye mchungaji wake . kuisahau familia ya Sabiti ambae anaishi Airport Kia ambapo baba alifanya kazi pia. Mungu alisikia maombi ya watu wake baba aliendelea vizuri na kurudi Arusha ingawa aliporudi hakuweza kwenda kazini aliendelea na mapumziko. Na mimi nilirudi nyumbani Uru kitanda nilipokuwa nikiishi na babu yangu ambae ni mjomba wa mama yangu Ruth Mwakalinga.

    Niliendelea na shule kama kawaida siku moja nikiwa shule nilianza tena kuumwa na baadae nilipelekwa nyumbani na mwalimu Rose Mery na kuendelea na mauguzi niliisi kuwa utakuwa ni mshtuko kutokana na ile hali ya baba yangu mlezi nilianza tena kutapika damu na nyingine kutoka puani hali yangu ikawa mbaya zaidi kwani kwa wakati ule mama yangu alikuwa katika wakati mgumu. Na pia kuja Moshi kwake ilikuwa ni ngumu kwani anamuuguza baba. Hali yangu ikawa mbaya zaidi na ndipo mchumba wangu Deodath Joseph Kimario alipofikishiwa ujumbe na mtoto wa babu yangu kwa jina la Deodath Hendry Chua. Alipoenda dukani kwa Deodath Joseph Kimaro na kumueleza hali yangu halisi alifika nyumbani na kumuomba babu anipeleke hospitali babu alikubali na baadae tuliondoka.

    Tulipokuwa kwenye gari alikuwa akiendesha aliniambia Ester tumeshaangaika kwa madaktari mbalimbali lakini bado hali ni hii jaribu tena kwenda, kwa wataalamu nikamwambia haitawezekana kwa waganga sintakaa niende alinijibu utakaa hivyo hadi lini? Nilimwambia nitakaa hivi hadi mwisho alinijibu hali hii siyo yakuchezea na usipoangalia utakufa. Nilimjibu acha nife kwani nitakuwa wakwanza kufa? Kwanza kufa mbona ni kitu cha kawaida. Alinijibu sitakubali nitaangaika na mimi nione.

    Tulifika hospitali na kupata matibabu na niliambiwa ni malaria na presha. Nilipewa dawa na baadae nilirudi nyumbani lakini nilipofika tu na kuanza kutumia dawa zile nilianza kutapika zaidi na hali yangu ikawa mbaya zaidi tulisita kumwambia mama kwani tuliisi atachanganyikiwa. Na pia mama alikuwa ni mjamzito kwa wakati huwo. Niliendelea kumuomba Mungu na pia Deodath Joseph ambae alikuwa ni rafiki yangu kwa msemo mwingine nilishaanza kumuona ni mchumba wangu aliendelea kuangaika. Baada ya muda mfupi aliniletea dawa akaniambia niwe naogea asubuhi na jioni nami nilijikuta nikifanya vile na nilishasema sitaki madawa ya waganga lakini nilijikuta naanza kutumia dawa zile hali ilibadilika na zile dawaza hospitali niliziacha. Na niliendelea na ile dawa ya kuoga lakini cha ajabu nikaifanya kuwa siri yangu sikupenda mtu aone. Siku zilisonga hali ikawa nzuri kabisa nilianza kwenda shule kama kawaida siku moja nilitoka shule na nilipofika nyumbani nilikuwa na hamu ya matembere.nikiwa shambani nilianza kuhisi kizunguzungu na maumivu makali ya kichwa yaliendelea ndani yangu nilichuma haraka haraka na kutoka shambani. Nilielekea nje na kuanza kuchambua mboga. Bibi yangu alirudi sokoni kwani alikuwa ni mfanya biashara wa maandazi sokoni, babu yangu alikuwa ni baba wa nyumbani kutokana na hali yake ya udhaifu wa mguu hivyo yeye alikuwa akiangalia mifugo yake pamoja na kazi za shamba.

    Nikiwa nafanya kazi zangu za hapa na pale na uku nikiwa nachambua mboga gafla simu ikapigwa na nilipopokea nilikuta ni mama yangu. Nilipokea na mama hakuwa na mazungumzo mengi maana nilimsalimia lakini hakuitika. Aliniambia moja kwa moja bila kujali Ester mwambie babu yako baba ameshafariki. Nakumbuka ilikuwa ni tarehe 6/4/2010 siku ya jumanne saa 2: kasoro dk 25 nilichanganyikiwa kwa sababu nilipokuwa na wasiliana na mama alituambia anaendelea vizuri ingawa kazini bado ajaweza kwenda. Baada ya simu ile sikujua kilichoendelea baada ya muda niliamka na kumbe nilikuwa nimezimia nilimpigia mchumba wangu Deodath simu na kumueleza na baadae nilianza kuondoka na kwenda Arusha siku ile ile niliondoka na kuelekea Arusha nakumbuka nauli pamoja na matumizi madogo madogo nilipewa na mchumba wangu huyo.

    Niliondoka Moshi saa 6:00 jioni nikiwa nimeambatana na mjomba wangu mdogo Deodath Hendry Chua. Tulianza safari na tulifika Arusha saa 10 usiku nilipokelewa na ndugu zangu, ilikuwa ni huzuni tupu kwani nilizidi kuumia nilipomwangalia mama yangu na ile hali aliyoachwa nayo. Tuliendelea na mipango ya msiba na muda ulipofika tulizika salama. Amini usiamini mama yangu aliachwa katika wakati mgumu sana kwani ni mjane aliyeachwa akiwa ni mjamzito bado kuna watoto wanahitaji kusoma. Tulimaliza msiba salama na baada ya mapumziko mafupi nilirudi Moshi kuendelea na masomo. Maswali yalianza kunijia, nikaanza kujiuliza moyoni mwangu. Sasa baba ndiyo hivyo Mungu kampenda zaidi yetu ada sijalipiwa bado kidogo kufanya mtihani na mwalimu anasema mtu ambae ajatoa ada atafanya mtihani sasa mimi si ndiyo nimekwisha. Nililia sana na hali yangu kiafya ilianza kubadilika nilianza kukonda tena na pia hali ya ugonjwa ikazidi kuendelea na yote hayo yaliendelea kutokana na mimi kufanya yale niliyoambiwa nisifanye kwani madaktari wengi walinishauri niepuke sana .

    i. Kukasirika

    ii. Kushtuka

    iii. Kukemewa kemewa

    iv. KutokuwazaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sasa yote yanaanza kutokea na hizi hali zinaendelea kutendwa, kutokana na mimi kutoeleweka na hasa pale unapokuta muda mwingi nikiwa nalia. Maana hata kulia pia nilinyimwa kutokana na yale maumivu ya kichwa. Siku moja nikiwa nyumbani Deodath alinipigia simu niende dukani kwake na nilipofika yaliendelea haya:-

    Deodath Vipi Ester

    Ester Poa

    Deodath Unaendeleaje?

    Ester Naendelea vizuri.

    Deodath Pole na msiba

    Emmy Asante

    Deodath Ester ngoja ni kwambie kitu huku siyo wakati wa wewe kuendelea kuumia na wala si wakati wa wewe kuanza kusema hivi Mungu hivi Mungu hivi Mungu hapana huu ni wakati wa wewe kuwaza mtihani wako sisi tuko katika safari moja leo yeye kesho sisi je tuweje? Na siyo kuwa katika hali hiyo ya mawazo na unajua hali yako ilivyo ebu jaribu kupunguza hayo unayo yawaza.





    Nilimjibu

    Ester Haiwezekani

    Deodath Haiwezekani nini?

    Ester Ni ngumu sana kutokuwaza kuwaza nilazima kwani sielewi nitaishije.

    Deodath Mungu atakusaidia Ester kama alieza kukuumba atashindwa kujua utaishi vipi?

    Ester Hapana Deo.

    Deodath Hapana nini hakuna linalo shindikana Ester muombe Mungu atakusaidia

    Ester Sijui maana hali ngumu.

    Deodath Kuna nini Ester mbona haueleweki na pia punguza kulia ebu ongea vizuri ili nielewe. Siyo wakati wako wakulia huu ebu sema.

    Ester Deodath hapa unaponiona sielewi mbele ni wapi wala nyuma ni wapi na sijui pazuri ni wapi na pabaya ni wapi.

    Deodath Kwa nini unaongea kauli kama hizo.

    Nilianza hivi:-

    Deodath rafiki yangu kwa sasa naona mambo magumu sana kwangu, kama nilivyokwambia baba yangu mzazi alishanikataa na hata mimi mwenyewe simpendi na ndugu zangu wenyewe ndio hao wamesikia babayangu mlezi amefariki lakini hata kuja kuzika imekuwa ni ngumu kwao na wakati wanajua ndiye aliyekuwa ananitunza lakini imekuwa ngumu kwao na isitoshe mama yangu ni mama wa nyumbani sasa kwangu itakuaje? Ndugu zangu hao tangu nikiwa mdogo hakuna mwenye mpango na mimi nimeteseka lakini hakuna aliyejigusa na hata kumsaidia mama yangu ela ya matibabu hawakuweza ukizingatia mimi ni damu yao na nimatajiri, sasa ndiyo wakati wa kuwa chokoraa umefika.

    Deodath Usiseme hivyo Ester unamkufuru Mungu Ester

    Ester Simkufuru Mungu simkufuru Mungu hata kidogo nina ndugu Deo, ni matajiri lakini hawataki kunisaidia sasa baba Mariamu aliyenijali aliyenipenda kama watoto wake, aliyenithamini aliyejua uchungu wa mtoto ni upi aliyejua kuwa nikiumwa natakiwa kupelekwa hospitali aliyejua nikirudishwa ada natakiwa ada sasa leo hayupo nitakuwa mgeni wa nani mimi.

    Deodath- Mungu atakupa msaada mwingine usiogope endelea kumwomba tu.

    Ester Hakuna na hatatokea baba kama baba mariamu.

    Baba anayejua utu ni nini anayemthamini mtu kama anavyojithamini mwenyewe.

    Deodath Ester tuachane na hayo kwani unatatizo gani?

    Ester- Kwanzia mwaka umeanza Deo sijalipiwa ada ya shule na mwalimu amesema mwanafunzi ambae ajatoa ada hatafanya mtiani.

    Deodath Kwani ada ni sh ngapi?

    Ester Bado sijajua

    Deodath Fuatilia alafu uje uniambie.

    Ester Asante Deo, nitafuatilia.

    Tuliachana na mimi kuelekea nyumbani baada ya kufika nyumbani bado niliendelea kumfikiria Deo na kujiuliza maswali kwa nini ameniambia vile?

    ******




    Niliendelea kumuweka Deodath moyoni nilimuona ni mtu wa pekee sana kwangu na ni msaada mkubwa sana maana siku ya msiba hakujali kuacha kazi zake na kuja kuambatana nasi katika wakati mgumu tulionao. Niliendelea kumuheshimu sana na kumuona ni mtu bora sana kwangu. Siku zilizidi kusogea niliona sinakimbilio tena. Nilienda shule na ile hali ikuwa imepotea nilimfuata mkuu wa shule na kumuuliza kiasi nilichokuwa nikidaiwa ilikuwa hivyi:-

    Emmy Shikamoo mwalimu

    Mwalimu Marahaba Emmy hujambo

    Mwalimu Pole na msiba

    Emmy Asante mwalimu

    Mwalimu Vipi Emmy kuna nini?

    Emmy Mwalimu naomba kujua nadaiwa sh ngapi?

    Mwalimu aliniambia kiasi nilichodaiwa kuwa ni laki mbili na kumi . nilishukuru nakuondoka kuelekea darasani niliendelea na masomo na baada ya masomo nilitoka shule na nilipofika nyumbani nilimpigia Deodath na kumueleza kwani alinimbia nikishauliza nimpe jibu. Nilimwambia na kuniambia kuwa atazilipa hizo fedha.siku inayofuata nilienda shule na alikuja kweli na kuzitoa zile fedha. Nilishukuru Mungu. Nilimpigia simu mama na kumweleza mama alishukuru sana na kusisitiza kumueshimu sana Deo. Siku zilisogea na mwaka uliendelea kusogea, na siku ya kufanya mtihani wa kuitimu elimu ya sekondari ilikaribia. Yapata kama mwezi tufanye mtihani hali yangu ikaanza kuwa mbaya tena, hali za damu zilianza upya kutapika kutoka puani, utosini na blidi isiyoisha.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mambo yalikuwa mabaya na hali nayo ikawa mbaya zaidi. Nikiwa nyumbani Deodath alifika na kuikuta hali ile. Alichukua uwamuzi wa kuniweka kwenye gari na kunipeleka kwa mtaalam aliyejulikana kama Dokta Chua yaani Mganga Chua niliudumiwa na kupewa dawa za koga na za chai pia. Niliporudi nyumbani kwa kuwa sikuwa naishi na Deo nilitupa dawa zile chooni na kuziacha zile za kuoga tu. Nilizitumia kwa muda mfupi na baadae nilizitupa chooni. Hali yangu ikawa nzuri kidogo nikaanza kwenda tena shule na siku ya kufanya mtihani ikawadia. Nilifika shule na kupangwa katika chumba cha mtihani na ninakumbuka ilikuwa ni tarehe 4/10/201. Baada ya kuingia tu darasani kichwa kilianza kuniuma lakini nilimuomba sana Mungu anisaidie, nilianza mtihani wangu wa kwanza na baada ya muda mchache nilianza kutoka damu puani na ilinibidi kutoka nje. Nilifanya mtihani kwa shida sana kwani nilitoka shule nikiwa namaumivu makali sana kichwani nab ado damu ziliendelea kutoka puani. Siku inayofuata nillienda shule na nilipofika nilimomba sana Mungu anisaidie nifanye mtihani ule salama. Niligiia darasani na kuanza mtihani wa kwanza nilifanikiwa kuumaliza salama tulitoka mapumziko kwa ajili ya kujiandaa na mtihani wa pili kukiwa tunajiandaa kuingia darasani hali ilikuwa mbaya na mkuu wa shule alichukua uwamuzi wa kumpigia mama yangu simu na kumueleza, mama alimwambia atakuja, na baada ya hapo aliwasiliana na mjomba wangu Paul na kumueleza maadamu yeye alikuwa anaidhi karibu na shule aliahidi kufika hali ilikuwa si yakawaida. Wenzangu waliingia darasani na kuanza mtihani niliumias sana nilimwambia mwalimu naomba nikajaribu tena mwalimu alikubali ni kaenda kukaa kwenye dawati langu ambalo lilikuwa nje ya darasa. Waalimu walibidi kuniweka nje barazani mwadarasa langu kutokana na ile hali ya kutapika damu.

    Kwasni iliwafanya wanafunzi wenzangu kulia badala ya kufanya mtihani. Nilikaa kwenye dawati langu na kusali baada ya hapo niligeuza karatasi ili nianze kufanya yale yaliyo nihusu kufanya. Baada ya kugeuza tu karatasi sikuweza kuona andishi ata moja niliona karatasi lote jeupe yaani halina kitu chochote. Niliinamisha kichwa chini msimamizi alinigusa na kuniambia vipi tena? Nilipoinuka tu damu zilianza kunitoka puani nilisitishwa tena kufanya mtihani ule na kupelekwa moja kwa moja hadi ofisinin. Waalimu walinisaidia lakini bado hali yangu ilizidi kuwa mbaya zaidi baada ya muda mfupi nilianza kutapika damu na hali hapo hapo ikabadilika kabisa. Nilianza kutapika na baadae mwili ulianza kufa nguvu muda mchache tu alikuja Deodath ambae ni rafiki yangu alifika aikwa na pikipiki kutokana na ile hali niliyokuwa nayo ilibidi arudi nyumbani baada ya muda tena mama yangu alifika na baadae kuondoka alichanganyikiwas na hali aliyonikuta nayo. Punde si punde Deodath alifika tena shuleni akiwa na gari na ndipo alipoamua kunipeleka hospitali. Tuliongozana na mkuu wa shule pamoja na Deodath tulifika hospitali na kufanyiwa vipimo, lakini vipimo havikuonesha chochote zaidi damu ziliendelea kutoka tu. Waliniingiza wodi na baadae walinitundikia driu na kunipa dawa. Kwa mara hii nilipelekwa hospitali ya mkoa wa Mawenzi nilikuwa pale kwa muda ambao mtihani uliendelea. Nilifanyiwa vipimo vyote lakini bado havikuonesha tatizo, mitihani ilimalizika na mimi nikawa mzima kabisa, niliruhusiwa kutoka hospitali lakini wenzangu walikuwa wamesha maliza mitihani yote siku na jinsi nililia sana na mwalimu wangu mkuu aliuzunika na kunipa pole lakini bado alikuwa na maswali moyoni mwake. Aliniambia kweli huyo mama wako wakambo ajakufanyia haki hata kidogo kwa nini wakati wamitihani unakuwa mgonjwa alafu ikiisha tu unakuwa mzima? Sikuwa na jibu nilibaki naila tu, sikuwa na njia ya kufanya kwa hiyo nitihani siku fanya zaidi ya mitihani mitatu tu lakini hata hiyo mitatu nilifanya nusu nusu sikuwa nimeimaliza. Nilizidi kuumia sana kwani hata nilivyokuwa shule matokeo yangu hayakuwa mazuri nilikuwa nasahau yaani mwalimu akisha fundisha akitoka darasani ukiniuliza mwalimu kafundisha nini nilikuwa sijui tena. Wazazi wangu walihuzumika sana ndugu zangu waliumia sana kwani mimi ndiye wa kwanza kwa mama yangu.

    Nilimshukuru sana Deodath kwa moyo aliouonyesha kwangu kwani aliangaika na mimi tangu shuleni na alionesha kuwa mtu wa karibu sana kuliko hata ndugu zangu. Alikuwa anamiliki pikipiki yake binafsi lakini nilipopata tatizo lolote hakusita kuomba magari kwa rafiki zake pale kijijini. Nilimwambia kuwa asante kwa kuwa bega kwa bega nami tangu kidato cha pili hadi sasa lakini kwa kuwa mtihani umemalizika na wanafunzi wameshaanza kusambaratika basi na mimi sina budi kumaliza taratibu zilizobaki shuleni alafu nirudi nyumbani Arusha. Kwani ndipo nilipokuwa naishi na wazazi wangu. Alinijibu Ester baki tu hapa Moshi kwani uanvyotaka kurudi Arusha ni kwamba unaenda kumsumbua tu mama yako na unaelewa kuwa Yule ameachwa ni mjane atafanya mangapi na mangapi aache? Nilimjibu hata hawa ninaoshi nao wamesha choshwa na hii hali acha tu nirudi nyumbani kama nitapona sawa kama nitakufa pia sawa. Alinijibu sawa yote ni maamuzi yako. Nilimaliza kufuatilia maswala ya shule na kuagana na waalimu wangu ingawa walilia sana lakini sikuwa na jinsi.



    Nilianza kujitayarisha kwa ajili ya safari ya kurudi nyumbani Arusha. Muda ulifika nilielekea moja kwa moja kwa Deodath na nilipofika nilimuaga na alinisaidia nauli na mi kuondoka alinisindikiza hadi stendi na kuhakikisha nimepanda gari kuelekea Arusha. Tuliagana na zaidi aliahidi kuendelea kuniombea na kunisisitizia kutoacha kumuomba Mungu. Nilimshukuru na hatimae kuagana nae.

    Nilifika salama nyumbani nilikutana na mama yangu pamoja na familia yetu walinipokea kwa huzuni na hata wengine walilia. Bado mama alikuwa na huzuni kwa mimi kutofanya mtihani. Tulianza maisha ya nyumbani pamoja na mama yangu mzazi Ruth Mwakalinga na maisha yalikuwa ni magumu sana kwa upande wetu kwani baba alifariki na kutuacha kwenye nyumba ya kupanga na mama akiwa ni mjane mwenye mtoto mchanga hivyo maisha kwa upande wetu yakawa magumu sana. Tuliishi kwa shida maisha yakazidi kuwa magumu sana kwa upande wetu. Baba alifanya kazi na alikuwa na mshahara mzuri lakini fedha zake zilikuwa zakusaidia yatima na wajane na watu wasiojiweza na kwa huduma za makanisani.hivyo kutuacha bado tukiwa kwenye nyumba ya kupanga. Ingawa alikuwa amejenga nyumba lakini bado hadi sasa. Baba yangu mlezi huyo alinilea tangu nikiwa darasa la sita hadi form four mwanzoni alipofariki.

    Baba alifariki kwa ugonjwa wa moyo alituacha katika wakati mgumu sana na hadi sasa bado, maisha hayajawa sawa kwa upande wa mama yangu Ruth Mwakalinga. Mungu amlaze mahali pema Ameni. Nilikuwa nyumbani kwa muda kama wa wiki mbili hivi na baada ya hapo nilipigiwa simu na rafiki zangu na waliniambia kuwa tunahitajika kupeleka passport za kuweka kwenye vyeti vya shule na hivyo kupelekea mimi kumueleza mama.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilimwambia mama na mama alinielewa na nilianza safari siku iliyofuata yakuelekea Moshi kwa babu yangu ambae ni mjomba wa mama na ndiko nilipokuwa nikiishi tangu nilipoanza kidato cha tatu. Nilifika Moshi na kupokelewa na Deodath ambae ndiye aliyenisindikiza wakati naelekea Arusha na ndiye tuliyeanza nae urafiki tangu nikiwa kidato cha pili. Nilifika salama na kuanza kufuatilia mambo ya shule baada ya muda mfupi Deodath aliniita na kuniuliza maswali machache.

    Alianza :-

    Deodath Vipi Ester kwanzia umeenda Arusha ulikuwa unafanya kazi gani?

    Ester- Amna kazi niliyokuwa nafanya zaidi ya kuwa nyumbani tu kama unavyoelewa mama yangu hana kazi yeyote ile kwa hiyo alikuwa anapika chapatti alafu mimi nabaki na mtoto nyumbani.

    Deodath Sasa ukimaliza kufuatilia masuala ya shule unataka kufanya nini?

    Ester- Nitarudi nyumbani.

    Deodath Sasa utakuwa unaangaliana na mama yako tu.

    Ester Hapana nitakuwa namsaidia mama kukaa na mtoto wakati anauza chapati zake.

    Deodath Hapana Ester njoo hata uuze dukani kwangu alafu mimi nitafungua lingine kuliko uende ukakae nyumbani tu.

    Ester Hapana siwezi kumuacha mama yangu peke yake nitarudi tu nyumbani.

    Deodath alinisisitizia zaidi mimi kutokurudi tena Arusha, lakini bado nikawa mkaidi sana. Nilifuatilia mambo yangu ya shule na baada ya kumaliza nilianza kujitayarisha kwa safari ya kurudi Arusha. Nilimshukuru sana babu yangu na kumwambia asante sana babu kwa kuishi na mimi vizuri na sasa nataka kurudi nyumbani zaidi babu naomba uendelekuniombea. Nilielekea kwa Deodath kwa ajili ya kwenda kumuaga tena. Lakini nilipofika kwake alinikaribisha na kuniandalia kinywaji na baadae aliondoka na kuniambia nisubiri nakuja sasa hivi alafu nitakusindikiza, nilikubali na alivyotoka alifunga mlanngo baada ya muda niliona saa zinazidi kwenda na Deodath harudi niliamua tu kuondoka niliandika karatasi kumjulisha kuwa nimeshaondoka kwa hiyo asinitafute. Nilisimama na kuusogelea mlango kwa lengo la kufungua mlango na kuondoka, lakini nilipofungua mlango haukufunguka ulikuwa umefungwa na ufunguo. Nilijiuliza maswali mengi ya siyo na majibu nilisema moyoni ameenda kuletsa watu waje waniuwe au? Niliwaza mengi na muda ulizidi kusogea.saa tatu bado hajarudi saa 4 usiku ndiyo akaingia . na baada ya kuingia sikuweza hata kuongea zaidi nilikuwa nikilia alinibembeleza nilimuomba anipeleke nyumbani kwa babu yangu kwani kutoka hapo kwao na kwetu si mbali ni maji rani.

    Alinijibu lala nitakupeleka kesho sasa watu wamesha lala nilibaki nalia tu lakini hakunielewa zaidi ya kunibembeleza tu. Nilimwambia kwa sasa babu yangu anajua nimeshafika Arusha alafu niko hapa je akimpigia mama itakuwaje? Lakini Deodath hakunielewa nilizidi kulia labda atanionea huruma lakini hakuliona hilo nilizidi kulia hadi nilipopitiwa na usingizi palikucha kwenda Arusha nikaogopa kurudi kwa babu nayo nikaona ni aibu kwani nilikuwa nimelala nje ya nyumbani hiyo nikaona ile ni aibu sana. Na hivyo huo ndiyo ukawa mwanzo wangu wa kuishi na Deodath.

    Nilianza kuishi na Deodath maisha kwa upande wangu yalikuwa mazuri, alienda kutoa taarifa kwa wazazi wangu na baadae walijua kuwa niko kwa Deodath. Ndugu zangu waliongea mengi walianza kusema huyo mwanaume hata weza kuishi na Ester, kwanza anamatatizo kibao na pia majirani wa Deo walimuambia acha na huyo mwanamke mwenye matatizo anaanguka mwenyewe anatoka madamu ovyo, kwanza ni tasa. Deo aliwajibu nimempenda kama alivyo pamoja na matatizo aliyonayo nimempenda hivyo hivyo. Walimjia kwa njia nyingi hadi mimi nikawa nakosa amani na kulia lakini Deo alinitia moyo na kuzidi kuniambia kuwa atakuwa bega kwa bega na mimi. Niliishi na Deo na mama yake ambae alishakuwa mama, mkwe wangu nilikaa kwa muda mfupi sana, matatizo yalianza damu zilianza kutoka tena upya. Nipo Deo alipoamua kunipeleka kwa mganga Chua na kupewa dawa ya kuweka kwenye chain a nyingine ya kuoga na yakuchoma. Nilizitumia dawa hizo kwa muda lakini bado hali ilizidi kuwa mbaya zaidi niliendelea tu kutumia kwa kujipa moyo labda ndiyo napona lakini nilizidi kuugua tu. Hali ilikuwa mbaya sana kuliko ile ya mwanzoni.ilibidi niache hizo dawa na baadae tulienda sehemu nyingine TPC msitu wa tembo nilikutana na babu ambae ni muuguzi na kuanza kumueleza. Nilikuwa na Deo a ndiye aliyenipeleka makusudio yake ni mimi kupona.

    Nilimueleza babu Yule na kunipa dawa ya chai yakuoga na yakuchoma na nyingine yakupaka nilizitumia na kuanza kuona mabadiliko lakini kila nilipo kasirika hali ile ilijitokeza kwani siku ruhusiwa

    i. Kulia

    ii. Kukasirika

    iii. Kugombezwa

    iv. Kuwaza

    v. Na hata kushtuliwa

    *****




    Kwani nilikuwa nikifanya haya hali inajirudia tena niliendelea kutumia hizo dawa na baadae hali iligeuka na kupelekwa hospitalini na kulazwa tena ingawa nililazwa lakini hakuna kilicho onekana. Deo aliendelea kuangaika na kulazimika kurudi tena kwa Yule babu wa TPC msitu wa tembo, natulipofika babu aliamuru wa watumishi wake kwenda kuchinja mbuzi baada ya muda alikuja na damu kwenye kiganja cha mkono na kuanza kutulambisha tulilamba mimi pamoja na Deo na kukabidhiwa dawa za kwenda kutumia.

    Tulirudi nyumbani na baada ya kwenda kutumia zile dawa hali haikubadilika hali ilizidi kuwa mbaya zaidi zilianza kutoka tena kila mahali.

    i. Utosini ingawa palikuwa hapajatoboka.

    ii. Masikioni ingawa yalikuwa hayana maumivu yoyote

    iii. Machoni kwani kila nilipolia machozi yalitoka machozi ya damu.

    iv. Puani damu zilipokuwa zikitoka nilisikia maumivu makali sana ya kichwa.

    v. Nilianza kutoka blidi isiyo katika

    Niliugua kwa muda mrefu na ilimbidi kurudi tena katika hospitali ya Mkoa wa Mawenzi na nilivyofika madaktari walitishwa sana na ile hali na baadae hata kabla ya kunipa huduma walisema hawawezi kunisaidia kwa hiyo tunaomba kama unaweza kwenda KCMC uende lakini hapa kweli hatuwezi, maana hatujawahi kuona hii hali Deo hakukata tamaa tuliondoka na kurudi nyumbani. Hatukuweza kurudi tena KCMC kwani ndiko nilikotibiwa tangu nikiwa kidato cha pili hadi namaliza lakini bado hali ni ile ile.

    Tulirudi nyumbani na palipokucha tulirudi tena kwa Yule babu na tulipofika tulimueleza babu hali halisi na baadae Yule babu aliniambia kuwa jina la Emiliana ni jina la bibi yangu ambaye alishafariki siku nyingi kwa hiyo huyo bibi alikuwa na bangili ambayo mimi natakiwa kuwa nayo, ili hayo matatizo yaniishe. Deo alikubali na kumwambia, tutarudi kesho. Tuliondoka moja kwa moja tulielekea hadi maduka ya wahindi na kutafuta bangili tulipata na Deo kuinunu kwa sh elfu kumi. Tulielekea hadi nyumbani hali ikizi kuwa mbaya zaidi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Palipokucha tuliendelea TPC msitu wa tembo kwa Yule babu na tulipofika tulimkabidhi ile bangili na aliifanyia mambo yake na kunivalisha na kuniahidi kutokuumwa tena. Alitukabidhi tena dawa za kwenda kutumia nakumbuka ilikuwa tarehe 23/11/2011 jumanne. Tulipofika nyumbani nilianza kutumia dawa zile nikiwa na ulinzi wa bangili mkononi nilitumia dawa zile hadi nilichoka lakini bado hali iliendelea kuyumba. Nilimaliza dawa na hali ikawa bado ni mbaya. Muda ulienda nikaendelea kuteseka baada ya muda mfupi matokeo ya kidato cha 4 yalitoka na Deodath, alifuatilia na aliporudi aliniambia jina lako lipo lakini hakuna kilichoandikwa haionyeshi kuwa una ziro wa laa, wameandika jina halafu wakaacha wazi. Ingawa Deo aliwasiliana na mkuu wa shule lakini mwalimu naealidai kuyapokea yakiwa hivyo hivyo. Niliendelea kuumia lakini bado sikuwa na njia nyingine ya msaada. Deodath aliendelea kunitia moyo na kuahidi kuwa maisha yake yakiwa mazuri ataniendeleza kielimu. Nilimshukuru sana.

    Siku zilisogea na bado hali yangu ilikuwa mbaya mama mkwe alianza kuchoshwa na hali yangu na hata upendo kwangu kupungua kabisa lakini namshukuru Mungu Deo aliliona hilo na kuendelea kunitia moyo huku akiniambia siku moja Ester utaishi kwa amani na furaha kabisa na mimi nitahangaika na wewe hadi sumli, yangu ya mwisho usijali Ester niko nawe bega kwa bega hadi Mungu atakapoamua. Niliendelea kulia na mambo yaliendelea kuwa magumu kwangu. Tulirudi tena kwa babu na alituambia turudi twende siku inayofuata. Siku inayofuata hatukurudi tena kutokana na hali yangu kuwa mbaya zaidi nakumbuka ilikuwa ni tarehe 3/12/2010 . niliamka nikiwa na hali mbaya zaidi Deo alibaki kulia tu kwani aliponipeleka hapakuwa na jibu niliumia sana kuona mwanaume akiwa analia mbele yangu lakini sikuwa na njia zaidi tulizidi kulia wote. Hakuna ambae hakuuumizwa na mwenzie Deo hakupenda mtu yeyote kunikera wazazi wake walianza kumwambia unirudishe kwetu alikerwa sana na hayo maneno ya wazazi wake na ndipo wazazi wake wakaanza kumchukia na yeye pia na kumwambia unaangaika na mwanamke ambae hana faida yoyote zaidi anakufilisi tu maana akiumwa tu kidogo hospitali na hospitali ni hela inatumika. Walizidi kusema walivyojua na baada ya muda mfupi nilianza kulazwa na njaa kutokana na Deo kuambiwa anirudishe nyumbani na kugoma ilimbidi kununua vyombo na kuanza kupika mwenyewe kwa ujumla alianza kufanya kila kitu peke yake kupika kufua na kuangaika wakati mwingine kuniogesha peke yake na huku akiendelea kuuza duka lake. Hali ilikuja kutulia na Deo alipata safari ya kwenda Dar es Salaam ilimbidi amuombe mtoto wa dada yake aje kuniudumia hadi atakaporudi kutokana na mama mkwe kukerwa na ile hali . Deo alisafiri na kwenda Dar es Salaam kwa muda wa wiki 1 kabla ya safari nilimwambia Deo sasa unasafiri si utakuwa mwanzo wa mimi kuanza kuishi maisha ya mateso na yakunyanywasa?





    Alinitia moyo na kuniambia

    Deodath Siyo kwamba naenda Dar kustarehe mke wangu na siyo kwamba nakukimbia. au labda na mimi nimekuchoka hapana.

    Nilimuliza :-

    Ester Mume wangu kama siyo kunikimbia unaenda Dar kufanya nini?

    Deodath Ester mke wangu usiwaze hayo unayowaza, nakupenda kuliko unavyofikiria na niko tayari hata wazazi wangu kunitenga lakini siko tayari kuendelea kuona wewe unaishi kwa mateso.

    Ester Sasa tufanyeje? Maana mimi kubaki na mama yako sita weza lakini bado ujanieleza unaenda Dar kufanya nini?

    Alianza kunieleza anachoenda kufanya Deodath Ester mke wangu nakupenda naomba usilie maana, unaniumiza mwenzako. Naomba uelewe naenda kuhangaika kwa ajili yako maana haya maisha ya wewe kuishi na mama mkwe wako bila amani sipendi kuona na wewe kila siku ya Mungu lazima ulie hali ambayo inaniumiza mimi. Hivyo naelekea Dar kuna chumba ambacho nilikuwa naishi kabla sijaja Moshi na wakati naondoka nilimpangisha mtu kwa kuwa kodi yangu inaisha 2013 kwa hiyo ikabidi nimuweke mtu sasa ngoja nikamuombe Yule niliyempangishia aame alafu nikirudi tuondoke tukaishi Dar hata kama utalala chini, hata ukila chumvi lakini nione unakaa kwa amani tu. Sawa mke wangu. Nakupenda Ester sifurahi ninapokuona unateseka nilimwambia haya:-

    Ester Sasa kutokana na hii hali yangu ukienda kuishi na mimi mbali huoni itakuwa ni mateso?

    Alijibu :- Deodath Acha niteseke na niko tayari kuteseka kwa ajili yako hadi nihakikishe umekuwa mzima.

    Nilimkubalia na hatimaye aliniaga na kuondoka na alivyo, ondoka aliniacha na mtoto wa dada yake ambae aliendelea kunihudumia huku akiendelea kuuza duka la mjomba wake ambae ni mume wangu. Alifika Dar es Salaam na kukamilisha mipango yake. Baada ya wiki kumalizika alirudi Moshi na alipofika alinieleza habari za LOLIONDO na kuniambia nitafanya juu chini nikupeleke mke wangu, yaani nitaangaika hadi nione mwisho. Nilimuuliza LOLIONDO nani amekwambia? Akaniambia nilivyokuwa Dar nilisikia stori nyingi za LOLIONDO na watu wanasema wanapona kwa hivyo twende tu mke wangu na wewe utapona.

    Nilimwambia siendi popote pale kama nikuzunguka nimeshazunguka na hadi sasa nimeshapewa hadi vitu vya ajabu kwa hiyo siendi popote pale sawa? Alinijibu usiseme hivyo huwezi kujua uponyaji wako uko wapi huenda uko ukapona. Nilikataa kata kata siku ziliendelea kwenda hali nayo ilibadilika zaidi tumbo liliendelea kunisumbua na Deo kaamua kunirudisha hospitali ya Mkoa wa Mawenzi na baada ya vipimo waliniambia nauvimbe kwenye tumbo la uzazi nilipewa dawa za kwenda kutumia kwa muda wa siku tano na baada ya hapo ni kae baada ya miezi mitatu nirudi tena.

    Niliendelea kujiuliza yaani natapika damu halafu wananiambia eti ni uvimbe kwenye uzazi kwa hiyo huwo uvimbe ndiyo unatoa damu kwa mdomoni? Sikupata jibu na Deodath aliendelea kuchanganyikiwa na majibu ya madaktari. Yanayoeleza mambo ambayo hayaendani na hali yangu. Nilitibiwa mawezi katika wodi namba 5 ya wazazi na dokta Masawe aliyetambulika zaidi ya jina la mkombozi wa wamama, na aliendelea kunitibu kupitia oda ya kutoka Muhimbili kwa jina la Mama TARIMO ambae alisaidiana na dokta. Masawe kwa maelekezo na mama huyu yuko Muhimbili hospitali Walihangaika na hali yangu lakini bado sikupona.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ndipo Deodath baada ya kuchoka na hospitali alinibembeleza tuelekee LOLIONDO kwa ajili ya kwenda tena kupata nako dawa. Nilimkubalia kutokana na hali halisi ambayo iliendelea kwangu na kuona kama vile kukataa namtesa maana anahangaika kwa ajili yangu na hakuna anayemsaidia hata mmoja na nilikuwa na ndugu pale Moshi lakini hakuna, aliyeungana nae kumsaida alibaki akiendelea kuangaika peke yake hakuna aliyekuwa akisaidiana nae hata kimawazo zaidi ya mama yangu mzazi kuwasiliana na Deo zaidi ya kuendelea kuwasiliana nae kwa njia ya simu, Deo hakupenda kumsumbua mama yangu kwani alimuonea huruma kwa kuwa ni mjane, na hana kazi na pia alishachoshwa na hali yangu sasa hata akimwambia juu ya hali yangu haitasaidia chochote zaidi mama aliendelea kulia tu kila alivyoambiwa juu ya hali yangu hivyo Deo kuamua libaki kama jukumu lake.

    Hakuna lakufanya kaka wa watu alikuwa na pikipiki yake kwa ajili ya kwenda nayo mjini kuchukua vyombo vya dukani, hivyo ilimlazimu kuuza hiyo pikipiki ili kupata fedha ya nauli ya kuelekea LOLIONDO. Na ndipo majirani walipoanza kumwambia lazima ufilisike mwaka huu kwa ajili ya mwanamke, si uachane nae kwani wanawake wameisha?deodath akuangalia hilo ingawa hadi wazazi wake walimwambia. Wakamwambia kila siku unashika madamu ya mwanamke hii unaona ni sawa? Aliwajibu :- ndio mimi naona ni sawa kabisa kwa kuwa Mungu ameamua kunipa kwa hiyo nimfukuze? Au nimuuwe? Walimjibu :- Achana nae tafuta mwingine, mbona wapo wazuri zaidi yake achana na mwanamke anayezidi kukufilisi mali zako, ona sasa leo umeuza pikipik kwa ajili ya mwanamke sasa kesho kutwa si utauza nyumba? Niliyasikia hayo niliumia sana lakini la kufanya sina na sikuwa na anaye nipenda hata mmoja kutokana na hiyo hali tofauti na mume wangu, mama mkwe yeye alivumilia kwa ile mara ya kwanza tu lakini siku zilivyozidi kwenda alinichukia kabisa na hadi kufikia kumchukia mwanae kwa ajili yangu.

    *******




    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog