Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

NISAMEHE MAMA - 5

    Simulizi : Nisamehe Mama

    Sehemu Ya Tano (5)

    Takribani sekunde tano nilikuwa katika mshangao uliojawa na maswali lukuki. Honi zilizokuwa zikipigwa mfulululizo ndizo zilinizindua na kunifanya niendeshe gari lakini si kuendelea na safari. Bali kupaki mita kadhaa ili niweze kupata maelezo kutoka kwa Sung'wa ni nini kilitokea.

    Wakati napaki gari akatokea askari wa usalama barabarani ambaye alinitoza fani kwa kile kilichotokea katika taa za kuongoza magari. Haikunisumbua kichwa kwani fedha nilikuwa nayo. Baada ya kumalizana na Traffic nikarudi nilipomuacha Sung'wa lakini hakuwepo. Nilizunguka kwa muda eneo lile ndipo nikampata msichana ambaye hakuwa tofauti na Sung'wa.

    Naye akiwa anafanya biashara kama ya Sung'wa. Huyo alinieleza kidogo kuhusu mahala pa kumpata Sung'wa. Mwisho aliniambia nisimfuatilie huko anakoishi kwani anaishi katika mitaa iliyosheheni wahuni.

    Kwakuwa alinipatia uhakika wa kesho yake atakuwepo pale, sikuona sababu ya kumfuatilia huko japo nilihitaji kuonana naye hata wakati huo. Nikarudi nilipokuwa nimeliacha gari langu ili niweze kurudi nyumbani.

    Hii yote ni kwasababu akili yangu ilishahama kabisa. Nilichokiwaza ni ilikuwaje hadi Sung'wa awe katika hali ile. Mama yake je yuko wapi? Majibu ya maswali yangu alikuwa nayo Sung'wa pekee.

    Nikiwa nafungua mlango wa gari langu ili niingie, sauti ya Sung'wa ikapenya kwenye masikio yangu ikiniita kwa upole. Nikageuza shingo yangu na kushuhudia machozi yakimtoka Sung'wa. Nilishindwa kumuelewa kama anaigiza au hapana.

    "Naomba unisamehe." Ni kauli aliyoitoa Sung'wa na kuzidi kuniweka kwenye mshangao.

    Pale hapakuwa mahala sahihi pa kuzungumzia. Nikamuomba aingie kwenye gari. Naye akakubali. Nikaliondoa na safari yetu ikakomea mbele ya jengo dogo lililokuwa likifanyiwa biashara ya kuuza juisi pamoja na vyakula.

    Nilihitaji kuwa sehemu tulivu ili tuweze kuzungumza. Nikaagiza juisi mbili lakini Sung'wa alionyesha hali ya kuhitaji chakula. Nikamwambia aagize.

    Nilizoea kumuona anakula chakula kimapozi lakini alishabadilika. Hakuna pozi tena ni mwendo wa kula kama anashindania kitu fulani. Hayo sikuwa na muda wa kuyafikiria tena. Lengo langu ni azungumze kilichomfanya vile kisha nimtimue kama mbwa mwizi.

    Alipomaliza kula, juisi ikaanza kupita kooni mwake taratibu. Alipotua glasi yake mezani, akaniangalia usoni kwa muda huku machozi yakimtoka. Sikuongea lolote. Aliporidhika kuniangalia akafungua kinywa chake na kuanza kunisimulia kwa maumivu ya wazi kilichompata.

    SUNG'WA ANASIMULIA.

    Katika kufahamiana sikuwahi kufikiria usaliti kwa Steve. Nilimpenda kwa moyo wangu wote kama alivyoonyesha kwangu. Lakini tamaa ya mama yangu nd'o ikawa chanzo cha usaliti wangu. Alikuwa ni mzazi wangu hivyo nisingeweza kupingana naye kiurahisi. Alicheza na akili yangu kabla ya kuniambia mpango wake wa kumfilisi Steve.

    Akafanya mapenzi na Steve nyumbani kwetu. Nilipomuona Steve akitoka chumbani kwa mama yangu, hasira juu yake zilinipanda kuliko ninavyoelezea. Upendo wangu kwake ukaisha kutokana na kitendo kile.

    Kumbe mama alidhamiria ili nimchukie Steve apate nafasi ya kunishawishi kirahisi. Kweli ikawezekana. Tukatafuta watu walioenda kuvunja duka la Steve kisha lile alilokuwa amenifungulia tukahamisha vitu na kubakisha vichache ndipo tukawasha moto ili isemekane limeungua moto kwa bahati mbaya.

    Kila kitu kilikuwa kikipangwa na mama. Mimi nilikuwa nikikubali tu. Mteja alikuwa tayari. Vile vitu tukaviuza na kubaki na fedha kwenye begi dogo ambalo alilibeba mama yangu kifuani. Alinichanganya zaidi nilipomuuliza kuhusu nyumba yetu.

    Kumbe alikuwa ameshaiuza siku nyingi pasipo kunipatia taarifa. Nilijiuliza maswali mengi sana chanzo cha yeye kuwa na roho ya namna ile lakini sikupata jibu. Siku hiyo alikodi chumba na kesho yake tukapanda basi kwa safari ya kuelekea jijini Mwanza kama alivyoniambia.

    Ndani ya basi sikuwa amani hata kidogo. Nilimfikiria sana Steve pamoja na mama yake ambaye alikuwa ni mgonjwa. Roho ilikuwa ikiniuma kiasi fulani kwa kuona Steve atataabika sana. Mbali na kuwaza, hakuna kilichopanguka.

    Saa mbili usiku basi likaingia stendi kuu ya mabasi jijini Mwanza. Kipindi hicho stendi hiyo ya Nyegezi ikionekana kama pori. Tulipoteremka, mama akakodi taksi na kumwambia dreva atupeleke hoteli yoyote nzuri. Wakaelewana bei na safari ikaanza.

    Mwendo wa takribani dakika kumi, dreva akakanyaga breki. Nikadhani tumefika. Haikuwa hivyo, kumbe ulikuwa umefika wakati wa kunyang'anywa kile tulichonyang'anya pamoja na cha kwetu.

    Kwa ustaarabu akaniambia nishuke ili nikapande mbele ambako alikuwa amekaa yeye na mama. Nilipomhoji akaniambia mbele kidogo kuna mizigo fulani ataweka huko nyuma. Sikuhoji tena na wala akili za udadisi zaidi sikuwa nazo.

    Nikateremka na kwenda kujibana pamoja nao. Nilivyoingia tu na kufunga mlango, akalock kabisa kisha akachomoa bastola na kumnyooshea mama kwenye paji lake la uso. Hadi leo huwa najiuliza ni vipi yule dereva alijua mama amebeba fedha.

    Kilichonishangaza ni kumuona mama katika hali ya kutobabaika. Alibaki amekodoa macho bila kuongea chochote. Yule dreva alizidi kuamrisha lakini mama hakuna alichotii. Nikaanza kutetemeka kwa kuona muda wa kufyatuliwa risasi umefika. Haikuwa maksudi mama kuwa katika hali ile.

    Mshtuko alioupata pindi tulipoonyeshewa bastola ulikuwa mkubwa mno hadi ukapelekea kifo chake palepale kwenye gari. Yule dreva alivyoona hatutii amri yake, akateremka kinyumenyume kisha akafunga mlango na kuzunguka upande wetu. Akafungua mlango huku bastola yake ikiwa mkononi kwa tahadhari. Akanitaka kuteremka.

    Hapo ndipo nilipogundua mama yangu kapoteza maisha kwani alianguka na kichwa chake kuning'inia nje. Alichokifanya yule dereva ni kuniamuru nimvute nje mama yangu. Nikafanya kama alivyotaka ndipo yeye akachukua kile kibegi kifuani mwa maiti ya mama yangu. Akawasha gari lake na kutokomea.

    Nilibaki nimeganda nisijue pa kuanzia. Sehemu aliyoniacha hapakuwepo na nyumba wala hakuna gari lililokuwa likipita karibu. Nilijaribu kupiga kelele za kuomba msaada lakini haikusaidia.

    Nikakaa chini na kuanza kuyatafakari maisha yangu yalivyokuwa mazuri huko Shinyanga. Lakini nisingeweza kurudi huko kwani hakuna ambacho kingeweza kunisaidia kimaisha. Vilevile nilikuwa nikiogopa kukutana na Steve kutokana na ubaya tuliomfanyia. Hadi panapambazuka, macho yangu yalikuwa makavu.

    Nikagundua tulikuwa kwenye barabara ya vumbi ambayo ilikuwa katikati ya kichaka. Nyumba za watu zilikuwa mbali sana kutoka mahali pale. Nikiwa natafakari kutembea hadi zilipo zile nyumba ili kuomba msaada, nikasikia muungurumo wa gari.

    Nikashusha pumzi kwa nguvu kisha nikasimama barabarani. Hazikupita dakika nyingi, likatokea gari la maaskari. Sikujua kama walipata taarifa au walikuwa wakielekea kwenye kazi zao. Wakanihoji maswali kwa muda ambapo niliwadanganya vya kutosha hadi wakanielewa.

    Hii ni kwasababu umri wangu ulikuwa mdogo. Vilevile hakuwa na jeraha lolote bali mshtuko tu. Wakanichukua hadi kituoni ambako waliandika maelezo ambayo sikuwa na muda nayo. Mazishi yake yakafanyika katika makaburi ya serikali na mimi nikaingia katika maisha ya mtaani. Ni maisha magumu yaliyojaa unyanyasaji lakini niliyavumilia kwasababu sikuwa na mahali pa kwenda kulilia tabu zangu.

    Nilichokifanya ili kujiokoa na unyanyasaji wangu, nikajigeuza kipofu. Nikawa ombaomba lakini kwa nia ya kutafuta mtaji mdogo tu. Nyumba yangu ikiwa ni chini ya karavati, nikafanikiwa kutimiza shilingi elfu sabini. Nikaachana na hiyo kazi. Nikaunda urafiki na msichana mwingine mdogo kama mimi tukapangisha chumba na kuanza kuuza karanga.

    Huo ukawa mwanzo wa urafiki wetu. Hatukuachana kila mahali. Mbali na biashara hiyo, bado hatukuithamini miili yetu. Aliyejitokeza kumtamani mmoja wetu haukuwepo ubishi. Mradi fedha.

    Ni muda mrefu katika biashara hii lakini hakuna mafanikio zaidi ya kuichosha hii miili yetu. Ni tabu tupu Steve. Naomba unisamehe kwa yote lakini tambua si mimi msababishaji bali mama yangu ambaye tayari alishaiga dunia. Nakupenda sana Steve na ndiyo maana nimekwambia yote hayo.

    STEVE ANAENDELEA ANASIMULIA

    Nilishindwa kuyazuia machozi yangu pale alipomaliza kunisimulia. Kauli yake ya mwisho kwamba ananipenda ndiyo ilipigilia msumari wa machungu nafsini mwangu. Hisia za mapenzi hazikuwa zimepotea japo nilikuwa nikimchukia.

    Lakini nilitafakari mengi pasipo kuongea lolote. Nilimtazama kuanzia juu hadi chini kwa jinsi alivyokuwa amechakaa vilivyo. Uzuri wa Sung'wa yule wa Shinyanga ulikuwa umepoteza kabisa. Katika kutafakari huruma ilinishinda na mwisho nikajikuta nanyanyuka kisha nikamuinua na kumkubatia.

    Si kama ni ishara ya mapenzi moyoni. Bali ni ishara ya kumpa pole kwa aliyoyapitia tangu atoke Shinyanga. Alilia sana pindi akiwa kifuani mwangu. Wakati huo mimi hisia zilianza kunitawala na kumuhitaji tena Sung'wa.

    *****

    "Jifunze kudhibiti hisia zako. Endapo utashindwa, basi tambua utakuwa ni pendapenda. Mapenzi ni hisia."

    *****

    Sikuona sababu ya kuharakisha kumrudisha mikononi mwangu. Nikamuondoa kifuani kisha nikaenda kulipia tulichokitumia. Nikamrudia na kumshika mkono hadi nje. Tukaingia kwenye gari na kauli niliyoitoa ni kumwambia anielekeze anakoishi.

    "Mbona umenyong'onyea ghafla?" Ni swali aliloniuliza Sung'wa lakini sikumpatia jibu.

    Nikazidi kukanyaga mafuta hadi tulipofika alipokuwa akiishi. Nikamwambia ateremke na bila ubishi akafanya hivyo. Nikaliondoa gari kwa kasi kurudi nyumbani. Nilifanya vile ili niweze kumfuatilia taratibu nyendo zake kwani tayari moyo wangu ulisharudi nyuma na kumuona ni sahihi kuwa mke wangu.

    Nilipofika nyumbani moja kwa moja nilijitupa kitandani. Nilimuwaza sana Sung'wa huku nikiona tayari ameshakuwa mke wangu na maisha yetu yakiwa yenye kutawaliwa na upendo usioelezeka. Siku hiyo ikapita mawazo yakiwa lukuki.

    Hata rafiki yangu sikumshirikisha. Upelelezi wangu juu ya maisha ya Sung'wa niliufanya mwenyewe. Takribani miezi miwili niliyomfuatilia niligundua aliyoyaongea ni kweli.

    Mwezi uliofuata ikiwa ni siku ya jumanne asubuhi nikamtokea Sung'wa mahali alikokuwa akiuzia karanga. Alistaajabu kuniona tena. Lakini sikwenda na gari. Lengo la kumfuata lilikuwa kumuhamisha pale alipopanga.

    Sikuwa muongeaji sana na vilevile sikukata atambue kama namuhitaji tena kimapenzi. Aliporidhia kuhama, nikampangishia chumba maeneo ya Mabatini kisha nikampatia mtaji wa shilingi laki mbili tu ili awe anauza ndizi ziwani.

    Hii ni maksudi kwasababu karanga hazifikishi elfu kumi. Alifurahi kwa kitendo changu. Akaanza biashara hiyo ndani ya miezi minne alianza kubadilika hali yake. Uzuri wake ukaanza kurejea lakini alikuwa ni msikivu kwangu kwa kila nilichomshauri.

    Sikuwahi kumuonyesha kwangu, alichotambua ni kwamba mimi ni dereva wa daladala. Miezi ikaendelea kusonga mbele huku akizidi kuchanua vilivyo. Alivumilia sana mwisho akachoka.

    Siku moja majira ya jioni nilienda kumjulia hali. Nilipofika nilimkuta anatoka bafuni kuoga. Hakika moyo wangu ulinienda mbio. Akanikaribisha ndani na mimi bila hiyana nikatangulia kuingia na yeye akafuata nyuma lakini akafunga mlango kwa ufunguo.

    "Mbona unafunga mlango?" Ni swali nililomuuliza huku nikiwa nimesimama katikati ya chumba chake. Yeye akiwa ameegemea mlango.

    "Hivi unanionaje?" Aliniuliza swali lililoniacha niduwae kiasi fulani.

    "Kama mwanamke mwingine." Nilimjibu.

    "Sifai kuitwa mke wa mtu?"

    Nilizidi kuduwaa kwa maswali yake.

    Nilichomjibu ni kwamba akapime afya yake ndipo atafaa kuwa mke wa mtu. Na yeye akaniambia tuandamane wote huko hospitalini. Baada ya hapo akafungua mlango na stori nyingine zikaendelea hadi nilipomuaga na kurudi nyumbani kwangu.

    Kesho yake tulielekea hospitali ambako tulipima kwa pamoja afya zetu kana kwamba tumeambizana tukikutwa salama ndipo tufunge ndoa. MUNGU akajaalia.

    Majibu yetu yakatoka tukiwa salama. Sung'wa alishindwa kujizuia. Akanikumbatia kwa nguvu huku akilia kilio kiluichoambatana na kwikwi. Hatukupitisha siku. Tuliporejea kwa Sung'wa tukarudia enzi zetu. Tukaufunua upya uhusiano wetu.

    Ikawa kawaida yangu kulala kwa Sung'wa hadi akataka kupajua ninapoishi. Ili isiwe tabu, nikafanya mpango wa chumba na kukilipia kisha nikaweka baadhi ya vitu vya ndani. Uaminifu katika mali zangu ulikuwa mdogo mno kwa Sung'wa. Nikampeleka akapaona na kulala kwa wiki nzima. Maisha yetu yakazidi kupambwa na tabasamu kila kulipopambazuka.

    Mapenzi yetu yakatawaliwa na nuru ya upendo na hatimaye nikafunga ndoa na Sung'wa pasipo kumpeleka nyumbani kwangu hadi pale tulipojaliwa mtoto wetu wa kiume. Siku anatoka hospitali, ndipo nikamfanyia mshangao kwa kumfuata kwa gari na kumpeleka nyumbani kwangu. Yote hiyo ilitokana na furaha ya kupata mtoto.

    Alipatwa na mshangao sana kuufahamu ukweli niliomficha kwa muda mrefu. Nilitambua fika hawezi kunigeuka ilihali yu na mtoto wangu. Na endapo atanigeuka mimi, basi mwanangu atanufaika. Vilevile hatakuwa amenikwamisha kwa kiasi kikubwa. Hii ni kwasababu benki ninacho kiasi cha fedha ambacho kinatosha kuniendesha kimaisha pasipo tabu.

    Yale maisha niliyoyawaza siku nilipokutana na Sung'wa ndani ya jiji la Mwanza, yakatimia. Sung'wa akawa mke wangu mwenye wingi wa usikivu pamoja na ushauri wenye tija kila nilipouhitaji kutoka kwake.

    Maisha yakabadilika kwa kasi mno huku mtoto wetu akizidi kukua. Sung'wa akaonekana kuwa chachu ya maendeleo yangu. Kwa upande wa marafiki sikuwa nyuma. Nilijikusanyia marafiki kutokana na kauli zangu zenye kipimo cha jinsi mtu ajavyo au aongeavyo.

    Baada ya mahangaiko ya muda mrefu hatimaye nuru ya furaha ikatawala familia yangu ya watu watatu pamoja na marafiki wasiokuwa na idadi. Nikakumbuka bado ahadi moja sikuitimiza. Ahadi niliyomuahidi mama yangu mzazi kabla ya kifo chake.

    "NANTEZA MAGIC HOTEL" nd'o ahadi niliyomuahidi mama kwasababu ya kupika chakula kitamu. Nilipomueleza mke wangu au mama Junior juu ya hilo akalibariki. Kikabaki kikwazo kimoja tu. Mahali pa kuiweka hiyo hoteli.

    Miujiza ya MUNGU hutendeka pale usipotajia. Nikiwa mjini Shinyanga kwa ajili ya kazi zangu za kimaendeleo, nikasikia tetesi za nyumba kuuzwa. Kwakuwa nia yangu ilikuwa kufungua hoteli pale Shinyanga, ikanibidi kufuatilia.

    Sikuamini nilipogundua mahali panapouzwa ni palepale nyumbani. Lilipo kaburi la mama yangu mzazi. Nikaona huo ndiyo muda muafaka wa kumuenzi mama yangu. Nilipauza kwa sababu ya shida na sasa napanunua tena nikiwa katika mwanga wa furaha.

    Nikalipa kiasi kilichohitajika ndipo nikafanywa mmiliki halali wa eneo lile. Sikuchelewa katika kufanikisha lengo langu. Nikairekebisha ile nyumba na hatimaye ikajulikana kama hoteli. Jina likaandikwa kwa maandishi makubwa. NANTEZA MAGIC HOTEL.

    Ahadi yangu ikatimia lakini moyoni machungu yakiwa makubwa. Yote hii ni kwasababu ya kumpoteza mama yangu kizembe. Kwani ningezichambua kauli zake, leo hii ningekuwa natoka na mama yangu, mke wangu, mtoto wangu Junior kwenye gari kuelekea kanisani kwa ajili ya maombi.

    Kumshukuru MUNGU kwa magumu niliyoyapitia lakini yenye kujenga fikra komavu. Kwa sasa naishi na familia yangu kwa amani pasipo mivurugano. Ila misingi yangu mikubwa ni kauli za mama yangu mzazi. Zenye ujazo mwingi wa mafumbo yenye kujenga mwenye kuhitaji kujengeka.

    *****

    "Mwanadamu ni moyo na si ngozi yake iwadanganyao wengi wetu kutokana na mmeremeto wake."

    *****

    MWISHO.!!

    Nilipigwa na butwaa nilipoishuhudia sura ya mwanadada Sung'wa. Ikiwa imechakaa vilivyo. Mwili wake haukuwa wa kuvutia tena. Bali umedhoofu vilivyo. Hasira zangu juu yake zikaniyeyuka ghafla kutokana na hali niliyomkuta nayo.

    Yeye pia alikumbwa na mshtuko uliosababisha sinia lake la karanga za kuchemsha, kuanguka chini. Nilizidi kutahamaki pasipo kukumbuka niko kwenye foleni na yapo magari yanahitaji kupita.

0 comments:

Post a Comment

Blog