Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

SHIDA - 4

 





    Simulizi : Shida

    Sehemu Ya Nne (4)





    "Naomba kila mtu atupishe tumshughulikie mgonjwa kwanza" akajibu Dokta

    Watu wote wakaondoka pale ndani huku wakiwa hawaelewi nini kimemtokea Shida

    Baada ya watu wote kutoka nje

    Shida aliamka na kukaa, hali ile ilimshtua sana dokta



    "Shhhhhhiiiiiiii!!!!" akamfanyia daktari ishara ili anyamaze



    Songa nayo sasa…



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Daktari alishtuka sana na kushangaa sana yule mgonjwa aliyeonekana kuwa hoi sasa ameamka mzima.

    "Dokta samahani, nahitaji msaada wako sana,tafadhali sana" alisema

    "Una tatizo gani binti? Mbona unanitisha?" akasema Daktar

    "Nina matatizo makubwa sana,naomba unisaidie tafadhali" aliendelea kuomba

    "Haya nieleze mwanangu" akasema

    Ikabidi Shida aanze kueleza historia ya maisha yake kutoka mwanzo!

    Shida aliendelea kumsimulia yule daktari matatizo yote aliyokutana nayo kabla hajafika pale hospitalini

    "Pole sana binti,sikujua kuwa umepitia matatizo makubwa hivyo" alisema

    "Ahsante dokta" akajibu

    "Kwa hiyo unachoogopa ni kuwapa taarifa polisi kwa nini?" akauliza dokta

    "Ana pesa dokta, anaweza kufanya chochote na kuniua kabisa, mimi nataka aamin kuwa nilishakufa basi" akasema Shida

    "Kwa hiyo unataka nikusaidie nini?" akauliza

    "Naomba unitafutie namna nitoloke hapa hospitalin mimi nitajua cha kufanya huko mbele ya sfari" akasema Shida

    "Unanipa wakati mgumu sana Shida,si unajua kuna askari anakulinda hapo nje?" akasema

    "Najua dokta ila nakuomba sana,fanya kama mimi mwanao nisaidie tafadhal" akasema

    "Sawa nitaangalia cha kufanya" akajibu

    Mchana askari walikuja ili wapate maelezo kutoka kwa Shida ila bado hakuwa tayali kuongea na daktari yule akaendelea kushaur wamwache mpaka atakapokuwa sawa

    Jioni wakati dokta anaondoka alimfata Shida pale chumbani kwake

    "Huu ufunguo ni wa madilisha haya,watakuja kuyafunga baadae,wewe unachotakiwa kufanya ni kufngua dirisha na kutoloka,utanikuta hapo nje ya geti nimepali Rav 4 nyeupe na tutaondoka wote" akasema dokta

    "Nimekwelewa dokta ila naomba nisikubebeshe mzigo,mimi nikishatoloka ntajua pa kwenda" akasema

    "Hapana Shida nimeamua kukusaidia kama mwanangu" akasema dokta

    "Nashukulu kwa wema wako dokta" akasema



    * * * *



    Dokta akaondoka na kumwacha Shida akiwa na matumaini makubwa sana.

    Kweli kama alivyoambiwa na dokta manesi walikuja kufunga madirisha na kisha wakahakikisha yuko katika hali salama wakaondoka

    Giza lilipoanza kuingia Shida alijiandaa na kufungua dirisha lile kama alivyoelekezwa na dokta na kisha akatoka nje

    Alifanikiwa kufika nje ya geti na kuiona gari ya dokta kama alivyoelekezwa na akaingia ndani

    "Nashukulu kama umeweza kufanikisha hili mwanangu" akasema dokta

    "Nashukulu sana dokta na uzidi kubalikiwa" akasema Shida

    Gari iliwashwa na kuondoka moja kwa moja kuelekea nyumbani kwa dokta yule

    "Naitwa dokta Eliasi" aliongea wakati wakifika nyumbani kwa dokta

    "Naishi na wafanyakazi wangu hapa,nina mtoto mmoja yuko Dar na yeye ni daktari kama mimi,mke wangu alifariki zamani sana" aliendelea kujitambulisha

    "Nashukulu kufaham hayo dokta" akasema Shida

    "Karibu sana nyumbani" akasema dokta

    "Ahsante sana dokta" akajibu

    Shida alianza maisha mapya pale nyumbani kwa Dokta Elia akiwa na amani kias tofaut na alipokuwa nyumbani kwao.

    Aliishi kama yuko nyumbani kwao, yule daktari alimtambulisha kama mwanaye kwa wale wahudumu wa pale.

    Kila jioni alikuwa akimchukua na kuanza kumtembeza sehemu mbali mbali za mji wa Singida ili awe mzoefu

    "Nataka nikutafutie shule nzuri uendelee na masomo yako unasemaje?" alisema siku moja dokta

    "Nataka sana na nataman sana" akajibu Shida

    "Jitahidi uishi hapa kwa aman,fata masharti yangu na utpata chochote kile" akasema dokta

    Alimtembeza sehemu mbali mbali huku akimnunulia nguo nzur nzur ambazo zilimpendeza sana

    "Nataka nikununulie zawadi nzuri sana" akasema dokta siku moja

    "Zawadi gani hiyo dokta" akauliza Shida

    "Usijal utaiona" akajibu

    Waliendelea kuishi kwa upendo na amani kwa muda mrefu sana .

    Baada ya miezi michache Shida alianzishwa masomo kidato cha tatu

    Siku moja usiku akiwa amelala dokta aliingia chumbani kwake

    Alipoingia alimwamsha Shida

    "Shida, nimekuletea zawadi yako niliyokuahidi" akasema

    "Dokta mbona ni usiku sana, iko wapi?" akasema Shida

    "Hii hapa ila ina masharti" akasema

    Alitoa laptop nzuri sana na simu ya gharama kubwa na kumpatia Shida

    Shida alifurahi sana na kumkumbatia dokta

    "Ahsante kwa upendo wako dokta" akasema

    "Usijal, utapata vitu zaidi ya hivyo,ila naomba unisikilize,tangu mke wangu afariki sijawah kuishi na mwanamke, ila tangu umekuja humu ndani, umeibadilisha akili yangu sana, nakuhitaji Shida, kubali niziondoe shida zako zote, naomba uwe wangu tafadhal" akasema dokta.

    Hakutegemea kukutana na kitu kama kile kutoka kwa yule Dokta.

    Kutokana na msaada aliompatia na jinsi walivyokuwa wakiheshimiana alimchukulia kama baba yake mlez

    "Lakini wewe si ni kama baba yangu?" aliuliza

    "Baba yako? Mimi sina nia mbaya na wewe Shida, mke wangu alishafariki na hilo unalifaham,sasa kuna ubaya gani nikikuoa? Nishasema sikuchezei bali nahitaji kukuoa" akasema

    "Sawa Dokta ila wewe ni mkubwa sawa na baba yangu mzazi" akajibu Shida

    "Nafaham hilo, lakin angalia faida zaidi na usiangalie hasara Shida, mimi sijakubaka na nimekusaidia mengi na bado naendelea kukusaidia, nimekwambia uwe mke wangu na sio kukuchezea" akajibu Dokta

    "Dokta mimi siko tayali kwa kweli,siwezi kukuvulia nguo,nakuchukulia kama baba" akasema Shida

    "Sikulazimishi ila kaa mwenyewe uangalie faida na hasara za kunikataa" akasema Dokta

    "Una maanisha nini dokta?" akaulizaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Namaaanisha angalia ni mambo mangapi nimekusaidia na ni mangapi nitaendelea kukusaidia na upime na misaada hiyo ikiondolewa na kupandikizwa chuki kitakachotokea ni nini?" akajibu Dokta

    "Dokta kuwa basi na utu, kwa nini mimi nimekuwa mtu wa kunyanyaswa peke yake?" akauliza

    "Nimekunyanyasa? Msaada wote niliokupatia bado unadai nakunyanyasa?" akajibu Dokta

    "Dokta nikikataa utanisemea polisi na kumfikishia taarifa baba kuwa niko hai?" akaendelea kuuliza Shida

    "Sijasema hivyo, ila usishangae tukifika huko,naamin hata wewe ukitendewa hivi unavyotaka kunilipa utachukia na matokeo ya hasira ni mengi" akajibu

    Shida akabaki kwenye mtihani mzito juu ya kufanya yale maamuzi

    Alifikilia kwa muda mrefu sa mwishowe akaona hana jinsi zaidi ya kukubaliana na hali halisi

    "Dokta naomba tuwe wapenzi peke yake ila sio kuwa mkeo, na naomba iwe siri tafadhal" akajibu huku akiona aibu Shida

    Dokta alipatwa na furaha ya ajabu,hakutegemea kumpata Shida kwa urahisi kiasi kile, alijipanga ikibidi kumbaka kama ataleta upinzani wowote.

    Alimsogelea na kuanza kumpapasa sehemu mbali mbali za mwili wake.

    Shida alionesha ushilikiano ingawa alikuwa akiona aibu kubwa sana.

    Baada ya muda kila mmoja alikuwa tayali kwa ajili ya mpambano ule.

    Dokta alijitahidi kumfanyia Shida kila kitu pale kitandani ili afuahie lile tendo

    Na kweli kwa mara ya kwanza Shida alijikuta akifurahia tendo lile

    Walipomaliza kila mmoja alikuwa amechoka na kugeukia upande wake na kulala.

    Asubuhi walipoamka kila mmoja alimuonea aibu mwenzake na kila mmoja akaondoka kuendelea na shughuli zake

    "Mmmh! Kumbe ni raha vile?" aliwaza Shida akikumbuka penzi tamu alilopewa na Dokta

    Taratibu upendo ukaanza kukua kati ya Shida na Dokta yule

    Kila sehemu wakaanza kwenda pamoja kwenye gari la Dokta

    Kwa wakati huo hakuogopa mtu yeyote yule aliona sawa kuwa na Dokta kwa sababu hakuwa na mke



    **********







    Ilifika hatua Dokta akiingia shifti ya usiku wivu ulimpata Shida na kufikilia kuwa labda atakuwa na mwanamke mwingine

    Baada ya miezi mitatu ya uhusiano nyumba ile ilipata mgeni.

    Kijana wa pekee wa Dokta huyu alikuja kuwatembelea baada ya kupata likizo

    Kuja kwa kijana huyu katika nyumba hii kulibadilisha kila kitu katika maisha ya Shida

    Baada ya kukaa siku chache pale nyumbani alianza kutengeneza mazoea na Shida

    "Ila David inabidi uniheshimu kama mamdogo wako,mimi ni mke mtarajiwa wa baba yako" alisema siku moja Shida baada ya kuona mazoea ya Daiv yanazid

    "Mamdogo wapi? Hutu mzee kabug vibaya mno,haiwezekan akuchukue wewe saiz yake inabidi wewe uwe wangu" alimjibu David

    "Haitawezekana David,huoni aibu kushare na baba yako?" akauliza Shida

    "Nikwambie kitu?" akasema David

    "Nambie mwanangu" akasema Shida

    "Leo lazima mimi na wewe tufanye mapenzi,siwez kukubali niwe nakuangalia ulivyoumbika anafaid baba yangu peke yake" alisema David

    Pale pale David akamsogelea Shida na kumshika kwa nguvu

    Vurugu ilianza pale pale sebuleni Shida akipambana kutoka mikononi mwa David na David naye akijitahid ili afanikishe lengo lake

    "Nabakwaaaaaaaaaa" aliongea kwa nguvu Shida

    Bahati nzuri kwa David ni kuwa yule mfanyakazoi wao wa ndani alikuwa ameenda sokon

    David alimuachia Shida na kisha akaongea

    "Kuna mawili hapa,ukubali kufanya mapenzi na mimi au nimtafute baba yako wa kambo na kumpa taarifa kuwa uko hai na hujafa" alisema kwa kujiamin David

    Shida alishtuka sana kusikia David anajua siri yake ile ambayo aliamin ni yeye na Dokta peke yao walioifaham.

    "Baba gani? Wewe una kichaa?" akasema Shida

    "Yawezekana kweli nina kichaa ila kwa taarifa yako namfaham Alex kuliko hata wewe,na nina ma wasiliano naye ya kalibu" akajibu David

    Pale pale David alichuku simu yake na kumwonesha Shida namba ya Alex

    "Haya sema hiyo ni namba yake au sio?" akauliza kwa mbwembwe.

    Shida alijikuta mkojo unapita kwa woga aliokuwa nao,hakutarajia kukutana na kitu kama kile kwa wakati huo

    "Sasa ni wakati wako wa kuamua kuwa mpenzi wangu au hapana,ila kaa ujue nakupenda sana Shida,niko tayali kukuoa achana na baba alishazeeka" akajitahidi kubembeleza David

    David hakusubiri Shida akubali ombi lake alimfata Shida na kuanza kumpapasa mwilini

    "Dokta umenisaliti,umetoa siri yangu kwa mwanao sasa nadhalilika kama mjinga" aliwaza Shida

    "David hapa tunaweza kukutwa,naomba twende chumbani basi" alilalamika Shida

    David hakuwa mbishi ingawa alikuwa na hamu kubwa ya kufanya mapenzi

    Alichofanya ni kumbeba Shida mpaka kwenye chumba chake yeye David na kumlaza kitandani

    Alianza kwanza kumwangalia Shida alivyoumbika, aliangalia kiuno kilivyogawanyika na alivyokuwa amebeba usafiri wa haja akajikuta mate yakimdondoka

    Alivua nguo na kisha akamvua na Shida nguo zake na kisha akamparamia moja kwa moja mwilini

    "David jaman hata huniandai" alilalama Shida

    "Aaaah! Samahan Shida unajua uzuri wako umenichanganya sana" akajibu David

    Taratibu alianza kumwandaa Shida na yeye alijitahidi kujibu mapigo yale na mwisho wote wakanogewa na kuanza kuelea kwenye bahari ya mapenzi.

    Penzi alilopewa Shida na David lilikuwa tamu sana kiasi kwamba mwenyewe alijishangaa,alifurahia kupata penzi la kijana mwenzake aliyeweza kumbusu bila aibu na kumshika popote alipotaka bila tatizo

    Baada ya penzi lile akili ya Shida ilijikuta kwenye wakati mgumu sana

    "Huu ni mtihani wa uhakika, ndani ya nyumba moja baba na mwanae wote wananipenda na wote wanafaidi penzi langu, baba amenisaidia mengi ila kosa lake ni kutoa siri, mtoto anapenzi tamu na nikiri nampenda yeye,nifanyeje?" Shida alijikuta katika kipindi kigumu sana.

    Maisha ndani ya nyumba ya Dokta yaliendelea kwa mtindo huo huo,mchana kijana anafaidi penzi la Shida na usiku mzee na yeye anafaidi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Shida alifurahia zaid penzi la David kuliko baba yake kwa sababu David alikuwa anajituma sana kitandani tofauti na baba yake ambaye yeye alikuwa akishaenda mshindo mmoja basi anachoka na kugeukia upande wake na kulala.

    "David nahisi nakupenda sana" siku moja Shida alimwambia David

    "Nini kinakufanya uhisi hivyo?"akauliza David

    "Penzi David,penzi unalonipa ni tamu sana" akajibu Shida

    "Mbona na mzee anakupa penzi tamu?" akasema David

    "Mzee mchovu sana,hawezi bana" akasema Shida

    Hayo ndo yakawa maisha ya kila siku pale ndani.

    Baada ya muda wa wiki moja wanasema penzi ni kikohozi na haliwez kujificha na ndivyo ilivyotokea kwa David na Shida

    Baada ya muda house girl wao alianza kushtukia nyendo zao pale ndani.

    Siku moja alipotoka sokoni alishangaa kutowaona Shida na David pale ndani wakati aliwaacha pale.

    Alishangaa na baada ya muda kumwona David akitoka chumbani mwa Shida huku akiwa kifua wazi

    Baada ya David akumwona yule binti alishtuka sana

    Aliingia chumbani kwake ghafla na kuanza kuwaza anachopaswa kufanya ili kuzuia hili swala lisifike kwa baba yake



    Baada ya kuwaza kwa muda mrefu sana ikabidi amfate Shida chumbani kwake

    "Mambo yameharibika Shida" akasema David

    "Kivip?" Shida akauliza

    "Housegirl amejua uhusiano wetu na iwe isiwe hawezi kutunza siri na nafikili unajua walivyokalibu na baba" akasema David

    "Umejuaje kuwa kajua?" akauliza Shida

    "Wakati natoka humu nimekutana naye hapo nje,nahisi alikuwa anatusikiliza kila tulichokuwa tunafanya na aliponiona amekimbia" akajibu

    "Mungu wangu tumekwisha,tutafanyaje David" akasema kwa hamaki Shida

    "Itabidi tutoloke na kwenda kuishi pamoja" akashaur David

    Hali ilikuwa tete kati ya Shida na David kwani kila mmoja aliona wazo lake kuwa bota zaidi.

    Wakati wakiendelea kubishana pale simu ya Shida ilianza kuita na alipochukua ili kuangalia aliyempigia akakuta ni Dokta

    "Mama yangu! Tumekwisha" alisema kwa hamaki Shida

    "Vip tena?" akauliza David

    "Anapiga! Anapiga" akasema tena Shida

    "Nani baba?" akauliza David

    "Ndiyo,anapiga" akajibu Shida

    David naye alishtuka sana,akamnyakua simu Shida na kuangalia na kweli akakuta alyekuwa akipiga ni Baba yake

    "Shida hatuna muda wa kupoteza,namjua baba yangu vizuri sana atatuua,hana mzaha"akasea David

    "David mimi siwezi kutoloka,baba yako ni mpole na mwelewa naamin atanielewa,nasubir nione kama ameambiwa nitaomba msamaha na mimi na wewe basi" akasema Shida

    "Wewe humjui baba ee? Mpole? Unajidanganya! Unajua kilichomuua mama? Na mamdogo je? Pole sana mimi nakimbia" akajibu David na kumwacha Shida njia panda

    Wakati wanabisha pale ujumbe ukaingia kwenye simu ya Shida



    "WEWE MBWA UMESAHAU MEMA NILIYOKUTENDEA? HAYO NDIYO MALIPO YAKO? KAMA ULIDHANI ATAKAYEKUUA NI BABA YAKO ALEX BASI ULIKOSEA,NITAKUUA KWA MIKONO YANGU" Ilisomeka hivyo



    Baada ya Shida kuisoma ile meseji alijikuta akipiga kelele mwenyewe bila kujielewa kutokana na uoga

    Baada ya Shida kupiga ile kelele David alishtuka na kuichukua ile simu akasoma ile sms na yeye akachanganyikiwa

    "Shida baba atatuua! Ila bora tutoroke yawezekana ikawa pona pona yetu na naamin kwa sasa yuko njian" akasema David

    Hakusubiri jibu la Shida alichokifanya ni kutoka na kwenda chumbani kwake na kuchukua ATM card na vitu vyake vichache kisha akaja na kumshika mkono Shida aliyekuwa kapigwa na bumbuwazi na kumvuta mkono ili waondoke

    Walipofika sebuleni walimkuta mfanyakazi akiwa anaongea na simu



    **********





    Alipowaona alipigwa na butwaa na kubaki akiwa na wasi wasi sana

    Hawakutaka kuongea naye chochote,walipita moja kwa moja na kutoka nje ya geti na kisha moja kwa moja wakaelekea kituo cha dala dala wakachukua pikipiki

    "Tupeleke iguguno" akasema David

    "Kwa nini tusiende stand David? Iguguno ndo wap? Na kwa nini tutumie pikipiki?" akasema Shida

    "Acha maswali twende, utajua mbele ya safari" akajibu David

    Wale boda boda hawakuhoji kitu bali waliwasha pikipiki zao na safari ikaanza na baada saa moja na dakika arobaini na tano wakawa wamefika Iguguno

    David aliwalipa na kisha wakaondoka na kutafuta gesti ili wapumzike

    Baada ya muda wakawa wamepata na walipoingia ndipo maongezi yakaanza.

    "Kwa nini tumekuja hapa David?" akasema Shida

    "Baba yangu sio mtu mzuri kabisa" akasema

    "Kwa nini?" akauliza Shida

    "Baba yangu nje ya udaktari anafanya biashara haramu ya madawa ya kulevya, ndiyo maana maisha ya pale nyumbani ni ya juu sana,

    Swala la kuua kwake si tatizo, ni kitendo cha kufanya tu

    Mama yangu aliuawa na baba nikiwa na miaka kumi na mbili ingawa baba alinificha ila baadae nilikuja kujua

    Kilichosababisha nijue ni mke wa pili ambaye baba alimuoa

    Yule dada alikaa na baba miezi saba na nilipokuja likizo akanielezea kuwa yuko hatarini kuuawa

    Nilipombana sana akanielezea biashara anazozifanya baba na kuwa baada ya yeye kugundua yule mzee amepanga kumuuaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Na hapo ndipo aliponiambia kuwa hata mama yangu aliuawa na baba mara baada ya baba kugundua kuwa ana mahusiano na kijana mmoja hivi

    Cha ajabu nilipovuta kumbukumbu nilikumbuka kuwa baada ya mama kufaliki siku chache baadae kijana huyo naye alifaliki

    Kutokana na hilo niliyaamin maneno ya baba yangu, nikaanza kufatilia nyendo zake bila yeye kujua

    Kweli baada ya siku chache nilimfatilia na kumshuhudia akumuua yule mamdogo kwa macho yangu

    Nilishtuka sana na ndipo nikaondoka kurudi kazini na sikutaka kurudi huku mpaka nilipopata taarifa kuwa baba anaishi na wewe

    Baba alinieleza historia yako nzima, nilipokuja hapa nilivutiwa na wewe na kukupenda nikaona nikuokoe ila kwa bahati mbaya tumewahi kushtukiwa kabla hatujatimiza lengo letu



    Ila nilipanga kukutolosha kutoka pale nyumbani

    Kilichosababisha nije hapa ni kuwa,baba ana mtandao mkubwa sana wa vijana wahuni wanaofanya nao kazi hii hivyo tungeenda stand tungepatikana haraka

    Nataka tujifiche hapa kwa siku chache ili asahau kisha tuendelee na safar yetu" akamaliza kusimulia David

    "Dah! Mbona sura yake haifanani na hayo mambo?" akauliza Shida

    Kabla hajajibiwa walishangaa mlango ukigongwa kwa nguvu na kubomoka kuingia ndani

    Mbele yao wakasimama vijana waliojazia na wenye sura za kutisha sana

    "Unadhani ni rahisi kumkimbia mzee wako?" mmoja wao aliuliza

    Wale vijana waliingia chumbani pale na kuanza kuwatoa David na Shida

    "Kwa akili yako ndogo unafikili unaweza kumkimbia baba yako?" akauliza mmoja wao

    David alinyamaza bila kuwajibu ila walipojalibu kuwanyenyua David alijalibu kuleta upinzani

    Wakaamua kufanya kama walivyoagizwa na bosi wao

    David alipigwa na kitako cha bunduki kalibu na jicho na kuanguka chini damu zikaanza kuvuja kwa speed kubwa sana

    Ilibidi Shida awe mpole ili kuepuka mengi

    "David tulia tu,watatuua hawa" akasema Shida

    Wakamnyenyua David na kuondoka naye pale gest wakiwa wamemwekea silaha kwa siri ili asijalibu kuleta ujanja wowote ule

    "Ukileta ubishi kifo kitakuwa haki yako,hayo ndiyo maagizo ya bosi" akasema yule jambazi

    Waliondoka pale gest bila kushtukiwa na mtu yeyote yule mpaka kwenye gari na moja kwa moja wakaiwasha na kuanza kurudi na njia ya kuelekea Singida mjini

    "Tafadhali ndugu zangu,naomba muwe na utu,niambie kias cha pesa mnachokitaka nitawapa mniachie na baba mkamwambie mmenikosa" akajalibu kujisaidia David

    "Hatujawahi kuhalibu kazi ya mzee wako hata siku moja kwa hiyo usitegemee kitu kama hicho" akajibiwa

    "Lakin naamin mkimwambia mmenikosa hatajua na mimi nitapotelea sehemu asiyoijua" akasema David

    "Nahisi unajisumbua kijana,kwa sababu sisi tunaijua roho ya baba yako,tukifika pale bila wewe sisi ni maiti" akajibiwa

    David akabaki bila ujanja wa kufanya ili kujinusuru na jangalile

    Walipotembea kilomita sita kutoka Iguguno wakakutana na basi mbele yao likipunguza kasi

    Wakataka kulipita ile mbele wakaona magogo yametegwa njian

    Ni kitendo cha ghafla sana vijana kumi wakatoka vichakan wakiwa na silaha kali sana na kupiga risasi juu na magari yote mawili yakawekwa chini ya ulizni

    "Vip mkuu tujibu mashambulizi?" akauliza mmoja akimuuliza kiongozi wao pale

    "Hapana,tulia kwanza,ila wakija hapa kuleta ujinga tunazaa nao" akajib

    Vijana watatu walilifata lile gari alilokuwepo David na wale vijana waliowateka na wengine saba wakaliteka basi lile

    Wale vijana walipolikalibia like gari la kina David wakaanza kuwaamuru wote watoke nje ya gari

    Majambazi wale walitoka vizuri mpaka nje na akina David pia wakatoka



    "Jisachi ulichonacho na utupe hapo mbele, ujanja hatutaki na msipotoa kitu itabidi mvue nguo zote na kurud kwenye gari uchi" agizo lilitolewa

    Kama kuna ujinga walifanya wale watekaji ni kujisahau kwani pale pale mmoja wa wale vijana wa Dokta alitoa bastola yake na kuwaua wale watekaji wote.

    Milio ya zile risasi zilileta kizazaa kwa wale watekaji waliokuwa wamelidhibiti basi

    Wakatoka speed na kuanza kutupiana risasi na vijana wa Dokta

    Pale pale kwenye ule mpambano David alimvuta Shida kwa nyuma pole pole bila kuwashtua wale vijana wa Dokta kushtukia

    Mapambano yalizidi kuwa makubwa huku risasi zikitawala eneo lile

    David alipoona vijana wa Dokta wamekazana kupambana akamshika mkono Shida na wakaanza kujongea kuelekea kwenye vichaka vilivyokuwa kalibu na eneo lile

    Wakati wanazama kichakani mmoja wa Vijana wa Dokta aliweza kuwaona

    "Oyaaa oyaaa wanatoloka wale kuleee" alisema

    Na wenzake wote wakashtuka na kuangalia upande ule walikooneshwa

    Walipiga risasi kuelekea upande ule kwa fujo na zikampata David na akaanguka chini na kutulia

    Kitendo cha kugeuka kuwaangalia akina David kiliwapa nafasi wale watekaji cha kuongeza speed ya mashambuliziCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Na ndani ya muda mfupi wale Vijana wa Dokta wakajikuta mmoja baada ya mwingine wakianguka chini baada ya risaasi kadhaa kupenya kwenye miili yao

    Ndani ta dakika chache wote walikuwa tayari wako chini.

    Wale watekaji wakawasogelea kuhakikisha kama wamekufa.

    Walipofika wakawamalizia kwa risasi nyingi za kwenye miili yao

    "Kuna wenzao wamekimbilia vichakani humo inabid na wao tuwamalize hawawezi kuwaua wenzetu kijinga hivi" akasema mmoja wao

    Hayo maneno Shida aliyasikia vizur akiwa kule kichakani na mwili wa David ukiwa chini pembeni yake

    "Mungu wangu nimekwisha!!!" aliwaza mwenyewe

    Dokta akiwa na jazba sana alisubiri wale vijana wake warudi ili apate nafasi ya kuwashughulikia David na Shida

    "Wapuuzi sana hawa vijana, na huyu binti pamoja na fadhila zote nilizompatia anafanya upuuzi wa kunichanganya na mwanangu? Hukumu yake ni kifo" aliwaza

    Kitu ambacho Dokta hakukumbukua ni kuwa yeye ndiye chanzo cha Shida kumsaliti, kwani kitendo cha kumwibia siri ya Shida kutaka kuuawa na baba yake wa kufikia Alex ndicho alichotumia David kumpata Shida kiurahisi

    Alisubiri sana ila wale vijana hawakurejea

    Alipochoka kusubiri ilibidi ajadiliane na vijana wachache waliobaki pale ili wajue cha kufanya

    "Kwani bosi huna namba ya Ally umpigie tujue kinachoendelea?" aliuliza mmoja wao

    "Kweli nimechanganyikiwa! Sijakumbuka hilo, ninayo ngoja nimpigie" akasema Dokta

    Alitoa simu yake na kujaribu kupiga namba ya Ally tall kijana wake anayemuamin katika kufanya matukio makubwa ya mauaji

    Simu ya Ally tall iliita mpaka ikakata bila kupokelewa, akajalibu tena hali ikawa ile ile

    "Hebu mpigie wewe labda anaogopa kupokea simu yangu" akasema Dokta

    Kila aliyejaribu kumpigia simu ya Ally tall iliita bila kupokelewa na walipojalibu kupiga za wengine nazo majibu yakawa hayo hayo hazikupokelewa





    **********



    :: Unavyodhani nini kitaendelea?



    :: Hii ni mojawapo ya riwaya kali sana kutoka kwa mwandishi chipukizi hapa uwanja wa simulizi.

    Hakika si ya kukosa kwani ni zaidi ya Riwaya kutokea hapa uwanjani.



    :: Onesha ushirikiano wako katika kumpa sapoti mwandishi wa riwaya hii kwa ku LIKE, ku SHARE na hata ku COMMENT kuhusiana na hii riwaya hapo chini.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog