Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

ULINIUA GLORIA - 1

 





    IMEANDIKWA NA : NYEMO CHILONGANI



    *********************************************************************************



    Simulizi: Uliniua Gloria

    Sehemu Ya Kwanza (1)





    Kelele za shangwe zilikuwa zikisikika kutoka katika nyumba ya mzee Steven. Vigelegele kutoka kwa wakinamama vilikuwa miongoni mwa sauti za shangwe ambazo zilikuwa zikiendelea kusikika kutoka ndani ya nyumba hiyo ambayo ilikuwa imejengwa kisasa katika mtaa wa Magomeni Kondoa.
    Magari kadhaa yalikuwa yamekusanyika ndani ya eneo la nyumba hiyo, idadi kubwa ya magari hayo yalikuwa magari ya kifahari ambayo wala hakukuwa na mtu ambaye alishangaa kuyaona yakiwa yamepakiwa ndani ya eneo la nyumba hiyo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Sauti ya muziki ilikuwa juu ingawa wakati mwingine ilikuwa ikipunguzwa kutokana na mtu yeyote ambaye alikuwa akitaka kuongea lake katika hafla hiyo fupi ya kuwapongeza Peter na Gloria ambao walikuwa wakitarajia kufunga ndoa mwezi mmoja baadae ndani ya kanisa la Praise and Worship lililokuwa Mwenge.
    Wote ndani ya nyumba hiyo walionekana katika nyuso zilizokuwa na furaha kupita kawaida, walipenda kuwaona watoto wao hao wakiingia katika maisha ya ndoa, maisha ambayo yalionekana kutamaniwa na watu ambao walikuwa nje nayo lakini kuchukiwa na watu ambao tayari walikuwa ndani ya maisha hayo.
    Gloria hakuwa mbali na Peter, muda wote alikuwa pembeni yake huku akipiga piga picha kwa kutumia simu yake katika kila tukio ambalo lilikuwa likiendelea mahali hapo. Kazi kubwa ya Peter ilikuwa ni kukishika kiuno cha Gloria, kumbusu mara kwa mara huku akimuachia tabasamu pana.
    Baba yake Peter, mzee Steven alionekana kuwa mwenye furaha kubwa, muda wote alipokuwa akiongea, alikuwa akitabasamu tu huku akionekana kuzidiwa na furaha ambayo alikuwa nayo kwa kile kitu ambacho kilikuwa kinaendelea.
    Katika maisha yake alibahatika kupata watoto wawili tu, wa kwanza alikuwa Rachel ambaye alikuwa amekwishaolewa na wa pili alikuwa Peter ambaye baada ya siku kadhaa nae angeanza maisha ya ndoa pamoja na Gloria Michael.
    Katika sherehe hiyo, wazazi wake Gloria, mzee Michael Mshama na Bi Justina walikuwa miongoni mwa watu ambao walikuwa wamekusanyika katika hafla hiyo fupi ya kuwapongeza kwa hatua ile ambayo walikuwa wameifikia kwa wakati huo.
    Mpaka kufikia katika kipindi hicho, wao pia walionekana kuwa na furaha kubwa, hawakuamini kama binti yao, Gloria alikuwa akitarajiwa kufunga ndoa na baada ya hapo kuitwa mke wa mtu huku ukichukua muda mchache kabla ya kuitwa mama.
    Gloria ndiye alikuwa binti yao ambaye walikuwa wakimpenda kupita kawaida, walimthamini na kumpa kila kitu ambacho kama wazazi walitakiwa kumpa binti yao mpendwa. Kwao, Gloria ndiye alikuwa kila kitu, yeye ndiye alikuwa tabasamu nyusoni mwao.
    Ukaribu wa Peter na Gloria ulianza tangu walipokuwa darasa la pili katika shule ya Mwl Nyerere huku baada ya kufika kidato cha nne katika shule ya Benjamini wakaanza kuingia katika uhusiano wa kimapenzi. Ingawa walikuwa na furaha lakini uhusiano wao ulionekana kuwa na vizuizi vingi huku kizuizi kimoja na kikubwa kikiwa ni masomo.
    Walitamani kufanya mambo mengi katika maisha yao kwa wakati huo lakini masomo ndio kilikuwa kizuizi kikubwa. Muda mwingi walikuwa wakitamani kusoma pamoja lakini kila walipojaribu kufanya hivyo, walijikuta wakianza kushikanashikana na hatimae kulaliana na kufanya mapenzi.
    Kila mmoja kichwani alikuwa na ndoto yake ambayo alikuwa amejiwekea. Peter alikuwa na hamu kubwa ya kuwa Mchumi mkubwa hapo baadae huku Gloria akiwa na hamu ya kuwa Mwanasheria mkubwa hapo baadae. Kila mmoja alikuwa akiishi katika ndoto yake ambayo ilikuwa ikiendelea kukua kadri siku zilivyozidi kwenda mbele.
    Wakamaliza kidato cha nne na kukaa nyumbani kusubiri matokeo, yalipotoka, kila mmoja alikuwa amefaulu vizuri ila kwa wakati huu kila mmoja alikuwa akielekea kusoma tofauti na mwenzake. Peter alichaguliwa kujiunga na shule ya Tambaza huku Gloria akichaguliwa kujiunga na shule ya Zanaki zote zikiwa jijini Dar es Salaam.
    Kidogo sana ukaribu wao ukaanza kupungua, mambo yakaanza kubadilika, kila mtu akaanza kuukumbuka ukaribu ambao alikuwa nao kwa mwenzake katika kipindi kile ambacho walikuwa shule moja, tena darasa moja.
    Simu ndicho kilikuwa chombo cha mawasiliano ambacho walikuwa wakipenda kukitumia kuwasiliana, ingawa walikuwa mbalimbali lakini simu zikaonekana kuwafanya kuwa karibu sana. Kila siku walikuwa wakiwasiliana usiku, walikuwa wakichukua muda mwingi kuongea simuni, mchana wakiandikiana meseji mbalimbali na wakati mwingine kuonana faragha.
    Ingawa walikuwa wakifanya mambo mengi kama wapenzi lakini kamwe hawakusahau kuhusu Elimu, walikuwa wakiendelea kusoma zaidi na zaidi huku upendo wao ukiendelea kukua kadri siku zilivyokuwa zikizidi kusonga mbele.
    Wakafanikiwa kumaliza kidato cha sita na wote kuchaguliwa chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Walionekana kuwa na furaha kupita kawaida, wakaanza kusoma huku ukaribu wao ukiwa wazi kabisa na kutambulishana kwa wazazi wao. 
    Hiyo ilikuwa ni furaha kwao na kwa wazazi wao pia, wakaamua kuanza kufanya vitu kwa wazi kabisa kwani hawakuwa wakihofia kitu chochote kwa wakati huo. Mwaka wa kwanza ukakatika, mwaka wa pili ukaingia na ndipo walipoamua kuwaeleza wazazi juu ya lengo lao la kutaka kufunga ndoa na kuwa pamoja.
    Taarifa hiyo ikaonekana kuwa ya furaha kwa wazazi wao, wakatoa baraka zote na kuwaruhusu kwa moyo mmoja vijana wao kuoana na kuishi pamoja. Siku zilikuwa zimekatika sana, maandalizi ya harusi yalikuwa yamefanyika vya kutosha na katika kipindi hiki zilikuwa zimebakia siku thelathini kabla ya kufungwa kwa harusi hiyo kanisani.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Wazazi waliongea sana katika hafla hiyo fupi isiyokuwa na watu wengi huku kila mmoja akijaribu kuionyesha furaha yake ya waziwazi mahali pale walipokuwa. Kila mmoja alipomaliza kuongea, Peter akatakiwa kuongea kitu chochote alichokuwa nacho moyoni hata kabla ya Gloria nae kuitwa na kuongea.
    “Sijui niseme nini. Yaani najiona nimezidiwa na furaha kabisa. Kila ninapomuangalia Gloria nakumbuka kipindi kile alipokuwa mdogo na kuanza kuelekea nae shuleni. Unakumbuka Gloria?” Peter alisema na kumuuliza Gloria.
    “Nakumbuka. Ila sikuwa mdogo peke yangu. Sema tulikuwa wadogo” Gloria alimwambia Peter na kuwafanya watu wote mahali pale kuanza kucheka.
    “Nafahamu. Ila si unakumbuka kwamba nilikuwa mtu wa kwanza kukuvusha barabara? Nisingekuwa makini na wewe ungekuwa umekwishagongwa na gari. Nilianza kukulinda toka zamani sana, japokuwa tulikuwa wadogo lakini bado nilikuwa nikikuonyeshea jinsi gani ninakuthamini na kukulinda, sikutaka uvuke barabara peke yako, nilikuwa nikikushika mkono na kukuvusha barabara. Ulinzi ule ule ambao nilikuwa nikikupa toka utotoni ndio ulinzi ule ule ambao nitaendelea kukupa hadi uzeeni” Peter alisema huku akimwangalia Gloria.
    Watu wote ambao walikuwa wamekaa sebuleni pale wakabaki kimya, maneno ambayo alikuwa akiyaongea Peter yalionekana kuwa maneno mazito ambayo kwa msichana yeyote angeyasikia ni lazima angejiona ni kwa namna gani alikuwa akipendwa na kuthamaniwa.
    “Naona siku ya harusi ni mbali sana, acha nianze kukuahidi leo hii hii hata kabla ya harusi yenyewe” Peter alisema huku akimnyanyua Gloria na kuupitisha mkono katika kiuno cha Gloria na kisha kuendelea.
    “Nakuahidi kuwa nawe katika maisha yangu yote, nakuahidi kukupenda katika shida na raha, magonjwa na afya, furaha na maumivu. Naahidi kukupenda katika kila hatua ya maisha ambayo tutayapitia baada ya kuingia katika ndoa” Peter aliwambia Goria ambaye alibaki kimya huku kwa mbali macho yake yakianza kulengwa na machozi.
    Peter akabaki kimya kwa muda, alikuwa akimwangalia Gloria usoni, kwake, Gloria akaonekana kuwa mtu mpya, msichana mpya ambaye alikuwa ameongezewa uzuri zaidi ya ule ambao alikuwa nao kabla. Lipsi za midomo yake zilikuwa zikichezacheza tu huku akizitamani lipsi za Gloria. Alipoona ameridhika kumwangalia Gloria, akayarudisha macho yake kwa wazazi wa Gloria, mzee Michael na Bi Justina.
    “Nimeahidi mengi, nimeahidi kumtunza binti yenu katika njia iliyo njema. Ninawaomba ninyi pia mniruhusu kumchukua binti yenu, muda wenu wa kumlea naona unafikia tamati, sasa hivi nadhani ni muda wangu kumlea binti huyu mrembo, binti huyu aliyeuteka moyo wangu” Peter aliwaambia mzee Michael na Bi Justina.
    Ilipofika zamu ya Gloria kuongea, akashindwa kabisa kuongea kitu chochote kile, akaamua kumkumbatia Peter na kuanza kulia. Maneno ambayo aliyaongea Peter yalikuwa yamemgusa, aliyaona maneno mazito ambayo yalikuwa yakijirudia rudia moyoni mwake.
    “Nakupenda Peter. Nakupenda mpenzi” Gloria alimwambia Peter huku wakiwa wamekumbatiana.
    “Nakupenda pia Gloria” Peter alimwambia Gloria.
    Baada ya hapo, wote wakatawanyika na kuyafuata magari yao. Peter hakutaka kumuacha Gloria mikononi mwake, alikuwa amemshikilia vilivyo japokuwa mzee Michael alikuwa akimuita. Wote wakabaki wakiangaliana tu, mapenzi ambayo waliyokuwa nayo mioyoni mwao yalikuwa yakiendelea kuchipuka.
    “Ninakupenda sana Gloria” Peter alimwambia Gloria.
    “Ninakupenda pia”
    Baada ya hapo, Gloria akaingia garini na kuondoka mahali hapo. Muda wote huo Peter alikuwa amesimama tu mpaka pale gari lilipotoka machoni mwake. Akaanza kupiga hatua na kuelekea ndani ambapo akapitiliza hadi chumbani.
    Alipofika chumbani, akaanza kuchati na Gloria huku akionekana kuwa na furaha tele. Waliendelea kuchati mpaka saa tisa usiku, muda ambao akapitiwa na usingizi kitandani pale. Ingawa meseji zilikuwa zikiendelea kuingia, Peter alikuwa amekwishalala kitambo kutokana na uchovu mkubwa ambao alikuwa nao siku hiyo.
    “Nakupenda mpenzi. Najua umeshalala, ila utakapoamka naomba ujue kwamba ninakupenda sana. Mwaaaaaaaa! Hiyo ni kwa ajili yako pekee” Hiyo ilikuwa ni meseji ya mwisho ambayo Gloria alikuwa amemuandikia Peter ambaye alikuwa amekwishalala.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Ilikuwa ni taarifa nzuri kwa Peter ambaye alikuwa amefungua barua pepe yake na kukutana na majibu ya barua pepe ambayo alikuwa ameituma miezi miwili iliyopita juu ya kujiunga na chuo cha Biashara cha St’ Victor kilichokuwa jijini Lusaka nchini Zambia.
    Taarifa ile ilikuwa moja ya taarifa nzuri ambayo ilimpa furaha sana siku hiyo, alichokifanya ni kuichua na kuiweka kwenye laptop yake na kisha kuifunga. Uso wake ukajawa na furaha, akajiona kukamilisha ndoto ambazo alikuwa amejiwekea toka kipindi cha nyuma, ndoto cha kusoma katika moja ya chuo kikubwa Afrika.
    Wazazi wake waliporudi nyumbani usiku, akawataarifu juu ya taarifa ile, kila mmoja alionekana kufurahia kupita kawaida, mafanikio ya mtoto wao yalikuwa yakiwapa furaha kupita kawaida. Siku hazikuwa nyingi sana na alikuwa akihitajika chuoni hapo, alikuwa amepewa wiki mbili kwa ajili ya maandalizi tu.
    Alichokifanya ni kuanza kuwasiliana na Gloria na kisha kumwambia kuhusu taarifa ile, Gloria nae akaonyesha furaha na kuahidi kwenda nyumbani kwa mzee Steven kwa ajili ya kuonana na Peter, mpenzi wa maisha yake ambaye alikuwa akimpenda kupita kawaida.
    Alipofika ndani ya nyumba hiyo, akapokelewa kwa mabusu mengi na safari yao kuishia chumbani ambako huko wakakaa wakicheza muziki huku wakishikanashikana kama kawaida yao. Kila mmoja kwa wakati huo alionekana kuwa na furaha, mafanikio ya mmoja kati yao yalionekana kuwa mafanikio ya kila mtu.
    Siku iliyofuata, Peter akaanza kufanya maandalizi katika maduka mbalimbali huku akiwa pamoja na mpenzi wake, Gloria. Walitumia zaidi ya masaa matatu kutembea katika maduka mbalimbali na ndipo waliporudi nyumbani.
    “Na vipi kuhusu harusi yetu?” Gloria aliuliza.
    “Tutaoana tu. Hilo halina kipingamizi mpenzi” Peter alimwambia Gloria.
    “Najua tutaoana ila je itakuwa muda muafaka uliopangwa?” Gloria aliuliza.
    “Yeah! Nitakachokifanya mara baada ya kuelekea chuo, nitakupigia simu na kunifuata kule na kisha tutaoana kule kule” Peter alimwambia Gloria.
    “Yaani tuoane hata wazazi wasishiriki ndoa yetu?”
    “Kwani tatizo liko wapi? Ila usijali, wao pia watatufuata. Si unajua Zambia si mbali sana” Peter alimwambia Gloria.
    “Sawa. Ila inabidi tuoane haraka sana, nina hamu ya kuingia katika ndoa”
    “Usijali mpenzi”
    Furaha bado kwao iliendelea kama kawaida, walishinda siku nzima chumbani huku wakifanya kila kitu walichokuwa wakitaka kukifanya siku hiyo. Kuanzia hapo, wakazidi kuwa karibu zaidi, ukaribu wao ukaongezeka kiasi ambacho kiliwashangaza hata wazazi wao pia.
    Siku ziliendelea kukatika mpaka kufika siku ambayo Peter alitakiwa kuondoka kuelekea nchini Zambia. Walipofika uwanja wa ndege, Peter akamshika mkono Gloria na kuanza kumuaga. Muda wote huo Gloria alikuwa akilia tu, hakuamini kama mtu ambaye alikuwa akimpenda na kumzoea alikuwa akijiandaa na safari ya kuelekea masomoni nchini Zambia.
    “Mbona unalia sasa?” Peter aliuliza.
    “Inaniuma mpenzi”
    “Usijali. Nitakapofika tu, nitafanya mpango wa wewe kuja huko”
    “Najua ila naona kama uachelewa sana”
    “Sitochelewa wala kuwahi, nitahakikisha nakuja muda muafaka” Peter alimwambia Gloria.
    “Sawa mpenzi” Gloria alijibu na kisha kukumbatiana.
    Baada ya hapo, Peter akaanza kuwaaga tena marafiki zake na wazazi wake na kisha kuondoka na ndege ya siku hiyo huku moyo wake ukiwa umegawanyika sehemu mbili, sehemu ya kwanza ilikuwa ikimtaka kutokuondoka kwa sababu ya Gloria lakini sehemu nyingine ilikuwa ikimtaka kuondoka ili kukamilisha ndoto alizokuwa amejiwekea toka zamani.
    Harusi ambayo waliipanga ifanyike baada ya mwezi mmoja ikaonekana kuingia doa, kwa wakati huo Peter alikuwa akiangalia kuhusu masomo yake tu, alijua fika kwamba harusi ingeendelea kuwepo hata kama kingetokea kitu gani, ila kwa wakati huo alijiona kuwa na kila sababu za kuenda nchini Zambia na kujiunga na chuo cha St’ Victor kilichokuwa katikati ya jiji la Lusaka.
    Saa 10:17 ndege ilikuwa ikitua katika uwanja wa ndege jijini Lusaka ambako Peter akateremka na kuanza kuelekea ndani ya jengo la uwanja huo. Alipochukua begi lake hasa mara baada ya kuchunguzwa, akachukua teksi ambayo alimtaka dereva kumpeleka katika chuo Kikuu cha St’ Victor.
    Saa 10:45 gari ikaanza kuingia katika eneo la uwanja wa chuo kile ambako moja kwa moja akaanza kuelekea katika ofisi za chuo kile na kisha kujitambulisha kwa uongozi wa chuo kile. Akakaribishwa, akafanya ulipaji wa vyumba ambavyo vilikuwa katika chuo kile na maisha yake ya Elimu kuanzia ndani ya chuo hicho.
    Mara kwa mara alikuwa akiwasiliana na Gloria pamoja na wazazi wake, kila siku walikuwa wakimkumbushia kuhusu harusi ambayo walipanga ifanyike baada ya wiki kadhaa, Peter alionekana kuwa muelewa japokuwa hakutaka kuwaambia wazazi wake kwamba walikubaliana kufungia harusi nchini Zambia katika siku ambayo Gloria angekwenda kule kwa ajili ya kumtembelea.
    “Usiwaambie kama nitakuita huku kwa ajili ya kufunga ndoa” Peter alimwambia Gloria.
    “Sawa. Ila usichelewe mpenzi, ninatamani kufunga ndoa nawe” Gloria alimwambia Peter.
    “Usijali. Ngoja maisha yangu yatulie kidogo, nafikiri siku chache zijazo nitakuita kwanza uje tukae kwa muda na kisha tufunge ndoa takatifu kanisani” Peter alimwambia Gloria.
    “Sawa”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Maisha yalikuwa yakiendelea nchini Zambia, kila siku Peter alikuwa akiingia darasani, wanachuo wengi walikuwa wakitamani kuwa karibu na Peter chuoni hapo kwa sababu tu alikuwa Mtanzania, watu ambao walikuwa wakisifiwa kwa kuongea sana nchini Zambia.
    Peter alikuwa muongeaji mkubwa sana chuoni kitu ambacho kilimfanya kupata marafiki wengi sana akiwepo Kaposhoo, mtoto wa tajiri Charles nchini Zambia. Mara kwa mara Kaposhoo alikuwa karibu na Peter jambo ambalo liliwafanya kuwa marafiki wakubwa chuoni hapo.
    Kutokana na kuwa na fedha nyingi, Kaposhoo ndiye ambaye alimfundisha Peter kwenda katika kumbi za starehe na kunywa pombe, maisha ambayo Peter hakuwa ameyazoea kabla. Kazi kubwa ya Kaposhoo ilikuwa ni kutembea na kila msichana ambaye alikuwa akionekana mrembo mbele yake, maisha hayo akawa ameyazoea sana, fedha ambazo alikuwa nazo ziliwafanya wasichana wengi kumpapatikia.
    Tangu katika kipindi ambacho Peter alikuwa amezoeana na Kaposhoo, hakukuwa hata na siku moja ambayo Peter alitumia fedha zake, Kaposhoo ndiye ambaye alikuwa akimgawia Peter kiasi kikubwa cha fedha ambacho Peter alikuwa akiendelea kufanyia mambo yake.
    Hosteli za chuo zikaonekana kuwabana sana jambo ambalo liliwafanya kupanga nyumba nzima katika mtaa wa Kingstone, mtaa ambao ulikuwa ukikaliwa na matajiri tu nchini Zambia. Maisha yalionekana kuwa ya furaha, walikuwa wakijiachia kupita kawaida, japokuwa Kaposhoo alikuwa akipenda kulala na wasichana mbalimbali lakini hali ilionekana kuwa tofauti kwa Peter. 
    Peter hakutaka kuwa na msichana mwingine yeyote, uaminifu wake kwa msichana Gloria bado ulikuwa ukiendelea katika moyo wake. Kaposhoo hakutaka kumuona rafiki yake akiwa katika lindi la mawazo, kila siku alikuwa akijitahidi sana kumletea wasichana wa aina mbalimbali lakini bado Peter alikuwa akionyesha msimamo wa kulilinda penzi lake na Gloria.
    Japokuwa alikuwa amepanga kufunga ndoa na Glory ndani ya mwezi huo lakini mambo yakaonekana kubadilika mara baada ya kuwasiliana na wazazi wake na kuwaambia kwamba alikuwa ameahirisha mpaka katika miezi ijayo. Hiyo haikuonekana kuwa taarifa nzuri kutokana na mambo mengi kuwa tayari lakini kwa sababu mtoto wao huyo alikuwa masomoni nchini Zambia, wakakubaliana nae.
    Mwezi wa kwanza ukakatika, mwezi wa pili ukaingia na ndipo ambapo Peter akaamua kumuita Gloria nchini Zambia. Kwa mara ya kwanza kufika nchini Zambia, Gloria alionekana kuwa mwenye furaha kubwa, mara kwa mara alikuwa karibu na mpenzi wake, Peter.
    Ulipita muda mrefu sana bila wawili hao kuonana, walipofika nyumbani, kituo cha kwanza kilikuwa ni chumbani ambako wakaanza kufanya mambo ya kiutu uzima. Tendo lile liliwachukua dakika zaidi ya themanini, kila mmoja akaridhika.
    “Umepanga nyumba hii peke yako?” Gloria aliuliza.
    “Hapana. Ninakaa na rafiki yangu hapa. Mtoto mmoja wa tajiri hapa Zambia. Yeye ndiye aliyegharamia kila kitu” Peter alimwambia Gloria.
    “Sawa” Gloria aliitikia.
    Saa 12:18 gari la Kaposhoo likaanza kupaki mahali hapo na moja kwa moja kuteremka. Kiu yake kubwa kwa wakati huo ilikuwa ikitaka kumuona Gloria, msichana ambaye alimfanya Peter kutotaka kumsaliti katika kipindi ambacho alikuwa peke yake nchini Zambia.
    Mara baada ya kuingia ndani, akaanza kumuita Peter ambaye akafika sebuleni pale huku akiwa pamoja na Gloria. Macho ya Kaposhoo yalipotua kwa Gloria, kwanza akashtuka, uzuri wa Gloria ukaonekana kumshtua kupita kawaida. Huku akionekana dhahiri kuchanganyikiwa na uzuri ule, akaanza kumfuata na kumpa mkono kwa lengo la kumsalimia. Aliposhikana mikono na Gloria, akauhisi mwili wake ukipigwa na shoti kali, kwa mbali kijasho kilikuwa kikimtoka.
    “Karibu G” Kaposhoo alimkaribisha Gloria.
    “Asante” Gloria aliitikia.
    Muda wote Kaposhoo alikuwa akimwangalia Gloria, tayari uzuri wake ukaonekana kumchanganya kupita kawaida. Ni kweli alikuwa amekutana na warembo wengi lakini kwa Gloria alionekana kuwa na urembo wa tofauti sana, urembo ule ulikuwa ukimtetemesha moyo wake kila alipokuwa akimwangalia.
    “Inabidi nifanye kitu. Ni mrembo sana. Inabidi nifanye mapenzi pamoja nae kwa gharama yoyote ile, nilikuwa natamani kukutana na wasichana wa Kitanzania, kwa huyu, simuachi, hata kama urafiki na Peter utakufa, poa tu” Kaposhoo alikuwa akijisemea katika kipindi ambacho alikuwa akimwangalia Gloria ambaye alikuwa amelala mapajani mwa Peter kochini.




    Gloria alionekana kuwa tofauti kwa Kaposhoo, muda wote alikuwa akimwangalia kwa macho ya matamanio, macho ambayo yalionyesha dhahiri kwamba alikuwa akitaka kulala nae tu. Uzuri wa Gloria ulikuwa ukiutetemesha moyo wa Kaposhoo, kila alipokuwa akimwangalia aliuhisi mwili wake ukiwa kwenye dimbwi zito la mapenzi, dimbwi ambalo alishindwa kabisa kuogelea na alijiona kama alikuwa akikaribia kuzama.
    Kitu alichokuwa akikitaka ni kulala na Gloria tu, hakuangalia kuhusu urafiki mkubwa ambao alikuwa nao kwa Peter, kitu ambacho alikuwa akikiangalia kwa wakati huo ni kukidhi tamaa za mwili wake tu. Kila siku alipokuwa akimwangalia Gloria alizidi kuwa mrembo kiasi ambacho Kaposhoo akaona ilikuwa heri kugombana na Peter lakini si kumuacha Gloria ambaye kila siku alizidi kuonekana mrembo.
    Alichokijua yeye ni kwamba alikutanana Peter chuoni, hakuwa amekua nae toka utotoni jambo ambalo lilimfanya kutokuhisi uzito wowote kama angeamua kutembea na Gloria, asingejisikia hukumu yoyote moyoni mwake. Hapo ndipo ambapo Kaposhoo akaamini kwamba wanawake wengi wa Kitanzania walikuwa warembo waliokuwa na figa nzuri ambazo kwa mwanaume yeyote anayejua kutamani basi ni lazima angeingiwa na pepo la uzinzi mara amuaonapo mwanamke kutoka nchini Tanzania.
    “Anazidi kunawili tu” Kaposho alijisemea moyoni katika kipindi ambacho alikuwa akimwangalia Gloria ambaye alikuwa akimvutia kupita kawaida.
    Kaposhoo hakujua ni mahali gani ambapo alitakiwa kuanzia ili kumteka Gloria, kila siku ndoto zake zilikuwa juu ya Gloria tu. Hakutaka kujihusisha tena na wanawake wa hapo Zambia kwa kuona kwamba hawakuwa wanawake wazuri kama alivyokuwa Gloria. Kuhusu kuchukua wanawake wa Kizambia, Kaposhoo akaiacha tabia hiyo, hakutaka kuonekana machoni mwa Gloria kwamba alikuwa mtu wa wanawake, alitaka aonekane mtu mwema jambo ambalo alifanikiwa kwa asilimia kubwa.
    Hata katika kipindi ambacho alikuwa akitafuta mazoea kwa Gloria, Peter hakuonekna kuhofia kitu chochote kile kwani kwake watu hao wawili walionekana kuwa waaminifu sana, kwa Gloria, Peter hakudhania kama msichana huyo angeweza kumsaliti na kumfuata mwanaume mwingine zaidi yake huku kwa Kaposhoo, alimuona kuwa rafiki yake mkubwa ambaye wala asingeweza kutembea na msichana ambaye alijua fika kwamba alikuwa msichana wake.
    Kujiamini huko kukaonekana kuwa kosa kubwa sana kwani kitendo cha Peter kuwaacha mara kwa mara peke yao sebuleni, Kaposhoo akaanza kupiga ndogo ndogo ambazo zilikuwa zikimfanya Gloria kuchekacheka tu. Kaposhoo hakuonekana kujali, alijua fika kwamba kwa mwanaume yeyote ambaye unamtaka msichana fulani, haukutakiwa kuwa na haraka, ulitakiwa kufanya mambo yako taratibu sana na mwisho wa siku msichana huyo anakuwa wako.
    Fedha kwake zikaonekana kuwa silaha kubwa kwa kila msichana ambaye alikuwa akimtaka. Kwa sababu alikuwa akimtaka sana Gloria, fimbo yake kubwa ilikuwa ni fedha ambazo kwa kiasi fulani zilionekana kumchanganya Gloria. Kaposhoo hakuona hasara kutumia zaidi ya kwacha laki moja kwa siku, kitu ambacho alikuwa akikitaka ni kumchanganya Gloria na mwisho wa siku anakuja kuwa wake na kuanza kutanua nae kama kawaida yake.
    “Unanawili sana siku hizi. Nini siri ya mafanikio yako?” Kaposhoo alimuuliza Gloria huku akitoa tabaamu pana.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    “Kula vizuri tu” Gloria alijibu huku akionekana kusikia aibu.
    Kaposhoo hakutaka kukaa kochini hapo tu, alichokifanya ni kuinuka na kisha kumsogelea Gloria ambaye alikuwa katika kochi jingine na kumuinamia kwa nyuma. Pumzi yake ikaanza kumpiga Gloria shingoni mwake, kutokana na kiyoyozi kilichokuwa ndani ya nyumba kile kilivyokuwa kikitoa kijiubaridi, Gloria akaanza kujisikia hali ya utofauti.
    “Leo tunakula nini?” Kaposhoo alimuuliza Gloria.
    “Sijui. Wewe unataka tule nini?” Gloria alimuuliza.
    “Chochote tu utakachopenda” Kaposhoo alimwambia Gloria.
    “Ngoja niandae chakula kizuri” Gloria alimwambia Kaposhoo na kisha kuinuka kochini hapo.
    Akaanza kupiga hatua kuelekea jikoni. Kaposhoo akatulia kochini pale, tayari alijiona kwenda kushinda kile alichokuwa akikitaka. Hakuonekana kuogopa, ndani ya nyumba walikuwa wawili tu huku Peter akiwa chuoni. Alichokifanya Kaposhoo ni kusimama na kisha kuelekea kule kule jikoni ambapo akamkuta Gloria akikata kata nyanya huku akiwa amesimama na kuupa mgongo mlango.
    Kaposhoo alivyoona hivyo, akaanza kupiga hatua ndogo ndogo, alipomfikia Gloria, akaipeleka mikono yake kiunoni mwa Gloria. Mategemeo yake yote alifikiri kwamba angepata upinzani kutoka kwa Gloria, kilichomshangaza, hakukuwa na upinzani wowote ule. Hiyo ikaonekana kuwa nafasi kwake, akaanza kuusogeza mdomo wake mpaka katika shingo ya Gloria na kisha kumbusu.
    Katika kila hatua ambayo alikuwa akiipiga mwilini mwa Gloria, msichana huyo alikuwa akitulia, hakuonyesha kipingamizi chochote kile. Mpaka kufikia hatua hiyo, tayari Kaposhoo akajiona kuwa mshindi ambaye alitakiwa kufanya kitu chochote kile. Mikono yake haikutulia, alichokifanya ni kuanza kuipeleka kwa juu mpaka kufikia sehemu iliyokuwa na matiti ya Gloria na kisha kuanza kuyashikashika.
    Hali ile ikamfanya Gloria kuanza kuunyonganyonga mwili wake huku akikiachia kisu alichokishika na kisha kuishika mikono ya Kaposhoo ambaye tayari alionekana kuchanganyikiwa na kuingiwa na mzuka wa kufanya ngono tu.
    “Niacheeeee.....” Gloria alimwambia kaposhoo kwa sauti ya mahaba huku akijaribu kuitoa mikono ya Kaposhoo ambayo ilikuwa ikiendelea kuchezea matiti yake.
    “Tatizo nini? Wewe si uendelee kukata nyanya tu” Kaposhoo alimwambia Gloria.
    “Niacheeee” Gloria alimwambia Kaposhoo katika sauti ambayo ilimwambia kuendelea kufanya vile.
    Kaposhoo hakuonekana kukubaliana nae, alichokifanya ni kuendelea kuyachezea matiti ya Gloria ambaye alionekana kuchanganyikiwa zaidi. Gloria akaonekana kuchoka, hatua ambayo alifikia Kaposhoo ikaonekana kumchosha hali iliyompelekea kumwachia mwanaume huyo afanye chochote kile alichokuwa akitaka kukifanya mwilini mwake.
    Hiyo ikaonekana kuwa nafasi zaidi kwa Kaposhoo, alichokifanya ni kuanza kuifungua blauzi aliyokuwa ameivaa Gloria na kisha kuyaacha matiti yake ya saa sita kuwa wazi. Kaposhoo akaona kutokufaidi, akamgeuza Gloria na kisha kuanza kuangaliana nae. Tayari Gloria akaonekana kuchanganyikiwa, macho yake yalikuwa yamelegea kupita kawaida, macho ambayo yalionyesha kwamba alikuwa tayari kwa kila kitu mahali hapo.
    Huku wakiwa wanaangaliana tu, ghafla mlio wa gari ukaanza kusikika kutoka nje, gari ambalo alikuwa akilitumia Peter. Kwa haraka sana Kaposhoo akachomoka jikoni pale na kisha kuelekea chumbani huku Gloria akianza kufunga vifungo vya blauzi yake na kuendelea kukata nyanya.
    Wala hazikupita sekunde nyingi, Peter akatokea mahali hapo, alipokwenda jikoni na macho yake kumuona Gloria, tabasamu pana likatawala usoni mwake, akaanza kumsogelea na kisha kumbusu.
    “Nilikumiss sana mpenzi” Peter alimwambia Gloria huku akiachia tabasamu pana.
    “Hata mimi. Nilikumiss pia” Gloria alimwambia Peter na kisha kubusiana.
    Hayo ndio maisha ambayo yalikuwa yakiendelea ndani ya nyumba hiyo, Peter alikuwa akinyeshewa unafiki wa mapenzi ya dhati kutokwa kwa Gloria lakini ukweli ni kwamba katika kipindi hicho msichana huyo akaonekana kubadilika, mapenzi ambayo alikuwa nayo juu ya Peter yakaonekana kuhama na kuhamia kwa mwanaume ambaye alikutana nae kwa mara ya kwanza hapo Zambia, Kaposhoo.
    Gloria hakuonekana kufikiria kwamba alikuwa na mpenzi wake, Peter ambaye alikuwa tayari kufunga nae ndoa, kitu ambacho alikuwa akikifikiria ni kuwa na Kaposhoo tu ambaye alionekana kuwa na fedha kupita kawaida. Ingawa Peter alikuwa akielekea chuoni kila siku lakini hali ilikuwa tofauti kwa kaposhoo, ratiba yake ya kwenda chuoni ikaonekana kupungua kabisa, alikuwa akitumia muda mwingi kukaa nyumbani jambo ambalo lilimchanganya Peter.
    “Siku hizi huendi kabisa chuo” Peter alimwambia Kaposhoo.
    “Nadhani kuna mchezo wa kishirikina nachezewa siku hizi” Kaposhoo alimwambia peter.
    “Kwa nini?”
    “Ninaumwa sana. Naweza kusema kwamba kesho nakwenda chuo, nitasoma sana ila hiyo kesho ikifika tu, naumwa mpaka siwezi kuamka” Kaposhoo alimwambia Peter.
    “Pole sana”
    “Asante sana” Kaposhoo alimshukuru Peter.
    Hiyo ndio ilikuwa kazi yake, hakutaka kwenda chuoni, tayari Gloria akaonekana kumchanganya kupita kawaida. Kila siku akawa mtu wa kuuchezea mwili wa Gloria lakini kufanya ngono kikawa ni kitu ambacho Gloria alikuwa akikipinga sana. Kaposhoo hakutaka kuonekana kuwa na haraka, kila siku aliamini kwamba Gloria asingeweza kuchomoka katika mikono yake, kama alikuwa akikaza sana, aliamini kwamba kuna siku angechoka kukaza na hatimae kufanya kile alichokuwa akikitaka, kuivua sketi ya Gloria na kufanya nae mapenzi.
    Kushikwashikwa na Kaposhoo kila siku kukaonekana kuzidi kumpagawisha Gloria, kila alipokuwa akimuona Kaposhoo, mapigo yake ya moyo yalikuwa yakimdunda sana. Japokuwa alijua fika kwamba alikuwa na mpenzi wake, Peter lakini hakuacha kumfikiria Kaposhoo, mwili wake ukaonekana kuanza kuwashwa na hakuona mwanaume yeyote ambaye angeweza kuukuna zaidi ya Kaposhoo ambaye tayari alikuwa ameingia ndani ya moyo wake na kuvuta kiti.
    Hali hiyo ndio ambayo ilimfanya Gloria kumvulia sketi Kaposhoo na kwa mara ya kwanza kumsaliti Peter kwa mwanaume huyo ambaye kwake alimuona kuwa mwanaume aliyekuwa na mapenzi ya dhati. Siku hiyo wakalala chumbani mchana wakifanya mapenzi tu. Gloria hakuonekana kujutia kile kilichokuwa kikiendelea kutokeaa, kwake, Kaposhoo alionekana kuwa mwanaume sahihi ambaye alistahili kumvulia sketi yake na hatimae kumsaliti Kaposhoo.
    Kwa Gloria wala hakujisikia hukumu hata mara moja, kitu ambacho alikuwa akikifanya alikiona kuwa sahihi kufanywa na mtu kama yeye, mtu ambaye alikuwa ameangukia katika mikono ya mwanaume mwingine, mwanaume ambaye alionekana kumjali zaidi ya kitu chochote kile, MOYO WAKE UKAMSAHAU PETER.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Peter hakuonekana kufahamu kitu chochote kile ambacho kilikuwa kikiendelea nyuma ya pazia, hakujua kwamba rafiki yake, Kaposhoo alikuwa akitembea na mpenzi wake, Gloria, msichana ambaye alikuwa akitarajia kumuoa katika kipindi kichache kijasho. Kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea kwake alikichukulia kawaida sana.
    Maisha yaliendelea kusonga mbele kama, Peter aliendelea kupigwa upofu katika kila kilichokuwa kikiendelea katika maisha ya Gloria. Hata Kaposhoo aliposema kwamba alikuwa akibaki nyumbani kwa kuwa hakuwa akijisikia vizuri, Peter hakuonekana kuwa na wasiwasi hata kidogo.
    Uaminifu wake alikuwa ameuweka kwa Gloria kupita kawaida, ilikuwa radhi aambie kitu chochote kile lakini si kuambiwa kwamba Gloria alikuwa akimsaliti. Uaminifu wake kwa Gloria ulikuwa mkubwa kupita kawaida, alimuamini zaidi ya mtu yeyote yule katika maisha yake..
    Gloria hakuonekana kujihukumu moyoni mwake, alikuwa akiendelea zaidi na zaidi kutembea na kaposhoo ambaye alionekana kutokuwa na wasiwasi hata mara moja. Katika kipindi ambacho Gloria aliendelea kubaki nyumbani hapo ndicho kilikuwa kipindi ambacho Kaposhoo akatoa wazo moja ambalo lilionekana kuwa zuri sana, wazo ambalo lingeendelea kumuwekea upofu Peter kwa kutokujua kile kilichokuwa kikiendelea.
    “Ndio hivyo. Msichana kukaa nyumbani tu si kitu kizuri, mtu kama huyu inabidi atafutiwe kazi na kuanza kuelekea kazini kwa ajili ya kujiingizia kipato” Kaposhoo alimwambia Peter ambaye alikuwa makini kumsikiliza.
    “Hilo ni wazo zuri sana lakini tatizo sijui nitaanzia wapi kumtafutia kazi hiyo, sijawa mwenyeji sana hapa Zambia” Peter alimwambia kaposhoo.
    “Hilo si tatizo, suala hapa ni kumuuliza yeye alikuwa akihitaji kazi gani” Kaposhoo alimwambia peter.
    Gloria akaitwa mahali hapo na kuulizwa kazi ambayo alikuwa akiihitaji. Kaposhoo hakuonekana kuwa na wasiwasi hata mara moja, kitu ambacho alikuwa akikiamini ni kwamba kazi yoyote ile ambayo Gloria angeichagua kwake lisingekuwa tatizo kuipata.
    Fedha za baba yake zilimfanya kujiamini kupita kawaida, umaarufu wa baba yake nchini Zambia ukaonekana kuwa mkubwa kiasi ambacho kusingekuwa na mtu yeyote yule ambaye angeweza kusema kitu chochote kile kwake. Ukiachana na hilo, heshima kubwa ambayo alikuwa ameitengeneza baba yake nchini Zambia ilikuwa ikimpa kiburi sana jambo ambalo aliamini kwa asilimia mia moja angefanikisha suala zima la Gloria kufanya kazi katika kampuni yoyote ile.
    “Kazi yoyote tu ambayo itanifanya kuondoka mahali hapa kila nyakati za asubuhi” Gloria alimwambia Kaposhoo.
    “Unaweza kuwa mhudumu wa hoteli, wa kukaa pale mapokezini?” Kaposhoo alimuuliza Gloria.
    “Ila sijasomea”
    “Hilo si tatizo. Bila kusomea, unaingia popote unapopataka, kila kitu kipo chini yangu. Utaweza?” Kaposhoo alimwambia Gloria na kumuuliza.
    “Hakuna tatizo” Gloria alimjibu.
    Kwa Kaposhoo, jambo lile likaonekana kuwa dogo sana ambalo wala halikuweza kumsumbua kichwani mwake Alichokifanya ni kuanza kujifikiria ni hoteli gani ambayo ilikuwa nzuri zaidi nchini Zambia kwa ajili ya kumpeleka Gloria kuanza kazi, kwake akaiona hoteli ya Paradise 5 ambayo ilikuwa pembezoni mwa jiji la Lusaka.
    Kitu alichokifanya kaposhoo ni kuwasiliana na baba yake, Bwana Charles Mbwana ambaye akalichukulia uzito suala hilo na kisha kuanza kuwasiliana na meneja wa hoteli hiyo kubwa na ya kitalii, Bwana Stewart Paul. Kutokana na heshima walizokuwa wakiwekeana wawili hao, Bwana Stewart hakuonekana kupinga, alichokitaka yeye ni kuonana na Gloria tu kwa ajili ya mahojiano kadhaa kabla ya kuanza kufanya kazi.
    “Niliwaambia, hili si tatizo hasa kwangu mimi” Kaposhoo aliwaambia huku akionekana kuwa na furaha.
    “Mbona mambo yamekwenda kirahisi namna hii?” Peter aliuliza huku akionekana kushangaa.
    “Mjini hapa, wenye fedha ndio wanaopata vile wanavyovitaka” Kaposhoo alimwambia Peter huku akionekana kuwa na furaha.
    “Nashukuru sana Kaposhoo...nashukuru sana” Gloria alimwambia Kaposhoo.
    “Usijali Gloria” Kaposhoo alimwambia Gloria.
    Kila kitu kilichokuwa kikiendelea machoni mwa Peter kilionekana kuwa msaada mkubwa kwa mpenzi wake kumbe ukweli ni kwamba ule ulikuwa mchezo mkali ambao ulitakiwa kumpoteza kabisa na hatimae aweze kuachana na Gloria na Kaposhoo amchukue jumla jumla.
    Siku iliyofuata ilikuwa siku ambayo Kaposhoo na Peter walikuwa na jukumu la kumpeleka hotelini. Ndani ya gari, Kaposhoo na Gloria walikuwa wakiangaliana kwa macho ya wizi huku wakionekana kuwa na kitu ambacho kilikuwa kinaendelea kati yao. Uwepo wa Peter ndani ya gari lile ukaonekana kuwanyima kufanya mambo fulani ambayo walitakiwa kufanya kama wapenzi.
    Peter alikuwa amekwishaondoka ndani ya moyo wa Gloria na nafasi yake kuchukuliwa na kijana mwenye pesa, Kaposhoo. Safari ile iliendelea zaidi mpaka walipofika katika eneo la hoteli ya Paradise 5 ambapo wakateremka na moja kwa moja kuelekea katika jengo la hoteli hiyo na kutaka kuonana na meneja ambapo wakaelekezwa katika ofisi aliyokuwepo.
    Bwana Stewart ambaye ndiye alikuwa meneja wa hoteli ile akawakaribisha na kisha kuanza kuongea nao. Wala hakukuonekana kuwa na tatizo lolote lile kwani Bwana Mbwana alikuwa amekwishaongea ne kila kitu.
    “Karibu sana” Bwana Stewart alimkaribisha Gloria huku akimshka mkono.
    “Asante sana” 
    Hiyo ndio ilikuwa siku ya kwanza kwa Gloria kuingia ndani ya hoteli ile kubwa ya kitalii, hakuamini kama kweli alikuwa akienda kuanza kazi ndani ya hoteli ile ambayo ilikuwa na jina kubwa nchini Zambia. Peter akashindwa kuvumilia, kila siku akawa mtu wa kumshukuru Kaposhoo kwa kile alichokuwa amekifanya bila kugundua mchezo mchafu ambao ulikuwa ukichezwa nyuma ya pazia.
    Mahusiano hayakukatika, japokuwa kila siku Gloria alikuwa akishinda hotelini lakini Kaposhoo alikuwa akiendelea kujiachia nae kama kawaida kiasi ambacho wafanyakazi wote wa hotelini wakajua kwamba Gloria alikuwa msichana wa Kaposhoo na si Peter.
    ****
    Jina la Stewart Paul lilikuwa ni miongoni mwa majina ya watu waliokuwa wakijulikana kuwa na fedha sana katika nchi ya Zambia. Mzee huyo aliyekuwa na miaka hamsini na mbili alikuwa akijulikana zaidi kutokana na kumiliki hoteli kadhaa zilizokuwa zikiitwa Paradise ambazo zilikuwa zikipatikana nchini Zambia, Zimbabwe na mbili ambazo zilikuwa zikijengwa nchini Tanzania katika mkoa wa Arusha na Dar es Salaam.
    Katika kipindi chote alichokuwa akikaa Zambia, Bwana Stewart hakutaka kumpa mtu nafasi ya umeneja, alijua fika kwamba alikuwa mkurugenzi lakini kutokana na kutokuamini mtu yeyote hasa katika mali zake, akajipa vyeo hivyo viwili, vyeo ambavyo vilimfanya muda mwingi sana kuwa bize.
    Bwana Stewart alikuwa mtu wa watu, alikuwa akipenda kumsikiliza kila mtu ambaye alikuwa na shida iliyokuwa ikihitaji fedha, hakuzichungulia fedha zake, kila mtu ambaye alikuwa akihitaji msaada, alikuwa akimpatia bila maswali yoyote yale.
    Jambo hilo likawafanya watu wengi kumpenda na kumthamini kutokana na mchango ambao alikuwa akiutoa kwa wananchi ambao walionekana kuwa na njaa kali nchini Zambia. Serikali ilimuona Bwana Stewart kuwa mtu wa maana sana, mtu ambaye alikuwa akihitajika katika kila jamii ya watu katika bara la Afrika, mali zake pamoja na fedha zake hakula peke yake, alikuwa akipenda kutumia na watu ambao walikuwa katika umasikini mkubwa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Hoteli za Paradise 5 ndizo zilikuwa hoteli pekee ambazo zilikuwa zikitoa vyakula kwa watu wasiokuwa na vyakula katika siku ya Ijumaa na Jumapili jambo ambalo liliwafanya watu wengi masikini kuendelea kumshukuru kila sku. Katika maisha yake yote, alikuwa akiwathamini sana masikini, aliyajua vilivyo maisha ambayo walikuwa wakipitia watu masikini, alikuwa akiyafahamu vilivyo maumivu waliyokuwa nao masikini kutokana na yeye kupitia maisha hayo.
    Aliuchukia umasikini, hakupenda kuwaona watu wakiwa masikini, wakilala bila chakula au wakiwa na uhitaji wa fedha. Katika kila pumzi ambayo alikuwa akivuta, alikuwa akiwafikiria masikini ambao bado walikuwa wakiendelea kuhitaji msaada kutoka kwake. Bwana Stewart hakuwaacha, aliendelea kuwajali na kuwasaidia kama kawaida yake.
    Kupitia misaada mbalimbali ambayo alikuwa akiitoa bila majivuno yoyote yale, Bwana Stewart akajikuta akipata fedha zaidi, baraka za Mungu zikaonekana kumjalia katika maisha yake. Mipango yake mingi ambayo ilikuwa haikamiliki ikakamilika kama alivyokuwa akitaka.
    “Wenye matatizo wanahitaji kusaidiwa, haitakiwi chakula kimwagwe hata mara moja. Hata hayo unayoyaona kwamba ni makombo, wape wasiokuwa na vyakula nao watayaona kuwa chakula bora kwao” Bwana Stewart aliwaambia wafanyakazi wake na kuendelea.
    “Unapomwaga chakula, unapata laana. Wewe unakimwaga na wengine wanakitafuta. Mteja akibakisha chakula, kiwekeni, kipasheni moto, mkiona mtu mwenye shida na chakula anapita, muiteni aje ale kuliko kwenda kukimwaga” Bwana Stewart aliendelea kuwaambia wafanyakazi wake.
    Katika mambo yote, hakupenda kuona chakula kikimwagwa jalalani na wakati kulikuwa na watu wengi ambao walikuwa wakihitaji chakula, kila siku akawa mtu wa kuwasisitizia wafanyakazi wake kwamba ilikuwa ni lazima kuwagawia vyakula watu ambao walikuwa na shida mbalimbali na si kuvimwaga kama walivyokuwa wakifanya wafanyakazi wa hoteli nyingine.
    Japokuwa alikuwa akisaidia watu wengi, japokuwa alionekana kuwa mtu muhimu katika jamii ya watu wa zambia lakini Bwana Stewart alikuwa na ulevi mmoja maishani mwake, wanawake. 
    Bwana Stewart alikuwa mtu wa wanawake sana, katika maisha yake hakuwa mtu wa kunywa pombe wala kuvuta sigara, vitu hivyo viwili alikuwa amepigana navyo sana na kuvishinda lakini katika suala la wanawake, alikuwa ameshindwa kabisa kupigana nalo.
    Kila siku alikuwa mtu wa kutembea na wanawake mbalimbali, kila siku akawa mtu wa kuwahonga wanawake mbalimbali na kulala nao kama kawaida. Nyumbani alikuwa na mke pamoja na watoto watatu lakini suala la wanawake kwake wala halikuisha. Kila mwanamke mzuri ambaye alikuwa akipita mbele yake alikuwa anahakikisha analala nae kama kawaida.
    Kutokana na fedha ambazo alikuwa nazo, wanawake walikuwa wakimpapatikia sana, kila siku walikuwa wakimfuata hotelini, aliwapa fedha na kuendelea na mchezo wake kama kawaida. Mke wake, Bi Hilda alikuwa ameongea sana lakini Bwana Stewart hakuonekana kubadilika hata mara moja. 
    “Wanawake...aisee siwezi kuwaacha. Ni bora uninyime chochote kile maishani mwangu lakini si kuacha kutembea na wanawake wazuri” Bwana Stewart alimwambia tajiri mwenzake, baba yake na Kaposhoo, Bwana Mbwana.
    “Hilo ndio la muhimu, unapokuwa na fedha lazima uwe na wanawake wengi hasa sisi kwa wazee ambao ujanani mwetu wazee wetu walikuwa wakituchunga sana” Bwana Mbwana alimwambia Bwana Stewart.
    Hiyo ilionekana kuwa kama kazi yao, wawili hao walikuwa wakipenda wanawake kupita kawaida. Hawakujali wanawake wa aina gani, wale wembamba, wanene, warefu kwa wafupi walikuwa wakilala nao kama kawaida. Kwa hapo hotelini, kwa kila msichana ambaye alikuwa akitaka kuanza kazi katika hoteli ile ilikuwa ni lazima alale nae na kisha kumpa kazi katika hoteli hiyo.
    Katika siku ambayo aliambiwa na Bwana Mbwana kwamba kijana wake, Kaposhoo alikuwa akimleta msichana wake kwa ajili ya kufanya kazi katika hoteli hiyo, Bwana Stewart wala hakuwa na uso wa tamaa, alichokuwa akikijua ni kwamba msichana huyo alikuwa ni wa kawaida tu, hivyo wala asingeweza kufanya jambo lolote lile kwani hakutaka kugombani mwanamke na mtu ambaye alionekana kuwa kama mtoto wake, Kaposhoo kisa mwanamke.
    Katika kipindi ambacho Gloria alikuwa ameingia mahali hapo, Bwana Stewart akaonekana kutokwa na kijasho chembamba, hakuamini kama macho yake yalikuwa yamemuona msichana mzuri kama alivyokuwa Gloria, kila alipokuwa akimwangalia, aliona ni bora kugombana na Kaposhoo lakini si kumuacha msichana huyo apite katika mikono yake.
    Hakuonyesha kipingamizi, tena kwa sababu Gloria alikuwa akihitaji kazi kwa udi na uvumba, akampa kazi na cheo juu cha kuwa msimamizi wa mambo ya usafi ndani ya hoteli ile. Suala lile likaonekana kuwashangaza wafanyakazi wengine lakini wakawa wamekwishajua kulikuwa na kitu gani ambacho kiliendelea moyoni mwa Bwana Stewart, wakakubaliana nae.
    Katika kipindi chote hicho, Bwana Stwewart alikuwa akimwangalia Gloria tu, umbo lake pamoja na sura yake ya kitoto vilikuwa vitu ambavyo vilimchanganya sana jambo ambalo lilimpelekea kujiapiza kwamba piga ua ilikuwa ni lazima kutembea na msichana Gloria. 
    Katika siku ya kuandika mkataba wa kufanya kazi ndani ya hoteli hiyo, mshahara wa Gloria ulikuwa ni mara mbili zaidi ya mishahara ya wafanyakazi wengine ndani ya hoteli ile. Gloria hakujua kama alikuwa amepewa ofa kubwa ya mshahara mpaka pale alipoambiwa na mzee huyo.
    “Huu mshahara ni mara mbili juu zaidi ya mishahara ya wafanyakazi wengine” Bwana Stewart alimwambia Gloria katika kipindi ambacho alikuwa akisaini mkataba ndani ya ofisi yake.
    “Asante sana. Ila kwa nini umeamua kufanya hivyo?” Gloria aliuliza huku akionekana kushangaa.
    “Kwa muonekano tu, unaonekana kuwa msichana muaminifu sana kuliko wafanyakazi wa hapa. Ukifanya kazi kwa kuniridhisha zaidi, utakuwa sekretari wangu, huyo mwingine nitampeleka sehemu nyingine na mshahara wako utakuwa juu zaidi” Bwana Stewart alimwambia Gloria ambaye alionekana kuwa na furaha zaidi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    “Asante sana” Gloria alimwambia Bwana Stewart ambaye akasimama kutoka kitini.
    “Usijali. Unajua unapokuwa na mamlaka sehemu fulani ni lazima uonyeshe kwamba una mamlaka. Hilo usitie shaka, onyesha ushirikiano kwa wenzako pamoja na mimi kila kitu kitakuwa sawa. Kuhusu hili la mshahara naomba usiwaambie wenzako” Bwana Stewart alimwambia Gloria.
    “Sitowaambia” Gloria aliitikia na kisha kuruhusiwa kuondoka ofisini hapo.
    Bwana Stewart akarudi kitini na kuweka mguu juu, hakuamini kama kweli msichana Gloria angeweza kumkatalia mara pale atakapoanza kupiga ndogo ndogo. Kwake, Gloria alionekana kuwa msichana mwepesi sana ambaye kama ungetumia silaha ya fedha basi wala asingeweza kuteteleka hata mara moja, angefanya kila kitu ambacho ungetaka akifanye, likiwepo suala la kufanya mapenzi.
    “Hanisumbui huyu. Nitatembea nae na sitohitaji lawama kwa mtu yeyote yule. Kama mtu anahitaji kulaumu, amlaumu yule aliyetengeneza fedha” Bwana Stewart alisema huku akionekana kuwa na furaha pamoja na uhakika wa kumpata Gloria bila kujua kwamba hata Kaposhoo nae alikuwa si msichana wake bali alikuwa amemuibia rafiki yake wa karibu, Peter.


    Fedha ilionekana kuwa kila kitu kwa Bwana Stewart, hakuamini kama kulikuwa na msichana yeyote ndani ya bara la Afrika ambaye angemuonyeshea pesa na kumuomba amvulie sketi angemkatalia, fedha kwake ilionekana kuwa kila kitu, alifanikiwa kuwapata wanawake wengi kutokana na fedha ambazo alikuwa nazo.
    Ndevu zake zilikuwa zimejaa mvi lakini hilo wasichana hawakuonekana kujali kabisa, ukiachilia uzee huo, Bwana Stewart alikuwa na kitu cha ziada, kitu ambacho kilionekana kuwa kama ulimbo kwa wanawake wengi, fedha. Alilala na wanawake wengi kwa sababu tu alikuwa na fedha ambazo zilionekana kuwa njia ya mkato kupata kila alichokuwa akikitaka maishani mwake.
    Kwa Gloria, kwake hakuonekana kuwa mgumu kabisa, alikuwa na uhakika kwamba angeweza kulala na msichana huyo bila tatizo lolote lile. Hakujali urafiki ambao alikuwa nao na Bwana Mbwana ambaye alikuwa baba yake Kaposhoo, mpenzi wa Gloria kama alivyokuwa akijua, kitu ambacho alikuwa akikijali mahali hapo ni kulala na msichana huyo mrembo.
    Kitu cha kwanza, Bwana Stewart hakuonekana kuwa na haraka, alikuwa akimfuatilia Gloria taratibu huku akimgawia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kufanyia mambo yake binafsi, fedha ambazo kwake zilionekana kuwa kama marupurupu, fedha ambazo zingeweza kubadilisha kila kitu kwa Gloria.
    Alichokifanya Bwana Stewart ni kuwa karibu zaidi na Gloria, mara kwa mara alikuwa akimuita ndani ya ofisi yake na kisha kumuuliza kama alikuwa na tatizo lolote ambalo lilikuwa likihitaji fedha. Gloria hakuwa akijisikia aibu, kwa sababu Bwana Stewart alikuwa amejiingiza kichwa kichwa kifedha, Gloria akayaweka matatizo yake mezani, matatizo ambayo yalikuwa yakihitaji kiasi kikubwa cha fedha.
    Kwa Gloria kiasi ambacho alikuwa akikihitaji kilionekana kuwa kikubwa sana lakini kwa Bwana Stewart hicho hakikuonekana kuwa tatizo, akamgawia na Gloria kufanyia mambo yake. Kama alivyokuwa akitaka Bwana Stewart ndicho ambacho kilianza kutokea moyoni mwa Gloria, fedha zile zikaanza kumbadilisha.
    Kwa taratibu, moyo wake ukaanza kuhama, kama ulivyokuwa umehama kutoka kwa Peter na kuhamia kwa Kaposhoo basi nao hapo ukahama kutoka kwa Kaposhoo na kuhamia kwa mzee huyo ambaye alikuwa sawa na umri wa baba yake. Taratibu Bwana Stewart akaanza kumchezea mapaja Gloria kila alipokuwa akimuita ofisini mwake, kutokana na fedha ambazo alikuwa akipewa, kutokana na uangalizi mkubwa ambao alikuwa akipewa na mzee huyo, Gloria hakuonekana kuwa na ugumu wowote ule.
    Fedha zikaonekana kumchanganya Gloria, kila kitu ambacho alikuwa akikihitaji kukifanya mzee huyo alikuwa huru kukifanya mwilini mwake kwa kutumia mikono yake tu. Kwa mara ya pili, kwa kutumia fedha, Gloria akajikuta akianza kuvua sketi yake mbele ya mwanaume ambaye alionekana kumpa kiasi kikubwa cha fedha na kumkaribisha mwilini mwake.
    Bwana Stewart alionekana kuwa na uhakika, alijua fika kwamba jambo lile ilikuwa ni lazima kutokea, kwa mara ya kwanza akaanza kufanya mapenzi na Gloria ofisini kwake huku mlango ukiwa umefungwa na kiyoyozi kupuliza. Siku hiyo ilionekana kuwa ya furaha zaidi, mchezo ambao aliuonyesha Gloria pamoja na muonekano wa umbo lake alipokuwa mtupu vikamfanya Bwana Stewart kuchanganyikiwa kupita kawaida.
    Gloria akajirahisisha kwa mzee huyo ambaye kuanzia siku hiyo akaanza kupokea fedha zaidi huku akivua sketi yake zaidi na zaidi. Watu watatu kwa wakati mmoja walikuwa wakifanya mapenzi na msichana huyo, Gloria. Alipokuwa nyumbani hasa nyakati za usiku, alikuwa akifanya mapenzi na mchumba wake ambaye alikuwa akijulikana nyumbani, Peter lakini katika kipindi ambacho Peter alikuwa akielekea chuoni alikuwa akifanya mapenzi na Kaposhoo na huku akiwa kazini Bwana Stewart nae akawa anajilia vyake kama kawaida.
    Gloria akaonekana kuwa kahaba bila kujijua, kitendo cha kufanya mapenzi na watu watatu kiuhalisia kilionekana kumharibia saikolojia yake, kichwa chake kilikuwa kinafikiria zaidi fedha, hakutaka kusikia habari za mapenzi ya kweli, kitu ambacho alikuwa akikifikiria kilikuwa fedha tu.
    Katika kila mchezo ambao ulikuwa ukiendelea bado ulionekana kuwa siri. Gloria hakutaka Peter ajue kwamba alikuwa akitembea na Kaposhoo huku kwa upande mwingine hakuwa akitaka Kaposhoo ajue kama alikuwa akitembea na Bwana Stewart. Mapenzi yakaonekana kuwa na mzunguko, mzunguko mbaya ambao ulionyesha kwamba kama kungetokea na mtu mmoja kuathirika na ugonjwa wa UKIMWI basi wote wanne wangeweza kuathirika.
    “Unanipenda?” Bwana Stewart alimuuliza Gloria katika kipindi ambacho walikuwa wamelala mchana katika moja ya vyumba ndani ya hoteli hiyo.
    “Ninakupenda” Gloria alimwambia Bwana Stewart huku akimchezea chezea kitambi chake.
    “Hebu kwanza nibusu mdomoni” Bwana Stewart alimwambia Gloria ambaye bila tatizo lolote akambusu.
    “Hivi inakuwaje kama yule mpuuzi atakuja kujua?” Bwana Stewart alimuuliza Gloria.
    “Nani? Peter?”
    “Hapana. Yule mpenzi wako, Kaposhoo” 
    “Atajuaje?”
    “Si unajua mapenzi hayana siri. Anaweza kujua halafu akajidai kusababisha matatizo”
    “Mmmh! Sidhani kama atakuja kujua”
    “Au nifanye jambo moja la kushtukiza?”
    “Jambo gani?”
    “Kumuua ili tuishi kwa raha”
    “Kumuua tena? Kwani si hata hivi tutakuwa tukiishi kwa raha baby”
    “Hivi tutakuwa hatujiachii inavyotakiwa. Inapaswa tumpoteze mtu yule, au wewe unaonaje?”
    “Sidhani kama ni wazo zuri, ila fanya utakavyo mpenzi” Gloria alimwambia Bwana Stewart.
    Bwana Stewart akaonekana kuchanganyikiwa katika mapenzi ya Gloria, kila wakati alikuwa akitamani kuwa yeye peke yake, hakutaka msichana huyo atembee na mtu mwingine zaidi yake. Alitaka kujiachia na msichana huyo, alitamani sana kumtambulisha kwa matajiri wenzake kwani Gloria alionekana kuwa msichana mzuri ambaye kila mtu alikuwa akitaka kuwa nae.
    Tayari kaposhoo kwake akaonekana kuwa tatizo, alijua fika kwamba endapo mtu huyo angekuja kufahamu kwamba alikuwa akimchukua msichana wake basi angeweza kufanya itu chochote kile kutokana na yeye baba yake kuwa na fedha nyingi na za kutosha. Bwana Stewart alikuwa akitaka kujilinda hata kabla ya mambo hayajaweza kubadilika.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Moyoni hakuwa akijua kwamba mvulana halali wa Gloria alikuwa Peter, kijana ambaye muda mwingi alionekana kuwa mpole na mkimya sana. Kichwani mwake alijua fika kwamba mvulana halali wa Gloria alikuwa Kaposhoo na ndio maana katika kipindi hicho alikuwa akihakikisha kufanya kila liwezekanalo kuweza kumuua kijana huyo ili mradi awe na uhakika wa kuishi na msichana huyo kwa amani.
    “Nitamuua tu” Bwana Stewart alijisemea.
    Bwana Stewart hakutaka kuishia kwa maneno tu, alikuwa akitaka kufanya na vitendo pia. Kitu alichokifanya ni kuanza kuwasiliana na vijana wa kundi la Kunta Kinte ambalo lilikuwa likipatikana hapo Zambia kwa ajili ya kuifanya kazi yake hiyo. Kazi wala haikuonekana kuwa kubwa sana kutokana na kundi hilo kuwa na uwezo wa kufanya kila kazi waliopewa ndani ya siku moja tu.
    Bwana Stewart alikuwa akiliamini sana kundi hilo ambalo mara kwa mara alikuwa akilitumia katika kufanya mambo yake ya mauaji. Alichokifanya ni kuanza kuwasiliana na mkuu wa kundi hilo ambaye akamtaka kwenda kuonana nae katika kambi yao iliyokuwa mafichoni.
    Alichokifanya Bwana Stewart ni kuelezea sababu ambazo zilimpelekea kutaka kumuua kaposhoo. Hakukuwa na mtu ambaye alishangaa au kushtuka kutokana na watu wengi nchini Zambia kutaka watu fulani wauawe kisa wanawake au wanaume hali ambayo husababishwa na mapenzi.
    “Hilo si tatizo. Tunahitaji kwacha milioni kumi” Mkuu wa kundi hilo alimwambia.
    “Fedha si tatizo. Kuna kingine kinahitajika?”
    “Kama tusingekuwa tukimfahamu tungehitaji picha ila kwa sababu tunamfahamu, hakuna tatizo” Kiongozi wa kundi lile alimwambia Bwana Stewart.
    “Kama kazi itafanyika ndani ya leo au kesho itakuwa safi sana” Bwana Stewart aliwaambia.
    “Hakuna tatizo. Wewe unataka afe kifo cha aina gani?”
    “Kwani kuna kifo kingine zaidi ya kupigwa risasi?”
    “Yeah! Labda unataka achinjwe, amwagiwe tindikali, tumgeuze mwanamke mpaka anakufa, ajali na vifo vingine vingi. Wewe tu kuchagua” Mkuu yule alimwambia Bwana Stewart.
    “Ninachokihitaji ni huyu mtu afe. Hakuna kingine. Kifo chochote tu sawa. Nyie muueni tu” Bwana Stewart alimwambia kiongozi yule.
    “Basi hakuna tatizo. Mpaka kesho usiku kazi yako itakuwa imefanyika” Kiongozi yule alimwambia Bwana Stewart.
    Kila kitu ambacho kilikuwa kikitakiwa kufanyika kilikuwa kimekwishapangwa na ni Kaposhoo tu ndiye ambaye alihitajika kuuawa katika kipindi hicho. Bwana Stewart akaongozana na kijana mmoja mpaka benki ambapo akatoa kiasi cha fedha kilichokuwa kikihitajika kama malipo na kisha kumpa.
    Mpaka kufikia hatua hiyo tayari Bwana Stewart alionekana kuwa na uhuru, kundi lile la Kunta Kinte lilionekana kuwa kundi ambalo lilifanya kazi zake kwa umakini mkubwa sana na hivyo hakutakiwa kuwa na wasiwasi hata mara moja.
    Katika mipango yote ambayo alikuwa akiifanya, Bwana Stewart hakumwambia Gloria, alitaka kile kitu kifanyike kimya kimya kwa kuona kwamba endapo angemwambia Gloria basi msichana huyo angeweza kuingiwa na roho ya huruma ambayo ingemfanya kutokukamilisha jambo lake.


    Bwana Stewart bado alikuwa mkimya, alijua kabisa kwamba alifanya makosa kumwambia Gloria kwamba kitu ambacho alikuwa akikitaka ni kumuua Kaposhoo lakini katika kipindi hicho akaona bora liwe la kutokea lakini si kumuacha Kaposhoo aendelee kuwa ndani ya dunia hii na wakati yeye mwenyewe alikuwa akitaka kuendelea kutanua na msichana huyo ambaye mpaka katika kipindi hicho alionekana kuufanya ukahaba bila mwenyewe kufahamu. 
    Fedha zikaonekana kumlevya, fedha zikayapoteza mapenzi ambayo alikuwa nayo moyoni mwake, fedha ambazo kwake alionekana kama kuziabudu tayari zilikuwa zimebadilisha kila kitu katika maisha yake. Mapenzi hayakukoma, bado Bwana Stewart alikuwa akiendelea kutanua na Gloria kisiri. Chumba chao kilikuwa chumba namba mia na tano ndani ya hoteli ile, chumba ambacho kilionekana kama kuwa staff ndani ya hoteli hiyo.
    Wafanyakazi wote wakajua ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea lakini hakukuwa na mtu ambaye alithubutu kuufungua mdomo wake na kuongea kitu chochote kile kibaya. Katika kipindi hicho bado Bwana Stewart alikuwa akisikiliza mchogo ambao alikuwa ameupanga pamoja na wauaji wa kundi la Kunta Kinte. 
    Bwana Stewart alikuwa akisikilizia kujua ni kitu gani ambacho kingetokea katika kila kitu ambacho alikuwa amekipanga, hakutaka kuona Kaposhoo akiendelea kuishi na wakati moyoni mwake alikuwa na uhitaji wa kuendelea kuishi na Gloria ambaye alionekana kuwa radhi kwa kila kitu.
    Bwana Stewart hakujali kuhusiana na ukaribu ambao alikuwa nao na Bwana Mbwana, baba yake kaposhoo, kitu ambacho alikuwa akikitaka kwa wakati huo ni kuona kwamba anaendelea kuishi na Gloria tu. Mapenzi yakamteka, uzuri wa Gloria ukazidi kumchanganya kupita kawaida, hakuamini kama fedha ambazo alikuwa nazo zingeweza kumpa msichana mrembo kama Gloria.
    “Fedha ndio kila kitu” bwana Stewart alikuwa akimwambia tajiri mwenzake, Bwana Andrew katika kipindi ambacho walikuwa katika mkutano wa matajiri ndani ya ukumbi mkubwa ambao ulikuwa katika hoteli ya Paradise 5 huku lengo la mkutano huo likiwa ni kuisaidia nchi ya Zambia ambayo kwa kiasi fulani uchumi ulionekana kuyumba.
    “”Kuna jipya lililotokea?” Bwana Andrew alimuuliza huku akinyanyua kinywaji chake na kupiga fundo moja.
    “Unapokuwa na fedha unaweza kupata msichana yeyote mzuri” Bwana Stewart alimwambia.
    “Hilo naamini”
    “Na unaweza kumpata msichana mzuri zaidi ya wazuri katika dunia hii. Unaamini hilo” Bwana Stewart alimwambia na kuuliza.
    “Inategemea”
    “Inategemea na nini?”
    “Wakati mwingine hawa watoto wa kike wanapenda watu maarufu”
    “Hilo si tatizo. Kwanza unapokuwa na fedha, moja kwa moja unakuwa maarufu. Unakubaliana na mimi?” Bwana Stewart alimwambia Bwana Andrew na kumuuliza.
    “Kivipi?”
    “Tafuta fedha ili uwe maarufu. Na kama ikitokea umekuwa maarufu, basi fedha zitakufuata zenyewe” Bwana Stewart alimwambia.
    “Hapo kidogo nimekuelewa. Ila kuna kitu gani kipo nyuma ya haya yote unayoniambia?” Bwana Andrew alimuuliza.
    “Ngoja kikao kiishe tutaongea zaidi” Bwana Stewart alimwambia Bwana Andrew.
    Kikao kikaendelea zaidi, matajiri zaidi ya kumi na mbili wa nchini Zambia walikuwa wamekusanyika katika ukumbi wa hoteli hiyo. Muda wote Bwana Stewart alionekana kwa na furaha kupita kawaida, bado hali ya kuwa na Gloria ilikuwa ikimpa furaha kupita kawaida. Muda mwingi mahali hapo alikuwa akimfikiria msichana huyo, kwake, kikao kikaonekana kuwa kirefu mno, alitamani kimalizike haraka na kisha kumuona tena Gloria.
    Moyo wake ulikuwa umetawaliwa sana na Gloria, hakuambiwa kitu chochote kile, kwake, Gloria alikuwa namba moja moyoni mwake. Alijua fika kwamba alikuwa na mke pamoja na watoto lakini kwake hilo halikuweza kuonekana kuwa kizuizi cha yeye kuwa na msichana huyo. Mapenzi yake yakawa zaidi kwa Gloria kuliko kwa mke wake ambaye aliahidi kanisani kwamba angempenda kwa moyo mmoja.
    Kila kitu ambacho alikuwa amekiahidi kanisani juu ya mke wake siku ya harusi kikaonekana kusahaulika moyoni mwake, wanawake walionekana kuuyumbisha moyo wake kutoka kwa mke wake lakini ujio wa Gloria, ule moyo ambao ulikuwa ukiyumbishwa ukaanguka kabisa. Japokuwa mkutano ulikuwa ukichukua muda mchache sana huku waziri mkuu, Bwana Mbwani akiwepo ndani ya mkutano huo lakini kwa Bwana Stewart ulionekana kuchukua muda mrefu sana.
    Kila wakati alikuwa akijisikia kuwa karibu na Gloria, kila alipokuwa mbali na msichana huyo, moyo wake ulikuwa ukimwambia kwamba alikuwa akichukuliwa na mwanaume mwingine jambo ambalo lilikuwa likimuumiza sana moyoni mwake. Japokuwa mkutano ulikuwa ukiendelea, Bwana Stewart akashindwa kuvumilia, alichokifanya ni kuanza kuwasiliana na Gloria kwa kutumia meseji jambo ambalo lilimfanya kuwa bize na simu yake. Mkutano huo mfupi wala haukuwa mrefu sana, ukamalizika.
    “Vipi?” Bwana Andrew alimuuliza Bwana Stewart ambaye alimfuata huku akiwa na tabasamu kubwa usoni mwake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    “Angalia hiyo picha” Bwana Stewart alimwambia huku akimgawia simu ambayo alikuwa ameiweka picha ya Gloria.
    “Mmmmh!” Bwana Andrew alibaki akiguna tu mara baada ya kuiona picha ile.
    “Vipi?”
    “Nani huyu”
    “Ndio maana nilikwambia kwamba fedha ndio kila kitu, msichana yeyote mzuri unaweza kutembea nae” Bwana Stewart alimwambia Bwana Andrew ambaye alibaki akiwa ameduwaa huku akiiangalia picha ya Gloria.
    “Ila haujaniambia, nani huyu?”
    “Subiri kwanza. Unamuonaje?”
    “Kabla sijasema namuonaje, nani huyu”
    “Malaika wangu”
    “Umemtoa wapi?”
    “Kwani yupo vipi?”
    “Mzuri mno. Halafu anaonekana kama sio Mzambia”
    “Hahaha! Huyo msichana katoka mbali sana”
    “Wapi?”
    “Tanzania”
    “Kweli kuna wasichana wameumbika, huyu kapewa kila kitu, kuanzia sura mpaka umbo. Anakaa wapi?” Bwana Andrew alisema na kuuliza.
    “Usijali. Nilitaka kukudhihirishia kile nilichokwambia kabla” Bwana Stewart alimwambia huku akiichukua simu yake.
    Mipango bado ilikuwa ikiendelea kusukwa huku Kaposhoo akitakiwa kuuawa ndani ya siku mbili tu kwa ajili ya kuwapa uhuru Gloria na Bwana Stewart ambaye alitaka kuwa huru pamoja na Kaposhoo. Kila wakati alikuwa akisikilizia simu yake, muda mwingi alikuwa akitarajia kupokea simu kutoka kwa vijana wa kundi la Kunta Kinte ambao alikuwa amewapa kazi ya kumuua Kaposhoo tu.
    Masaa yaliendelea kukatika lakini hali bado ilikuwa kimya, hakupokea simu yoyte kutoka kwa vijana hao ambao tayari alikuwa amewalipa kiasi kikubwa cha fedha kwa kufanya kazi ile tu. Bwana Stewart alikuwa na presha kubwa, kila wakati alikuwa akiangalia saa yake kama mtu ambaye alikuwa akitaka kuwahi jambo fulani ambalo lilikuwa likitarajiwa kutokea mahali fulani. Saa nne usiku, simu yake ya mkononi ikaanza kuita, kwa haraka sana, akaichukua na kisha kuipeleka sikioni.
    “Vipi?” Bwana Stewart aliuliza mara baada ya kupokea simu ile na kugundua kwamba mpigaji alikuwa mmoja wa vijana wa kundi la Kunta Kinte.
    “Kila kitu tayari”
    “Unasemaje?”
    “Kazi imefanyika”
    “Mmemuua?”
    “Kama kawaida”
    “Asante Mungu! Mmemuua kwa kifo gani?”
    “Risasi tatu mwilini mwake. Kashatangulia kabla yetu” Sauti ya kijana yule ilisikika simuni.
    Bwana Stewart hakutaka kuendelea kuongea, katika kipindi hicho furaha ilikuwa imemshika kupita kawaida, alichokifanya huku akiendelea kuwa katika hali hiyo ni kuanza kumpigia simu Gloria kwa kuona kwamba Kaposhoo hakuwepo nyumbani. Mara baada ya kuona kwamba simu inaita, akaanza kusikilizia.
    Simu ile iliita zaidi na zaidi lakini wala haikupokelewa kabisa. Bwana Stewart hakuonekana kuwa na wasiwasi kwa kuamini kwamba simu ile ingepokelewa tu. Simu iliita, iliita na kuita lakini wala haikupokelewa hadi ikajikata. Bwana Stewart hakuonekana kukata tamaa, alichokifanya ni kuanza kupiga tena, alipiga zaidi na zaidi mpaka katika kipindi ambacho simu ile ikapokelewa.
    Tofauti na mategemeo yake, Gloria aliipokea simu ile huku akilia na sauti ya mwanaume ikisikika kwa mbali huku ikilalamika. Bwana Stewart akaonekana kushtuka, hakujua ni mwanaume gani ambaye alikuwa na Gloria katika usiku huo na wakati Kaposhoo alikuwa ameuawa kama alivyoambiwa simuni.
    “Hallow....!!” Sauti ya Gloria iliita huku akilia.
    “Kuna nini tena mpenzi? Huyo nani?” Yalikuwa ni maswali mawili yaliyotoka mfululizo mdomoni mwake.
    “Ni Peter”
    “Peter! Anafanya nini hapo usiku huu” Bwana Stewart aliuliza huku akionekana kushtuka.
    “Ame......” Gloria alijibu lakini hata kabla hajamalizia jibu lake, simu ikakatika.
    Bwana Stewart akaonekana kuchanganyikiwa, hakuelewa ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea. Kitendo cha Gloria kulia huku Peter akisikika akiropoka kilionekana kumchanganya kupita kawaida. Kitu ambacho alikuwa akikijua ni kwamba Gloria alikuwa msichana wa Kaposhoo na Peter alikuwa ni rafiki wa kawaida tu ambaye wala hakuwa akiishi katika nyumba hiyo, ilikuwaje katika usiku huo Peter alikuwa ndani ya nyuba hiyo? Kila alichokuwa akijiuliza akakosa jibu.
    “Hebu subiri” Bwana Kaposhoo alijisemea na kisha kuanza kupiga tena simu.
    Simu ikaanza kuita, iliita zaidi na zaidi mpaka ikakata. Bwana Stewart akaonekana kukasirika kupita kawaida, kichwa chake kikazidi kuchanganyikiwa zaidi juu ya kile kilichokuwa kikiendelea. Bwana Stewart hakuishia hapo, akarudia tena kuipiga simu ile lakini hali ikawa ile ile, simu haikupokelewa zaidi ya kukatwa.
    Hapo ndipo ambapo kichwa chake kilipoanza kuhisi kitu, akajua kabisa kwamba kulikuwa na kitu ambacho kiliendelea nyumbani hapo, alichokifanya ni kutoka nje na kisha kuchukua gari lake na kisha kuanza kuelekea Maluba, mtaa ambao Kaposhoo alipokuwa akiishi.
    Bwana Stewart akaliingiza gari lake katika barabara ya Chilimbulu na kisha kuanza kueleka upande wa Kaskazini Magharibi. Bwana Stewart alikuwa akiendesha gari huku akionekana kuchanganyikiwa. Katika usiku huo, hakukuwa na magari mengi barabarani kitu ambacho kilimfanya kuendesha kwa kasi.
    Hakuchukua muda mrefu, akawa amekwishafika katika Makumbusho ya Taifa ya Lusaka ambapo baada ya kuyavuka tu akachukua barabara ya Burma ambapo akaonganisha nayo mpaka kufika katika barabara ya Kanisa ambayo ilikuwa ikionganisha mpaka katika jengo la makao makuu ya Aitel nchini Zambia.
    Bwana Stewart hakutaka kwenda na barabara ile moja kwa moja kwani baada ya sekunde chache akaingia katika barabara nyingine ndogo ya Belt ambayo ilimpeleka moja kwa moja mpaka katika mtaa wa Maluba, mtaa ambao ulikuwa na nyumba nyingi zilizoonekana kuwa za kifahari. Aliendelea mbele zaidi na zaidi mpaka kufika katika eneo ambalo kulikuwa na nyumba aliyokuwa akiishi Kaposhoo, akateremka na kisha kuanza kulifuata geti ambapo kulikuwa na mlinzi nje.
    “Gloria nimemkuta?” Lilikuwa swali la kwanza ambalo aliliuliza Bwana Stewart kwa mlinzi ambaye alikuwa getini pale. Hata kabla mlinzi hajajibu swali lile, wote wakashtuka mara baada ya kumuona Gloria akitoka nje huku akikimbia, alikuwa akilia kwa sauti kubwa, miguuni hakuwa na viatu, walipoona hivyo, wote wakaanza kumfuata na kisha kumzuia.
    “Kuna nini?” Bwana Stewart alimuuliza Gloria huku kila mmoja akionekana kushangaa.
    “Anataka kuniua”
    “Nani?”
    “Peter”
    “Anataka kukuua! Kwa nini?”
    “Huyo hapo anakuja” Gloria alisema huku akilia.
    Peter akatokea mahali hapo, alionekana kuwa na hasira kupita kawaida, mkononi mwake alikuwa ameshika kisu hali ambayo ilionekana kumshtua kila mmoja. Peter hakuonekana kuwa katika hali ya kawaida hata mara moja, alionekana kuwa radhi kumuua Gloria kwa kumchoma kisu kile, hakuona kama msichana huyo alistahili kuwa hai katika kipindi hicho.
    “Kuna nini?” Bwana Stewart alimuuliza Peter ambaye alionekana kuwa na hasira huku akiwa hatua kumi kutoka kwake aliposimama na Gloria.
    “Nataka kumuua huyo malaya” Peter alijibu na kisha kuanza kumsogelea Gloria huku akionekana kuwa na hasira kupita kawaida, hasira ambazo ziliwaonyeshea kwamba endapo wasingemzuia basi angeweza kumchoma Gloria na kisu kile.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Je nini kitaendelea?
    Je Peter ataweza kumuua Gloria?
    Je Kaposhoo ameuawa kama taarifa ilivyotolewa?
    Je kwa nini Peter anataka kumuua Gloria?
    Je amegundua kilichotokea au?
    Kama umeipenda kutoka moyoni, dondoshea LIKE yako moja ya ukweli.


    ITAENDELEA


0 comments:

Post a Comment

Blog