Simulizi: Uliniua Gloria
Sehemu Ya Pili (2)
Kaposhoo na Peter walikuwa wakitoka katika matembezi yao huku wakiwa ndani ya gari. Katika kipindi hicho, bado unafiki ulikuwa ukiendelea kama kawaida. Kaposhoo hakutaka kabisa kuonyesha tofauti zozote kwa Peter, alikuwa akimuonyeshea mapenzi ya ukweli kama rafiki yake kumbe nyuma ya pazia alikuwa akiendelea na mchezo wake wa usaliti kwa mpenzi wake, Gloria.
Peter hakuonekana kuelewa kitu chochote kile, kwake, Kaposhoo bado alionekana kuwa rafiki wa kweli ambaye alitakiwa kuaminika kwa kila mtu. Alionekana kuwa rafiki wa kweli ambaye alionekana kumthamini kupita kawaida. Msaada wa kifedha ambao alikuwa akiutoa katika maisha yake ukaonekana kuwa mkubwa na wala hakumfikiria vibaya.
Fedha za Kaposhoo nazo zikamtia upofu kwa kuona kwamba mtu huyo aliendelea kuwa mwema kwake na hivyo hakutakiwa kuhofia kitu chochote kile. Fedha zikatengeneza uaminifu mkubwa moyoni mwake juu ya Kaposhoo ambaye aliendelea kutembea na mpenzi wake kama kawaida.
“Maisha ni mazuri sana kama utapata kila kitu unachokihitaji” Kaposhoo alimwambia Peter mara baada ya ukimya wa muda mrefu.
“Huo ni ukweli kabisa. Wakati mwingine tunatakiwa kutafuta fedha ili mradi tupate kila kitu katika maisha yetu” Peter alimwambia Kaposhoo.
“Ulikwishawahi kufikiri kwamba kuna siku unaweza kuja kuwa tajiri sana hapa duniani?” Kaposhoo alimuuliza Peter.
“Huwa ninafikiri sana juu ya hilo”
“Na umekwishawahi kuamini?”
“Sidhani ila nadhani ninavyoyaangaikia maisha ni imani tosha”
“Hapana Peter. Kila kitu kinachotokea duniani kinafanyika kwa imani kubwa sana. Unatembea kwa sababu una imani, unakula kwa sababu una imani, yaani unafanya kila kitu kwa sababu ya imani, na hata kuwa tajiri unatakiwa kuwa na imani pia kwamba unaweza kuwa tajiri” Kaposhoo alimwambia Peter ambaye alibaki akimsikiliza.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kiasi fulani sijakuelewa”
“Wapi ambapo nimekuacha?”
“Hapo unaposema kwamba kila tunachofanya tunafanya kwa imani”
“Mbona ipo wazi sana Peter! Usikifanye kichwa chako kufikiria sana na wakati kila kitu kipo wazi kabisa” Kaposhoo alimwambia Peter.
“Kivipi? Hebu jaribu kunifafanulia”
“Ishu ni kwamba hata unapopiga hatua huwa unakuwa na imani”
“Kivipi?”
“Unapoanza kupiga hatua unaamini kwamba utaweza kuunyanyua mguu wako na kukanyaga sehemu fulani salama. Na unapoamini, unafanya, unapounyanyua, kweli unakanya ardhini, unakuta kweli ni salama, hiyo imetokana na imani yako ambayo ilikupelekea kuona kwamba pale utakapopakanyaga ni salama. Umenipata?” Kaposhoo alimwambia peter na kisha kumuuliza.
“Kidogo” Peter alijibu.
“Hautakiwi kunipata kidogo Peter. Wakati mwingine unapounyanyua mguu na kuamini kwamba unapokanyaga ni salama, kweli unaamini, unapoupeleka mguu unakutana na kishimo, bila kutegemea mguu wako unaingia kwenye kishimo. Hapo imani yako imeyumba, umeamini kitu ambacho hakikuwa kama ulivyoamini. Baada ya kukutana na kishimo usichokiona kutokana na giza, unaanguka na pia unaweza kuvunjika mguu. Kila kitu tunachokifanya tunafanya kwa imani Peter. Na hapo vipi, umenielewa?” Kaposhoo alimwambia Peter huku akiendelea kuendesha gari.
“Labda asilimia themanini”
“Okey! Tufanye niongeze mpaka ifike mia moja. Hapa tunaelekea nyumbani, ninaendesha gari kwa sababu ninaamini kwamba ninaweza kuendesha gari na kutufikisha salama. Kila kitu kinachotokea katika maisha yetu tunakifanya kwa imani na tunafanikiwa Peter” Kaposhoo alimwambia Peter.
“Umeniambia mengi sana. Lengo ni nini?”
“Lengo ni kukwambia kwamba unapoamini kwa moyo mmoja kwamba utakuwa tajiri, imani yako itafanya kazi na kweli utakuwa tajiri” Kaposhoo alimwambia Peter.
“Naelewa, ila.....”
“Najua unachotaka kukisema. Imani bila matendo imekufa. Si ndio”
“Haswaaaa”
“Kuwa na imani na kisha ifanyie kazi. Nakumbuka zamani tulikuwa masikini tu, baba akaamini kwamba angekuwa tajiri, akafanya kazi kwa bidii usiku na mchana, imani yake ikafanya kazi, akawa tajiri. Hata sisi wanafunzi inatupasa kuwa na imani pia. Hatutakiwi kusema kwamba tutafeli, hapana, inatupasa tuwe na imani ya kuamini kwamba tutafaulu bila wasiwasi, ila pamoja na imani hiyo inatupasa tufanye matendo, yaani tusome na Mungu ataifanya imani yetu ifanye kazi” Kaposhoo alimwambia Peter.
“Wewe mtu kichwa sana” Peter alimwambia Kaposhoo huku akicheka.
“Hapana. Kuna watu vichwa zaidi katika dunia hii. Mungu amenipa uwezo mdogo sana kujua mengi kuhusu maisha. Una ratiba gani kesho?” Kaposhoo alimwambia Peter na kisha kumuuliza.
“Nadhani nitashinda chuoni mpaka jioni”
“Safi sana” Kaposhoo alimwambia Peter.
“Safi?”
“Yeah! Yakupasa kusoma sana Peter” Kaposhoo alimwambia Peter.
Bado walikuwa wakiongea maneno mengi kwa wakati huo, kila kitu ambacho alikuwa akiongea Kaposhoo kwa Peter kikaonekana kuwa kitu kigeni sana, Kaposhoo akaonekana kuwa na akili ya ziada kichwani kwake. Kwa Peter, baadhi ya maneno yakaonekana kuwa mapya kabisa kichwani mwake, maneno ambayo yalimfanya kumuona Kaposhoo kuwa na kitu cha ziada kichwani mwake.
Uaminifu wake juu ya Kaposhoo ulikuwa ukiendelea kama kawaida, alimuamini kupita kawaida na hakujua kwamba katika upande mwingine Kaposhoo alikuwa mtu mbaya sana ambaye alikuwa akitembea na mpenzi wake, Gloria.
Safari yao ya kurudi nyumbani ilikuwa ikiendelea zaidi na zaidi mpaka pale walipoingia katika barabara ya Makishi iliyokuwa karibu na mtaa wa Chilulu na kisha kusonga mbele huku lengo lao likiwa ni kuingia katika mtaa wa Maluba walipokuwa wakiishi. Katika kipindi ambacho waliingia katika barabara ya Luzi, kilometa tatu kabla ya kuingia Maluba, ghafla gari moja aina ya Range Rover ambayo ilikuwa katika mwendo wa kasi ikawapita na kisha kusimama mbele yao.
Kaposhoo akafunga breki za kushtukiza na kuligusa kidogo gari lile. Kila mmoja akaoneana kuchanganyikiwa, hawakujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kimesababisha dereva wa gari lile kulisimamisha kwa ghafla sana mbele yao. Huku kila mmoja akijiuliza, mara ghafla viaja wanne waliokuwa na vinyago nyusoni mwao wakateremka garini mule na kisha kuanza kulifuata gari lao huku mikononi wakiwa na bunduki.
Kila mmoja akaonekana kuhofia kupita kawaida, tayari waliona kwamba katika kipindi hicho wangekwenda kuuawa na watu hao ambao walionekana kuwa watu wabaya wasiokuwa na huruma hata kidogo. Walichokifanya ni kuvifunga vioo vya gari lile lakini watu wale walipolifikia wakavipiga vioo vile kwa bunduki zao na kuvipasua.
Wakatoa loki za milango na kisha kuingia ndani. Mionekano yao haikuwa ya kawaida, bado walikuwa wakionekana kuwa watu wabaya ambao hawakuwa hata na chembe ya huruma. Peter na Kaposhoo wakabaki wakiwaangalia kwa wasiwasi mno, tayari waliona kama muda wowote kuanzia kipindi kile wangeweza kuuawa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mnahitaji nini tuwape?” Lilikuwa swali la kwanza alilouliza Kaposhoo huku akionekana kuwa na wasiwasi, midomo ya bunduki ile ilionekana kumtisha.
“Tunahitaji roho yako” Mwanaume mmoja alisema kwa sauti iliyokuwa na mikwaruzo mingi.
“Nimefanya nini jamani?” Kaposhoo aliuliza huku akianza kulia.
“Jibu ni jepesi sana. Unatembea na msichana wa bosi wetu” Mwanaume yule alimwambia huku vijana wengine wakiwa wamesimama wakisubiri amri.
“Hapana. Nimeachana na wasichana. Sitembei na msichana yeyote yule” Kaposhoo alijibu huku akionekana kuogopa kupita kawaida.
Mpaka katika kipindi hicho Peter alikuwa kimya akitetemeka, tayari alikwishaona kwamba endapo angeongea kitu chochote kile angeweza kupigwa risasi, alibaki kimya huku akionekana kuwa mpole kupita kawaida.
“Sikiliza broo, ukweli ni kwamba sitembei na msichana yeyote wa bosi wenu, nishaachana na mambo ya wanawake” Kaposhoo alisema huku akionekana kuwa mpole.
Sikiliza, sisi kabla ya kuua huwa tuna utamaduni wa kukwambia kosa lako ili hata ukifika kwa Mungu ujue uliuawa kwa kosa gani. Kosa lako ni kutembea na msichana wa bosi wetu” Mwanaume yule alimwambia Kaposhoo.
“Bosi gani?”
“Hutakiwi kumjua”
“Hapana. Sijatembea na msichana yeyote”
“Sawa. Utaongea mbele ya safari”
“Naombeniiiiiii, naombeni mnisamehe jamani”
“Si umesema haujatembea na msichana wa bosi wetu, twende, utatuambia ukweli tu”
“Kweli sijatembea na msichana yeyote”
“Unamjua Gloria Michael, msichana kutoka nchini Tanzania? Umekuwa ukitembea nae kisiri, bosi kakasirika na sasa tunakwenda kukua ili aendelee kuwa na amani moyoni mwake na kwenye mahusiano yao” Mwanaume yule alimwambia Kaposhoo.
Peter akaonekana kushtuka, alipolisikia jina la Gloria akauhisi moyo wake ukipigwa ganzi kupita kawaida. Akabaki akimwangalia Kaposhoo ambaye alionekana kuwa na wasiwasi mwingi, Kaposhoo akayapeleka macho yake usoni mwa Peter, alionekana kuwa mtu mwenye aibu nyingi. Walichokifanya vijana wale ni kumtoa Kaposhoo ndani ya gari lile na kisha kumpeleka ndani ya gari lao na kuondoka nae mahali hapo.
Peter akabaki akiwa amechanganyikiwa, hakuamini kile ambacho alikuwa amekisikia kutoka kwa watu wale. Hakuamini kwamba mtu ambaye alikuwa akimuamini, Kaposhoo alikuwa akitembea na mchumba wake. Hapo hapo Peter akajikuta akijipiga pajani kwa hasira. Ukiachana na Kaposhoo, Gloria alikuwa akitembea na mwanaume mwingine ambaye alitambulishwa kama bosi masikioni mwa Kaposhoo.
Peter akachanganyikiwa zaidi, hakuamini kama kumleta Gloria ndani ya nchi ya Zambia kungeweza kusababisha yale yote, alichokifanya ni kuhamia katika kiti cha dereva na kisha kuliondoa gari mahali hapo. Peter alionekana kuwa na hasira, bado kichwa chake hakikuwa kikiamini kile ambacho alikisikia kwa vijana wale, alionekana kuwa na hasira kupita kawaida, mpaka kufikia hatua hiyo, tayari alimuona Gloria kuwa msaliti, alikuwa amemvisha pete kidoleni mbele ya wazazi wao lakini msichana huyo hakuonekana kuuona umuhimu wa pete ile hali ambayo ilimpelekea kumsaliti kwa wanaume wawili, wa kwanza alikuwa Kaposhoo na wa pili alikuwa mtu ambaye alitambulishwa kama bosi.
“Nitakuua” Peter alisema kwa hasira huku akiendesha garil kuelekea nyumbani..
Peter akasimamisha gari baada ya dakika kumi, akawa amekwishafika nje ya geti la nyumba kubwa ambayo alikuwa akiishi pamoja na Kaposhoo. Akaufungua mlango na kuteremka, hakutaka hata kuliingiza gari ndani kwani aliona kama angechelewa vile. Akalisogelea geti na kisha kuanza kuligonga kifujo fujo. Kwa wakati huo hasira zake zilikuwa juu ya Gloria tu, kichwa chake kilikuwa kikifikiria kitu kimoja tu, kumuua kutokana na kile ambacho alikuwa amekifanya.
Peter hakutegemea kusalitiwa maishani mwake, alimuanmini sana Gloria na kumuona kwamba alikuwa msichana maalumu aliyeletwa katika maisha yake kwa ajili ya kumfariji na kumletea furaha maishani mwake. Kila kitu ambacho alikuwa akikifikiria katika kipindi hicho kilionekana kuwa kinyume, mtu ambaye alikuwa amemuamini na kumpa kila kitu katika maisha yake alikuwa ameamua kumsaliti.
Moyo wa Peter ulikuwa katika maumivu makali mno, maumivu ambayo wala hakuyatarajia hata mara moja. Kichwa chake kikaanza kukumbuka mambo mengi ambayo alifanya akiwa pamoja na Gloria, mambo yote ambayo alikuwa akiyakumbuka katika kipindi hicho yalikuwa yakimuumiza kupita kawaida.
Baada ya sekunde chache, geti likafunguliwa na kisha Peter kuingia ndani huku akimwambia mlinzi aliingize gari lile. Kadri Peter alivyokuwa akipiga hatua kuufuata mlango wa kuingilia sebuleni na ndivyo ambavyo hasira zilivyozidi kumkamata, alipoufikia, akaufungua na kisha kuingia ndani.
Macho yake yalipotua usoni mwa Gloria ambaye alikuwa amekaa kochini, ghafla moyo wa Peter ukaanza kubadilika, zile hasira ambazo alikuwa nazo moyoni zikaonekana kuyeyuka.
Tabasamu la Gloria ambalo alikuwa amelitoa usoni mwake likaonekana kumbadilisha Peter, Gloria akainuka na kisha kuanza kumfuata Peter, alipomfikia, akampiga busu zito shavuni na kumkumbatia. Matendo hayo yakaonekana kumbadilisha kabisa Peter kwa kuona kwamba inawezekana ule ulikuwa ni mchezo ambao ulikuwa umefanywa, mchezo ambao ulikuwa na nia ya kumuachanisha na Gloria, mchumba wake ambaye alitarajia kumuoa. TABASAMU, KUMBATIO NA BUSU YAKABADILISHA KILA KITU KATIKA KIPINDI HICHO. HASIRA ZOTE ALIZOKUWA NAZO MOYONI MWAKE, ZIKAPOTEA.
Peter akaonekana kuridhika kabisa, yale mawazo ya kufikiria kuhusu Gloria kumsaliti yakawa yamepotea kichwani mwake. Moyo wake ukaanza kufikiria kitu kingine kabisa, aliamini kwamba kila kilichokuwa kimetokea kilionekana kuwa kama mchezo fulani ambao ulikuwa na lengo la kumgombanisha na Gloria, mchumba wake ambaye alikuwa akimpenda sana.
Bado waliendelea kukumbatiana huku wakipeana mabusu mfululizo. Peter akaonekana kuridhika kupita kawaida. Pamoja na kuridhika huko bado kichwa chake kilikuwa na mawazo lukuki kuhusiana na Kaposhoo. Alichokuwa akijiuliza kichwani pale ni kuhusu vijana wale ambao walikuwa wamemteka Kaposhoo, hakujua kama ule ulikuwa mchezo ambao ulikuwa umepangwa au kilikuwa ni kitu cha kweli.
Peter akajitoa kifuani mwa Gloria na kisha kuanza kuelelea chumbani, alipofika, akakifuata kitanda na kisha kujilaza. Wala hakukaa sana Gloria akatokea chumbani hapo, alichokifanya ni kuanza kumsogelea Peter kitandani pale na kisha kumlalia kifuani. Peter akaonekana kuwa katika hali ya mawazo ambayo ilionekana kumchanganya Gloria.
“Kuna nini?” Gloria aliuliza huku akionekana kushangaa.
“Yaani sielewielewi kabisa” Peter alimwambia Gloria.
“Jambo gani limekuchanganya?”
“Nilikuwa na Kaposhoo kwenye gari” Peter alijibu.
“Kwanza Kaposhoo mwenyewe yupo wapi? Mbona umerudi peke yako?” Gloria alimuuliza Peter.
“Kuna watu walivamia gari letu na kisha kumteka” Peter akatoa jibu ambalo lilimfanya Gloria kushtuka, akakitoa kichwa chake kifuani mwa Peter.
“Umesemaje?”
“Hao watu walimteka. Walitufuata na bunduki. Walichokisema ni kwamba wanakwenda kumuua” Peter alimwambia Gloria ambaye akaonekana kuanza kuchanganyikiwa.
“Peter....!”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Achana nao. Najua huu ni mchezo wa kutaka kunitenganisha nawe” Peter alimwambia Gloria.
“Hapana Peter, Kaposhoo yupo kwenye hatari kubwa, huo si mchezo Peter, huo ndio ukweli. Kuna watu nilisikia walitaka kumteka Kaposhoo” Gloria alimwambia Peter ambaye akainuka kitandani na kukaa.
“Umesikia wapi?”
“Nilisikia kwa juu juu tu”
“Wapi?”
“Sikumbuki ni wapi, ila nilisikia hivyo” Gloria akatoa jibu ambalo likaanza kuubadilisha moyo wa Peter.
“Kwa hiyo hii si utani hata kidogo?” Peter aliuliza.
“Peter, wataarifu polisi, huu si utani. Wataarifu polisi Peter, Kaposhoo atauawa” Gloria alimwambia Peter.
Moyo wa Peter ukazidi kubadilika, tayari akili yake ilikwishamwambia kwamba kulikuwa na kitu ambacho kiliendelea nyumba ya pazia. Huyu Gloria alionekana kufahamu mambo mengi sana, hapo ndipo maneno ya mwanaume yule aliyoyaongea ndani ya gari yalipoanza kujirudia kichwani mwake, kama Gloria alimwambia kwamba ule haukuwa utani, basi kulikuwa na asilimia mia moja kwamba maneno aliyoyaongea mwanaume yule hayakuwa na utani.
“Kwa hiyo ni kweli wanakwenda kumuua?” Peter aliuliza huku akijifanya kushangaa.
“Ni kweli. Wanakwenda kumuua. Peter wataarifu polisi” Gloria alimwambia Peter.
“Kwa hiyo kila kitu walichokisema ndani ya gari kilikuwa ni kweli?”
“Ndio Peter, kama wamesema wanakwenda kumuua ni kweli. Peter waambie polisi” Gloria alimwambia Petr huku machozi yakianza kumtoka.
Peter aabaki akiwa ameduwaa, tayari akili yake ilikwiishawambia kwamba Gloria alikuwa akitembea na Kaposhoo na ndio maana katika kipindi hicho alionekana kuchanganyikiwa zaidi. Peter ndiye alikuwa karibu sana na Kaposhoo, yeye ndiye ambaye alionana nae kwa mara ya kwanza kabla ya Gloria, kulikuwa na sababu gani ambayo ilimfanya Gloria kuwa na uchungu mkubwa zaidi yake? Kila alipokuwa akijiuliza hilo, akaonekana kugundua kwamba msichana wake alikuwa akimsaliti.
“Gloria” Peter aliita huku akionekana kubadilika.
“Abee”
“Kwa nini umekuwa ukinisaliti kwa Kaposhoo?” Peter alimuuliza Gloria ambaye alionekana kukaa kimya.
“Kukusaliti?”
“Usijifanye haujasikia Swali. Naomba unijibu, kwa nini umekuwa ukinisaliti kwa Kaposhoo?” Peter aliuliza swali kwa mara ya pili.
Kadri muda ulivyokuwa ukizidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo Peter alivyoonekana kuwa na hasira, tayari akili yake ilimwambia kwamba kwa asilimia mia moja Gloria alikuwa akimsaliti kwa Kaposhoo. Gloria hakujibu kitu, alibaki kimya kwa muda huku akiangalia chini kwa aibu. Hali ambayo aliionyesha Gloria mahali pale ndio ambayo ilionekana kumkasirisha sana Peter, alichokifanya ni kumshika Gloria mkono na kisha kumuinua kichwa chake.
“Kwa nini unanisaliti?” Lilikuwa swali jingine ambalo liliulizwa kwa sauti ya juu iliyokuwa na hasira kupita kawaida.
Peter akabadilika, Gloria akaonekana kuogopa kupita kawaida. Kwa muonekano ambao alikuwa nao Peter katika kipindi hicho alionekana kuwa tofauti, alionekana kuwa katika hasira kali ambazo Gloria hakuwahi kumuona akiwa katika hali hiyo. Gloria akazidi kutokwa na machozi, Peter alionekana kufahamu kila kitu.
“Niambie...nimekwambia niambie, kwa nini umenisaliti Gloria?” Peter aliendelea kuuliza kwa sauti ya juu yenye hasira.
“Naomba unisamehe” Gloria alimwambia Peter ambaye akamuachia mkono na kisha kusimamama.
Peter akaonekana kuchanganyikiwa, akaanza kutembea chumbani pale, mwili wake ulikuwa ukimtetemeka kupita kawaida. Kichwa chake kikaanza kufikiria mambo mengi ambayo yalitokea katika kipindi cha nyuma, akaanza kufikiria toka kipindi ambacho alikuwa mtoto pamoja na Gloria, katika kipindi ambacho walisoma pamoja na kufanya mambo mengine mengi.
Peter akaonekana kuumia kupita kawaida, hakuamini kama kweli yule msichana ambaye alitumia muda mwingi sana kuwa nae leo hii ndio alikuwa ameamua kumsaliti. Peter akayarudisha macho yake kwa Gloria, kila alivyokuwa akiiangalia pete ya uchumba ambayo alikuwa ameivaa Gloria ikaonekana kumuumiza kupita kawaida.
Kila kitu ambacho alikuwa akikifikiria mahali hapo kilionekana kumuumiza. Kila kitu ambacho alikuwa amekifanya maishani mwake kikaonekana kuwa si kitu kabisa, kumvalisha pete, kujulikana kwa wazazi wake pamoja na vitu vingine vikaonekana kuwa si kitu kwa Gloria, vitu hivyo vyote havikuonekana kuwa na nguvu ya kuachana kumsaliti kwa mwanaume aliyekuwa na fedha.
“Yaani pamoja na mambo yote haya, yaani mambo yote haya Gloria umenisaliti! Yaani pamoja na kukuvarisha pete na kukupa ahadi nyingi haya ndio malipo yake?” Peter aliuliza huku akionekana kuchanganyikiwa.
Peter aliendelea kubadilika, alikuwa na hasira kali kupita kawaida. Akaanza kuongea maneno mengi kwa sauti ya juu, katika kipindi chote hicho Gloria alikuwa akilia tu. Katika kipindi hicho, majuto yakaanza kuonekana moyoni mwake, akaonekana kujuta kwa kila kitu ambacho alikuwa amekifanya, aliumizwa na hali ambayo alikuwa nayo Peter katika kipindi hicho.
“Umenisaliti...umenisaliti Gloria” Peter alimwambia Gloria.
“Naomba unisamehe” Gloria alimwambia Peter huku akipiga magoti na kulia kwa uchungu.
“Tena umenisaliti kwa wanaume wawili. Hivi kitu gani sikukupa wewe mwanamke, yaani hizi fedha ndizo zimekuchanganya? Yaani hii nyumba ndio imekuchanganya, hebu niambie, ulihitaji nini ambacho sikukupa?” Peter aliuliza huku akionekana kuwa na hasira sana.
“Naomba unisamehe mpenzi”
“Nikusamehe! Hivi nikikusamehe utanirudishia furaha yangu? Hivi nikikusamehe utaurudisha moyo wangu kuwa katika hali ya kawaida. Gloria...Gloria ulihitaji nini sikukupa? Hebu niambie, ulihitaji nini sikukupa. Umevuliwa sketi zako kwa ajili ya fedha, umevuliwa sketi yako kwa ajili ya mali....ulitaka nini sikukupa wewe malaya?” Peter aliuliza kwa hasira.
Gloria alitambua fika kwamba Peter alikuwa kwenye hasira kali mpaka kumuita jina la ‘malaya’ ambalo kamwe hakuwahi kulisikia kutoka mdomoni mwake. Tayari mambo yalionekana kuharibika, tayari kila kitu kikaonekana kuwa katika hali ya ugomvi mahali hapo.
“Niambie wewe malaya. Nataka uniambie huyo bosi ni nani, niambie huyo bosi anayetaka kumuua Kaposhoo kwa ajili yako ni nani” Peter alimwambia Gloria ambaye alikaa kimya.
Tayari jina la ‘Bwana Stewart’ likaanza kuja kichwani mwake, tayari aliona kwamba Bwana Stewart ndiye alikuwa nyuma ya kila kitu. Gloria hakujibu chochote kile, alijua fika kwamba Peter alikuwa na hasira kali katika kipindi hicho, endapo angejibu kitu chochote kile basi angeweza kumpandisha hasira zaidi..
“Peter....!”
“Niambie huyo bosi ni nani....niambie kabla sijakuua wewe malaya” Peter alimwambia Gloria huku akianza kuondoka chumbani hapo.
Bado Peter alionekana kuwa na hasira kupita kawaida, japokuwa alikuwa ameondoka chumbani hapo lakini bado alikuwa akiongea kwa hasira sana. Huku Gloria akiwa pale chumbani kitandani, mara simu yake ikaanza kuita, alipoichukua na kuangalia jina, akakutana na jina la Stewart. Gloria hakuipokea simu ile, akaitupa pembeni huku ikiendelea kuita mpaka kukata.
Gloria alibaki akilia tu, hakuamini kama mchezo mzima ambao alikuwa ameucheza Peter alikuwa ameufahamu. Kichwa chake kikaanza kuwafikiria wazazi wake, alijua fika kwamba ilikuwa ni lazima Peter kuwaambia wazazi wake kile kilichokuwa kimetokea nchini Zambia. Huku akiendelea kujiuliza, mara simu yake ikaanza kuita tena, alichokifanya ni kuipokea huku Peter akisikika kuongea kwa hasira san tena kwa sauti ya juu.
“Hallow....!!” Gloria iliita huku akilia.
“Kuna nini tena mpenzi? Huyo nani?” Yalikuwa ni maswali mawili yaliyotoka simuni kutoka kwa Bwana Stewart.
“Ni Peter”
“Peter! Anafanya nini hapo usiku huu” Bwana Stewart aliuliza huku akionekana kushtuka.
“Ame......” Gloria alijibu lakini hata kabla hakjamalizia jibu lake, Peter akarudi mahali hapo huku akiwa ameshika nondo mkononi mwake.
“Niambie wewe malaya. Leo nataka uniambie, huyo bosi ni nani” Peter alimwambia Gloria.
Gloria akaonekana kuwa mgumu kujibu swali la Peter, alichikuwa akikisema ni kuomba msamaha mahali hapo. Peter hakuonekana kumuelewa hata mara moja, tayari alionekana kuwa na hasira kupita kawaida. Mwili wake ulikuwa ukimtetemeka tu, kitendo ambacho alikifanya Gloria kilionekana kuumiza moyo wake.
Mapenzi yalimuumiza sana, wivu ulikuwa umeuchimba moyo wake, shimo la wivu kukawa kumeingia hasira, hasira kali ambazo zilimfanya kumuona Gloria kama mtu ambaye alistahili kuuawa kwa mkono wake mwenyewe. Peter aliendelea kuuliza, kitu ambacho alikuwa akikihitaji mahali hapo ni kumfahamu huyo mtu aliyetajwa kama bosi.
Gloria hakuonekana kuwa tayari kulijibu swali lile, Peter alitumia dakika saba nzima kuuliza swali lile lakini bado Gloria aliendelea kuwa kimya, badala yake ndio kwanza akawa anaomba msamaha. Peter akatamani kumpiga na nondo ile lakini akaamua kuahirisha, aliona kwamba endapo angempiga na nondo ile asingeweza kumuua, alichokifikiria mahali hapo ni kutaka kumchoma kisu, alijua kama angemchoma na kisu, hata mara moja tu Gloria angeweza kufa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Peter akachomoka chumbani hapo, kichwa chake kilikuwa kikiwaza kisu tu. Gloria hakuondoka, bado alikuwa akiendelea kulia huku akiwa amepiga magoti pale chini. Siku hiyo, Peter alionekana kuwa kama mbogo, hakuonekana kuwa na chembe ya huruma. Kijana ambaye alijulikana kwa upole leo hii alionekana kuwa na hasira kupita kawaida.
Gloria aliendelea kubaki chumbani pale, wazo moja likamjia kichwani mwake, alijua fika kwamba Peter alikuwa ameondoka chumbani pale kufuata silaha nyingine hivyo kama angeendelea kubaki chumbani pale basi angeweza kurudi na kisha kumuua, alichokifanya ni kuinuka na kuanza kukimbia.
Alipofika sebuleni ndicho kilikuwa kipindi ambacho Peter alikuwa akitoka jikoni huku akiwa na kisu mkononi, alipomuona Gloria akikimbia kuelekea nje huku akiwa pekupeku, nae akaanza kutoka nje huku kisu kikiwa mkononi. Peter aliendelea kumkimbiza, alipofika nje, bosi wa hoteli za Paradise ambapo alikuwa akifanya kazi Gloria akatokea na kisha Gloria kumfuata na kisha kumuomba kumsaidia.
“Kuna nini Peter?” Bwana Stewart aliuliza huku akionekana kushangaa Peter ambaye alikuwa na kisu mkononi.
“Nataka kumuua huyo malaya” peter alijibu huku akionekana kuwa na hasira, akaanza kumsogelea Gloria huku kisu kikiwa mkononi mwake.
Gari lilikuwa likiendeshwa kwa mwendo wa kasi kuelekea Maipompo, upande wa mashariki mwa jiji la Lusaka. Katika kipindi chote hicho, ndani ya gari hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akiongea kitu chochote kile, wote walikuwa kimya. Kaposhoo, mtu ambaye alikuwa amechukuliwa mateka kwa wakati huo hata yeye nae alikuwa kimya kabisa huku akionekana kuwa katika lindi la mawazo.
Mpaka muda huo, kichwa chake kikaanza kujiuliza maswali mengi kuhusiana na watu ambao walikuwa wamemtuma kwa ajili ya kumteka na kisha kuwapa amri ya kumuua. Katika kipindi hicho kila kitu ambacho alikuwa akijiuliza hakuwa na jibu lolote lile, alikuwa akiendelea kujiuliza bila mafanikio yoyote yale.
Kila kitu kikaonekana kuharibika, tayari siri ambayo alikuwa nayo kwa muda mrefu juu ya kutembea na Gloria, siri ile haikuwa siri tena kwani ilikuwa imekwishajulikana kwa Peter muda ule ambao alikuwa akitekwa kutka katika gari ambalo alikuwepo pamoja na Peter.
‘Bosi’ hilo ndio neno ambalo lilikuwa likija kichwani mwake mara kwa mara, hakuwa akijua ni mtu gani ambaye alikuwa nyuma ya mpango ule wote jambo ambalo likaanza kumuingizia maswali mengi kichwani mwake. Mtu wa kwanza kumfikiria alikuwa Peter. Kichwa chake kikaanza kujipa uhakika kwamba Peter ndye ambaye alikuwa ndani ya kila kitu kwa kuona kwamba alikuwa amewaitia watu wamteke na kisha kumuua kwa sababu alikuwa ametembea na mpenzi wake, Gloria.
Wazo hilo likaendelea kudumu kichwani mwake, alijua fika kwamba Peter alikuwa amegundua kila kilichokuwa kikiendelea toka zamani na ndio maana alikuwa ameamua kumuua kwa ajili ya kumaliza kila kitu. Mawazo yake hayo ndio ambayo yakamfanya kugundua kwamba ile ilikuwa moja ya sababu ambayo ilimfanya Peter kuachwa hai ndani ya gari lile kwa sababu tu yeye ndiye alikuwa amepanga kila kitu.
Mawazo hayo yakaonekana kumletea chuki moyoni mwake juu ya Peter, akatokea kumchukia Peter kwa kumuona msaliti kwani alikuwa amemfanyia mambo mengi kama kumsaidia ndani ya nchi hiyo huku yeye akiwa njiani kuulipiza uzuri kwa ubaya. Kaposhoo hakutaka kufikiria kuhusu mahusiano ya siri ambayo alikuwa ameyaweka pamoja na Gloria, hakutaka kuyafikiria maumivu ambayo Peter alikuwa ameyapata, kwake, wakati mwingine alijichukulia kufanya kitu kilichokuwa sahihi ambacho kilitakiwa kufanywa na mwanaume yeyote ambaye alijiita lijari kama alivyokuwa.
“Huyu atakuwa Peter tu” Kaposhoo alijisemea katika kipindi ambacho gari lilikuwa likiingizwa katika barabara ya Katima Mulilo.
“Yaani kisa msichana tu ameamua kuuvuja urafiki wetu kwa kutaka kuniua! Haiwezekani, hivi Peter ameamua kufanya haya kweli? Nimeamini watanzania hawatakiwi kusaidiwa” Peter alijisemea huku kila mtu ndani ya gari lile akiwa kimya.
Mawazo yake bado yalimwambia kwamba Peter ndiye ambaye alikuwa amehusika katika kila kitu, kila alipotaka kuyapinga mawazo hayo bado aliendelea kupata msukumo wa kuhisi kwamba Peter ndiye ambaye alikuwa amehusika katika kila kitu.
“Nikinusurika, namuua yeye” Kaposhoo alijisemea huku akionekana kuwa na hasira.
Kadri dakika zilivyokuwa zikizidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo Kaposhoo alivyoona kwamba muda wake wa kuendelea kuishi ukiendelea kupungua. Moyoni, hasira kali zikamuingia, akajihisi kuwa na kiu ya kumuua Peter ambaye aliamini kwamba ndiye aliyemletea vijana wale kwa ajili ya kumuua.
“Mmh! Lakini Peter anaweza kufanya hivi?” Kaposhoo alijiuliza mara baada ya dakika kadhaa.
“Haiwezekani, nahisi kuna mtu. Peter hana fedha za kutosha kuwakodisha watu waje kuniua. Ok! Kama si Peter, atakuwa nani?” Kaposhoo aliendelea kujiuliza, maswali mfululizo.
Katika kipindi hicho alionekana kuwa kigeugeu, kila alipokuwa akijiuliza maswali zaidi na zaidi na ndivyo alivyokuwa akipata majibu kadhaa kutokana na maswali hayo yaliyokuwa yakizidi kumiminika kichwani mwake. Kipindi cha nyuma alikuwa na uhakika kwamba Peter ndiye ambaye alikuwepo ndani ya mpango wote lakini kadri muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo alivyoona kwamba Peter hakuwa amehusika bali kulikuwa na mtu mwingine nyuma ya pazia.
Maswali hayo ndio ambayo yakamfanya kugundua kitu kwamba Gloria hakuwa msichana mwaminifu kabisa. Aliweza kumsaliti Peter na kisha kutembea na yeye na wakati huo huo aliweza kumsaliti yeye na kutembea na mtu ambaye alitambulishwa kama bosi. Katika kipindi hicho, kwake Gloria akaonekana kuwa mwanamke mbaya ambaye hakutakiwa kuishi na mtu yeyote yule kwa kuwa tu alikuwa msaliti kupita kawaida.
“Mmmh! Huyu anajua ukweli. Yaani nisinusurike, nikinusurika, nitaua mmoja baada ya mwingine” Kaposhoo alijisemea.
Kujiuliza maswali ndani ya gari lile hakukuisha kabisa, aliendelea kujiuliza zaidi na zaidi. Kikafika kipindi ambacho akaona kwamba ilikuwa ni bora kuwauliza vijana wale kuhusiana na watu ambaye alikuwa amewatuma kwa ajili ya kumteka na kumuua. Hakujua kama vijana wale wangekuwa radhi kumwambia ukweli au la.
“Naomba kuuliza swali” Kaposhoo alisema huku akionekana kuwa na hofu.
“Hautakiwi kuuliza maswali. Ukiongea kitu chochote kile, tunakumiminia risasi” Mwanaume mmoja ambaye alionekana kuwa kiongozi alimwambia Kaposhoo.
“Mimi ni mfu ninayetembea kwa sasa. Tayari mmekwishaniua ila ningependa kujua kitu fulani. Kama mnataka kunimiminia risasi, nyie nimiminieni tu, tayari nimekwishakufa” Kaposhoo aliwaambia vijana wale ambao wakabaki wakiangalia. Kijana mmoja akaikoki bunduki yake.
“”Naomba mniambie ukweli. Nataka kumfahamu bosi wenu aliyewatuma mniue” Kaposhoo aliwaambia lakini hakukuwa na mtu ambaye alimwambia kitu chochote kile.
Mambo yakaonekana kuwa magumu kwa Kaposhoo, alichokifanya mahali hapo ni kuanza kuomba msamaha kwa kuamini kwamba vijana wale wangeweza kumsamehe kwa kuwalipa kiasi kikubwa cha fedha zaidi ya walichopewa.
“Tumeagizwa kukua tu” Mwanaume yule alimwambia.
“Naombeni mnisamehe, nitawalipa kiasi chochote mtakachohitaji” Kaposhoo aliwaambia vijana wale.
“Hilo ni jambo lisilowezekana. Tusipokuua wewe, tutakuwa tumeisaliti kazi yetu” Mwanaume yule alimwambia Kaposhoo.
Japokuwa alijifanya kutokuwa na hofu kabisa lakini katika kipindi hicho ndicho ambacho hofu ikaanza kumuingia moyoni mwake, akaanza kuhofia kwa kuona kwamba muda wowote ule vijana wale wangeweza kumuua na kisha kwenda kufanyiwa malipo. Machozi yakaanza kutiririka maashavuni mwake, hakuona kama kungekuwa na msaada wowote ule ambao ungemfanya kunusurika kutoka katika mikono ya watu wale.
Gari lile likazidi kutembea katika barabara ile ya Katima Mulilo mpaka ilipofika katika bustani ya kupumzikia ambapo wakaendelea mbele zaidi. Kwa wakati huo lengo lao lilikuwa ni kufika Maipompo ambapo hapo ndipo walipokuwa wakitaka kumuua Kaposhoo na kisha kuendelea kufanya mambo yao mengine.
Safari iliendelea zaidi, wakafika katika eneo lililokuwa na shule ya msingi ya Ngwerere, wakazidi kusonga mbele na baada ya dakika kadhaa karibu na shule ya msingi ya Olympia Park ambapo wakakata kushoto na kuchukua barabara ndogo ambayo ilikuwa ikielekea Maipompo mpaka Atakata. Walipofika Maipompo, wakalisimamisha gari lao na kuanza kuelekea katika pori dogo ambalo lilikuwa katika eneo hilo.
Maipompo ulikuwa ni eneo kubwa ambalo ulionekana kama kutengwa na watu waliokuwa wakiishi katika nchi ya Zambia. Eneo hilo lilitengwa kutokana na imani kubwa ya kishirikina ambayo ilikuwa ikivuma sana katika kipindi hicho nchini Zambia. Kwa Tanzania, sehemu kama Maipompo ilikuwa ni Gamboshi, sehemu ambayo ilikuwa juu kwa mambo ya kishirikina, sehemu ambayo ilionekana kuwa kama makao makuu.
Wazambia wengi hawakuwa wakitaka kukaa katika eneo hilo, watu wengi ambao walikuwa wakikaa katika eneo hilo walikuwa wakipatwa na magonjwa ya mara kwa mara hali ambayo iliongeza hofu kwa wakazi wa Zambia.
Wauaji wa kundi la Kunta Kinte ndio ambao walikuwa wakipenda sana kulitumia eneo hilo kwa ajili ya kufanya mauaji yao, mauaji mengi ambayo walikuwa wakiyafanya katika kijipori kidogo kilichokuwa kikipatikana katika eneo hilo. Watu wa Zambia walionekana kama kutokuliamini sana eneo hilo, hata kama kulikuwa na watu ambao walikuwa wakiuawa kwa kupigwa na risasi, imani zao zilikuwa zikiwapelekea kuhisi kwamba ni ushirikina ndio ambao ulikuwa umefanyika na watu hao kuonekana kama walikuwa wamepigwa risasi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Imani zao za kishirikina ndizo ambazo zikawafanya watu wa kundi hilo la Kunta Kinte kulitumia pori hilo dogo vilivyo huku mambo ya ushirikina yakionekana kuwa kama mwamvuli wao wa kujikingia na watu ambao walikuwa wakihisi mambo mabaya.
Bado walikuwa wakielekea katika kijipori kile kidogo huku wakiwa wamemshika Kaposhoo ambaye muda wote alikuwa akilia huku akiomba msamaha. Tayari alijua fika kwamba katika dakika chache zijazo angekuwa marehemu, hakutaka kuuawa, alikuwa akiendelea kuwaomba wale watu msamaha huku akiahidi kuwapa fedha nyingi zaidi endapo wangeweza kumuacha hai lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye alionekana kukubaliana nae.
“Kadri unavyotupigia kelele na ndivyo unavyotufanya tufikirie kukua kwa kifo kilichojaa maumivu makali” Mwanaume yule ambaye alikuwa muongeaji mkubwa alimwambia Kaposhoo.
“Naombeni mnisamehe” Kaposho alisema huku akivikutanisha viganja vyake.
“Hivi umekwishawahi kusikia Kunta Kinte tukamsamehe mtu?” Mwanaume yule alimuuliza Kaposhoo.
“Naombeni mnisamehe.
“Ni ngumu. Hicho ni kitu kisichowezekana Kaposhoo. Wewe kufa kupo pale pale” Mwanaume yule alimwambia Kaposhoo.
Wakaingia katika kipori kile kidogo na kisha kumpiga mtama Kaposhoo ambaye akaanguka na kichwa chake kugonga katika jiwe lililokuwa chini na kukifanya kichwa chake kutokwa damu. Kaposhoo aliendelea kulia zaidi na zaidi, alijua fika kwamba zilibakia sekunde chache sana hata kabla hajafa na kuungana na mama yake ambaye alikufa miaka kadhaa iliyopita.
“Naombeni mnisamehe” Kaposhoo aliwaambia huku akiwa amepiga magoti chini.
“Huo msamaha ungemuomba Bwana Stewart” Mwanaume yule alimwambia Kaposhoo huku akianza kuikoki bunduki yake.
“Bwana Stewart!!” Kaposhoo aliuliza huku akionekana kushangaa.
“Huyo ndiye wa kumuuliza” Mwanaume yule alimwambia Kaposhoo.
“Yeye ndiye aliyewatuma mje kuniua! Yeye ndiye natwembea na Gl....” Kaposhoo alisema lakini hata kabla ya kumalizia sentensi yake, milio mitatu ya risasi ikasikika mahali hapo, Damu zikatapakaa, Kaposhoo akapiga uyowe mmoja tu, akaanguka chini, mwili wake ulikuwa umetobolewa na risasi maeneo matatu, damu zilikuwa zikimtoka, baada ya sekunde chache, akabaki kimya, hakukusikika sauti yoyote ile kutoka kwake.
“Tuondokeni” Mwanaume yule aliwaambia vijana wenzake na kisha kuondoka mahali hapo huku kila mmoja akiwa amekishuhudia kifo cha Kaposhoo porini
Peter alionekana kuwa mwenye hasira kali, kisu kilikuwa mkononi mwake, kwa wakati huo, kichwa chake kilikuwa kikifikiria kufanya mauaji tu. Moyo wake ukawa umekwishabadilika kabisa, hakumpenda Gloria, mapenzi yote ambayo alikuwa nayo kwa Gloria yalikuwa yamekwishapotea na ni chuki tu ndio ambazo zilikuwa zimeutawala moyo wake.
Mwili wake ulikuwa ukitetemeka kutoka na hasira kali ambazo alikuwa nazo katika kipindi hicho, hakuamini kama msichana Gloria, msichana ambaye alikuwa na pete ya uchumba kidoleni mwake ndiye ambaye alikuwa ameamua kuyafanya yale aliyokuwa ameyafanya.
Huku akiwa hatua saba kumfikia Gloria, mlinzi akamuwahi na kisha kumshika. Peter akaanza kuleta purukushani lakini kutokana na kushikwa vilivyo na mlinzi yule, akajikuta akiishiwa nguvu, machozi yaliendelea kumtoka lakini hakuwa na la kufanya.
“Nitakuaa....nimesema nitakuua” Peter alimwambia Gloria kwa sauti kubwa.
Mambo yakaonekana kubadilika mahali hapo, alichokifanya Bwana Stewart ni kumchukua Gloria na kisha kumpeleka nje ya jengo lile na kumuingiza garini mwake. Katika kipindi chote hicho Gloria alikuwa akilia kama mtoto, Peter alionekana kubadilika katika mabadiliko ambayo Gloria hakuwa ameyaona kwake katika kipindi chote cha maisha yake.
“Kwa nini Peter anataka kukuua tena?” Lilikuwa swali la kwanza ambalo lilitoka mdomoni mwa Bwana Stewart ambaye alikuwa akiliwasha gari lake.
“Sijui kwa nini. Amekuja na kuonekana mwingi wa hasira” Gloria alidanganya huku akilia.
“Ndio akuite malaya!”
“Hata mimi nimemshangaa sana”
“Kwani alikwishawahi kukufunua?”
“Kivipi”
“Alikwishawahi kufanya mapenzi na wewe?” Bwana Stewart aliuliza huku akiendesha gari.
“Peter ni mchumba wangu” Gloria alisema maneno ambayo yakamfanya Bwana Stewart kushtuka na kusimamisha gari lile pembeni ya barabara.
“Umesemaje?”
“Peter ni mchumba wangu. Hii pete alinivarisha yeye mbele ya wazazi wangu” Gloria alimwambia Bwana Stewart.
“Unanichanganya. Kwa hiyo Peter ni Mtanzania kama wewe?”
“Ndio”
“Na vipi kuhusu Kaposhoo?”
“Yule si mpenzi wangu” Gloria alitoa majibu ambayo yalimfanya Bwana Stewart kuchanganyikiwa.
“Mbona haukuniambia? Mimi nilijua Kaposhoo ni mpenzi wako kutokana na ukaribu wenu” Bwana Stewart alimwambia Gloria.
Hapo ndipo ambapo Gloria akaanza kumhadithia Bwana Stewart toka katika kipindi ambacho Peter alikuwa amemvarisha pete katika sherehe ndogo iliyofanyika nyumbani kwao. Gloria hakuishia hapo, aliendelea kumhadithia mpaka katika kipindi ambacho Peter aliamua kuondoka nchini Tanzania na kuelekea Zambia kwa ajili ya kusoma. Katika kipindi chote hicho Bwana Stewart alikuwa kimya kabisa, kichwa chake kilikuwa na maswali mengi yasiyokuwa na majibu.
“Kwa hiyo Kaposhoo alikuwa rafiki wa Peter?” Bwana Stewart alimuuliza Gloria.
“Ndio”
“Kwa hiyo nimeua damu isiyo na hatia?” Bwana Stewart aliuliza.
“Kivipi?”
“Niliwatuma vijana wamteke Kaposhoo na kumuua. Wamekwishaifanya kazi hiyo” Bwana Stewart alimwambia Gloria.
“Umemuua kaposhoo”
“Ndio. Mbona umeshtuka sana na wakati tulikuwa tushakubaliana?”
“Usingefanya hivyo”
“Sasa haukuniambia mpenzi, unafikiri ningefanyaje”
“Ok! Hakuna tatizo”
“Ila kuna kitu nimefikiria”
“Kitu gani?”
“Kwanza futa machozi, sipendi kuyaona machozi yako yakitiririka mashavuni mwako” Bwana Stewart alimwambia Gloria ambaye akaanza kuyafuta machozi yake.
“Bado kuna kizingiti kikubwa mbele yetu” Bwana Stewart alimwambia Gloria.
“Kizingiti gani?”
“Peter. Anaweza kukua huyu mtu”
“Hawezi kuniua”
“Hawezi! Haujaona pale alivyotaka kukuchoma kisu, hivi yule mlinzi asingemuwahi si ungekuwa marehemu pale”
“Kwani si hata wewe ungemzuia”
“Na uzee wangu huu, si angeniua hata kwa ngumi moja”
“Ok! Baby, wewe unataka nini kifanyike?”
“Tumuue Peter ili tuwe na amani. Tusipomuua, atakuua yeye” Bwana Stewart alimwambia Gloria.
“Mmmh!”
“Usigune. Hilo ndio la msingi”
“Tutaanzia wapi?”
“Hilo si swali la kujiuliza sana, cha msingi ni utayari tu. Upo tayari” Bwana Stewart alimwambia Gloria na kisha kumuuliza swali.
“Kwa sababu anataka kuniua, nipo tayari” Gloria alimwambia bwana Stewart.
“Basi hakuna tatizo”
Huo ndio mpango ambao walikuwa wameufikiria kufanyika katika kipindi hicho. Kwa sababu tayari Peter alionekana kuwa mtu mbaya ambaye angeweza kuweka kizingiti katika mahusiano yao basi nae alitakiwa kufa kama alivyokufa Kaposhoo. Kwa wakati huo, Gloria hakuonekana kuwa na roho ya huruma hata mara moja, kitu alichokiona cha kumuua Peter kwake kilikuwa sawa kabisa, hakujisikia huruma yoyote moyoni mwake, kumuua Peter kwa ajili ya kulilinda penzi lake na mtu aliyekuwa na umri kama wa baba yake kilionekana kuwa sahihi kabisa.
Bwana Stewart akaonekana kuridhika, kitendo cha Gloria kukubali kumuua Peter kilionekana kumpa furaha sana, alijiona kuwa stering ambaye alikuwa akifanya kila kitu ambacho alitaka kukifanya kwa wakati huo. Hakutaka mtu yeyote aingilie mahusiano yake na Gloria, alimpeda sana Gloria, kwake, alionekana kuwa msichana mrembo sana ambaye hakutakiwa kumpoteza hata mara moja.
Suala la kumuua Peter wala halikuwa kubwa kabisa, tukio hilo alilifananisha na kumsukuma mlevi katika mteremko mkali. Kufanya mauaji kwa ajili ya kulilinda penzi lake hakukuonekana kama kulikuwa na kosa lolote lile, alikuwa na uhuru wa kufanya kitu chochote kile kwa ajili ya kuliokoa penzi lake kwa Gloria.
“Ngoja nifanye mipango, kesho tu utasikia taarifa kwamba huyu mtu ni marehemu” Bwana Stewart alimwambia Gloria.
“Utafanyaje?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kama Kaposhoo alivyouawa. Usijali mpenzi” Bwana Stewart alimwambia Gloria.
Kilichoamuliwa ndicho ambacho kilitakiwakufanyika, alichokifanya Bwana Stewart ni kuwafuata vijana wa kundi la Kunta Kinte na kisha kuwaambia juu ya mpango wake kabambe ambao alikuwa ameuweka kwa ajili ya kumuua Peter. Mpango huo ukapokelewa kwa mikono miwili na aliahidiwa kwamba ndani ya siku mbili tu kila kitu kingekuwa tayari endapo angewakabidhi picha ya marehemu mtarajiwa.
“Wanahitaji picha yake” Bwana Stewart alimwambia Gloria.
“Nafikiri ninazo kwenye simu. Subiri” Gloria alimwambia bwana Stewart na kisha kuanza kuipekua simu yake ambapo mara baada ya kuziona picha kadhaa za Peter, akampa Bwana Kaposhoo.
Siku iliyofuata, Bwana Stewart akaanza kuelekea katika makao makuu ya kundi la Kunta Kinte na kisha kuwapa picha zile. Kila kitu ambacho kilitakiwa kukamilishwa hasa kuhusiana na alipo kikakamilishwa na kisha kupewa ahadi kwamba baada ya siku mbili kazi yake ingekamilika kwani kamwe hawakuwa wameshindwa katika kazi yoyote ile hasa ya kufanya mauaji.
“Kama ilivyotokea kwa Kaposhoo, itatokea kwa huyu mjinga pia. Atamiminiwa risasi nyingi tu” Kiongozi wa kundi lile alimwambia Bwana Stewart.
“Kwa hiyo ndani ya siku ngapi itakuwa tayari?”
“Leo usiku tutakupigia simu ya ushindi. Kazi itafanyika leo usiku” Kiongozi yule alijibu kwa kujiamini.
“Itakuwa safi sana”
Bwana Stewart hakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, kwa kuwa alikuwa amekwishafanya kila kitu kuhusu malipo, akaondoka mahali hapo na kurudi nyumbani. Ndani ya gari alikuwa na furaha kwa kuona kwamba kila kitu ambacho alikuwa amekipanga kilikuwa kikienda kukamilika muda si mrefu. Moyoni hakujua, hakujua kwamba unapoingia ndani ya vita kupigana na adui yako huku ukimuwinda na risasi nawe pia unawindwa na adui huyo. Hayo ndio yalikuwa maisha yaliyoanza kutokea, wakati yeye akimuwinda adui yake, nae huku nyuma alikuwa akiwindwa pia.
Maisha ya mapenzi yakawa yamekwishabadilika moyoni mwake, kipindi kile ambacho alikuwa akikitumia kucheka kwa sasa hivi alikuwa akilia tu, kila kitu katika maisha yake kilikuwa kimekwenda ovyo sana, nyakati zile za furaha zikageuka na kuwa nyakati za huzuni zenye kuumiza.
Gloria hakuwa mikononi mwake tena, msichana ambaye alikuwa akimpenda zaidi ya mtu yeyote katika dunia hii alikuwa amemkimbia maishani mwake. Peter aliumia, maumivu yalikuwa makubwa moyoni mwake, aliona ilikuwa ni bora kuchomwa na msumali wa moto moyoni mwake lakini si kupatwa na kile kilichokuwa kimempata kwa wakati huo.
Akawa mtu wa mawazo, wakati mwingine alijuta sana kumchukua msichana kama Gloria ambaye alikuja kumuumiza kwa maumivu makuu moyoni mwake, alijuta muda ambao aliupoteza kwa msichana huyo katika kipindi chote cha maisha yake. Mtu ambaye alikuwa akimpenda kwa moyo wa dhati leo hii alikuwa ameamua kumsaliti kwa kutembea na rafiki yake, Kaposhoo kisa tu alikuwa na fedha na mali nyingi.
Peter hakutegemea kama Gloria angeweza kufanya kitu kama kile, hakutegemea kama Gloria angeweza kumsaliti kwa sababu tu alikuwa ameona fedha na mali. Hapo ndipo akili yake ilipokaa sawa kwa kuona kwamba mwanamke hakuwa mtu wa kuwekewa dhamana kwani hubadilika kwa haraka sana kama upepo mara tu wanapokutana na mtu ambaye yupo tofauti na mpenzi wake.
Ndoto zote za kutaka kumuoa zikawa zimepotea kama upepo, kichwa chake kikaanza kuwafikiria wazazi wake, hakujua ni kwa maneo gani ambayo alitakiwa kuwaambia ili waweze kuamini kile ambacho kilikuwa kimetokea. Alijua fika kwamba taarifa ile ingekuwa taarifa ya mshtuko sana kwa wazazi wa pande zote mbili lakini hakuona kama kulikuwa na sababu ya kukaa kimya na kutokutoa taarifa ile.
Alichokifanya Peter usiku huo ni kuchukua simu yake na kisha kuanza kuwapigia wazazi wake na kuwaelezea ukweli juu ya kile ambacho kilikuwa kimetokea nchini Zambia. Kama alivyotegemea ndivyo ilivyokuwa, wazazi wake walishtuka kupita kawaida, hawakuonekana kuamini kile ambacho walikuwa wakikisikia kutoka kwa Peter.
“Haiwezekani” Mzee Steven alisema, hakuonekana kuamini kile alichokisikia simuni kutoka kwa Peter.
“Huo ndio ukweli baba. Gloria amebadilika sana, amekuwa mtu wa kutembea na wanaume huku Zambia” Peter alimwambia baba yake, mzee Steven.
“Yupo wapi kwa sasa?”
“Ameondoka hapa nyumbani. Kaja kuchukuliwa na mzee mmoja ambaye ni bosi wake katika hoteli ambayo anafanya kazi:” Peter alijibu huku akionekana kuumia kupita kawaida.
“Bado siamini Peter”
“Naomba uniamini baba. Kwa mara ya kwanza nilipofahamu sikuamini lakini kwa sasa niamini, Gloria kabadilika sana” Peter alimwambia baba yake.
“Kwa hiyo kakuacha?”
“Ndio”
“Hapana. Hebu muite na muongee pamoja, wakati mwingine mahusiano hupitia nyakati mbaya sana, nyakati kama hizo si za kukaa chini na kuanza kulalamika, kama wapenzi, muite na kisha kuongea, muyamalize, hayo yanapaswa kumalizwa nanyi, ila mkishindwa ndio mtuambie wazazi Peter” Mzee Steven alimwambia Peter.
“Baba....”
“Naam”
“Naomba unielewe, Gloria hayupo na sijui yupo wapi. Hapa nilipo nina hasira, ninaweza hata kumuua nitakapomuona” Peter alimwambia baba yake.
“Hayo si maamuzi mazuri Peter, usijaribu kufanya jambo wakati una hasira, ngoja hasira zipungue na ndio ufanye maamuzi, unapokuwa na hasira na kisha kufanya jambo fulani, utakuja kujutia baadae” Mzee Steven alimwambia mtoto wake, Peter.
“Imeniuma sana baba”
“Najua”
“Acha nimuue, yule mwanamke hanistahili hata kidogo, ameuumiza sana moyo wangu” Peter alimwambia baba yake.
“Unafikiri hilo ni suluhisho?”
“Nadhani litakuwa suluhisho”
“Unadhani! Usifikiri hilo litakuwa suluhisho Peter, yakupasa kumtafuta na kisha kukaa nae chini na kuongea” Mzee Steven alimwambia Peter.
“Nitajaribu”
“Sawa sawa. Jaribu kwanza, utakaposhindwa na ndipo hapo tutakapoona nini kifanyike” Mzee Steven alimwambia Peter.
“Sawa baba” Peter alijibu.
****
Mzee Steven akaonekana kuchanganyikiwa, maneno aliyoongea Peter yakaonekana kumchanganya kupita kawaida, moyoni hakuamini kama Gloria angeweza kufanya jambo lile. Alichokifanya ni kumuita mke wake, Bi Stela na kisha kuanza kumwambia kile ambacho kilikuwa kimetokea nchini Zambia, kitu ambacho aliambiwa na Peter katika kipindi kichache kilichopita. Kama ilivyokuwa kwa mzee Steven, nae Bi Stela hakuonekana kuamini.
“Haiwezekani, Gloria hawezi kufanya hivyo. Kwanza umalaya ameanza lini? Nadhani kuna kitu kingine Peter hataki tukifahamu” Bi Stela alimwambia mume wake, mzee Steven.
“Hata mimi nililifikiria hilo, huko kutakuwa na kitu. Sasa tufanye nini?”
“Nadhani itatakiwa tuongee na Gloria mwenyewe”
“Sawa sawa” Mzee Steven alimwambia mke wake.
Kilichofuata baada ya hapo ni kuanza kumpigia simu Gloria kwa ajili ya kuwaambia ukweli kile ambacho kilikuwa kinaendelea nchini Zambia, tofauti na siku nyingine, siku hiyo simu ya Gloria haikuwa ikipatikana kabisa. Hali hiyo ikaonekana kuwatia wasiwasi, haikuwahi kutokea hata siku moja simu ya Gloria kutokuwa hewani, kitu hicho kikaanza kuibua maswali mengi mioyoni mwao.
Hawakutaka kukaa kimya juu ya jambo hilo, walichokifanya ni kuelekea Mwenge walipokuwa wakiishi wazazi wake Gloria kwa lengo la kuwaambia kile ambacho alikuwa amekizungumza Peter. Maneno yao yakaonekana kutokuaminika vichwani mwa wazazi wake Gloria, Bwana Michael na Bi Justina, wakabaki wakiwaangalia mara mbili mbili.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Gloria hawezi kufanya hivyo. Kwanza ameokoka” Bi Justina aliwaambia.
“Ila kwenye hali ya mapenzi, hebu tusahau kuhusu wokovu” Mzee Steven alimwambia Bi Justina.
“Hivi unafikiri Gloria anaweza kufanya hilo, au kama kuna jambo jingine lakini si hilo” Bi Justina aliwaambia.
Bi Justina alikuwa akimuamini sana binti yake, alijua fika kwamba binti yake alikuwa ameokoka na hivyo asingeweza kufanya kile ambacho alikuwa akiambiwa katika wakati huo, kwake, maneno yale yakaonekana kuwa maneno mageni ambayo wala hayakuwa na ukweli wowote ule.
“Hata mimi ninaamini kwamba Gloria hawezi kufanya hivyo. Sisi kama wazazi hebu tujaribuni kufanya uchunguzi” Bwana Michael aliwaambia.
Nchini Tanzania, wazazi wakaonekana kuwa wagumu kuamini kile kilichokuwa kikiendelea nchini Zambia, hawakuamini kama Gloria angeweza kufanya kile ambacho Peter alikuwa amekiongea, walichokuwa wakikihisi wao ni kwamba kulikuwa na tatizo jingine kabisa ambalo Peter alikuwa akilificha na hivyo hakutaka walifahamu.
“Cha msingi ni kuongea na Gloria tu. Kwa jinsi anavyompenda Peter, kamwe hawezi kufanya kitu kama hicho” Bi Justina aliwaambia.
Bado kulionekana kuwa na tatizo nchini Zambia, wazazi hawakutaka kuyaamini maneno ya Peter kwamba Gloria alikuwa akimsaliti nchini humo, jambo ambalo walikuwa wakilihisi ni kwamba kulikuwa na kitu kingine ambacho kilikuwa kikiendelea nchini humo, kitu ambacho kamwe peter hakutaka kukiweka wazi.
Walichoakiamua kama wazazi ni kuanza kufanya uchunguzi wa chini chini kugundua ni wapi kulipokuwa na tatizo, walichokiamua ni kuendelea kuwasiliana na Peter na kisha kumchimba mpaka pale ambapo wangeambiwa kitu ambacho wangekuwa wakiyaunganisha matukio na kufahamu dhahiri kujua ya kile kilichokuwa kikiendelea nchini Zambia.
****
Peter hakutaka kukaa nyumbani kabisa, usiku huo huo akachukua simu yake na kisha kumpigia mzee Mbwana na kumueleza kuhusiana na tukio la utekaji ambalo lilikuwa limetokea kwa mtoto wake. Simu ile ikaonekana kumshtua sana mzee Mbwana ambye baada ya dakika kadhaa akafika ndani ya nyumba hiyo huku akionekana kuchanganyikiwa.
“Umesemaje?” Lilikuwa swali la kwanza alilomuuliza Peter.
Alichokifanya Peter ni kuanza kuelezea kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea ndani ya gari, mzee Mbwana akaonekana kuchanganyikiwa, akahisi kwamba kulikuwa na mtu nyuma ambaye alikuwa akimchezea.
“Ulikwenda polisi?”
“Hapana. Nilitaka kukupa taarifa kwanza” Peter alijibu.
“Safi sana. Twende tukawape taarifa polisi” Mzee Mbwana alimwambia Peter.
Hawakutaka kubaki mahali hapo, walichokifanya ni kuondoka kuelekea katika kituo cha polisi cha Mansansa. Ndani ya gari kila mtu alikuwa kimya, tukio ambalo lilikuwa limetokea lilionekana kuwachanganya kupita kawaida. Wala hawakuchukua muda mrefu, wakafika katika kituo cha polisi cha Mansansa na kisha kuanza kuwapa taarifa polisi juu ya kile kilichokuwa kimetokea.
Polisi waliokuwa mahali pale wakaonekana kushtuka, hawakuamini kama nchi Zambia kitu kama kile kingeweza kutokea, ni kwa kipindi kirefu sana hakukuwa na kesi kama hiyo, hakukuwa na mtoto wa tajiri ambaye alikuwa ametekwa na watu wasiojulikana kwa kipindi kirefu sana.
“Tutaanza kumtafuta” Polisi mmoja alimwambia mzee Mbwana.
Ukubwa wa jina lake, utajiri wake na heshima ambayo alikuwa amejijengea nchini Zambia vikaonekana kuwa vitu ambavyo viliwahamasisha polisi kufanya msako kwa haraka sana, wakaonekana kuwa na haja ya kufanya hivyo kutokana na mtu ambaye aliwataka kufanya hivyo kuwa mwenye fedha na jina kubwa nchini hapo.
“Mkipata chochote nipeni taarifa. Pia nitataka kumfahamu aliyefanya mchezo huu” Mzee Mbwana aliwaambia na kisha kuondoka maali hapo.
Akaanza kumpeleka Peter Maluba, mtaa ambao alikuwa akiishi na kisha kumuacha nyumbani hapo na yeye kuondoka huku akitaka kuonana na Peter siku inayofuatia. Usiku huo, Peter hakulala, alikuwa na mawazo tele, kichwa chake kilikuwa kikimfikiria mpenzi wake ambaye alikuwa ameondoka mikononi mwake, kwake, hakujali sana kuhusu Kaposhoo, mtu aliyekuwa akimjali alikuwa Gloria tu.
Kuuawa kwa Kaposhoo wala hakukuonekana kumtia mawazo moyoni mwake, mtu ambaye alikuwa akimfikiria kwa wakati huo alikuwa Gloria tu. Japokuwa alikuwa na kiu ya kumuua msichana huyo lakini moyoni mwake alikuwa na mapenzi ya dhati kwa msichana huyo kitu ambacho kikamfanya kusitisha mara kwa mara mpango wake wa kumuua msichana huyo.
Siku hiyo alichelewa sana kulala, akajikuta akilala usiku wa saa tisa huku kichwa chake kikiendelea kuwa na mawazo lukuki kuhusiana na mpenzi wake, Gloria. Asubuhi ilipofika, akaamka na kisha kuanza kuelekea kwa mzee Mbwana ambaye alionekana kuwa tofauti sana, toka kipindi ambacho aliwapa polisi juu ya utekaji wa mtoto wake ambao ulikuwa umefanyika, hakuwa amepata majibu yoyote yale juu ya kazi yake.
“Ukimya huu unamaanisha nini sasa! Wameshindwa kazi niingie kazini mwenyewe au?” Mzee Mbwana aliuliza huku akionekana kuwa na hasira.
“Nadhani wanaendelea kufanya kazi” Peter alimwambia mzee Mbwana.
Kila wakati alipokuwa amekaa, kichwa chake kilikuwa kikimfikiria mtoto wake, alimpenda sana na kumhitaji, aliona kwamba kuna mtu ambaye aliamua kumsababishia kidonda moyoni mwake, mtu ambaye hakutaka kumuona akiwa na amani. Alichokifanya mzee Mbwana ni kuwasiliana na Bwana Stewart kwa ajili ya kukutana sehemu na kuongea juu ya suala hilo.
“Ni lazima nitaua mtu Stewart” Mzee Mbwana alimwambia Bwana Stewart ambaye alionekana kuwa na huzuni ya kinafiki.
“Sawasawa. Hivi nani anatutafuta hivi?” Bwana Stewart aliuliza huku akijifanya amekasirika.
“Sijajua ni mpumbavu gani. Nitaua mtu” Mzee Mbwana alimwambia Bwana Stewart.
Mzee Mbwana alikuwa katika upofu mkubwa, amoyo wake ulikuwa ukimuamini sana Bwana Stewart kiasi ambacho alikuwa akimambia mambo mengi sana kuhusiana na familia yake na mambo mengine ambayo ylikuwa yakimhusu. Moyo wake haukuonekana kujua kwamba mzee huyo ndiye ambaye alikuwa amehusika katika kila kitu ambacho kilikuwa kimefanyika.
Katika habari ya saa nne asubuhi, redio za ZNBC FM, Phoenix FM, Flava FM, Q FM pamoja na vituo vingine vya redio nchini Zambia vikaanza kutangaza kuhusiana na taarifa ya kutekwa kwa mtoto wa tajiri, mzee Mbwana, Kaposhoo taarifa ambayo ilionekana kumshtua kila mtu aliyeisikia kwani halikuonekana kuwa jambo la kawaida katika kipindi hicho.
“Nahakikisha mpaka mhusika namjua. Nitahakikisha namuua kwa mikono yangu” Mzee Mbwana alimwambia Bwana Stewart.
“Tena huyo ni wa kunyonga kabisa. Nipo bega kwa bega pamoja nawe kwa ajili ya kumnyonga mtu huyo” Bwana Stewrt alimwambia mzee Mbwana.
Hiyo ndio hali ambayo ilikuwa ikiendelea, wakati mzee Mbwana alipokuwa akilalamika kuhusiana na mtoto wake kwa bwana Stewart, mtu huyo alionekana kuwa na huzuni usoni mwake na wakati moyoni mwake alikuwa akifurahia sana juu ya kile kilichokuwa kimetokea. Mpango wake ambao alikuwa ameupanga na kwa jinsi ulivyofanyika, alikuwa na uhakika kwamba katika kipindi hicho Kaposhoo alikuwa marehemu kwani kamwe kundi la Kunta Kinte halikuwa kundi la kuchezea, walikuwa wakifanya kitu kwa wakati muafaka.
“Mtoto wako amekwishakufa, subiri utaambiwa maiti yake ipo wapi” Bwana Stewart alijisemea maneno haya moyoni kila alipokuwa akimwangalia mzee Mbwana.
Peter alikuwa ametulia sebuleni, mawazo yake bado yalikuwa yakimfikiria mpenzi wake ambaye alikuwa ameondoka nyumbani hapo, Gloria. Akili yake akaiona kutokaa sawa, mapenzi juu ya Gloria bado yalikuwa yamemtawala kupita kawaida. Nyakati za usiku kwake zilikuwa zikionekana kuwa ndefu, hakuwa na raha, furaha yote ambayo alikuwa nayo katika kipindi cha nyuma hakuwa nayo tena.
Alikaa katika hali hiyo kwa dakika kadhaa, mara akausikia mlango ukigongwa, alichokifanya ni kuinuka na kuanza kuusogelea mlango ule. Alipoufikia, akaufungua, macho yake yakatua katika mdomo wa bunduki iliyokuwa imeshikwa na kijana mmoja ambaye alikuwa pamoja na vijana wengine.
Peter akapigwa na mshtuko mkubwa, kile ambacho alikuwa amekiona mbele ya macho yake hakikuweza kuaminika kama kilikuwa ni kitu halisi au ilikuwa moja ya ndoto zake za kusisimua ambazo mara kwa mara alikuwa akiziota. Akaamriwa kurudi ndani ya nyumba ile, akatii, akaamliwa akae kochini, akatii bila kuuliza swali lolote lile.
Vijana wengine watatu ambao walikuwa pamoja na kijana yule aliyekuwa na bunduki wakaingia ndani ya sebule ile na kisha mmoja wao kuchukua kamba na kisha kuanza kumfunga mikono, walipoona kwamba hiyo ilitosha, wakatoka nae nje. Muda wote huo Peter alionekana kuwa na wasiwasi kupita kawaida, hofu ilikuwa imemkamata na hakuamini kama kweli kile kilichokuwa kimetokea ndicho ambacho kilikuwa kikiendelea kutokea.
Mawazo yake yakarudi kwa Kaposhoo, vijana wale ambao walikuwa wamemuweka chini ya ulinzi hawakuwa wageni machoni mwake, alikuwa amekwishawahi kuwaona sehemu, ndani ya gari katika siku ambayo walikuwa wamemteka Kaposhoo na hatimae kumuua. Peter akajua fika kwamba siku ile ndio ilikuwa siku ya mwisho ya yeye kuvuta pumzi ya dunia hii, moyo wake ukaendelea kujuta, kwake, Gloria alionekana kama shetani ambaye alikuwa ameletwa katika maisha yake.
“Huyu atakuwa Gloria” Peter alijisemea.
“Kwa nini Gloria ameamua kunifanyia hivi? Yaani wema wote na mapenzi yote yale niliyomuonyeshea haya ndio malipo yake! Kwa nini ameamua kunifanyia hivi?” Peter alijiuliza huku akionekana kutokuwa na jibu lolote lile.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ndani ya gari, kila mmoja alikuwa kimya, bunduki ambazo walikuwa nazo vijana wale zilionekana kumuogopesha sana Peter, alijua fika kwamba endapo angeanzisha varangati ndani ya gari lile, matokeo yake yangekuwa ni kufyatuliwa risasi kadhaa na kufa papo hapo.
Safari ilikuwa ikiendelea huku kila mmoja akiwa kimya kabisa. Peter alijua fika kwamba alikuwa akienda kufa, alijua fika kwamba watu wale wasingeweza kumuacha hai kutokana na Kaposhoo ambaye alichukuliwa kama yeye kuuawa siku mbili zilizopita. Peter akaanza kutokwa na machozi, mawazo yake yalikuwa yameanza kuwakumbuka wazazi wake, hakuamini kama alikuwa akienda kufa bila kuwaona wazazi wake, alikuwa akienda kuuawa ndani ya nchi ya ugeni.
“Jamani nimefanya nini?” Peter aliuliza huku akionekana kuwa na hofu.
“Hatuhitaji maswali” Mwanaume mmoja alimwambia Peter.
“Jamani mimi sijafanya kitu, mnanionea tu, mimi wala sihusiki na msichana yeyote” Peter alimwambia kijana yule.
“Yaani wewe ndiye mlengwa kabisa. Malaya wako amesema wewe ndiye uliyekuwa ukikusudiwa kuuawa na si Kaposhoo” Mwanaume yule alimwambia Peter.
“Jamani Gloria, kwa nini ananifanyia hivi? Hivi nimemfanya nini mwanamke huyu?” Peter aliuliza maswali huku akianza kutokwa na kijasho chembamba.
“Utamuuliza siku nae akifa na kukufuata kaburini. Kwanza wewe yakupasa kutangulia” Mwanaume yule alimwambia Peter.
“Sikiliza braza, yaani Gloria nashindwa kumuelewa kabisa, unajua nilikuwa nampenda sana, nilimchukua kutoka nyumbani nchini Tanzania, nilikuwa na ndoto nae, ndoto nyingi ambazo kama zingekamilika tungekuwa katika hatua nyingine kabisa. Sikiliza broo, mimi simtaki Gloria, kama anataka aishi na maisha yake mimi nipo radhi kumuachia aendelee na maisha yake. Hivi kweli hapo nina kosa bro?” Peter alimuuliza mwanaume yule.
“Kosa unalo”
“Kosa lipi bro, kama kumuacha aendelee na maisha yake nimekwishamuacha, kosa langu lipo wapi?” Peter aliuliza huku akianza kulia, tayari alionekana kuwa na uhakika kwamba siku hiyo ndio ingekuwa siku yake ya mwisho kuvuta pumzi ya dunia hii.
“Kosa lako moja tu ambalo litakufanya tukuue fasta kama mwenzako” Mwanaume yule alimwambia Peter ambaye alionekana kuchanganyikiwa.
“Kosa gani bro?”
“Nilikwambia hakuna maswali, wewe unauliza maswali” Mwanaume yule alimwambia peter.
“Naombeni mnisamehe. Naombeni mniache jamani. Mkiniachia mimi naondoka kurudi nchini Tanzania, hata huyu Gloria nitamuacha aendelee na maisha yake” Peter alimwambia mwanaume yule.
“Sasa kwa nini hukumuachia toka zamani mpaka umesikia kwamba unakwenda kuuawa?”
“Sikujua. Kweli tena broo sikujua, kama ningejua unafikiri ningemng’ang’ania, walaaaa nisingemng’ang’ania. Haki ya Mungu tena nisingemng’ang’ania” Peter alimwambia mwanaume yule.
Japokuwa Peter alikuwa akiongea maneno mengi lakini hakukuwa na mtu ambaye alionekana kumuelewa, safari yao ya kuelekea Maipompo ilikuwa ikiendelea kama kawaida. Katika kipindi hicho, wote kwa pamoja walikuwa na dhumuni moja, kumuua Peter na kisha kuendelea na maisha yao kama kawaida.
Wala hawakuchukua muda mrefu sana, wakafika katika kipori cha Maipompo ambapo wakamteremsha Peter na kisha kuanza kuelekea ndani kabisa mwa kipori kile. Njia nzima peter alikuwa akilia, hakuamini kama siku hiyo ingekuwa siku yake ya mwisho kuvuta pumzi ya dunia hii, kwake, zilikuwa zimebakia sekunde kadhaa hata kabla risasi mfululizo hazijaingia mwilini mwake, kwa jinsi hali ilivyokuwa ikionekana, hakuwa na uhakika kama angeweza kunusurika.
“Tukamuulie wapi?” Kijana mmoja aliuliza.
“Kama kawaida. Pale pale alipokufa mwenzake” Kijana mwingine alimjibu mwenzake.
Wakaanza kuelekea huko huku Peter akiwa amefungwa kamba. Bado machozi yalikuwa yakitiririka mashavuni mwake, hakuamini kama siku hiyo aligeuzwa ng’ombe ambaye alikuwa akipelekwa machinjioni.
Moyo wake ulikuwa ukimuomba Mungu aweze kumuepusha na hatari ambayo ilikuwepo mbele yake, hakuamini kama Mungu angejibu sala zake au la, yeye alizidi kuomba tu. Walichukua sekunde chache sana wakawa wamekwishafika katika eneo hilo, wakamlaza Peter chini, kiongozi wao ambaye alimpiga risasi Kaposhoo akachukua bunduki na kisha kumuelekezea Peter ambaye alikuwa amepiga magoti huku akiomba msamaha ili aachiwe huru na kuondoka mahali hapo.
“Umekwishamaliza sala yako ya mwisho?” Kijana yule alimuuliza Peter huku akiikoki bunduki yake.
“Naomba unisameheeee” Peter aliomba msamaha huku akivikutanisha viganja vyake.
“Huwa hatuna desturi ya kuwasamehe watu kama nyie, hatuwezi kuwasamehe watu ambao wanaleta ufala kwenye mapenzi” Kijana yule alimwambia Peter, bila kuchelewa, hapo hapo risasi nne mfululizo zikasikika mahali hapo, ghafla Peter akadondoka chini, alijichukulia kama tayari amekwishakufa.
*****
Urafiki wa kinafiki kati ya Bwana Stewart na mzee Mbwana ulikuwa ukiendelea, kila siku mzee Mbwana alikuwa akilalamika kuhusiana na mtu ambaye alikuwa amehusika katika mauaji ya mtoto wake ambaye mpaka katika kipindi hicho mwili wake haukuwa umeonekana, alijua dhahiri kwamba kulikuwa na mtu ambaye alikuwa amehusika katika kufanya mauaji ya mtoto wake, alichokuwa akikihitaji ni kumfahamu muuaji na kisha kumlipizia kisasi kwa ajili ya mtoto wake.
Kichwa chake hakikumfikiria Bwana Stewart, ukaribu ambao walikuwa nao ulimfanya kutoweza kumfikiria mzee huyo hata mara moja. Katika kipindi chote hicho kigumu Bwana Stewart ndiye ambaye alionekana kuwa mfariji wake mkubwa, ukaribu ule ukaonekana kumtia upofu, hakuweza kugundua kabisa kama mzee huyo alikuwa amehusika katika kila kitu.
“Unajua wakati mwingine nina wasiwasi na Peter” Bwana Stewart alimwambia mzee Mbwana.
“Kivipi?”
“Peter anaweza akawa anajua kila kitu. Watanzania si wa kuwaamini kabisa” Bwana Stewart alimwambia mzee Mbwana.
“Una wasiwasi nae katika lipi?”
“Kumuua mtoto wako. Inawezekana kwamba akawa amehusika” Bwana Stewart alimwambia mzee Mbwana ambaye alikuwa ametegesha umakini wote kumsikiliza.
“Sidhani”
“Usiseme hivyo. Hivi unajua kwamba Peter alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Gloria?” Bwana Stewart alimuuliza mzee Mbwana.
“Unasemaje?” Mzee Mbwana aliuliza huku akiwa ameshtuka
“Kwani ulikuwa haulijui hilo?”
“Sijakuelewa”
“Ni lazima ufahamu kwamba Peter alikuwa na mahusiano na Gloria. Unajua kwamba Peter ni Mtanzania?” Bwana Stewart alimuuliza mzee Mbwana.
“Najua”
“Na unajua kwamba Gloria nae ni mtanzani?”
“Hilo najua”
“Ndio maana ninakwambia kwamba Peter ndiye aliyehusika katika kila kitu. Amefanya hivyo mara baada ya kugundua kwamba Kaposhoo alikuwa akitembea na Gloria” Bwana Stewart alimwambia mzee Mbwana.
“”Daah! Inawezekana. Ndio maana hata nilipotaka kuonyesha ushirikiano nae alikuwa akisita sita” Mzee Mbwana alisema huku akionekana kuyaunganisha matukio ambayo wala hayakuwa ya kweli, ila kichwani mwake aliyaona kuunganika.
“Ndio hivyo. Kaposhoo alikuwa akila mali ya Peter, nae Peter akaamua kuwatuma watu kumuua Kaposhoo. Hivi nilikwambia kwamba Gloria yupo hotelini kwangu akiishi pale utaamini?” Bwana Stewart aliuliza.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hapana. Haukuniambia”
“Peter alitaka kumuua Gloria. Baada ya kuona kwamba Kaposhoo ametekwa na kuuawa, akataka kumuua Gloria kwa mikono yake” Bwana Stewart alimwambia mzee Mbwana ambaye akaonekana kuanza kuamini.
“Yaani huyu huyu Peter?”
“Ndiye huyo huyo. Watanzania si watu wa kuwaamini kabisa. Wanabadilika kama vinyonga” Bwana Stewart alimwambia mzee Mbwana.
“Nitamuua Peter”
“Sikiliza. Hautakiwi kuwa na haraka. Peter hakuwa na haraka katika kumuua mtoto wako na ndio maana na wewe hautakiwi kuchukulia haraka mno” Bwana Stewart alimwambia mzee Mbwana.
“Kwa hiyo nifanye nini?”
“Tukamuue kesho asubuhi. Unaonaje?”
“Kesho mbali. Huyu mjinga kanikera. Kwa nini nisiende sasa hivi?”
“Usiwe na haraka kwanza”
Mzee Mbwana akaonekana kuwa na hasira kupita kawaida, akavimba na macho yake kuwa mekundu, hakuamini kama kijana ambaye alikuwa akimuamini, Peter ndiye ambaye alikuwa amefanya mchakato mzima wa kumuua kijana wake. Kwa jinsi mapenzi yalivyokuwa yameshika kasi, alikuwa na uhakika asilimia mia moja kwamba Peter alikuwa amehusika katika kufanya mauaji ya mtoto wake.
Hakutaka kubaki na kuyafikiria maneno ya Bwana Stewart, maishani mwake alikuwa akimuamini mzee huyo kupita kawaida, aliamini kwamba ni kweli Peter alikuwa amefanya mauaji ya mtoto wake. Kichwa chake kikaanza kutengeneza picha, hakuona kama kulikuwa na watekaji ambao wangeweza kumteka Kaposhoo na kisha kumuacha Peter hai, mpaka kulifikiria hilo, alikuwa na uhakika kwamba Peter alikuwa amehusika.
Mzee Mbwana hakutaka kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kulifuata gari lake, akaingia na kisha kuondoka mahali hapo. Kichwa chake kwa wakati huo kilikuwa kikimfikira Peter na alikuwa akielekea Maluba kwa ajili ya kufanya mauaji tu. Akakigusa kiuno chake, bunduki yake ilikuwepo.
“Nitamuua” Mzee Mbwana alisema huku akionekana kuchanganyikiwa.
Safari yake iliishia katika nyumba ya mtoto wake, akateremka kutoka garini na kumlifuata geti. Alipolifikia, akaanza kugonga lakini wala mlinzi hakutokea mahali hapo. Mzee Mbwana aliendelea kugonga zaidi na zaidi lakini wala mlinzi hakutokea, alichokifanya ni kuanza kulisukuma geti, ule mlango mdogo, geti likafunguka.
Mzee Mbwana akaingia ndani, akaanza kuangalia huku na kule, mlinzi hakuonekana mahali pale. Alichokifanya ni kutoa bunduki yake, akaonekana kuwa na wasiwasi kwamba kulikuwa na kitu ambacho kilikuwa kimetokea. Akaanza kukifuata kijengo kidogo cha mlinzi, alipokifikia, akachungulia, mlinzi alikuwa amelala chini huku akiwa amefungwa kamba miguuni na mikononi kwa nyuma huku mdomoni akiwa amewekewa vitambaa.
Mzee Mbwana akaonekana kushtuka kupita kawaida, hakuamini kile ambacho alikuwa amekiona, akaufuata mlango wa kijengo kile na kisha kuingia ndani ambapo akamfuata mlinzi na kumfungua kamba huku akivitoa vitambaa vile vilivyokuwa mdomoni mwake.
“Kuna nini?” Mzee Mbwana alimuuliza mlinzi.
“Kuna watu walikuja”
“Watu gani?”
“Siwajui. Ila walikuwa na bunduki mikononi mwao” Mlinzi alijibu.
“Walikuwa wakitaka nini?”
“Sijui. Waliniweka chini ya ulinzi, wakanifunga kamba na kisha kuniingiza ndani ya hiki kijengo changu” Mlinzi alimwambia mzee Mbwana.
“Baada ya hapo?”
“Sijui kitu gani kiliendelea mpaka ulipokuja mahali hapa” Mlinzi alimwambia mzee Mbwana.
“Peter yupo?”
“Alikuwepo ndani” Mlinzi alimwambia mzee Mbwana.
Mzee Mbwana hakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kutoka ndani ya kijumba kile na kisha kuanza kupiga hatua kuelekea ndani ya jengo lile. Akaingia ndani, televisheni ilikuwa ikiwaka lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa akionekana. Mzee Mbwana akaanza kuingia chumba kimoja baada ya kingine, hakukuwa na mtu yeyote yule.
Mzee Mbwana akaonekana kuchanganyikiwa, hakuamini kama Peter hakuwepo ndani ya nyumba ile. Maswali mengi yakaanza kumiminika kichwani kwake, swali la kwanza lilikuwa juu ya vijana ambao walikuwa wamekuja ndani ya nyumba ile na kisha kumfunga mlinzi na swali la pili lilikuwa ni kitu kilichotokea mara baada ya kuingia ndani.
“Peter hayupo” Mzee Mbwana alimwambia mlinzi.
“Basi watakuwa wamemteka”
“Wamemteka au wamemchukua? Mtu wao yule, watakuwa wamemchukua” Mzee Mbwana alimwambia mlinzi.
“Kuna kitu gani kinaendelea?” Mlinzi aliuliza huku akionekana kutokuelewa kitu chochote kile.
“Peter ndiye aliyemuua Kaposhoo”
“Unasemaje?”
“Peter ndiye aliyemuua Kaposhoo. Hivi unavyojua Gloria alikuwa msichana wa nani?” Mzee Mbwana alimuuliza mlinzi.
“Msichana wa Peter”
“Ulikwishawahi kumuona Kaposhoo akitembea na Gloria?”
“Ndio. Alikuwa akiniambia iwe siri”
“Siku ambayo Kaposhoo alitekwa, nini kilitokea nyumbani?”
“Peter alitaka kumuua Gloria kwa kumchoma na kisu huku akimuita kuwa ni malaya” Mlinzi alijibu.
“Stewart alikuwa sahihi kabisa. Huyu mpumbavu lazima nimsake na nimuue, haijalishi nitatumia kiasi gani cha fedha, nitahakikisha nampata na kumuua kwa mikono yangu. Kwanza atakuwa yupo hapa hapa Zambia, cha kwanza kutoa taarifa polisi na kisha waanze kumsaka huku nikiwandaa vijana wangu wanifanyie kazi ya kumsaka pia. Ataiona hii nchi kuwa mbaya” Mzee Mbwana alisema huku akionekana kuwa na hasira. Baada ya kuongea kwa dakika kadhaa, akaingia ndani ya gari lake na kuondoka mahali hapo.ira kali.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Je nini kitaendelea?
Je Mzee Mbwana atafanikiwa kumpata Peter na kumuua?
Je peter ameuawa?
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment