Simulizi : Mungu Pekee Ndiye Atakayenisamehe
Sehemu Ya Tatu (3)
Ilipoishia jana..
akaanza kupiga hatua kuondoka, kilio cha kwikwi kikaanza kusikika, alikuwa amemkosa Albertina, wakati mwingine alijiona kuwa ndotoni ambapo baada ya muda angeamka na kumkuta Albertina akiwa pembeni yake.
“ALBERTINA...!” Kelvin alilitaja jina hilo kwa sauti huku akionekana kama mtu aliyechanganyikiwa.
Songa nayo sasa…
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nchi ya Mexico ilikuwa kwenye matatizo makubwa sana kwa wakati huo. Nchi ikaonekana kuharibika sana na matatizo mengi yakaonekana kuikumba nchi hiyo ambayo ilikuwa na wananchi zaidi ya milioni mia moja na kumi. Kila siku watu walikuwa wakizaliwa kwa wingi kuliko kufariki, vijana walikuwa wakiongezeka sana mitaani lakini ajira zilikuwa zikikosekana kabisa.
Rais aliyepita wa nchi hiyo, Bwana Salvador alikuwa ameziachia sana fedha, wananchi walikuwa na fedha nyingi sana katika akaunti yao kiasi ambacho fedha yao ikashuka sana thamani. Kila siku watu walikuwa wakitumia sana fedha, wananchi wakawa na fedha nyingi mno kuliko serikali jambo ambalo likaonekana kusababisha matatizo makubwa sana.
Nchi haikupiga hatua kimaendeleo, kila mtu alikuwa na fedha na hivyo hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akihitaji kazi. Uongozi wa Bwana Salvador ulikuwa mbaya sana, ulikuwa umeruhusu kiasi kikubwa sana cha fedha kukaa mikononi mwa wananchi kuliko serikali. Miaka ikaendelea kwenda mbele zaidi, watu waliendelea kuwa na fedha sana huku uchumi wa nchi hiyo ukizidi kushuka kila siku.
Marekani ikaingilia kati, na si Marekani tu bali hata Umoja wa Mataifa nao ukaingilia kati. Suala la kushuka uchumi nchini Mexico lilionekana kuwaumiza vichwa wamarekani. Walikuwa wakiitegemea Mexico katika mambo mengi sana, walikuwa wakiwataka wananchi wa mexico wawafanyie kazi katika vuwanda vyao ambavyo vilikuwepo nchini humo lakini kwa kipindi hicho kila mtu alikuwa akiacha kazi na hivyo viwanda kudorora.
Kila mtu alikuwa na fedha mkononi hivyo hakukuwa na umuhimu wa kufanya kazi. Hayo ndio maisha ambayo walikuwa wakiyatamani Wamexico, kila siku walikuwa wakiishi maisha ya starehe tu. Miaka ikakatika zaidi mpaka kufikia kipindi ambacho muda wa kukaa madarakani wa Bwana Salvador ulipokwisha na ndipo Marekani ikamuweka mtu wao kisiri, huyu alikuwa Puto Mendez.
Kitu cha kwanza alichoambiwa ahakikishe kinafanyika ni kuzichukua fedha zote kutoka kwa wananchi na kuzileta kwa serikali yake. Hilo ndilo lilikuwa sharti la kwanza ambalo Bwana Puto alitakiwa kulifanyia kazi. Kwake wala halikuonekana kuwa tatizo, kwa sababu alikuwa amepewa mipango mingi ya kufanya kutoka kwa Wamarekani akahakikisha jambo hilo linafanyika kwa haraka sana.
Kitu cha kwanza akapandisha bei ya bidhaa madukani na sehemu nyingine, fedha ambazo zilikuwa zikiingia serikalini zikazuiliwa kutoka. Wananchi walizitumia fedha kwa kununua vitu ambavyo vilikuwa vimepanda bei mpaka pale ambapo fedha zao zilipoanza kupungua. Kwa sababu wengi hawakuwa wakifanya kazi, wwakaishiwa na fedha na hapo ndipo ambapo walifikiria jambo moja tu, kutafuta kazi.
Bwana Puto hakuishia hapo, kila siku alikuwa akiendelea na staili hiyo hiyo, ndani miaka miwili, fedha zote ambazo zilikuwa kwa wananchi zikarudi serikalini na hivyo wananchi kutokuwa na fedha za kutosha. Hilo ndilo ambalo Wamarekani walikuwa wakilitaka, wananchi wa Mexico wakaanza kutafuta fedha kwa nguvu zote, wengi wakaanza kurudi kazini kwani bila kurudi kazi hakukuwa na uhakika wa kupata fedha.
Wananchi wakaanza kumiminika katika viwanda vilivyokuwa chini ya Wamarekani na kisha kuanza kufanya kazi, hivyo ndivyo ambavyo Wamrekani walivyokuwa wakitaka, walitawa Wamexico wawafanyie kazi katika viwanda vyao. Fedha ikawa ngumu kupatikana, wananchi wa Mexico wakaanza kupita katika wakati mgumu, wakati wa kutafuta fedha kwa jasho kubwa.
Hapo ndipo ambapo watu wengine wakaanza kufanya biashara za magendo huku wengine wakidiriki hata kutoroka na kuelekea Marekani. Mexico ilikuwa ikipita katika ugumu sana, mishahara maofisini ilikuwa imepunguzwa, hiyo yote ilikuwa ni kuziacha fedha ziendelee kuwa serikalini tu.
Fedha ikawa ngumu kupatikana, wananchi wakalia sana, Bwana Puto akaonekana kuwa mtu mbaya ambaye alikuwa akifurahia kuwaona wananchi wake wakiangaika kila siku. Kutokuwa na fedha ndipo kulipopelekea nchi kutawaliwa na rushwa. Mambo mengi ambayo yalikuwa yakitakiwa kufanyika kwa wananchi kihalali yalikuwa yakifanyika kimagendo, hospitalini madaktari walikuwa wakichukua rushwa, shuleni walikuwa wakichukua rushwa, yaani kila kona rushwa ilikuwa imevamia.
“Fungua buti la gari lako” Mwanajeshi yule alimwambia Bwana Maxwell.
Akili yake kwa wakati huo ikafunguka na kuanza kukumbuka mambo mengi, alikumbuka kwamba katika kipindi hicho nchi ya Mexico ilikuwa katika wakati mgumu sana, fedha zilikuwa adimu sana kupatikana, rushwa ilikuwa imetawala sana na hivyo kuona kwamba hiyo ilikuwa ni nafasi yake ya kutoa rushwa ili apite.
Bwana Maxwell hakutaka kujiuliza, kitu cha kwanza alichokifanya ni kuchukua kibunda cha dola elfu ishirini na kisha kukitupa juu ya buti la gari, wanajeshi wale walipokiona kibunda kile cha fedha, macho yakawatoka, wakaanza kuzitamani fedha zile.
“Dola elfu ishirini hizo hapo. Mnasemaje?” Bwana Maxwell aliwaambia na kuwauliza.
“Mmmh! Una uhakika ni dola elfu ishirini?” Mwanajeshi yule aliuliza, tayari akaonekana kubadilika, fedha zikawa zimelegeza msimamo wake, si wake tu, hata wale wenzake.
“Nina uhakika” Bwana Maxwell aliwaambia, akakirusha tena kibunda kingine, kilikuwa ni dola nyingine elfu ishirini.
“Nyingine hizo. Hizo za kwanza ni za kuniruhusu kupita na hizo za pili ni za usumbufu” Bwana Maxwell aliwaambia na kisha kurudha kibunda cha tatu.
“Hizo nyingine ni dola ishirini endapo mtaniruhusu kupita bila kunipekua, hasa kwenye buti la gari langu, nataka kuwahi” Bwana Maxwell aliwaambia.
“Hakuna tatizo” Mwanajeshi yule alimwambia Bwana Maxwell, alikuwa amewaachia dola elfu sitini, kwa wao wanne kwanza kulikuwa na uhakika wa kuchukua dola elfu kumi kumi kabla ya hizo nyingine kuzipiga pasu.
Fedha zilionekana kuwa msaada mkubwa kwake, hakukuwa na mwanajeshi ambaye alikumbuka kulipekua buti la gari lake, wakamruhusu kuingia nchini Mexico ambapo baada ya umali wa kilometa nne, akasimamisha gari na kumtoa Alan ambaye akatoka na kukaa kiti cha mbele.
“Imekuwaje?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Wewe unahisi imekuwaje?”
“Nilisikia kuhusu fedha”
“Nikwambie kitu”
“Niambie”
“Nimeacha kiasi cha dola elfu sitini pale ili wewe uingie nchini Mexico” Bwana Maxwell alimwambia Alan huku akionekana kuumia.
“Usijali. Nitakulipa mara mbili zaidi tukirudi Marekani” Alan alimwambia Bwana Maxwell.
“Hakuna tatizo. Hapo sawa”
“Kwa hiyo uliwapa rushwa?”
“Yeah! Nilijua tu kwamba nchi hii inanuka rushwa” Maxwell alimwambia Alan na wote kuanza kucheka, tayari walikuwa wameingia nchini Mexico.
****
Kelvin alikuwa akitembea kwa mwendo wa taratibu kurudi nyumbani kwao, kichwa chake kilikuwa na mawazo mengi juu ya msichana Albertina. Moyoni mwake alikuwa ameumia kupita kawaida mara baada ya kuambiwa kwamba Albertina alikuwa amekwenda nchini Marekani na kuolewa na mzungu. Majuto hayakutoka moyoni mwake, kila wakati alikuwa akijutia kitendo chake cha kumkubalia mama yake na kisha kumuacha Albertina.
Majuto yale ndio ambayo yalimpelekea kuwa na hasira tele, alimchukia mama yake kwani aliamini kwamba huyo ndiye alikuwa chanzo cha kila kitu kilichokuwa kimetokea katika maisha yake. Albertina, msichana ambaye alikuwa akimpenda sana kwa wakati huo alikuwa nchini Marekani. Kichwa chake hakikuishia hapo, kikaanza kuleta picha mbalimbali, alikuwa akimuona Albertina akiwa amesimama kanisani pamoja na mzungu huku wakifunga pingu za maisha.
Albertina alikuwa amependeza ndani ya shela lake huku mzungu huyo ambaye hakuwa akimfahamu akiwa amevaa suti nzuri nyeusi. Moyo wake ulizidi kumuuma zaidi, alikuwa akitamani kumtoa mzungu na kujiweka yeye. Hali yake ya kutokuwa na msimamo ndio ambayo ilikuwa imesababisha kila kitu kilichokuwa kimetokea katika maisha yake.
Mawazo yalikuwa lukuki, kuna wakati alikuwa akipigiwa honi na magari ambayo yalikuwa yamefika karibu na miguu yake. Hakuwa akiyaona magari hayo, kwa jinsi kichwa chake kilivyokuwa na mawazo hakuwa na uwezo wa kutambua alikuwa akielekea upande upi, wakati mwingine alijiona kama ngeweza kukosea njia na kuelekea sehemu ambayo hakutakiwa kwenda.
“Mama...yote kayataka mama haya” Kelvin alijisemea huku akionekana kukasirika.
Mara baada ya mwendo mrefu wa kutembea, Kelvin akafika nyumbani, kitu cha kwanza akajikalisha kochini, alikuwa ameuinua uso wake juu, bado alikuwa akiendelea kuwa na mawazo lukuki kichwani mwake. Hasira hazikumtoka, bado alikuwa akimchukia sana mama yake kwani aliona kuwa huyo ndiye alikuwa chanzo cha kila kitu kilichokuwa kimetokea.
Baada ya dakika kadhaa, Bi Agnes akafika mahali hapo, alipomuona Kelvin amekaa huku akionekana kuwa na mawazo, akalisogelea kochi lile na kisha kumshika begani kitendo ambacho kilimshtua Kelvin kutoka katika lindi la mawazo.
“Kuna nini?” Bi Agnes alimuuliza Kelvin.
Kitendo cha kumuona mama yake kilimtia hasira zaidi, hasira zake zikaendelea kumjaa moyoni kiasi ambacho akaona endapo angeongea lolote mahali pale basi maneno hayo yangekuwa ni matusi tu. Bi Agnes hakuonekana kuwa na furaha, kijana wake alikuwa kwenye hasira kali, alitamani ajue ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea katika maisha ya kijana wake.
“Kelvin mtoto wangu, kuna nini?” Bi Agnes alimuuliza Kelvin.
“Umenimaliza mama” Kelvin alimwambia mama yake huku machozi yakianza kumtoka.
“Kuna nini tena jamani?”
“Umenimaliza mama. Albertina ameolewa. Albertina amekwenda Marekani kuolewa” Kelvin alimwambia mama yake maneno ambayo yalionekana kumshtua.
“Amekwenda Marekani kuolewa?”
“Ndio”
“Kakwambia nani?”
“Haijalishi kaniambia nani, wewe jua kwamba Albertina amekwenda Marekani kuolewa” Kelvin alimwambia mama yake kwa hasira.
“Usijali, Lucy yupo”
“Lucy yupo...unasema Lucy yupo, atanisaidia nini? Lucy atanisaidia nini? Hivi unafikiri ataweza kuniletea furaha ambayo nilikuwa nayo katika kipindi cha nyuma? Hivi unafikiri ataufanya moyo wangu kuwa na furaha pamoja na kupata faraja kama niliyoipata kwa Albertina? Umenimaliza mama...umenimaliza mama” Kelvin alimwambia Bi Agnes.
Kelvin alikuwa amebadilika, alionekana kuwa na hasira kwa kila kitu kilichokuwa kimetokea, maisha yake bila Albertina kwa wakati huo yalionekana kuwa si kitu kabisa. Maisha ya furaha ambayo aliishi na Albertina katika kipindi cha nyuma yakabakia kuwa kama historia katika maisha yake, historia ambayo kamwe isingeweza kujirudia.
“Nitajiua” Kelvin alisema.
“Unasemaje”
“NITAJIUA” Kelvin alirudia neno lake, neno ambalo lilimfanya Bi Agnes kuchanganyikiwa, mtoto wake wa pekee alikuwa akitaka kujiua, kumkosa Albertina, kuikosa furaha, kukosa faraja na tumaini ndvyo vitu ambavyo vilimpelekea kufikiria kitu kimoja tu kwa wakati huo, KUJIUA.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Safari bado ilikuwa ikiendelea kama kawaida, katika kipindi hicho kila mmoja alionekana kuwa na furaha tele, kitendo cha kuvuka mpakani bila tatizo lolote kilionekana kuwafurahisha wote wawili. Bado walikuwa wakiendelea kupiga stori za hapa na pale huku lengo lao katika kipindi hicho ni kufika katika jiji kubwa la Monterrey.
Barabara ilikuwa nzuri japokuwa hapo walipokuwa wakipita kulionekana kama pori fulani ambalo halikuwa kubwa sana. Kulikuwa na kona kona nyingi na ni mara chache sana walikuwa wakipishana na magari mengine ambayo yalikuwa yakielekea mpakani. Maongezi ndicho kilikuwa kitu kikubwa ambacho kiliwafanya kuwa kuiona safari yao kuwa fupi japokuwa ukweli ni kwamba safari yao ilikuwa ndefu.
Walitumia muda wa masaa matatu na ndipo walipofanikiwa kuingia katika mji mdogo wa Sabinas Hidalgo. Hapo, hawakutaka kuunganisha safari yao, walichokifanya ni kuteremka kutoka garini na moja kwa moja kuelekea hotelini ambapo wakapata chakula na kisha kuelekea katika kituo cha mafuta, wakajaza gari lao mafuta na kisha kuondoka mahali hapo.
“Tunaweza kutumia muda gani mpaka kufika Monterrey?” Alan aliuliza swali.
“Masaa kumi na mbili”
“Mmmh! Kwa hiyo itatupasa kufika sehemu na kulala?”
“Ndio. Ni saa saba mchana kwa sasa, nadhani tutafika Salinas Victoria baada ya masaa manne, baada ya hapo tutaingia Parque Grutas na kisha kuingia Monterrey” Bwana Maxwell alimwambia Alan.
“Sawa”
“Utarudi baada ya muda gani ukishaingia huko?” Bwana Maxwell alimuuliza Alan.
“Ninakwenda mara moja, nitakaa siku moja, baada ya hapo tutarudi Marekani na kisha nitaondoka kuelekea nchini Tanzania” Alan alimwambia Bwana Maxwell.
“Tanzania! Ni wapi huko? Asia, Afrika au sehemu gani?” Bwana Maxwell alimuuliza Alan.
“Afrika. Hauifahamu?”
“Hapana”
“Inakupasa uifahamu hasa kwa watu kama nyie ambao mnahusika na mambo mengi ya kiserikali” Alan alimwambia Maxwell.
“Hebu niambie ni sehemu gani, huwa ninaliona sana hilo jina” Bwana Maxwell alimwambia Alan.
“Unaufahamu mlima wa Kilimanjaro?” Alan alimuuliza Bwana Maxwell.
“Ndio”
“Sasa huo mlima upo Tanzania?”
“Sikuwa nikifahamu hilo, nilichokuwa nikikifikiria ni kwamba mlima ule umechukua jina la nchi, yaani nchi nayo inaitwa Kilimanjaro” Bwana Maxwell alimwambia Alan.
Walikuwa wakiongea hili na lile huku safari ikiendelea zaidi na zaidi. Shauku ya Alan ya kuingia nchini Mexico aliiona tayari ikiwa imekamilika na katika kipindi hicho alikuwa akitaka kumuona rafiki yake, Antonio tu. Kila wakati maswali yalikuwa yakiendelea kumiminika kichwani mwake juu ya onyo ambalo alipewa na baba yake la kufika nchini Mexico.
Hakujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea, hakujua sababu ambayo iliwapelekea wazazi wao kumkataza kuelekea nchini Mexico. Alan alikuwa akitaka kuona madhara ya kuelekea nchini Mexico, hakutaka kuendelea kubaki nchini Marekani na wakati nchi ya Mexico ilikuwa karibu yake. Alitamani sana kwenda nchini Mexico, pia alitaka kuona kitatokea nini mara baada ya kuingia huko.
“Kuna kitu najiuliza” Alan alimwambia Maxwell, walikuwa wamebakisha kilometa kumi kabla ya kuingia Salinas Victoria.
“Kitu gani?”
“Baba alikuwa akinizuia kuingia nchini Mexico”Alan alimwambia Bwana Maxwell.
“Umenikumbusha. Hivi kwa nini baba yako amekuzuia kuingia nchini Mexico?” Bwana Maxwell alimuuliza Alan.
“Hata mimi sifahamu ni kwa sababu gani. Baba alivyokwambia kwamba unichukue na kunirudisha Washington hakukuambia sababu?” Alan alimuuliza Bwana Maxwell.
“Hapana. Alinipa amri tu”
“Haukumuuliza kabisa?”
“Hapana”
“Kwa nini sasa?”
“Haikuwa ikinihusu, kilichokuwa kikinihusu ni kukurudisha Washington” Bwana Maxwell alimwambia Alan.
“Sawa. Nimekuelewa”
“Kwa hiyo hata wewe haujui sababu ya kukukataza kuja nchini Mexico?” Bwana Maxwell alimuuliza Alan.
“Hapana”
“Kwa nini haukumuuliza?”
“Mpaka sasa hivi nashindwa kuelewa sababu zilizonifanya kutokumuuliza” Alan alimwambia Bwana Maxwell ambaye alikuwa akiendesha gari kama kawaida.
“Na haukumuuliza hata mama?”
“Hapana”
“Sawa. Sasa kipi kinakupeleka huku Mexico?”
“Ninakwenda kumuona rafiki yangu”
“Nani?”
“Anaitwa Antonio. Huyu anafahamu sababu zilizomfanya baba kunizuia kuja nchini Mexico” Alan alimwambia Bwana Maxwell ambaye akaonekana kushtuka.
“Kivipi tena?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Yaani sijajua, sijajua ni kipi kinaendelea”
“Huyo Antonio ni ndugu yako?”
“Hapana. Ni rafiki yangu”
“Ndiye anayeishi hapo Monterrey?”
“Ndio”
“Ulimuuliza sababu iliyomfanya baba yako akuzuie kuingia nchini Mexico?” Bwana Maxwell alimuuliza Alan.
“Ndio”
“Alikujibu nini?”
“Hakutaka kuniambia ila alisema kwamba anafahamu” Alan alimwambia Bwana Maxwell.
“Inawezekana vipi yeye afahamu na wewe usifahamu? Alikwishawahi kuongea na baba yako?” Bwana Maxwell alimuuliza Alan.
“Ndio ila nilikuwa pamoja nao kila walipokuwa wakiongea”
“Sasa amejua vipi hiyo sababu?”
“Mimi mwenyewe ndicho kinachonishangaza, mwisho wa siku nikajiuliza kama wewe unavyojiuliza” Alan alimwambia Bwana Maxwell.
“Inaelekea kuna kitu kinaendelea nyuma ya pazia”
“Kitu gani?”
“Sikijui na hata wewe haukijui. Ila ukiniambia zaidi kuhusu huyu Antonio naweza nikagundua kitu” Bwana Maxwell alimwambia Alan.
“Antonio ni rafiki yangu”
“Sawa. Umeniambia hilo. Anaishi na nani huku Mexico?” Bwana Maxwell alimuuliza Alan.
“Na wazazi wake”
“Ulikwishawahi kumuona baba yake?”
“Hapana”
“Hata kukuonyeshea picha?”
“Hakuwahi kufanya hivyo”
“Huyo Antonio ni mtoto wa nani?”
“Baba yake anaitwa Sanchez”
“Sanchez nani?”
“Santana. Santana Sanchez” Alan alimwambia Bwana Maxwell ambaye akaonekana kushtuka.
“Unamaanisha huyu mzee ambaye ni tajiri mkubwa ambaye anamiliki kiwanda cha magari cha Nacho?” Bwana Maxwell alimuuliza Alan huku akimtolea macho.
“Ndio”
“Ooopppsss...sasa kwa sababu gani hakukwambia sababu yenyewe?”
“Sijui”
“Kuna kitu nimegundua”
“Kitu gani?”
“Labda niseme nimehisi”
“Umehisi kitu gani?”
“Huku unapokwenda si sehemu salama” Bwana Maxwell alimwambia Alan.
“Kwa nini? Umegundua nini?”
“Unajua ugomvi kati ya baba yako na mzee Sanchez?” Bwana Maxwell alimuuliza Alan.
“Hapana”
“Sawa. Najua hauwezi kujua. Ila kuna kitu kinaendelea. Ushawahi kutazama filamu ya Romeo and Juliet?” Bwana Maxwell alimuuliza Alan.
“Ndio”
“Uliziona familia mbili ya Capulet na Montigue walivyokuwa na uhasama?” Bwana Maxwell alimuuliza.
“Ndio”
“Familia zile ni sawa na familia zenu”
“Kivipi?”
“Zina uhasama”
“Haiwezekani. Sasa kisa ni nini?”
“Baba yako anamiliki kiwanda cha magari cha McLloyd, si ndio?”
“Ndio”
“Mzee Sanchez anamiliki kiwanda cha magari cha Nacho, si ndio?”
“Ndio”
“Sawa. Nadhani umekwishajua sababu”
“Sababu gani?”
“Kwani wewe ulitaka kujua kuhusu nini?”
“Mimi kukatazwa kuingia nchini Mexico”
“Unajua kwa sababu gani baba yako alikukataza?”
“Hapana”
“Ni kwa sababu utauawa. Antonio analifahamu hili, labda aliambiwa na baba yake na ndio maana hakutaka kukwambia” Bwana Maxwell alimwambia Alan.
Hapo ndipo Alan alipoonekana kupata picha juu ya kila kitu kilichokuwa kikiendelea, hapo ndipo alipokuja kugundua kwamba kulikuwa na ugomvi mkubwa kati ya familia yao na familia ya mzee Sanchez. Hiyo ndio ikaonekana kuwa sababu kubwa ambayo ilimfanya baba yake kumzuia kuelekea nchini Mexico. Akagundua kwamba mzee Sanchez angeweza kumuua kutokana na ugomvi ambao alikuwa nao na baba yake.
Alan hakuonekana kuelewa. Antonio alikuwa amesoma nchini Marekani kwa muda wa zaidi ya miaka mitatu lakini hakukuwa na baya lolote lile ambalo lilimtokea, alikuwa akiishi nae kama ndugu yake, alimpenda na hata wakati mwingine kuelekea nae nyumbani kwao na kuwaona wazazi wake. Alipolifikiria hilo, akaona kwamba mzee Sanchez asingeweza kumuua kwa sababu Bwana Maxwell hakufanya hivyo kwa mtoto wake, Antonio.
“Kwa hiyo?” Alan alimuuliza Bwana Maxwell.
“Turudi”
“Hapana. Hicho ni kitu kisichotokea. Kama tumeamua kusonga mbele, wewe tusonge mbele” Alan alimwambia Bwana Maxwell.
“Ila kuwa makini”
“Siwezi kufa. Antonio alikuwa akinitembelea sana nyumbani, kwa nini baba hakumuua? Hiyo ndio sababu itakayomfanya baba yake kutokuniua” Alan alimwambia Bwana Maxwell.
“Una uhakika?”
“Asilimia mia moja”
“Sawa. Tumekwishafika Salinas Victoria, tuchukue chumba hapa na kesho tuendelee na safari yetu. Tutatumia masaa matano tu na kuingia Monterrey” Bwana Maxwell alimwambia Alan.
“Sawa”
“Huyo Antonio anaishi wapi hapo Monterrey?” Bwana Maxwell alimuuliza Alan.
“Anaishi Espinosa. Unapafahamu?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Napafahamu sana. Huo ni mtaa wanaoishi matajiri tu nchini Mexico. Kuna wanawake wazuri sana na pia kuna cassino moja inaitwa Microplaza. Nimekwishacheza sana kamari huko. Najulikana sana kama wanavyomjua rais wao” Bwana Maxwell alimwambia Alan.
“Basi hakuna tatizo” Alan alimwambia Bwana Maxwell.
Hiyo ndio safari yao nzima ilivyokuwa, mpaka wanaingia Salinas Victoria, kila mmoja alionekana kuchoka sana, wakachukua vyumba. Bwana Maxwell hakutaka kutafuta cassino kwa ajili ya kwenda kucheza kamari, mwili wake ulikuwa umechoka sana, alichokifanya ni kununua pombe na kisha kuingia nazo chumbani.
Alan hakuonekana kuwa na amani, muda mwingi alionekana kuwa mtu mwenye mawazo mengi, kichwa chake kilikuwa kikijiuliza maswali mfululizo juu ya baba yake kutokumueleza ukweli kuhusiana na mzee Sanchez. Ukweli ambao alikuwa akiutaka kwa kipindi kirefu akawa amekwishaupata, alifahamu sababu ambazo zilimfanya baba yake kumzuia kuingia nchini Mexico.
Pamoja na kuupata ukweli huo, bado Alan hakutaka kuacha kumtembelea rafiki yake, Antonio, hakuona kama mzee Sanchez angeweza kumuua, alichukulia kila kitu kawaida, alivyoona, kwa sababu baba yake hakuwa amemuua Antonio katika vipindi vyote alivyokwenda nyumbani kwao basi hata mzee Sanchez asingeweza kumuua, hivyo ndivyo alivyokuwa akifikiria, hakujua, hakujua kwamba mzee Sanchez alikuwa tofauti, hakujua kwamba mzee Sanchez alikuwa na roho ya kinyama. Kila siku alikuwa akitamani sana Alan afike nchini Mexico ili akamilishe kile alichokuwa amekipanga. Muda na wakati huo, mzee Sanchez alikuwa akitamani kumuona Alan, sababu kubwa iliyomfanya kutamani hilo litokee lilikuwa ni kutaka kumuua.
Kelvin alikuwa amekata tamaa kabisa, hakuona kama kulikuwa na sababu ya kuendelea kuishi na wakati mtu ambaye alikuwa akimpenda kwa moyo wote hakuwa nae wakati huo na mbaya zaidi tayari alikuwa amepata mwanaume na kumuoa nchini Marekani. Moyo wake ukafunikwa na majonzi mazito, akakosa amani, furaha ikampotea katika maisha yake.
Kila siku akawa mtu wa kuziangalia picha ambazo alikuwa amepiga pamoja na Albertina. Picha zile zilimfurahisha kwa asilimia chache lakini zilimuumiza kwa asilimia kubwa moyoni mwake. Sura ya Albertina ilikuwa ikionekana katika picha zile lakini mtu huyo wala hakuwa pamoja nae tena katika kipindi hicho.
Alifanya matukio mengi pamoja na Albertina katika miezi kadhaa ipite na matukio yote hayo yalionekana kuwa kama historia fulani ambayo kamwe isingeweza kurudi maishani mwake. Aliumia, alikuwa na majonzi sana, kila kitu kilichokuwa kimetokea kati yake na Albertina alikuwa akimpa lawama mama yake.
Alimuona mama yake kuwa chanzo juu ya kile kilichokuwa kimetokea, almchukia mama yake, mapenzi yote ambayo alikuwa nayo juu ya mamayake yakawa yamemtoka moyoni mwake na katika kipindi hicho alikuwa akitamani kitu kimoja tu, kujiua.
Kelvin hakuona sababu ya kuendelea kuishi ndani ya dunia hii na wakati mtu ambaye aliamini kwamba angempa furaha katika maisha yake yote hakuwa pamoja nae, alihitaji furaha na hakutaka kuhuzunika tena na hiyo ndio sababu ambayo ilimpelekea kufikiria kitu kimoja tu kwa wakati huo, kujiua, kwani hilo ndio suluhisho ambalo aliliona katika maisha yake.
“Nitajiua tu, siwezi kuishi bila Albertina” Kelvin alijisemea.
Siku zikaendelea kwenda mbele. Mwili wake ukaanza kudhoofika kwa kuwa alikuwa akiishi kwenye maisha ambayo yalimuumiza na kumkumbusha mambo mengi ya nyuma, maisha ambayo yalimfanya kuwa katika lindi la mawazo. Albertina akawa amekaa katika moyo wake na hakutaka kuondoka, kila alipojaribu kutokumfikiria, Albertina hakutoka moyoni mwake.
Msichana Lucy hakuwa chaguo lake na ndio maana alishindwa kumletea furaha katika maisha yake. Alijitahidi kumpenda msichana huyo ili mwisho wa siku aweze kuwa na furaha kama aliyokuwa nayo katika kipindi cha nyuma pamoja na Albertina lakini kitu hicho hakikuweza kutokea. Lucy hakubadilisha kitu chochote moyoni mwake, alikuwa akimchukulia kuwa msichana wa kawaida sana katika maisha yake.
Siku zikakatika zaidi na zaidi lakini furaha ambayo alikuwa akiitaka irudi moyoni mwake haikuwa imerudi. Katika kipindi hicho chote Kelvin hakuwa akiongea na mama yake , Bi Agnes, chuki ambayo alikuwa nayo juu ya mama yake ilikuwa kubwa, hakuona kama kulikuwa na sababu ya kuongea na mwanamke huyo na wakati yeye ndiye alikuwa chanzo cha hali ambayo alikuwa nayo moyoni mwake.
“Mbona siku hizi umekuwa hivyo mpenzi?” Lucy alimuuliza Kelvin walipokuwa chumbani.
“Nimekuaje?”
“Unaonekana una mawazo sana, tatizo nini?” Lucy alimuuliza Kelvin ambaye akabaki kimya kwa muda.
“Nipo kawaida tu Lucy” Kelvin alimwambia Lucy.
“Hapana. Haupo kawaida. Huwa ninakukera?” Lucy alimuuliza Kelvin.
“Hapana”
“Sasa tatizo nini?”
“Hakuna tatizo”
“Naomba usinifiche, niambie ukweli” Lucy alimwambia Kelvin.
“Nipo kawaida tu”
“Sawa. Na mbona siku hizi unamchukia mama yako?” Lucy alimuuliza Kelvin.
“Nani kakwambia?”
“Mama mwenyewe”
“Hakukwambia sababu?”
“Hapana. Hebu niambie, sababu ni nini?”
“Kwa sababu amekuruhusu kuingia ndani ya maisha yangu” Kelvin alimwambia Lucy.
“Unamaanisha nini?Kuingia kwenye maisha yako ndio kunakufanya kumchukia mama yako?” Lucy alimuuliza Kelvin.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hiyo ndio sababu kubwa”
“Kwa hiyo haunipendi?”
“Nakupenda ila..”
“Ila nini?”
“Haukunipa kile nilichokuwa nakitarajia kukipata kutoka kwako” Kelvin alimwambia Lucy, akajiweka vizuri kochini.
“Kitu gani?”
“Furaha”
“Kwa hiyo sijakuletea furaha maishani mwako?”
“Hiyo ndio maana yangu”
Lucy akanyamaza kwa muda, akaanza kumwangalia Kelvin kwa macho ya mshangao. Maneno ambayo alikuwa ameongea Kelvin yalimuumiza sana. Alikumbuka kipindi cha nyuma, kipindi ambacho alikuwa akiongea na mwanaume huyo, alikuwa akipenda sana kutabasamu na kucheza michezo hii na ile kama wapenzi, hapo akagundua kwamba tabasamu ambalo Kelvin alikuwa akimuonyeshea halikuwa lile tabasamu ambalo lilimaanisha furaha moyoni mwake bali lilikuwa ni tabasamu la kinafiki.
“Nakupenda Kelvin. Naomba unioe” Lucy alimwambia Kelvin.
“Haiwezekani”
“Kwa nini?”
“Kwa sababu haiwezekani tu” Kelvin alimwambia Lucy.
Lucy akaonekana kuchoka, majibu ambayo alikuwa akiyatoa Kelvin mahali hapo yalionekana kumchosha na kumkera sana, alichokifanya ni kusimama na kisha kuanza kuufuata mlango, alipoufikia, akaufungua na kisha kusimama, akageuka na kumwangalia Kelvin.
“Umeniona takataka sio?” Lucy alimuuliza Kelvin, tayari alikuwa amebadilika na kuwa mwenye hasira nyingi.
“Inawezekana kwa sababu haukuwa chaguo langu” Kelvin alimjibu Lucy ambaye wala hakutaka kuendelea kubaki chumbani hapo, akaondoka zake.
Hicho ndicho ambacho alikuwa akikitaka Kelvin, hakuwa na mapenzi kabisa juu ya Lucy, alikuwa akimchukulia kuwa msichana wa kawaida sana na wala hakuwa na mapenzi yoyote juu yake. Mapenzi yake yalikuwa kwa mke wa mtu, Albertina ambaye katika kipindi hicho alikuwa nchini Marekani.
Mapenzi yakaendelea kumuumiza moyoni mwake, kadri siku zilivyokuwa zikizidi kusonga mbela na ndivyo ambavyo hamu ya kutaka kujiua ilivyokuwa ikizidi kuujaza moyo wake. Wakati watu wengine wakiendelea kupata furaha na faraja katika maisha yao, kwa upande wa Kelvin maisha yalionekana kuwa kama jehanamu, maisha bila ya kuwa na msichana aliyekuwa akimpenda yalionekana kumuumiza.
“Ninajiua leo” Kelvin alisema na kisha kutoka chumbani humo.
Hilo ndio lilikuwa lengo kubwa ambalo alikuwa amejiwekea moyoni mwake, kujiua. Hakutaka kuendelea kuvuta pumzi ya dunia hii ambayo ilionekana kuwa kama jehanamu katika maisha yake. Hakuona sababu ya kuendelea kuishi ndani ya dunia hii na wakati kila siku alikuwa akiendelea kupata maumivu na mawazo kumuumiza.
Safari yake hiyo ikaishi dukani. Hakutaka kuchelewa, alichokifanya ni kununua kamba za katani tano na moja kwa moja kuelekea nyumbani kwao ambapo akaingia mpaka chumbani kwake na kisha kuanza kuzinganisha, si kwa urefu bali kwa upana, alitaka ziwe ngumu ili afanye kile alichokuwa amekusudia kukifanya muda huo.
Alipoona kwamba kamba zile zimekuwa tayari, Kelvin hakutaka kuendelea kusubiri, alichokifanya ni kuelekea jikoni ambapo akachukua kistuli, akarudi chumbani, akaichukua ile kamba na kisha kuifunga katika feni lililokuwa juu, alipojaribu kuning’inia katika mamba ile, haikukatika wala feni kung’oka, hapo akaona ipo safi.
“Nimechoka kuishi ndani ya dunia hii” Kelvin alisema katika muda ambao alikuwa akimalizia kufunga kitanzi, kilipokamilika, akaingiza kichwa chake kwenye kitanzi kile.
“Naomba unisamehe Mungu” Kelvin alisema, akashusha pumzi ndefu, akakisogeza kistuli kile pembeni na kisha kuanza kuning’inia, macho yakamtoka, mabega yakaanza kupanda juu, muda huo alikuwa amegawanyika, nusu ilikuwa jehanamu na nusu ilikuwa duniani.
*****
Asubuhi ilipofika, wakaamka na kisha kuendelea na safari yao ya kuelekea katika jiji la Monterrey. Mila mmoja kwa wakati huo akajiona akiwa amepata nguvu za kuendelea na safari hiyo kwani walikuwa wamebakisha masaa machache kabla ya kumalizia safari yao hiyo ambayo iliwachukua siku kadhaa njiani.
Stori za hapa na pale bado zilikuwa zikiendelea kama kawaida. Kwa kawaida kutoka Salinas Victoria mpaka Monterrey kuna umbali wa kilometa mia nne ambako kwa kuangalia mwendo ambao walikuwa wakiutumia, wakaona kwamba wangeweza kutumia masaa matano mpaka kuingia ndani ya jiji hilo.
Safari ya masaa mengi ilikuwa ikiendelea, waliendelea zaidi na zaidi huku barabara ikionekana kuwa na kona kona nyingi jambo ambalo lilimfanya Bwana Maxwell kupunguza kasi kila wakati. Kama ambavyo ilivyotakiwa kuwa na ndivyo ilivyokuwa, baada ya masaa matano wakafanikiwa kuingia katika jiji kubwa la Monterrey ambapo bila kupoteza muda, wakaanza kuelekea katika mtaa wa Espinosa.
Muda mwingi Bwana Maxwell alikuwa makini, alikuwa akiufahamu vizuri mtaa wa Espinosa na hiyo haikuwa mara yake ya kwanza kuingia ndani ya mtaa huo ila kitu ambacho kilikuwa kikimpa umakini mkubwa kwa wakati huo ni kumtafuta mtu yeyote ambaye alikuwa akikatiza sehemu na kumuuliza juu ya nyumba aliyokuwa akiishi mzee Sanchez.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mtaa ulikuwa kimya, mazingira yalikuwa mazuri huku kukiwa na nyumba nyingi zilioonekana kuwa za kisasa na kifahari sana. Muda wote huo Bwana Maxwell alikuwa akimtafuta mtu yeyote kwa ajili ya kumuulizia mahali alipokuwa akiishi mzee Sanchez. Walizunguka katika mtaa huo mkubwa wa kifahari kwa zaidi ya dakika tano na ndipo walipomuona mwanaume mmoja akitoka getini huku akiwa amevaa fulana nyekundu, kwa haraka bila kupoteza muda wakaanza kumfuata.
“cómo estás (Habari yako!)” Bwana Maxwell alimsalimia mwanaume huyo kwa kutumia lugha ya kispanyiola ambacho hakuwa akikifahamu sana.
“Estoy bien (Salama tu)” Mwanaume yule aliitikia.
“Estamos buscando a alguien. Dónde vive Sanchez (Kuna mtu tunamuulizia. Sanchez anaishi wapi?)” Bwana Maxwell alimuuliza mwanaume yule.
“Hay muchos Sanchez aquÃ. Cuál te necesita más? (Kuna Sanchez wengi wanaishi mahali hapa. Mnamtaka yupi?)” Mwanaume yule aliwauliza.
“Santana Sanchez” Bwana Maxwell alimjibu mwanaume yule.
Hiyo kidogo ikaonekana kuwa afadhali, alichokifanya mwanaume yule ni kuanza kuwaelekeza mahali kulipokuwa na nyumba ya mzee Sanchez. Bwana Maxwell alikuwa akisikiliza kwa makini sana kwani hakuwa akifahamu sana lugha ya kiispanyiola, hivyo alikuwa akilichambua neno moja baada ya jingine. Mwanaume yule alipomaliza kuwaelekeza, wakaondoka mahali hapo kuelekea kule walipokuwa wameelekezwa.
“Stop the car (Simamisha gari)” Alan alimwambia Bwana Maxwell ambaye akasimamisha gari na kumwangalia Alan.
“Is there anything you wanna do? (Kuna chochote unachotaka kukifanya?)” Bwana Maxwell alimuuliza Alan.
“I have to call Antonio (Nataka kumpigia simu Antonio)” Alan alimwambia Bwana Maxwell huku akichukua simu yake na kisha kuanza kubonyeza vitufe vya simu ile.
“What do you wanna tell him? (Unataka kumwambia nini?)” Bwana Maxwell alimuuliza Alan.
“Just wait (Subiri kwanza)” Alan alimwambia Bwana Maxwell ambaye akakaa kimya.
Simu ikaanza kuita, Alan alionekana kuwa kwenye presha kubwa, simu ile iliendelea kuita zaidi na zaidi, kitu ambacho alikuwa akikitaka ni kuisikia sauti ya Antonio ambapo angeanza kuongea nae na kisha kumtaarifu kwamba tayari alikuwa amekwishafika mahali hapo. Simu iliita kwa muda wa sekunde kadhaa, ikapokelewa na Alan kuanza kuongea na Antonio. Waliongea kwa muda wa sekunde kadhaa, Alan akakata simu na kisha kumwangalia Bwana Maxwell usoni.
“What next? (Nini kinafuata?)” Bwana Maxwell alimuuliza Alan.
“You have to go (Inabidi uondoke)
“Why? (Kwa nini?)”
“Nobody knows you are here. I will call you tomorrow (Hakuna anayejua kwamba upo hapa. Nitakupigia simu kesho)” Alan alimwambia Bwana Sanchez.
“Why? Just give me reasons, why do wanna me leave? (Kwa nini? Naomba unipe sababu, kwa nini unataka niondoke?)” Bwana Maxwell alimuuliza Alan.
“You have already done fiffty percent of your work. Now, its my turn to do mine (Tayari umekwishafanya asilimia hamsini ya kazi yako. Sasa hivi ni zamu yangu kufanya yangu)” Alan alimwambia Bwana Maxwell.
“So I have to leave? (Kwa hiyo natakiwa kuondoka?)”
“Thats right (Sawasawa)
“Should I leave with this car? (Natakiwa kuondoka na hili gari?)”
“No (Hapana)
“Ok! (Sawa)” Bwana Maxwell alimwambia Alan.
Bwana Maxwell hakutakiwa kubaki mahali hapo, alitakiwa kuondoka na kumuacha Alan pamoja na gari lile. Bwana Maxwell alionekana kushangaa lakini hakutaka kuuliza maswali zaidi, kwa sababu alikuwa akiufahamu sana mtaa huo wa Espinoza, akaanza kuelekea katika sehemu ambayo kulikuwa na cassino kubwa ya Microplaza kwa ajili ya kucheza kamari pamoja na kuangalia ni msichana yupi alikuwa akifaa kulala nae usiku wa siku hiyo kabla ya kupigiwa simu na Alan na kisha kumpa taarifa kwamba ni muda gani walitakiwa kuondoka kurudi nchini Marekani.
****
Alan alikuwa ameongea na Antonio na kumueleza kwamba tayari alikuwa amekwishafika mahali hapo na tayari alikuwa amekwishaelekezwa mahali alipokuwa akiishi na hivyo alikuwa akitaka kumfuata huko kwa ajili ya kumtembelea. Antonio akaonekana kushtuka sana, hakuamini kama kweli Alan alikuwa amedhamiria kama ambavyo alikuwa amemwambia na mpaka muda huo kuwa ndani ya nchi ya Mexico, ndani ya jiji la Monterrey katika mtaa wa Espinoza.
Antonio hakuwa na jinsi, alichokifanya ni kumkaribisha ndani ya nyumba yao. Alan akaonekana kufurahi, akaliwasha gari na kisha kuondoka mahali hapo huku akimuona Bwana Maxwell akiondoka kuitafuta cassiono ya Microplaza kwa ajili ya kwenda kucheza kamari. Alan hakuchukua muda mrefu, akawa amekwishafika nje ya jumba hilo la kifahali, alipopiga honi, geti likafunguliwa, ujio wake ulikuwa umekwishatolewa kabisa kwa walinzi.
Alan akaliingiza gari lile ndani ya jumba lile la kifahari, walinzi zaidi ya saba wenye bunduki kali walikuwa wamesimama ndani ya eneo la nyumba hiyo. Kila mmoja alionekana kuwa makini mahali hapo, walikuwa wakiliangalia sana gari lile aliloingia nalo Alan, halikuonekana kuwa gari ambalo lilistahili kuingia ndani ya eneo la nyumba hiyo.
Alan aliposimamisha gari, mlango ukafunguliwa na mlinzi mmoja na kisha kuteremka. Moja kwa moja akakaribishwa ndani ya nyumba hiyo na kuanza kuufuata mlango na kuingia. Katika kipindi chote hicho Alan alionekana kushangaa, ni kweli kwamba alikuwa amemtaarifu Antonio kuhusiana na ujio wake na alimwambia kwamba alikuwa nyumbani, swali ambalo lilikuja kichwani mwake ni kwa sababu gani Antonio hakuonekana mahali hapo?
Alan akakaa juu ya kiti kimoja ambacho kilionekana kuwa cha kifahari ndani ya sebule hiyo. Katika kila kona kulikuwa na kamera ndogo za CCTV ambazo zilikuwa zikiendelea kuchukua kila kitu kilichokuwa kikiendelea mahali pale. Wala haukupita muda mrefu, Bwana Sanchez akatokea mahali hapo, mkononi alikuwa na bunduki tena huku akiwa ametangulizana na vijana wake walioonekana kutokuwa na roho ya huruma, hawakutaka kuuliza swali wala kusikia kitu chochote kile, walipofika mahali pale, wakamchukua Alan ambaye akaanza kupiga kelele za kuomba msaada huku akiliita jina la Antonio.
“Mpelekeni ardhini)” Bwana Sanchez aliwaambia vijana wale waliombeba Alan na kisha kuanza kuondoka nae mahali hapo.
Moja kwa moja wakaelekea sehemu ambayo kulikuwa na mlango wa kuelekea katika chumba kilichokuwa chini ya ardhi, chumba ambacho kilikuwa na kazi ya kuwatesa watu mbalimbali ambao walikuwa wakileta masihala kwa Bwana Sanchez. Walipoufikia mlango wa chumba kile, wakaufungua na kisha kumsukumia Alan ndani, chumba kilikuwa na giza kubwa, taa zilipowashwa, ni michirizi ya damu tu ndio ambayo ilikuwa ikionekana ukutani pamoja na kiti cha umeme pamoja na kiti ambacho sehemu ya kukaliwa ilikuwa wazi, na hicho kilikuwa kiti maalumu kilichokuwa kikitumika kwa kuzipiga korodani za mtu aliyekamatwa wakati akikalishwa mtupu kitini pale, kilikuwa ni kama kile kiti ambacho kilitumika katika muvi ya James Bond, Skyfall.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Bwana Kurt na mkewe walionekana kuwa na mawazo mengi, kitendo ambacho alikifanya Bwana Maxwell hakikuonekana kuwafurahisha kabisa. Wao walimwambia kwamba amchukue Alan na kisha kumrudisha Washington lakini badala ya kufanya hivyo alikuwa amefanya kinyume chake. Akili zao zilichanganyikiwa na hawakujua wafanye nini kwa wakati huo. Waliendelea kulala huku wakiwa wamekumbatiana mpaka asubuhi.
Asubuhi ilipofika, kitu cha kwanza walichokifanya ni kuanza kumtafuta Alan kupitia simu yake ya mkononi, hakuwa akipatikana kabisa jambo ambalo liliendelea kuwachanganya kupita kawaida. Hawakujua kama Alan alikuwa amezima simu kipindi chote hicho au alikuwa akiiwasha na kuwasiliana na watu wengine na kisha kuizima. Walikuwa wakihitaji kuongea nae kwa wakati huo na kumwambia ukweli juu ya sababu ambayo iliwafanya kumkataza kuelekea nchini Mexico.
“Bado haipatikani?” Bi Bertha alimuuliza mume wake ambaye kila wakati alikuwa akijaribu kumpigia simu Alan.
“Hapatikani”
“Ni nini kimempata mwanangu?” Bi Bertha aliuliza na kisha kuanza kutokwa na machozi.
“Subiri kwanza mke wangu, ngoja nimtafute Maxwell” Bwana Kurt alimwambia mke wake.
Bi Bertha alionekana kuwa na presha kubwa, kila wakati alikuwa mtu wa kulia tu huku akitaka kumuona tena mtoto wake. Muda mwingi alikuwa na wasiwasi juu -ya hali aliyokuwa nayo mtoto wake katika kipindi hicho, alikuwa akimpenda sana na hakutaka kumuona akipata tatizo lolote lile. Bwana Kurt alijaribu kumtafuta Bwana Maxwell, alimpigia simu zaidi na zaidi lakini napo majibu yalikuwa ni yale yale kama yaliyokuwa kwa Alan, simu haikupatikana.
Wasiwasi uliendelea kuwajaa mioyoni mwao, hawakutaka kurudi Washington mpaka pale ambapo wangesikia ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea. Siku hiyo ikapita na siku ya pili kuingia, bado walikuwa hapo Austin, siku ya tatu ikaingia na siku ya nne nayo kufika.
Siku hiyo ndio ilionekana kuwa siku mbaya sana kwao hasa mara baada ya kuona kulikuwa na namba ngeni ambayo ilikuwa ikiingia katika simu ya Bwana Kurt. Bwana Kurt hakutaka kuipokea haraka haraka, alichokifanya ni kubaki akiiangalia, aliiangalia kwa makini sana kiasi ambacho kilimfanya mke wake, Bertha kuwa na wasiwasi.
“Mbona haupokei simu?” Bi Bertha alimuuliza mume wake.
“Nina wasiwasi na simu hii” Bwana Kurt alimwambia mke wake.
“Wasiwasi wa nini?”
“Si namba kutoka nchini Marekani” Bwana Kurt alimwambia mke wake.
“Ni namba kutoka wapi?”
“Mexico” Bwana Kurt alijibu.
“Haina jinsi, ipokee tu” Bi Bertha alimwambia mumewe huku akionekana kuwa na wasiwasi zaidi.
Bwana Kurt akaipokea simu ile na moja kwa moja kuipeleka sikioni. Akakutana na sauti nzito, sauti ambayo wala haikuwa ngeni masikioni mwake, alikuwa mzee Sanchez.
****
Katika kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea Antonio hakuwa akikipenda kabisa. Hakutaka kabisa kumuona Alan akielekea Mexico kwa sababu alijua fika kwamba baba yake angeweza kumuua kutokana na uhasama ambao alikuwa nao kwa Bwana Kyrt. Antonio alikuwa amejitahidi kwa nguvu zote kumzuia Alan lakini Alan hakuonekana kuwa muelewa, kitu alichokuwa akikitaka ni kuelekea nchini Mexico tu.
“Anakuja” Antonio aliwaambia wazazi wake.
“Nani?” Bwana Sanchez alimuuliza Antonio.
“Alan”
“Unasemaje?”
“Alan anakuja nchini Mexico. Anakuja kunitembelea mahali hapa” Antonio aliwaambia wazazi wake.
“Unasema kweli?” Mzee Sanchez aliuliza kwa mshtuko.
“Ndio”
“Safi sana”
“Sikiliza baba, sitaki umfanye kitu chochote kile, Alan ni rafiki yangu sana, nisingependa kuona akiingia kwenye matatizo wakati anakuja kunitembelea” Antonio alimwambia baba yake.
“Sikiliza Anto......”
“Nakuomba uniahidi kwamba hautomfanya kitu chochote kile” Antonio alimwambia baba yake.
“Huyu ni mtoto wa adui yetu Antonio”
“Ni mtoto wa adui yako lakini si adui yako”
“Yeye ni uzao wa adui yetu, tukimuacha inamaanisha kwamba uzao wake utaongezeka na kuwa na kutufanya kuwa na maadui wengi Antonio” Mzee Sanchez alimwambia mtoto wake, Antonio.
“Hapana baba. Sijakubaliana nawe”
“Huo ndio ukweli. Ni lazima tufanye kitu kama tusipofanya kitu kunaweza kukawa na tatizo baadae” Mzee Sanchez alimwambia Antonio.
“Hapana baba. Niahidi kwamba hautomfanya kitu chochote kibaya” Antonio alimwambia baba yake, mzee Sanchez.
“Ila......”
“Niahidi baba”
“Nakuahidi” Mzee Sanchez alimwambia Antonio.
Muda wote Antonio alionekana kuwa mwenye furaha tele, hakuamini kwamba katika kipindi hicho Alan alikuwa safarini kuingia ndani ya nyumba hiyo. Moyo wake ukajawa na furaha tele, hakuamini kwamba alikuwa ameunguziwa mzigo mkubwa wa kumtafuta Alan. Japokuwa alikuwa amemuahidi mtoto wake kwamba asingeweza kumfanya kitu chochote kile kibaya Alan lakini moyo wake ulikuwa ukikataa kabisa, alijiona kuwa na kila sababu ya kumjeruhi Alan, na ikiwezekana kumuua kabisa.
Alichokifanya mzee Sanchez ni kuwandaa vijana wake wa kazi tayari kwa kuifanya kazi hiyo. Viaja watatu ambao aliamini kwamba walikuwa na roho mbaya wakaandaliwa na ni Alan tu ndiye ambaye alikuwa akisubiriwa nyumbani hapo.
Siku zikakatika, mzee Sanchez kila siku alikuwa na kazi kubwa ya kumshawishi mtoto wake, Antonio akubaliane nae kwamba Alan alikuwa mtoto wa adui wa familia hiyo na ilitakiwa kuuawa ili kupunguza maadui katika maisha yake ya mbele. Antonio alionekana kuwa mgumu kukubaliana nae lakini mwisho wa siku, akaonekana kulegeza kamba na yeye kukubaliana na baba yake kwa kuamini kwamba Alan alikuwa mtoto wa adui yao na hivyo alitakiwa kuuawa.
“Hakuna tatizo” Antonio alimwambia baba yake.
“Safi sana. Hapa ninatengeneza maisha yako ya baadae, tusipofanya hivi utaweza kupata tatizo huko mbele na ikiwezekana huyu huyu Alan kukuua wewe” Mzee Sanchez alimwambia Antonio.
Baada ya siku moja, Alan akawa amekwishafika Mexico na alikuwa njiani kuelekea nyumbani kwa mzee Sanchez. Alipofika katika mtaa wa Espinoza, moja kwa moja akampigia simu Antonio ambaye akamueleza baba yake kwamba tayari Alan alikuwa ndani ya mtaa huo na ni muda wowote ule angeweza kuingia ndani ya nyumba hiyo.
“Ondoka” Mzee Sanchez alimwambia Antonio.
“Niende wapi?”
“Alan hatakiwi kukuona”
“Sasa ndio mpaka niondoke?”
“Basi kakae hata chumbani kwako”
“Hakuna tatizo” Antonio alimwambia baba yake.
Vijana ambao walikuwa wameandaliwa wakawekwa tayari kwa ajili ya kukamilisha kazi, walinzi wakapewa taarifa juu ya Alan na hivyo hawakutakiwa kumuuliza kitu chochote kile zaidi ya kumkaribisha kuingia ndani ya nyumba hiyo, walinzi wakaonekana kuelewa, na baada ya dakika kadhaa Alan kufika ndani ya nyumba hiyo, hawakumuuliza kitu, wakamruhusu kuingia ndani ya eneo la nyumba hiyo.
“Amefika” Mzee Sanchez aliwaambia vijana wake huku akiwa anamwangalia Alan katika televisheni yake, picha ilichukuliwa kwa kutumia kamera ndogo za CCTV ambazo ziliwekwa katika kila kona pale sebuleni.
Mzee Sanchez hakutaka kubaki chumbani pale, alichokifanya ni kutoka pamoja na vijana wake ambao walikuwa na miili mikubwa na kwenda sebuleni ambapo walimkuta Alan akiwa amekaa kochini huku akionekana kutokuwa na wasiwasi wowote ule. Kbla ya kuongea kitu chochote kile, Mzee Sanchez akawaagiza vijana wale kumchukua Alan na kisha kuanza kumpeleka katika chumba maalumu cha mateso, katika kipindi chote hicho Alan alikuwa akipiga kelele za kumuita Antonio aje kumsaidia.
Hapo moyo wake ukaonekana kuridhika, kile alichokuwa akikihitaji kwa kipindi kirefu tayari alikuwa nacho chumbani kwangu. Hakutaka kuchelewa, alitaka kumpa taarifa Bwana Kurt juu ya mtoto wake ambaye katika kipindi hicho alikuwa mikononi mwake. Alichokifanya ni kumpigia simu na kisha kumwambia ukweli.
“Nimefurahi kijana wako kuja Mexico” Mzee Sanchez alimwambia Bwana Kurt.
“Sikiliza Sanchez....”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hapana. Siwezi nikakusikiliza. Kama unamtaka mtoto wako, njoo umchukue” Mzee Sanchez alimwambia Bwana Kurt.
“Nakuomba usimfanye kitu, ni mtoto wangu pekee”
“Najua. Kama kweli unamhitaji, njoo umchukue” Mzee Sanchez alimwambia Bwana Kurt.
“Utakapokuja, njoo peke yako, kinyume na hapo, nitakuletea kichwa cha mtoto wako” Mzee Sanchez alimwambia Bwana Kurt simuni.
“Unamaanisha nini?”
“Namaanisha utakapotua Mexico na mtu yeote tofauti ya wewe mwenyewe, utaikuta maiti ya mtoto wako tu” Mzee Sanchez alimwambia Bwana Kurt.
Huo ndio ulikuwa mpango ambao ulikuwa kichwani mwake katika kipindi hicho. Kwa kipindi kirefu sana alikuwa akimhitaji Alan na siku hiyo mtu huyo tayari alikuwa ameingia mikononi mwake. Hakumpenda Alan na wala hakuwapenda wazazi wake. Sababu kubwa ambayo ilimpelekea kumhitaji Bwana Kurt ni kwamba alikuwa akitaka kuwaua wote wawili, hakutaka kumuacha yeyote akiwa hai. Ubishi wa Alan ukaonekana kusababisha mambo mengine.
Bwana Kurt alikuwa amechanganyikiwa, simu ambayo aliipokea kutoka kwa mzee Sanchez ilionekana kumchanganya sana. Alibaki akitetemeka kwa presha, hakuamini kwamba jitihada zote ambazo zilikuwa zimefanyika za kuhakikisha kwamba Alan haingii ndani ya nchi ya Mexico zilikuwa zimeshindikana na muda huo alikuwa ndani ya nchi hiyo.
Alibaki akiiangalia simu ile ambayo ilikuwa mkononi mwake, hakuamini kama angeweza kupokea simu kutoka kwa mzee Sanchez ambaye mpaka muda huo alikuwa akimshikilia mtoto wake, Alan. Bi Bertha hakuelewa ni kipi kilichokuwa kikiendelea, alichokifanya ni kumshika bega mume wake.
“Kuna nini?” Bi Bertha alimuuliza.
“Alan”
“Amefanya nini? Amepatikana?”
“Hapana. Amefika Mexico” Bwana Kurt alimwambia mkewe.
“Mungu wangu! Amefika Mexico?”
“Ndio, tena mbaya zaidi ametekwa na Sanchez” Bwana Kurt alimwambia mke wake.
“Unasemaje?”
“Ndio hivyo mpenzi”
“Nani amekupigia simu?”
“Sanchez”
“Amesemaje?”
“Amenipa taarifa kwamba amemteka mtoto wangu” Bwana Kurt alimwambia mke wake kwa sauti ya chini iliyojawa na majonzi.
“Unasemaje?”
“Amemteka mtoto wetu”
“Mungu wangu! Tuwataarifu polisi”
“Hapana. Usifanye hivyo”
“Kwa nini?”
“Atamuua Alan”
“Polisi ndio msaada uliobakia mpenzi”
“Ameniambia niende Mexico, tena peke yangu, hauoni kama ukiwaambia polisi anaweza hata kumuua?” Bwana Kurt alimwambia mke wake.
“Uende Mexico kufanya nini?”
“Sijajua. Ila ameniambia niende”
“Hapana mume wangu. Ni lazima uende na polisi” Bi Bertha alimwambia mume wake.
“Hilo ni kosa. Ameniambia nikienda na polisi atamuua Alan na kuniletea kichwa chake” Bwana Kurt alimwambia mke wake.
“Basi twende wote mpenzi”
“Hapana. Amekataa”
“Kwa nini amekataa?”
“Sijajua kwa sababu gani”
“Unahisi kuna amani huko?”
“Hapana. Amani haiwezi kuwepo”
“Sasa hauoni kama hiyo ni hatari?”
“Naiona hiyo hatari, haina jinsi mke wangu, ngoja niende huko” Bwana Kurt alimwambia mke wake, Bi Bertha.
“Nina wasiwasi mpenzi” Bi Bertha alimwambia mume wake huku machozi yakianza kumtoka.
“Haina jinsi, sisi tumekuwa chanzo cha kila kitu, tumemkataza Alan kuelekea nchini Mexico ila hatukumwambia sababu. Haina jinsi, lolote litakalotokea litakuwa limesababishwa na ujinga wetu” Bwana Kurt alimwambia mkewe, Bi Bertha.
Huo ndio ulikuwa wakati mgumu katika maisha yao, kitendo cha mtoto wao waliyekuwa wakimpenda, Alan kutekwa na mbaya wao kilionekana kuwasikitisha na kuwatia hofu mioyoni mwao, walikuwa wakifahamu fika kwamba mzee Sanchez hakuwa na masihala, chuki ambayo alikuwa nayo juu ya familia yao ilikuwa kubwa kiasi ambacho ingekuwa ngumu sana kumuacha Alan.
Bwana Kurt hakuwa na jinsi, kwa sababu alikuwa akimpenda kijana wake na alikuwa kitaka kumuona tena kwa mara nyingine tena, hakutaka kubaki nchini Marekani, alitakiwa kuelekea nchini Mexico kama alivyoambiwa. Hakuwa na sababu zozote za kuwataarifu polisi kwamba Alan alikuwa ametekwa kwani aliamini kwa kufanya hivyo lingekuwa kosa moja ambalo lingemfanya kutokumpata mtoto wake, Alan.
Siku iliyofuata Bwana Kurt akaianza safari yake ya kuelekea nchini Mexico kwa kutumia ndege yake ya kukodi. Muda wote ndani ya ndege alikuwa na majonzi, hakuonekana kuwa na furaha hata kidogo, kitendo cha kuelekea nchini Mexico kwa mzee Sanchez kilimaanisha kwamba siku hiyo ingeweza kuwa mwisho wa kila kitu katika maisha yake pamoja na mtoto wake ambaye alikuwa akimpenda sana, Alan.
Baada ya masaa matatu, ndege ile ya kukodi ilikuwa ikitua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa General Mariano Escobedo uliokuwa hapo Monterrey. Hali ya hewa haikuwa mbaya, ilikuwa ikifanana na Washington hivyo hakupata tabu sana. Bwana Kurt akaanza kupiga hatua huku lengo lake likiwa ni kuelekea nje ya jengo la uwanja wa ndege ambapo huko angejua ni kipi cha kufanya ila hata kabla hajatoka uwanja wa ndege, kulikuwa na gari ambalo lilisimamishwa umbali wa mita mia moja kutoka mahali amnapo ndege ile ilipokuwa imesimama.
Kijana mmoja ambaye alisimama nje ya lile gari la kifahari akaanza kupiga hatua za haraka haraka kumfuata, alipomfikia, akaanza kuongea nae na kumtaarifu kwamba alikuwa uwanja wa ndege kwa sababu alikuwa ameagizwa na mzee Sanchez kwa ajili ya kuja kumpokea.
“Mtoto wangu anaendeleaje?” Bwana Kurt alimuuliza kijana yule, walikuwa wawili tu ndani ya gari.
“Mtoto yupi?” Kijana yule aliuliza.
“Alan”
“Ndiye nani?”
“Mtoto wangu”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Wala simfahamu” Kijana yule alimjibu.
Bwana Kurt hakutaka kuongea kitu kingine kuhusu Alan kwani alijua kwamba inawezekana mzee Sanchez hakuwa amewaambia vijana wake wote kuhusu Alan, hivyo akabaki kimya. Safari ile iliendelea kwa muda wa dakika kumi, wakaingia katika mtaa wa Espanoza ambapo moja kwa moja wakaanza kuifuata njia ya kuelekea katika jumba kubwa la kifahari la mzee Sanchez, gari lilipofika nje ya geti, geti hilo likafunguliwa.
Bwana Kurt akaingiwa na wasiwasi zaidi, kitendo cha kukanyaga ndani ya nyumba ya mzee Sanchez kilimtia wasiwasi sana na alijua fika kwamba asingeweza kutoka salama ndani ya nyumba hiyo. Walinzi wote walikuwa bize, walionekana kutokuwa na habari juu ya kile ambacho kilikuwa kikiendelea mahali hapo.
Mlango wa kuingilia sebuleni ukafunguliwa, mzee Sanchez akatoka na vijana wake wa kazi ambao walionekana kupewa kazi ya kuwatesa watu wote ambao walikuwa wakipelekwa ndani ya nyumba hiyo hasa ndani ya chumba kile cha mateso. Bwana Kurt alipomuona mzee Sanchez, akaonekana kuchoka, hofu ikamuingia zaidi.
“Hatimae umekuja” Mzee Sanchez alimwambia Bwana Kurt huku akitabasamu.
“Mtoto wangu yupo wapi?”
“Usiwe na haraka, si unajua nina kazi na nyie” Mzee Sanchez alimwambia Bwana Kurt.
“Alan ahusiki kwa lolote lile, hajui chochote kinachoendelea” Bwana Kurt alimwambia mzee Sanchez.
“Familia yako inahusika, si wewe tu, uzao wako wote unahusika” Mzee Sanchez alimwambia Bwana Kurt.
“Nakuomba umuache mtoto wangu aondoke. Nimetii kila kitu na kuja mahali hapa. Nakuomba umruhusu aondoke” Bwana Kurt alimwambia mzee Sanchez.
“Sasa hapo nitakuwa nimefanya nini? Huo ni ujinga. Nitamuacha vipi aondoke na wakati nimepanga kuwaua wote wawili? Ni lazima niwaue, yaani shauku yangu ni kuwaona mkiuawa, tena kwa mkono wangu” Mzee Sanchez alimwambia Bwana Kurt.
Maneno yale yakaonekana kumtia hofu zaidi Bwana Kurt, uso wa mzee Sanchez ulionekana kumaanisha kila kitu ambacho kilikuwa kikitoka mdomoni mwake na hakuonekana kama alikuwa na chembe ya utani. Katika kipindi cha miaka mingi ambacho alikuwa akikisubiri, siku hiyo kikaonekana kufika na wote ambao alikuwa akiwahitaji walikuwa ndani ya himatya yake.
Alichokifanya mzee Sanchez ni kuwaagiza vijana wake ambao walikuwa na asili ya Kirusi wamchukue Bwana Kurt na kisha kumpeleka ndani ya chumba kile cha mateso. Vijana wale hawakutaka kuchelewa, walichokifanya ni kuwafuata na kisha kumchukua Bwana Kurt na moja kwa moja kumpeleka ndani ya chumba hicho cha mateso.
Chumba kilikuwa na giza nene, Bwana Kurt hakuwa akiona kitu chochote ndani ya chumba hicho, taa zilipowashwa, mbele yake sakafuni kukaonekana kuwa na mtu ambaye nguo zake zote zilikuwa zimetapakaa damu. Hakutaka kujiuliza, akili yake ikamwambia kwamba mtu yule alikuwa mtoto wake, alichokifanya ni kumsogelea na kisha kumgeuza, alikuwa Alan.
Bwana Kurt akahisi maumivu makubwa moyoni mwake, akauhisi moyo wake ukiwaka moto. Ni kweli mtu ambaye alikuwa pale sakafuni alikuwa mtoto wake, Alan lakini hali ambayo alionekana kuwa nayo haikuonekana kuwa ya kawaida. Asilimia kubwa ya nguo ambazo alikuwa amezivaa zilikuwa zimetapakaa damu, uso wake haukuwa ukitamanika na kama haukuwahi kuona majeruhi wa ajali basi uasingeweza kumwangalia Alan mara mbili usoni.
Ilikuwa ni vigumu sana kumtambua, uso wake ulikuwa umeharibiwa vibaya, damu zilikuwa zimetapakaa usoni na katika kipindi hicho hakuwa amepata fahamu, alikuwa amezimia, hakuwa akijua kwamba baba yake alikwishafika ndani ya chumba hicho.
“Alan...Alan...Alan...” Bwana Kurt alimuita Alan huku akiwa amekiegemeza kichwa cha Alan mapajani mwake.
“Alan...Alan...Alan...” Bwana Kurt alizidi kuita lakini Alan hakutikisika, alikuwa amepoteza fahamu, kipigo ambacho alikuwa amepewa kilikuwa kikubwa.
*****
Bwana Maxwell alikuwa akijisikia furaha muda wote, hakuamini kwamba katika kipindi hicho alikuwa amerudi tena ndani ya Cassino kubwa ya Microplaza kwa ajili ya kucheza kamari pamoja na wenzake ambao alikuwa amewaacha kipindi kirefu kilichopita. Alionekana kuwa mwenye furaha kubwa kila wakati alipokuwa akiziangalia karata pamoja na fedha ambazo zilikuwa zimewekwa mezani.
Kama kawaida yake hakuwa na miwani usoni, wenzake wote ambao alikuwa akicheza nao walikuwa na miwani ambayo ilikuwa ikiwasaidia kuziangalia karata za wenzao bila kugundulika ila kwa Bwana Maxwell hali ikaonekana kuwa tofauti kabisa. Alionekana kuwa makini na alijitahidi kucheza kwa umakini mkubwa sana.
Wadau wengine ambao walikuwa wafuatiliaji wazuri wa mchezo wa poker walikuwa wakifuatilia kwa karibu sana. Watu wengine ambao hawakuwa wakipenda michezo mbalimbali ya kamari iliyokuwepo humo, macho yao yalikuwa yakiwaangalia wanawake ambao walikuwa wakicheza muziki huku wakiwa wanazunguka mamboma makubwa huku wakiwa mitupu miilini mwao.
Katika kila kitu ambacho kilikuwa kikionekana ndani ya cassino hiyo kilionekana kuwa fedha. Kucheza kamari kulihitajika fedha, kunywa vinywaji pia kulihitajika fedha na hata kuwasogelewa wanawake ambao walikuwa wakicheza watupu ndani ya cassino ile pia kulihitajika fedha. Watu walikuwa wakitengeneza fedha katika nyanja mbalimbali ndani ya Cassino ile.
Kama kawaida yake, Bwana Maxwell alionekana kuwa moto wa kuotea mbali, alikuwa ameweka kiasi kikubwa cha fedha na kutokana na umahili wake katika kuucheza mchezo ule akaingiza kiasi kikubwa zaidi. Japokuwa kulikuwa na wataalamu wengi ndani ya Cassino ile katika mchezo wa poker lakini Bwana Maxwell alionekana kuwa moto wa kuotea mbali, alikuwa akicheza, aliwapuna fedha zao huku akiwatolea maneno ya kejeli.
“Mbona mmenitunza sasa hizo fedha zetu? Yaani unaweka karata hiyo, haujui kama hapa nina karata ya kumaliza mchezo mzima? Nachukua fedha zenu zote, nitawabakishia wake zenu tu, na kama mlikuwa mnataka kuwekeana wake kwa fedha, nipo tayari” Bwana Maxwell aliwaambia baada ya kuona amewala fedha nyingi na huku nyingine zikiwa zinakuja.
Wamexico wakabaki kimya. Ni kweli maneno ya Bwana Maxwell yalikuwa yakiwakera sana lakini hawakuwa na jinsi, waliamua kunyamaza na kuendelea kuucheza mchezo ule huku wakiutilia umakini zaidi.
“Ayaaaa! Sasa mbona mmenipa hela ya bure? Mna mabinti zenu wadogo wadogo wasiozeeka kama wake zenu? Kama mnao waleteni nao niwapiganie kwa fedha zangu nikalale nao usiku wa leo” Bwana Maxwell aliwaambia.
Kila neno ambalo alikuwa akiongea mbele ya meza ile lilikuwa neno lenye kuwaumiza mioyo yao. Wakajikuta wakashikwa na hasira lakini hawakuwa na cha kufanya zaidi ya kuendelea kucheza mchezo ule ambao kwa kila hatua waliendelea kuliwa fedha zao. Kwa mbwembwe nyingi, Bwana Maxwell akaweka dola mia moja pembeni na kisha kumuita mhudumu kwa ishara na kisha kumgawia kiasi kile cha fedha.
“Niletee John Walker...hawa wenzangu waletee Pepsi” Bwana Maxwell alimwambia mhudumu.
Watu wote ambao walikuwa wamekaa katika meza ile wakaanza kucheka. Hiyo ndio ilikuwa kauli ambayo ilionekana kuwakasirisha zaidi. Mchezaji mmoja akaitoa bunduki yake ambayo ilikuwa kiunoni na kisha kuiweka juu ya meza, alionekana kukasirika sana na kwa jinsi alivyoonekana, alikuwa tayari kwa kila kitu.
“Badala ya kuweka fedha unaweka bunduki. Kila mtu ana bunduki humu” Bwana Maxwell alimwambia yule jamaa na kisha kuitoa bunduki yake, akamuonyeshea na kisha kuirudisha.
“Tucheze tu mchezo, huu si muda wa kuonyesheana bunduki” Bwana Maxwell aliongezea.
Kitendo cha kutoa bunduki yake kilionekana kuwashtua watu wengine kwa kuona kwamba hata yule ambaye walikuwa wakicheza nae alikuwa mpiganaji mzuri wa kutumia bunduki na tofauti ya walivyofikiria katika kipindi chote ambacho alikuwa akija ndani ya cassino ile.
Mchezo ukaendelea zaidi mpaka pale ambapo Bwana Maxwell alipoona imetosha, akasimama na kisha kuelekea kaunta. Kwa wakati huo alijiona kuwa na fedha nyingi, mchezo wa kamari ulikuwa ukiendelea kumuingizia kiasi kikubwa cha fedha katika kila sehemu ambayo alikuwa akienda na kucheza kamari.
“Nahitaji Ciroc...chupa moja” Bwana Maxwell alimwambia msichana ambaye alikuwa kaunta.
Msichana yule akaifuata sehemu ambayo ilikuwa na chupa kadhaa na kisha kuchukua chupa moja ya kinywaji cha Ciroc na kisha kukiweka juu ya kaunta. Bwana Maxwell akaifungua na kuchukua glasi moja ndogo ambayo iliwekwa na mhudumu yule na kisha kuimimina kidogo na kuanza kunywa.
“Nataka kukuuliza kitu” Bwana Maxwell alimwambia msichana yule.
“Uliza, hakuna tatizo”
“Unaitwa nani?”
“Caroline”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ninahitaji mwanamke wa kulala nami usiku wa leo” Bwana Maxwell alimwambia msichana yule.
“Una kiasi gani mfukoni”
“Kwani huwa ni dola ngapi?”
“Kwa wazuri huanzia dola mia tatu”
“Hao wana uzuri gani?”
“Kama yule” Msichana yule alimwambia huku akimuonyeshea msichana mmoja ambaye alikuwa akicheza kwenye chuma moja kubwa huku akiwa mtupu.
“Hana uzuri wa kulipwa dola mia tatu” Bwana Maxwell alimwambia msichana yule.
“Wewe unataka wa dola ngapi?”
“Kwani wewe thamani yako dola ngapi kwa usiku mmoja?”
“Unanitaka mimi?”
“Ndio maana nimeuliza gharama yako”
“Hahaha! Utaniweza?”
“Kwani una nini mpaka nishindwe kukuweza?”
“Una nguvu chumbani?”
“Kwani ishu ni mimi kuwa na nguvu au wewe kunifanyia kazi usiku kucha?”
“Hahah! Sawa. Una dola mia nne?”
“Hilo si tatizo. Utanipa huduma zipi?”
“Hii unayoitaka wewe na hata ile usiyoitaja”
“Kama ipi?”
“Kukandwa usiku mzima”
“Mmmh!”
“Nini tena?”
“Hilo tu?”
“Na mengine mengi”
“Sawa. Kwa hiyo nikushtue muda gani?”
“Hata sasa hivi”
“Sasa hapa atakaa nani?”
“Kuna mhudumu mwingine atakuja”
“Sawa. Kama vipi twende”
“Hakuna tatizo. Ngoja nimuite mhudumu mwingine”
Caroline akaondoka mahali hapo. Bwana Maxwell alibaki pale kaunta akiendelea kunywa kama kawaida. Muda mwingi macho yake hayakutulia, yalikuwa yakiangalia huku na kule kana kwamba alikuwa akimtafuta mtu fulani. Baada ya muda wa sekunde kadhaa, Caroline akarudi mahali pale huku akiwa na mwanamke mwingine aliyeonekana kuwa na umri mkubwa kidogo. Kwa haraka sana Bwana Maxwell akayapeleka macho yake usoni mwa mwanamke yule aliyekuja pamoja na Caroline. Kwanza akashtuka, alionekana kumfananisha mwanamke yule, akamuangalia vizuri, alikuwa yeye, alikuwa ni mwanamke ambaye kila siku alimuita “Mwanamke wa ndoto zake” mwanamke ambaye alikuwa amezaa nae watoto na kisha kuondoka zake kuelekea nchini Mexico bila kutalakiana kutokana na ulevi wake. Alikuwa Jocelyn.
“Jocelyn....!” Bwana Maxwell alijikuta akimuita mwanamke yule, alipouinua uso wake, Jocelyn akaonekana kushtuka.
“Maxwell....” Bi Jocelyn alijikuta akiita kwa mshtuko, hakuamini kama angemkuta mumewe ndani ya cassino hiyo nchini Mexico.
Hakukuwa na kitu chochote kile ambacho alikuwa akikifikiria mahali hapo zaidi ya kujiua, kitanzi ambacho alikuwa amekifunga shingoni mwake ndicho ambacho kilikuwa kikiikaza shingo yake, mishipa kuonekana na mwili kuanza kukakamaa. Hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa akijua kuhusiana na kile ambacho kilikuwa kikiendelea chumbani kwamba Kelvin alikuwa amejifunga kitanzi na alikuwa akijinyonga.
Hakukuwa na mtu wa kutoa msaada baada ya stuli kuanguka, Kelvin alikuwa akiangaika huku na kule, mwili wake ulizidi kukakamaa na mwisho wa siku kutulia kabisa, akaning’inia huku kamba ikiwa shingoni mwake.
Hicho ndicho ambacho alikuwa akikitaka, alikuwa amekata tamaa ya maisha yake na ni kitu kimoja tu ndicho ambacho alikuwa amekifikiria, kujiua kama alivyokuwa amefanya. Historia yake mbaya ya mapenzi ndio ambayo ilikuwa imebadilisha kila kitu na ndio ambayo ilikuwa imemfanya kuwa na uamuzi huo ambao haukuonekana kuwa uamuzi sahihi katika maisha yake.
Bi Agnes hakuwa akifahamu kitu chochote kile ambacho kilikuwa kikiendelea chumbani, alikuwa amekaa kochini huku akisoma gazeti lake la Ijumaa. Kitendo cha mtoto wake kumchukia kilimuumiza sana, hakutarajia kwamba kile alichokuwa amekifanya cha kumtenganisha na Alberrtina ndicho ambacho kingesababisha yale yote yaliyotokea mpaka kutishia kujiua.
Bi Agnes akaonekana kuzidiwa, alichokuwa amekubaliana moyoni mwake ni kumuomba msamaha mtoto wake, Kelvin na kuhakikisha anafanya jitihada za kuonana na wazazi wa Albertina kwa ajili ya kuwaomba msamaha kutokana na matusi aliyokuwa amewatukana. Hicho ndicho ambacho aliamua kukifanya, japokuwa alijua fika kwamba asingeweza kumfanya Albertina kurudiana na Kelvin kwa kuwa msichana huyo alikuwa ameolewa na mzungu nchini Marekani.
“Nitajitahidi tu” Bi Agnes alijisemea.
Hakutaka kuendelea kubaki sebuleni hapo, alichokifanya ni kuanza kuufuata mlango wa kuingilia chumbani kwa Kelvin. Alipoufikia mlango akaanza kuugonga huku akimtaka Kelvin aufungue na kisha kuongea nae. Kelvin hakusikika na wala mlango haukufunguliwa. Bi Agnes hakutaka kuihsia hapo, aliendelea zaidi na zaidi lakini hakukuwa na sauti yoyite ya mtu ambayo ilisikika kutoka ndani. Bi Agnes akaonekana kuwa na wasiwasi, alichokifanya ni kutoka nje na kuwaita majirani ambao wakafika mahali pale, nao wakaita lakini kukawa kimya, walichokifanya ni kuuvunja mlango, walipoingia, hawakuamini walichokiona, Kelvin alikuwa akining’inia kwenye kitanzi, Bi Agnes akazimia kwa presha.
*****
Bwana Kurt aliumia moyoni, hakuamini kwamba mtu ambaye alikuwa amemkumbatia mahali pale alikuwa mtoto wake aliyekuwa akimpenda sana, Alan. Kuumia kwake moyoni ndio kulifanya kuanza kutokwa na machozi na kuanza kulia kama mtoto. Alimpenda sana Alan na hakutaka kijana wake aingie kwenye matatizo yoyote yale na ndio maana kitendo cha kumkuta yupo namna ile kilimfanya kutokwa na machozi.
Alan alikuwa kwenye muonekano mpya, muonekano ambao ulimfanya kutokugundulika mara moja kama alikuwa yeye au la. Damu zilikuwa zimetapakaa mwilini mwake hali iliyoonyesha kwamba alikuwa amepitia mateso mazito mahali hapo. Hakuwa na fahamu, alikuwa amepoteza fahamu zake na hakuwa akijua kama baba yake alikuwa amefika mahali hapo.
“Alan....Alan....wake up Alan....just look at me my son...(Alan...Alan...amka Alan...niangalie kijana wangu” Bwana Kurt alisema huku akitokwa na machozi mfululizo.
Japokuwa muda wote alikuwa akimuita Alan lakini hakukuweza kubadilisha kitu chochote kile, Alan alikuwa hoi, hakuwa amefumbua macho yake, uso wake ulikuwa umevimba sana huku akionekana kutokutambulika kabisa. Bwana Kurt hakuishia hapo, aliendelea zaidi na zaidi kumuita Alan lakini kila kitu kilibaki kuwa vile vile.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku hiyo hakukuwa na mtu mwingine aliyeingia ndani ya chumba hicho, Bwana Kurt alibaki akiwa amempakata mtoto wake, Alan tu huku akiendelea kutokwa na machozi kama kawaida. Wakati mwingine taa ilikuwa ikizimwa na chumba kizima kuwa na giza kubwa. Hayo yote yalionekana kuwa mateso kwa Bwana Kurt, alikuwa akipata tabu kupita kawaida.
Usiku ulipoingia, kiyoyozi kikafunguliwa kwa kasi ya juu, chumba kikatawaliwa na baridi kali sana. Hayo nayo yakaonekana kuwa kama mateso kwake pamoja na kwa kijana wake ambaye hakuwa amerudiwa na fahamu. Usiku hakulala, alikuwa macho huku akimsubiria Alan ayafumbue macho yake na kuangalia tena na kumwambia kwamba alikuwa amefika mahali hapo kwa ajili yake tu.
Asubuhi ilipoingia, saa mbili asubuhi akaletewa chai pamoja na vitafunio. Haikuwa kama chai ambayo alizoea kunywa nyumbani kabla hajaelekea ofisini. Hiyo ilikuwa chai ya tofauti sana, chai ambayo mbele ya macho yake au mbele ya chai alizozoea kunywa haikustahili kuitwa chai. Bwana Kurt hakutaka kujali, kwa sababu njaa ilikuwa ikimuuma, akavumilia na kisha kuanza kunywa.
Ilipofika saa saba mchana, Alan akarudiwa na fahamu, akaanza kuyafumbua macho yake, macho yalikuwa mazito, akajitahidi kuyafumbua zaidi na zaidi, akakutanisha macho na baba yake, Bwana Kurt. Alan hakuonyesha mabadiliko yoyote, hakuonyesha hata dalili ya mshtuko kumuona baba yake mahali pale, alimtambua baba yake na ila kila alipotaka kuongea pamoja nae, mdomo wake ulikuwa mzito kufunguka.
“Say something my son (Ongea chochote kijana wangu)” Bwana Kurt alimwambia Alan.
Ukimya bado ulikuwa ukiendelea kama kawaida, Alan hakuongea kitu chochote kile zaidi ya kuendelea kubaki kimya. Bwana Kurt aliumia zaidi lakini maumivu yake ya moyoni hayakuwa yamebadilisha kitu chochote kile kwa wakati huo.
Masaa yalizidi kusogea, ilipofika saa saba mchana, mzee Sanchez akaingia ndani ya chumba kile huku akiwa ametangulizana na vijana wake waliokuwa na asili ya Urusi ambao walikuwa na miili mikubwa. Kabla ya kuongea kitu chochote kile, Bwana Kurt akafuatwa mahali pale alipokuwa amekaa, akavuliwa nguo zake na kubaki mtupu na kisha kukalishwa kwenye kiti cha umeme.
“If you want to kill me, just kill me but him go (Kama unataka kuniua, wewe niue tu ilakini muache aondoke)” Bwana Kurt alimwambia mzee Sanchez ambaye wala hakutaka kuongea kitu chochote kile.
Mikono yake ikafungwa kamba katika kiti kile na kilichofuatia ni kuanza kupigwa ngumi za uhakika. Warusi wale walikuwa wakimpiga ngumi mfululizo, hawakuchagua ni wapi ambapo walitakiwa kumpiga, waliupiga sana uso wake, wakazipiga sana mbavu zake pamoja na kifua chake kitu kilichompelekea kuanza kutokwa na damu mdomoni.
Vijana wale walionekana kutokuwa na huruma, kitu ambacho walikuwa wakikifanya ni kutii kile ambacho walikuwa wakiambiwa mahali hapo. Kipigo kiliendelea zaidi na zaidi, walipoona kwamba vidole vyao vimechoka, hapo ndipo walipoanza kumpiga na mikanda ambayo walikuwa wameivua kutoka katika suruali zao.
Yalikuwa ni mateso makali mno, Bwana Kurt akavimba huku uso wake ukiwa umetawaliwa na damu. Hakukoma, muda wote alikuwa akiyarudia maneno yale yale kwamba alitakiwa kuuawa lakini kijana wake ilibidi aachiwe huru na kuondoka. Hakukuwa na mtu ambaye aliemuelewa, waliendelea kumpiga zaidi na zaidi huku mzee Sanchez akiendelea kuangalia tena akiwa amechukua sigara yake na kuanza kuivuta.
“Mnayamazisheni...hatakiwi kuongea” Mzee Sanchez aliwaambia vijana wake.
“Hakuna tatizo” Kijana mmoja alisema.
Alichokifanya ni kuondoka ndani ya chumba kile ambapo baada ya dakika mbili, akarudi huku akiwa ameshika gongo moja kubwa ambalo lilikuwa ba nichirizi ya damu. Bwana Kurt akaonekana kuogopa, gongo lile lilimtia hofu sana na hakuamini kwamba lilikuwa limeletwa chumbani pale kwa ajili ya kutumika kumpiga nalo.
Kipigo kikaanza upya, akaanza kupigwa na gongo lile kuanzia usoni na sehemu nyingine za mwili. Alibaki akilia kama mtoto, maumivu ambayo alikuwa akiyasikia mahali pale yalikuwa makali mno. Warusi wale walioonekana kuwa na roho mbaya hawakutaka kujali, gongo lile likaamishwa sehemu nyingine tena, ikaanza kupigwa miguu yote miwili kitu ambacho kilipelekea mifupa ya miguu kusikika na kuvunjika.
Hilo ndilo lilikuwa lengo lake, kwa wakati huo mzee Sanchez alitaka kuwaua wote wawili lakini akataka kuwaua katika vifo vilivyojaa maumivu makali. Miguu ya Bwana Kurt ikavunjwa na kisha zamu ya mikono kuingia. Japokuwa katika kipindi cha nyuma Bwana Kurt alikuwa akipiga kelele lakini kikafika kipindi ambacho sauti yake haikusikika kabisa,
Kila alipokuwa akitaka kupiga kelele, sauti haikutoka. Mikono ikavunjwa mara mbili na kisha zamu ya mabega kuingia. Katika kipindi chote hicho Alan alikuwa akiangalia, moyoni alikuwa akijisikia uchungu sana lakini hakuwa na la kufanya. Mwili wake haukuwa na nguvu hata kidogo, macho yake yalikuwa mazito kufunguka na kuangalia tukio zima lilivyokuwa likiendelea mahali pale.
Bwana Kurt alipofunguliwa kamba, akaanguka chini mzima mzima kama gunia la mahindi. Huo ukaanza kuonekana kuwa mwisho wake, mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa mbali sana wakati huo. Alilala chini huku akiwa kimya. Japokuwa Alan alikuwa ameharibika vibaya lakini kwa Bwana Kurt hali ilionekana kuwa zaidi ya Alan, aliharibiwa vibaya zaidi ya mtoto wake, Alan.
“Safi sana. Hii familia nilikuwa nikiichukia sana” Mzee Sanchez aliwaambia vijana wake ambao wote walionekana kuchoka kutokana na kumpiga Bwana Kurt mfululizo bila kupumzika.
“Nini kinafuata bosi?” Zhikov alimuuliza mzee Sanchez.
“Hebu sikiliza mapigo ya moyo wake, yanadunda?” Mzee Sanchez alimuuliza Zhikov ambaye akaanza kuyasikiliza mapigo ya Bwana Kurt.
“Yanadunda ila kwa mbali” Zhikov alijibu.
“Hebu yasimamishe, hayatakiwi kudunda” Mzee sanchez alimwambia Zhikov.
Hilo wala halikuonekana kuwa tatizo, alichokifanya Zhikov ni kulichukua lile gongo lake na moja kwa moja bila ya kujiuliza akaanza kukipiga kichwa cha Bwana Kurt. Alipiga ovyo kana kwamba alikuwa akipiga kitu kisichokuwa na uhai hata kidogo. Aliendelea kukipiga kichwa ambacho kilipasuka na kuanza kutoa damu ovyo mahali pale.
“Yasikilize tena mapigo yake” Mzee Sanchez alimwambia Zhikov.
“Hayasikiki kabisa” Zhikov alimwambia mzee Sanchez huku tabasamu pana likiwa usoni mwake.
“Unaweza kunionyeshea ubongo wake nikaridhika?” Mzee Sanchez alimwambia Zhikov.
“Hakuna tatizo”
Hicho ndicho ambacho mzee Sanchez alikuwa akikitaka mahali hapo, alikuwa akitaka kuuona ubongo wa Bwana Kurt. Hakuamini kama kweli Bwana Kurt alikuwa amekufa, alichokuwa akitaka ni kuuona ubongo wake tu. Zhikov akaanza kukipiga tena kichwa cha Bwana Kurt ambaye alikuwa amekwishakufa, alikipiga kwa mapigo matano makubwa, kichwa kikapasuka zaidi, kichwa kikabonyea na hatimae ubongo kumwagika sakafuni.
“Nimeridhika” Mzee Sanchez alimwambia Zhikov.
“Na huyu mtoto wake tumfanye nini?”
“Huyo zamu yake kesho asubuhi”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sawasawa hakuna tatizo mkuu” Zhikov alimwambia mzee Sanchez.
Hapo moyo wake ukawa mweupe, kitendo cha Bwana Kurt kufariki kikaonekana kumfurahisha kupita kawaida. Hicho ndicho ambacho alikuwa akikitaka mahali hapo, hakutaka kumuona mzee huyo akiwa hai, kutokana na utajiri ambao alikuwa nao ulionekana kutokumfurahisha kwani biashara zake hasa za magari zilikuwa juu hata zaidi ya biashara zake jambo ambalo lilionekana kutokumfurahisha kabisa.
Alan alibaki chumbani, kila kitu kilichokuwa kimetokea kwa baba yake kilimpa majonzi makubwa, akaanza kutokwa na machozi mfululizo, alitamani kulia kwa sauti na kuisogelea maiti ya baba yake lakini akashindwa kufanya hivyo,mwili wake haukuwa na nguvu hata mara moja.
Huo ndio ukaonekana kuwa mwisho wa Bwana Kurt, historia ya maisha yake suniani ikaishia hapo, jina la marehemu ndio ambalo lilikuwa jina lake la kwanza. Kila kitu ambacho alikuwa amekifanya katika maisha yake kikabaki na kuwa historia, fedha nyingi ambazo alikuwa ameziacha zikabaki mikononi mwa familia yake ambapo nae mtoto wake alikuwa njiani kuuawa. Utajiri ambao alikuwa akiutamani toka kipindi cha nyuma ndio utajiri ambao ulimfanya kuuawa kikatili ndani ya chumba hicho.
Bwana Maxwell hakuonekana kuamini, alibaki akimwangalia mke wake mara mbili mbili, hakuamini kwamba angeweza kumkuta ndani ya cassino ile akifanya kazi kama mhudumu. Uso wake ukajawa na aibu kubwa, kitendo chake cha kutaka kumchukua Caroline kilionekana kumpa aibu mbele ya mke wake.
Ni kweli walikuwa wametengana kwa muda mrefu kutokana na ulevi ambao alikuwa nao Bwana Maxwell lakini katika kipindi hicho ambacho walikuwa wameonana kila mmoja akamuona mwenzake kuwa mtu mpya. Jocelyn ndio kwanza alikuwa na miaka thelathini na mbili, alionekana kuwa mwanamke mbichi ambaye kwa mtu yeyote yule hasa mwanaume rijali asingejiuliza mara mbili mbili kumfuata.
Kifuani alikuwa na matiti yake yale yale, matiti ambayo wala hayakulala japokuwa alikuwa amezaa, sura yake ilikuwa vile vile, ilikuwa ya kitoto sana huku nywele zake zikiwa na mvuto kutokana na dawa ambazo alikuwa akizitumia kila siku. Machoni mwa Bwana Maxwell, Jocelyn alionekana kuwa mwanamke mpya, mwanamke ambaye hakutakiwa kuachwa na mwanaume yeyote ambaye alibahatika kuwa nae.
Bwana Maxwell akasahau kamba alikuwa amemwambia Caroline ajiandae ili waweze kuondoka mahali hapo na kuelekea hotelini kwa ajili ya kuvunja amri ya sita mpaka alfajiri. Macho yake yalikuwa yakimwangalia mke wake ambaye alikuwa ameondoka Marekani miaka kadhaa ya nyuma.
“What are you doing here? (Unafanya nini hapa)?” Maxwell alimuuliza Jocelyn.
“I think, I should ask you the same question Maxwell (Nadhani natakiwa kukuuliza swali hilo hilo Maxwell)” Jocelyn alimwambia Bwana Maxwell.
“(Do you know each other?(Mnafahamiana?)” Caroline aliuliza huku akionekana kuwashangaa.
“Yes. This is my husband, he lives in U.S.A (Ndio. Huyu ni mume wangu, anaishi nchini Marekani)” Jocelyn alimwambia Caroline.
“Is he the one that you told me....a drinker(Ndiye yule uliyeniambia....mlevi?)”
“Yes, he is the one(Ndio, ndiye huyo huyo)
Jocelyn hakutaka kuongea kitu chochote kile, akaamua kubaki kimya na kumwangalia Bwana Maxwell ambaye muda wake mwingi alikuwa akiangalia chini kwa aibu. Jocelyn aliendelea kumwambia Caroline kuhusu maisha ambayo aliishi na mume wake kitu ambacho kwa muonekano ambao alikuwa akionekana mahali hapo katika kipindi hicho, Caroline hakuonekana kuamini. Bwana Maxwell alionekana kuwa mtu mwenye fedha ambaye alikuwa radhi kufanya kitu chochote au kulala na mwanamke yeyote yule.
“Kwa hiyo?” Caroline alimuuliza Bwana Maxwell.
“Haitowezekana tena” Bwana Maxwell alijibu.
“Kwa sababu umekutana na mkeo?”
“Hapana. Ni kwa sababu nimekutana na mwanamke ambaye nilimchagua kwa moyo wangu wote, mwanamke ambaye ninakiri kwamba nilikuwa namhitaji sana, mwanamke ambaye niliigundua thamani yake mara baada ya kuondoka nyumbani” Bwana Maxwell alimwambia Caroline.
Jocelyn akaonekana kushtuka,kwanza akamwangalia vizuri Bwana Maxwell, maneno ambayo alikuwa ameyaongea mahali hapo yalimfanya kujisikia tofauti sana. Aliishi na mume wake kwa zaidi ya miaka mitano lakini maneno matamu kama yale alikuwa ameyasikia katika kipindi kile cha uchumba tu, kipindi ambacho kilikuwa siku kadhaa baada ya kumficsha pete ya uchumba katika mghahawa wa Mc Donald nchini Marekani.
Hapo ndipo ambapo Jocelyn akajisikia kuwa mwanamke wa tofauti, akili yake ikafunguka kwa kuona kwamba katika kipindi chote ambacho alikuwa ameondoka na kurudi nchini Mexico mume wake alikuwa akimkumbuka huku kwa namna moja au nyingine alikuwa akijutia kila kitu ambacho alikuwa amekifanya ambacho kilisababisha kuondoka nyumbani.
“Naomba tuanze upya Jocelyn, ninataka kubadilika na kuwa mtu mpya, bila wewe, bila uwepo wako pembeni yangu sitoweza kubadilika” Bwana Maxwell alimwambia Jocelyn.
“Unataka kubadilika, kuwa vipi?” Jocelyn alimuuliza Bwana Maxwell huku Caroline akiwa pembeni.
“Kuwa tofauti na nilivyokuwa”
“Kivipi?”
“Nataka kuacha ulevi na kucheza kamari” Bwana Maxwell alimwambia Jocelyn.
Jocelyn akabaki kimya kwa muda, akaanza kumwangalia Bwana Maxwell huku akionekana kutokuyaamini maneno ambayo aliyasikia kutoka kwa mume wake. Alimjua fika, alijua fika kwamba mume wake alikuwa akipenda sana kunywa pombe na kucheza kamari, alikuwa radhi kukosa kitu chochote kile maishani mwake lakini si kuacha kufanya vitu hivyo.
Aliyakumbuka maisha ambayo aliishi na mume wake katika kipindi cha nyuma, yalikuwa maisha yenye kukera sana kwa sababu Bwana Maxwell alikuwa akipenda sana kunywa pombe na kucheza kamari na ndio maana aliamua hata kutokuijali familia yake. Leo hii, Bwana Maxwell alikuwa amesimama mbele yake akitaka kurudiana nae huku akiwa radhi kuacha vitu vyote ambavyo vilimsababishia kuondoka nchini Marekani na kurudi kwao, nchini Mexico.
“Umemaanisha?” Jocelyn alimuuliza Bwana Maxwell.
“Nimemaanisha. Ninataka kurudiana nawe na kuwa pamoja na watoto wangu” Bwana Maxwell alimjibu Jocelyn.
“Kwanza huku Mexico umekuja kufanya nini na wakati huu si muda wako wa kupewa likizo?” Jocelyn alimuuliza Bwana Maxwell.
“Kuna mtu nimemleta”
“Nani?”
“Alan”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ndiye nani? Na umeleta kufanya nini?” Jocelyn alimuuliza Bwana Maxwell.
Hapo ndipo ambapo Bwana Maxwell akamvuta pembeni Jocelyn na kisha kuanza kumhadithia kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea toka katika kipindi ambacho alipigiwa simu na Bwana Kurt na kumwambia kwamba alitakiwa kumrudisha mtoto wake jijini Washington. Jocelyn alibaki kimya akimsikiliza mume wake ambaye alitumia muda wa dakika kumi na tano, akawa amemaliza kumwambia kila kitu.
“Kwa hiyo huyo Alan yupo hapa Mexico?” Jocelyn alimuuliza Bwana Maxwell.
“Ndio. Tena kwenye mtaa huu huu” Bwana Maxwell alijibu.
“Unamjua vizuri huyo Sanchez?”
“Hapana”
“Haujawahi kusikia hata sifa zake?”
“Hapana”
“Mmmh! Mbona hatari”
“Kivipi?”
“Huyo mzee ni hatari sana, ana roho mbaya hata zaidi ya Hitler” Jocelyn alimwambia Bwana Maxwell.
“Kwa hiyo unataka kuniambia kwamba Alan yupo kwenye mikono ya mtu hatari?” Bwana Maxwell aliuliza huku akionekana kutokuamini.
“Ndio hivyo”
“Haiwezekani”
“Kubaliana nami. Alan yupo kwenye mikono hatari sana. Mzee huyo anajulikana Mexico nzima kwa ukatili, anaua watu lakini serikali haimchukulii hatua yoyote ile kwa sababu hufanya mambo mengi hapa nchini hivyo serikali humuheshimu” Jocelyn alimwambia Bwana Maxwell.
“Kwa hiyo anaweza kumuua Alan?”
“Kama ana ugomvi nae, anaweza kumuua”
“Haiwezekani. Lazima nifanye jambo”
“Jambo gani?”
“Kwenda kumuokoa Alan”
“Utaweza? Utaweza kuingia ndani ya jumba lake na kuua walinzi wote?” Jocelyn alimuuliza mume wake.
“Hapo sitoweza”
“Sasa utamuokoa vipi?”
Bwana Maxwell akabaki kimya kwa muda, akaanza kufikiria jambo. Aliendelea kubaki katika hali hiyo kwa muda kadhaa, hakutaka kuongea kitu chochote kile. Kitu ambacho alikuwa akikifikiria ni namna ambayo alitakiwa kwenda kumuoko Alan. Tayari maneno ambayo aliongea Jocelyn yalionekana kumtia wasiwasi.
“Ila subiri kwanza” Bwana Maxwell alimwambia Jocelyn.
“Kwa nini?”
“Tusubiri mpaka kesho kwanza” Bwana Maxwell alimwambia Jocelyn.
“Kwa nini tena?”
“Alan alisema atanipigia simu. Ngoja tusikilizie kwanza. Inawezekana hakuna kitakachotokea na kesho anaweza kupiga simu, asipopiga simu hapo ndipo nitatakiwa kwenda kumuokoa” Bwana Maxwell alimwambia Jocelyn.
“Una uhakika atapiga?”
“Hiyo ndio ilikuwa ahadi yake”
“Na kama hatopiga?”
“Itanibidi niende kumuokoa”
“Utamuokoa vipi?”
“Hapo bado sijajua, ila nitamuokoa tu. Mimi ni polisi, ninayafahamu mapigano ya kikatili pamoja na kutumia bunduki vilivyo. Nipe muda nifikirie juu ya hilo” Bwana Maxwell alimwambia Jocelyn.
Usiku wa siku hiyo Bwana Maxwell hakuonekana kuwa na furaha japokuwa Jocelyn alikuwa amekubali kuanza maisha na yeye na hatimae kurudi nchini Marekani kuendelea na maisha yake. Muda mwingi alikuwa kifikiria njia ambayo angeitumia kuingia ndani ya jumba la kifahari la mzee Sanchez na hatimae kumtoa salama na kuondoka nae kurudi nchini Marekani.
Kila alichokuwa akikifikiria alikosa jibu, hakujua ni kipi kilitakiwa kufanyika. Ukatili ambao alikuwa ameuelezea Jocelyn juu ya mzee sanchez tayari ulikuwa umemuwekea mashaka mengi kwa kuona kwamba Alan angeweza kuuawa kikatili, ila kabla ya kufikiria hayo kwa sana alitaka kuona kama Alan angempigia siku siku inayofuata kama alivyomwambia au asingefanya hivyo.
Asubuhi ikaingia, Bwana Maxwell hakutaka kutoka chumbani, alikuwa amelala pamoja na mke wake, Jocelyn. Kwa sababu alikuwa na fedha za kutosha, kila kitu kilifanyikia chumbani. Wakaletea chai mpaka chakula cha mchana chumbani mule, wakanywa na kula huku wakiendelea kusikilizia simu kutoka kwa Alan. Hakukuwa na simu ambayo iliingia kitu ambacho kilimpelekea Bwana Maxwell kuanza kuhisi kwamba tayari kulikuwa na jambo baya ambalo lilikuwa limetokea, alichokifanya ni kumpigia simu Alan, haikuwa ikipatikana.
“Inanibidi nifanye kitu” Bwana Maxwell alimwambia Jocelyn.
“Kitu gani?”
“Kwenda kumuokoa”
“Sasa utaingia vipi?”
“Hapo ndipo inabidi tushirikiane” Bwana Maxwell alimwambia Jocelyn.
“Nimepata wazo” Jocelyn alimwambia Bwana Maxwell huku uso wake ukionyesha tabasamu pana.
“Wazo gani?”
“La kuingia mule ndani”
“Nini kifanyike?”
“Tufanye hivi………” Jocelyn alimwambia na kisha kuanza kumwambia kitu ambacho kilitakiwa kufanyika kuingia ndani ya hilo jumba.
****
Mzee Sanchez alionekana kuridhika, kitendo cha kumuua Bwana Kurt kwa mauaji ya kutisha kilimpa furaha kubwa moyoni mwake, akajiona kama alikuwa ameutua mzigo mkubwa ambao ulikuwa umempa uzito mkubwa moyoni mwake. Hakuwa akimpenda Bwana Kurt, alikuwa akimchukia kupita kawaida.
Usiku wa siku hiyo hakulala, furaha kubwa ilikuwa imekusanyika moyoni mwake, alikuwa akimwangalia mke wake huku dhahiri akionekana kuwa na furaha. Hakujua ni kwa namna gani alitakiwa kuizungumzia furaha ambayo alikuwa nayo katika kipindi hicho. Mbaya wake ambaye hakuwa akimpenda, mbaya ambaye alikuwa akimchukia hata zaidi ya alivyokuwa akimchukia shetani tayari alikuwa amekwishamuua na katika muda huo alikuwa kifikiria kitu kimoja tu, kumuua mtoto wake, Alan.
Huyo ndiye ambaye alionekana kuwa tatizo kwa wakati huo, alitakiwa kumuua kwa ajili ya kuweka siri ili watu wengine wasifahamu kile ambacho kilikuwa kikiendelea. Kuua watu kwake lilikuwa suala dogo sana lakini kwa mtu kama Kurt hilo likaonekana kuwa tatizo kutokana na mtu huyo kuwa tajiri, mtu muhimu hasa katika nchi kama Marekani.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Bado mtoto wake” Mzee Sanchez alimwambia mke wake, Shakira.
“Unataka kumuua mpaka mtoto wake?” Bi Shakira aliuliza huku akionekana kushtuka.
“Lengo langu ni kuua familia nzima”
“Na unataka kumuua lini?” Bi Shakira alimuuliza mume wake.
“Kesho ndio nakamilisha kila kitu. Baada ya hapo nitawatuma vijana wangu waende kumuua mke wake huko huko Marekani” Mzee Sanchez alimwambia mke wake.
“Nakutakia kila la heri mume wangu, ila kuwa makini katika kila hatua utakayochukua” Bi Shakira alimwambia mume wake.
“Usijali mke wangu” Mzee Sanchez alimwambia mke wake, Bi Shakira.
Usiku huo wakalala japo walichelewa sana kulala kutokana na kuongea mambo mengi kuhusiana na Alan. Ilipofika asubuhi, kwa haraka haraka bila kupoteza muda mzee Sanchez akaanza kuelekea katika chumba kile kilichokuwa chini ya ardhi. Lengo lake lilikuwa ni kutaka kumuona Alan. Alipokifikia chumba kile, akaufungua mlango, macho yake yakatua kwa Alan ambaye alikuwa amekaa chini huku uso wake akiwa ameupitisha katikati ya miguu yake akilia.
Mzee Sanchez wala hakuonekana kuhuzunika, akamwangalia Alan pamoja na maiti ya Bwana Kurt na kisha kutoa tabasamu pana. Hilo ndilo ambalo alikuwa akilitaka mahali hapo, Alan alikuwa akilia kwa hasira lakini kwa mzee Sanchez kila kitu kikaonekana kuwa kama sikukuu, hakuonekana kuwa na huzuni hata mara moja. Huku akiendelelea kumwangalia Alan na uso wake ukionekana kuwa na furaha, mara sauti ya simu yake ikaanza kusikika, kwa haraka akaupeleka mkono wake mfukoni na kuitoa simu, alipoiangalia simu ile, ilikuwa ni namba ya Mendez.
“Kuna nini” Mzee Sanchez aliuliza huku akionekana kukasirika, alijiona kuingiliwa wakati alikuwa katikati ya kufanya jambo fulani.
“Nimekuja kuchukua mzigo mzee” Sauti ya Mendez ilisikika.
“Kuchukua mzigo? Nani alikwambia kwamba kuna mzigo leo?” Mzee Sanchez aliuliza huku kidogo akionekana kubadilika.
“Nilipigiwa simu”
“Na nani?”
“Na Zhikov”
“Sawa. Njoo kwanza uuchukue huu mzigo mmoja na kisha baadae uurudie huu pale ambapo Zhikov atakuwa amekamilisha kila kitu” Mzee Sanchez alimwambia Mendez.
“Sawa mkuu”
“Umefika wapi kwa sasa?”
“Nipo sebuleni”
“Basi njoo” Mzee Sanchez alimwambia Mendez.
Mendez alikuwa mmoja wa vijana ambao walikuwa wakifanya kazi nyumbani kwa mzee Sanchez. Kazi kubwa ya Mendez ilikuwa ni kuchukua miili ya watu ambao walikuwa wakiuawa ndani ya nyumba hiyo na kisha kwenda kuwazika porini. Hiyo ndio ilikuwa kazi yake kubwa ambayo ilikuwa ikimuweka mjini. Kila mtu alipokuwa akiuawa, Mendez alikuwa akipigiwa simu na Zhikov au hata mzee Sanchez mwenyewe na kisha kuelekea nyumbani hapo na kuchukua maiti na kisha kuelekea porini kwenda kuzizika.
Hiyo ndio ilikuwa kazi yake ya kila siku na ilikuwa ikimlipa sana. Mendez alikuwa mwaminifu sana na kazi hiyo alikuwa akiifanya kisiri sana na hakutakiwa mtu yeyote kufahamu. Japokuwa kazi ilikuwa ni ya siri lakini baadae siri ikaonekana kuwa si siri tena. Pombe….pombe…pombe ambazo alikuwa amekunywa katika baa moja hapo Monterrey ndizo ambazo zilimfanya kuropoka ovyo na hata kuitangaza kazi yake ambayo ilikuwa ikimuweka mjini.
Watu wakaifahamu kazi yake lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa na uwezo wa kufanya kitu kwa sababu mzee Sanchez alikuwa ameshika mpini na serikali kushika makali. Mara kwa mara Mendez alikuwa akipigiwa simu na kuelekea huko, kazi yake ilikuwa moja tu, kwenda kuchukua maiti na kwenda kuzizika.
Leo alikuwa amempigia simu mzee Sanchez kwamba alikuwa amekwishafika nyumbani hapo kwa ajili ya kuichukua maiti na kwenda kuizika. Mzee Sanchez hakutaka kuhoji maswali mengi kutokana na suala la kumpigia simu Mendez alikuwa akilifanya yeye au hata mmoja wa kijana wake, Zhikov.
Baada ya sekunde kadhaa, mlango ukafunguliwa na Mendez kuingia chumbani hapo huku mkononi akiwa amevaa glaves kama zile zinazovaliwa na madaktari hospitalini. Tofauti na Mendez, leo alikuwa amekuja na mtu mwingine, hiyo haikuwa kawaida, mtu huyo alionekana kuwa mgeni nae alikuwa ameingia kwa ajili ya kuchukua maiti ile.
“Huyu ni nani?” Mzee Sanchez aliuliza.
“Huyu ni mwenzangu, nimemwambia leo aje kunisaidia bosi” Mendez alimwambia mzee Sanchez maneno ambayo yalionekana kutokumuingia akilini.
“Aje kukusaidia?”
“Ndio bosi”
“Basi ichukue na maiti yake ukaizike, hii ni kazi yako na sitaki mtu mwingine ajue” Mzee Sanchez alimwambia Mendez huku akiupeleka mkono kiunoni kwa lengo la kutoa bunduki yake na kumfyatulia mtu ambaye alikuwa ameingia pamoja na Mendez.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Je nini kitaendelea mahali hapo?
Je huu ndio mwisho wa kila kitu?
Je ni mpango gani ambao Jocelyn anataka kumwambia Bwana Maxwell waufanye?
Je mpango huo utaweza kuwafanikisha kuingia ndani ya nyumba hiyo?
Je mzee Sanchez ataweza kumuua mtu huyo?
Je msaidizi huyo ni nani?
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment