Simulizi : Plastic Tears
Sehemu Ya Tano (5)
“kwanini hunipendi Asphaa?” swali hilo lilimtoka Joakim likiambatana na chozi lililomtoka kwa spidi kabla hata hajamaliza kutamka maneno hayo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“unataka kujua kwanini sikupendi?” aliuliza swali Asphaa kabla hajajibu swali aliloulizwa na Joakim.
“ndio… nahitaji kujua.” Alijibu Joakim.
“kwanza kabisa dini zetu haziendani. Mimi sitoweza kusimama kanisani na wewe hutoweza kusimama msikitini. Hiyo ndio kasoro kubwa, mengine ni madogo madogo tu ambayo wewe unayo na mimi huwa sivutiwi na watu aina yenu,” aliongea Asphaa na kumuangalia Joakim ambaye muda huo alirudi tena kwenye kiti haraka baada ya kusikia majibu ya Asphaa.
“kwa hiyo nikibadili dini utakubali kuolewa na mimi?” aliuliza Joakim haraka baada tu ya kukaa.
“sijakuambia ubadili… ukiamua kubadili hayo yatakua maamuzi yako.” Aliongea Asphaa na kunyanyuka.
“mi naenda kupanga nguo zangu. Tutaonana siku nyingine.” Aliongea Asphaa na kuamua kwenda chumbani kwake na kumuacha Joakim peke yake sebuleni.
“ kumbe dini inaweza kuwa kikwazo cha kuwa na Asphaa…. Kwa nini nisibadili dini tu ili nitimize ndoto zangu. Maana uislamu hautanipa shida kabisa. Nimelelewa katika familia ya kiislamu na ninaishi katika misingi hiyo japokua sijasoma vitabu vyao…. Ngoja niamue kitu.”
Hayo yalikua mawazo yalikua ytakijisoma ubongoni mwa Joakim baada ya kuambiwa maneno hayo na Asphaa. Aliamka kwenye kiti na kuondoka zake.
Safari hiyo ilimpeleka moja kwa moja msikitini. Kwakua saa kumi ilikua inakaribia kufika, alikuta watu wengi wakiingia msikitini hapo. Kwakua nguo alizovaa zilimruhusu kuingia, kwa mara ya kwanza alivua viatu vyake na kuingia msikitini.
Hakufanya chochote zaidi ya kukaa mpaka muda wa swala ulipofika ambapo aliigiza wanavyoswali na baada ya swala alisubiri watu watoke na ndipo alipomfuata imamu wa msikiti huo na kumuambia dhamira yake ya kutaka kusilimu.
Baada ya kutia udhu na kutamkishwa shahada mbili, tayari Joakim akaambiwa achague jina la kislamu analolipenda kwakua zoezi lilishakwisha.
KARIM ndio jina alilolichagua baada ya kulifisha jina la Joakim. Alipoulizwa sababu ya kubadili dini alitaja sababu nyingine kabisa na kuuficha ukweli kuwa mapenzi ndio yaliyo mpelekea afanye hivyo.
Alirudi nyumbani na kumkuta mama yake Maheer akiwa sebuleni.
“shikamoo mama.” Alisalimia Karim ( Joakim) baada ya kumuona mama yake huyo.
“marahabaa,… nina shida na wewe mwanangu.” Aliongea mama huyo na kumfanya Karim akae pale sebuleni kusikiliza wito.
“mwanangu sasa umeshakua mtu mzima na nadhani ni umri sahihi kabisa na wewe ukapata mwenza. Wewe unalichukuliaje swala hili?” aliongea mama huyo huku akionyesha wazi kua hakua kwenye utani muda huo.
“ni kweli mama, ila huyo mtu wa kumuoa ndio bado sijampata. Ila nia ninayo.” Aliongea Karim kwa heshima zote.
“sisi kama wazazi wenu, tumeamua kujenga nyumba mbili kwa ajili yenu nyinyi watoto wetu. Maheer yupo kwake na mke wake, na wewe tumepanga ukioa ndio tukukabidhi hiyo nyumba kama zawadi yetu kama wazazi wako.” Aliongea huyo mama ambaye alikua anampenda sana Karim kutokana na heshima pia utiifu uliokithiri ndio kilichompandisha cheo kuliko hata mtoto wake kumzaa.
“nitashukuru sana mama.. halafu kuna jambo jema nataka nikuambie mama.” Aliongea Joakim na kumfanya mama yake awe makini kumsikiliza.
“kitu gani hicho?” aliuliza mama huyo.
“kizuri upande wangu… nimeamua kwa ridhaa yangu kubadili dini na kuwa muislamu.” Aliongea Karim na kumfanya mama huyo atabasamu.
“sisi hatukutaka kukulazimisha kufanya hilo ndio maana tulikuacha na dini yako na wala haikua kikwazo cha kukupenda. Ila taarifa hizi zimenifurahisha pia… enhee, waitwa nani hivi sasa?” aliuliza mama yake Maheer.
“naitwa Karim.” Alijibu haraka.
“jina zuri sana…karibu kwetu.” Aliongea huyo mama na kucheka.
“nimeshakaribia.” Alijbu Karim na kunyanyuka na kwenda chumbani kwake.
Alipofika nyumbani kwake, alimpigia simu rafiki yake Maheer na kumpa taarifa hizo ambazo zilimfurahisha sana Maheer na yeye akaamua kumkaribisha kama alivyofanya mama yake.
Hakuna aliyemlaumu, japokua ukweli wa kufanya hivyo ulibaki moyoni mwake.
Siku ya pili yake, aliamua kwenda kwa kina Asphaa huku safari hii akiwa katika jina lingine badala ya Joaki alilozoeleka.
“umekuja na jipya gani,.. maana siku hizi umenogewa na kwetu?” aliongea Asphaa baada ya kumfungulia mlango Karim na kukaa sebuleni.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“leo nimekuja na mpya kweli,.. nadhani unaweza kufurahi baada ya kuisikia.” Alijibu Karimu bila kujali kebehi za Asphaa ambazo kwa muda mfupi alishazizoea.
“ongea haraka,.. nataka kutoka muda huu.” Aliongea Asphaa na kuangalia saa yake ya mkononi.
“ nimebadili dini tayari,… naitwa Karim hivi sasa.” Aliongea Karim na kumuangalia Asphaa ambaye aliangua kicheko cha haja mpaka akataka kudondoka kwenye sofa alilokaa.
“hii kweli mpya..hahahaaaaaaa” aliongea maneno hayo huku kicheko kikichukua nafasi yake mpaka machozi yakaanza kumtoka.
“naomba nenda maana nimecheka mpaka mbavu zinaniuma.” Aliongea Asphaa baada ya kunyamaza kucheka.
“mi nakuambia swala la msingi halafu unanicheka?.” Aliongea Karim huku akionyesha wazi kuwa kile kicheko cha Asphaa kinamuuma.
“tatizoo wewe ni bwege mtozeni ndio maana siwezi kuwa na wewe, yaani nilivyo kuambia kuwa dini ndio tatizo basi wewe mbio ukaenda kubadilisha,….. mwanaume usiyekua na maamuzi binafsi, utaweza kuishi na mimi wewe?... haya, sura yako hainivutii…. Utaweka ya bandia??” aliongea Asphaa maneno yaliyomfanya Karim kuondokewa na furaha yote aliyokuja nayo siku hiyo.
“nikufanyie nini Asphaa ili uamini kuwa nakupenda?” aliongea Karim huku analia.
“yaani unavyolia ndio kabisaa… mwanaume wa kulia lia simtaki mie… kiufupi usiupoteze muda wako kwangu… sikupendi na haitakaa itokee milele.” Aliongea Asphaa na kunyanyuka.
“naomba utoke nataka kufunga mlango nitoke mie… maana unaleta uchuro hapa kwa kulia lia toka jana.” Aliongea Asphaa na kuendea mlango na kuufungua akimsubiri Karim ambaye wakati huo machozi yalishalowanisha mashavu yake.
“sawa.. umeshinda wewe…. Nimeshindwa mimi. Nimekubali kuishusha bendera yangu na nakruhusu upandishe bendera ya mtu mwengine. Ila kumbuka kua mimi ni mgeni sana katika swala zima la mapenzi. Na umenikaribisha na maumivu makali yanitoayo machozi yasiyokauka machoni na moyoni pia….. umenifanya nimebadilisha hadi dini ilimradi ujue kua una thamani kiasi gani moyoni mwangu, bado unaona haitoshi.. .. nitakutumia smsm ya mwisho kabla ya kupoteza mawasiliano na mimi na hii inaweza kuwa mara ya mwisho katika maisha yako kuiona sura hii tena…. Nakutakia maisha mema Asphaa.” Aliongea Karim huku machozi mazito yaliyozingira kope na mboni za macho yake mpaka kumsabababishia ukungu yakimbubujika kama maji usini kwake. Aliamua kuondoka huku masikio yake yakisikia masonyo yakitoka nyuma yake.
Alirudi nyumbani kwao na kupaki nguo zake kwenye mabegi.
“unaenda wapi mwanangu, halafu ni ghafla na hujatupa taarifa wala sababu ya kusafiri kwako.” Aliongea mama yake Maher baada ya kumuona Karim akitoka na mabegi sebuleni.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“samahani mama kwa kutokuaga, ila hata mimi nimepata taarifa leo hii kuwa nahitajika Morogoro kwenye interview kesho asubuhi. Na pia kuna kampuni huko huko naenda kufanya kazi kwa miezi mitatu tu wakati najishikiza kabla ya kupata kazi kabisa.” Aliongea Karim na kujitahidi kutabasamu ilimradi asishtukiwe na mama yake huyo.
“haya. Nakutakia safari njema.” Aliongea huyo mama na kumfuata karim na kumkumbatia.
Alipotoka nje, alipanda Taksi iliyokuja kumchukua baada ya kumpigia simu dereva wa taksi hiyo.
Aliingia kwenye gari na kumruhusu dereva ampeleke kituo cha mabasi yaendayo mikoani ubumgo. Wakati gari inaenda, Karim akaamua kuandika sms nzito huku machozi yanmtoka.
“ kwaheri mwanamke niliyetokea kukupenda kuliko maisha yangu katika sayari hii. Nimeamua kutimiza ahadi yangu kwa kukutumia ujumbe wa mwisho kama nilinyokuahidi nilipokua hapo kwenu. Nimeamini kua mapenzi ni makubaliano kati ya mpenda na mpendwa. Nilichofanya ni kukubali kubeba mambo ambayo sikujua uzito wa aliyekubebesha. Ila kumbuka kua tabasamu la mtu aliachialo pindi akuonapo linaweza kukudhihirishia ni kiasi gani anathamini uwepo wako kwake. Kupenda nisipopendwa ndio kitu kilichofanya niukimbie mji wa Dar na kwenda sehemu ambayo sihitaji mtu yeyote afahamu nilipo ili niweze kuishi mbali kabisa na wewe. Sikutarajia kuwa kuna siku ningeweza kuiacha familia iliyonidhamini na inaendelea kunijali kama mzawa kwa sababu yako, ila kuwa karibu na wewe ni kujiumiza na naweza kuchukua maamuzi mazito ambayo sitaki yatokee kwako wala kwangu. Hakuna anayenipenda wala kuonyesha kua yupo pamoja na mimi. Sikulaumu wewe kwa kutonipenda, ila naulaumu moyo wangu kwa kuanguka katika penzi la mtu asiyejali hisia zangu. Nakutakia maisha mema.”
Ujumbe huo uliochukua sms tano kwa moja aliutuma kwenye namba ya simu ya Asphaa na kuendelea na safari yake.
Alifika ubungo na kukata tiketi tayari kwa safari ya kuelekea Tanga. Hakukua na usafiri wa mkoa wowote ule zaidi ya mkoa ya karibu kutokana na muda kuenda sana.
Alipata tiketi yake na kutulia pembeni huku akijaliribu kupata soda na Bites mbali mbali huku akisubiri gari hiyo ambayo ilikua inaondoka lisaa limoja mbele.
Baada ya dakika zipatazo ishirini, aliona simu yake inaita huku jina la Ahlam likiwa limejitokeza katika kioo cha simu yake.
Aliangalia hiyo simu mpaka ikakata bila kuipokea. Hakuhitaji kupokea simu ya mtu yeyote yule. Hata alipoiona simu yake ikiita na rafiki yake Maheer akiwa ndio mpigaji wa hiyo simu, pia hakuipokea. Sana sana alimjibu kwa kumtumia sms.
“sorry bro, nakutakia maisha mema na shem… si dhani kama tutaonana tena.”
Aliiandika hiyo sms huku machungu ya moyo yakimjia tena na kujizuia kwa kuamua kuizima kabisa hiyo simu. Alijua kua rafiki yake lazima atajibu na kumuhimiza abaki kwakua alikua anampenda sana.
Aliamua kuondoka na kusahau kila kitu katika jiji hili na kuamua kuanza maisha mapya kabisa huku akiwa hafahamu ataanzaje kuishi na wapi ndio yatakua makazi yake mapya.
Baada ya dakika kusogea na kubaki kama dakika kumi na tano ndio basi liondoke, akaamua kuingia kwenye basi hilo na kukaa kwenye siti yake na kujiinamia.
Gari ya Ahlam ilifika ubungo haraka na kuingia ndani. Alishika Ahlam haraka na kuanza kuingia kwenye kila gari na kumuangalia Karim kama atakua katika basi hilo.
Baada ya kumkosa kwenye magari kadhaa, kwa mbali aliona gari lililokua linaondoka. Alipoliangalia, aligundua kua hakupata nafasi ya kuingia . hisia zake zilimuambia kua alikuwemo mule. Haraka alikimbia na kudondoka mara kadhaa huku akiliwahi gari hilo lilikua linakaribia kuingia katika bara bara kuu.
Konda alimuona na kumwambia dereva wake asimamishe gari.
Ahlam alilifikia lile gari na kuingia bila kumuonyeshea konda tiketi. Alipoingia tu, alianza kukagua watu waliokua katika siti za gari hilo.
Alimuona mtu mmoja aliyekua amejiinamia. Muonekano wake ulimfahamisha kuwa mtu huyo ni Karim.
“JOAKIM!”
Aliita Ahlam na kumfanya yule mtu kuinua kichwa chake na kugundua kua alikua amemfananisha. Hakua Joakim, ila ni mtu mwengine tu aliyekua na muonekano kama wa Joakim kwa nyuma.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ahlam alishuka na kuanza kukimbia tena na kuingia ndani. Alipochoka. Alisimama na kuanza kuangaza huku na huko na asijue afanye nini.
“AHLAM”
Ilisikika sauti ikitokea nyuma yake. Sauti hyo alikua anaifahamu vilivyo. Ghafla akajikuta uchovu wote umemuisha na akajikuta anatabasamu hata kabla hajamuona mtu aliyemuita. Aligeuka na macho yake yakakutana na Karim. Alikimbia mbio na kwenda kumkumbatia Karim.
“NAKUPENDA JOAKIM…. Ungeondoka mji huu. Usingekua unamkimbia Asphaa kama unavyofikiria. Ila ungekua unauumiza moyo uliojaa siri ya kukupenda toka siku ya kwanza nilivyokuona….. sms yako nimeiona na ndio imeniumiza sana kuliko mlengwa… nakupenda Joakim na naomba ukubaliane na matakwa ya moyo yangu…. Usiniumize kwakua sikuwahi kumuumiza mtu yeyote.”
Ahlam alijikuta anaongea maneno hayo huku machozi yanamtoka. Alimkumbatia kwa nguvu kuonyesha ni jinsi gani alikua anamuhitaji.
Maneno ya Ahlam yalimfanya Karim aishangae dunia na ulimwengu mzima wa mapenzi. Hata siku moja hakuwahi kuwaza kua Ahlam alikua anamfikiria ndio maana na yeye hakuweka mawazo yake tena juu ya mrembo huyo.
Slogan ya mpende akupendaye ndio iliyochukua nafasi yake na Karim nae hakufanya makosa. Akaamua kukisikiliza kilio cha Ahlam na kumkubali kama mtu aliyekuja kuirudisha furaha yake iliyopotea masaa machache yaliyopita.
Walirudi nyumbani baada ya kwenda kukaa katika restaurant moja na kupanga yao. Walirudi nyumbani kwa Ahlam na kumkuta Asphaa sebuleni.
“ si ulisema kua hautarudi tena…..” aliongea Asphaa na kukatishwa na dada yake.
“kuwa na heshima Asphaa…. Karim ni shemeji yako kuanzia sasa na sihitaji maswali wala mjadala kuhusu hili.” Aliongea Ahlam na kumfanya Asphaa apigwe na butwaa. Yalikua maamuzi ya haraka ambayo hata Asphaa mwenyewe hakuwahi kuyafikiria.
Yale aliyokua akiomba mama yake Maheer yalitimia baada ya Karim kumtambulisha kwa familia hiyo kuwa ndio mke wake mtarajiwa. Wazazi wa Maheer hawakua na shaka na Ahlam, walimjua na kumkubali kutokana na heshima aliyokua nayo.
Harusi kubwa ilifungika huku Maheer akiwa ndio best man wa Karim. Asphaa alishindwa tena kwa mara ya pili kuhudhuria harusi hiyo ya dada yake kutokana na aibu aliyokua nayo.
Ahlam alimuachia nyumba mdogo wake na wao wakaenda kukaa makazi mapya huko kwenye nyumba ya Karim iliyojengwa karibu kabisa na nyumba ya Maheer.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakajenga familia hizo mbili na kuwa moja huku Karim akijikuta ndio mshindi wa vita ya mapenzi kwakua na Ahlam ambaye awali kila mmoja alikua na mahesabu nae.
……..MWISHO……….
0 comments:
Post a Comment