Search This Blog

Friday, July 15, 2022

PLASTIC TEARS - 4

 







    Simulizi : Plastic Tears

    Sehemu Ya Nne (4)





    Joakim alijiinamia kwa muda na baadae akanyanyua sura yake na kumtazama Asphaa na kuitikia kwa kichwa.

    “thenks mine.” Aliongea Asphaa na kumfuata Joakim na kumkumbatia.

    “acha niwahi sababu kuna sehemu nimeagizwa na mama.” Aliongea Joakim na kunyayuka bila ksubiri majibu yoyote kutoka kwa Asphaa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliondoka kwa kasi na kwenda kwenye gari yake. Hapo macozi ndipo yalichukua nafasi yake na kuanza kulia kwa uchungu huku akiupiga piga usukani wa gari hiyo.



    Aliondoa gari kwa spidi huku akiwa amejaa hasira na uchungu juu ya penzi lake linaokaribia kupotea tena yeye akiwa ni mmoja kati ya anayetakiwa kuchukua kisu na kujimaliza mwenyewe.



    Kwa nusura za Mwenyezi Mungu alifika nyunbani kwao salama baada ya kunusurika ajali mara kadhaa alipokua barabarani.



    Alipofika nyumbani alisalimia wazazi wake hao wa hiyari na kwenda chumbani kwake na kujilaza. Maheer alikua bafuni anaoga. Alipotoka alimfuata Joakim na kumuomba funguo ya gari.

    “twende basi kwa kina Lailati.” Aliongea Maheer.

    “siko poa, utanisalimia tu kwa shem.” Aliongea Joakim na kuendelea kulala.

    “malaria imerudi tena?” alioliza Maheer na kurudi kitandani alipokua Joakim.

    “hapana….. sipo sawa tu.” Aliongea Joakim bila kumuangalia Maheer.

    “mimi ni zaidi ya rafiki yako, kwa hiyo nina haki ya kujua kila kinachokusibu.” Aliongea Maheer na kumuamsha Joakim kwa kumtikisa kidogo.



    “we nenda tu kwa shem,.. ukirudi nitakuambia kinachonisibu.” Aliongea Joakim baada ya kunyanyuka pale kitandani na kukaa.



    “poa… ila nilimwambia kua tunaenda wote.” Aliongea Maheer kinyonge.

    “mwambie tu ameanza kujisikia vibaya ghafla… hivyo aniwie radhi.” Aliongea Joakim na kujilaza tena kitandani.



    Maheer alimuangalia Joakim kwa muda bila kupata majibu sahihi. Aliamua kuondoka zake na kumuacha rafiki yake huyo akiwa amelala kifudi fudi.



    Alitoka na kwenda kwa kina Lailati na kumpigia simu. Lailati alitoka nje na kumfuata mpenzi wake.

    “twende basi.”aliongea Maheer baada ya kukumbatiana na kipenzi cha roho yake.

    “shem yupo wapi?... si umesema unakuja nae?” aliuliza Lailati.



    “amesema hawezi kuja.. nahisi anaumwa maana nimemuona jinsi alivyopooza.” Alijibu Maheer na kumfungulia mlango wa gari mpenzi wake huyo.



    Lailati aliingia kwenye gari hiyo na safari ya kuelekea beach komba ikaanzia hapo. Walifika eneo la tukio na kujikuta wameya furahia mandhari ya siku hiyo kupita kiasi kutokana na mapambo ya watu waliokua wakisheherekea harusi ya wazi iliyofanyika pembezoni mwa beach hiyo.



    Walikaa kwa muda wa masaa yapatayo matatu. Walipiga story za mapenzi yao na jinsi watakavyofikia malengo yao ya kufunga pingu za maisha.



    Giza lilipoanza kuchukua nafasi yake, waliamua kuondoka kwa sababu Lailati hakutakiwa kukaa muda mrefu bila kuonekana nyumbani kwako.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kumrudisha Lailati kwao, alirudi nyumbani na kumkuta Joakim amelala. Alipigwa na butwaa kwa sababu sio utaratibu wa Joakim kulala mapema. Hakumsumbua, alimuacha na ilipofika asubuhi aliamua kumuuliza rafiki yake kitu kilichomsibu rafiki yake huyo ili ajue atamsaidia vipi.



    “kaka,… siku nyingi huwa ukiniuliza juu ya mahusiano yangu, na jibu langu hua moja tu… huwa nakwambia kua bado sijaona. Ila kwa sasa macho yangu yameona na moyo wangu nahisi umepotea. Sijui ni nani atanitafutia moyo wangu. Hakika nampenda sana huyo mtu ambaye sina uhakika kua na yeye ananipenda au hahitaji hata kuniona.” Aliongea Joakim huku akionyesha ni jinsi gani alivyokua akipata maumivu moyoni juu ya huyo mtu anaemuelezea.



    “niweke wazi Joakim,… ni msichana yupi huyo anayekufanya uwe hivyo?” aliongea Maheer huku akionyesha ni jinsi gani alivyokua hatamani mambo kama yale yajitokeze kwa rafiki yake huyo.



    “Asphaa… hakika na mpenda sana na siwezi kumuelezea jinsi moyo wangu unavyoumia na kusulubika juu yake. Najihisi siwezi kubembeleza wala sina sentensi tamu za kumfanya msichana aweze kunielewa ni nini ninachomaanisha. Ananinyima raha

    sana na sijui nafanyeje?” aliongea Joakim na kumfanya Maheer kumuonea huruma rafiki yake huyo kwa jinsi alivyokua anaongea unafikiri alikua anataka kulia.

    “hilo swala wewe niachie mimi, nitajua jinsi ya kulishughulikia. Nitaongea nae na atanielewa tu.” Aliongea Maheer na kumpooza Joakim kwa kumshika kwenye bega.



    “najua hujawahi kuniangusha kwa lolote.. nakutegemea Maheer, nampenda sana Asphaa kuliko msichana yoyote hapa duniani. Nampenda kuliko ninavyoweza kukuelezea.” Aliongea Joakim huku akionyesha ishara za upendo aliokuwa nao juu ya mrembo huyo aliyetokea kumuweka moyoni kabla hajamtongoza na kusikiliza maamuzi yake.



    “yaani kwa maelezo yako tu, nimeshaelewa ni jinsi gani unavyompenda kwa dhati Asphaa, kwa hiyo we usijali wala nini. Mimi nitamaliza kila kitu. Labda kama nikitakiwa kukushirikisha ndio nitafanya hivyo.” Aliongea Maheer na kumfanya Joakim atabasamu kidogo.

    “nitashukuru sana ndugu yangu.. undugu si kufanana bali kufaana.” Aliongea Joakim na kuweka methali kama njia ya kutilia mkazo maneno aliyoyaongea.



    Bila kuchelewa, alichukua simu yake na kumuendea hewani Asphaa.

    Asphaa alijikuta anashangilia sana baada ya kuona jina la Maheeer likiwa limejitokeza kwenye kioo cha simu yake. Aliipokea kwa mapozi yote 66 na kujilaza kitandani kumsikiliza huyo mwanaume aliyetokea kumpenda hata kabla hawajaonana.



    “hallow babie.” Alipokea Asphaa na kuukumbatia mto uliokua pembeni ya kitanda chake.

    “hallow Asphaa.” Aliita jina hilo Maheer na kumfanya Joakim akae kwa makini baada ya kulisikia jina la mtu ampendaye.

    “niambie wangu.” Aliongea Asphaa kwa tabasamu huku akionyesha kua amechangamka kuliko siku zote.

    “unaweza ukapata muda tukakutana mimi na wewe faragha kidogo tukazungumza kitu?” aliongea Maheer na kumuangalia Joakim ambaye alikua makini akiyafuatilia maongezi hayo.

    “hata sasa hivi ukiniambia nipo free… tukutane wapi?” aliuliza Asphaa kwa hamu kubwa ya kutaka kujua kitu anachoitiwa.

    “tukutane stears hapo posta.” Aliongea Maheer.

    “saa ngapi sasa?” aliuliza Asphaa

    “si umesema upo huru kuanzia muda huu?” aliuliza Maheer.

    “ndio.” Alijibu haraka Asphaa.

    “tukutane hapo baada ya saa moja kutoka sasa.” Aliongea Maheer na Asphaa akakubaliana na muda huo.

    Maheer akakata simu na kumgeukia Joakim.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “usijali kaka, leo hii nitajua niongee nae vipi mpaka aelewe. Yule ni wetu na kwa jinsi ananyonikubali sana, hawezi kupindua.” aliongea Maheer huku anatabasamu na kumuangalia Joakim aliyekua anajilazimisha kutabasamu.



    “naona mdogo wangu unanitenga siku hizi,…. Haya hata leo unataka kwenda peke yako. Kuna kitu gani huko uendapo?” aliuliza Ahlam baada ya mdogo wake kumaliza kujiandaa na kuomba funguo ya gari.

    “hamna dada, hakuna kitu chochote dada yangu. Naenda mara moja narudi sasa hivi.” Aliongea Asphaa huku akiwa anajigonga gonga katika matamshi yake. Hali hiyo ilimfanya dada yake ahisi kitu.



    “najua kama umepata mwanaume, ila kuwa makini sana na hao wanaume wa hili jiji. Maana ni matapeli sana wa mapenzi.” Aliongea Ahlam na kumuangalia mdogo wake aliyekua amepigwa na butwaa baada ya kuhisi ukweli wa safari yake.



    “umejuaje dada kama naenda kukutana na mwanaume?” aliongea Asphaa huku akionyesha wazi kushangazwa na ugunduzi wa dada yake.



    “nimetangulia kuliona jua kabla yako, hivyo si ajabu nikiwa na upeo zaidi yako.” Aliongea Ahlam na kuendelea kusoma jarida alilokua analisoma toka mwanzo.



    “huyo mwanaume mwenyewe ni mpole na mtulivu sana dada… yaani hata nikimleta hapa na nikimtambulisha kwako, basi wewe mwenyewe utakiri na utakubali niolewe nae bila ya kipingamizi.” Aliongea Asphaa huku anatabasamu.



    “usimuwekee mwanaume dhamana hata siku moja mdogo wangu… wana rangi nyingi kama alivyo kinyonga. Na anaweza kubadilika hata sehemu ambayo huwezi amini kama anaweza kubadilika.” Alongea Ahalam na kumuangalia mdogo wake usoni.

    “acha niende dada, nachelewa.” Aliongea Asphaa baada ya kuangalia saa yake na kumjulisha kua zimebaki dakika ishirini tu kufikia muda walikubaliana kukutana na Maheer.

    “okey.. nadhani umenielewa mdogo wangu.. nakutakia safari njema.” Aliongea Ahlam.



    “haya dada,,, na wewe take care.”aliongea Asphaa na kuufunga mlango na kuingia kwenye gari huku anatabasamu tayari kwa safari ya kuelekea mahali walipopanga kukutana na Maheer.





    Walikutana eneo walilopanga kukutana na kusalimiana kisha wakachagua sehemu yenye utulivu kidogo na wakanza maongezi yao.

    “za siku nyingi Asphaa.” Alianza kuongea Maheer huku akiachia tabasamu mwanana.

    “nzuri tu, hofu kwako.” Aliongea Asphaa na yeye akilipizia tabasamu kama alilolitoa Maheer.

    “nimefurahi sana kwa jinsi ulivyoitikia wito wangu vizuri na kufika kwa wakati.” Aliongea Maheer kama sehemu ya kuanzisha mjadala uliomleta pale.

    “hata mimi, maana wito wako nahisi ni wa heri kwangu na utaniacha nikiwa na furaha zaidi ya hii niliyokua nayo.” Aliongean Asphaa bila kujua kua Maheer alikua ana jambo jingine kabisa alilokuja kumuambia na si lile analolifikiria muda huu kwenye kichwa chake.

    “ni kweli, maana haya nitakayo yaongea ni ukweli tupu na yanatoka moyoni.” Aliongea Maheer na kumuangalia Asphaa ambaye alijitayarisha tayari kuyasikia hayo mambo mazuri yatakayomuacha akiwa katika furaha.

    “nayasubiri kwa hamu hayo ya moyoni.” Aliongea Asphaa na kumuangalia Maheer.



    “unajua kila mtu hua na chaguo katika moyo wake. Uchaguzi mzuri au mbaya ni matokea ya baadae sana kwakua mwanzo siku zote huwa mzuri. Kwakua wewe na kijana unayejitambua basi utakua na fikira pembuzi juu ya hiki nikiongeacho. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Katika moyo kuna nafasi moja tu ya ukweli ambayo binaadamu tumetunukiwa na mungu katika swala zima la mapenzi. Japokua una uhuru wa kuanzisha mahusiano mengiine na ukawapenda pia ila yule moja ukawa na upendo nae zaidi kwakua swala la kuudhibiti moyo upendao liko nje ya uwezo wako. Sijajua kwako wewe unalichukuliaje swala hili la mapenzi, ila kwangu mimi nalichukulia kwa umakini na kulitazama kwa macho yote mawili. Joakim amenituma nije kwako nikuambie kuwa kwa dhati ya moyo wake ametokea kukupenda sana sema hajui tu ni wapi aanzie kukuelezea hisia zake… nakuomba usikatae.” Aliongea Maheer na kumfanya Asphaa kupigwa na butwaa. Maana alitegemea baada ya maongezi Maheer angemjibu kuwa anaempenda ni yeye, ila mwishoni amemchomeka mtu mwengine wakati yeye alimtuma huyo mtu amuelezea hisia zake juu ya Maheer.



    “mbona sijakuelewa Maheer… Joakim tena?” aliuliza Asphaa huku akionyesha kuwa yupo katika hali ya mshangao uliokuwa dhahiri kabisa.

    “yeah.. Joakim anakupenda sana, toka siku ya kwanza alipokuana kwenye simu yangu kupitia mtandao wa whatsapp, ndio siku aliyokutia moyoni hata kabla hajakuona.” Alifunguka Maheer.



    “mimi simpendi Joakim, mimi nakupenda wewe Maheer, hata yeye mwenyewe nilimambia jana na akaniambia kuwa atanisaidia kukuambia kua nakupenda. Sasa nimeshangaa sana kusikia eti anakutuma na wewe uje uniambie kuwa ananipenda???...hilo ni swala ambalo haliwezekani… toka siku ya kwanza nilipokuana kwenye siu ya dada yangu, nilitokea kukupenda na ikafikia hadi nikachukua hatua ya kukupigia kabisa ilimradi nisikie sauti yako… nakupenda sana Maheer.” Aliongea Asphaa huku machozi yakianza kumlenga lenga.



    “hiki kweli ni kizungumkuti.. ila ungenisikiliza tu mimi. Maana swala la wewe kuwa na mimi ni swala lisilowezekana.” Aliongea Maheer na kumkazia macho mrembo huyo aliyekua akionyesha ishara zote za kutaka kulia.



    “kwanini Maheer?” aliuliza Asphaa huku machozi yakianza kutiririka katika mashavu yake.

    “mimi nina mpenzi wangu, hata ukimuuliza dada yako atakuambia. Tena nampenda na nipo njiani kumuoa. Hivyo swala la kuwa na wapenzi wengi sio dili kwangu.” Aliongea Maheer na kumfanya Asphaa aanze kulia na kutoa sauti japo ilikua ndogo aliyoisikia mwenyewe tu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Maheer nipende mimi, moyo wangu nimeuweka rehani kwa ajili yako. Usinikatili kiasi hiki Maheer. .. mimi sio muhuni mpaka useme kua sina sfa za kuwa wako. Usinikatili Maheer.” Aliongea Asphaa huku analia na kusababisha Maheer kujisikia vibaya kidogo.



    “nikisema nakupenda, utafurahi leo tu na siku chache, ila utapata maumivu makali pindi utakapogundua kuwa si wewe unayeishi moyoni mwangu. Utamchukia kila mwanaume kama si kuyachukia mapenzi yenyewe. Kwa sasa unalia ila maumivu haya yataisha pindi uwapo na Joakim kwa sababu tayari umeanza kuishi moyoni mwake bila wewe mwenyewe kujua. Naomba usilipize kwa kumkataa Joakim kwa sababu ukimuumiza yule ni zaidi ya kuniumiza mimi. Kama kweli unanipenda na huhitaji kuniumiza, kubali kuwa na Joakim daima utaliona tabasamu langu likichomoza kwako kila nikuonapo.” Aliongea Maheer na kumuangalia Asphaa ambaye muda huo uso wake uliloa kwa jasho na mifereji ya machozi ilijijenga mashavuni bila kukakuka.

    Asphaa hakujibu kitu, bali alinyanyuka na kuondoka haraka na kumuacha Maheer akiwa pale anasikitika.



    Safari yake ilikua ya furaha wakati anatoka nyumbani, lakini ikaja kuwa ya huzuni pale alipoambiwa ukweli kuwa hatakiwi na huyo mwanaume aliyetokea kumpenda kupita kiasi.



    Alirudi nyumbani na huku akiwa anaendelea kulia. Hali hiyo ilimshtusha dada yake baada ya kumuona Asphaa akimpita pale sebuleni na kuelekea chumbani kwake huku analia.

    “umepatwa na nini mdogo wangu?” aliuliza Ahlam baada ya kuingia chumbani kwa mdogo wake ambaye wakati huo alikua amejilaza kitandani huku akiendelea kulia.

    “nampenda dada, nampenda sana lakini hataki kuusikiliza moyo wangu juu ya maumivu niyapatayo juu yake… nahisi siwezi kuishi bila yeye dada.” Aliongea Asphaa huku akiendelea kulia kwa kwikwi.



    “pole mdogo wangu. Ila wakati unatoka nilikuambia kuwa wanaume wana rangi nyingi zaidi ya kinyonga. Pia huweza kubadilika mahali ambapo huamini kama wanaweza kubadilika. Ungeyatafakari haya basi ungezichunga hatua zako na usingekuja unalia kama uliavyo sasa. Ni nani huyo anayekufanya mpaka ukose furaha ya maisha mdogo wangu?” aliongea Ahlam na baadae akauliza swali lililomfanya Asphaa anyanyuke pale kitandani.

    “MAHEER dada,…nampenda sana.”



    Alipolitaja hilo jina, dada yake alivuta pumzi ndefu na kumuangalia tena mdogo wake kwa mshangao. Maana hakulitarajia lile tukio kwa muda ule.



    “umeanza lini mahusiano ya kimapenzi na Maheer mpaka hivi sasa mfikie hatua ya kuumizana moyo?” aliuliza Ahlam kwa mshangao mkuu.



    “ni mmi ndio nilitokea kumpenda toka nilipomuona kwenye picha zako. Nilivutika sana nae ndio maana nikakuliza siku ile umeli save vipi jina lake katika simu yako. Ulipo niambia ndio nikaanza kuwa karibu naye. Hivi leo ndio tulikua tunakutana kwa ajili ya kunipa jibu langu. Amenikataa dada.” Aliongea kwa uchungu Asphaa.



    “Maheer ni mvulana makini sana na si muhuni kama ukimuangalia kwa umakini. Ana mpenzi wake na anampenda kupita maelezo. Japo kua huwezi kuwakuta pamoja kwakua bado wana mipango ya kuoana na familia zao zinaishi katika maadili ya kidini sana. Kwa hiyo swala la kuwa nae kimapenzi hilo sahau.” Aliongea dada yake na kumuangalia Asphaa na kutikisa kichwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “naomba niache kidogo dada maana nimechanganyikiwa sana.” Aliongea Asphaa na dada yake akatoka chumbani kwake.



    Baada ya kujifkiria kwa muda baada ya kulala muda mrefu.ndipo Asphaa alipoamka na kuchukua simu yake na kumpigia Joackim.

    “nashukuru kwa yote uliyonitendea, kama ulikua hutaki si ungeniambia kuliko kufanya hayo uliyoyafanya?” aliongea Asphaa baada tu ya Joakim kuipokea simu yake.

    “sikua na jinsi kukubali kuwa mtumwa siku ile. Ila kumbuka hata mimi nina moyo wa nyama, sina chuma mie useme naweza kuvumilia vitu vizito kama hivyo. Moyo wangu umekuchagua wewe Asphaa. Unafikiria naumia kiasi gani wewe unaponitamkia kuwa unampenda mtu mwengine tofauti na mimi? Nakuomba unisamehe kama nimekosea, ila hayo ndio niliyoamua kufanya kwakua sikuweza kumuambia Maheer yale uliyonituma.” Alijitetea Joakim.

    “siwezi kukuelewa Joakim hata ukisema nini…. Ukweli ni kwamba sikupendi na nimetokea kukuchukia sana kwa uliyonitendea.” Aliongea Asphaa na kukata simu.



    Maneno hayo yalimfanya Joakim agande na simu sikioni kama vile alikua bado anaongera naAsphaa. Alijikuta anakaa chini na kuanza kulia. Hakuwahi kupenda katika maisha yake na huyo ndio msichana wa kwanza kumtia moyoni hata bila makubaliano kati yao.

    Machozi ya kutendwa hata kabla hajapata matamu ya mapenzi yali mmiminika kwa uchungu Joakim.



    Maheer aliporudi nyumbani, alimkuta rafiki yake akiwa kavimba macho huku akiendelea kulia kama vile ameletewa taarifa ya msiba wa mtu wa karibu kabisa. Alimfuata na kunyamazisha huku akimpa matumainai juu ya kumpata mrembo huyo.

    “kuwa na moyo wa kiume Joakim. Wasichana wapo wengi sana na kila mmoja ana uzuri wake. Yule ananielewa sana mimi, hivyo kwa kutumia udhaifu wake huo ndio itakua njia ya kuwa karibu na wewe na baadae kuwa wako kabisa. Ondoa shaka Joakim.” Aliongea Maheer maneno yaliyompa kidogo faraja na kumfanya aweze hata kula na kupata usingizi,



    Mateso juu ya kukataliwa na mtu ampendaye kwa moyo wake wote yaliendelea kumtesa Joakim. Kuna wakati alitamani kuachana na huu mji na kukimbilia mahala ambapo Asphaa atakua mbali na upeo wa macho yake, lakini bado ilikua haitoshi. Aliifuta namba ya Asphaa kwenye simu yake, lakini bado ilibaki ubongoni na mara zote alitamani kumpigia ingawaje huambulia majibu yalimnyon`gonyesha na kumfanya alie kila siku.



    Mwili wa Joakim ulianza kupoteza uzito kila siku iendayo kwa mungu. Hakuna alichokua anakifikiria zaidi ya Asphaa.



    Asphaa nae hakuchoka kulibembeleza penzi la Maheer ambaye nae hakua na hamu hata ya kumuona kwakua alikua anamtesa rafiki yake ambaye wamekuwa kama ndugu kabisa kutoka tumbo moja.



    Ahlam na Maheer walikua na kazi kubwa sana ya kuwabembeleza wawili hao kwakua kila mmoja alikua anaumizwa na mapenzi ambayo yaliwakataa kabisa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kadi za mwaliko wa harusi ya Maheer ndio kilichomfanya Asphaa atamani hata kujiua kwakua ilivunja ndoto zake kabisa za kuwa Maheer siku moja.

    Ilikua kazi kubwa sana kuwa bembeleza watu hawa ambao hawakua na raha kabisa katika maisha yao.

    Ilifikia kipindi mpaka Ahlam alimfuata Maheer na kumuomba amuoe na mdogo wake kwakua dini iliruhusu kufanya hivyo. Maheer alikataa katu katu na kumwambia kua kufanya hivyo ni sawa na kuamua kumkatili ndugu yake mwenye ndoto kede kede na Asphaa.



    Ndoa ilipita kati ya Maheer na Lailat. Machozi yasiyo na kifani yalimtoka Asphaa siku hiyo ingawaje hakuweza kuhudhuria. Hakuna kitambaa kilichoweza kukausha machozi yake. Hakuna mtu aliyeweza kumbembeleza baada ya kumuona akiwa katika katika hali kama ile. Mimi nayaita MACHOZI YA PLASTIKI.



    Kwa Joakim ilikua faraja kidogo japokua hakua na uhakika kua yeye ndio chaguo la pili la Asphaa baada ya kutoswa kiroho mbaya na chaguo la kwanza.

    Aliamua kumfuata kwao baada ya kupita wiki mbili toka harusi ilipopita.



    “karibu Joakim” alikaribisha Ahlam

    “nimeshakaribia, vipi…Asphaa yupo?” aliuliza Joakim kabla hata hajapiga hatua hata moja kuingia ndani.



    “yupo chumbani kwake.” Alijibu Ahlam.

    “naomba niitie.” Aliongea Jakim na kumungalia usoni Ahlam ambaye alikua anamshangaa kidogo.



    “ingia ndani sasa” aliongea Ahlam na Joakim akaingia ndani na kukaa kwenye sofa la mtu mmoja. Ahlam akaingia ndani na kwenda kumuita mdogo wake. Baada ya dakika mbili, Ahlam alishuka chini na kumfuata Joakim alipo.

    “msubiri anakuja.” Aliongea maneno hayo Ahlam na kwenda chumbani kwake.



    Baada ya dakika zipatazo kumi kupita, ndipo Asphaa alipotoka chumbani kwake na kwenda sebuleni na kukaa sofa lililokua mbali kidoga na Joakim.



    “sema kilichokuleta.” Aliongea Asphaa bila hata salamu

    “nimekuja hapa ili tufikie muafaka wa hili sakata kati yangu mimi na wewe.” Aliongea Joakim kwa uoga kidogo.



    “sakata??... sakata gani hilo?” aliongea Asphaa huku akibinjua midomo yake kwa dharau.



    “naweza sema utata juu ya wewe na mimi katika swala zima la mapenzi. Mwanzoni ulikua unampenda sana Maheer ambaye kwa sasa ameshakua mume wa mtu na wee huna nafasi tena kwake. Ila nafasi ya ukweli ni hii yangu ambayo hata mimi wewe ndio chaguo langu la kwanza.” Aliongea Joakim huku akimuangalia Asphaa ambaye alikua bize kuzichonga kucha zake na kifaa maalumu alichotoka nacho ndani.

    “unachekesha sana wewe, yaani mimi nikae na kufikiria utumbo kama huo?.... yupo mwanaume ambaye nitakua nae na nitampenda lakini sio wewe.” Aliongea Asphaa huku akimkazia macho Joakim kuonyersha ni jinsi gani alivyokwazika na maongezi ya Joakim.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “usiseme hivyo Asphaa.. naumia mwenzako unapo ninyanyapaa.” Aliongea Joakim kwa huzuni kidogo.

    “bwana eeeh.. kama huna jipya nakuomba nyanyuka na upige hatua kama ulizokuja humu na kutoka. You west my time.” Aliongea Asphaa na kumuangalia Joakim ambaye hakuweza kuhimili maneno hayo na kuamua kunyanyuka.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog